Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Polisi Wakanusha Karatasi za Kura Zilizompa Alama Ya VEMA Magufuli Kukamatwa Masasi.

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limekanusha taarifa zinazodaiwa kuandikwa katika mtandao mmoja wa kijamii, zikidai kukamatwa kwa baadhi ya watu katika kituo cha polisi wilaya ya Masasi mkoani hapa wakiwa na masanduku na fomu za kupigia kura zipatazo 2000 zikiwa tayari zimetumika.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, alisema taarifa hizo zilidai kuwa, fomu hizo zilimpa alama ya vema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Masasi kupitia chama hicho.

 Alisema taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa, mkuu wa wilaya ya Masasi aliingilia kati na watuhumiwa hao ambao hawakutajwa majina waliachiwa huru kwa dhamana kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya ambaye ndiye aliewadhamini na kwamba masanduku hayo na karatasi yamehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani humo.

Kamanda Mwaibambe alisema taarifa hiyo ni uzushi na upotoshaji mkubwa na kwamba hakuna mtuhumiwa wala masanduku yaliyokamatwa mkoani hapa wala katika wilaya hiyo.

“Tunachofahamu kupitia kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (Nec), vifaa vya kupigia kura bado havijawasili nchini na alituahidi vitaanza kuwasili mwishoni mwa mwezi huu kutoka nchini Afrika Kusini.” alisema.

Alisema Jeshi la Polisi linamsaka mhalifu huyo wa mtandaoni na akitiwa mbaroni atafikishwa katika vyombo vya sheria.

Mke wa Edward Lowassa Atoa Siri Nzito ....Adai Ana Uhakika Mumewe Atashinda Urais

$
0
0
Mke wa Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Regina Lowassa Mke wa Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Regina Lowassa, amesema ana uhakika mumewe atashinda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu kutokana na muitikio mkubwa anaoupata katika mikutano yake na pia kiu ya wazi ya wananchi katika kufanya mabadiliko.
Kadhalika, ametaja vipaumbele vinne alivyojiwekea katika kumshauri mumewe ili mwishowe aliongoze taifa kwa mafanikio makubwa katika kipindi chake cha kuwa madarakani.
Mbali na Chadema, Lowassa anawakilisha pia muungano wa vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NLD, NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF).
Mama Lowassa alielezea mambo hayo jijni Dar es Salaam jana katika mkutano wake na wanawake walio katika Baraza la Wanawake wa Chadema( Bawacha), Wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza katika mkutano huo kuitikia shangwe zilizokuwa zikimtaja Lowassa kama rais ajaye, Mama Lowassa alisema amejawa na imani kuwa mumewe atashinda kwa sababu ameshuhudia mwenyewe muitikio wa wananchi katika mikoa mbalimbali waliyopita katika harakati za kampeni zinazoendelea nchini kote.

“Awali, nilikuwa ninafahamu kwamba Watanzania wengi wana matatizo. Lakini baada ya kutembea zaidi katika kila pembe ya nchi, sasa nikiri kugundua kwamba nilichokuwa nakifahamu juu ya matatizo ya Watanzania kilikuwa kidogo sana kulinganisha na ukweli uliopo... sasa nimejionea, ni matatizo makubwa na ndiyo maana wana kila sababu ya kuamua kufanya mabadiliko,” alisema Mama Lowassa.
ATAKAVYOKUWA 'FIRST-LADY'
Akieleza zaidi, Mama Lowassa ambaye atakuwa 'first lady' kama mumewe atashinda na kuwa rais baada ya Oktoba 25, mwaka huu, alisema atajielekeza katika kushauri na kupigania vipaumbele vinne kwa ajili ya wanawake nchini. Alivitaja vipaumbele vyake hivyo pindi atakapokuwa mke wa rais kuwa ni katiba, elimu, afya na uchumi.

