Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mgombea Urais 2015 Edward Lowassa Amweka Kikwete Kitanzini

$
0
0
Ndivyo alivyosema na bila shaka ndivyo anavyoamini Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, lakini kauli ambazo amekuwa akizitoa tangu kuanza kwa mbio za urais zinamuweka katika hali ngumu Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Lowassa alirudia moja ya kauli hizo juzi alipokuwa Dar es Salaam kuendelea na kazi ya kutafuta wadhamini aliposisitiza kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa “Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje,” akisisitiza kuwa yeye ndiye anayeweza kuleta mabadiliko hayo.

Mbunge huyo wa Monduli ametoa kauli hizo kabla ya vikao vya juu vya kufanya uamuzi wa mgombea urais wa CCM vitakavyoongozwa na Rais Kikwete. Vikao hivyo vitaanza Julai 8.

Tayari makada 42 wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho kikongwe kugombea urais na kutoa ahadi mbalimbali, lakini Lowassa, ambaye amekuwa akipata wadhamini wengi kuliko makada wengine, ndiye ambaye ametoa kauli zinazomuweka Kikwete kwenye hali ngumu.

Tangu alipoanza kuzungumzia urais kwenye kikao cha kwanza na wahariri Mei 25 mjini Dodoma, Lowassa amekuwa akitoa kauli kadhaa katika mikoa mbalimbali nchini, akianzia Arusha ambako alitangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM na baadaye kwenye harakati za kusaka wadhamini.

Asiyenipenda ahame CCM

Akijibu swali kwamba anaweza kuhama chama iwapo jina lake litakatwa kwenye mchakato wa ndani ya CCM, Lowassa alieleza jinsi alivyokitumikia chama na imani yake.

“Sina mpango wa kuhama chama changu, sina Plan B. Mimi ni Plan A tu. Tangu nimalize chuo kikuu mwaka 1977, nimekuwa mwana-CCM. Sijafanya kazi nje ya CCM ukiondoa miaka ambayo nilikuwa vitani Uganda na nilipohamishiwa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha. Maisha yangu yote ni CCM,” alisema Lowassa.

“Kama kuna mtu ambaye hanitaki ndani ya CCM, yeye ndiyo ahame, siyo mimi.”

Safari hii JK ataniunga mkono

Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mei 30 wakati akitiania, Lowassa alielezea tukio la kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM kuwania urais mwaka 1995 wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Kikwete, ambaye pia alichukua fomu hizo.

“Wakati ule sote tulikuwa wanasiasa vijana. Pamoja tulikwenda kuchukua fomu na baadaye kwa pamoja tukazungumza na waandishi wa habari. Tulileta hamasa kubwa pale tulipofanya jambo ambalo halikuzoeleka kwa Watanzania kwa kutangaza kwamba yeyote atakayepita kati yetu, mwenzake ambaye hangefanikiwa angemuunga mkono mwingine,” alisema Lowassa na kuongeza kuwa wakati ule alimuunga mkono Kikwete...“Natarajia safari hii, Kikwete ataniunga mkono.”

Mwaka huo, Kikwete alishindwa na Benjamin Mkapa ambaye baadaye akawa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu. Mwaka 2005, Lowassa hakuchukua fomu na badala yake alimuunga mkono Kikwete aliyeshinda na mbunge huyo wa Monduli kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Pengine kauli hiyo ya Lowassa kutaka amuunge mkono ndiyo iliyosababisha Rais Kikwete kutupiwa swali na mwanadiplomasia wa Marekani Juni 9 wakati akizungumza na Jumuiya ya Watanzania waishio Uholanzi katika hoteli ya Chawnie Plaza. Rais Kikwete alijibu kuwa hana mtu wake na kwamba wote ni wagombea wake, na kama ni suala la kuchagua, ana kura moja tu kama wajumbe wengine.

Mabadiliko aliyotabiri Nyerere

Akiwa mjini Iringa Juni 20, Lowassa alitumia kauli hiyo ya Nyerere kuhusu mabadiliko ndani na nje ya CCM.

“Baba wa Taifa alisema kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM,” alisema Lowassa.

“Huu ni wakati wa mabadiliko. CCM ikijipanga inaweza kuleta mabadiliko na mtu wa kuleta mabadiliko hayo ni mimi,” alisema Lowassa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Pia aliwaambia wahariri mjini Dodoma kuwa hawezi kuondoka CCM na kama kuna watu wanadhani hivyo, waondoke wao. Alikuwa akijibu swali kama atakuwa tayari kuondoka CCM iwapo ataenguliwa kwenye mchujo wa wagombea urais.

Hakuna wa kumkata jina

Juni 22, akizungumza mara baada ya kuwasili mkoani Ruvuma alisema hatarajii jina lake kukatwa katika vikao vya CCM vitakavyoketi kumteua mwanasiasa atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais.

“Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? Anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu,” alisema Lowassa.

Anayemtuhumu kwa ufisadi amtaje

Siku ya kuchukua fomu Juni 5, Lowassa alijibu kwa kifupi maswali ya wanahabari na kusema kama kuna mtu ana ushahidi wa tuhuma za ufisadi dhidi yake amtaje jina.

Mpambano wa Mengi na Manji Wapamba Moto...Manji Atangaza Kuwa Atajiuzulu yanga iwapo Aliyosema Mengi yatakuwa ni Kweli..Ataka Mdahalo wa Yeye na Mengi

$
0
0
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amesema atajiuzulu wadhifa wa uenyekiti iwapo itabainika kuwa kweli yeye ni fisadi, mwizi na muongo kama ambavyo Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amekuwa akisukuma mashambulizi dhidi yake.

Manji amezungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Yanga, jana na kueleza hayo huku akisisitiza kumtaka Mengi ajitokeze na wakutane kwa ajili ya kufanya mdahalo wa wazi ambao utadhibitisha kuhusiana na tuhuma hizo.

Alisema kuendelea kuiongoza Yanga wakati imethibitika ni fisadi na mwizi, ni utovu wa nidhamu na wanachama wa klabu hiyo watamtilia shaka.

Bilionea huyo aliyasema hayo jana Jumapili, mbele ya wanachama wa klabu hiyo kwenye mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Yanga, makutano ya Mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar.

Manji alifunguka kuwa Mengi amekuwa akimsakama kwa muda mrefu na sasa amesema amechoka.

Manji anadai kilichomchefua zaidi ni habari iliyotoka kwenye Gazeti la Nipashe kuwa kampuni yake ya Farm Equip Tanzania and Quality Garage, ijulikanayo kama QG Engineering ilishindwa kulipa kiasi cha bilioni 9.055 serikalini.

Manji amekanusha taarifa hiyo na kuomba Julai 3, mwaka huu kukutana na mmiliki wa gazeti hilo, Mengi kwenye mdahalo ‘live’ na kila upande uje na ushahidi wa kutosha kisha Watanzania wapige kura ili muongo na mkweli ajulikane kuliko kuchafuliwa jina.

“Iwapo itabainika kweli mimi ni fisadi, muongo na mwizi, niko tayari kuachi ngazi ya uenyekiti wa Yanga na sitagombea cheo chochote hapa, maana klabu itakuwa inaongozwa na mtu asiye na vigezo sitahiki vya kuwa kiongozi,” alisema Manji.

"Watu wanapaswa kujiuliza, mimi ni fisadi ninayejulikana na vyombo vya habari vya IPP tu? Wengine hawaoni hilo? Je, kwa nini IPP pekee ndiyo waone mimi ni fisadi? hapo watu wajiulize," alisema Manji.

Ommy Dimpoz Aambulia Matusi Kutoka Kwa Mashabiki Wake Baada ya Kupost Picha ya Ali Kiba Kwenye Page yake ya Instagram

$
0
0
Mwimbaji Ommy Dimpoz wa bongofleva yamemfika hapaaa na ikapelekea aamue tu kutoa ya moyoni mwake baada ya kupost picha ya tangazo la video mpya ya Ali Kiba kuonyeshwa TRACE TV June 28 2015 ambapo aliambulia Kutukanwa na Mashabik kwa kile kinachoonekana amemsaliti Rafiki yake Diamond ambae ana ugomvi wa chini chini na Ali Kiba...

Ali Kiba Aliifuta hiyo post na Kuandika Haya:

Sasa ndugu zangu tukipost kuhusu Wasanii wenzetu mnatukana, tukikaa kimya tuna roho mbaya…. tufanyeje?? matusi tu hamjali kama watu wana wazazi unamtukania mzazi mwingine kafa, lakini kwa taarifa yenu hainiumi ng’o‘ – Ommy Dimpoz

Msanii wa Afrika aliyegoma kwenda kwenye tuzo za BET kwa makusudi Awachana Laivu BET Kwa Kuwabagua Wasanii wa Africa kwa Kuwapa Tuzo Backstage

$
0
0
Kitendo cha BET ambayo ni Television kubwa ya Marekani kwenye ulimwengu wa burudani kuwapa Wasanii wa Afrika tuzo zao kwa time tofauti na tuzo wanazoshinda wasanii wakubwa wa Marekani kama Beyonce na Chris Brown kiliwahi kulalamikiwa na wengi akiwemo Ommy Dimpoz.

