Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Huu Ndio Mpango wa Ex wa Zari na Mpambe Wake wa Kutaka Kuharibu Furaha ya Ujio wa Tiffah Kwa Diamond na Zari

$
0
0
Ulimwengu una maajabu mengi na mitandao ya kijamii inatusaidia kuyafahamu. Uhusiano wa Diamond na Zari the Bosslady haujawahi kupokelewa vizuri na ex wake Ivan aliyezaa naye watoto watatu wa kiume.

Watoto hao wameendelea kuwa karibu na wazazi wote wawili. Uhusiano wa ulipoanza tu, Ivan kupitia mpambe na rafiki yake wa karibu, King Lawrenc walianzisha vita kwenye mitandao ya kijamii kuwashambulia Diamond na Zari. Hakuna shaka kuwa Ivan amekuwa akionesha hisia zake za kutoupenda uhusiano wao kupitia Lawrenc ambaye amekuwa akiwashambulia mfululizo.

Katika kipindi ambacho tension kati ya Diamond na Alikiba zimefika kileleni hususan kipindi cha kuelekea tuzo za KTMA 2015, Ivan mwenyewe pia alishiriki katika kampeni za kumuombea kura Alikiba. Ni wazi kuwa Ivan bado hajakubali yaishe, na kumuona mke wake wa zamani akiwa na furaha na Diamond ni kitu kinachomkera zaidi.

Na sasa wakati uhusiano wa Diamond na Zari upo katika kilele cha furaha baada ya kujaaliwa mtoto wa kike, Latiffah, kambi ya Ivan kupitia mpambe wake Lawrenc imedhamiria kuitilia doa furaha hiyo.

King Lawrenc ameanza kutupa mashambulizi kwa Diamond na kueleza kile anachoamini kuwa Tiffah ni mtoto wa Ivan! Kwa historia ya kile Lawrenc amekuwa akikisema tangu mastaa hao waanzishe uhusiano, ni wachache wanaoweza kuamini ‘upuuzi’ huu lakini kiukweli hiki ni kitu kinachoweza kuwakosesha raha Diamond na Zari, kama wakiamua kumjali.

Lawrenc alianza kupost picha ya mtoto mchanga na picha ya Ivan na kuandika, “No DNA Needed. The best revenge has shown itself after 9months. Anamaanisha kuwa mtoto huyo ni Tiffah na kwamba Ivan ndio baba yake.

Hadi sasa hakuna picha iliyotolewa inayoonesha sura halisi ya Tiffah hivyo ni ujinga kuamini kuwa aliyoweka Lawrenc ni yake. Na katika yote yanayoondolea, Zari na Diamond hawawezi kuruhusu picha ya mtoto wao ifike kwenye mikono ya adui yao labda kama wao wenyewe wakiamua kuipost kwenye mitandao ya kijamii, kitu ambacho bado hawajakifanya hadi sasa.

Na pengine mambo kama haya ndio yanamfanya mama mzazi asite kuionesha sura ya binti yake huyo. “I swear I wanted to show you her face but she turned away saying, nope i want no drama. She knows y’all can be dramatic. She’d rather stay safe for now… too many judges, advisors, teachers you name it you’ll find it on IG. I bet she can’t deal,” aliandika Zari.

Mafuriko ya LOWASSA Yatanda Kila Kona ya Nchi.....Wanachama Maarufu wa CCM Wahamia UKAWA

$
0
0
KAMBI kuu ya upinzani katika siasa za Tanzania, imezidi kuimarika. Matukio mawili, moja la jana, jingine leo hii, yametokea na kuongeza nguvu ya kampeni ya kuitoa CCM madarakani chini ya kaulimbiu ya “Toroka uje.”

Katika tukio la kwanza jana jioni, kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ilimpokea Omari Ayubu Kimbau, kada machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akihamia Chama cha Wananchi (CUF) anakotarajia kupewa dhamana ya kugombea ubunge jimboni Mafia, Mkoa wa Pwani.

Kimbau ni mmoja wa watoto wa Kanali Ayubu Shomari Mohamed Kimbau, mwanasiasa mstaafu aliyekuwa mbunge wa muda mrefu wilayani Mafia.

Uamuzi wa Kimbau kuhama CCM umefanikishwa mara tu alipobaini kudhulumiwa kisiasa kulikotimia juzi kwa kutupwa nje ya mbio za uteuzi ka mara ya pili mfululizo, ili kugombea ubunge.