Akifafanua, Mama Lowassa alisema ataendeleza mapambano kuhakikisha kuwa ukombozi wa mwanamke unapatikana kwa dhati kupitia Katiba ya nchi, ambayo serikali itakayoundwa na Ukawa imeeleza wazi kuwa itaisimamia ili iandikwe upya kwa maslahi ya Watanzania.
Alisema yeye kama Mke wa Rais mtarajiwa, atahakikisha elimu kwa wanawake inapewa kipaumbele na kuingizwa kwenye katiba kwani huo ndiyo ufunguo wa ukombozi wa kweli.
Akielezea kuhusu afya, alisema ni dhamira yake pia kuona eneo hilo linaboreshwa kwani waathirika wakubwa wa huduma duni ya hospitali ni pamoja na wanawake. Alizungumzia pia umuhimu wa kuwainua wanawake kiuchumi ili hatimaye waondokane na umaskini.
Alisema hapendi kuona wanawake wanakuwa tegemezi na kwamba atahakikisha mara zote anamshauri Rais ili kuhakikisha wanawake nao wanajitegemea kiuchumi kwa kuhakikisha wanapata fursa za kujipatia mikopo, elimu bora na afya bora tofauti na ilivyo sasa.

Aliwataka wanawake wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 na kumpigia Lowassa kura nyingi za ndiyo ili aingie madarakani na kuleta mabadiliko kwa manufaa ya taifa.
Alisema mabadiliko na kuijenga Tanzania mpya yanawezekana, wala si kwa kutumia gharama kubwa na nguvu kubwa isipokuwa kwa kuweka mikakati mizuri, thabiti na kuitekeleza kwa vitendo.
“Ninaomba wanawake mniamini katika hili...kwa sasa siwezi kusema mengi, ila ninanawahakikishia kuwa baada ya Lowassa kuchaguliwa, nitarudi kwenu na tutapanga kwa pamoja mikakati zaidi ya kuishauri serikali ya Ukawa katika kutimiza dhamira ya kuwakomboa wanawake na Watanzania wote,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha, Kunti Yusuph, alisema katika vipindi vyote vya uchaguzi, wanawake wamekuwa wakirubuniwa na chama tawala kwa vizawadi vidogo kama khanga na kisha kutelekezwa baada ya uchaguzi, lakini sasa hawapaswi kukubali hali hiyo bali washiriki kwa dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli kupitia Ukawa.
CHANZO: NIPASHE

Gazeti la Mwananchi Lafunguka Vikali Kuhusu Kumchafua James Mbatia Kwa Mfano wa Gazeti la Mwananchi

$
0
0
Mapema wiki hii, watu wasio na nia njema walitengeneza mfano wa gazeti la Mwananchi kwenye mitandao ya kijamii likionyesha habari ya kumchafua Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, James Mbatia.
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen, imelaani vikali upotoshaji wa makusudi unaolenga kutumia jina la Mwananchi kuwachafua wanasiasa na watu wengine hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Mapema wiki hii, watu wasio na nia njema walitengeneza mfano wa gazeti la Mwananchi kwenye mitandao ya kijamii likionyesha habari ya kumchafua Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja wa vyama vinavyounda Ukawa, James Mbatia. Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu alishauri timu za kampeni za vyama vyote, kunadi sera zao na kuonyesha jinsi watakavyozitimiza badala ya kusambaza propaganda zinazolenga kuchafua jina la kampuni ya Mwananchi. Alisema MCL inapanga kuwasilisha malalamiko rasmi kwa vyombo vya sheria ili vichukue hatua kutokana na udhalilishaji huo.


Hii si mara ya kwanza kwa watu wenye nia mbaya na magazeti ya kampuni ya Mwananchi kutengeneza mfano wa gazeti na kuandika vichwa vya habari ambavyo vina lengo la kuichafua.
Machumu alisema ingawa MCL haihusiki kwa vyovyote vile na gazeti feki hilo lililokuwa linasambaa kwenye mitandao, inamuomba radhi Mbatia na wengine wote walioumizwa na kitendo hicho

Picha 6 za Edward Lowassa Mbele ya Wananchi wa Babati na Mto wa Mbu Oct 2.

$
0
0
l2
Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA Edward Lowassa October 2 2015 alisimama mbele ya Wananchi wa Jimbo la Babati Mjini katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kwaraha, Babati Manyara.
L1
l3
l4
l5
l6
Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kwa Chadema kupitia mwamvuli wa UKAWA, Julius Karanga, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni

Mgombea Ubunge CCM Aanguka Jukwaani Akiruka Kichurachura........Alitaka Kunogesha Mtindo wa CCM wa Push Up za Magufuli

$
0
0

Mgombea ubunge wa tiketi  ya  Chama  Cha  Mapinduzi (CCM) katika  jimbo  la  Tunduru  Kaskazini,Mhandisi Ramo Makani alianguka jukwaani  wakati  akijaribu  kuruka  kichura chura.

