Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

BOB JUNIOR AWACHANA WASANII WA BONGO MOVIE WALIOJIUNGA NA CCM

0
0
Kufuatia baadhi ya wasanii wa Bongo Movies na mmoja wa Bongo Flava kutangaza kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi huko Mbeya katika Maanzimisho ya miaka 37 ya chama hicho. Kumekuepo na mawazo tofauti kuhusu uamuzi waliochokua wasanii hao. Wengine wakisema kua wasanii hao wamepewa mshiko ili waipaishe CCM wengine wakisema kua walichofanya ni jambo zuri.

Leo msanii Bob Junior kupitia mtandao mmoja wa kijamii aliamua kuwachana wasanii waliojiunga na CCM, alisema kua hakukua na ulazima wa wao kujiingiza katika siasa na pia alisisitiza kua hakukua na ulazima wa wao kujitangaza kua wameiunga na chama hicho. Moja ya kauli aliyoisema ni "muelewe kwamba iyo ni janja ya nyani kwani sio kuingia kila sehem mpaka watu wajue bongomoves so mjipange kwan mtaanguka kisanaa "

Itakumbukwa kua mwaka 2010 mwanadada Nakaya na msanii Marlow walijiingiza katika siasa jambo ambalo lililowafanya kushuka kimziki hadi leo hawasikiki. Msanii Marlow kupitia gazeti moja alisema kua anajutia kitendo chake cha kujiingiza katika siasa kwani kilimshusha sana kisanaa.

MWIGIZAJI MAINDA HOI HOSPITALINI..MWENYEWE AJIFARIJI NA UJUMBE HUU

0
0
Msanii wa Filamu Bongo,Ruth Suka 'Mainda', akiwa Hospitali na mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambayo jina lake hakutaka kulitaja mara moja. 
SOMA UJUMBE ALIOUANDIKA KWA MKONO WAKE HAPO CHINI...

maindasmallbabyTrowback.......imebaki historia tu......maana magonjwa sasa hayana nafasi kwangu....nimejua kwa kupigwa kwake Yesu mimi nilishaponywa kitambo. Asante yesu kwa kuchukua udhaifu wangu,magonjwa yangu,unyonge wangu...na Umenipa Tumaini maisha yangu yote acha nikutumikie ipasavyo.japo najua nitakutana na vikwazo ila nitashinda coz wewe ulishafanya njia siku nyingi.mapambano yanaendelea huku nikizidi kukukili wewe Yesu kuwa ndie Bwana na Mwamba wangu....EMMANUEL:GOD with US.........

TIKETI ZA ELEKTRONIKI MARUFUKU....HAIJAKAA VIZURI HII

0
0
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesitisha matumizi ya tiketi za kielektroniki kwenye viwanja vinane mpaka itakapotolewa taarifa nyingine.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana, zilisema TFF imeamua kufanya hivyo baada ya kubaini madudu mengi katika tiketi hizo.

Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambao unatumika kwa tiketi hizo, haukutumia tiketi hizo katika mechi yake ya juzi dhidi ya Kagera Sugar ya Kagera.

Hata hivyo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura alipotafutwa kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila majibu na hata ujumbe ufupi wa maneno aliotumiwa, hakuujibu.

Lakini Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF Kanda ya Kaskazini (Tanga na Kilimanjaro), Khalid Mohamed alisema mfumo huo sio tu unachanganya, lakini pia mashine zimeharibika.

“Sisi jana (juzi) hakukuwa na mechi kwenye Uwanja wa Mkwakwani, lakini katika mechi zijazo, hatutatumia tena mfumo wa kielektroniki, maana sio kwamba hatutaki, lakini hata hizo mashine zenyewe mbili zilizofungwa zimeharibika,” alisema Mohamed.

Lakini mtoa habari wetu alithibitisha jana kuwa licha ya kusimamishwa kwa tiketi hizo, pia jana kulikuwa na kikao kuzungumzia suala hilo ambalo limegonga vichwa tangu kuanza kutumika katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ulioanza Januari 25, mwaka huu.

