Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

HASHEEEM THABEET HALI NI TETE NBA MAREKANI HATARI KUACHIA NGAZI.

$
0
0
Mtanzania Hasheem Thabeet amejikuta akikumbwa na hofu ya kupoteza namba yake baada ya mchezaji Steve Adams anayechipukia raia wa New Zealand ambaye amesajiliwa mwaka jana na club ya Oklahoma city thunder alisainiwa na timu hiyo july 2013 mpaka sasa ameonyesha uwezo mzuri hvyo kutishia namba ya Hasheem, tangu asajiliwe amefanikiwa  kufunga point 17 rebounds 10, assist 3 na blocks 3 ambapo ana wastani wa point 3.8 na rebound 4.6... 
Kutokana na umahiri huo kumekuwa na vita ya namba baina ya wachezaji hao

LIBYA MABINGWA CHAN 2014

$
0
0
TIMU ya taifa ya Libya imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2014 baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana Jumamosi Uwanja wa Cape Town.

Ushindi huo ni sawa na Libya kulipa kisasi kwa Ghana baada ya kufungwa kwa penalti 7-6 miaka 32 iliyopita kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

WASANII HAWA WA BONGO MOVIES NA BONGO FLAVA WAMEAMUA KUJIUNGA CCM..WAPEWA KADI NA RAIS

$
0
0

Wasanii kadhaa kutoka kambi ya Bongo movies na Bongo flava leo hii Wameamua kukata shauri na kuchagua kujiunga na chama cha CCM , Wasanii hao ni JB , Banana Zorro, Rich Richie, Mboto , Irene Uwoya, Johari na Wastara...Wasanii hao wamepewa kadi za CCM leo hii na JK kwenye Sikukuu za kutumiza miaka 37 ya CCM Mjini Mbeya.......Toa maoni yako
Udaku Special Blog

SIRI YAFICHUKA MAUAJI YA WAFARANSA WALIOTUPWA KWENYE KISIMA CHA MAJI Z’BAR

$
0
0
Zanzibar Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji (KZU) na Polisi wamefanikiwa kuvunja zege lililokuwa limejengwa kufunika kisima walichotupwa raia wawili wa Ufaransa, baada ya kuuawa na kupata sehemu za miili yao ikiwamo fuvu la kichwa.
Aidha, siri za mauaji hayo zimeanza kuvuja, ikielezwa kwamba waliotekeleza unyama huo walilenga kupora nyumba na kiasi kikubwa cha fedha.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi na Makosa ya Jinai Zanzibar (DCI) Yussuf Illembo, alisema kuwa hadi jana mchana, mifupa miwili ya mapaja, fuvu la kichwa na miwili ya mbavu imepatikana kutoka ndani ya kisima hicho.
Alisema kwamba Kikosi Kazi cha Uokoaji kinaendelea kufanya kazi eneo hilo la Matemwe lililopo Shehia ya Kaskazini, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Kazi bado ni ngumu, tunaendelea kuzamia ndani ya kisima na itakapokamilika tutatoa taarifa. Tuacheni kwanza tufanye kazi hii nzito na ngumu kwa wakati huu,” aliomba DCI Illembo.
Zoezi hilo lilifanyika huku likishuhudiwa na ofisa mmoja wa Ubalozi wa Ufaransa nchini na kuelezwa kuwa marehemu hao walinunua eneo la ardhi na nyumba kwa Sh150 milioni kwa kutumia jina moja la mzawa wa Zanzibar, kutokana na sheria kutoruhusu wageni kumiliki ardhi visiwani humo. 
 Watu hao, Francios Chererobert Daniel, aliyekuwa mtumishi mstaafu wa ngazi za juu wa Serikali ya Ufaransa na mkewe Brigette Mary, walipotea tangu Desemba 27 mwaka jana.
Baadaye taarifa za kupotea kwa watu hao zilifikishwa Polisi ndipo msako wa kuwatafuta ulipoanza na baadaye kugundulika kuwa, kuna watu wameuawa na miili yao kutupwa katika kisima cha maji kilichopo ndani ya ua wa nyumba hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya waokoaji na mashuhuda wa tukio hilo, waliliambia gazeti hili kwamba sehemu hizo za mwili zinazosadikiwa kuwa za Wafaransa hao, zimefukuliwa baada ya kazi kubwa ya kuvunja zege kwa kutumia mashine maalumu inayofanywa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hilo.
“Tumefanikiwa kutoa sehemu ya miili, imehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyeomba jina lake lisitajwe.
Alisema kuwa kazi ya kuvunja zege hilo ilikuwa ngumu, walilazimika kuwachukua vijana wengine raia wa kawaida ili kuifanikisha.
Akielezea mazingira waliyokutana nayo chini ya kisima walichotupwa Wafaransa hao, alisema kuwa baada ya zege kuvunjwa walikuta nguo nyingi zimejazwa chini yake na juu yake kujengwa zege hilo kabla ya kumwagwa saruji isiyochanganywa kitu ili kufunika kisima kwa lengo la kupoteza ushahidi. 
Hata hivyo, vyanzo vya habari vinaeleza kuwa zoezi hilo lililazimika kusitishwa kutokana na sehemu ya chini ya kisima kupita mkondo wa maji ya bahari, hivyo kulazimika kutafuta mashine ya kuvuta maji.
“Kazi hiyo ikiweza kufanyika ndipo tutakapoweza kwenda katika kina kirefu zaidi cha kisima hicho ili kukusanya mifupa. Tukipata idadi ya mifupa na mafuvu yote, tutaweza kujua waliouawa ni wangapi,” kilieleza chanzo kimoja.
Sheha wa Shehia ya Matemwe Kusini, Denge Khamis Silima alisema kuwa wanapata faraja kuona zoezi hilo limepata mafanikio tofauti na siku ya kwanza na kwamba kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa umakini huku akiitaka Serikali kuwapatia vifaa waokoaji ili kufanikisha kazi hiyo.

