Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mzindakaya: Msipige Kura kwa Ushabiki

$
0
0

MWANASIASA mkongwe nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Chrisant Mzindakaya amewataka Watanzania wasikubali kupiga kura kwa ushabiki. Ameonya kuwa upigaji kura kwa ushabiki, utaligharimu taifa hivyo Watanzania wapige kura wakijua wanachagua kiongozi ambaye atawakilisha nchi kitaifa na kimataifa.

Mzindakaya alisema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wake na waandishi wa habari. Alisema ameamua kujitokeza kutoa ushauri kwa Watanzania, kama mwananchi wa kawaida na pia kama kiongozi ambaye anawafahamu kwa ukaribu wagombea wote wanaowania kiti cha Urais.

“Naomba Watanzania, wapiga kura wenzangu wasikubali kupiga kura kwa ushabiki, wapige kura wakijua wanachagua kiongozi wa Mungu, kiongozi ambaye atawakilisha nchi yetu kitaifa na kimataifa, na katika hili mimi sina maslahi yoyote,” alisema Dk Mzindakaya.

Mzindakaya alisema yeye ni mstaafu baada ya kutumikia taifa kwa muda mrefu, hivyo hana maslahi yoyote binafsi katika kutoa ushauri huo kwa Watanzania, ambao ndio wapiga kura watakaomchagua kiongozi.
 
“Mimi ni mstaafu, sina maslahi yoyote katika hili, sihitaji kuteuliwa uwaziri au ukuu wa mkoa wala nafasi yoyote ile, lakini naipenda nchi yangu na ninayaona mafanikio ya nchi yangu ambayo yako waziwazi,” alisema Mzindakaya.

Dk Mzindakaya alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kuwa na mipango madhubuti ya kuliletea taifa maendeleo na kufanya mabadiliko makubwa, ambayo yanaonekana na kuwanufaisha watu wengi.
 

Lakini, alisema kuna baadhi ya watu hawapendi kuona na kusifu maendeleo ya nchi yao, badala yake wanaendelea kubeza kwamba hakuna kilichofanyika.

Alisema kuna watu wanaingiza ushabiki kwa kisingizio cha kutaka mabadiliko. Aliwashauri vijana wajue kuwa nchi hii ni mali yao, hivyo hata kama wanataka mabadiliko waangalie ni kiongozi gani wanataka kumkabidhi nchi awaletee mabadiliko.

“Vijana chungeni nchi hii ni mali yenu, ni nchi yenu msipige kura kwa ushabiki nawapeni ushauri na ushauri huu hauna gharama, ila usipozingatiwa mtakuja kuona gharama yake baadaye, sisi ni wazee tumetumikia taifa hili na sasa tumestaafu,” alisema.

Dk Mzindakaya alisema Ikulu ni mahali patukufu kwa sababu serikali za dunia zinatambuliwa na Mungu, hivyo Rais anamwakilisha Mungu duniani.
 
 Alisisitiza kuwa nchi inahitaji kuwa na Rais, ambaye sio tu atakuwa na uwezo mzuri wa kuongoza nchi, lakini pia awe na mikono safi.

Alisema amekuwa mbunge kwa miaka 44 na viongozi wote wanaotafuta urais, anawafahamu kwa sababu amefanya nao kazi, hivyo anajua vizuri utendaji kazi wao kwa undani zaidi.
 
 Mzindakaya alisema mamlaka ya Rais ni makubwa mno, ambayo yanahitaji mtu makini asiye na pupa na mcha Mungu, ambapo yeye alisema ukilinganisha na wagombea wengine, kwa maoni yake, anaona mgombea wa kupitia CCM, Dk John Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri.

“Tusipige kura ya ushabiki baadaye tukaja kujuta, kura ya rais inatufanya tuchague kiongozi atakayewakilisha nje pia ya mipaka ya nchi, na kwa maoni yangu naona Magufuli anafaa sana,” alisema Mzindakaya.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi ijayo, nchi hii itakuwa tajiri barani Afrika kutokana na misingi iliyowekwa na viongozi waliopita kuibua vitu, ambavyo vitapandisha uchumi wa nchi, kama vile uchimbaji wa gesi, kiwanda cha chuma cha Liganga na uzalishaji wa magadi soda.

Lipumba Akana Kutumiwa na CCM Kuvuruga Upinzani

$
0
0

Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanaodhani wanatumika CCM wamekosa mwelekeo kwani alikuwa kinara wa kuitaka itoke madarakani.

Profesa Lipumba aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alijiengua kwenye wadhifa huo kwa kile alichodai nafsi yake itamhukumu kwa kumkaribisha kundini, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Lowassa aliyejiunga na Ukawa Julai 28, amepitishwa na vyama vya Chadema, NLD, CUF na NCCR-Mageuzi kuwania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Akizungumza juzi usiku kwenye mahojiano maalumu na Kituo cha Televisheni cha Azam, Profesa Lipumba alisema wanaosema wanatumika hawana hoja kwa kuwa walipambana kuitoa CCM madarakani.

“Hivi inaingia akilini kweli? Unapambana kuitoa CCM madarakani halafu hao hao uliokuwa unawapiga, wakutumie kuitetea?,” alihoji Profesa Lipumba.

Akizungumzia msimamo wake, Profesa Lipumba alisema dhamira yake inamsuta kuendelea kubaki ndani ya umoja huo kwa kuwa bado anakumbuka mapambano waliyokuwa wakiyafanya dhidi ya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma na uadilifu huku akidai kwa sasa ajenda hiyo haipo tena kwenye upinzani.

