She Claims to Have a Big Behind than Ageness Masogange And it’s Natural (PHOTOs)
↧
↧
Ikitokea Lowassa Akashindwa! Mwana CCM Yeyote Atakaembeza Lowassa Kutokana na Kushindwa Huko Atakuwa ni "Mpumbavu na Zuzu
LOWASSA ATABAKI KUWA SHUJAA WA MABADILIKO..!!
Nikiwa mwanachama wa CCM imenipasa kuamini kuwa chama changu kitashinda uchaguzi huu. Pamoja na imani hii sitashangaa kama CCM yangu itaanguka ingawa nitasikitika. Ikitokea, Mh. Lowassa akashindwa katika uchaguzi huu; mwana CCM yeyote atakaembeza Mh. Lowassa kutokana na kushindwa huko atakuwa ni "mpumbavu na zuzu". Kwa nini? Ni kwa sababu chama chetu CCM kilijisahau mno na kilishafika hatua ya kuwa na kiburi cha madaraka(na ndio maana mgombea wetu kaamua kujinadi kwa jina lake badala ya jina la chama kutokana na wananchi wengi kukasirishwa na mwenendo wa baadhi ya waliopewa dhamana ya kuongoza serikali kwa mgongo wa chama na chama kuonekana hakifai)! Kimsingi hakukuwa na namna yeyote ya kukizindua CCM na kukishikisha adabu zaidi ya kutokea kwa ushindani kama huu aliouleta Mh. Lowassa na UKAWA kwa ujumla.
Kampeni zinapoanza CCM sio tu ilibeza mabadiliko bali pia ilitumia muda mwingi kuwatukana wapiga kura wanaotaka mabadiliko(nikiwemo mimi mwanachama wake); lakini hadi sasa kumekuwa hakuna jinsi zaidi ya kuhubiri na kutafutia kura kwa jina la mabadiliko ya kweli. Kutokana na rekodi za kiutendaji zilizotukuka na uwezo wake binafsi natumaini Magufuli anaweza kushinda(ushindi wa kawaida na sio wa kishindo).
Lakini ikitokea Mh. Lowassa ameshindwa, mimi sitahesabu kama ameshindwa bali nitamweka kwenye kumbukumbu ya mashujaa waliolazimisha mabadiliko katika wakati sahihi. Mwanachama anaekitakia mema CCM huko mbeleni, atakuwa mvivu wa kufikiri asipompongeza Mh. Lowassa kwa mabadiliko ya kweli yanayotegemewa kuletwa na Dk. Magufuli pindi achaguliwapo kuwa Rais wa JMT. Kwa maana bila "mziki" wa Lowassa kutikisa nchi, CCM ilishashupaza shingo kukubali kuwa wananchi wamechoka tambo za kuimba eti, "CCM ni ile ileeeee...." bali wananchi na wanachama(hasa wa zama mpya) tunataka mabadiliko.
Hivyo basi, kutokana na mwenendo wa kampeni hadi sasa nimejiridhisha kuwa hata Dk. Magufuli anao uwezo wa kwenda kinyume na mfumo na kuleta mabadiliko[kama akiamua kuwaua nyani pasipo kuwaangalia usoni], [maana ni yeye aliewazindua wenzie pale juu; kuwa ikiwa wataendelea kubeza mabadiliko basi CCM itaanguka mchana kweupe!]. Kwa hiyo ukiamua kumpa kura yako Dk. Magufuli, mpe tu bila wasiwasi! ~SmartVoter~
↧
Baada ya Kutoka Hijja: Majuto Hafanyi Tena Filamu za Aina Hii
Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini, Alhaj Athumani King Majuto, amesema baada ya kwenda kuhiji Mecca, atakuwa hafanyi tena filamu ambazo ndani yake kutakuwa na matendo ya kumchukiza Mungu.
“Sasa hivi filamu kama za kunywa pombe au kuna matukio ya kumchukiza Mungu siwezi kufanya,” Majuto ameiambia Bongo5.
“Lakini ambazo zitakuwa hazima matukio kama hayo nitaendelea kufanya. Mimi sasa hivi ni Alhaj, natakiwa kuwa mfano kwa kumcha Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha watu kufanya mambo mema,” ameongeza.
Chanzo: Bongo 5

Mohammed Dewji Anataka Kuinunua Klabu ya Simba, Kuwekeza Bilioni 20
Mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohammed Dewji ameweka wazi mpango wake wa kuinunua klabu ya Simba inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara.
Akizungumza na kipindi cha Mkasi TV kinachoruka kupitia EATV, Dewji alisema tayari wapo kwenye mazungumzo na rais wa klabu hiyo ili kukamilisha mpango huo.
“Unajua kila mtu ana interest, hakuna interest ya klabu, mimi nimeona sitaki nijihusishe na klabu ambayo haitafanikiwa, ndio maana mimi nilikuwa nasema Azam itakuja kufanya vizuri zaidi kuliko Simba na Yanga na wameanza,” alisema.
“Nimeongea na rais wa Simba na ameniambia nimwandikie paper. Unajua mimi nimemwambia ‘wewe unafikiria mimi nikinunua hisa 51% ya Simba, maana yake nitaipeleka wapi? Mimi ni mtu wa hapa hapa na naipenda Simba. Leo mashabiki wa Manchester United, Arsenal they don’t care klabu ya nani, wanachohitaji ni mafanikio. Mimi nimewaambia nipo tayari niwekeze bilioni 20. Leo Katumbi wa TP Mazembe ni timu yake na inafanya vizuri. Mimi nimewaambia hata nikiwekeza bilioni 20 sitaona hela, mimi na biashara mia nyingine ninapata hela.
Kwenye mpira ni mapenzi na timu basi. Tunataka kuendeleza mpira tuendeleze Simba yetu, tupate raha Simba ikishinda. Tayari nimeshamwandikia paper sasa tunakamilisha tutapeleka kama tutafanikiwa, kama ilishindika nitaanza na Mo Football Club,” aliongeza Mo.
Aliongeza, “Tuliwafunga Zamalek, watu laki mbili walikuja kutupokea na bahati mbaya watu walikufa siku hiyo, sasa baada ya kushinda mimi niliitisha mkutano, nikasema jamani tumebahatika tumeshinda lakini hebu tujilinganishe na klabu ya Zamalek. Leo bajeti yetu ni shilingi ngapi na bajeti ya Zamalek ni shilingi ngapi? Leo Simba bajeti yake ni bilioni moja kwa mwaka it’s a joke!
Mimi nimekuja na fikra nimesema kwamba jamani kwanini kuna watu wamesema wamejenga Simba? Tunawapa hisa bure za milioni 10 kila mmoja, tumefanya projection tunaweza kuraise zaidi ya bilioni 30 mpaka bilioni 40. Ukishapata bilioni 40 leo, ukienda kununua treasure bond unapata asilimia kumi tano.”
“Sasa ukiwa na 40 bilioni , 10% ya 40 bilioni ni 4 na 5% ni 2 bilioni maana yake 6 bilioni. Unatoka kwenye 1 billion ya leo unaingia kwenye 6 bilioni, maana yake nini? Unaweza kumwajiri kocha mzuri, unaweza kuwa na gym pamoja na viwanja, unaweza kununua wachezaji ukashindana na Zamalek na hatimaye baada ya miaka mitano unaweza kushinda African Champions League,” alisisitiza.

Chadema Yaweka Wazi Msimamo Kuhusu Midahalo
CHAMA cha Demokrasi na Maelendeleo (Chadema), kimetoa ufafanuzi wa suala la kutohudhuria kwa mgombea urais kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa katika Mdahalo wa Mgombea urais uliondaliwa na Taasisi ya Twaweza pamoja na Tanzania Media Foundition.
Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alipokua akijibu maswali ya waandishi wa habari katika ufunguzi wa kituo kipya cha mikutano ya waandishi wa habari cha UKAWA,amesema kuwa mdahalo huo haukidhi viwango vya ubora wa kuweza kuwapima vizuri wagombea
Akitaja vigezo vya midahalo mikubwa ya mgombea urais amesema kuwa kigezo hawakuweka kigezo cha wagombea kuulizana maswali,pia waandaaji hao hawana sifa ya kuandaa midahalo kutokana kukosewa imani na umoja huo kwa kutoa tathimin zinazobeba upande mmoja ambao ni wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM).
Aidha Makene aliwashangaa waandaji wa midahalo ambao tayari wameshajipambanua kuwaunga mkono wagombea wengine halafu wanajificha katika pazia kuandaa midahalo ili kuhadaa umma wa watanzania.
Hivi karibuni, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilimkataza mgombea wake Edward Lowassa kuhuduria mkutano ulioandaliwa na Taasisi Watendaji wakuu wa makampuni (CEORT) baada ya Mwenyekiti wake Ali Mfuruki kujipambanua kumuunga mkono John Magufuli mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi.
Mmoja ya waandaaji wa mdahalo wa marais, akiwa katika kampeni ya mmoja wa mgombea Urais

