Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104744 articles
Browse latest View live

Steve Nyerere Aongea Maneno Haya Baada ya Kupigwa Chini Ubunge Jimbo la Kinondoni.....

$
0
0
‘Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu lakini niwashukuru Wananchi wa wiliaya ya  Kinondoni wamenionesha upendo ambao sikutarajia kwao, la pili sikubahatika kulishika gurumo hili la kuwa kiongozi na sitaweza kukata tamaa kwasababu hivi vitu vinahitajika uvumilivu kidogo,  siasa inahitaji kuwa mvumilivu na kila kitu kinachofanywa kama mwanadamu kinachotaka kupigiwa kura au kutafuta maisha ni uvumilivu unaohitajika kusonga mbele’ – Steve Nyerere

Kwasasa nipo kidogo mapumziko nikitafakari kuna yale niliyoyafanya na changamoto nilizozipata katika uchanguzi huo nimejifunza mambo mengi mengi ambayo kwangu yanatija kwa hiiyo kwangu ni changamoto kubwa sana’ – Steve Nyerere

Diamond Platnumz named Highest Royalty Earner by Copyright Society of Kenya

$
0
0
Tanzania Superstar Diamond Platnumz has been named the Highest Royalty Earner by Music Copyright Society of Kenya popularly known as MSCK.

Here is part of the Press Statement from MCSK.


The MCSK has declared the delayed June 2015 SCIENTIFIC PPP distribution of kshs 30.3 million . The declaration relates to the revenue collected between April to June 2015 and has been apportioned using log sheets obtained from the new monitoring system ” VERICAST ” as adopted by MCSK .

Secular music has regained the top position which had previously been dominated by Gospel music with SAUTI SOL emerging as the highest earners and most popular group during the period April to June 2015 . Closely following SAUTI Sol was BAHATI who emerged as number two and reaffirmed the presence of Gospel music with WILLY PAUL at number 4 . At number three was vernacular singer LADY WANJA who is a sister to the LATE QUEEN JANE with another vernacular singer MUM CHEROP rounding up the top five highest earners and most popular artistes based on air play logs in Kenya for the period APRIL to JUNE 2015 .

The full list of the top ten LOCAL ARTISTS is as follows;

1) Sauti Sol
2) Bahati
3) Lady Wanja
4) Willy Paul
5) Mum CHEROP
6) H-Art The Band
7) Gloria Muliro
8) Rabbit ” King Kaka ”
9) John De Mathew
10) Hellena Ken

In the INTERNATIONAL CATEGORY, DIAMOND dislodged ANGELA CHIBALONZA as the highest earner and most popular Non – Kenyan artist .

COMBINED LOCAL AND FOREIGN TOP TEN LIST

1) DIAMOND (Tanzanian)
2) SAUTI SOL ( Kenyan )
3) CHRISTINA SUSHO (Tanzanian)
4) ALI KIBA (Tanzanian)
5) BAHATI ( Kenyan )
6) LADY WANJA ( Kenyan )
7) JOSE CHAMELEON (Ugandan)
8) ROSE MUHANDO (Tanzanian)
9) WILLY PAUL ( Kenyan )
10) KOFFI OLOMIDE (D.R.C).

Source: Msetoea

Bi Harusi Apandisha Mashetani Kanisani!

$
0
0
Chande Abdallah na Deogratius Mongela
Mshtuko! Bi harusi Agnes Omari (26) amezua kizaazaa baada ya kudaiwa kupandisha mashetani kanisani wakati akivishwa pete ya ndoa, hali iliyosababisha tendo la kufungishwa ndoa kusimama kwa muda kwa ajili ya kutafuta msaada wa maombi.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, bwana harusi, Arnold Martin alisema sakata hilo lilijiri hivi karibuni kwenye Kanisa Katoliki la Parokia ya Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Alisema kwamba, alipata taarifa usiku wa kuamkia siku ya ndoa kutoka kwa msimamizi wa bi harusi kuwa mchumba’ke amepandisha mashetani, tatizo ambalo hakuwa nalo katika kipindi chote walichoishi pamoja.
Kutokana na tatizo hilo, Arnold alisema alivunja utaratibu na kwenda kumuona mchumba’ke huyo na kumkuta akijigaragaza huku akipiga makelele na kuzungumza lugha za ajabu.

