Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Mh. Lowassa Aongezewe Ulinzi Kumlinda na Kila uovu na Hila Ambao Utapelekea Asitimize Lengo Lake.....

$
0
0
Mh. Laigwanan Edward Ngoyai Moringe Lowassa anastahili ulinzi wa ziada ili kumlinda na wabaya wake kwani hawakawii kumfanyia kitendo cha kigaidi ili kutotimiza lengo lake la kuchukua nchi kutoka chama Tawala...

Ulinzi madhubuti na makini unatakiwa kutolewa na wana UKAWA na kila mtanzania mpenda maendeleo kwa kuwa Edo ndiye tumaini pekee kwa watanzania kujikomboa kutoka utumwa wa CCM.

Nitoe rai kwa uongozi wa UKAWA kumpa ulinzi wa ziada kiongozi huyu wa kitaifa na kimataifa ili kumlinda na kila uovu na hila
 Lowassa ndiye mboni pekee inayowapa nuru watanzania itakayowaangazia na hatimaye kuwawezesha kutoka msitu wa giza nene.

Tafakari, chukua hatua!

Baba Haji Ashangilia Anguko La Wema Sepetu..Afurahia Wema Sepetu Kushika Nafasi ya Mwisho

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ juzikati aliangusha sebene la nguvu kwenye Viwanja vya Ngome Kongwe, Zanzibar baada ya kupata taarifa kuwa staa wa kike nchini aliyekuwa akiwania nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu ameangushwa.

Akionekana mwenye furaha huku akiserebuka muziki alisema kuwa mbunge wenu amekosa ubunge, jambo lililowafanya baadhi ya wasanii wenzake waangue kicheko kwa kuwa inafahamika kuwa ana bifu naye.

Jamani mmesikia majibu? Mbunge wenu kashika nafasi ya mwisho, ngoja mimi niendelee kucheza sebene langu,” alisikika Baba Haji huku akiangua kicheko.

Bifu la Baba Haji na Wema lilianza kitambo ambapo wawili hao walikutana kwenye Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar ambapo Wema alimchana jamaa huyo kuwa ananuka jasho.

Chanzo: GPL

Shamsa Ford:Mchawi wa Maisha Yako ni Wewe Mwenyewe

$
0
0
NIDHAMU ni silaha kubwa katika maisha.kuna ambao Mungu aliwabariki kwa nafasi zao lakini hawakuweza kutumia nafasi zao vizuri kwasababu ya kukosa nidhamu.walihisi wao ni bora kuliko wengine ndo maana walibarikiwa.

Mwisho wa siku wakishapotea au mambo kwenda tofauti na walivyokuwa wanadhania wanaanza kulaumu watu.Wengine wataingia hadi kwenye ushirikina kwa kusemwa wamerogwa..Mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe...MUWEKE MUNGU MBELE,KUWA MVUMILIVU,ACHA TAMAA,FANYA KAZI KWA BIDII, PENDA KUJIFUNZA NA KUBALI USHAURI

Shamsa Ford "@shamsaford" on instagram

Nora Awananga Wanaodai Ameshazeeka..Adai yeye Ajagalagazwa Ovya Kama Hao Wengine wa Bongo Movies.....

$
0
0
Nora Bongo Movies
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa Instagram, mkali wa sanaa ya uigizaji hapa Bongo, Nora amefunguka haya kwa wale wote wanaomponda eti amezeeka

Hivi nyinyi mnaoniambia mzee amuoni aibu loooo..hahahahhaaa mana mnafanya siku yangu iwe nzuri ni jinsi gani nawaumiza mpaka mnalopoka kama mmetoka usingizini.Hivi mimi mnaweza kujifananisha na nyinyi, hoooo ninamiaka mingi kweli na nimewazidi vingi sana, tabia, muonekano…haaaa mi sijagalagazwa ovyo nilijiheshimu tangu usichana wangu, nimeshafanya maisha yote hakuna cha ajabu kwangu nyi kinachowatoa roho sasahivi, tena nikiwa na mume wangu wa ndoa sio wakushobokea kwasababu nipate kitu na yeye anivuruge tu.

