Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104745 articles
Browse latest View live

Snura:Sitaki Unafiki na Makundi ya Kuwadiss Wengine

$
0
0
MWIGIZAJI wa filamu na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi ‘Mama wa Majanga’ amesema kuwa anakerwa sana na unafiki unaofanywa na baadhi ya wasanii kwa kushirikiana na wapenzi wa kazi zao kwa kufanya kampeni za kuangushana katika medani za kimataifa.

“Naepukana na unafiki tena naweza kusema roho mbaya chuki kwa baadhi ya wasanii kuunda makundi ambayo yantumia muda mwingi kuwadisi wengine, mfano hivi sasa wakati Diamond anagombea Tuzo kimataifa eti kuna watu wanaungana na watu wa nje kumfanya kampeni ashindwe,”anasema Snura.

Snura anadai kuwa siku hizi makundi ambayo yanaundwa na wasanii au wapenzi wenyewe ambayo yanatumika vibaya katika kutengeneza ugomvi, au kushabikia wasanii wakigombana kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwatusi au kukatisha tamaa hata kama wanafanya kazi zinazotangaza Taifa.

Listen And Download New Audio | NAY WA MITEGO | SINA MUDA

$
0
0
Listen And Download New Audio | NAY WA MITEGO | SINA MUDA

Hivi Unamchukuliaje Mpenzi Wako Mwenye Majibu Kama Haya Ukichat Nae

$
0
0
Eti ukiwa unachat mpenzi wako anakupa majibu kama haya unamchukuliajeee
mfano

1.ukimwambia kila ukimwambia bby i love you much au nakupenda sana mpenzi wangu
yeye hujibu asante au thanks badala ya kusema i love you too mpenzi wangu

2.ukimtumia vocha hukaa kimya ukimpigia hujibu asante nimeipataa.

3.ukimwambia nimekumic mpenzi wangu hujibu asante au thanks au k thanks

4.ukimwambia kuhusu sex huandika k au sawa au bila kujibu

jee unamuongeleajee mpenzi kama huyu kwa wale wataalamu saikolojia

Akina Dada Msijidanganye la Sivyo Mtaishiwa Kufunuliwa tu Mpaka Akili ziwakae Sawa

$
0
0
Leo nimeona niwape vipande vyao hawa akina dada kuanzia umri wa miaka 30 na kuendelea ambao bado hawajaolewa, utakuta mdada mtu mzma kabisa ana umri wa miaka zaidi ya 30 anatafuta wanaume wa kumuoa kwa kuweka masharti lukuki tena magumu Kinoma

Mara nataka Mwanaume Handsome, Mcha Mungu, mwenye elimu ya degree, awe ameajiliwa au anabiashara.

Nabaki kuwashangaa sana nyiyi viumbe, unataka mwanaume mcha Mungu je wewe ni mcha mungu? Ungekuwa na tabia nzuri ungefikisha umri huo ukiwa nyumbani?

Tambua kuwa kitendo cha kufikisha miaka 30 nyumbani na huna mume wala mchumba inabidi ujiulize mara mbili ulikosea nini huko nyuma Kwasababu Kupata Mume umri huo kwa sasa ni Bahati , Wengine Kabisa wanakataa wachumba wakiwa kwenye early 20's Wakijua watastay young Forever...

Utakuta mwingne alizalia nyumban halafu anakuja naye na sifa zake eti nataka mwanaume mnyenyekevu na ambaye hajawai kuoa nyambaaafu wewe umezalia nyumban halafu leo unataka mwanaume ambaye hajawahi kuoa for what?

Mimi nawaambia msijidanganye hata kidogo, mkitaka masharti hayo mtaishia kufunuliwa tu mpaka akili ziwakae sawa.

KWAHERINI

Wabunge 35 wa UKAWA Wafukuzwa Bungeni

$
0
0
Wabunge  35 wa kambi ya upinzani bungeni jana walitolewa nje ya ukumbi wa bunge na spika wa bunge  Anne Makinda na kupewa adhabu ya  kutokuhudhuria vikao vitano kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge .

Mara baada ya kikao cha bunge kuanza spika wa bunge alinza kwa kuwakumbusha wabunge namna ya kufuata kanuni hasa pale wanapotaka kuondoa muswada wowote.

Hali ilibadilika ghafla Bungeni baada ya Mbunge Ezekiel Wenje kuomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… ndipo spika aliamua  kuwatoa nje.

Hata hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo ni  ya sheria ya petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pamoja na sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania iliwasilishwa Bungeni.

Majina ya Wabunge waliotimuliwa  ni,
Ezekiel Wenje
Mussa Kombo
Masoud Abdallah Salim
Rebecca Ngodo
Sabrina Sungura
Khatib Said Haji
Dr. Anthony Mbassa
Maulidah Anna Valerian Komu
Kulikoyela Kahigi
Cecilia Pareso
Joyce Mukya
Mariam Msabaha
Grace Kiwelu
Israel Natse
 Mustapha Akonaay
Konchesta Rwamlaza
Suleiman Bungura
Rashid Ali Abdallah
Ali Hamad
Riziki Juma
Rukia Kassim Ahmed
Azza Hamad
Khatibu Said Haji
Kombo Khamis Kombo
Ali Khamis Seif
Haroub Mohammed Shamisi
Kuruthum Jumanne
Mchuchuli
Amina Mwidau
Mkiwa Kimwanga
Salum Baruhani
Marry Stellah Malaki
Rashid Ally Omary
Mwanamrisho Abama
Lucy Owenya

Nyota ya Diamond Platnumz Inazidi Kung'ara.......Katajwa Kuwania Tuzo za Uganda (Uganda Entertainment Awards 2015 )

$
0
0
Diamond Platnumz ameendelea kutajwa kuwania tuzo mbalimbali barani Afrika.

Akiwa ni miongoni mwa wanaowania tuzo za MAMA zitakazotolewa mwezi huu, muimbaji huyo wa ‘Nana’ ametajwa kuwania tuzo zingine za Uganda zijulikanazo kama Uganda Entertainment Awards 2015 (UEA)

Platnumz anawania kipengele cha Best African Act akichuana na Wizkid (Nigeria), Patoranking (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria) na Active

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Septemba 4, 2015 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort (Speke Ball) jijini Kampala, Uganda.

AZAM TV Waja na Mpya Sasa Kuonyesha Ligi ya Uingereza Kwa Kiswahili.....

$
0
0
Mambo yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha runinga nchini kurusha ‘live’ mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili.

Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha unarusha ligi hiyo live kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema.


  • “Tunafanya juhudi kubwa ili tulifanikishe hilo mapema, ila wahusika ndiyo wenye uamuzi wa mwisho katika kutupa haki ya matangazo hayo, tumedhamiria pia kuonyesha Ligi ya Hispania.



  • “Wakati tukipanga haya, tuna nia ya kuboresha muonekano wa ligi yetu ya Tanzania (Ligi Kuu Bara) msimu ujao ambapo tunataka ionekane katika ubora wa hali ya juu zaidi,” alisema Tido.


Katika hatua nyingine, Tido alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi hadi utakapofanyika, watakuwa wakiwaletea watazamaji wao matangazo ya matukio mengi kuhusu uchaguzi huo.