Tayari mipango ya kumkabidhisha bendera ya kugombea kiti hicho kupitia CUF, inakamilishwa na taarifa za ndani ya CUF zinasema atatambulishwa rasmi jimboni Jumatano wiki ijayo.

Kimbau amekosa uteuzi katika vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC-CCM) vilivyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, ambako ugombeaji alipewa Mbaraka Dau, ndugu wa damu wa Dk. Ramadhan Dau, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Katika kura za maoni zilizohusisha matawi ya CCM jimboni, Kimbau alipata kura 1,480 huku Dau anayeishi Dubai, kwa shughuli za biashara, akipata kura 2,620. Injinia Omari Kipanga alipata kura 1,156; Shah 568 na Njalale 23.

Jimbo la Mafia ambalo Abdulkarim Shah (Bulji) ameliwakilisha vipindi viwili, kwa makubaliano ya UKAWA, limeachwa ligombewe na mwakilishi atokaye CUF, chama chenye historia ya kuwa ngome kwa CCM wilayani Mafia.

Wachambuzi wa siasa za Mafia, wanasema Kimbau ameingia kambi ya UKAWA akiwa na mtaji wa zaidi ya wanachama 6,900 waliohakikiwa kujiunga Chadema kufikia sasa; CUF zaidi ya 6,000; watu 1,480 waliompigia kura za maoni CCM.

Tukio la pili ni la jijini Arusha ambako mgombea urais anayewakilisha UKAWA, Edward Lowassa, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara wa kutambulishwa na kupata wadhamini, ametinga kambini Lawrance Masha.

Masha, waziri wa mambo ya ndani kwa awamu ya kwanza ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete (Novemba 2005/2010), alipigwa kumbo katika uchaguzi mkuu uliopita, jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza analowakilisha Ezekiel Wenje.

“Maamuzi magumu yamefanyika hivi leo, lakini ni maamuzi muhimu sitaongea leo. Nitangaze tu kwamba nimejiunga rasmi Chadema,” amewaambia wana-UKAWA waliojazana viwanja vya Tindigani.

 Masha ni mtoto wa Dk. Fortunatus Masha, aliyestaafu siasa akiwa Chama cha United Democratic Party (UDP) alikofikia ngazi ya makamu mwenyekiti.

Amehama CCM siku chache baada ya kuthibitisha kutupwa na CCM katika uteuzi kutokana na kushindwa kura za maoni safari hii akiwinda jimbo la Sengerema.

Baada ya mkutano wa Arusha, Lowassa, ambaye alihama CCM tarehe 28 Julai akijibu pigo la kukatwa jina katika walioomba uteuzi wa kugombea urais, akiwa miongoni mwa waombaji 38, atakuwa jijini Mwanza kesho Jumapili.

Mtoto wa OSAMA BIN LADEN Aibuka..Atoa Ujumbe Mzito Kwa Marekani...Aagiza Mashambulizi

$
0
0
Kundi la kigaidi la A Qaeda limetoa ujumbe wa sauti ambao unadai kwamba umetoka kwa Hamza Bin Laden ,mwana wa Osama Bin Laden.

Ujumbe huo unaaminika kuwa wa kwanza wa propaganda za Al Qaeda kumshirikisha Hamza Bin Laden kama mwanachama wa kundi hilo.

Katika ujumbe huo uliosambazwa na Al Qaeda katika mtandao wa twitter,Hamza Bin Laden anaagiza mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake.

Osama bin Laden aliuawa na vikosi maalum vya Marekani mnamo mwaka 2011 katika uvamizi nyumbani kwake huko Abbotabad,Pakistan.

Nilipoona Picha Sikuyaelewa Vizuri Mafuriko ya Mbeya... Lakini Baada ya Kuona Hii Video ndo Nimekubali Kweli Yalivunja Rekodi

$
0
0
Nilipoona Picha sikuyaelewa Vizuri Mafuriko ya Mbeya... Lakini baada ya kuona hii Video ndo nimekubali kweli yalivunja rekodi

Tazama Mwenyewe Video:

Rais J.Kikwete Kumjibu Lowassa Kwenye Shughuli za Kiserekali ni Sahihi..Au Amepaniki?

$
0
0
Ipi mipaka yake anapokuwa kwenye shughuli za kiserikali? Ni sawa kuitupia madongo upinzani wakati akiwa kwenye shughuli za kiserikali? Kwa nini asisubiri ajibu akiwa kwenye shughuli za chama?Je,huku ni kupaniki?