Hata Davido aliposhinda mwaka jana kwenye sehemu ya Interview Diamond alieleza kwamba tuzo za wasanii wa Afrika huwa hazitolewi pamoja na zile za kina Beyonce, wasanii kwenye kipengele cha Afrika waliitwa asubuhi na mapema wakati ukumbi ukiwa mtupu bila watu ndio mshindi akakabidhiwa tuzo alafu badae jioni ndio kina Beyonce wakakabidhiwa kwenye event yenyewe lakini ukitazama kwenye TV huwezi kugundua sababu wanaunganisha kijanja.

fuse 20Baada ya hayo yote, mwimbaji staa Mwafrika ambaye makazi yake ni Uingereza FUSE ODG ametangaza wazi kwamba sababu za yeye kutokwenda kwenye tuzo hizo mwaka huu ni kwa sababu tuzo hizo hazitolewi sawa na za kina Beyonce.

Fuse ambaye alikua anawania tuzo kwenye tuzo hizi za BET mwaka huu amesema mambo ya kupeana tuzo backstage inaonyesha kabisa BET hawawaheshimu wasanii wa Afrika wanavyojituma kwenye kazi zao.

Picha 4 za ajali ya gari waliyoipata Wachezaji Nizar Khalfan na Shaban Kado

$
0
0
Ajali imetokea Bahi Dodoma na kwenye gari miongoni mwa waliokuwemo ni pamoja na golikipa Shaban Kado na mchezaji Nizar Khalfan wa Mwadui FC na chanzo ni airi la nyuma kuchomoka.

 Kado amesema hakuna yeyote aliyepoteza maisha kaisipokuwa majeraha waliyoyapata akiwemo Shaban Kado ambaye ameumia pia mkono wake wa kulia ambapo walikua watu wanne ndani ya gari.

TID Afunguka: Natumia Dawa ya Kulevya Aina ya Bangi ila si 'UNGA' Cocaine Kama Watu Wanavyonishutumu

$
0
0
Kwa mara ya kwanza, ‘mnyama’ katika anga la muziki wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘Top In Dar’ (TID) amekiri kutumia mihadarati aina ya bangi huku akijiapiza kuwa hajawahi kutumia madawa mengine ya kulevya ‘unga’ ikiwemo cocaine kama ambavyo amekuwa akinyoshewa vidole na baadhi ya watu.

Akizungumza na Gazeti  la  Ijumaa katika mahojiano maalum wikiendi iliyopita, TID ambaye ni mmiliki wa Top Band alifunguka kuwa miongoni mwa mambo yanayomkosesha raha na amani ya moyo, ni pamoja na kuhukumiwa kujihusisha na matumizi ya unga na wengine kwenda mbele kwa kusema hata kushuka kwake kisanii kumechangiwa na ishu hiyo.

Staa huyo wa Ngoma ya Kiuno alisema kuwa, wakati mwingine watu wanamsakama hadi mama yake mzazi wakimtaka amkanye mwanaye kujiepusha na maisha ya ‘kubwia unga’ jambo ambalo linampa wakati mgumu na kujiona kuonewa katika jamii.

Kuhusu kushuka kimuziki, TID alisema miongoni mwa sababu zilizosababisha kuporomoka katika anga la muziki ni kile alichokiita ‘hujuma’ kutoka kwa baadhi ya wadau wakubwa wa muziki (majina yapo), kwa kushindwa kumpa fursa za kimuziki zikiwemo promosheni na mialiko ya shoo kwa kuwa wana vinyongo na fitina dhidi yake.

Kaka, naonewa kabisa nikihusishwa natumia madawa ya kulevya, wanamsumbua mama eti akae na mimi anionye.

“Jamani situmii madawa ya kulevya kama cocaine, ila kwa upande wa bangi ni sawa nakubali kuwa navuta.

“Lakini pia, kuvuta kwangu bangi siyo sababu ya mimi kushuka kisanii, zipo sababu zingine kabisa kama kuhujumiwa na wadau wakubwa wa soko la muziki kutokana na mabifu yanayotokana na sababu binafsi.

“Hivi kweli mtu anayetumia madawa ya kulevya kama cocaine, anaweza kumudu maisha kama kununua nyumba? Kununua magari? Hata kuendelea kuimba kweli? Siyo sawa jamani,” alisema TID.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Tarehe 29 Juni 2015

$
0
0





















Habari Zilizopo  Katika  Magazeti  Ya  Leo  Jumatatu  Ya  Tarehe  29  Juni 2015

You Won’t Believe What will Happen when OBAMA Visits Kenya. Just Read This.

$
0
0
It’s official that US President Barrack Obama will be on his first official visit to Kenya this July and many Kenyans are excited about this but even as most of us celebrate the good news that the world’s most powerful leader is coming to Kenya, his 8 hour visit will bring business to a stand-still in our beautiful country.

Below is what will happen during his short stay in Kenya.

-The US Navy will be in charge of Kenya’s water bodies.