“Kulipokucha, hali yake ilionekana kuwa nzuri kiasi kwamba majira ya saa 3:00 asubuhi, aliondoka na msimamizi wake kwa ajili ya kubadilisha gauni la harusi maeneo ya Mbagala-Kizuiani baada ya lile la awali kuonekana kumbana huku na mimi nikijiandaa kwenda saluni,” alisema Arnold.
Baada ya kutoka na msimamizi wake huyo, haukupita muda mrefu akapigiwa simu kuwa hali hiyo imejirudia, akamfuata na kumbeba kwenye gari lake kisha kumkimbiza katika Parokia ya Mbagala-Zakhem kwa ajili ya msaada wa maombi na kutoa taarifa kwa paroko kuhusu hali  ya mchumba’ke huyo.

Bi harusi huyo aliombewa lakini wakati akimvisha pete ya ndoa kanisani hapo hali hiyo ilijirudia ndipo alipohamishiwa katika Kanisa la Nabii Yaspi lililopo Buza-Kipera jijini Dar ambapo wakiwa huko, walikutana na wachungaji ambao waliwaombea na hali ikatulia.

“Hali hiyo ilijirudia tena wakati tukipiga picha palepale kanisani akaanza tena kupandisha mashetani, akaombewa lakini hali ilizidi kuwa mbaya, wakaja watu wa Karismatiki nao ikashindikana ikabidi tufunge safari tena kuelekea kulekule kwa Nabii Yaspi ambako aliombewa, akapona.
“Wakati tukiingia ukumbini, hali hiyo ilijirudia tena ambapo sherehe nzima iliharibika na kuwa majonzi hivyo kila mtu akaondoka kimyakimya.

“Bi harusi aliondoka na ndugu zake usiku ule hadi kesho yake nilipoambiwa amerudia hali yake ya kawaida ila kinachonishangaza nilipoenda pale nyumbani kwao alikuwa akionesha kama vile hanifahamu kabisa pamoja na kwamba nilifunga naye ndoa,” alisema Arnold ambaye alidai kuwa anatarajia kurudi tena kwa Nabii Yaspi ili kumaliza tatizo hilo.

Mwenyekiti wa Wenyeviti CCM Taifa, Mgana Msindai Ahamia CHADEMA

$
0
0
Mhe Mgana Msinda  akiwasalimia  wajumbe  wa  Baraza  Kuu CHADEMA
****
Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai jana alijiunga na Chadema na kutambulishwa katika mkutano wa Baraza Kuu la Chadema.

Mgana, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Iramba Mashariki (2000-2010) alitambulishwa pamoja na Mbunge wa Arumeru Magharibi (CCM), Goodluck Ole Medeye na ofisa mwandamizi wa chama hicho, Matson Chizii.

Makada hao wa CCM jana usiku waliambatana katika kikao hicho na aliyewahi kuwa waziri mkuu Edward Lowassa.
 
Habari zinasema kuna makada zaidi wa CCM watakaotambulishwa katika mkutano mkuu wa Chadema leo.

Nape Asema Wanaohama CCM ni sawa na Mafuta Machafu.......Amtakia Kila la Heri Edward Lowassa

$
0
0
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema wanachama waliokihama chama hicho wamejivua nguo mbele za watu na kwamba wapinzani wanaowachukua wanahangaika na mafuta machafu.

Aidha, amesema aliyekuwa Mbunge wa Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Milton Mahanga, alikuwa anatafuta sababu za kuihama CCM na anamtakia kila la heri, yeye na rafiki yake, Edward Lowassa.

Nape aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, alipotakiwa kueleza kuhusu kuhama kwa Lowassa na Dk Mahanga ambao wote kwa nyakati tofauti wamekimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Lowassa alijitoa CCM wiki moja iliyopita baada ya kukwama uteuzi wa CCM wa kuwa mgombea wake wa urais na kukimbilia Chadema ambako anatarajiwa kuwa mgombea wake wa urais na kuungwa mkono na Umoja wa Vyama vinne vya Upinzani (Ukawa).

