Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Makanisa Matatu yachomwa Moto Bukoba Leo Septemba 22,2015

$
0
0
Makanisa yaliyochomwa moto ni Pentecostal Assembilie of God (PAG) kata bakoba eneo la buyekera,Living Water International na Evangelical Assemblies of God (EAGT) kata ya Kibeta yote ya mjini Bukoba .Chanzo chake hakijafahamika ambapo wachungaji na viongozi wa kiroho wanaomba vyombo vya dola kuwabaini wahusika.

kamanda wa polisi mkoani kagera Augstine Oromi amedhibtisha kutokea kwa tukio hilo na amemweleza mwandishi wa mtandao huu kuwa yupo katika ziara ya kazi wilayani ngara hivyo atatoa taarifa baadaye.

Matukio ya makanisa kuchomwa yameshamiri katika manispaa ya bukoba ambapo hili ni tukio la sita kwa kipindi cha mwaka mmoja




UTAFITI wa TWAWEZA...Msoma Utafiti Ametumia Muda Mwingi Kudefend Matokeo Kuonyesha Uhalali wake Badala ya Kuacha Watu Waamue

$
0
0
Kwa walioangalia Wakati Matokeo ya Utafiti Yanasomwa Main presenter wa huu utafiti Alishindwa kuwa professional kwa kupresent takwimu kulingana na utafiti waliofanya ( kama kweli ni legitimate results) anatumia muda mwingi kudefend matokeo hata kama umati haujauliza swali, kuonyesha uhalali wa matokeo yao, ameonyesha mapenzi ya dhati kwa CCM hasa aliposisitiza Magufuli hana ufisadi, sijui ndo anataka akumbukwe kwenye nafasi za kuteuliwa na magufuli, anaonekana very arrogant, Please be professional, it is a shame to academicians and intellectuals

Ukaribu wa Mkurugenzi wa Twaweza Aidani Eyakuze na January Makamba wa CCM Wazidi Kutia Doa Utafiti Uliotolewa na Taasisi Hiyo

$
0
0
Aidani Eyakuze ni Mkurugenzi mkuu wa Tweweza east africa, namfahamu sana kijana huyu aliechukua nafasi ya Rakesh pale Twaweza. Eyakuze ni rafiki mno tena wa karibu sana na January Makamba, na katika ile proposal concept ya Makamba pale Mlimana city ya kutanganza nia pale mlimani Eyakuze ndie aliekuwa consultant mkuu wa ile proposal ambayo leo kwa kiasi kikubwa imekuwa adapted na Mgombea wa CCM Magufuli na makamba kuwa karibu kuhakikisha inatekelezeka mfano kuipa kila kijiji sh milioni 50.

BADO naconect urafiki wa Eyakuze na Makamba katika takwimu alizozitoa Juzi ktk media january na leo za twaweza....ni km watu wanalala na kuamka pamoja.

Kwa thread hii, Aidani Eyakuze ameidhalilisha taasisi kubwa kama Twaweza kwa kununuliwa na ccm kupitia January na kupika tafiti zenye kuifurahisha ccm...hii ni hatari sana kwa taaluma ya Aidan Eyakuze ambaye Taasis yake inaeshimika kwa tafiiti zenye kulenga kuboresha mambo mbali mbali kwa serikali kwa watu wake. mfano mmoja ni Elimu kwa kupitia mradi wake wa UWEZO Tanzania inafanya tafiti na kuipa mrejesho serikali kwa chanamoto mbali mbali za ukweli toka kote nchini na serikali kupitia wizara ya elimu na TAMISEMI mara nyingi imeonyesha mabadiliko na kufanya utekelezaji kwa baadhi ya maeneo hayo Muhmu. sasa My take ....kama ccm inakununua Aidan..hivi chama hiki kikiwa madarakani kiendelee kuamnini na kufanyia kazi tafiti zako zijazo?? na hasa sasa nasikia mtaongeza evaluation katika afya na mazingira?

Aidani..sio masikin wa hela kwa elimu na nafasi yake pale twaweza...uswahiba wake tena wa siku nyingi na January anaamua kupindisha taaluma yake na taasis yake kutoa matokeo ya kufurahisha ccm hii aitosh kuzuia maamumuzi ya wananchi wanaotaka mabadiliko ambayo UWeZO Tanzania imevumbua madudu mengi tu uko chini katika tafit zake za elimu kwa miaka 5 mfululizo.Aidan wanishangaza sana.
IMAGE ya Twaweza na UWEZO Kenya, Uganda na Tanzania inaenda kuingia doa na dosari kubwa sana kwa upenzi huu binafsi wa Aidan Eyakuze na January Makamba.

Hivi dhambi hii kwa CCM, January na Aidan mtaungamia wapi ili hali nafsi zenu zinajua mnafanya hujuma ya makusudi.....shame on YOU Aidan na Shame on Makamba.

Mungu akupe uhai mrefu Mr Rakesh, ata kama Mkapa alikuwa rafiki yako sana ulimkosoa sana na kumpa fact wakat wa "HAKI ELIMU" hadi ulipooingia TWAWEZA hukusita kufanya hivyo kwa Kikwete na mengi tumeyaoona yanabadilika.....lakini kwa aliechukua Kijiti chako AIdan eyakuze huku sio tena ameendeleza ameamua kufanya Twaweza na UWEZO kuwa taasisi Ndogo za CCM.Shame na kwa washauri wake Uganda, Tanzania, na Kenya..

