Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Unajua Athari za Kuitana Sweet, Dear na Baby Kwa Watu Ambao Sio Wachumba ama Mke na Mume?

$
0
0
BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby!

Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine).

Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji.

HUTUMIKA WAPI HASA?
“Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.”

Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya kimapenzi 

huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo. Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile, ila iwe inatambulika vizuri na anayetamkiwa.

ATHARI SASA!

Kwa upande mwingine kuna athari za kutumia maneno hayo. Zama hizi, maneno hayo yanaonekana ya kawaida tu. Mtu yeyote anaweza kumuita yeyote mpenzi, honey, baby n.k. Hapo ndipo kwenye tatizo lenyewe.

Kwa ujumla wanawake ndiyo wanaongoza zaidi kuitana majina hayo. Wakati mwingine huenda mbali zaidi na kuwaita hata wanaume majina hayo ya kimapenzi. Si rahisi kuona athari zake kwa haraka na moja kwa moja, lakini zipo na wengi zimewasababishia matatizo. Ngoja tuone..

HUPUNGUZA THAMANI

Kama nilivyotangulia kusema awali, maneno 
niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo, basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.

Kama unaweza kumwita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.

HUKARIBISHA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Veronica, mfanyakazi wa saluni moja ya kiume iliyopo Sinza, Dar alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi saluni. 

Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kumfurahisha mteja na wakati mwingine kumfanya akupe tipu baada ya kumaliza kazi.

“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.

“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.

“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake. Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”

Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu zangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka sana – hujiona wenye bahati na mara hushawishika kuingia mapenzi.

Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo? 

ANGALIA TOFAUTI
Rafiki zangu, kati ya maneno niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano lakini wawe na undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.

Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye maana ya moja kwa moja ya kimapenzi. Umenipata? Akili za kuambiwa, changanya na zako kisha unazifanyia kazi! Chukua kinachokufaa!
Hadi wiki ijayo kwa mada nyingine. Wewe ni muhimu sana kwangu. 

TOA MAONI YAKO JE NI KWELI NIYASEMAYO?

TCRA yawaonya Channel Tena: Kwa kuonyesha 'live' maelezo ya Ask. Gwajima dhidi ya tuhuma za Dr Slaa!

$
0
0
Nimesikia sasa hivi kupitia Voice of America (Idhaa ya Kiswahili). TCRA waliwaonya Channel Ten kwa kuonyesha 'live' maelezo ya Askofu Gwajima akijibu tuhuma za kichochezi za Dr Slaa!

Hili Taifa linahitaji kufanyia 'overhaul' wala sio mabadiliko tena, maana naona kama mabadiliko hayatoshi kabisa!

Kesho yake ikumbukwe Magazeti karibu yote yameandika stori ya Gwajima tena kurasa za mbele. Sasa unaweza kujiuliza ni kwa nini kutangazwa 'live' kuwe nongwa lakini kuandikwa kusiwe 'nongwa'?

Hakika mabadiliko ni lazima nchi hii.

Televisheni ya Star TV yatuhumiwa kuchochea vurugu kwa kumkashifu Edward Lowassa

$
0
0
Kituo cha Televisheni cha StarTV ni kati ya vituo vikubwa vya habari hapa nchini kilichowahi kupata heshima ya kipekee kwa habari zake zilizokuwa hazina upendeleo.

Hata hivyo tangia kuanza kwa harakati za kampeni wiki mbili zilizopita kituo cha StarTV kimekuwa kimekuwa kikirusha matangazo yanayoonyesha ubaguzi na chuki kwa mgombea Urais kupitia UKAWA Edward Lowassa.

Tangazo la hivi karibuni linalorushwa na kituo hicho mpaka sasa ni lile linalochochoea udini likimhusisha Edward Lowassa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Watu kadhaa waliohojiwa kuhusiana na matangazo ya kituo hicho yanayokuwa ni maalum kumdhalilisha mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa wamesema kituo hicho cha StarTV kimepoteza uhalali wa kuwa chombo cha habari.

Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa Peter Kuga Mziray ameshangazwa na TCRA na Tume ya taifa ya uchaguzi NEC kunyamaza kimya bila kukemea upuuzi unaofanywa na kituo hicho.

Naye mhadhiri wa chuo kikuu Professa Gaudence Mpangala amesema mauaji ya halaiki Rwanda yalisababishwa na chombo cha habari kufanya uchochezi wa kuwagawa watu kama wanavyofanya StarTV.Amesema ni kitendo cha aibu chombo cha habari kinachojiita kinajitegemea kuegemea upande mmoja hadi kufikia kuandaa matangazo ya kukashifu mgombea wa urais anayeonekana tishio kubwa kwa watawala.

Mwananchi mmoja kutoka Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Said Yusuph alisema itafika mahali vijana wafuasi wa UKAWA Mwanza wataishiwa uvumilivu na wanaweza hata kuvamia kituo hicho kutokana na vitendo visivyo na maadili vya kumkashifu mgombea wa UKAWA Edward Lowassa.

Kituo cha StarTV kinamilikiwa na Anthony Diallo ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza.

Ni LOWASSA Kila Kona ya Nchi....Mpaka Watoto Lowassa Lowassa

$
0
0
Hakuna shaka kwamba jina la Edward Lowassa (pichani), ndilo linalozungumzwa zaidi kwenye kampeni za urais zinazoendelea sasa;iwe kwa mazuri au mabaya.

Wakati Chadema na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vikiendelea kulinadi jina la Lowassa kwa mazuri katika mikutano ya kampeni, CCM na vyama vingine vimekuwa vikeleza kuwa mgombea huyo wa Ukawa hafai kuwa Rais.

