Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Kingunge Aendelea Kumlilia LOWASSA......Asema CCM ni Chama cha Watu wote na Lowassa si fisadi kama inavyodaiwa.

$
0
0
Mwanasiasa Mkongwe katika medani za siasa nchini Tanzania ameibuka na kuzungumza na Waandishi wa Habari leo  kuhusiana na  mchakato wa kumpata mgombea Urais CCM uliopelekea jina la Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kukatwa.

Akizungumza katika mkutano huo Kingunge amesema   Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika  kuwajadili wagombea  lakini safari hii Kamati ya Maadili imefanya kazi isiyowahusu kikatiba  ikiwemo  kukata majina ya wagombea.

Amesema  Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama kwa kujipa madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.

“Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.” Amesema Kingunge.

Kingunge  amedai kwamba  CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani, amedai kuwa  kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama wengine.

"Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya."

Amesisitiza kuwa kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote. Kamati Kuu ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu,  na Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo haukuwepo

Kingunge amesema  anawaheshimu sana Mzee  Benjamin  Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini amesikitika kuwa  ndio  waliotoa  michango  ya  kutotoa  haki kwenye Kamati Kuu.
 
"Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6,” alisema Kingunge.

Akizungumzia yaliyokea NEC Kingunge amesema wajumbe walihoji kwa nini  Jina La Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie kwenye orodha. "......Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama ulijaribiwa baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 5."

Kwa upande mwingine, amewapongeza wajumbe walijitokeza kukataa  maamuzi ya Kamati Kuu ikiwemo  Adam Kimbisa, Mbunge wa Songea Emmanuel  Nchimbi na Sophia Simba.

Akizungumzia kauli ya Mbunge huyo kuhusishwa na ufisadi Kingunge amesema,

"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu."

Kingunge  ameongeza kuwa  Lowassa sio wa kwanza kuwajibika kisiasa .Amesema katika  awamu ya kwanza ya Mwalimu –walikuwemo   viongozi wa kisiasa waliouzulu.
 
Amewataja waliowahi kujiuzulu  kuwa   ni Waziri wa Mambo ya Ndani,  Ali Hassani Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.

“Lowassa alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.

“Yote haya yalipangwa na ‘Kitengo’ kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” amesema  mzee Kingunge.

Amesisitiza kuwa  Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu

Ametumia mkutano huo pia kuwaomba viongozi ndani ya CCM warudi kusoma ahadi za mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM na kusisitiza kuwa  kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.

Wema Sepetu na Aunty Ezekiel Beef Upya...Chanzo Nimekuwekea Hapa

$
0
0

URAFIKI wa mashaka! Mastaa wawili wa filamu Bongo, ambao walikuwa mashosti  kwa muda mrefu kabla ya kidudumtu kuingilia kati hivi karibuni na kusuluhishwa, hivi sasa bifu kati yao limeanza upya, Risasi Mchanganyiko linakujuza.

Chanzo chetu ambacho hakipepesi macho kinasema tangu Aunt ajifungue mtoto, Wema hakuwahi kukanyaga nyumbani kwake kwa ajili ya kumuona, kutoa hongera au hata pole kwa rafiki yake huyo, isipokuwa wamekuwa wakichati kupitia simu za mikononi, kitu ambacho si sahihi.

Lakini kali zaidi, ni kitendo cha Wema kushindwa kuhudhuria sherehe ya kutimiza siku 40 tangu azaliwe mtoto huyo, Cookie, kitu kilichomfanya mwenzake kumuondoa kabisa katika orodha ya marafiki zake.

“Yaani Aunt kipindi chote alimvumilia akijua huenda yuko ‘bize’, lakini kwa kutofika kwenye siku hiyo muhimu, amemtoa kabisa akilini mwake,” kilisema.

Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Aunt ili kuthibitisha ubuyu huo, lakini akakubali tu juu ya kutohudhuria kwenye tukio hilo muhimu la mtoto wake, licha ya kuwa alimpa taarifa.

“Hakuja, lakini siwezi mlaumu sana, labda alikuwa na majukumu mengi, ukizingatia hivi sasa ana mambo ya ubunge,” alisema.

Wema hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutopokelewa kwa muda wote alipopigiwa.

ROSE MHANDO Amkimbia Meneja Wake

$
0
0
NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kumkimbia meneja wake, Alex Msama licha ya kuwepo kwa makubaliano kati yao yaliyohusu kulipiwa deni la kiasi cha shilingi milioni sita alizokuwa akidaiwa msanii huyo mwenye jina kubwa.

Alex Msama ambaye ni meneja wa Rose muhando.

