Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

MASHEIKH Sita wa Tanzania Waliotekwa na Waasi DRC Waachiwa

0
0
MASHEIKH sita wa Tanzania waliochukuliwa mateka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameachiwa huru usiku wa kuamkia jana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Liberata Mulamula, alisema Balozi wa Tanzania nchini DRC kwa sasa yupo njiani kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Goma kwa ajili ya kuwaona mateka hao.

Alisema taarifa za kutekwa watu hao zilitolewa mwanzoni mwa Agosti mwaka huu ambapo Serikali ilifanya juhudi ya kufuatilia na kufanya uchunguzi juu ya taarifa hizo.

Mulamula alisema  inasemekena watu hao wa taasisi ya kuhubiri dini ya Kiislamu walitekwa na kikundi cha waasi ambapo hadi sasa hakijajulikana.

Alisema watekaji wao walidai wapewe kiasi cha dola za Marekani 40,000 (sawa na Sh milioni 128.7 ) ili wawaachie Watanzania hao huru ambapo waliwaomba kupunguziwa hadi kufikia dola 20,000.

“Nchi yetu haijawahi kutokea kukamatwa mateka, lakini tunaipongeza Serikali ya DRC kulifuatilia hili na kutupatia taarifa,” alisema Mulamula.

Aliwataka wananchi wanaokwenda nchi za ugenini kutoa taarifa katika ubalozi au Wizara ya Mambo ya Ndani ili waweze kutambua haraka linapotokea tatizo kama hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya nje Zanzibar, Silima Kombo Haji, alisema watekaji hao walitumia ujanja wa kupiga simu kwa ndugu zao pamoja na watu wa karibu na Kijiji cha Goma.

Alisema juzi watekaji hao walikuwa wakipiga simu wakisisitiza kuwa muda umekwisha, hivyo fedha hizo zipelekwe haraka kabla hawajawadhuru.

Diamond Platnumz Admits Why Tiffah Dangote's Face Will Be Shown After 40 Days.

0
0


In a new interview with Dina Marious on E-EF Diamond admitted they decided not to reveal their daughter Tiffah Dangote's face beacause they were in talks with some companies which want to endorse the celebrity kid.
Diamond said that they will show her face after 40 days as they agreed with the companies because they wany to advertise their products through Tiffah's first photos which are expected to go viral on social media, blogs, even TVs and magazines.

"We were waiting for some companies which wanted to endorse since the photos showing her face will go viral" said Diamond.


Ukatili wa Kutisha!!! Mwanafunzi Achinjwa na Kutolewa Utumbo Baada ya Kupora Simu

0
0
Kijana anayedaiwa ni denti wa sekondari aliyetajwa kwa jina la Manka Omari (19), mkazi wa Golani-Kimara jijini Dar, anadaiwa kuuawa kikatili kwa kuchinjwa na kutolewa utumbo na watu wenye hasira kali akituhumiwa kupora simu kutoka kwa mtu.

Tukio hilo lililozizima maeneo hayo lilitokea usiku wa manane wa kuamkia Agosti 31, mwaka huu ambapo awali inaelezwa kuwa Manka alipoteza simu yake siku chache zilizopita lakini Agosti 30, aliiona akiwa nayo mtu mwingine mtaani, akamnyang’anya baada ya kutoelewana, jambo lililosababisha aitiwe kelele za mwizi.

Akizungumza na waandishi wetu, jirani aliyejitambulisha kwa jina la Mama George alisema kuwa, Manka alikimbia na kujificha nyumbani kwao ambapo ghafla wananchi wenye hasira walifika kisha wakamuangushia kipigo mama huyo hadi akazimia wakimtuhumu kuwaficha wezi huku wakimtaka awatoe Manka na watoto wake wengine ili wawaue.

Akizungumza na Amani, bibi wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwanakombo alisema kuwa mjukuu wake alifika siku hiyo akiwa ana majeraha na kuwaelezea kuhusu simu yake na baadaye mwenyekiti wa mtaa huo, Laurent Mtou alifika nyumbani hapo na kuwataka siku ya pili yake wafike kwenye ofisi za serikali ya mtaa kwa ajili ya kutatua mgogoro huo huku akiondoka na simu iliyolalamikiwa.

“Baadaye, tukiwa tumelala usiku wa manane tulishtushwa na kundi la watu waliokuwa na mapanga, shoka na nondo wakiwa wanapigapiga mlango na kutishia kutuchoma moto.