Source: Jamii Forums

Wakati Watu Wanajadili Utafiti Wa TWAWEZA, Lowassa Azidi Kufanya Maajabu Masasi, Shuhudia MAFURIKO Yake Hapa

$
0
0
Wakati Watu Wanajadili Utafiti Wa TWAWEZA,  Lowassa Azidi Kufanya Maajabu Masasi, Shuhudia MAFURIKO Yake Hapa

Jack Wolper Awatupia Dongo Kina Wema Sepetu na Wenzake wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao

$
0
0
Jack Wolper Awatupia Dongo Kina Wema Sepetu na Wenzake wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao...Soma Hapa Chini Dongo Lenyewe..


Baada ya TWAWEZA kusema CCM inakubalika 66 %, haya ni maneno 15 ya Lowassa na 26 ya Zitto Kabwe

$
0
0
Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, C.U.F 1%,ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%.
Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo.

Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter

 ‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata‘

Dr. Magufuli hakuwa ameandika chochote kuhusu utafiti huu huku tweet yake ya mwisho ikiwa inaeleza furaha yake kwa jinsi Wananchi wa Bukoba walivyojitokeza kumsikiliza.

Wananchi wa Bukoba nimefarijika pasipo na wasiwasi kwa namna mlivyojitokeza kwa wingi kukiunga Chama Cha Mapinduzi. 

Kwa upande wa ACT Wazalendo, kiongozi wake Zitto Kabwe aliandika kwenye Twitter ‘Chama chetu kinaamini kwenye tafiti haijalishi zina matokeo mazuri au mabaya kutuhusu, tumepokea matokeo haya kama changamoto… tutaongeza nguvu yetu kuhakikisha tunapata asilimia zaidi kwenye kura‘

Our party believe in research and accept results whether positive to us or not. Our trust in @Twaweza_NiSisi work is unshakable

January Makamba wa CCM kwenye sehemu ya Tweets zake aliandika kwamba hajashangazwa na matokeo ya utafiti wa TWAWEZA sababu imeendana na utafiti na CCM ambao ulitangazwa siku chache kabla.

I'm not surprised by Twaweza poll that gave @MagufuliJP a resounding 65% against Lowassa's 25%. It is consistent with our internal research.

TUSKER FANYA KWELI YAWAFIKIA WAKAZI WA TEGETA NA TEMEKE WIKI HII

$
0
0

 Mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Naomi Mahela akipokea zawadi yake ya fulana, mfuko pamoja na bia za bure toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (kulia) pale promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi katika kiwanja cha baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker yenye lengo la kuzihamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye utoaji huduma kwa wateja. Promosheni hiyo inaendelea pia katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Morogoro na Mbeya. (Kulia) ni Mtangazaji wa redio Efm na mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash.


Mkazi wa Tegeta Kibaoni Goodluck Kagoma (katikati) akipokea zawadi yake ya mfuko, fulana pamoja na zawadi ya bia toka kwa balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi (kulia) wakati wa wa hafla ya kuipongeza baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi siku ya Ijumaa katika kuipongeza baa hiyo iliyoibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio E-fm Gadner Habash.



Mkazi wa Temeke Maimuna Seif akiifurahia zawadi yake ya fulana toka kwa Afisa Masoko anayejifunza kwa vitendo toka Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Josephat Shelukindo katika hafla ya kuipongeza baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Kiwanjani inayodhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. Promosheni hii ya Tusker imejikita katika kuziunga mkono baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka ili kuhakikisha kuwa zinatambulika kwa wateja wa eneo husika na kufanya kweli kwenye utaoji wa huduma.



Mkazi wa Tegeta Kibaoni na mpenzi wa bia ya Tusker Bi. Leonarda Shayo akiifurahia zawadi yake ya mfuko na fulana aliyokabidhiwa pale promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi ndani ya baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo ambayo inadhaminiwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. Akikabidhi zawadi hiyo (Kulia) ni Balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi na (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash.


Mpenzi wa bia ya Tusker ambaye pia ni mkazi wa jiji la Mbeya Monalisa Makangila(Katikati) akipokea zawadi ya fulana na mfuko toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio Efm Gadner Habash.


CCM Makao Makuu Wameongea na Vyombo Vya Habari LEO........Wameongelea Utafiti wa Twaweza na Wamesisitiza Kuhusu Mdahalo

$
0
0

Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.

Mwenendo wa Kampeni
Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni.

Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi.
 
Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.

Tunaridhika sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu na mikakati mipya.

Midahalo ya Wagombea
CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:

1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais

2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.

3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa.

UTAFITI WA TWAWEZA
CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:

1. Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua.

2. Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.

3. Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa.

4. Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.

5. Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.

Lakini vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi.
 
Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi. Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu.

CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini.

Utafiti ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki. Itakumbukwa kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa asilimia 61.

Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa na Synovate.

Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.