Dk Mahanga naye alijitoa juzi baada ya kukwama katika kura za maoni jimboni Segerea. “Wanahangaika na oil chafu. Hawa ni wale wale kama ilivyokuwa Mrema (Augustino) mwaka 1995, akabebwa kiasi cha Mwalimu Nyerere kusema mwacheni abebwa.

"Hebu jiulizeni wanaona ubaya wanapotoka, lakini mambo yakiwanyookea hawasemi, wakitoka ndio maneno mengi,” alisema Nape.
 
Alisema kuondoka kwa Lowassa na wengine wachache, si jambo la kwanza kutokea CCM, na pia si la ajabu wala haliwezi kuwa la mwisho huku akimtuhumu Dk Mahanga kuwa alikuwa akitafuta sababu ya kuondoka CCM.

Akizungumzia mchakato wake Mtama, Nape alisema kulifanyika juhudi kubwa za mafisadi kuhakikisha anashindwa, lakini anashukuru ameshinda na kwamba endapo atapitishwa na chama hicho kugombea ubunge, ana hakika atashinda kwani ni mwadilifu na anayezingatia ya chama hicho ikiwamo kupiga vita rushwa.

Ang'atwa na Nyoka Akizini na Mke wa Mtu Kichakani

$
0
0
Kijana mmoja shija kasamwa mwenye umri wa miaka 28,leo mchana amejikuta akipata masahibu ambayo iwapo atapona kamwe hatayasahau kabisa ktk maisha yake.

Kijana huyo mkazi wa mkoa wa Shinyanga ktk kijiji cha Chela ameng'atwa na nyoka mwenye sumu kali akiwa msituni akivunja amri ya sita na mke wa mtu.

Inasemekana ndio ilikuwa tabia yake kufanya uchafu huo na mwanamke huyo asiye mwaminifu ktk ndoa yake.

Sasa leo kama kawaida yao walijirusha msituni,wakiwa huko kabla hawajaanza kufanya mapenzi walisikia sauti za watu wakija upande waliokuwepo ndipo wakaamua kuingia kichakani kwa hofu ya kuonekana,ndani ya kile kichaka kikubwa kilichokuwa kimefungasha miti mingi kiasi kwamba haikuwa rahisi kuonekana kwao,ndipo wakaamua kufanya uchafu wao eneo hilo ndipo wakiwa bado wanaendelea na starehe ilihali yule kijana akiwa kashusha suruali yake na makalio yake kubaki wazi alishtuka ghafla kang'atwa na nyoka huyo anayesadikiwa kuwa ni aina ya cobra,kelele za maumivu zikakusanya wanakijiji na mke wa mtu akakimbia kwa hofu.

Utafanya Nini Ukimfumania Mpenzi Wako Katika Hali Kama Hii?

$
0
0
Kila Mtu anajua Kutendwa katika Mapenzi ni Jambo Linalouma Sana kupita maelezo yahitaji moyo wa ziada kuvumilia ..Je endapo ikakutokea ukamfumania mke ama mume akiwa katika hali hiyo hapo juu nini cha kwanza utafanya?

When your heart is broken it is the saddest thing in the world. All your energy leaves you and everything in your life seems to lose all meaning. You gave your heart and soul to this love, and now it is no more. How can your heart ever be whole again?

Uwezi Amini Kuwa Lowassa Sio Sababu ya Dk. Willibroad Slaa Kutoonekana Hadharani na Kwenye Vikao vya Chama..Sababu Hii Hapa

$
0
0
Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa , ukweli wa jambo hilo umeibuliwa.

Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho amesema, madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo.

“Kwa taarifa yako, Dk. Slaa ndiye aliyemtaka Lowassa ajiunge Chadema. Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Taifa Chadema) hakumtaka kabisa huyu jamaa aje kwetu. Kwa sababu hakuona jinsi gani wangewaeleza wananchi juu yake, lakini mzee ndiye aliyeshawishi na vikao vya kumjadili vikaanza mfululizo. Ukiangalia picha za awali, Dk. Slaa yupo.

