Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

CCM Kuzidisha Muda wa Kampeni, NEC Waitupia Mpira Polisi

$
0
0
Sarakasi zinaendelea.Tume ya uchaguzi NEC imenukuliwa ikiwatupia mpira jeshi la polisi kuwa ndilo linalohusika kuhakikisha kampeni hazizidi saa 12.Tume imeruka kimanga baada ya kupokea hoja kutoka kwa wadau kuwa juzi CCM wakati wakizindua kampeni Jangwani walizidisha muda zaidi ya nusa saa kinyume na taratibu...

Waziri wa Zamani wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha Aendelea Kusota Segerea..Juhudi za Kumtoa Kwa Dhamana Zashindikana

$
0
0
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kutoa lugha ya matusi kwa maofisa wa polisi hapo jana.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, Masha amekana na kurudishwa Segerea hadi hapo nyaraka zake zilizowasilishwa kwa ajili ya dhamana zitakapohakikiwa.

Masha amefikishwa mahakamani hapo akiwa na vijana wengine 19 ambao wamesomewa shitaka la kutaka kukusanyika bila kibali.

Awali taarifa zinasema Masha alifika katika Kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam jana jioni kwa lengo la kutaka kuwadhamini vijana hao na baadaye alishikiliwa na polisi kituoni hapo.

Masha alikihama Chama cha Mapinduzi hivi karibuni na kujiunga na Chadema na kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Sengerema katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.

Lowassa Apewa Onyo na Kamanda Kova...Staili yake ya Kampeni ya Kuwatembelea Wananchi Kwa Kushtukiza yaweza Kutumiwa na Maadui Kumdhuru

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtahadharisha mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa kuwa kampeni alizoanza kwa kuyatembelea makundi kadhaa zinaweza kutumiwa na maadui wa kisiasa kumdhuru.

Hata hivyo, wanasiasa wametakiwa kufuata ratiba ya kampeni kwa kuzingatia mwongozo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kulisaidia jeshi hilo kukabiliana na vitendo viovu.

Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku ya pili tangu Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji walipoanza kuwatembelea wananchi huku wakitumia usafiri wa umma.

Kwa kutumia staili hiyo, leo Lowassa akiwa na Duni Haji wametembelea maeneo ya Tandika, Tandale na Kariakoo jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema ziara iliyofanywa leo maeneo ya Swahili, Kariakoo zimesababisha mikusanyiko isiyo ya lazima na kusimamisha shughuli za maendeleo.

Baada ya CCM kuzindua kampeni zake mwishoni mwa juma lililopita viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Chadema nacho kinajiandaa kufanya hivyo Agosti 29 maeneo hayohayo.

Nape: Ni Upuuzi Mkubwa Mahakama ya Kimataifa ICC Kusema Inaangalia Uchaguzi wa Tanzania Kwa Karibu Kwani si Kazi yao

$
0
0
Baada ya Muendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kusema kuwa wanaufuatilia kwa makini uchaguzi mkuu wa Tanzania kuhakikisha hakuna haki za binadamu zitakazo kiukwa, Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema anadhani ni upuuzi kwa mahakama hiyo kusema inaangalia uchaguzi kwani si kazi yao. 

Amesema kama kweli wanafuatilia mambo hayo basi wafuatilie na nchi za Ulaya.

Chanzo: (ITV).

Ni Kampeni za Mtaa kwa Mtaa: LOWASSA Aibukia Tandale Sokoni Kuzungumza na Mama Ntilie na Wafanyabiashara Wengine

$
0
0


Mgombea wa Urais wa Ukawa Edward Lowassa  pamoja na mgombea mwenza Juma Duni Haji leo wamewashitukiza wafanyabiashara  katika soko la Tandika jijini Dar es salaam.

Aidha, wagombea hao waliwasili katika soko hilo asubuhi ya leo ambapo shughuli zilisimama kwa muda.


Kabla ya kuanza mazungumzo na wafanyabishara  hao,Lowassa   alikaribishwa  chai  na mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.