“Hivi wapinzani watazungumzia kuhusu ufisadi? wanasimamia wapi kwenye uadilifu?,” alihoji Profesa Lipumba wakati akihojiwa kwenye televisheni hiyo.

‘Ukomedi’ Wamsaidia Kingwendu Kuomba Kura Jimbo la Kisarawe

$
0
0


Mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe kupitia Cuf, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ juzi alikuwa kivutio wakati akitambulishwa na mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri, Juma Duni Haji.

Juma Duni Haji ni mgombea mwenza wa Edward Lowassa anayegombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, lakini wakiwa chini ya mwamvuli wa vyama vinavyounda Ukawa (Chadema, Nccr-Mageuzi, Cuf na NLD).

Kingwendu ambaye ni msanii wa fani ya uchekeshaji (komedi), alitumia fani hiyo kuomba kura pale alipotambulishwa na mgombea mwenza Juma Duni Haji.

Huku akitumia fani yake ya uchekeshaji, dakika sita alizopewa kuomba kura alizitumia vizuri kwa kuiteka hadhara alipoingiza maneno ya uchekeshaji kwa kusema; “Jamani ndugu zangu ebu niangalieni mie, mbunge nameremeta kwa raha zangu,” alianza hivyo huku macho akiyatoa nje mithili ya mtu aliyepatwa mshtuko wa shoti ya umeme.

“Hebu angalieni jamani yaani wametumwemwenya mwemwenya kama panya tangu uhuru,” alisema huku akiangusha kicheko.

Kila kauli aliyoitoa meza kuu ya mgombea mwenza Juma Duni Haji, ilikuwa ni vicheko tu huku maelfu ya waliofurika viwanjani hapo akimshangilia kwa nguvu na kelele.

“Angalia vijana mtaani wamebadilika kuwa omba omba yaani ukiwapita tu kidogo wanakudakia, oyaaa sasa kaka unatuachaje, tupoze basi braza...yaani tunatembea kwa wasi wasi mtaani,kumbe tatizo ni ajira hakuna na CCM bado wanatuongoza,” alisema na kuongeza:

“Hebu angalia ukitoa na gunia moja tu la mkaa kwenye gari, labda unatoka kusalimia unadakwa na watu wa malia asili unaombwa ushuru, jama mkaa nimepewa zawadi harafu mnaniomba ushuru inakuwaje?.

“Jamani CCM ni sumu kali tena haifai kabisa..., tusifanye makosa kabisa mwaka huu, angalia barabara zimejaa vumbi yaani ukitembea kidogo tu vumbi linakujaa!”

Kilichobadilika kwake ni mavazi tu katika mwonekano wake, lakini bado ni mchekeshaji aliyeamua kutumia nafasi hiyo hiyo kufikisha ujumbe na kujenga hoja za kuishawishi jamii ya wana-Kisarawe kumpigia kura Oktoba 25.

Magufuli awahakikishia neema wahandisi wazawa

$
0
0

Waziri  wa Ujenzi, Dk John Magufuli amewahakikisha wahandisi kwamba endapo atachaguliwa kuwa Rais wa serikali ya Awamu ya Tano hatawaangusha na atahakikisha anawatumia vyema kwa ajili ya kujenga uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati.

Dk Magufuli ambaye pia ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2015 yaliyowashirikisha wahandisi kutoka ndani na nje ya nchi.

“Nawahakikishia wahandisi Mungu akijaalia kule mbele siwezi kuwaangusha, siku za nyuma nilikuwa naagizwa ila sasa nitakuwa naagiza mimi, hivyo msiwe na wasiwasi na maamuzi nitakayoagiza na kufanya yatakuwa kwa faida ya wahandisi na Watanzania wote,” alisema.

Alisema amekuwa serikalini miaka 15 na amekuwa wizara ya ujenzi na katika miaka hiyo maisha yake yamekuwa na uhusiano mkubwa na wahandisi na amejifunza mengi kupitia wao na ni sekta ambayo anatambua manufaa yake na changamoto zake, hivyo hataweza kuwaacha.

“Duniani popote sehemu iliyofanikiwa ni sehemu ambayo palikuwa na wahandisi na wametumiwa vizuri, hivyo nami nitahakikisha nawatumia sana katika kujenga uchumi na tunataka kuhakikisha sekta ya maji na viwanda inakuwa,” alisema.

Aidha alisema endapo akichaguliwa ataanzisha mamlaka katika halmashauri itakayohusu masuala ya wahandisi kama ilivyo Tanroads ili kuwawezesha kupata bajeti yao watakayoisimamia wenyewe bila kuingiliwa na wanasiasa.

Aliongeza kuwa, “pamoja na kwamba sijaja kuwaomba kura ila ni vyema mkamchagua mtu anayewafahamu wahandisi vizuri maana hatawaangusha… lakini naomba niwaombe kura msije mkasema sikuwaomba, naombeni kura zenu”.

Aliwakemea baadhi ya wahandisi ambao wamekuwa wakiharibu sifa ya wahandisi kwa kufanya kazi chini ya kiwango na kuwataka kubadilika na kufanya kazi kwa weledi ili kuendelea kujenga sifa nzuri na kupata kazi nyingi zaidi.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Joseph Nyamuhanga alisema tangu mwaka 2005-2015 ujenzi wa barabara umeimarika ambapo barabara nyingi zimejengwa na zingine zipo katika hatua mbalimbali.

