Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Tundu Lissu ‘anusa’ bao la mkono Singida Mashariki

$
0
0
Mgombea ubunge wa jimbo la Singida mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu  Antiphas Mughwai Lissu, amesema kwamba anahofia uchaguzi mkuu  hautakuwa huru na wa haki akidai kwamba Jeshi la Polisi limeandaliwa kuhakikisha yeye hatangazwi kuwa mshindi.

Lissu alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani humo ambapo alibainisha kuwa amepata taarifa kupitia njia ya simu kutoka kwa meneja  wa mkoa wa benki moja mjini hapa na askari polisi wawili, kwamba jeshi la polisi limeandaa nguvu kubwa kupindua maamuzi ya wapiga kura, ili mgombea wa CCM atangazwe mshindi

Tundu  Lissu ambaye ni Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, alisema kwa nyakati tofauti, alipigiwa simu na askari polisi wawili akiwemo wa FFU, na kumpa taarifa ile ile aliyopewa na meneja wa benki.

Alisema askari hao walimwambia kuwa jeshi la polisi litatumia magari matatu ya dareya (yanayotumika kumwaga maji ya kuwasha) na kundi kubwa la askari na kwamba wameagizwa na viongozi wao,wahakikishe liwalo na liwe, yeye (Tundu) hatangazwi kushinda ubunge.

Mgombea huyo alisema kwa akili ya kawaida, jeshi la polisi halipaswi kutuma nguvu kubwa jimbo la Singida mashariki ambalo toka kampeni zianze, hapajatokea tukio au dalili za uvunjivu wa amani.

Katika hatua nyingine, Tundu Lissu ameahidi kwamba endapo atashindwa kihalali, atakubaliana na matokeo na hatakuwa na kinyongo chochote.Lakini endapo atashindwa kwa mbinu chafu, hatakubaliana na matokeo hayo machafu.

Naye  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Sedoyeka, alisema wamemtaka Lissu kwa kuwa ni mwanasheria, athibitishe tuhuma zake hizo, ndipo jeshi la polisi liweze kuchukua hatua stahiki.

Katika jimbo hilo  Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemsimamisha  Bw.Jonathan Njau kupambana na Tundu Lissu katika uchaguzi huu.
Mpekuzi blog

Lowassa Atoa Onyo kwa NEC na Polisi Mchana Huu......Sumaye Asema CCM Wamejipanga Kuwanunua Mawakala wa Chadema

$
0
0
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ameionya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jeshi la Polisi kuchochea vurugu.

Onyo la Lowassa limekuja ikiwa imebaki siku moja kabla ya Watanzania kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa rais, ubunge na madiwani.

Akihutubia wakazi wa Ifakara Jimbo la Kilombero, Morogoro leo mchana katika Uwanja wa Shule ya Jagwani, Lowassa amesema “polisi waache kuwafuatafuata vijana wetu na kuwapiga.”

Lowassa amesema, “Tume ya Taifa ya Uchaguzi wanapaswa kutambua kwamba, uchaguzi huu ni muhimu. Watu wamejitolea kujiandikisha na kwenda kupiga kura ifika Jumapili, watu hawa wana matumaini. Tume itende haki.”

Mbali na onyo hilo, Lowassa amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, ataanza kutatua changamoto za sekta ya elimu kwa kutoa elimu bure kwanzia Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu.

Mbali na elimu, kipaumbele changu cha pili ni kilimo. Nitahakikisha tunakuwa na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji. Mkulima atakuwa na haki zake. Serikali yangu itafuta ushuru wa mazao yote. Wakulima watauza mazao popote watakapotaka duniani,” amesema Lowassa.

Kuhusu maslahi ya wafanyabiashara ndogondogo na wenyeviti wa vijiji amesema “mimi ni rafiki wa bodaboda, mama lishe na machinga. Nikiingia madarakani nitaanzisha benki maalum kwa ajili ya makundi haya. Pia nitawalipa mishahara wenyeviti wa vijiji,” amesema Lowassa.

Lowassa ameahidi kutatua kero za Jimbo la Kilombero ambalo linawakilishwa na mgombea Peter Lijualikali kwa tiketi ya Chadema.

Kero zinazowakabili wananchi katika jimbo hili ni kutozwa ushuru kwa wakulima wa mpunga, tatizo la maji, watu wa Sanje kudhulumiwa ardhi yao, kutokamilika kwa daraja linalounganisha Mahenge, Kilombero na Malindi na kivuko kilichopo muda wowote kinaweza kuzama,” amesema Lijualikali.

Aidha, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amewataka wananchi kuwahi katika vituo vya kupigia kura huku kila mpiga kura kubeba kalamu yake badala ya kutegemea kalamu za maofisa wa NEC.

Tuwahi katika vituo vya kupiga kura alfajir. Kazi ya kwanza Jumapili ni kupiga kura, kila mtu aende na kalamu yake. Mtu ambaye hajui kusoma na kuandika amchukue mwenzake anayemwamini,” amesema Sumaye.

Mbali na wito huo, Sumaye amewataka mawakala wa watakaolinda kura za vyama vinavyounda Ukawa kutohadaika na rushwa itakayotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kuna dalili kwamba CCM wanataka kuwanunua mawakala wetu. Kweli unakubali kupewa Sh. 20,000, 30,000 au 50,000 halafu mtoto wako atesekeke miaka mitano kwa kukosa dawa? Wakala wetu siku hiyo unapokwenda kwenye kituo chako cha kazi, uwe umekula nyumbani. Usiende kudoea chai inayoletwa humo, huwezi kufa kwa njaa kwa siku moja,” amesema Sumaye.