Faiza Ally Afunguka Tena 'Katika Sheria ya Tanzania na Duniani Hakuna Kipengele Kinacho Mfanya Mama Apokonywe Mtoto Kupitia Mavazi Alitumia Rushwa Au Cheo Chake'

$
0
0
Repost from @faiza_ally
Poleni marafiki mlio sikitishwa na tukiwa langu la kupokonywa mtoto- nimeona mnahitaji kujua ili muache masikitiko na tufurahie wakati uliopo- ni Kweli baba yake alishinda KESI lkn sheria hairuhusu nazani alitumia rushwa au labda cheo chake maana haijulikani alishindaje - any way nataka tu mjue mtoto wangu ninae na mimi si mwanamke regerege wa kupokonywa haki zangu za kumlea mwanangu ! Nimekwenda kwenye vyombo vya sheria na vinafanya kazi na. Niwahikikishie tu ntashinda kwa kuwa nina haki na ni mama bora- nitasimama mpaka kieleweke bila kujali cheo wala pesa - sheria zimewekwa na haki zinatendeka- mpaka sasa niko vizuri tu- niko na sasha na ntaendelea kuwa nae mpaka umri utakapo ruhusu lkn si leo wala kesho hayo ya mbele mungu ndio anayajua.....na niwaambie tu wale watoa hukumu wa humu ndani- KATIKA SHERIA YA TANZANIA NA DUNIANI HAKUNA KIPENGELE KINACHO MFANYA MAMA APOKONYWE MTOTO KUPITIA MAVAZI- KUNA VITU VYA KUZINGATIA VYA MUHIMU LKN SI MAVAZI! Aacheni ujinga wa kupeana hukumu - kuna watu wana mamlaka yao waliosomea kazi zao sio nyie wajinga mnaojivisha joho la ujaji hahahahahahaaaa..... Na msisahau hakimu mkuu ni MUNGU - ANAONA ANASIKIA NA ANATENDA 🙏🙏🙏 Alhamdulillah - feeling bless

Stori ya Msichana Anayejiita WEMA DAILY Kwenye Instagram na Jinsi Instagram Inavyompa Pesa Mpaka Kuacha Kazi ya Kuajiriwa-Must Read Story

$
0
0
Kuna Watu Hii Mitandao ya Kijamii Kama Instagram na Mingine mingi wanaichukulia poa tu na kuona sehemu ya Kufanya mzaha na kutukana watu wakati kama ikitumika vizuri ni Ajira tosha ya kujipatia kipato bila shida..Hapa chini nimekuweka Stori ya Msichana anayejiita Wema Daily huko Instagram....Jisomee Mwenyewe Hapo chini si ya Kukosa itakufungua Macho:

'MWANZO......As a young girl binafsi sikuwai kua na ndoto za kuajiriwa japo kua Mungu alinsaidia sjawai kufeli wala kukwama Darasa lolote mpaka namaliza chuo kikuu.Nilisoma kwasababu everyone else was studyng and My mother put every single sent for us ili tupate elim. Elim inasaidia sana especially ukikaa na watu mnakua mnaongea lugha moja , but still skuwai kujiona kama muajiriwa HONESTLY. .
.
Nikiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu nlijaribu kujiunga na wenzangu kikund kimoja and we opened an NGO tulikua wanafunz wa vyuo tofaut kama kum na nne tulifight sana but tulikosa grants coz tulikua wanafunz they figured tutakua busy na masomo. Baadae watu nguvu ziliwaisha kila mtu akaendelea na shule walio maliza wakawa madaktari ikaishia ivo...
Mwaka ulio fata since kila mtu alikua busy nkaanza kufanya kazi za tempo mwaka wa kwanza mpaka wa pili nkiwa chuo ... Pesa nliyo ipata ilinsaidia hata nkiwa likizo nisiombe pesa kwa mzazi..... Ukichanganya na boom la chuo tena mambo yanaenda fresh. But mazingira ya kazi za Tempo nlizo kua nkifanya nlitaman sana nije kua na kampun inayo fanana na ile. So ndoto zangu zote Ikawa ( bado zipo) kuwaza kufungua kitu kinacho fanana na ile.

Badae walikuaja watu wakasema wanasaidia vijana kufungua makampun na kuwapa muongozo. Ada ni laki moja. Sikua na hela ( ki chuo chuo) nlipiga sim kwa kaka angu akantumia hiyo ela nkajiunga. Tulifunguliwa kweli makampun tukaanza kupewa seminars. Na project za kufanya na kutu ahid kutusaidia kutupmbea mikopo. I must say ilinipa hope sana na ikaonyesha mwanga wa maisha yangu Baada ya Chuo.

Ila baadae it turn out vikao na seminar haziiahi ahad ahadi mwisho wa siku tena watu wakakata tamaa. Nguv zikaisha Watu wakaendelea na mambo yao . Wenye kazi zao na wenye biashara na wanao soma masters. Hakukua na watu tena kwenye iyo kampuni, Sasa kwasababu option ziliisha nikarud kwenye wazo langu la kufungua Kampun nlo kua nkiitaka .... Nliomba ushauri wa watu waliopo kwenye iyo fieild they told me how Good my idea was. Coz ilikua kidogo tofaut . And they liked it

Tatizo ikawa pesa ya kufungulia kampun sasa natoa wap? Nika stak na idea yangu mpaka nikamaliza chuo sina foundation yoyote now where do i start? Sina kazi ( sitaman kuajiriwa ) na ndo nimemaliza nikawa kula kulala nyumban. Ila uzur nkawa siomb hela sana since nlikua na tempo works nazo fanya now and then

With the boredom ya kukaa nyumban kutuma ma cv kila kona .. Am a social person and i love pics and edits more over nlikua nampenda sana rihanna to kill time na ili nsiboreke na maisha nliyo nayo nkafungu account ya instagram FAN PAGE  ya rihanna. I met cool people Navies are the best . I got friends walontumia hadi nguo za rihanna river island .. I had friends from all over the place na kusema ukweli nlikua siborek. Napika na sim yangu i hated kulala usiku hehe.

So pressure za kutafuta kazi nkawa sina sana coz nlikua najichanganya na watu na hali yangu yakutokua na kazi ikawa hainisumbui.

But one day nkakaa chini and thought ivi why am i having rihs fan page? Atakuja lin Tanzania ? Why nsifanye kwa mtu nnaempenda hapa hapa TZ?
Nkifungua fan page ya kibongo kwasabu na mpenda sana wema ... Then i decided kufungua inayo muhusu wema .... Wanna tell u one thing wakat niko na Navy account kama fan page u do it for love. Without expectation za kua utamuona hiyo msanii wala yeye siku kulike pocha yake utakayo weka .

Nlipo fungua fanpage turned out to be the first fanpage hapa bongo and in my mind skua hata na wazo kama wema atanotice na alivo famous hehe i was just busy showing love.

Ila ajabu nkashangaa @wemasepetu kuona amenifollow and all her crew and a was like ok hahaha now this is new thing.

The worse side of it ilikua watanzania walikua tofaut kidogo maybe ni tabia tuliyo nayo ya kudiss vya nyumban na kupenda vya wenzetu. Nlinza kusemwa sana kua nataka sijui lunch some lame stuffs. Some of my friends kwasabu account ilianza kukua walianza kunisema that am being lame nakua kama sijasoma naanzishaje fanpage msomi mzima. Thy got toe kiukweli nlikua najiskia vibaya sana. Ila napenda sana so i didn care

Baadae when the page grew i started helping watoto wa shule za msingi ... Kupitia same page. Watu walikua wanasaidia sana tena sana walikua wanajitoa and at somepoint nkasema nifungua foundation Same song coz sipend kuajiriwa bora nifungue foundation nsaidie watu and use the page for something positive

I tried jaman and it was a success untill some people start kunisema instagram na kuniwekea vikao kua am using hela za watu kuish while all the cash zilikua zinaenda direct kwa watoto.

Or else i used some for transport to their schools. Sasa na mzazi akaanza kunjia juu kua ntafute kazi coz nlikua nsha move out nimepanga chumba expensie ka nna hela vile af naomba nyumban kulipiwa kodi.

Kila mtu akanijia juu. Thats when i decided to drop the charity thing and focus kutafuta kazi ambayo nlifanikiwa kupata. Nlitishiwa kwamba nsipo pata kazi kodi inayo kuja ntalipa mwenyewe or else njue pakwenda

Na nkiona pesa yenyewe ndefu nkasema isiwe tabu ngoja niende mzigon. Kazin sasa.. I was smart hard working ... My table would tell but nlikua nachelewa sana kazin. Nimewahi ni saa tatu. Kuamka wala stressful works wasn hard for me.

Tatizo lilikua mshahara. I wont tell kiasi nlichokua napata but it was awful. Hapo nimeamia nyumba nalipa laki mbili . Mshahara na kod ya mwez vinakaribia kulingana.

Lakin nlivumilia coz they wanted me to work was waiting prob iishe niongezwe mshahara. But maisha yaliongezeka kua magim zaid kila kukicha. Nkienda hospita naambia BP iko juu hapo hata miaka 25 sijafikisha. Na mtoto sina.  I had to work for 6 months ilikua kama mwaka.

