Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Baada ya Mchezaji Ramadhani Singano Kushinda Kesi Dhidi ya Simba na Kuwa Huru...Hii Ndio Team Iliyomchukua na Kumsajili...Simba Wacharuka na Kusema Haya

0
0
Baada ya TFF kuvunja Mkataba wenye Utata wa Mchezaji Ramadhani Singano na Timu ya Simba , Ramadhani Singano amesajiliwa na Team ya Azam kwa Mkataba wa Miaka Miwili ..Hii imekuja baada ya Siku moja tu kwa mkataba wa Simba Kuvunjwa kitu ambacho kimewauma sana simba ..leo jione msemaji wa Simba Amesikika Akiongea Redioni Akisema kuwa ishu hii ya Singano imepikwa na Azam toka mwanzo ili wamchukue Ramadhani.....

Je wewe Unamaoni Gani kwa hili ?

By Udaku Specially

Picha Sita za Mrembo Anayekimbiza Kenya Corazon Ambazo Zimebuma na Kutoka Vibaya ambazo Hujawahi Kuziona Hizi Hapa

0
0






6 Ugliest Photos of Corazon Kwamboka You Have Never Seen Before

Majibu ya Wema Sepetu Kwa Waliosema Siasa Imeingiliwa Baada ya Yeye Kutangaza Nia, Pia Aliyeigiza Sauti Yake

0
0
Mwigizaji Wema Sepetu alifanya Interview na mtangazaji Millard Ayo kuhusu ishu kadhaa zinazohusu kutangaza kwake kuingia kwenye siasa ambako anagombea viti maalum ambapo amejibu comments za watu waliombeza kwa kusema siasa imevamiwa, nafasi ya juu ya Uongozi aliyowahi kuitamani, aliyeigilizia sauti yake na mengine bonyeza play hapa chini.

Source:Millard Ayo

Maneno ya Diamond Platnumz Kuhusu Beef, Timu za Insta na Facebook, Uchawi na Wanaompigia Kura Davido Mengine.

0
0
Diamond Platnumz alikaa kwenye Exclusive Interview na XXL ya CloudsFM na kuzungumzia ishu mbalimbali ikiwemo beef na Ali Kiba, team za Instagram ambazo nyingine zimekua zikihamasisha Davido apigiwe kura na mengine.

Watoto Watano Familia Moja Wateketea Kwa Moto

0
0
Watoto watano wa familia moja wamefariki dunia na mama yao mzazi kujeruhiwa, baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuteketea kwa moto katika kitongoji cha Muleba kijiji cha Muleba kata ya Rwabwere wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe.
Tukio hilo lilitokea Julai 6 mwaka huu ambapo chanzo chake ni kibatari kilichokuwa kimewashwa kuanguka na moto kushika nyumba hiyo ambayo ilikuwa imejengwa kwa makuti ya migomba.
Watoto waliopoteza maisha ni Zaituni Mohamed mwaka mmoja na miezi 3, Atwaibu Mohamed (4) Sajira Mohamed (3) na Shine Mohamed (7), ambao walifariki papo hapo na Khadija Mohamed (5) alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Nyakahanga
Katika tukio hilo mama mzazi wa watoto hao Sania Mohamed akizungumza katika hospitali ya wilaya Nyakahanga ameleza amepatwa na ajali hiyo wakati akiwa katika harakati za kuwaokoa watoto wake lakini hakufanikiwa kutokana na moto kumzidi nguvu.

Licha ya Kujitosa Kugombea Ubunge, Wema Sepetu Ashtakiwa Kwa KOVA..Maimartha Amfungia Kazi, Diamond Naye Atajwa

0
0
Waandishi wetu
KIMENUKA! Mtangazaji na MC (master of ceremony) maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ameivalia njuga tabia ya mastaa kuhusika na matusi ya mtandaoni na kupiga picha za utupu ambapo kwa kuanza amemshitaki mwanadada Wema Isaac Sepetu kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akimtuhumu kuwa kati yao.

Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum huku akirekodiwa ili kuweka kumbukumbu vizuri, Mai alisema yeye ni mmoja wa wahanga wa matusi ya mtandaoni na amegundua wanaomtukana ni kundi linalojiita Team Wema.