Juzi, Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kuiagiza Sekretarieti, Benki ya CRDB na Bodi ya Ligi kufanya kikao cha dharura kwa ajili ya mapitio ya tiketi hizo ambazo zimekuwa na malalamiko.

Viwanja vilivyofungwa mfumo wa tiketi za kielektroniki ni Azam Complex, Kaitaba Bukoba, Jamhuri Morogoro, Kumbukumbu ya Sokoine Mbeya, Shekhe Amri Abeid Arusha, CCM Mkwakwani Tanga na CCM Kirumba Mwanza.

CHANZO HABARI LEO

SHILOLE HAKAMATIKI , AKIRI KUCHUNA MABUZI KAMA KAWAIDA YAKE

0
0
MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya na Filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,jana alianika wazi tabia yake ya uchunaji mabuzi alipokuwa kwenye moja ya mahojiano na watangazaji wa Kipindi cha Leo tena cha Clouds FM, baada ya kuulizwa swali liloendana na jina la kibao chake kipya ambacho jana ndiyo ilikuwa siku rasmi akikiachia hewna kupitia stesheni za radio hiyo,baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la NACHUNA BUZI...

Mmoja ya watangazaji wa kipindi hicho alimuuliza ni kitugani kilichompelekea hadi kutunga wimbo wa namna hiyo na kuupa jina hilo,Shilole katika majibu yake alisema kuwa ameamua kukipa jina hilo kufuatia historia mbalimbali za maisha yake,hususani wimbo wake uliopita ambao aliupa jina la Nakomaa na jiji la Dar,sasa kudhihirisha kauli hiyo ameamua kuchuna mabuzi ili aweze kupata mkwanja wakutosha kulihimili jiji la Dar es Salaam na Igunga abaki kwenda kusalimia ndugu na jamaa tu.Baada ya maneno hayo Shilole pia aliandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram:- 

MSEKWA:WAPINZANI WAKIUNGANA WANAWEZA ING'OA CCM MADARAKANI

0
0
Kiongozi Mstaafu wa CCM, Pius Msekwa amesema endapo vyama vya upinzani vikiungana na kuweka mikakati makini ya muda mrefu, vinaweza kuking’oa CCM madarakani.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wetu jana, Msekwa alisema kwa mtindo wa sasa wa vyama vya upinzani kila kimoja kusimama peke itakuwa ndoto kukishinda CCM.

“Kama vyama vya upinzani vinataka kuwe na upinzani wenye nguvu dhidi ya CCM ni lazima viungane vyote. Tena viweke mikakakati ya muda mrefu ya kujiimarisha,” alisema Msekwa kwenye mahojiano hayo.

Hata hivyo, alisema kuiondoa CCM madarakani siyo kazi rahisi kwa sababu mizizi yake imeenea kila kona ya nchi huku akisema wazo la upinzani kuungana halitakuwa rahisi kwa kuwa wengi wao ni walafi wa madaraka na hakuna atakayekuwa tayari kuvunja chama chake na kuunda kimoja kwa hofu ya kukosa uongozi.

Akijibu swali kuhusu nguvu ya Chadema kwa sasa Msekwa alisema: “Wanapambana na CCM kwenye majukwaa ya kisiasa lakini si kuwa na watu wengi wanaokiunga mkono.”

Alisema CCM kina mizizi hadi ngazi za chini kabisa nchi nzima tofauti na vyama vingine.

Alisema Chadema kiko katika baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara wakati Zanzibar hakina nafasi, tofauti na CUF ambacho alisema angalau kinaonyesha kuwa na nguvu visiwani huko.

Kuhusu Chadema kuwa na wabunge wengi Tanzania Bara, Msekwa alisema ni neema iliyokiangukia baada ya CCM kufanya makosa ya uteuzi kwa baadhi ya majimbo.

Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge alisema pamoja na neema hiyo, Chadema hakiwezi kufikia asilimia 40 ya wabunge wote.

“Kweli Chadema kimejitahidi lakini ukichunguza utabaini ni neema iliyowaangukia kutokana na makosa ya CCM kuteua watu ambao wapigakura walikuwa hawawataki,” alisema Msekwa.