Ilikuwa ni siku ya jana, katika viwanja vya mnazi mmoja katika tukio la Wizara ya Ujenzi na wakandarasi wakimuaga Kikwete kwa kumaliza muda wake wa miaka kumi wa kuongoza nchi. Na hapo Kikwete akaanza kumsifia Magufuli kiCCM kiCCM na kwa woga, aibu na kujihami kabisa akasema kimafumbo kuwa MAFURIKO YA LOWASSA yanayoendelea kuitikisa nchi kwa sasa ni MOTO WA MABUA TU, hautadumu hata kidogo.

Mbowe na Lowassa Yawezekana Wakawa Tatizo CHADEMA

$
0
0
Watanzania huenda wakijua biashara ya Mbowe na Lowassa watajiona wanavyo fanywa wajinga. Na zaidi wanachama wa CHADEMA, Mbowe sasa ni Mungu mtu ndani ya chama kiasi cha kuwanyima haki ya kuwachaguwa wabunge wanao wahitaji katika majimbo yao. Wakati majimbo ya Kaskazini akigawana na marafiki zake. Nchi inaingia matatani akifikiri nchi inaongozwa na mashairi yake jukwaani.

Maoni Binafsi Kutoka Kwa Bwana Haki

Msafara wa Lowassa Ulivyopigwa MABOMU Na Polisi Jana jijini Arusha

$
0
0
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana kwa mara ya kwanza alikumbana na joto la upinzani baada ya msafara wake kushambuliwa na mabomu ya polisi.

Tukio hilo, ambalo lilifanyika mbele ya msafara wa Lowassa, lilitokea jana eneo la Daraja la Nduruma katika Jiji la Arusha na kusababisha umati wa watu kutawanyika na wengine kutelekeza magari yao.

Wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkaribisha kwenye chama hicho wakati wa mkutano mkuu alimwambia; “Mzee huku inabidi uwe unafanya mazoezi kidogo, kuna mabomu huku.”

Lowassa alikumbwa na kadhia hiyo, akiwa njiani na mgombea mwenza, Juma Duni Haji na viongozi wengine wa Ukawa, wakitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), huku wakiwa wamesindikizwa na umati wa watu na magari.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema kuwa polisi walilazimika kupiga mabomu ya machozi ili kutawanya watu waliokuwa wakiwarushia mawe polisi na wengine kufunga barabara.

“Kwa hali ile, tungefanya nini? Wanatupa mawe kwa polisi na wamefunga barabara na kuzuia magari mengine yasipite…ikumbukwe kulikuwa hakuna kibali cha maandamano na hata kingekuja, matamko ya kuzuia maandamano yameshatolewa,” alisema Sabas.

Katika tukio hilo, idadi kubwa ya polisi walikuwa kwenye magari na silaha mbalimbali ambao baadaye walianza kurusha mabomu kutawanya watu na magari kwa eneo la daraja hilo.

Hata hivyo, katika tukio hilo, lililotokea saa nane mchana hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa na kutokana na nguvu hiyo ya polisi watu walitawanyika, na barabara hiyo ya Arusha- Moshi ilifunguka baada ya kutopitika kwa saa tano kuanzia saa nne asubuhi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Tindigani, Mbunge wa jimbo la Arusha, Godbless Lema alisema wamesikitishwa na kitendo cha polisi kumpiga mabomu Lowassa na msafara wake.

“Tunajua polisi wamepata maelekezo na sasa wanataka kuwatisha wananchi, lakini tunasema leo ndiyo mwisho hatutakubali tena kunyanyaswa,” alisema Lema.

Akihutubia mkutano huo Lowassa alitahadharisha viongozi wa polisi, kuacha kutumia nguvu kupita kiasi, kwani anaweza kuwafikisha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iliyopo The Hague nchini Uholanzi.

Lowassa alisema alikuwa akiiamini polisi, lakini alichokiona jana cha kupigwa mabomu ni jambo baya.

Kuhusu suala la Babu Seya aliyefungwa kifungo cha maisha gerezani alisema atafuatiliwa kwa kutumia suala la utawala bora kwa kuangalia vyombo vya sheria na hatua zingine zitafuatwa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wanachama wanaojiunga sasa wana haki sawa na mwasisi wa chama hiki Edwin Mtei mwenye kadi namba moja.

Alisema mara baada ya wanachama wapya kujiunga, kwa kipindi cha wiki moja nilipokea matusi mengi kuliko niliyowahi kutukanwa baada ya kupokea wanachama wapya.

Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Taslima alisema kuna watu ambao wamejenga desturi ya kuwabeza watu wanapohama vyama kwa hiari kwa kuwaita oili chafu au makapi anavunja Katiba.

Alisema Ibara ya 20 ya Katiba ya mwaka 1977 inasema kila mtu yeyote ambaye ni Mtanzania, yuko huru kujiunga na mtu yeyote, chombo chochote, taasisi yoyote atakayopenda na hatazuiliwa.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema; “Mabomu yamepigwa katika mkutano wa Chadema, watu wakafa Arusha, Arusha tunayoitegemea kwa uchumi leo hii zaidi ya asilimia 19 ya pato ya taifa linatokana na utalii, lakini leo (jana) tunaingia Arusha alipozaliwa Lowassa tunapigwa mabomu, ukweli utatuweka huru.

Breaking News: Polisi Watumia Mabomu ya Machoz Mwanza Kuwatawanya wafuasi wa Lowassa

$
0
0
Muda  huu  polisi  wanapiga mabomu  uwanja  wa  ndege   jijini  Mwanza kuwatawanya  wananchi  waliokusanyika  kumpokea  Lowassa.

Mabomu  yamepigwa  muda  mfupi  baada  ya  ndege  inayosadikiwa  kuwa  ni  ya  Lowassa  kutua  uwanjan, hali  iliyowafanya  wananchi  walipuke  kwa  furaha  huku  wakiimba  nyimbo  za  Chadema.

Kadhia  hiyo  iliwafanya  Polisi  watumie nguvu  ya  ziada  kuwatawanya  wananchi hao  waliokuwa  wametanda  barabarani.

Breaking News..Kingunge Ngombale Mwiru Avuliwa Ukamanda wa UVCCM Taifa..Atoa Mazito

$
0
0
Kikao cha baraza kuu uvccm kinachoendelea hivi sasa katika ukumbi wa mwalimu J. Nyerere dar es saalamu chini ya mwenyekiti wake Sadifa J. khamis.
kimemuenguwa na kumfukuza KAMANDA wao wa taifa nd KINGUNGE NGOMBALU MWILU.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya baraza kuu kujadili na kutathimini mwenendo wa kamanda huyo hasa kipindi hichi cha mapambano.

kikao hicho cha baraza kimefikia maamuzi hayo baada ya kuamini kuwa kamanda huyo kwa sasa hataweza kuivusha jumuiya hiyo katika kupata ushindi wa kishindo oct 2015


Miaka 130 Jela Kwa Kosa la Kumuambukiza Mtoto wa Miaka 9 Ukimwi

$
0
0
Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela kwa kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 ukimwi.
Katika kikao hicho Mahakama kuu ya Kenya mjini Kisumu imempata na hatia bwana John Okewo mwenye umri wa miaka 25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limebanwa.

Hakimu mwandamizi Aswani Opande alimpata na hatia bwana Okewo kwa kumabaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo cha miaka 100 jela.
Katika shtaka la pili hakimu huyo mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni alimhukumu mstakiwa kifungo cha miaka mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa Ukimwi.

Hakimu alimpata na hatia bwana Okewo kutokana na kukiri makosa yake mwenyewe.
Upande wa mashtaka unasema kuwa bwana Okewo alimpa mtoto huyo pipi na biskuti mnamo tarehe 27 mwezi Machi kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake.
Yamkini Okewo aliwaambia wachunguzi kuwa alimdhulumu mtoto huyo mara kadha.

Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi biskuti na ''kumlalia''
Mtoto huyo alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi na ''kumlalia''
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.

Alipopewa fursa ajitetee, mshtakiwa aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo.

Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa kumuonea huruma na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake.
Alipewa siku 14 kukata rufaa.

Jack Wolper Amkubali Lowassa, Ajiita Jaquline Wolper Lowassa.

$
0
0
Katika kile kinachoonekana kwamba ameridhika na mgombea Urais Tanzania, kupitia CHADEMA/UKAWA actress na mrembo kiwango Bongo Jaquline Massawe Wolper, amejinadi kura yake ya Urais Oktoba anaipeleka kwa mgombea huyo Edward Lowassa.

Kupitia Instagram Jack, anashare picha kadhaa za matukio yanayoendelea kwenye kambi ya UKAWA.

Katika ‘line’ nyingine, Wolper amewaacha midomo wazi followers wake zaidi ya laki 6 Instagram baada ya kutangaza kuanzia kipindi hiki ataitwa Jaquline Wolper Lowassa.