Ziara hiyo ya kushitukiza iliyoanzia Mbagala siku ya jana ni maalumu kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa hali ya chini kuhusiana na matatizo yanayowakumba  katika maisha yao ya kila siku.

Je, Unataka kufahamu kesho Lowassa atakuwa wapi? Endelea kufuatilia mtandao  huu.

Baada ya Baadhi ya Mashabiki Kumshambulia kwa Maneno, JB Asema Haya

$
0
0
Kufuatia kitendo baadhi ya mashabiki kumshabulia kwa maneno makali staa wa Bongo Movies, JB kwa kuonyesha mapenzi yake kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, JB amefunguka haya kwenye ukurasa wake mtandaoni kuwataka wabadilike kimtazamo.

Hakuna kitu muhimu kwenye maisha kama furaha....lakini furaha ina ambatana na kufanya mambo ambayo moyo wako unapenda bila kuvunja sheria.

Kuishi maisha ya kuogopa kitu unachopenda kwa sababu ya watu ni kuinyima furaha roho yako...watanzania wenzangu tuanze tabia ya kuheshimu maamuzi ya wenzetu.

Angalia hata kwenye mahusiano yetu watu wakiachana ni uhasama..kisa hatukubali kuwa mwenzako moyo wake uko kwingine.

Eti lazima akupende ww tu..haa...kwenye siasa ndio usiseme mtu akipenda upande mwingine ashakuwa adui.Aaah tubadilike.....sambaza upendo..+255 kwanza.

Nora: Jamani Naolewa Mie, Nikiachika Tena…!

$
0
0
MUIGIZAJI wa muda mrefu katika tasnia ya filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ yuko katika siku za mwisho za kuhitimisha harakati za kufunga ndoa, huku akijiapiza kuwa, endapo ataachika tena, basi atakuwa na nuksi.

Akipiga stori na paparazi wetu juzi, mmoja wa marafiki wa muda mrefu na Nora, ambaye pia ni msanii wa filamu (jina lipo kwenye droo zetu), alisema kwa sasa Nora yuko ‘bize’ kuhakikisha mambo na mipango ya harusi yake na mwanaume ambaye alitajwa kwa jina moja la Omary inakwenda sawa.

Katika kujua ukweli wa habari hiyo, Nora alitafutwa na alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Jamani, kwani kuolewa ni kitu cha ajabu, ni kweli niko kwenye maandalizi hayo na ikitokea nimeachika tena, basi itabidi nijiangalie upya, ila naamini huyu wa sasa ndiye niliyekuwa namhitaji.”

Mawela ya Sinza na Havannah ya Segerea Ndio Baa za Wiki Shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani

$
0
0
MAWELA YA SINZA NA HAVANNAH YA SEGEREA NDIO BAA ZA WIKI SHINDANO LA TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI
 Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Godwin Mawanja akiamsha ari ya kiwanja cha Havannah kilichopo Segerea mwisho jijini Dar wakati wa shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani linaloendeshwa na bia ya Tusker lilipotinga kwenye baa hiyo katika uhamasihaji wa kufanya kweli kwenye upande wa huduma sambamba na hilo promosheni hiyo ilikua na zawadi lukuki za fulana, bia za bure na kalamu kwa wapenzi wa bia hiyo waliofika kiwanjani hapo.

 Mkazi wa Segerea aliyetambulika kwa jina la Gaudence Mgeja pamoja na Dj wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani Dj Con wakishindana kucheza mziki kwenye hafla ya kuipongeza baa ya Havannah iliyopo Segerea mwisho jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo yenye lengo la kuhamasisha kwa vitendo baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli inapokuja kwenye suala la huduma kwa wateja wao.

Meneja bia ya Tusker SBL, Nandi Mwiyombella (Kushoto) akikabidhi zawadi ya mfuko wenye fulana na kalamu kwa mkazi wa Segerea mwisho Bw. Rodride Nyange katika hafla ya kuipongeza baa ya Havannah iliyopo Segerea mwisho jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo yenye nia ya kuhamasiha baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye upande wa huduma inatarajiwa pia kuwafikia wakazi mbalimbali wa mikoa mingine nchini kama;- Arusha, Mbeya, Moshi, Mwanza na Morogoro.

