Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Profesa Lipumba Aondoka Nchini Akiwa Chini ya Ulinzi

0
0
Saa chache baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kujiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ametoweka nchini.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja amekwenda nchi gani na atakaa kwa muda gani.

Profesa Lipumba aliondoka nchini baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacok jijini Dar es Salaam, ambako alitangaza kujiondoa katika chama chake na katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Taarifa zilizopatikana, baada ya kumaliza mkutano na waandishi, alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na aliondoka nchini kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda (Rwanda Air).

Awali kiongozi huyo ambaye alivaa suti ya ‘dark blue’ na shati jeupe alikuwa apande ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) 485, lakini alibadili mwelekeo baada ya kufika uwanjani na kuamua kupanda Rwanda Air kuelekea Kigali saa 9 alasiri.

Chanzo cha uhakika kutoka uwanjani hapo, kilieleza  kuwa Profesa Lipumba, alifika saa 7:00 mchana akiwa na vijana wawili wa kiume ambao walionekana kama walinzi wake.

Katika muda huo ambao Profesa Lipumba alikuwa katika taratibu za kuondoka, palikuwapo na ndege nne tu za kwenda nje ya nchi.

Vijana hao ambao hawakujulikana majina yao, walikuwa wakifuatilia kila hatua ya kile alichokuwa akikifanya Profesa Lipumba, huku yeye akionekana mwenye wasiwasi na msongo mkubwa wa mawazo.

“Profesa Lipumba anaonekana hayuko katika hali ya kawaida, anaonekana ni mtu mwenye msongo wa mawazo, na pia ana wasiwasi kama vile kuna jambo linamsumbua.

“Macho yake yalionekana ni mekundu mithili ya mtu aliyekuwa akilia kwa muda mrefu, huku uso wake ukionekana hauna furaha,” kilisema chanzo chetu.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amelazimika kukatisha shughuli za kiserikali alizokuwa nazo Zanzibar na kwenda jijini Dar es Salaam kunusuru hali ya sintofahamu ndani ya chama hicho.

“Ndiyo hivyo imeshatokea, lakini tayari katibu mkuu amekuja bara kuhakikisha mambo yanakaa sawa na chama hakiyumbi,” alisema kiongozi wa CUF ambaye hakupenda kutajwa jina.

Dr. Slaa Akubali Kurejea Ofisini

0
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, anatarajiwa kuwasili ofisini kwake leo, baada ya kutoweka tangu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alipojiunga na chama hicho hivi karibuni.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Baraza Kuu la chama hicho kuridhia apumzike kwa muda, baada ya kutofautiana na Kamati Kuu kwa kile kilichoelezwa kumkaribisha Lowassa.

Vyanzo vya uhakika ndani ya Chadema vimesema  kuwa Dk. Slaa huenda akarejea ofisini leo kutokana na mazungumzo yaliyofanyika kwa nyakati tofauti na viongozi waandamizi wa chama hicho.

“Jana (juzi) mzee Philemon Ndesamburo na makada wengine wa chama walikwenda nyumbani kwa Dk. Slaa kwa ajili ya mazungumzo, na kwamba amekubali, amesema atarejea ofisini kesho (leo),” alisema mtoa habari huyo.

Vyanzo hivyo vilisema Dk. Slaa amekubali kurudi ofisini na kuendelea na shughuli za chama baada ya Ndesamburo na makada wengine wanaoheshimika ndani ya chama hicho kuzungumza naye.

Mazungumzo hayo yanadhihirishwa pasipo shaka na picha zilizosambaa mitandaoni juzi, zilizomwonyesha Ndesamburo akiwa na Dk. Slaa na makada wengine wa chama hicho.

Mmoja wa makada wa chama hicho aliyeshiriki mazungumzo hayo juzi, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alilidokeza gazeti hili kuwa walielewana na Dk. Slaa na akaahidi kuwa atarejea ofisini muda wowote.

“Ni kweli tumezungumza na Dk. Slaa, na amekubali atarejea ofisini muda wowote, mengine tuliyozungumza siwezi kukwambia,” alisema kada huyo.

Akihutubia wajumbe wa Baraza Kuu wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema amekutana na Dk. Slaa kwa mazungumzo na kwamba wameelewana apumzike.

“Nilichukua uamuzi wa kukutana na Dk. Slaa kwa sababu ni kiongozi anayeheshimika na kupendwa, na ameshiriki katika hatua zote na vikao vya ujio wa Lowassa kikiwamo cha Kamati Kuu.

“Tulikubaliana kwa pamoja baada ya kupitia mawasiliano ya kitakwimu, kisayansi na tafiti mbalimbali, kwamba kiongozi huyo (Lowassa) ni mpango wa Mungu, na atatusaidia kuwaunganisha wenzetu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Wakati nimezungumza naye aliomba muda wa kupumzika huku akitoa ruhusa ya chama kuendelea na mipango yake ya kuelekea uchaguzi mkuu, tukatumia usemi unaosema maji yakikupwa na kujaa hayamsubiri mtu, hivyo hatuwezi kumsubiri mtu ili tuendelee.

“Tumekubaliana na Katibu Mkuu, apumzike kwa muda na sisi tuendelee, na pindi atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari. Sisi hatuwezi kuzuia mabadiliko kwa sababu ya Mbowe au Slaa,” alisema Mbowe

Kwa yaliyonikuta Sifikilii kupenda Tena.