Kinachotokea kwa Dk. Slaa ni shinikizo kutoka familia yake. Kuna watu walikuwa na matumaini makubwa ya kufaidika endapo yeye angegombea tena na kushinda urais mwaka huu, hivyo wameamua kununa kwa sababu kilichotokea hakina masilahi kwa familia." alisema mjumbe huyo wa kamati kuu

Nape Anasema Lowassa Amejivua Nguo...Najiuliza Alitegemea Aendelee Kuvaa Nguo Chafu?

$
0
0
Nape anasema Lowassa amejivua nguo...najiuliza alitegemea aendelee kuvaa nguo chafu? vazi la kijani alionyeshi uchafu na ndiyo maana upendelewa na Mafisadi. Ilikuwa ni jambo muhimu kwa Lowassa kuueleza umma juu ya Richmond na sasa tumejua. CCM na menejiment yake inawajibika kutoa maelezo ni wapi fedha za umma zilipelekwa. Tunamshukuru Mh. Lowassa kwani aliwajibika kwa mujibu wa sheria kuinusuru serikali na sasa ni wazi kabisa ni mtu safi haswa anapoendelea kuchukua maamuzi magumu ya kujiunga vema upinzani kuyakataa makabaila ndani ya CCM.

By Philip Mlay

Dr. Magufuli Afutika Ghafla Kwenye Vyombo vya Habari......

$
0
0
Wadau mtakubaliana na mimi kwamba ni jambo kubwa na la ajabu sana kuona kwa hali ilivyokua mwanzoni mwa mwezi huu kule Dodoma media zote silihamia kule lakini hivi sasa ni UKAWA,CHADEMA,DR SLAA na LOWASSA basi.

Nauliza mbona kwa sasa Magufuli hasemwi kama alivyotoka Dodoma? Kwani na yeye si anafaa pia kua Rais jamani? Tusimsahau na yeye maana ana mazuri yake pia katika ujenzi wa Taifa hili.

Angalizo Kwa Dr. Slaa na Edward Lowassa!

$
0
0
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taaluma ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata badiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya CHADEMA na hata nje ya CHADEMA wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASSA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:

(1)Lowassa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.

(2)Lowassa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM

(3)LOWASSA ana hasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM

(4)LOWASSA kama waziri Mkuu mstaafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea

(5) Lowassa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miaka zaidi ya 40

(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowassa ambaye ameshika nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki.Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai

(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowassa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowassa ambaye hawajajipanga na ni Pigo kubwa

(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani.Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU

MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine,
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.

(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi

(3)Slaa aliwahi kusema kuwa anapata Nyaraka kwa watu wa Tiss , sasa angalia Mkurungezi wa zamani Tiss Apson ameonekana kwa Lowassa, Kingunge ambaye hajawahi kukaa na Slaa amejitokeza kwa Lowassa , akina Emmanuel Nchimbi na Sophia Simba ambao ni watu wa ndani serikalini na wameshiriki kukuibia wewe Slaa kura wamejitokeza Nyuma ya Lowassa na wala hawawezi kujitokeza kwako. Je, wewe huna akili ya kuona haya?

(4) Lowassa hadi leo ana ulinzi wa Ikulu ambao hauwezi kuhujumiwa , wewe Slaa juzi tu mlinzi wako amenunuliwa.
Lowassa hawezi kupewa nyaraka feki toka ikulu kwa kuwa kuna akina Apson , je wewe una nani zaidi ya Mkeo ambaye umempora kutoka kwa watu wa CCM?

Nina hasira na wewe Slaa pamoja na mkeo toka haraka huko uje huku Mungu anakuita kwa mara ya mwisho umuunge Lowassa katika urais vinginevyo utapotea Kisiasa bado wiki moja tu utapoteza mwelekeo

MAONI KWA LOWASSA

(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi

(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama.Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena

(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimpa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowassa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.

(4)Kama Lowassa ni mwizi na dhaifu kisiasa kwanini CCM wanahangaika baada ya Lowassa kuchukua form??

(5)Kama Lowassa ni mgonjwa , Kwanini CCM wananahaha baada ya Lowassa kuchukua form? Je, wanamuogopa mgonjwa??