Mbali na vyama hivyo, katibu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa naye amekuwa gumzo katika siku za karibuni, akipinga chama hicho kumkubali Lowassa kuwa mgombea urais, hali kadhalika, mchambuzi maarufu wa siasa, Humphrey Polepole ambaye amekuwa akieleza mara kwa mara kuwa Ukawa imevunja misingi ya kuanzishwa kwake kwa kumpokea Lowassa na kumpa fursa hiyo.

Anavyotajwa CCM
Kwenye kampeni za CCM, Lowassa huwa hatajwi na mgombea urais wa chama hicho, Dk John Magufuli, lakini makada ambao hutangulia kuzungumza kabla yake, wamekuwa wakiporomosha tuhuma nzito kujaribu kushawishi wananchi kuwa waziri huyo mkuu wa zamani hafai.

Miongoni mwa makada hao ni mgombea ubunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alidiriki kusema kuwa Lowassa anaweza kushtakiwa wakati wowote kutokana na kuhusika kwake kwenye sakata la mkataba wa uzalishaji umeme wa dharura baina ya Serikali na kampuni ya Richmond Development ya Marekani.

Pia, katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba amekuwa akieleza udhaifu wa Lowassa katika mikutano ya hivi karibuni, huku mgombea ubunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akirusha makombora kuhusu hali ya mgombea huyo wa Ukawa.

Anavyotajwa Ukawa
Lakini Ukawa na Chadema, ambayo ilijipatia umaarufu kutokana na kupiga vita ufisadi, wamekuwa wakimtaja Lowassa wakati wakimtetea dhidi ya kashfa za ufisadi, huku wakimtangaza kwa kutumia msemo wa “Lowassa, mabadiliko; mabadiliko Lowassa”.

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ambaye alitangaza kuondoka CCM na kujiunga na harakati za Ukawa bila ya kutaja chama anachohamia, amekuwa akijaribu kuwashawishi wananchi kuwa CCM ndiko kuliko na ufisadi mwingi zaidi ya huo wanaomtuhumu Lowassa, huku akimtetea kuwa katika sakata la Richmond alifanya hivyo kwa maelekezo ya mkuu wake.

Amekuwa akijenga hoja yake kwa kutumia ufisadi uliotokea baada ya Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, kama kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya EPA, uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, utekelezaji mbovu wa Operesheni Tokomeza na uchelewashaji wa malipo ya makandarasi wa barabara ulioligharimu Taifa Sh900 bilioni.

Maoni ya wadau
Kashfa hizo na kampeni za kumnadi, zimelifanya jina la Lowassa kutajwa zaidi kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

“Ni kweli viongozi wa CCM wanatumia muda mwingi kumshambulia Lowassa,” alisema kada wa chama hicho, Aman Ngowi alipoulizwa kuhusu sababu za jina la waziri mkuu huyo kutamba kwenye karibu mikutano ya vyama vyote.

“Lakini pia, vyombo vya habari vinachangia. Viongozi wetu kwenye msafara wa mgombea wa CCM, Dk Magufuli wanaweza kuzungumza mambo mazuri 20, lakini likitajwa moja tu linalomhusu Lowassa, magazeti yote kesho yake ni Lowassa,” alisema Ngowi.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na ambaye amekuwa akisimama kwenye kampeni kumshambulia Lowassa, alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la ufisadi na rushwa.

Makongoro, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, alisema kwa kuwa ufisadi bado ni tatizo, wataendelea kuwaeleza Watanzania katika kampeni zao kuwa mgombea huyo wa Chadema ni fisadi.

“Hatuwezi kunyamaza wakati tunamwona fisadi anaomba nafasi ya urais, ni lazima tuwaeleze Watanzania kuwa huyo ni mtu hatari kwenu,” alisema.

Alidai viongozi wa Chadema wamenunuliwa ndiyo maana hawakemei tena ufisadi wakati ndiyo walioanza kumwita kwa jina hilo.

Alisema siyo Chadema pekee yao ambao hawazungumzii ufisadi, bali vyama vyote vinavyounda Ukawa.

“Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi wako kimya hawataki kusikia neno ufisadi kwa sababu wamehongwa,” alisema.

Kauli ya Makongoro iliungwa mkono na Lusinde ambaye alisema kwa kuwa Chadema hawazungumzii tena ufisadi, CCM wataendelea kuwaambia wananchi kuwa mgombea huyo ni fisadi.

“Tunayemtafuta hapa ni Rais, ndiyo maana tunasema tutaendelea kuwaeleza Watanzania kuwa Lowassa ni fisadi na wasimchague,” alisema.

“Muda huu ndiyo natoka Bagamoyo kwenye mkutano wa kampeni, nimewaeleza wananchi kuwa wamwogope Lowassa kama ukoma kwa sababu akichukua nchi itakuwa ya mafisadi na wala rushwa.”

Lakini, Dk Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anatetea hali hiyo akisema ni vigumu wanasiasa kuepuka kutaja udhaifu wa wapinzani kwenye mikutano yao.

Alisema Watanzania ni lazima wakubali kwamba katika kipindi hiki cha kampeni, wagombea watatangaza sera zao, lakini hawawezi kuacha kutaja udhaifu wa washindani wao

“Ndiyo sababu ya kumtaja Lowassa,” alisema mkuu huyo wa kitengo cha sayansi ya siasa.

“Chadema ndiyo walioanza kumwita Lowassa fisadi na wanachokifanya CCM hivi sasa wanarudia tu. Lakini waasisi wa hilo ni Chadema.

“Unategemea leo CCM wataacha kusema kwenye kampeni kuwa Lowassa ni fisadi wakati kuna ushindani mkali?”

Alisema jambo la muhimu hapo ni matumizi ya lugha yenye staha na vyama kufanya kampeni za kistaarabu.

Lakini Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco), anaona kutajwa huko kwa jina la Lowassa kunatokana na mgombea huyo wa urais wa Chadema kuwa tishio kwa CCM.