Sioni kipya na bado nawaumiza kichwa mkinitafari ni jinsi gani mnanipenda na mnanikubali moyoni. Asanteni kwa hilo mnazidi kunipa nguvu Mungu awabariki sana sijajua kabisa kama bado ninanguvu kiasi hichi, mbarikiwe sana tim matusi ila muombe sana muwe mnalipa mpaka age yangu mana sura zimeshawashuka watoto wadogo mwili ndo usiseme nikisimama na nyinyi mnaonekana vizee vya miaka 70 na mnavyotumika sipati picha sehem nyingine hata tukisimamishwa uc** bado i will look young puuuu natamani kuwatema mate niki imagin mlooooh mnataka nini mbona mambo ni yale yale

 Embu tulieni watoto wakike mjiheshim yani na Mungu anavyojua kuwadhalilisha mnalopokaje mitusi yenu wenyewe nadhani mnajiangalia mlivyo used halafu mnawambia wenzenu mana mngekua hamko hivyo mmgekua na haya kutamka vitu vya ajabu kama ujawai onamm na myinyi tofauti sanaaaana kama bado mlikua hamjaja mjini wakati na miaka 26'mi sikua kama nyinyi nivute nikuvute na wala umaarufu sijauvalia bukta ndo mana haunisumbui wala haunipeleki puta naishi maisha yangu an am happy siofii chochote zaidi ya akhera yangu nipo tofauti nyinyi mnaona kama dunia imeshushwa jana kila kitu kwenu kipya

Muwe na hekima kama adabu imewashinda mbarikiwe katika kheri na maovu Mungu awaondolee watoto wazuri najua sio kosa lenu poleeeeni eeeh ndo mliambiwa umaarufu huo ooooo poyeeeee vitotooooo chilieeee come to dadaaaaa.

Mwanadada Mwingine Mtanzania Akamatwa na Madawa ya Kulevya Indonesia..Alikuwa Ameyaficha Tumboni Kama Pipi

$
0
0
Dada wa Kitanzania kakamatwa na madawa ya kulevya Indonesia.

Alikamatwa alipotua uwanja wa ndege Jakarta wa Soekarno-Hatta baada ya maofisa wa usalama kumshuku.

Alikamatwa tarehe 4, Julai na vidonge 32 tumboni vya heroine na meth venye uzito wa gramu 540.

Taarifa za maofisa hao wa uwanja wa ndege, zinasema kuwa alishukiwa tangu Tanzania kutokana na mwendo wake lakini karuhusiwa kuendelea na safari kuja Jakarta kupitia Doha, Qatar.

Hawajasema vipi walipata habari hizo za kuachwa huru Tanzania na Qatar.

Pengine alihonga Tanzania au Qatar hawakutaka kuhangaika nae kwa kuwa alikuwa Transit na kumchomea Indonesia.

Kinachojulukana ni kuwa amefunguliwa shitaka, chini ya kifungu 113 cha mwaka 2009, kinachotoa hukumu ya kifo kwa makosa ya kukamatwa na madawa ya kulevya nchini Indonesia.

Anajulikana tu kwa jina la MA.


Mume Wa Zari Abambikiwa Mimba na Msichana Mtangazaji wa TV....Alitaka Kulipa Kisasi kwa Zari ....

$
0
0
Wakati staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akisubiri mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ajifungue mtoto wa kike ‘taimu’ yoyote kutoka sasa, aliyekuwa mume wa mwanamama huyo, tajiri Ivan Ssemwanga anadaiwa kubambikiwa mimba na mtangazaji wa runinga aitwaye Doreen Kumhangi, Ijumaa limeidaka.

TUJIUNGE JIJINI KAMPALA
Habari kutoka jijini Kampala, Mji Mkuu wa Uganda zilidai kwamba, Ivan na Doreen ambaye ni Mtangazaji wa Kipindi cha Morning Breeze cha Televisheni ya NBS ya Uganda, wamekuwa wakionekana wakiwa wamegandana kama ruba kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka jana.
dd“Muda wote Ivan akiwa Kampala anajirusha na Doreen. Mara kadhaa wameonekana viwanja tofauti wakila bata. Hata Doreen anapokwenda South Africa (Sauz) amekuwa akipokelewa na Ivan ambaye ana makazi mengine huko kisha kufanya yao,” kilidai chanzo ambacho ni mfuatiliaji wa masuala ya burudani nchini Uganda.

