Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104664 articles
Browse latest View live

Vijana 100 Arusha Wanaomuunga Mkono Dr. Slaa Wahama UKAWA na Kujiunga ACT-Wazalendo

$
0
0

WANACHAMA zaidi ya 100 wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF wameandamana mjini Arusha na kuchoma moto bendera na kadi za vyama hivyo, wakimuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Watu hao waliandamana jana na maandamano hayo yamefanyika siku mbili baada ya Dk Slaa kutangaza hadharani, Dar es Salaam kuwa ameachana na siasa.

Wakiwa katika maandamano yaliyoambatana na kubeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wanachama hao wengi wao wakiwa vijana, walijiunga na Chama cha ACTWazalendo, wakidai kuwa hawawezi kuviunga mkono vyama vyao vya zamani kwa kuwa vimenunuliwa na mafisadi.

Huku wakiimba nyimbo za kuvishutumu vyama vyao vya zamani (Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF), vijana hao walidai kuwa hawako tayari kuendelea kuviunga mkono vyama hivyo kwa sababu vimeonesha wazi kuwa havina ajenda ya kuwasaidia Watanzania masikini, bali vinawakumbatia matajiri na hivyo kupoteza mwelekeo wa kisiasa.

Mmoja wa viongozi wa maandamano hayo, Hassan Juma aliyedai kuwa mwanachama wa Chadema tangu mwaka 2005, alisema chama hicho kimenunuliwa na mafisadi na kuwa hakiwezi tena kuwasemea wanyonge ambao ndio wamekuwa tegemeo lao na hivyo hawana sababu tena ya kukiunga mkno katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

“Mimi nilikuwa naamini katika sera za Chadema za kupambana na ufisadi tangu nilipojiunga nacho mwaka 2005, lakini sasa imedhihirika walikuwa wanatutumia vijana kwa ajili ya malengo yao binafsi na kwa hiari yangu nimeamua kuachana nacho na nataka kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo ambao ni tegemeo la wanyonge hivi sasa nchini,” alisema Juma akiungwa mkono na wenzake wakiwa katika ofisi za ACTWazalendo Arusha.

Mwanachama wa NCCR-Mageuzi aliyejitambulisha kwa jina la Eliphas, alisema viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekuwa na tabia ya kuwaburuza kwa kufanya maamuzi ya kuwanufaisha wao wenyewe na hilo limewachefua na wameamua kuachana na chama hicho ili kujiunga na chama chenye mwelekeo unaofanana na watu wa chini.

“Kwa hali ilivyo hivi sasa ndani ya Ukawa ni afadhali hata kule CCM ambako tulikimbia zamani kwa kuwa hakuna demokrasia kabisa, viongozi wananunuliwa ovyo, hatuna ajenda ya kuisimamia sasa ni bora tuachane na walanguzi hao wa kisiasa na tuungane na vyama ambavyo tunaona wazi kwamba vitatetea maslahi yetu.
 
 “Hatuwezi tukalaani ufisadi ukiwa ndani ya CCM halafu ukija kwetu tunaukumbatia na kuuhalalisha. Tuliondoka CCM kwa sababu ya ufisadi na mizengwe na sasa tunaona kwamba viongozi wetu wameyakaribisha na kuyakumbatia bila aibu yoyote mambo hayo na kamwe hatukubaliani na hilo na ndio maana tunaondoka na wenzetu wengine wengi wapo njiani kutufuata,” alisisitiza Eliphas huku akichoma moto kadi yake ya NCCR-Mageuzi.

Miongozi mwa maneno yaliyoandikwa katika mabango waliyobeba wanachama hao ni pamoja na ‘Mbowe ameuza chama chetu kwa fisadi Papa,’ ‘Lowassa angekuwa mwanao amelawitiwa ungemwachia Babu Seya?’ na Bye bye Chadema, bakini kwa mafisadi wenu.’

Hata hivyo, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema vijana hao ni mamluki waliopangwa na CCM na kwamba wana taarifa za mikakati ya kuwanunua vijana ili waandamane wakionesha kuwa wanaipinga Chadema wakati ni mamluki tu wa kisiasa ambao hawana chochote zaidi ya kuganga njaa.

Tanesco Yamshtaki Askofu Gwajima Polisi

$
0
0

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeishtaki polisi Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kutokana na kuharibu miundombinu ya umeme katika maeneo ya shirika hilo Jumamosi iliyopita na kusababisha umeme kukatika kwa baadhi ya mikoa na Jiji la Dar es Salaam.

Kutokana na kukatika kwa umeme kwa muda huo, shirika limepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 30 ambayo ni mapato kama kungekuwepo umeme mbali na usumbufu mwingine waliopata kama kuwasha mitambo upya.

Meneja Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin alisema shirika hilo limefungua jalada namba 4397/2015 dhidi ya kanisa hilo katika Kituo cha Polisi Kimara katika Manispaa ya Kinondoni kwa sababu hiyo.

Severin alisema kuwa Agosti 29, mwaka huu kuanzia saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni, umeme ulikatika katika Jiji la Dar es Salaam na mikoa iliyoungwanishwa katika gridi ya Taifa.

Alisema baada ya uchunguzi wa kina waligundua chanzo cha kuzimika umeme siku hiyo ilikuwa ni hitilafu ya umeme iliyotokea eneo la Ubungo Chai Bora kwenye kanisa hilo la Askofu Gwajima.

“Watu wanaosadikiwa kuwa watumishi wa kanisa hilo walikuwa wakishusha kontena kwa kutumia crane (winchi) chini ya nyaya za umeme wakati wakinyanyua kontena hilo liligusa laini ya msongo mkubwa wa kilovoti 132 inayopeleka umeme Zanzibar,” alifafanua Meneja Uhusiano wa Tanesco.

Severin alieleza kuwa tukio hilo lilisababisha mlipuko mkubwa ulioambatana na kuzimika kwa kituo kikubwa cha kupoozea umeme na mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Kukatika huko kwa umeme kuliathiri shughuli za uchumi na kijamii ikiwemo mikutano ya kampeni za siasa kwa baadhi ya vyama iliyokuwa unaendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine,” alisema ofisa huyo.

Siku hiyo ilikuwa na uzinduzi wa kampeni za urais za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadhi ya watu walihusisha tukio hilo kuwa ni makusudi na hujuma za kisiasa; jambo linalothibitika si kweli.