Msikie Mai
“Kuna watu kwenye hii mitandao ya kijamii wamejipa majina bandia lakini ukiwafuatilia sana utagundua ni watu wa Wema, ni watu ambao ukimtibua Wema watakuvaa kwa kukutukana sana.

“Hao hao ndiyo wanaoongoza kwa kumsifia sana Wema kwenye mitandao. Ili ujue kwamba Wema anawajua, huwa wanampelekea hadi zawadi na juzijuzi hapa walihamasishana kuchanga fedha ili wampelekee Wema.

“Sasa kama ni watu anaowajua, kwa nini asiwazuie kutukana ovyo watu? Tutakuwa tunakosea kusema anawatuma?
“Hebu fikiria Wema anataka kugombea ubunge, hilo ni jambo jema na sisi wenzake tunamuunga mkono lakini nafasi hiyo ataimudu kweli kama anashindwa ‘kuwakontroo’ watu walio nyuma yake ambao wanawakosesha amani wenzao?
“Kitu ambacho nakiamini ni kwamba, usimuone Wema kakaa kimya kwenye akaunti yake lakini hawa mastaa unaowaona wanatukanwa, baadhi ya watukanaji wanatumwa na Wema, wanaambiwa fulani tukana, fulani tukana,” alidai Mai.

Wema anahusikaje?
Kwa madai yake, Wema anahusika kwenye kushamiri kwa tabia hii kwa kuwa, watu wake ndiyo wamekuwa wakisumbua na dalili za wazi zinaonesha ‘anawa-push’ kiaina kufanya hivyo.

Awagusa Diamond, Kajala, Aunt
“Mara kadhaa tumekuwa tukiona Wema akiwaambia Team Wema wasimtukane Diamond (Nasibu Abdul), tunaona mastaa wakitofautiana na Wema kidogo wanashambuliwa kwa matusi, mfano Kajala (Masanja) na Aunt (Ezekiel).

“Wanaofanya hivyo siyo mashabiki wa Wema, ni marafiki wake damdam na ni jambo ambalo Wema analijua, ndiyo maana anaweza kuwaambia wasimtukane f’lani.
“Kwa nini asiwazuie waache tabia ya matusi mtandaoni ambayo ni kinyume na sheria?” alihoji Mai.

Agusia picha chafu
Katika kufunguka kwake, Mai alienda mbele zaidi kwa kumtaka Wema kujiangalia upya ikiwa ni pamoja na kuwakontroo marafiki zake wasitukane watu lakini pia aache kupiga picha za utupu, alizopiga huko nyuma zinatosha, ajitahidi kuwa msafi.

Ashitakiwa kwa Kova
Huku akionekana kuwa makini sana na kutaka taarifa anazotoa zilifikie jeshi la polisi na kuzifanyia kazi, Maimartha aliamua kumshitaki Wema moja kwa moja kwa Kamanda Kova akimtaka achukue hatua stahili ili kukomesha tabia hiyo.

“Sasa naomba leo niseme kwamba, mtandaoni hatutaki matusi na doria zipo, wapo wana usalama, mimi nakuambia Kamanda Kova, hili nalifikisha kwako nikijua jeshi lako linahusika.

“Mitandaoni watu wamechoka kutukanwa, naomba hizo doria zifanye kazi na kama utataka ushirikiano, mimi nipo na nitatoa ushahidi ukitaka.
Wema anasemaje?

Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Wema ili kuzungumzia tuhuma hizo lakini simu yake iliita bila majibu na hata alipotumiwa meseji hakujibu.
Aidha, wanahabari wetu walifunga safari hadi nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar lakini waliishia getini baada ya kuambiwa hayupo. Jitihada za kumtafuta zinaendelea ili naye afunguke.

Ofisini kwa Kova
Kutokana na mashitaka hayo ambayo Mai alitaka yamfikie Kamanda Kova, waandishi wetu walimtafuta ‘afande’ huyo lakini jitihada hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.