Baadhi ya wapenzi wa bia ya Tusker wakifurahia burudani ya muziki katika hafla ya kuipongeza baa ya Havannah iliyopo Segerea mwisho jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo yenye nia ya kuhamasiha baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye upande wa huduma inatarajiwa pia kuwafikia wakazi mbalimbali wa mikoa mingine nchini kama;- Arusha, Mbeya, Moshi, Mwanza na Morogoro.

 Meneja wa bia ya Tusker SBL, Nandi Mwiyombella akikabidhi zawadi ya mfuko wenye fulana na kalamu kwa mkazi wa Sinza Bw. Kamara Mambosasa katika hafla ya kuipongeza baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo yenye nia ya kuhamasiha baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye upande wa huduma inatarajiwa pia kuwafikia wakazi mbalimbali wa mikoa mingine nchini kama;- Arusha, Mbeya, Mwanza,Moshi  na Morogoro.

 Meneja wa bia ya Tusker SBL, Nandi Mwiyombella akikabidhi zawadi ya mfuko wenye fulana na kalamu kwa mkazi wa Sinza Bi. Zalia Ally katika hafla ya kuipongeza baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo yenye nia ya kuhamasiha baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye upande wa huduma inatarajiwa pia kuwafikia wakazi mbalimbali wa mikoa mingine nchini kama;- Arusha, Mbeya, Mwanza na Morogoro.

Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash (kushoto) akizungumza na mpenzi wa bia ya Tusker na mkazi wa Sinza Bw. James Lui katika baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar es salaam wakati wa kusherekea ushindi wa baa hiyo kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo inatarajiwa kuifikia mikoa mingine mbalimbali Tanzania kama;- Arusha, Mbeya, Moshi, Mwanza na Morogoro.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 26

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 26













Eti Kisa Kwenda Ukawa; Wasanii Wamponda Aunt Ezekiel

$
0
0
Kisa na mkasa! Kama hujasikia ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amejikuta akila za uso kutoka kwa mastaa wenzake mara tu baada ya kutangaza kuwa yeye ni Timu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akimuunga mkono mgombea wake wa urais, Edward Ngoyai Lowassa.

Mastaa mbalimbali waliozungumza na Ijumaa Wikienda wakiongozwa na Wema Isaac Sepetu, walimponda na kumshangaa Aunt ambaye awali alikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimuunga mkono mgombea wake wa urais, Dk. John Pombe Magufuli ‘JM’.

“Yaani Aunt ametushangaza kwani alikuwa Team Magufuli. Ameonesha ni kiasi gani ni kigeugeu, sisi tunatarajia ushindi kwa asilimia kubwa. Sisi tumezaliwa na kukulia CCM hivyo hatuwezi kusaliti,” alisema Wema kwa niaba ya wenzake walipokuwa wakitangaza kuzindua kampeni za CCM zilizoanza jana. Jitihaza za kumpata Aunt hazikuzaa matunda.

SIKILIZA Jinsi Diva Loveness na Diamond Platnumz Walivyopeana za Uso Kwenye Kipindi cha XXL Clouds FM

$
0
0
Tukio hilo lilitokea juzi mchana kwenye kipindi cha XXL ambapo mtangazaji wa kipindi hicho, Bdozen alitaka kujua kwanini wawili hao hawaelewani. Diamond alidai kuwa Diva amekuwa akimuongelea vibaya kwenye kipindi chake.

Mimi nimewahi kukuzungumzia vibaya where,” Diva alimuuliza Diamond. “Unazungumza vibaya sana,” alisema Diamond na kuongeza, “Tatizo na mimi mpaka najilaumu labda ningekuwa nimekukaza usingekuwa unaniongelea hivi, I am telling you.” “You are not my type, hauwezi kunikaza,” alijihami Diva.