Meneja Uhusiano wa Tanesco alisisitiza kwamba kukatika kwa umeme siku hiyo, haikuwa makusudi au kwa nia ya kuhujumu vyama vya siasa, kama ambavyo imekuwa ikielezwa na baadhi ya watu kwenye vyombo vya habari na hasa mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake, Askofu Gwajima alipoulizwa kwa simu kuhusu tuhuma hizo, alisema hana taarifa na ndiyo kwanza anazisikia kutoka kwa mwandishi, licha ya kuwepo taarifa za Tanesco kuonana na uongozi wa kanisa hilo na kuzungumzia jambo hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema hajapata taarifa hizo na atazifuatilia.

Wiki Chache Baada ya Kujifungua, Zari Awashangaza Wengi...

$
0
0


Ikiwa ni wiki chache tu baada ya Zari Hassan kujifungua Tiffah, Mrembo huyo amewashangaza wengi baada ya mwili wake kurudi katika hali yake ya zamani haraka kupita kiasi, sio nwengi wanaweza kufanya hivyo. Inahitaji mazoezi na moyo sana.


Pregnant Kim Kardashian na Mwanae North West Wakiwa wamevaa Bikinis za Kufanana Beach.. PICHA

$
0
0

The two-year-old matched her mum's beach style in a mini version of pregnant Kim's black bikini,
The cute toddler was seen building sandcastles with Kim, 34, on the beautiful beach, enjoying some one-on-one time with her mum during the Kardashian-Jenner family vacation.



SOURCE: Mail Online

Gazeti la Mwanahalisi Lafungulia Rasmi.......Kubenea Ashinda Kesi Mahakama kuu

$
0
0

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita.

Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.

Katika uamuzi wa shauri lililofunguliwa mara baada ya MwanaHALISI kufungiwa, Jaji Bongole amesema gazeti hilo liko huru kuchapishwa kuanzia sasa.

Jaji huyo amesema pamoja na uamuzi huo, kampuni iliyolalamika imepewa mafao yote iliyoyaomba katika kufungua shauri hilo la mapitio ya uamuzi wa Waziri – prerogative orders.

Miongoni mwa maombi ya faida ni HHPL kulipwa gharama za kesi pamoja na fidia kutokana na hasara iliyopatikana kwa muda wote wa gazti hilo kuwa kifungoni.

Wakati Waziri alipofungia gazeti la MwanaHALISI, alieleza kwamba sababu ni kuandika habari na makala za uchochezi.

Habari hasa iliyoikera serikali hata kujilazimisha kuchukua hatua hiyo katili, ilikuwa ni iliyohusu uchunguzi wa tukio la kutekwa na kuteswa hadi karibu na kifo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (TMA), Dk. Steven Ulimboka.

Dk. Ulimboka alikumbwa na mkasa huo mnamo Juni 2012 alipotekwa usiku eneo la Tazara, karibu na viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambako aliitwa na mtu aliyemtaja kuwa ni ofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye alikuwa na mawasiliano ya karibu naye kwa saa kadhaa siku chache na usiku huo siku ya tukio.

Daktari huyo aliyekuwa mtumishi wa taasisi ya Marekani nchini, alifika eneo la Tazara akifuatana na daktari mwenzake aitwaye Deo, ambaye mara baada ya tukio hilo, wakati wa alfajiri, alimpigia simu Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa, kumjulisha kuhusu kutekwa kwa Dk. Ulimboka.

Kufuatia habari za kuachiwa huru kwa MwanaHALISI, Mhariri huyo amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya Tanzania, kwa kuwa umethibitisha kosa la serikali la kujichukulia maamuzi mkononi chini ya kuvunja sheria ilizoahidi kuzilinda.

“NImefurahi sana kuthibitishiwa kwamba serikali ilikosea katika kufungia gazeti. Uamuzi wa jaji umesema waziri hakufuata hatua za kisheria alizopaswa kuchukua kabla ya kufungia gazeti, ikiwemo ya kuwapa wamiliki na mhariri nafasi ya kujitetea,” amsema Idrissa.

“Lakini pia uamuzi huu unatakiwa uwe funzo muhimu kwa utawala kwamba hauwezi kudumu na kudumu kwa msisitizo wa kuhifadhi na kufurahia sheria zilizopitwa na wakati ambazo miaka kadhaa nyuma zilishatangazwa kuwa ni sheria kandamizi,” alisema.

Mhariri amesema anawasiliana na mmiliki na mchapishaji wa MwanaHALISI, kampuni ya HHPL, kukamilisha taratibu za kuchapisha toleo la kwanza haraka iwezekanavyo. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa mara moja kwa wiki siku ya Jumatano.

Maneno ya Steve Nyerere baada ya msanii wa kike wa filamu kuondoka UKAWA kuhamia CCM

$
0
0

Chuchu hans alitoroka na sasa hivi amerudi nyumbani sifa ya kwanza unapotimiza miaka 18 unaruhusiwa kwenda kujitegemea lakini ukiona maisha ni magumu baba ni baba na mama ni Mama kwa hiyo sio dhambi mtoto kurudi nyumbani na mimi kama Baba na Mama Samia tumempokea Chuchu Hans katika chama cha Mapinduzi’ – Steve Nyerere

‘Chuchu Hans mpaka sasa hivi ana siku ya tano tangu tumempokea na mganga siku zote haruhusiwi kusema kwamba nani alikuja na mimi kama Mwenyekiti wa Mama ongea na Mwao Tanzania siruhusiwi kusema  wangapi wanahitaji kuja katika chama cha Mapinduzi lakini viashiria vinaonesha wangapi wanahitaji kurudi’– Steve Nyerere

.

