Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

DIVA LOVENESS NDANI YA PENZI ZITO LA CRAZY GK WA EAST COAST

$
0
0
Diva akipenda, ulimwengu wote utajua. Hajui kuficha siri na haoni shida kuweka wazi hisia zake wote wajue. Na kwakuwa Valentine’s Day ndio hii, mtangazaji huyo wa redio ambaye kwa sasa ana uhusiano na rapper wa East Coast Team, King Crazy GK, amewaonesha followers wake wa Instagram kuwa kwa sasa si Diva the Bawse tu, bali ni ‘Diva the Queen’.

Diva amepost picha inayomuonesha akipigwa busu shavuni na Mfalme wake na kuandika: Me and My GK….. closer .. kisses from US.”

SNURA"UKWELI NIMEUMIA SANA NA MWAKA HUU UMEKUWA NI WA MAJANGA KWANGU"

$
0
0

BAADA ya hivi karibuni kufungiwa video ya wimbo wake, staa wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi amesema ameendelea kuandamwa na majanga ambapo hivi karibuni alipata msiba wa babu yake huku mdogo wake akipata ajali.
Akizungumza kwa huzuni, Snura alisema mwaka huu umekuwa wa majanga kwake kwani babu yake huyo alimlea na kushika nafasi ya baba yake tangu alipozaliwa hadi kufikia utu uzima.

“Ukweli nimeumia sana na mwaka huu umekuwa ni wa majanga kwangu kwani babu yangu huyo nilikuwa namuita baba kwa sababu yeye ndiye aliyenilea mpaka nikafikia umri huu nilionao, mdogo wangu naye alipata ajali mbaya yuko hoi hospitali, utumbo ulitoka nje na kwenda kufanyiwa oparesheni, nimechanganyikiwa,” alisema Snura.

LADIES:JINSI YA KUMUWEKA MUMEO KIGANJANI

$
0
0
Jamani ngojeni niwape habari ya kuboresha mapenzi kwa waume zenu hata mkawa mmewaweka kwenye viganja na unamshika utakavyo bila mwanamke yeyeote kumsumbua na kumrubuni mumeo.
1. Mume kama mume anachoka kitu kimoja au hikohiko kila siku hivyo anataka mabadiliko, sio tu kwenye chakula kwenye kila kitu kinachohusu nyumba hivyo ni jukumu lako mama/mke kuwa na mabadiliko hayo.

2. Mke kama ulizoea kuvaa suruali mara kwa mara hebu uwe unabadilisha mara moja moja na kuvaa sketi fupi usawa wa magoti iwe ya kubana kidogo (hakikisha mumeo anaona mabadiliko hayo). Kama ulikuwa wa kuvaa sketi ndefu basi siku hiyo vaa pensi usawa wa magoti (mkiwa nyumbani kwenu na si vazi la kazini) hakikisha mumeo anakuona hii huleta hamasa ya kutaka kujua mke wangu kesho atatokaje hivo kumuongezea hamasa ya kukuangalia kila siku.

3. Unajua tabia za haose girl nyumbani kwako anapomuhudumia mumeo au hata anapowahudumua wewe na mumeo, mfano anavowaandalia chakula na kuwakaribisha, anavokuwa amevaa, sauti na lugha yake anapoongea na nyie. (hapa ni kuwakamata waume wanaotamani kutoka/kutembea na housegirls) siku moja moja hasa week end ondosha watu wote nyumbani kwako na ubaki wewe na mumeo kisha vaa kama haouse girl (like kanga ya lubega kiblose simple na sketi simple) anza kumkaribisha mumeo karibu kuoga (kwa sauti ya kinyalu) mnisamehe wanyalu si kwamba housegirl wote ni wanyalu. 
Huku ukiwa unajibinya vidole kama mto mwenye woga unamuita mumeo, samahani shemeji chai tayari na kagoi kwa mbali cha heshima. Hapa mumeo lazma akutizame na hakikisha siku hiyo hatoki.
Akiwa anakunywa chai unamwambia samahani shemeji naomba nikakusaidie kutandika kitanda, akikuruhusu unakimbia mbio huku unatandika kwa mikao ya kimitego mitego lazima aje akuchungulie leo nini kimekupata hapo ataona mikao yako ya kimitego ukitandika kitanda ukimaliza unamtaarifu chumbani pako tayari shemeji(hii unajifanya wewe ni house girl na akili yake itawaza u r a house girl so anapata huduma tofauti). 