Alisema kinachotakiwa ni kuwaeleza wananchi sera za vyama vyao ili kuwashawishi, lakini utaratibu wa siasa za kupakana matope hauna maana kwa wananchi.

“Kila siku Lowassa fisadi, hizi ni siasa za majitaka, wananchi wanahitaji kufahamu mtawafanyia nini endapo mtachaguliwa,” alisema.

Maoni kama hayo yalitolewa na mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoani Kilimanjaro, Peter David ambaye alieleza kutofurahishwa na aina hiyo ya kampeni.

Alisema kampeni zinazofanywa na baadhi ya makada wenzake wa CCM za kuchafuana majina majukwaani, si nzuri na akataka wanadi sera.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo - Bisimba alisema CCM haijiamini, ndiyo maana hivi sasa inazungumzia mtu badala ya masuala.

“Muda wote Lowassa fisadi, Lowassa fisadi, watu hawajui vyama vitasimamia masuala gani. Waache kushughulika na mtu, waeleze hoja, waseme watafanya nini kama watachaguliwa,” alisema.

“Ukiona wanazungumzia mtu, ujue hali ni ngumu kwao lakini watu wanaojiamini huzungumzia hoja.”

Alisema wagombea kuzungumzia kashfa za ufisadi kila siku badala ya sera, matokeo yake watajikuta wanaangushwa kwenye uchaguzi.

“Watu wanawapima kwa sera zenu, sasa kama muda mwingi unautumia kuwatuhumu watu utajikuta huna sera ulizoziuza kwa wananchi,” alisema.

Wakili wa kampuni ya MM Law Chamber, Mohamed Menyanga alikuwa na maoni kama ya Kijo-Bisimba.

“CCM inamwogopa Lowassa ndiyo maana kila wakati inamhusisha na kashfa ya ufisadi wakati haina ushahidi,” alisema Menyanga.

“Muda mwingi wautumie kuwaeleza wananchi kwa nini ahadi walizozitoa hawajazitekeleza na siyo kila wakati Lowassa fisadi. Hii haitawasaidia wananchi,” alisema.

Aliungana na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dk Emmanuel Mallya aliyesema ushindani ni mkali katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndiyo maana wagombea wanatumia kila aina ya ‘silaha’ ili kuwashinda washindani wao.

Alisema wananchi wana haki ya kusikia sera za vyama badala ya kashfa za ufisadi kuanzia mwanzo wa kampeni hadi mwisho.

Wakili mwingine wa kujitegemea, Carnelius Kariwa wa Dar es Salaam, alisema anachokiona kwa sasa, kampeni za CCM zinapoteza mwelekeo na malengo.

“Polepole wameanza kupoteza malengo ya msingi ya kampeni. Lengo la kampeni ni kuuza sera siyo kuchafuana. Wamelenga mtu badala ya kuangalia nini Watanzania wanataka.

“Walidhani wakipiga propaganda dhidi ya Lowassa, Sumaye na makada wa CCM waliohamia Ukawa wangechafuka lakini wameshindwa kusoma alama za nyakati nini wanachokitaka Watanzania,” alisema.

Wakili Kariwa, alikwenda mbali akisema Watanzania walio wengi wanataka mabadiliko, hivyo hata Dk Magufuli angekuwa anagombea kwa tiketi ya Ukawa na Lowassa CCM, Dk Magufuli ndiye angeng’ara.

Mawazo ya Wakili hiyo yanatofautiana na yale ya kada wa ACT – Wazalendo, Buni Ramole aliyesema CCM imetambua kuwa adui yao mkubwa katika suala la urais kwa sasa ni Lowassa na ndiyo maana inatumia nguvu kubwa kumshambulia.

“Kwa hali ya kawaida, chama kikongwe kama CCM kilichokaa madarakani kwa miaka zaidi ya 50 hakikupaswa kujinadi kwa kuwasema watu, bali kujinadi kwa mafanikio wala siyo ahadi tena,” alisema Ramole.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), Jesse Angowi alisema kitendo cha makada wa CCM kutumia muda mwingi kumshambulia Lowassa hakimchafui, badala yake kinamng’arisha.

Hata hivyo, Askofu huyo alisema kwa jinsi mwelekeo wa kampeni ulivyo, ni dhahiri rais atatoka ama CCM au Chadema kupitia Ukawa.

Askofu Angowi alisema haridhishwi na namna CCM ilivyobadili mwelekeo wa kampeni na kutumia muda mwingi majukwaani kumshambulia Lowassa badala ya kutumia muda huo kunadi sera zake.

“Lowassa na Sumaye walikuwa mawaziri wakuu walikuwa wasafi walipokuwa CCM hadi wakashika nyadhifa hizo. Leo ghafla wamekuwa makapi na kushambuliwa hivyo?”

Lowassa amekuwa na nia ya kugombea urais kwa muda mrefu tangu mwaka 1995 wakati jina lake lilipokatwa. hakuchukua fomu mwaka 2005 wakati Jakaya Kikwete, aliyekuwa rafiki yake wa karibu, alipogombea.

Lowassa alisema kuwa walikubaliana na Kikwete kwamba waunganishe nguvu ili awamu inayofuata iwe zamu ya mbunge huyo wa Monduli.

Hata hivyo, mwaka huu jina la Lowassa lilikatwa na ya makada wengine 33, na ndipo akaamua kujiunga na Chadema kuendeleza ndoto yake ya kuingia Ikulu.

Sakata la Vijana Kupewa Pesa ili Wachane Mabango ya Lowassa...Kubenea Afunguka Makubwa....

$
0
0
Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea amefichua mbinu za Tume ya uchaguzi (NEC) kukutana na mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hoteli.
Kubenea amesema kuwa Maofisa wa tume hiyo walikutana na mgombea ubunge kupanga mbinu ya kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura ameahidi kutaja jina lake wakati wa ufunguzi wa Kampeni za ubunge siku ya Jumapili.

