Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104762 articles
Browse latest View live

Mama Diamond Platnumz Amfunika Zari kwa Mbizi Kwenye Bwawa la Kuogelea

$
0
0

MAMA’KE Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ameonesha umahiri mkubwa wa kuogelea kiasi cha kumfunika mkwe wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwenye bwawa la kuogelea lililopo nyumbani kwa Diamond, Tegeta-Mivumoni jijini Dar.

Mama huyo alionekana akipiga mbizi na mtoto wake Esma, huku akionyesha manjonjo ya kuogelea kwa kasi tofauti na Zari anavyoogelea katika bwawa hilo.

“Bi mkubwa yuko vizuri sasa maana anapiga mbizi siyo mchezo kabisa hata Zari haoni ndani, spidi yake ni kali kuliko Zari,” alisema mwanafamilia mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini huku akimtumia mwandishi wetu picha za mama Diamond akiogelea.

Nilimnunua Kahaba Nikamtambulisha Nyumbani Kwa Wazazi, Utata Ukatokea..!!!

$
0
0
"Unata nife ndo uoe? Nataka kuwaona wajukuu zangu"Ni kauli alioitamka baba yangu mzazi Siku moja alipokuja kunitembelea, iliniuma sana.

Nadhani hata nyie mnalifahamu suala la kuoa au kuolewa ni mipango ya mtu mwenyewe pale mda wake utakapofika atafanya maamuzi yake mwenyewe hii ni kutokana na mtu kujipanga kwake.

Ni muda mrefu wazazi wananisumbua nioe na mimi bado sijampata mwanamke ninaemtaka,nikaona ili niwaridhishe wazazi nikaona ngoja niwapake mafuta kwa mgongo wa chupa.

Nikachukua maamuzi nikaenda sehemu zile wanazojiuza wadada wale wa High quality nikamchagua mmoja mzuri sana nikamueleza nia na dhumuni langu tukakubaliana nimlipe kwa dau flani niende nae kama mpenzi wangu na awe na nidhamu zote kwa wazee.

Basi nilifanikiwa na walifurahi sana tafrija fupi ikapita Mara wanandugu wakaitwa njooni mmuone mchumba wa flani kila mmoja alimpenda huku nikiambiwa umechagua kifaa.

Niliona kama maigizo flani ambayo mbeleni pataishia pabaya na kweli ikawa hivyo.Sasa nimeletewa taarifa kwamba ndugu wamekaa kikao wameshapanga kila kitu kuhusu suala la harusi hadi tarehe.Nimechanganyikiwa vya kutosha na yule kahaba kachapa zake kona

Nipeni mawazo jamani nifanye nini?

Hizi Hapa Sababu Halisi za Ukawa Kutokufungua Kampeni Kama ilivyotarajiwa

$
0
0
Panaposemwa uongo na kuachwa kuukanusha basi waweza kuaminiwa. Zimesikika taarifa kwenye mitandao kuwa kutokufungua kampeni leo au kesho ni kutokana na afya ya lowassa kudhoofu.

Sababu ambazo zimefanya Ukawa kutozindua kampeni kama ilivyotarajiwa leo ni kama zifuatavyo:-

1.Maandalizi ya kuandaa kikosi cha kumnadi mgombea yanamalizwa leo
2. Kumaliza mgogoro wa majimbo yaliobaki kutokana na sintofahamu iliyotokea
3. Kuuzima upepo wa magufuli utakaovuma kesho
4. Kuandaa hoja nzito zakujibu baada ya matarumbeta ya ccm yatakayoropoka kesho
5. Kutafuta uwanja wa kampeni utakaokidhi haja
6. Viongozi wa chama wamikoani na wabunge bado hawajawasili Dar kutokana na urudishaji wa fomu za ubunge jana.


chanzo: mwandishi wa habari aliyewasiliana na JJ mnyika muda huu.

