Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live

CCM Wamjibu LOWASSA........Wasema Kuhama kwake Hakuna madhara na kwamba Watapata ushindi wa kishindo

$
0
0
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Dar, Juma Simba Gaddafi  jana  aliongoza  mkutano  wa  CCM  na  waandishi  wa  habari  uliofanyika  Peacock Hotel Dar, na  haya  ndo  mambo  aliyoyasema;


"CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru

"Tume ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM tuna uhakika tutashinda.

"Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura…

"Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri…

 "Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika."

Akiongelea  sakata  la  Lowassa  kuhamia  CHADEMA, Gaddaf  alisema;

"Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka.

"Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe…

"Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara."

Akiongelea  kuhusu Uteuzi wa Mgombea wa Urais CCM Dodoma, Gaddaf  alisema;

"Mkutano Dodoma tuliumaliza, lakini tumekwenda kwenye NEC Wajumbe wako 360, walipiga kura majina matano na Wagombea wote wa Halmashauri Kuu akiwepo Rais, Waziri Mkuu na Lowassa walikuwepo… kama asingekuwepo hayo yangesemwa, lakini alishiriki na alipiga Kura"

LOWASSA Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais LEO kwa Mbwembwe na Shamrashamra!!

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alitambulishwa rasmi kuhamia CHADEMA July 28 2015 Dar es Salaam akiwa ameongozana na mke wake, Regina Lowassa pamoja na watoto wao.

Kwenye Orodha ya Viongozi wa UKAWA ambao walikuwepo kumpokea na kumkabidhi kadi ya CHADEMA, alikuwepo James Mbatia, Prof. Lipumba, Dk. Emmanuel Makaidi, Salum Mwalimu na Freeman Mbowe.

Salum Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, jana  alisema haya kuhusu mapokezi hayo;
 
"Tunashukuru sana Watanzania, sidhani kama kuna kiongozi wa CHADEMA simu yake iliwahi kuzidiwa kama jana, simu zilizidiwa kwa pongezi… Kila mtu amezungumza kwa sababu ya Historia ya tendo lenyewe.

"Kesho(LEO) Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA… pengine kutakuwa na shamrashamra nyingi itategemeana na Mgombea mwenyewe, akiamua kuja na mdundiko haya… lakini tunaamini kutakuwa na shamrashamra nyingi."

Salum Mwalimu pia  alizungumzia  sababu  za  viongozi  wengine  wa  UKAWA  kutokuwepo(  Tundu Lissu  na  Dr. Slaa)   ambapo  alisema;

"Tuna mambo mengi tuna mikakati mingi, tumegawanyika… sio kila tukio wote tuwe pamoja.
 
"Jana mliuliza Tundu Lissu yuko wapi na leo huyu hapa hata hamumuulizi… Tuko kwenye kipindi cha Uchaguzi,tuna mambo mengi hatuwezi wote kuwa sehemu moja, tunagawanyika kutokana na ratiba tuliyonayo."

Mwigulu Nchemba Atoa Ufafanuzi Baada ya Kuhojiwa na TAKUKURU

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Mashariki ameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Singida kwa kumwita yeye na kumhoji kwa kuwa hilo ndilo jukumu lao la msingi.

Mwigulu aliyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya kuhojiwa kwake na taasisi hiyo kuhusu tuhuma za kukiuka Sheria ya gharama za Uchaguzi na Sheria za Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini.

Alisema yeye kama kiongozi wa serikali hana budi kuwapongeza Takukuru kwa kutimiza wajibu wao ipasavyo, kwani kisheria taasisi hiyo ikipokea tuhuma au malalamiko yoyote, inapaswa kumhoji, kumchunguza na hatimaye kumchukulia hatua stahiki mtuhumiwa anayehusika.

Hata hivyo, alisema hajawahi kutoa rushwa ya aina yoyote tangu mchakato huo wa uchaguzi uanze jimboni Iramba na kudai kuwa anakubalika kwa wananchi.
 
“Hata kama nisingekwenda kufanya kampeni, nina uhakika ningepata robo tatu ya kura kwa kila kata kwa kuwa nakubalika jimboni kwangu”.

Alisema yeye ni mmoja wa watu ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na rushwa nchini; hivyo haoni sababu ya kutoa rushwa.
 
 “Hata sababu ya kutoa rushwa sina. Nimefanya kazi yangu vizuri jimboni na kila mtu ananikubali,” alisema Mwigulu na kuongeza:
 
“Hiki walichofanya Takukuru ni jambo jema. Isiwe kwa Iramba tu bali pia lifanyike maeneo mengine ambako wana mashaka kuna vitendo vya rushwa. Hii ndiyo kazi ya serikali katika kuhakikisha wale wote wanaokiuka kanuni na taratibu za uchaguzi wanashughulikiwa ipasavyo.”