Siri ya mauaji
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa siri ya mauaji hayo ni baadhi ya watu kutaka kupora nyumba, waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao pamoja na fedha zinazodaiwa walikuwa nazo raia hao wa kigeni wakitaka kununua eneo la kujenga hoteli kwenye ufukwe wa Urowa.
Inelezwa kuwa kabla ya kuingia Zanzibar, Wafaransa hao walifikia Nairobi nchini Kenya ambako inadaiwa kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini humo aliwashauri kwenda Zanzibar kuishi na kuwekeza.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa kabla ya watu hao kuuawa, mbwa wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Allan, alipewa chakula chenye sumu na kufa na kwamba sehemu ya mabaki ya chakula hicho yaliliwa na mbwa wa jirani ambaye pia alikufa.
Aidha, mifuko mitupu ya saruji inayosadikiwa kutumika katika ujenzi wa zege la kisima hicho, imeokotwa nyuma ya ukuta wa nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao. 

MWANANCHI

MWANAFUNZI ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUCHOMWA MSHALE WA JICHO

$
0
0
Mwanafunzi wa miaka 11 nchini China amenusurika kufa baada ya mshale uliorushwa na rafiki yake kuzama kichwani kwake kupitia kwenye jicho lake, aliwahishwa hospitali huku mshale huo ukiwa bado umezama kwenye kichwa chake
-Boss Ngasa

JOKATE NA WEMA NO BEEF...WENYEWE KWA RAHA ZAO JAPO WOTE WALISHATOKA NA DIAMOND

$
0
0

Kama ulikuwa unadhani Jokate na Wema Sepetu Wana Beef baada ya wote kuwahi kutoka na Diamond na kama ulishuhudia Show ya Diamond pale mlimani City jinsi Diamond na Jokate walivyomfanyia Wema Sepetu <<Kwa Taarifa yako Wenyewe now wapo poa ...Check hizo picha wakiwa pamoja wakicheza na kutunzana kwa furaha Pale arusha jana kwenye usiku wa Divas Pale Tripple A

SEREKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME MAJUMBANI

$
0
0
Serikali imetangaza kupunguza gharama za kuunganisha umeme kutoka Sh177,000 za awali hadi Sh27,000 vijijini.