Tabia za KAJALA Mtaan Zamliza Mumewe Ambaye Yuko Jela Akitumijkia Kifungo

$
0
0
Baada ya kuenea kwa madai kuwa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amepangishiwa bonge la mjengo na kigogo mmoja (jina kapuni), mumewe Faraji Agustino anadaiwa kulizwa na vitendo vya mkewe huyo vinavyomuumiza akiwa jela.
Mbali na kigogo huyo, pia mwanadada huyo anadaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Abbott Charles ‘Quick Rocka’, habari iliyoripotiwa na gazeti hili toleo lililopita ambayo nayo wambeya walimfikishia na kumfanya ajisikie vibaya.

Habari kutoka kwa mmoja wa ndugu wa Faraji ambaye amekuwa akimtembelea jela kumjulia hali zilidai kwamba, Kajala amekuwa akimliza mwenza wake huyo kutokana na maneno ambayo amekuwa akipelekewa kuhusu tabia zake za sasa huko mtaani.

“Kuna siku Kajala alikwenda kumtembelea kule gerezani, Faraji akajisikia faraja sana na kuona kumbe mkewe bado anampenda na kumjali. Siku chache baadaye akapata taarifa kuwa, mkewe huyo anatoka na yule mwanamuziki sijui wanamuita Quick Rocka aliumia sana na kujikuta akitokwa na machozi,” alisema mtoa habari huyo.
Quick Rocka.
Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Kajala na kumuuliza juu ya madai hayo, alipopatikana alisema: “Kama mwezi mmoja hivi kabla ya kwenda mikoani kwenye hizi harakati (kampeni) za CCM (Chama Cha Mapinduzi) nilikwenda kumuona na kumjulia hali, yupo vizuri tu na wala hamna shida yoyote. Hayo ni maneno ya watu tu.”


Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Gereza la Segerea hadi leo.

Katika msala huo uliomweka Faraji gerezani, Kajala alihukumiwa miaka mitano kwenda jela na mumewe huyo lakini mwanadada huyo alilipiwa faini ya Sh. milioni 13 na Wema Isaac Sepetu.

John Pombe Magufuli Amaliza Kazi Aliyotumwa na CCM, Takwimu Zaonyesha Amefanya Mikutano Mingi Kuliko Mpizani Wake Lowassa

$
0
0
MGOMBEA Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, (pichani) amemaliza kazi huku akitarajia kumwaga sera za mwisho katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam kabla ya kesho kuhitimisha fainali kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Magufuli, ambaye ameongeza kasi na kubadili mitazamo ya watu kadiri siku za kampeni zilivyokuwa zikisonga, anaelezwa na wachambuzi wa masuala ya siasa kwamba kwa taswira iliyopo, ana alama nyingi za ushindi ikilinganishwa na wagombea wengine, hususan Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa.

Takwimu zinaonesha kwamba, hadi gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni jana, Magufuli alikuwa ametembea umbali wa kilometa 44,467 katika majimbo 247 ndani ya mikoa 30, ambapo ametumia gari na boti wakati mgombea wa Chadema ametembea kilometa zisizozidi 3,000 kwa gari, ametembelea majimbo 137 yaliyo kwenye mikoa 25.

Aidha, takwimu zinaonesha kwamba, Magufuli amefanya mikutano rasmi 265 na mikutano midogo 908 ikilinganishwa na Lowassa ambaye amehutubia mikutano mikubwa 103 tu tangu kuanza kwa kampeni wakati ambapo idadi ya mikutano isiyo rasmi ambayo haipo kwenye ratiba ni michache mno kwa vile amekuwa akitumia helikopta, hivyo kukosa fursa ya kusalimiana na wananchi.

Takwimu hizo zinaonesha kwamba, Magufuli amehutubia kwa saa 311 ukiwa ni wastani wa dakika 45 kwa kila mkutano mkubwa wa hadhara, wakati Lowassa amehutubia kwa saa 26, sawa na dakika 8.93 kwa kila mkutano rasmi.

Rekodi zinaonesha kwamba, Dk. Magufuli anakadiriwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 12 ana kwa ana na takriban milioni 36 kwa njia za mawasiliano ya redio, magazeti, televisheni na mitandao ya kijamii, wakati mgombea wa Ukawa amewafikia wananchi wasiozidi milioni tano ana kwa ana katika mikutano ya hadhara michache aliyofanya na amewafikia wananchi wasiozidi milioni 11 kwa njia za televisheni, magazeti, redio na mitandao ya kijamii.

CCM ina wanachama wanaokadiriwa kufikia milioni 8 nchi nzima, wakati Ukawa wana wanachama milioni 4, na ikiwa wanachama wa

CCM wanaoamini katika Lowassa watampigia kura, chama hicho tawala kinaweza kupoteza kura 800,000 za wanachama wake, japokuwa historia inaonesha kwamba wanaCCM huwa wagumu kumchagua kada mwenzao pindi anapohama chama kama ilivyokuwa kwa Augustine Mrema mwaka 1995.

Aidha, wachambuzi wanasema, ikiwa wanachama wa Ukawa wanaoamini katika Profesa Ibrahim Lipumba, Dk. Wilbrod Slaa, Mchungaji Christopher Mtikila, Dk. Emmanuel Makaidi (marehemu) na Zitto Kabwe wataamua kuchagua uadilifu wa Magufuli, CCM inakadiriwa kuvuna kura milioni moja na nusu kutoka upinzani.