Hata hivyo, mmoja wa maafisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar aliyeomba hifadhi ya jina alisema, kama Mai ana madai yake hayo anatakiwa ayawasilishe kwa Kova ‘fizikale’ na kama ataridhika naye, atayachukua na kuyapeleka kwa ofisa upelelezi wa kanda ‘Zonal Crime Officer’ ambaye atayafanyia kazi bila kujali majina ya wahusika.
GPL

Simba Wamesema Haya Baada ya Ramadhani Singano Kusajiliwa na AZAM Siku Moja Baada ya Kusinda Kesi

0
0
Baada ya aliyekuwa winga wa Simba Ramadhani Singano ‘Messi’ kumwaga wino wa kukitumikia kikosi cha ‘wanalambalamba’ Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili, klabu yake ya zamani (Simba) imesema dili hilo lilipangwa na Azam ili mkataba wa mchezaji huyo na klabu ya Simba uvunjwe na wao wamnase kirahisi.

Afisa habari wa Simba Hajji Manara amesema Azam walipanga jambo hilo kwasababu Singano alishasema kwenye kikao cha kwanza kuwa Azam ni miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zikimuhitaji wakati bado akiwa na mkataba na Simba.

“Hili jambo limepangwa, na mkiuliza nani amelipanga mnamajawabu. Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji juzi imemtangaza Messi ni mchezaji huru wamevunja mkataba wetu, leo amesaini Azam. TFF hawajatuletea barua, huyu mchezaji mpaka juzi sisi tunatambua ni mchezaji wa Simba mpaka hivi sasa barua ‘official’ haijaja ndio maana nasema hili jambo lilipangwa sikunyingi na TFF wanalijua hili”, amesema Manara.

“Itawezekana vipi mchezaji ambaye sisi barua hatujapata ya kuvunjwa kwa mkataba wake asaini kwenye klabu nyingine? Kwakutopewa barua mpaka leo maana yake nini? Sisi tunashindwa kutoa ‘official statement’ ya klabu na tunashindwa kuchukua hatua zozote wakati hawajatuletea barua tayari mchezaji kaenda Azam”, Manara alihoji  

“Na kwenye kikao aliwataja Azam kuwa ni miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zinamsumbua”, alimaliza.

Leo mchana Singano amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu ya Azam FC baada ya mkataba wake na Simba kuvunjwa na kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji kufuatia Simba kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya mkataba kati ya mchezaji na klabu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya July 10

0
0

























Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Ijumaa  ya  July  10

Moshi Mweusi Watanda CCM.......Rais Kikwete Apangua Ratiba ya Vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati Kuu, Kingunge Amvaa Kinana

0
0
WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akipangua ratiba ya vikao muhimu vya Kamati ya Usalama na Maadili pamoja na Kamati Kuu vilivyotarajiwa kufavyika juzi na jana, Mwanasiasa maarufu, Kingunge Kombale-mwiru  jana alikuwa uso kwa uso na Katibu Mkuu wa chama hicho katika jitihada za kumuokoa Edward Lowassa.

Katika siku ya jana kulikuwe na minong’ono ya hapa na pale iliyokuwa imeenea katika korido za Makao Makuu ya CCM na viunga vya mji wa Dodoma, ikidai kuwa jina la mwanasiasa huyo halitakuwemo katika orodha ya majina ya tano bora itakayopelekwa ndani ya NEC kutoka Kamati Kuu.

Minong’ono hiyo ya kuwepo uwezekano wa jina la Lowassa kutotoka Kamati Kuu, iliongeza hofu zaidi miongoni mwa wapambe wa mwanasiasa huyo, baada ya mwanasiasa mkongwe nchini anayejulikana wazi kuwa katika kambi ya mgombea huyo, Kingunge Ngombale-Mwiru kutinga katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho mchana wa kati ya saa 8:00 na saa 9:00.

Baada ya kushuka kwenye gari lake na kuelekea moja kwa moja katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Kingunge alisikika akisema “Nina miadi ya kuonana na Katibu Mkuu saa 8.30 mchana huu, ameniita.”

Mwanasiasa huyo ilimchukua takriban saa nzima akiwa katika ofisi ya Kinana. Alipotoka tu nje, kada mwingine wa CCM, Hamis Mgeja, ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Shinyanga aliingia katika ofisi ya Kinana akidaiwa kuitwa pia.

Mgeja, kama ilivyo kwa Kingunge, ni miongoni mwa makada wa CCM ambao wamekuwa wakijipambanua wazi wazi kuwa katika kambi ya Lowassa kiasi cha makada hao kushiriki kikamilifu katika mchakato wa mgombea huyo wa kutafuta wadhamini 450 katika mikoa 15 ya Tanzania, kati ya hiyo mitatu ikiwa ni ya Zanzibar.