DOREEN ATOA SIRI NZITO
Ilidaiwa kwamba, baada ya bata zote hizo, hivi karibuni, Doreen alitoa siri nzito kuwa ana ujauzito uliosababishwa na Ivan, jambo lililomfanya jamaa huyo ‘kupaniki’.
Ilisemekana kwamba, kufuatia Ivan kukanusha kwa nguvu zote, kuna madai kwamba Doreen anambambikia mimba hiyo akiamini kwamba watu watakubaliana naye kwa kuwa ndiye amekuwa naye katika kipindi alichonasa mimba.

ALITAKA KULIPA KISASI KWA ZARI?
Katika mapenzi yao, ilielezwa kuwa, kuna kipindi Ivan alitaka kumhalalisha Doreen kuwa mkewe na haikujulikana ishu hiyo iliishia wapi huku nyuma kukiwa na madai kwamba alitaka kumrusha roho au kumlipiza Zari.
“Sijawahi kutembea na Doreen kwa hiyo mimi sihusiki na ujauzito alionao,” alisema Ivan juzikati alipobanwa na gazeti moja nchini humo.
“Anachokisema (Doreen) si kweli, anataka kunibambikia mimba,” alisema jamaa huyo aliyezaa na Zari watoto watatu wa kiume huku akiendelea kukanusha ishu hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na Instagram.

DOREEN NI NANI?
Habari zilieleza kwamba, Doreen ni mtangazaji anayesoma habari kwenye kipindi hicho cha asubuhi cha NBSTV.
Kabla ya kudaiwa kuwa na Ivan, Doreen alikuwa shosti wa karibu na Zari na kwamba walishafanya kazi pamoja ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema ndiye mbadala sahihi wa Zari kwa jamaa huyo.

FAMILIA YA DIAMOND CHEREKO
Wakati hayo yakiendelea kwa Ivan, jijini Dar chereko zinasubiriwa za kumpokea mgeni kwenye familia ya Diamond ikielezwa kwamba Zari atajifungua muda wowote kutoka sasa.

Mzazi Mwenziye Sugu Mahakamani Tena....Aamua Kudai Haki ya Mtoto wake yake Upya....

$
0
0
Imelda Mtema
FAIZA Ally, ambaye ni mzazi mwenzie na mbunge wa Mbeya mjini kwa ‘leseni’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Mr. Sugu’ anadaiwa kukata rufaa na kurudi mahakamani kudai upya haki yake juu ya malezi ya mtoto wake.

Mrembo huyo mwenye vituko kwenye suala la uvaaji ‘alitinga’ mahakamani hapo sanjari na mwanasheria wake, ndugu na baadhi ya watu wa karibu kwa lengo la kupinga hukumu iliyotolewa awali katika Mahakama ya Mwanzo ya Sinza jijini Dar, iliyoamua kuwa hana haki ya kuishi na mwanaye (Sasha).

Hata hivyo, Faiza alikataa kuzungumzia suala hilo, kwa kile alichokiita… “suala liko mahakamani, tuiachie uhuru wake”. Kesi hiyo itaanza kuunguruma upya mnamo Agosti 18, mwaka huu.

Wema Sepetu Akubali Kushindwa Adai Siasa Bila Kujipanga Utoki... ‘Utakatwa’ tu!

$
0
0
Leo tunaye msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu ambaye hivi karibuni alithubutu kugombea ubunge kupitia viti maalum mkoani Singida.

Kwa bahati mbaya kura za msanii huyu hazikutosha. Mwandishi wetu alionana na mwanadada huyo nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar na kumpiga maswali 10 mujarabu. Ungana nami…

Ijumaa: Hongera kwa kujitosa kwenye siasa, nini kilikusukuma kuingia huko?

Wema: Nilikuwa nashauku ya kuwa mheshimiwa, hata baba yangu aliwahi kuniambia naweza hivyo nikajaribu bahati yangu.

 wema (8)Ijumaa: Ukiacha marehemu baba yako, nani alikupa sapoti kubwa na ukajiona unaweza?
Wema: Namshukuru mama yangu, alinipa sapoti kubwa nikajiona naweza kwani alinitoa hofu niliyokuwa nayo.