‘Kwa hiyo Chuchu Hans kafungua milango kama Mwanamke jasiri kurudi kwa Mama yao na kaamua kurudi kwa Dkt John Pombe Magufuli sasa si dhambi hata kwa hao wengi wakiamua kurudi nyumbani huku hakuna yale maandamano, kwa hiyo ninachotaka kusema ukitaka kuishi kwa Amani cha kwanza kabisa ni lazima ujitambue na ndio maana Chuchu Hans kajitambua’ – Steve Nyerere

‘Lakini mimi nataka niwaambia wasanii wenzangu tusipotoke na hayo yansyokuja ni mchanganuo  baada ya wenzetu wakiapishwa maisha mengine yanaendelea isije kutokea tukachukua tukashindwa kufanya kazi zetu huko kwenye kazi za uigizaji naomba nilisisitize hilo’ – Steve Nyerere

Polisi Wakimbilia Kumuokoa Mtoto aliyekua Kafungiwa kwenye Gari na Kupigwa na Butwaa

$
0
0


Team ya polisi huko Oakland, California walipigiwa simu na wananchi baada ya mtoto mchanga kuonekana akiwa kaachwa kwenye gari na madirisha yakiwa yamefungwa. Ili kumuokoa mtoto huyo walivunja dirisha la gari hiyo kwa haraka na huku wakiwa tayari na madaktari wakisubiri kuokoa maisha ya mtoto huyo mchanga.

Baada ya kuingia kwenye gari, hawakuamini macho yao.



Huwezi kuamini hakua mtoto bali alikua mdoli, mdoli aliyefanana na mtoto kabisa. Mapolisi hao walimuelewa raia aliyewapigia kwasababu hata wao walipomuona walishangaa sana.

Inachekesha Beyonce, Oprah, Rihanna and Kim K Wakiwa Wamevalia Mavazi ya Kiafrika (photos)

$
0
0

Yaani haya mavazi yamebadilisha muonekano wa  Beyonce, Oprah, Rihanna and Kim K kabisa kwanza Kim sikumtambua kabisa na Rihanna komwe vepee..

Msimamizi wa Mitihani Aingiza Mkono Sehemu za Siri za Mwanafunzi wa Kike, Huwezi Kuamini Alichokikuta

$
0
0

Hii imetokea huko Nigeria baada ya Mwalimu msimamizi wa mitihani kua gumzo  baada ya kumhisi mwanafunzu kaingia kwenye chumba cha mtihani na majibu. Alikutana na  mwanafunzi huyo akichechemea na ndipo alipomshuku na kuingiza mkono wake kwenye sehemu zake za siri jambo lililowashangaza sana  wanafunzi wengine waliokua kwenye chumba hicho cha mitihani.

Alikuta karatasi yenye majibu kwenye chupi yake!!

Duu hatarii...

Ladies, See Signs That A Man Is Using You For His Own Pleasure! Walk Out If You Are Experiencing The Following Things!

$
0
0

Babes, have you ever felt like there is something wrong with your relationship? Like there is something missing? Or have you ever felt like the man is just using you? Have you ever had this gut feeling that he is not really into you? To answer your fears, here are the 7 signs that show he is just using you:-

1. He has cheated on you

When a man cheats and you found out and all that he can say is that he is sorry, then just know he doesn’t care about you, he doesn’t respect you enough not to cheat on you. He is not into you and bottom line he is using you.

Even if he begs for another chance and you give him, he would still behave in such manner. So please when a man cheats on you it means he doesn’t want you and he doesn’t deserve you. He may give excuses that he had a lapse of judgement and you should forgive him. Please don’t.

2. He doesn’t want to be seen with you in public

There are many ladies out there who have this kind of a problem. Why would a man not want to be seen with you and you are dating? Why? It doesn’t make any logic. If he is dating you, he should be happy and more eager to be seen with you in public.

If you see this kind of a sign then he has kept you as an option and doesn’t want you to destroy his chances of getting other women he likes.

Even if one day you end up going out let’s say to a club or something, he would most likely go and talk to other ladies like you aren’t there watching. If you see this just run for your life and I know you are going to find that person who would not be ashamed being seen with you.

3. His friends keep on telling you to leave him

If by any chance you are close with his friends and they keep on advising you to leave him. Then there is a red light there. If they tell you that the man is not in-love with you then please listen to them. Do not think that they want to destroy your relationship, they are just concerned. You may not know what this guy is saying whenever you are not around.

4. He constantly speaks of his ex-girlfriend

Men are complicated to know sometime, some do not open up, some do and some pretend like nothing happen. If you find a man who speaks a lot about his girlfriend, how she used to smell, how her hair was smooth, how she bought him presents then please just know you are on a wrong bus You are just a rebound and he would never take you serious. There are these extreme cases where he compares you to her and most definitely praise her.

5. He calls you when he needs you

If he calls you whenever he needs you, most definitely se’x. He most definitely is using you. This is the easiest sign to notice so please be on the lookout. If you have never sat down and have a real conversation with him, all you do is just se’x then he is using my sister. Or maybe he calls you to borrow some cash when he is low on cash

6. He doesn’t help you at all

I thought relationship was all about helping each other out and making life easier for the other person? If the man always gives an excuse whenever you ask him to help you with something and he doesn’t keep him promises then he is not into you. Even if it is a small favour you asked him to do but he always turns you down.

7. He has never bought you any present

The most romantic thing a man can do to a woman is surprise her with a present. Make her feel worth feel like a queen and real lady. This sign says he is not ready to invest in you and basically shows you that he is not sure of you. So the whole thing you are calling a relationship is just not I am not saying that a man is not allowed to check other women out but when he does it in front of his girlfriend then that’s a problem. If he checks them out and points to you to check it out also, then you have big problem on your hands lady. You can choose to leave him or stay to see him cheat on you. Your choice.

WENJE Abebwa Kifalme Mwanza

$
0
0

Wenje afurahiwa sana jijini mwanza na kubebwa jujuu kama mfalme

#TUKUTANE OCTOBER 2015

Lowassa Atikisa Kigoma, Angalia PICHA

$
0
0

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea saluti kutoka kwa Askari Polisi, wakati alipowasili kwa Helkopta, kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Jimbo la Kigoma Kusini, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015

.





Mji wa Kigoma Kusini, wakionyesha furaha yako kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.






