Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

YA MOYONI KUHUSU MANCHESTER UNITED..........

$
0
0
Habari zenu mashibiki wote wa Man U na wadau wote wa soccer,

Awali ya yote naomba ni declare interest, mi ni die hard Man U fan, nina zaidi ya mapenzi na timu hii mi nina mahaba na timu hii. na nasukumwa na mahaba hayo kuongea haya

Ni wazi kwamba wengi wa mashabiki wa timu hii tumeipenda timu hii sio tu kwa sababu ilikua inafundishwa na SAF bali ni kwa sababu ilikua ni timu ya washindi, timu yenekuleta ushindani mpaka dakika ya mwisho, how many times tumechomoa magoli dk za 90,94 au 96 wakati wapinzania washaamini ushindi upo kwao it was in our DNA, that is Manchester I used to know, je Man U hiyo imeenda wapi…?
Naelewa na kuamini msemo usemao mvumilivu ula mbivu lakini vilevile dalili ya mvua ni mawingu na chelewa chelewa utakuta mwana sio wako.
Wapo wadu wanajaribu kusema hii hali ya timu yetu sa hivi ni kawaida tu hata SAF aliipitia, katika swala la kuipitia sina ubishi nalo ila kusema ni kawaida hapo ndio tunatofautiana,
Hivi expectation za Man u wakati Fergie anakabidhiwa timu zilikua sawa na za Man U ya sasa…? Aliikuta timu hipo katika level gani katika timu za Uingereza…? Hivi expectations walizonazo washabiki wa Swansea kwa kocha wao mpya ni sawa na za mashabiki wa Man U…? je mnataka kusema lengo la kuleta kocha mpya ilikua ni kutoka level zetu za big 4 kwenda kuwa wafalme wa big 7…?
Mpaka hapo nimeshaonesha mlengo wangu ni hupi, YES simkubali Moyes na I put all blames on him kwa kiwango kibaya cha timu yetu cha kihistoria, wanao msupport Daudi wamekua wakisema tumpe muda anajenga timu, nafikiri wangesema tumpe muda maana anabomoa iliyokuwepo kwanza ndio baadae aje kujenge timu mpya….
Timu hii iliyoonekana mbovu leo hii ndio timu hiyo hiyo iliyochokua vikombe msimu uliopita under SAF na benchi lake la ufundi, cha kustaajabisha daudi alipokuja akataka kuonesha ulimwengu ye ni mjuzi wa mambo akafukuza bench lote la ufundi nakuleta lake amabao limeprove failure, binafsi nilifikiri Moyes angekua na short term plan na long term plan, short term plan ingekua ni kuimantain hadhi ya Man U kwa kupitia timu hii hii aliyokuta nahilii ingewezekana kwa kuliacha bench la ufundi alilolikuta maana ndio linaimudu hii timu while long term plan ingekua kutengeneza timu yake mweneyewe kwa kufanya mabadiliko kidogo kidogo amabayo hayata athili timu yote, matokeo yake katuletea wakina Philip Nevell….kweli of all legends wa man U huyu dogo ndio ameona awe mshauri wake…
Na ikumbukwe Moyes ni Manager na sio coacher/mkufunzi na kazi ya manager sio kumfundisha RVP kufunga au Vidic kukaba bali ni kuleta game plan afu wachezaji wanaifollow hiyo game plan, na ili kuwafanya wachezaji wamaiweze game plan yako kwanza ni mpka wae na imani na wewe, pili hiyo game plan yako hiwe workable na mwisho kabisa laziama uwe the good MOTIVATOR, na manager mazuri dunianiani ni good motivator hata kama timu inamapungufu as long as kocha wao yupo wataperform tu kwa kiwango sawa na timu zilizo bora, Moyes kashindwa kabisa hii…. Mbinu za man U siku hizi the are very obvious and predectable mpaka timu zinazaotaka shuka daraja can crack our plans easily and use them against us, mfano game ya juzi na Fulham, mbinu za moyes zilikua old school kabisa, tanua uwanja then piga long crosses, by the way tulipiga cross zaidi ya 80 and then what…!! I wonder mata alinunuliwa kwa ajili gani kama hii ndio game plan ya Moyes
“Moyes the chosen one” hii kauli ndio inatuua sasa man u, sijui ni nini SAF alikiona kwa Moyes mpaka akaamini is the right guy for the Job, na sijui alishindanishwa na nani na kuibuka kinara au kipi exactly walikiona kwa Moyes, binafsi nilipoona The Boss kampendekeza sikua na shaka kabisa ni kiaamini thr Boss siku zote huwa yuko sawa kwenye maaamuzi yake, ila sas nahisi na naaamini on this he gotta it all wrong, ikumbukwe huyo Fergie before coming to Man he was already the winner, he had already won the Scottish League with Aberdeen and he kills the domination of Rangers and Celtics akaja England akaikuta man U hiko dhoofu bin hali, lakini akawatoa waflme Liverpool kileleni, Moyes c.v yake inaonesha alishawai kushinda nini au nini kilichomfanya apewe timu kubwa kiasi hiki…? 
Hivi tumekua West Ham united kwamba tunamantain kubakia kwenye league tu….timu imekosa ushindani kabisa afu watu tuansema apewe muda, sa apewe muda wa nini….
MWISHO; nothing personal, ila Moyes kaishaprove he gotta nothing to offer for Man U tukubali tu tulibugi hapo, na ka nakosa Moyes prove me wrong leta ushindi nyumbani, ntakuja hapa na kusema YES you are the right person for our team after all hakuna shabiki anafurahia kushindwa wala hakuna shabiki anajinyonga au kumchoma mtu kisu timu yake inaposhinda kwa kuwa hatupati ushindi as we used to get basi something is wrong somewhere, and it is my duty as a fan to shout about it
By Mbeky From JF

URAIS 2015:LOWASSA, SUMAYE, MEMBE, MAKAMBA NA WASIRA WAITWA KUHOJIWA

$
0
0
Vigogo wanaowania au wanasemwa kuwa wameanza kampeni za urais 2015 sasa wameandikiwa barua na kuitwa ili kuhojiwa na kamati ya maadili juu ya dhamira yao.

Dar es Salaam. Baadhi ya makada wa CCM ambao wataitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho, wanakabiliwa na shtaka la kutoa rushwa kwa lengo la kushawishi kukubaliwa kwao, Mwananchi limebaini.

Makada hao ni wale wanaodaiwa kuwa katika harakati za kuwania urais wa 2015, hatua ambayo imekigawa chama hicho katika makundi yasiyo rasmi ya yanayowaunga mkono wagombea hao.