Ijumaa: Unadhani kipi kimekuangusha kwenye uchaguzi ule?

Wema: Uchanga wangu kwenye siasa lakini naamini muda ulikuwa bado.

Ijumaa: Ingawa hukufanikiwa kupata nafasi ya ubunge umejifunza nini kupitia siasa?

Wema: Kwa kweli nimejifunza vitu vingi maana haviendani hata na umri wangu na nimepata ujasiri mkubwa. Kikubwa ukiingia kwenye siasa ujipange sana.

Ijumaa: Je, kwa hatua uliyoifikia unategemea kuendelea na siasa?

Wema: Niache? Siwezi kwani itakuwa kazi yangu, kama gari ndiyo limewaka sasa.

Ijumaa: Najua siasa ni hela hasa kipindi cha kampeni, uliwezaje kumudu gharama zote?

Wema: Ni rahisi sana ukiwa na watu wanaokupenda, walijitokeza watu kunichangia kwa ajili ya kuhakikisha nafanikiwa. Siwezi kuwataja lakini nawashukuru sana.

Ijumaa: Tulipata habari kwamba baada ya kushindwa uliangua kilio, kwa nini?

Wema: Unajua unapoenda kufanya kitu lazima una matumaini japo kuna kushindwa lakini kushinda ndiyo lengo sasa usipofanikisha lazima roho inauma.

Ijumaa: Ulijisikiaje ulipokuta nyomi la watu wakikusubiri kwa ajili ya kukupokea wakati hukuwa umeshinda?

Wema: Niliamini nina watu wengi ambao wananipenda na nilijifunza mengi kupitia ujio wao, pia walinitia moyo wa kuendelea na siasa.
Ijumaa: Kuna madai kuwa baada ya kushindwa una mpango wa kuhamia Ukawa, hilo unalizungumziaje?

Wema: Ninachojua watu wa Ukawa wamenitafuta na ilikuwa tukutane jana (Jumatatu) ila tutakutana Jumatano (juzi), nikijua wanachoniitia ndiyo nitafanya uamuzi.

Ijumaa: Baada ya kuingia kwenye mambo ya siasa tumtegemee Wema wa aina gani?

Wema: Mtarajieni Wema wa tofauti na yule mliyemzoea, mambo ya skendoskendo hayatakuwa na nafasi kwenye maisha yangu.

Je, Ntakuwa Nimemuharibu Mtoto? Nimefanya Mapenzi na Mwanaume Ambaye si Baba wa Mtoto...

$
0
0
Mimi nina mtoto wa miezi 10 sasa, niliachana na aliyenipa ujauzito nikiwa na mimba ya miezi 2 mwaka jana mwezi wa 2, na tangu mwaka jana nilikua sijakutana kimwili na mwanaume yoyote yaani nimekaa mwaka 1 na miez 5.

Miezi mitatu iliyopita nilikutana na kaka mmoja akawa anataka kunioa, but juzi nikashiriki nae tendo kibinadamu, na mimi na hisia kweli.Nilisex nae mara 1 tu na nilienda kuoga kabla sijamnyonyesha mtoto.

Naomba kuuliza inaweza kumdhuru mtoto?

Je, nifanyeje?

Msinielewe vibaya ndugu yangu baba mtoto yuko mbali na ana mwanamke mwingine .

Hana muda na mimi kabisa, mimi ni binadamu hisia zilinizidi tu nikawa nimefanya hivyo.

Breaking News...Ester Bulaya Apeta Kura Ubunge na Chadema Kupitia Kura za Maoni...

$
0
0
ESTER BULAYA  Ameingia Tatu Bora ...KATIKA WILAYA YA BUNDA NA KUWA MTU WA TATU

MATOKEO YA BUNDA MJINI
PIUS KURA 61
MAGEMBE KURA 40
BULAYA KURA 37
FRANK KURA 35
MAGANJA KURA 5
JANE KURA 0
CHACHA KURA 0

Katika Ukurasa Wake wa Facebook Ameandika Hivi:

CHADEMA tunaendelea tulianza na mungu tunamaliza na mungu, nawashukuru sana wanachadema Bunda kwa kunipokea na kunipa heshima kubwa, mbali ya ugeni wangu ndani ya chama mmeonyesha mnaniamini. mmenipendekeza kwenye majina matatu ili kusubiri uteuzi wa vikao vya kamati kuu vitakavyoamua nani apeperushe bendera katika jimbo la Bunda. Lakini pia mkanipendekeza kuwa namba moja kwenye viti maalum kwa kura nyingi. Nawaahidi sitowaangusha, yeyote atakae pita kati yetu tutashinda Bunda Mjini. Mungu ibariki Chadema ibariki Tanzania.