I remember kuna hela nlitakiwa kulipa ya kodi mshahara umechelewa.. Nkaenda kwa boss ansaidie mshahara ukitoka nimpatia akanambia THEY CANT HELP ME. Naomba niwambie in mylife sjawai hongwa. Halaf kama nlivyo jikiza sipend kuomba msaada kwa mzazi. Worse enough nna fanya kazi. The frustrations were on PEAK. Hapo bado nna account yangu ya instagram. Sasa nika mtext Wema this day and asked her kama its ok nkitumia the page kuweka matangazo kwa kulipia.. And she told me its ok baby haha. .
.
Since my page ilikua na watu wengi nkaanza kuweka matangazo ya watu coz they wanted to and i have many followers and wema gave me go ahead nkaanza kufanya matangazo ya Instagram. Which helped me sana and at the end of the day nkaacha kazi yangu ya kuajiriwa and stayed home and kufanya account yangu ya instagram inilipe.

Saiz i have the coolest place am living the best life and nkaacha kazi ya kuajiriwa. So ikawa kinda kama kazi ya kujiajir though not much.. Ambayo kwa mwez i get more million moja na laki tano toughly hapo ni kwa zile nazo save nimetoa nazo timia. My passion turned out to be my working place. And toka nimeanza kufanya kazi za kutangaza ig.. Av been reading alot about Internet marketing Saiz i have opened my company special for INTERNET MARKETING , SOCIAL MEDIA MANAGEMENT AND DIGITAL PR. Which am going to launch soon. Hiyo ni only one project ukiacha the next big thing coming around the corner.

THATS MY STORY'
.
.Wemadaily story yako pia imebadili mtizamo wangu. Kila la heri katika yote

Wakaka na Uongo Uongo na Maisha Feki Wanapomtaka Msichana..Mnaboa Sana....Hamjui tu

$
0
0
Wakaka wengine wana haraka sana kuanzisha mahusiano ya kimapenzi mpaka ku fake maisha. Hata muondoko na kuzungumza atabadilisha, ataazima gari na kudanganya ni lake, nguo ataazima, au hata kazi hana lkn atadanganya eti nina degree au nafanya kazi mahali fulani kumbe muongo...atasema ana kiwanja mahali fulani, ana hiki na kile kumbe anataka ampate msichana msichana fulani....tena ukute msichana mwenyewe atampenda kwa dhati si sababu ya maneno matamu na mali alizotajiwa.... Msichana ukikutana na mkaka wa hivyo anaanza kujinadi nina hiki, kampuni, baba yangu bosi mama yangu vile...kaka yangu anaishi ulaya...huyo kaka ni muongooo hata kama kuna ukweli ni asilimia 5/100

Jaman wakaka msijaribu kufanya hivyo. Sawaa utampata msichana kwa njia hizo...lkn hamtadumu na mwisho utakua mbaya sana maana umejenga mahusiano yako kwenye uongo. Uwe wewe, huna pesa, huna gari huna lolote mtu atakupenda jinsi ulivyo si ulivyonavyo.

~Mrekebishatabia

ZITTO KABWE Awaacha Wananchi Njia Panda Viwanja vya Mwembeyanga...Ashindwa Kutaja Laivu Majina ya Walioficha Mabilioni Nje ya Nchi

$
0
0
KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Zitto Zuber Kabwe jana amewaacha njia panda wananchi waliokuwa wakisubiria kutaja orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa kuwa na akaunti zenye mabilioni ya fedha nje ya nchi, baada ya kusita kuyataja kutokana na sababu za kisheria.

Akizungumza na umati mkubwa uliofurika katika viwanja hivyo jana jijini Dar es Salaam, kusikiliza azima ya kiongozi huyo huku wakiwa na shauku kubwa ya kufahamu orodha ya majina hayo, Zitto alisema kuwa atawapatia karatasi waandishi wa habari yenye orodha ya majina hayo ili waende kuifanyia kazi kwa kuwahoji wahusika kulingana na taaluma yao.

Alisema kuwa mwisho wa hotuba yake angegawa karatasi kwa wanahabari yenye majina hayo, ambapo wananchi walionekana kuwa na shauku ya kupata karatasi hiyo yenye majina 99 ya wafanya biashara maarufu ndani na nje ya nchi, lakini Zitto akasema hakuwa tayari kuwapatia nakala hiyo wananchi, hivyo akawataka wafuatilie katika mitandao ya kijamii pamoja na kwenye vyombo vya habari kwani wao kwa kutumia taaluma yao wanao uhuru wa kuyaanika hadharani.
Aidha, aliongeza kuwa kati ya majina hayo ya watu wenye mabilioni ya fedha nchini Uswisi, kuna wengine wanamiliki kihalali lakini wengine wamejilimbikizia kinyume cha sheria.

“Nimeweka leo orodha ya majina hayo wazi ili kuiwezesha serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo, majina 99 mtayapata kupitia kwa wanahabari niliowapatia nakala yenye orodha ya vigogo hao ama Watanzania walio na akaunti kwenye HSBC ya Uswisi ikiwa na akiba ya Dola 114 milioni za Marekani,” alisema Zitto.
Baada ya kuhitimisha mkutano hao, kiongozi huyo wa ACT aligawa karatasi hiyo kwa baadhi ya waandishi wa habari.

Hotuba ya Zitto Kabwe - Julai 04, 2015 na Orodha ya walioweka fedha Uswisi

$
0
0
Dar Es Salaam 04.07.2015

Ndugu Wanadar es salaam

Kwanza nianze kwa kutoa shukran kwa kuitikia wito wetu wa kujitokeza kwa wingi kuja kutusikiliza leo hii katika Viwanja hivi vya Mwembeyanga, TUNAWASHUKURU SANA.

Kwetu nyie mna umuhimu wa kipekee, maana mnatokea katika Jiji ambalo misingi ya ujenzi wa Taifa hili ilianzia, kuanzia kuasisiwa kwa Chama cha Tanganyika African Association mpaka harakati za Chama hicho cha Kijamii kurithiwa na Chama cha Siasa za TANU.

Siku zote historia inawaonyesha watu wa Dar es salaam kuwa ndio waasisi wa harakati hizi za siasa za kizalendo nchini. Kutokea nyakati zile za kina Mwalimu Nyerere, Bibi Titi Mohammed, kina Sykes, Dossa Aziz Ally, John Rupia na Zuberi Mtemvu mpaka leo bado wanadar es salaam mnao umuhimu wa kipekee katika siasa za nchi hii. Kwa kutambua umuhimu wenu huo, tumeona leo tufanye Mkutano huu Maalum viwanjani hapa ili kukitambulisha tena chama hiki kwenu, na pia kukikabidhi mikononi mwenu ili harakati hizi za kurudisha misingi ya Uzalendo wa Taifa hili mzishike nyie wenyewe waasisi wa harakati husika.

Na hili tunalolifanya leo si jambo geni kwenu, labda niwakumbushe tu, ni kwa huo umuhimu wenu Rais wetu wa kwanza na baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alijenga Utamaduni wa kuzungumza na Taifa juu ya mambo yote mazito ya nchi hii kupitia wazee wetu wa Jiji hili, utamaduni ambao umeendelea kurithiwa, nasi tunaona ni utamaduni mwema wa kuuendeleza. Japo sisi tunakwenda mbele zaidi, kwamba tumekuja kwenu Vijana, Wanawake na Wazee wetu wa Dar es salaam kuzungumza nanyi juu ya jambo hili zito, kukikabidhi kwenu chama chetu cha ACT Wazalendo.

Ndugu Wanadar es salaam

Tumewaiteni leo tukiwa na mambo Machache Muhimu kwa chama chetu na Taifa kwa ujumla ambayo tungependa kuyaeleza kwenu na kwa Umma wa Watanzania wenzetu kwa ujumla.

Kama mnakumbuka Machi 29 mwaka huu tulizindua chama chetu hapa jijini Dar es salaam na baada ya uzinduzi huo tulifanya ziara katika mikoa 22 na baadhi ya majimbo nchini, pia tokea wakati huo operesheni mbali mbali za chama zimekuwa zikifanyika wakati wote huo, ikiwa ni pamoja na kuzindua Azimio la Tabora – Tamko la Kimuongozo, Kiitikadi, Kisera na Kimaadli la Chama chetu ambalo limehuisha Azimio la Arusha. Tunawashuku sana wananchi wa Mikoa mbalimbali kwa mapokezi yao makubwa waliyotupa pamoja na kulipokea kwao kwa mikono miwili Azimio la Tabora.