Mtu huyo aliendelea kuelezea kuwa wanaume akili zao huwa zinawaza kitu kilichopo mbele yake na si cha baadae sana hivo ukifanikiwa kuiteka akili yake kwa wakati huo ndo umemnasa. Mwanaume pia hapendi kuambiwa kuwa amekosea hata kama amekosa hivo mke usipende sana kumwambia mumeo makosa yake hata kama amekosa, ikibidi unatumia lugha ambayo hatajisikia vibaya.
Kila siku umpende na kumjali mumeo tuu hata kama yeye hakurudishii mapenzi hayo vile wewe unamuonesha. 

4. Siku nyingine unakuwa baa medi wewe mke ndio na siku hiyo unampa ofa mumeo akiwa nyumbani kwenu. Mke unavaa kama baa medi wanavovaa kisha baada ya mlo unaanza kumkatia kanywaji na ukiwa nae mezani wewe usinywe sana ili uweze kumuhudumia, unafanya kama baa medi wanavofanyaga, unamkaribisha kinywaji na baada ya bia mbili tatu unamuomba kukaa nae muongee obvious atakubali. Hapo nawe unaomba uagize kinywaji kimoja akulipie (kumbuka unafanya kama uko baa ila uko nyumbani kwako) lengo ni kumteka mume akili asikuone kama mke akuone kama baa medi na unampa huduma zote za baa medi. Ili kesho yake ukirudi kuwa kama mke anakuwa ameshabadili mtazamo wa kuwa mke wangu nimemkinahi.
Akikuruhusu kukununulia kinywaji hunywi kwanza unaka tuu nakuanza kustorisha nae habari za kawaida tuu za kitaa au za maisha. Akikuuliza mbona hunywi kinywaji nilichokununulia unamwambia ntakunywa baadae niko kazini, hapo unakuwa umezidi kumteka kiakili na anakuwa anajiuliza niko baa niko nyumbani, kwakuwa kanywaji katakuwa kamemtembelea vizuri tayari atakubembeleza tuu kunywa bana hata moja tuu hutalewa maana wanywaji huwa wanapenda kampani ya kunywa. (waweza mtolea sababu kinywaji ulichoninunulia nimelipia short ya jana hivo siwezi kunywa, atakununulia kingine) kunogesha uhalisia wa baa ukiwa nyumba

5. Siku nyingine unakuwa mama ntilie, pata vionjo vyo te wanavyofanya mama ntilie kuwakaribisha wateja wao kisha nawe umkaribishe mume kwa staili hiyo. 

Wenyeji wa hilo eneo waliendelea kuelezea mengi ila haya ndo yalinikodolesha masikio nikaona niwashirikishe wenzangu.

Kazi kwenu wadada wenye waume na P.O.Box zao
Valentine njema wapendwa wote
By Mkunde Original

NAPE ATOFAUTIANA NA JAJI WARIOBA BUNGE LA KATIBA

$
0
0
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba, litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.

Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.

Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.

Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba likipewa jukumu la kuandika Katiba linaweza kubadili mambo mengi, lakini kama Katiba itakuwa imeandaliwa na chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa kutobadili hoja za msingi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: “Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja.”

Nape alisema kulingana na sheria hiyo, Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho kadri itakavyoonekana kuwa inafaa.

“Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge hilo kwisha wananchi watapiga kura ya maoni,” alisema.

Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si kubadili hoja za msingi, Nape alisema: “Maboresho maana yake ni kubadili. Ukiwa na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?”

Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe katika uamuzi wake.

KESI YA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI MWANGOSI YANGURUMA

$
0
0
Dar es Salaam na Iringa. Kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi inayomkabili aliyekuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mwenye namba G. 2573 Pacificus Cleophase jana ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa mmoja kati ya 11 wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi, Longishu Losingo (29) amelalamika kuwa wanalishwa mchuzi wa maharage gerezani.

Kesi hiyo ya Mwangosi inasikilizwa na Jaji Mfawidhi, Mary Shangali.

Wakili wa Serikali, Adolf Maganda alidai kuwa mtuhumiwa Cleophase ambaye alikuwa askari polisi mkoani Iringa alifanya mauaji hayo Septemba 2 mwaka 2012 katika eneo la Nyololo, wilayani Mufindi.

“Mshtakiwa alitenda kosa hilo wakati alipokuwa akiwaamuru wafuasi wa Chadema kuondoka katika eneo la tukio walipopanga kufanyia mkutano,” alidai.

Maganda alidai kuwa katika tukio hilo, mtuhumiwa alifyatua risasi na kumpiga marehemu.

Wakili huyo alidai kuwa wafuasi wa Chadema walifika katika eneo hilo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano ambao katibu mkuu wa chama hicho alikuwa anatarajia kuhutubia.

Alisema mkutano huo ulikuwa ufanyike licha ya polisi kuwaandikia Chadema ikiwataka wauahirishe ili kupisha zoezi la sensa.