Alisema katika kipindi hicho wamejenga madaraja makubwa 12 na yamekamilika pamoja na madogo 7,200 na mengine saba yanaendelea kujengwa likiwemo la Kigamboni na Kilombero.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Profesa Ninatubu Lema alisema wamejipanga kuendelea kulitumikia taifa ili ifikapo 2025 waweze kujivunia kulitoa taifa kutoka uchumi wa chini kwenda wa kati.

Mabango ya LOWASSA Yazua Kizaazaa

$
0
0

Mabango yenye picha ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, yanayoendelea kubandikwa katika maeneo mbalimbali nchini yamezua kizaazaa, baada ya mengine kuondolewa na wale wanaofanya kazi ya kuyaweka kutishwa na hata kuwekwa ndani na Jeshi la Polisi.

Hali hiyo imejitokeza mkoani Iringa, ambako vijana wanaofanya kazi ya kuweka mabango hayo waliwekwa ndani na Jeshi la Polisi na jijini Dar es Salaam ambako bango lililokuwa limewekwa katika Soko la Kariakoo liliondolewa saa chache tu baada ya kubandikwa na hivyo kuzua mjadala kila kona.

Wakati wale waliokamatwa mkoani Iringa wakidaiwa kuwekwa ndani pasipokuwa na sababu yoyote hadi pale walipotolewa na maofisa wa Chadema, Jijini Dar es Salaam bango hilo liliondolewa na uongozi wa Soko la Kariakoo kwa madai ya kubandikwa kimakosa.

Juzi saa 12 jioni wafanyakazi wa kampuni ya Platnum Media Co. Ltd walifika sokoni hapo na kuanza kubandika bango hilo lililokuwa na picha ya Lowassa, ikiambatana na maandishi yanayosomeka; ‘Edward Lowassa…Ni wakati wa mabadiliko’.

Wakati bango hilo likibandikwa umati mkubwa ulikusanyika karibu na eneo hilo na kuanza kushangilia, huku wengine wakiimba “Rais…rais…rais”.

Akizungumza na mtandao  huu, Meneja wa Soko la Kariakoo, Florens Seiya, alisema yeye ndiye aliyetoa amri ya kuondolewa kwa bango hilo kwa kuwa soko hilo ni taasisi ya umma na hairuhusiwi kuwekwa mabango ya kampeni.

“Ni kweli tunamfahamu aliyebandika bango hilo, ni mtu ambaye tuna mkataba naye wa kutumia ubao huo kubandika mabango, lakini hili lilibandikwa kimakosa bila kutushirikisha,” alisema Seiya.

Alisema katika mkataba wa soko hilo na kampuni ya Platnum Media Co. Ltd, kifungu cha sita kinamtaka aonyeshe maudhui yaliyomo katika mabango kabla ya kubandika, kitu ambacho yeye (Platnum) hakufanya.

“Jana (juzi) baada ya kufunga ofisi na kuondoka ndipo alipofika na kuanza kuweka bango hilo, jambo lililofanya watu wakusanyike kwa wingi utafikiri pana mkutano wa siasa huku wengine wakishangilia,” alisema Seiya.

Alisema kutokana na soko hilo kuwa ni taasisi ya umma, hairuhusiwi kuweka tangazo lolote linalohusu kampeni za kisiasa kwa kuwa wao hawafungamani na chama chochote.

“Hebu angalia mwenyewe (huku akionyesha rekodi ya video ambayo inaonyesha watu walivyojaa huku wakishangilia wakati bango hilo likiwekwa) nani angeweza kuilinda amani mahali hapa,” alisema.

Aliongeza kuwa hata hivyo, wamemwandikia barua mteja wao huyo, Platnum ajieleze kwa nini alivunja kifungu hicho kinachomtaka apeleke maudhui kabla ya kubandika chochote.

“Kifungu cha sita cha mkataba kinasema kuwa soko la Kariakoo lina haki ya kukataa matangazo yasiyoruhusiwa kisheria na tamaduni za nchi… hawa Platnum tunafanya nao biashara kwa takribani miaka nane na hajawahi kubandika chochote bila sisi kukiona,” alisema Seiya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo walisema kuwa hizo ni njama za wana CCM kwa kuwa watu walijaa na kushangilia sana.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Hamisi Napinda, alisema saa 12 jioni wakati bango hilo likiwekwa, polisi walifika muda huo huo na baada ya wao kuondoka tu wakaliondoa.

“Jana (juzi) muda mfupi baada ya kubandikwa bango la Lowassa askari walifika na difenda mbili walipoondoka tu likabanduliwa, hii ni hujuma wanazomfanyia,” alisema Napinda.

UKAWA  kushitaki
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kufanya siasa za uchochezi na badala yake wafanye siasa safi zinazojikita katika hoja.

Umoja huo pia leo unatarajia kuwasilisha andiko la kisheria kwa Tume ya Uchaguzi (NEC) ambalo litakuwa na malalamiko kuhusu matukio na hujuma zinazoendelea katika kipindi hiki cha kampeni.

Mashehe waliotekwa DRC warejea Dar

$
0
0

MASHEHE sita waliokuwa wametekwa na waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC) wamerejea nchini jana, huku wakieleza kuwa kulitaja jina la Tanzania kumewaokoa na kifo kutoka kwa waasi hao.