Breaking News:Sumaye Ang'atuka CCM Kuanzia Leo

$
0
0
Waziri mkuu wa zamani amejitioa CCM rasmi kuanzia Leo. Akizungumza na wanahabari kwenye
ukumbi wa Court yard jijini hapa anasema amechoshwa na democrasia uchwara ndani ya CCM.

Je Kuna Ukweli Kuwa Wafuasi wa Lowassa na CHADEMA, Hawajui Wanafuata Nini

$
0
0
Nimekutana na Hii Mahali eti ...Naomba niwaulize Kama kuna ukweli juu ya hii kauli hapa chini"

"Nimefikiria akili za hawa wafuasi wa huyu mtu aliekatwa nimegundua ni kama nyumbu tu wale wa serengeti ambao hufuata mkumbo tu bila hata kujua wanakwenda wapi na kwa nini wavuke mto sehemu ya hatari wakati sehemu salama ya kuvuka ipo"

Breaking News! YUSUF MANJI Akatwa UDIWANI MBAGALA!!!

$
0
0

YUSUF MANJI akatwa UDIWANI MBAGALA!!!
VURUGU kubwa zimetokea katika ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam baada ya Wanachama wa chama hicho, kupinga hatua ya uongozi wa CCM mkoani hapa kutengua ushindi wa kura ya maoni kwenye ngazi ya Udiwani kata ya Mbagala kuu aliopata Yusuf Manji, ushindi huo kupatiwa na aliyeshika nafasi ya pili katika ngazi hiyo Abubakari Athumani.Anaandika KAROLI VINSENT

Lowassa Avunja Rekodi ya Mapokezi Jijini Mwanza....CCM Mpo ?

$
0
0
 
Siku ya leo Mwanza ilikuwa ni noma zaidi ya noma yaani nimekuwekea picha Hapo juu ujionee mwenyewe mafuriko,,,,,,,,Hivi CCM mpo ? mbona simsikii magufunguo tena?
Lowassa Avunja Rekodi ya Mapokezi Jijini Mwanza....CCM Mpo ?

Good News..Mabasi ya Mwendo Kasi Dar es Salaam Kuanza Kazi Leo...Hizi Hapa Njia na Vituo yatakapo Pita....

$
0
0
Ninayo Good News imenifikia mtu wangu ambayo Watanzania wengi na wakazi wa Dar es salaam tulikua tukiisubiri kwa muda mrefu ni kuhusu kukamilika kwa mradi wa Mabasi yaendayo haraka ambayo zaidi ya mwaka na nusu yaliingia kwenye headlines za kuwa yatatoa huduma hizo.

Habari ikufikie kuwa Mabasi hayo rasmi yanaanza kazi leo Jumatatu kuanzia  saa 3 asubuhi nje ya kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo ambako kutafanyika uzinduzi wa kuanza huduma ya mpito kisha Wananchi wataruhusiwa kupanda mabasi hayo kutoka Ubungo kwenda Kimara na kutoka Kimara hadi Kivukoni Bure.

Kwa bara la Afrika,jiji la Dar es salaam litakua la pili kutekeleza mradi huu mtu wangu baada ya Afrika Kusini na litakua jiji la kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki,Kaskazini na Kati.

DeusiDedith Mutasingwa ambaye ni Afisa wa masuala ya fidia katika mradi wa mabasi haya yaendayo haraka yaliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa,amesema yapo mabasi ya aina mbili kuna yale ya mita 18 ambayo yana uwezo wa kubeba abiria 140 na yapo yenye uwezo wa kubeba watu 80.

Amesema mabasi hayo pia yamezingatia watu wenye mahitaji maalum kama Walemavu na Wajawazito,pia Wafanyabiashara wanaopanga vitu vyao pembeni ya Barabara na kwenye vituo wameombwa kuviondoa na kwa wale watakaonekana kukaidi amri hiyo faini yake si chini 250,000.