Tovuti hili imedokezwa kuwa mgombea mmoja wa nafasi hiyo mwenye ushawishi mkubwa aligawa fedha Sh200,000 zilizoambatana na kadi za kuwatakia heri ya Krismasi na Mwaka Mpya 2014 idadi kubwa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.

Kadhalika, habari kutoka ndani ya chama hicho zinasema baadhi ya wanaojiwinda kwa ajili ya uongozi, pia waligawa fedha kwa kigezo cha kuwashukuru wajumbe waliowachagua kuingia katika Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo, taarifa zaidi zinasema baadhi ya wajumbe waliopelekewa kadi hizo na fedha, walitoa taarifa kwa uongozi wa juu wa CCM pamoja na kuzirejesha, huku wakitaka wahusika wachukuliwe hatua.

“Kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya chama kwamba ugawaji wa fedha nyingi kiasi hicho haupaswi kuvumiliwa hata kidogo, kwa hiyo ni dhahiri kwamba suala la chama kuchukua hatua halina mbadala, lazima hatua zichukuliwe,” alisema mmoja wa watendaji wa CCM makao makuu Dodoma na kuongeza:

“Waliorejesha hizo kadi na fedha hatukuwaruhusu waondoke hivihivi, bali tuliwataka waandike barua za malalamiko maana tunaweza kuwahitaji kwa ajili ya kutoa ushahidi mbele ya Kamati ya Maadili.”

Uchunguzi unaonyesha kuwa miongoni mwa waliorudisha fedha na kadi hizo ni wenyeviti wa wilaya na wajumbe wa NEC wa wilaya ambao ni sehemu ya walioshinikiza kuchukuliwa kwa hatua.

Akizungumzia suala hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Philip Mangula alisema mwanachama yeyote wa chama hicho hatakiwi kutoa michango, misaada, zawadi kwa mtu au katika shughuli yoyote bila kupata ridhaa ya uongozi.

“Kufanya jambo hilo ni kwenda kinyume na kanuni za chama. Ndani ya chama kila ngazi ina Kamati ya Maadili, wote ambao wameanza kwenda kinyume na kanuni za chama watahojiwa katika kamati hizo,” alisema Mangula na kuongeza:

“Hairuhusiwi kuwasafirisha wajumbe, kuwapa malazi, chakula, vinywaji na ukifanya hivyo utakuwa unakwenda kinyume na utaratibu uliowekwa na Kamati ya Sheria, Katiba na Kampeni.”

Akihutubia kilele cha maadhimisho ya miaka 37 tangu kuzaliwa kwa chama hicho, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliziagiza Kamati za Maadili na Usalama, kuwachukulia hatua stahiki viongozi na wanachama wake wanaomwaga fedha ili kupata uongozi.

Kadhalika, Rais Kikwete alipozungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Mbeya, alisema kuanza kwa kampeni kabla ya wakati wake ni moja ya mambo yanayosikitisha na kwamba suala hilo limekabidhiwa kwa Mangula kwa hatua zaidi za kinidhamu.

Source: Mwananchi

WADADA MMEZIDI SASA...KHAAA

$
0
0
Kuna mdada nimeanzisha naye uhusiano kama wiki moja iliyopita. ni mtu mwenye ajira yake, mshahara analipwa. siku tumekutana kwa first date alikuja na rafiki yake tukanywa na kula aafu tukaagana. mkononi alikuwa na simu ya kama laki 5 hivi. Siku tatu baadaye nikampigia simu hapokei aafu akanitumia msg "simu imetumbukia kwenye maji hi yo siwezi kupokea". Jana kanambia anaomba mimsaidie ili apate mawasiliano, nikamwambia ntanunua ya elfu 50 ili awepo hewani anapotafuta nyingine. Cha ajabu ananambia anataka kama ile ile hivyo nimwongezee laki 2 nyingine ataongeza! Nikacheka kimya kimya huku nikishangilia kusave 50 yangu! Jamani mishahara yeti ina bajeti yake na so kwa ajili deny! na wengine tunataka kuwa na watu wa kudumu nao,mnatutisha na hizo harakati zenu za usakaji was hela! Tipelekane taratibu jamani, looh!

BEN POL ATOA WIMBO ALIYOMSHIRIKISHA JOH MAKINI..UNANICHORA..SIKILIZA NA DOWNLOAD HERE

$
0
0
Ile single iliyokuwa ikisubiriwa kwa ham , leo hii imedondoka kwenye maskio yako.Mkali wa R&B kipenzi cha akina dada, Ben pol leo hii ameachia mzigo wake mpya chini ya mkono wa producer Fundi Samweli "Unanichora" akiwa na Joh  Makini

FUKWE ZA TANZANIA NI UCHOCHORO WA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Wakati vita ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya ikiendelea nchini, wasafirishaji wa dawa hizo wameanza kutumia fukwe ndogondogo za bahari nchini kuziingiza kutoka Mashariki ya mbali, gazeti hili limebaini.

Januari 10, mwaka huu saa 6:30 usiku, mwandishi wetu alishuhudia mzigo unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya, ukishushwa kutoka kwenye boti, eneo la Salender Bridge, nyuma ya Kituo cha Polisi kilichopo eneo hilo.

Baada ya boti hiyo kutia nanga, walishuka watu zaidi ya 10; Wazungu wawili, Waafrika kadhaa na mmoja mwenye asili ya Asia na kuungana na wengine wanne ambao tayari walikuwa katika eneo hilo wakiwa ndani ya magari mawili.

Mara moja walianza kupakua mizigo iliyokuwa imefungwa kwenye maboksi na kupakia kwenye magari ambayo yalikuwa yameegeshwa mbali kidogo na ufukwe huo. Kazi hiyo ilichukua muda usiozidi nusu saa na baada ya mizigo kupakiwa, magari hayo moja likiwa ni Land Cruiser liliondoka na kuelekea upande wa Morroco na jingine aina ya Nissan liliondoka kwenda uelekeo wa Posta Mpya.

Wakati magari hayo yakiondoka kwa mwendokasi, boti iliyokuwa na mzigo huo nayo iling’oa nanga na kuelekea katikati ya Bahari ya Hindi.

Chanzo chetu kilisema mzigo ulioshushwa ni dawa za kulevya na kwamba boti hizo ndogo hufika eneo hilo hata mara mbili kwa wiki.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa dawa hizo huingizwa nchini kwa meli kubwa za mizigo, hasa zile zinazotoka Iran, Pakistan na Afganistan.