Tukio  hilo  lilitokea  katika  mkutano  wa  ufunguzi  wa  kampeni  za  mgombea  huyo, uliofanyika  kwenye  viwanja  vya  baraza  la  Idd  mjini  hapa.

Inasadikiwa  kuwa  alikusudia  kunogesha  staili  ya  mgombea  urais  wa  tiketi  ya  CCM,Dr. John Magufuli  ya  kupiga  Push Up..

Ingawa  tukio  hilo  lilionekana  kumfedhehesha,mgombea  huyo  alijikakamua  kuinuka  huku  akisaidiwa  na  walinzi  wake  na  kuendelea  kunadai  sera  zake.

Alisema  kuwa  katika  kipindi  kilichopita  alitekeleza  ilani  ya  chama  chake  kwa  kusimamia ujuenzi  wa  barabara  ya  Namtumbo-Tunduru  hadi  wilayani Nanyumbu  inayoendelea  kujengwa  kwa  kiwango  cha  lami.

Msanii wa Nyimbo za Asili Mkoani Mwanza Ahukumiwa miaka 10 Jela kwA Kumiliki FISI Wawili Bila Kibali

$
0
0

MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, imemhukumu msanii wa ngoma za asili, Mng’ahwa Kazanza (42), kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kumiliki fisi wawili na kuwatumia kwenye sanaa zake bila kibali.

Awali akisomewa mashtaka katika mahakama hiyo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Doroth Mgenyi, ilielezwa mahakamani hapo kuwa mnamo Septemba 28, mwaka huu, kwenye Kijiji cha Sisu wilayani Misungwi, majira ya saa 7:30 mchana, Mng’ahwa Kazanza (42) alikamatwa akiwa na fisi wawili wenye thamani ya Sh milioni 4.8.

Mara baada ya kusomewa mashtaka, msanii huyo alikiri kosa hilo na kudai alikuwa akiwatumia fisi hao katika sanaa zake bila kutambua kama ni kosa kuburudisha mashabiki wake kwa lengo la kuongeza kipato.

Kutokana na kukiri huko, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi, alimtia hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali kinyume cha sheria Na. 5 ya mwaka 2009 na kumhukumu kwenda jela miaka 10 au kulipa faini ya Sh 4,840,000 ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaomiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Msanii huyo alishindwa kulipa faini hiyo na hivyo kwenda jela kutumikia adhabu hiyo ya miaka 10.

Breaking News: Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Afariki Dunia Nchini India

$
0
0
Waziri  wa  Viwanda  na  Biashara,ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Handeni Dr.Abdalah Kigoda amefariki  dunia leo  majira  ya  saa  kumi  jioni  nchini  India  alikokuwa  amelazwa  kwa  matibabu.

LOWASSA Kavunja Rekodi Jijini Mwanza.......Haya Sio Marufiko, NI GHARIKA. Zaidi ya watu 50 Wamepoteza Fahamu

$
0
0

Lowassa  amelitikisa  jijini  la  Mwanza  jioni  hii  ambapo  mwandishi  wetu  ameshuhudia  zaidi  ya  watu 50  wakipoteza  fahamu  baada  ya  uwanja  huo  kujaa  kupita  uwezo  wake
Source: Mpekuzi blog

University LADY Exposes Men Who Refused to Pay Her for S£X And Threatens to Post Videos

$
0
0

Multimedia University college student has threatened to post videos of 11 men having s*x with her after they refused to pay for her services.

The girl, who goes by the name Zuhura Jane, sells her services to men in her room and records them.

She charges Sh. 2,000 per session and 11 of them have failed to pay up.

Here is her post on facebook;

Kuona picha zao Ingia Hapa=>PICHA

Jack Wolper Ndoa Yamtia ‘Uchizi’

$
0
0
CHIZIKA! Wakati hekeheka za maandalizi zikipamba juu ya ndoa ya karne ya staa wa sinema za Kibongo, Wolper, mwanadada huyo anaonekana kuingiwa na ‘uchizi’ juu ya suala hilo ambapo muda wote anawaza ni kwa namna gani ataweza kuweka historia juu ya shughuli yake. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Jozi

Village, jijini Dar, Wolper alisema: “akili haijakaa sawa kabisa, nawaza juu ya ndoa yangu ambayo muda si mrefu itatimia, silali, sili na sipumui vizuri, kila kitu kimesimama, ni kama imenitia uchizi, muda wa kuishi na mwanaume kwenye ndoa takatifu umewadia,” alitiririka Wolper.