“Meneja wake alikubali kumlipia pesa zote (6,500,000) ambazo Rose alikuwa anadaiwa baada ya kushindwa kuhudhuria tamasha moja huko mikoani, alitakiwa baada ya siku chache aingie studio kufanya kazi, lakini ametoweka na haifahamiki yupo wapi,” kilisema chanzo chetu.

Msama alipotafutwa alikiri kutokea kwa tukio hilo, akisema haeleweki Rose ana matatizo gani kwani walikubaliana baada ya siku chache aingie studio na kurekodi, lakini mpaka hivi sasa haijulikani alipo na hata simu yake ya mkononi haipatikani.
GPL

Gazeti hili lilimtafuta Rose bila mafanikio kwani simu yake haikuwa hewani.

Shamsa Ford:Naomba USINITESE, USINIUMIZE NA USINILIZE, Kama Sina Thamani Yoyote Kwako Naomba Ukae Mbali na Mimi ....

$
0
0
Nina upendo kwa kila mtu bila ubaguzi, naishi maisha yangu halisi wala siigizi, nina huruma kwa kila mtu, sipendi ugomvi na mtu.

Nakuomba na wewe binadamu kabla hujafikilia kunibania riziki yangu kumbuka nina mtoto ambae anahitaji hiyo riziki.

Wewe binadamu kabla hujanifanyia ubaya wowote kumbuka nina mtoto ambaye kitamuumiza zaidi ya mimi coz furaha yake ni kumuona mama yake.

Wewe binadamu kabla ya kutaka kuniumiza na kutaka kunipa stress za kijinga naomba umfikilie mwanangu ambaye ananitegemea mimi.

Ukinipa stress nitashindwa kufanya kazi na mwanangu atakosa haki zake za msingi.

Naomba wewe binadamu USINITESE,USINIUMIZE,USINILIZE, kama sina thamani yoyote kwako naomba ukae mbali na mimi kuliko kuwa mnafiki kwangu au kwa ajili ya masilahi yako binafsi....

Shamsa Ford on instagram

Mwigizaji Vicent Kigosi ‘Ray’ Akana Kata Kata Kujichubua Ngozi yake...Asema Haya

$
0
0
Staa wa Bongo Movies, Vicent Kigosi ‘Ray’ amekanusha madai kuwa anajichubua.

Ray ameiambia Bongo5 kuwa anasikitishwa na watu wanaodai kuwa anajichubua bila kujua kuwa mtu akiwa na maisha mazuri anaweza kubadilika.

“Kwanza sijichubui, tatizo unajua baadhi ya watanzania wengi, hawaelewi mimi sijichubui, ila maisha yamebadilika,” amesema.

“Unajua unapokuwa na maisha magumu ya kwanza, unaposhindwa kujikimu, kujinunulia nguo, yaani kufanya unachokitaka kwa muda unaoutaka, unakuwa mweusi kwa sababu huna hela ya kujikimu, sasa unapopata pesa kidogo ya kujikimu, unapokuwa na maisha mazuri , kwako kuna AC, kwenye gari yako kuna AC, hupati jua huwezi kuwa mweusi,” amesisitiza.

“Pia ukishakuwa star lazima muonekano wako uwe tofauti kidogo ili uwe tofauti kidogo. Hawa wanaoona mimi najichubua labla wanaona vibaya! Mimi sijichubui na waache waendelee kuzungumza kwa sababu mtanzania huwezi kumzuia kuzungumza.”

Bongo5

LINAH SANGA: Nimempata Mwanaume wa Ndoto zangu, Alinikuta Nikiwa kwenye Maumivu ya Mapenzi

$
0
0
Linah Sanga amedai kuwa amempata mwanaume aliyekuwa akimtafuta kwa muda mrefu na alikuja katika maisha yake muda aliokuwa ameumizwa kimapenzi.

Akizungumza na Bongo5 leo, Linah amesema mwanaume aliye naye kwa sasa ni mwanaume aliyekuja kumuokoa akiwa katika wakati mgumu wa kimapenzi.

“Kiukweli malengo yetu ni ndoa na wala haitachukua muda mrefu. Mungu akijalia mwakani,” amesema Linah. “Sasa hivi nataka ndoa mambo ya kuzini sitaki. Mimi sidhani kama ndoa ina ugumu wowote. Nataka sasa hivi kuwa wa halali kwa mtu mmoja na baadaye tupate watoto. Kwa jinsi tulivyoongea kazi ni kazi na mapenzi ni mapenzi, kwahiyo nafasi yangu ya kazi itakuwa pale pale. Na ninafikiri huyu ni mtu sahihi kwangu, ninafikiri ni mtu ambaye anaweza akawa mume wangu ndio maana nimekimbilia ndoa,” ameongeza.

“Amekuja kwangu kama mtu anayenipenda, ameona jinsi ninavyoumia kimapenzi. Kwahiyo huyu amekuja kama mtu mwenye nia, ni aina ya mwanaume ambaye nilikuwa namtafuta kwa muda mrefu na hatimaye amefika, sasa hivi nafurahi.”