-The USA Secret Service, CIA, FBI will take over the role of Kenya’s VIP protection unit (RECCE Coy).

-Jomo Kenyatta International Airport will be closed for almost 2 hours to only accommodate Air-force One. No Kenyan Airport Staff will be allowed to get inside or near the airport’s VIP lounge. The USA aviation authority and pentagon will take charge of that section.

- Our airspace will be directly controlled and monitored from Washington DC and with US radars based in North Africa and in Indian Ocean.

-The USA Abraham Lincoln Naval War Ship and Naval Carrier will dock at the Mombasa Coast of Indian Ocean and it’s expected to be a launch pad for the USA B52 Bombers. The US War Ship manufactured for instant electricity supply will be stationed in Indian Ocean to add to electricity supply to the US installments and CIA operations command centers in Kenya.

-All the major in roads between JKIA, State House and Gigiri will be closed and controlled by satellite from Texas, US, and their operations will be controlled by the USA security apparatus in Nairobi.

-No commercial ship will be allowed to dock in Mombasa for 8 hours.

- President Obama’s motorcade will consist of over 100 Hi-Tech Armored vehicles which can repulse and control a B10 or any other bomb device.

- The Presidential guard of Kenya will not be allowed near Uhuru Kenyatta apart from his ADC and a secretary.

-The US NASA will ensure that the world above the earth which is controlled by USA will control Kenya’s space and the entire E. Africa space using NASA satellites.

-The NATO (North Atlantic Treaty Organization) will take charge of Radars and flight control in all African countries for 8 hours.


Wema Sepetu will make a great member of parliament – Colonel Mustafa

$
0
0
Rapper wa nchini Kenya, Colonel Mustafa amemmwagia sifa kibao Wema Sepetu kuwa atakuwa mbunge mzuri kama akishinda nafasi ya ubunge wa viti maalum anaouwania mkoani Singida mwaka huu.

Kupitia Instagram, rapper huyo ameandika:

“It is my distinct honor and pleasure to give my unqualified support to my long-time friend Wema Sepetu in her race for the Tanzanian parliamentary bid,” ameandika Mustafa.

“Wema has distinguished herself over the years as a staunch conservative on fiscal and social issues, who stands resolutely on principle. I know she will support President partys as she seeks to let the people of SINGIDA keep more of their money via tax cuts, give them more freedom through fewer government regulations, and stand for Pro-Life and Pro-Family values. Wema will make a great member of parliament , because she has great courage, integrity, honesty, and character. Go wema Sepetu.”

Kumekuwepo na mitazamo tofauti kuhusiana na kama Wema anafaa kushika nafasi hiyo.

Tazama Hapa VIDEO Mpya Iliyosubiriwa Kwa Hamu ya Navio Feat. Mr. Blue- AYAYA

$
0
0
Mwezi February 2015 Rapper kutoka Uganda, Navio alitua TZ kwa ajili ya show ambayo ilifanyika Club Billz, Dar es Salaam ilimshuhudia star huyo alipofanya uzinduzi wa Video ya Hit song ya ‘Kigozi‘.

Uwepo wa Navio ndani ya TZ ulikuwa na kingine kizuri, walikutana na Mr. Blue na kupiga collabo ambayo tayari imefanyiwa video… kama hujakutana na video hiyo basi unaweza kuchukua kama dakika nne hivi kuicheki hapa.

Nape: Fisadi akipitishwa na CCM nitaongoza kundi la vijana kumpinga

$
0
0
Akiongea leo jijini Mwanza, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa kamati kuu ya CCM ndugu Nape Nnauye amesema kuwa hana msalie mtume na wanaotumia fedha kununua uongozi.

Aidha Nape Nnauye ameweka wazi kuwa endapo CCM itampitisha fisadi kuwania uongozi wa juu kwa tiketi ya chama hicho basi ataongoza kundi la vijana kumpinga.

Nape ametahadharisha kuwa anayetumia fedha kusaka uongozi ili kuwaaminisha wana-CCM kuwa anakubalika hana nafasi kamwe. Nape ameonya kuwa anayetumia fedha kusaka uongozi akishaupata ataanza kurudisha gharama alizotumia kwanza.

Mwanaume Akishakupata Baada ya Muda Mfupi Upendo Wote wa Awali Huisha

$
0
0
Hiyo ni kauli kutoka kwa baadhi ya wanawake.

Je kauli hiyo ina ukweli kiasi gani?

Kuna bahati mbaya moja, ambayo baadhi ya wanawake hawaijui. Hii ni ile yakudhani kwamba, mwanaume akishaanzisha uhusiano na mwanamke au wakioana, kiwango cha kupendana kitakuwa ni kile kile milele. 