HOJA DHAIFU KWA CCM

(1)CCM walisema Lowassa ni Mwizi na anatakiwa kujivua Gamba sasa Lowassa ameondoka kwanini munahofu???

(2)Kama Lowassa ni mwizi Kama wanavyoamini CCM basi nawashauri CCM wasihangaike na jina la Lowassa kwenye tume ya Uchaguzi , waliache harafu wapime nguvu ya Lowassa na Mangufili!!
Kikwete alisema Chama si mtu sasa uje umnadi Magufuli wakati anapambana na Lowassa!!

(3)Nawaomba CCM waje na ushahidi kwenye majukwaa ya Siasa kuonesha kuwa Lowassa ni fisadi, wasikimbilie kwenye kamati ya maadili na NEC.Wakifanya hivyo basi wananchi watachambua pumba na mchele.

By King Cobra/JF

Unamkumbuka Mwanamuziki Defao ? Aonekana Akiwa 'Mchovu' Kenya Huku Sura yake Ikiporomoka kwa Sababu ya Mkorogo

$
0
0
Defao Kulia
Staa mkongwe wa muziki kutoka DR Congo, Jenerali Defao baada ya kutosikika kwa muda mrefu ameonekana huko Kenya, akiwa na muonekano tofauti na alivyozoeleka kutokana na kupungua mwili kwa kiasi kikubwa, na weupe wa ngozi yake ukitia mashaka.

Defao ambaye hata hivyo haijajulikana rasmi ni shughuli gani imempeleka huko Kenya, kutokana na muonekano huo, hisia za wengi zimetafsiri kuyumba kisanaa na kiafya kwa msanii huyo aliyewahi kuwa gumzo kwa sanaa yake katika bara la Afrika na Ulaya.
Hata hivyo, kuyumba kwa msanii huyo pia kunahusisha na kupungua kwa mvuto wa aina ya muziki wa dansi kutoka DR Congo ambao ulifanya vizuri sana katika miaka ya nyuma.

Urais 2015: Lowassa, Haji Duni Wapitishwa Rasmi Kupeperusha Bendera ya Ukawa

$
0
0
Mkutano Mkuu wa Chadema kwa pamoja umempitisha Mwanasiasa Edward Lowassa kama mgombea Urais na Juma Haji Duni kuwa mgombea Mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25 oktoba 2015.

Katika upigaji kura  Kanda zote zimepiga  kura ya NDIYO kwa Mh. Edward Lowassa  na hakuna kanda iliyosema HAPANA, huku wakishangilia kwa nguvu.

Kanda ya Kaskazini, Kanda ya kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kusini na nyingine zote pia zimepiga kura ya NDIYO kwa Juma Haji Duni kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi nkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Kufuatia matokeo hayo Mwanasiasa Edward Lowassa  atapambana na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na wagombea wengine akiwemo Mchungaji Christopher  Mtikila wa chama cha DP aliyechukua fomu ya urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) jijini Dar es salaam wiki iliyopita.

Kinana Asema CCM Inashindana Na MAKAPI Yake

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amesema kwamba chama Chama Mapinduzi kinatarajia kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi oktoba mwaka 2015.

Akizungumza na Wanachama wa CCM leo katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es salaam mara baada ya mgombea wake wa Urais Dk.John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais tume ya Taifa ya Uchaguzi  amesema kwamba chama hicho kwa bahati nzuri mwaka huu kinashindana na makapi yake ambayo kamwe hayawezi kuishinda CCM.

“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi nani mshindi?” Amehoji  Kinana

Ameongeza kuwa kila mwanachama akitengwa na CCM mahala pake ni wapi? Huku mamia ya wananchi wakijibu ‘Chadema’ kwa sauti ya juu.

Naye Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete amesema kwamba  serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya Maendeleo na mwaka huu wana waahidi watanzania ushindi wa kishindo.

Kwa upande wa Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli amesema kwamba ikiwa atachaguliwa kuwa rais  anakwenda kufanya wananchi walicho mtuma kwa kuwa shida za watanzania anazifahamu huku akirejea kauli yake Maendeleo hayana chama.