Alisema kuwa katika uchaguzi wowote ni lazima kuwepo na changamoto mbalimbali, lakini kwa masuala anayolalamikiwa na wagombea wenzake, kimsingi walishakubaliana kwenye vikao vya kamati ya siasa ya chama hata kabla ya kuanza mchakato; hivyo yeye anashangaa wenzake walivyomgeuka.

“Kwa mfano, tulikubaliana tuwe na gari moja kila mgombea kwa ajili ya matangazo, mimi la kwangu ni Fuso wao wanatumia Canter na zina spika. Sasa kama spika zangu zimezidi nguvu za kwao hiyo siyo hoja… ni mambo tuliyokubaliana wenyewe tuendelee na mchakato,” alisema na kuongeza kwa lugha ya utani:
 
"Wasilete mambo ya mpira wa kizamani ambapo timu isiyo na viatu hugomea mchezo hadi wenzao nao wavue viatu ndipo wacheze (yaani: ‘hatuchezi mpaka na ninyi mvue viatu’)”.

Ne-Yo Aeleza Kwanini Alikuwa na Hamu ya Kuonana na Diamond Platnumz Alipoenda Afrika Kusini

$
0
0
Muimbaji wa Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo ameitaja sababu iliyomfanya atake sana kukutana na Diamond Platnumz.

Baada ya watu kusikia kuwa nilikuwa nakuja kwenye MAMAs jina pekee ambalo walikuwa wakilitaja kwangu ni Diamond Platnumz,” Ne-Yo alimwambia Vanessa Mdee kwenye interview ya MTV Base.

Nikasema ni lazima nikutane na huyu jamaa, nahitaji kumuona,” aliongeza.

Siku moja kabla ya tuzo hizo pia, Diamond alielezea jinsi Ne-Yo alivyomtafuta. “Wakati nazungumza na D’banj @salaam_sk alinifata na kuniambia @neyo anakutafuta anataka kukuona…” Ungependa kujua kilichofata??? Kaa karibu na TV, Radio yaani Kiufupi Media zako Soon utayaskia,” aliandika Diamond kwenye Instagram.

Ne-Yo na Diamond ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye MTV MAMA 2015.

Video: Tazama alichokifanya Kanye West huko Canada Baada ya Mic Kupata Hitilafu Akiwa Jukwaani

$
0
0
Hakuna kitu kinachokera kwa msanii awapo jukwaani , kama mitambo kuleta hitilafu ambazo zitasababisha ashindwe kutoa burudani nzuri , au wakati mwingine kufanya aonekane amefanya show mbaya.

Jumapili iliyopita Kanye West aliacha gumzo huko Toronto, Canada baada ya kukatisha onesho lake ghafla na kuondoka jukwani.

Baada ya kupanda jukwaani mbele ya watazamaji elfu 40 kwenye onesho la Pan Am Games, Kanye aliamua kukatiza onesho lake ghafla dakika ya 13 tu toka aanze kutumbuiza, na kuondoka jukwaani huku akiacha watu wamepigwa butwaa.

Uamuzi huo wa Kanye ulifuatia hitilafu ya kiufundi iliyojitokeza na kusababisha kipaza sauti alichokua akitumia kisifanye kazi ipasavyo.

Akiwa anaendelea kuwapa burudani mashabiki ghafla alirusha mic hiyo juu na kuondoka jukwaani hapo ‘like a boss’, na kuwaacha watu wakishangaa sababu hawakutarajia kuona kilichotokea.

Tazama alichokifanya Kanye:

Picha: Ubora na Viwango Vyangu, TBS Nimeshindikana-Lulu

$
0
0
Staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejifangilia kwa kusema kuwa viwango vyake katkaia maswala mazima za kijipodoa ni ya kiwango cha juu.

Lulu ameandika haya kwenye ukurasa wake wa instagram mara baada ya kuweka picha hizo hapo juu.

Diana Elizabeth Michael...! Miss Balozi katika Ubora na Viwango vyangu (TBS nimeshindikana)
Unaweza kuniita Mkali Wa Hizi Kazi pia.Pale Make up Artist wako anapotaka Kukugeuza Mzungu na Nusu…"

Akaandika tena

"Ubora na Viwango vilivyoshindikana na TBS..Kuna mtu atapanic tu".

Jacqueline Wolper… Amfuata Edward Lowassa Ukawa!