Mbunge wa CCM Awakimbia TAKUKURU.......Ni Baada Ya Kunaswa Akigawa RUSHWA Kwa Wapambe Wake

$
0
0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Manyara, imemhusisha Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri (pichani kulia), na tuhuma za kutoa hongo katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Takukuru inadai kuwa mbunge huyio alinusurika kukamatwa juzi usiku akiwa na wapambe wake waliokuwa wanagawa rushwa.

Kamanda wa Takukuru mkoani Manyara, Mogasa Mogasa, alisema Chambiri akiwa na wezake watatu ambao wanashikiliwa na taasisi hiyo, alinusurika kwa kutimua mbio usiku majira ya saa nne na kuacha kitita chaSh. 500, 000 alizokuwa nazo katika kijiji cha Kiongozi akitaka kuzigawa kwa baadhi ya watu wake.

Pia taarifa ya kamanda huyo ilieleza kuwa Chambiri alifanikiwa kukimbia akiwa na viongozi kadhaa wa kijiji hicho ambao kamanda huyo hakuta kuwataja majina, akisema kuwa wanaendelea kutafutwa na kumtaka Chambiri ajisalimishe.

Kamanda huyo aliwataja waliyokamatwa kuwa ni Samuel John Barani ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha CCM wilaya; Thomas Cosmas Darabe na Ally Ayubu Ramadhani, ambao walikuwa na mgombea huyo katika harakati hizo.

Kamanda Mogasa aliongeza kuwa baada ya watuhumiwa hao kukutwa katika eneo hilo na Chambiri kutokomea, walifanikiwa pia kukamata makaratasi yenye majina ya watu waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya mgawo huo.

Hata hivyo, alisema wanaendelea na mahojiano watuhumiwa hao na kwamba baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mahakamani na kuongeza kuwa wanalishikilia gari la mbunge huyo.

Chambiri alipoulizwa, alikana kuhusika na kudai kuwa ni mbinu zinazotumiwa na baadhi ya watu wasiyomtakia mema.

Aidha, alidai kuwa yeye kama mgombea na mtetezi wa jimbo hilo, amekuwa akipata taarifa mara kwa mara za kupangiwa njama kama hizo ili kudhoofisha juhuddi zake za kurejea madarakani.

“Hivi walishindwaje kunikamata wakati wanadai walitukuta tukiwa ndani kama siyo uzushi, mimi nafahamu kuna watu wamewekwa kunichunga hata kama naenda nyumbani kisa tu mimi nisichanguliwe, na hiyo ni baada ya kuona watu wameonyesha upendo kwangu,” alisema Chambiri

Batuli 'Amwaga Machozi' Baada ya Picha zake za Nusu Uchi Kusambazwa Mitandaoni

$
0
0

Staa wa mrembo wa Bongo Movie, Batuli ameonyesha kuchukizwa kwake kwa kitendo cha staa mwenzake, Kitale kuvujisha picha hizi  akiwa faragha na mwigizaji chipukizi, Stanbakora ikiwa ni kati ya moja ya kipande cha kazi yao mpya, kwa madai kuwa anaipa ‘promo’.

 

Kupitia ukurasa wake mtandao Batuli ameeleza kuwa Kitale alimpa picha hizo Mateja ambaye ndiye aliezisambaza kwenye mtandao wa Instagram.

 

“Kwanza mniwie radhi Watanzania mnachokiona na kinachoelezewa ni vitu viwili tofauti mwenye akili timamu anapata jibu kamili. @mkudesimbaoriginal nikuulize hivi wakati unampa @matejamusa picha ulimwambia ni za nini!? hivi naweza kuwa faragha mbele ya camera!? 