Imetolewa na:

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM

Lowassa Atumia Mahakama ya Wananchi Kuchagua Mbunge Baada ya Dk Makaidi Kukataliwa Mbele Yake

$
0
0

Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa jana alimwomba mwenyekiti mwenza wa umoja huo, Dk Emmanuel Makaidi kujitoa kugombea ubunge katika Jimbo la Masasi na kumwachia mgombea wa CUF, Ismail Makombe baada ya kukataliwa na wananchi.

Uamuzi huo ulifikiwa katika Uwanja wa Bomani mjini Masasi, baada ya Lowassa kuwasimamisha wagombea hao jukwaani kuwanadi, lakini akapata upinzani mkali kutoka kwa wananchi alipompa nafasi Dk Makaidi.

Lakini kabla Makaidi hajasema chochote aliondoka katika mkutano huo na meza kuu ilijadiliana, ndipo mke wa Makaidi, Modesta aliposhauri waachwe wote wawili wachuane hoja ambayo ilikubaliwa na Lowassa ambaye alitangaza tena kuwa wagombea hao kila mmoja atapambana kivyake.

Awali, Lowassa alipotoa uamuzi wa kumuomba Dk Makaidi amwachie kijana huyo, uwanja mzima ulilipuka kwa nderemo na vifijo huku wananchi wakinyoosha mikono juu kuonyesha kukubaliana na uamuzi huo.

Hata hivyo, alivyobadilisha uamuzi huo, umati huo ulionekana kutomuunga mkono.

Lowassa alifika katika mkutano huo saa 7.28 mchana akitokea Mtwara baada ya kushindwa kufanya mkutano Tunduru kutokana na helikopta kukosa mafuta yaliyokuwa yameagizwa Dar es Salaam na yalipopatikana aliamua kwenda moja kwa moja Masasi.

Ilivyokuwa
Dk Makaidi alipopewa nafasi ya kuzungumza, wananchi walipiga kelele huku wakionyesha mikono juu kumkataa na kukatisha hotuba aliyokuwa ameanza kuitoa.

Lakini aliposimamishwa mgombea wa CUF, Makombe maarufu kama Kundambanda, alishangiliwa huku akimweleza Lowassa kuwa kura zake za urais anazo mfukoni kwa kuwa ndiye wananchi wanayemkubali.

Mgombea wa Chadema katika jimbo hilo, Mussa Sakaredi alijitoa ili kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa na Ukawa.

Ndanda yaleyale
Kama ilivyokuwa Masasi, katika Jimbo la Ndanda, pia mgombea mmoja kati ya wawili wa Ukawa waliojitokeza kuwania ubunge alikataliwa na wananchi mbele ya Lowassa na kumfanya alikimbie jukwaa.

Hali hiyo ilijitokeza pale Meneja Kampeni wa Chadema, John Mrema aliposema anafahamu kuna mgogoro wa nani atakayegombea ubunge chini ya mwamvuli wa Ukawa kati ya NLD na Chadema, hivyo akatoa nafasi kwa kila mgombea kueleza matatizo ya jimbo hilo jipya.

Mgombea wa NLD, Angelous Gabriel alipopewa nafasi aliishia kumsifia Lowassa, jambo lililowafanya wananchi kupiga kelele wakisema anapoteza muda.

“Toka unapoteza muda, tokaaaaa,” walisikia wakipaza sauti.

Ilipofika zamu ya mgombea wa Chadema, Cecil Mwambe uwanja mzima ulilipuka huku akieleza kuwa katika jimbo hilo kuna tatizo la bei ya mazao, hivyo kama Lowassa akiingia madarakani, serikali yake iwatatulie matatizo yao.

Baada ya Mwambe kusema hayo wananchi walimshangilia na Lowassa alipopanda jukwaani aliwaita wagombea wote wawili na kuwahoji wananchi wanamtaka nani kati yao ambapo kwa sauti ya pamoja walijibu “Mwambeeeeeeeee”

Jambo hilo lilimfanya Gabriel wa NLD kushuka jukwaani na kuondoka. Alipoulizwa sababu ya kukataliwa alisema: “Kuna watu wameandaliwa na kununuliwa ili nisigombee Ndanda.”

Hata hivyo, wakazi wa Ndanda waliohojiwa walisema hawamjui mgombea huyo na wanashangaa kwa nini anang’ang’ania kugombea huku wakisema hajajiandikisha kupiga kura katika jimbo hilo, jambo ambalo Gabriel alikiri.

Mmoja wa wakazi hao, Charles Mtutu alisema: “Hatumjui hata jina na NLD haina kiongozi katika jimbo hili na hawajawahi kufanya mikutano.”

Mkazi mwingine, Athuman Hassan alisema: “Kwanza hatumjui, pili hajawahi kufanya kampeni zozote tangu Jimbo la Ndanda lilipopatikana.”

Magufuli Atikisa Mji Mdogo wa Katoro Mchana Huu

$
0
0

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria


Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi Wagombea Ubunge wa jimbo la Bukombe na Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.