Breaking News: Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Fredrick Sumaye Amekihama Chama cha CCM na Kujiunga na Chadema

$
0
0

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa miaka 10 (1995 - 2005) akifanya kazi na Rais Mkapa, mhe. Fredrick Sumaye, anaiaga CCM na kujiunga UKAWA muda huu jijini Dar Es Salaam katika mkutano maalum wa UKAWA na vyombo vya habari.
Sumaye anakuwa waziri mkuu wa pili kujiunga UKAWA baada ya mwenzie Edward Lowassa kufanya hivyo. +255Kwanza

Wanachama zaidi ya 500 wa CHADEMA wahamia ACT...Kadi Zachomwa Moto Laivu

$
0
0
Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.

Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo.

Wanachama hao wamefikia maamuzi ya kukihama chama hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga.
Mamia ya wanachama hawa kutoka wilaya ya Ludewa, wamefanya maandamano ya amani kutoka mtaa wa Kilimahewa hadi katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Ludewa wakiwa na mabango ya aina mbalimbali yakilaani viongozi wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata Okol Haule aliyeshinda katika kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Hata mara baada ya wanachama hawa kuwasili katika ofisi za CHADEMA wilaya, viongozi waliingia mitini na kufunga ofisi, lakini dhamira ya wafuasi hawa wa CHADEMA wakiwemo viongozi wa juu kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Ludewa, haikuishia hapo na wote wakiwa hawana imani tena na CHADEMA wakaelekea ofisi za ACT Wazalendo mtaa wa Sokoni na kujiunga nacho.
Huku wakidhamiria kuisambaratisha kabisa CHADEMA wilayani humo, wanachama hao wakiungana na mgombea wao wanayemuhitaji bwana Okol Haule wakachoma moto nguo aina ya kombati alizokua akizitumia mgombea huyo, bendera na kadi za CHADEMA ambapo bwana Haule anasema ameshindwa kuvumilia ubakaji wa demokrasia uliofanywa na viongozi wa CHADEMA.

Hizi Hapa Sababu Kuu Kwanini Sumaye Amekihama Chama Cha CCM na Kuamua Kuingia Ukawa..Je Unajua Amehamia Chama Gani?

$
0
0
MBOWE: Ameomba pole kwa kuwashtukiza wanahabari kwa kuwapa taarifa ya ghafla, amemualika Sumaye azungumze na waandishi wa habari pia na watanzania wote, atakaefunga atakua mwenyekiti wa NCCR mageuzi, Sumaye atakuwa na jambo la kulieleza taifa, ni mtu mwenye uwezo mkubwa na anamkaribisha aje kuzumngumza na wanahabari.

Sumaye: Mheshimiwa Lowassa, viongozi, wenyeviti wa UKAWA, ndugu zangu viongozi mbalimbali wanaounda UKAWA. Nimewaita hapa juu ya mambo mawili makubwa.

Moja ni kutoa ufafanuzi kwa jambo lililotokea hivi karibuni kama wiki moja hivi, kuna taarifa zilitoka katika mitandao ya kijamii kadri ya wiki moja iliyopita kuwa nimejitoa CCM na kuhamia UKAWA. Ile taarifa ilikuwa uongo.

Basi kulikuwa na ndugu yangu, ndugu yangu kabisa anayeitwa John Mrema, alipoiona akanipigia simu wakati nipo nje ya nchi kwamba kuna taarifa umejitoa CCM nikamwambia hapana, akasema basi naomba uikanushe, nikamuomba aikanushe kwa niaba yangu ila kwa bahati mbaya naamini kwa nia njema ili kutia msisitizo alienda mbele zaidi na kusema Sumaye hatajitoa CCM maisha yake yote, hiyo si sahihi, hakuna mtu anaweza akafunga nadhiri na chama cha siasa.

La pili akasema Sumaye atazunguka nchi nzima na Magufuli kumnadi, hili nalo si sahihi na bahati nzuri CCM wameshamjibu kwa kutoa orodha ya watu wataomnadi mgombea wa CCM. Napenda kumshukuru ndugu Lema kukanusha taarifahii hata kama aliongezea chumvi za hapa na pale.

