Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Kwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa

$
0
0
Kwa  Nini  UKAWA  Wameamua  LOWASSA  Awe  Mgombea  wao  wa  Urais??..... Tundu  Lissu  Amelijibu  Swahi  hili  kwa  Ufasaha  Kabisa  hapo  chni:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.

Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

 Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.

Mtangaza nia ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Ramesh Patel Amekamatwa na TAKUKURU Akitoa Rushwa

$
0
0
Ramesh Patel Mgombea Ubunge Ukonga Dar, akamatwa na Takukuru akitoa Rushwa Check Point Pugu

Je kwa mfumo huu wa kutoa rushwa katika Hatua ya Kura za maoni na hata kampeni kubwa,wananchi wataweza kuwachagua viongozi bila ushawishi wa Fedha?na Kiongozi kama Ramesh Anatufundisha nini?

Sikubaliani na Hoja ya LOWASSA Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

$
0
0
Dr.Slaa pengine ndiye mwanasiasa wa upinzani anaeheshimika na kusikilizwa zaidi Tanzania.

Yote hii ni sababu ya misimamo yake kupinga ufisadi, kusimamia na kutetea maslai ya Taifa bila kuogopa.

Amewahi kutaja hadharani listi ya mafisadi 11 Lowasa akiwa namba tisa na Kikwete akiwa namba kumi na moja.

Alienda kule Arumeru alimtuhumu Lowasa waziwazi kwa ufisadi na kukwepesha miradi ya Arumeru na kuipeleka Monduli.

Lakini leo tunaambiwa kuwa Lowasa anakaribishwa ndani ya Chadema na kuungama dhambi na atasamehewa.

Sina tatizo na ujio wa Lowassa ndani ya chama tatizo langu ni heshima na taswira ya Dr. Slaa aliyojijengea kwa muda mrefu kwa kuukemea ufisadi.

Je leo yupo tayari kutangaza hadharani kuwa Lowasa amekuwa msafi sio fisadi tena, yupo tayari kupunguza ile list of shame ya Mwembeyanga kutoka kumi na moja na kubaki kumi.?

Japo siasa hazina adui wa kudumu wala urafiki wa kudumu, kwa hili naona heshima ya Dr.Slaa na Chadema kwa ujumla ikiporomoka.

Maana heshima ya Dr Slaa na Chadema imejengwa kwa kuukemea ufisadi, lakini tunakoelea Hali itabadilika na kuwa Chadema ni chama cha kuwasafisha Mafisadi.

Nb.Ni mtazamo tu wadau msijenge chuki.