Alisema Chadema kimekuwa kikionekana kufanya vizuri kwenye siasa za majukwaani kwa sababu kina nafasi kubwa ya kukosoa na hata kutoa madai ya kutunga dhidi ya CCM ili mradi yawe yanawagusa wananchi.

Kuhusu uwezekano wa vyama vya upinzani kuchukua nchi kutokana na CCM kuwa na makundi mengi ambayo yanaweza kukisambaratisha katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Msekwa alisema: “Hakuna mtu anayeweza kuondoka CCM na kuivunja nguvu. Hata akiwa ni kiongozi mwenye nguvu ya kisiasa kiasi gani ataondoka mwenyewe na CCM kubaki imara.”

UTAFITI:NGONO YA MDOMO NI HATARI

0
0
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.

Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,

 pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.

Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa  ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.

Katika utafiti  huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747  na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.

Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni  kuwavutia wapenzi wao katika  kushiriki ngono.

Vijana  wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.

Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.

Daktari  Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya  koo ni  ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume  nchini, ikiongozwa na ile ya  ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.

Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya  koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na  umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.

“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze  kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,” anasema  Dk Kahesa na kuongeza.

MBOWE AMJIBU KIKWETE"NAOMBA USIINGIZE UTANI KATIKA JAMBO ZITO LA TAIFA"

0
0
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemjibu Rais Jakaya Kikwete kwamba asiingize utani katika masuala mazito ya taifa. Mbowe alisema Katiba ya Tanzania, itaamuriwa na wananchi wenyewe na si Chama Cha Mapinduzi (CM) ambacho kimekuwa na mkakati mkali wa kutaka kuua maoni ya wananchi.

Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais Kikwete kudai amesikia kiongozi huyo wa upinzani akitangaza kutumia nguvu kupata Katiba mpya.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, wakati akihutubia sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa CCM. Alisema amesikitishwa na kauli hiyo na kuwataka Watanzania kutobabaishwa.

Kikwete alisema Katiba mpya itapatikana kwa hoja za kila upande kulingana na mapendekezo yake. 

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mbowe alisema Rais Kikwete hapaswi kuchukulia utani katika mambo mazito ya taifa.

“Namuomba Rais Kikwete asichukulie utani mambo ya taifa suala la Katiba mpya. Anapaswa kuzungumza mambo ya msingi ambayo yanaleta tija.

“Siku zote Katiba ya nchi inapatikana kwa dhamira nzuri lakini tumebaini wenzetu hawa CCM hawaheshimu hoja za wananchi.

“Hebu tujiulize jinsi Jaji Joseph Warioba alivyotumia fedha nyingi kukusanya maoni ya Watanzania, leo CCM hao hao wanayakataa tuwaeleweje?” alihoji Mbowe.

Alisema Jaji Warioba ametoa hoja za msingi lakini kwa sababu ya uoga wa CCM wanataka kupindisha ukweli wa mambo.

“Mzee wa watu huyu amezunguka taifa zima kwa fedha za walipa kodi wa nchi hii, sasa wanataka watumie wabunge wao kukwamisha mchakato huu,”alisema Mbowe.

Alisema kama utawala wa Rais Kikwete utashindwa kuleta Katiba mpya ambayo inakidhi matakwa ya Watanzania, wao wataendelea kudai utawala mpya utakapoingia madarakani uwe ni wa Chadema au CCM.

“Nawahakikisha Watanzania, ikija Katiba mbaya tutaendelea kuidai kwa nguvu zote iwe CCM imeingia madarakani au sisi, Kikwete awe madarakani au asiwepo hatulali kamwe.

“Katiba ni maridhiano ambayo yanabeba maoni ya Watanzania sasa kwa nini CCM hawataki kuyafuata?” alihoji Mbowe.

Alisema CCM haina hatimiliki ya Katiba mpya na kwamba wakati wa kufanya uamuzi mgumu wa kupindisha maoni ya Watanzania umefika.