DIAMOND NA DAVIDO Wakutana Tena Laivu Huko South AFRICA...Hichi ndio Kilitokea Baada ya Kuonana

$
0
0
Imekuwa story ambayo kiukweli kwa mtu anayefuatilia muziki haitaji hata kusimuliwa kilichokuwa kinaendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja kati ya Davido na Diamond Platnumz ambao ilidaiwa kwamba wameingia kwenye beef au kutoelewana.

Ukaribu wa mastaa hao wawili ulizaliwa baada ya collabo ya My Number One Remix, baadae mambo yakageuka, kukawa na kama uhusiano mbaya na kila kitu kilikuwa kikibebwa na story za mitandaoni hasa Facebook na Instagram, mashabiki kwa upande mwingine huenda ndio waliohusika pia kuifanya ishu kuwa kubwa zaidi.

Davido aliwahi kupost picha ya Bendera ya TZ alafu akaweka alama ya love.. leo Meneja wa Diamond Platnumz, Hamis Taletale aka Babu Tale amepost picha inayowaonesha wakiwa pamoja, Diamond, Davido, na Mameneja wa Daimond, Salam na Babu Tale mwenyewe.

Pia Davido alipost picha akiwa na mastaa wengine pamoja na Diamond Platnumz kama inavyoonekana hapa chini na kuandika with my ni*** na akamention Diamond kwenye Instagram.

Utendaji wa Magufuli na Mfano wa Msichana wa Kazi za Ndani...

$
0
0
Kuna wanaume wengi sana walio wahi kuoa wasichana wao wa kazi (house girl) sio kwamba wanaume hao wanaamua kuwaoa wafanyakazi wao wa ndani bila sababu, sababu kubwa kabisa huwa ni kuvutiwa kwa uchapa kazi wao, utiifu nidham na heshima ambazo huonyesha mbele ya mabosi wao.

Unakuta mfanyakazi huyo wa ndani anafanya mambo Makubwa hata kumzidi mke ambae hajui watoto wamekula au hawajala, wanaumwa ama la.

Kwa vile wanaume wengi huvutiwa na tabia hizi za kujituma wakati mwingine hupelekea mwanaume kuanza mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi wake ambae humjali kwa kila kitu hapo nyumbani, mapenzi yakikolea mwanaume wakati mwingine huchukua maamuzi ya kufunga ndoa na mfanyakazi wake.

Lakini bahati mbaya kabisa mwanamke huyu baada ya kuolewa huanza kuziacha zile tabia ambazo ndo zilizomvutia mwanaume mpaka akafikia maamuzi ya kumuoa, majuto makubwa hufuata kwa mwanaume kwakuwa huwa hana uwezo tena wa kuachana nae.

Ninavyo fikiri mimi, kila kiongozi wa ngazi ya juu huwa tunamchagua kwa kuvutiwa na sera zake lakini baada ya muda mfupi huwa tunajuta na kuanza kujilaumu kwa uchaguzi wetu.

Swali, je? Tukimpa nchi Magufuli ataendelea na uchapa kazi wake au atabweteka baada ya kuwa rais?

Wakenya kumpokea Obama wakiwa uchi ?

$
0
0
Kundi la Wakenya, limejiapiza kumkaribisha rais wa Marekani, Barack Obama, nchini kwao wakiwa hawajavaa nguo ili kuonesha kuwa hawajakubaliana na kitendo cha kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.

Obama anatarajiwa kutembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu kuwa rais na kutegemea kuwa na mkutano na wafanyabiashara kuanzia Julai 24-26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa barua iliyosambazwa na kundi hilo la wakenya, imedai kuwa watafanya maandamano ya amani jijini Nairobi, Julai 22 na 23 mwaka huu kuanzia Uhuru kona.

Wamedai kuwa maandamano hayo yatafanywa na wanawake pia wanaume takriban 5,000 wakiwa watupu bila nguo yoyote kupinga Umoja wa nchi za Amerika kupitisha sheria ya mashoga kutambuliwa kisheria.

Wamesema lengo kuu la maandamano wakiwa uchi ni kumuonesha na kuelewesha rais Obama, utofauti uliopo kati ya wanawake na wanaume.

Wiki iliyopita, Wakenya hao walienda katika mitaa kuandamana wakimuonya rais Obama, kutothubutu kuzungumzia suala la haki za mashoga kwenye ziara yake ya kutembelea nchi hiyo.

Mbunge Charles Njagagua, pia aliwataka wabunge kumfukuza Obama, nje ya Bunge mara moja akigusia haki za mashoga.