Hivi karibuni chama cha Mapinduzi kimepata mtikisiko mkubwa kufuatia  wanachama wake kuhama chama hicho na kutimkia Upinzani hususani Chama cha Chadema akiwemo Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa, Makongoro Mahanga, James Lembeli  pamoja na Ester Bulaya

Aunt Ezekiel Anaimani na Lowassa au Magufuli?, Jibu Liko Hapa

$
0
0
Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wasanii kwenye tasnia ya Bongo Movie wao walishatangaza hivi karibuni kuwa imani yao katika uchaguzi mwaka 2015 wanaamini CCM kitashinda kupitia mgombe wake Dk. John Pombe Magufuli.

Agosti 4, 2015 kupitia kwenye mtandao wa instagram mwigizaji Aunt Ezekiel ameamua kuyatoa ya moyoni na kumtaja mgombea wa urais  ambaye anaimani naye kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuyaandika haya :

Tunaimani na Lowassa..Mungu bariki Tanzania, Mungu bariki Africa

Sauti ya Nuh Mziwanda akiongea na Wema Sepetu imetengenezwa? mwenyewe kazungumza..#UHeard (Audio)

$
0
0
Baada ya ile sauti ya Nuh Mziwanda akidaiwa kuzungumza na Wema Sepetu kuvuja sana kwenye mitandao ya kijamii,  leo Nuh amezungumza na kusema ni uvumi.

Nuh amezungumza na Soudy Brown na kusema iyo sauti ni watu wanatafuta wameamua kuitengenzea kwa masilahi yao wenyewe na si yeye kama inayodaiwa, amesema hakuna kitu kama hicho, na hataki kuongelea sana mambo hayo.

Amesema imemuharibia sana na hata simu yake kuvunjwa na Shilole pia, nguvu ya kufanya kazi kwake imepungua..na anaamini watu waliofanya hivyo ni anaokutana nao na kuchekea nao kila siku.

Msikilize mwenyewe akizungumza na Soudy Brown hapa…

Who Is The Star Now? Here How ERIC OMONDI Landed in Tanzania And Left Tongues Wagging

$
0
0
Over the weekend, Eric Omondi flew to neighboring Tanzania for a show dubbed #EricOmondiLiveInDar. Here is how he landed in style;

“TANZANIA! Aliye na macho haambiwi Tizama! Let me introduce thisBeautiful, Gorgeous Kenyan women…They are Kenya’s finest dancers… The show began at the
Airport…TANZANIA! TANZANIA!”





To all MEN, this is how you spot a Chips Funga in the Club.

$
0
0
They come, in different shapes and sizes. They pamper you with love (or is it lust) in a club and the next moment she is snoring beside you in your apartment.

If you are lucky, the ‘chips funga’ disappears before cock crow and if your stars are not right, she hangs around for the better part of the day. And when you are completely unlucky, you wake up to an empty house, drugged and robbed. Then you sit on the floor wondering how all this started.

And because it’s my responsibility to be my brothers’ keeper, I chose to enlighten you on how to spot a ‘chips funga’ and run, as fast as your legs can carry you. Unless waking up to a total stranger or getting robbed sits well with you.

1. Offers to buy you drinks – Nothing is for free in this world my friend. I also think that no man worth his salt should accept a free drink from a lady he has met for the first time 15 minutes ago.


Not that ‘chips fungas’ have lots of money to go buying people drinks. They are luring you with it, their eyes on the price. They know everybody likes free stuffs.
Gents, when a stranger woman offers you a drink, laugh it off and offer her one yourself.

2. Talks about herself – If you strike a conversation with a stranger and she starts to talk about her six digits pay slip job or business, how she hangs out with who is who, how she lives in a leafy suburb, buddy be warned.

We all know it is the nature of women to talk (much) but there is a difference between talking and bragging. She is trying to win your confidence and do away with any doubts you could be having on her.

3. Is all over you – No woman falls in true love that quickly, even the Kalenjins who are the marathon legends. Dude, if you give in to this kind of woman who is caressing you 10 minutes after meeting her, you are dead meat.

She is holding your hand as if her life depends on it. She only wants to use you for a night and steal your new flat screen TV. Want to be safe?