Aliendelea kuieleza mahakama kuwa baada ya kuzuiwa kufanya mkutano, wafuasi wa chama hicho walianza kurusha mawe na kuwaumiza baadhi ya askari polisi, hatua iliyowalazimisha kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya kuwasihi kutokufanya mkutano huo.

Maganda alidai kuwa mshtakiwa akiwa na bunduki alikwenda katika eneo la tukio alilokuwa marehemu na kufyatua risasi na kumpiga marehemu ambaye alikufa papohapo. Alidai kuwa taarifa ya daktari inaonyesha kuwa kifo cha Mwangosi kilisababishwa na kupatwa na majeraha yaliyotokana na mlipuko mkali.
Credits:Mwananchi

AMUUA MWENZAKE WAKIGOMBEA SIGARA

$
0
0
Uvutaji wa sigara umeleta maafa, baada ya mtu mmoja kukatwa mkono na kuuawa na mwenzake wakati wakigombea sigara.

Katika tukio hilo lililotokea Korogwe, Jumapili iliyopita, Februari 2, mnamo saa nne asubuhi, Idi Mkono, mwenye umri wa miaka 30 alimkata mkono Ramadhani Gudelo (35) na kumuua baada ya kutokea ugomvi uliohusu sigara.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Massawe alisema kuwa Polisi Tanga wako katika msako mkali wa kumtia nguvuni Iddi Mkono (30) kwa tuhuma za mauaji.

Kamanda Massawe ameitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, badala yake wafuate taratibu na sheria zilizopo.

Wakati huo huo, watu wawili wanashikiliwa na polisi, mkoani hapa kwa tuhuma za kukamatwa na lita 147 za pombe haramu ya gongo maeneo ya Handeni, mkoani Tanga.

Kamanda Massawe alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa watuhumiwa hao lilitokea Februari 2 mwaka huu saa 5:30 asubuhi.

Massawe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hussen Muhadu (48), pamoja na Ramadhani Ugarawe (40), wote wakazi wa Chanika Handeni.

Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Aidha Kamanda Massawe aliwaonya wananchi kuchukua tahadhari na matendo ya uhalifu wa aina yoyote ambao unaweza kusababisha kuvunja sheria, huku akionya kuwa kwa yeyote atakayekiuka sheria zilizowekwa atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

KESI YA KIFO CHA KANUMBA, LULU AKESHA AKIOMBA

$
0
0
Stori: imelda Mtema na Mayasa Mariwata
STAA wa Filamu ya Foolish Age, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema hivi sasa anakesha akiomba ili mambo yaende vizuri katika kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, Ijumaa lina maelezo yake ya kutosha.

Lulu amemwambia paparazi wetu kuwa alishaanza kuyasahau matatizo hayo lakini hataweza kupingana na amri ya mahakama iliyopanga kuanza kusikiliza kesi hiyo kuanzia Februari 17, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar.

“Lazima kesi iendelee na sheria ichukue mkondo wake, pamoja na kwamba nimekaa uraiani kwa kipindi kirefu na kuanza kusahau mambo hayo,” alisema Lulu.

Alipoulizwa anachokitegemea katika kesi hiyo, msanii huyo alidai kwamba hana cha kukitegemea zaidi  ya kukesha akimuomba Mungu.

“Nakesha nikiomba, namwamini Mungu atanisaidia kama alivyosikia kilio changu cha kuomba dhamana,”aliongeza.

Msanii huyo anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia aliyepata kuwa msanii nguli katika tasnia ya filamu za Kibongo, Kanumba Aprili 7, mwaka 2012.

Aidha, baada ya kuachana na Lulu, Ijumaa lilizungumza na mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa juu ya kutajwa kwa kesi hiyo na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo; 
Ijumaa: Unajisikiaje kuona Lulu akipandishwa kizimbani tena?

Mama Kanumba: Mmmh! Kwa kweli najisikia vibaya sana jamani.
Ijumaa: Unajisikia vibaya  kwa kuwa Lulu anapandishwa kizimbani au...?
Mama Kanumba: Pamoja na hilo lakini kesi hii inanikumbusha machungu ya mwanangu, naona mambo ndiyo yamefufuka upya wakati nilishaanza kuyasahau.