Warembo wachanjana viwembe kisa, Wema kukatwa ubunge Singida

$
0
0
KAMA kawaida ni Ijumaa nyingine ambayo Mapaparazi Wetu, Musa Mateja ‘Mtanashati’, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ na Mpigapicha Wetu Mkuu, Richard Bukos walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kuwasiliana moja kwa moja na mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili, Bamaga-Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Saa 3:56 usiku
SHAROBARO MVAA MLEGEZO AUNGUZWA MAKALIO
Mkuu akiwa ofisini anampigia  simu  Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ na kumtaka amjulishe kiwanja alichopo.
Makao Makuu: Shekidele nijalie hali yako kwanza.
Shekidele: Naam Mkuu wangu huku Moro hatujambo sijui huko Dar!
Makao Makuu: Dar nako ni salama, enhe haya nipe ripoti ya huko una tukio gani?
Shekidele: Mkuu niko maeneo ya Kichangani kuna sharobaro mmoja, hawa wanyoa ‘viduku’ na kuteremsha suruali alikuwa akiendesha bodaboda kisharobaro si imemshinda wakati akikata kona ya Mbuyuni na kulivaa banda la chipsi la mama Abdul.
Makao Makuu: Duh! Hali ilikuwaje hapo sasa?
Shekidele: Mkuu huyu sharobaro kaungua vibaya na mafuta ya chipsi hasa sehemu za makalio yaani ni balaa!
Makao Makuu: Huo msala, vipi mama Abdul anasemaje?
Shekidele: Kachachamaa anataka kulipwa vitu vyake ndipo jamaa mmoja kaenda kumuita diwani wa hili eneo, John Waziri aje kuwasuluhisha.
Makao Makuu: Sawa Shekidele piga kazi ngoja nimcheki Musa Mateja.
Shekidele: Sawa Mkuu.
Saa 4:56 usiku
WAREMBO WACHANJANA VIWEMBE KISA, WEMA KUKATWA UBUNGE SINGIDA
Makao Makuu: Halooo, halooo Mateja uko wapi kijana wangu?
Mateja: Mkuu nilikuwa Maisha Basement lakini nimepigiwa simu niende Ukumbi wa Mashujaa Grill and Lounge kuna mtu kaniambia kuna tukio la wadada kuchanjana na viwembe.
Makao Makuu: Enhe natumai umefika eneo la tukio nini kinaendelea?
Mateja: Mkuu ni kweli nimekutana na hilo tukio warembo wamechanjana viwembe eti kisa Wema Sepetu jina lake kukatwa kwenye harakati za kuwania ubunge wa viti maalum huko Singida.
Makao Makuu: Sasa ikawaje mpaka wachanjane?
Mateja: Leo si ndiyo majibu ya wagombea viti maalum yametoka na jina la Wema limekatwa, sasa wadada wa Timu Wema na wale wa Timu Diamond wakaanza kunangana ndipo dada mmoja wa Timu Wema alikuwa na kiwembe kwenye pochi yake akaanza kumchanja nacho mwilini dada wa Timu Diamond ambaye kumbe naye alikuwa na kiwembe pia, akajibu mashambulizi ndipo mabaunsa wamewaamulia lakini kila mmoja anatokwa damu.
Makao Makuu: Kweli hilo bonge la tukio, muhimu sana upate picha, sawa Mateja?
Mateja: Ondoa shaka Mkuu wangu.
 Saa 6:12 usiku
WALIOJIFANYA KWENDA KUKESHA KWENYE FOLENI YA BVR WANASWA WAKIFANYA UFUSKA
Makao Makuu: Haya Bukos natumai uko vizuri na unanipata, uko pande zipi?
Bukos: Mkuu nimeamua kupitia kwenye vituo vya kujiandikisha kupiga kura ‘BVR’ ambapo wapiga kura wanajifanya kukesha kwenye foleni na sasa niko Shule ya Msingi Makongo Juu naona wake na waume za watu wamejiachia kwa raha zao wakijifanya kulinda foleni zao huku wengine wakiwa kwenye vichaka usiku huu. Yaani wale walio vichakani wanafanya ufuska mtupu Mkuu.
Makao Makuu: Wapige picha tuwarushe hewani ili kuanika mambo ya aibu wanayofanya kisha wapigie simu wenzako mkapumzike.
Bukos: Sawa Mkuu nitafanya hivyo.

Fedha alizochangiwa Lowassa na kundi la Marafiki wa Edward Lowassa zatafunwa....

$
0
0
Na Makongoro Oging’
WANACHAMA wa kundi la Marafiki wa Edward Lowassa waliochanga fedha za kumwezesha waziri mkuu huyo wa zamani kuchukua fomu ya kugombea urais, wamemtuhumu aliyekuwa naibu katibu wao, George Kivuyo  kutafuna fedha hizo.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wanachama hao wanaojulikana kama Team Lowassa 4 President, zinadai naibu katibu mkuu huyo ambaye pia ni mweka hazina wao, alitafuna kiasi cha shilingi laki saba zilizochangwa.
Walidai fedha hizo ziligunduliwa kutotumika ilivyopaswa baada ya kutojulikana zilipo na alipoulizwa hakuwa na majibu ya kueleweka.
Baadhi ya wanachama hao, Fauzia Ally, Hassan Mollel na Yussuf Hamis walisema kutokana na kitendo hicho, wanachama hao wameanza kufarakana kutokana na mgogoro.
“Hizi fedha zilitumiwa tofauti na ilivyokusudiwa, zinatakiwa zirudishwe, akabidhiwe mzee Lowassa,” alisema Hassan Mollel.
Naibu katibu mkuu huyo alipopigiwa simu na mwandishi wetu juzi Jumapili alisema kwamba madai hayo ni ya uongo na fedha hizo hazikuwa laki saba bali zilikuwa Sh. 526,000.
“Mimi ni mweka hazina msaidizi na tatizo limekuja baada ya kuhoji kuhusu fedha hizo alizokabidhiwa bosi wangu.”
Katibu mkuu wa chama hicho, Mohamed Mkindi alipoulizwa alikiri kusikia malalamiko hayo lakini alidai yupo mikoani na akirudi jijini Dar es Salaam atazifuatilia.