“Nchi ya marekani na nchi nyengine wanakuwa na Taasisi maalum zenye kuamika ambazo huanda midahalo iliyo bora na yenye vigezo bila kukibeba chama fulani” amesema Makene.
Wiki hii katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kulifanyika mdahalo uliorushwa na kituo cha televisheni cha Star tv uliohudhuliwa na wagombea wanne ambao ni Chief Lutaselo Yemba wa chama cha Allience For Democry Change (ADC), Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Maximilan Lyimo wa Tanzania Labour Party (TLP) na Mgombea aliyechelewa kufika kutokana na alichodai ni kuchelewa njia, Hashim Rungwe wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Source:Mwanahalisi

Alichoongea Davis Mwamunyange Jana Alipokutana na JK. Aweka Wazi Kwamba Kwa Upande Wake...
Kwa upande wake mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuliimarisha jeshi la Tanzania ingawa zipo changamoto ndogo ndogo lakini anaamini serikali itazifanyia kazi ili kuweza kuwa na jeshi imara...
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua uwanja wa ndege katika kambi ya kijeshi ya anga iliyoko Ngerengere mkoani Morogoro ambapo amesema anajivunia kutoka madarakani akiwa ameiacha nchi katika hali nzuri ya kiusalama.
Rais Kikwete akizungumza katika uzinduzi huo amesema katika kipindi cha uongozi wake amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuliacha jeshi likiwa katika hali nzuri ambapo ameeleza hakuna nchi inayoweza kuwa na maendeleo kama haina jeshi imara.

January Makamba Ataja Sababu Tisa kwanini CCM itashinda katika Uchaguzi Mkuu Jumapili hii, Oktoba 25
Na;January Makamba
Tarehe 25 mwezi huu Oktoba, Watanzania watapiga kura kumchagua rais wao wa tano, wabunge na madiwani.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu umekuwa na msisimko mkubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa siasa za vyama vingi mwaka 1995.
Mengi yamendikwa kuhusu uchaguzi huu, hususan kutokana na hisia kwamba safari hii Upinzani una nafasi ya kukiondoa madarakani moja ya vyama vikubwa na vyenye muundo bora barani Afrika, chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Matukio mbalimbali kuelekea uchaguzi huo yameleta shauku inayoweza kutengeneza hadithi ya kusisimua.

Nikiwa sehemu ya Timu ya Kampeni ya CCM,na kwa manufaa ya wote ambao wangependa kuwa na mtizamo tofauti, ninatoa sababu 9 kwa nini tunaamini kuwa CCM itaibuka mshindi na kwanini Dkt John Pombe Magufuli atakuwa Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1. Ugombea ‘fyongo’ (flawed) wa Edward Lowassa
Ilishabainika kuwa uchaguzi huu ungekuwa mgumu kwa CCM bila kujali nani angekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Upinzani.
Lakini matokeo ya uchaguzi huu yalielemea upande wa CCM pale Upinzani ulipomchagua Lowassa kuwa mgombea wao. Ni rahisi kwa CCM kuchuana na Lowassa kuliko laiti mgombea wa Upinzani angekuwa Dkt Wilbrod Slaa, ambaye ndiye aliandaliwa kuwa mgombea kabla ya ‘kusukumwa kando’ na nafasi hiyo kupewa Lowassa.
Slaa alikuwa na uadilifu katika maeneo mengi, na aliaminika. Kwa Lowassa, ni vigumu na inanyima raha kuchuana na mfumo aliyoshiriki kujenga na ambao ulikuwa sehemu ya maisha yake hadi Agosti mwaka huu alipohamia Upinzani. CCM ilikuwa na nafasi ya kumpitisha Lowassa kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais.
Hatukufanya hivyo kwa sababu rahisi tu kwamba ingekuwa vigumu mno kumkabidhi kwa wananchi mgombea wa matarajio ya baadaye ambaye ni kiashirio cha yale yasiyowaridhisha wananchi kuhusu CCM. Kuna wanaoamini kuwa uchaguzi huu ni mgumu kwa vile Lowassa ndiye mgombea wa Upinzani.
Sisi twaamini kwamba uchaguzi huu ungekuwa mgumu mara kumi zaidi laiti Lowassa angekuwa ndiye mgombea wetu.

2. Upinzani umesalimisha ajenda yake ya kupinga ufisadi
Kipindi cha miaka 10 iliyopita kimetawaliwa na matukio mbalimbali ya kuwabainisha mafisadi na kuwachukulia hatua.
Vyombo vya habari, taasisi za kiraia na Bunge vimefanya kazi nzuri kushughulikia suala hilo. Rais Jakaya Kikwete ameweka historia kwa kuamuru ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupatikana kwa wananchi na kujadiliwa kwa uwazi Bungeni.
Waziri Mkuu aliyekuwa madarakani, si mwingine bali Lowassa, alijiuzulu kwa sababu ya kashfa ya rushwa. Mawaziri kadhaa walitimuliwa kazi na manaibu waziri wawili wanatumikia vifungo jela. Huu ni uwajibikaji wa hali ya juu japokuwa kuna wanaoweza kudhani ni hatua ndogo. Umma umeamka.

Upinzani ulijenga hadhi yake kwa kuongelewa sana kuhusu ufisadi. Kilele cha Upinzani kilijiri mwaka 2007 katika mikutano mkubwa wa hadhara ambapo walitangaza majina 10 ya watu waliowaita mafisadi wakubwa zaidi, katika kilichokuja kufahamika kama Orodha ya Aibu (List of Shame). Lowassa alikuwa kinara kwenye orodha hiyo.
Ilitarajiwa kuwa Uchaguzi Mkuu huu uwe ‘hukumu’ kwa CCM kuhusu ufisadi. Upinzani ulitarajiwa kuitumia ajenda ya ufisadi ambayo inawagusa watu wengi. Lakini ghafla, kwa kumteua mwanasiasa, ambaye kwa jitihada zao wenyewe Wapinzani, amefahamika zaidi kwa ufisadi, iliwalazimu kuzika ajenda hiyo.
Kilichofuata baada ya hapo ni kituko na kichekesho. Wale mashujaa wa mapambano dhidin ya ufisadi walijikuta wakilazimika ‘kulamba matapishi yao.’
Wengi wao waliokuwa mahiri katika mitandao ya kijamii walilazimika kufuta historia ya baadhi ya waliyoyaandika mtandaoni walipokuwa wakikemea ufisadi, lakini si kabla ya maandiko yao kunaswa kwa ‘screenshots.’ Ulikuwa ni ukweli wa kushangaza.
Ni Dkt Slaa na Professa Ibrahmi Lipumba, viongozi muhimu wa Upinzani tangu miaka ya Tisini, walioamua kujiuzulu nyadhifa zao kwa kukerwa na uamuzi wa Upinzani kumpokea Lowassa.
Matokeo yake, Upinzani walijikuta wakichana kadi yao turufu- ajenda dhidi ya ufisadi. Ni nadra kwao kuongelewa suala hilo, na wanapojaribu kufanya hivyo, ni kwa kujitetea tu.

Jioni moja mwezi Agosti, nilimwona Mbunge wa Upinzani, Peter Msigwa, katika mdahalo kwenye runinga. Aliongelea kitu ambacho kilijumuisha mtizamo wa Upinzani kwa muda huo, na kiliniacha hoi. Alisema, kabla hawajampokea Lowassa, walifanya utafiti wao, na “ufisadi sio ajenda muhimu kwa taifa letu.”
Alidai kwamba wenye ushahidi kuhusu ufisadi wa Lowassa wajitokeze hadharani.Alionekana kusahau kuwa walipomtaja Lowassa katika List of Shame, walitangaza hadharani kuwa wana ushahidi.
Muda si mrefu uliopita, CCM ilikuwa ikiwaomba Wapinzani kuleta ushahidi kila yalipojitokeza madai ya ufisadi dhidi ya viongozi wa chama na serikali allegations were leveled against the party and its leaders.
Haikupendeza kuingiza hoja za kisheria katika masuala ya kimaadili. Upinzani sasa umeamua kwa hiari yao kuchukua ‘chembemoyo’ wakati ambapo viongozi wa CCM wanaongelea ufisadi kwa ujasiri na msisitizo.