“Watu hao walimtaka Manka atoke nje, tukasikia wamefika na mwenyekiti wa serikali ya mtaa, tukaona kuna usalama hivyo Manka alitoka nje na hakurudi tena hadi tuliposikia ameuawa kinyama,” alisema bibi huyo kwa uchungu huku akiangua kilio.


Naye mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Rashid alisema kuwa kaka yake aliwaambia ndugu zake kuwa hataki wauawe kwa ajili yake ndipo akatoka yeye peke yake. Rashid alisimulia kuwa alishuhudia kaka yake akicharangwa kwa mapanga kabla ya kuburuzwa akipelekwa eneo la Msauzi ambapo mwili wake ulikutwa ukiwa umeunguzwa kwa moto na kukatwa kichwa.


Akizungumzia tuhuma za kuhusishwa kwenye tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Golani, Laurent Mtou alisema: “Namtambua Manka fika na siku ya tukio nilikwenda nyumbani kwao kusuluhisha na kuchukua simu na nilimchukua na yeye ili twende naye ofisini kwangu akiwa na yule aliyelalamika kuporwa simu.


“Sasa Manka akaambiwa na wenzake kuwa ninampeleka polisi ndiyo akanikimbia na kuelekea kusikojulikana.

“Leo asubuhi nikaambiwa kuna tukio la mauaji, nilipokwenda, nikamkuta ni yeye na kuna mwenzake mmoja aliokolewa na sungusungu akitaka kuuawa tukampeleka Kituo cha Polisi Mbezi, sasa sielewi mimi nahusishwaje hapo,” alisema mwenyekiti huyo na kudai kuwa watuhumiwa wanasakwa na polisi huku Manka akizikwa maeneo hayo ya Golani.


Chanzo:Gazeti la Amani

Mke Halali wa DR SLAA Rose Kamili Ajitokeza Akiwa na Watoto Halali wa Slaa na Kumchana Slaa na Kudai Ametumwa na CCM

0
0
Mbunge wa Viti  Maalumu kupitia chadema,Rose Kamili,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo jioni kuhusiana na tuhuma alizozitoa mume wake kwamba waliishi kwa maisha ya kula mihogo na familia yake ili kuhakikisha chadema inastawi na kuimarika jambo ambalo si la kweli walikuwa na maisha mazuri ya kawaida tu na kusema kuwa Dk.Slaa anapaswa awaombe radhi wataznzania kwa kufafanisha kula mihogo kuwa ni umaskini na kuongeza kwa kusema mbona ukienda katika mahoteli makubwa mihogo na viazi ipo na watu wenye pesa zao wanakula kama kawada.

akizungumzuia kuhusu matamshi aliyasema Dk.Slaa kwamba haongei na waziri mkuu mstaafu,Sumaye,mama rose kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita waziri mkuu huyo mstaafu aliomba namba za dk.slaa akampatia wakaongea vizuri bila shida yoyote ila anamshangaa juzi aliposema mbele ya waandishi wa habari kwamba hazungumzi na sumaye.
akizungumzia kuhusu kuja kwa lowassa chadema mama huyo alisema kuwa Dk.slaa alikuwepo katika kumkaribisha waziri mkuu mstaafu,Edward Lowassa kujiunga na chama hicho ni jambo la kushangaza akizungumza kwamba hakushiriki na pia wakati chokochoko hizo za kustaafu ukatibu wake alisema kuwa viongozi waandamizi wa chama cha mapinduzi walimfuata na kumshawishi kutoludi kwenye ukatibu mkuu wake huo atapewa ubunge wa kuteuliwa na rais atakayeapishwa na kupewa uwaziri katika serikali ya awamu ya tano.

Kamili alimaliza kwa kutoa rai kwa watanzania wote nchini kutomsikiliza Dk.Wilbrod Slaa na kuwasihi kuendelea kuwa na matumaini na mgombea wa urais wa Chadema,Edward Lowassa aliyesimamishwa na chama chao pamoja na umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ili kukiondoa madarakani chama tawala.
 Linus Slaa.
 Emiliana Slaa.
 Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kushoto ni mtoto wake aliyezaa na Dk.Slaa aitwaye,Emiliana Slaa.
 Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kulia ni mtoto wake, Linus Slaa.


 Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini leo

Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rose Kamili, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mume wake Dk.Wilbrod Slaa kuzungumza wakati akiwa Katibu mkuu wa chadema familia yake ilikula kwa shida kwa sababu ya kujenga chama hicho jambo ambalo si la kweli. Wengineo ni watoto wake, Linus Slaa (kulia) na Emiliana Slaa.

Lipumba, DR Slaa and Nchemba In One Table...

0
0
I can’t say anything about these pictures because of the new cyber crime low. Anyone with more information about these pictures please feel free to tell us in the comment box bellow.


Sura ya Mtoto wa Diamond itaonyeshwa Kwa Fedha Siku ya Arobaini yake

0
0
Diamond na Mtoto wake 
MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ na mpenzi wake, Zarina Hassani ‘Zari’, wamekubaliana kutoonyesha sura ya mtoto wao wa kike, Tiffah hadi atakapofikia siku arobaini tangu kuzaliwa kwake.

Alisema makubaliano ya kuendelea kumficha mtoto huyo asionekane kwa jamii yametokana na makubaliano waliyonayo na makampuni mbalimbali yanayomdhamini.

Diamond alieleza hayo juzi katika kipindi kipya cha Uhondo kinachorushwa na Redio Efm chini ya uongozi wa Dinna Marios.

Alisema yeye na Zari walikuwa katika mazungumzo ya makubaliano na baadhi ya makampuni yanayotaka kuionyesha picha ya mtoto wao huyo kwa mara ya kwanza siku hiyo ya arobaini itakapofika.

“Hayo makampuni ndiyo yataionyesha picha ya mtoto wetu kwa mara ya kwanza siku hiyo ya arobaini itakapofika ndiyo maana tumekuwa tukijitahidi kuzuia watu wasipige picha na kuzisambaza mitandaoni hadi atakapotimiza siku hizo arobaini ili mchongo wetu usivuje,’’ alifafanua Diamond.

CHADEMA Wadai Vijana Walioandamana Kumsisitiza Lowassa Amjibu Dr Slaa Walitumwa na CCM

0
0


Baada ya maandamano ya jana kumsisitizia mgombea urais kupitia CHADEMA 'Edward Lowassa' kujibu kauli za Dkt. Slaa alizotoa siku ya Jumanne, Katibu mkuu baraza la wazee taifa Bw. Roderick Lutembeka alifafanua zaidi suala hilo leo alipoitisha mkutano na Waandishi wa habari.
"Asante waandishi wa habari kwa kuitikia wito, jambo la msingi la kuwaita ni kutoa ufafanuzi kwa tukio la jana na kutoa tamko kama baraza la wazee kwa kukemea kitendo cha uvamizi katika ofisi ya CHADEMA makao makuu ambao walitumwa na Viongozi wa chama tawala CCM, viongozi wa chama tunakemea kwa kitendo cha kihuni na kihalamia kilichopangwa kupotosha amani na vijana waliodai wametumwa na viongozi ndani ya chama tawala kwa kupewa hela kuanzia sh 1000 hadi laki moja ili wavae sare za CHADEMA na kufanya maandamano kuelekea makao makuu ya chama eti kumshinikiza mgombea wa CHADEMA  ajibu hoja za Dkt. Slaa, vijana hao wakiwa kwenye sare za Chadema waliowatuma kuelekea makao makuu ya chama kufanya vurugu, tunashukuru kwa nia hiyo kwa viongozi wa CCM waliowatuma haikuweza kufanikiwa kutokana walinzi wa chama na majirani kuwathibiti waliokuwa maeneo ya ofisi, baadhi ya vijana walikamatwa na kuhojiwa na chama na  baadae kuthibitisha walipewa hela na kiongozi mmoja wa chama tawala jina tunalihifadhi ili wafanye maandamano hayo, chama kina ushahidi wa kina... Pamoja na kitendo hiki baraza la wazee tunaomba tume ya uchaguzi itoke hadharani na kukemea kitendo hiki cha aibu na kuashiria kuvunja amani kipindi hiki cha uchaguzi.
Tunawaomba wananchi wote kuwa tayari kutoa taarifa juu ya mipango yote miovu inayopangwa na watu kutaka kuvuruga amani na kutoa taarifa mapema." Roderick Lutembeka

Utata Mwanaume Aliyemvalisha Pete Jack Wolper, Picha Yavuja Mitandaoni Akiwa na Mkewe wa Ndoa

0
0

Juzi mitandaoni habari iyomake headline sana kwa upande wa wasanii ilikuwa ni habari ya Mwigizaji Jack Wolper kuvishwa pete ya uchumba.. Sasa jana Watu wameibua jipya huku instagram imetapakaa picha ikimuonyesha mwanaume aliyemvisha pete Jack Akiwa na Mkewe ikimaanisha tayari ana ndoa ..
Kitu ambacho wengi hatujaelewa na wengine wakisema labda ile ya Jack akivishwa pete ni. Movie mpya..
Picha hii hapa chini!