LOWASSA Aiangamiza Ngome Ya CCM, Jimbo La Mtama Kwa Nape Nnauye Jiioni Hii ......Mamia Warudisha Kadi za CCM Na Kujiunga UKAWA

$
0
0

Sumaye akiwa ameshika cadi za uana Chama wa CCM zilizorudishwa




 Kadi zilizorudisha kwa ajili ya kuangamizwa..




Magufuli Atikisa Mji Mdogo wa Katoro Mchana Leo

$
0
0

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria


Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi Wagombea Ubunge wa jimbo la Bukombe na Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.

Utafiti wa Twaweza Wapingwa Kila Kona........LOWASSA Asema Majibu Kamili ya Utafiti Ni Octoba 25

$
0
0

Matokeo ya utafiti wa Twaweza kuhusu Uchaguzi Mkuu yamepingwa na wasomi, wanaharakati na wanasiasa, akiwamo mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ambaye ameuponda na kueleza kuwa matokeo halisi yatapatikana Oktoba 25.

Utafiti huo unaonyesha kuwa kama kura zingepigwa kati ya Agosti na Septemba, mgombea wa CCM, Dk John Magufuli angeibuka na ushindi wa asilimia 65, wakati Lowassa angepata asilimia 25.

Lakini wadau  wanasema utafiti huo haujaakisi hali halisi inavyoonekana kwenye mikutano ya kampeni, ambayo inaonyesha wawili hao wanachuana vikali kutokana na kukusanya mashabiki wengi.

“Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki. Tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata,” alisema Lowassa kwenye akaunti yake ya twitter.

Kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Ndanda jana, ikiwa ni muda mfupi baada ya Twaweza kutangaza matokeo ya utafiti huo, Lowassa alisema anashangazwa kwa kuwa wananchi wanaomuunga mkono ni wengi.

“Kuna utafiti wa kura ya maoni umetolewa ukisema eti Magufuli amepata asilimia 65 na mimi 25. Nawashangaa kwa kuwa wanaoniunga mkono wako wengi,” alisema Lowassa na kuwaoji wananchi wangapi watampigia kura katika uwanja huo.

Huku wakishangilia wananchi hao walimjibu Lowassa “Tutakupigia” huku wakinyoosha mikono juu.

Baadaye Lowassa alisema: “Tutawajibu kwenye kura tarehe 25 na hamuwezi kukosea kwa kuwa mnaziona mvi hizi. Nangojea mafuriko ya kura kutoka kwenu.”

Lowassa alijiondoa CCM baada ya jina lake kuenguliwa na Kamati Kuu na kujiunga na Chadema Julai mwishoni. Chama hicho kilimpa fursa ya kugombea urais, akiungwa mkono na vyama vingine vya NLD, NCCR-Mageuzi na CUF vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
 
Maoni  ya  Wadau
Mbali na Lowassa kutokubaliana na matokeo ya utafiti huo, watu  mbalimbali pia wameupinga utafiti huo.

Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama amesema matokeo ya utafiti wa Twaweza hayalingani na hali halisi ya kisiasa inavyoendelea nchini.

“Kile kinachoonekana huko nje ni picha mbili tofauti,” alisema Profesa Mlama.

Amesema licha ya kwamba Twaweza wamefanya utafiti huo kwa kutumia vigezo vyao, matokeo yasingeonyesha tofauti kubwa kati ya wagombea hao.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Profesa Kitila Mkumbo ambaye alisema: “Matokeo halisi tutapata baada ya wananchi kupiga kura Oktoba 25.”

Wakati wadau hao wakizungumzia tofauti ya uhalisia wa hali ilivyo na matokeo ya utafiti, mhadhari wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Paul Loisulie aliwataka wapinzani kutopuuzia maoni hayo ya wananchi, hasa kutoelewa nafasi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Wanaweza wakapuuzia utafiti huo kwa kuwa unampa ushindi Dk Magufuli, lakini sio hili la Ukawa si chama cha siasa kilichosajiriwa kwa sababu itakapofika Oktoba 25 watu wanaweza kwenda kwenye karatasi ya kupigia kura kutafuta Ukawa,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema licha ya kukosa uhalisia kwa hali ya kisiasa iliyopo, matokeo hayo yanaweza kuwa changamoto kwa Ukawa, kujipanga upya na kuangalia mbinu za kuongeza ushawishi kwa siku zilizobakia.

Hata hivyo, Mbunda alisema matokeo hayo hayawezi kutabiri ushindi wa urais kati ya Dk Magufuli na Lowassa.

“Haileti mantiki kwa mashabiki wa Lowassa halafu utafiti uonyeshe amepata asilimia 25 ya kura. Ningependa ufanyike utafiti mwingine ili kuondoa maswali yaliyopo kwa sasa,” alisema.

Wakili wa kujitegemea na makamu mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari alisema matokeo hayo ya Twaweza ni sehemu ya CCM kutapatapa na utafiti aliouita “feki na wa kutengeneza”.

Profesa Safari alisema haiingii akilini, muungano wa Ukawa na Lowassa ukatoa asilimia 25.

“Nusu ya vijana tumeshiriki kampeni za kuhakikisha wanajiandikisha kupiga kura na hata utafiti wetu unaonyesha CCM watashindwa. Kwa hivyo wanatafuta kurubuni taasisi ziwatengenezee uhalali wa kukubalika,” alisema Profesa Safari.