Wakati CCM itakamilisha kampeni zake kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Chadema (Ukawa) watakamilisha kampeni zao kwenye Viwanja vya Jangwani wakati ACTWazalendo watafunga kazi kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Lowassa Azizima Mikumi. Prof Jay Ubunge Tayari...Kesho DAR Kufunikwa na Mafuriko ya Lowassa

$
0
0

Leo Lowassa amefanya mikutano mitano. Mlimba, Ifakara, Mikumu/Ruaha, Chalinze na Kibaha. Pote Lowasaa ametikisa kwa nafuriko ya balaa kama iilivyo kawaida yake. Amehitimisha kampeni za mikoani na kesho atazizima jijini dsm kwa mkutano wa kihistoria ambao watu nusu milioni wanakadiriwa kuhudhuria. Picha zifuatazo ni Mikumi kwa Prof Jay.
Tukutane kesho uwanja wa nyumbani Jangwani ambapo leo Magufuli ameshindwa kufikia rekodi zetu tuliyoweka wakat wa Ufunguzi wa Kampeni pamoja na mabasi zaidi ya 50 ya kampuni ya UDA kufanya kazi ya ziada kupita jiji lote kusomba watu. Kesho tunawapoteza kabisa

Uchumba wa Wastara Wavunjika...Wastara Achoka na Usaliti wa Bond

$
0
0
Uchumba wa mastaa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma na Bond Bin Suleiman ambao ulikuwa umepamba moto huku hivi karibuni ikidaiwa wataoana baada ya uchaguzi, umevunjika baada ya Wastara kusalitiwa.

Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, wawili hao walikuwa wakienda vizuri lakini hivi karibuni Bond alibainika kumsaliti mwezake kwa kuwa na mwanamke mwingine aliyezaa naye.

Uchumba wao ulikuwa unaenda vizuri tu lakini mara kwa mara Bond amekuwa akimliza mwenzake kwa kuchepuka. Wastara akawa anaziba masikio kwa kuwa anampenda.
“Kuna wakati Bond alidaiwa kumpa mimba mwanamke aliyefahamika kwa jina la Grace, Wastara akafunika, sasa naona amechoka maana inadaiwa Bond ana mtoto mdogo aliyezaa na mwanamke mwingine.

Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwandishi wetu alimwendea hewani Wastara ambaye alikiri kusikia habari za Bond kuwa na mtoto ila akasema anafuatilia na akijua ukweli atalazimika kujiweka pembeni.

Mh! Kama hizo habari na nyinyi zimewafikia basi, maana mimi nilizisikia kijuu juu nikaona nitazifanyia kazi ila kiukweli kama ni hivyo, najiweka pembeni. Nimekuwa nikimpigia simu lakini simpati kwa takriban wiki nzima sasa, sijui shida iko wapi,” alisema Wastara.

Source:Global Publishers

Taarifa Sahihi Baada ya Taarifa ya Kuwa Dr Mary Nagu Amekamatwa na Masanduku Kumi ya Kupiga Kura yakiwa na Karatasi za Kura zilizokwisha Pigwa

$
0
0

Taarifa ya awali ya uzushi iliyosambaa Mtandaoni:

Wakuu kwa habari za hivi punde kutoka Hanang ni kuwa Dr Mary Nagu amekamatwa na maboksi kumi ya kura yakiwa yashapigiwa kura tayari huko Hanang. Sasa hivi amekamatwa yupo Polisi,taarifa zaidi zinakuja.

TAARIFA SAHIHI:

JamiiForums imemtafuta RPC wa Mkoa wa Manyara, Christropher Fuime na kufahamishwa kuwa taarifa hizi ni za uwongo na zenye malengo ya kisiasa.

Masanduku yote ya kupigia kura yapo mikononi mwa mamlaka husika na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na sanduku la kura wala wao kama Polisi hawana taarifa toka jimbo lolote mkoani humo kuhusiana na hili.

Source:JF


Note: Epuka Kusambaza Taarifa zisozokuwa na uhakika wakati huu wa Uchaguzi Mkuu...

Hotuba Ya Mgombea Urais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Tiketi Chadema , Edward Ngoyai LOWASSA - Oktoba 23, 2015

$
0
0
Ndugu watanzania wenzangu.
Imebaki siku moja tu kabla hatujapiga kura katika Uchaguzi Mkuu hapo tarehe 25 mwezi huu.

Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka na rehema zake kwa kutufikisha hapa hii leo tukiwa na afya njema. Katika kipindi hiki cha kampeni tumewapoteza, kwa masikitiko makubwa, ndugu zetu kadhaa ambao walikuwa wagombea Ubunge na udiwani na wengine waliyokuwa wakishiriki katika mchakato huu wa uchaguzi kwa namna mbalimbali.
 
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani, Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mzee wetu Dk. Emmanuel Makaidi, mawaziri Mama Celina Kombani na Dk. Abdallah Kigoda, vijana wetu Mohamed Mtoi na Deo Filikunjombe, Mchungaji Christopher Mtikila na Estom Mallah ambao wote walikuwa wagombea ubunge. Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi. Amen.
 
Katika kipindi cha kampeni nimefika katika kila kona ya nchi yetu, ninatoa shukrani za dhati kwa mapokezi makubwa, mapenzi na ukarimu wa Watanzania kwangu, kwa msafara wangu na mgombea mwenza, Mheshimiwa Juma Haji Duni.

Aidha natoa shukrani zangu za pekee kwa wenyeviti wenza wa Ukawa, Freeman Mbowe, James Mbatia, Twaha Taslima na marehemu Dk. Emmanuel Makaidi kwa mchango wao mkubwa katika kuchochea mabadiliko na msaada wao kwangu wakati wa kampeni.
 