Kitendo cha mashehe hao kutaja wanatokea Tanzania kimewasaidia kwani kwa mujibu wao, waasi hao walisema hawana shida na Tanzania, lakini Wakongo waliwadanganya hivyo hawawapendi.

Akizungumza baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kiongozi wa mashehe hao, Mohammed Abdallah Khamis alisema, wakiwa njiani kuelekea nchini humo walivamiwa na watu hao wakiwa na silaha za kivita kisha kutekwa na kupelekwa porini.

“Mwanzo hatukuelewa kama ni wanajeshi wa serikali au wanajeshi wa porini, tulipofika nao porini ndiyo wakajitambulisha wao ni askari wa porini na wanahitaji fedha ili watuachie ama watatuua,” alisema Khamis.

Akisimulia jinsi walivyoishi porini alisema, walikuwa wanapata tabu kwani hata chakula walikuwa wakipewa ndizi, maharage na magimbi ambayo waliambiwa wale ili wasife, huku wakati mwingine wakiteswa na waasi hao kwa kupigwa na magongo na vibao.

Alisema waasi hao walihitaji wapewe kiasi cha dola za Marekani 20,000 (zaidi ya Sh milioni 60) ili waweze kuachiwa. Khamis aliishukuru serikali ya Tanzania kwa jitihada ilizofanya ili kuhakikisha wapatikana wakiwa salama.

 “Kwa kweli tunaipongeza sana serikali ya Tanzania na DRC maana wamefanya juhudi kubwa sana za kutuokoa.

"Bora kuishi mwaka mmoja gerezani lakini si kukaa na watu wale siku moja,” alisema.

Khamis alisema, hata hivyo baadaye waliachiwa na waasi hao baada ya kuona hawana fedha lakini pia ni wazee, hivyo waliwaachia kwa huruma na hasa kwa kuzingatia hawana shida na Watanzania.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim akizungumza baada ya kuwapokea mashehe hao alisema, wakati wote serikali ilikuwa ikifuatilia suala hilo ili kujua usalama wao.

Hata hivyo, alisema kuna umuhimu kwa Watanzania wanaosafiri kwenda katika nchi tofauti kwa shughuli mbalimbali kuhakikisha wanatoa taarifa katika Balozi zilizopo katika nchi hizo ili serikali iwe na taarifa ya Watanzania hao.

“Tunaishukuru sana serikali ya Congo na jamii nzima ya watu wa Goma ambao walitoa msaada mkubwa na hata walinzi wa amani wa Congo walishiriki vizuri katika kuhakikisha mnapatikana mkiwa salama,” alisema.

Alisema kutokana na kuwa vikosi vya usalama vilikuwa vikifuatilia tukio hilo kwa ukaribu, hata baada ya kuachiwa kwa mashehe hao, vikosi hivyo vilifanikiwa kuwakamata watekaji hao.

Balozi wa Tanzania nchini DRC, Anthony Cheche alisema, baada ya kupokea taarifa hizo walifuatilia na baada ya kubaini ni Watanzania ndiyo juhudi za kuwakomboa zikaanza.

Alisema alikuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa vyombo vya habari na ndugu, jamaa na marafiki za kutaka kujua hali za mashehe hao lakini wakati mwingine alilazimika kuficha ukweli ili kuepusha kuhatarisha usalama wa mashehe hao.

“Tulipewa tahadhari kuwa kuna mazingira hatarishi, hivyo kuna baadhi ya taarifa zikitolewa zinaweza kusababisha tukawapoteza watu wetu na ndiyo sababu kuna taarifa nilikuwa nikiziminya,” alisema.

Baada ya kuachiwa kwa mashehe hao ambao wote ni wakazi wa Zanzibar, walipokewa na Jeshi la DRC na kupewa ulinzi hadi Mji wa Goma ambapo walikutana na viongozi wa mji huo pamoja na Balozi Cheche ambaye waliondoka naye hadi mjini Kigali, Rwanda kwa ajili ya kurejea nchini.

Mashehe hao ambao walienda nchini humo kwa ajili ya kutangaza dini, walirejea jana kwa ndege ya Shirika la Rwanda saa 9:55 mchana ambapo pia jana hiyohiyo waliondoka saa 12:00 kuelekea Zanzibar kwa ndege ya Shirika la Precision.

Lol. See what this person tweeted

$
0
0
hahahah dahh watu wanamambo jamani eti huyu jamaa anashangaa huyo dada anavyomuangalia akitumia deodorant ya supermarket na kuirudisha kwenye shelf! HAHAH ni kitu cha kawaida sana kwake!

Kubenea Kumvaa Dr. Slaa Asema Ataanika Maovu yake Yote Watanzania Wajue Kwanini Amehasi Chama Chake

$
0
0
Katika taarifa yake kwa Mwanahalisi Online, Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) wachapishaji gazeti la MwanaHALISI, (ambaye amechimba kwa undani sakata la Richmond lililotokea mwaka 2007) amesema:

NIMEMSIKILIZA kwa makini, Dk. Willibrod Slaa, aliyeacha Ukatibu mkuu wa Chadema na katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) akizungumza katika mahojiano na kituo cha telebisheni cha Star TV.

Dk. Slaa ambaye ni msomi wa thiolojia, amemtuhumu Mgombea Urais anayewakilisha UKAWA, Edward Lowassa kwamba ni fisadi na hafai kuchaguliwa na wananchi.