Ameongeza kuwa wanajua njama zinazofanywa na NEC na watakuwa wanaweka wazi kila kitu ambacho tume hiyo katika mikutano yao ya kampeni alisema katika kampeni zao wataelezea madhaifu ya chama tawala kwa miaka 54.

Kubenea amesema kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM ameanza kufanya kampeni chafu ambapo aliandaa vijana feki wa chama hicho na kuwavalisha nguo za chadema na kuwaambia waandamane na kusema wanamuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilibroad Slaa.

Ameongeza kuwa tayari amemwagiza mwanasheria wake pamoja na wachama kupeleka malalamiko Nec ambayo wataambatanisha na Cd inayomuonyesha Mgombea huyo akiwa anajisifia kwa kitendo alichokifanya.

Amesema kitendo alichokifanya Masaburi ni kinyume na utaratibu wa maadili ya uchaguzi pia ameongeza kuwa kama wao wasivyochana mabango ya vyama vya upinzani nao wasichane ya kwao “Tutawachukulia hatua za kisheria vijana wanaopewa Sh 10,000 na wagombea kuchana mabango yetu kwa sababu tunaushaidi,”
Kubenea amemtupia lawama Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe kwa kuwatisha waangalizi wa Uchaguzi kutoa maoni, matokeo kabla ya NEC kutangaza matokeo na kusema mgombea wa CCM ndiye atakaye shinda.

Hili Jimama Litaniua, Kila Akitaka Mambo Anamtoroka Mume Wake na Kuniita Hotelini Nimshughulike

$
0
0
Admin Udaku Specially
Huyu Mama Hapo kwenye Picha Anataka kuniua tu mimi kijana bado mdogo, Nilikutana naye Mlimani City Pale Game alikuwa akifanya shopping na watoto wake wadogo sasa vitu alivyonunua vilikuwa vingi nikamsaidia kuvipeleka kwenye gari lake , akanishukuru na kuniomba number yangu ya simu, sasa kuanzia hapo tukawa tunawasiliana lakini siku zilivyozidi kwenda tukajikuta tunachat mambo ya mapenzi na siku moja tukakutana nikampa dozi 3 za nguvu, sasa imekua shida maana kila week ananitafuta mara mbili nimpe mambo eti anasema mume wake hawezi mambo , kila mara huwa analipia hoteli yeye na kila kitu mpaka vinywaji mimi kazi yangu ni dozi , sasa nimejaribu kumchumguza nimengundua ni Mke wa Mwanasiasa Maarufu hapa Tanzania. Nimeingiwa na Woga nahofia maisha yangu mimi bado mdogo ndio natafuta maisha.. Naomba Ushauri ...

Wanawake Wengi Wanaoolewa ni Darasa la Saba na Form 4 Wenye Degree Hamfai na Degree Zenu.

$
0
0
Wenye degree hamfai na degree zenu.
Mwanaume ni kichwa cha nyumba. Wanawake wenye elimu ya darasa la saba na form 4 hawasumbui wanaume. wanajua wajibu wao kutii na kumjali Mume,ila wenye zaidi ya hapo,wachache .

Rest hawajielewi baada ya kujiona wanajua,ila hawafai kuolewa hawana sifa ya kuwa wake,ni wanaume wenzetu. Mtazalishwa,mtalea watoto,mtadanganywa na hamtaolewa. Mtaongezewa watoto na majukumu ila wataolewa wa darasa la saba na form 4.

Na hata maprofesa wake zao ni la saba na form 4 au wanaojielewa,mnaojifanya mna figure, degree,mkoo wapi? mna familia za maana na mmeolewa?.......wife material ni anayemsikiliza mme wake, uwe na elimu au vipi bila kujinyenyekeza huna heshima.
Je Hii Kauli inaukweli Wowote?

I will Sacrifice My Mother for Sh. 20 Million and to Join Freemanson! Listen to This Foolish JALUO

$
0
0
Friday, September 11, 2015 – There is this clip of a young man who says he is ready to sacrifice his mother and father just to be rich.


The man has been desperate to join Freemanson for years with no luck until he got this call;

Listen to it below



Ne-Yo Sings In Swahili In His Collabo With Diamond Platnumz.

$
0
0
Expect to see Ne-Yo singing in Swahili in his collabo with Tanzanian Diamond Platnumz. According to Sheddy Clever, producer of the most awaited single, Diamond wanted the American superstar to use some few Swahili words in his verse.
"Ne-Yo sang in Swahili in that single, I can't mention those words but stay tuned" Clever



TANZIA..Mgombea Ubunge Afariki Dunia Kwa Ajali ya Gari

$
0
0
TANZIA: Mgombea wa Ubunge jimbo la Lushoto kwa tiketi ya CHADEMA , Ndg. Mohamedi Mtoi Kanyawana amefariki dunia katika ajali ya gari aliyoipata akitokea kuzindua Kampeni tarafa ya Mlola.

Walikuwa wamemaliza Kampeni na Mtoi aliwapeleka Wenzake Mpaka Lushoto Mjini Kisha akaondoka kuelekea Nyumbani Kwake Ndio Njiani Gari Likapata Ajali na Ndipo Kamanda Mtoi Akafariki Dunia.....

Taarifa za hivi punde ni kuwa kamanda Mohamedi Mtoi amepata ajali na kufariki dunia 

Maelezo haya yamethibitishwa na katibu wa chama wilaya Lushoto Kamanda Dulla.