Ijumaa: Unasemaje kuhusu kushtakiwa kwa Lulu?
Mama Kanumba: Binafsi sijamshitaki Lulu ni serikali ndiyo iliyofanya hivyo, tuache sheria ichukue mkondo wake.
Credits:Global Publishers

NIMEKUTA PICHA ZA UTUPU ZA GIRLFRIEND WANGU KWENYE SIMU YAKE..USHAURI PLEASE

$
0
0
Jamani Wapendwa Valentines imenikalia Pabaya leo yaani, My girl kaja kulala kwangu ili leo tusherekee wote hii siku kuna mahali tunaenda out of Town, ila sasa asubuhi ya leo wakati tunajiandaa nikachukua simu yake nikawa nampiga picha alivyopendeza baada ya kuvaaa sasa katika kuziangalia zile picha nikakutana na picha zingine za utupu alizopiga like one week ago, Sasa najiuliza hizo picha alipiga kwa ajili ya nani je alimtumia mtu maana kama ni mimi hakunitumia, nimemuuliza anasema alijipiga kujifurahisha, yaani hapa niko nae ila kama simwamini tena jamani naombeni ushauri.
By Lewis

MASANJA"SIKUWA NA UWEZO WA KUNUNUA HATA CHIPS KAVU-NAMSHUKURU MAREHEMU KANUMBA"

$
0
0
Masanja Mkandamizaji si jina geni masikioni mwa watu wengi  kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu watazamaji pale anapoonekana katika runinga na Kundi la Original Comedy.

Licha ya kufika hapo alipo sasa, anakiri wazi kuwa amepitia katika maisha magumu hususani wakati alipoamua kuanza maisha binafsi ya kujitegemea baada ya kutoka nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi.



Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake alimuomba amtafutie chumba ili ajitegemea na kuanza maisha binafsi kama kijana . Nilimwambia dada anitafutie chumba na alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia kama nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya Tabata Aroma na nilitakiwa kulipa kodi ya TSh. 5,000 kwa mwezi, anasema Masanja. Anakiri wazi kuwa changamoto katika maisha ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa kwani licha ya kuwa katika hali ngumu

Hakukata tamaa bali alizidi kujituma kwa nguvu zake zote. Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata hata hiyo hela ya kodi kwahiyo ilikuwa inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda unapofikia wakati kulipa kodi. Yaani hiyo TSh. 5,000 kuipata ilikuwa shughuli maana ilikuwa ikifika karibu na mwisho wa mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo ili mama mwenye nyumba ajue nimesafiri,anasema. Anasema alianza kwa kulala chini mpaka siku alipofanikiwa kupata fedha kidogo iliyomuwezesha kununua godoro la sufi jambo ambalo anajivunia nalo kwani aliweza kununua kwa jasho lake.

Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau marehemu Steven Kanumba pamoja na mtu mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na mchango wao uliosaidizi kumfikisha hapo alipo sasa.

Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa anakuja kunichukua kule Tabata tunaenda kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia pesa kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha yalikuwa magumu. Wakati naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata ya kununua chipsi kavu lakini siku moja nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki moja sikuamini macho yangu, kwa mara ya kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa nikitamani mlo huo nililazimika kusaidia kumenya viazi kwa washikaji” alieleza Masanja.

Sambamba na uchekeshaji Masanja pia amejiingiza katika shughuli za kumtukuza Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya vizuri pia katika uimbaji wa nyimbo za injili na kesho Jumapili atazindua albamu yake ya pili ya muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini ya jua.

-Habari kwa hisani ya mwandishi John Minja-

AKINA DADA WANAOJIONA WAZURI HII INAWAHUSU

$
0
0
Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri na
mrembo,usidhani utatetemesha kila
Mwanaume,kuna wanaume na akili
zao kichwani,urembo wako
hauwasumbui,kama bichwa lako ni
kanyaboya,uzuri wako hausaidii
kitu,na utashangaa no one is paying
attention,watu utakaowapata ni
walewale kanyaboya wenzako,na
hawana futuretabaki unaliwa bure
kila siku unatoa macho.
Ukipata mwanaume anakupenda
unaanza drama zako na kupiga watu
danadana,madai yako hujali na
unadhani hata akiondoka utapata
mwingine kisa wewe ni mzuri,la
hasha! Mwanaume akijitoa mhanga
kukupenda kwa uzuri wako
mheshimu,maana viumbe wa kike
wakiwa wazuri ni shida na matatizo
hakuna mtu anataka,sasa
ukimwongezea na drama pamoja na
yeye kujigeuza mpalestina kwako
utajikuta umeolewa na kioo cha
chumbani kwako,maana hicho ndo
kinakudanganya sana kwamba we ni
mrembo,Watch out,drama zina
mwisho,leo unacheza na mioyo ya
watu unajiona we kifaa,usidhani
wanaume hawaumii,tunaumia sema
hatusemi tu,machozi yetu kama ya
samaki,tunalia ndani kwa ndani