Ikiwa ni mara yake ya pili kutokeza hadharani tangu aliposusa kufanya kazi za katibu mkuu katikati ya mwezi Julai mwaka huu, ameeleza kwanza Watanzania wamchague “Mgombea mwenye nafuu ya ufisadi...” akamtaja John Pombe Magufuli.

Kwa taarifa mpya aliyonayo na ambayo aliitumia katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumanne iliyopita, kuhusu sakata la Richmond, aliipata kutoka kwa Dk. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati Teule ya Bunge, juu ya Richmond.

Kubenea amesema ameshindwa kuvumilia taarifa anazozitoa Dk. Slaa kuhusu sakata hilo na sasa ataeleza anachokijua kuhusu sakata la Richmond na msukumo uliopo hata Dk. Slaa kujitokeza wakati huu wa kampeni za uchaguzi katika mlengo wa kumshambulia na kumchafua Lowassa.

Niliamua kutojibizana na Dk. Slaa – rafiki yangu wa miaka mingi – katika mradi wake huu. Lakini kwa hapa alipofika, uvumivu umenishinda. Sitaruhusu mtu mzima, anayejiita padri na ambaye alitaka kuwa rais wetu, kuendelea kulindanganya taifa na kuwapotosha wananchi.

“Hivyo basi, nimeamua kuanzia leo hii, kukabiliana na Dk. Slaa kwa kila kona ili ukweli ufahamike. Kwa kuanzia, leo hii – Jumamosi, naelekea mkoani Mbeya ambako nitahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kyera, linaloshikiliwa na Mwakyembe, swahiba mpya wa Dk. Slaa.

Nikiwa Mbeya nitaeleza ukweli wa kilichotokea na kile ambacho Dk. Slaa anakificha.

Aidha, nikirejea Dar es Salaam, nimepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari, kueleza ukweli uliokamilika kuhusu Dk. Slaa na mkewe Josephine Mushumbuzi na sababu ya yeye kususia chama.”

Magufuli Afanya Kitu Mbaya Morogoro..Tinga Tinga Lake la Mafuriko Lafunika Vibaya Moro..Picha Hizi Hapa

$
0
0
Dr Magufuli ameongeza kuwa yeye si mwanasiasa mzuri bali ni mtendaji zaidi na kwamba baraza la mawaziri atakaloliunda litakuwa ni baraza la mawaziri la kuwatumikia wananchi kwa kutatua kero zao hasa wale wa hali ya chini na kuwataka watakaoteuliwa katika baraza lake wajipange.
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Dr Jakaya Kikwete amewahakikishia watanzania kuwa hawatajuta kumchagua Dr Magufuli kuwa rais wa awamu ya tano kwa kuwa ni mwadilifu na mzalendo na kwa kuchaguliwa kwa Dr Magufuli yeye rais Kikwete atapata usingizi mwema.
Dr Magufuli amefanya pia mikutano katika maeneo ya Ruaha, Mikumi, Kilosa na kisha Morogoro mjini ambapo baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema akiwemo mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kilosa Bwana Selemani Simba, katibu wa Chadema wilaya ya Kilosa Ibrahimu Selemani na katibu wa jimbo kilosa kati Bwana Musa Ngongi.
Mchakamchaka wa kampeni za uraisi zikizidi kupamba moto, leo hii Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM Ndugu John Makufuli ametia tim Manispaa ya Morogoro.
Akiwahutubia maelfu waliofurika katika uwanja wa Jamhuri, Ndugu Magufuli ameahidi kushughulikia tatizo la ajira kwa kuhakikisha anafufua viwanda vilivyokufa ili kuhakikisha wakazi wa Morogoro wanapata ajira.
Aidha Mh: Magufuli maarufu tingatinga, amesema katika uongozi wake atahakikisha anawashughilikia wala rushwa hasa mapapa ya rushwa ili kuhakikisha anaiweka Tanzania yenye usawa.
Mgombea Ubunge Morogoro Mjini ndugu Azizi Abood
Mzee Yusuph Makamba

Mgombea urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli amesema serikali yake itatilia mkazo suala la ukusanyaji wa kodi hasa kwa wawekezaji wa nje pamoja na kuangalia upya misamaha ya kodi ili kuiwezesha serikali kukusanya fedha nyingi zitakazosaidia kutoa huduma za kijamii kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
Dr John Pombe Magufuli ameyasema hayo katika uwanja wa amhuri uliopo mkoani Morogoro wakati akinadi sera zake kwa mamia kwa makumi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo ambapo amempongeza rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuongeza mapato ya serikali na kuongeza kuwa serikali yake itaongeza mapato ya serikali kwa kuangalia upya suala misamaha ya kodi kwa wawekezaji hususani wa kigeni.
Sehemu ya wakazi wa Morogoro




Rais Jakaya Kikwete




Ndugu John Magufuli
Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro Innocennt Karogeres


Maelfu ya wakazi wakimsikiliza Magufuli 
Nukuu:
Mzee Makamba "Lowassa alitaka kuondoka CCM tangu 1995, Nikamsihi, alishakataliwa kutokana na ufisadi wake. Namuomba kwenye mdahalo, tuliushangaa utajiri wake akiwa mdogo, Hatufai"

Innocent -" TunakuombMagufuli ukawafunge mafisadi na waliopora ardhi"

Kikwete- " Magufuli anatosha"

Jionee Basi Walilopewa Wakina Wema Sepetu Kufanyia Kampeni na CCM....Wale wa Ukawa Je ?