Mtoto wa Miaka (4) Amekufa Kwa Kuteketea kwa Moto Wakati Baba yake Akimimina Petrol

$
0
0
Nyumba yenye familia ya watoto watatu ya Mbala Jijini Dar es Salaam, jana majira ya saa mbili usiku iliteketea kwa moto baada ya Baba mzazi wa familia hiyo kufungua petrol iliyokuwa ndani kwake na kupelekea nyumba kuwaka moto na kusababisha kifo cha mtoto mdogo wa miaka minne (4).


Baba na mtoto wake waliteketea kwa moto (Baba aliokolewa) ambapo wakati huo Baba na mwanae huyo walikuwa ndani huku mke wake aliyetambuliwa kwa jina la Catherine Abiria, akiwa na watoto wengine wawili nje.



Mashuhuda wa tukio wanasema katika hatua za kumimina petrol hiyo kwa bahati mbaya ndipo palipotokea mlipuko ambao ulipelekea kifo cha huyo mtoto ambaye alizikwa jana hiyo hiyo kutokana na kuungua vibaya.



Baba wa familia ameumia vibaya amelazwa katika Hospitali ya Tumbi na hali yake inaelezwa kuwa ni mbaya sana.



Funzo; Tuepuke kuweka vimiminika vinavyoweza kusababisha ajali kama hizi na kuwapoteza wapendwa wetu.

Wanaume Wenye Wake Wazuri, Huwa na 'Nyumba Ndogo' Zisizotazamika Kwa Sura Wala Umbo...!

$
0
0
Kwa mujibu wa utafiti wangu nilioufanyia kwenye eneo langu la kazi na kwa majirani zangu nimebaini kwamba, kati ya wafanyakazi watano niliofuatilia nyendo zao, ni wawili ambao walikuwa na ‘nyumba ndogo’ nzuri na zenye mvuto kuliko wake zao. Watatu walikuwa na ‘nyumba ndogo’ ambazo zinaweza kumpelekea mtu kujiuliza inakuwaje mwanaume huyo kuwa na ‘nyumba ndogo’ hiyo ambayo hata kwa mbali sana haiwezi kulingana na mkewe. Kwa jirani zangu wanne hali haikuwa nzuri, kwani hapa watatu walikuwa na ‘nyumba ndogo’ zilizo kinyume na wake zao kwa sura na umbo.

Watu saba niliowahoji kuhusu jambo hili, watatu walisema kwamba, wana ushahidi kuhusu wanaume wanaowafahamu wenye ‘nyumba ndogo’ zisizotazamika ukilinganisha na wake zao. Wengine wanne walitoa ushahidi wa wanaume wanaowafahamu ambao wana ‘nyumba ndogo’ nzuri sana ukilinganisha na wake zao.

Ni kitu gani kinatokea?

Ni kwamba, kuna ukweli kuwa wanaume wanaweza kuacha wake zao wazuri sana nyumbani na kufuata wanawake wabaya wasiotazamika kwa sura na umbo huko nje. Lakini pia wanaweza kuacha wake zao wabaya kwa sura ndani na kwenda kufuata wanawake wazuri kwa sura na umbo huko nje.

Hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba kuna mkanganyiko kwenye jambo hili. Lakini kwa bahati nzuri mkanganyiko huu kamwe siyo mkubwa na unaoweza kuumiza kichwa cha mtu.

Binadamu ana kitu kiinachoitwa ukinaifu. Ukinaifu ni hali ya mtu kuchoka kukiona kitu kilekile mara zote. Kwa mfano, mtu anaponunua nguo mpya leo huipenda sana. Lakini baada ya muda fulani, ikiwa bado haijachakaa hujikuta kiwango cha kuipenda kikishuka.

Lakini ni vizuri nikarudi nyuma na kusema kwamba, kwenye suala la mapenzi. Ukinaifu huwapata wanaume kuliko wanawake. Inawezekana sababu ni za kimaumbile na hivyo ni vigumu kusema ni kwa nini inakuwa hivyo.

Kwa sababu ni suala la kimaumbile inakuwa kama lazima kwa mwanaume kupata ukinaifu. Anapopata ukinaifu siyo lazima atoke nje, yaani dawa yake au ufumbuzi siyo kutoka nje ya ndoa, ingawa wanaume wengi hufanya hivyo. Wanapofanya hivyo siyo kwamba, wanajua kwamba, wamepata ukinaifu, hapana. Wao hudhani tu kwamba, wamempenda mwanamke fulani kwa sababu hizi au zile.

Nadharia moja kuhusu ukinaifu ni kwamba, ili ukinaifu ushibishwe ni lazima mtu apate kitu kilicho kinyume na kile ambacho kimempa ukinaifu huo, au kuwa nacho mbali kwa muda fulani. Kwa mfano, kama mwanaume amepata ukinaifu wa umbile la mkewe ambaye ni kimbaumbau, ni lazima kama ataamua kwenda kutafuta mwanamke wa nje, atatafuta mwanamke tipwatipwa.

Kwa mkabala huo, ndiyo pale tunapokuta mwanaume akimfuata mwanamke wa nje mbaya ukilinganisha na mkewe. Labda anaamua kumfuata mwanamke huyo kwa msukumo wa ukinaifu – amekinaishwa na umbo au sura ya mkewe na hivyo angetaka kuona sura ya aina nyingine, ili afute ukinaifu wake. Kinyume cha sura nzuri ni sura mbaya, kwa hiyo atatafuta mwanamke mwenye sura kinyume na ile ya mkewe.

Kuna ukinaifu wa aina nyingi kwenye maisha ya ndoa. Mwanaume anaweza akakinaishwa na mtindo wa nywele wa aina moja wa mkewe. Kama mwanaume huyu hatakuwa mwangalifu, atajikuta akitafuta ‘nyumba ndogo’ yenye mtindo tofauti na mkewe. Inawezekana mkewe anatumia mtindo wa ‘twende kilioni’ kila akisuka nywele zake. Mwanamume anapokwenda kutafuta kilicho kinyume huko nje, anaweza akajikuta amevutiwa na mwanamke mwenye kunyoa na kuchana nywele zake fupi.