0
0
Kwa yalionikuta sifikili kwamba ipo siku1 nitatamani kuwa na girl frend, Nakumbuka nikiwa kidato cha 4 kuna bint nilimpenda xana tena sana ila sikuwai kumwambia nampenda. Nafikili sababu zinajulikana kwanza nilikua muoga, hofu ya kukataliwa isitoshe nilikuanae darasa mmoja na sababu zinginezo ikapelekea nishindwe kuongea kwake! Maisha ya shule yaliendelea na hatimae tukamaliza kidato cha nne, tukiwa mtaani namaanisha baada ya kumaliza shule sikumoja nilimpigia sim nikamueleza juu ya upendo wangu kwake! Hakua na tatizo xana katk hilo alizingu zingua siku kadhaa but but akaja akakubali na mahusiano yakaanzia hapo. Siku zilipita matokeo ya kidato cha 4 yakatoka kwamimi sikufaulu xana but nikapata nafasi ya kwenda kidato cha 5 (PCM) Upande wa bint matokeo hayakua mabaya xana lakini alipoteza mwaka mmoja nyumbani na mwaka uliofuata akajiunga na chuo cha ualimu (level ya certificate)

Japokua alikubali kua na mim ila mda huo wote tulikua wapenzi jina tu kwan hatukuwai kukutana kimwili na kila nilipo mwambia kuhusu hilo alikua hanipi jubu la kueleweka ananizungusha tu siku zote hizo. Binafsi kwakua nilimpenda kwa dhat na niliamini ipo cku1 tutakua mke na mume xo sikuona kuwa ni tatizo saana kutonipa penzi lake.
Hali iliendelea hvyo yeye akiwa chuoni kwao (certificate ya Education) Namimi nikiwa advance na kipndi chote hicho tunawasiliana tu swala la kitandani hatujawai kukutana. Ilifika kipindi nikamaliza kidato cha sita yeye akiwa bado anamalizia mwaka wake wamwishochuoni kwao.

Masaa yalienda sikuzilipita na matokeo ya fom6 yalitoka, nashukulu mungu sikufanya vibaya xana nilia apply chuo na kam unavyojua TCU ndo kilskitu kwenye selection za vyuo wakanipangia facult fln hv BACHEROL OF EDUCATION SPECIAL NEED kwenye chuo flan hapa bongo. Kipnd hicho mawasiliano na yule bint bado yapo japokua yalipungua baada ya yeye kwenda chuo lakini sikujali hilo niliendelea kumpenda na hii ni kwakua2 upendo wangu kwa huyu bint ni zaid ya ujuavyo wewe kupenda ( Siwez kuelezea kwan nilimpenda sana huyu bint).

Nikiwa chuo mwaka wakwanza nilikua na msaidia vitu ving xana huyu bint japo hajanipa penzi lake hata cku mmoja, nilikua kam ----- mbele yake kila alichotaka nilimpa na hii ni kwakua tu nilimpenda xana na niliamin nitamuoa, Sikumoja kabla hajamaliza chuo nilikuja hom kipindi nayeye akiwa likizo tukapanga tukutane mahali na hapo ndo akanipa penzi lake kwa mara yakwanza ( Binafsi nili enjoy xana ila nahisi yeye hakufurahia game) Hii ni kwakua sikuwaifanya mapenzi katka maisha yangu xo nilikua fast kumaliz na sikuludia game But bint alinambia nisijali kuhusu hilo kuwa akimaliza chuo atakujakunitembelea chuoni kwetu.

Oky sikumoja baada ya yeye kumaliza chuo alinambia nimtumie nauli aje chuoni kwetu (mie chuon naish geto sikai hostel) nikamtumia akaja. Nakumbuka alikaa geto kwangu cku2 tulipeana mapenzi motomoto ila aligundua weaknes kwangu xo akaniuliza ujawai kua na mtu, Nikamwambia NO uar the first girl in my life. Nahisi alikua hafurahii ninavyomtia NILILIA SANA USIKU NILIPOGUNDUA HAFURAHII GAME NA MIMI alikuja kunibembeleza na kuniahidi haweze kuniacha kwani nimemsaidia vitu ving, Na nikweli nimemsaidia vitu ving mno hasa kipesa sitak kusema sana juu ya hilo ila alinichuna na ni kutokana tu NILIMPENDA SANA,

Alivyoludi kwao mawasiliano na mimi yakapungua nikimpigia cm mara ananambia yupo busy, xaiv nipo nyumbani wik ya pili sasa FIELD nikimuomba tuonane anasema atanistua akiwa na nafasi huku cku zinaenda na kunamda ananikatiaga sim yani kifupi AMENIBWAGA mara yamwisho nikam2mia TEXT nikamwambia IPO SIKU UTANIKUMBUKA ndo ukawa mwisho wa mawasiliano na yeye Ila bado namuhitaji sema hainajinsi kwan kulazimisha PENZ nako ni UTUMWA.

Je tatizo Langu Hapo ni Nini Jamani?

UVCCM Yamvaa Lowassa, Wasema Watamnyosha

0
0
Ndugu waandshi wa habari 
Assalama Alaykum 
Ndugu waandishi wa habari, 

Nchi yetu hivi sasa inapita katika hekaheka za kuelekea uchaguzi Mkuu. UVCCM tumewaita hii leo ili kuwapa taarifa yetu juu ya mwenendo wa kisiasa, suala la vijana na uchaguzi mkuu, mkakati wa UVCCM kuhakikisha wagombea wa Urais kupitia CCM kuhakikisha wanashinda kwa kishindo kikubwa na kuwapa idhari viongozi wa CHADEMA wajiandae kuwahakikishia watanzania kama Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa alihusika na vitendo vya ufisadi kama walivyodai au laa.

Aidha UVCCM tunampongeza kwa dhati mgombea wa CCM Dk John P. Magufuli kwa kuchukua fomu ya urais wa Jamhuri ya Muungano kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC) akiambatana na mgombea mwenza wake Mhe, Samia Suluhu Hassan, 4 August 2015.

Pia Furaha yetu haijifichi na tunapenda kumhakikishia Dk Magufuli na Dk Shein tutabaki nao bega kwa bega ambapo pia hatutasita wala kurudi nyuma kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo cha ajabu kitakachowashangaza na kuwashtua wasaka vyeo na madaraka na wanaotumia gharama za fedha ili kupata uongozi.

UVCCM tunapenda kuwasihi vijana wenzetu wajiweke kando na wanasiasa wachovu waliochoka kifikra na kimwili ambao hawahimili mikiki ya siasa za kileo wanaopania kuwachochea vijana washiriki vurugu na fujo.