Ukamataji polisi

Mwandishi wetu aliwasiliana na polisi kuhusu njia hiyo ya kuingiza dawa za kulevya nchini na jeshi hilo kuahidi kutoa majibu baada ya kufanya ufuatiliaji. Kabla ya kutoa majibu juu ya ufuatiliaji huo, polisi ilikamata meli kutoka Iran ikiwa na kilo 201 za heroini katikati ya Bahari ya Hindi.

Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kama taarifa hizo zingeripotiwa katika vyombo vya habari, ingekuwa vigumu kwa jeshi hilo kufanikisha kukamatwa kwa wahusika.

Katika wiki moja iliyopita, kilo 846 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh38 bilioni zimekamatwa kwenye mipaka ya Tanzania iliyoko katika eneo la Bahari Kuu, kiwango ambacho ni kikubwa katika rekodi ya kukamatwa kwa dawa za hizo.

Dawa hizo zilikamatwa kati ya Februari 2 na 5 mwaka huu. Kilo 350 za heroini zilikamatwa Februari 5 na wadhibiti wa dawa za kulevya wa Australia na kilo 265 za heroini zilikamatwa na wadhibiti wa kimataifa wa Canada, zote zikiwa zinaelekea Tanzania.

BILIONEA DAR ADAIWA KUTUMIA MABUNSA WAKE KUMLAWITI MWAJIRIWA WAKE.

$
0
0

Ni Ally Awadh wa kampuni ya mafuta ya Lake Oil
Atuhumiwa kumfanyia unyama mtumishi wake
Polisi Oysterbay, Kanda Maalumu wamgwaya
Jumanne, Februari 11, 2014
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua “kujipima uzito” dhidi ya bilionea Mtanzania, Ally Edha Awadh ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaaminayoagiza, kuuza na kusafirisha mafuta na biashara nyingine nyingi. Awadh anayetajwa kama mmoja wa mabilionea vijana nchini, amefunguliwa mashitaka Polisi ya kumteka, kumdhalilisha kinyume cha maumbile na kumpora mali mmoja wa wafanyakazi wake.
Uamuzi wa Waziri Mkuu Pinda umekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini, katika kile kinachoonekana ni kumgwaya bilionea huyo, kupuuza kumsaidia mlalamikaji huyo mwenye umri wa miaka 32. Kwa sababu za kiutu na za kitaaluma, jina la mlalamikaji tunalihifadhi kwa sasa.
Hatua ya Pinda imetokana na barua ya mlalamikaji ya Novemba 29, mwaka jana aliyomwandikia baada ya Jeshi la Polisi-kuanzia Kituo cha Oysterbay, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na hata Makao Makuu, kupuuza kumsaidia mlalamikaji ili aweze kutendewa haki.
Baada ya kuipata barua ya mlalamikaji, Pinda alimwagiza msaidizi wake, Leila Mgonya, amwandikie barua Katibu wa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kazi hiyo ilifanywa Desemba 29, mwaka jana.
Katika barua hiyo ya Pinda iliyoandikwa kwa niaba yake na Mgonya, inasema, “Miongoni mwa mambo aliyofanyiwa mlalamikaji na mwajiri wake (Awadh) ni pamoja na kupigwa na kujeruhiwa mwili mzima kama picha zilizoambatanishwa na barua ya mlalamikaji zinavyoonyesha, kudhalilisha pamoja na kudhulumiwa mali zake kama inavyobainishwa katika barua ya mlalamikaji.
“Kwa kuwa suala hili limejikita zaidi katika utendaji wa Jeshi la Polisi, imeelekezwa kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ishughulikie suala hili kikamilifu kwa lengo la kumsaidia mlalamikaji kupata haki yake kwa mujibu wa sheria na kuona kuwa haki inatendeka.
“Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu angependa kupata mrejesho kuhusu suala hili. Tafadhali mfikishie Mheshimiwa Waziri maelekezo hayo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.”
Pamoja na maagizo hayo ya Waziri Mkuu, JAMHURI imebaini kuwa hakuna hatua zozote za maana zilizokwishachukuliwa dhidi ya Awadh na washirika wake.

Barua ya mlalamikaji kwa Waziri Mkuu
Mlalamikaji katika barua yake kwa Waziri Mkuu, anaanza kwa kusema, “Mheshimiwa, jina langu lipo hapo juu ni kijana wa Kihidi (Mtanzania) umri wangu ni miaka 32 mzaliwa wa Tanga, nina mke na watoto.
“Mheshimiwa, nimesomea uhasibu na nimefuzu mwaka 2004 masomo yangu… na nikaajiriwa na Ally Edha Awadh katika kampuni yake iitwayo Lake Oil Ltd Septemba, 2010 na kuwa Finance Manager (Meneja Fedha) katika kampuni yake.
“Bila matarajio yangu, ilipofika Mei 2, 2013 mwajiriwa mwenzangu aitwaye Ahmed alifika ofisini kwangu na kuniarifu ya kwamba naitwa na Mkurugenzi Ally Edha, ilikuwa saa 11:30 za jioni Alhamisi na bila kusita nikaongozana naye hadi kwa Ally Edha nikifahamu naitwa kwa ajili ya kazi kiofisi.
“Nilishangaa nilipofika tu ofisini kwake akahitaji simu yangu, nikampa mara akamuagiza stafu mwingine aitwe Fahim akafuate laptop yangu na vifunguo ya gari yangu ofisini kwangu na ofisini kwake tulipobaki mimi, yeye na Ahmed. Alianza kunitukana na kuniambia mimi ni mwizi nimemwibia dola milioni 10 za Marekani (Sh bilioni 16).
Mara ilipoletwa laptop yangu na funguo za gari akanichukua na kuniagiza nimfungulie e-mail yangu. Nilikataa na kumwambia hii ni mail yangu binafsi na siyo ya ofisi yake, siwezi kufungua pana kazi za wateja wangu wengine (mimi ni mhasibu wa wengi). Akanitishia kunipeleka Polisi, nami nikamkubalia.
“Mheshimiwa, tukifuatana na wafanyakazi wake wengine, Ahmed, Fahim, yeye na K.V Choudry, tulishuka chini na kuingizwa katika gari ya Ahmed. Gari ikawashwa na mara akamuagiza dereva Ahmed lile gari tulilopanda lipelekwe godown (ghala) ili abadilishe gari kwenda Polisi. Cha kushangaza nikaamrishwa nishuke pale godown na kuingizwa ndani, pamoja na wale tuliofatana nao. Nilishangaa kuwakuta wengine wawili (yeye Ally Awadh anadai ni mabaunsa wake) wanaitwa Waitey na mwingine ni Abeid.
Mabaunsa waanza kumlawiti
“Mheshimiwa, wakajumuika pamoja wakanivua nguo, wakanilawiti. Wakanipiga sana kwa kutumia nondo, mikanda mizito, makonde ya nguvu na huku huyo mtumishi mwenzangu Ahmed akiwa ameielekeza pistol (bastola) kichwani kwangu kwa kuniambia leo ni kifo changu endapo nitakataa kuyakubali anayotaka bosi wake, yaani Ally.
“Mheshimiwa, mateso haya yalikuwa zaidi ya masaa mbili na nusu (zaidi ya saa mbili na nusu) nikilazimishwa nikubali kutoa kila kitu changu (assets) nimpatie yeye, vinginevyo wataniua na wakanionesha picha za maiti wawili zilizokuwepo katika simu ya baunsa wake akidai (Ally) angeniua kama hao, na kunifunga katika mfuko wa plastiki na kunipeleka shambani kwake Soga kunizika.”
Mlalamikaji anaendelea kumweleza Waziri Mkuu kwamba kutokana na mateso makali na vitisho alivyopewa, alilazimika kukubaliana na maelekezo aliyopewa, yote hiyo ikiwa ni mbinu ya kunusuru uhai wake.
Apigwa picha akiwa uchi