Kwa hiyo, inawezekana kabisa mwanaume akatoka nje ya ndoa yake kutafuta kinyume ambacho siyo sura wala umbile. Inawezekana akatoka kwa sababu amekinaishwa na ukimya wa mkewe, hivyo anatafuta kelele. Huyu anaweza kujikuta akiwa na mwanamke wa nje muongeaji na chakaramu sana, ambaye kisura na kiumbile anaweza kuwa sawa na mkewe.

Mafuriko ya LOWASSA Yahamia Singida......Apokelewa Kifalme, Shughuli zasimama kwa Muda

$
0
0

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo jana Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida jana Septemba 12, 2015.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo jana Septemba 12, 2015.

Wasanii wa Bongo Movie Wanogesha Kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais Wa -CCM

$
0
0

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
 
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akisalimiana na baadhi ya viongozi na wananchi baada ya kuwasili katika eneo la mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani jana.
 
 
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
 
 
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Kibaha Vijijini, akizungumza na wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
 
 
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
 
Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Septemba 13


Wimbo Mpya wa Roma Ulioifanya BASATA Itoe Onyo Kwa Wasanii........"Viva Roma Viva"

$
0
0
Msanii wa Hip-hop ametoa track yake mpya inayoitwa VIVA ROMA. Kama kawaida, kwenye track hiyo amezungumzia mambo mengi yanayohusu Siasa za Tanzania;

Haya  ni  Mashairi  ya  Wimbo  huo:

Nimeshapigwa sana mkwala na jumbe za vitisho, ila siamini huu msafara ni vibaraka wa Mrisho, si tulianza sawa vita ya kuitetea Ikulu? Leo umeisaliti UKAWA kwenye sherehe za uhuru! 

Uhuru uko wapi mnasherekea uhuru!? Uhuru wa kutowafilisi viongozi wakijiuzulu? Na wanaokufa maskini wanangu wa Burya Nkulu, Mungu aliwapa madini mnambinafisisha Mkaburu!
 


Bungeni sioni kinachoendelea, naona wasomi wakisutana umbea, wengine walishikwa ugoni picha zilienea, hamuwaoni jimboni afu bado mnawalea!
 


Mambo ya.... Spika anabadilisha mada, akiona chama tawala amezalilishwa kada! Spika wa Bunge ona analinda watu wa chama chake, na bunge ni la watu wote siyo chombo cha watu wachache!
 


Safari ya Rais eti Tume inaundiwa Tume, wakati Mwananyamala wanatibu Tezi dume!
 


Kadi ya chama nachana, nanyongea ganja navuta, nikamateni si mlimshindwa Tibaijuka? Leta Defender, leta Wajeda, leta Wagambo Roma nimejitoa sadaka. Na mkitaka kuniua hiki kichwa sifii hapa, nichinjeni mkanitupe kwenye daraja la Mkapa.. 


Mother**** Walafi wa madaraka, hata Nyerere, Gaddafi si walikufa kwa mashaka?! So hakuna kiongozi msafi, je nani mwenye mamlaka, anitajie mtoto wa Rais anayesoma shule ya Kata!
 


VIVA ROMA VIVA X4
Katiba ni sauti ya umma na kuna uhuru wa kuongea. Na nyie si ndio mmenituma, mpo tayari kunitetea? Wilaya mnafanya Mkoa ili wapangwe washikaji, Mkuu wa Wilaya Changudoa hii ni miradi ya upigaji! 


Watasafirisha Nyani, sisi tunashangaa Twiga? Utamfunga nani yeye na Mwanasheria Mkuu ni maswahiba, na wasanii tuombee Rais ajaye asipende tu vikuu, wataliikwa wapemba hatutamuona hata Lukuvi!
 


Unampigiaje Kura Fisi awaongoze Mbuzi, kwa hongo ndogo ya kipisi unampa Ikulu mlanguzi! Geita mlinyimwa dhahabu watawalaghai kwa vitenge, napata kwa gadhabu propaganda za wabunge wasee**** ngerema
 


Ukistaajabu ya Lema utayaona ya Mrema, ona pepo la usaliti linaitafuna CHADEMA, kwetu Rais ni taasisi inayochaguliwa na mfumo, sisi wawakilishi na kwenye maamuzi hatumo!
 


Watoto wao wanauza Ngada, Baba Fisadi, Mama anafanya Ukahaba, yupi mwema kiitikadi? Na vita ya Mahakama ya Kadhi ni uhasama wa wazi, yaani unaisaka bikra ndani ya wodi ya wazazi?!! 


Nipige risasi ya utosi si ndo nidhamu ya utawala, maana waliomuua Mwangosi waliongezewa mshahara, Dr. Mvungi Ona dah! Wakamzawadia jeneza, na hawafungwi! Nipe case nitaimba ndani ya gereza..
 


(Peperusha Bendera, VIVA ROMA VIVA)
Mbona mama yako anauza gongo, na gongo ndio iliokulea hadi leo umekuwa polisi, na humpeleki Segerea, life is not fair 


Polisi mna maisha gani? Mnakufa maskini kwa kuwatetea wanyang'anyi!


(Peperusha Bendera, VIVA ROMA VIVA) 
Hakuna mtoto asiye na mzazi yupi wa serikali ya tatu? Mikataba iweke wazi Demokrasia ni watu, ona sasa kila msomi anaikimbilia siasa, nchi itajengwa na nani? Ajira imekuwa serious! 


Wanafanya biashara haramu , bado hawalipi kodi, nani atahoji, na hao ndio Wadhamini wa Bodi!? Jasho analila Mzungu wachimbaji wadogo wa Migodi, au mnataka Ivan aje awe mfuasi wa Panyaroad?!
 