Chanzo: GPL

Mgombea Urais wa CCM John Magufuli Akabidhiwa Faili la Wasaliti Wanaojifanya Wako CCM Kumbe Wanamsaidia Lowassa

$
0
0
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameombwa kuwafuta kazi baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamebainika kuwa wanakihujumu kwa kumsaidia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Katika hali inayoonesha kuwa kuna mchwa wanaokitafuna kwa kificho chama hicho, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM mkoani Arusha, Victor Njau alimuomba Dk. John Magufuli kuwafukuza kazi mara moja watendaji ambao wanakihujumu chama hicho katika harakati hizi za kampeni.

“Kuna viongozi wanatumia magari ya CCM, wanalipwa mishahara lakini wanaendesha kampeni za kuwaangusha wagombea wa chama tawala. Tunamtaka Dk. Magufuli akishinda aanze na wasaliti hawa,” alisema.

Hii inaonesha kuwa viongozi wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wanafahamika na tayari ‘faili’ lao limewekwa sawa wakisubiri adhabu yao mara tu baada ya Dk. Magufuli kuingia ikulu, endapo atachaguliwa na wananchi Oktoba 25, mwaka huu.

Hili sio suala geni kwa mgombea huyo wa urais kwani alishawahi kuweka wazi kuwa anawafahamu baadhi ya watu wanawasaliti kwa kumsaidia mgombea wa Chadema, Edward Lowassa. Aliwakanya watu hao na kuahidi kuwawajibisha pindi atakapoingia madarakani, la sivyo waache usaliti huo.

Sheria ya Mitandao Yamnasa Mwingine...Huyu Aliwatukana TCRA Wenyewe Kupitia Mtandao wa Facebook

$
0
0
Sheria Mpya ya Makosa ya Mtandaoni ya 2015 imeendelea kuonyesha meno yake kufuatia kijana Israel William (20), kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, akishitakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akisoma mashitaka dhidi ya mtuhumiwa huyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Renatus Rutatinisibwa, Mwendesha Mashitaka wa serikali Estazia Wilson, amesema kijana huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Septemba 10 na Oktoba 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Estazia amesema mshitakiwa aliandika na kusambaza katika mtandao wa Facebook taarifa zisizo sahihi, kuwa wafanyakazi wa TCRA wamekuwa wakilawitiwa, akijua kuwa taarifa hizo sio sahihi na ni kashfa.

Mshitakiwa huyo amekana mashitaka hayo na upande wa mashitaka umesema uchunguzi wa suala hilo bado haujakamilika.

Mtuhumiwa huyo amepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Israel anakuwa mhanga wa pili wa sheria hiyo mpya ya makosa ya mtandaoni, kufuatia pia kufikishwa mahakamani kwa mwanafunzi wa Chuo cha DIT Benedict Ngonyani, kwa kusambaza taarifa za uongo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) Jenerali Adolph Mwamunyange amelishwa sumu.

Mwanasheria Mkuu wa TCRA Kalungula, kwa mara nyingine amewaonya vijana dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kuwashauri kufuata kanuni na taratibu za mawasiliano na matumizi ya mitandao hiyo kwa mujibu wa sheria.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu atakayeachwa kwa kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni.

Shilole Shows Off New Tattoo Of Nuh Mziwanda On Her Bo0bs.

$
0
0

Shilole and boyfriend Nuh Mziwanda have no plans to end their relationship as the actress and singer decided to have a new tattoo of Nuh's name. Look photos  here.




Mambo Matano Ya Ajabu Yaliyojitokeza Mwanza Jana Lowassa Akiwa Kwenye Kampeni

$
0
0


Mamba Matano Ya Ajabu Yaliyojitokeza Mwanza Jana Lowassa Akiwa Kwenye Kampeni
Watu Kadhaa Wazimia kutokana na Msongamamo wa watu





















































Mwigizaji WASTARA Atishiwa Kuuawa na Ustaadhi

$
0
0
Hatari! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadai kutishiwa maisha kwa kutumiwa  ujumbe wa WhatsApp na ustaadhi ambaye aliwahi kutangaza kutaka kumuoa, jambo lililosababisha staa huyo kuamua kumfungulia mashtaka.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wastara alifunguka kuwa kutokana na vitisho anavyotumiwa na ustadhi, hivyo akitua Dar kutoka mikoani atakwenda kumfungulia mashtaka kituo cha polisi kwani vitisho hivyo vinahatarisha usalama wake.