$
0
0
Liwalo na liwe! Kinara wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameahidi kuambatana na waziri mkuu wa zamani ambaye ni Mbunge wa Monduli kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Ngoyai Lowassa kwenye safari yake ya kuhamia kwenye muungano wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wolper alisema kwa mapenzi aliyonayo kwa Lowassa yupo tayari kwenda kokote hata kama siyo Ukawa.

Mimi ni ‘Team Lowassa’, atakapohamia nami niko nyuma yake hata kama siyo Ukawa, nitamfuata, mimi na Lowassa ni damdam, hilo halina ubishi,” alisema Wolper

Prof Mwandosya Afunguka: Jakaya Kikwete Alikuwa na Wagombea Wake Mfukoni Wakati wa Mchakato wa Kutafuta Mgombea CCM

$
0
0
Waziri mwandamizi katika serikali J.K amemtuhumu bosi wake kuwa alikuwa na majina ya wagombea tano bora mfukoni mwake.Rais Kikwete,ndiye aliyeongoza kikao cha maadili cha CCM,kilichowakata akina EL,Mwanndosya,Pinda,Dr Bilal.
Chanzo:RFA,Habari magazetini

Prof.Mwandosya: Magufuli Hajawahi Hata Kuwa Mjumbe wa Tawi la CCM...Iweje Apewe Urais Leo...

$
0
0
Prof. Mwandosya amenukuliwa akisema kuwa Magufuli haifahamu na haijui CCM kwa kuwa hajawai kuwa hata mjumbe wa tawi la CCM.

Aidha ameweka wazi kutoridhishwa na mchakato uliofanywa na Kamati Kuu kuipata tano bora na hatimae Magufuli.

Anasema kamati kuu haikuwa na mvuto kiasi kwamba Mwenyekiti J.Kikwete hakuwa anajiamini,alifika wakati ana-adress kwa mwenyekiti na kujishtukia "kumbe mwenyekiti ni mimi mwenyewe".

Profesa amesisitiza kuwa watu walikuja na majina mifukoni kwani majina yalivuja kabla hata vikao.

Akina Dada huu utaalamu utawacost sana: hivi inakuwajue unaweka viungo sehemu za siri kama pilau?

$
0
0

Nimekutana na huyu dada anaomba ushauri kwa Joyce Kiria

Miaka 3 ilopita nimekuwa katika matatizo makubwa sana.....nawashwa sana sehemu za siri (uken). nilienda baadhi ya hospitali wanasema ni fungus nikatumia dawa baada ya wiki tatizo likajirudia. Nimekuwa mtu wa kujikuna wakati wote. Ukeni panawaka moto kwa kujikuna, nimeendelea na tiba mpaka likaibuka tatizo jingine . kila ninapofanya tendo la ndoa napata maumivu ambayo hayaelezeki wakati mwingine mpaka naanza kubleed.

Kurudi tena hospitali wakasema nipime vipimo vya kansa lakini tatizo likazidi kuongezeka na sasa siwezi hata kufanya tendo la ndoa. madaktari ktk vipimo wakagundua kwenye uk-e kuna wekundu mwingi sana badala ya rangi ya pink. 
Kumbe ile rangi nyekundu ni sehemu ambayo imeshambuliwa na bacteria wasiosikia dawa. Wakajaribu kupeleka dawa sehemu iliyoathirika bado ikashindikana kuwaua!

Baadae madaktari wa Muhimbili wakaniuliza ninavyofanya usafi katika sehemu zangu za siri na nikawambia ukweli kwamba, "NASAFISHA KWA KUINGIZA VIDOLE NDANI, NAJIINGIZA ASALI NA PAMBA NDANIILI UKKE UWE UMEBANA NA VINGINE VINGI tu tunavyoshauriana na wasichana (VIUNGA SEHEMU ZA SIRI).

Madaktari wakasema sababuya tatizo langu nimeua bakteria wote walinzi ndani ya ukke ndo maana nimmeshambuliwa na bacteria ambao hawaskii dawa

Ndugu zangu nilikuwa nikiunga sehemu za siri (ukke) kwa VIUNGO na naingiza kucha pamoja na sabuni ili uwe ubane na upendeze. Sasa nimeshauriwa nitoe kizazi katika umri wa miaka 29 kwani nikiacha itakuwa kansa. Najua mna ndugu zenu wa kike au wake zenu. Wape tahadhari juu ya hili.

My take: Hivi hadi uweke asali, vidole, pamba nk ndani ya ukkke ili ubane unatafuta nini? Kuna mashindano ya zinazobana, na wanawapa tuzo gani hadi utake risk kias hiki?

Mume wa Mtu Mbona Haniachi Jamani Miaka Sita Sasa Ameniganda Kama Ruba....