CCM, Ukawa Jino kwa Jino

$
0
0


KAMPENI za uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, sasa umepamba moto na kuonyesha upinzani mkali wa jino kwa jino baina ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wanaoungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Risasi Jumamosi linathibitisha.Habari zilizopatikana kutoka mikoani ambako kampeni zinaendelea, zinasema watu wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano ya wagombea wa vyama vyote, ili kusikiliza sera zinazotolewa, kitu kinachoonyesha kuwa kutakuwa na upinzani mkali kwani wingi wa watu hautoi picha ya mshindi.
“Ni ngumu kubashiri, ukienda kwenye mkutano wa CCM unaweza kudhani huyu ndiye mshindi, lakini kesho unapoenda kwenye mkutano wa Ukawa, hali ni kama kule tu, Magufuli (John-CCM) anajaza watu, Lowassa (Edward, Ukawa) anajaza nyomi, watu hawatabiri,” alisema Tiom Khane, aliyejitambulisha kuwa anatoka taasisi isiyo ya kiserikali inayozunguka kufuatilia mwenendo wa kampeni.


wamehudhuria mikutano ya kampeni ya wagombea wa Ukawa na CCM katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Rukwa na Mtwara na kugundua kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na matokeo ya kushangaza, kwani hakuna dalili za ushindi wa kishindo kama ilivyopata kutokea miaka ya nyuma.
Katika nafasi ya urais, CCM inajivunia Dk. John Pombe Magufuli wakati Ukawa wanaye Edward Lowassa, watu wawili wanaosadikika kuwa mmoja wao ndiye atarithi mikoba ya Jakaya Kikwete baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo unaosubiriwa kwa hamu nchini

DK. Slaa Awavaa Maaskofu Waliojitokeza Kumjibu Kuhusu Kuhongwa Na Lowassa

$
0
0

Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa amedai kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya maaskofu kujitokeza kujibu hoja yake juu ya maaskofu kuhongwa bila kusikiliza hotuba yake.Akizungumza katika kipindi cha mahojiano maalam, Dkt. Slaa ambaye amesisitiza kauli yake aliyoitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa baadhi ya maaskofu hao wamejibu hoja yake kwenye vyombo vya habari wakati akidai hawakusikiliza hotuba yake.
Ametumia muda huo kujibu baadhi ya hoja ambazo zimeibuliwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa, Wasomi na Wanasiasa kwa ujumla tangu atangaze kuachana na siasa.
Amesema kuwa amezungumza na kiongozi mmoja wa dini, ambaye amesema amekiri kutosikiliza hotuba yake licha ya kujibu hoja yake.

UVCCM: Magufuli akubalika asilimia 85

$
0
0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeonesha mafanikio makubwa kwa mgombea wake wa urais, Dk John Magufuli kukubalika kwa wananchi katika kampeni zake mikoani, huku Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ukisema mgombea wake, Edward Lowassa anakubalika vivyo hivyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kusema imefanya tathmini ya mgombea wake urais, Dk. John Magufuli na kubaini kuwa amekubalika kwa asilimia 85 kwenye maeneo aliyopita kufanya kampeni.

Tathmini hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Katibu wa Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano wa UVCCM, Egla Mamoto kuwa baada ya Dk. Magufuli kuzunguka katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kufanya kampeni CCM imezidi kukubalika zaidi kwa wananchi.

“Wiki mbili zilizopita utafiti wetu ulionesha CCM inakubalika asilimia 78, lakini baada ya Magufuli kuanza kuzunguka maeneo mbalimbali CCM imekubalika kwa asilimia 85, hii imechangiwa na mambo mengi ukiachilia mbali rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi wa mgombea wetu,” alisema.

Alisema kilichosababisha tathmini hiyo kupanda ni kutokana na ilani ya uchaguzi mwaka huu na uwezo mkubwa wa Dk. Magufuli katika kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi.

Mamoto alisema hadi sasa Dk. Magufuli ametembelea mikoa sita ambayo ni Mbeya, Ruvuma, Njombe, Katavi, Rukwa na Mtwara pamoja na majimbo yote yaliyopo katika mikoa katika kampeni ya kuomba wananchi wamchague Oktoba 25, mwaka huu.

Alisema katika mikoa hiyo aliweza kufanya mikutano ya hadhara zaidi ya 49 na mikutano 126 ya barabarani ambayo wananchi walikuwa wakimsimamisha ili wamsalimie na kumueleza matatizo yao.

“Maeneo yote hayo amezunguka kwa kutumia mitumbwi, gari na kutembea kwa miguu kwa zaidi ya kilometa 5,900 na bado matazunguka na kutembea mikoa yote na majimbo yote,” alisema.

Lowassa kaingia mitini

Katika hatua nyingine, Mamoto alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilitoa ratiba ili kila mgombea kuwafikia wananchi na kunadai sera zao, lakini baadhi ya wagombea wamekuwa wakienda kinyume cha ratiba.

“Kwa mfano, Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameshaanza kuonesha dalili za kuchoka ma kushindwa kufika katika maeneo aliyohitajika afanye mikutano,” alisema.

Katibu huyo alisema Lowassa alitakiwa afike Ludewa (Njombe) na Tunduru (Ruvuma), ambako wananchi walikwisanyika wakimsubiri wamsikilize sera zake lakini hakuonekana.

“Jambo hili limewaudhi wananchi wale na hakika wameapa kutompa kura maana amewadharau, kutokana na kitendo cha yeye kuchagua baadhi ya maeneo muhimu ambayo ndiyo atakayoyafikia tu.

“Hali hiyo imeanza kuwatia mashaka Watanzania kuwa ni mbaguzi, amekosa hoja za kuzisimamia baada ya wimbo wa ufisadi kupamba moto kila kona, ama amechoka au ni uoga uliyowaingia kuona dalili za kutokukubalika,” alidai.

Chadema

Pia, alisema tuhuma ambazo zinasambazwa nchi nzima kuwa wao ndiyo wanapanga vurugu kwa kuwachafua Chadema si za kweli.

“CCM ni chama ambacho kinaamini katika maadili, hivi sasa tunajikita katika kutafuta kura na si kukaa na kupanga kufanya vurugu,” alisema.

Alisema Chadema wasimtafute mchawi, mchawi wanao wao wenyewe, wao wakae wasubiri ushindi wa kishindo kutoka CCM na kwamba wanaosambaza taarifa hizo wapuuzwe.

Mamoto alisema udhaifu wa wapinzani ndiyo utakaowafanya washindwe katika uchaguzi huu, kwa sababu muda mwingi wanatumia kujitetea na kujisafisha badala ya kuzungumzia matatizo ya wananchi.

Mwito kwa Watanzania

Katibu huyo alitoa mwito kwa Watanzania kuwa waungane pamoja bila kutazama tofauti zao za udini, rangi na ukabila na kuwataka watu wanaowagawa mafisadi, wala rushwa na wanaoamini kuwa wanaweza kuwanunua Watanzania wawapuuze.