“Hebu fikiria mtu ananiandikia ujumbe kuwa atahakikisha nimeua ndiyo ataniacha, ina maana yale yanayonitokea ni yeye ananisababishia!” alisema Wastara.

Wastara alimtumia mwandishi ujumbe wa ustadhi huyo unaosomeka; ‘na bado siyo unatamani kuua na utaua, nitahakikisha umeua ndiyo na mimi nakuacha’.

Vitisho vya jamaa huyo vinakuja baada ya gazeti dada la hili, Ijumaa linalotikisa mitaani kila Ijumaa kuandika habari ya Wastara iliyosikitisha ambayo staa huyo alielezea namna anavyopatwa na hasira na kutaka kuua mtu ndipo  ustadhi huyo akamjibu kwa ujumbe huo.

Ustadhi huyo aliwahi kuripotiwa na gazeti ndugu na hili, Risasi kuwa ana tatizo la kumsema Wastara hata awapo katikati ya swala, jambo lililomfanya awatafute waandishi ili wamsaidie kumuunganisha na mwigizaji huyo akitaka kumuoa lakini mwanadada huyo alidaiwa kumtolea nje.
GPL

Agness Masogange Flaunts Her Assets...Ladies Can you Wear Like This and Go Out?

$
0
0

Agnes Masogange is a popular model and video vixen from Tanzania 



LOWASSA Atoa Kauli Nzito Jinsi Atakavyoshughulikia Matatizo Mbali Mbali ya Wananchi ili Wanufaike na Uchumi Katika Muda Mfupi

$
0
0

Lowassa Ameandika Haya Hapa Chini Kwenye Ukurasa wake wa Facebook:

Tutarekebisha kodi ya Misitu ili iweze kuchangia zaidi kwenye pato la Serikali.
Tutaimarisha sekta ya utalii kwa kuhakikisha kwamba nchi inavuna maradufu ya viwango vya sasa. Mkakati mkuu ni kuitangaza zaidi Tanzania nje, hususan kwenye nchi za Asia na Mashariki ya Kati.
Tutadhibiti biashara nje ya nchi kimagendo maarufu kama Panya Routes (PANYA RUTI).


Tutajenga mazingira rafiki ya kodi kwa makampuni ya nyumbani ili kuwapa motisha kulipa kodi na kuchangia taifa lao. Kwa mfano, hivi sasa idadi ya watu walioandikishwa na TRA kulipa VAT ni karibu laki 5, ingawa wanaolipa ni asilimia ndogo sana.
Tutaongeza ufanisi wa Bandari ya Da-es-salaam ili iweze kushughulikia mizigo mingi zaidi na hatimaye kupata wateja wengi zaidi, hususan kutoka nchi zilizotuzunguka. Bandari zetu ni chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.
Tutahakikisha kwamba Halmashauri zetu zinajitegemea badala ya kutegemea ruzuku kutoka serikali kuu. Lazima Halmashauri zibuni njia madhubuti za kukusanya mapato yao badala ya kutegemea serikali kuu.


Tutahakikisha kwamba mikoa mingine ya nchi yetu inachangia zaidi kwenye makusanyo ya kodi. Kwa sasa asilimia 70 ya mapato yanayokusanywa na TRA yanatoka Dar es Salaam.
Tutaongeza idadi ya walipa kodi kwa kuja na sheria mpya ambayo itahakikisha kwamba kila Mtanzania anayefikisha umri wa miaka kumi na nane anasajiliwa kama mlipa kodi na kama ana shughuli ya kumuingizia kipato, analipa kodi inayostahili bila kuonewa.
Tutaboresha mfumo wa kodi kwa lengo la kuwawezesha wananchi waone faida ya kulipa kodi kwa kuwapatia huduma za kijamii zinazoendana na kodi wanazotozwa.