Kwanza niseme wazi sina tatizo na mgembea wa CCM ndugu Magufuli na nina raha moyoni yeye ndie mgombea kupitia CCM, ninaamini hakuhonga, mtu anae chapa kazi japo ana mapungufu yake mengi, hakuna mwanadamu aliekamilika.

Mimi nina tatizo na mfumo wetu au mfumo wao katika uchaguzi, kwa sababu kile chama cha mapinduzi ni cha zamani. Mimi kwa imani yangu na naamini imani ya wengi safari hii yametokea sana katika chama cha CCM. Ni vizuri tuige kwa wenzetu waliokomaa kidemokrasia.

Binafsi nilitarajia sitafika mbali katika mchakato huo. Tatizo la rushwa katika CCM, hili linathibitishwa na pesa nyingi zilizotumika wakati wa mchakato, watu waliwanunua wapiga kura.

CCM haikufanya tathmini, kama mgombea urais anadondoka karibu asilimia 20, chama kilitakiwa kishtuke lakini CCM haikustuka, CCM haikuhamasisha uandikishaji na upigaji wa kura. Walizunguka nchi nzima lakini walikuwa hawahamasishi bali wanaivua nguo serikali yao. Umeiweka wewe pia ni kazi yako kuirekebisha wewe. Sura ya utawala katika vyama vingi, lengo ni ili siasa itoe ushindani, lazima ujunge sifa mbili muhimu. Moja mgawanyo wa dhahiri kati ya siasa na utumishi wa umma, kama mgawanyiko huu upo vizuri wanasiasa wanaweza kubadilishwa hata baada ya miezi sita. Katika nchi yetu, mgawanyo huu si dhahiri, inabomoa misingi ya utumishi, jamii hata watu binafsi. Huwa tunasikia nchi kama Italy na nyinginezo waziri mkuu na serikali imeanguka lakini huwezi kusikia athari.

Vyama vingi pia lazima Ijenge sura ya kuwa na vyama viwili vikubwa vinavyolinganangana, hata marekani wana vyama viwili vikubwa, pia Uingereza. Usipokuwa na chama mbadala, ipo siku wananchi wataingiza chama ambacho hakipo tayari madarakani. Hakuna chama cha siasa kinachokaa milele hata kifanye vizuri namna gani, watu watakichoka tu.

Niligombea urais kupitia CCM kutaka kuleta mabadiliko hayo mawili, katika marekebisho hayo, nafasi ya wakuu wa wilaya ningeitoa katika siasa. Ningejenga chama mbadala ndani ya CCM, kwa sababu nilijua kufanya nje ya CCM ni jambo gumu.

Natoka CCM, mimi leo nimeamua kutoka CCM na kujiunga na upinzani wa UKAWA. Uamuzi huu si rahisi watu wetu kuuelewa, nitajaribu kuueleza ili mnielewe, sitoki kwa sababu nina hasira, kukatwa, Simpendi mgombea wake Magufuli bali nakiimarisha chama cha mapinduzi. Mimi ni mwanachama tu na sina nafasi yoyote hata ujumbe wa tawi sina hivyo CCM hawana sababu ya kusikitika.

Nadhani huko nitakapoenda wataona umuhimu wangu, naamini na CCM wataona umuhimu wangu. Better late than never, kuuondoka kwangu CCM sikidhoofishi bali sasa watakuwa na upinzani mkali. They have to pull up their socks, sijadai shilingi.

Sijaingia huku kwa sababu tu Lowassa anatoka Kaskazini au Mbowe ni wa Kaskazini, nilipiga vita siasa za kaskazini. Kina Mbatia, Dr Slaa na Lipumba wamefanya kazi kubwa, Lowassa ana ujuzi hwa wengine wameenda shule lakini hawajakaa katika serikali, CCM imezubaa wanajifanya watashinda lakini wananchi wanataka mabadiliko, ni lazima sisi ambao tuna uchungu na nchi hii tuwasaidie hawa waweze kuendesha nchi hii. Lowassa peke yake na Mbatia hawataweza, lazima wawepo watu wachache wataoweza kuwasaidia kupiga mbizi kwa haraka.