 

"Hata kama unapromote movie hii sio kiivyo kama kupromote kitu ndio hivi basi fani yetu imejaa mazumbukuku, hii ni scene iliyopo kwenye movie sioni sababu ya kunichafua kijinga hivi, kizuri kinajiuza @mkudesimbaoriginal  kuandika shit sio njia sahihi ya kupromote kazi yako”- Batuli aliandika.


LOWASSA Aahidi Kuishinda CCM Uchaguzi Mkuu 2015

$
0
0


Waziri mkuu wa Zamani Edward  Lowassa  amewaahidi wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na wale wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.

Lowassa alisema hayo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Demkorasia na Maendeleo ambayo itampa ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja wa Katiba ya wananchi ukawa unaundwa na vyama vinne vya siasa nchini Tanzania ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, Cuf na NLD.

Aidha, Lowassa aliyekabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe katika ofisi za Chadema makao makuu yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam jana,alichangiwa kiasi kadhaa cha pesa kitakachomsaidia katika yake ya matumaini iliyofufukia Ukawa. Katika hafla hiyo  Lowassa aliongozana na Mkewe pamoja na wana familia na ndugu wengine mbalimbali.

Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba  ili mgombea ameweze kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni lazima awe mwanachama wa chama chochote cha Siasa nchini Tanzania, hivyo Lowassa ni mwanachama halali wa Chadema pia amechaguliwa na vikao mbalimbali vya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hadi usiku wa manane.

Uamuzi wa Lowassa kugombea Urais ulipokelewa kwa shangwe na umati wa wananchi uliohudhuria hafla hiyo makao makuu ya Chadema kinondoni jijini Dar es salaam.

Mwanasiasa huyo Mkongwe atapambana  na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi Dk.John Magufuli katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utakaokuwa wa aina yake  mwaka huu wa 2015.

Lowassa arudisha fomu za kuwania urais Chadema

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa  Abdallah Safari (kushoto)  akipokea fomu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Zamani,  Edward Lowassa.

Wagombea Ubunge Tarime Wakamatwa Kwa Kutengeneza Kura FEKI

$
0
0

Uchaguzi wa kura za maoni kupitia CCM katika jimbo la Tarime Mjini na Vijijini umeahirishwa hadi kesho baada ya kukamatwa makaratasi maalum ya kupigia kura (kura feki ) zaidi ya elfu 20 zikiwa na majina ya wagombea, Nyambare Nyangwine na Gaudencia Kabaka yakiwa tayari yameshawekewa alama ya NDIO kuonesha kura zimekubaliwa


Wanachama CCM Zanzibar wakataa kumuunga mkono Lowassa

$
0
0


Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, wamesema hawapo tayari kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kwa kitendo cha kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema.
 

Wametoa tamko hilo jana mbele ya waandishi wa habari katika ofisi kuu za CCM Kisiwandui.

Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya wanachama wezake, Katibu wa mkoa wa mjini CCM, Muhammed Nyawenga, alisema Lowassa asidhani kuwa wanachama wengi wa CCM walimuunga mkono wakati alipotangaza nia ya kugombea urais wa Muungano kupitia chama hicho, akadhani kuwa na sasa watakuwa pamoja naye.

Alisema wanachama wa CCM hususan kutoka Zanzibar wanachoangalia kwanza ni chama na mtu baadae hivyo kama kaamua kujiunga Chadema hawako pamoja naye.

“Tunamwambia Lowassa kama mvuvi wa pweza basi tutakutana mwambani,”alisema kupitia tamko hilo.

Walisema wanashangazwa na baadhi ya vyama vya upinzani hasa vile vinavyouunda Ukawa namna wanavyoendelea kuendesha siasa za ubabaishaji na ulaghai kwa Watanzania.

Alisema ni jambo la aibu na la kufedhehesha kuona kwamba hata baada kufikisha umri wa miaka 23 tangu kuanzishwa rasmi kwa vyama vya upinzani bado vyama hivyo vimeshindwa kuandaa wagombea wenye uwezo wa kuwaongoza Watanzania na kuishia kudaka mapumba yanayotoka CCM.