Naye Makamu wa rais nchini Kenya, William Ruto, hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wananchi wake kuwa wamesikia kuwa Marekani wameruhusu uhusiano wa mashoga na mambo mengine yasiyo na maadili na kuwataka viongozi wa dini kutetea nchi yao na kusimamia imani ya nchi yao.

Habari Kuhusu Blogger Maarufu Mange Kimambi Kukamatwa na Kutiwa Rumande

$
0
0
Kutoka Instagram:

Mrekebishatabia: Habari nyingine, blogger maarufu Mange Kimambi amekamatwa na kupelekwa rumande. Watu walikua wakimfuatilia mpaka alipoenda kuchukua fomu ya kugombea viti maalumu jimbo la Ubungo ndipo akakamatwa, Anasubiri Kufikishwa Mahakamani Wakati Wowote. Tutajua zaidi kwanini amekamatwa! 2h

Lemutuz_nation: OK guys so far nimerpoti the TRUTH and FACTS on ishu ya Mange na mpaka sasa kuna Watu wengine maarufu 2 zaidi waliojitokeza kumfungulia mashitaka so sasa wanafikia 4......NOW BADO I AM TRYING TO DIGGEST ALL THESE nilienda Polisi mwenyewe kupata Ukweli na walinipa ruhusa ya kumuona ila sikujisikia kumuona BUT ANYTIME FROM KESHO NITASEMA NENO ON HER ISHU.....kama kawaida I AM THE KING OF ALL BONGO SOCIAL MEDIA NETWORK hii habari ni my territory so NI WAJIBU WANGU KUTIA NENO AND TRUST ME THAT KESHO I WILL U KNOW TENA ON MY TIME NITAWEKA NENOZZZ so stay tuned!

Lemutuz_nation: Hapa ulikuwa MCHANA Mange alipokwenda kuchukua fomu ya Ubunge WA Kinondoni akiwa na kaka yake kulia Tawi LA CCM Mkwajuni Kinondoni.kumbe Nje kulikuwa na Polisi Mmoja wa Kiume na mwingine wa Kike waliokuwa wakimsubiri na Mtu mwingine anayedhaniwa kuwa ni kutoka Usalama wa Taifa...baada ya kumaliza kuchukua fomu tu akakutana na hawa watu 3 wakamuamuru aongoze Makao Makuu ya Polisi ambako alikaa kwa muda na kuelekea Polisi Osterbay ambako anashikiliwa mpaka sasa...TAYARI WATU WAWILI MAARUFU WAMESHAMFUNGULIA KESI MPAKA SASA SAA TANO KAMILI YA USIKU MWANAMKE MMOJA NA MWANAUME MMOJA MUME WA MTU MAARUFU SANA HAPA MJINI...pia juhudi za kumtoa kwa dhamana zinaendelea kwa nguvu kubwa sana.....BINAFSI BADO SINA LA KUSEMA HOWEVER SOON NITASEMA SOMETHING ABOUT THIS ISHU.....stay tuned! - le Mutuz
Read more at http://websta.me/n/lemutuz_nation#vlitRaJRkJkKTdU5.99

JOYCE KIRIA: Jamani Tumsaidieni MANGE KIMAMBI Mwanaharakati Aliyethubutu Kujitosa Mithili ya Swala Katikati ya Msitu Ulojaa Simba Wenye Njaa, Mpiganaji wa kweli Aliyejaaliwa Kipawa cha Kusema Bila Kumung'unya

$
0
0
‪#TAHADHARI‬! Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi, Tanzania Human Rights Defenders, Tawla, Wlac, Legal Human Right Center, Wildaf, Tume ya Haki za Binadam, Tamwa, Tgnp, Wananzania wote wapenda Maendeleo ya Halali, msaidieni huyu Mwanaharakati aliyethubutu Kujitosa mithili ya Swala katikati ya msitu ulojaa Simba wenye njaa, Mpiganaji wa kweli aliyejaaliwa Kipawa cha kusema bila kumumunya, ambae amejitokeza kupigania Haki za Binadamu kwa kupiga vita Madawa ya kulevya nchini mwetu!!

Kiukweli @mangekimambi_ Amejitosa upande ambao wengi wetu tunaojiita "Wanaharakati" tumeufumbia macho na tunaogopaaaaa kuwanyooshea vidole wanaohusika kwenye mtandao huo 🙌 Ila huyu Bi @mangekimambi_ Ni mtanzania pekee alieamua kujitoa Sadaka kwa ajili ya Watanzania wenzake hususan vijana wanaoangamia kwa kubwia unga au madawa ya kulevya kila kukicha....
Huyu @mangekimambi_ naona ana uthubutu wa hali ya juu mno katika kukemea maswala mbalimbali kwa maslahi ya wengi hasa Taifa likiwepo la madawa ya Kulevya, na hivyo kuhatarisha uhai wake. Kwa sasa ametangaza kutishiwa Uhai kwenye accont yake ya Insta kwamba kashikiwa BASTOLA jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho kabisa...