Pia namshukuru kwa dhati mzee wetu, Kingunge Ngombale Mwiru, Waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye, viongozi mbali mbali wa CHADEMA na UKAWA ambao kwa pamoja walijitoa kwa moyo wao wote kungoza harakati hizi za mabadiliko. Ahsanteni sana
 
Kwa namna ya pekee, pia nimshukuru mke wangu mpenzi, Regina Lowassa kwa upendo, msaada na mchango wake katika kuhamasisha Watanzania na hususan wanawake wakati wote wa kampeni. Ahsante sana Regina.
 
Ndugu Watanzania wenzangu
Katika ziara hizi, nimeshuhudia vuguvugu la mabadiliko, kiu na ari ya Watanzania kuyapokea mabadiliko hayo. Lakini pia nimejionea shida zinazowakabili wananchi hao.
 
Nimesikia na nyakati nyingine kujionea kilio chao cha kunyanyaswa na kunyimwa haki zao na watendaji wa serikali na baadhi ya vyombo vya dola.
 
Nimekisikia kilio chao cha umaskini, afya na elimu duni. Nimekisikia kilio kikubwa cha vijana kukosa ajira na matarajio ya kesho bora.
 
Nimesikia rai za Watanzania na ndoto zao za kupata maendeleo, maji safi, makazi bora na barabara madhubuti.
 
Nimesikia malalamiko ya wakulima na wafugaji kukosa maji na ardhi. Nimesikia kilio cha madaktari, wauguzi, walimu, askari na watumishi wa taasisi za umma kuhusu mazingira magumu ya kazi, kodi za juu na maslahi duni.
 
Nimesikia kilio cha wafanyabiashara wadogo wadogo kuhusu ugumu wa mazingira ya kufanyia shughuli zao, kodi kandamizi na kukosa mitaji.
 
Nimesikia kilio cha wanawake kuhusu haki zao na ushiriki wao mdogo katika shughuli za kiuchumi. Nimesikia kilio cha wazee na wastaafu wasio na bima ya afya, wanaolipwa pensheni isiyokidhi mahitaji yao na ugumu wa maisha yao uzeeni.
 
Nimesikia kilio cha Watanzania dhidi ya rushwa iliyokithiri na utawala dhaifu ulioshindwa kuondoa umaskini au kutetea haki za raia.
 
Jibu langu ni fupi. Nimeona, nimesikia, nimeelewa na nitatenda.
 
Uchaguzi wa mwisho wa wiki hii ndiyo utakaotupa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais mpya wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Ni uchaguzi muhimu na wa kihistoria kwetu sote.
 
Nawaomba nyote mliyojiandikisha mjitokeze kwa wingi kutimiza haki na wajibu wenu wa Kikatiba. Sehemu muhimu ya mabadiliko tunayodhamiria kuyaleta ni kujitokeza kupiga kura.

1. Ipo dhana potofu inayojengwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwamba wafuasi na wanachama wa vyama vyetu vinavyo unganishwa na UKAWA wataleta fujo wakati wa kupiga kura. Ni maneno ya kipuuzi.
 
• Hata hivyo nawaomba nyote muwe wastaarabu, muheshimu sheria zilizopo. Tukusanyike na kupiga kura kwa amani na utulivu.
 
• Katika kampeni zetu nchini kote hadi hivi sasa tumedhihirisha kwamba vyama vyetu vya upinzani na wanachama wake hatuvunji, hatujavunja na hatutavunja sheria.
 
• Hatuna sababu ya kufanya hivyo. Nia na dhamira yetu ni kushinda Uchaguzi huu na kuing’oa CCM madarakani.
 
2. Dhana na fikra zingine potofu zinazojengwa na uongozi wa CCM kwa nia ya kuwaogopesha Watanzania ni kwamba eti Watanzania wakichagua upinzani nchi itaingia kwenye machafuko. Wapuuzwe wenye fikra hizi wameshasahau hata historia ya hivi karibuni ya nchi tunazopakana nazo.
 
• Wote ni mashahidi kwamba chama cha UNIP cha Zambia kilipoondolewa madarakani kwa kura za ndugu zetu wa Zambia, hapakutokea fujo zozote Zambia. Ukweli ni kwamba Mzee wetu mpendwa Mzee Keneth Kaunda aliyekuwa anaongoza chama tawala wakati huo yuko Zambia na anaendelea kufurahia maisha yake wakati Wazambia wakipiga hatua katika maendeleo ya Taifa lao.
 
• Chama cha Malawi Congress Party pia kiling’olewa madarakani kwa kura za ndugu zetu wa Malawi. Malawi kwa miaka yote imeendelea kuwa tulivu.
 
• Chama cha KANU Kenya pia kiliondolewa madarakani mwaka 2002. Ukweli ni kwamba matatizo yaliyojitokeza Kenya miaka mitano baadaye hayakutokana na kuondolewa kwa KANU. Yalikuwa ni madai yaliyotokana na taarifa za kuwepo kwa udanganyifu katika matokeo ya uchaguzi mkuu. La kujifunza hapa ni kwamba udanganyifu uliwaletea wenzetu wa Kenya matatizo. Ni lazima watanzania tuepuke udanganyifu wa aina hiyo.
 
• Wako hata wanaotuogopesha sisi Watanzania kwa kutulinganisha na Walibya. Hawa wapuuzwe na waonewe tu huruma kwa kuwa wamesahau misingi na uimara wa nguzo za Taifa letu ambazo uongozi wa Baba wa Taifa Mwal. Julius Kambarage Nyerere aliotujengea. Kwanza hawajui hata kwa nini Libya wanapigana. Ukweli ni kwamba machafuko yao hayakutokana na uchaguzi. Yalisababishwa na watawala kung’ang”ania madaraka na kugawana rasilimali za taifa kwa misingi ya familia zao.
 