Ukawa

Katika hatua nyingine, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umesema utashinda kwa asilimia 80 katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema katika uchaguzi huo hakutakuwa na ushindi wa kupishana kwa asilimia moja au mbili kama ilivyozoeleka na badala yake umoja huo kupitia mgombea wao urais, Edward Lowassa watashinda kwa kishindo.

Mbatia alisema wameendelea kufanya uchunguzi katika kila mahali ambapo hadi sasa wagombea wao wamefika na kuona namna wanavyopokelewa. Alisema umoja huo umejipanga, umejiratibu, umesimamia na kuelekeza vizuri hivyo wana uhakika wa kushinda.

Kampeni

Akizungumzia kuhusu hali ya kampeni za vyama hivyo inayoendelea katika mikoa mbalimbalali nchini, alisema tangu walivyoanza kampeni zao na hali ya kupokelewa kwao kuna matumaini makubwa ya kufanya mabadiliko.

“Kwa namna tunavyopokelewa kuna matumaini makubwa ya kushinda na kufanya mabadiliko kwani kwa umoja wetu tumesimamia mabadiliko,” alisema.

Alisema hata kule ambako iliaminika ni ngome za CCM wamekubalika na kubainisha kuwa hiyo ni raundi ya kwanza, lakini vyama vingine vitegemee cheche kwani hizo ni rasharasha.

Mweyekiti huyo alisema mbali na mwanzo huo lakini wamejipanga kuhakikisha Ukawa wanazunguka mikoa yote kwa kugawanyika kuhakikisha wanamnadi mgombea wao na kutangaza sera na ilani yao.

Agenda

Mbatia alisema kuwa pamoja na kuzunguka katika mikoa mbalimbali nchini agenda yao kuu ni sauti ya umma na umoja wa katiba ya wananchi kwani wanahitaji Watanzania wapate katiba wanayoitaka na yenye maridhiano yao.

“Tutaondoa katiba hii iliyoundwa na muungano wa ASP na Tanu kandamizi na tutaleta katiba itakayobadilisha mfumo mzima wa katiba hii kwani maendeleo yanaletwa kwa kujenga mfumo ambao mtu hawezi kuuvunja,”alisema.

Alisema kuwa ilani na agenda yao kubwa ni kuwa na katiba mpya ya Tanzania.

Uchochezi

Akizungumzia hali ya vurugu zinazojitokeza na zilizojitokeza katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, Mbatia alisema licha ya ukimya wao wanaona ni vema Serikali ikaona umuhimu wa kuangalia maslahi ya taifa na si ya chama.

“Kuna mambo hapa yametokea yanatia hasira, yanajenga chuki na kusababisha uchochezi katika imani za kidini, ukabila, ukanda, misingi ya itikadi katika vyama vya siasa na kutotenda haki katika kusimamia amani.

“Ndiyo kwanza uchaguzi umeanza sasa mambo haya tukiyaacha ukiangalia bado kuna siku nyingi hadi kuukaribia uchaguzi tunaweza kupata matatizo,” alisema.

Alisema katika hali iliyotokea Dar es Salaam juzi, vijana waliojitokeza kufanya vurugu kumpinga Lowassa huku wakijitambulisha kuwa ni vijana wa Chadema lakini cha kushangaza watu wema wamesema si wa chama hicho na badala yake ni vijana waliotengenezwa kufanya vurugu.

“Hali hii ni kama ile iliyojitokeza nchini Kenya kwa uchochezi ambapo mbali na nchi hiyo, pia katika nchi nyingi hali kama hii hutokea mara tu inapotokea chama tawala kinapoondoka madarakani,” alisema.

Hata hivyo, alisema kuwa licha ya uwepo wa matukio ya uchochezi lakini Jeshi la Polisi halichukulii hatua jambo ambalo linashangaza.

Alisema kutokana na matukio hayo hadi hivi sasa jopo la wanasheria katika umoja huo tayari wameanza kuchukua vielelezo hivyo kama ushahidi kwani mambo hayo si ya kufumbiwa macho kwani haijulikani kesho itatokea nini.

Pia aliongeza kuwa vitu vyote vinavyojitokeza katika kipindi hiki tayari wamefikisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Polisi lakini la kushangaza havichukuliwi hatua.

“Mfano Agosti 23 wakati CCM inazindua kampeni zake walimaliza saa moja kasoro lakini jana mgombea wetu wa ubunge Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amezidisha dakika 6 tu amekamatwa jamani vitendo hivi vinaongeza chuki,” alisema.

Alisema vitendo hivyo vinakiuka sheria na haki za binadamu kwa kiasi kikubwa kutokana na kutawala kwa matusi, kashfa, udhalilishaji unaofanyika katika maeneo mbalimbali na hata vituo vya habari lakini bado havichukuliwi hatua.

Mbatia alisema jambo lingine ambalo waliwahi kuliripoto katika mamlaka husika ni pamoja na kuchanwa kwa mabango ya wagombea wao pamoja na kukamatwa kwa watu wanaobandika mabango katika Mkoa wa Iringa na kukataliwa kwa baadhi ya maeneo kutoyabandika.

Alisema pamoja na mambo hayo yote wasifikiri upole wao na ukimya wao lakini ikifika wakati watasema hapana wamechoka.

“Sisi tunaambia Watanzania wasifanye vurugu pamoja na kuwasimamia vizuri lakini ikifika mahali tutawaachia Watanzania wafanye uamuzi wao. Tayari tumeitaarifu NEC, na wanasheria wetu wanashughulikia mambo haya na tutayapeleka mahakamani,” alisema Mbatia.

Aliwataka Watanzania wasichoke na kwamba CCM itakapotangaza uchochezi, uvunjifu wa amani, chuki Ukawa utatangaza amani na kudumisha umoja.

Mke Mdogo wa Dr. Slaa Naye Ajibu Mapigo......Asema Mumewe ameachana na Siasa na Anampango wa Kuwekeza Katika Shule na Hospitali

$
0
0

Hatimaye mke mdogo wa Dk. Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi, ameibuka na kujibu baadhi ya hoja ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake yeye binafsi na kwa mume wake na zaidi akisema yote yanayosemwa dhidi yao hayako katika fikra zao kwani kwa sasa baada ya kuachana na siasa wanajipanga kuelekea upande mwingine wa kuwa wawekezaji.