“Ndipo Ally Edha akanipiga picha nikiwa uchi na kusema endapo nitaenda Polisi, yeye atazitoa hizo picha kwenye mitandao ya intaneti kunidhalilisha. Hivyo nikapewa shati langu nivae na kupelekwa ofisini kwake na kulazimishwa niandike kukubali kwamba vitu vyangu vichukuliwe,” anasema.

Kwa mujibu wa mlalamikaji, mali zilizochukuliwa ni:

A: Nyumba yangu na mke wangu iliyopo Nairobi, Kenya
B: Gari zangu mbili (i) Toyota IST T786 BZG (ii) Toyota Fortuner T503 BQC
C: Bastola yangu 6mm niliyonunua Mzinga.
D: Fedha taslimu dola 100,000 (Sh zaidi ya milioni 160)
E: Mkataba wangu wa nyumba na duka (vyangu) vilivyoko Uhuru Heights
F: Ofa zangu tatu za viwanja Kigamboni

Asainishwa kwa nguvu
“Ndipo nikasainishwa; na majira ya saa 3 za usiku wakanitia katika gari aina ya Navara nyekundu mali ya kampuni –dereva akiwa Ahmed wakiwamo mabaunsa wawili, Ally Edha, na mimi. Hadi nyumbani kwangu Upanga.
“Mheshimiwa, inasikitisha kwa sababu mke wangu alipopiga simu nikiwa kwa Ally alinilazimisha niongee na mke wangu kwa lugha ya Kiingereza, na siyo Kihindi. Alikuwa anapiga kwa kutoamini kwa nini niongee Kiingereza badala ya Kihidi hadi simu ikaisha pesa ndipo tulipofika tukamkuta yupo chini anangoja aletewe vocha na mlinzi.
“Wakanibadilisha shati na kunivisha la Abeid (langu lilijaa damu). Wakamweka chini ya ulinzi mke wangu. Tukapanda juu nyumbani hadi sitting room wakamnyang’anya simu na kumkalisha chini. Ally Edha akanilazimisha nimpeleke bedroom (chumba cha kulala), ndiye akazichukua documents (nyaraka) zote na hizo pesa na mara wakaingia Choudry, Sree Kumar na Ramana ambao wote ni wafanyakazi wake; na ni Wahindi wakiwa na laptop na printer.
“Ghafla wakiwa na hizo laptop huyo Choudry na Kumar wakaelekezwa kuandika maneno ya mkataba ambayo mimi na mke wangu tukalazimishwa kuweka sahihi zetu kukubali kuzitoa mali zetu kwa huyo jambazi Ally. Nakumbuka hata watoto wanalia kutaka maziwa nyumbani Ally Edha alizuia wasipewe.”
Mlalamikaji anaendelea kusema kwamba akiwa na maumivu makali, Ally Edha alitaka siku ya pili amtolee pesa katika akaunti yake iliyopo katika Benki ya STANBIC, Tawi la Nyerere Road; na akasema angezifuata hizo fedha siku ya Jumamosi.
“Alizijua hizo fedha kwa sababu ni akaunti niliyoitumia kuweka pesa za mshahara. Mshahara wangu ulikuwa Sh. milioni 6 kwa mwezi. Kama hilo halikutosha, alikuta chumbani kwangu vitabu vitatu vya hundi za akaunti ya pamoja na mke wangu; Standard Chartered (Nairobi, 2), Benki ya Exim (3), Benki ya NBC, akatulazimisha tuzitie sahihi zetu- na tukafanya hivyo.”
Mlalamikaji, mkewe waonywa watauawa
“Siku hiyo aliniambia mimi na mke wangu kwamba kama angesikia tumemueleza mtu yeyote haya mambo, angetuua. Kweli tukaogopa sana hadi siku ya tarehe 4, 2013 ndipo alipomtuma Sree Kumar kuja kuchukua zile milioni 22 alizoagiza nizitoe katiba akaunti yangu ile siku ya tarehe 2 Mei 2013. Nilimkabidhi Sree Kumar akampelekea Ally Awadh.
“Mheshimiwa, nakumbuka namna tarehe 8 Mei, 2013 Choudry (Mfanyakazi wa Ally Awadh) alinitumia meseji mbili kwa kutumia simu yake kwamba angependa aje nyumbani waniletee pochi waliyochukua siku ya tukio nyumbani kwangu ambayo ni ya mke wangu yenye kadi yake ya ATM na kopi ya leseni ya udereva. Nikawaambia sitokutana nyumbani, tukapanga anikute Mtaa wa Morogoro/Jamhuri akaleta akanikabidhi bila ya kunisalimu.”
Danadana za Polisi Oysterbay
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, siku ya Jumamosi tarehe 4 Mei 2013 nilipatiwa wakili aitwaye Mwanganga. Nikamueleza, akaamua tukamuone RPC Kova (Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam). Tulifika saa za mchana, nikamueleza na nilipotaka kumwonyesha majeraha yangu alikataa na kusema kuangalia majeraha sio kazi yake ila alipiga simu Oysterbay akatuagiza twende. Tukafuatana na wakili hadi Oysterbay.
“Mheshimiwa, hiyo tarehe 4 Mei 2013 tulifika Oysterbay tukamuona ofisa mmoja simfahamu jina ila sura namfahamu (wakili wangu anamfahamu). Hakuonekana kujali sana, ndipo akatupeleka ofisi nyingine (wakili anaifahamu). Hapo huyo askari akamuita mama mmoja polisi ndipo akatupeleka ofisi nyingine, ofisa akamuagiza andike maelezo naye akanisikiliza na akanipeleka kwa ofisa mwingine. Huyo ndiye aliandika maelezo yangu.
“Cha kushangaza huyo ofisa alianza kusema ‘wewe tayari umetajwa kwenye kesi nyingie ya Lake Oil’, lakini tukamwambia aandike maelezo yangu. Yeye alidai ‘pana Mhimdi mmoja, Mukesh ambaye ni Internal Auditor (Mkaguzi wa Ndani) wa Lake Oil yupo ndani rumande hapo, na wewe pia unapaswa uwekwe ndani’. Lakini huyo ofisa na mwanasheria wangu walitoka nje. Cha kunishangaza wakili akanimbia eti inatakiwa niweke dhamana nikatibiwe ili Jumatatu nirudi au nipelekwe kutibiwa nirudishwe rumande. Lakini wakili baadaye alinifahamisha wameyamaliza- kampatia Sh 100,000; hivyo ningepaswa nimrejeshee hizo pesa.
“Hivyo statement (maelezo) iliandikwa na nikapewa medical examination report yenye case file no. OB/RB/7853/2013 ya tarehe 4 Mei, 2013. Ndipo nilipoenda Sinza Hospitali kwa matibabu.”
Woga wamfanya akimbilie Zanzibar