Bongo Star Search ni Janga la kitaifa...Mchakato Umejaa Dharau, Kejeli na Kukatishana Tamaa

$
0
0
Kwa mtu yeyote intellectual ambaye huwa anatazama Bongo Star Search atakubaliana nami kuwa mchakato huo wa kusaka mwanamuziki bora mwenye kipaji umejaa dharau,kejeli na kukatisha tamaa,hawa Master Jay na Salama Jabir ni majaji feki kabisa wanaowakatisha tamaa vijana wenye vipaji,namsifu sana Madam Rita, dada huyu hajawahi kumkatisha tamaa mshiriki yoyote,hata anapoonekana kushindwa yeye humtia moyo ama kukaa kimya,lakini salama na master jay huwatolea maneno ya kejeli,vijana wangu wa Tanzania wenye vipaji mbalimbali msikatishwe tamaa na hizi taasisi za kihuni zinazojifanya zina uwezo wa kubaini vipaji vyenu,leo hii Diamond, Lady Jay Dee, Prof Jay, Dully sykes na wengineo wangeenda kutafuta vipaji vyao Bongo Star Search wangerudi wakiwa wamekata tamaa kwa kukutana na kina Master jay na Salama, simameni wenyewe achaneni na hawa wahuni, mtapoteza vipaji vyenu bure, historia inaonyesha kuwa, hakuna mtu aliyefanikiwa maishani kwa kuwekwa katika mizani ya ushindani bali alifanikiwa kwa kujituma mwenyewe akiamini atafanikiwa

By  Dilemma.

LOWASSA Alitofautiana na Misimamo ya CCM Hata Kabla Hajaenguliwa Kugombea Uraisi Kwanini?

$
0
0
Mgogoro au tofauti kati ya Lowassa na chama cha awali ulionekana mapema hata kabla ya kufanyiwa mizengwe katika uchaguzi wa mgombea uraisi wa chama hicho kutokana na misimamo yake.

1. Alikubali kuwajibika kisiasa jambo ambalo ni nadra kwa kiongonzi wa CCM

2. Alitamka hadharani kutofautiana na kipaumbele cha "kilimo kwanza" yeye alitaka "elimu kwanza" .

3. Alidai ajira ya vijana ni "bomu linalosubiri kulipuka" muda wowote, wakubwa wake wakamnunia wakidai mambo yako shwari.

 4. Anachukizwa na umasikini watanzania wenzake walidai hali ya uchumi ni nzuri labda kwa wenye kuvaa miwani ya mbao.

5. Anaamini katika mabadiliko sasa (Time 4 Change now) wenziwe BRN . Toa maoni yako na kama yapo niliyoyasahau ongeza tafadhali.

Ridhiwani Kikwete Kaiweka hii Video ya Lowassa na Kuandika Haya Maneno.

$
0
0
Hii ni post ya Ridhiwani Kikwete kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, aliiweka hii video ya Edward Lowassa na kuandika ‘Raha ya mja kunena, kwa muungwana ni vitendo ushahidi tosha kuwa mgombea wa CCM anakubalika na ni bora kwa kazi’

Kwenye page yake ya Instagram aliweka video hiihii akaandika ‘Ni thawabu pia kutoa sifa na ni dhambi kutokubali mema yanapofanyika, hongera sana mgombea kwa kuyaona mazuri yatendekayo na mtendaji wa hayo, ‪#‎Magufuli2015 #‎MzikiwaMagufuliUtauweza?

Lowassa 1Hii ni post ya Ridhiwani Kikwete kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, aliiweka hii video ya Edward Lowassa na kuandika ‘Raha ya mja kunena, kwa muungwana ni vitendo ushahidi tosha kuwa mgombea wa CCM anakubalika na ni bora kwa kazi’

Kwenye page yake ya Instagram aliweka video hiihii akaandika ‘Ni thawabu pia kutoa sifa na ni dhambi kutokubali mema yanapofanyika, hongera sana mgombea kwa kuyaona mazuri yatendekayo na mtendaji wa hayo, ‪#‎Magufuli2015 #‎MzikiwaMagufuliUtauweza?


Kwenye hii video Lowassa anasema >>> ‘Namsifu sana Dr. Magufuli kwa kazi nzuri aliyofanya, kazi nzuri sana ya barabara, nzuri sana‘

Waziri wa CCM arusha Ngumi wakati wa Kutangaza Mshindi wa Kura za Maoni-VIDEO

$
0
0
Ona Waziri wa CCM wa Mifugo Dr. Kamani baada ya kukatwa kwenye kura za Maoni hahahahah jamani hizi kura ni nomazzzz U know....I mean mtumzima Waziri halafu PhD ona alivyofanywa na kura AMEKATWA hahaha me I love it CHEZEYA WANANCHI hahahah U know this is Funny bana! YAANI MI NGACHOKA KABISA NA HIZI gademu mazafantazz KURA

Angalia Video Hapa Chini:

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images