“Hawa watu hawana hatimiliki ya Katiba mpya, kwa nini wanajawa uoga kiasi hiki? Wanaogopa serikali tatu, nakwambia sitaki utani kwenye ya msingi,”alisema Mbowe.

KINGWEDU"NIMEJIPANGA VYA KUTOSHA KUINGIA BUNGENI 2015"

0
0
Mwigizaji wa Comedy (Futuhi) Anajulikana kwa Jina la kingwendu Amweka wazi Nia yake ya kuwania Ubunge katika kinyanganyiro cha 2015, Amesema kwa sasa Amejipanga vya kutosha kuingia mjengoni , Kuhusu chama atakacho gombea kwa sasa ni siri yake ila atakitaja mambo yakikaribia....
UNAONAJE ATAWEZA AU NDIO ATAPELEKA BUNGENI VICHEKESHO?

NINA MWAKA KWENYE NDOA LEO NDIO NINAGUNDUA MKE WANGU ANA TATTOO YA JINA LA MWANAUME MWINGINE

0
0
Habari Wadau wa Udaku...
Leo nimeuzika sana wadau Asubuhi wakati napata morning Glory kwa Mke wangu nimegundua Kwenye Titi Sehemu ya chini ana Tatto imeandikwa "I lov u James" kwa Maandishi Madogo sana kama haupo makini unaweza usiyaone...Nimekaa nae Mwaka mzima Leo ndio nakuja ona Nilivyojaribu kumuuliza anakuwa mkali na kusema ni jina la Ex Wake kabla hajakutana na Mimi....Wadau Hapo Mnanishaurije ? Kila nikiona hiyo Tatoo Am Sure Mood zitakuwa zikiniisha

SIKILIZA HEKA HEKA YA LEO JINSI TICHA WA TUITION ALIVYOMPA MWANAFUNZI WAKE MIMBA

0
0
Hizi ni mishe zinazotokea kila siku inayoitwa leo,sasa leo kupitia Idara ya Hekaheka inayo taarifa juu ya huyu Mwalimu aliyekua akimfundisha mwanafunzi masomo ya jioni lakini kilichokuja kutokea baadae ni Ujauzito,sikiliza mazingira jinsi ilivyokuwa,sikiliza kupitia 98.6 Clouds Fm Musoma.
Bonyeza play kusikiliza.
Source:Millardayo

SHILOLE SIKIO LA KUFA, AKANA MAAGIZO ALIYOPEWA NA MCHUNGAJI

0
0
STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amedhihirisha kuwa ni sikio la kufa baada ya kusema yeye ni miongoni mwa wanawake wanaojua  kuchuna mabuzi.
Kauli hiyo imechochea vigezo vya kumfanya Shilole aonekane hasikii kwani wiki kadhaa zilizopita mchungaji wa kanisa moja lililopo Ubungo, jijini Dar ambaye hakujulikana jina lake, alimtaka kuishi katika sura ya kumpendeza Mungu lakini inaonekana amempuuza.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, jijini Dar es Salaam, Shilole alisema alitunga wimbo wa Nachuna Buzi kwa sababu anajua kuwa wanawake wengi ni mafundi wa tabia hiyo akiwemo yeye mwenyewe!

“Unajua mwanamuziki unatakiwa kuchagua wimbo ambao unaigusa jamii nzima kwani mambo ya kuchuna mabuzi kwa wanawake yapo sana, hata mimi mwenyewe ni mtaalamu wa kuchuna mabuzi,” alisema Shilole.
Hata hivyo alisema japokuwa ana tabia hiyo lakini anatambua siyo nzuri hivyo anawasihi wanawake wengine kuachana nayo kwani ipo siku itawaingiza matatizoni.
Mbali na mchungaji huyo, juzi Jumapili,  Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Ukonga –Mazizini, Dar, Emmanuel Kapande alimtumia ujumbe wa watoto wa Shule ya Jumapili (Sunday School) nyumbani kwake kwa lengo la kuimba na kufanya maombi.
Watoto hao walifika nyumbani kwa Shilole, Mwananyamala - Manjunju, wakiwa wameongozana na walimu wao, Jonas Timotheo, Rehema Ezra na Catherine Libogoma.
Ujumbe huo, ulimpelekea baraka ya maombi nyumbani kwake na kumshauri aishi katika mazingira yanayompendeza Mungu.
Katika hafla hiyo, vinywaji baridi vilichukua nafasi yake huku Shilole akipata nafasi ya kuzungumza na watoto hao kisha kupiga nao picha.