Haikuweza kufahamika kwa undani ni kwanini makada hao wa CCM waliitwa na Kinana ofisini kwake, lakini baadhi ya wadadisi wa mambo walielezea tukio hilo kama sehemu ya juhudi za kambi hiyo ya Lowassa kuokoa jahazi la mgombea wao huyo jina lake kuondolewa mapema na Kamati Kuu.
 
Hata hivyo, kwa mujibu wa ratiba ya awali ya mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, vikao hivyo muhimu katika mchakato huo vilitarajiwa kufanyika juzi na jana, lakini vikao vyote viwili hivyo havikuweza kufanyika kama vilivyopangwa, huku kukiwa hakuna taarifa yoyote rasmi kwanini havikufanyika.

Kwa kawaida kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ambacho huongozwa na Rais Kikwete mwenyewe akisaidiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahiman Kinana, ndicho kinachotoa dira ya mwelekeo kwa wajumbe wa Kamati Kuu, kikao ambacho kina mamlaka ya kuteua majina matano kutoka miongoni mwa wote waliojitokeza kuomba nafasi hiyo.

Kikao hicho cha Kamati ya Usalama na Maadili ndicho kinachopokea majina ya wote waliojitokeza kuomba nafasi hiyo, kabla ya kujadili mienendo ya kimaisha ya kila mmoja wa wagombea, hasa katika suala zima la kimaadili na uzingatiaji wa miiko na viapo vya utii kwa chama hicho.

Baada ya Kamati hiyo kukamilisha kazi hiyo, majina yote ya walioomba uteuzi huo huwasilishwa ndani ya kikao cha Kamati Kuu, kila jina likiwa limetendewa haki kwa kubeba maelezo ya sifa za miendendo hiyo ya kiamaadili na uzingatiaji huo wa miiko na viapo vya utii kwa Chama, kabla ya kikao hicho kuteua majina matano yanayopelekwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kwa hatua zaidi.

Kutofanyika kwa vikao hivyo muhimu katika mchakato huo wa uteuzi ndani ya CCM hadi jana kama ilivyokuwa imepangwa awali, kwa kiasi fulani kumeongeza hofu na kukoroga vichwa vya baadhi ya wapambe wa wagombea wa urais kutokana na kutofahamu sababu na malengo ya kuahirishwa huko kwa vikao hivyo.

Hadi jana jioni ya Julai 9, 2015, vikao hivyo muhimu viwili vinavyoongozwa na Rais Kikwete mwenyewe, havikuwa vimefanyika kutokana na kile kilichoelezwa na watu wa karibu na kiongozi huyo mkuu wa nchi na chama chake hicho kwamba ni kukabiliwa na majukumu mengine mazito ya kitaifa.

Kwa siku ya jana Alhamisi pekee, Rais Kikwete alikuwa na jukumu la kuzindua ukumbi wa kisasa wa Mkutano Mkuu wa CCM uliojengwa kwa gharama za chama hicho katika eneo lililopo karibu na majengo ya Ofisi za Hazina Ndogo mjini Dodoma, hafla iliyofanyika kuanzia asubuhi hadi mchana kabla ya alasiri kiongozi huyo kwenda kulihutubia Bunge na kufunga shughuli za Bunge la Bajeti.

Katika korido na viunga vya Ofisi za Makao Makuu ya CCM pamoja na maeneo ya Dodoma Hotel na NAM Hotel ambako wengi wa wapambe hao wa Lowassa wamechukua vyumba kwa ajili ya malazi, wengi wao walikuwa wakionyesha nyuso za huzuni, huku wakionekana kuchanganyikiwa bila kufahamu ni nini hasa kilichokuwa kikiendelea ndani ya chama hicho.

TETESI: Mwigulu Nchemba Apeta Urais 2015

0
0
Breaking news kutoka Dodoma....

Katika hali ya kushangaza,mwigulu nchemba ameibuka kuwa kinara kati ya watangaza nia wote wa urais...