Kama kweli tunaipenda nchi yetu basi ni wakati wa kuwalinda Wanaharakati wanaojitokeza kuokoa kizazi cha vijana na Taifa hasa pale wanapojaribu kukemea uovu na kukumbwa na changamoto kubwa kama hiyo ya kutishiwa kuondolewa Uhai wao... Tusisubiri mtu auliwe ndo tuanze kutoa salam za pole bali tuchukue Tahadhari mapema...

Binafsi Nikijaribu kuvaa viatu vya kina RayC, Banza, na wengine wengi nadata na nazidi kukuombea Bi @mangekimambi_ Mungu akulinde kwenye hayo Mapambano maana yeye pekee ndo Mtetezi na Mtenda Haki Milele...
Nimeumizwa sanaaaaaa ila ndo ivo nchi hii tunawatukuza wanaopata pesa kwa kuangamiza watu wengine

Mchezaji Mwingine wa Tanzania Ala Shavu Kubwa South Africa..Apewa Mshahara wa Dola 5000 kwa Mwezi

$
0
0
Tumetoka kushuhudia mchezaji Singano akisaidi mkataba na Azam F.C na kuanza kulipwa mshahara wa Tsh millioni mbili kwa mwezi. Huyu hapa ni mchezaji mwingine wa Tanzania ambae amesaini mkataba na club ya South Africa inaitwa Jomo Cosmos kwa mshahara wa $5000 kwa mwezi baada ya kukatwa kodi.

Taarifa hii exclusive imeinifikia kutoka kwenye vyanzo vya uhakika japokua signing fee imegomwa kutajwa. Mchezaji mwenyewe ni Uhuru Suleimani ambae amewai kucheza kwenye club za Mwadui F.C, Coastal Union, Mtibwa na Simba. Club hii imepanda ligi kuu maarufu kama PSL, so atacheza na wakina Ngassa.All the best na hizi ni picha ambazo nimezipata kwa ajili yako.

KIM Kardashian Achafuka Tena, Video Nyingine Akifanya Ngono na Mwanaume yazangaa Mitandaoni

$
0
0
Los Angeles , Marekani
MTANGAZAJI maarufu wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian amezidi kuchafuka baada ya video yake nyingine aliyorekodi akifanya ngono kuzagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Video hiyo inamuonesha Kim akifanya ngono na mwanaume ambaye hakuweza kufahamika jina lake lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari Marekani vinadai si mumewe, Kanye West.

Hiyo inakuwa video ya pili kwa mwanadada huyo ikimuonesha akifanya ngono baada ya ile ya awali ambayo alijirekodi akiwa na ‘Ex-boyfriend’ wake Ray J.

Hatunae Tena Mwanamuziki Banza Stone, Afariki Dunia Leo Mchana

$
0
0
Muimbaji wa muziki wa dansi aliyewahi kutamba akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta na TOT Band, Ramadhan Masanja maarufu kama Banza Stone amefariki dunia mchana wa Ijumaa, July 17.

Banza alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Taarifa kuhusu kifo chake zimethibitishwa na kaka yake pamoja na mmiliki wa Twanga Pepeta, Asha Baraka. Kwa mujibu wa kaka yake, Jabir Masanja, msanii huyo alikuwa anasumbuliwa na fangasi kichwani mwake na dawa alizokuwa anatumia zilikuwa kali kiasi cha kumpotezea hamu ya kula.

Hivi karibuni mama yake mzazi aliongea na kituo cha redio cha EFM na kukiambia kuwa afya ya mwanae ilizidi kuzorota na alianza kugoma kula chakula wala kunywa kunywa dawa. Mama huyo alisema hadi siku hiyo Banza alikuwa amegoma kula kwa siku tatu mfululizo. AliongeZa kuwa pamoja na kuugua hivyo bado wasanii wenzake walishindwa kwenda kumjulia hali.

“Mpaka sasa sijamuona mtu yeyote aliyekuja kumshughulikia na kumwangalia, wamemwacha hivi hivi. Na mimi siwezi kuwalaumu kwanini hamjaja kumwangalia, kila mtu na moyo wake, mwenye kuja atakuja, mimi ntahangaika na mtoto wangu mpaka pale atakapoamua mwenyezi Mungu,” alisema Mama Banza.

Kabla ya hapo muimbaji huyo alizushiwa kufariki mara nyingi. Wiki chache zilizopita Banza alimongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM kukanusha.