Maoni kama hayo yalitolewa na Profesa Gaudence Mpangalla kutoka Chuo Kikuu cha Ruaha ambaye alisema ni matokeo ya propaganda za CCM.

Alisema Lowassa akiwa CCM, matokeo ya utafiti wa taasisi hiyo yaliyonyesha alikuwa anaongoza kwa ushawishi katika nafasi ya urais.

“Nina shaka na hiyo methodolojia waliyoitumia kwa kweli,” alisema Profesa Mpangalla.

Dk James Jesse, mhadhiri wa UDSM, Kitivo cha Sheria pia alikuwa na shaka na utafiti huo.

“Matokeo haya yanaonesha walihoji watu fulani walioandaliwa na hawakuhoji watu mchanganyiko,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku), Stephen Mwakajumulo alisema kama Twaweza iliweka vigezo sahihi vya utafiti, basi upo uwezekano wa majibu kuwa sahihi.

“Kumbuka mwaka 2005 ilifanya utafiti wa aina hiyo na kueleza kwamba mgombea wa CCM Rais Jakaya Kikwete angeshinda kwa asilimia 80 na matokeo yake yakawa kweli,’’ alisema na kuongeza mara nyingi utafiti unafanyika ili kutafuta mwelekeo wa ukweli kwa kutumia vigezo muhimu.

Wanasiasa
Mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), January Makamba alilalamika kuwa utafiti huo umewapunguzia asilimia za ushindi kwani wanaamini itakuwa zaidi ya asilimia 65.

“CCM haishangazwi na matokeo hayo kwa sababu, Magufuli amefika maeneo ya vijijini zaidi kuliko mgombea yeyote, ameeleza sera zinazoeleweka na ana sifa za uadilifu lakini wanaojadili mabadiliko hawaendani na historia yao, mwonekano wao ndiyo sababu wananchi wamekatishwa tamaa na hoja zao,” alisema ambaye wiki iliyopita alitangaza matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ambayo hakuitaja unaoonyesha kuwa Magufuli anaongoza kwa asilimia 69.

“Mafuriko ya (mgombea wa NCCR-Mageuzi mwaka 1995) Agustine Mrema na (mgombea wa Chadema 2010) Dk Willibrod Slaa hayajawahi kutokea hadi sasa. Haya yanayojitokeza kwa Lowassa badala ya kuwasaidia yanawadhalilisha kwa kuwa mgombea wao hana uwezo hata wa kujieleza jukwaani kwa hivyo matokeo hayo yanaakisi ukweli wa hali halisi iliyopo...sasa wanaopinga na wao waje na utafiti wao tuone.”

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kabla ya kuzungumzia utafiti huo wataujadili kwa kina kuangalia mazingira yaliyotumika kuufanya.

“Kwanza tuone ulivyofanyika ndiyo tutatolea ufafanuzi,” alisema.

Katibu Mkuu wa chama cha Sauti ya Wananchi (Sau), Ali Kaniki alisema matokeo hayo hayawezi kuaminika kwa asilimia kubwa.

“Kuna taasisi Uingereza walifanya utafiti kama huo na chama cha Labour Party kilioneokana kuongoza sana, lakini hadi matokeo yanatangazwa kilianguka vibaya,” alisema.

“Lakini inatakiwa kuheshimu utafiti huo na tusidanganyike na hoja za mafuriko. Wanaojitokeza kwenye mafuriko siyo wote wanaopiga kura.”

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabi alisema matokeo hayo ni chanzo cha kuashiria hatari ya machafuko, hivyo kusingekuwa na sababu ya kutoa utafiti huo kwa muda mfupi uliosalia.

“Ukiangalia ndani yake kuna propaganda za kisiasa zinazochezwa na CCM na inaweza kutuletea shida. Watu wako kwenye presha sana nadhani ingekuwa sahihi kusubiria uchaguzi ufanyike tu.”

Mwenyekiti wa UDP mkoani Dar es Salaam, Joachimu Mwakitinga alisema hakuna uhusiano wa hali halisi na matokeo ya asilimia 65 kwa Magufuli. Mwakitinga ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Mamlaka na Taratibu za Uendeshaji Uchaguzi, alisema matokeo hayo ni uchochezi wa kampeni unaoweza kusababisha madhara makubwa kwenye Uchaguzi Mkuu.

Wanaharakati
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk.Hellen Kijo-Bisimba alisema sampuli iliyotumika kwa matokeo ya utafiti huo inaweza kuwa imeathiriwa na mazingira ya maeneo husika. “Wakati mwingine sampuli inaweza kudanganya na kuwa tofauti kabisa na uhalisia wa hali ilivyo na wakati mwingine kuelezea uhalisia wenyewe.”

Mkurugenzi wa Taasisi ya Sikika, Irinei Kiria alisema sampuli ya Watanzania 1,848 ni idadi ndogo na isiyoakisi Watanzania milioni 23 wanaotarajiwa kupiga kura mwaka huu.

“Lakini pia, wiki mbili tangu kufanyika uchaguzi huo ni muda unaoweza kubadili upepo mkubwa wa kisiasa kwa hivyo haiwezi kuwa matokeo halisi kwa hali ya sasa.”