Mlalamikaji anasema kutokana na woga wa ahadi za mateso zaidi au kuuawa kama alivyoahidi Awadh, aliamua Mei 5 aende mafichoni Zanzibar.

“Tarehe 6 Mei nilipigiwa simu na Mutafungwa aliyejitambalisha kwangu kwamba yeye ni OCD wa Kinondoni akisema amesikitishwa kuisoma statement yangu na angependa kukuona. Hivyo nikarejea Dar es Salaam na tarehe 7 Mei nikaenda na kaka yangu na wakili wangu. Tukamwona, akaagiza kwa ofisa mwingine wa CID kumweleza hiyo kesi ni ya ukweli kwa hiyo wakamatwe wahusika mara moja na kuniagiza nishirikiane naye.
“Baada ya siku mbili, yaani Mei 9, nikapigiwa siku na Salum (CID Osysterbay) akanieleza yeye ndiye mpelelezi wa kesi yangu na angependa kuniona. Tahere 12 Mei nilimuona Salum. Kwa sababu ya kuwa Zanzibar ndiyo maana nilichelewa kumuona. Akanisikiliza na kusema angepeleleza hiyo kesi na angeniita.
“Mheshimiwa, kila mara huyu Salum hakunipa msaada ipasavyo kwa madai kwamba hajamuona Ally Edha. Nilishangaa sana sababu ofisi ya Ally Edha ipo, wanaijua na iweje waseme hawamuoni? Baada ya muda, katikati ya Mwezi wa Ramadhani, Salum aliniita na kuniambia mwenzake aitwae James angeweza kunisaidia kuipata silaha yangu kutoka kwa Ally na nikamuona huyo James ambaye aliahidi Ally Edha akirudi safari yake kwa asilimia 90 nitapata pistol (bastola) yangu. Akasisitiza pia akimuona siku ya kwanza tu Ally angenipatia hiyo bastola.”
Aombwa chochote akishasaidiwa
“Nakumbuka katikati ya Oktoba, mwaka jana Salum alinipigia simu akasema James anauliza endapo akinisaidia kuipata hiyo bastola mimi ningempa zawadi gani. Nikamjibu, ‘Nitampatia anachotaka’ ilimradi nipate bastola na vitu vyangu.
“Mheshimiwa, Nashangaa tangu wakati huo walipoanza kutaka chochote kwangu, hawajanipigia tena, wala kunisaidia.

Nami nilishajiandaa kuwakamatisha kwa rushwa. Nikaendelea kupata matatizo ya kujificha kwa kuamini Ally Edha ana mamlaka ndani ya Jeshi la Polisi na anaweza kunifanyia chochote atakacho.
“Mheshimiwa, Nikashauriwa niende kutoa taarifa Makao Makuu ya Polisi (wizarani). Hivyo tarehe 27 Novemba, mwaka jana nilienda huko nikamuona Bwana Laizer ambaye ni Kamishna. Nikamueleza na nikamuonesha vielelezo. Alisikitika sana na hapo alimuagiza RPC wa Kinondoni ashughulikie hilo jambo na amueleze kwa kila kinachoendelea.
“Hadi leo tarehe 29 Novemba, nimeamua nikatumie barua hii na vielelezo vyangu ili unisaidie, kwani polisi hawanisaidii tangu nifanyiwe unyama huu. Najiuliza na kujiona mkiwa kwa kuamini kwamba huyu Ally Adha Awadh yupo juu ya sheria? Iweje polisi wamlinde tangu Mei 2013 hadi leo pasipo kukamatwa? Mheshimiwa Naomba msaada wako.”
Barua hii ya mlalamikaji aliweza kupeleka nakala kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Utawala Bora, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.
Kwa upande wake, Awadh amegoma kuzungumza na JAMHURI. Mara kadhaa amepigiwa simu yake, lakini amekataa kuzungumza hata pale simu ilipopokewa. Ametumiwa ujumbe kwa nyakati na siku tofauti, lakini hadi tunakwenda mitamboni alikuwa hajajibu.
Ujumbe mmoja ulisema, “Habari za kazi.

Hapa ni gazeti JAMHURI. Tuna habari za kesi ya … dhidi yako. Tunaomba kujua kama hili suala unalijua kabla hatujaichapisha. Tangu jana tunaomba utupatie majibu- bila mafanikio. Tumetekeleza wajibu wetu kitaaluma kwa hiyo hatustahili lawama. Mhariri”. 

CHANZO: Gazeti la Jamhuri

RAY AVUNJA UKIMYA"NIMEMISS KUWAKATIA VIUNO MASHABIKI WANGU STEJINI"

$
0
0
Ray C ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila, ameahidi kurudi kazini (kwenye muziki) muda si mrefu sababu hata yeye ameimiss mic na jukwaa, “Naimiss steji vibaya mno!!!!” ameandika Ray C katika Instagram yake.

“Likizo ya mwaka mzima alhamdullilah!!!!Mungu ni mwema sana!!!!!!!Asante kwa afya baba yangu!!!!!muda si mrefu ntarudi Kazini na uhakika mashabiki wangu wapenzi mmenimiss sana!Kila kitu tayari kimeshapikwa bado tu kuwaambia lini tu but niombeeni heri wapenzi wangu najua sana mmeimiss sauti ya Ray C All over the world!!!!jinsi ninavyowapenda na jinsi mlivyoniombea zawadi Kama kumi hivi nimewaandalia!!!mtashauaje sasa!!kama nawaona vile!!!!!!Bila nyie hakuna Ray C!!!!!!!Thank you so very much guys!!!!!!My fans!My everything!!Nawapenda mno!!!!”.

