Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

WASTARA: NIKIKUMBATIWA NAKUWA HOI

$
0
0
Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu, Wastara Juma amefunguka kuwa starehe yake kubwa duniani ni kukumbatiwa na anapofanyiwa kitendo hicho na mtu wa jinsia yoyote huwa hoi.

Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema: “Mimi napenda sana kukumbatiwa au kukumbatia, awe ni mwanaume au mwanamke, ndugu yangu au hata kama siyo ndugu yangu, tukikumbatiana tu najisikia raha sana.

“Unajua kila mtu anakuwa na kitu anachokipenda duniani sasa mimi starehe yangu ndiyo hiyo hata marafiki zangu wanajua kwamba mimi napenda kukumbatiwa.
Source:Global Publishers

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA SHILOLE-CHUNA BUZI

$
0
0
Baada ya nakomaa na jiji ...Shilole aachia Chuna buzi..Sikiliza ama download hapa chini:

MTANGAZAJI WA TELEVISHENI YA EAST AFRICA(EATV),KEN KIDAGO AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha East Africa aliyekuwa akifanya kipindi cha 5 sports, Ken Kidago amefariki dunia.
Taarifa ambazo pia zimethibitishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho zinaeleza kuwa tangu jana januari 30,2014 Ken hakuonekana kazini ambapo simu zake zilikuwa zikipigwa bila majibu ikabidi uongozi wa EATV kutoa taarifa kwa jeshi la polisi nchini Tanzania,walipofika nyumbani kwake Mlalakua jijini Dar es salaam wakagonga mlango hakufungua kabidi wavunje na kuingia na kukuta amefariki.

Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa sababu ya kifo chake.

Ken Kidago aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Ukweli ya mjini Morogoro kabla ya kwenda Arusha ambapo alirejea jijini Dar es salaam hivi karibuni na kujiunga na East Africa Television

ANGELINA JOLIE AONYESHA WIVU LIVE BAADA YA MUMEWE BRAD PITT KUWA KARIBU NA LUPITA NYONG'O WA KENYA

$
0
0
Katika kipindi cha hivi karibuni, mrembo wa Kenya Lupita Nyong’o ameipeperusha vyema bendera ya nchi yake kwa kuteka vichwa vingi vya habari akiwa anang’aaa katikati ya mastaa wa Hollywood baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya ’12 Years A Slave’ aliyocheza na Brad Pitt na mastaa wengine.

Kwa mujibu wa Jarida la National Inquirer, muigizaji wa kike mwenye mafanikio makubwa ambaye ni mpenzi wa Brad Pitt, Angelina Jolie ameonesha wivu kutokana na mgongano uliooneshwa na Brad Pitt kwa Lupita Nyong’o.

Brad Pitt alimwagia sifa hadharani mrembo huyo wa Kenya kwenye ‘Producers Guild Awards’, na kudai kuwa ni ‘special’ na kwamba wataona vitu vikubwa kutoka kwake.

“She’s very special, a very special young lady. We’re going to see great things from her.” Alisema Brad Pitt kuhusu Lupita Nyong’o.

Baada ya tukio hilo, Brad Pitt alisafiri hadi Australia kuungana na Angelina Jolie na watoto wao sita, ambapo chanzo kimoja kililiambia The Inquirer kuwa Angelina alionesha hali ya kukasirishwa na anachokiona kati ya Brad Pitt na Lupita.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa Brad amekuwa akizunguka sehemu mbalimbali duniani na kuonekana kama mtu ambaye hana mke na yuko huru.

“He wasn’t welcomed with open arms. She told him that he didn’t need to make his ‘crush’ on Lupita so obvious to the entire world. Angie is working her tail off, juggling directing duties and caring for their kids. Meanwhile, Brad is running around on the other side of the globe acting like a carefree bachelor.”

Inasemekana kwamba Brad alikuwa karibu sana na Lupita wakati wa Producers Guild Awards na kwamba wakati ambapo Leonardo Dicaprio alipombusu mashavuni Lupita Nyong’o, Brad Pit alimtania, “Hey, man stay away from my girl!”

Bado ukweli wa mambo haujajulikana kwa kuwa kuonesha wivu bila vitendo ni vigumu kuthibitisha!
Source:Times Fm

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA JOH MAKINI, NIKKI WA PILI NA G-NAKO-GERE

$
0
0
Sikiliza wimbo mpya toka kwa wakali wa Viburi Flow, Weusi. Nikki wa Pili amesema wimbo huu unaoitwa Gere umefanywa na Nahreel kwa asilimia 80 na Chizan Brain amemalizia asilimia 20.

GRAMMY:KENDRICK LAMAR AZUNGUMZIA USHINDI WA MACKLEMORE, ATOA USHAURI KWA WAANDAAJI

$
0
0
Baada yakushuhudia tukio la utoaji tuzo za Grammy mwaka huu lililofanyika January 26, ulimwengu wa muziki hasa wa hip hop ulipaza sauti nyingi na minong’ono kuhusu ushindi wa Maclemore & Ryan Lewis hasa kwenye kipengele cha ‘Best Rap Album’, huku mkali wa michano Kendrick Lamar akiondoka mikono mitupu licha ya kuwa katika vipengele saba.

Rapper huyo toka Compton, California ameelezea tukio hilo wakati akifanya mahojiano na mtandao wa XXL wa Marekeni, na kutoa mtazamo wake kuhusu kushindwa na Macklemore katika kipengele cha Best Rap Album.