Akizungumza na gazeti  la  mtanzania jana, Mushumbusi aliitaja mipango yao hiyo kuwa ni pamoja na kujenga shule na hospitali.

Mushumbusi ametoa kauli hiyo wakati ambapo gharama zinazokadiriwa kufikia shilingi milioni 50 alizozitumia mume wake katika mkutano wake na waandishi wa habari mapema wiki hii zikizua mjadala mpana wa alikopata fedha hizo zote.

Pamoja na hilo, Mushumbusi ambaye anatajwa kuwa katikati ya mpango wa kumrubuni mume wake licha ya kupuuza hoja kama hizo alipoulizwa walikopata fedha za kutekeleza miradi mikubwa kama hiyo alisema zimetoka kwa watu aliodai kuwa ni marafiki zao na kiasi kingine ni asilimia 20 ya vipato vyao ambavyo walikuwa wakiviweka kwa muda mrefu.

Mushumbusi ambaye tangu Dk. Slaa azungumze na waandishi wa habari Jumanne wiki hii hajawahi kuzungumza lolote, alianza kujibu yale yaliyozungumzwa na mke mwenzake ambaye ni mke wa ndoa wa Dk Slaa aitwae Rose Kamili ambaye juzi alizungumza na vyombo vya habari na kumtupia tuhuma nzito yeye (Mushumbusi) na mume wake huyo wa zamani.

Rose alikaririwa na vyombo vya habari akimtuhumu mumewe kuwa ni muongo na anapelekeshwa na mwanamke anayeishi naye kwa sasa ambaye ni Mushumbusi.

Akijibu shutuma hizo, Mushumbusi alisema yeye ni zaidi ya siasa rahisi zinazoenezwa dhidi yake.

Alimpuuza Rose kwa kusema kuwa ameamua kuchanganya matatizo binafsi ya familia na propaganda za kisiasa, hivyo jambo hilo liko mbali na uwezo wa fikra na mipango yake kwa sasa.

Mushumbusi alisema yeye si mwanasiasa kwani ana mambo mengi anayoyafanya mbali na siasa hivyo shutuma alizotoa Rose kwa Dk. Slaa zingefaa pia kama angewaeleza Watanzania sababu za kuachwa kwake.

“I’m above with that cheap politics, you know? (Unajua niko juu ya siasa hizo rahisi?), I’m activist, I can’t deal with them and I have a lot of things to do out of politics by the way, I’m not a politician as I told you (mimi ni mwanaharakati, siwezi kushughulika nao na nina mambo mengi ya kufanya nje ya siasa, hata hivyo mimi sio mwanasiasa kama nilivyokueleza),” alisema Mushumbusi.

Mushumbusi alifafanua kuwa hivi sasa yuko mbali na mambo ya siasa na anaangalia mbele kulisaidia taifa katika nyanja za elimu, afya na uchumi.

Alisema mipango yao kwa sasa ni kujenga shule, hospitali pamoja na kuwasaidia kina mama katika masuala ya ujasiriamali.

Alisema tayari mipango yao hiyo mipya ilikwishapangwa kwa kushirikiana na Dk. Slaa.

Alisema mbali na fedha za marafiki yeye ni mfanyabiashara wa nafaka na kwa muda mrefu pamoja na mumewe wamekuwa wakiweka akiba.

Hata hivyo, wakati Mushumbusi akisema kuwa anafanya biashara ya nafaka, gazeti moja la kila siku (Si MTANZANIA) liliwahi kumkariri hivi karibuni akidai kuwa kwa sasa anafanya biashara ya mkaa.

“Brother I’m not there as they think, I’m a focused woman (Kaka sipo hapo kama wanavyofikiri, mimi ni mwanamke makini), nina mambo mengi ya kulifanyia taifa langu, nashangaa hata hiyo hoja ya kutelekeza watoto, waulizeni hao watoto kama hawapajui kwangu, huyo kijana wa kiume kila mara anakuja kwangu hata wadogo zake wanamfahamu vyema, eti  wanasema Dk. Slaa kawatelekeza wanataka awafanyie nini na wakati watoto wote hao ni above eighteen (zaidi ya miaka 18) na tayari wamezaa kila mmoja, hoja nyingine you must think big (kufikiri zaidi),” alisema Mushumbusi.

Kuhusishwa na Kinana, Lukuvi
Akijibu madai ya kutuhumiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, William Lukuvi ili kumpa maelekezo mumewe juu ya nini afanye baada ya kujiengua Chadema, Mushumbusi alikana madai hayo kwa kusema kuwa hana mawasiliano yoyote na watu hao.

“Sina mawasiliano na Kinana wala Lukuvi kwanza ni watu ambao sijawahi kufikiria hata siku moja kama nitazungumza nao, kwanza simpendi huyo Kinana,” alisema Mushumbusi.

Dk. Mwakyembe na Dk. Slaa
Kuhusu kukutana na Dk. Mwakyembe katika moja ya vyumba vya Hoteli ya Serena akiwa yeye na mume wake, Mushumbusi alikana taarifa hizo.

Hata hivyo, gazeti  la  mtanzania linafahamu kuwa Mushumbusi alikuwepo katika moja ya vyumba vya hoteli hiyo ambavyo mume wake alivitumia kukutana na Mwakyembe saa chache kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Pamoja na ukweli huo, Mushumbusi alisema hana mawasiliano na Mwakyembe ingawa alikiri mume wake kukutana naye ili kupata ufafanuzi wa baadhi ya hoja za sakata la Richmond.

“Dk alihitaji kupata ufafanuzi fulani wa hoja za Richmond, kumbuka ripoti ya Richmond iliandikwa kisheria zaidi hivyo alimuhitaji Dk. Mwakyembe kwa ajili ya kupewa ufafanuzi wa baadhi ya vipengele ndipo walipokutana saa chache kabla ya mkutano na wanahabari,” alisema.

Chanzo:  Mtanzania

Dr. Slaa Aishambulia CHADEMA Kwa Mara ya Pili.......Asisitiza Kuwa Lowassa ni Fisadi

$
0
0
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbrod Slaa amejitokeza hadharani kwa mara nyingine na kujibu watu waliojitokeza kuponda hotuba yake, aliyoitoa hivi karibuni kuwa hawana hoja zaidi ya kumtukana.