Uchaguzi huu Mkuu ni muhimu sana kwa Upinzani. Kimsingi, unaweza kuwa na madhara makubwa. Endapo watashindwa hapo Jumapili, ‘watapotea’ kwa muongo mzima ujao. Ndio maana inashangaza kuona wamechukua uamuzi wa kukimbia ajenda yao kuu ya kupambana na ufisadi ambayo iliwatambulisha na kuwaimarisha. Na kuwapa nguvu kukubalika kwa wapigakura. Kuona wanatarajia kushinda ni miujiza mkubwa.
3. Mabadiliko ambayo kamwe huwezi kuyaamini
Ukizinguka jijini Dar es Salaam utakutana na mabango ya Upinzani yanayodaia “Ni Muda wa Mabadiliko.” Lakini ukisikiliza mikutano yao ya kampeni, ni porojo na hasira tu. Wasemaji wakuu katika mikutano hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani na kada wa muda mrefu wa CCM, Frederick Sumaye na Lowassa mwenyewe.
Kwa pamoja, wamekuwa wana-CCM na katika nyadhifa za juu serikalini kwa zaidi ya miaka 50. Kwa hiyo inasikitisha kusikiliza kauli zao – zinazokosa imani na kupalizwa na aibu – wakipambana na mfumo walioshiriki kujenga, uliojenga tabia zao za kisiasa, na ambao walikuwa wakiusifu miezi mwili tu iliyopita.

Kutokuwa wakweli na kuweka mbele maslahi binafsi kwawatuma kudai kuwa CCM haijafanya chochote katika miaka miaka 50 iliyopita. Inapotokea viongozi wawili waandamizi wa chama na serikali kwa zaidi ya miaka 30, wote wakiwa walioshika Uwaziri Mkuu, kudai kuwa hakuna chochote kilichofanyika katika miaka 50 iliyopita, wajihukumu wenyewe.
Si kwa muundo, mwonekano au ukweli, wanasiasa hao wanasimamia mabadiliko. Yayumkinika kuhitimisha kuwa mabadiliko wanayoongelea ni kuhusu kubadili chombo kilichowaingiza madarakani, mabadiliko ya sare tu za chama. Hawana habari na mabadiliko ya maisha ya wananchi wa kawaida. Wapigakura wameanza kushtukia ukweli huo.

4. Migogoro na mkanganyiko ndani ya UKAWA
Huko nyuma, kila ulipojiri uchaguzi, Upinzani ulijaribu kuunganisha nguvu ili kuing’oa CCM madarakani.Na kila mara jitihada za ushirikiano zilishindikana. Mwaka 2014, mjadala kuhusu Katiba Mpya kuataka serikali tatu uliwapatia ajenda ya kuwaunganisha pamoja. Kisha wakaamua kutafsiri ushirikiano huo kuwa wa kisiasa, wakaafikiana kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais na kugawana majimbo.
Baada ya hapo kukajitokeza unafiki wa wazi. Kuonyesha kuwa matamanio yaliwekwa mbele ya kanuni zilizopatikana kwa jitihada ngumu, chama ambacho jina lake linajumuisha maneno ‘demokrasia’ na ‘maendeleo’ kilitemea mate mchakato wake chenyewe wa kidemokrasia na mshikamano kupata mgombea wake wa urais, na kukurupuka kumpitisha kada wa muda mrefu wa CCM ambaye jitihada zake kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala ziligonhga mwamba.
Waliamini kwamba uamuzi wa Lowassa kuhama CCM ungekiathiri chama hicho tawala, wakitarajia vigogo kadhaa wangemfuata huo Upinzani. Badala yake, ujio wake huko ukapelekea kuondoka kwa wanasiasa wawili waliokuwa nguzo muhimu kwa Upinzani, Dkt Slaa na Prof Lipumba.Kadhalika, wanachama wengine muhimu waliohama na kujiunga na chama cha ACT- Wazalendo, ambacho hakikujiunga na UKAWA.
Kana kwamba hiyo haitoshi, makubaliano ya UKAWA kusimamisha mgombea mmoja kila jimbo yalikumbwa na mushkeli katika majimbo kadhaa na kupelekea malalamiko yaliyosababisha ugumu katika kampeni za Lowassa.
Huko Masasi, mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni, alilazimika kuokolewa jukwaani baada ya waliohudhuria mikutano wake wa kampeni kupiga kelele kuwa wataipigia kura CCM. Katika jimbo la Nzega, Lowassa alilazimika kuendesha ‘kura ya sauti’ kuwauliza waliohudhuria mikutano wake wa kampeni wanamhitaji mgombea gani kati ya wawili wa UKAWA waliokuwa wanachuana. Mpango mzima wa ushirikiano miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA umekwenda mrama.CCM sasa ipo katika nafasi nzuri ya kujinyakulia majimbo ambayo vinginevyo yangekwenda kwa wagombea wa Upinzani.
Lakini kilele cha unafiki wa UKAWA ni hiki. Umoja huo uliundwa ili kutetea Katiba Pendekezwa iliyoshauri muundo wa Muungano wa serikali tatu. Kanuni hiyo ya msingi iliwekwa kando pale UKAWA walipomchagua mgombea wao wa tiketi ya urais, Lowassa, ambaye alikuwa mtetezi mkubwa wa muundo wa Muungano wa serikali mbili. Kwa wengi wasioendeshwa na propaganda, uamuzi wa kutelekeza suala la msingi lililopelekea umoja wa vyama hivyo, kwa ajili tu ya imani ya kufikirika ya kushinda urais, yaashiria uchu wa madaraka na sio mabadiliko yanayohubiriwa kwa wananchi.
5. Lowassa kushindwa kufanya kampeni nchi nzima
Lowassa anaonekana kutokuwa na uwezo wa kusafiri kwa urefu na upana wa Tanzania kufanya kampeni. Mara nyingi amekuwa akitumia usafiri wa anga kwenda mikoani ambako hufanya mikutano mikubwa kwenye makao makuu ya mikoa, kutembelea majimbo mawili au matatu ya jirani kwa helikopta, na kurejea jijini Dar es Salaam. Huko Tanga, kwa mfano, alifanya kampeni katika majimbo matatu tu kati ya tisa mkoani humo. Mkoani Ruvuma, alifanya kampeni katika majimbo matatu kati ya tisa, Kigoma majimbo mawili kati ya manane, na Kagera majimbo matatu tu.
Kinyume chake, mgombea wa CCM, Magufuli amekuwa barabarani tangu Agosti 23, huku akipumzika kwa siku tatu. Anatumia usafiri wa gari, akitembelea kijiji baada ya kijiji, na kufanya mikutano kati ya minane hadi 12 kwa siku. Aina hii ya kufanya kampeni ‘kwa rejareja’ inabaki kuwa nguzo pekee ya kujihakikishia ushindi kwenye uchaguzi mkuu nchini Tanzania, hususan katika maeneo ya vijijini ambayo usikivu na kuonekana kwa vyombo vya habari ni mdogo.
Wakati Lowassa anavutia wahudhuriaji wengi katika mikutano yake katika miji mikubwa, Magufuli anajipatia wahudhuriaji wengi katika kila kona ya Tanzania. Kama idadi ya wahudhuriaji katika mikutano hiyo ya kampeni inamaanisha wingi wa kura, basi kwa hakika CCM itashinda. Lakini tofauti na Upinzani, CCM haidanganyiki na wingi huo wa wahudhuriaji katika mikutano ya kampeni.
Rekodi ya mahudhurio makubwa ilikuwa ikishikiliwa na Agustino Lyatonga Mrema, mgombea maarufu wa kiti cha urais kwa tiketi ya Upinzani mwaka 1995 (ambaye pia alijiunga na Upinzani akitokea CCM). Hata hivyo alishindwa kwenye uchaguzi huo. Sie twategemea kitu kingine.

6. Mfumo imara wa CCM katika uhamasishaji kuanzia ngazi ya chini kabisa.
Katika Tanzania, vyama vichache mno vinavyoweza kuchuana na uwezo wa CCM kuhamasisha wananchi. Wakati Wapinzani huhadaiwa na ‘mahaba’ wakati wa kampeni za uchaguzi, mahudhurio makubwa kwenye mikutano yao ya kampeni na vichwa vya habari magazetini, CCM hutumika nguvu yake ya kimuundo na kuwasha ‘mashine zake za kisiasa,’ kuanzia ngazi ya mtaa (ujumbe wa nyumba kumi) kwa nchi nzima.
Kimuundo, jumiya ya wanawake wa CCM (UWT) pekee ni kubwa kuliko Chadema, chama kikuu cha upinzani. CCM Haihitaji kusafiri ili kufanya kampeni. CCM ipo kila mahala, ikifanya kampeni katika makundi madogo, vijijini na mitaani, kila siku na mbali ya upeo wa vyombo vya habari. Kwa wanaofahamu muundo wa chama hicho, ushindi kwake si jambo la kushangaza.