Bonyeza Hapa Chini Kusikiliza:

Ray C Adaiwa Kuzua Fujo Tena Baada ya Kunyimwa Methadone, Asema Wanafanya Makusudi

$
0
0
Ray C amedaiwa kuzua timbwili Jumapili hii katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dat es Salaam baada ya kukosa huduma ya methadone.

Akizungumza na 255 ya XXL leo, mratibu mkuu wa hospitali ya Mwananyamala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai suala hilo tayari limeshafika polisi.

“Kuna muda maalum wa kugawa dawa, sasa ule muda unapoisha wanafunga,” amesema. “Sasa yule amekuja wakati muda umeshaisha sasa baada ya hapo akaamua kufanya fujo kwa huyo famasia ambaye anagawa dawa na kutoa lugha ambazo hazikuwa nzuri sana kwa huyo famasia. Hakuna mtu aliyeumia ila walisukuma geti la mlango ndio likagonga mlango,” aliongeza.

Hata hivyo Ray C ameiambia Bongo5 kuwa wahusika wa hospitali hiyo wanamfanyia makusudi.

“Mimi nimetoka kwenye madawa ya kulevya, ina maana nilipata matatizo na nilipoteza kila kitu, kwahiyo mimi nikipata mafuta ya elfu 30,000 ya kuweka kwenye gari yangu, elfu 30,000 kila siku ni pesa nyingi. Mimi sina kazi sasa ninavyofika mpaka hapa na nimetumia elfu 20,000 yangu halafu unaninyima dawa na nimemkuta famasia yupo ndani sio nimekuta kumefungwa, yupo ndani anatuona, ‘tunamuomba dada hatujakunywa dawa jana naomba utupatie,” amesema muimbaji huyo.

“Ni kweli wamenipeleka Oysterbay wananiambia mimi sijui nimefanya fujo, lakini sisi tulinyimwa dawa juzi Jumamosi na Jumapili ndio tukawa tunalalamikia tunataka dawa hawajui sisi tunaumia, wao wanacheka tu. Sasa na sisi ni binadamu na tulikuwa wengi na tuna hasira kwa sababu tunaumia, ndio akatoka kwa fujo na gari yake kwa kutuogopa sisi ndo akajikwaruza yeye mwenyewe. Sasa nashangaa polisi amenipeleka mimi. Halafu leo nimeenda pale sijui walitaka niende Segerea, ukiongea nao kidogo wanapaniki mtu katoka Mbagala na shilingi 1,000 ya nauli anakuja mpaka hapa jasho limamtoka mnaanza kumwambia hatukupi dawa?” amehoji.

Bongo5

Nikiwa Mbunge Msinitegemee Sana Kuongelea Matatizo ya Wasanii – Professor Jay

$
0
0
Wasanii wasitegemee msaada wa maana pindi Professor Jay akiingia bungeni. Rapper huyo anayewania ubunge kwenye jimbo la Mikumi mkoani Morogoro amesema atatumia wadhifa huo kuwahudumia wananchi wa Mikumi.

Professor amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi hivyo atatumia muda kuwatumikia watu wake.

“Nimewaambia wasanii wangu na wanajua nimechaguliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye jimbo la Mikumi, lakini wengi wamesema watanisaidia kwa maneno lakini bado sijalaunch kampeni yangu rasmi. Natarajia kulaunch natarajia rasmi tarehe 5 mwezi wa tisa, sasa tunaangalia nani atani-support,” amesema.

“Mimi ni kijana na mimi ni mwanamuziki, watu waelewe naingia bungeni kwenda kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Mikumi, kwahiyo tutafanya kazi sawa za wananchi wa jimbo la Mikumi na Professor atakuwa anaishi Mikumi na nitakuwa napatikana huko Mikumi.”

“Watu wasitegemee nitaingia bungeni kwenda kuongea masuala ya wasanii sana kuliko hata kuwawakilisha watu wa Mikumi. Watu wajue Professor Jay atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi ni vile ni mwanamuziki nitapigania kwa hali na mali maslahi ya muziki ili kuweka sanaa katika level za juu zaidi.”