Ameeleza kuwa kila kitu kinafanyika kwa sababu na kwamba Macklemore alistahili tuzo hiyo kwa kuwa aliihangaikia.

“It’s well deserved; he did what he did, man. He went out there and hustled and grinded. Everything happens for a reason; the universe comes back around, that’s how it go.”

Hata hivyo, Kendrick Lamar hakurithika na ushirikishwaji wa wana hip hop hasa katika kutumbuiza katika jukwaa hilo, ambapo mwaka huu walipata nafasi chache zaidi kuliko muziki mwingine.

Aliwashauri waandaaji wangeupa nafasi utamaduni wa hip hop kama walivyozipa nafasi aina nyingine za muziki, na kuongeza kuwa sio tuzo za Grammy pekee bali iwe hivyo katika tuzo nyingine zote kwa kuwa wao pia ni sehemu ya ulimwengu wa muziki.

Album ya Macklemore & Ryan Lewis ‘The Heist’ ilishinda tuzo ya Album bora ya Rap, na inasemekana kwamba ushindi wao umesababishwa na uungaji mkono wa mapenzi ya jinsia moja, na hivyo kupigiwa kura na watu wengi ambao wanaisapoti sera hiyo.
Source:Times Fm

AJALI YA GARI MAENEO YA KARIBU NA ZANTEL JIJINI DAR

$
0
0
Gari ndogo aina ya Toyota Corolla lenye nambari za Usajili T 379 AGL, likiwa ndani ya mtaro mara baada ya kupoteza mwelekeo wakati likiwa kwenye Mwendo mkali. Tukio hililimetokea mchana huu katika Barabara ya Migombani kama unaelekea Makao Makuu ya Kampuni ya simu za Mikononi ya Zantel. Ndani ya Gari hii kulikuwa na watu watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika kwa haraka kutokana hali iliyokuwa, watu wawili kati yao wameumia vibaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu. Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa, gari hiyo ilionekana ikiwa kwenye mwendo kasi hali iliyopelekea kushindwa maarifa kwa dereva wakati akipishana na Bajaj.
 Wasamalia wema wakihangaina namna ya kumuokoa mmoja wa majeruhi kwenye ajali hiyo, ambaye alikuwa amenasa kutokana na kubanwa na sehemu ya gari hilo. 
  

 Huu ndio mwonekano wa gari hiyo baada ya kuingia kwenye mtaro huo.
 Mdau akionyesha kibao cha namba cha Gari hiyo ambacho kiling'oka na kuingia mtaroni.
 Wasamalia wakiengelea kuhakikisha kama kuna mtu mwingine ndani ya Gari hiyo. 
 Majeruhi wakipakiwa kwenye Gari tayari kwa kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Gari iliyowapakia Majeruhi hao ikiondoka eneo la tukio. 
PICHA ZOTE NA MTAA KWA MTAA BLOG

BREAKING NEWS: ASKARI WATANO WAFARIKI DUNIA

$
0
0
Na: Halima Kiondo

Kwa taarifa zilizotufikia HIVI PUNDE. Askari WATANO wafariki papo hapo baada ya bus aina ya Mohamed Trans, kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Corola iliyokuwa ikitokea Dodoma mjini ambayo lilikuwa na sakari hao kisha kupoteza maisha.

Akizungumza na Radio One, Kamanda wa polisi Mkoani Dodoma, David Misime, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 usiku kuamkia leo katika kijiji cha Namtumba Mkoani Dodoma na abiria waliokuwemo kwenye Bus hilo hakuna aliyejeruhiwa.

"Hakuna aliyejeruhiwa kutoka kwenye Bus hili, lakini Dereva aliyekuwa anaendesha abiria hao anafahamika kwa jina la Juma Mohamed, amekimbia mpaka sasa haijafahamika yuko wapi, ameongeza kuwa gari ndogo aina ya Toyota Corola imeharibika vibaya na baadhi ya miili ya askari hao imeharibika. " Tumeipeleka miili hiyo hospital kwa ajili ya kuihifahi huku tukisubiri mipango ya mazishi," amesema David.

MAMA JOHARI AMFUMUA RAY NA KUMCHAMBUA KAMA KARANGA

$
0
0
Stori: Mayasa mariwata,Shani ramadhani.

Makubwa! Kwa mara kwanza mama mzazi wa mwigizaji mkongwe Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye hakupenda jina lichorwe gazetini ameibuka na kumfumua staa wa filamu ‘mbia’ wa mwanaye, Vincent Kigosi ‘Ray’, Risasi Jumamosi lina cha kushika.
Akizungumza na mapaparazi wetu katika mahojiano maalum nyumbani kwake, Ubungo External, Dar, wiki hii, mama Johari alifunguka kuwa hamjui wala hajawahi kumuona Ray ambaye ni mkurugenzi mwenza wa Johari. Ndiyo wamiliki wa kampuni ya kufyatua filamu ya RJ Productions.

Mama Johari ambaye pia ana makazi yake mkoani Shinyanga alisema alitua jijini Dar kwa matibabu ya presha.

Baada ya kumjulia hali, mapaparazi wetu walitaka kujua mama huyo anamzungumziaje Ray ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu na bintiye na kwamba ilishasemekana ni wapenzi.
Ndipo mama huyo alipokuja juu akisema huyo Ray mwenyewe hamjui na hajawahi kumtia machoni zaidi ya kumsikisikia tu kama wengine.