Mwishoni mwa mwaka jana Ray C alisema ameanza kuingia studio na tayari amemaliza kurecord album yake mpya, hivyo naamini comeback yake itakata kiu ya mashabiki wake.

MAHAKAMA YAAMURU JENGO LINALOCHUNGULIA IKULU LIPUNGUZWE UREFU

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu, Richard Maliyaga, kila mmoja kulipa faini ya Sh15 milioni au kwenda jela miaka tisa baada ya kuwatia hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuruhusu ujenzi wa jengo la ghorofa 18 karibu na Ikulu.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo alisema jengo hilo lilipaswa kuwa la ghorofa sita na kuamuru kubomolewa kuanzia ghorofa ya saba kwenda juu.

Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 13 wa upande wa mashtaka, vielelezo 20 vilivyowasilishwa na ushahidi wa utetezi uliotolewa na washtakiwa wenyewe, upande wa mashtaka ulithibitisha pasipo shaka mashtaka dhidi ya vigogo hao waliodaiwa kuruhusu ujenzi wa ghorofa 18.

Hivyo aliwahukumu washtakiwa hao kila mmoja kulipa faini ya Sh5milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa lililokuwa likiwakabili. Kila mshtakiwa alilipa kiasi cha Sh15 milioni mahakamani hapo na kuepuka kifungo.
Baada ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alisema ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya hukumu hiyo kutolewa, Kifungu cha 40, namba 1 na 2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kinawaruhusu kutaifisha jengo hilo.
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na Mawakili Majura Magafu na Paschal Kamala.

YOUND DEE AWA MBOGO KWA ANAYE TUMIA JINA LAKE KUTAPELI WATU MTANDAONI

$
0
0
Kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa watu maarufu kutokana na kuwepo kwa watu wanaofungua akaunti za facebook  kwa majina yao na kufanya utapeli.

Rapper anaewakilisha kundi la Mtu Chee, Young Dee, amedai kuwa ingawa hayuko kabisa facebook, kuna mtu ambaye amekuwa akitumia jina lake kufanya utapeli licha ya kuzungumzia mara kwa mara kuhusu mtu huyo kwenye vyombo vya habari.

Rapper huyo wa ‘Kijukuu’, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa japokuwa alitangaza zawadi kwa mtu atakayefanikisha zoezi la kumpata mtu huyo bado hajafanikisha na kwamba mtu huyo anaendelea hadi leo.

Amesema aliwahi kwenda polisi kufungua mashitata dhidi ya mtu huyo akiwa na utambulisho wa BASATA kuwa yeye ndiye ‘Young Dee’, lakini polisi walidai ampeleke mtu ambaye ametapeliwa ndipo aweze kufungua kesi hiyo.

Tayari Young Dee ameshajipanga kwa ajili ya kuupeleka ushahidi utakaofanikisha zoezi la kumpandisha kizimbani tapeli anayetumia jina lake kwenye Facebook.

“Bado naendelea na zoezi langu, lakini sasa hivi nachokitafuta…kuna mtu wa sheria amenishauri kuna jinsi ambavyo hiyo kesi tunaweza kuifungua ikamake sense. Kwa hiyo ndio niko nae naconfirm naye, lakini bado tunakusanya ushahidi, kuna mtu mmoja nimempata ambaye ameshatapeliwa, natafuta mwiningine. Kwa hiyo tukishapata ushahidi wa kutosha tunaweza kum-sue. Young Dee ameiambia tovuti ya Times Fm.

Kama uko facebook na unachat na Young Dee, sanuka, jamaa hayuko facebook kabisa!

MWANAMUZIKI T.I AMCHANA MKEWE LIVE KWENYE INSTAGRAM BAADA YA KUPOST PICHA YA MAKALIO YAKE

$
0
0
Clifford Joseph Harris Jr. aka T.I, rapper wa Atlanta Marekani, ameshindwa kuvumilia baada ya kuona mke wake ‘Tiny’ amevuka mipaka kwa kupost kwenye Instagram mfululizo wa picha zinazoonesha makalio yake.

Ingawa rapper huyo toka Atlanta alikuwa na uwezo wa kumpigia simu ama kumtumia message mkewe huyo kumuonesha alichokuwa hapendi kwenye picha hizo, jamaa aliona dawa inatakiwa iwekwe pale pale kwenye kidonda! Hivyo akaandika pale pale palipomuudhi!!

“You have so much more going for u other than your a$$. Although it is so magnificent, I think u should spend just as much time showcasing those other things as u do ya #booty…awesome pic thou. Lov.” Ameandika T.I kwenye post hiyo.

Mkewe Tiny nae akamjibu kwa kung’ata na kupuliza, kwa kuwa inasemekana kuwa ameshachoshwa na ugomvi uliopo katika ndoa yake.

Alimjibu kwa kejeli T.I kuwa yeye hakuwa na nia ya kuonesha makalio yake bali alikuwa anataka kuonesha kiuno chake, na kwamba kumbe mmewe alikuwa anaangalia makalio tu.

“I wasn’t showing off my ass in this pic it was about my waist… u just looking at the ass bae! U know I wasn’t saying getting my sh*t together about my ass now don’t U? But glad u like it bae.”

Majibishano hayo kati ya wanandoa na mastaa wa kipindi cha TV cha Family Hustle kinachowaunganisha wao na watoto wao saba, yalisababisha mashabiki wao kushangaa na wengine walitoa ushauri kuwa T.I angetakiwa kutumia simu.

Tangu mwezi uliopita kumekuwa na ripoti kuwa wawili hao wako katika mgogoro mkubwa kiasi cha kusemekana kuwa wanataka kupeana talaka.

Tetesi hizo zilichochewa na picha za Tiny alizopost zikionesha mkono wake wa kushoto ukiwa bila pete ya ndoa. Iliripotiwa pia kuwa mwanamke huyo anaewaelewa watoto saba wa T.I na wake kwa ujumla wao, amekuwa akiparty sana akiwa na rafiki zake, tofauti na zamani.

MISS TZ AKIRI KUTEMBEA NA KONDOM KWENYE MKOBA SAA 24!

$
0
0
Na Jelard Lucas
MISS Tanzania 2011, Salha Israel ameweka bayana bila ya woga wowote kuwa, kwenye pochi yake hakaukiwi na mipira ya kiume ‘kondom’, Amani linakupa kila kitu kinagaubaga.