Awali, punguzo hilo lilitolewa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara, ambako bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam limeanzia, lakini sasa gharama hizo zitakuwa kwa vijiji vyote nchi nzima.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema gharama hizo zitahusu miradi inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika kipindi ambacho makandarasi watakuwa wakiendelea na awamu ya pili ya miradi inayotarajiwa kuanza Machi mwaka huu.

Muhongo alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya miradi iliyomalizika Desemba mwaka jana, wanavijiji walilipa gharama kubwa, hivyo Serikali imeamua kupunguza malipo hayo, ili huduma hiyo ya nishati iwafikie watu wengi zaidi.

Hata hivyo, ofa hiyo itadumu kwa mwaka mmoja na miezi mitano pekee, kwani awamu ya pili ya miradi hiyo inatarajiwa kuanza Machi, 2014 na kumalizika Juni, 2015.

“Gharama hizo ni kwa kipindi ambacho makandarasi watakuwa kazini tu. Makandarasi msiwakatalie wanavijiji kuwafungia umeme,” alisema Muhongo.

Waziri Muhongo aliwanyooshea kidole makandarasi wa miradi ya umeme vijijini akisema kuwa wanalalamikiwa kwa kuomba rushwa kwa wanavijiji ili wawaunganishie umeme kwenye nyumba zao.

“Kule Bunda kuna mwanakijiji alimtaja mfanyakazi wa kampuni inayoomba rushwa… kampuni hiyo imeshapewa onyo, ninapendekeza isipewe tena kazi,” alisema Muhongo.

Pia alilitaka Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco) na REA kutokutumia gharama kubwa kulipa fidia za majengo au mashamba ya wanavijiji kwa kuwa historia inaonyesha kuwa zoezi hilo huambatana na rushwa.

“Tuna historia mbaya linapokuja suala la fidia, limejaa rushwa tupu,” alisema.

HUYU NDIO BINADAMU WA KWANZA KUFIKISHA FOLLOWERS MIL 50 KWENYE MTANDAO WA TWITTER

$
0
0
Mwanamuziki Ajulikanae kama Katy Perry amekuwa mtu wa kwanza kufikisha followers Milion 50 kwenye mtandao wa Twiiter ...Anae fuata kwa nyuma ni Justiner Birber ambae ana followers Mil 49 na wa Tatu ni Raisi wa Marekani Amabe ana followers Mil 41....Mwee wewe Unawangapi ? Mie hata buku hawafiki lol...

LAMAR"NINA MPANGO WA KUNUNUA NDEGE BINAFSI HIVI KARIBUNI"

$
0
0
Producer Machachari wa Hapa Bongo Anaejulikana kama Lamar Amehabarisha Radio Moja hapa Bongo Kuwa ana Mpango wa Kununua Ndege yake Binafsi ili kumrahisishia Mizunguko yake Sehemu Mbali Mbali ...Amesema hizo ndoto alikuwa nazo muda mrefu na Ameshaanza Kuongea na Wauzaji wa ndege kuona kama atapata Moja ...Big Up Lamar...Utakuwa msanii wa kwanza Tz kuwa na Ndege Binafsi....

Mwanamuziki Mwingine mwenye ndoto kama hizo ni Ay ambae nasikia ameanza kujifunza kuendesha ndege ili kujiandaa atakapo nunua yake .....

PICHA:RAIS KIKWETE AKIWAKABIDHI KADI WALE WASANII WA BONGO MOVIES NA BONGO FLAVA WALIOINGIA CCM

$
0
0

 B akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo. 
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji.

EXCLUSIVE..JIDE AOMBA TALAKA, GARDNER APATA MSHITUKO..AELEZA KILA KITU

$
0
0
Stori:  Shani Ramadhan
UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo kuomba aandikiwe talaka, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuripoti mkasa wote.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Jide au Lady Jaydee alifikia uamuzi huo baada ya Gardner kupata kazi ya kutangazia redio moja nchini Kenya.
HABARI KAMILI
Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa mara baada ya mume huyo kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati hiyo.
“Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe.
“Pia katika safari ya kwenda Kenya kupiga mzigo ilikuwa aende na mkewe huyo kwa sababu lilikuwa suala la kuhamisha makazi yao Tanzania,” kilisema chanzo hicho.