Kwenye miaka ya 1950s, wakati wa harakati za kusaka uhuru kutoka kwa mkoloni, uwezo wa TANU kuhamasisha ulikuwa nguzo muhimu kwa Tanganyika kupata uhuru wake.CCM imerithi vinasaba vya TANU.
Mwalimu Nyerere aliijenga CCM kuwa imara kwa nyakati kama hizi. Mwaka jana, huku umaarufu wake ukiwa umepungua, CCM ilimudu kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa asilimia 80 dhidi ya umoja Huohuo wa Upinzani inaokabilina nao katika uchaguzi huu Mkuu.
Tofauti haipo kwenye nini kinachoonekana kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii bali jinsi gani makada wa chama hicho tawala walivyofanya uhamasishaji katika kila mtaa na kijiji. Uchaguzi huo wa serikali za mitaa, ambao hufanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, hutoa dalili nzuri kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu.

7. Umahiri wa Dkt Magufuli
Mwaka jana, baadhi ya waandishi wa habari walikiri kwamba ni vigumu mno kumshambulia na kumshinda Dkt Magufuli. Ana rekodi imara ya usafi, uchapakazi na anayetaka kuona matokeo sahihi. Hajawahi kuvutiwa na harakati za kisiasa, na ilikuwa mshangao alipotangaza kuwania urais. Na alipotangaza, hakufanya mbwembwe wala kijitangaza kwenye vyombo vya habari.
Alizingatia kanuni za chama kwa ukamilifu. Dkt Magufuli analeta kumbukumbu za mgombea mwingine aliyekuwa hajulikani mwaka 1995 - Benjamin Mkapa. Wakati umaarufu wa CCM ukiwa chini, huku ikikabiliwa na upinzani kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu aliyehama kutoka chama hicho tawala, CCM ilimchagua turufu yake ambayo ilikuwa ngumu kuikabili.Miaka 20 baadaye, ikikabiliwa na upinzani wa Waziri Mkuu maarufu wa zamani aliyehama chama hicho na kujiunga na Upinzani, CCM imefanya tena ‘vitu vyake.’ Siku zote, CCM hujua ‘kufanya pigo la haja.’

8. Ufanisi wa CCM katika maeneo ya vijijini
Mimi ni Mbunge wa jimbo lisilo mjini, lenye idadi ya wastani ya wapigakura. Mwaka 2010, katika uchaguzi ulionekana kuwa mgumu, CCM ilishinda jimbo langu kwa asilimia 80., na kitaifa kwa asilimia 61. Hivi sasa, tunatarajia ushindi wa CCM kuwa wa asilimia 90 hivi.
Tanzania ina majimbo kadhaa yaliyo kama jimbo langu. Upinzani hupenda kuwapuuza wananchi katika majimbo yasiyo ya mijini, kama jimbo langu, kwa kudai kuwa wanaichagua CCM kutokana na ujinga wao. Wasingeweza kukosea zaidi ya hivyo.

Popote walipo, watu hupiga kura kulingana na mahitaji yao. Mwaka 2000, vijiji vinne tu katika jimbo langu ndivyo vilikuwa na umeme. Leo, vijiji 44 vina umeme. Japo hatujaweza kutoa huduma zote kwa kiwango cha kumfurahisha kila mtu, lakini hali halisi yaonyesha wingi wa wanafunzi mashuleni, walimu zaidi, madaktari na manesi zaidi, zahanati nyingi zaidi zimejengwa, huduma za mawasiliano ya simu zinapatikana kwa wingi, barabara nyingi za lami, nk.
Porojo kuwa hakuna kilichofanyika Kwahiyo wapigakura wasiichague CCM haieleweki katika maoneo hayo ambay kimsingi ndiyo yenye wapigakura wengi. Na wagombea wa CCM wanaposema watafanya zaidi ya waliyokwishafanya, kwa kuzingatia mafanikio yaliyokwishapatikana, wananchi wanawaamini. Hotuba za kampeni ni mwonekano na mantiki.

Chaguzi sio kuhusu ahadi tu bali jinsi gani ahadi hizo zitaandaliwa na kutekelezwa. Jukwaa ambalo kila chama kitanadi ajenda zake za uchaguzi hujengwa wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama husika. Yahitaji mtu kuangalia tu uzinduzi wa kampeni za za Lowassa na Magufuli.
Lowassa aliongea kwa dakika 9 tu - akiahidi, pamoja na mambo mengine, kuwaachia huru wabakaji (sio kama ninazusha hili) wanaotumikia vifungo vyao na watuhumiwa ugaidi wanaosubiri kesi zao. Bila kujali alikuwa na malengo gani wakati anatoa ahadi hizo, makosa hayo hayastahili msamaha wa rais.
Kwa upande wake, Magufuli aliongea kwa dakika 58, akielezea kwa undani ajenda za maendeleo katika nyanja za elimu, ajira, afya, ufisadi, huduma za maji, na miundombinu. Kuanzia hapo, kwa muda wote wa kampeni, mwenendo umekuwa hivyo, kwa uzito wa ujumbe kwenye hotuba zake na muda wa kuhutubia

Wanaohudhuria mikutano ya Dkt Magufuli huondoka katika mikutano hiyo wakiwa na matumaini na wenye nguvu. Kwa upande mwingine, wahudhuriaji katika mikutano ya Lowassa huondoka wakiwa wamekanganywa. Siku ya kupiga kura, wapigakura wanamkumbuka jinsi mgombea alivyoonekana na alivyoongea, na jinsi walivyojisikia walipomwona jukwaani. Kwa kigezo hiki, ni bora ningekuwa upande wa Magufuli.
9. Uongo, uongo na takwimu
Tanzania haina utamaduni wa kura za maoni kupima nafasi za wagombea katika uchaguzi. Tuna utaratibu wa muda mrefu wa kupata maoni ya wananchi katika maamuzi makubwa ya kisera – kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa, marekebisho ya Katiba, na kadhalika. Mwaka 2005, kulifanyika kura ya maoni, iliyobashiri ushindi mkubwa kwa CCM.
Na kwa hakika, CCM ilishinda kwa asilimia 80. Mwaka 2010, kura ya maoni iliyoendeshwa na kampuni ya Ipsos-Synovate iliashiria kuwa idadi ya kura za CCM ingepungua hadi kufikia asilimia 61. CCM ilipinga matokeo ya kura hiyo ya maoni ikidani kuwa yalikuwa kiasi kidogo sana. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama yalivyotabiriwa katika kura hiyo ya maoni. CCM ilipata asilimia 61 ya kura zote.

Hivi karibuni, kura mbili za maoni zilichapishwa. Zote zilifanywa na taasisi huru zinazoheshimika. – Twaweza and Synovate-Ipsos tena- zote zikijihusisha na utafiti wa kusaka maoni. Taasisi mbili tofauti, zilizotumia mbinu tofauti za kufanya utafiti, katika nyakati tofauti, matokeo yaleyale. CCM itashinda kwa asilimia 62 ya kura zote.
Inaruhusiwa, na kwa yumkini ni jambo zuri, kupingana na sababu hizi tisa za kwanini CCM itashinda. Lakini namba zina tabia ya ukandamizaji. Ndio mwelekeo wa kura huwezi kubadilika.
Lakini kwa kuzingatia yote yaliyokwishaongelewa kuhusu kinachodaiwa kuwa ufuasi mkubwa kwa Upinzani, basi muda huu ingetarajiwa tuwa tunajadiliana kuhusu ufuasi wa wengi kutoka Upinzani kuelekea CCM– na sio kutarajiwa ufuasi wa wengi kutoka CCM kuelekea Upinzani.
Na ndiyo, kura za maoni zaweza kukosea, na tusiwekee mkazo sana.Lakini hoja hii sasa ndiyo hupendelewa zaidi na upande unaelekea kushindwa kwenye uchaguzi.
Makala Hii Imeandikwa Na:

January Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
↧
Full Time ya Arsenal Vs FC Bayern Munich na matokeo ya mechi nyingine za UEFA October 20 (+Video)
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea leo October 20 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya. Miongoni mwa mchezo uliyovuta hisia za mashabiki wengi wa soka ni mchezo kati ya Arsenal dhidi ya FC Bayern Munich yaUjerumani ambayo kabla ya mchezo huo kumalizika ilikuwa haijapoteza mechi hata moja.
Kikubwa kilichokuwa ni kivutio cha mechi hiyo ni mashabiki wa soka walitaka kuona kamaArsenal ingevunja rekodi yake yenyewe, Arsenal ambayo ilikuwa imeshapoteza michezo miwili ya awali, ilikuwa haijawahi kupoteza mechi tatu mfululizo za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Klabu ya Arsenal ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya FC Bayern Munich.
Mchezo ambao ulikuwa hukichezwa kwa tahadhari kwa timu zote hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika kulikuwa hakuna timu iliyokuwa imeona nyavu za mwenzake.Arsenal ambayo ilikuwa na wakati mgumu wa kutaka kufufua matumaini ya kutaka kufuzu hatua ya 16 ilianza kupachika goli dakika ya 77 kupitia kwa Olivier Giroud kabla ya dakika ya 90 Mesut Ozil kuhitimisha kwa kufunga goli la pili.
↧
Dada Zangu wa Kichaga Jisafisheni Kimapenzi Maana Sehemu Kubwa ya Jamii inawaogopa Kimapenzi
Ukipata mchumba hasa mmachame wanafamilia wanakuwa wagumu kubariki mahusiano yenu.Hii imetokana na baadhi ya jamii kutendwa baada ya kuoa wachaga.Lakini naamini kuna baadhi ya dada zangu wa kichaga ni wema kabisa na wanamtegemea Mungu na upendo wao unaweza kufuta mabaya yaliyojengeka ktk jamii zetu kwa vizazi vilivyopita.
Hapo awali wanaume wa kikurya walikuwa wanaogopwa na mabinti wengi sana kwa sababu ya kutoa kichapo lakini siku hizi baada ya jamii kuona baadhi ya wadada wameolewa na watu hao na wamepewa mapenzi ya dhati jamii imewakubali.Leo hii ukipata mchumba wa kikurya halafu ukampeleka nyumbani anakubalika.
Hivyo dada zangu jisafisheni kufuta mfumo dume uliojengeka ktk jamii pia mnaweza kutujuza tatizo liko wapi mpaka jamii inaogopa?

Masha akamatwa na polisi kwa kufanya kampeni kambi ya wakimbizi
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha pamoja na viongozi wengine wa Chadema Wilaya ya Mpanda, wamekamatwa na polisi leo , kwa kile kinachodaiwa kufanya kampeni katika kambi ya wakimbizi ya Katumba, wilayani Mpanda bila kuwa na kibali maalum.
Masha ambaye alikihama chama cha CCM hivi karibuni na kujiunga na Chadema amezungumza nasi na kusema ameshikiliwa katika kituo cha polisi cha Mpanda baada ya kufanya kampeni katika kambi hiyo.
“Nilikwenda kufanya kampeni katika kambi hiyo ambayo ina wakimbizi ambao mimi mwenyewe niliwapa uraia mwaka 2009,” amesema Masha na kuongeza:
“Kampeni zinafanyika kule lakini kwa sababu wanazojua wao wametukamata wakati hao wanaoitwa wakimbizi niliwapa uraia kwa amri ya Rais.”
Pamoja na Masha wengine waliokamatwa ni Mgombea ubunge jimbo la Nsimbo, Gerald Kitabu, Abraham Mapunda, Mwenyekiti wa Chadema, Mpanda. Katibu wa Chadema jimbo la Nsimbo, Stanslaus Selemani, Dalas Damian, Lameck Constantine Momose na Francisco Sylvester .
Kwa mujibu wa Masha, polisi wamewachukua maelezo viongozi hao wa Chadema kuanzia saa 9 mchana na wamemaliza saa 10 jioni.
“Tulikamatwa kuanzia saa 7:15 mchana tukachukuliwa chini ya ulinzi mkali wa polisi toka Katumba hadi Mpanda mjini na kuanza kuhojiwa,” amesema.
Akizungumza na mtandao huu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, SACP Dhahiri Kidavashari amesema Masha amekamatwa leo saa 4 asubuhi akiwa na watu wengine sita kwa makosa ya kufanya mkutano bila kibali katika makazi ya wakimbizi.
Kamanda Kidavashari amesema viongozi hao wa Chadema walitumia uwanja wa kambi ya wakimbizi ya Kanoge na baadaye Katumba bila kuwa na kibali maalum baada ya kuona kuwa hakuna ratiba ya mkutano mwingine katika eneo hilo.
“Kufanya mkutano si tatizo, tatizo walifanya hivyo bila kibali, yale ni makazi ya wakimbizi wengine wamepewa uraia lakini wengine hawajapewa,” amesema.

TV stations za Kenya na Uganda zina Upendeleo Sana kwa Lowassa, Kwanini?
Huwa napitia kwa ufupi taarifa za habari za TV stations za Kenya na Uganda.
Vituo kama WBS, NTV, CITIZEN TV, K24, KTN nk. Haiwezi kupita siku mbili ktk taarifa yao ya habari za kimataifa bila kumwonyesha Lowassa na kampeni zake.
Swali:
1. Kwanini wasioneshe na ile ya Magufuli na CCM yake?
2. Zile picha za video wanachukua youtube au reporters wao wako field ktk msafara wa rais Lowassa?
3. Nini lengo hasa la kumpa upendeleo wa kumnadi mmoja na sio wote?
4. Ina maana Magufuli hana heshima kimataifa hata hapa A/mashariki?
5. Ingawa mke wangu(mwana CCM) huwa ananiambia kuwa Kenya na Uganda hawatokuja kupiga kura, hao wanajifurahisha tu. Je ni dhana sahihi?

Familia ya Mwanamuziki Diamond Yammwaga Rasmi Zari..Sababu Hizi Hapa
THE game is over! Sasa ni wazi kuwa familia ya staa mkubwa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnamz’ imemtema rasmi mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile wanachodai …. “Tumechoshwa na uzungu wake”, Risasi Mchanganyiko linaweza kuandika.
Chanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti hili kuwa kina taarifa kuwa mama Latiffa ‘Tiffah’ hatarejea tena nchini kutokana na kushindwana na wanafamilia, kwani wanaendekeza uswahili, kitu ambacho yeye hakiwezi.
“Familia ya Diamond ndiyo imemchoka, unajua yule hajazoea mambo ya kiswahili swahili, ametofautiana nao sana na ndiyo maana hata wao wamesema hawamtaki tena, wanahitaji mswahili mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
FAMILIA YA DIAMOND HII HAPA
Ili kujua ukweli wa maelezo hayo, mwandishi wetu alimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kupitia simu yake ya mkononi, na alipoulizwa, alihamaki na kuanza kufoka, akidai hataki kuingiliwa mambo yake ya ndani na kwamba kama kuna mtu anataka kujua zaidi amfuate Zari huko kwao (South Afrika).
“Hata kama ni kweli, mimi na huyo sijui Zari wenu tumegombana wewe yanakuhusu nini? sipendi kuingiliwa kwenye mambo ya familia yangu, ninachojua ni kwamba hayupo hapa na maisha yanaendelea,” alisema Mama Diamond na kukaa kimya huku simu ikiwa hewani.
Wakati simu ikiwa hewani, ghafla sauti ya kiume ilisikika na kujitambulisha kwa jina la Anko Salum, aliyemtaka mwandishi kuachana na habari hizo, kwani ni za ndani na zitamalizwa na wenyewe kama familia.
Wakati mwandishi wetu akiendelea kuzungumza na Anko Salum, ghafla tena sauti nyembamba na kali masikioni ilisikika na mwanahabari wetu akaibaini kuwa ni ya Esma, ambaye ni dada wa Diamond.
“Mbona mnatufuatilia sana jamani? Nani anafuatilia mambo yenu? Nafasi ya Zari imefika mwisho, tunamkaribisha mwingine yeyote, kama kuna msichana mrembo unamjua, tuletee nyumba yetu ni kubwa sana, na sisi tunaruhusiwa kuoa hata wanawake wanne, Zari ameishia hapo, tena hatujagombana naye, lakini tumechoshwa na uzungu wake, awamu hii tunahitaji mswahili mwenzetu.
“Zari ameenda kwao, kulea watoto wake na kuangalia ustaarabu mwingine, tunamtakia kila la kheri, lakini hatuna ugomvi naye kabisa,” alisema Esma.Jitihada za kumpata Diamond hazikuzaa matunda kutokana na namba yake ya mkononi kutokuwa hewani kila alipopigiwa, hata hivyo jitihada zaidi zinaendelea kumtafuta.
Source:Global Publishers

Sababu ya Shilole Kujichora Tattoo ya Nuhu Mziwanda Kwenye Ziwa Lake Imegundulika
STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoboa siri ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh’ akisema alifanya hivyo ili kumpa imani mwanaume huyo kuwa anampenda sana.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Shilole alisema siku zote mpenzi wake hakuwa akiamini kama anampenda, licha ya ukweli kwamba naye alikuwa amechora tattoo yenye jina lake.
“Nuh alikuwa haamini kama kweli nina mapenzi ya dhati kwake, niliamua kuchora tattoo ya jina lake na sasa ameamini nampenda, mapenzi yetu yameimarika kuliko mwanzoni, amejiona ni mtu muhimu sana kwangu, kwani hata mwanaume yeyote akiona nimejichora jina hili, lazima ashtuke na aone kwamba nina mtu tunayependana,” alisema.
GPL