JOHN MAGUFULI: Polisi Atakae ua Jambazi Hata Shtakiwa

0
0

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake haitamshtaki askari polisi ikiwa ataua jambazi mwenye silaha.
Mgombea huyo alitoa ahadi hiyo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye  uwanja wa Mashujaa, mjini Mtwara.
“Katika serikali yangu askari akimpiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi. Kila mara (majambazi) wanavamia vituo vya polisi, mbona hawavamii kambi za jeshi, Jeshi la Kujenga Taifa au Ukonga FFU?, wanaona polisi wana nidhamu sasa wanawaonea na kuwaua,” alisema Magufuli.
Mgombea huyo wa urais wa CCM pia aliahidi kwamba ataboresha maslahi ya askari polisi ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na wakiwa na furaha.
Kadhalika, aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais, atahakikisha makusanyo ya kodi kwa mwezi yanaongezeka mara mbili kutoka yanayokusanywa sasa ya Sh. bilioni 900 hadi Sh. tirioni 1.8.

Mke Wa Mwanamziki Wa Nigeria Peter (PSquare) Asifiwa Na Mumewe

0
0

 SEPTEMBA 2, mwaka huu ilikuwa ni siku nzuri ya kusherehekea kuzaliwa kwa mke wa staa wa muziki nchini Naija anayeund la P-Square, Peter, Lola Omotayo ambapo staa huyo alimfagilia balaa.



Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Peter alishea na mashabiki wake kumtakia heri ya kuzaliwa kwa kuandika maneno matamu.“Maisha yangu bila ya wewe ni sawa na mto pasipo maji. Umefanya maisha yangu yawe mazuri kila muda. Wewe siyo mke wangu tu, bali ni maisha yangu.
Heri ya kuzaliwa mpenzi,” aliandika.Peter na mkewe wana watoto wawili aliozaa na Lola ambao ni Cameron na Aliona.


AUNTY EZEKIEL: Sijawahi Kutamka Kwamba Mimi ni CCM

0
0

 STAA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ‘mama Cookie’ amewajia juu wanaomsema kuwa amekikacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa hajazaliwa na chama hicho bali amezaliwa Kisarawe.

Aunt amesema kuwa hata kama huko alipo wakishindwa atakubali matokeo kwa kuwa lazima katika mchezo kuna upande utashinda na mwingine utashindwa hivyo atakubali yote.


 “Ninachojua mwisho wa siku lazima kuna mshindi na mshindwa hivyo nakubali yote kwa sababu nampenda Lowassa na sijawahi kutamka kuwa mimi ni CCM kwa kuwa sijazaliwa kwenye chama hicho, nimezaliwa kijijini kwetu Kisarawe  "alisema Aunt kwa jazba.


Shamsa: Wasanii Tusiwekeane Mabifu Kisa Siasa

0
0

STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford amewaasa wasanii kuwa wasigombane na kuwekeana mabifu kisa siasa kwani baada ya mchakato huo watarudi kukaa pamoja na kufanya kazi zao kama kawaida.

Akipiga stori na Ijumaa, Shamsa alisema mastaa kwa sasa wanagombana na kutoleana maneno machafu, kitu ambacho si kizuri kwa kazi zao kwani wote wanategemeana.

“Hiki ni kipindi cha mpito tu, mimi nawashauri mastaa wenzangu wasifikishane pabaya kisa siasa, tushindane kwa sera kupitia vyama vyetu lakini si kugombana na kutoleana maneno machafu, kesho na keshokutwa najua tutakutana tu kwenye kazi zetu tena,” alisema Shamsa.