Tunawaomba watu wengine waliopo CCM waje watusaidie, tukiwaacha wataweza lakini watachukua muda mrefu sana.

Mwisho niwashukuru wote ambao nimeshirikiana nao, naishukuru sana familia yangu. Nimekuwa CCM tangu nina miaka 35, mtu ambae anajua miaka yote niko CCM alafu asubuhi anaamka namwambia nimeamka CCM, namshukuru sana, pia nawashukuru wanangu japo walikubali kwa shingo upande.

Chama gani ndani ya UKAWA nitajua mbele ya safari.

CCM Mna Maoni Gani Kuhusu Mh. Sumaye na Kukimbiwa na Mawaziri Wakuu Walio na Jina Kubwa Nchi Hii?

$
0
0
CCM MNA maoni gani kuhusu mh. Sumaye na kukimbiwa na mawaziri wakuu walio na jina kubwa nchi hii? Je! Wananchi mnawaeleza nini Juu ya usafi wa CCM?

Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Yamshtua Rais Kikwete...Yadai Inatazama Kwa Umakini Yanayotokea Tanzania Sasa...

$
0
0
KATIKA kile ambacho kwa wakati huu kinaweza kuonekana kama kimemshtua Rais Jakaya Kikwete, ni hatua yake ya kurejea kauli ambayo imekuwa ikitolewa na viongozi wa Afrika dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).

Kwamba viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete ambayo aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC, imekuja siku moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, amekaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo  inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa siku chache zilizopita na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Wiki iliyopita akiwa katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa alilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.

Zaidi Lowassa pamoja na viongozi wa Ukawa walisema endapo vyombo vya dola vitakiuka haki za binadamu hawatasita kumshtaki Rais Kikwete katika mahakama hiyo huku wakisema tayari wameanza kukusanya ushahidi wa kwenda kushitaki.

Hata hivyo, Rais Kikwete akizungumza na wanasheria hao wa SADC, aliutaka umoja huo kuwa imara katika kuzungumzia uonevu unaofanywa na ICC dhidi ya viongozi wa Afrika.

“Kuna hizi kauli zinazotolewa na viongozi wa Afrika kwamba Mahakama ya Kimataifa inazionea nchi za Afrika na kuyaacha mataifa mengine ambayo yanaonekana kabisa kuwa na machafuko lakini viongozi wake hawashughulikiwi,” alisema Rais Kikwete.

Alisema mfumo wa Mahakama hiyo unaonekana kuwa ni wa kibaguzi na hivyo kushindwa kutenda haki.

“Kuna viongozi katika sayari hii wanafanya makosa lakini mahakama hizi haziwashughulikii. Mahakama hizi zinatakiwa kutenda haki.

“Haiwezekani viongozi wa mataifa madogo ndio wanaonekana kufanya uhalifu lakini wale wa mataifa makubwa wanaachwa,” alisema Kikwete huku akitolea mfano wa Rais wa Syria, Bashir Al-Asaad, ambapo alisema aliwahi kuzungumza na Luis Ocampo kipindi akiwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC kuhusu kushughulikia mataifa haya makubwa.

“Nilimuuliza Ocampo mbona mataifa makubwa yanaonekana waziwazi kufanya uhalifu dhidi ya binadamu lakini ICC haifanyi kitu? Lakini cha ajabu alinijibu itafanya nini…hii inaonyesha hakuna usawa,” alisema Rais Kikwete.

Pamoja na hayo, Rais Kikwete alisema ataachia madaraka kwa amani na kwamba baada ya hapo atarejea kijijini kwake kujishughulisha na kilimo na ufugaji.

Matokea ya Mechi Kati ya Yanga na Azam Nimekuwekea Hapa.....

$
0
0
Leo Palikuwa na Mtanange wa Shoka Kati ya Yanga na Azam Kugombania Ngao ya Hisani ya Ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania ..Na Matokeo ni Kama yafuatayo...
Yanga wameshinda ngao ya hisani kwakuifunga Azam kwa Penati 8 kwa 7

Je, TBC watarusha habari ya SUMAYE kujiunga Na Makamanda?