UVCCM tunawataka vijana wenzetu kutokubali kughilibiwa, kutumiwa na wanasiasa wachovu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Badala yake sote kwa pamoja tutenge muda na wakati wetu kulinda amani, utulivu na umoja kitaifa kama sera ya CCM inavyosisitiza siku zote..
UVCCM tunachukua nafasi hii kuwakumbusha viongozi wa upinzani husasan CHADEMA kuyakumbuka matamshi walioyatoa na kuyasambaza nchi nzima miaka kadhaa iliopita sasa ni wakati wao kutoa majibu sahihi mbele ya wananchi.

Viongozi wa chama hicho kwa nyakati tofauti walitoa madai mazito dhidi ya mwanachama wao mpya Edward Lowasa na wengine kwa kuwatuhumu kuhusika na ufisadi wakati viongozi wa chama hicho wakihutubia kwenye majukwaa ya kisiasa.
Tunafikiri watatenda ungwana kuwathibitishia watanzania kama wao ni wakweli na si wanafiki wa kisiasa, wababaishaji na wazushi wasiofaa kusikilizwa.

Yale walioyasema, kuyaamini na kuyaeneza sasa ni wakati wao muafaka kuyafafanua, kusema ukweli na kama waliongopa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa wawatake radhi wananchi na wakiri wao ni wataalam wa kuzua na watamke kwa kukiri CCM si chama chenye makandokando ya ufisadi.

Wakati wakijiandaa kumkosha kila waliyemtuhumu katika kina kikubwa cha maji wajue kuwa bila ya kutoa ufafanuzi tope za madai ya ufisadi zitawachafua viongozi wa CHADEMA na kiongozi wanaembeba wakati huu wanapojaribu kutaka kuwashaulisha watanzania. Ni vyema viongozi hao wakatambua kuwa neno likishatamkwa ni vigumu kulirudisha mdomoni.

Ndugu waandishi wa habari.

Tokea kupitishwa na kutangazwa jina la Dk. John Magufuli, kuwa mgombea wa Urais, zama mpya imepambazuka mbele ya upeo wa macho ya watu . Ngurumo za kusafisha mafisadi zimeanza wa kasi kwenye vyama vya upinzani .Kasi hiyo na kusafishana ni hofu walionayo wapizani baada ya kuona ni vipi vyama hivyo vitashindana na mgombea urais wa CCM asiyekabiliwa na tuhuma,
asiyetiliwa shaka huku akiamainiwa na makundi ya vijana, wanawake, wazee, wasomii, wakulima na wafanyakazi kwa utendaji na uchapakazi wake mahiri.

UVCCM chini ya Chama Cha Mapinduzi tunaipongeza Kamati ya Madili, Kamati kuu, NEC na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kushiriki mchakato wa kuyapitisha majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Tunaona fahari kupata wagombea waadilifu, waaminifu, wachapakazi na waaminifu kwa CCM na Taifa letu wakipeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba mwaka huu.

Tunavipongeza vikao hivyo kwa kupitisha wagombea ambao CCM haitapata kazi na gharama ya kuwanadi kwa wananchi wakati wa kuomba kura. Wagombea waliochaguliwa mikono yao ni misafi, hawatiliwi shaka na hawana uchovu zaidi ya kuwa na weledi, uzalendo na kuheshimu kwao misingi ya utawala bora.
Ndugu waandishi wa habari,

Tunampongeza na kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa katika viwanja wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar Es Salam kuwa "tumejiandaa kushinda na tutashinda, tuna uzoefu wa kutosha tunayo maarifa mwaka huu tutatapata ushindi mkubwa." Kauli hiyo imetupa nguvu na ari vijana wa CCM tukiamini CCM ni chama kikubwa kilichosheni hekma na mikakati mizito ya kulivusha taifa wakati wowote wa misukosuko ya pepo za kisiasa. Vijana wa CCM imetulazima kukumbuka historia ya pepo za misukosuko kabla na baada ya uhuru 1961 na Mapinduzi ya 1964.
Historia inaonyesha mwaka 1958 kiongozi wa juu katika TANU Zubeir Mtemvu alijitoa na kuanzisha chama cha ANC na TANU hikugawanyika, mwaka 1967 Waziri muandamizi katika serikali ya TANU Osca Kambona alijiondoa na TANU ilikuwa imara, Mwaka 1959 ASP iliwatimua kina Mohamed Shamte Hamad na kuenda kuanzisha chama cha ZPPP na ASP ilizidi kuwa imara na kujipanga hatmae 1964 ikafanya Mapinduzi.

Mwaka 1984 CCM inayotokana na TANU na ASP ilimvua madaraka aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi CCM haikutetereka, mwaka 1984 ilimfukuza Seif Shariff Hamad na wenziwe 6 CCM haikugawanyika, mwaka 2014 CCM ilimfukuza unachama waziri wake muandamizi (MNEC) Mansour Himid Yussuf CCM haikubabaika, 2015 CCM ilimfukuza unachama mkongwe wa siasa Hassan Nasoro Moyo bado hatujahamanika wala hatukujutia.

Hatuna la kupoteza wala kujutia kwa sababu ya kuondoka Lowasa ndani ya CCM, sisi vijana tunamini kuwa sasa LOWASA si agenda tena ndani ya CCM inayoweza kutusumbua CCM imefunga mjadala.
Vijana tunaendelea kujifunza na kuamini kuwa CCM iliyotokana na TANU na ASP imepita katika misukosuko mingi na imeweza kuhimili vishindo bila kugawanyika na harakati za ukombozi ziliendelea hadi wazee wetu wakitimiza malengo waliyoyakusudia.