Tutaongeza makusanyo ya mapato ya ndani kutoka Asilimia Kumi Na Tano (15%) ya pato la taifa na kufikia Asilimia Ishirini kama wenzetu Kenya n.k.
Tutadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia vibaya mfumo wa kodi kutoa mizigo yao bandarini.
Tutahakikisha kwamba Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) inakagua gharama za uwekezaji zinazofanywa na makampuni ya nje ili kutoza kodi sahihi. Udanganyifu wa baadhi ya makampuni husababisha upotevu wa mapato ya serikali" LOWASSA

Membe Amtaka Lowassa Aache Kujifananisha na Yesu.......Asema Hana Ubavu wa Kumfufua Balali

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia anaungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, hana uwezo wa kumfufua aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT),  marehemu Daud Balali.

Membe ambaye jana alionekana kwa mara ya kwanza katika kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, alisema Balali alikufa kifo cha kawaida na hataonekana tena.

Akizungumza na wakazi wa Lindi Mjini kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais wa CCM, Membe alisema anajua vizuri namna Balali alivyougua hadi kufariki dunia, hivyo mgombea kuahidi kumleta mtu aliyekufa ni jambo la kushangaza.

Membe alisema Balali aliugua maradhi ya utumbo na kwenda kutibiwa nchini Marekani mwaka 2008 na baadaye alifariki dunia na kuzikwa kwenye makaburi ya huko huko.

“Lowassa aache kujifanya Yesu kwamba atafufua wafu,” alisema...."nimesikia hata hapa Lindi ameshafika, sasa kamwambieni yeye si Yesu na wala hana uwezo wa kumfufua Balali,” alisema Membe.

Membe alisema kama kweli  Lowassa anaamini kwamba Balali amefichwa na serikali, basi aende akamtafute alikofichwa na amlete na kumwonyesha hadharani.

Aidha, alisema Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, wamekuwa wakidai kwamba serikali haijafanya lolote tangu uhuru wakati nao walikuwa na nafasi kubwa serikalini.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Salma Kikwete, naye aliibuka jana kwenye kampeni za Dk. Magufuli kwa mara ya kwanza na kusisitiza kuwa Dk. Magufuli ndiye chaguo bora.

Alisema rais mwenye uwezo wa kuwaletea maendeleo ya kweli na ya haraka, ni Dk. Magufuli.

Kwa upande wake, mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, alisema ingawa kuna wanaomwandama, lakini tayari yeye ndiye atakuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo.

Alisema wananchi wa Lindi na Mtama wameshaamua kumpa kura zote Dk. Magufuli kwa sababu wanaami kuwa rasilimali gesi  na mafuta iliyogundulika mkoani humo itakuwa salama.

Kwa upande wake, Dk. Magufuli alisema anataka gesi iliyogunduliwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi iwanufaishe Watanzania wote wakiwamo wa mikoa hiyo.

Alisema atahakikisha makampuni ya nje yanayokuja kuwekeza kwenye mikoa hiyo yanaajiri wakazi wa mikoa hiyo kwa nafasi mbalimbali badala ya kwenda na watu wao.

Taswira ;Magufuli CUP Yawa Gumzo la JIJI Dar...Hapa Kazi Tuu Ndio Mpango Mzima

$
0
0
Vijana wameamua kuonesha support yao kwa Mgombea Urais Kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha MAGUFULI CUP ambayo imekuwa gumzo mtaani. 










Shutuma za Magufuli Kutumia Bendera ya Taifa na Wimbo wa Taifa Katika Matangazo ya Redio na TV

$
0
0
Jana usiku nilikuwa naangalia habari kwenye kituo kimoja cha runinga. Likatoka tangazo likimuonyesha Dr. Magufuli akijieleza kwa unyenyekevu kwa watazamaji akiomba kura, nyuma kulikuwa na background ya bendera ya Taifa na pia hata vituo kadhaa vya radio nimesikia mara kadhaa wakitoa tangazo la huyo huyo Magufuli na wimbo wa Taifa ukipigwa.

Maoni yangu:

Kwa kuwa uchaguzi bado basi vyama vya siasa vizuiwe kutumia wimbo na bendera ya Taifa kwenye kampeni zao. Badala yake watumie nembo na bendera zao na ikibidi nyimbo za vyama vyao vinginevyo naona hii haiko vizuri.

By Sajenti/Jamii Forums
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live




Latest Images