JIDE AHAMAKI
Chanzo kikatoboa kwamba Gardner alipofika nyumbani kwake na kumweleza mkewe, alikumbana na kitu ambacho hakukitarajia.
“Komando (Jide) alihamaki na kumjia juu akisema yeye hawezi kuondoka Tanzania kwenda kuishi Kenya, kama Gardner analiona jambo hilo ni heri kwake, amuandikie talaka yake na kuachana ili kila mmoja achukue hamsini zake,” chanzo kilizidi kuporomosha maneno.
KWA NINI JIDE HAKUPENDA? 
Habari zilizidi kuanikwa kwamba Jide au Binti Machozi alifikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa kitendo cha kwenda kuishi Kenya kitaua bendi yake ya Machozi na sehemu ya biashara ya Nyumbani Lounge iliyopo Ada-Estate, Kinondoni, Dar.
MBAYA ZAIDI
Taarifa zikazidi kumiminika kwamba, mbali na Jide au Anakonda kuhofia biashara zake kufa, lakini pia hakupenda Gardner aondoke hata peke yake kwa sababu yeye ndiye meneja wa miradi hiyo miwili.
“Mimi nilipopata habari hizo nilikutana na Jide nikamuuliza, akanijibu ameamua iwe hivyo tu, kikubwa mumewe (Gardner) aamue moja kati ya hayo mawili kwani yeye ana haki akiwa kama mkewe wa ndoa,” kilisema chanzo kikimkariri Jide.
GARDNER AISHIWA NGUVU
Kufuatia majibu ya mkewe, taarifa zinasema mtangazaji huyo ambaye alishawahi kupiga mzigo kwenye kituo cha Radio Clouds FM cha jijini Dar alijikuta akiishiwa nguvu na kuachana na dili hilo mara moja.
“Gardner alisalimu amri kwa mkewe, akaamua kuachana na dili la kwenda kutangaza Kenya. Lakini alifikiri sana akasema ni kweli kuhamia Kenya kungeua miradi yao ya Tanzania maana ingekosa msimamizi wa kuaminika,” chanzo kiliweka wazi.
KAMA ANGEKWENDA KENYA 
Siri hiyo iliyovujia mikononi mwa Ijumaa Wikienda haikuishia hapo, ilizidi kuanikwa kwamba kama Kapteini angekwenda Kenya na kuanza kazi, ilikuwa alipwe mshahara wa shilingi za Kenya laki 3 kwa mwezi (kama milioni 6 za Tanzania).