“Mimi simjui huyo Ray na wala sijawahi kutambulishwa wala kuonana naye, kwanza siishi hapa nitamuonea wapi, nimekuja zangu kutibiwa tu kutokana na matatizo yangu ya presha na kisukari.”

“Kwanza mwanangu hana muda wa kukaa na kumuumizia kichwa huyo Ray kwani yeye ni baba yake? 
“Hata siku moja (Johari) hawezi kuishi kwa kumtegemea yeye (Ray),” aliongeza mama huyo.

Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, mama huyo alisema kamwe hawezi kuumiza kichwa kuingilia mambo ya mwanaye, kwa kuhofia maradhi aliyonayo na kujitia matatizoni kwa mambo asiyoyajua undani wake.

Alisema anamshukuru Mungu kutokana na hali ya mwanaye aliyekuwa anaumwa kupata ahueni na kundelea na kazi zake.
Alipotafutwa Ray ili kuelezwa kile alichokisema mama Johari, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Source:Global Publishers

KIKONGWE AKAMATWA CHUMBANI KWA MTU AZANIWA KUWA NI MCHAWI-PICHA

$
0
0
Hili ni tukio lilitokea huko Bukoba ambalo linamhusisha Kikongwe mmoja ambaye jina lake bado halijapatikana kukutwa chumbani kwa mtu huku akiwa mtupu chumbani kwa mtu.
25Mpaka sasa bado haijajulikana kama ni Kigarura au pengine alipata matamani ya mwili akaona pengine chumba kile kingemfaa kumpatia msaada wa mambo yake.
28Bibi Kizee huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 70,ambapo amekamatwa alfajiri ya leo January 31 hata hivyo polisi wamefanikiwa kumnusuru na kifo baada ya kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi.
30Mashuhuda wa mwanzo wanadai walimkuta bibi huyo akitapatapa bila kujua nini la kufanya huku akiwa mtupu na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kilichotafsiriwa kwamba pengine bibi huyo anaweza kuwa mchawi,huku wengine wakisubiri taarifa ya polisi na wengine wakisema huenda bibi huyo alipatwa na matamanio ya kimwili.
Story na picha:bukobawadaublog.

VITA KATI YA MALECELA NA LOWASSA NI YA MUDA MREFU...SIRI YA UTAJIRI WA LOWASSA HII HAPA

$
0
0
Tokea enzi ya uhai wa Julius Kambarage Nyerere Faili la LOWASA kufahamika kuwa na utajiri wa kutosha linafahamika sana,na haijaanza leo kwa Lowasa kusemwa na kupewa shutuma kama hizo wala hazikuanza jana.

Zimeanza tokea kipindi Mwalimu Nyerere yuko hai,na hadi alishafikia hatua ya kuhoji utajiri wa Lowasa enz hizo akiwa kijana kama wa miaka 42 hivi,na kwa wakati huo miaka 42 huonekana kijana kweli kweli tofauti na sasa vijana katika umri kama huo washakuwa wazee tayari kutokana na ugumu wa maisha na frustuations zake.

Je,unafaham ni kwa nin MALECELA kwa kawaida tuh tokea hapo kale hampendi Edward Lowasa??

Hii vita haikuanza leo.,wanaccm hawa wawili na wenye ushawish kwenye chama hiko wameanza msuguano na malumbano tokea enzi hizo John Malecela akiwa Waziri Mkuu na Lowasa akiwa Waziri mwandamizi katika ofisi ya waziri ya waziri mkuu,kwa mantiki hiyo kwamba alikuwa chini ya malecela na kwa kumsaidia majukumu ya kazi ya siku zote za kuendesha serikali.

Enzi hizo wabunge wa jamhuri ya muungano wa tanzania walikuwa hawana magari ya kusafiria kama haya wanayokopeshwa kwa sasa,hali iliyokawa inawapa ugumu sana kuwatembelea wananchi wao majimboni hata wakati mwingine ugumu pia wa kuwahi bungeni kwa wakati kutokana na aina ya magari waliyokawa wanayatumia kipindi hiki kukosa stability ya kumudu safari na ukizingatia ubovu wa bara bara wa kipindi huko maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.

Hili suala lilikua linaumiza sana serikali kipindi hiko chiniya utawala na usimamiz wake wazir mkuu wa kipindi hicho ndug john malecela.

Kutokana na kuwaza na kuwazua likaja wazo la kupeleka idea kwa serikali ya watu wa japan ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kuwasaidia kihali na mali ili iweze kujikwamua katika tatizo hilo,

Mungu si Athumani,serikali ya japan enzi hizo wakakubali kuwaunganisha serikali ya tanzania na kiwanda cha toyota na kuwapa ushirikiano wa hali ya juu katika mazungumzo baina yao na kiwanda hicho hadi ikafikia tamati ya makubaliano kwamba serikali ya tanzania inaweza kukopeshwa magari hayo kisha wakawa wanalipa pole pole ili kusaidia kukizi na kuikubali changamoto hiyo.

Serikali baada ya kufanikisha plan hiyo ikaja kwa wabunge na kuwaeleza kwamba wanaweza kukopeshwa magari kwa mkopo,wabunge waliingia na wasi was kias flan na kusema wao wataweza kulipa vpi gharama hzo ukizingatia pesa waliyokawa wanachukua kipindi hiko isingetosha kulipa mkpo huo??

Serikali kupitia kw wazir mkuu malecele wakawaambia nyinyi chukuen tuh,sisi serikali tutajua tunawasaidia vipi,kwaiyo chukuen kwanza ili mukabiliane na changamoto ya usafiri kwanza.