Tunarejea tena hatuna cha kupoteza wala kujutia Lowasa kaondoka CCM aende tu na mjadala huo umefungwa tunaimani kubwa na umakini wa viongozi wetu CCM ndio ile ile, wembe ni ule ule, kinyozi ndio Yule Yule hakuna jipya Oktoba 25 kitaeleweka baada ya kumaliza kazi ya safari ya Magufuli na Shein Kuipatia ushindi CCM.
Kubwa tunawakumbusha wapizani wetu hatudharau adui UVCCM tumejipanga kulinda heshima ya Chama, tunasema mwaka huu Mlingoti Chuma, Bendera Chuma na upepo Chuma tunasonga mbele kwa uwezo wa MwenyeziMungu.

waandishi wa habari,
UVCCM tukiwa ni jeshi la msitari wa mbele la CCM tunataingaza rasmi vita ya mapambano ya hoja kwa hoja katika siasa na sasa tunasema Aluta kontinua. Mapambano yanaendelea dhidi ya mawakala wa ubeberu na ukabaila waliojipenyeza katika siasa za nchi yetu, Sisi UVCCM tunawaambia kamwe Ikulu ya Magogoni kule Dar es Salaam na ile ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar katu haitakuwa mahamia au machaka ya kujificha Mafisadi.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
Naibu Katibu Mkuu UVCCM (Tz) Zanzibar
6. Agost 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya August 8

0
0















Habari  Zilizopo  Katika  Magazeti  ya  Leo  Jumamosi  ya  August  8

Shamsa Ford na Nay wa Mitego Waweka Mambo Hadharani.. Wadai Wao ni Wapenzi

0
0


Hatimae Mwanamuziki Ney wa Mitego na Mrembo Shamsa Ford Wamekubali live Bila chenga kwamba wao ni Wapenzi na wanapika na Kupakuwa...Hiii imekuja baada ya Muda Mrefu Kukataa kuwa wao ni wapenzi...Nay na Shamsa Wameongea Hayo Kwenye Global Online TV ya Global Publishers......

CHENGE Akanusha Kuhusika na Tuhuma za Escrow na Wala Hajawahi Kuwa na Mgongano wa Maslahi Kati ya IPTL na VIP.

0
0
TUME ya Maadili chini ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, leo katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar imezidi kumhoji, Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi anayemaliza muda wake anayetuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow anazodaiwa kupata kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineerung, James Rugemalira.

Awali Mwanasheria huyo alifikishwa mbele ya baraza hilo akidaiwa kukiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kupata mgawo wa fedha kutoka kwenye akaunti hiyo ambazo zinakadiriwa kuwa ni sh. bilioni 1.6.

Akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Jaji Hamis Msumi, Chenge alikanusha kuwa hahusiki na tuhuma za fedha za Escrow na wala hajawahi kuwa na mgongano wa maslahi kati ya IPTL na VIP.

Chenge alisema kuwa aliingia mkataba na Kampuni ya VIP katika kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya kampuni binafsi zilizowekeza IPL na kwamba hakuiingia mkataba wa makubaliano na kampuni hiyo ambayo iliingia mkataba na serikali.

Mambo yaliyoainishwa na shahidi wa upande wa serikali ni pamoja na kutumia wadhifa wake kama mtumishi wa umma kupata maslahi binafsi ambayo ni kinyume cha kifungu cha sheria, huku akidai kuwa Chenge amejihusisha na mngongano wa maslahi kutokana na uchunguzi uliofanyika katika vipindi mbalimbali akiwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Change akipangua hoja za mwanasheria wa serikali alisema kuwa serikali iliingia mktaba wa makubaliano ya kuzalisha umeme na Kampuni ya IPL wakati akiwa mwanasheria na baada ya kustaafu aliingia makubaliano ya mdomo na mmiliki wa VIP ya kutoa ushauri kuhusu masuala ya kitaalamu kwa IPL tu.

Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji Mstaafu, Hamis Msumi aliahirisha kusikilizwa kwa shauri hilo kwa madai ya kuwa upande wa wanasheria wa serikali uende kuandaa taarifa iliyosahihi ili kumpelekea Chenge Agosti 11 kwa ajili ya kupitia na baadaye taarifa hizo kupelekwa kwa mwenyekiti wa tume Agosti 14 kwa ajili ya kutoa uamuzi sahihi

Nisha: Natamani Kuzaa Tena Ila….

0
0
Staa wa Bongo Movies , Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye ni mama wa mtoto mmoja kiutani utani  amefunguka kutamani kuzaa ila anahitaji ushauri azae na nani.

Nisha ambaye kwa sasa yupo nchini China, alitanhaza nia yake hiyo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.

"Mwaka huu mastaa wengi wamezaa  na mimi nimetamani kuzaa tena dah.. lakini wakuzaa naye sasa nanii ...  sponsor ana mkewe
gandalandizi?? atanifilisi...

Pls nishaurini jamaniii nna hamu kweliii...Niolewe na kuzaa na sponsor anipe kila nnachotaka Ila kulala kwa mkewe,au kaserengeti boy nimpe kila anachotaka nikifulia atoke nduki??".

Wema Sepetu Hadharani na Rafiki wa Diamond Platnumz

0
0
KABAANG! Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amenaswa kimalovee na rafiki wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku ikidaiwa ni ‘mtu’ wake.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba jamaa huyo ambaye anajiita Dangote Kifyagio ni rafiki wa Diamond ambaye alikuwa akimsaidia mambo yake kimuziki ili awe juu.
wema (3)“Wema yuko karibu sana na huyu jamaa (Dangote), hata Singida alikuwa akizunguka naye sehemu mbalimbali.

Ndiyo maana kuna picha kibao ambazo zinawaonesha wakiwa romantic kiasi kwamba wapo wanaokwenda mbali na kusema ni wapenzi, watu bwana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:

Unajua yule Kifyagio alikuwa rafiki wa Diomond sana huko nyuma, sasa isije ikawa kaamua kujiweka kwa shemeji yake maana si unawajua tena hawa mastaa wetu, nyie fuatilieni mtaujua ukweli.”

Baada ya gazeti hili kunasa ‘ubuyu’ huo pamoja na picha za Wema na jamaa huyo wakiwa kimahaba sehemu tofautitofauti, lilimvutia waya mrembo huyo na kumbana kuhusu uhusiano =wake na Dangote Kifyagio ambapo simu yake haikupokelewa.