$
0
0
Habar ndugu zangu, Nashindwa kuelewa mpaka sasa nimetokea kupendwa na mume wa mtu tangu niingie kwenye mahusiano cjawahi kuwa na mahusiano na mwanaume ambaye yupo single, amekuwa akinisaidia sana katka maendelea yangu mume wa mtu huyu ndie mshaur wangu hata iweje yupo mbele yangu kunijali ananipenda sana mara nyingne nawaza siwez kufika naye mbali tayar yy ameshakuwa na familia yake na Mimi nilazima nitakuwa na familia Yang tutaishi maisha haya mpk lini na tangu tujuane huu ni mwaka wa 6 najitahidi kumuacha lakini jamaa na yeye anapigana kutokuniacha mke wake mpk leo hajui kama mume wake ana mchepuko nje, nishaurini nahitaji na Mimi kuwa na maisha yangu nimpata mume wangu nitamtumikia huyu jamaa mpk lini?
Nipeni hata njia mbadala matata ili niachane naye

Tundu Lissu Azungumzia Wanaotaka Kuihama CHADEMA Baada ya Lowassa Kupokelewa na Chama Hicho

$
0
0

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa CHADEMA ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Lissu alisema,

“Kama wapo watakao jiondoa CHADEMA, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze. Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapobomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”

“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.

"Tunamkaribisha kwetu siyo kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya”

Akizungumza kuhusu CHADEMA kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu alisema;

“…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”

“Alijiuzulu Uwaziri Mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje? Hilo ni vumbi, litakapotulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini. Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,”

Edward Lowassa Aitikisa Dar...Makomandoo Wamiminika Kuhakikisha Lowassa Anachukua Fomu ya kuwania Urais Katika hali ya Usalama

$
0
0


Edward Lowassa akionesha fomu ya kuwania urais aliyokabidhiwa leo Makao makuu ya Chadema,D ar.
CLJ5hSGWoAACCU3
Umati wa watu waliojitokeza kumpokea Lowassa wakati akichukua fomu ya urais kupitia Chadema.
CLJ8fhkW8AA6IKB
…Akisaini katika kitabu cha wageni.
CLJ9y4iWEAAZWy7
Mnadhimu Mkuu kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu akitoa yake machache.CLJ52JsWwAA--Yc
CLKRw2sWcAAzeL9
Lowassa akiwasiri kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Dar leo.
mbowe na lowassa
Baada ya kuchukua fomu.
Mwenyekiti wa Chadema (kushoto) Mhe. Freeman Mbowe Mhe. Edward Lowassa (katikati) wakati wa zoezi la kuchukua fomu lililofanyika leo Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar .
LOWASA (1)
LOWASA (2)
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.
 **
WAZIRI MKUU wa zamani, Mhe. Edward Lowassa hivi punde amechukua fomu ya kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Lowassa amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
Lowassa alijiunga rasmi na Chadema juzi akitokea CCM baada ya kuondolewa kwenye mchakato wa kuwa mgombea urais wa chama hicho akidai kuwa jina lake liliondolewa kwa mizengwe.

Nimempata Tundu Lissu, kaongelea kwanini hakuwepo wakati Lowassa anapokelewa CHADEMA

$
0
0
Mbunge Tundu Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa CHADEMA alikutana na ripota Fredy Mwakikato wa TZA (millardayo.com & AyoTV) na kuzungumzia ishu kadhaa ikiwemo ya Lowassa kujiunga na CHADEMA.

Tazama hii video hapa chini uone yote aliyoyasema Tundu Lissu.

Wadada Tubadilike Tabia ya Kuomba omba Kwa Wanaume si Nzuri inatuzalilisha

$
0
0
Wadada tubadilike jamani kuomba omba sana utazoeleka hata siku ukipata shida ya serious mtu atashindwa kukusaidia coz ni kawaida yako, Hii tabia ndio inafanya mnamegwa ovyo ovyo

Wengine sasa sio hata kwa boyfriend tuu yaani yeye asikuzoee kidogo tu kosa kesho yake ataomba hela. Ombaomba Siku Hizi Hawapo Barabarani tu Hata Kwenye Simu zetu Wapo Jamani ..

Hii ni tabia mbaya jamani tubadilikeni hata siku ikitokea umeomba hela mtu anashangaa anajua kweli umebanwa coz sio kawaida yako.

Breaking News: BASATA imemfungia Shilole Mwaka Mmoja, Hakuna Kufanya Muziki

$
0
0
Shilole Akiwa Jukwaani Huku Mali zake Zikiwa Nje Nje...
Breaking news zilizoifikia usiku wa July 30 2015 kutoka Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) ni kwamba baraza hili limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.