ANGALIA NAFASI MPYA ZA KAZI CRDB

$
0
0
Senior Web Officer

Company:CRDB 
POSITION DESCRIPTION:
BACKGROUND
CRDB Bank PLC is the largest bank in Tanzania in terms of Total Assets with a network of over 100 branches throughout Tanzania. Established on I st July 1996. It is owned by more than 11.000 shareholders and is one of the fastest growing banks in the country offering a wide range of microfinance, agent banking, retail, SME and corporate banking services. Additional information about the bank can be obtained from our website http://www.crdbbank.com CRDB Bank Plc is urgently looking for suitable persons to fill vacant positions that exist in the Department of Marketing Research & Customer Service at the Head Office.
SUMMARY OF MAIN RESPONSIBILITIES:
Develop, maintain and update the bank's website. 
This includes production of web contents in audio, video and written forms. 
Maintain a consistent look and feel through all web properties. 
Copy, edit and proofread all web contents. 
Crafting site promotions, email newsletters and online outreach campaigns. 
Manage all online marketing and communications. 
Prepare and upload weekly press releases of products and services. 
Assure web-based information is achieved for future needs and references Manage the mobile commerce platforms. 
Prepare and upload features stories necessary for brand enhancement Effectively manage the CRDB Bank social media sites to increase visits and followers Ensure domain registration and hosting is current.
ACADEMIC QUALIFICATIONS
Bachelors in Science, communication, public relations, technical writing or related field. Having excellent command over English and Kiswahili (knowledge of French will be an added advantage).An additional qualification in IT would be an added advantage
EXPERIENCE
The candidate should have minimum 5 years' experience in communications/marketing public relations, of which at least 2 years must be as a Content/Campaign Writer and related with Web site development or maintenance of an organization.
Having experience of handling social media, applications from different industries will also be considered but preference will be on for candidates from Banking Industry.
GENERAL PROFILE AND ATTRIBUTE FOR ALL APPLICANTS
Proficiency in MS Word, Excel, Outlook and Adobe Photoshop skills. 
Experience with website analysis tools (Google analytics, MOZ) Exceptional professional communication skills to create content that will motivate users to access the site. 
Have combination of technical knowledge and skills in written and graphic communication. 
Ability to work under pressure Self motivated and good team player Good planning and organization skills
-----------------------------------
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Interested candidates who meet the above criteria should submit an Application Letter accompanied with copies of academic transcript, certificates and with a detailed up to date CV with two work related referees addressed to the Director of Human Resources. 
Only applicants shortlisted for interview will be notified. 
E-mailed & faxed applications will not be accepted. 
Director of Human Resources CRDB Bank Plc 
P.O.Box 268 
DAR ES SALAAAM
Deadline:20th Feb 2014
Source:The Guardian, 10th February 2014

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&


Sales Manager
Company:CRDB 
POSITION DESCRIPTION:
BACKGROUND
CRDB Bank PLC is the largest bank in Tanzania in terms of Total Assets with a network of over 100 branches throughout Tanzania. Established on I st July 1996. It is owned by more than 11.000 shareholders and is one of the fastest growing banks in the country offering a wide range of microfinance, agent banking, retail, SME and corporate banking services. Additional information about the bank can be obtained from our website http://www.crdbbank.com CRDB Bank Plc is urgently looking for suitable persons to fill vacant positions that exist in the Department of Marketing Research & Customer Service at the Head Office.
SUMMARY OF MAIN RESPONSIBILITIES:
Collaborate with Senior Manager Personal Banking to develop and implement retail sales strategies to improve market share in all products. 
Identifying and analyzing lead generation and cross selling/up selling opportunities. 
Lead the team in product/services sales while promoting sales culture through sales campaigns, training and motivation. 
Create and executes strategies to promote sales through branches. 
Formulate retail sales policies and procedures. 
Initiate sales campaign to increase retail sales. 
Motivate and engage the sales team initiatives to bring new business through incentivisation scheme. 
Generate proposals and other communication mediums to be used by the team directly to customers. 
Provide exceptional level of client service and promote sales culture through coaching, guidance and staff motivation. 
Participates in community affairs to increase the Bank's visibility and enhance new and existing business opportunities Analyzing the market, competitors and recommend where changes need to be made. 
Monitor analyze and report individuals and branch sales performance on monthly basis.
ACADEMIC QUALIFICATIONS
Bachelors Degree or its equivalent in Business Administration with biases in Marketing and Sales Possession of postgraduate or masters degree will be an added advantage. 
The candidate should have minimum 7 years' experience in the field of Direct Sales. 
Working in any client facing sales driven industry as a' supervisor or manager for at least three (3) years will have added advantage,
GENERAL PROFILE AND ATTRIBUTE FOR ALL APPLICANTS
Demonstrated aptitude and desire for sales achievement, strong interpersonal skills in a team environment . 
Ability to motivate staff to achieve a high level of performance. 
Excellent communication (verbal and written) and people skills. 
Creative problem-solving skills, self starter, ability to work independently. 
Persuasive sales and negotiating skills. 
Confident with effective presentation skills. 
Understanding of basic banking products is an added advantage
------------------------------------
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Interested candidates who meet the above criteria should submit an Application Letter accompanied with copies of academic transcript, certificates and with a detailed up to date CV with two work related referees addressed to the Director of Human Resources. Only applicants shortlisted for interview will be notified.
E-mailed & faxed applications will not be accepted.
Director of Human Resources
CRDB Bank Plc
P.O.Box 268
DAR ES SALAAAM
Deadline:20th Feb 2014
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&