“Ndio naumwa kichwa kina nisumbua sana lakini sasa hivi naendelea vizuri yaani hizo habari za kuzushiwa kifo naona sasa hivi kwangu sijui hata itakuwa mara ya ngapi, maana nimeshazushiwa sana. Mimi mzima na huyo anayeeneza azunguke na mikoa mingine aeneze vizuri,” alisema Banza.

“Lakini mimi nipo nyumbani hapa Sinza kwa Mama yangu sasa hivi hapa napata juice yaani marehumu anaongea,” aliongeza Banza kwa kicheko.

“Inshallah nikiwa vizuri mashabiki wangu wataniona tu lakini nipo mzima.”

Msiba upo nyumbani kwao Sinza, Dar es Salaam. Kwa wale wanaopenda kuchangia msiba wake wanaweza kumchangia kwa kutumia namba: 0715407088 au 0753786016.

Mungu ailaze mahali pema peponi. Amen.

Madiwani kwa Lowassa wasusa.....Kata zao zakosa Wagombea, Wasema Wanasubiri Tamko la Lowassa

$
0
0
Kasi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuomba nafasi za udiwani na ubunge katika Jimbo la Monduli, inasuasua na tayari chama hicho kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Siasa kitakachokutana leo kukuna vichwa kutafuta ufumbuzi wa hali hiyo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alisema jana kuwa kusuasua kwa wanachama kuchukua fomu za kuomba kugombea nafasi hizo kunatokana na kushuka kwa morali ya wanachama baada ya Mbunge wa zamani, Edward Lowassa, aliyekuwa akiwania kuteuliwa na chama chake kugombea urais, kukatwa jina lake.

“Zoezi la uchukuaji wa fomu za udiwani linasuasua, lilianza juzi na siku ya mwisho ni Julai 19, mwaka huu saa 10 jioni.

“Zoezi hili ni gumu sana, hata hivyo bado ni mapema sana kutoa taarifa, lakini morali ya wanachama kuchukua fomu za kuomba kugombea imepungua,” alisema.

Alisema ameitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Siasa chenye wajumbe 16 kuzungumzia suala hilo ili kwa pamoja wahamasishe wanachama kugombea.

“Tunawahimiza wanachama wajitokeze kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo,” alisema na kuongeza: “Hili jimbo ni ngome ya CCM na wala sina shaka na hilo.”

Alisema kusuasua huko kunatokana na baadhi ya madiwani waliomaliza muda wao kufanya propaganda ya kuwazuia wanachama kwenda kuchukua fomu kwa madai kwamba wasubiri kwanza kauli ya mbunge wao.

“Baadhi ya madiwani wa zamani wanatengeneza propaganda, hawa ni madiwani wale ambao hawakubaliki katika kata zao…wanawahamasisha watu wasichukue fomu kwa kigezo kwamba wasubiri kauli ya Mbunge Lowassa, jambo ambalo siyo kweli," alisema.

Aliongeza: “Lowassa hajawahi kufanya kitu kama hicho cha kuwaambia wanachama wasichukue fomu hadi atakapotoa kauli yake…jana (juzi), alikuja hapa Monduli kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hakutamka lolote, alisema tu hana la kusema.”

Alisema watu hao wanatumia mgongo wa Lowassa kueneza propaganda.

Alisema kwa upande wa ubunge hadi sasa amejitokeza mwanachama mmoja tu, Mbayani Tayayi, aliyechukua fomu yake jana saa 4:00 asubuhi, wakati kwa upande wa udiwani waliochukua fomu ni mwanachama mmoja mmoja katika kata za Mswakini, Lepurko na Engutoto.

Pamoja na kusuasua huko, Kimaro alisema atahakikisha kata zote 20 zinapata wagombea wa udiwani na kumpata mgombea ubunge.

Alizitaja kata hizo kuwa Engaruka, Engutoto, Esilalei, Lepurko, Loksale, Majengo, Makuyuni, Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mfereji, Mswakini, Mto wa Mbu, Migungani, Selela, Sepeko na Lashaini.

Alisema tangu kumalizika kwa mchakato kupata mgombea ndani ya chama hicho Julai 12, mwaka huu, mjini Dodoma ambapo jina la Lowassa lilikatwa katika mazingira ya kutatanisha, kumekuwa na maneno mengi yakisambaa kwenye mitandano ya kijamii kwamba Lowassa anakihama chama hicho.

“Hizi habari si za kweli, bado tuna imani na Lowassa,” alisema.

Alisema mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama hicho tayari umemalizika kwa kumpata mgombea wake, Dk. John Magufuli.

Hali ilivyo:
Baadhi ya wakazi mjini Monduli walisema kitendo cha kuenguliwa kwa mbunge wake katika kinyang’anyiro cha urais, kimewavunja moyo kwa maelezo kuwa utaratibu haukufanyika kwa haki.