Wabunge walikubali wazo lile na deal likafanyika,mambo yakafana kisawa sawa.

Sasa baada ya hapo mtu pekee ambae alikuwa anafuatilia mchakato mzima ni wazir wa nchi ofisi ya wazir mkuu enzi hizo akiwa ni edward lowasa,alikuwa anafuatilia suala hilo kwa ukaribu sana.


Wale wajapan walipolipwa chao,kumbe kuna makubaliano ambayo yakishafiikiwa baina yao na wazir mkuu malecela ya kumpatia kifuta jasho kwa kufanikisha deal ile kufanyika kwa ukamilifu wake.

Na yasemekana kifuta jasho hiko kilikuwa cha maana sana,cha maana sana sana,

Bahati mbaya sana wale wajapan walipofika ofcn kuleta kifuta jasho kile walianzia kwanza kwa ofisi ya wazir wa nchi ili wapate nafas ya kumuona wazir mkuu,sasa walipokutana na lowasa yasemekana akawauliza mnafuatia nin tena mheshimiwa ili hali deal ilishafanyika kikamilifu??kwan kuna tatizo??wale wajapan wakamwambia kwamba kuna kifuta jasho yapasa tumkabidh muheshimiwa wazir mkuu malecela.

Lowasa,,akastaajabu..!!akasema ,,"mnasema"???hicho kifuta jasho mnataka kumfikishia vipi mheshimiwa hamjui kuwa yule ni mtu mkubwa sana??kuna utaratibu wa kumfikishia kwa protokali ya serikali,sasa sikilizen bwana....

Hiyo pesa nipen mimi nitamfikishia,kwan kwa sasa hata hivyo yupo safarin hadi arudi,so nipeni mimi nitamkabidh,wale wajapan kwa kuwa wanafaham katika mchakato mzima wa ile deal lowasa nae alikuwa anaifuatilia kwa karibu hawakuwa na was was sana kumwachia amana kama ile.,,wakamwachia na kusign nae kisha wakageuza zao.

Kilichotokea hapo sasa mungu mwenyew ndie anaejua,

Lowasa akapiga kimya,kimya na yeye,yeye na kimyaa,muda ukawa unazid kwenda naskia ile pesa akaanza kuifanyia michakato ya kuizungusha na kuwekeza kwenye biashara ya real estate kwa haraka haraka na kuzikodisha kwa taasisi binafsi hata balozi mbali mbali za nchi mbali mbali,

Naskia ipo moja ambayo aliikodisha kwa ubaloz wa south afrika hapa hapa nchini,na hadi leo naskia iyo nyumba ni mali ya lowasa pamoja na vitu vingine vingi,kwa ufupi lowasa kawa DON tokea kitambo sana.

Sasa maskin mzee malecela akaona siku zinakwenda na kifuta jasho kutoka japan hakifiki,,akaamua kunyanyua simu na kuwavutia uzi jamaa na kuwauliza,ebwan vipi ile kitu yangu??mbona nyinyi wajapan wabaya kias hiko??ina maana baada ya deal kufanyika mnatupa jongoo na mti wake??

Wajapan wakasema Booossi,mbona kifuta jasho tulishaleta mda mrefu sana??tulimkabidh bwana Edward yule wazir wako wa nchi katka ofc yako na alisema atakukabidh kwan ulikuwa safarini..!!!

Malecela kikamshuka,kikampoa na asijue hata awajibu nini,

Ikabid sasa amwite edward na kumuuliza,wewe edward pesa yangu iko wapi??na nani alikuambia uichukue kwa niaba yangu??

Edward akasema Boooss,kwa kweli pesa nilichukua lakin sasa kwa kuwa ulikua safarini nikaona niiweke kwanza hadi urudi,,sasa kama unavyojua pesa tena mzee,kulitokea fursa za uwekezaji nikaamua kujikopesha ili niizungushe kisha nitakurejeshea lakin sasa mambo hayajaenda kama yalivyopangwa ndio kwa maana unaona kimya hiv sijakutafuta.

Sasa malecela presha ikampanda na kumshukaaa,atasema nini??na ile pesa ni chafu na ya deal ukizingatia yeye ni wazir mkuu??kumbuka nyerere yupo hai kipindi hicho na akifaham ishu kama hizo panakua hapatoshi..!!

Ikabid malecela ajikaze kisabun na kufa na tai yake shingoni huku lowasa akiendelea kupimp na kujitanua kwa raha zake.

Kwa kias kikubwa hapo ndipo LOWASA alipoanza kuwapiga GAPE LA KIPATO wenzake walio wengi,na kwa kias kikubwa wenyewe hao ambao wako ndan ya system wanalijua hilo.

Ndio kwa maana tokea zama hizo VITA baina ya LOWASA na MALECELA haiwez kuisha kamwe,kwan mambo waliyofanyiana wawili hao yanatishaa.

Hiyo ndiyo siasa ya bongo ilivyo,DO OR DIE.
Source:Jamii Forums

MARLAW:SINA MPANGO WA KUSHIRIKI KAMPENI ZA KISIASA TENA..ZIMENISHUSHA KIMUZIKI

$
0
0
Msanii aliyepata kuvuma sana kabla ya mwaka 2010 alimaarufu kwa jina la Marlaw, amejutia uamuzi wake wa kukipigia kampeni chama cha ccm kwani kimemporomosha kimuziki.