Jeshi la Polisi Lamuweka Wazi Mfadhili wa Matukio Mbalimbali ya Kigaidi Tanzania

$
0
0
 Hatimaye Jeshi la Polisi Tanzania (PT) limeanika picha ya mtu anayedaiwa kuwa ndiye mfadhili mkuu wa matukio mbalimbali yanayohusishwa na ugaidi likiwemo lile la mauaji ya watu saba kwenye Kituo cha Polisi Stakishari, Dar lililotokea saa 5 usiku, Julai 12, mwaka huu na yale mapigano ya Amboni, Tanga.

Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Ally Mtozen Hery ambaye anadaiwa kuishi kwa kujibadili kama kinyonga kwa muonekano wa sura, wakati mwingine huvaa mavazi ya kike ili asijulikane kirahisi.

Akizungumza na Uwazi juzikati, Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi uliyofanywa na kikosi kazi cha jeshi hilo umebaini kuwa, mtuhumiwa huyo ana mtandao mpana na ndiye mfadhali mkuu wa matukio mbalimbali ya uvamizi, mashambulio na uporaji wa silaha yanayotokea nchini.

Kova aliongeza kuwa, hivi karibunim Hery amehusika katika kufadhili tukio la Amboni Tanga, Mkuranga, Stakishari na mengineyo lakini hatimaye jeshi la polisi kwa kutumia kikosi cha intelijensia kimeweza kubaini nyendo zake na kuinasa picha yake hiyo.

“Tunachotaka mtu huyo ajitokeze mara moja na kujisalimisha polisi. Kwani hata afanyaje lazima tutamkamata tu,” alisema Kamishna Kova.

Akaongeza: “Ile milioni 50,000,000 iliyotangazwa na IGP Ernest Mangu sasa imefikia mahala pake kwa mtu atakayeweza kusaidia kupatikana kwa mtuhumiwa huyo.”

Kova aliendelea kusema mtuhumiwa huyo wakati mwingine hupenda kutembelea Pemba, Tanga, Dar na ukanda mzima wa Pwani.Katika mahojiano na Kamishna Kova alisema hadi sasa, watuhumiwa tisa wanashikiliwa na jeshi hilo kutokana na tukio la Stakishari.
“Si vyema kuwataja kwa majina tunaowashikilia kwa sababu za kiupelelezi lakini hadi sasa kwa jitihada za jeshi letu makini tunawashikilia watuhumiwa tisa na mahojiano yanaendelea,” alisema Kova.

Mbali na mtuhumiwa huyo kusakwa na jeshi la polisi, mtuhumiwa mwingine aliyekuwa akisakwa na jeshi hilo amejisalimisha polisi akiwa na wake zake wawili na sasa anahojiwa kwa kina.

Aliongeza kusema mtuhumiwa huyo aliyejisalimisha polisi aliwahi kuwa mtumishi ndani ya jeshi la polisi lakini alifukuzwa kazi mwaka 1998 kutokana na kutoeleweka kwa nyendo zake.

Polisi huyo aliyeachishwa kazi akiwa na cheo cha sajenti anafahamika kwa jina maarufu la Mzee Mzima ambapo akiwa kazini kitengo cha redio (999) ambacho hushughulikia matukio ya uhalifu kwa haraka nyendo zake zilikuwa hazieleweki ndani ya jeshi hilo.

“Hatuwezi kuvumilia damu za askari wetu zikipotea bure. Ni lazima tuhakikishe kazi tunaifanya ipasavyo na hao watuhumiwa tisa tunaowashikilia wanaendelea kutupa taarifa muhimu,” alisema Kova.

Ugaidi: Watanzania 6 Wenye Silaha Wamekamatwa Kenya Wakielekea Somalia Kujiunga na Al-Shaabab

$
0
0
Polisi nchini Kenya wanawashikilia Watanzania 6 kwa tuhuma za ugaidi. Wamekamatwa Garisa na inasemekana walikuwa wakielekea Somalia Kujiunga na magaidi wa Al Shabab. Wameshikwa wakiwana silaha zikiwemo bunduki na magrunedi.