Manager Call Centre
CRDB 
POSITION DESCRIPTION:
BACKGROUND
CRDB Bank PLC is the largest bank in Tanzania in terms of Total Assets with a network of over 100 branches throughout Tanzania. Established on I st July 1996. It is owned by more than 11.000 shareholders and is one of the fastest growing banks in the country offering a wide range of microfinance, agent banking, retail, SME and corporate banking services. Additional information about the bank can be obtained from our website http://www.crdbbank.com CRDB Bank Plc is urgently looking for suitable persons to fill vacant positions that exist in the Department of Marketing Research & Customer Service at the Head Office.
SUMMARY OF MAIN RESPONSIBILITIES - MANAGER CALL CENTRE
Driving the strategy for a full-fledged multilingual call center both inbound and outbound with the view of creating a virtual customer experience for the customers of the Bank. 
Prepare annual budget plan for the Centre to ensure that all activities and expenses are controlled within the agreed limits. 
Manage lead and motivate staff to achieve the set performance targets for the Centre within the specified time and ensure the operational level of excellence in maintained. 
Ability to initiate,launch and manage various call campaigns as per the requirement of the Business units Manage Service Level Agreement (SLA) with suppliers of key systems to the call center to ensure that quality services are offered as per expected level of performance and standards. 
Manage Customer Response Time with the respective business units on customer complaints queries to ensure that solutions are availed to customers in a timely manner as per Banks standard. 
Monitor and control optimal staffing levels and devise or create a conducive working environment at the centre that will foster quick delivery of solutions to customers' problems and service innovations to ensure there is smooth delivery of service to customers in line with the overall business strategies. 
To carry out any other related duties as may be assigned by the relevant Director.
ACADEMIC QUALIFICATIONS
Degree/Advanced Diploma or its equivalent in Business Administration from a recognized Training Institution Possession of a Master's degree will be an added advantage.
EXPERIENCE
The candidate should have minimum 5 years' experience in a Call center of which at least 3 years must be as a Call center Supervisor /Manager. 
Having experience of both Inbound and outbound call operations and at least managed a call center team size of 50 or above. 
The call center may be of any industry telecom, insurance, banks, utilities etc Applications from call center experts from different industry will also be considered .
-------------------------------------
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Interested candidates who meet the above criteria should submit an Application Letter accompanied with copies of academic transcript, certificates and with a detailed up to date CV with two work related referees addressed to theDirector of Human Resources.
Only applicants shortlisted for interview will be notified. 
E-mailed & faxed applications will not be accepted.
Director of Human Resources
CRDB Bank Plc
P.O.Box 268
DAR ES SALAAAM
Deadline:1st March 2014
Source:The Guardian, 10th February 2014

DIAMOND PLATINUM AFANYA JEURI KUBWA SANA KWA WATU WANAOMFUATA

$
0
0
Wote tunajua kwamba diamond platnumz kwasasa anafanya kazi na coca-cola kama brand ambassador na Vodacom Tanzania pia. lakini chini ya kapeti hauwezi kuamini deals diamond anazozipata kila kukicha na kuzipiga chini. Diamond alifunguka hivi kuhusiana na hilo.