MBOWE: Hatutakuwa Tayari Kuyakubali Matokeo Kama Itabainika Yamepikwa!!
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amefichua mazito baada ya kueleza hadharani kuwa kamwe chama chake na washirika wao wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hawatakubali matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayobainika kuwa yamepikwa.
Kadhalika, alisema ni vyema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na mamlaka za serikali iliyopo madarakani kuheshimu maamuzi ya wananchi yatakayotokana na kura watakazopiga kwenye uchaguzi mkuu Jumapili ijayo, kwani kinyume chake ni kuhatarisha amani iliyopo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Dk. Emmanuel Makaidi wa chama cha National League for Democracy (NLD) aliyefariki dunia wiki iliyopita, Mbowe alisema watakubali matokeo ikiwa mchakato wote wa uchaguzi utakuwa huru, wa haki na usiokuwa na chembe ya mizengwe katika kila hatua.
Chadema na vyama vingine vinavyounda Ukawa vya Chama cha Wananchi (Cuf), NCCR-Mageuzi na NLD, vimemsimamisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa mgombea wao wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku pia wakishirikiana kusimamisha wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani na uwakilishi.
Akieleza zaidi, Mbowe aliyekuwa akijibu swali aliloulizwa na waandishi kuhusu namna walivyojiandaa kupokea matokeo baada ya uchaguzi mkuu Jumapili ijayo, alisema Ukawa itakuwa tayari kupokea matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ikiwa wataridhika kuwa hatua zote za kisheria na haki za mchakato wa uchaguzi huo kuanzia katika kampeni hadi upigaji kura zimezingatiwa ipasavyo.
Aliongeza kuwa kinyume chake, wao (Ukawa) hawatakuwa tayari kupokea matokeo yatokanayo na hila za namna yoyote ile.
Akifafanua, Mbowe alisema Ukawa haiwezi kukataa matokeo kwa sababu ya kushindwa katika uchaguzi, bali wanachoangalia ni kuzingatiwa kwa haki, sheria na uwazi katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi huo.
“Kupokea matokeo ni mchakato ambao unaanzia katika hatua za kampeni, upigaji kura hadi wakati matokeo yanatangazwa. Siwezi kusema eti tutakataa matokeo kwa sababu tu Nec imetangaza halafu tukaonekana tumeshindwa… la hasha. Bali tutapokea matokeo kama haki, uwazi, sheria na taratibu nyingine zimezingatiwa mpaka kupatikana kwa matokeo,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Sisi Chadema na Ukawa tunaamini kwamba wananchi watamchagua kiongozi wanayemuamini. Lakini kama watu wengine wenye mamlaka ndani ya nchi wakaamua kupindisha sheria na kupindisha maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura, kamwe hatutakubali matokeo hayo. Na hapo amani tunayoihubiri inaweza kuwa ngumu ‘kui-control’ (kuidhibiti),” alisema.
Kuhusiana na mvutano juu ya wananchi kuondoka vituoni baada ya kupiga kura na siyo kukaa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kura, Mbowe alisema msimao wao wa kulinda kura uko pale pale kwa kuwa wana amini kuwa hiyo ni haki yao kisheria.
“Kura ni mali na kama hivyo ndivyo ni lazima tuilinde, tumepanga kulinda kura zetu kwa amani na utulivu nje ya mita 200 kama sheria inavyosema… tunaomba kila mtu na vyombo vya dola viheshimu,” alisema.
Aliongeza: “Kuhubiri amani bila haki ni kulishana upepo. Mamlaka zote za taifa zina wajibu wa kuheshimu sheria za nchi na kuacha kutumia mamlaka zao vibaya na bila vitisho. Kila mmoja akitekeleza wajibu wake kwa misingi ya sheria, hiyo amani wala haitatafutwa, itapatikana tu.”
Mbali na Mbowe, wengine waliojitokeza katika shughuli ya kuuaga mwili wa Dk. Makaidi ni Lowassa, Mgombea Mwenza wa Ukawa, Juma Duni Haji, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi , Waziri Mkuu Mstaafu aliyehamia kambi ya Ukawa, Frederick Sumaye, Kaimu Katibu Mkuu wa Cuf, Twaha Tasilima, Katibu Mkuu wa NLD, Tozzy Matwanga na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.
Wengine waliokuwapo ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee.
Jaji Mkuu Ataka Mahakama Iachiwe Swala la Mita 200
Wakati Mbowe akisisitiza msimamo wa kuwataka wafuasi wa Ukawa kutorudi nyumbani baada ya kupiga kura na badala yake kukaa umbali wa mita 200 kutoka vituo vya kupigia kura ili kulinda kura zao, Jaji Mkuu Othman Chande alikataa kuzungumzia suala hilo na badala yake kutaka mahakama iachiwe ili itoe uamuzi wake kwa haki.
Jaji Chande aliyasema hayo jana wakati alipoulizwa na waandishi baada ya kufungua mafunzo kwa majaji na Wasajili Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam, juu ya wajibu wa mahakama katika uchaguzi mkuu na namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika kusimamia kesi za uchaguzi, yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).
Tayari Mahakama Kuu imeshapanga majaji watatu kushughulikia suala hilo lililoibua mvutano mkali hivi karibuni baina ya viongozi wa Ukawa na wakuu wa Nec na Jeshi la Polisi. Kesi hiyo itaanza kunguruma rasmi leo.
Katika hatua nyingine, Jaji Chande alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni wenye mchuano mkali na kwamba mahakama zimejiandaa kumaliza kesi zitakazotokana na uchaguzi huo kabla ya miezi sita inayotajwa kisheria.
Alisema mwaka 2010 kulikuwa na kesi 44 za uchaguzi kwa ngazi za Ubunge na kati yake, 17 zilikwenda hadi hatua ya mwisho baada ya kutolewa ushahidi huku nyingine zikiisha katika hatua za awali.
“Ushindani ni mkali katika uchaguzi huu, tunatarajia kupokea kesi nyingi za uchaguzi. Tumejiandaa kupokea, kusikiliza kwa haraka ili kuwezesha wapigakura kujua mshindi halali ni yupi,” alisema.
Akieleza zaidi, alisema sheria imeweka wazi kuwa anayestahili kufungua kesi siyo mpigakura bali wagombea wenyewe.
Mratibu THRDC, Onesmo Olengurumwa, alisema wameshirikiana na Ofisi ya Jaji Kiongozi kuandaa mafunzo hayo kwa kutambua kuwa ni wadau muhimu katika kushughulikia kesi za uchaguzi ili kuwezesha haki kutendeka kwa haraka
Goodluck Jonathan Akiri Ushindani Ni Mkali Kati Ya CCM na UKAWA
Mkuu wa Jopo la Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola na aliyekuwa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amekiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu nchini Tanzania una ushindani mkali kutokana na namna vyama vilivyojiandaa lakini akawataka wagombea wote wa nafasi za urais kujiandaa kukubali matokeo kwa maslahi mapana ya taifa lao.
Wagombea wanaochuana kwa karibu ni, Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Lowassa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili nchini, Jonathan aliyekubali kuondoka madarakani Mei mwaka huu na kumpisha Muhammad Buhari baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu nchini mwake, alisema katika uchaguzi wowote kuna kushinda na kushindwa na hivyo wagombea wajiandae kwa matokeo yoyote ili kuiacha nchi yao ikiwa salama.
Alisema ijapokuwa ushindani ni mkali, Jumuiya ya Madola inaamini kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba imani yao kubwa ni Tanzania kusimamia demokrasia iliyokuwapo wakati wote tangu ipatre uhuru wake mwaka 1961.
Jonathan anaongeza jopo lenye waangalizi 14 kutoka mataifa mbalimbali yaliyo wanachama wa Jumuiya ya Madola
Source:Mpekuzi blog