Alipotumiwa ujumbe juu ya madai kuwa anatembea na jamaa huyo alijibu kwa hasira kama ifuatavyo:
“Halafu sikia nikwambie, vitu vingine ni upuuzi tu hivyo vitu vinaniharibia deal zangu na mipango yangu yote, sipendi hata kidogo, yaani sipendi kwanza kufuatiliwa, amekuwa mtu wangu?

 Nishawahi kumposti na kusema ni bwana’angu zaidi ya mimi na yeye kuheshimiana? Nina bwana wangu ambaye ndiye kila kitu kwangu jamani sipendi wallah…sipendi.”

Wema Sepetu Awavua Nguo Nuh Na Shilole..Baada ya Wao Kudai Sauti ya Nuhu Akimtongoza Wema si ya Nuhu Bali Wema Ametengeneza Kuwagombanisha

0
0
Lile sakata la mrembo Wema Sepetu kutakwa kimapenzi na mpenzi wa msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Nuh Mziwanda limeendelea kushika kasi ambapo Wema ameibuka na kuwavua nguo kwa kuwatolea maneno ya shombo.

Wema alitoa maneno hayo hivi karibuni baada ya Shilole na Nuh kumgeuka na kusema kwamba aliwachezea mchezo mchafu ili kuwagombanisha kwa sababu anawaona wanapendana hivyo alimtafuta mtu ambaye anaendana na sauti ya Nuh ili tu amharibie.

“Sijui kwa nini Wema kanifanyia hivi najua anataka tu kunigombanisha na mpenzi wangu kwa sababu hata ukisikiliza hiyo rekodi utasikia sauti ya Mirror akizungumza, hapo ndiyo ujue kuna mchezo mchafu sana na kwa hilo amefanikiwa lakini sisi huku mapenzi yetu yanaendelea,” alisema Nuh.

Kutokana na maneno hayo Wema alicharuka na kusema kwamba hawezi kutoa rekodi ya uongo na kumsingizia Nuh kwani ni mpuuzi na hawezi kujilinganisha naye kutokana na kwamba ni staa mkubwa.

“Nuh alinipigia na kunitaka kimapenzi ndipo nikaamua kumrekodi na hiyo ni sauti yake haijatengenezwa kama wao wanavyodai, kwanza nawashangaa hivi ningetengeneza sauti feki ili iweje, Nuh na Shilole siyo levo yangu ni wasanii wachanga sana, mimi ni staa mkubwa Tanzania na hakuna wa kulinganishwa na mimi labda nje ya Bongo.

"Nitafute kiki kwa kina Shilole  na Nuh kweli? Si bora nitengeneze kiki kwa kina Davido na wasanii wengine wakubwa duniani, hao si levo yangu jamani,” alisema Wema kwa sauti ya hasira.

Kabla ya kupatana, Nuh na Shilole waligombana hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni baada ya mrembo huyo kupokea sauti hiyo iliyosikika Nuh akimtongoza Wema.

Mamia ya Wanachama Wamiminika Ofisi za Chadema ‘KUMLAKI’ Dk Slaa

0
0
Mamia  ya wanachama na mashabiki wa Chadema jana walifika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni Dar es Salaam kumsubiri Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa baada ya kuenea  habari kuwa angeingia ofisini.

Hata  hivyo,wanachama hao waliokuwa na shauku ya kumwona kiongozi huyo, hawakufanikiwa baada ya kuambiwa kuwa Dk Slaa asingefika katika ofisi hizo kinyume na taarifa zilizokuwa zimetolewa kuhusu kurejea kwake.

Juzi mzee Philemon Ndesamburo na makada wengine wa chama walikwenda nyumbani kwa Dk. Slaa kwa ajili ya mazungumzo, na kwamba alikubali akasema angerejea ofisini jana

Kwa muda mrefu Dk Slaa hakuonekana kwenye matukio muhimu ya Chadema na yale ya Ukawa, kama wakati wa kumkaribisha Edward Lowassa ndani ya chama hicho, wakati Lowassa alipochukua kadi na alipochukua fomu ya kuwania urais.

Kadhalika kiongozi huyo hakuonekana katika Baraza Kuu la Chadema, mkutano wa Kamati Kuu na Mkutano Mkuu uliompitisha kwa kauli moja kuwa Lowassa aipeperushe bendera ya urais chini ya mwamvuli wa Ukawa.

Akihutubia Baraza Kuu la chama hicho wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa chama kiliridhia Dk Slaa apumzike wakati mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ukiendelea baada ya Katibu Mkuu huyo kutofautiana katika uamuzi wa kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Baraza Kuu lilipiga kura ya wazi na kushauri kuwa endapo atafikiria kubadili uamuzi wake, anaweza kuendelea na harakati za chama hicho kuelekea Ikulu chini ya muungano wa Ukawa.

Mwandishi wetu aliyefika katika ofisi za Chadema zilizopo katika Mtaa wa Ufipa, Wilaya ya Kinondoni, alishuhudia idadi kubwa ya wanachama wakiwa wamekusanyika katika vikundi wakijadili masuala mbalimbali huku wakimsubiri Dk Slaa.

“Nimesikia taarifa kuwa kuna watu hapa wanamsubiri Dk Slaa nikaja kushuhudia, watu wanaongea mambo mengi kama vile Ukawa imevunjika wakati kila kitu kinakwenda sawa hapa,” alisema Ali Mundu mmoja wa wananchama hao.

Zitto Kabwe Asema Magufuli ni FISADI.......Awaponda UKAWA Kumteua Lowassa Kuwa Mgombea Urais Kwa Kuwa naye ni FISADI

0
0
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli  si msafi katika utendaji kazi wake kama inavyoelezwa kwa Watanzania.

Moja ya kigezo kinachotumiwa na Zitto ni madai ya ‘kukwapuliwa’ kwa Sh. bilioni 87 za Wizara ya Ujenzi anayoongoza.