NAFASI YAKE BADO IPO
Mpashaji wetu alisema kwamba nafasi ya Gardner kwenye kituo hicho cha redio ambacho hakikutajwa, bado ipo lakini tamko la Jide nalo li hai, kwa vile hakubatilisha, endapo mumewe atataka kwenda hata kesho (Jumanne) aandike talaka.
WIKIENDA NA GARDNER
Baada ya kunyetishiwa taarifa nzima, juzi gazeti hili lilimsaka Gardner. Kwa njia ya simu lilimkosa, likamfuata Nyumbani Lounge. Lilipomkuta lilimsimulia kisanga chote cha ndoa yake kutikiswa na kitendo cha yeye kupata kazi Kenya ambapo alijibu hivi:
“Ndoa ni nzuri, ni kweli ilikuwa niende Kenya, nilipata kazi kule lakini kama familia ilikuwa lazima tukae na kupanga, mwenzangu hakuafiki.”
Wikienda: “Ni kweli shemeji ameomba uchague mawili, umwandikike talaka au uende Kenya?”
Gardner: “Ndiyo maana nimesema ndoa nzuri, lazima makubaliano yawepo, mke anaweza kuonesha msimamo wake na mume kama utakaa chini na kuufikiria ukapata jibu unakubaliana na mke wako wala hakuna ubaya.”
Wikienda: “Kule mshahara wako ungekuwa shilingi ngapi?”
Gardner: “Hiyo sasa ni siri ya makubaliano.”
Wikienda: “Kwa nini usiamue kwenda tu?”
Gardner: “Nimekwambia ndoa nzuri.”
JIDE BIZE
Juhudi za kumpata Jide ziligonga mwamba baada ya muda wote kuwa bize na shoo ya kukata na shoka aliyokuwa akiifanya siku hiyo kwenye ukumbi huo akikimbiza na nyimbo zake kali za zamani na hizi mbili zilizogeuka nyimbo za taifa, Joto Hasira na Yahaya.
RAFIKI WA GADNER AMCHAMBUA JIDE
Rafiki wa karibu na Gardner (jina tunalo) ambaye alisikia mahojiano ya mtangazaji huyo na Ijumaa Wikienda, alisubiri jamaa aondoke ambapo alianza kumchambua Jide.
“Nataka kuwaambia kitu, Jide ni mwanamke jasiri sana. Ana msimamo na anaposhikilia msimamo wake hatengui hasa kama atabaini kuwa yupo sahihi.
“Ni kweli jamaa (Gardner) alipata kazi Kenya tena mshahara mzuri tu, lakini mama (Jide) akaweka ngumu hakuna kwenda,” alisema rafiki huyo.

CREDIT:Global Publishers

MASKINI SHILOLE..KUMBE BWANA'KE MZUNGU ALIYEMNADI NI "MWANAUME TATA"

$
0
0
Yeleuuuwi! Siku chache baada ya msanii wa sinema na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kujinadi na mchumba wa Kizungu aliyejulikana kwa jina moja la Ankar, siri imefichuka kwamba jamaa huyo ni mwanaume tata. 
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda kutoka London, Uingereza, wikiendi iliyopita, chanzo hicho makini kilisema mwanaume ambaye hivi karibuni Shilole alijinadi kuwa ni bw ana’ke siyo kwani huko London baadhi ya watu wanamfahamu kama mwanaume tata kijinsia.“Yule jamaa anapenda sana kukaa na wanawake, sijawahi kumuona na wanaume wenzake, kazi kukata tu mauno na wanawake. Nilishangaa sana Shilole kusema eti ni mc humba’ke wakati hapa London (Uingereza) ni maarufu sana kwa kushiriki pati za wanawake. “Maskini Shilole, pale imekula kwake, hakuna chochote,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Shilole ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Jamani imeniuma sana kwani nilikuwa sijui, nimeligundua hilo baada ya kuambiwa na watu, nilipigiwa simu kutoka Uingereza kwamba yule mwanaume siyo hivyo sina mpango naye tena kwa kweli,” alisema Shilole anayetamba na kideo cha Nakomaa na Jiji.

GPL

KUNDI LA WASANII KUJIUNGA CCM KWA PAMOJA...NI KUPENDA KWAO AMA KUNA USHAWISHI?

$
0
0
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na Mtindo wa Wasanii wa Fani Mbali mbali kujiunga na Siasa hasa wasanii kutoka kambi ya Bongo Flava...Mfano Sugu , Vick Kamata, Afande Sele, Roma na Wengine...Hii imekuwa sasa kama staili ukichukulia kwamba wasanii hao wana ushawishi mkubwa kwa Jamii yetu ya Kitanzania
Jana kuna Kundi la wasanii ambao wamejiunga CCM...Nilipost habari hiyo na Watu wametoa hisia tofauti tofauti kuhusu tukio hilo la Wasanii Wengi kwa Pamoja kuingia CCM wengi wamekuwa na shaka kuhusu hilo na kuuliza maswali yasio na majibu ...Wasanii hao walionekana wakipanda ndege ya Fast Jet Kuelekea Mbeya kwa Makundi ...Je wewe Unaona ni sawa na wamejiunga kwa kupenda kwao ama kuna ka ushawishi ? TOA MAONI YAKO
Udaku Specially Blog