Ninachokiona; Serikali ya Magufuli Inayokuja na Shaka iliyopo...
Ndugu zangu,
Naziona kila dalili, na nimelisema hili zaidi ya mwezi mmoja uliopita, kuwa mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli ndiye atakayeunda Serikali ijayo ya Awamu ya Tano. Na sasa naiona pia shaka moja kubwa katika utawala ujao wa John Magufuli. Ni shaka ya kweli na naamini ndiyo kimsingi imetufikisha hapa tulipo leo.
Kwenye kampeni zake, John Magufuli amefaulu kuibeba ajenda ya kupambana na rushwa na ufisadi. Kupambana na watendaji wazembe. Kati ya nyingi, ukweli hizo ndio kero kubwa za Watanzania. Ni bahati mbaya kwa UKAWA ikiongozwa na Chadema, kuwa hii ndio ilikuwa ajenda yao waliyoibeba huko nyuma , nayo ikawabeba kisiasa. Wameipoteza, hivyo kupoteza pia dira kisiasa. Zikiwa zimebaki siku nne tu kabla ya Watanzania kupiga kura, ni miujiza tu ya kisiasa itakayopelekea Ukawa waliopoteana kurudi kwenye reli kuu na kupewa na wapiga kura, dhamana ya kuunda Serikali.
Na kwa hakika, ujio wa John Magufuli utaambatana na matarijio makubwa ya umma juu yake. Shaka kuu inajengwa na swali la je, atakidhi matarajio hayo katika mazingira ambayo yamepelekea Chama chake kuwa mbali na wanyonge kwa kukubali wafanyabiashara kuwa karibu sana na chama, na pengine hata baadhi ya viongozi wa dini ? Na bahati mbaya umma hautataka kusubiri mwezi mmoja upite, utataka kusikia kwa kauli na matendo utekelezaji wa yale ambayo John Magufuli amekuwa akiyahubiri kwenye majukwaa ya kampeni.
John Magufuli anayekuja, atakuwa na nafasi ya kipekee inayofanana na ya Mwalimu Nyerere kwa kuweka rekodi ya kuingia madarakani kwa kufanya kampeni ambazo hazikuhusisha sana matumizi makubwa ya fedha ambayo mara nyingi huambatana na michango ya wafanyabiashara wakubwa. Hivyo, John Magufuli hatakuwa na wadeni wake wa kuwalipa fadhila, isipokuwa, kuwahakikishia wafanyabiashara hao, uwepo wa mazingira mazuri ya kufanya biashara zao na walipe kodi ili zisaidie maendeleo ya wananchi wengine walio wengi. Kuna haja ya kutenganisha biashara na siasa, kuwa hata watendaji wakiwamo mawaziri, mbali ya Magufuli kuwasainisha mikataba, lakini umma ungetaka pia kwenye mikataba hiyo mawaziri na watendaji wakuu wawe tayari kutenganisha uongozi wa kisiasa/utendaji wa kiserikali na shughuli zao za kibiashara.
Na kwa kweli hili za kampeni za urais kuchangiwa na wafanyabiashara wakubwa lina mifano hai ya athari hata kwa wenzetu walioendelea kidemokrasia mfano wa Marekani.
Kwenye kampeni za kuwania Urais wa Marekani mwaka 1996, ambapo, mbali ya Bill Clinton kupambana na George Bush ( Baba) alikuwepo mgombea binafsi bilionea Ross Perrot aliyegharamia kampeni za urais wake kwa fedha za mfukoni mwake. Wamarekani hawakuwa tayari kutawaliwa na Rais bilionea Ross Perrot, na pamoja na ushindi wa Bill Clinton, Wamarekani walitilia shaka pia michango aliyopewa Bill Clinton na wafanyabiashara wakihofia kuwa wafanyabiashara hao wangenufaika zaidi kwa misamaha ya kodi. Katika hili, Bill Clinton mwenyewe, mwaka ule wa 1996, alikiri udhaifu huo kwa kutamka;
" Mistakes were made in raising money for my re-election campaign, but contributors did not buy influence with me and the system is not corrupt.." ( Mwandishi, The Guardian, Juni 30, 1996)
Tafsiri hapo ni kuwa, Clinton alikiri kuwa makosa yalifanyika katika kuchangisha fedha kumwezesha kushinda awamu ya pili ya urais, lakini, wachangiaji wa fedha hawakuweza kununua ushawishi kwake na kwamba mfumo haujaathirika na rushwa/ufisadi.
Kimsingi, katika nchi zetu hizi, hatari ya Rais na chama cha siasa kutokuwa na mipaka inayoonekana wazi yenye kutenganisha siasa na biashara, ina matokeo ya rais aliye madarakani na chama husika, kuwa mbali na wanyonge walio wengi.
Kuna wakati, akiwa madarakani, Benjamin Mkapa aliwaambia wazi wana CCM wenzake kule Dodoma, kuwa kihistoria, TANU na CCM imekuwa kimbilio la wanyonge. Mkapa akabainisha, kuwa CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara. Hili ni kosa la kisiasa.
Na nilipata kuandika, kuwa kama Chama Cha Mapinduzi kina nia ya kupunguza kupotea kwa imani ya umma kwa chama hicho, basi, kutahitajika, si tu kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya muundo wa Serikali na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, bali kufanyika kwa mabadiliko makubwa yenye kishindo. Moja ya matarajio ya umma sasa, sio tu Wana-CCM, ni kuwa kwenye urais wake, John Magufuli ataongoza mabadiliko hayo makubwa na ya kishindo.
Kuna watakaopuuza, lakini, ni ukweli, kuwa tuhuma za ufisadi zimekipaka matope mno Chama Cha Mapinduzi. Kwenye macho ya umma, chama hicho kimechafuliwa na tuhuma hizo za ufisadi. John Magufuli ni ' kofia mpya' kiutawala. Jumapili ijayo, kwa hali ilivyo sasa, Watanzania watakwenda kuchagua ' Kofia Mpya'. Hivyo, watakuwa na matarajio makubwa yanayoweza kugeuka anguko kuu la Magufuli na CCM kwa chaguzi zijazo, kama Magufuli asipotimiza matarajio hayo.
Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yawe ni fundisho kwa chama tawala. Kama CCM itataka kubaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi, kuwa na uhalali wa kubaki madarakani, basi, ina lazima ya kujipambanua kwa vitendo kutoka kwenye yote makubwa yenye kuhusiana na ufisadi na maovu mengine. Ibaki kuwa kimbilio la wanyonge. Isifike mahali, chama kikajikuta katikati ya mgogoro na umma. Hilo laweza kuharakisha mazishi ya chama hicho, yasiyo na kisomo.
Maggid,
Iringa.