EXCLUSSIVE.KUWA WAKWANZA KUTAZAMA PICHA ZA JOKATE NA MPENZI WAKE MPYA

0
0

MWANAMITINDO daraja la kwanza Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemwanika mwanaume mpya mtandaoni huku wakiwa wamepozi katika staili ya wapendanao.
Awali, paparazi wetu alitonywa na sosi aliyeomba hifadhi ya jina lake kuwa amemuona mwanaume mpya wa Jokate katika mtandao wa Instagram.
“Nimemuona Jokate na mwanaume wake mpya lakini simjui kwa jina, kama huamini ingia kwenye mtandao wa Instagram uone mtoto wa kike alivyojiachia katika pozi za kimahaba,” alisema sosi huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliingia kwenye kilongalonga chake na kuperuzi katika mtandao huo kisha kujionea picha hizo, haraka sana akazisevu katika simu yake.
Aidha, wadau mbalimbali waliopo katika mtandao huo walitoa maoni mbalimbali huku wengi wao wakimpongeza.
Baada ya paparazi wetu kuzitia kibindoni picha hizo, alimsaka Jokate kwa njia ya simu ili azitolee ufafanuzi.
Mwandishi: Haloo Jokate…
Jokate: Nitumie meseji nipo kwenye kikao.
Mwandishi wetu alimtumia meseji kama alivyoshauri staa huyo ambapo alimtaka amtambulishe mwanaume huyo na aeleze kama ndiye mpenzi wake mpya, hakujibu chochote.
Paparazi wetu alimtumia meseji ya pili kumsisitiza atoe majibu ndipo alipojibu kwa kifupi:“Hapana mumy!”
Pamoja na majibu hayo, paparazi wetu alimtumia meseji nyingine kumuuliza kama siyo mpenzi wake ni nani lakini hadi tunakwenda mitamboni, hakujibu chochote
Kabla ya kumuanika mwanaume huyo, Jokate aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku pia akitajwa kutoka na mcheza kikapu, Hasheem Thabeet.

POLISI WAKAMATA KILO 200 ZA HEROIN DAR

0
0
Kikosi kazi cha Jeshi la Polisi cha Kudhibiti Uharamia Baharini kimekamata kilo 201 za dawa za kulevya aina heroini zilizokuwa zikiingizwa nchini kutoka Iran.

Kamishna wa Polisi, Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema jana kikosi hicho kikiwa kwenye doria ya kawaida kiliona boti ambayo haikuwa na bendera wala kiashiria chochote ndipo walipoitilia shaka na kuamua kuifuatilia.

Nzowa alisema kuwa mzigo huo ni mkubwa zaidi wa heroin kuwahi kukamatwa na vikosi vya doria vya Tanzania.

Alisema mara ya mwisho kwa mzigo mkubwa zaidi wa heroin kuwahi kukamatwa ilikuwa mwaka 2012 wakati zilipokamatwa kilo 70 za dawa hizo jijini Dar es Salaam.

Nzowa alisema Kikosi cha Wanamaji kiliposhuku boti hiyo, kiliisimamisha na kugundua kuwa ilikuwa na watu 12.

Alisema baada ya uchunguzi wao waligundua kuwa kulikuwa na raia wanane wa Iran na wanne wa Pakistan.

“Boti hiyo ilivutwa hadi ufukweni ambako leo (jana) ilifanyiwa uchunguzi na ndipo zikakutwa na kilo 201 za heroin,” alisema Nzowa.

Nzowa alisema boti hiyo iliyosajiliwa Kunarak, Iran, ilikuwa inaongozwa na nahodha mwenye uraia wa nchi hiyo, Ayub Hot (50).