MSAADA:NAKUFA KWA MAWAZO KWA MESEJI HII NILIYOIKUTA KWA SIMU YA MPENZI WANGU

$
0
0
Mwenzetu nimekoma kuchungulia simu ya mpenzi wangu, Maana nimekuta message moja mpaka sasa nafikiria najiona kama mimi sijui mapenzi ....na nikizubaa ntaibiwa Gal wangu ..ki ukweli sijawahi mtumia msg tamu mpenzi wangu huyo kama hiyo na sina uwezo wa kutunga msg yenye mvuto...Nahisi ntaibiwa na wajuzi wa Mapenzi 
Meseji yenyewe hii hapa chini:

"Ki ukweli Mpenzi , Nakupenda kutoka rohoni na nimevutiwa na wewe kiasi kwamba natamani unipe moyo wako uwe wangu niutunze mpaka siku ya mwisho wetu, Nakuona kama furaha ya maisha yangu toka tuonane ewe malkia, Naomba usiniangushe naona matumaini ya penzi kwako, Nakuhaidi kukupa furaha katika kipindi chote tutakachokuwa pamoja huta juta kuwa na mimi, Nahitaji uwepo wako katika dimbwi hili la Mapenzi"

Mwee Nifanyaje? ..Nimeuchuna sijamwambia kitu ila Roho inaniuma

WEMA SEPETU"NIKIFA MIMI LEO AU KESHO NIAGWE UWANJA WA TAIFA"

$
0
0
Wema aachi vituko, Siku za Karibuni Wema amekaririwa na Gazeti moja la Udaku hapa Tanzania  aka Bongo akisema kuwa Akifa yeye Basi Aagwe uwanja wa Taifa kwa vile jina lake ni kubwa Ndani na Nje ya Tanzania hivyo pale Leaders walipozoelea kuaga Watu maarufu hapata Tosha ,Alisema uwanja wa taifa utampaka kila mtu chance ya kumuaga....Mweeeeee Makubwa
Udaku Specially

JUSTIN BIEBER AVURUGWA...AMVAMIA STRIPPER NA KUANZA KUMNYONYA MATITI MBELE ZA WATU

$
0
0

Huyu Dogo Angekuwa Bongo Basi tungesema anatafuta KIKI kwa Mambo anayoyafanya kipindi hichi akiwa ndio amefikisha miaka 19 tu, Kuachana na Skendo yake ya madawa ya kulevya juzi amefanya kioja kimoja kwenye Party yao huku LA ..Baada ya yeye na rafiki yake kumrukia mchezo show wa uchi na kuanza kumnyonya chakula cha mtoto Stripper huyo kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini ...cha kushangaza aliruhusu watu wampige picha akifanya kitendo hicho...jioneeee 


UWEZI AMANI YAANI BAADA YA KUDHALILISHANA INSTAGRAM STALISHA NA PREZOO WARUDIANA

$
0
0
Baada ya matusi ya kila aina aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake, Starlisha Tillya aka ‘Mdoli wa Kichaga’ (Chagga Barbie), Prezzo aliandika: President” is like a drug (highly addictive) he’s the best up until the drugs runs out, withdrawal symptoms can be seen from miles.”

Kauli hiyo ilikuwa na ukweli kwa asilimia 100, kwakuwa ni kweli Starlisha ameshindwa kumsahau rapper huyo anayejiita Mfalme Mswati na hivyo kuamua kurejea tena kwenye himaya yake.

Mtanzania huyo anayeishi nchini Marekani, jana alipost picha ya Prezzo kwenye Instagram na kudai kuwa ameamua kumsamehe Prezzo na kwamba hakuna mahusiano rahisi duniani.

Let De Movie Continue #MapenziniUpofu #HakunaNgechuBilaChaggabarbie #MunguAnajuaKwanini #SihitajiyeyoteZaidiYake #NawaombaMtuombee #HakunaMahusianoRahisiDuniani NimeaminiUkimpendamtuhataitokeeniniHuwezikuukimbiaMoyo. Nawatakia Jumapili Yenye Amani, Furaha, Upendo, Kusamehe na Mumtangulize Mungu Jamani Ndio Kila Kitu. Kwa Neema Yake Kanipaujasiri wakuwaeleza haya Leo,” aliandika kwenye picha hiyo.