$
0
0
Ni wazi kuwa TV ya Taifa imekuwa hairushi kabisa habari za ukawa...sasa leo tutegemee kurushwa habari hii ya waziri mkuu mstaafu mh.sumaye kujiunga na makamanda?

Mgawanyo wa Mali Wasababisha Mauaji Bagamoyo, Mke Ataka Mali zote na Watoto, Mume Amchoma Kisu na yeye Kujiua pia

$
0
0
Mauaji ya kutisha yametokea Wilaya ya Bagamoyo siku ya leo. Chanzo cha mauaji haya ni kuhusu talaka na mgawanyo wa mali.

Baada ya kwenda BAKWATA kusuluhishwa Mwanamke (Mwenyendoa) alitaka mali zote aandikiwe yeye na sio watoto kama ilivyokuwa...Mwanaume ( Mwenyendoa) alichomoa kisu alichokuwa amekificha kiunoni na kumchoma mkewe na yeye kujichoma kisu cha tumboni na kujiwekea mchanga kwenye utumbo uliokuwa umetoka nje ili asiweze kupona kabisa.

Picha zinatisha ila naweka baadhi zenye maadili.

Picha 19 za matukio mbalimbali yaliotokea Uwanja wa Taifa katika mechi kati ya Yanga Vs Azam FC.

$
0
0
Mtu wangu wa nguvu nimekusogezea picha za matukio mbalimbali yaliotokea ndani ya Uwanja na nje ya Uwanja wakati mabingwa wapya wa ngao ya hisani Yangawakishangilia ushindi walioupata dhidi ya Azam FC, timu ambayo ilikuwa ina miliki ngao hiyo.
2X6A1973 - Copy
Wachezaji wa Yanga wakiwa na Ngao ya Hisani walioitwaa mbele ya Azam FC
2X6A1879
2X6A1880
2X6A1884
2X6A1887
2X6A1919
2X6A1923
2X6A1927
2X6A1528
2X6A1743
2X6A1744


2X6A1794

2X6A1765

2X6A1789

2X6A1779

2X6A1744

2X6A1746

2X6A1833
2X6A1775
Source:Millard Ayo

Ujumbe Wa Maandishi Kutoka kwa Lowassa Kwenda Kwa Sumaye Kumkaribisha UKAWA

$
0
0
"Karibu Ndugu Frederick Sumaye katika mabadiliko ya kweli. Tushikamane na tusimame pamoja na wananchi kuongoza hamasa ya watanzania wanaotaka mabadiliko kwa kuiondoa CCM kupitia UKAWA. Hakuna anayeweza kusimama kuzuia nguvu ya umma katika kufanya maamuzi sahihi na magumu Oktoba 25, Mwaka huu. Karibu mpambanaji Sumaye".-Edward Ngoyai Lowassa

Kauli Ngumu Alisozisema Mh Sumaye Bila Kuogopa CCM Alipotangaza Rasmi Kujiunga na Ukawa

$
0
0


  • ‪ Hakuna mtu ambaye anaweza kufunga nadhiri na chama cha siasa"
  • Sina tatizo na mgombea wa CCM, nina amini hakuhonga na anachapa kazi,japokuwa ana mapungufu mengi katika nafasi hiyo"
  • Mwenyekiti alikuja na majina yake mfukoni, na yalikuwa yanafahamika,na mimi niliyafahamu"
  • Tatizo la rushwa katika chama cha mapinduzi wakati wa uchaguzi,limezidi"
  • Fedha nyingi zimetumika kwenye michakato ya urais, ubunge na udiwani"
  • Watoa rushwa wengi wametangazwa ndio wagombea wa ccm"
  • Maisha ya kuona hamna maisha nje ya ccm yamepitwa na wakati"

Lowassa, wapo wapi wabunge 50 na wenyeviti 15 waliokufata?