Akizungumza kupitia kituo kimoja cha Televisheni jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema madai yote, yaliyotolewa juu yake na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa Chadema na vyama vinavyounda Ukawa, baada ya hotuba aliyoitoa, hayana msingi wowote na kwamba ni kuishiwa hoja, ndio maana walimtukana badala ya kujibu hoja.

“Nashukuru hoja zangu zote hawajazijibu, sasa wanapiga tu propaganda, hata Rostam Aziz alijaribu kujibu, lakini akatukana tu kama alivyonitukana mwaka 2007 badala ya kujibu hoja na mimi nasema ufisadi ni hoja,” alisema Slaa.

Aidha, Dk Slaa alisema hawezi kumpeleka mahakamani Rostam ambaye ni kada wa CCM, ambaye amemtaka Dk Slaa ampeleke mahakamani kama anao ushahidi kuwa anaunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Slaa amesema yuko tayari kutoa ushahidi wake pale Jamhuri itakapomfungulia mashitaka. “Wale ambao hawaelewi taratibu za kesi, kuna kesi za madai ambapo mtu binafsi anafungua kesi na kesi za jinai ambazo mtu binafsi hawezi kufungua ila Jamhuri, kesi za Jamhuri mtu huwezi kufungua, wewe ni shahidi… mimi nikiitwa nitakwenda kutoa ushahidi dhidi ya Rostam Aziz,” alisema Dk Slaa.

Aidha, alisema ni kweli vijana wanataka mabadiliko na ni hoja ya msingi na pia wakulima ambao hawafaidiki na kilimo chao, wanataka mabadiliko, vivyo hivyo kwa makundi mengine.
 
 “Nimesema mimi Lowassa hafai, leo, lini ameanza kuwa rafiki wa masikini?

"Lini ameanza kuwa safi?Watanzania waache ushabiki usiofaa wapime kwa vigezo, ushabiki usio na tija utatuangamiza,” alisema Dk Slaa, akijibu hoja mbalimbali ambazo zimejitokeza baada ya hotuba yake hiyo, aliyoitoa mwanzoni mwa wiki hii baada ya kutangaza kuachana na mambo ya siasa na kubaki mshauri wa wananchi.

Akijibu shutuma dhidi yake baada ya kutuhumiwa kutoa habari za upotoshaji juu ya maaskofu, Slaa alisema alichokieleza siku ile anatangaza kujiengua kwenye siasa ni alichoambiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwamba maaskofu 30 kati ya 34 walihongwa.

“Tatizo halikuwa fedha bali askofu anaona sifa mimi kumuunga mkono mtu ambaye alitumia fedha kununua maaskofu, na Watanzania nawaomba mtulie msikurupuke na maneno bila kuyachambua, taifa linaangamia kwa sababu ya ushabiki usio na tija, nimeshtushwa na kauli yake, kiongozi anayepaswa kukemea rushwa, maovu… baba askofu piga magoti Mungu wako atazame dhamira yako,” alisema.



Dk Slaa alisema yeye ana uwezo wa kupambanua siasa na mambo mengine na kwamba ni kweli alikutana na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe katika Hoteli ya Serena na hiyo ni katika kupata taarifa alizozihitaji kwa ajili ya kazi yake ya utafiti na kwamba Mwakyembe ni chanzo cha taarifa cha kwanza na kwamba hakufanya kwa siri.

Akizungumzia picha yake ambayo ilizunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha yeye akiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema picha hiyo ni wakati wa mkutano wa vyama vya siasa na Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck alipokuja kwenye ziara ya kikazi Februari mwaka huu.

“Kwenye picha hizo ambazo zinatuonesha mimi, Mwigulu na Profesa Lipumba tukimpokea Rais wa Ujerumani alipotembelea Tanzania, leo ndio zinaletwa kuonesha eti haya ndiyo mazungumzo ya kumng’oa Slaa, naomba niwaambie warudi nyuma waangalie hizo picha ni za lini hazina uhusiano na mimi kujiondoa,” alisema Dk Slaa.

Aidha, Dk Slaa alisema kuwa kuna propaganda nyingine ambayo imetumika ambapo watu wametuma pia picha ambazo zinamuonesha akiwa kwenye ndege, ikisemekana kwamba ametoroka nchini baada ya hotuba, sio kweli.

Alikiri kusafiri lakini sio kwa kutoroka, kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu na kwamba amekuwa akipiga picha na watu kwenye ndege na kwamba picha hiyo ni ya safari ambayo alishasafiri na kurudi.

“Magazeti na mitandao wanasema Dk Slaa hayuko nchini, lakini nadhani sasa Watanzania wanaona sasa niko hapa studio Dar es Salaam na siko Marekani,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa uongo huo unaonesha ni aina gani za siasa zilizopo hapa nchini.

Alisema hoja ya wapi amepata fedha kwenda Serengeti na kuishi hotelini ni hafifu. “Nilikwenda Marekani na kukaa kwa zaidi ya miezi 12 na kutembelea majimbo 13 na sikulipiwa na mtu yoyote zaidi ya chama changu kulipia shilingi 500,000 kwa mshauri aliyeandaa nyaraka ya kunisaidia katika ziara hiyo, mbona hawakuniuliza nimepata wapi fedha hizo?”

Kubenea Kumvaa Dr. Slaa......Asema Ataanika Maovu yake Yote Watanzania Wajue

$
0
0

Katika taarifa yake kwa Mwanahalisi Online, Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) wachapishaji gazeti la MwanaHALISI, (ambaye amechimba kwa undani sakata la Richmond lililotokea mwaka 2007) amesema:

NIMEMSIKILIZA kwa makini, Dk. Willibrod Slaa, aliyeacha Ukatibu mkuu wa Chadema na katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) akizungumza katika mahojiano na kituo cha telebisheni cha Star TV.

Dk. Slaa ambaye ni msomi wa thiolojia, amemtuhumu Mgombea Urais anayewakilisha UKAWA, Edward Lowassa kwamba ni fisadi na hafai kuchaguliwa na wananchi.

Ikiwa ni mara yake ya pili kutokeza hadharani tangu aliposusa kufanya kazi za katibu mkuu katikati ya mwezi Julai mwaka huu, ameeleza kwanza Watanzania wamchague “Mgombea mwenye nafuu ya ufisadi...” akamtaja John Pombe Magufuli.