"Unajua mimi mwaka 2010 nimeburudisha ktk kampeni za ccm lakini nimeambulia kushuka kimuziki sijui ni siasa imehusika au la kwa sababu toka hapo nimetoa nyimbo nyingi lakini hazivumi tena, sasa sitaipigia ccm tena labda chama kingine si unajua vijana wako wapi mzee ha ha haaa si kwamba nimejitoa ccm hapana mi ni msanii naburudisha watu wote" 

Mwananchi lilipotaka kujua ni chama gani amekilenga kukipigia kampeni kwa malipo alisema bado muda wa kukiweka hadharani.

Wasanii someni alama za nyakati msije jikuta mko njia panda kimuziki huu ni mfumo wa vyama vyama vingi.

SLAA:TUNAHITAJI MWAKA MMOJA TU KUIGEUZA TANZANIA IWE NCHI YA VIWANDA

$
0
0
Akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Simiyu Dr Slaa amesema haoni sababu Tz kuwa hatuwezi hata kutengeneza kishikizo nakuviagiza nje.Amesema haoni sababu nchi hii kuwa na viwanda vingi vikiwepo vya magari.

Alisema wakipewa tu ridhaa wanaomba mwaka mmoja tu kuanza shughuli ya kuigeuza Tz kuwa nchi ya viwanda.

source ITV

What is your Take....Wataweza Kweli? ama ni Campaign tu

TIMES FM WAPIGWA FINE BAADA YA DIDA KUGEUZA KIPINDI KUWA CHA UGOMVI BINAFSI NA MSANII KURYA

$
0
0
Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) imekitaka kituo cha Radio Times FM ya Dar es salaam kuomba radhi mfululizo siku tatu na kumlipa tsh 500,000 msanii wa Taarab, Karya Temba baada ya mtangaji wake, Dida kupitia kipindi cha ‘Mitikisiko ya Pwani’ kumshambulia binafsi msanii huyo.

Kamati imesema mtangazaji Hadija Shaibu maarufu Dida aligeuza kipindi anachorusha redioni hapo kuwa cha ugomvi binafsi kati yake na mlalamikaji ambaye ni Karya na kwamba alichochea wasikilizaji kutuma meseji za kejeli kwa mlalamikaji jambo ambalo sio lengo la usajili wa kituo hicho. 
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo wakati akifafanua juu ya malalamiko ya msanii huyo akidai kipindi hicho kilimdhalilisha na kumharibia sifa kama mwanamuziki.
Jaji Mihayo alisema baada ya kamati kusikiliza pande hizo mbili, inaagiza redio hiyo kumwomba radhi mlalamikaji kupitia kipindi hicho katika vipindi vitatu mfululizo kuanzia Februari 5 na maudhui ya radhi hiyo yataridhiwa na MCT. 
Alisema kituo hicho, pia kimlipe mlalamikaji Sh 500,000 kama gharama za kutayarisha malalamiko na kimuandikie barua ya kumwomba radhi ndani ya wiki moja kuanzia jana na nakala kutumwa MCT. Katika shauri hilo namba 28, 2013, Temba analalamika kushambuliwa, kukashifiwa na hata kubaguliwa na mtangazaji huyo katika kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani anachokirusha redioni hapo.
Vile vile Kamati hiyo imesema redio hiyo ilikiuka maadili ya utangazaji kwa kurusha kipindi kinachoshutumu watu kwa kutumia kabila lao na kilikuwa na maudhui ya udhalilishaji wa kijinsia, kinyume cha maadili na kanuni bora za uanahabari

MAN UTD KAMA KAWAIDA YAO, WALALA 2-1 KWA STOKE CITY

$
0
0
Mmmmh Jamani mie sio mshabiki wa Mpira kiivyo ila navyoona na ninavyosikia kila kona Man u jumba limewaangukia mwaka huu kila siku wakicheza lazima wapigwe 2 something ....mmmh wanahitaji maombi tena ya Mwakasege.........Au unaonajeee? tuwakesheeee

VIONGOZI WAMETAFUNA FEDHA ZA BANK YA DUNIA, ASEMA DK SLAA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amedai kuwa  baadhi ya viongozi wa Serikali wamegawana na kutafuna fedha zilitolewa na Benki ya Dunia, ili kugharimia miradi ya kuchimba visima 10  vya maji katika kila wilaya nchini.

Dk Slaa alitoa tuhuma hizo juzi jioni, alipokuwa akihutibia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo, mjini  Musoma.

Kiongozi huyo wa Chadema yuko katika Operesheni ya M4C Pamoja Daima.

Alisema kitendo hicho kinafanywa wakati Watanzania na hasa wanawake wakikabiliwa tatizo kubwa la kukosa huduma za maji kiasi cha kushinda hata kwa siku tatu bila kuoga.

“Ngoja niwaambie hivi sasa Serikali imekuwa ikiweka vikwazo vingi katika utekelezaji wa mradi wa maji kupitia Benki ya Dunia, ukweli ni kwamba fedha zote zilizotolewa zimeliwa sasa wameanza kuhaha wasijue cha kufanya,” alisema na kuongeza.

Wakati huohuo, Geofrey Nyang’oro na Raymond Kaminyonge wanaripoti kutoka Iringa kuwa viongozi wa Chadema Taifa wakiongozwa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wamekamatwa na polisi mkoani hapa na kushikiliwa kwa muda wakituhumiwa kuzidisha muda katika mikutano waliyoifanya katika Jimbo la Kalenga wilayani hapa juzi.