Hivi Kwanini Baadhi ya Wanawake Wanajichubua Wawe Kama Wazungu?

$
0
0
Kuna jambo linanishangaza sana, ni hivi kwanini wanawake wa kibongo wanapenda kujichubua ngozi na kutumia mikorogo,makalorite, hili wawe weupe na wafanane na wazungu.

Lakini sijawahi kumuona mwanamke wa mzungu akijichubua eti awe mweusi kama msichana wa Kiafrika.

Hivi kuna shida gani hapa wakuu?

Hali ngumu ya uchumi ikamfanya Mbunge aoneshe nguo za ndani Bungeni!!

$
0
0
Unamkumbuka yule Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola aliyeingia Bungeni na bidhaa za kichina huku akiilaumu Serikali kushindwa kutumia rasilimali zake na kutegemea bidhaa za nje?.

Hii nyingine imetokea Zimbabwe na kuzua kizaazaa baada ya Mbunge wa upinzani Priscilla Misihairabwi kutinga Bungeni akiwa na nguo za ndani za wanawake huku akisisitiza hatma ya raia wake maskini kutokuwa na uwezo wa kununua nguo hizo.

Katika kikao chicho cha bunge kilichokuwa kikirushwa live na Televisheni ya Taifa, mbunge huyo wa Chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change ‘MDC‘ alitoa mfuko wa plastiki uliokuwa na nguo hizo.

Baada ya kutoa akamuuliza Waziri wa Fedha na sera za serikali kuhusiana na uingizwaji wa nguo hizo za mtumba  ambazo bei yake ni ndogo na husababisha madhara kwa akina mama.

Akijibu swali hilo Waziri wa Fedha Patrick Chinamasa alimtania Mbunge huyo kutokana na uamuzi wake wa kubeba nguo za ndani za akina mama lakini akasema Wizara yake  inachunguza suala hilo.

Kufuatia kitendo hicho Mbuge huyo alitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa chama tawala cha ZANU PF  kwa madai ya kutumia matamshi ya kibaguzi.

Uchumi wa Zimbabwe umedorora miaka ya hivi karibuni hali iliyosababisha viwango vya umaskini kuongezeka kutokana na kuwepo idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Jamaa Aliachiwa Mtoto Mchanga Akaamua Kumnywesha Maziwa Aliyochanganya na Pombe..

$
0
0
Dunia ina vituko vyake mtu wangu, na kwa wenzetu wa Marekani wakati mwengine vituko huzua madhara makubwa.

Nimekutana na hii moja inayomhusu Dontavian Eagle McCree mwenye miaka 19 aliyeachiwa jukumu la kukaa na mtoto wa dada yake wakati yeye akiwa kazini.

Siku moja wakati akiwa nyumbani na mtoto wa dada yake, Dontavian aliamua kumpatia mtoto huyo wa miezi 10 pombe, akachanganya pombe kwenye maziwa ya mtoto na kumnywesha.
Dontavian Eagle McCree,19.

Siku chache baadae mtoto alianza kuumwa na baada ya mama yake kugundua aliamua kumpeleka mtoto hospitali na ndipo alipogundua kuwa mtoto alinyweshwa pombe.