• Kama ilivyotokea Zambia, Malawi na Kenya, Watanzania wamedhamiria kuleta mabadiliko kidemokrasia na kuiondoa CCM madarakani kwa kura zao.

Ndugu zangu,
 CCM imekuwa madarakani kwa miaka mingi mno – zaidi ya nusu karne. Haina jipya; imechoka na haina pumzi ya kuongoza Taifa letu tena. CCM imebaki kuonyesha jeuri na kubeza tu. Imeishiwa nguvu ya hoja.
 
• Watanzania wamechoshwa na ahadi hewa za CCM za miaka nenda, miaka rudi. Tusiruhusu CCM kuendelea kurubuni na kuhadaa wananchi.
 
• Watanzania sasa wanataka MABADILIKO; mabadiliko ya kweli na ya uhakika.
 
• Tarehe 25 mwezi huu tuhakikishe tunaing’oa CCM madarakani na kuanza safari mpya ya kuleta mabadiliko.
 
• Nini maana ya haya mabadiliko endapo mtanipa ridhaa yenu ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Yapo maeneo manne ya msingi katika mabadiliko tunayodhamiria kuyaleta katika kuliongoza Taifa letu katika zama mpya:
 
1. Kwanza kabisa, ni ukombozi mpya wa Mtanzania. Hakuna maendeleo bila uhuru na haki.
 
• Mtanzania hana budi kuwa na madaraka ya Kikatiba juu ya maisha yake na kuweza kujisikia ana haki kamili na yuko huru katika nchi yake.
 
• CCM ilikwamisha ukombozi huu baada ya kuikataa Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba. Tusisahau kwamba hii Rasimu imetokana na juhudi za wengi na Jaji Warioba akiwa tu ni mmoja wao.
 
• Nikichaguliwa kuwa Rais, suala hili la Katiba mpya yenye maslahi kwa mwananchi litapewa kipaumbele.
 
2. Pili, ni ukombozi katika hali za maisha ya mwananchi. Wananchi hawawezi kuboresha hali za maisha yao kupitia takwimu nzuri za Pato la Taifa zinazopambwa na CCM ambazo hazionyeshi maisha halisi ya Mtanzania.
 
• Watu hawali takwimu. Watanzania wanataka milo mitatu yenye lishe bora; wanataka huduma bora za elimu, afya, maji safi na salama; wanataka umeme vijijini na ajira toshelezi kwa vijana;
 
• Wanataka mapinduzi katika kilimo chenye tija na bei bora za mazao.
 
• Watanzania wamechoka na umaskini.
 
• Haishangazi kusoma katika taarifa ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2015 kuhusu hali ya furaha ya wananchi katika nchi mbali mbali katika mwaka 2013, kwamba kati ya nchi 156 zilizofanyiwa utafiti, Tanzania inashika nafasi ya chini kabisa ya 151 ikidhihirisha kwamba watanzania hawana furaha kabisa.
 
• CCM na Serikali yake imeshindwa kuwapa wananchi wake hali bora ya maisha na hivyo kuwanyima furaha.
 
• Mwanasiasa maarufu wa Marekani Marehemu Seneta Hubert Humfrey aliwahi kusema kwamba kipimo maalum cha maadili na dhamira ya Serikali yeyote na hata haki ya Serikali hiyo ya kutawala ni jinsi inavyowajali na kuhudumia watu wafuatao:
 
• Wale wanaoingia duniani kwa mara ya kwanza – yaani watoto;
 
• Wale ambao wanafikia mwisho wa maisha yao baada wa kutumikia jamii – wazee; na,
 
• Wale waliomo kwenye hali na mazingira ya maisha hatarishi –Hawa ni wagonjwa, wenye mahitaji maalum, na walemavu
 
• Kwa vipimo hivi vitatu, Serikali ya CCM imeshindwa vibaya sana. Imefilisika!
 
• Baada ya zaidi ya miaka 50 ya Uhuru tunashuhudia wakina mama wengi wanaotuzalia watoto wa taifa hili na vichanga vyao vikizaliwa sio kwenye kitanda kilichotayarishwa bali sakafuni;
 
• Tanzania katika mwaka wa 2015 inashika nafasi ya 91 kati ya nchi 96 zilizofanyiwa utafiti na Taasisi ya Dunia iitwayo HelpAge kuhusu hali ya wazee wenye umri zaidi ya miaka 60. CCM na Serikali yake imeshindwa kutekeleza wajibu wake. CCM haiwajali wazee wetu.
 
• Wagonjwa hawapati dawa hospitalini nahata wanaojiweza lazma wakatibiwe nje ya nchi; wenye mahitaji maalumu ya kibinadamu na ambao hawana njia ya ajira hawayapati; huduma za walemavu ni finyu na, pamoja kuendelea kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
 
3. Tatu, wananchi wanataka mabadiliko ya uongozi na mfumo; wanataka uongozi wenye fikra mpya, utendaji wa kuaminika; na uongozi wa uwajibikaji na uongozi shirikishi.
• Wanataka uongozi makini wenye ubunifu, wenye upeo mpana na unaongozwa na nidhamu na hasa ile ya matumizi mazuri ya fedha za Serikali.
 
• Serikali ya CCM imeingiza nchi katika deni kubwa katika historia ya nchi. Deni hili ni karibu shilingi trillioni 35 hivi sasa. Deni hili limetokana na matumizi mabaya ya Serikali ya CCM ya Rais Kikwete.
 