Mbowe alikuwa ameambatana na viongozi wa chama hicho juzi, walifanya mikutano mbalimbali mkoani hapa, ambapo katika Jimbo la Kalenga walifanya mikutano katika Vijiji vya Wassa,Nzihi, Kidamali na kisha kushindwa kufanya mkutano mmoja uliotakiwa kufanyika katika Kijiji cha Mgama kwa madai muda ulikuwa umekishwa.

Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wawili wa Chadema, Mbunge Peter Msigwa na Halima Mdee walikamatwa saa tatu asubuhi wakati mwenyekiti huyo alipokuwa akijiaandaa kuondoka mkoani humo kwenda mkoani Pwani kuendelea na mikutano ya Operesheni M4C pamoja Daima inayoendelea kwa sasa kote nchini. Hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo kukamatwa na kuhojiwa  ambapo mara ya kwanza ilikuwa Agosti 25 mwaka jana.
Source:Mwananchi

SIKILIZA KIONJO CHA WIMBO MPYA WA BARNABA BOY-JASHO LA MNYONGE

$
0
0
Barnaba ni Mwanamuziki ambae mimi pekee namkubali kuliko wanamuziki wote wa bongo flava ana kipaji kikubwa sana cha kuimba na kupiga vyombo....Sikiliza kionjo cha wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa siku za karibuni:

NAPANDAGA GARI YA HUYU DADA MARA NYINGI, ILA NGUO ANAZOVAAGA HUNIFANYA NIMUWAZE YEYE SIKU NZIMA

$
0
0
Tunaishi wote mtaani hivyo mara nyingi tu hunipaga lift nikiwa labda natoka kazini au nikiwa naelekea kazini, wakati mwingine akiwa mjini hunipigia simu ili turudi wote mtaani ila niko na wakati mgumu sana huyu dada mrembo sana yani siwezi kuelezea hapa mkanielewa , nguo anazovaaga akiwa anaendesha ni za hatari sana yani hunifanya nimuwaze yeye tu siku nzima, sijui kwakweli nifanyaje wakati mwengine natamani hata nipenyeze mkono hata ni mguse tu lakini naogopa labda msaada wa lift unaweza kuishia hapo kama unavyojua usafiri ni mgumu sana hapa mjini. Naombeni ushauri wadau..!!

MZEE MALECELA NA PAUL MAKONDA WAOMBE RADHI KWA VIONGOZI WA DINI NA KWA LOWASSA

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARITAREHE 1 FEBRUARI 2014
MZEE MALECELA NA PAUL MAKONDA WAOMBE RADHI KWA VIONGOZI WA DINI

0.1 Kitendo alichokifanya hivi karibuni Ndugu Paul Makonda Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji pale alipoongea na vyombo vya Habari pamoja na mambo mengi aliyoyaongea kubwa zaidi ni alipotamka wazi kwa kuwatuhumu baadhi ya Viongozi wa Dini kwa kutoa maneno ya kejeri na dharau dhidi yao kuwa “MASHEIKH NA MAASKOFU WAKIWEMO NA VIJANA WANAOTAKA FEDHA ZA BURE WAENDE KWA EDWARD LOWASA” kitendo ambacho hakuwatendea haki wala adabu Viongozi hawa wa Dini.


Kitendo hicho cha kuwakejeri na kuwadhalilisha ni utovu wa Nidhamu wa hali ya juu sana, kwani kauli aliyoitoa kila Muumini ilimshitua sana, kwani ni kauli haikupaswa kutolewa na Kiongozi wa Vijana aliyekuwa katika nafasi Muhimu ya Uongozi wa Jumuiya Kitaifa, kwani kauli yake hiyo yenye ukakasi wa hali ya juu sana imempa kichefuchefu kila mmoja anaewaheshimu Viongozi wa Dini, kwani Viongozi wa Dini wanaheshima zao binafsi na kuheshimika Duniani kote na mpaka Serikali huwaomba Viongozi wa Dini kushiriki pamoja kutatua na kushauriana katika maswala mbalimbali yanayoizunguka jamii.

Kauli hiyo ni nzito sana aliyoitoa Ndugu Paul Makonda sio ya kuipuuza hata kidogo na kuicha hivi hivi nina muomba kwa Heshima na taadhima Mwenyekiti wa Vijana wa Taifa awathibitishie Watanzania kuwa kauli aliyoitoa Ndugu Paul Makonda ni ya Umoja wa Vijana au ni yake binafsi. Kwani mimi binafsi nimekuwa katika Umoja wa Vijana kama Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Shinyanga mstaafu na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa lakini pia Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wa Vijana Taifa, nafahamu kauli au matamko mazito kama yaliyotolewa na Ndugu Paul Makonda hutolewa na Mkutano mkuu wa Taifa, Mkutano wa Baraza Kuu Taifa na hata kamati ya Utekelezaji Taifa.Mimi siamini kama hiyo ni Kauli ya Umoja wa Vijana kwa kadri ninavyofahamu utaratibu ndani ya Jumuiya na Chama kwa ujumla, sasa tunajiuliza huyu kijana kauli hizi nzito nzito ambazo hazilingani na umri wake na wala hadhi ya kiuongozi aliyonayo anazitowa wapi huenda tunaamini kuna kundi au genge la mahafidhina liko nyuma yake lililoamua kumtumia aidha kwa kujua au kwa kutokujua.