Alisema fedha hizo ni sehemu ya Sh. bilioni 252 za miradi ya umeme, barabara na miradi maalumu zilizokosa maelezo yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali aliyowahi kuiongoza akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Zitto alisema kukosekana kwa fedha hizo ni kiashiria cha kuwapo matumizi mabaya katika wizara iliyoongozwa na Magufuli.

Awaponda  UKAWA.
Zitto alivibeza vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa vimepoteza dira baada ya kumpokea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kutoka CCM na kumteua kuwa mgombea urais wao.

Alisema Zitto alipinga hoja iliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wa Ukawa kuhusu ufisadi kuwa ni mfumo na si mtu binafsi.

Zitto alisema ACT-Wazalendo inalenga kujenga siasa mpya nchini zinazojielekeza katika utii wa maadili na kiongozi wa umma kutangaza mali zake hadharani.

Alitoa wito kwa wapiga kura kuwachagua wagombea wa chama hicho kwa madai kuwa vyama vinavyounda Ukawa vina taswira isiyotofautiana na CCM.

Naye Mweyekiti wa chama hicho, Anna Mughwira, alisema chama chake kitakapompitisha rasmi kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Singida Mjini, ataelezea namna atakavyofanikisha kuleta mabadiliko na kuharakisha maendeleo.

“Singida iliachwa nyuma kwa maendeleo tangu enzi ya mkoloni…sasa ni lazima tubadilike ili tupate maendeleo,” alisema.

Maalim Seif Amlipua Profesa Lipumba........Asema Wanachama Waliojiunga CUF Kwa Sababu ya Lipumba Wanaweza KUONDOKA Pia

0
0
Wafuasi  wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na pia mwenyekiti mwenza wa muungano wa wapinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba, wameanza kushughulikiwa na kutakiwa kuchagua moja; kuendelea kuwa ndani ya chama hicho au kutoka.

Ingawa Profesa Lipumba alipojiuzulu uenyekiti, alisema ataendelea kuwa mwanachama wa CUF, lakini Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wanachama waliokuwa wakimuunga mkono, kuamua moja, kubaki ndani ya chama hicho kama alivyoamua mchumi huyo mashuhuri duniani, au kutoka.

“Profesa Lipumba kajiuzulu CUF, wale waliojiunga CUF kwa sababu ya Profesa, wanayo fursa ya kuamua kubaki CUF au kutoka,” alisema Hamad juzi usiku.

Mbali na kuwataka wanaomuunga mkono Profesa Lipumba kuamua kutoka ndani ya chama hicho au kubaki, wakati kiongozi wao akiwa ameweka wazi kuwa hana nia ya kutoka katika chama hicho, Maalim Seif alitoa kauli zingine kuashiria kutohitaji hata uanachama wa Lipumba ndani ya CUF.

“Kama ni treni inayokwenda Mwanza, ikifika Morogoro abiria watashuka, lakini wengine watapanda, ikifika Kaliua watashuka abiria lakini wengine watapanda,” alisema Maalim Seif alipofanya ziara ya ghafla katika Makao Makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam juzi usiku.

Hamad amewahakikishia wanachama wa chama hicho waliokuwa wamezingira ofisi hiyo, kuwa uamuzi wa Profesa Lipumba kujiuzulu wadhifa wake hautausambaratisha Ukawa na CUF, ambayo kwa sasa haina Mwenyekiti wala Makamu Mwenyekiti, lakini akasema imeendelea kubaki katika mikono salama.

Alisema akiwa Katibu Mkuu na viongozi wenzake waliobaki, watahakikisha kwamba chama hicho kinafikia malengo ya kuanzishwa kwake, ambayo ni kuhakikisha kinakamata dola.

Alisema mwishoni mwa wiki hii, chama hicho kitaanza vikao vyake kuzingatia hatua iliyotokea, ili wachukue uamuzi thabiti wa kukiongoza chama hicho na kuhakikisha kinabaki katika mikono salama, hadi hapo uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti utakapofanyika.

Akizungumzia Ukawa, Hamad alisema baada ya hatua hiyo ya Profesa Lipumba, alizungumza na viongozi wakuu wa umoja huo, akiwemo Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema), James Mbatia (Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) na Emmanuel Makaidi (Mwenyekiti wa NLD) pamoja na mgombea urais wa umoja huo, Edward Lowassa na wamehakikishiana kuwa hawatarudi nyuma.

“Tumehakikishiana kwamba Ukawa upo na umeimarika zaidi na hatutarudi nyuma… Tumeona kwa namna unavyoungwa mkono na wananchi walio wengi, Magufuli (mgombea urais wa CCM) Ikulu ya Magogoni hataiona,” alidai Maalim Seif.

Hatuwezi Kuiondoa CCM Madarakani kwa wimbo wa Ufisadi, Tunahitaji watu Wenye Ushawishi

0
0
Ingekuwa ufisadi ni jambo linalowakera sana watanzania,upinzani usingekuwa na hata haja ya kufanya campaign kuiondoa CCM madarakani bali ufisadi uliofanyika katika awamu hii ya Kikwete, ulikuwa unatosha kabisa kuiondoa CCM madarakani mwaka huu.

Watanzania wangekuwa wanakerwa na ufisadi wa viongozi mithili ya wizi unaofanywa na kibaka wa kuku au simu,CCM wengeshaondoka madarakani tangu mwaka 2010.

Watanzania wako radhi waongozwe na mafisadi kuliko kuwapa nchi wapinzani kwa kwa imani potufu kuwa;

1.Upinzani hauna watu wa kutosha kuongoza hii nchi

2.Viongozi wa upinzani hawajawahi kushika dola(kuwa mawaziri n.k) hivyo hawana uzoefu wa kuongoza nchi

3.Watanzania wengi wana imani ya kijinga kuwa ni bora hawa mafisdi wa leo wakaendekea kubaki madarakani kuliko kuwapa uongozi wa nchi watu ambao wakiingia madarakani ndio kwaanza watakuwa wanaanza kujijenga hivyo wataiba zaidi kuliko hata hawa mafisadi wa CCM.