PICHA: Magufuli Alitikisa Jiji la Dar es Salaam Wakati Akichukua Fomu ya Kugombea Urais

$
0
0

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.

Kumbe Askari Magereza Ndiye Aliyetoa Mafunzo Mauaji ya Polisi Stakishari

$
0
0
Na Makongoro  Oging’
Kuna taarifa kwamba kumbe askari magereza mstaafu wa Gereza la Dondwe,Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani (jina linahifadhiwa) anadaiwa kuhusika katika zoezi nzima la utoaji wa mafunzo ya kijeshi kwa watu waliovamia Kituo cha Polisi Stakishari jijini Dar es Salaam Julai 12,mwaka huu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonesha kwamba askari huyo anatajwa kuhusika kutoa mafunzo ya kijeshi na mbinu za medani kwa watu walioshiriki kitendo cha kinyama cha kuvamia kituo, kuiba silaha na kuua raia na askari.

Mwandishi wetu alielezwa na vyanzo makini vya habari kwamba askari huyo alikuwa akitoka kijijini kwao ambacho kipo mbali na makazi ya wanaodaiwa wahalifu wa tukio hilo na kuja kwenye ngome hiyo kwa ajili ya kutoa mafunzo.

“Alikuwa akijidai kuja kwenye ibada lakini alikuwa akipita   nyumba nyingi za ibada, kitu kilitotushangaza wengi kwani hata kama mvua ikinyesha, hakukosa kwenda kwenye ngome ya wahalifu wale.
Imeelezwa kwamba askari huyo alikuwa akiwatembelea watuhumiwa hao huko porini kwenye ngome yao bila vikwazo lakini  raia wa kawaida hawakuruhusiwa kwenda au kupita maeneo hayo jambo liliokuwa likileta maswali mengi juu ya uhusiano wa askari huyo na watuhumiwa hao.
Hivi karibuni wananchi wa Kijiji cha Mandikongo, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani walipokuwa wakiishi watuhumiwa hao wa mauaji wa Polisi wa Kituo cha Stakishari walikaa katika mkutano kujadili  kuhusu suala la ulinzi na usalama, wakakubaliana kwa pamoja kushirikiana na polisi na vyombo vyote vya usalama kuwasaka waliohusika na tukio hilo waliokuwa wakiishi katika pori la kijiji hicho.

Hata hivyo,  wananchi hao walisema askari huyo mstaafu wa magereza lazima asakwe na kukamatwa ili ahojiwe na vyombo vya serikali kuhusu urafiki wake na watuhumiwa hao ambao kwa sasa wamekimbia na familia zao na hawajulikani walipo.

“Unajua huyu askari tuna wasiwasi naye maana angekuwa mtu mzuri angeweza kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kuhusu kikundi hicho hatari,” alisema mwanakijiji mmoja wa kijij hicho ambaye hakupenda kuandikwa jina gazetini.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mandikongo, Issa Said Mchalaganga alisema kwamba kamati ya ulinzi na usalam  kijijini hapo wamedhamiria
 watuhumiwa wote wanapatikana pamoja na silaha nzito za kivita walizokimbia nazo.
Watuhumiwa saba wanaosadikiwa kuhusika katika uhalifu mbalimbali likiwemo tukio la Stakishari hawajapatikana na vyombo vya dola vinaendelea kuwasaka.

Polisi hivi karibuni walisambaratisha kambi ya kikundi hicho na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja, bunduki 15 na fedha shilingi milioni 170 zilizochimbiwa chini katika kambi ya watuhumiwa hao.
Polisi wanne na raia watatu waliuawa katika uvamizi wa Kituo Kikuu cha Polisi Stakishari cha Wilaya ya Kipolisi Ukonga, Julai 12, mwaka huu na watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika na uvamizi huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Lucas Mkondya alipohojiwa alisema anaendelea kuwasaka watuhumiwa.

“Nawaomba wananchi kutoa taarifa kituo chochote cha polisi, vyombo vya usalama au kwa wenyeviti wa serikali ya mitaa wakiwaona watu wanaowatilia shaka,” alisema.
Viewing all 104744 articles
Browse latest View live




Latest Images