Ndugu Wana-Dar es salaam

Tuna uchumi unaojenga Matabaka. Hivi sasa uchumi wetu umeshikwa na watu wachache hususan wafanyabiashara ambao pia wameshika siasa au kwa wao kushiriki kwenye siasa moja kwa moja au kufadhili wanasiasa wa kutetea maslahi yao.

Tuna kansa ya ufisadi ambapo watu hutumia nafasi zao za uongozi kujilimbikizia mali. Ufisadi ni tatizo zaidi la viongozi walioshika madaraka ya umma. Tunahuisha Azimio kwa lengo la kusimika miiko ya Uongozi wa Umma ambayo itakuwa msingi mkuu wa mapambano dhidi ya ufisadi.

Azimio la Tabora kwa kiasi kikubwa linakuja kuleta Mwarobaini wa Kimaadili juu ya suala husika, kwa kuwa linahuisha Azimio la Arusha kwa kurudisha miiko ya Uongozi na Utumishi wa Umma, na pia kujenga misingi ya uchumi wa Ujamaa wa kisasa utakaojikita katika kuongeza uzalishaji mali na ugawaji sawa wa keki ya Taifa na hivyo kupunguza matabaka nchini kwetu.

Ndugu Wanadar es salaam

Mtakumbuka kuwa Mwezi Novemba mwaka 2012 Bunge lilipitisha Azimio namba Tisa la Mwaka 2012 ambalo lilielekeza Serikali kufanya uchunguzi kuhusu Watanzania na makampuni ya kitanzania waliotorosha na kuficha fedha kwenye mabenki ughaibuni. Uchunguzi pia ulikuwa uhusike na Mali za Watanzania zilizopo nje ya nchi katika juhudi za kuhakikisha kuwa fedha chafu na ufichwaji wake vinakomeshwa. Bunge lilitoa muda wa miezi sita kwa Serikali kufanya uchunguzi huo. Mwaka mzima ulipita Serikali haikutoa maelezo yeyote na baada ya kubanwa ndani ya Bunge Serikali ikaomba miezi sita zaidi. Hata hivyo mpaka leo Serikali haijatoa kauli yeyote kuhusu taarifa hiyo ya uchunguzi.

Takwimu zinazohusu fedha za Watanzania nje ya nchi bado sio za uhakika sana. Kwa mfano, Taarifa ya Serikali ya kisiwa cha Jersey kilicho chini ya himaya ya Uingereza inaonyesha kuwa Fedha na Mali za Watanzania katika mabenki kisiwani humo ni paundi za Uingereza 440 milioni ambazo kwa bei ya sasa ni sawa na shilingi za kitanzania 1.4 trilioni. Vile vile taarifa rasmi ya Benki Kuu ya Uswiss inaonesha kuwa Watanzania wenye akaunti katika mabenki ya nchi hizo imefikia dola za kimarekani 304 milioni kutoka dola 213 milioni mwaka 2012. Hatuna takwimu kwa nchi nyingine duniani.

Fedha hizi zaweza kuwa halali ama haramu. Kuna watu ama ni Watanzania wanaishi ughaibuni na kufanya kazi huko ni lazima wawe na akaunti za benki. Pia kuna Watanzania ambao ni wafanyabiashara na masharti ya biashara zao ni lazima wawe na akaunti katika mabenki ya nje. Hata hivyo mfumo mzima wa ufunguaji na ufungaji wa akaunti katika mabenki ya nje umewekewa masharti ya kisheria na kibali cha Benki Kuu kinahitajika. Kuna Watanzania wenye kuficha fedha ambazo zimepatikana kwa rushwa na biashara haramu mbalimbali kama vile madawa ya kulevya na biashara ya nje ambayo haingii kwenye rekodi za Benki Kuu. Iwapo Serikali ingefanya uchunguzi na kuukamilisha tungeweza kujua kwa hakika katika orodha ya watu wenye akaunti nje ni wepi wana fedha zao halali na wepi wana fedha haramu. Serikali imetunyima haki hiyo kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa. Bunge la Kumi linavunjwa mnamo tarehe 9 Julai mwaka huu na hakuna dalili yeyote ya Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi ndani ya bunge kama ilivyoagizwa na Bunge.

Ndugu Wanadar es salaam

Mara baada ya Azimio la Bunge kutolewa mwaka 2012 nilipata mialiko kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwenda kushirikiana nao katika jambo hili. Jambo hili sio changamoto ya Tanzania peke yake. Nchi mbalimbali duniani kama Marekani, India, Nigeria, Ujerumani nk zinahangaika na jambo hili. Kila nchi ilichukua hatua inavyoona yenyewe inafaa ili kukabiliana na suala hili. Hatua ya Tanzania kufanya uchunguzi kufuatia agizo la Bunge ilikuwa ni ya kipekee na wachunguzi wengi wa kimataifa wakashawishika kuwa Tanzania itakuwa nchi ya mfano katika kupambana na tatizo la utoroshwaji wa fedha na ukwepaji wa kodi.

Katika safari hizo mbalimbali nilizofanya duniani nilipata taarifa ambazo niliziwasilisha Serikalini kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wetu. Jaji mmoja wa Mahakama ya Ufaransa ambaye anafanya uchunguzi dhidi ya Benki ya HSBC alinipa ushirikiano wa kutosha na taarifa muhimu ambazo niliziwasilisha Serikalini ili waweze kuchukua hatua. Serikali haijafanya kitu. Miongoni mwa taarifa hizo ni orodha ya Watanzania 99 wenye akaunti 288 katika tawi moja la Benki ya HSBC nchini Switzerland. Orodha hiyo niliiwasilisha kwa Gavana wa Benki Kuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya uchunguzi. Serikali mpaka sasa ninapozungumza nanyi haijatoa Taarifa licha ya kupewa kila aina ya ushirikiano.

Nimeamua leo kuiweka orodha hii wazi kama shinikizo kwa Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo. Kila mwandishi wa habari aliyepo kwenye mkutano huu nimempatia bahasha yenye majina 99 ya Watanzania au watu wenye mahusiano na Tanzania ambao wana akaunti HSBC ya Uswiss. Jumla ya akiba katika akaunti Benki hii pekee ni dola za kimarekani 114 milioni.

Narejea kusema kuwa sisi hatuna uhakika kama fedha hizi ni halali au haramu. Kuna ambazo zinahusiana na washirika 2 wa kashfa ya rada ambao ni Sailesh Vithlani aliyetuhumiwa kumhonga Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi na mmiliki wa kampuni ya Shivacom. Hizi zaweza kuhusishwa na ufisadi wa rada. Hata hivyo nyingine ni ngumu sana kusema zinatokana na nini kama vyombo vyetu vya uchunguzi vikiendelea kukalia kimya taarifa ya uchunguzi. Wito wangu ni kwa Serikali kuwasilisha taarifa ile Bungeni ili wenye fedha halali watofautishwe na wenye fedha haramu na wale wenye haramu wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwemo fedha hizo kurejeshwa nchini.

Ndugu Wanadar es salaam

Suala hili ni tone tu ya namna tatizo la kimaadili lilivyo kubwa nchini, na pia namna lilivyo na athari kisiasa na kiuchumi, ni suala ambalo kama Taifa tunapaswa kulitafutia dawa, Chama cha ACT Wazalendo tumewaletea dawa ya tatizo – Miiko ya Uongozi kama ilivyoainishwa katika katika Azimio la Tabora.

Ahsanteni sana.

Majina ya wenye mahela Uswisi.



Picha za Mrembo na Mwigizaji JACK WOLPER Akipiga Mbizi Baharini Hizi Hapa

$
0
0

 I can feel love all over me

 Pain is inevitable, suffering is optional... #Ciroc life .... Good morning fans.