Petit Man Mume wa Dada Yake na Diamond Akanusha Kutoka na Wema

$
0
0
Mume wa dada yake na Diamond, Esma, Petit Man ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni ya Wema Sepetu, Endless Fame Film amekanusha kutoka kimapenzi na na bosi wake huyo.

Akizungumza kwenye kipindi cha na FNL cha EATV jana, Petit alisema anamheshimu Wema kama bosi wake.

“Niko na Wema huu ni mwaka wa nane inasemekana vitu hivyo hivyo,” alisema. “Lakini Wema akiwa tu karibu na mtu basi watu wanasema hivyo. Ilikuwa kwa Mirror wakasema hayo, maneno hayo ni maneno wanayoyaongea. Hakuna kitu chochote, Wema ni bosi wangu tena wa uhakika,” aliongeza.

Breaking News..Umeme wa Tanesco Kukatika Nchi Nzima Ndani ya Siku Saba..Kisa Gesi Kutoka Mtwara

$
0
0
BAADA ya kufika kwa gesi asilia jijini Dar es Salaam ikitokea Mtwara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), itaingiza gesi hiyo katika mitambo yote ya umeme nchini, hivyo kuanzia leo kutakuwa na ukosefu wa umeme katika mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa.

Hatua hiyo inatokana na kuzimwa mitambo yote ya umeme katika kituo kikubwa cha kuzalisha umeme cha Ubungo, Dar es Salaam kwa nia ya kuingiza gesi asilia katika mitambo huo. 
  
Imeelezwa kuwa tatizo hilo la umeme, litadumu kwa wiki nzima ambao umeme utakatika kwa saa kadhaa usiku na mchana, lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwa siku ya leo.

Akizungumza katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi One jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema mitambo yote ya umeme itazimwa ili kuingiza gesi asilia kuanza kuzalisha umeme katika kituo hicho kikubwa.

“Wiki hii umeme utakatika sana kutokana na kuunganishwa gesi kutoka Mtwara kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kuanzia kesho mitambo yote itazimwa,” alisema Mramba. 
  
Alisema kwa saa za mchana na usiku ndani ya wiki hii itakuwa mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa itakosa umeme.

Alisema baada ya majaribio ya kupitisha gesi asilia kukamilika sasa wanaingiza kwenye mitambo hiyo ili kuanza kuzalisha megawati 150 za umeme huku mitambo ya megawati 200 iliyokuwa haifanyi kazi kutokana na gesi kutotosha nayo itaanza kufanya kazi.

Alisema baada ya kuunganisha bomba hilo na umeme kuanza kuzalishwa mwishoni mwa wiki Watanzania watakuwa na uhakika wa umeme pamoja na bei ya umeme ya uhakika kwa muda mrefu.

“Kutokana na kuwa na gesi ya uhakika naamini mdhibiti ataangalia na bei inaweza kupungua ingawa siyo kesho au mapema,” alisema bosi huyo wa Tanesco.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio alisema kwa sasa mitambo ya Kinyerezi imejaa gesi na wameishaingiza gesi yenye mgandamizo wa tatu na inatakiwa kufika mgandamizo 50 hadi 51 ili kuzalisha umeme.

Alisema kwa muda wa wiki watakuwa wamefikisha mgandamizo huo kwa kuingiza polepole baada ya kufanya majaribio na kuona kuna uwezo wa kuingiza mgandamizo 90.

“Kuanzia kesho (leo) mpaka baada ya wiki mbili tutakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kwa gesi kwa kufikia mgandamizo huo wa 50,” alisisitiza na kuongeza kuwa uzalishaji huo, Serikali itaokoa dola bilioni moja zilizokuwa zikitumika kwa uzalishaji umeme wa mafuta.

Mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam ulikamilika Julai mwaka huu.

Askofu Gwajima Ashindwa Kumvumilia DR Slaa, Kesho Kumwaga Hadharani Yote ya DR Slaa Kwa Waandishi wa Habari

$
0
0
Askofu Gwajima Kesho Ametangaza kuwa Ataongealea yote aliyotuhumiwa na Dr Slaa na Kuitwa Msenga mbele ya Wahandishi wa Habari ...Askofu Gwajima Amesema Atafunguka yote anayoyajua kuhusu Dr Slaa kukimbia chama.....

CCM waumbuka Uwanja wa Taifa, January Makamba Akumbana na Nguvu ya UKAWA Baada ya Kuwaingiza Watu Bure Uwanjani

$
0
0
Juzi kwenye uwanja wa taifa katika mechi ya Stars na Nigeria bwana Januari Makamba akajitia pedezjee kulipia watu wote walokuwa nje waingie ndani bure, ilipofika half time mtangazaji wa PA ya uwanja akaanza kumnadi Januari kwa mbwembwe zote, cha ajabu uwanja mzima ulilipuka na kuanza kuzungusha mikono kuashiria mabadiliko bendera na picha za Lowassa hata sijui ziliibukia wapi huku wakiimba People Powers Ambayo ni Slogan ya UKAWA... ilikuwa patashika nguo kuchanika. Kweli Lowassa kiboko yenu.