Lilian Kamazima: Najuta Kubeba Taji 2015

0
0

Mrembo wa Tanzania 2014-2015, Lilian Kamazima amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa kuna kipindi anajuta kwa nini alijiingiza kwenye mambo ya urembo kwa mwaka huo kwani hakufaidi nafasi hiyo kutokana na adhabu ya kufungiwa ambayo ilimuathiri sana.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Lilian alisema kuwa mara nyingi unaposhiriki unakuwa na matumaini ya kushinda na baada ya hapo uweze kufanya vitu vingi kwa jamii yako kama inavyotakiwa kwani hata waliopita walifanya hivyo, lakini inapokuja kinyume huwezi kuwa sawa.

“Nilipopata taji la urembo kutoka kwa Sitti, nilikuwa na malengo mengi sana kwa jamii yangu kama walivyofanya warembo wengine, lakini nilishindwa kwa sababu ya kufungiwa kwa mashindano hayo kwani hata kama ningeamua kufanya jambo fulani nisingeweza kwa kuwa ningetamka natokea Miss Tanzania nisingepewa msaada,” alisema Lilian.

Kim Kardashian Asheherekea 45 Million IG Followers Kwa Picha ya Maziwa Yake

0
0

Usiku wa jana Kim K alipost picha hizi huku akionyesha maziwa yake (Cleavage) akiwa anasheherekea Followers Millioni 45 kwenye account yake ya instagram. Hivi hapa Tanzania kuna mtu mwenye Follower millioni kweli??...am wonders


Mwanamke Mjamzito Achezea Kichapo Cha Mbwa na Umati wa Raia Wenye Hasira Huko China

0
0


The horrific moment a young mum-to-be is tied up and savagely beaten in China because she is suspected of being a thief. A shocking video, which has emerged on social media in China, shows the pregnant woman tied to a pole with her hands behind her back.

She is only just conscious, and a man can be seen pulling her hair, while another kicks her in the face as she slumps to the ground.
The incident took place on August 29 in a village near Taizhou city, eastern China, reports Bowen Press .
The woman, known only as Ms Lu, was subjected to the brutal assault because people in the village thought she was a habitual thief, reports suggest.

 

She is said to have been caught stealing in the past, and when she reappeared in the township again it was the last straw for residents.

A large crowd gathered to watch the medieval-style punishment Ms Lu is said to be 28 years old and came from the nearby city of Ningbo.
Reports suggest she has already been charged for theft three times.

A police statement confirmed that she had broken into the home of a man named as Mr Feng on August 18 and tried to steal 900 Yuan (£90) cash.

She was caught on that occasion, but released because she is pregnant.
One villager said:
"This is not the first time she came to steal things from the village.
"Last time she was let go but then she came back.
"Otherwise she wouldn't have been beaten so brutally."
After the beating, an old woman can be seen checking if the alleged thief is alright.
She was taken to hospital, but wasn;t seriosuly hurt.

A man named as Mr Yin is said to have handed himself in for the beating.

He was given eight days in jail and a 300 Yuan (£30) fine.



UK Mirror



Tanesco Yamshtaki Askofu Gwajima Polisi

0
0

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeishtaki polisi Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kutokana na kuharibu miundombinu ya umeme katika maeneo ya shirika hilo Jumamosi iliyopita na kusababisha umeme kukatika kwa baadhi ya mikoa na Jiji la Dar es Salaam.

Kutokana na kukatika kwa umeme kwa muda huo, shirika limepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 30 ambayo ni mapato kama kungekuwepo umeme mbali na usumbufu mwingine waliopata kama kuwasha mitambo upya.

Meneja Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin alisema shirika hilo limefungua jalada namba 4397/2015 dhidi ya kanisa hilo katika Kituo cha Polisi Kimara katika Manispaa ya Kinondoni kwa sababu hiyo.

Severin alisema kuwa Agosti 29, mwaka huu kuanzia saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni, umeme ulikatika katika Jiji la Dar es Salaam na mikoa iliyoungwanishwa katika gridi ya Taifa.

Alisema baada ya uchunguzi wa kina waligundua chanzo cha kuzimika umeme siku hiyo ilikuwa ni hitilafu ya umeme iliyotokea eneo la Ubungo Chai Bora kwenye kanisa hilo la Askofu Gwajima.

“Watu wanaosadikiwa kuwa watumishi wa kanisa hilo walikuwa wakishusha kontena kwa kutumia crane (winchi) chini ya nyaya za umeme wakati wakinyanyua kontena hilo liligusa laini ya msongo mkubwa wa kilovoti 132 inayopeleka umeme Zanzibar,” alifafanua Meneja Uhusiano wa Tanesco.