Salha alisema hayo, juzi Jumanne katika mahojiano maalum, chumba cha habari cha Magazeti Pendwa Bongo, Global Publishers, Bamaga – Mwenge jijini Dar es Salaam.

HABARI KAMILI
Katika mahojiano hayo, Salha aliwekwa mtu kati ambapo alifafanua ishu hiyo pamoja na mambo mengine ndani na nje ya urembo, bila kusahau tasnia ya sinema ambayo kwa sasa ameingia kwa miguu miwili.

Swali la msingi lililozaa jibu hilo ni pale alipoulizwa kama aliwahi kutoa mimba tangu alipoanza kuelea kwenye bahari ya mapenzi, ambapo alikana kisha akafafanua: “Mimba! Weeeee.... hapana. Sijawahi kupata wala kutoa mimba.”

Akaongeza: “Mimi natumia kondom bwana, mimba itaingia wapi hapa!”
AMANI: Kama ukienda kwa jamaa na akawa hana kondom unafanyaje?
SALHA: Na kwa nini asiwe nayo? Lakini siyo tatizo sana, ndiyo maana mimi huwa nakuwa nazo kwenye pochi muda wote. Nikijua nakwenda kwa jamaa, basi zinakuwa tayari.

Sitaki kisingizio, kama atakuwa nazo fine (sawa) but (lakini) akiwa hana natoa zangu. Unajua mimi ndiye nitakayeingia kwenye matatizo ndiyo maana nakuwa makini mwenyewe.

AMANI: Kwa hiyo hata sasa hivi hapo unazo kondom kwenye pochi yako?
SALHA: (Anacheka) Hapana, hapana... kwa sasa sina na hii ni kwa sababu sina mtu muda huu ila nikiwa naye huwa siachi kuzibeba muda wote.
Credits:Global Publishers

LEO KUMEKUCHA KESI YA MBUNGE MAARUFU WA CHADEMA NA CHAMA CHAKE MAHAKAMA KUU HAPATOSHI LEO LIVE

$
0
0
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alifungua kesi hiyo dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema, akiiomba mahakama hiyo ikizuie chama kujadili uanachama wake, hadi rufaa anayokusudia kuikata Baraza Kuu la chama kupinga kuvuliwa nyadhifa, itakaposikilizwa.


Katika kesi hiyo namba 1 ya 2014, Zitto pia aliiomba mahakama hiyo imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichomvua nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mbunge wa Kigoma Kaskazini.


Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Jaji John Utamwa imepangwa kuanza kutajwa leo kabla ya kupangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa rasmi.

Tayari mahakama imeshatoa amri ya zuio la muda kwa Chadema kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake.


Uamuzi huo ulitolewa Januari 7 na Jaji Utamwa, kutokana na maombi ya Zitto, kupitia kwa Wakili wake Albert Msando.


Awali mawakili wa Chadema, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Mkurugenzi wake wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya kupewa zuio la muda.

Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa maombi hayo yametimiza matakwa yote ya kupewa zuio hilo.
CHANZO NI MWANANCHI

HAYA SASA SEREKALI YATOA TAHADHARI KWA UPATU HARAMU KAMA ULE WA TELEXFREE

$
0
0
Serekali imetoa tahadhari kwa wale wanao cheza michezo ya Upatu haramu ambayo sio uwekezaji halali ...Mfano ni kama wale Deci na sasa hawa Telexfree....Niliongea kuhusu hilo kwenye makali zilizopita na sasa Serekali nao hao ...Shauri zenu Sasa Akili Kimkichwa....

YANGA YAZUIWA UWANJA WA NDEGE KWA MUDA WAKAGULIWA KWA KUHISIWA NA MADAWA YA KELEVYA

$
0
0

Leo Asubuhi Team ya Yanga Imekiona cha Moto baada ya kuzuiwa uwanja wa Ndege wa JKIA Hapa Dar Wakielekea Comoro Kwa Ajili ya Mchezo wa Marudiano ...Mtoa nyeti Amehabarisha kuwa Walihisiwa wamebeba mzigo ikabidi upitishwe ukaguzi wa nguvu na kusababisha safari yao kuchelewa kwa muda wa Nusu saa...Habari Kamili kama walikutwa na Mdawa ama la itatolewa baadae

DUH..HAKIKA POMBE SIO CHAI...NJEMBA YAFANYA VITUKO HADHARANI BAADA YA KILAJI KUMZIDIA.

$
0
0
Jamaa atoa kali na kuwaacha watu midomo wazi kwa makeke yake..! Du! hadi Dada aliona aibu maana hakutegemea tukio hilo..! Ama kweli pombe sio chai. 
Kila kitu kinahitaji uzoefu, Chupa mbili tu Jamaa amechangamka kama ameogea ndimu..!

MDAHALO WA WAZI KATI YA DR SLAA NA DR KITILA MKUMBO

$
0
0
Bila shaka huu ni wakati muafaka sana ambapo inafaa kuwa na mjadala wa wazi kati ya Dr. W.Slaa na Dr. Kitila mkumbo juu ya "Tanzania na siasa tunayoitaka"

Nasema hivi kwa sababu, Kwa takriban miezi miwili mfululizo, Dr.Kitila amekuwa akiandika makala zenye maudhui mazito ambayo hayawezi kupuuzwa.Katika makala zake zote, zimekuwa zikionesha maudhui ya ujumla kwamba siasa za upinzani tanzania kwa sasa zimegeuka na kuwa ni sawa sawa tu na zile za CCM au pengine hata kuwa na udhaifu zaidi hata ya zile za CCM.kwa ujumla Dr.Kitila yeye anadhani pengine hilo linaweza kuwa ndio sababu kuu ya watanzania kuamua kuichagua CCM tu(LICHA YA UDHAIFU WAKE), huku upinzani ukianguka.

Kwa mfano Kitila Katika moja ta makala zake anasema "Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua."

Bila shaka unahitajika mjadala kati ya hawa Madaktari wawili ambao wote wana shahada ya juu ya falsafa (Dr.Slaa Vs Dr.Kitila), ili kupitia mjadala huo mambo haya yote yakawekwa sawa kwa hoja na vielelezo vya wazi na watanzania wakapata picha kutoka kwa watu wenye weledi na uelewa wajuu.

Naamini kama mjadala huo utafanyika, basi kutokea hapo, wadau wataweza kujadili wakiwa na msingi mzuri na imara wa marejeo, Badala ya utaratibu huu wa kila mtu kuibuka na kutoa hoja yake kwa wakati wake.
Credits:Jamii forums

LOWASSA, SUMAYE NA NGELEJA WAHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI..MEMBE AKACHA

$
0
0
Wadau habari zilizopo nikwamba Bernard Kamilius Membe amekacha kikao cha maadili alichotakiwa kuingia leo kuhojiwa.Habari zilizopo nikwamba Lowassa ndiye aliyefunguwa dimba lakin mpaka muda membe ajaonenakana viwanja vya mahojiano na simu wakijaribu kupiga haipatikani.