4.Bado kuna wajinga wachache wanaamini CCM ikitoka madarakani,basi amani(ukweli ni utulivu na wala si amani) itatoweka.

Hizo ndio fikra,japo ya kijinga,lakini dio zinawaongoza watanzania wengi wakiwamo wasomi wenye shahada na mashahada-kubali au ukatae huu ndio ukweli ingawa ni wa kusikitisha.

Hivyo basi,hata angesimama Dr.Slaa au Lipumba kupitia UKAWA, bado tungekuwa na wakati mgumu wa kuiondoa CCM madarakani licha ya ukweli kuwa CCM imechoka na haistahili kuendelea kuwepo madarakani.

Kwasababu hizo nne nilizotaja hapa juu, ndio maana binafsi naunga mkono ujio wa Lowassa na wana-CCM wengine ndani ya UKAWA kwani kuwepo kwao kuna punguza hofu au kwa maneno mengine kunasaidia kutoa suluhisho kwa maswala hayo manne hasa ikizingatiwa kuwa Lowassa alishawahi kuwa wazi mkuu.

Matumaini pekee ni kuwa hizo sababu nne zinaenda zikitokomea au kukosa nguvu kadri mika inavyosonga mbele ila bado tuhahitaji miaka mingine 10 kuondokana na hizi fikra potufu miongoni mwa watanzania hasa kwenye nafasi ya uraisi na kwa mawaziri wa kuongoza wizara.

Tukitaka mabadiliko ya haraka kabla ya muda huo wa hiyo miaka 10 na kuendelea kwa nafasi ya uraisi,hatuna budi kuwa-accomodate wana CCM wenye ushawishi wanaojitoa katika chama chao na zaidi tuwape nafasi katika vyama vyetu hivi vya upinzani.


Ushahidi mdogo tu kuwa kwa watanzania ufisadi kwa sio "big deal",ni kupeta katika kura za maoni za hivi karibuni kwa watuhumiwa wa Escrow na mtakuja kushangaa watu kama Chenge,Karamagi,Ngeleja wanarudi Bungeni tena kwa kura nyingi tu.

Tusijidanganye tukambeza Lowassa kuwa ni fisadi na hatoweza kutuletea ushindi kisa tu anatuhumiwa kwa ufisadi wakati watanzania ufisadi kwao sio big deal unless tunataka kuwa wapinzani wa kudumu.

Thruogh Lowassa I believe we can make those politics that seem impossible in our country to be possible at least for the first in our countrty political history.

Video: Tazama Trailer Mpya ya Empire Season 2

0
0
Msimu wa pili wa tamthilia ya Empire unatarajiwa kuanza kuoneshwa Jumatano ya September 13. Tofauti na msimu wa kwanza uliokuwa na episode 12, msimu mpya utakuwa nazo 18. Tazama trailer yake hapo chini.

Lowassa Kuchukua Fomu za Urais Katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jumatatu Saa tatu Kamili Asubuhi.

0
0
Chama  cha  Demokrasia  na  Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa kuhusu utaratibu wa Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa kuchukua Fomu za  Urais  katika  ofisi  za  Tume  ya  Taifa ya  Uchaguzi.

Akitoa  taarifa  hizo  mbele  ya  waandishi  wa  habari  leo  mchana, Naibu Katibu  Mkuu  wa  Chadema, ndg  Salum  Mwalimu  ambaye  kwa  sasa  anakaimu  nafasi  ya  Katibu  Mkuu  wa  Chadema  amesema  Mh. Lowassa  atachukua  fomu  hizo  Jumatatu  ya  tarehe 10, Agosti  2015, saa  tatu  kamili  asubuhi.

Mwalimu  amesema  msafara  wa  Lowassa  utaanzia  katika  ofisi  za  CUF  zilizopo  Buguruni  ambapo  utaelekea  ofisi  za  Tume  ya  Uchaguzi  kwa  ajili  ya  Kuchukua  fomu.

Baada  ya  zoezi  la  kuchukua  fomu, msafara  huo  utaelekea  makao  makuu  ya  CHADEMA  Yaliyoko  Kinondoni  ambapo  kutakuwa  na  shamrashamra  kidogo.

Hapa  kuna  sentensi 14  ambazo  mwalimu  amezitamka  wakati  akiongea  na  waandishi  wa  habari.

1.Tupo ktk Kipindi cha Uchaguzi na Wagombea Urais wa Z'bar na TZ Bara tayari tumewatangaza'-

2.Tarehe 10 Mgombea Urais wa TZ ataongozana na Mgombea mwenza wake kwenda kuchukua Fomu NEC.

3.Mh. LOWASSA atasindikizwa na Viongozi Mbalimbali wakubwa wa Vyama vinavyounda Umoja wa UKAWA.

4.Zoezi la Uchukuaji wa Fomu msafara utaanzia Ofisi za CUF Buguruni kuelekea Tume ya Uchaguzi.

5.Msafara utaishia Ofisi za CHADEMA K'ndoni ambapo kutakuwa na shamrashamra kidogo.

6.Mh. LOWASSA atazunguka Mikoani kutafuta wadhamini, Watz wana hamu kumuona LOWASSA akiwa na combat ya CDM.

7.Mtaniwia radhi kwamba hatoweza kuzunguka nchi nzima, tutatangaza maeneo ambayo atapita.

8.Baada ya Uzinduzi wa Kampeni Dar, LOWASSA atapita Majimbo yote kama alivyoahidi.

9.LOWASSA Tarehe 13 atashiriki na Viongozi wengine kwenye Mazishi ya Mzee KISUMO Mkoa wa K'njaro.

10.Hatuwezi kuwazuia watu wanaotaka kumsindikiza LOWASSA kuchukua Fomu Ofisi za NEC.

11.Kazi ya kugawanya Majimbo ya Ubunge imekamilika, kazi imekamilika salama na kwa amani.

12.Kuna jambo linaendelea watu wanaambiwa wakusanye Kadi zao za Kupigia Kura.