Dontavian amekamatwa na kupelekwa kituo cha polisi na thamani ya dhamana yake ni dola 15,000 ambayo ni sawa na Mil.30 za Kitanzania. Hali ya mtoto sio nzuri kabisa.

safari Hii Nampa Kura Yangu Fisadi.............

$
0
0
Jamani nimechoka, mwaka 1995 nilitapeliwa, niliuziwa mbuzi kwenye gunia baada ya kuletewa mmachinga mmoja nikaambiwa ni mr. clean na bila hiana nikatoa kura yangu. Matokeo, amekaa ikulu miaka 10 akaua viwanda vyangu, akauza benki yangu ya taifa na akafungua ya kwake, akaua shirika langu la bima ili afungue la kwake, akafungua kampuni kwa anuani ya ikulu na kujimilikisha migodi yangu mimi mpiga kura, akawa na kiburi cha ajabu na kuanza kuniita mchwara, akauza nyumba zangu zote akishirikiana na ma-padlocks. Siku hizi anatembelea magari ya tinted ili asizomewe kwa jinsi alivyochafuka, sasa eti amesafiri hadi Chato kumuibua another mr clean kama yeye! Sikubali.

Ok hayo yakapita ikaja 2005, nikaletewa malaika mwenye sura nzuri kutoka Msoga hana kitu chochote zaidi ya sura yenye mvuto. Akaja na ahadi kemkem za maisha bora kwa kila mtanzania lakini baada ya miaka mingine 10, amefanikiwa kutimiza hiyo ahadi kwa familia yake tu, taifa zima bado tunasubiria hizo ahadi. Tumeshuhudia mambo ya ajabu kama escrow, utapeli kwenye bomba la gesi na mikataba ya kuchimba madini, gesi, nk.

Safari hii sifanganyiki, hawa ninaoletewa wanaoitwa wasafi halafu nikishawapa kura yangu wananiliza, wanasema kwamba kwa miaka yote 10 waliwasahau wazazi wangu wakulima, wanachomoka na mali zangu mimi mpiga kura, halafu hawataki hata niwaulize chochote.

Safari hii nimebadilisha mawazo. NAMCHAGUA FISADI maana yeye sitamshangaa akiniibia maana mmeshasema kwamba ni fisadi. Naumia sana ninaposhawishiwa kumchagua "msafi" halafu ananiibia. SAFARI HII SIDANGANYIKI, NAMCHAGUA FISADI.

By Mwananchit/JF

Msaada: Ninafika Kileleni Ndani ya Dakika 1....Nashindwa Kumridhisha Msichana

$
0
0
Wakuu poleni na majukumu!

Sina tatizo la uume kusimama (erection) kwani unasimama tena ngangari kweli kweli!

Tatizo langu ni kuwahi kufika kileleni yaani ndani ya dakika 1 na nusu tayari kwisha habari yangu baada ya dakika kama 10.

Unasimama tena lakini ndani ya dakika kama hizo tayari nimemwaga huku nikimwacha mke wangu anaugulia.

Je wataalamu nitumia mizizi ama dawa gani ili kunusuru ndoa yangu?

Natanguliza shukrani kwenu wataalamu.

Mrembo Akuhumiwa Jela Kwa Video Tata Mtandaoni

$
0
0
Mnenguaji wa kike nchini Misri, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kuonekana kwenye video yenye utata mtandaoni.

Hukumu hiyo imetolewa na mahakama moja nchini humo kwa kosa la kuchochea ngono baada ya kuonekana katika video yenye utata katika mtandao.

Mrembo huyo aliyetambulika kwa jina la Reda al – Fouly alitiwa mbaroni, mara baada ya video hiyo ya miondoko ya Pop kuoneshwa hadharani na baadaye kudhihakiwa kuwa imeenda kinyume na tamaduni za kiarabu.

Muimbaji huyo wa kike alitakiwa kufafanua mavazi -aliyoyava kwenye wimbo unaoitwa Sib Eddi au let it go of my hand.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mkurugenzi wa video hiyo, Wael Seddiki , aliondoka nchini Misri wakati wimbo huo ulipoanza kupondwa kwenye mitandao ya kijamii ili kukwepa lolote ambalo lingeweza kutokea..