Jambo jingine muhimu alitutuhumu pia sisi yani mimi Khamis Mgeja, Mzee Mgana Msindai na Ndugu John Guninita kuwa alidai t--------- na Ndugu Edward Lowasa, tuhuma hizi si za kweli hata kidogo napenda Watanzania wafahamu tuhuma zote mbali mbali ambazo kijana huyu amekuwa akitushutumu si za kweli na ni za kipuuzi ninaiomba jamii kumpuuza kwani Ndugu Makonda bado mchanga kisiasa anatafuta umaarufu kwa kasi kwa kutumia migongo yetu sisi wakongwe kisiasa, kwani sisi aliotutuhumu atambue sisi ni wakongwe na ni Magwiji katika siasa za kiungwana hapa Tanzania, tunauwezo wetu binafsi wa kufikiri na kuamua kile tunachokiamini kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla, kwa ujumla tunataka Ndugu Paul Makonda na washirika wake waache kelele ambazo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara hii ni dalili ya kuelemewa ndio maana hawaishi kumsemasema na kumkejeri Ndugu Edward Lowasa wakati ambapo jamii inamuona kuwa ni mtu wa msaada mkubwa katika kuchagiza maendeleo kwa kushirikiana na jamii. Kijana Makonda atambue sisi tumewekeza jasho jingi katika chama hiki na kamwe hatutokubali kudhalilishwa na kijana mchanga wa kisiasa kama huyu, pia kama ni kuwekeza jasho sisi tuna debe ishirini yeye hata robo hajafikisha katika medani za kisiasa kwa hivyo anafanya maajabu ya kisiasa ni maajabu ya panya kufukuza paka na anacheza ngoma asiyoijuwa.Pia jamii inamuona Ndugu Edward Lowasa ni mtu muungwana, mwenye uwezo mkubwa wa kiutendaji, mwenye ushauri na ushawishi mkubwa katika machangizo ya maendeleo, sifa kubwa nyingine ya ziada ni uvumilivu na hasa kuwavumilia watu wenye kumrushia madongo kama Paul Makonda na genge lao la mahifidhina.

Kuhusu kauli aliyoitamka Ndugu Makonda ya kwamba Ndugu Edward Lowasa hawezi kuwa Rais kauli hii imetoa picha ya kuyajuwa yaliyofichika katika fikra za kundi hili la wahifidhina lakini pia watambue maamuzi yote hufanywa na Vikao halali vya chama na jumuiya zake, na wakati ukifika vikao vitaamua na si Makonda na marafiki zake.

0.2 MZEE MALECELA KUPONGEZA KAULI ZA KASHFA DHIHAKA NA KEJERI DHIDI YA VIONGOZI WA DINI Kufutia tukio la hivi karibuni la kijana Paul Makonda kutoa maneno ya kashfa kejeri na dhihaka dhidi ya viongozi wa Dini, baadhi ya wanasiasa na vijana maaajabu makubwa kutokana na kauli hizo za Makonda tumemshangaa Mzee Malecela kuibuka na kuunga mkono na kumpongeza kijana huyu mtovu wa nidhamu.

Tulitegemea kila Mtanzania kwamba baada ya kauli hizo Mzee Malecela angeibuka na kumuongoza njia sahihi na kumpa ushauri kijana huyu aliyepotea kimaadili wa kwenda kuwaomba radhi na kuwaangukia viongozi wa Dini, ndugu Edward Lowasa, Ndugu Khamis Mgeja, Ndugu Mgana Msindai, Ndugu John Guninita ikiwemo na vijana kwa ujumla.Maajabu makubwa jambo ambalo Watanzania hawakutegemea jinsi wanavyomfahamu Mzee Samwel Malecela na heshima yake, tulitaraji kuwa Mzee angemkemea kijana huyu mtovu wa Nidhamu badala yake anampongeza na kumuunga mkono na kuwataka Watanzania wamuunge mkono kwa kauli zake za utovu wa Nidhamu ambazo hazina tija kwa Chama na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, pia katika maajabu mengine Mzee Malecela alimshambulia mwanachama mwenzake Ndugu Edward Lowasa kwa kumtuhumu kwa tuhuma nyingi mbalimbali ambazo hana ushahidi nazo.Mzee Malecela amesahau huko nyuma yeye alishawahi kutuhumiwa kuwa alipewa fedha kutoka nchi za uarabuni na mpaka kubadilisha dini na kuitwa jina la JUMANNE ili aungwe mkono kupewa nguvu za kugombea Urais.

Kuhusu uchu wa Urais anaomtuhumu Ndugu Lowasa amesahau yeye ndiye ana uchu mkubwa sana wa Madaraka alikuwa akiomba nafasi za ndani ya Chama haswa kwa kiti cha Urais kwa awamu mbalimbali akaonekana hafai na hatoshi na mpaka jina lake likawa halipitishwi na chama baada ya kumgundua ni dhaifu na anakasoro kubwa za kimaadili na mpaka ikapelekea Baba wa Taifa akachoka kumvumilia na hatimae alimtungia kitabu “UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA” hii ni kuonyesha kuwa Mzee Malecela alikuwa sugu wa matatizo yaliyokuwa yakikiuka maadili.Jambo jingine alilokuwa nalo la uchu wa madaraka Mzee Malecela ni pale alipong’ang’ania kiti chake cha ubunge bila kujali umri wake na wananchi wa jimbo la Mtera ilifika mahala walimchoka baada ya kugundua anasinzia Bungeni na kwenye jimbo laketulishuhudia Kibajaji kikiliangusha Katapila maana yake aliangushwa ubunge na mtoto mdogo Mhe Livingstone Lusinde.Jambo jingine Mzee Malecela ameshindwa kutambua wanaokivuruga chama ni wale wanaozungumza nje ya vikao halali vya chama na jumuiya zake na kuyageuza kuwa ndio msimamo wa chama au jumuiya. 