13.Yoyote anayeambiwa atoe kadi au atoe namba ya Kadi yake ya Kupigia Kura akatae.

14.UKAWA haijayumba kwa namna yoyote kwa kuondoka kwa Prof. LIPUMBA, tunasonga mbele.

MAONI: Nani Anaandikaga ‘Subtitles’ za Movies za Bongo?

0
0
Mwenzenu sikuwahi kuwa na mazoea ya kuangalia movie zetu za hapa nyumbani kwa maana mara nyingi huwa actors wana overdo hadi nikawa naboreka. sasa last weekend kwa kufuata ushabiki wa watoto nikakaa kuangalia, kwa kweli nilikuwa shocked na nikawa nashindwa kuelewa. Kwani ni nani anayewaandikia zile subtitles za kiingereza, halafu it seems ni myu mmoja ndiye huwa anapelekewa kwa jinsi zilivyo.

Ni aibu jamani, kama bado hamjafikia level hiyo ya lugha, acheni tu, wekezeni zaidi kwenye kiswahili basi ieleweke tu kwamba movie ni ya kiswahili. Au kama mnataka mpate soko la kimataifa, hebu mu-invest sana mpate professionals wanaoweza kuwaandikia lugha ya kueleweka, otherwise mnajiabisha na kuiabisha nchi hii, can you imagine unaeangalia movie ndo unaona aibu kwa niaba yao. Maana ile lugha inayoandikwa pale si english, bali direct translation from kiswahili inaishia kuwa pigini, au mnajaribu kutengeneza lugha ingine? Mi sijaelewa jamani.

Kama vipi muwe mnaniletea japo nina uelewa mdogo wa hii lugha naamini i can do better than that. Ni ushauri tu, najua kina Kanumba sijui Ray huwa mnapita humu, next time kwenye baraza lenu la wasanii hebu wekeni hii kama agenda, naamini wapo watu kibao ambao hata kwa kuvolunteer wanaweza ku edit na kusaidia kutoa lugha inayoeleweka.

By Carmel on Jamiiforums

Mtoto wa Zari Amliza Mwanamuziki Diamond Platnumz

0
0
HII ni kali! Muda mchache baada ya mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kujifungua salama, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejifungia chemba kisha kuangua kilio akisema Mungu ni mwema huku akiwataja waliowahi kuwa wapenzi wake, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Jokate Mwegelo kwa maneno yao ya shombo.

TUJIUNGE AGA KHAN
Tukio la kujifungua mchumba wa Diamond, Zari lilijiri Agosti 6, mwaka huu mishale ya saa 10:40 alfajiri katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar  ambapo alipelekwa usiku huo baada ya kujisikia uchungu ambapo alijifungua mtoto huyo wa kike.
Chanzo cha habari kilieleza kwamba, siku hiyo, wakiwa hospitalini hapo, muda mfupi tu baada ya Diamond kuambiwa kuwa tayari Zari amejifungua, jamaa huyo alilipuka kwa shangwe na baadaye akajifungia chemba na kuanza kulia.

Kilipenyeza kuwa baadhi ya watu walioshuhudia walijiuliza kisa cha kulia ambapo baadaye alisema kuwa watu walikuwa wamemsema mengi juu yake na ishu kupata mtoto.
AANGUA KILIO
“Diamond alijikuta akiangua kilio, suala ambalo mwenyewe lilianza kunitia hofu maana kabla hajaanza kulia alikuwa akichekelea na hatukujua aliingiwa na nini hadi akaanza kulia huku akimshukuru Mungu kwa kumletea mtoto.
“Ila nilipomuuliza zaidi kinachomliza alisema kuwa amejikuta akifurahia hadi kulia kwani kabla Zari hajajifungua, alikuwa akiwaza sana kutokana na maneno ya watu ambao wengine walikuwa wakimwandikia meseji na kumtishia kuwa hawezi kuzaa salama,” kilitiririka chanzo hicho na kuongeza:

“Eti alisema kwamba, kuna siku alikuwa hapati kabisa usingizi kufuatia ishu ya kutopata mtoto hasa anapowaza maneno ya watu na mara nyingine alipokuwa akikumbuka maneno ya Penny na Jokate ambao walikuwa wakisema hana kizazi hivyo Mungu alikuwa amewajibu bila kinyongo yote waliyokuwa wakimuombea mabaya.

HUYU HAPA DIAMOND
Baada ya kupenyezewa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilimtafuta Diamond ili kumdadisi zaidi juu ya kilio hicho ambapo alipopatikana alisema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kutimiza ndoto yake na kwamba sasa milango ya heri imefunguliwa hivyo hana sababu ya kueleza machungu yote aliyokuwa nayo zaidi ya kumshukuru  Mungu kwa kuwa yeye ndiye mweza wa yote.
“Siwezi kuweka wazi hilo ila kikubwa ninachoweza kusema kwa sasa namshukuru Mungu kwa kunianzishia historia mpya hivyo namuomba aendelee kumlinda mke wangu na familia yangu,” alisema Diamond.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, bado Zari alikuwa hospitalini huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akimhudumia mtori huku mtoto huyo akipewa jina la Latifah a.k.a Princes Tifah au Queen Latifah.
GPL

Is this Right or insanity? Couple Making Lov3 In Front of Their Daughter

0
0
This is absolutely WRONG! Nothing can justify this abuse, When this lady went to visit her boyfriend she took her daughter with her, she couldn’t simply leave the child with someone knowing very well the guy live’s in a single room

Not only did they make lóv3 in front of the child, the guy also recórded the whole thing and later on sent it to his friends. This cóuple needs to be sued for child abuse… the world has finally lost it!

Kwa Maoni yako, Hili Ndio Penzi la Kweli au Uzoba?

0
0
Unasemaje kuhusu Mwanaume Kupiga magoti mbele za watu kama kwenye hiyo picha nakuomba msamaha kwa mpenzi wake? 
Je ni Uzoba ama Mapenzi ya Kweli ?
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images