Barua iliyoifikia  imeandikwa kutoka BASATA imesema >>> ‘Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili‘

‘BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ – BASATA

‘Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA

Je ni Sawa Kwa Shishi Kufungiwa?

Hatimaye kaka Yake Zari Amchumbia Mwanamuziki Linah Sanga....

$
0
0
Hatimaye staa wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amechumbiwa rasmi na yule jamaa wake, Wiliam Bugene ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka kiukoo wa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.’

Akizungumza na Amani kwenye mahojiano maalum alipotimba katika Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Zanzibar hivi karibuni, Linah alisema kuwa ana furaha maishani mwake kwa kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye atafunga naye ndoa ‘soon’.

Tayari ameshanichumbia, anajulikana kwetu na mimi najulikana kwao. Kifuatacho ni ndoa yangu,” alisema Linah ambaye hivi karibuni amesema ataachia wimbo mpya utakaokuwa gumzo.

Furaha ya Linah inakuja kufuatia kumpata mwanaume huyo ambaye amekuwa akionekana naye kila kiwanja wakiwa wamegandana kimahaba ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipodai kuporwa bwana’ke, Nagari Kombo anayedaiwa kakwapuliwa na Wema Sepetu.

Kabla ya Boss Mtoto na Kombo, huko nyuma Linah aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye uchumba ‘serious’ na msanii mwenzake, Amini Mwinyimkuu.

Kwa Mara ya Kwanza no Mabomu Maandamano yasio Rasmi ya Chadema, Barabara zafungwa, Polis Watia Doria Kila Kona Kuhakikisha Kuna Amani

$
0
0
Imekua kama desturi maandamano ya wapinzani kumbana na mabomu ya polisisiemu lakini kwa mara ya kwanza jana maandamano yasio rasmi ya wapinzani hayakupigwa mabomu pale mmoja wa watia nia wa chama cha upinzani Edward lowassa alipoenda kwa maandamano ofisi za chadema kuchukua fomu na baadae kwenda mpaka ofisini kwake mikocheni bila mabomu huku baadhi ya barabara zikilazimika kufungwa..

Sio Dada yake ila Mdogo Wake Ndiye Chaguo Langu..Dada Kanitongoza Kabla Sijamtongoza Mdogo wake niliyekuwa Namnyatia.....

$
0
0
Upendo wangu na haupo kwake kiukweli upo kwa mdogo wake, lakini nilishindwa kuwa wake kabla ya dada yake kufanya mambo yake kweli nimeamini chelewa chelewa utakuta mwana si wako'.

Kwa jinsi nilivyompenda mdogo wake sijui ni nini kilichonifanya nisimwambie.

Nahisi ule usemi wa 'subira huvuta heri' ulinipumbaza, ona sasa kaniwahi dada yake na mdgo wake katambua.

Jamani nilimpenda na bado nampenda mdogo wake ila mazoea ya dada yake kwangu yamechukua sura nyingine.

Niliona njia rahisi ya kumpata mdogo wake ni kuzoeana na dada yake, lakini sasa dada yake kanizoea vibaya .

Hadi kufikia kuniomba namba yangu ya simu haikutosha akaamua kunitamkia kabisa eti anataka kuwa nami bila kujua kama mimi nina malengo na mdogo wake.

Nahisi ndoto zangu kupotea, nipo katika wakati mgumu sana sijui nimjibu vipi dada yake na sijui nitampata vipi nimpendae na wote wanakaa nyumba moja.

JAMANI EEH!

NIMETONGOZWA NA DADA YAKE MSICHANA NINAEMPENDA bado sijamjibu chochote nimekata mawasiliano kwa muda ili kutafakari.

Tafadhali anayeweza kunishauri.

By Alphaking mahena

Majina ya Wabunge Walioshinda Kabla Hata ya Uchaguzi October.....

$
0
0
Kwenye ukweli tuweke mambo ya vyama pembeni kwa maslahi ya taifa.
Kuna baadhi ya wabunge lazima warudi bungeni kwa ushindi wa kishindo na wengine hata wakionga migodi hawawezi kurudi mfano ni Tibaijuka na Asumpta Mshana.
Baada ya kuzunguka nchi nzima nikifanya research nimepata haya majina ya wabunge walioshinda kabla hata ya uchaguzi
.Sugu, Wenje, Lissu, Mnyika, Mbatia, Mdee, Joseph haule, Msigwa, Mkosamali na Kafulila

Embu na wewe nipe majina ya wabunge ambao tayari wameshinda kwa AJILI ya bunge lijalo
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live




Latest Images