Nzowa alisema kitakachofuata sasa ni kufanya upelelezi na kujua walikuwa wanataka kupeleka wapi mzigo huo, kufahamu mtandao wao na walipanga kufanya nini katika ufukwe wa Dar es Salaam.

Alisema baada ya upelelezi wao kukamilika watu hao watafikishwa mahakamani.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Polisi, ACP Mboje Kanga alisema watu hao 12 hivi sasa wamewekwa mahabusu ya wanamaji na kikosi hicho kwa kushirikiana na Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya wataendelea na upelelezi.

Taarifa ya mwaka 2011 ya Kitengo cha Dawa za Kulevya iliyochapishwa katika ripoti ya Kitengo cha Dawa za Kulevya cha Marekani inaeleza kuwa, heroini huingia Tanzania kupitia Bahari ya Hindi ikitokea Afghanistan, Iran, Pakistan na Falme za Kiarabu.

Hapa boti ndogondogo hutumika kuzipeleka China na Bara la Ulaya kwa vifurushi vidogo vidogo.

Pia dawa za kulevya aina ya cocaine huingia Tanzania kutoka Brazil, Columbia, Peru, Trinidad na Tobago, Venezuela na Curacao, kisha hupelekwa Afrika Kusini, Ulaya, Australia na Amerika ya Kaskazini.

BAADA YA BAADHI KUJIUNGA CCM-BONGO MOVIES VIPANDEVIPANDE!

0
0
Stori: Waandishi Wetu
MPASUKO mkubwa umeikumba tasnia ya filamu Bongo baada ya baadhi ya wasanii wanaong’ara kuchukua kadi rasmi za kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

Tukio hilo lilitokea juzi, Jumapili jijini Mbeya kulipokuwa na sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Mashabiki mbalimbali wa sinema za Kibongo, waliingia kwenye mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, mara baada ya wasanii hao kuonesha uamuzi wao, kila mmoja akieleza mtazamo wake.

WASANII WENYEWE
Baadhi ya wasanii waliochukua kadi za CCM ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’, Irene Uwoya, Haji Salum ‘Mboto’, Tamrina Posh ‘Amanda’, Blandina Chagula ‘Johari’, Wastara Juma na Haji Adam ‘Baba Haji’.

MIJADALA
Watoa maoni walikuwa na mawazo tofauti kuhusiana na uamuzi wa wasanii hao wenye mashabiki wengi, wengine wakiwapongeza huku upande wa pili ukiwashutumu kwa maelezo kuwa wanawagawa mashabiki wao.

Mtoa maoni aliyejitaja kwa jina la Mussa Juma aliandika: “Sijui hawa wasanii wetu watakua lini? Huwezi kuonesha itikadi yako ya kisiasa wakati una mashabiki wengi. Hapo wamechemka. Mfano mimi siyo CCM na siwezi kununua tena filamu za JB.”

IPYANA LWIGA:
“Hii ndiyo demokrasia, unawavuta watu wajiunge kwako kwa kuwapa usafiri na mahitaji yote muhimu! Wameona mbali sana, nawapongeza sana! Wajifunze kwa Marlaw!”

BENATUS MARWA NYAMBORI:
“Huo ni uamuzi wao. Hauhusiani na kazi zao. Kama umechukia, chukua kazi zao zote piga moto. Kiukweli Chadema mnafikiri watu wengi wanawasapoti? Hapana... huko vijijini wanakuja kuangalia helikopta maana hawajawahi kuiona.”

JACOBS KING:
“Sasa hivi ndiyo watakoma kabisa, najua hakuna wa kununua kazi zao, wataibiwa mpaka wakome, CCM wanataka kuwatumia kwenye kampeni mikoani ili wawavutie wananchi kwenye mikutano yao lakini kwa sasa Watanzania tunajielewa.”