Kwa taarifa mpya aliyonayo na ambayo aliitumia katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumanne iliyopita, kuhusu sakata la Richmond, aliipata kutoka kwa Dk. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati Teule ya Bunge, juu ya Richmond.

Kubenea amesema ameshindwa kuvumilia taarifa anazozitoa Dk. Slaa kuhusu sakata hilo na sasa ataeleza anachokijua kuhusu sakata la Richmond na msukumo uliopo hata Dk. Slaa kujitokeza wakati huu wa kampeni za uchaguzi katika mlengo wa kumshambulia na kumchafua Lowassa.

“Niliamua kutojibizana na Dk. Slaa – rafiki yangu wa miaka mingi – katika mradi wake huu. Lakini kwa hapa alipofika, uvumivu umenishinda. Sitaruhusu mtu mzima, anayejiita padri na ambaye alitaka kuwa rais wetu, kuendelea kulindanganya taifa na kuwapotosha wananchi.

“Hivyo basi, nimeamua kuanzia leo hii, kukabiliana na Dk. Slaa kwa kila kona ili ukweli ufahamike. Kwa kuanzia, leo hii – Jumamosi, naelekea mkoani Mbeya ambako nitahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kyera, linaloshikiliwa na Mwakyembe, swahiba mpya wa Dk. Slaa.

“Nikiwa Mbeya nitaeleza ukweli wa kilichotokea na kile ambacho Dk. Slaa anakificha.

“Aidha, nikirejea Dar es Salaam, nimepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari, kueleza ukweli uliokamilika kuhusu Dk. Slaa na mkewe Josephine Mushumbuzi na sababu ya yeye kususia chama.”

Magufuli: Nikiwa Rais Nitachukua Mashamba Yasiyotumika

$
0
0

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kunyang’any’a mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo.
 
Alisema hayo alipozungumza na wananchi wa wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro jana.

Dk Magufuli alisema akiwa rais, kuna mambo mengi anaweza kufanya, kukabiliana na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na mojawapo ni kutoa ardhi zaidi kwaajili ya wakulima na wafugaji, ili kuondoa uhaba wa ardhi, unaosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia mifugo na kulima.

Alisema kuna watu wanamiliki maelfu ya eka za ardhi bila kulima na kwamba atanyang’any’a mashamba hayo ambayo yamehodhiwa na watu hao bila kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo.
 
Akihutubia maelfu ya wananchi, pia Dk Magufuli alisema kuwa anajivunia uzoefu wa marais wastaafu wa Awamu ya Pili mpaka Awamu ya Nne na wa Zanzibar, kwamba ndio atakaowafuata kwa ushauri akikwama popote.

Alisema hiyo ni moja ya tofauti kubwa kati yake na wagombea wengine wa urais.
 
“Nitaingia Ikulu nikiwa na washauri wazuri, nikikwama mahali nitakwenda kwa Rais Jakaya Kikwete, nikikwama nitaenda kwa mzee Benjamin Mkapa, nikikwama tena nakwenda kwa mzee Ali Hasan Mwinyi.

“Wako wengi, upo ushauri nitauchukua kutoka kwa mzee Salmin Amour (Rais Mstaafu wa Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein na kwa Amani Abeid Karume,” alisema.
 
Kutokana na fursa hiyo ya kiuongozi aliyonayo ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Dk Magufuli aliomba Watanzania wote bila kujali vyama vya siasa, makabila wala dini kumpa kura kwa wingi kwa kuwa atakuwa na washauri wazuri wenye uzoefu.

Alisema wagombea wengine, akiwemo wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa, hawataweza kupata ushauri wa washauri hao kama ilivyo rahisi kwake.

Kutokana na uhakika huo wa washauri wazoefu, Dk Magufuli alisema ndio maana baadhi ya wagombea hao wanaweza kuja na ahadi za uongo, ikiwemo ya kuondoa nyumba za tembe na za nyasi.

Aliwataka wananchi kuwapima wagombea hao katika ahadi zao, kwa kuwa baadhi walikuwepo ndani ya Serikali kwa muda mrefu, lakini walishindwa kuondoa nyumba hizo katika majimbo walikotokea.

Dk Magufuli alisema yeye hataahidi kuondoa nyumba hizo, bali anaahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi wanaofanya kazi wajenge nyumba bora.

Katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, serikali yake itatoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake na vijana.

Alisema atataka kila anayefanya kazi apate kipato kizuri kitakachomsaidia kukabiliana na mahitaji ya maisha yake, ikiwemo kujenga nyumba bora kutokana na kushushwa kwa bei za bidhaa za ujenzi.
 
Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao.

Kinana Amsafishia njia Magufuli

$
0
0


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameongoza timu ya chama hicho kumsafishia njia Mgombea Urais wao, Dk John Magufuli mkoani Kilimanjaro, huku akiwaambia wananchi wa mkoa huo kuwa mgombea huyo ndiye kiongozi anayestahili kuongoza Tanzania.

Akizindua kampeni za CCM mjini Moshi, Kinana aliongozana na mgombea ubunge wa Jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher ole Sendeka na yule wa Mtera mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaj.

Kinana alimuelezea Magufuli kuwa ni kiongozi anayestahili kuongoza Tanzania kutokana na historia yake ya uadilifu na uchapakazi katika maisha yake yote ya utendaji serikalini.

Alisema katika utendaji wake akiwa Waziri kwa miaka 20, amefanya kazi kubwa kwa uadilifu na kujituma.

Akimuelezea zaidi Magufuli, Kinana alisema mgombea huyo ameahidi Baraza dogo la Mawaziri, hajatumia fedha kupata nafasi ya kugombea urais wala hana makundi.

“Hana makundi...wapo waliochangisha fedha wamekusanya watu baadaye wanakuja kuwa mzigo.

"Yeye Hana makundi wala hana mzigo. Hajaenda wilayani ama mikoani bali alienda matawini,” alieleza Kinana ambaye pia alimuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha.

Kwa upande wake, Ole Sendeka alisema ni lazima Watanzania wawapime wagombea kwa kujua ukweli, si kwa kudanganyana na kuepuka dhambi ya ubaguzi wa aina yoyote.
Viewing all 104664 articles
Browse latest View live




Latest Images