Lakini ukweli ambao hawaujui ni kwamba, binadamu ana hisia na hisia hizi huweza kuchoka. watu wanapokaa pamoja au wanapokuwa pamoja katika uhusiano kwa muda mrefu, hufikia mahali ambapo kiwango cha hisia za upendo hushuka kwa maana kwamba, zimechoka.

Hebu fikiria inakuwaje ndugu au jamaa yako ambaye umekuwa ukitamani aje kukutembelea kutoka mbali anapokaa kwa muda fulani kwako, zile cheche za hamu zinapungua, wala bila kukosana au tatizo lolote? 

Ni hisia zimechoka, hata unaponunua nguo au kiatu kizuri sana, baada ya kuda fulani, ule 'mchecheto' wa awali kukihusu,hupungua au kwisha. Ni suala la hisia pia, si kwamba, hiyo nguo au kiatu hukipendi tena. Kama mwanamke halijui jambo hili, linapotokea, hudhani kwamba, mwenzake sasa hampendi, na ndipo hapo kauli kama:

''Mwanaume akishakupata baada ya muda mfupi upendo wote wa awali huisha''

Haya ni malalamiko ya wanawake katika kujaribu kuonyesha ushahidi wa hali hii. wanashindwa kujua kwamba, kabla ya kuanzisha uhusiano au kuoana, hisia zilikuwa bado ziko juu, kwa sababu bado watu hawa walikuwa hawajaanza kuwa pamoja kwa muda mwingi

Ni mwongo anayeweza kusema kwamba, katika mahusiano yake au ndoa yake hajawahi kuhisi hisia za upendo kwa mwenzake kushuka angalau kidogo. kuna kutofautiana tu katika viwango vya kushuka kwa hisia hizo. lakini kila binadamu hisia zake za upendo hushuka.

Kuna sababu nyingi zenye kufanya kiwango cha hisia za upendo kushuka lakini kubwa huenda ni maumbile, sababu nyingine ni uwezo wa kila mmoja kubadilika kufuatana na mazingira, uwezo wa kutenda na kutoa kauli nzuri kwa mpenzi wake katika mahusino. lakini pia utayari kwa kila mmoja kuondoa zile tabia ambazo mwenzake anasema zinamkera.

Kushuka kwa hisia za upendo hakuna maana ya kuondoka kwa upendo. Upendo unapoondoka umeondoka, lakini hisia za upendo zinaposhuka zinaweza kurudishwa na hali ikarejea kama zamani tu. wakati mwingine hurudi zenyewe kama zilivyopotea.

Lakini wapo baadhi ya wanawake hisia za upendo za wenzi wao zinapopotea,hubabaika na kuharibu mambo

HUDDAH MONROE scared to death ….. You Will Never Believe What Safaricom Did to Her

$
0
0
Huddah claims that she is scared to death after a she bought a Safaricom line and it turned up to be a dead Indian’s phone number.

Huddah could not understand why callers kept asking her how she got that line. Here is what she wrote on social media;

Dear @safaricomltd , Today I bought a new line and my phone can’t stop ringing . The callers keep asking me where I got my number from. The callers of Indian decent claim my newly acquired number belongs to their DEAD brother!!!!!!!!!!What is really going on ? Do you people repeat numbers? Or make them twice? What if you repeat numbers aftera while and maybe it belongs to someone who got murdered? Please help me with answers!!!! I’m scared to death!!!

Polisi wampiga vibaya Mwandishi wa Habari Zanzibar

$
0
0
Mwandishi wa Habari kwa jina Omar Ali mzaliwa wa Mkoani Kangani kisiwani Pemba, jana mida ya asubuhi ameshambuliwa na kupigwa vibaya sana na jeshi la Polisi Zanzibar na kutupwa maeneo ya Maisara mjini Zanzibar.

Mwandishi huyu alikuwa anachukua habari kutoka kituo cha uandikishaji dafatari la kudumu maeneo ya Migombani Zanzibar na polisi hao inasadikiwa walisema ni mwandishi wa Chama cha Wananchi CUF na ndipo walipomshika na kuanza kumpiga vibaya sana na kumvunja miguu kama anavyoonekana kwenye picha akiwa hospital mahutui miguu ikiwa imevujika.

Ikumbukwe:
Matukio haya yanakuja baada ya wananchi wa Zanzibar kuhakikisha kila kituo hawezi kuandikishwa mtu ambaye hahusiki kama ambavyo tumeona na kuskia kupitia vyanzo mbali mbali mpango wa CCM kupeleka mamluki visiwani Zanzibar kujiandikisha kwaajili ya kukiokoa Chama cha Mapinduzi hasa Zanzibar ambako kuna kila dalili kungoka madarakani Oktoba mwaka huu.

Chanzo: Nilikuwepo eneo la tukio.