LEMUTUZ 'Jikombe na Jipendekeza kwa Watu Wenye Akili Kubwa na Wewe Uwe na Akili Kubwa...Achana na Mburalazzz Wanaompigia Kura Davido'

$
0
0
LEMUTUZ  STRAIGHT TALK:- Coffee time live at the Office of my Super Friend Le Mpiganaji Bilionea Davis Mosha...sasa hivi yupo Downtown Moshi but all the plans comes from here hahah halafu hapa nasafisha nyota pia U know....a hahaha it is also my SUPER DREAM one day kuwa na BIG MONEY ya kuwa na SUPER OFFICE LIKE THIS..now akili ndogo ni kwamba NINAJIDAI NA KUJIPENDEKEZA ila AKILI KUBWAZZ like mine ni UKIWA KARIBU NA WARIDI UTANUKIA WARIDI TU hahaha na UKIWA KARIBU NA super gademu mburulazzz with no gademu brain guess what? na wewe utakuwa tu kama sio tayari....na kama huamini pitia hapa Instagram utakuta mburulazzz Mkubwa anafuatwa na followers kibao mburulazzz kama yeye hahaha yaani hamna mwenye nafuu kiongozi ni empty brain so are followers . wanachopigania hakieleweki na wanachosimamia hakieleweki in fact hata wanachofanya hakieleweki una mfollow mtu hata Ofisi hana hahaha unakuwa na rafiki kazi yake kukunulia mapombe tu huwezi kushituka kuwa akili yake imeoza so anataka na yako ioze kama yeye...people wachana na marafiki wajinga kama it takes KUJIKOMBA kuwa na MARAFIKI wenye AKILI KUBWAZZ do that cha muhimu ni MATOKEO sio PROCESS watu watakuheshimu ukionyesha matokeo like me nimerudi Majuu na AKILI KUBWAZZ hapa bongo imekubalika na Matajiri wengi wenye makampuni makubwa na sasa in just 4 years na Mimi Nina Kampuni yangu hata kama ndogo lakini Mimi na Hawa Matajiri wakubwa wote tunajisajili BRELA na TRA ganda la Certificates ni lile lile na wakiitwa wenye kampuni na Mimi nachechemea naenda hahahaha....wakiitwa watu wanaoajiri wafanyakazi na Mimi nachechemea naenda hahahaha ndio maana ya AKILI KUBWAZZ unajkomba kwa wenye makampuni na wewe unafungua yako ...jikombe kwa mburulazzz wakufundishe namna ya kumpigia kura Davido hahahaha gademu mburulazzz dead brain wamekufwa mazafantazzz akili ndogo NDIO MAANA NEVER IN MY LIFE KUJIHUSISHA NA akili ndogo nasema NEVER! hata kuwa follow siwezi cause NITAKUFWAZZ HAHA KAMA gademu WAO! - le Mutuz

Ruge Afunguka Kwanini Baadhi ya Wasanii Wanamchukia...Adai Lady Jay Dee Waliniumiza Kichwa Sana

$
0
0
Ruge Mutahaba anaweza kuwa ametajwa kwenye masakata mengi ya ubaya dhidi ya wasanii, akibebeshwa lawama kuliko mtu mwingine yeyote kwenye tasnia ya muziki, lakini kwake ni mambo matatu tu ndiyo anaona yamemsumbua sana.

Mtaje Mr ll, mtaje Lady Jay Dee na mtaje Q Chief, utakuwa umemkumbusha mbali mkurugenzi huyo wa vipindi wa Clouds Media, ambaye pia amefanya kazi ya kusimamia wasanii wengi na ndiye kiongozi wa chuo cha Tanzania House of Talents (THT).

Katika makala haya, Ruge anazungumzia mambo mbalimbali kwenye sanaa na kutaja migogoro mitatu ambayo hataisahau tangu aanze kujihusisha na shughuli za burudani.

Endelea…

Swali: Baadhi ya wasanii ambao waliwahi kufanya kazi na wewe wamekuwa akilalamika mara baada ya kutoka katika uongozi wako, kwamba uliwanyonya, walidhulumiwa na mengine mengi kuna ukweli kuhusu haya?

Ruge: Sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kusema jambo hivihivi. Mfano THT haina tofauti na chuo kingine.

Inatakiwa uhitimu na uende. Ukiamua kuendelea kufanya mambo yako pale hukatazwi na wala hakuna anayekufukuza, lakini lazima uondoke na wengine wapate nafasi.

Sasa ukiona mtu ameondoka na kisha anashuka kimuziki ni yeye mwenyewe ameshindwa kujisimamia.Nimefanya kazi na wengine wengi kama kina Patricia Hilary ambao walifanikiwa kujenga nyumba zao. Iweje starehe zako unilalamikie mimi?

Swali: Unadhani ni kwanini wanakutusi?

Ruge: Nilichokigundua ni kwamba hawa wasanii wanaopita kulalamika huko pembeni wanashindwa kujisimamia kutokana na mambo wanayoyafanya. Wengi wao ni kama watoto wanatafuta pa kulilia hawapapati, wanatafuta mtu wa kuongea naye lakini hawana.

Mwingine alisema anapata Sh40 milioni kwa mwezi aliviambia vyombo vya habari kwamba kila wiki anatengeneza Sh10 milioni, wewe mtu wa kupata hizo kwa mwezi ni wa kunilalamikia mimi?

Sasa kama alipata milioni 40 kwa mwezi, kwa mwaka mzima hukuwekeza usinilaumu. Jilaumu kwa sababu kwa mwaka ni Sh480 milioni, mimi mwenyewe siwezi kupata faida hiyo kwenye biashara zangu.

Ninavyoona waandishi wengi hawafanyi tathmini kuhusu hawa watu wanaolalamika, kuna watu wakubwa ambao nilishawahi kufanya nao kazi, leo hii nikiwaitia kazi wanakataa nisiwalipe fedha. Kuna kina Issa Matona, Bi Shakira, Mwanahela, Patricia Hilarry mnawaangalia hawa au hao wengine?

Juma Nature amemtukana Fella mara ngapi? Kina Keisha, MB Dogg wamemtukana Tale mara ngapi? Mb Dogg alikuja na malapa hapa na wimbo wake wa “Latifa”, Tale akaniambia tumsimamie huyu kijana.

Swali: Ni kweli kwamba wasanii wakiondoka katika usimamizi wanabaniwa katika vituo vyenu vya redio na sehemu nyingine?

Ruge: Ninarudi palepale hawawezi kujisimamia. Wengine wanachosahau ni kwamba walikosea hawakupata baraka.

Mwishowe wanarudi na kusema kwamba walionewa, wanabaniwa kwa sababu ya mtu fulani, si sahihi. Mimi mwenyewe napoona mtu anamtukana mwingine, naangalia mpaka nakasirika.

Hii kitu ipo kila mahali sema ni habari zaidi ikitokea kwenye muziki wa bongo fleva. Kwanini Clouds? Mbona Mengi aliwapiga stop Ali Kiba na Ray C kwa sababu hakwenda kwenye hafla ya walemavu, mbona haikuwa dili? Magic FM walimpiga stop Diamond kwa miaka miwili?

Kwanini sisi tukiamua kwamba hatupigi wimbo wa msanii fulani inakuwa ni ishu kubwa na ndiyo habari ya mjini? Kama ni sera ya ndani ya Clouds, kwa nini Ruge Mutahaba anakuwa wa kwanza kulaumiwa?

Swali: Ni bifu ngapi tano za wasanii ambazo zilikusumbua zaidi?

Ruge: Mimi nimekuwa nikichukulia kama kunisumbua kwa sababu sijawahi kuwa na bifu na msanii, lakini wao wanakuwa nazo kwangu. Nawashangaa watu wenye mabifu. Mfano kwangu bifu lililonishangaza au kunisumbua ni lile la ANTI VIRUS.

Si kwa sababu ya Sugu, bali wale waliomfuata. Kwa sababu kuna watu ambao waliingia kiasi kwamba nikawa nashangaa hata walitokea wapi. Kwa sababu nusu yao sikuwa nawajua ni kina nani.

Nilishangaa ni kina nani ambao wanaweza kuingia kwenye ugomvi na mtu wasiyemjua? Wapo katika maisha gani ya kuambiwa tu ‘gombana na mtu fulani’, na wewe ukagombana na tena unatukana? Kilichokuwa kinanitatiza ni chanzo ambacho (hao watu) hawakukijua na wala hawakutaka kukijua.

Na kwa sababu nilikuwa najua tatizo la Sugu, haikunisumbua. Tatizo ni hao wengine ambao sikujua wametoka wapi.