Pesa sherehe za Muungano amzingatii Itifaki, wanafunzi mnawachoma jua na shule hawana madawati, mnalipa mishahara hewa, na hamlipi mafao walimu, na mlimpiga Warioba alivyowaletea Rasimu!
 


Nchi inalima, Pamba nyinyi mmeua Viwanda, tunauzia wawekezaji ona Dola inapanda! Tunageuka waagizaji kisha wanatuuzia mitumba, uchumi unayumba leta fujo upigwe kama Lipumba!
 


Na kutabiri nani afuate? Karibu Tanga kunani ... 

Round hii kombe linaenda Monduli? (Masai yellow subhai) ... Au Kombe ni la Magufuli? Kama kawa kama dawa, Je, Kombe linabaki UKAWA?! 


Mmarekani anataka Wese (we hakuna atakayepona), Na mchina akifuata gesi? Mwambie nangwanda sijaona..

  
VIVA ROMA VIVA.......<<<<  UDownload Hapa >>>>
 =======

Usikilize hapo  Chini

Mbasha, Askofu Gwajima Kimenuka Upya Mbaya..Siri Mpya Yavuja

$
0
0
NI kweli kimenuka! Siku chache baada ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kujibu mapigo ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, sasa kimenuka upya, Risasi Jumamosi linakupa zaidi!
Kimenuka kwa nani? Ni kwa Emmanuel Mbasha ambaye ni mume aliyetengana na mkewe, Flora Mbasha huku mwanaume huyo akisimamia madai yake kwamba, Gwajima alisimamia mchakato mzima wa yeye na mkewe kutengana.
AIBUKA UPYA
Akizungumza na Risasi Jumamosi katika mahojiano ya takribani dakika thelathini juzi jijini Dar, Mbasha alisema alimshuhudia Gwajima, Jumanne wiki hii akitupa shutuma kwa Dk. Slaa tena kwa kuyaanika mambo yake ya ndoa, yeye akashangaa sana.
“Na mimi leo nataka kumjibu Gwajima kama yeye naye alivyojitokeza kumjibu Dk. Slaa. Gwajima niliwahi kumshutumu kwa kuhusika na kuvunjika kwa ndoa yangu. Leo hii anasimama kwa kujigamba akisema Slaa si msafi, yeye ana usafi gani?.
AFICHUA SIRI MPYA 
“Lakini kiko wapi sasa! Hata huyo Flora mwenyewe ameshamkimbia, yuko kwingine. Kwa hiyo kama ishu ni uchafu, Gwajima pia si msafi. Ana mambo anajua alikuwa akiyafanya kwa mke wangu, mimi nayajua na nina ushahidi.”
Hata hivyo, Mbasha hakufafanua, Flora amemkimbia Gwajima kivipi? Na huko kwingine alikokwenda ni kwa nani na kwa sababu gani!
ANA MAZITO YA GWAJIMA
Lakini alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Naomba leo niseme kwamba nina mambo mazito sana ya Gwajima
ambayo siku ikifika nikienda kuyasema kanisani kwake waumini wake watashangaa wote. Muda bado haujafika lakini ukifika nitamlipua.”
Risasi Jumamosi: “Je, kuibuka kwako upya tukisema umetumwa na chama kimoja cha siasa umchafue Gwajima, utasemaje?”
Mbasha: “Kwani ye’ alitumwa na nani? Mimi nimeibuka kwa sababu hata yeye ameibuka. Kama angesimama pale (Ukumbi wa Hoteli ya Landmark) akasema mambo yake bila kukosoa ndoa ya Dk. Slaa hata mimi nisingepanua kinywa kusema. Hawezi kusema siri za mwenzake kama mtumishi. Tena anasema mpaka ishu ya Dk. Slaa kulala ndani ya gari.”
“Nimeamua kusema kwa sababu yeye amemwona mwenzake si msafi. Yeye usafi wake ni upi? Niliachana na Flora, akaenda kwake, yeye akampokea. Angekuwa msafi angemshauri Flora kwamba alichofanya si kizuri. Hapo ningesema ni msafi.”
AMKUMBUSHA GWAJIMA KUHUSU MOROGORO
“Gwajima akumbuke kabla ya ukaribu wetu haujafa, mimi, Flora na yeye tulikwenda Morogoro kwa ajili ya huduma ya Mungu. Nini kilitokea? Lakini sijasema. Ajitokeze anijibu na mimi halafu nitasema nini kilitokea. Kwa sasa sitoi risasi zote, nasubiri ajibu.”
NDANI YA MITANDAO
Ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii, majibu ya Gwajima kwa Dk. Slaa yamekuwa gumzo. Timu ya Mbasha imemtupia shutuma kali Gwajima ikikumbushia mgogoro wa Flora na mumewe huku kundi jingine la Gwajima likitetea kuwa, hakuna uhusiano wowote wa mgogoro wa Mbasha na mkewe na majibu ya Gwajima kwa Dk. Slaa.
GWAJIMA SASA
Juzi, gazeti hili lilimsaka kwa njia ya simu Mchungaji Gwajima ili aweze kujibu shutuma za Mbasha ambazo ni kama ameziibua upya lakini simu yake haikuwa hewani.
Hata hivyo, katika mkutano wake na wanahabari Jumanne, Gwajima alisema: “…kwa hiyo Dk. Slaa si msafi. Dk. Slaa huyu wa leo si yule wa mwaka mmoja uliopita! Lakini ukiangalia kwa makini sana, si yeye, matatizo yapo kwa yule mke wake, amemkamata.”
Pia, Gwajima alianika siri akidai kuwa, Dk. Slaa aliwahi kutupiwa virago nje akalala kwenye gari baada ya kubaini kuwa, ameridhia, Chadema kumpokea waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kugombea urais.
FLORA NAYE ANA MAMBO MENGI
Wakati Mbasha akirusha madai hayo huku akisema mkewe amemkimbia Gwajima na yuko kwingine, kwa upande wake, Flora aliwahi kusema: “Nina mambo kibao ya Mbasha, nikiyasema watu
watashangaa! Lakini siku zote mimi namwachia Mungu tu. Yeye ndiye muweza wa yote.”
MKE WA DOKTA SLAA
Kuhusu madai ya kumfukuza mumewe nje na kulala kwenye gari, mke wa Dk. Slaa, Josephine Mushumbuzi aliwahi kusema: “Najiuliza nini
kinaendelea, kuna mambo mwanamke huwezi kumfanyia mwanaume. Mume atabaki kuwa mume tu siku zote.”
SLAA AHOFIA
Kuhusu madai ya kukatiliwa kuingia ndani ya nyumba na mkewe na kulala ndani ya gari, Dk. Slaa alipoulizwa kihabari, alisema: “Mambo hayo ni ya kifamilia sana. Sitaki tu kuzungumzia mambo ya familia za watu nikiyasema utatokea mpasuko! Tuache tu.”
Source:Global Publishers