Faiza:Sugu Amedanganya Bunge Kuhusu Matunzo ya Mtoto...Adai Hayupo Tayari Kuyamaliza Kifamilia

$
0
0
Mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi, Faiza Ally jana amesema 'Sugu' alidanganya Bunge alipodai hutoa sh.500,000 kila mwezi za matunzo ya mtoto.

Na ingawa Sugu alidai bungeni pia kuwa hulipa ada ya sh. milioni tatu kwa mwaka kwa ajili ya elimu ya mtoto huyo, Faiza amedai ni kwa nusu ya pili tu ya kipindi cha miaka miwili ambayo amekuwa akisoma.

Aidha, mwanamitindo Faiza amesema hayupo tayari kumaliza kifamilia mvutano wa malezi ya mtoto na 'Sugu', kama Mbunge huyo alivyoeleza bungeni juzi.

Akizungumza katika chumba cha habari cha Nipashe jijini jana, Faiza alisema 'Sugu', mwanamuziki wa hip hop pia, hutoa sh.500,000 za matumizi ya mtoto lakini si kila mwezi.

"Bahati nzuri fedha hizi huwa anazituma kwa njia ya simu, kuna rekodi ya miamala (itathibitisha)... hatumi kila tarehe moja kwa mfano," alisema.
"Katika miezi sita iliyopita? Katika miezi sita iliyopita ametuma si zaidi ya mara nne."

Faiza alisema Mbunge wa Mbeya Mjini huyo alianza kulipa ada ya shule hivi karibuni, lakini mtoto huyo wa miaka miwili na miezi nane alianza kusoma akiwa na mwaka mmoja na miezi saba.

Kuhusu nia ya Sugu ya maridhino, Faiza alisema "haya mambo hayataisha kifamilia.

"Kama angekuwa anataka suluhu ya kifamilia kama alivyodai bungeni, wazazi wangu anawajua. Wazazi wake na ndugu zake wote nawajua, hakuwahusisha akakimbilia mahakamani.

"Siwezi. Acha haya mambo tukaamuliwe na mahakama (ili) haki itendeke."
Faiza anakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo Manzese kumpa 'Sugu' haki ya kuishi na mtoto.

Mahakama ilimpa 'Sugu' haki hiyo baada ya Mbunge huyo kuonyesha hofu ya mtoto kukosa malezi mema kutoka kwa mama yake kutokana na mapenzi ya Faiza katika mavazi mafupi, ikiwemo pedi za wagonjwa au wazee, na nguo ziachazo wazi sehemu kubwa ya mwili.

Faiza amesema ingawa Sugu anamtuhumu kukosa maadili kwa sababu ya mavazi mbunge huyo amewahi kutolewa kwa nguvu bungeni na kurekodi CD zenye matusi za 'Anti Virus', vitendo ambavyo ni picha mbaya kwa mtoto siku za usoni.

Faiza alikutana na Sugu kupitia mtandao wa kijamii wa 'facebook' 2011 na aliondoka nyumbani kwa Mbunge huyo "baada ya kushindwa"; Januari mwaka jana, alisema.

Nipashe,28/06/2015

Lowassa Awaburuza Wenzake Urais CCM...... Ni matokeo ya utafiti kwenye wilaya 20

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu, Monduli, Edward Lowassa ametajwa kuongoza katika kutaja vipaumbele vya maendeleo ikiwamo kupunguza tatizo la Ajira nchini na kuinua Elimu, miongoni mwa kundi la wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 Kadhalika, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ametajwa kuwa ndiye kiongozi wa siasa aliyeshuhudiwa na wananchi wengi katika hotuba zake kuliko wanasiasa wengine waliokwisha kutangaza nia.

Hayo yamo katika ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Maendeleo la Utafiti la Elimu (Tedro), iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Katerri, alisema ripoti hiyo ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu 2,000 kutoka vijijini na mijini.

 Alisema katika ripoti hiyo kipengele cha watangaza nia walioshuhudiwa na watu wengi katika hotuba, Lowassa anaongoza kwa kushuhudiwa kwa asilimia 54, akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (46), Naibu Waziri wa Fedha ,  Mwigulu Nchemba (44), Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira (40) na Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani(39).

 Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba(34), Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (31), Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki,  Makongoro Nyerere (27), Waziri wa Ujenzi, John Magufuli (23), na Mbunge wa Sengerema, Willium Ngeleja (19) na wengine wakifuata.

Katika Kipengele cha kupunguza tatizo la ajira, ripoti hiyo ilieleza kuwa wananchi walipohojiwa walieleza kuwa wana imani na Lowassa kwa asilimia 19,  Nchemba (14), Magufuli (13).

 Makamba (13), Membe (12), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (10), Mwandosya (7), Dk. Harrison Mwakyembe (7), Wassira (2) na wengine (3).