Kiria alisema matokeo ya utafiti huo kwa Lowassa na Magufuli ni sawa na usiku na mchana kutokana hali halisi ya kisiasa ilivyobadilika katika uchaguzi wa mwaka huu.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi za Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema matokeo na hali ya kisiasa nchini yanaonyesha tofauti kubwa.

Mwenyekiti wa mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Arusha (Angonet), Petro Ahham alisema utafiti ni mzuri, lakini pengo la ushindi wa CCM ni kubwa sana.

“Kwa hali ilivyo sasa huwezi kusema kuna mshindi wa asilimia 65, labda tuelezwe walioulizwa maswali ni waliojiandikisha tu sio hawa tunaowaona kwenye mikutano,” alisema.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, Alline Ngirwa alisema utafiti huo umeonyesha ni maeneo gani hasa ambayo wananchi wanakerwa, kwa hivyo utawasaidia katika kipindi hiki wanapojiandaa kuamua.

“Wananchi wanakerwa na huduma za afya, ukosefu wa maji na elimu duni. Kwa hiyo matokeo ya utafiti huu yanatoa mwangaza kwa wapiga kura na wagombea juu ya vitu wanavyohitaji kwenye serikali ijayo,” alisema Ngirwa.

Mkurugenzi wa taasisi ya Compas Communication, Maria Salungi alisema utafiti huo si matokeo ya uchaguzi na kwamba katika kipindi kilichobaki kuelekea Uchaguzi Mkuu, yanaweza kubadilika.

“Haya sio matokeo ya uchaguzi ni maoni ambayo yanaweza kubadilika kulingana na wagombea watakavyoendelea kufahamika zaidi kwa wananchi, hivyo jamii isipokee kama ndio matokeo halisi,” alisema

Alisema katika utafiti huo, wengi waliohojiwa walitoa majibu kulingana na wagombea kufahamika zaidi, kutokana na majina yao kutajwa mara kwa mara ikiwemo kwenye vyombo vya habari na mabango.

Alishauri vyama vinavyounda Ukawa kuwaelimisha wananchi ambao wanaamini kwamba siku ya kupiga kura, watachagua Ukawa chama ambacho hakipo.

LOWASSA Amfuata NAPE MNAUYE Jimboni Kwake Mtama...Kilichotokea Nape Awezi Amini..Mamia Warudisha Kadi na Kujiunga na UKAWA

$
0
0

LOWASSA Amfuata NAPE MHAUYE Jimboni Kwake Mtama...Kilichotokea Nape Awezi Amini..Mamia Warudisha Kadi na Kujiunga na UKAWA....Waonyesha Wazi wazi Kumuunga mkono Lowassa na Team yake

CCM Makao Makuu Wameongea na Vyombo Vya Habari LEO........Wameongelea Utafiti wa Twaweza na Wamesisitiza Kuhusu Mdahalo

$
0
0
Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.

Mwenendo wa Kampeni 
Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni.

Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi.
  
Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.

Tunaridhika sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu na mikakati mipya. 

Midahalo ya Wagombea
CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:

1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais

2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.

3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa.

UTAFITI WA TWAWEZA 
CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:

1. Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua.

2. Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.

3. Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa.

4. Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.

5. Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.

Lakini vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi. 
  
Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi. Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu.

CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini.

Utafiti ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki. Itakumbukwa kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa asilimia 61.

Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa na Synovate.

Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.

Imetolewa na:

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM

23.09.2015

Edward Lowassa Amenifanya Nimkuchukie Mwanamuziki Diamond Platnumz

$
0
0
Kati ya mashabiki waliokuwa wakikupigania huku mtaani Ni mm!

Kati ya mashabiki waliokuwa wakiperuzi page zako za facebook,instagram na tweeter kila saa Ni Mimi!

Kati ya shabiki ambaye nili kuwa nikiwachukia wabaya wako tena labda zaidi ya ulivyokuwa uliwachukia wewe Ni Mimi!

Kila nilipokua nikisikiliza habari zinazo kuhusu nilikua napata mvuto WA ajabu kuzisikiliza!

Hadi huku mtaani walikua wananitania eti mm Ni msemaji WA diamond!

Hata hapa jamii forums nilikua nakutetea Sana katika post zilizo kua zinakuponda,lakini dah kwa sasa naona bora Tu wakuponde!

Sababu Kuna jambo ambalo umelifanya yaani NATURALLY nimejikuta naanza kutovutiwa na wewe,sina stimu tena yaani najikuta Tu sivutiwi na staffs zako sio Kama napenda ila najikuta Tu.

Mfano nina Kama mwezi sasa sijui ishu zako maana nimeacha kukufatilia;kila nikitaka kufanya hivyo najickia hivyoo Tu!

Yaani hii ishu inatokea Tu automatic!

Sababu kubwa ya Mimi kuingiwa na hali hii Ni pale nilipo ona Kama msanii wangu nayekuthamini umeshindwa kujali hisia zangu za kisiasa.