===========

More by this Author Six Tanzanian nationals were Sunday arrested and a cache of weapons recovered from them by police in Garissa.

Seven pistols and seven grenades were recovered during the arrest.

It is suspected that they were heading to Somalia to join Al-Shabaab terror group.

Addressing journalists in his office in Garissa Town, the north eastern Regional Coordinator Mohamud Saleh said the Tanzanian men who are aged between 20 and 40 were intercepted in Dadaab Town as they were planning to cross into Somalia.

Mr Saleh said the men were being held in Garissa where they will be interrogated for more information.

He added that two other women, a Kenya and Tanzanian, were also arrested early this week as they were heading to Somalia to become Al-Shabaab brides.

ACCOMPLICES SOUGHT

“We arrested six Al-Shabaab militiamen with two pistols, seven grenades, 20 rounds of ammunition and 15 magazines in Garissa Ndogo trading centre in Garissa Town on Sunday and we are looking for more accomplices who are on the run,” he said.

He said the suspects are being held at Garissa Police Station for more interrogation by officers from the anti-terror police unit.

He added that police are still following crucial leads that will help them apprehend more suspected Al-Shabaab militants hiding in the town.

Mr Saleh said the suspected militants were planning to carry out deadly attacks targeting some vital institutions.

The regional coordinator said the security officers got a tip off from the public about the presence of the men.

“We are happy that the locals are cooperating very well with the security agencies in providing intelligence. We are now receiving intelligences even from herders in remote areas,” he told reporters.

He further said a security operation to flush out suspected members of Al-Shabaab believed to be hiding in the dense Boni Forest that extends from the coastal strip to Ijara in Garissa County will begin soon.

He added that security officers have also recovered three automatic assault rifles and eight rounds of ammunition from notorious bandits who were responsible for highway robbery along the Mandera-Arabia road.

Source: Daily Nation

Swali kwa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa

$
0
0
Kaka Ben nakusalimu!

Mtani wangu na kada mwenzangu chamani,pia Mwenyekiti wangu na Rais wangu wa zamani,natumai uko salama. Pole kwa mihangaiko na purukushani za kimaisha na za kikampeni. Kwanza nikupe habari kuwa mimi Mzee Tupatupa toka mkoani Ruvuma nimejiondoa kwenye timu ndogo ya kamepeni za Dr. Magufuli. Wewe na wenzako,na aina mpya yenu ya siasa za kejeli na 'mipasho' mmeniondoa kampenini.

Leo,sikuja kuchambua kilichosemwa Jangwani siku ya Jumamosi kwa ujumla wake. Nimekuandikia kukuuliza swali moja tu mtani wangu na kaka yangu Ben. Umesema kuwa chama au vyama vinavyojiita ni vya ukombozi, wakati ukombozi wa Tanzania ulishapatikana, ni wapumbavu na malofa. Ukasema kuwa ukombozi ulipatikana kwa harakati za TANU na ASP ambazo zimezaa CCM. Nimekuelewa kivyangu.

Sasa, kaka Ben, chama kinachojiita CHAMA CHA MAPINDUZI, wakati mapinduzi yalishafanyika huko Zanzibar mwaka 1964 na kwasasa hakuna mapinduzi mengine kinaitwaje na waliomo humo waitwaje? Tafadhali tuchagulie jina sisi wanachama na wafuasi wa chama cha mapinduzi ambayo kwasasa hayapo tena!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Undumilakuwili

$
0
0
Wakati CCM wanazindua kampeni zao pale jangwani walizidisha muda ya ule unaokubalika wa saa 12 jioni hatukuona kalipio lolote lile toka NEC kuwa CCM walivunja kanuni. Wapinzani walipoanza kuwatambelea wapiga kura wao NEC imeamka usingizini na kudai wamevunja kanuni. Tunaomba NEC popote pale walipo wanijibu hili kwa ushahidi ni lini waliwaandikia CCM kuvunja kanuni

Nuh Mziwanda Azidi Kumkana Wema,Afunguka Haya Redioni

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva,Nuh Mziwanda amemkana tena staa wa Bongo Movie,Wema Sepetu kuwa hajawahi kumtongoza na sauti iliyorekodiwa kwenye simu akimtongoza mwigizaji huyo siyo yake.

Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM,alipokuwa akiachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Hadithi’ alisema kuwa Wema hakuwa na nia nzuri na penzi lake na Shilole na alitaka kuwagombanisha na mpenzi wake huyo.

Sijawahi kumtongoza Wema na hakuwa na nia nzuri na penzi langu na Shilole alitaka kutugombanisha na nasisitiza ile sauti haikuwa yangu,’’alisema Nuh Mziwanda.

cloudsfm.com

Ombi la Ukawa Kufanya Mkutano Jagwani Jumamosi hii 29 Agosti Lakataliwa...

$
0
0

Jiji la Dar es Salaam wamemzuia Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa kuzindua kampeni yake kwenye viwanja vya Jangwani Jumamosi ya 29 Agosti, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia amesema jiji umewagomea kufanya uzinduzi huo Jangwani kwa madai kuwa tayari kuna mtu mwingine ambaye ameshalipia uwanja huo.
Mbatia anasema pamoja na kufanya juhudi za kuomba kutajiwa aliyelipia uwanja huo ili wazungumze naye, Jiji walikataa.
Mbatia anasema viongozi wengine wa UKAWA wanashughulikia suala hilo ikiwa pamoja na kumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Damian Lubuva kuingilia kati.

Ray Aangua Kilio Ukumbini!..Kisa Mshindi wa TMT Kufanana na Kanumba..Kisa Kizima Hichi Hapa

$
0
0
BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta, jijini Dar kulipokuwa na fainali za Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki 10 ndiyo walikuwa wakiwania kitita cha shilingi milioni 50.

Mara baada ya mshindi wa shindano hilo kutangazwa, ukumbi mzima ulizizima kwa kelele za furaha na kwenda kumpongeza Dennis Laswai aliyeibuka kidedea na wengi walikubaliana kuwa ni haki yake kutokana na kufanya vizuri.

Wakati mshindi na mashabiki wake wakiendelea kufurahia ushindi, kundi la vijana lilipanda jukwaani wakiwa wameshika fulana yenye picha ya marehemu Kanumba huku wakisema mrithi wake amepatikana.

Ndipo ghafla, Ray ambaye alikuwa na upinzani wa kisanii na muigizaji huyo, alipoanza kumwaga machozi hadharani na kujikuta amezungukwa na watu wakimshangaa.

“Jamani mrithi wa Kanumba amepatikana rasmi baada ya miaka mitatu kuishi bila yeye, sasa jembe limerejea tena, mama yetu hapaswi kuwa na simanzi kila siku,” kijana mmoja alisikika akisema huku akienda kumshika mkono mama Kanumba.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Ray baada ya mmoja wa vijana hao kumfuata na kumuonesha fulana hiyo ambapo alizidisha kilio kiasi cha wenzake kumfuata na kumtuliza ili awe katika hali ya kawaida.

Mtu mmoja ukumbini hapo alibeza kilio hicho, akisema hiyo yote ilitokana na kuzidisha ‘kiburudisho’ na wala haikuwa kwa sababu ya kummiss sana marehemu kwani hawakuwahi kuwa na ukaribu wa kiwango hicho.

“Ray hana lolote, pale amezidisha kiburudisho tu, hakuwa na mapenzi na Kanumba kiasi hicho mpaka leo hii alie vile, ni usanii tu hakuna lolote. Wapo watu wa kulizwa na kitu kama kile na si yeye, halafu Ray huwa hana ushirikiano mzuri na wasanii wenzie hasa wa kiume,” alisema mtu huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Kwa upande wake Ray alisema kilichomtoa machozi ni ukweli kwamba mshindi ana kipaji cha hali ya juu na yeye binafsi alipenda ushindi wake kiasi kwamba mawazo yake yalimfikisha mbali.

Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Mayasa Mariwata na Musa Mateja.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images