Severin alieleza kuwa tukio hilo lilisababisha mlipuko mkubwa ulioambatana na kuzimika kwa kituo kikubwa cha kupoozea umeme na mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Kukatika huko kwa umeme kuliathiri shughuli za uchumi na kijamii ikiwemo mikutano ya kampeni za siasa kwa baadhi ya vyama iliyokuwa unaendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine,” alisema ofisa huyo.

Siku hiyo ilikuwa na uzinduzi wa kampeni za urais za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadhi ya watu walihusisha tukio hilo kuwa ni makusudi na hujuma za kisiasa; jambo linalothibitika si kweli.

Meneja Uhusiano wa Tanesco alisisitiza kwamba kukatika kwa umeme siku hiyo, haikuwa makusudi au kwa nia ya kuhujumu vyama vya siasa, kama ambavyo imekuwa ikielezwa na baadhi ya watu kwenye vyombo vya habari na hasa mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake, Askofu Gwajima alipoulizwa kwa simu kuhusu tuhuma hizo, alisema hana taarifa na ndiyo kwanza anazisikia kutoka kwa mwandishi, licha ya kuwepo taarifa za Tanesco kuonana na uongozi wa kanisa hilo na kuzungumzia jambo hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema hajapata taarifa hizo na atazifuatilia.

Vijana 100 Arusha Wanaomuunga Mkono Dr. Slaa Wahama UKAWA na Kujiunga ACT-Wazalendo

0
0

WANACHAMA zaidi ya 100 wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF wameandamana mjini Arusha na kuchoma moto bendera na kadi za vyama hivyo, wakimuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Watu hao waliandamana jana na maandamano hayo yamefanyika siku mbili baada ya Dk Slaa kutangaza hadharani, Dar es Salaam kuwa ameachana na siasa.

Wakiwa katika maandamano yaliyoambatana na kubeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wanachama hao wengi wao wakiwa vijana, walijiunga na Chama cha ACTWazalendo, wakidai kuwa hawawezi kuviunga mkono vyama vyao vya zamani kwa kuwa vimenunuliwa na mafisadi.

Huku wakiimba nyimbo za kuvishutumu vyama vyao vya zamani (Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF), vijana hao walidai kuwa hawako tayari kuendelea kuviunga mkono vyama hivyo kwa sababu vimeonesha wazi kuwa havina ajenda ya kuwasaidia Watanzania masikini, bali vinawakumbatia matajiri na hivyo kupoteza mwelekeo wa kisiasa.

Mmoja wa viongozi wa maandamano hayo, Hassan Juma aliyedai kuwa mwanachama wa Chadema tangu mwaka 2005, alisema chama hicho kimenunuliwa na mafisadi na kuwa hakiwezi tena kuwasemea wanyonge ambao ndio wamekuwa tegemeo lao na hivyo hawana sababu tena ya kukiunga mkno katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

“Mimi nilikuwa naamini katika sera za Chadema za kupambana na ufisadi tangu nilipojiunga nacho mwaka 2005, lakini sasa imedhihirika walikuwa wanatutumia vijana kwa ajili ya malengo yao binafsi na kwa hiari yangu nimeamua kuachana nacho na nataka kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo ambao ni tegemeo la wanyonge hivi sasa nchini,” alisema Juma akiungwa mkono na wenzake wakiwa katika ofisi za ACTWazalendo Arusha.

Mwanachama wa NCCR-Mageuzi aliyejitambulisha kwa jina la Eliphas, alisema viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekuwa na tabia ya kuwaburuza kwa kufanya maamuzi ya kuwanufaisha wao wenyewe na hilo limewachefua na wameamua kuachana na chama hicho ili kujiunga na chama chenye mwelekeo unaofanana na watu wa chini.

“Kwa hali ilivyo hivi sasa ndani ya Ukawa ni afadhali hata kule CCM ambako tulikimbia zamani kwa kuwa hakuna demokrasia kabisa, viongozi wananunuliwa ovyo, hatuna ajenda ya kuisimamia sasa ni bora tuachane na walanguzi hao wa kisiasa na tuungane na vyama ambavyo tunaona wazi kwamba vitatetea maslahi yetu.
 