Sasa yapo maswali mengi yakujiuliza je mh membe hajahudhuria makusudi? au anaumwa? au lengo lilikuwa ni mh Lowassa???? habari za upande wa pili zinasema yuko na jk uingereza,nachojiuliza mh rais alikuwa hajui kuwa huyo aliyeandamna naye alikuwa akihitajika na chama ili ahojiwe??au ni upendeleo?

Zaidi najiuliza kichwani mwangu angekuwa Lowassa ndiye kakacha leo wangezungumza nn?

Nafuatilia, nitawapa habari kamili

Source:Jamii Forums

NIKKI WA PILI ATOA DARASA..SOMA ALICHOANDIKA HAPA

$
0
0
Hii makala imeandikwa na rapper Nikki wa II, ukishaisoma unaweza kusema chako chochote…
Anaanza kwa kuuliza >>>> thamani ya sanaa ni KIKIII? ? ?
Nakutana na wasaniii wachanga wengi, Kwenye show, mitandaoni, mtaani, studio na wengine wananipigia
Wengi huomba kolabo, ushauri, namba za simu za watu mbali mbali wa Kwenye industry hii
80% huomba ushauri wa kutoka, kolabo kwa dhana ya kuwasaidia kujulikana mapema, ama kusaidiwa kufikisha cd zao kwa watu Fulani Fulani.
Ni Ngumu sana kukutana na msanii mchanga akakuuliza namna ya kuboresha uwezo wake wa ku rap, kuimba ama kuwa mwandishi mzurii…kwa kifupi kuwa msanii bora
Msanii wa kwenda Kwenye concert anataka kwenda studio, msanii Ana nyimbo Moja na nusu Ana taka umtafutie Dili ya kurekodi….Mimi mpaka naenda studio nilikuwa nishaperfom matamasha mengi ya kushindanisha vipaji na nilikuwa na nyimbo mbili mpya kila wiki hazikuwa Kali ila ndio zilikuwa hatua za kujifunza ku rap na kuandika mashairi.
Wakati natafakari nini msingi wa Sanaa kuonekana rahisi namna hii na kua maarufu kuwa ndio inspiration kwa wasaniii wachanga na wala sio usaniii bora…nikawasha TV Mara nikaona nyimbo ya kiwango sawa kabisa na jamaa Mmoja ananiimbiaga nikienda saloon,
ikafuata nyingine na nyingine za aina hiyo
Theni ikaja interview mtangazaji anamuuliza msanii kwa nin mziki haulipi?? Nikacheka utalipaje wakati ni kitu rahisi sana nikitoka nje tu hapo nakipata, na hata mfanya kazi wako wa ndani anaimba sawa tu na unaye muona kwenye TV. hamna kitu kisicho na thamani kinacholipa….kitu ambacho sina uhakika ni Kama na yeye akiwa gheto kwake huwa Ana angalia play list anayoipangaga
Nibiashara Binafsi sio sahihi kumjaji MTu kwa anachofanya…lakini je haujiskii furaha kipindi ulikuta una fans 200 ukafanya wakawa 2000 loyal fans, hautajisikia furaha kizazi kinachofuata nao wakaja kalia kiti hicho. Biashara zetu ni binafsi lakini Jamii yetu sio na nijukumu letu la ujumla kuandaa mazingira bora kwa watoto na wadogo zetu.
Any way turudi Kwenye mada, natafakari watu Kama kendrik lamar, 50 cent, iliwachukuwa si chini ya miaka 10 kufika mainstream, kina keri hillson miaka 5 yakuwa backup singer, nikakumbuka mfuko wa joh makini uliokuwa umejaa mashaiiri tumeutundika pale sebleni kwetu.
Nikakumbuka kuwa gemü ya mziki wa kizazi kipya ina Kama miaka 15 ila ina zaidi ya wasanii 50 walio wika na kupotea wakati NAs, snoop, jay z wana karibia miaka 20 Kwenye gem on top. Radio Kama hot 97 na host Kama funk master flex toka miaka ya 90 mpaka Leo wanakimbiza New York, source magazine, alafu nawaza baadhi ya vipind vikubwa vilivyo poteza umaarufu hapa bongo, shows za TV ambazo nilikuwaga naziota kuwepo, sikumbuki Mara ya mwisho nimeaangalia lini
Shows za kujaza diamond jubilee, msanii mmoja ndio alikuwa na thamani ya show Moja ya club Leo ni wasanii 8.
Thamani…value…hujengwa na nini?………na hujengwa na nani?,…….na unawezaje kuilinda kulingana na mabadiliko ya muda na tamaduni za kinyakati?………..towa maoni yako uki ya elekeza kujibu maswali hayo…..
Unaweza niandika on my twitter account Nick mweusi @nikkwapili ama on Instagram @nikkwapili

ZITTO AFUNGUKA KUHUSU WAFANYABIASHARA NA MASHINE ZA TRA

$
0
0
Hii ni Kauli ya Zitto Kabwe kuhusu madai ya Wafanyabiashara na TRA.
Posted by: TZA two February 13, 2014 General News108 views
zittoMbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema Zitto Kabwe muda mfupi uliopita kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ametoa yake ya moyoni kwa hili seke seke linaloendelea nchini juu Wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania[TRA]kuhusu mashine za kutolea risiti za EFD.
Zitto alianza kwa kuandika>>’EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni’
‘Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000′
‘Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika’
‘Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila kusubiri kurejeshewa kupitia kodi’
‘Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa matumizi).
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?’
‘Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?’
‘Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba………’.

AGNES MASOGANGE AFUNGUKA KUHUSU KUTONGOZWA NA WANAUME WAKWARE

$
0
0
VIDEO Queen matata Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ amewajia juu kundi kubwa la wanaume linalomtaka kimapenzi wakati wanatambua vyema kuwa ana mtu wake.

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Masogange alisema tangu atoke Sauz aliponaswa kwa msala wa kusafirisha malighafi haramu, wanaume wakware wamekuwa wakimsaka kama fisi aliyeona mfupa kitu ambacho hakubaliani nacho.“Sitaki kutongozwa kabisa, waniache. Kinachonikera zaidi wanaonitongoza wengi wanatambua kabisa nina mchumba wangu (Evance), watu wengine sijui wapoje!” alisema Masogange.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images