COCU BATENGA: 
“Wasanii wana haki ya kuchagua chama chochote wakipendacho. Wakati wa kazi ni kazi, siasa ni siasa. Mbona Sugu (Joseph Mbilinyi – Mbunge wa Mbeya Mjini) yupo bungeni? Mbona Afande Sele (Seleman Msindi) ametangaza kujiunga Chadema, mbona hayasemwi? Hakuna mantiki hapa.”

JB BUNGENI
Hivi karibuni, JB alitangaza nia yake ya kugombea ubunge ingawa bado hajataja jimbo, kitendawili cha atagombea kwa tiketi ya chama gani, kimeshateguka baada ya kuchukua kadi ya CCM.

Hata hivyo, minong’ono inasema kwamba, JB huenda atagombea Jimbo la Kinondoni (kwa sababu ndiyo eneo analoishi) au Same (kwa sababu ni mzaliwa wa huko).

WHATS APP MESSENGER INANIVUNJIA NDOA YANGU

0
0

Leo nina tatizo naomba ushauri na msaada kimawazo..

Nimekuwa na mme wangu kwa miaka minne sasa na tumebahatika kupata mtoto ana 2 years old girl

Jmos moja mme wangu alinipa simu yake kuongea na mama mkwe baada ya kumaliza kuongea nikawa najifunza kutumia smart phone ya husb tukiwa kwenye sherehe nilishawishika kuingia kwenye picha na whatsApp pia

Huko nikaanza kuingia kila sehemu..Ile nafika WhatsApp walahi niliumia oho sana 

Mme wangu alikuwa anachat na wakina dada tofauti tofauti mambo ya mapenzi na kuombana kutumiana picha ...na mengineyo sipendi kusema 
Pia nilikuta kwenye Picture profile mme wangu ana picha zaidi ya sita za kina dada waliomtumia kwenye WhatsApp

Nilimuuliza mme wangu hakunipa maneno ya kueleweka ,na mimeshajua mwenzangu ananicheat wakati mie nimejituliza nyumbani nalea mwanangu wa miaka miwili.

Lakini Bado nimesikia sasa ni kilio cha wanandoa wengi na mahusiano yanavunjika kwa sababu ya hizi wasapu..

Wapenzi niambieni nifanyeje roho inaniuma sana!naichukia ndoa kama ndo kuna usaliti wa hivi

Wenu Egyps

RAIS KIKWETE:WANASIASA ACHENI KUINGILIA NA KUROPOKA KWENYE MASWALA YA KITAALAMU

0
0
Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha kutoa majibu ya kisiasa katika masuala na changamoto za kitaalam na kiufundi.

Amesema matatizo na changamoto za kitaalam na kiufundi ziachiwe kutafutiwa majawabu ya kiufundi badala ya kupatiwa majawabu ya kisiasa.

Rais Kikwete alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki, wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Mbeya.

Alisema hayo kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi kulalamikia ubora wa mbolea ya Minjingu.

Zambi aliuambia mkutano huo kuwa wakulima wa mkoa wa Mbeya wanakataa kutumia mbolea ya Minjingu kwa madai kuwa haifai kwa matumizi katika mkoa huo pamoja na kwamba ilifanyiwa utafiti wa kitaalam na kupitishwa na wataalam wa Kituo cha Utafiti cha Kilimo cha Uyole kilichoko Mbeya.

Baada ya kusikiliza kauli hiyo ya Zambi, Rais Kikwete alisema kama kuna tatizo la mbolea ya Minjingu litakuwa linatokana na hali ya udongo katika sehemu mbali mbali za mkoa huo lakini siyo kutokana na ushauri wa kitafiti wa Kituo cha Uyole.

“Kituo cha Uyole kilifanya utafiti na kuona kuwa mbole ya Minjigu inafaa kwa matumizi ya mkoa wa Mbeya. Nyie mnasema kuwa haifai.

Ushauri wangu ni kwamba kama mnaona kuna tatizo, nawashaurini rudini tena kwa wataalam wa Uyole waangalie tena ili wataalam hao warudi kwenye drawing board,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Utatifi wa udongo ni muhimu sana katika kuamua mbole ya aina gani inafaa katika eneo gani. Hivyo, nashauri kuwa warudieni wataalam wa Uyole waangalie kuna tatizo gani?.