Mi nadhani Kama ungekua unajua kuwa ilikupasa hata Kama unafanya kazi za chama flani nadhani ilikua poa ungezifanya Kama kazi lakini kitendo cha kuanza kujihuaisha na ushabiki WA kisiasa kwa kuanza kuuponda upande flani WA siasa bila kujali hisia za mashabiki zako tena wale WA damu umekosea mkuu.

Hisia zako za kichama ungebaki nazo moyoni mwako;kumbuka wewe Ni star mkubwa hapa nchini epuka kutengeneza confront za kihisia za mashabiki zako.

Kama management. Yako haikuliona Hilo mi nadhani hakukuwa na ulazima WA wewe kuanza kukandia upande flani kwa kejeli.


Una haki kuwa na chama ukipendacho lakini ungetumia busara katika kuwasilisha hisia zako hizo mbele ya uma.

Ukweli umenikwaza naamini hata wengine walio Kama Mimi watakua wamekwazika poa!

Epuka kuwauwa mashabiki zako kwa sababu ambazo zingekwepeka!


Sijajisikia poa!Isn't the same again.

By Nyuli/JF

Diamond Kuwa Msanii wa Kwanza Kuumizwa na Siasa Mwaka Huu, Soma Hapa

$
0
0
Msanii Diamond ni mmoja wa wasanii vijana waliopata umaarufu kwa juhudi zake na support ya washabiki wake hasa vijana wenzie katika siku hizi za karibuni.

Kwa sasa amependekezwa kuwania tuzo za MTV EMA na ameomba support ya kura ili kupata ushindi.

Lakini response ya safari hii ni tofauti kabisa na huko nyuma hasa baada ya kukubali kujiingiza katika kampeni za kisiasa. Watu kadhaa walimuonya kuwa siasa zitamharibia na kumpotezea washabiki lakini alidharau na wapo Waliompa ushauri eti asijali kwani hata US wasanii wanajihusisha ma kampeni utadhani kampeni zinafanana.

Ukisoma mitandao inaonyesha kuwa wengi hawatamsapoti kwa kura safari hii na kumganya kuwa msanii wa kwanza kiazibiwa na siasa. Wasanii wajifunze kuwa uchaguzi ni kila baada ya miaka 5 ila maisha ya kazi zao ni kila siku.

Wasanii wa Kike Walio Katika Mapenzi na Wadogo Zao

$
0
0
Aunt Ezekiel na Moze Iyobo

Mwigizaji wa filamu za bongo, Aunt Ezekiel, mwenye miaka 29, yupo kwenye mahaba mazito na Moze Iyobo, mwenye miaka 23, ambaye ni mnenguaji wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Kuzidiana huko kwa umri hakukuwafanya washindwe kuendeleza familia yao, kwa sasa wana mtoto mmoja. Aunt Ezekiel anasema: “Kitu muhimu katika uhusiano wetu ni mapenzi tunayopeana ambacho ndicho kitu tunachotaka katika uhusiano wetu na si suala la umri’’.



Shilole na Nuh Mziwanda

Mwingine ni Zuhena Mohammed ‘Shilole’, ambaye ni mwimbaji na mwigizaji wa filamu za Bongo, naye amedondokea katika mapenzi ya msanii mwenzake, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

Umri wa Shilole ni mkubwa kuliko wa Mziwanda, lakini ukubwa wa umri huo hauwazuii kujivunia mapenzi yao na kufanya mambo yao mengine kama kawaida, ingawa mara kwa mara mashabiki wao wamekuwa wakiwapigia kelele kuhusiana na umri wao, lakini majibu ya Shilole ni kwamba; “Sikushawishiwa na mtu kumpenda Nuh Mziwanda, bali moyo wangu ndiyo ulimpenda na hakika ananidatisha siwezi kutengana naye kwa kuwa ni mwanamume kama walivyo wanaume wengine,” hayo ni maneno ya Shilole.

Riyama Ally na Idd Mwalimu

Mwigizaji mwingine ni Riyama Ally, huyu humwambii chochote kwa msanii wa muziki wa kufokafoka (hip hop), Idd Mwalimu Mzee, aliyemchumbia hivi karibuni.

Ingawa Riyama anadaiwa kumzidi mpenzi wake huyo kwa miaka saba, lakini umri huo haumkatishi tamaa mwigizaji huyo, ambaye muda wote amekuwa akiweka wazi kwamba wamepanga kufunga pingu za maisha.

Chanzo: Mtanzania

Siri Nzito Yafichuka Kuhusu Mastaa Kuhama Kutoka Ukawa Kwenda CCM

$
0
0
Mwigizaji wa tasnia ya filamu nchini, Aunt Ezekiel, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Kajala Masanja Kay’ wakiwa CCM. Stori: Na Erick Evarist
NYUMA ya wimbi kubwa la mastaa waliokuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuna siri nzito zilizojificha na Amani limechimbua kutoka kwa wahusika.
Aunt Ezekiel na Vincent Kigosi ‘Ray’ walipokuwa Ukawa.Hivi karibuni, mastaa mbalimbali akiwemo mwigizaji Aunt Ezekiel na Vincent Kigosi ‘Ray’ waliokuwa wakishabikia Chadema kinachoungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walitangaza kuhamia CCM na kuzua taharuki kwa wafuasi wao.