• Ni kazi kubwa kulipa deni hili. Na ndiyo maana Watanzania wanalazimika kuing’oa Serikali ya CCM na kuleta mabadiliko ya kiuchumi yatakayo wapunguzia kizazi hiki na kijacho mzigo wa madeni ambayo Serikali ya CCM inaendelea kuwalimbikizia kutokana na matumizi yasiyo na busara
 
• Nataka kuwahakikishia kwamba uongozi wangu na ule wa mwenzangu visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, si wa kuyumba au kuyumbishwa; ni uongozi wa kuthubutu katika utatuzi wa matatizo ya wananchi; ni uongozi wa uchapa kazi na wa kuchukua maamuzi magumu kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kizazi kijacho.
 
• Ni uongozi wenye dhamira ya kuwaunganisha watanzania bila kujali madhehebu, rangi au makabila yao.
 
• Ni uongozi utakaojenga Taifa linalojitegemea, siyo la omba omba kama ilivyo hivi sasa.
 
4. Nne, Uongozi wangu na wa wenzangu utaheshimu, utalinda na kutetea Katiba ya nchi. Nitakuwa mfano wa uadilifu; nitapiga vita vitendo vyote vya rushwa na ufisadi; Nitahakikisha kwamba rushwa hakika inakuwa adui wa haki na maendeleo yetu.

Ndugu watanzania wenzangu,
Baada ya kufafanua maeneo haya manne ya msingi kuhusu mabadiliko nitakayo yaleta na kuyasimamia, sasa naomba niingie kwa undani kuhusu mambo ambayo Serikali nitakayounda itatekeleza ni mambo 16.
 
1. Kwanza, Serikali nitakayoongoza itapambana na umaskini, ujinga na maradhi kikamilifu.
• Itaboresha elimu kama hatua ya kwanza ya kuwapa Watanzania uwezo wa kujikomboa. Kila Mtanzania atapata elimu bora itakayogharimiwa na serikali kutoka ngazi ya elimu ya awali hadi Chuo Kikuu.
 
• Tutapiga marufuku michango kama vile ya kujenga maabara na tutaboresha maslahi na vitendea kazi kwa waalimu na kurudisha posho ya kufundishia.
 
• Tutapanua wigo wa mafunzo ya kijeshi na kujitegemea yanayotolewa katika Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuongeza idadi ya wanaojiunga mara tano zaidi kuliko ilivyo sasa ili kuboresha mafunzo ya stadi za maisha, ufundi na ujasiriamali.
 
2. Pili, tutaondoa kodi zote za kero kwa wafanya biashara hususani wafanya biashara wadogo wadogo, mama lishe, boda boda, na machinga.
• Aidha, tutaondoa kodi zote za mazao kwa wakulima, wafugaji, na wavuvi wadogo wadogo ili tuongeze kipato na uwezo wao wa kuwekeza na kuliwezesha Taifa kujitosheleza kwa chakula na lishe bora.
 
• Tutahakikisha kuwa elimu inatolewa kwa makundi haya ili kuinua kiwango cha uzalishaji kwa kusimamia shughuli zao kitaalam kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
 
• Vile vile, tutayawezesha makundi haya kwa mikopo ya riba nafuu kutokana na benki mahsusi itakayoanzishwa kusimamia sekta ya ufugaji na uvuvi.
 
3. Tatu, tutakuza na kulinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi ili waimarike na waweze kuhimili ushindani.
• Tutawapa upendeleo katika zabuni na manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri zaidi ya biashara.
 
• Serikali nitakayoongoza itajenga uhusiano wa karibu na wawekezaji katika biashara na viwanda katika kuhakikisha sera na mikakati ya Serikali haipingani na mazingira ya uzalishaji na mienendo ya biashara.
 
• Tanzania ina kodi nyingi kuliko nchi zote Afrika ya Mashariki na zile za SADC. Tutaweka mfumo wa kodi utakaotuwezesha kushindana kimataifa.
 
• Kazi hii ni nzito kwa sababu Serikali ya CCM imeacha dosari kubwa katika mazingira yanayovutia uwekezaji.
 
• Ukweli ni kwamba Tanzania imepoteza uwezo wa ushindani katika soko la ndani na la nje kutokana na ubovu wa miundombinu pamoja na urasimu hali ambayo imesababisha gharama za usafiri na usafirishaji kuwa kubwa kupita kiasi.
 
• Taarifa ya Benki ya Dunia ya mwaka 2015 ambayo hupima ubora wa miundombinu ya usafiri kwa madhumuni ya biashara inaonyesha kwamba kati ya nchi 160 zilizofanyiwa utafiti, Tanzania imeshika nafasi ya chini ya 138.
 
• Hata nchi zinazopitisha bidhaa zao Tanzania (landlocked) kama vile Malawi, Rwanda na Burundi zimeshika nafasi za 73, 80 na 107. Kenya inashika nafasi ya 74.
 
4. Nne, tutakuza viwanda vidogo vidogo ili viwe mhimili wa uchumi wa nchi. Lazima tuimarishe uzalishaji na kusindika mazao yetu ili kuongezea thamani na kutengeneza vyanzo vya ajira.
 
5. Tano, tutaimarisha mfumo wa afya ya msingi na kuboresha huduma za kinga ili kuepukana na gharama kubwa za tiba.
• Serikali nitakayoongoza itaandaa taratibu na mifumo ya kuwapatia wananchi wote huduma za afya na matibabu kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
• Tutaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na kuepukana na gharama kubwa za tiba za nje ya nchi.
 