Naamini kuwa utafiti wa Uyole hauwezi kuwa wa makosa. La msingi ni aina na ubora wa ardhi ambayo mbole hiyo inatumika.”

CHANZO: NIPASHE - 4th February 2014

TUNDU LISSU:WABUNGE WENGI BONGO HAWAJUI KINGEREZA

0
0
Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge. 

Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.

Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.

source; cluods fm na star tv.

SNURA AJA JUU "KWANINI WAMEIFUNGIA VIDEO YANGU"

0
0

“Ni video ya kawaida kabisa na nimeicheza mwenyewe na wacheza shoo wangu.Nilifanya hivyo baada ya video yangu ya ‘Majanga’ kulalamikiwa kuwa
sikucheza.
Imeniuma sana video ya "Nimevurugwa" kufungiwa na BASATA kuonyeshwa kwenye TV bongo wakati kama kukatika ni tamaduni yetu watanzania kuna video kibao za nje za ovyo kabisa wanavaa nusu uchi ila azifungiwi" 

BASATA WAONGEA KUHUSU KUFUNGIWA VIDEO YA SNURA NIMEVURUGWA

0
0
Siku kadhaa zilizopita kupitia millardayo.com kuna taarifa ziliztoka kuhusu kufungiwa kwa video ya Nimevurugwa ya Snura,taaarifa hizi alizi-amplify meneja wake Snura ‘Hk’ akidai kuwa sababu maalum bado hawajazipata ingawa kila kituo anachoenda wanampa sababu tofauti.
Millardayo.com haikuishia hapo ilienda moja kwa moja kwenye Baraza la Sanaa la Taifa(Basata)ili kuujua undani wa sakata hili ikiwemo pia kuulizia video ya Jux(uzuri wako)ambayo nayo ilitoka taarifa ya kufungiwa kwa video hiyo.
Kutoka Basata huyu hapa Godfrey mungeleza ni kaimu katibu mtendaji  anataarifa zaidi>>Unaposema kufungia video moja kwa moja kuna chombo kingine cha serikali kinashughulikia hilo ambao ni bodi ya filamu Tanzania’
‘Bodi ya filamu wanaangalia video zote suala zima la filamu wanapoona hii haikidhi au haifai kwa jamii za Kitanzania basi wanaisimamisha kidogo wanamshauri aweze kuirekebisha ili iweze kulingana na maadili ya kitanzania’
‘Sisi tunaangalia Audio kabla haijaingia sokoni katika urasimishaji tunakaa tunausikiliza muziki wake tunashauriana kwamba akarekebishe hapa na tunaangalia mambo mengi ikiwemo ubunifu wake mwenyewe’
‘Suala la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la maadili na limeandikwa sana na sisi Baraza kama Baraza tunaangalia sana suala la maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia msanii mwenyewe’
Bonyeza play kumsikiliza Kaimu Katibu mkuu akielezea suala hili.

TAARIFA YA KUKATIKA KWA MAWASILIANO YA VODACOM‏

0
0
Dar es Salaam, 5 Februari, 2014.Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari  5, 2014. Hii imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na  nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.
Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha vituo vyetu vya kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi juu kushindwa kufanya kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana kumesababisha kushindwa kutoa huduma za mawasiliano.
Kutokana na hilo wateja hawakuwa na uwezo wa kupiga simu, kutumia intaneti na hata  huduma za kifedha. Tunatambua usumbufu ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara nyingine tena tunaomba radhi na tunashukuru kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho huduma zilikosekana. 
Mafundi wetu wameweza kurekebisha uharibifu uliotokea barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli za ujenzi  wa barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea katika Barabara ya Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na nyaya zilizo katika mkonga wa mawasiliano kuungua kulikosababishwa na zoezi la uchomaji taka lililokuwa linaendelea katika sehemu ambayo mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo. 
Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, Tumejidhatiti katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee  wakati wote watakapokuwa wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna ambavyo wameendelea kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo yanapojitokeza. 
Rene Meza 
Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images