Kwa hivyo Mzee Malecela kuendelea kutushambulia hatutendei haki kwani hakuna shughuli yoyote ya chama iliyokwama kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa kwa sababu yetu sisi.NINAPENDA KUTOA USHAURI KWA MZEE MALECELA, MAKONDA NA WATANZANIA WENZANGU KWA UJUMLA, Tanzania kama taifa tumefika pabaya kwani kila mmoja amebaki kuwa mlalamikaji na kutuhumiana pasipokuwa na ushahidi hili jambo ni hatari kwa mustakbali wa nchi kwani hivi sasa baadhi ya watu wanamgeuza Ndugu Edward Lowasa kuwa ni agenda ya kitaifa huku wakiacha mambo muhimu ya nchi na maisha ya watanzania.kwani tulitegemea wazee wetu kama kina Mzee Malecela watushauri vipi taifa linaweza kukabiliana na changamoto zilizopo hivi sasa kwa mfano deni la taifa, mchakato wa Katiba Mpya, matatizo ya umasikini, tatizo la ajira kwa vijana, hombwe kubwa kuwahi kutokea baina walionacho na wasionacho, mauaji yanayotokea sasa maeneo mbalimbali kati ya wakulima na wafugaji ikiwemo kuchomeana nyumba, mauaji ya kikatili kule Tarime na maeneo mbalimbali nchini, ajali mbali mbali za barabarani zinazouwa nguvu kazi ya Taifa, tatizo kubwa la rushwa, uporaji wa rasilimali za Taifa na ujangili wa kutisha, Tanzania kutumika kama korido la kupitishia madawa ya kulevya na binadamu, oparasheni tokomeza, wananchi kujichukulia sheria mkononi, ubadhilifu wa mali za umma haswa ukizingatia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na taarifa za kamati mbalimbali za bunge, jambo jingine kubwa lilipo kwa sasa ni kuhusu rasilimali ya gesi iliyovumbuliwa kwa wingi nchini wakati taifa lipo katika mchakato wa kutunga sera na sheria ya gesi na mafuta.

Mzee Malecela na wenzake hayo yaliyotajwa hapo juu ndio mambo muhimu yanayogusa nchi na sio mtu Lowasa Lowasa Lowasa tulitegemea atushauri Tanzania kama taifa tufanye nini Watanzania kwa kushirikiana na Serikali yetu kwani matatizo hayo yanahitaji ushirikishwaji baina ya wananchi na Serikali yao, Watanzania wangeyapata hayo kupitia uzoefu wake kama alivyowahi kuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM kuliko maajabu ya kuonyesha Flana yenye maneno ya “FRIENDS OF LOWASA” kuwa kama ndio tatizo la Taifa.

Mzee Malecela kuwaonyesha Watanzania Flana ya Lowasa ndio tatizo la taifa hii inaonyesha wazi Mzee amechoka na amefilisika kifikra na anazeeka vibaya ninapenda nimpe ushauri wa bure Mzee wangu atulie alinde heshima yake.Pia napenda nitoe ushauri kwa Mzee Malecela, Paul Makonda pamoja na washirika wao wasome alama za nyakati na waangalie mahitaji ya siasa kwa sasa na waone Watanzania wanamuhitaji Kiongozi wa namna gani wa Tanzania ya kesho, ninawaomba wakubali yaishe wasije kupinganaTanzania na nguvu ya umma na upepo wa kisisa kwa sasa na pia watambue mpaji ni MUNGU alitakalo MUNGU hakuna mwanadamu atakaelizuia. 
NAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA UJENZI WA TAIFA

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

TAARIFA HII IMETOLEWA NA NDG KHAMIS MGEJA

…………………………………………….

01/02/2014

FORBES MAGAZINE REVEALS MO AND MAKAMBA JR AMONG 10 POWERFUL MEN IN AFRICA 2014.

$
0
0
Mohammed Dewji, Tanzania, Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania Limited
Dewji is the Group Chief Executive Officer of Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) and at 39 is the youngest member of the Forbes’ Africa’s 50 Richest list with an estimated net worth of USD $500 million.
The MeTL Group began as a family business, a small trading company which Mohammed transformed into one of the largest industrial conglomerates in East Africa, with interests ranging from real estate, agriculture, finance, distribution and manufacturing.
The company employs more than 24,000 people across Tanzania and according to Dewji, generates annual revenues of USD$1.3 billion.
Dewji has been a Member of Parliament in the National Assembly of Tanzania since 2005. Dewji graduated from Georgetown University with a degree in International Business and Finance with a minor in Theology.
January Makamba Tanzania, Deputy Minister of Communication, Science & Technology and Member of Parliament
Makamba is one of Tanzania‘s rising stars in government. He is currently the Deputy Minister of Communication, Science and Technology and is rumored to run for President in 2015.
Makamba is a Member of Parliament for Bumbuli constituency in the National Assembly of Tanzania. Before running for the Bumbuli parliamentary seat, Makamba was aide to Tanzanian President Jakaya Kikwete for 5 years.
Named Young Global Leader class of 2012 by the World Economic Forum, Makamba comes from a political family; his father, Yusuf Makamba was Secretary General of the ruling CCM party under Julius Nyerere.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images