Ubora wake umechochewa na uadilifu wake ndani ya chama na serikali,ambapo hkn mazingira yyt yanayomzungumzia mwigulu nchemba juu ya ubadhirifu ama utendaji mbovu ktk ngazi alizowahi shikilia.
Mwigulu nchemba amekua bora na wa mfano ktk kujenga hoja makini zenye kujenga taifa na chama kwa ujumla,ni mtu mwenye uthubutu,jasiri anayesimamia maamuzi yake yaliyo makini,ni mkweli,mpenda haki na mtulivu pia mwenye hekima na busara.....

Amejaribu kulinganishwa na wagombea wengine ktk nyanja mbalimbali kama
Uchapakazi,
Uzoefu ktk chama na serikali....hapo ameonekana mwiba haswaa kutokana na nyadhifa kubwa alizotumikia ndn ya chama tena kwa mda mfupi ktk hilo amejikuta akiwapiku mbali wagombea wote...

Uadilifu....bado kete ilionekana ikimwangukia yeye akipambana vikali na jaji ramadhan pmj na mama migiro...

Lingine pia uwezo binafsi wa kisiasa....bado mwigulu alizidi kukimbiza wenzake kutokana na historia yake ya ushiriki wa aina zote za siasa.....

Zaidi ya yote ajenda aliyoibeba imegusa matumaini ya wana ccm wengi kuelekea kwa wananchi ambapo imeonekanika mwigulu nchemba ameeleweka kwa watanzania wengi kwa ajenda yake hivyo ni rahisi kuuzika pasipo na shaka...

Mwigulu nchemba anatafsiriwa kama mtu pekee asiye na makundi ndani ya CCM kiasi ambapo ana uwezo wa kuwaunganisha wana ccm wote kutoka ktk makundi yao...

Kwa ufupi amevishinda vigezo vyote 13 tena kwa kishindo haswaa...

Uhakika wa jambo ulichagizwa na kijembe cha mh rais jana wkt wa hotuba yake bungeni ambapo aliwashukuru viongozi wote aliofanya nao kazi akiwemo Edward lowasa,
Mara tu baada ya kutaja jina la lowasa JK akamalizia kwa kwa kusema mpo wengi sana na wengine ni vigogo.....tusinuniane kwa watakaokatwa....

Hapa Dodoma watu hawaamini kiasi ilianza kusikika jana baadhi ya wagombea wameanza kukata tamaa kutaka kujitoa...

Jaji Mutungi Atumika Katika Jaribio la Kumuengua Lowassa Katika Uteuzi CCM

0
0
JAJI MUTUNGI ATUMIKA KATIKA JARIBIO LA KUMUENGUA LOWASSA

MIKAKATI YATENGENEZWA KUONESHA LOWASSA ALIANZA KAMPENI MAPEMA

SIRI NYETI ZAVUJA


Wakati Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikiendelea na hekaheka za vikao vya uteuzi wa wagombea ili kumpata mgombea atakaye peperusha chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, jaribio jipya lakutaka kumzuia kada wa chama hicho ndugu Edward Lowassa imefahamika.

Habari kutoka vikao vya ndani vya siri vilivyo kaa kuanzia juzi, jana, na leo vimeripoti kuwa mkakati huo mahususi na wa siri uliowakutanisha vigogo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) umeazimia kumshinikiza msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kuandaa taarifa itakayo mtia hatiani ndugu Edward Lowassa kwa kuonesha kuwa alianza kampeni kabla ya wakati.

Mkakati huo wenye Baraka za vigogo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) umeratibiwa kwa umakini mkubwa kwa msukumo wa wagombea wanatajwa kwa majina ya Bernard Membe, Mizengo Pinda, Januari Makamba na John Pombe Magufuli, ambao pia wamepata Baraka kutoka kwa baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi.
Mkakati huo wa kumtumia Jaji Francis Mutungi unakwenda sambamba na matamko ya hivi karibuni yaliyo ratibiwa na Mchungaji Christopher Mtikila kwa kuwataja makada wa Chama Cha Mapinduzi kuwa wamekiuka kanuni na kuvunja sheria ya uchaguzi lakini mhusika mkuu akiwa ni ndugu Edward Lowassa.