Baada ya wawili hao kuhamia CCM, yaliibuka madai kuwa wamehongwa mamilioni ya shilingi ili waachane na Ukawa na wahamie CCM.
“Hawana lolote tunajua wamehongwa fedha na CCM ili waikane Ukawa, njaa hizi zitatuua jamani,” yalisomeka madai hayo katika mitandao mbalimbali.

Mwanahabari wetu baada ya kushuhudia madai hayo yakizidi kusambaa mitandaoni, kwa nyakati tofauti aliwapigia simu Ray na Aunt ambao kwa pamoja waliyakana na kuwataka Watanzania kusikia siri iliyowafanya wao kushtuka na kuhamia CCM.
“Jamani niwaambie ukweli, sijahongwa na chama chochote. Nimetafakari kwa makini na kuamua kuhamia CCM kutokana na ukweli ndiyo chama kilichotufikisha hapa tulipo na kinachoweza kutufikisha mbali zaidi.

“Ninawashangaa wanaozungumzia kuwa tumehongwa ili tuhamie CCM, mbona hawasemi Edward Lowassa na Fredrick Sumaye (mawaziri wa zamani-CCM) wamehongwa kuhamia Ukawa?
“Nisiwafiche, nafsi ilikuwa inanisuta sana kuwa Ukawa. CCM ndiyo kila kitu, maendeleo ya kweli yanaletwa na mtu anayezungumza sera na kumaanisha kile anachozungumza, CCM wamesimamisha mgombea ambaye hata kama wewe ni mpinzani utakubali tu ni mchapakazi.

“Niwasihi vijana wenzangu kujitambua, kusikiliza sera za wagombea wote na kufanya uamuzi sahihi, wasisukumwe na mhemko tu inayohusishwa na mabadiliko. Wampime mgombea anayehubiri mabadiliko anamaanisha?”

Kwa upande wake Aunt alisema: “Kwanza nikatae sijapewa hata shilingi na CCM. Kilichonihamisha Ukawa ni sera na Ilani. Sera na Ilani ya Chadema haizungumzi moja kwa moja kumkomboa Mtanzania wa hali ya chini.

“Wanahubiri mabadiliko tu bila kueleza watayaletaje? Busara wala kusisitiza amani hakuna. CCM ina sera na Ilani inayotekelezeka. Nimeilewa ndiyo maana nikaamua kuunga mkono. CCM ina viongozi waadilifu, wenye hofu ya Mungu, wasiokuwa na tamaa ya madaraka tofauti na wale wa Ukawa.
“Niwaase vijana na Watanzania wote ambao bado hawajashtuka, washtuke na kuja CCM ambako kunaeleweka.”

Diamond Platnumz Azua Kizaazaa Kampeni za Magufuli Bukoba....

$
0
0
Kundi kubwa la vijana wakigombea kumuona mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’, katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba.
Stori: Richard Bukos aliyekuwa Kagera
UNAZI! Kundi kubwa la vijana wa kike na kiume, mwanzoni mwa wiki iliyopita walizua kizaazaa baada ya kumgombea kumuona kwa karibu na kutaka kuzungumza na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ mara baada ya kumaliza kutumbuiza katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli uliofanyika katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba.
Baunsa wa Diamond akiwatoa vijana na akina mama waliolizonga gari alimokuwa Diamond.
Baada ya kumaliza ngwe yake ya kuburudisha, msanii huyo aliteremka jukwaani na kwenda alikopangiwa kukaa, lakini alifuatwa na dada mmoja aliyetaka kuzungumza naye, huku vijana wengine wakisogea eneo hilo, kitu ambacho mabaunsa walikikataa na kumfanya msanii huyo kukimbilia katika basi dogo aina ya Coaster lililokuwa limetayarishwa kwa ajili yake na wacheza shoo wake.
…Wakilikimbilia gari hilo baada ya kuondoka viwanjani hapo.
Hata hivyo, wakati mkutano huo ukiendelea, umati zaidi wa vijana uliendelea kulifuata basi hilo na kujazana katika dirisha alilokaa Diamond, jambo lililowapa wakati mgumu mabaunsa kuwasogeza, hadi polisi walipofika na kufanikiwa kuwatawanya, huku gari hilo likiondolewa eneo hilo.
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Hata hivyo, baada ya basi hilo kupata upenyo wa kumkimbiza mwanamuziki huyo, kundi kubwa la vijana wa kike na kiume walilifukuza gari hilo mpaka dereva alipoongeza kasi.

Kabla ya mkutano huo mkoani hapa, Magufuli alianza kunadi sera zake katika Vijiji vya Kaziramuyagwa, Kyamyorwa, Kasharunga, Rulanda na kufanya mkutano mkubwa katika Uwanja wa Zimbihile uliopo Muleba Kusini jimbo analogombea Prof. Anna Tibaijuka.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Baada ya hapo kampeni zilihamia Muleba Kaskazini ambapo Magufuli alimwaga sera katika maeneo ya viwanja vya wazi vya Kamachumu, Maruku na Jimbo la Bukoba vijijini kabla ya kufanya mkutano wa kihistoria katika viwanja vya Bukoba mjini.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images