Video  Yenyewe  Iko  Hapo  Chini


VIDEO IMEVUJA: Hivi Ndivyo Wema Sepetu Alivyomwaga Machozi Baada ya Jina Kukatwa Singida Ubunge Viti Maalumu

$
0
0
VIDEO IMEVUJA: Hivi Ndivyo Wema Sepetu Alivyomwaga Machozi Baada ya Jina Kukatwa Singida Ubunge Viti Maalumu

Breaking News : LOWASSA Kwa Mdomo wake Atangaza Kuamia Chama cha Chadema...Adai CCM Sio Mama Wala Baba Yake

$
0
0
Wakati Huu Lowassa yupo Hewani ITV akiongea na Kusema CCM sio Baba Yake wala Mama Yake na Amehamia Chadema Kwani nia yake ya Kugombea Urais ipo paleplae Japo jina lake lilikatwa CCM, Adai Safari yake ya Matumaini Bado inaendelea....


LOWASSA Adai Anachukia Sana Umaskini...Ndio Maana Marafiki zake ni Matajiri.....Ataka Watanzania Wote wawe Matajari Kama Kina Mengi na Bakhresa

$
0
0
Wakati akitangaza Kujiunga na Chama cha Chedema leo hii mmoja wa waandishi ameuliza swali kwanini yupo karibu sana na matajiri ..Lowassa amejibu swali hilo kwa kusema kuwa anachukia sana umaskini ndio maana yupo karibu nao na nia yake ni kufanya watanzania wote wawe matajiri kama kina Mengi na Bhakresa......

Toa Maoni yako.....

Kiwete’s Latest tweet… Does it Have Anything To do With Lowassa

$
0
0

While everyone is talking about Hon. Edward Lowassa and UKAWA right now, the is one of the more recent tweets from the President of Tanzania Hon. Dr. Jakaya Kiwete. I’m just wondering if it has anything to do with the Lowassa-UKAWA issue.



Basi la Sabuni Express limegongana na gari la Kanisa Katoliki. Ajali imetokea Bugorora Kyaka Wilayani Misenyi.

$
0
0
Ajali mbaya imetokea eneo la Bugorora Kyaka leo, inahusisha Basi la kampuni ya Sabuni lililokuwa likitokea Karagwe na Land Cruiser ya Kanisa.

Taarifa za hawali zinasema watu si chini ya watano wamepoteza maisha kwenye eneo la tukio.

Basi la Kampuni ya Sabuni linalofanya safari kati ya Kagera na Mwanza limegongana na gari ndogo aina ya Land Cruiser iliyokuwa na mapadre na masista katika eneo la Bugorora nje kidogo ya Kyaka wilayani Misenyi mkoani Kagera.

Basi hilo nambari za usajiri T650 BFI na Cruiser T166 AGU ambapo waliotajwa kupoteza maisha kwa taarifa za awali ni Padre Onesmo Kahabwa na Michael Mwelinde pamoja Sista Magret Tadebe ambao ni wa Parokia ya Katoke waliokuwa wakitokea Rulenge wilayani Ngara.

VIDEO Lowassa Akijibu kuhusu RICHMOND baada ya Kujiunga na UKAWA

$
0
0
Dakika chache baada ya kutangaza kutangaza kujiunga rasmi na UKAWA kupitia Chadema, waandishi wakamuuliza kuhusu Sakata la RICHMOND.... Sikia alivyojibu hapa kwenye hii Video:

CCM’s Post after Lowassa joining UKAWA

$
0
0
CCM’s Post after Lowassa joining UKAWA


Sentesnsi 50 Alizosisema Edward Lowassa Leo Wakati Akikabidhiwa Rasmi Kadi ya CHADEMA.......Yapo pia maneno ya Mbowe,Lipumba, Makaidi na Mbatia

$
0
0
1.Nimetumia wiki mbili kutafakari hatma yangu ktk Siasa, najua wengi wamesubiri kwa hamu.