$
0
0

Tuliaminishwa kuwa Edward Lowassa ataondoka na wabunge hamsini pamoja wenyeviti mikoa kumi na tano Kutoka CCM mbona hatuwaoni au wamekutosa?

Utabiri wa TB Joshua Uko Palepale Uchaguzi 2015

$
0
0
Taarifa kutoka kwa watanzania walio enda TB Joshua walifika wakasema mbona ulisema Lowasaa atakuwa rais alafu akakatwa? Tb Joshua akawambia uchaguzi umesha fanyika wakasema apana akawambia nendeni nchini kwenu mkafanye uchaguzi Lowasa ndo raisi, siku wanafika Tanzania wakakuta ndo siku Lowassa anajiunga na CHADEMA ...Yakawafika Hapaaaaaa.........!!!

Haya Ndio Anayoyapenda Mume Wangu na Kuiharibu Ndoa Yangu

$
0
0
Ndugu zangu,
Nilishawai kuwaambia hali ngumu ya mapenzi ninayoipitia ndani ya miaka miwili,kwa kifupi ni kuwa mwanaume unalalanae miezi 2 hajakugusa, ukimgusa anasema amechoka.

Juzi nilikuwa napitia Fb yake nimekuta amewa add wadada wa 4 hivi tofauti na katika wadada hao wote ni ambao mtu anaejiheshimu na mwenye busara hawezi kuwa add, ni watu wasio na maadili mema, picha zao zimekaa kikujiuza, na ata ukiangalia friends wao hao kina dada ni wanaume zaidi ya 600.

Wanawake unaweza kuta wa4 tu, mr. uwa anasafiri sana kikazi anaenda jiji flani hapahapa TZ na hao aliowa add wanapatikana jiji hilohilo nikiangalia profile zao, naanza kuamini kuwa hii hali ngumu ya mapenzi ninayopitia anaisababisha yeye kwa makusudi na wala sio shetani bali anaudekeza moyo wake unachoona.

Hivohivo, sijamuuliza na sitomuuliza naona tabu kumuuliza maana nishalalamika sana lakini sioni mabadiliko, sio wanaume wote wanaosafiri kikazi wanaendea kazi wengine wanaendea ufuska tu.Nilijaribu kwenda katika fb page nikaingiza namba yake nimekuta ana account nyingine nayo haieleweki.

Kaiita kama majina kama vile (Zanzibarbongo) sio jina halisi, hapa mnielewe namaanisha hivi namba ya simu ukiisajili katika kufungulia account ya fb inaonesha hiyo account, so baada ya kuweka namba yake nimekutana na hiyo account it means kwamba ya kwake, wakati huohuo ana account ambayo inafahamika,

Najiuliza anatafuta nini? Mke wake mie msichana tu, najimudu, nafanya kazi mzuri, nina umbo zuri, na kazi zote nifanyazo lazima nihakikishe napika chakula cha usiku kwa mkono wangu, na mengine yote ya kumfanyia mume namfanyia, jamani huyu mwanaume asieridhika na alichonacho anatafuta nini?

All in all nimechoka na hii hali na siku zinavoenda mapenzi yanaisha kabisa kwake.

Nifanye nini ndugu zangu?

Mafuriko ya Magufuli Kuishika Dar Leo Wakati Akizindua Kampeni

$
0
0

John Pombe Magufuli
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajiwa kuzindua kampeni zake za urais, ubunge na udiwani nchi nzima katika viwanja vya Jangwani leo, katika mkutano utakaorushwa moja kwa moja na televisheni na redio mbalimbali nchi nzima.

Katika uzinduzi huo, CCM pia inatarajiwa kuweka ilani yake ya uchaguzi hadharani, itakayonadiwa na mgombea urais wake, Dk John Magufuli na wagombea wengine wa ubunge na udiwani nchi nzima.

 Moja ya mambo ambayo CCM inatarajiwa kufafanua ni matumaini makubwa ya uwezo wa mgombea wake katika kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo, kutokana na historia yake ya utendaji ndani ya Serikali katika nafasi mbalimbali alizokabidhiwa, ikiwemo Waziri wa Ujenzi.