Alisema uamuzi wa Lowassa kutoka CCM sio jambo la kukishtua chama, wanachama wala viongozi wa chama hicho na kamwe CCM haiwezi kudhoofika wala kupasuka kwani sio mara ya kwanza kwa CCM kuondokewa na kiongozi muandamizi na kujiunga na upinzani.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi ambae alikuwa kinara katika kumuunga mkono Lowassa wakati akiomba ridhaa ya chama hicho kugombea urais kupitia CCM, Borafya Silima Juma, alisema kiongozi huyo anapenda madaraka na ukubwa na ndio maana baada ya jina lake kutopita ameamua kujiunga na Chadema.

Je Wajua Kuwa Diamond Anapendwa Kenya Kuliko Tanzania ? Ona Jinsi Alivyopokelewa Nchini Kenyaaa

$
0
0

Nimekuwekea picha hapa jinsi Dimond alivyopokelewa kwa shangwe la nguvu huko Nairobi...

AZAM FC Waleta Heshima Kwa Tanzania, Wawatuliza Wakenya Kwa Bao Mbili..Wachukua kombe la Kagame

$
0
0
Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Kagame Cup 2015 imemalizika August 2 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa kupigwa michezo miwili wa mshindi wa tatu na mchezo wa fainali.

Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulipigwa kuanzia saa 7:30 mchana kwa kuzikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Khartoum ya Sudan, mchezo ambao umemalizika kwa KCCA kushinda kwa jumla ya goli 2-1.

Baada ya hapo ulipigwa mchezo wa fainali uliozikutanisha timu za Azam FC kutokea Tanzania na Gor Mahia kutokea Kenya huo ni mchezo wa sita kwa Azam FC kucheza bila kufungwa katika michuano ya Kagame.

Azam FC imeifunga Gor Mahia ya Kenya goli 2-0 huku magoli ya Azam FC yakifungwa na nahodha wa timu hiyo John Bocco dakika ya 16 kipindi cha kwanza huku goli la pili likifungwa na Kipre Tchetche dakika 65, kwa matokeo hayo Azam FC ni bingwa wa Kagame Cup 2015.

Wastara: Yusuph Mlela Anafanana Vitu Vingi na Sajuki

$
0
0
Staa wa Bongo Movies, Wastara Juma amefunguka na kumwagia sifa muigizaji mwenzake, Yusuph Mlela kuwa ni mtu ambaye anafanana vitu vingi na aliyekuwa mume wake, marehemu Sajuki  na kusisitiza kuwa huwa hachoki kufanya naye kazi.

Kupitia ukurasa wakekwenye mtandao wa instagram, Wastara aliweka picah hiyo hapo juu na kuandika;

Mama na mwana mama na baba nimeipenda kma ilivyo ila kiukweli huyu jamaa nampenda mfano hakuna mpole muelewa hana makuu anao ubinadaamu hana ugomvi na mtu mpole ajui kufoka wala kugombana akikasirika dakika 2 tu anarudi kuwa normal sichoki kufanya naye kazi namchukulia ni mdogo wangu wa tumbo moja namfananisha vitu vingi na Sajuki si mwingine ni Yusuph Mlela au Mlelandro

MWIGIZAJI Ray Afichua Siri ya MREMBO Chuchu Hans!

$
0
0
Muigizaji mahiri wa kiume hapa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’amefichua siri iliyomfanya kunasa kwa staa mwenzake Chuchu Hans, na hata kupata msukumo wa kumuweka hadharani tofauti na tabia yake ya nyuma ya kutopenda kumuanika mpenzi wake.

Akizungumza na gazeti la Risasi akiwa kwenye tamasha la kimataifa la Filamu ‘ZIFF’ lililofanyika visiwani Zanzibar, Ray alisema kilichomsukuma kumuanika Chuchu ni mambo yake adimu ambayo huwezi kupata kwa mwanamke mwingine.

Alisema anamuona kuwa na tabia zote za mke, ndiyo maana aliweza kumtambulisha kwa jamii kwa kuwa ana imani naye kwa kila kitu hivyo yuko huru watu kumfahamu.

“Bwana huyu mwanamke ana vitu vyake adimu sana, na kwa kweli nampenda na ana chembechembe zote za kuwa mke ndiyo maana nilikuwa huru kumuweka wazi bila wasiwasi wowote,” alisema Ray ambaye pia aliwahi kutoka kimapenzi na Johari.

Chano:GPL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live


Latest Images