Shaffih Dauda Awakalia Kooni TFF na Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars..Adai ni ya Kisela na ni Wapigaji wa Fedha tu
Juzi tumetangaziwa kamati ya ushindi itakayo hakikisha Stars inachomoka na ushindi katika mchezo ujao dhidi ya Algeria, mchezo ambao umechachawisha na kukurupisha akili za watu makini tunaowaamini.
Tumewahi kuwa na kamati za aina hii ambazo hazikusaidia chochote, kamati zilizosheheni watu wa mipango na wenye ushawishi mkubwa kwa Watanzania, pamoja na kuwa na wajumbe mahiri haikutimiza lengo lake. Leo hii inaundwa kamati ya ‘kisela’ na kuwapa ujumbe ‘washikaji’ na kutuaminisha wanaweza kuifanya kazi iliyo shindwa kufanywa na watu ‘wenye akili zao’.
Sijajua vigezo walivyotumia kuwapa ujumbe hawa ‘washkaji’ ambao kila siku wanahusika na timu
hii, sasa kama sio upuuzi ni nini? Upigaji au Mazingaombwe? Sasa kuna haja gani kuunda kamati ya ushindi ya wadau wa TFF ambao michango yako imeshindwa kusaidia timu? Watapata wapi mawazo mapya, connnection mpya na changamoto mpya? Hamuoni ni sawa na abiria kusukuma gari wakiwa ndani ya gari? Watalisogeza kwa miujiza gani?
Labda tuelezwe kamati hii ina dhima tofauti na kamati zilizopita, zilizoundwa na watu sahihi
kama aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskzani Mheshimiwa Zitto Kabwe, alikuwemo
pia Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za jamii NSSF Dr. Ramadhan Dau, kamati iliyoundwa baada ya Taifa Stars kuifunga moja ya timu ngumu barani Afrika, timu ya Morroco kwa mabao 3-0, na baada ya ushindi huo mtamu tukaamini tumeshafuzu kombe la Dunia.
Lakini safari tuliyoitegemea na kuamini tumeshafika, tukawapa jukumu wadau hawa
wakubwa wenye uwezo kiushawishi na hata kifedha ili kushika usukani, tulijikuta gari inakata kona na kurudi Dar es Salaam. Sasa TFF haikumbuki au ni makusudi? Kuna faida gani ya kamati hii?
Moja ya kazi za kamati ya juzi ya ‘kisela’ ni hamasa kwa wachezaji na mashabiki, sasa tujiulize ni kweli tunahitaji kamati itufanye kazi hiyo? Wachezaji wanapewa hamasa na kamati? Na kuhusu mashabiki jamani tuna kitengo cha habari TFF ambacho mkuu wake wa Idara ni mjumbe wa kamati hii pia, rafiki yangu Baraka Kizuguto, sasa kama alishindwa kutumia nafasi yake kama mkuu wa Idara ataweza vipi kuitumia leo akiwa kwenye kamati? Huku sio kusukuma gari ukiwa ndani ya gari?
Kuwapa hamasa mashabiki ni kwanini TFF isishirikiane na media kufanya kazi hiyo? Kwanini TFF isipunguze au kuondoa viingilio katika michezo ya Taifa Stars? Mambo madogo haya ya kuamua mara moja mpaka kuwe na kamati? Hamasa haijengwi kwa maneno, fanya yanayooneka.
Dhima nyingine tutaambiwa ni ukusanyaji wa pesa. Hapa ndio nilipochoka kabisaa! Ni kweli
kwa sasa Taifa Stars udhamini wake haujitoshelezi mahitaji yake kiasi kwamba tunatakiwa tuwe na kamati ya kuitafutia pesa?
Kwa nini badala ya kuwa na kamati hii, Rais wa TFF Ndg. Jamal Malinzi asiimarishe kitengo cha masoko cha TFF ili kifanye kazi ya kiuweledi zaidi kutafuta co-sponsors (wadhamini pacha) wa Taifa Stars kitu ambacho ninaamini ni cha kudumu maana ukipata udhamini kwa miaka mitano unakuwa na uhakika wa kupata fedha za kuigharamia timu kwa miaka mitano na sio fedha ya kamati ambayo ni ya hisani na tutambue hisani hua inatoka pale tu timu inapofanya vyema, lakini ikiboronga kamati hua zinakufa ‘automatically’.
TFF irejee na ituambie tija iliyopatikana wakati ule ilipoundwa kamati ya kina Dr Ramadhan Dau
na kina Mh. Zitto, je lengo la Taifa stars lilifanikiwa? Hamasa ilikuwepo? Kwa bahati mbaya sana watu ambao wako mbali na TFF hudhani watu wa hizi kamati huwa wanatoa pesa zao mfukoni kuchangia timu hapo ndipo tunakosea, hizi kamati zitakwenda kutumia pesa za TFF imefika mahali hata vikundi vya kushangilia vinalipwa pesa na hata tiketi vingine vinapata, je hii ndio hamasa?
Huu ni nini kama siyo mpango wa upigaji na kuimomonyoa TFF? Mna sababu gani za kuungwa mkono na wadau wa soka la Tanzania? Hiyo haitoshi basi tuje na ‘vivid example’ nchi fulani imefanikiwa katika mashindano kwa kuwekeza kwenye kamati kama hizi.
Kila siku mwenyewe Malinzi anakiri Madagascar wanafanikiwa sasa hivi katika soka kwa kuwa wamewekeza katika soka la vijana wamewekeza katika ujenzi wa miundombinu ya soka, sasa kama tunaifahamu njia ya mafanikio kwanini hatutaki kufanya kama wenzetu wanaofanikiwa na badala yake sisi tunataka njia zetu za upigaji tu?
Wiki iliyopita kituo cha kulelea vipaji cha Kidongo Chekundu kimefunguliwa hatukuona coverage kubwa kupewa hicho kituo wala TFF haijatuambia itakitumiaje hicho kituo katika kuendeleza soka la vijana lakini kamati za ‘upigaji’ zinapewa covourage kubwa kwa kua zina watu wenye fedha na majina mjini, hapana sio kila kitu kina tija.
Tunahitaji Malinzi aje na mpango mkakati imara kwa ajili ya timu ya Taifa na sio hizi kamati za vipindi kama ‘tumbo la period’ kwa kina dada, Watanzania wanapenda mpira sana huhitaji kamati kuwapendesha, unachohitaji ni kuwaonesha tumaini katika kiwanda cha soka, ‘otherwise’ niwatakie upigaji mwema wa pesa za serikali ambazo tunaambiwa hazina macho, pia niwatakie magumashi mema na mzidi kula na sisi vipofu, lakini siku tukifumbua macho kama Bartholomayo mnatueleza nini mmefanya wakati tupo gizani.
Source: Shaffih Dauda
↧
Matusi kwa Lowassa Yalivyobuma na Kumuongezea Umaarufu zaidi
Matusi ni silaha sawa na zilivyo silaha nyingine za kupambana na adui, lakini silaha hii haijafua dafu kwa Lowassa. Wanaompenda Lowassa hawakatishwi na matusi kwa Lowassa. Wanaompenda Lowassa na UKAWA wanaposikia matusi dhidi ya Lowassa na UKAWA wanajihisi kama vile wametukanwa wao pia. Hivyo, wanapambana na matusi hayo kwa njia mbalimbali kama vile kuzidisha mahaba kwa Lowassa, kuhudhuria mikutano yake, kukaa kimya bila kuyajibu, kuzima na kususia vyombo vya habari (redio, tv na magazeti) vinayotumika kupeperusha matusi hayo, kuongeza zaidi mbinu za kampeni na hatimaye kujiandikisha na kwenda kupiga kura kwa wingi. Baada ya matusi kushindwa kufanya kazi yake iliyokusudiwa kwa Lowassa mbinu gani mpya itafuata?
↧
↧
Wife Kanibambaa na Condom Moja, Sasa Anataka Kujua Mbili Zilikwenda Wapi
Wadau na wakuu wote hapa Jf amani iwe kwenu, nimekaa pembeni kwa muda mrefu kidogo kutokana na kuwa bize kwenye kipindi hiki cha kampeni lakini nimekuja hapa kwa dharula tu.
Nimekuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya ushindi kwenye kampeni ktk jimbo flani ambalo lipo ndanindani sana, baada ya kukaa kwa kwa zaidi ya mwezi nikiwa nje ya mji juzi wife kaja kunitembelea akiwa kaongozana na mke wa mgombea maana familia zetu marafiki, tena ujio wao ni wa kushtukiza bila taarifa (cku umepandishwa daraja wanasema alini surprise)
Mwanzo tulipoonana alikuwa ni mtu mwenye bashasha tena aliyejawa muwashawasha, nikajua hapa leo kazi ni moja kuviringishana mwanzo mwisho usiku baada ya msosi yeye akatangulia kulala sisi tukabaki na vikao vyetu vya mikakati, saa 6 hivi naingia chumbani namkuta kakaa kitandani amefura kwa hasira hadi nikapata hofu (hapo nikaona lile tumaini la kuviringishana linayeyuka taratibu)
Akaniuliza (hapo akataja jina langu halisi, hicho ndo kipimo cha kuonesha hasira zake ni kuniita kwa jina) kisha akanionesha "condom nyingine mbili zimeenda wapi" ilikuwa imebaki moja tu! moyo ukafanya paaaaah! Ujanja wote mfukoni sura ikanishuka halafu nikahisi inapauka nikahisi kama vile moyo unasinyaa pumzi zikabana moyo ukapoteza mwenendo wa mapigo yake, kwa kweli alinishtukiza kwa shambulio baya sana.
Tangu siku hiyo hadi alipondoka cku mbili baadae tulikuwa tunalala na nguo tu, hakuna maelewano jamani hebu nipeni vi mbinu viwili vi3 vya kumlainisha huyu mtu ikiwemo uongo wa level za juu maana naona anaelekea kufika kiwango cha mwisho cha uvumilivu wake, nitamkosa hivi hivi hii ni serious jamani.

Never Seen Before Throwback PHOTO of VERA SIDIKA! She Was Once a Nobody
↧
Kiongozi Aliyeshindwa Nigeria Ashauri Watakaoshindwa Uchaguzini Tanzania
Kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Tanzania waliotoka Jumuiya ya Madola ametoa wito kwa watakaoshindwa uchaguzini Tanzania kukubali matokeo.
Goodluck Jonathan, ambaye mwenyewe alishindwa uchaguzini na upinzani amesema uchaguzi ni kama biashara.
“Kuna kushinda na kushindwa,” amenukuliwa na gazeti la The Citizen la Tanzania.
Amesema kukubali matokeo kutasaidia kuepusha mzozo wa kisiasa.
Kutokana na kupanda kwa joto la kisiasa nchini humo, Watanzania wengi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu yanayoandikwa magazetini.
Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba aliwapata wengi wakizingira vituo vya kuuzia magazeti Dar es Salaam kujipasha habari.
Jonathan, aliyeshindwa uchaguzini na Muhammadu Buhari mwezi Machi, alikubali matokeo upesi baada ya kushindwa na kupuuzilia mbali ushauri wa waliomtaka kupinga matokeo.
Mwandishi wa BBC aliyeko Zanzbar Aboubakar Famau aliwapata raia huko wakikusanyika mapema vikuo vya kuuzia magazeti kutazama vichwa vya habari.
Jumuiya ya Madola ina waangalizi 14 wa uchaguzi nchini Tanzania na wanatarajiwa kuwa nchini humo hadi Oktoba 31.

More Pages to Explore .....