Walisema wanahamasishana kuwapigia kura wagombea watakaosimamishwa na vyama vya upinzani wakidai CCM imefia mikononi mwa Mwenyekiti wao wa Taifa.

Katika kituo cha mabasi cha Monduli, wapiga debe walikuwa wakiwataka abiria ambao ni wanachama wa Chadema kuingia daladala za Arusha zilizopo kituoni hapo huku wakiwataka abiria ambao ni wanachama wa CCM kwenda kusubiri magari yao (mashangingi) yaliyopo eneo la CCM.

Wiki iliyopita, CCM walifanya vikao vya uteuzi wa mgombea wao.

Chama hicho kilimteua Dk. John Magufuli kwa asilimia 87.1 na Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mwenza ili kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Picha: Wema Sepetu Akichukua Fomu za Ubunge Mkoani Singida

$
0
0
Hizi ni baadhi ya picha za staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu akiwa na team yake alipokuwa mkoani Singida akichukua fomu kwenye ofisi za chama cha mapinduzi (CCM).

Wema anawania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kupitia jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya chama hicho.

Baada ya Lowassa KUKATWA........Vijana 30 wa CCM-Vyuo Kikuu Wahama na Kujiunga na CHADEMA

$
0
0
VIJANA takribani 30 wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), jana  wamesalimisha kadi zao za CCM katika tawi la Chadema lililopo Mwananyamala, jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa hawakuridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea wa urais wa CCM.

Vijana hao wa vyuo vikuu mbalimbali waliokuwa wakiimba wimbo wa tunaimani na Lowassa wamekabidhi kadi zao za CCM kwa Kaimu Mwenyekiti wa Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni ya Chadema, Bi. Esther Semaja na kukabidhiwa kadi za uanachama wa Chadema.

Msanii Ester Kiama Amwaga Machozi baada ya Kudaiwa ana UKIMWI

$
0
0
Msanii anayekuja kwa kasi katika anga la filamu, Ester Kiama amejikuta akiangua kilio kufuatia madai yanayoenezwa kuwa ana ‘ngoma’.

Taarifa ya ‘kuungua’ kwa staa huyo zimekuwa zikisambaa kama moto wa kifuu kwenye mitandao ya kijamii huku mwenyewe akidai anasingiziwa na hivyo juzi kati akaamua kwenda kupima.

“Hizi habari kwamba nina ngoma zimekuwa zikienea sana na hakuna kitu kibaya kama kumnyooshea mwenzako kidole bila kuwa na uhakika na unachokisema. Nakumbuka mara ya kwanza kuna mwanamke aliandika mtandaoni kuwa nimeathirika hivyo Dude ajihadhari.

“Niliumia sana lakini ili kuwakomoa nikaenda kupima na majibu yakaonesha niko safi, nikajikuta nalia sana, si unajua inavyouma kusingizwa kitu? Sasa ili kuwakata kilimilimi hao wanaonizushia, majibu haya nitayabandika mtandaoni pia,” alisema Ester.

Lowassa KUKATWA: Nape Amjibu Kingunge.......Amtaka Afanye Lolote Analotaka

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka mwanasiasa mkongwe, Kingunge-Ngombale Mwiru kufanya anachotaka kufanya.

Juzi Kingunge alijitokeza hadharani na kuzungumzia na waandishi wa habari huku akiwaambia kwamba kilichofanywa na CCM katika kumpata mgombea wa urais, Dk. John Magufuli ni haramu.

Dalili ya CCM kupasuka vipande zimeanza kuonekana dhahiri, baada ya Kingunge kujitokeza hadharani kupingana na maamuzi yote yaliyofanywa hususani kukata jina la Edward Lowassa katika hatua za mwanzo za kuteua mgombea urais.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (pichani), akizungumza na mtandao huu jana kuhusu tuhuma zilitolewa na Kingunge ambaye kadi yake ya uanachama ni namba nane, alijibu kwa kifupi kwamba afanye anachotaka kufanya na kwamba hana maoni zaidi.

“Sina Comment (maoni) wewe unataka niseme nini? kaandike hivyo nilivyosema kwa sababu na mimi ni mwandishi na nilishawahi kuwa mhariri kwa hiyo najua,” alisema na kukata simu.

Chama hicho tawala kilimteua Dk. John Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wake mwenza kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwakani.

Jumla ya watia nia 38 majina yao yaliingia katika vikao vya awali, lakini waliovuta kuingia tano bora ni Magufuli, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ali, Januari Makamba na Bernard Membe.

Hata hivyo, Halmashauri Kuu (NEC) iliwachuja Makamba na Membe na kuwabakiza Magufuli, Amina na Migiro kisha Magufuli kuibuka mshindi

Anayedai Kuwa ni Wifi wa Zari Kwa Diamond Azuiwa Getini Kwa Diamond....