Makamba Asema Lowassa ni Fisadi.......Aipongeza CCM Kulikata jina Lake

$
0
0
Mzee Makamba
KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amepongeza chama hicho kwa kukata jina la Edward Lowassa, katika kundi la wawania urais wa chama hicho kwa kuwa hakuwa na sifa za kuwa Rais.

Makamba amesema hayo jana katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi wa Morogoro, ambapo aliamua kutoa baadhi ya siri ambazo hazijawekwa hadharani.

Alimtuhumu Waziri Mkuu huyo wa zamani kwa ufisadi wa kupora ranchi za taifa katika mikoa ya Tanga na Arusha na kumpatia zabuni zote dada yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, ambako Lowassa alikuwa mbunge.

Akizungumzia madai ya Lowassa kwamba anachukia umasikini wa Watanzania, Makamba alisema Lowassa hachukii umasikini wa Watanzania, bali anachukia umasikini wa kwake na ndio maana hajaacha kujilimbikizia mali.

Makamba alidai kuwa Lowassa alipokuwa Waziri wa Maji na Mifugo, alipora iliyokuwa Ranchi ya Taifa ya Mkata iliyopo Tanga, ambayo imezungukwa na vijiji vya Tototwa, Mabwegere, Kiduhu na Tambara.

Katibu Mkuu huyo alihoji kama Lowassa alikuwa na uchungu na wananchi, kwa nini hakuwapa wananchi wa vijiji hivyo, badala yake akaichukua yeye na rafiki yake aliyedai ni wa Hoteli ya Nam.

Ranchi ya pili anayodaiwa kuipora ni ya Mzeri iliyopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, ambayo Makamba alidai kuwa ranchi hiyo iliyokuwa ya Ushirika, Lowassa aliipora na ina ng’ombe ambayo akiitembelea hawezi kuimaliza bila kutumia helkopta.

Makamba alikwenda mbali zaidi na kusema mkoani Arusha wakati akiwa Katibu Mtendaji wa CCM, Lowassa alipora tena ranchi nyingine ya Leteni. 

Mbali na uporaji huo wa ardhi, Makamba alisema Lowassa pia amempa dada yake, ambaye hakumtaja jina, zabuni zote za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, mpaka zabuni za kuiuzia halmashauri hiyo penseli.

Baada ya kutoa tuhuma hizo, Makamba alisema ameweka akiba maneno mengine na kumtaka Lowassa, atoke hadharani aseme hayo ili na yeye Makamba ajibu mahali pengine.

Alisema Lowassa alitaka kujitoa CCM mwaka 1995 wakati alipokatwa katika kinyang’anyiro cha kumpata mgombea urais wa CCM mkoani Dodoma.

Makamba alidai kuwa walipokwenda katika kikao cha NEC ambacho kilihudhuriwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alihoji kwa nini jina la Lowassa halikuletwa miongoni mwa wagombea watano wenye sifa.

“Nilijibiwa Lowassa ni kijana mdogo, lakini ana utajiri mkubwa ambao haujulikani alikoupata. Nikauliza ameulizwa nikajibiwa hapana nikasisitiza aulizwe maana ndio utaratibu wa chama. Lakini Mwalimu Nyerere alinijibu Lowassa akija muulize wewe mwenyewe. 

“Lowassa alipoingia katika kikao, nikaitwa Makamba ulikuwa na hoja, nikasimama nikamwambia bwana wewe Lowassa umekatwa jina lako kwa kuwa una utajiri ambao haujulikani ulipoutoa,” alidai Makamba.

Kwa mujibu wa madai ya Makamba, Lowassa alijibu kuwa ni kweli ana utajiri lakini ni kama wa watu wengine na alishindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusu alikotoa mali hizo

Sumaye: Nimenunua Shamba Kwa Kiinua Mgongo Changu, Mimi si Fisadi

$
0
0
"Mimi ni mkweli sana, ni kweli nina shamba langu Morogoro nimelinunua kwa kiinua mgongo changu.

Mimi sikutaka kuwekeza kwenye majumba kwa kuwa nilikuwa sina pesa nyingi za kununua magorofa ndio maana nikaamua kuwa mkulima"

OFFER OFFER Kutoka Markson Beauty Products..Dawa Zisizo na Madhara za Kukufanya Uwe Mrembo zaidi na Muonekano wa Kupendeza

$
0
0
OFFER,OFFER,OFFER
         MARKSON BEAUTY PRODUCTS 
Katika kusherehekea miaka kumi na nne ya kampuni hii tumetoa punguzo kubwa la bei kama shukran kwa wateja wetu. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na hazina kemikali wala madhara.
    TUNAZO ZA:-
1.Kerefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @80,000/=
2.Kuongeza shepu (hips na makalio) @120,000/=
3.Kuondoa mvi milele zisirudi @100,000/=
4.Kupunguza unene na manyama uzembe
@100,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa (a)Gely ya kupaka @90,000/=(b)Vidonge maalum @100,000/= (c)Handsome up original (@)170,000/=
6.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito @90,000/=
7.Kupunguza tumbo  (kitambi) na nyama za pembeni kwa :- (a)Dawa ya kunywa au kupaka @80,000/=  (b)Mkanda wa kawaida  @80,000/=  (c)Micro-computer belt @300,000/= 
8.Kuwa mweupe na soft mwili mzima  @90,000/= 
9.Kubust maziwa na kuyasimamisha  @90,000/=
10.Kushepu miguu na kuwa minene @90,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @80,000/=
12.Kubana uke na kuongeza hamu ya tend la ndoa kwa mwanamke @80,000/=