Wageni mbalimbali pia wamealikwa kuhudhuria uzinduzi huo vikiwemo pia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa CCM Mkoa, Juma Simba alisema vile vile wanatarajia wageni kutoka ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam kuhudhuria mkutano huo leo.

“Tumetuma mialiko ya mkutano wa kesho (leo) sio tu kwa wana CCM wenzetu bali pia kwa vyama vingine vya siasa ikiwa ni pamoja na kwa vyama vya ‘Ukawa’,” alisema.

Simba alisema mkutano huo utakuwa mkubwa na wa aina yake ambapo viongozi mbalimbali wa chama wanatarajiwa kushiriki na kwamba mkutano huo ratiba yake itaanza asubuhi saa tatu kwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali na wananchi kuendelea kuwasili uwanjani.

Sifa za Magufuli Mgombea huyo amekuwa akitajwa kuwa na sifa ya mchapakazi, makini, asiyependa uvivu, ambapo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alimpachika jina “Tingatinga”.

Rais Kikwete alimpachika Magufuli jina hilo, baada ya kutangazwa kuwashinda makada wengine wawili waliokuwa wakiwania kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Dodoma.

 “Kila mtu anaitwa jembe lakini huyu ni zaidi ya jembe. Ni tingatinga… Magufuli ni bulldozer. Magufuli havumilii ujinga, ni mtu ambaye anataka kuona kazi zake zinafanyika kama alivyoagiza,” alikaririwa akisema.

Kikwete aliendelea kummwagia sifa Dk Magufuli kuhusu utendaji wake akisema kuwa alipokuwa akifuatilia makandarasi kwenye miradi ya ujenzi, alidiriki kuwatimua pale alipobaini walikuwa wakifanya kazi kinyume na makubaliano.

Baadhi ya watu waliofanya naye kazi wamekaririwa wakisema iwapo atachaguliwa kuwa rais basi wavivu wajitayarishe kukimbia kwani Waziri huyo ni mchapa kazi wa hali ya juu.

Mrembo Lulu Michael Amrushia Vijembe Husna Maulid

$
0
0
STAA mdogo kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameonekana kumrushia vijembe hasimu wake mkubwa mlimbwende Husna Maulid kwa kile alichodai kuwa anamuibia maelezo yake ya picha (caption) kwenye mtandao wake wa Instagram.

Staa huyo ambaye hakumtaja Husna moja kwa moja, alisema kwa sababu amekuwa akiweka maelezo ya picha katika mtandao na mtu kuyaiba kama yalivyo na kuweka katika picha zake, ameamua kutoa onyo ili asiibiwe.

“Naweka caption lakini ina hati miliki, wewe unayechukua na kuhamishia kwako, tafadhali.” Aliandika Lulu mtandaoni ambapo alipoulizwa na mwandishi wetu kama alimtupia vijembe Husna, alisema:

“Jamani sijataja jina la mtu yoyote lakini kama kuna ambaye anajihisi basi ndio huyohuyo.”

Husna amekuwa akikopi maneno ambayo Lulu anayaweka katika kurasa zake kama: “You can copy my things but you can’t be me.” Husna naye anaandika hivyohivyo.

Wawili hao waliwahi kuwa marafiki kisha kutofautiana wakituhumiana kuibiana bwana.

Unaambiwa Hii ni Zaidi ya Mafuriko..Hii ya CCM Sasa Tunaiita Sunami la CCM..Tazama Picha Kumi Kutoka Jagwani leo Ambapo CCM ilikuwa inazindia Kampeni za Uchaguzi 2015

$
0
0

Unaambiwa Hii ni Zaidi ya Mafuriko..Hii ya CCM Sasa Tunaiita Sunami la CCM..Tazama Picha Kumi Kutoka Jagwani leo Ambapo CCM ilikuwa inazindia Kampeni za Uchaguzi 2015
Viewing all 104762 articles
Browse latest View live




Latest Images