“Before mimi, wapo wasanii kibao walikua wakitumiwa na makampuni ya kibiashara,lakini maslahi ya kiuchumi hayakua makubwa kutokana na wasanii wenyewe kutojipa thamani. Ukiniona mie nimekubali kufanya kazi na makampuni ya kibiashara ujue lazima akaunti yangu imekaa vizuri sana. Naijua thamani yangu vizuri,i’ve worked hard kufika hapa nilipo and no one should take me for granted. Nashukuru mungu ubishi wangu umenisaidia nalipwa vizuri kama wasanii wengine barani afrika wanavyolipwa,though nimekua (Usisahu kulike page yetu mpya kwa kuclick HAPA)vilevile na lose sana,mfano hivi karibuni kuna kampuni moja ya simu ilinipa deal ya $200,000 but i turned it down coz walishidwa kufikia dau langu,also there was a deal na kampuni moja ya unga walitaka kunipa ubalozi , i told them to pay me $120,000 wakasuasua mpaka ilipotoka my number 1 wakarudi tena nikawaambia thamani yangu imepanda waongeze mtonyo na wakishidwa wafanye kazi na msanii mwingine kwa bajeti hiyo,haikua kwa ubaya it was a pure business. Ukweli ninastahili kulipwa fedha ninazowaambia kwasababu huwa nazifanya vizuri kazi zangu zote kibalozi na ndio maana coca cola wananitreat vizuri”.

LE MUTUZ LIVE TSRAIGHT TALK!!:- KWA WALE LE MBURULAZZ MSIOWEZA KUTUMIA AKILI

$
0
0
@ LE MUTUZ LIVE TSRAIGHT TALK!!:- KWA WALE LE MBURULAZZ MSIOWEZA KUTUMIA AKILI SAWA SAWA NI KWAMBA HAYA MASHATI KAMA KWENYE HII PICHA NINAYO MENGI SANA KUANZIA YA MIKONO MIFUPI MPAKA MIREFU, SIO KWAMBA NINA SHATI MOJA KAMA MBURULAZZZ WENGI MNAVYODHANI NA NINAFANYA MAKUSUDI KUYAVAA KILA SIKU KWA NIA MOJA TU, NAYO NI KUYATANGAZA CAUSE UWE UNAPENDA AU HUPENDI MIMI NOW NI A BIG CELEBRITY AND I KNOW IT, SO!
- KESHO NINAONDOKA KWENDA WEST AFRICA PAMOJA NA MENGINE NIA NA MADHUMUNI YA SAFARI YANGU NI BIASHARA SO NAKWENDA KUTAFUTA BETTER MATERIALS KWA AJILI YA KUYABORESHA HAYA MASHATI YAWE NA GREAT SHAPE ZAIDI KWA SABABU TAYARI NIMESHAFUNGUA BIASHARA YA LINE YA HAYA MASHATI, NIKIRUDI NDIO NITAANZA RASMI KUYAINGIZA KWENYE THE BIG MARKET, AKILI NI MALI NA AKILI NI NYWELE, MIAKA 30 YA KUISHI KWA WAZUNGU WALINIFUNDISHA ONE THING MAANA YA UBEPARI NI KUTUMIA KILA KIZURI CHAKO NA HASA KIPAJI KUTENGENEZA MAHERA SIO KUTENGENEZA UJINGA! UJINGA! NILIPO VAA SHATI LA KWANZA LA AINA HII WANANCHI WENGI WALINIPIGIA NA KUNI-SMS KWAMBA WANAYATAKA SO NIKAAMUA KU-CREAT BIASHARA ON IT, ONE OF THIS DAYS UTAKUJA KUNIELEWA VIZURI KWAMBA EVERYTHING ARROUND ME WORKS FOR ME ON KUTAFUTA MAHERA NDIO UTAAMKA USINGIZINI, I PLAY!! I JOKE!! I BLOG! I POLITICS!! I MABEBEZ!! LAKINI ALWAYS MY GOAL HUWA HOW I CAN MAKE MONEY OUT OF ANYTHING AROUND ME!! SO KABLA HUJAFUNGUA MDOMO WAKO ON ME AND MY LIFE TAFAKARI KWANZA KAMA UNAJUA UNACHOKISEMA!!OK!! HA! HA! HA! JAMANI JIONI NJEMAZZZ!! - LE MUTUZ
Source:Wiliam Macela Blog

WIMBO WA DIAMOND WASHIKA NUMBER MOJA KWENYE RADIO KUBWA NAIGERIA..

$
0
0
Diamond na Wimbo wake aliyo mshirikisha Davido Number 1 Remix ni SHIDA huko Nigeria..Washika Number moja kwenye chat za Muziki leo siku ya Valentines Day kwenye Radio inayoitwa BEAT FM 99.9(check hapo chini:

WIMBO MPYA WA MAREHEMU ALBART MANGWEA HUU HAPA UMEACHIWA NA MAMA YAKE MZAZI LEO

$
0
0
Bonyeza Kusikiliza ama Kudownload..Bonge la Wimbo

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA JUMA NATURE FEAT. LADY JAY DEE

LEMA CHUPUCHUPU KUTIWA NGUVUMI BAADA YA KUANDIKA UJUMBE WA KUMPONDA JK

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema jana alinusurika kukamatwa na makachero wa Jeshi la Polisi ili kuhojiwa kutokana na ujumbe wake aliouposti kwenye mtandao wa kijamii akiandika: “Rais Kikwete mbona umeamua kuliangamiza taifa.”