$
0
0
Mrembo aliyedai ni dada wa hiyari wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliyejitambulisha kwa jina moja la Rose akijiita wifi wa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, hivi karibuni ameumia kupita maelezo baada ya kuzuiwa kuingia nyumbani kwa mastaa hao, Ijumaa lina mkanda mzima.
Rose ambaye ni ‘msichana wa mujini’ alijikuta akitiliwa ngumu na mlinzi nyumbani kwa Diamond maeneo ya Tegeta-Madale, Dar ambapo alikwenda kumuona Zari baada ya kusikia yupo Bongo.

Mlinzi akiwakatalia kuingia ndani.
Kwa mujibu wa Rose, kabla ya Diamond kuwa na uhusiano na Zari walikuwa wapo vizuri lakini baada ya kuwa na mama kijacho huyo, hajawahi kumuona na amekuwa akitamani waonane laivu bila mafanikio.

“Zari ni wifi yangu kwa Diamond (bila kufafanua uwifi kivipi). Pia napenda sana kazi za Diamond lakini tangu waanzishe uhusiano kila ninavyojitahidi niwaone inakuwa ngumu. Ningepata msaada wa kuwaona ningefurahi.
“Nilijaribu kuomba msaada kwa kaka mmoja ambaye ni rafiki wa Diamond lakini akaniambia Zari akiwepo pale nyumbani kwa Diamond hasa kipindi hiki ambacho ni mjamzito, ni ngumu mtu yeyote kuingia,” alisema mrembo huyo.
Ijumaa laamua kumpeleka

Baada ya kushindikana kumuona wifi yake amabaye ni ‘Zari’, Rose aliamua kurudi nyumbani.
Katika kuhakikisha kama alichokuwa akikisema kina ukweli, mmoja wa waandishi wa gazeti hili juzi Jumatano aliamua kumsindikiza Rose hadi nyumbani kwa staa huyo lakini katika hali ya kushangaza, mlinzi binafsi aliyekutwa aliweka ngumu kumfungulia mlango mdada huyo.
“Wewe kama unasema Diamond ni kaka yako na Zari ni wifi yako, ungewapigia simu kabla ya kuja, siwezi kuwafungulia geti,” alisema mlinzi huyo.
Rose: Lakini kaka ungenisaidia tu nikaingia ndani, Diamond akiniona hawezi kunizuia.
Mlinzi: Haiwezekani, tena naomba muondoke.
Kufuatia kuwekewa ngumu huko, mdada huyo aliondoka eneo hilo huku akiwa amenyong’onyea ambapo wakati hayo yote yakiendelea, mmoja wa mapaparazi wetu alikuwa akipiga picha kwa simu ya mkononi.

Kumbe ulinzi mkali
Baada ya dada huyo kutokubaliwa kuingia ndani ya nyumba ya Diamond licha ya kudai ni wifi wa Zari, Ijumaa lilizungumza na baadhi ya watu wanaoishi eneo hilo ambapo walisema ni ngumu sana kupenya kuingia ndani ya mjengo huo.
“Pale bwana wapo wengi wanakuja na kudai ni ndugu wa Diamond lakini wanaishia nje na kuondoka, bila taarifa mlinzi hawezi kukufungulia geti, kwa hiyo kuzuiwa kwa huyo anayedai ni wifi wa Zari siyo ishu,” alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shebe.

DIAMOND ANAMJUA?
Kama kawaida yake ya kutoa ujumbe upande mmoja na kupeleka upande wa pili ili kupata mzani, ‘kijumbe’ wa gazeti hili alimtafuta Diamond kwa mahewa akiwa kwenye ‘pipa’ kuelekea nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambapo alijibu kwa kifupi: “Nimekwambia simjui huyo dada.”

SIYO ROSE PEKEE
Mbali na Queen Darleen na Esma ambao ni dada zake wa ukweli wanaofahamika, wapo wasichana wengine kibao mjini ambao nao hudai ni dada zake wa hiari ambapo ukimwacha Rose pia yumo Halima Haroun ‘Kimwana’ ambaye hata Zari anamuita wifi licha ya kwamba hana undugu na Diamond.
DIAMOND K
ULAMBA TUZO
Wakati hayo yakiendelea, wikiendi hii Diamond anatarajiwa kulamba tuzo zinazofanyika Sauzi za MTV Music (Mama) baada ya kuteuliwa kuwania Vipengele vya Msanii Bora wa Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora wa Kiume Afrika na Wimbo Bora wa Kushirikiana Afrika.

KILA LA HERI DIAMOND
Dawati la Ijumaa linamtakia Diamond kila la heri ili ailetee heshima Tanzania katika anga la muziki wa Bongo Fleva. -Mhariri.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images