Kwangu mimi sikuwa na ugomvi na mtu. Bifu ni kitu ambacho kipo pande zote mbili. Kama kwako hauna bifu kunakuwa hakuna, labda kama upande wa pili umeamua kuwe na bifu.

Ugomvi wa pili ni dhidi ya Lady Jaydee. Ilikuwa ya ajabu sana kwa sababu maneno mengi yalianzia mitandaoni hadi tukaamua kufungua kesi, ambayo hadi leo haijaisha mahakamania. Kinachotakiwa sasa ni yeye kuomba radhi, lakini mahakamani hatokei.

Haya mambo ni bahati mbaya yalishatokea, kwa hiyo mtu yeyote akitaka kusema jambo lolote lenye malalamiko lazima amtaje Ruge ili kitu chake kijulikane zaidi.

Pia Q Chief aliwahi kunitukana sana kipindi cha msiba wa Mangwea, nikamfuata na kumwambia unanitukana, nitukane basi mpaka hamu yako iishe nikiwa hapa hapa. Niliwahi kuambiwa kwamba nimezuia kibali cha (mwimbaji kutoka Nigeria) Davido Basata, siyo kweli. Kwa bahati mbaya najua vitu vingi.

Mtu anaweza kufanya jambo akakataliwa Basata mimi nikaenda nikafanikiwa akadhani kwamba nimembania, kumbe hajui sheria na mipaka ya Basata ni ipi. na kwingine ni kupi.

Sisi tulitaka kunyimwa kibali, tukawaambia Basata kwamba wakitunyima tunakwenda mbele kwa waziri ndiyo utaratibu. Sasa mwingine akinyimwa anadhani tumewabania.


AY ndiye aliyefanikisha collabo yangu na Davido na kuniunganisha na Godfather – Diamond

$
0
0
AY amefungua njia ya mafanikio kwa wasanii wengi wa Tanzania. Miongoni mwa watu walionufaika na mashavu yake ni Diamond.

Katika ujumbe wake wa kumpongeza AY kwenye siku yake ya kuzaliwa Jumapili hii, Diamond amedai kuwa AY ndiye aliyemuunganisha na Davido hadi wakafanya remix ya wimbo wake ‘Number One’ uliobadilisha maisha yake.

“Misingi na Daraja Imara la kimataifa ulio tujengea na unayozidi kutujengea ndio leo inatusaidia vijana wako nasi kuweza kupenyeza na kutangaza kazi zetu kimataifa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.

“Pengine watu hawajui kuwa wewe ndio uliyeniwezeshea kufanikisha Collabo langu na Davido, Kuniunga na Godfather na vingi ambavyo naamini ndio Mwanzo wa safari yangu ya Kimataifa… Nakuheshim sana Brother, na daima nitahakikisha sikuangushiemoji…Happy birthday Bro.”

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, AY ameandika:

July 5, 1982 Ambwene Yessayah alizaliwa. Namshukuru Mungu kwa kuiona siku hii ya leo. Nawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani. Mungu awalaze mahali pema peponi. Natamani mama yangu angekuwa hai aone jinsi kijana wake alivyokuwa mkubwa na pengine afurahie jasho lake la kunizaa, kunilea na kunitunza.

Nawashukuru wote walio na mchango mkubwa kwenye maisha yangu, ni wengi siwezi kuwamaliza kuwataja. Navikushukuru vyombo vya habari vyote kwa support kubwa inayoendelea kunipa. Nakushukuru pia wewe shabiki yangu kwa kuendelea kuniunga mkono. Thank You!!

Breaking News:Dr Shein Apitishwa Kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM.

$
0
0
Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa kauli moja imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa Zanzibar wanounda kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika ofisi kuu ya CCM na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena  kiti hicho cha urais baada ya wajumbe karibu 102  ambao ni aslimia 83  kuridhia Dr Shein agombee.
Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao ambapo kiti hicho kilishikwa kwa muda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu wa rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein aliwahidi wanachama wa CCM kuwa  uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza ilani ya CCM ya kuitumikia Zanzibar.
Katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar akizungumza baada ya kikao hicho alisema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala la majimbo,wao wanasubiri maamuzi ya tume na wako tayari kwa umauzi wowote utakaotolewa na tume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo mapya leo asubuhi.
Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na kamati maalum ni hatua ya kwanza na sasa shuguhli yote inahamia Dodoma ambapo jina la Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar inaamuliwa na NEC na siyo na mkutano mkuu waccm.

Pamoja na Upinzani Kuugomea na Wabunge 43 Kusimamishwa, Bunge Laupitisha Muswada wa Petroli wa Mwaka 2015 Uwe Sheria

$
0
0

Pamoja na Upinzani Kuugomea na Wabunge 43 Kusimamishwa, Bunge Laupitisha Muswada wa Petroli wa Mwaka 2015 Uwe Sheria ...Je una Maoni Gani Kuhusu Kupitishwa kwa Nguvu kwa Mswada Huo bila kuwepo kwa Wabunge wa Upinzani?

Chama cha Wanasheria Kufungua Kesi Mahakamani Kudai Kutenguliwa Kwa Miswada ya Petroli na Gesi!

$
0
0
Chama cha wanasheria wa mazingira-LEAT-kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa kimepanga kufungua kesi mahakamani kudai kutenguliwa kwa miswada ya Petroli wa 2015 na mswada wa kumudu ya mafuta na gesi kutokana na kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 27 inayotaka rasilimali za nchi zitumike kwa maslahi ya watanzania wote.

Akizungumza na waandsihi wa habari mkurugenzi wa FOE Tanzania Dokta Rugemeleza Nshala amesema kulikuwa hakuna sababu ya miswada hiyo kupelekwa kwa hati ya dharura bila kuhusisha maoni ya wadau ambao wengine ni wataalam katika sekta hiyo na kusisitiza iwapo sheria hizo zitapishwa watanzania wataendelea kutonufaika kwa rasilimali za nchi yao kwa miaka mingi zaidi huku wawekezaji wakiendelea kuchota utajiri wa rasimali za watanzania.

Aidha wakizungumzia kuhusu rasilimali za madini baadhi ya wanasheria kutoka nchi za Afrika kusini, Togo, Nigeria, Uganda na Cameroon wamesema viongozi wanapashwa kutambua rasilimali za mafuta, gesi na madini ni mali ya wananchi wote, hivyo wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu namna bora zinavyoweza kutumika kwa maslahi ya taifa, badala ya viongozi kufanya maamuzi binafsi bila ya ushiriki wa wananchi wote.

Chanzo: ITV

Hizi Ndizo Rekodi Anazojivunia Zitto Kabwe, Hakuna Mbunge Yeyote Aliwahi Kuzivunja

$
0
0
Hizi ndizi Rekodi za Zitto kiutendaji tangu alipokuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini mwaka 2005-2015.
Yeyote anaempinga Zitto Kabwe ,aweke rekodi Mbadala wa Zitto.
Weka rekodi ya mtu mwenye rekodi zaidi ya hizi.
Naomba niwaletee kwa muhtasari kabisa baadhi ya kazi ambazo Ndugu Zitto Kabwe amezifanya katika kusukuma mbele guruduma la maendeleo katika nchi yetu.

1. MABADILIKO SEKTA YA MADINI
Zitto alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa mbunge mwaka 2005 akiwakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini ambalo halina mgodi hata mmoja wa madini ukiachana na wachimbaji wadogo wa udongo wa Pemba ambao una soko kubwa hapa Kariakoo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo ajenda inayomtambulisha Zitto Kabwe kwa Taifa ni ajenda ya mabadiliko makubwa aliyoanzisha katika sekta ya Madini nyakati ambayo hakuna mwanasiasa aliyethubutu kukosoa sera za uwekezaji kwa namna aliyofanya. Baada ya kudokezwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Bwana Nazir Karamagi amesaini mkataba mpya wa Madini akiwa hotelini nchini Uingereza, Zitto alimtaka Waziri kujieleza ndani ya Bunge kuhusu mkataba huo na masharti yake ya kikodi. Waziri huyo aliposhindwa Zitto aliwasilisha Hoja Binafsi Bungeni (akiwa mbunge wa kwanza kufanya hivyo katika Bunge la Tisa na la Nane kwa pamoja). Hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa ubunge kwa miezi 4. Hata hivyo mnamo Septemba 10, 2007 alitangaza Azimio la Songea lililomshinikiza Rais Jakaya Kikwete kuunda Kamati ya Bomani ili kupitia mikataba yote ya Madini nchini. Kutokana na kazi yake hiyo leo Tanzania ina Sera mpya ya Madini na Sheria mpya ya Madini ambayo imeboresha nafasi ya Tanzania kufaidika na Madini, imeruhusu kisheria Serikali kuwa na hisa kwenye migodi ( na hivi tunavyoongea, kwa mfano, sasa Serikali inamiliki 50% ya Mgodi wa TanzaniteOne). Makampuni ya Madini ambayo yalikuwa yanatangaza hasara kila mwaka leo yanalipa kodi ya Mapato na Halmashauri zenye migodi zinalipwa ushuru wa huduma wa mabilioni ya fedha. Huyu ndiyo Kiongozi wetu wa ACT Wazalendo. Hawa ndio Viongozi Taifa hili linawataka. Viongozi wanaotenda na kutoa majawabu ya changamoto za nchi. Sio Viongozi wanaolaumu tu eti wakisubiri kushika dola ndio watende. Nani anayebisha rekodi hii?