Katika mkakati huu Jaji Francis Mutungi ameshinikizwa kueleza kisheria kuwa Edward lowassa amevunja kanuni wakati wa kukusanya wadhamini pia mtoa taarifa wetu alieleza kuwa Jaji Francis Mutungi ameahidiwa nafasi nyeti serikalini endapo atafanikiwa kujenga hoja zenye mashiko ya kumtia Edward Lowassa hatiani. Alipotafutwa kwa simu, Jaji Francis Mutungi simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno pia hakujibu.

Ripoti ya mkakati huu inatarajiwa kuwasilishwa kesho mapema na Jaji Francis Mutungi kwa vigogo wa Chama Cha Mapinduzi na baadae Kamati Kuu lakini kwa masharti kwamba Jaji Francis Mutungi awahakikishie kwa hoja za kisheria vigogo hao namna ya kumtia hatiani Edward Lowassa ili apoteze sifa za kuteuliwa na hatimaye kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi.

Wakati hayo yakiendelea, imeelezwa kuwa Mwenyekiti wa chama amekuwa akipata shinikizo kubwa kutoka kwa watu wasio kitakia mema Chama Cha Mapinduzi na hata shinikizo kutoka kwa familia yake kuwa Edward Lowassa akiteuliwa kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi na hatimaye kushinda kiti cha urais kwamba anampango wa kulipa kisasi kwa vigogo wa serikali ya sasa.

Mwandishi wetu alipo fanya mahojiano na wajumbe wa Nec wa mikoa ya Morogoro na Mwanza juu ya mikakati hii haramu dhidi ya mdugu Edward lowassa mmoja wa waNec hao alisema “ndugu yangu sikia nikuambie unajua ni kwa nini Nape alitoa tamko kuwa muda wa kukata rufaa hautoshi, na kwa nini vikao vya maadili na kamati kuu vimesogezwa mbele hii yote ni kuanda mikakati ya kumtosa Edward Lowassa lakini nikuhakikishie ndugu yangu mwisho wa hiki chama utakuwa kesho kwenye vikao vya Nec kwa sababu mambo yote wanayo yafanya tunapata taarifa, ndugu mwandishi kama hauamini subiri kesho kwenye vikao vya Nec” alisikika mmoja wa wajumbe wa Nec kutoka mkoa wa Morogoro.

Mnyetishaji wetu huyo alitaja majina ya vigogo wanao pigiwa chepuo kuwa ni Bernard Membe, John Magufuli, Garib Bilal, January Makamba na Dr. Asha Rose Migiro huku mikakati ikiwa kumfanya Bernard Membe awe Mgombea wa CCM kwa kumwekea wagombea dhaifu.

Wakati huohuo Ndugu Sendeka aliitwa na mh Benard Membe nakutaka kumpatia kitita cha shilingi za kitanzania milioni kumi ili amsemee vizuri katika vikao vya Nec na ndugu Sendeka kukataa mradi huo.

Ni Mimi Mwalimu Julius/Jamii Forums

Bagamoyo Road Haipiti Kuanzia Bunju A, Baada Ya Ajali iliyoua Mtoto wa Shule..Wanafunzi Walala Barabarani

0
0
Kama ulikua na ratiba ya kwenda bagamoyo acha kabisa.

Watoto wa shule ya msingi wamelala barabarani baada ya mwenzao mmoja kugongwa na gari na inasemekana amefariki dunia, hvyo kuanzia Bunju A Bunju B kuendelea ni balaa hata baiskeli hakuna wameshika mifagio na magongo na raia wako makini kuangalia kinacho endea.

Stay tune for update.

CCM wakanusha taarifa inayosambazwa kwa kasi kuhusu Kamati ya Usalama na Maadili

0
0

TAARIFA KWA UMMA

Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa na juhudi za uzushi na upotoshaji zinazofanywa na baadhi ya watu kwa malengo binafsi.

CCM inasisitiza kuwa hakuna taarifa yoyote ya Usalama na Maadili iliyoandaliwa na kuchapwa na kwamba kinachosambazwa mtaani ni uzushi wenye lengo la kuwachafua baadhi ya wanaoomba ridhaa ya CCM kuwania nafasi ya Urais kwa malengo mabaya.

CCM haitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote watakaobainika kuendesha harakati za kuandaa na kusambaza uzushi wa aina yoyote dhidi ya shughuli za Chama.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Umma - CCM HQ

Rose Muhando: Nafikiria Kurudi Kwenye Uislamu

0
0
NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.

Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.

“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.

Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.

Chanzo: GPL

Ushauri: Mume Hataki Kufanya Mapenzi na Mimi, Anamtaka Mtoto Niliyezaa Kabla ya Kunioa

0
0
Naombeni ushauri wenu,

Mawazo ya wengi ndio nitakayoyafanyia kazi. Nimefunga ndoa na mwanaume mwenye watoto 4 wawili wakike wawali wa kiume. Mama yao alifariki kwa ajali ya gari aliwaacha wadogo wakiwa primary.

Na mimi niliolewa nikiwa na mtoto mmoja wa kike ambae kiumri analongana na mtoto wake watatu. Kusema ukweli mwanzoni iliniwia ngumu sana kukubali ombi lake hasa nikifikiria kulea watoto wa mama mwingine wanikubali, je, vipi kuhusu huyu nilienae?

Baada ya muda kupita na kukolea kimapenzi nilijubaliana nae tukafunga ndoa tukaunganisha familia wote wakawa kitu kimoja. Mungu akabariki tujaliwa kupata mtoto mmoja. Kiukweli niliwapenda sana hawa watoto, niliwalea kama wangu.

Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuwafanya wasijione wakiwa. Kama zawadi nk nilitowa mezani bila kubagua sikupenda kuweka makundi na hili shahidi ni Mungu pekee. Watoto watatu wapo chuo kikuu na mmoja wa kwake yupo form six.

Katika ndoa yangu kulikua na migongano upande wa tendo la ndoa, kabla ya ndoa tukiwa kwenye stori za mapenzi niliwahi kumweleza mwenzangu kuwa mimi sio mtundu sana upande wa sex ivyo ningependa yeye awe mwalimu kwangu kwani tangu mwanaume wa kwanza anidanganye na kunipa ujauzito sikuwa tena kuwa na byfriend.

Akiniambia sawa. Tulipoingia kwenye ndoa mwenzangu alianza kubadilika wakati mwingine alikaa hata miez 8-10 bila kutaka sex.Nikimuuliza husema amechoka au hajisikii.

Hata huo muda anaokaa mpaka mimi nimchokoze na hii nikutakana na kushindwa kuvumilia. Kuna wakat aliamua kuniambia ukweli kuwa sijui mapenzi, niliumia ila nilikubali kuwa ni kweli sijui ila anisaidie kujua.

Hakufanya ivo. Ilifikiwa wakati nikaona ngoja nikae nisimsumbue ila nilijiuliza nitaishi hivi mpaka lini na kusaliti ndoa siwezi. Nilimwomba Mungu sana anipe uvumilivu ila pia Mungu aseme na mimi juu ya hii ndoa.

Mungu ni mwaminifu. Baada baada ya maombi ya zaidi ya mwaka mke wa shemeji yangu alileta malalamiko kuwa mume wangu amekua akimsubua sana kimapenzi ikiwa ni pamoja nakumtumia picha za ex.

Niliziona hakuishia hapo akasema hata hawa wadada wa kazi huwa anatembea nao. Nilipowabana waliopo na walioondoka walikubali na kunipa ushahidi. Mbaya zaidi hata huyu mwanangu alishamtaka kimapenzi sina uhakika kama alifanikiwa au la.

Ninaumia sana sana. Mtaani ndoa yangu imekua mfano wa kuigwa hio ni kutokana na jinsi tunavoonekana kwa watu. Lakini hii yote onatokana na jinsi nisivopenda watu wajue mambo ya ndani. Ninampenda, ninamheshim, ninamjali.Siruhusu nguo au chakula cha mume wangu afanye mwingine nikiwepo.

Hata kama tumegombana nisingependa yoyote ajue, nilijitahidi sana, kuwa mtiifu na mnyenyekevu kwake. Hii nikutokana na malezi niliyolelewa. Hata kama amesafiri watoto watajua baba anarudi kwakua wataniona jinsi ninavokua busy jikoni na kuandaa juisi na matunda.

Ushauri wenu muhimu sana kwangu

Asanteni

Vikao Vyote vya CCM Kufanyika Leo Na Majina ya 5 Bora na 3 Bora Yatajulikana leo

0
0
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11, 2015.

Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu.

Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau ingawa hakueleza ni wadau gani. Video:

UPDATES:Ajali ya Gari Bunju iliyouwa Mwanafunzi wa Shule Yasababisha Wananchi Wachoma Kituo cha Polisi..Picha hizi Hapa

0
0
Wananchi wamechoma moto Kituo cha Polisi Bunju 'A' na kusababisha Askari Kukimbia Kituo hicho cha Polisi, kwa ujumla hali haikuwa shwari  kwa Masaa manne hadi kusababisha Bara bara kufungwa kwa Muda....

Mahabusu waliokuwa ndani wametoka salama baada ya kufunguliwa na msamaria mwema





Hata Yesu Alipingwa Pia, Usijali Edward Lowassa Kitaeleweka Tu

0
0
Yule Mwalimu Mkuu wa Walimu na Mtakatifu wa Watakatifu kuliko wote waliowahi kuishi Dunia hii na Mwanzilishi wa Dini ya Kikristo, Yesu Kristo pia alipingwa sana kuanzia alivyozaliwa tu watu hasa maelite, Wafalme wenye madaraka makubwa walimpinga, wakamdhihaki na hata kumkamata na kumweka ndani, sasa ni kwa nini walifanya hivyo? ni kwa sababu ya Woga wa mabadiliko, walijua sasa Utawala wao wa dhuluma uko hatarini hivyo haya yanayotokea na anayofanyiwa Bw.Lowasa ni ishara tosha kwangu mimi kama Muumini na mfuasi mkubwa wa Mafundisho ya Mwalimu Yesu Kristo naamini kabisa ya kwamba Bw.Lowasa ndiyo anyefaa klk wote kuiongoza TanZania!

Hapo mwanzo sikumkubali lkn hizi chuki na kampeni chafu anazofanyiwa zimenifanya nijiulize maswali mengi na magumu, ni kwa nini haswa? Kama ni Ufisadi mbona kila anayegombea ana wake, ni kwa nini yeye tu? Hapo ndipo nikajua kuna kitu na siyo Bure!

Dunia nzima haya yanayotokea siyo mageni watu ambao huwa wanakuja kuleta mabadilko huwa wanapingwa kwanza, kuanzia Martini Luther (orijino na siyo mchumia tumbo wa USA) kama vile Mlm.Yesu Kristo pia alipingwa na Kanisa Katoliki na Mapapa wa wakati huo lkn mapendekzo yake Kanisa Katoliki liliyachukuwa na kuyatumia, Mandela alipingwa mpaka na kuwekwa jela leo hii waliompinga, kumkebehi na kumuita Gaidi wameweka sanamu yake kwa kumkumbuka kwenye Miji yao (London)...

Dedicated to Bw. Lowassa!

Huu Ndio Mshahara Mchezaji Ramadhani Singano Anaopewa na AZAM FC Baada ya Simba Kumzengua kwa Mkataba Feki

0
0
Stori kubwa leo hii  ni aliyekuwa winga wa Simba SC, Ramadhan Singano ‘Messi’ kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Azam fc, ikiwa ni siku mbili tu tangu TFF wavunje mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.
Messi amesaini mkataba mnono kwa dau la milioni 50 na atakuwa analipwa mshahara wa Milioni 2 kwa mwezi.
Kabla ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na Simba, Wekundu wa Msimbazi walitaka winga huyo asaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la milioni 30 na mshahara wa milioni 1.5, lakini alikataa.

Dully Sykes Achukua Maamuzi Magumu Kama Alivyofanya Ali Kiba...Aamua Kuwa Unfollow Watu Wote Kwenye Page yake ya Instagram..Sababu Hizi Hapa

0
0
Mwimbaji mkongwe Dully Sykes ameamua kufuata nyayo za Mwanamuziki Ali Kiba Kwa kuamua kutomfollow mtu yoyote kwenye page yake ya Instagram, Baada ya kuulizwa Sababu kwanini amefanya hivyo Dully Sykes Amesema amefanya hivyo kuepuka pressha za watu ambao wana tabia za kuwasema watu wengine na kushawisha watu wengine wamchukie fulani au kupost vitu asivyopenda ..Dully Amedai ni bora afollow page za kutoa Habari kuliko kumfollow mtu mmoja mmoja ambao wamekuwa ndio vyanzo vya Beef za mitandaoni....

Una maoni Gani?
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images