2.Watu wangu wamesema fanya maamuzi magumu.. Namshukuru Mke wangu na familia wamekuwa na mimi ktk kipindi kigumu-

3.Nawashukuru watu wengi waliojitokeza kuniunga mkono wakati natafuta wadhamini-

4.Uchaguzi wa Mgombea CCM ulijaa chuki dhidi yangu, Kamati ya Maadili haikutakiwa kuchagua Mgombea-

5.Kilichotokea Dodoma kinaitwa 'kubaka Demokrasia'

6.CCM iliwatumia vijana wachache kunikashifu na baadae wakapewa Madaraka makubwa

7.Kibaya zaidi kilikuwa kuwanyima Wagombea 38 wa CCM haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu

8.Nilinyimwa haki ya Msingi ya kusikilizwa na kujieleza CCM, nitakuwa mnafki kusema nina imani na CCM

9.CCM niliyoiona Dodoma sio CCM iliyonilea Kisiasa, mimi km Mtanzania mwenye Uhuru nasema sasa basi

10.Mwalimu NYERERE alisema CCM sio baba yangu wala mama yangu,nimeamua kuanzia leo naondoka CCM na kujiunga CHADEMA

11.Namshukuru sana James MBATIA na Viongozi wa UKAWA kwa kuniamini na kunipokea

 12.Naamini UKAWA tutaondoa mfumo wa Utawala wa Chama kimoja, naomba Watz wajiunge nasi ktk SAFARI YA MATUMAINI

13.Naomba Watz wajiandikishe ktk Daftari la Kupiga Kura,watunze Shahada za kupigia Kura ili tuiondoe CCM Madarakani

14.Mimi nauchukia UMASKINI, Kiongozi kujionesha maskini ni upuuzi. Natamani Watz wawe Matajiri km MENGI na AZAM

15.Kulipa kisasi ni upuuzi, umefanya nini mpaka useme nitalipa kisasi? Waulizeni wamefanya nini nilipe kisasi?

16.Kulipa kisasi ni upuuzi, umefanya nini mpaka useme nitalipa kisasi? Waulizeni wamefanya nini nilipe kisasi?

17.Msiwatishe, kama wamefanya madhambi yao waambieni nimewasamehe mimi sitalipa kisasi

18.LIPUMBA- 'UKAWA tumekubaliana maliasili na Rasilimali zitumike kwa manufaa ya Watz wote'

19.MBOWE- 'CCM imekuwa na Wabunge wengi ndani ya Bunge, imefanya waangalie maslahi yao zaidi kuliko Taifa

20.MBOWE- 'Tumekubaliana Wabunge wa UKAWA wakiingia Bungeni November 2015 waangalie zaidi maslahi wa Watz'

21.MBATIA- 'Tunawakikishia Watz kwamba nguvu kubwa ya Serikali ya UKAWA itaangalia maslahi ya Watz'

22.Nilisema mtu ambaye ana ushahidi wowote kuhusu mimi kuhusika na RICHMOND peleka Mahakamani, kama huna kaa kimya

23.Tulikuwa na tatizo la Umeme, tukahangaika kuleta Mitambo ya kuzalisha umeme.

24.Tulipata taarifa kuwa mtu ambaye tunampa kazi ya kuzalisha umeme hakuwa na uwezo

25.Niliondoka Madarakani lakini tatizo limeongezeka, mikono yangu ni misafi mwenye Ushahidi peleka Mahakamani

26.MAKAIDI- 'Nashukuru mmetuletea kifaa LOWASSA, nilimfahamu LOWASSA kupitia mtoto wangu

27.MAKAIDI- 'LOWASSA amekuja UKAWA afuate na Sisi tunavyotaka asahau kidogo mambo ya CCM'

28.MAKAIDI- 'Watanzania wamekwama, najua LOWASSA amekuja UKAWA kutukwamua.. Karibu sana LOWASSA'

29.Salum MWALIMU- 'Kuna taarifa kuwa sehemu kubwa ya Mikoa ya Mbeya, Singida na Arusha umeme umekatwa'