2. KUZUIA UBINAFSISHAJI WA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC )
Zitto Kabwe alikuwa Waziri Kivuli wa Mipango na Uchumi mwaka 2006 wakati Shirika la Bima la Taifa likiwa kwenye mchakato wa Ubinafsishaji. Wafanyakazi wa TUICO Tawi la Bima walimfuata wakielezea kwa ushahidi namna mali za Shirika zilivyopangwa kuuzwa na wajanja wachache kutaka kujiuzia Shirika na Mali zake hasa jengo la kitega uchumi kwa bei ya kutupwa. Zitto aliwakilisha hoja hiyo kwenye Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Abdallah Kigoda na kuishawishi Kamati kukataa ubinafsishaji wa NIC na badala yake kuunda kikosi kazi cha kurekebisha Shirika na liendelee kuwa Mali ya Umma. Mwezi Novemba Mwaka 2006 Baraza la Mawaziri lilikubaliana na hoja za Zitto alizotoa kwenye Kamati ya Bunge na ndani ya Bunge na kuamua kuliondoa Shirika kwenye mchakato wa ubinafsishaji na leo hii Shirika limebaki kuwa la Umma na limeanza kurudi kwenye hali yake. Aliendelea kulisaidia Shirika la Bima kwa kuagiza (akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ) kuwa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma yaweke Bima kupitia Shirika la Bima la Taifa na agizo hilo kutekelezwa na Mashirika mengi ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania. Sio Bima tu, Zitto akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma aliagiza kuondolewa katika orodha ya ubinafsishaji Shirika la STAMICO ili liweze kushiriki kikamilifu katika sekta ya Madini na liliondolewa. Huo ndio Ujamaa wa kidemokrasia ambao Chama chetu cha ACT-Wazalendo kinautangaza, na huyo ndio Kiongozi wetu ambaye ana uzalendo wa dhati kwa mali za Watanzania. Nani anayebisha rekodi hii?

3. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Mwaka 2008/2009 Zitto Kabwe aliweka rekodi nyingine ya kuwa Mbunge wa kwanza kuzungumzia mabadiliko ya sheria ya viongozi wa umma ili kuipa meno secretariat ya maadili ya viongozi na kutengenisha biashara na siasa. Alipeleka Bungeni Muswada Binafsi wa Sheria ili kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria Maadili. Hata hivyo muswada ule ulizuiwa na Serikali kuingia Bungeni licha ya kukamilisha kila hatua iliyopaswa. Leo hii Chama chetu kinazungumzia kurejesha Miiko ya Viongozi kuna watu wanadhani Zitto kaanza haya hivi sasa, la hasha. Huu ni mwendelezo wa yale aliyokuwa anaamini miaka kadhaa iliyopita na kwa kuwa yeye anapenda kutembea anayoyasema alitushawishi wenzake kufanya Miiko ya Viongozi kuwa sehemu ya Katiba ya Chama chetu. Yeye ni Kiongozi wa kwanza wa kisiasa kuweka hadharani Mali na Madeni yake hapa nchini. ACT Wazalendo ni chama pekee cha siasa hapa nchini ambacho Viongozi wake wanatakiwa kikatiba kutangaza Mali zao, Madeni yao na Maslahi yao ya kibishara. Nani anabisha rekodi hii?

4. UKAGUZI WA MAHESABU WA VYAMA VYA SIASA
Katika kuhakikisha kuwa kila senti ya fedha ya umma inakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, Ndugu Zitto Kabwe aliwasilisha Bungeni mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria namba 5 ya Mwaka 1992 na kuwezesha CAG kukagua fedha za vyama ambazo zinatoka Serikalini kama ruzuku. Sheria ya Vyama vya siasa inataka kila Mwaka Serikali kutenga kiwango kisichozidi asilimia mbili (2%) ya Bajeti ya Serikali kama ruzuku kwa vyama vya siasa. Vyama hupewa wastani wa Shilingi bilioni 20 kila mwaka na kugawana miongoni mwao lakini fedha hizi zilikuwa hazikaguliwi kinyume na Sheria za Fedha. Baada ya Sheria hiyo kupitishwa na Bunge mwaka 2009, Zitto alisimama kidete kuhakikisha inatekelezwa jambo ambalo lilimletea uhasama mkubwa sana na viongozi wenzake katika chama chake cha zamani akiwa Naibu Katibu Mkuu. Zitto alipigana kwa kushirikiana na Wazalendo wenzake katika Kamati ya Bunge ya PAC na kufanikiwa na hivi sasa vyama vyote vinakaguliwa na kuweka rekodi nyingine katika nchi nyingi za Afrika. Kwa kazi hii iliyotukuka Zitto Kabwe amedhibiti fedha za umma kwa vyama vya siasa na hivi sasa taarifa za mahesabu ya vyama ipo wazi, na tumeona vyama vyote vikiwa na hati chafu, vikiwemo vyama vya upinzani vya zamani. Ni wajibu wa wanachama wa vyama hivyo kuwawajibisha viongozi wao wanaogeuza fedha za ruzuku kuwa ni fedha zao binafsi. Nani anabishia rekodi hiyo ya Kiongozi wetu?

5. KUFUFUA ZAO LA MKONGE
Mwaka 2012 Zitto Kabwe aliweka rekodi nyingine tena akiwa mbunge wa kwanza katika Bunge la 10 kuwasilisha Hoja Binafsi. Aliwasilisha Hoja Binafsini Bungeni akitaka Serikali kufufua Kilimo cha Mkonge kwa kuwanyanganya wawekezaji wakubwa mashamba waliyobinafsishiwa na kuyaacha bila kulimwa na badala yake mashamba yale wapewe wakulima wadogo. Zitto alitaka kubadilisha mfumo wa kulima Mkonge kutoka mashamba makubwa yanayomilikiwa na tajiri mmoja na kulimwa na manamba mamia na kwenda kwenye mfumo ambao wakulima wadogo wadogo wanalima Mkonge na hivyo kushirikisha wananchi wengi zaidi kwenye uchumi wao. Hoja hiyo ilipingwa na Wabunge kutoka Tanga lakini iliungwa mkono sana na wananchi wa mkoa huo na hivyo kumwona Zitto kama mwakilishi wao licha ya kwamba alikuwa akiwakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Katika Chama chetu ajenda ya kumilikisha Ardhi wananchi ni ajenda kubwa na ACT Wazalendo kimekua chama cha kwanza nchini kutangaza kinagaubaga kuwa kitazuia uporaji wa Ardhi na kumilikisha wananchi ardhi yao wenyewe. Nani anabishia rekodi hiyo?