• Wazee na wananchi wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya msingi ili waishi kwa heshima ndani ya familia na jamii zao.
 
6. Sita, tutadhibiti matumizi serikalini na katika mashirika ya umma kama vile kupiga marufuku matumizi ya magari ya anasa, kupunguza safari za ndani na nje,usafiri wa anga wa daraja la kwanza na semina na makongamano yasiyo ya lazima.
 
7. Watanzania watapewa fursa maalum ya kushiriki katika uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi. Sambamba nahili, Serikali yangu itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
 
8. Nane tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika au makampuni yote ambamo serikali ina hisa na kuipa ofisi hiyo mamalaka kamili.
 
• Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
 
9. Tisa, tutadhibiti vitendo vya rushwa iliyo kithiri katika bandari zetu, ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya fedha yanayopotea kila wiki.
 
• Sambamba na hayo, tutarahisisha utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti makusanyo ya kodi tutaweza kupata fedha zaidi za kugharimia huduma za msingi kikamilifu.
 
10. Kumi, tutaimarisha utendaji na uwajibikaji katika sekta ya umma na kuhakikisha kuwa rushwa, urasimu na kero zinazodumaza maendeleo ya wananchi zinakomeshwa.
 
• Sambamba na hayo, tutaboresha maslahi na vitendea kazi kwa wafanyakazi wa Serikali na sekta ya umma.
 
11. Kumi na moja, tutahakikisha tunatengeneza vyanzo vipya vya ajira kwa kukuza sekta za kilimo, viwanda na utalii.
 
12. Kumi na mbili, tutaimarisha miundombinu na kujenga mtandao wa reli tukianza kwa kujenga upya na kwa viwango vya kisasa Reli ya Kati na Reli ya Tanga-Arusha-Musoma.
 
• Pia tutajenga barabara za viwango vya juu kuliko sasa zikiwemo za vijijini ili kuchochea biashara na maendeleo.
 
• Tutaboresha bandari za baharini na maziwani na kujenga zingine mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani. Tutanunua meli mpya za usafiri wa watu na mizigo kwa ajili ya usafiri katika ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.
 
• Tutajenga upya Shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
 
• Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
 
• Tutasimamia uzalishaji na usambazaji wa umeme mijini, vijijini ili kufikia zaidi ya asilimia sabini na tano ya Watanzania ifikapo mwaka 2020.
 
• Tutasimamia upanuzi na usambazaji wa umeme wa uhakika na kufanya mgao wa umeme kuwa historia hapa nchini.
 
13. Kumi na tatu, tutahakikisha Katiba ya wananchi inakuwepo ili kujenga misingi ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari na kuwapa nafasi asasi za kiraia, vyombo vya dola, Bunge na wananchi kusimamia uwajibikaji nchini.
 
• Tutasimamia utawala bora kwa kuamini kuwa kama nchi itaendeshwa kwa misingi ya sheria na utawala bora, haki itatendeka, rushwa itadhibitiwa, barabara bora zitajengwa kwa viwango, shule na hospitali bora zitajengwa na kupewa vifaa na kwamba mashirika yetu yataendeshwa kwa tija.
 
14. Kumi na nne, tutaimarisha mchango wa wataalam wetu,wanawake na vijana, katika kuandaa sera na kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
 
• Serikali nitakayoongoza itaunda Tume Maalum ya Kupendekeza mishahara ya watumishi Serikalini, sekta ya umma na binafsi kwa maana ya kima cha chini cha mshahara.
 
15. Kumi na tano, tutaimarisha Muungano wetu ikiwa ni pamoja na umoja, usalama na udugu wa Watanzania kwa misingi ya haki na usawa.
 
16. Kumi na sita, tutaimarisha uhusiano na kuongoza ushirikianona nchi nyingine ndani ya Jumuia ya Afrika ya Mashariki, SADC, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Taasisi nyingine za Kimataifa.
 
Ndugu Watanzania wenzangu,
Napenda kusisitiza kwamba ili haya yote tunayokusudia yaweze kufanikiwa, ni lazma tuimarishe mihimili ya Taifa letu na vyombo vyake maalum.
 
Serikali ina wafanyakazi wengi mahiri, wadilifu na wenye weledi mkubwa. Ili kuhakikisha ufanisi mzuri wa Serikali na taasisi zake, mishahara ya wafanya kazi wa Serikali itaboreshwa, ushauri wao wa kitalaamu utawekwa maanani na vitendeakazi vyao vitatiliwa mkwazo;
 
Ulinzi wa taifa utaimarishwa kwa kuzingatia mahitaji na maslahi askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi na Magereza ikiwa ni pamoja na kuboresha vitendea kazi vyao.
 
Maboresho hayo yatahusisha pia taasisi zote zenye dhamana ya masuala ya ulinzi na usalama wa nchi, ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB).
 
Katiba tutayoipitisha itakuwa ni ya kuimarisha Mhakama kwa kiasi kikubwa pamoja na Bunge letu
 
Serikali yetu itahakikisha suala la michezo, utamaduni na sanaa linapewa kipaumbele maalum.
 
Pamoja na kwamba Tanzania kwa sasa inazidi kung”aa kupitia wasanii wa muziki wa kizazi kipya, lakini bado juhudi kubwa haijawekwa katika kukuza na kuendeleza sanaa, utamaduni na michezo.
 
Timu zetu za mpira bado hazifanyi vizuri kimataifa na zimeendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu.
 
Kuodokana na hali hiyo, Serikali yetu itafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
 
Itafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi.
 