LOWASSA Atangaza KIAMA Kwa Viongozi Hawa!

$
0
0
KIAMA kwa Viongozi hawa na hakika neema inakuja!Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataunda serikali itakayokuwa na viongozi wenye uwezo wa kuchukua hatua na kutatua matatizo ya wananchi na atahakikisha utaratibu wa wananchi kulalamika na viongozi pia kulalamikakama ilivyo sasa unabaki kuwa historia.
Mh Lowassa ambaye amefanya mikutano minne katika majimbo ya Mtera, Bahi Chilonwa na Dodoma mjini pia amewaomba watanzania kumpa nafasi ya kukamilisha ndoto yake ya kuleta usawa wa huduma za kijamii ikiwemo elimu aliyoanza kuonyesha mfano kupitia shule za kata alipokuwa waziri mkuu.

Nao Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye na mwanasheria wa Chadema Mh Tundu Lisu wakihutubia juzi mjini Dodoma walisema kukithiri kwa malalamiko ya wananchi kukosa huduma huku wanaotakiwa kuchukua hatua wakiendelea kutoa ahadi inatosha kuonyesha kuwa uwezo wao wa kupata ufumbuzi umefika mwisho na ndio maana UKAWA inaomba nafasi ya kuondoa tatizo hilo.

Wananchi na viongozi wa jimbo la Mtera walisema ubinafisi wa viongozi wa CCM, na ahadi zisizotekelezeka umesababisha wapoteze matumaini ya kuondokana na umaskini hasa kwa vijana.
Akihitimisha mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Dodoma uliofanyika jana Dodoma mjini, Mh Lowaasa ambaye sasa yupo mkoa wa Singida aliendelea kunadi sera za UKAWA na kutoa ufafanuzi wa namna ya kuzitekeleza kwa wakati na kwakasi inayostahili.

Jokate: Sijaona wa Kumwamini Kimapenzi...Kila Ninayemuamini, Anaishia Kuniliza..Sasa Yatosha

$
0
0
Jokate
LICHA ya kuzagaa kwa tetesi juu ya uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, mwanamitindo Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amesema kutokana na kuumizwa na mapenzi mara kwa mara, kwa sasa hajaona mwanaume wa kumuamini hivyo anaelekeza nguvu na akili zake kwenye kazi.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Jokate alisema ni ngumu kwa watu kuamini kuwa amekuwa akiumizwa na mapenzi mara kwa mara, kutokana na muonekano wa urembo alionao, lakini ukweli unabaki kuwa, anaumizwa na mapenzi na kwamba hana imani tena na wanaume.
“Kwa muonekano wangu wa juu, ni ngumu sana kuamini kuwa huwa naumizwa na mapenzi, hakika huwa naumia mno, kila ninayemuamini, anaishia kuniliza, sasa yatosha, simuamini mtu tena, sijamuona wa kumpa imani yangu kimapenzi, acha nielekeze nguvu na akili zangu kwenye kazi,” alisema Jokate.

Katikati ya wiki hii, Ali Kiba alinaswa Morogoro akiwa na mwanamke mwingine katika mazingira ambayo yaliashiria wana uhusiano wa karibu na kufanya watu waibue maswali.
GPL

Eti Lulu Alilia Kuzaa Mtoto Kwa Gharama Yoyote Mwaka Huu

$
0
0
Lulu Michael
Imelda Mtema
MAKUBWA! Akiwa angali na umri wa miaka 20, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amenyanyua kinywa chake na kutamka kuwa anataka kuzaa kwa gharama yoyote kwani anatamani sana mtoto.
Kauli hiyo ameitoa Lulu mara baada ya mwanahabari wetu kumuuliza sababu za yeye kupenda kuweka watoto wadogo katika mitandao ya kijamii ndipo Lulu alipofunguka kuwa anatamani sana kupata mtoto.

Yaani asikwambie mtu, nalilia kweli kupata mtoto japo wengi wanaweza kuona kwamba bado umri wangu  ni mdogo lakini kwangu mimi naona kama umri unaniacha hivi natamani hata huu mwaka usiishe niwe tayari na mimi napakata kichanga changu,” alisema Lulu na kuongeza:
Kwa kweli hata kama ni kwa gharama yoyote itabidi inigharimu ili na mimi niitwe mama maana furaha yangu ya moyo haiwezi kukamilika kama sijaitwa mama na mimi.”

Lulu aliwahi kuwa mpenzi wa marehemu mwigizaji Steven Kanumba, hawakufanikiwa kupata mtoto achilia mbali wanaume kadhaa kudaiwa kutembea naye lakini bado mambo hayajajipa!
GPL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images