Bado Prezzo hajasema lolote.

Bongo5

RAIS KIKWETE:MBOWE ANAKOSA UWEZO, JAMBO LA WENGI HALITAAMULIWA KWA NGUMI

$
0
0
Rais Kikwete: Mbowe anakosa uwezo, jambo la wengi halitaamuliwa kwa ngumi
Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 37 ya CCM alimwambia Mheshimiwa Mbowe kuwa nashanganzwa na kauli yake kwamba isipopatikana Serikali tatu atapambana kwa ngumi na mateke mpaka ipatikane.

“uliona wapi jambo la wengi likiamuliwa kwa ngumi?” aliendelea Kikwete kwa kusema “hakuna katiba ya nchi dunia iliyopatikana kwa kutumia ngumi na hata Mbowe akiamua kupigana sina hakika kama atamshinda John Komba au Mheshimiwa Mnyika kumpiga Mheshimiwa Missanga”.

Bunge la katiba ndilo litakalopitisha aina ya katiba tunayoitaka kwa niaba yetu na lina uwezo wa hata kuja na rasimu ya katika yao tofauti kabisa na ya sasa na ikawa halali.

Alimalizia kwa kusema “katiba mpya ikikwama tutaendelea na katiba ya sasa”.

AT KATIKA AIBU NZITO 2014, MGANGA AIBUKA NA KUDAI AMESEPA NA LAKI TISA ZAKE

$
0
0
Leo asubuhi nilipoamka nilifungulia radio yangu nikakuta Dk Sharifaa akifunguka na kudai kuwa yeye ndio mganga wa A.T
Huu ndio ujumbe wa Dk Sharifaa (Mganga)
‘‘Tangu bado hajafahamika yaani sio mwanamuziki mimi nilikutana naye Zanzibar Unguja,tena nakumbuka kwa mara ya mwisho alikuja na Gerry Rhymes lakini Gerry alikuwa afahamu kitu chochote, chakushangaza tangu nilipomfanikishia mahitaji yake maana mimi ni mganga basi amenisahau kabisa nikijaribu kumpigia simu hapokei mpaka anapokei tuzo anapata safari za kwenda muscat amenisahau mimi ninaomba anipatie vile vitu alivyoahidi kwangu anipatie,sio kwa ugomvi ila sheria zetu sisi waganga kwasababu hizi ni kazi namdai deni la laki tisa nikimpigia simu hapokei ndio maana nimekuja hapa kuripoti’Alisema Mganga huyo.
‘Vitu vingine nilivyomsaidia vipo vingi kwa mfano anapotarajia kuachia wimbo mpya basi anakuja na Cd kwangu na mimi nafanyia taaluma yangu ya Uganga mwisho wa siku unakuta nyimbo zake nyingi zinapamba.Mimi naitwa Doctor Shariffa
SOURCE: Edwin Tanzania a.k.a 255

THAMANI YA MALI ALIZOKUWA ANAMILIKI HAYATI NELSON MANDELA ZATANGAZWA

$
0
0

Mandela alifariki mwezi Disemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 95
Hayati Nelson Mandela, aliachia familia yake mali yake yenye thamani ya dola milioni 4.1.
 Sehemu ya mali hiyo pia itatolewa kwa chama tawala ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.

Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wasia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.
 Afisaa Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la kusoma wasia huo wenye kurasa 40 na kuhakikisha unatekelezwa ,alisema hapajakuwa na pingamizi zozote kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya Mandela.
 Wafanyakazi wa karibu wa Mandela watapata randi 50,000 kila mmoja. Shule ambazo Mandela alisomea zitapata randi laki moja kila shule.
 Hayati Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95.
 Familia ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana kuhusu urithi wa hayati Mandela na kuna hofu kuwa huenda wasia huu ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu mali hiyo.
 Mali ya hayati Mandela inajumuisha nyumba na hakimiliki za vitabu ikiwemo kimoja kuhusu maisha yake kwa jina ''Long walk to freedom''
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images