“Utafiti huu umebaini kuwa watangaza nia wengi pamoja na mambo mengine walijikita sana katika kusema watatatua tatizo la ajira kwa vijana,” alisema  Kaserri.

Kadhalika ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha kuinua elimu nchini, ambacho wananchi waliohojiwa walitoa nafasi kubwa ya uwezekano wa kutekelezewa kwa kipaumbele hiki kwa Lowassa kwa asilimia 25.

Nchemba (18), Membe (16),  Makamba (13), Magufuli (12), Mizengo Pinda (12), Wasira (3) na wengine (9).

 Pia ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo waka 2025, na wananchi walikuwa na imani na Nchemba kwa asilimia 13.4 kuwa ataweza kulipeleka taifa kufikia kipato cha kati.

Lowassa (11), Wasira (9), Membe (9.20),   Magufuli (9.0), Makamba (5.3), Mwandosya (4.60),  Pinda (3.5) na Dk.  Mwakyembe (1.40).

Hata hivyo, utafiti huo ulielezea kipengele cha kuinua sekta ya Kilimo na Mifugo nchini ambacho kwa watangaza nia hao, wananchi walikuwa na imani kwa Pinda kwa asilimia 23.

Lowassa (17), Nchemba (16), Membe (11) Wasira (9),  Makamba (7), Magufuli (5), Waziri wa Maliasili na Utalii,  Lazaro Nyalandu (3.3), Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangala(3.2) na Mwakyembe (2.6).

Katerri alisema utafiti huo pia ulihusu kipengele cha Utawala bora na vita dhidi ya ufisadi ambapo ulionyesha kuwa Mwigulu Nchemba amepata asilimia 17.4 ya uwezo wa kupambana na tatizo hilo.

Wengine waliomfuata ni Magufuli (14.2), Membe (11), Lowassa (6.10), Jaji Ramadhani (6) na Mwandosya (5).

Wengine ni Mizengo Pinda (8),  Mwakyembe (8),  Makamba (7), Samuel Sitta (6), Dk. Kigwangala (3).

Katika kipengele za Uadilifu usiotiliwa shaka katika utumishi Nchemba alipata asilimia 15, Membe (13), Mwandosya (13), Pinda (8), Makamba (8) Jaji Ramadhani (7),  Lowassa (10%).

Katika kipengele cha hotuba iliyo bora, Katerri alisema Nchemba alipata alama (A), Wasira( B+), Membe (B+),  Mwandosya (B+) Lowassa (B) na Membe (B). Katerri Alisema lengo la utafiti huo ni  kutathmini Elimu katika Nyanja ya uraia kwa watanzania kupitia vipaumbele katika hotuba za waliokwisha kutangaza nia kupitia CCM.

Alizitaja wilaya ambako utafiti huo ulifanyika kuwa ni  Kinondoni, Kibaha Vijijini, Kilombero, Rombo, Arumeru, Mbulu na Babati, Lindi, Mtwara, Njombe mjini, Njombe Vijijini, Mbeya Mjini, Nyamagana, Biharamulo, Tabora, Nzega, Bahi, Chamwino na Kasulu.

Huyu kijana wa Jirani nimfanyeje? Kila House Girl wangu anampa mimba

$
0
0
Kuna kijana hapa anaangalia si te ya Jirani na anachunga ngombe za huyo Jirani

Huyu kijana ameshawapa mimba ma hg wetu watatu

Wawili aliwakana na hatukua na ushahidi Wa kumkamata moja kwa moja, hivyo tukalazimika kuwatimua hao mabinti kurudi makwao kwa nyakati tofauti

Muda ulivyopita tukasahau yakapita hayo, mwaka umepita sasa, tukaleta hg mmoja hivi ambae tulimtoa Mwanza, mm nilishasahau masuala ya huyo kijana Muda hadi juzi niliporudi home ghafla baada ya kushikwa na vidonda vya koo vilivyoniletea homa Kali

Nilipofika home nilipiga honi sana bila majibu, nikashuka nikafungua Geti dogo kwa ufunguo wangu na nilipoingia nikajifungulia Geti kubwa, cha ajabu binti Wa kazi hakutoka, nikadhan ameenda dukan, nilipoingia ndani nikasikia sauti Kali ya mahaba ikitokea chumbani kwa hg, nikasukuma mlango ahamadi dogo kamgeuza hg doggie, pamoja na kwamba nilikua naumwa nilimpa kipigo kikali yule kijana, akaniponyoka na kukimbia uchi akaenda akaruka ukuta hadi kwao, nikamwamuru hg kuvaa, kwa jinsi nilivyomwona uchi kaumbika mno Basi tu