“Hatuwezi tukalaani ufisadi ukiwa ndani ya CCM halafu ukija kwetu tunaukumbatia na kuuhalalisha. Tuliondoka CCM kwa sababu ya ufisadi na mizengwe na sasa tunaona kwamba viongozi wetu wameyakaribisha na kuyakumbatia bila aibu yoyote mambo hayo na kamwe hatukubaliani na hilo na ndio maana tunaondoka na wenzetu wengine wengi wapo njiani kutufuata,” alisisitiza Eliphas huku akichoma moto kadi yake ya NCCR-Mageuzi.

Miongozi mwa maneno yaliyoandikwa katika mabango waliyobeba wanachama hao ni pamoja na ‘Mbowe ameuza chama chetu kwa fisadi Papa,’ ‘Lowassa angekuwa mwanao amelawitiwa ungemwachia Babu Seya?’ na Bye bye Chadema, bakini kwa mafisadi wenu.’

Hata hivyo, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema vijana hao ni mamluki waliopangwa na CCM na kwamba wana taarifa za mikakati ya kuwanunua vijana ili waandamane wakionesha kuwa wanaipinga Chadema wakati ni mamluki tu wa kisiasa ambao hawana chochote zaidi ya kuganga njaa.

Hekaheka ya msichana wa kazi kufanyiwa unyama Oman, Wizara ya mambo ya nje imezungumza..

0
0


Baada ya Hekaheka ya binti wa kazi aitwaye Sada kupelekwa Oman kufanya kazi za ndani na kufanyiwa unyama na wenyeji wake kias chakurudi akiwa hawezi kuzungumza wala kusikia, leo Wizara ya Mambo ya nje kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu Simba Yahya amezungumza.

Simba Yahya amesema ni kweli wamekuwa wakipata malalamiko mengi  kutoka kwa ndugu wa wasichana wanaokwenda huko lakini wengine wakienda huko wanafanikiwa vizuri.

Wameweka mkataba baina ya mwajiri na msichana anayekwenda kufanya kazi, lakini wengi wa hao wasichana hawapati mikataba hiyo kwa kupitia njia za panya.

Amesema pia kwa sasa Wizara hiyo imesitisha kutoa ruhusa ya Wasichana kwenda nchi za Uarabuni kufanya kazi za ndani ..

Tamasha la MultiChoice Africa! Genevieve Nnaji na wengine ndani.

0
0


Ni utaratibu ulioanza mwaka 2014 kwa kampuni ya Multichoice kukutana na Waandishi wa habari/Watangazaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuonyesha na kuyazungumzia kwa upana vipindi na mengine mengi yanayopatikana kupitia bidhaa yake ya DStv.

Tamasha hili linafanyika kwa wiki nzima kwenye kisiwa cha Mauritius kuanzia September 1 -6 likiitwa MultiChoice Africa Content Showcase Extravaganza ambalo mwaka huu limehudhuriwa na Waandishi mbalimbali wakiwemo wa Tanzania pamoja na mastaa kutoka nchi mbalimbali wakiwemo Genevieve Nnaji, Ramsey Noah na Mr. Flavour wa Nigeria.

MC alikua IK na Eku



Moja ya vitu alivyozungumza C.E.O wa MultiChoice Tim Jackobs ni kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma kwa ubora na kuendeleza malengo yake makubwa ya kuhakikisha kila mteja anapata zaidi ya matarajio yake kwenye TV.

Ugeni mwingine kwenye familia ya Mr Blue…

0
0

Msanii wa muziki wa Bongo Flava Mr Blue ana sababu kubwa sana ya kufurahia siku hii ya leo, dakika chache zilizopita Mr Blue ameshare na sisi furaha yake kubwa ya kumkaribisha mtoto wake pili duniani… kupitia Instagram yake Mr Blue amepost picha ya mtoto wake na ujumbe wa shukrani unaosema..

>>>>>“Alhamdulilahi Mungu ni mwema sana sana… hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuabudu kumtukuza na kumshukuru, namshukuru sana Mungu wangu na nashukuru pia mke wangu @wahyda_bysers_heart kwa kuniletea zawadi nyingine nzuri… nimepata mtoto mwingine wa kike ndugu zangu anaitwa #khairriyaaa… ahsante Mungu kwa kunipa baba na mama wa kunilea tena uzeeni…”<<< @mrbluebyser1988.



hONGERA  BLUE!

Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images