Akizungumza na gazeti hili jana akiwa njiani kuelekea Dodoma kushiriki Kikao cha Bunge la Katiba, Lema alisema maafisa wawili wa polisi walimfuata katika hoteli aliyofikia Dar es Salaam kwa lengo la kumkamata na kumpeleka makao makuu ya polisi.

Lema alisema maafisa hao, ambao walikuwa wanatumia gari dogo, baada ya kufika hotelini hapo, waliomba aitwe na aliposhuka walimtaka kuandamana nao, hadi makao makuu ya polisi kwa mahojiano.

“Niliwauliza nikaandeke maelezo juu ya nini, walijibu kifupi wao ni chombo cha dola na walisema wametumwa na viongozi wa juu wa polisi na hawakuwa tayari kutaja tuhuma zangu,” alisema Lema.

Alisema baada ya polisi hao kusisitiza kutaka kumchukua, aliwaomba aende chumbani kujiandaa kabla ya kuwasiliana na viongozi wa chama chake na familia yake.

“Niliposhuka chini sikuwakuta na ndipo nikashauriana na viongozi wa chama hicho na kuamua kuondoka jana mchana Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Hata hivyo, alisema Chadema leo wanatarajia kutoa tamko juu ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wanachama wa CCM kuondoa unyonge dhidi ya wapinzani hasa pale wanapodaiwa kupigwa.

MBOWE, MBATIA WAFURA KUTOKANA NA KAULI YA KIKWETE

$
0
0
Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka wanachama, wadau na makada wa CCM, kuondokana na unyonge, imepokewa kwa hisia tofauti huku ikielezwa kuwa ni ya vitisho.

Juzi, wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala alisema: “Ni wakati wa kuacha unyonge na uvumilivu una kikomo chake.”

Alisema CCM inaingia kwenye uchaguzi huku ikishindana na wagomvi: “...Ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wao kufanya siasa,” alisema Kikwete bila kutaja jina la chama chochote cha siasa.

Alisema amechoshwa na vitendo vya ugomvi huku akitolea mfano wa tukio la Kahama mkoani Shinyanga ambako kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi na mwingine kumwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, mkoani Tabora.

Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete akisema: “Nimeipokea kwa mshtuko na ninawataka wafuasi wa chama changu kuwa watulivu na kuchukua tahadhari kubwa.”

“Nilichokifanya ni kuwaagiza wafuasi wa Chadema kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutolipiza kisasi ili kuhakikisha kwamba hakuna damu ya Mtanzania itakayomwagika Kalenga,” alisema.

Hatua ya Rais Kikwete, imekuja baada ya CCM kumtangaza, Godfrey Mgimwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga. Mgimwa ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha, hayati Dk William Mgimwa aliyefariki mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.

Mgombea huyo atachuana na mgombea wa Chadema, Grace Tengega.

Jana, Mbowe alisema ingawa Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM, alitakiwa kufahamu kwamba ni kiongozi wa nchi na ni Amiri Jeshi Mkuu ambaye vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo chini yake.

“Anapotoa kauli nzito kama hiyo, inatakiwa afahamu kwamba yeye si Mwenyekiti wa CCM tu, bali ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu, hakustahili kutoa kauli kama hiyo inayoweza kuamsha hisia,” alisema Mbowe.

Alisema kauli zake za kiitikadi za kupendelea chama chake wakati akifahamu kuwa yeye ni kiongozi wa Watanzania wote, zinawafanya wananchi wagawanyike kwa misingi ya vyama.

“Rais Kikwete anadai kwamba mtu wao alimwagiwa tindikali na mwingine kutolewa macho kwa bisibisi, lakini hazungumzii viongozi na wanachama wa Chadema waliouawa kwa kupigwa risasi na wengine kwa mabomu. Anasema hayo huku akifahamu fika kwamba kuna vyombo vya dola na Mahakama ambavyo vinashughulikia matukio hayo.”

DAVIDO AWABEEP WATU ATUPIA PICHA INSTAGRAM AKIMKISS DEMU NA KUIDELETE MUDA HUO HUO

$
0
0
Davido himself shared the photo on his instagram page but deleted it almost immediately. Anyone know who the girl is?

MCHAWI WA UNGO ADONDOKA, AGEUKA KUKU

$
0
0
Stori: Joseph Ngilisho, Arusha
HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji  la  Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika  kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo, Uwazi limeona mengi.

Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.

Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.

“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo  mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.

Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images