Usiku tulishauriana sana na wife, akashauri twende police tukapewe ushauri Wa kisheria kuhusu huyu kijana maana ametusumbua kwa Muda mrefu sana
Ijumaa ya Jana tukaenda kumuona mkuu Wa kituo, akatuambia huyo dawa ni kumpa kesi ya ujambazi au madawa ya kulevya ili akakae segerea Muda mrefu hivyo nimpe laki mbili kwa kazi hiyo na hukumu ikitoka nimuongezee zingine

Hivi navyowaeleza amelala ndani tangu jana, Jumatatu karandinga litakuja kumchukua kumpeleka mahakamani kwa kesi ya ujambazi Wa silaha, kuna silaha moja ipo pale kituoni watampeleka nayo ilikosaga mtuhumiwa

Kwa kweli huyu kijana ametusumbua kwa Muda mrefu sana, mwenzie wanae kaa pamoja hapo kwao katuambia mwenzie hupewa juice, hukaangiwa mayai na kupelekewa, vyakula mbalimbali na hata wine zetu humpa
Na ndio maana tunashangaa matumizi ya ndani yamekua makubwa sana, sasa hiyo si dharau wakuu

Huyu binti tunajiandaa kumsafirisha wakati wowote, huu ni ukosefu Wa adabu kuleta jitu ndani?

Mabosi Wa huyu kijana wamekua wakinipigia simu tangu Jana wakiniomba nimuachie safari wanamfukuza, kila tukishtaki huwa wanasema hivi hivi watamfukuza

Safari hii lazima nihakikishe ananyea debe next time anaweza kulamba.....

STEVE NYERERE Atikisa Jimbo la Kinondoni Mbio za Ubunge 2015..Nimekuwekea Picha Hapa

$
0
0

 Staa wa Bongo Movies, Steven Mangere ‘Nyerere’ amewaomba wanawake wasihadaike na kanga na vitenge wakipewa na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongoziili wawachague.
Steve aliitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) nakuwahimiza vijana wa Kinondoni wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu ili waweze kuchagua viongozi watakaoweza kuifikisha Kinondoni sehemu wanayotaka.

Katika mkutano huo, Steve alisindikizwa na wasanii mbalimbali akiwemo JB, Wasta, Bi Mwenda, Chuchu Hans, Johari,Ray Nyamayao, Esha Buheti, Thea na Bi Star

“Kinondoni tunaweza kuondokana na mafuriko kama tutachagua kiongozi atakayeweza kurekebisha miundombinu ya wilaya yetu”alieleza Steve huku akishangiliwa.

Mtanzania

NAY WA MITEGO: Sitaki Watoto Wangu Wasome kwa Shida Ndiyo Maana Nimewanunulia Gari la Kuwapeleka Shule.

$
0
0
Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amefunguka kuwa hataki watoto wake,Curtis na Munie wasome kwa shida kama yeye alivyosoma kwa tabu,ndiyo maana amewanunulia gari la kuwapeleka shule.

Akipiga stori na Clouds FM,alisema kuwa gari hilo lina vitu muhimu ndani kama meza ya kulia chakula,sinki la kunawia mikono,kitanda cha kulalia,TV na huduma nyingine ambalo wataanza kulitumia mwakani.

‘’Unajua mimi nilisoma kwa shida sana,sasa sitaki watoto wangu wapate shida ndiyo maana nimewanunulia gari la kuwapeleka shule wataanza kulitumia mwakani,na nitaajiri dereva wa kuwapeleka shule,’alisema Nay.

Wizkid naye asusia tuzo za BET kutokana na ubaguzi kwa wasanii wa Afrika

$
0
0
Staa wa Nigeria, Wizkid ambaye alikuwa akiwania kipengele cha Best International Act:Africa katika BET Awards 2015, ni msanii wa pili aliyesusia tuzo hizo zilizotolewa Jumalipi iliyopita huko L.A, Marekani.

Baada ya Fuse ODG kutweet akisema sababu zilizomfanya asihudhurie utolewaji wa tuzo hizo, Wizkid naye amesema hatakuwa akihudhuria pre-shows na nominee parties kama utaratibu wa kuwapa tuzo wasanii wa Africa mapema kabla ya show yenyewe (saa 4 asubuhi) backstage utaendelea.

Alianza kwa kutweet:

Lol, nasikia BET wamemaind kwa sababu sikuhudhuria pre-shows na Interviews! LOl


Wizkid ameongeza kuwa utaratibu wa kuwabagua wasanii wa Afrika katika tuzo hizo ndio ilikuwa sababu ya kutohudhuria hata aliposhinda tuzo ya BET kwa mara ya kwanza.

Ameongeza kuwa hiyo ndio sababu kubwa pia ya kutopost kitu katika mitandao ya kijamii kuhusu nominations au tuzo hizo kwa ujumla sababu yeye hajali.

Hizi ndio tweet zake:





Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images