      NB...Matokeo ni garantii na hakikisha unapata risiti yake ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. Popote ulipo utapata huduma zetu.
      Wasiliana nasi kwa no (+255) 0767-447444  na 0714-335378

Ni Watoto na Ndugu wa Viongozi wa CCM tu Ndio Waliobaki Kuipigania Kufa na Kupona

$
0
0
Nimekuwa nikifuatilia mielekeo ya kisiasa ya viongozi wa CCM na watoto wao pamoja na watu wao wengine wa karibu kinasaba, na kushuhudia kuwa, ukiacha viongozi wenyewe wa CCM, kundi la pili ambalo linafanya kila kinachowezekana kujaribu kukinusuru chama hicho ni la watoto wa viongozi hao. Wapo watoto wengi wa viongozi wa CCM, hasa katika magroup ya WhatsApp na mitandao ya kijamii, wanapigana kufa na kupona kunusuru ulaji wa wazazi wao.

Kete yao kubwa ambayo wanaitumia kuonyesha umma kuwa upinzani haufai ni kuwa "Lowassa ni fisadi". Wengi wamejitoa ufahamu, wana uwezo mdogo wa "kureason" unaoambatana na kuchanganyikiwa, na hoja wanazojenga wakati wa malumbano ni za kushangaza mno!

Hutaamini majibu, ushindani na hoja zao pindi utakapokutana nao na kujaribu kuwaeleza kuwa tulipofika kuna haja ya mabadiliko!

Hoja zao zinatia hasira vibaya sana na kuashiria kuwa wao wana hatimiliki ya hatma ya Tanzania.

By LifeHacker/JF

Masogange, Davido ndani ya "PENZI" zito..Wanaswa Club Wakinyweshana Pombe Kwa Raha zao

$
0
0
Davido
PENZI ni kikohozi, kulificha huwezi ! Habari ya mjini kwa sasa ni mahaba niue ya muuza nyago kwenye nyimbo za wanamuziki wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange ’ na staa wa muziki nchini Nigeria ‘Naija’ , David Adedeji Adeleke ‘Davido ’ baada ya kuoneshana penzi zito hadharani .

Habari kutoka kwa chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa Masogange aliyeko Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz ’ kimelieleza gazeti hili kwamba, wawili hao kwa sasa ni wapenzi wa kupika na kupakua .

Chanzo hicho kililimwagia gazeti hili ‘ubuyu ’ kwamba , katika tukio la hivi karibuni , Davido ambaye ni staa wa Ngoma za Skelewu na Aye alitokea nchini kwao, Nigeria na kwenda kukutana na mwanadada huyo nchini Afrika Kusini ambako wanaponda raha kwa sasa .

“Yaani Masogange na Davido ni mahaba niue, wanaponda raha kwa kwenda mbele maana hata juzi tu walikuwa kwenye klabu moja hivi wanakunywa na kula pamoja huku wakifurahia vilivyo uumbaji wa Mungu .

“Davido ametinga hapa Sauz akitokea Nigeria kwa ajili tu ya kuja kukutana na Masogange ambaye mara nyingi anakuwa Sauz, ” kilisema chanzo hicho.

WANASWA KLABU , WANYWESHANA POMBE
Chanzo hicho kilienda mbele zaidi na kutuma video ambayo inamuonesha Davido akimnywesha pombe Masogange huku wakiwa wamelewa tilalila bila kujali kwamba walikuwa klabu ambako kuna watu wengi.

“Angalieni hiyo video kwa ushahidi zaidi, Davido alikuwa akimnywesha pombe kali Masogange na kuna wakati Masogange naye alikuwa akimnywesha Davido .

“Nilikuwa nao klabu wakifanyiana vitendo vya kimahaba kama kunyweshana pombe kwenye chupa moja bila kujali macho ya watu ,” kilidadavua chanzo hicho na kuongeza:

“Nakwambia huku ( Sauz ) Masogange na Davido wanakula bata hadi kuku wanaona wivu . Yaani ni mapenzi mazito usiwapimie . ”

DIAMOND ATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Davido ambaye ni rafiki wa karibu na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz ’ inadaiwa ndiye aliyemuunganishia jamaa huyo kwa Masogange kwani alikuwa akimsikia na kumuona kwa muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii na akampenda .

“Si bure , kilichomvutia Davido ni ule mzigo wa Masogange ( makalio ) maana kila siku huwa anautundika kwenye Instagram ‘so ’ akaona mtu wa kumpigia pande ni Diamond , ” kilidai chanzo hicho.

MASOGANGE ATAFUTWA
Baada ya kuzipata habari hizo na ushahidi wa video, gazeti hili lilimtafuta Masogange ambapo jitihada hizo ziligonga mwamba kutokana na mwanadada huyo kutumiwa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp bila kujibu.

Chanzo: GPL

Petitman Refutes Rumors of Dating His Boss Wema Sepetu.

$
0
0
Wema Sepetu and Petit Man
Petitman Wakuache who is a husband of Diamond Platnumz' sister Esma Platnumz has denied dating Wema Sepetu. On Friday Night Live(EATV) he admitted

"I'm with Wema for 8 years now and the same things are talked about, When Wema is seen with any man people talk the same things, even to Mirror that happened, there is nothing like that, Wema is my boss"

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images