30.MBATIA-'Siku ya leo nina amani kutoka sakafu ya moyo wangu, ninawahakikishia Watz kuwa TZ bila CCM inawezekana'

31.MBATIA- 'UKAWA hatutamwaga damu lakini walio Madarakani wasituchokoze, uwezo wa kupambana kwa hoja tunao'

32.MBOWE- 'Tunapenda kumkaribisha LOWASSA pamoja na familia, marafiki zako na kundi la Watz wapenda haki'

33.MBOWE- 'Ujio wako CHADEMA umezua hofu nyingi kwa sababu hii ni nchi ya hofu'

34.MBOWE- 'Watu wengi wa CCM wamenipigia simu wakasema kumkaribisha LOWASSA ni kuharibu Chama'

35.MBOWE- 'Niliwajibu ni kweli ataharibu Chama, lakini nikajiuliza lini CCM ikawatakia mema CHADEMA?'

36.MBOWE- 'Kumleta LOWASSA kwenye meza hii haikuwa kitu chepesi, tumekaa Vikao viingi usiku na mchana'

37.MBOWE- 'Naongea kwa ujasiri,hatuwezi kufikiri mambo mema mapya kama tutaendelea kufikiri mambo mabaya ya zamani'

38.MBOWE- 'Chama cha Siasa ni watu, mimi niletewe watu Milioni niwakatae mimi ni mwendawazimu?'

39.MBOWE- 'Mimi na Viongozi wa UKAWA hatufikirii kulipiza kisasi'

40.MBOWE- 'Tumeshuhudia Vita ya makundi ndani ya CCM na wengine wakaadhibiwa. Wengi wanalalamika, wanaona ukweli lakini hawana uhuru kuongea'

41.MBOWE- 'Tumeshuhudia Vita ya makundi ndani ya CCM na wengine wakaadhibiwa. Wengi wanalalamika, wanaona ukweli lakini hawana uhuru kuongea'

42.MBOWE- 'Hatujamkaribisha LOWASSA pekeyake, tumemkaribisha na Mamilioni ya Watanzania

43.MBOWE- 'Chama cha Siasa ni watu, mimi niletewe watu Milioni niwakatae mimi ni mwendawazimu?'

44. MBOWE- 'Mimi na Viongozi wa UKAWA hatufikirii kulipiza kisasi'

45.MBOWE- 'Umesaidia kumfungua kifungoni Mbunge Ole MEDEYE na Wabunge wengi ambao tutaendelea kuwakaribisha'

46.MBOWE- 'CHADEMA haiongozwi kwa kauli za MBOWE, inaongozwa kwa Katiba na Kanuni za Chama

47. MBOWE- 'Namshukuru sana Rais JK, umesaidia kutujenga Upinzani kuelekea Uchaguzi wa mwaka huu'

48.MBOWE- 'LOWASSA ujitahidi sana Mazoezi kwa sababu huku kuna mabomu'

49.MBOWE- 'LOWASSA alipokuwa analalamika Dodoma sisi tulikuwa tunafurahi'

50. MBOWE- 'Umesaidia kumfungua kifungoni Mbunge Ole MEDEYE na Wabunge wengi ambao tutaendelea kuwakaribisha

Hapa Kuna Picha 5 Za Lowassa Na Mkewe Wakikabidhiwa Rasmi Kadi Za CHADEMA

$
0
0

Mhe. Freeman Mbowe (katikati) kulia kwake ni Regina Lowassa (mke wa Lowassa) na kushoto kwake ni Edward Lowassa baada ya kukabidhiwa kadi cha Chadema.
4
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,  James Mbatia akimpongeza Edward Lowassa punde baada ya kujiunga na CHADEMA chama kimojawapo kinachounda umoja wa UKAWA.
6
Mke wa Edward Lowassa, Regina Lowassa akikabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.
5
Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba akimpongeza Mhe. Edward Lowassa baada ya kujiunga na CHADEMA chama kimojawapo kinachounda umoja wa UKAWA.
3


Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images