6. KURASMISHA KAZI ZA SANAA NA BURUDANI NCHINI
Kwa muda mrefu sana wadau wa tasnia ya sanaa na burudani nchini walikuwa wanalalamika kazi zao kutokuwa rasmi na hivyo kuibiwa na mchango wao katika uchumi kutotambuliwa. Mwaka 2012 Zitto Kabwe akiwa Waziri Kivuli wa Fedha alifanya kampeni maalumu ya kuhakikisha kuwa wasanii hawanyonywi na kazi zao kutambuliwa rasmi. Aliwasilisha Bungeni mabadiliko ya Sheria ya Ushuru bidhaa ili kutambua rasmi kazi za sanaa na burudani na kuhakikisha kuwa wasanii wanalipwa wanavyostahili katika biashara ya miito ya simu. Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge na Mamlaka ya Mapato Tanzania ikaanza kutoa stempu rasmi katika CDs za kazi za sanaa ili kudhibiti wazalishaji kuwanyonya wasanii. Katika Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya mwaka 2015 tasnia ya Sanaa na Burudani imekuwa sekta rasmi ya Uchumi na imeripotiwa kuwa sasa ina thamani ya shilingi 270 bilioni kama mchango wake katika Pato la Taifa. Hivi sasa Wasanii wanafaidika maradufu kwa kazi zao kuuzwa kama miito ya simu na wengine wanapata mamilioni ya shilingi na kuboresha maisha yao kwa jasho lao. Nani anabisha rekodi hii?

7. KUDHIBITI UKWEPAJI KODI NA MISAMAHA YA KODI
Wawekezaji kutoka nje wamekuwa wakiibia nchi yetu kwa kubadilisha badilisha majina ya makampuni yao na kubadili wamiliki bila ya kulipa kodi hapa nchini. Watanzania mnakumbuka jinsi majina ya mahoteli makubwa yalivyokuwa yakibadilishwa. Kwa mfano kutoka Sheraton kwenda Moevenpick na kwenda Serena sasa. Makampuni ya Simu yalivyokuwa yakibadilishwa. Kwa mfano kutoka Mobitel kwenda Buzz kwenda Tigo. Vile vile kutoka Celtel kwenda Zain na kwenda Airtel. Haya yamekuwa yakitokea kwenye maeneo mengi zaidi ya haya. Yote haya yalitokea bila ya Serikali kupata kodi yeyote. Kwenye mauzo ya Zain kwenda Airtel Serikali ilipoteza dola za Kimarekani 312 milioni ( zaidi ya shilingi bilioni 600 kwa bei za sasa za dola ). Kwa uchungu kwa nchi yake Zitto Kabwe aliwasilisha Bungeni muswada wa sheria wa kurekebisha sheria ya kodi ya Mapato na kuanzisha tena kodi ya ongezeko la mtaji ( Capital Gains Tax ). Marekebisho hayo yalipitishwa na Bunge kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2012 na mwaka huo huo Tanzania ilipata mapato ya shilingi bilioni 50 kwa mauzo ya Kampuni ya BP kwenda PUMA. Mwaka 2014 Tanzania ilipata dola za kimarekani 222 milioni ( zaidi ya tshs 450 bilioni )kwa mauzo ya sehemu ya vitalu vya gesi asilia vya kampuni ya Ophir kwenda kampuni ya Pavilion ya Singapore.
Zaidi ya hapo Zitto na wazalendo wenzake katika Kamati ya PAC walitoa maagizo ya kuhakikisha kuwa Misamaha ya kodi yote inakaguliwa na ukaguzi wake kuwekwa wazi ili kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania CAG anakagua misahamaha ya kodi na PAC iliweka wazi taarifa ya kwanza ya ukaguzi wa misamaha ya kodi. Nani anabishia rekodi hizi?

8. MABILIONI YA USWISS
Mwaka 2012 mwezi Novemba Zitto Kabwe aliwasilisha Bungeni Hoja Binafsi kuhusu mabilioni ya Uswisi ikiwa na lengo la kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu Watanzania wanaoficha fedha nje ya nchi kinyume cha sheria. Bunge lilipitisha hoja hii binafsi na kuitaka Serikali kufanya uchunguzi kuhusu Watanzania wanaotorosha fedha kwenda nje na kuchukua hatua stahiki za kisheria. Tanzania iliingia katika rekodi ya kuwa nchi ya kwanza katika nchi za Jumuiya ya SADC kupitisha Azimio la Bunge kuhusu suala la utoroshaji wa fedha. Licha ya kwamba Serikali haijatoa taarifa yake miaka miwili sasa toka Azimio la Bunge namba 9 la mwaka 2012, na baada ya danadana ya muda mrefu kutoka vyombo vinavyohusika Kiongozi wetu Zitto Kabwe ameamua leo kupasua jipu la hoja hiyo kwa kuweka wazi orodha ya kwanza ya Watanzania 99 wenye akaunti katika Benki ya HSBC ya Uswiss. Uongozi ni umakini, na sio kukurupuka na kujitafutia sifa za harakaharaka. Ilikuwa ni muhimu Ndugu Kabwe kufuata taratibu zote kabla ya kuanika majina hayo hadharani. Sasa leo baada ya kujiridhisha pasipo shaka atayaanika majina hayo hadharani na wale waliokuwa wanambeza kwamba kashindwa wanyamaze milele! Huyo ndio Zitto, mwenye uvumilivu na ujasiri usio kifani. Anatenda anayosema. Nani anabisha rekodi hii?

9. KUWAJIBISHA MAWAZIRI
Katika historia ya Tanzania ni Wabunge wawili tu walioweza kutoa hoja zilizopelekea Mawaziri wengi kuondolewa madarakani kwa mpigo. Ni Zitto Kabwe na Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye aliongoza kamati teule ya Bunge iliyochunguza Mkataba wa kampuni feki ya kufua umeme ya Richmond. Hoja hii ilipelekea Waziri Mkuu kuwajibika kwa kujiuzulu na hivyo kumlazimisha Rais wa Jamhuri ya Muungano kuunda upya Serikali kwa kuteua Waziri Mkuu mwingine.
Zitto ana rekodi ya kipekee. Kwanza mwaka 2012 baada ya Taarifa ya CAG kuonyesha madudu katika matumizi ya fedha za umma, Zitto alikusanya sahihi za wabunge 75 na kuandika hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Shinikizo hili lilipelekea Rais kufukuza kazi mawaziri 8 ambao Wizara zao zilitajwa kuwa na mahesabu machafu. Pili mwaka 2013 baada ya Kamati ya Mali Asili na Mazingira kutoa taarifa yake Bungeni kuhusu Operesheni Tokomeza, Zitto alisimama ndani ya Bunge na kubadilisha mjadala kwa kutaka Mawaziri wote ambao watendaji wao walitesa wananchi kuwajibika. Mawaziri 4 waliwajibika.
Tatu, mwaka 2014 katika Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC kuhusu uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ya Benki ya Tanzania, Zitto na wazalendo wenzake wa kamati hiyo walipelekea Mawaziri wawili maarufu kama mawaziri wa Escrow na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwajibika. Uwajibikaji umekuwa ni ajenda kubwa ya Kiongozi wetu na amekuwa hana aibu hata kwa watu anaowaheshimu na rafiki zake. Alitaka wawajibike huku akiwatazama usoni. Ni Viongozi wachache sana wenye ujasiri wa aina hii. Huyu ndio Kiongozi wa chama chetu cha ACT Wazalendo. Nani anabisha rekodi hii?
10. KUKATAA POSHO ZA KUKAA
Mwaka 2010 chama chake cha zamani waliweka katika Ilani yao ya Uchaguzi kupinga posho kama hatua ya kubana matumizi ya Serikali. Wakakubaliana kuwa wabunge wa chama chao hawatapokea posho ya kukaa (sitting allowance). Hata hivyo, ilipokuja katika utekelezaji wenzake wote wakagwaya na Ndugu Zitto Kabwe ni mbunge pekee aliyepinga posho za vikao na kuzikataa kata kata kwa miaka mitano (5) mfululizo, ambazo ni takribani shilingi milioni 21 kila mwaka. Katika kipindi hicho cha miaka mitano Zitto alikaa kuchukua jumla ya Shilingi Milioni Mia Moja na Tano (105,000,000)!! Kukataa pesa yote hii kwa sababu ya ‘principle’ tu ni jambo nadra sana kutokea katika mazingira yetu. Zitto anatembea maneno yake. Zitto anatenda anayonena. Sasa kwa yote hata kwa nini wasimchukie wenye roho zao za kwa nini?
Ndugu Wananchi,
Huyu ndio Kiongozi wa Chama chetu. Tunachoomba Watanzania mumhukumu Zitto kwa rekodi zake na si kwa propaganda za mahasimu wake.
Viewing all 104745 articles
Browse latest View live




Latest Images