Itajenga shule za kukuza vipaji vya soka (Youth Academies) na michezo mingine ili kuhakikisha ndani ya miaka mitano, Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka, riadha na michezo mingine.
 
Ndugu Watanzania wenzangu,
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo:
1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua kuwa Rais wenu, nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka na kwa uadilifu mkubwa.
 
2. Mimi nawaheshimu Watanzania na namuogopa Mungu. Nawaahidi kwamba nitawatumikia Watanzania kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote.
 
3. Mabadiliko yanaendana na kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua.
 
4. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM na ndiyo nyenzo yao kuwakandamiza Watanzania. Tukatae. Tuchague mabadiliko
 
5. Mabadiliko ni fikra. Ni mabadiliko ya kufikiri na kutenda tofauti na hali ilivyo.
 
6. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kana kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili.
 
7. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao.Tanzania pia itaweza; tukichagua Mabadiliko.
 
8. Tuwe taifa linalotumia rasilimali zake kwa ufanisi zaidi kujiendeleza na siyo kwa kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana katika nchi yao.
 
9. Tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na kuuvaa umaskini kama vile ni joho la fahari. Hakuna faraja katika umaskini.
 
10. Mabadiliko hayawezi kuletwa na CCM. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wake watanzania bado ni maskini. Tusitegemee kuwa wanalo jipya hii leo.
 
11. Kama alivyosema Baba wa Taifa “maendeleo ni watu”. Magorofa marefu yanapendeza na tuendelee kuyajenga. Lakini maendeleo ya watu ndiyo msingi.
 
12. Kwa kuwa CCM imeshindwa kuwakomboa Watanzania kimaisha, basi imepoteza haki na haina sifa ya kuendelea kutawala. Tuikatae CCM. Tuchague mabadiliko.
 
13. Watanzania wameichoka CCM.
 
14. CCM imethibitisha pasipo na shaka kwamba ipo tu kwa maslahi ya wachache.
 
15. CHADEMA na UKAWA hatuna ajenda nyingine bali kuwahudumia Watanzania katika kuharakisha maendeleo yetu.
 
16. Mimi, CHADEMA na UKAWA tunaamani kwamba tutashinda uchaguzi kwa sababu Watanzania tupo pamoja katika kuleta mabadiliko.
 
17. Hivyo basi, kura ya kila mmoja wetu inayonichagua mimi na mgombea mwenza, Mheshimiwa Juma Haji Duni, mgombea urais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wabunge, wawakilishi na madiwani ndiyo itakayokuwa mkombozi wetu.
 
18. Tuhakikishe tunapiga na kulinda kura zetu. Wakati wa mabadiliko ni sasa.
 
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Asanteni kwa kunisikiliza.

Agnes Masogange Adai Sababu iliyomfanya Tekno Amkane ni Ukaribu Wake na Davido!

$
0
0
Mrembo Agnes Masogange ameendeleza episode nyingine ya drama yake na mwimbaji wa Nigeria, Tekno miles, iliyoibuka wiki hii baada ya mwimbaji huyo kukanusha kuwa hajawahi kuvunja naye amri ya sita!

Katika muendelezo wa kutaka kuthibitisha kuwa alichokisema Tekno sio kweli, Agnes ameweka wazi sababu anayodai kuwa ndiyo iliyomfanya mwimbaji huyo wa ‘Duro’ amkane, kuwa ni wivu baada ya kuona amekuwa karibu na super star mwingine wa Naija, Davido.

Agnes alipost picha aliyowahi kupost miezi kadhaa iliyopita akiwa anakula bata na Davido na kuandika caption, “Kumbe brother alipanick kitambo kisa OBO Baddest”, post ambayo baadae aliifuta.

Mwigulu Nchemba: Siasa si Uadui, Acheni Kuumizana...Kuna Maisha Baada ya Uchaguzi

$
0
0
Mbeya. Mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, Mwigulu Nchemba amewataka wakazi wa Mbeya kuacha chuki kwa sababu za kisiasa kwani hata viongozi wa CCM na Chadema ni marafiki hawana uadui.

Akizungumza juzi kwenye viwanja vya Uyole na Nzovwe jijini hapa, Nchemba alisema alisikitishwa na taarifa za kuuawa kwa wana CCM wawili katika Mji Mdogo wa Tunduma wakati wa kampeni za Chadema.

“Nimesikitishwa na hatua hii mliyofikia, nimesikia kuna watu wawili Tunduma wameuana kwa sababu za kisiasa,” alisema Nchemba.

Alisema ubishi wa kisiasa unapaswa kulenga katika kuimarisha maendeleo ya watu na Taifa, lakini udugu lazima ubaki palepale.

Aliwasihi wakazi hao kutokubali kuumizana kwa sababu ya siasa kwani haitawasaidia.

Mgombea udiwani wa Kata ya Nzovwe, Mlaga alisema endapo wananchi watamchagua atahakikisha kivuko cha Mto Swaya kinatengenezwa.

Source:Mwananchi

Has DIAMOND Divorced ZARI HASSAN? Yes, His Family Is Tired of Her ‘Uzungu’

$
0
0

The media in Tanzania carried a story today that Diamond’s family has decided to chase Zari Hassan away because they are tired of her diva antics.

This was as a result of Zari’s repudiation to return back to Tanzania with their daughter, Latiffah, almost a month after she traveled to South Africa to see her sons.

See this:




This Is How VERA SIDIKA Dresses When She Goes To Negotiate For S3X With CEOs (PICs)

$
0
0

This Is How VERA SIDIKA Dresses When She Goes To Negotiate For S3X With CEOs (PICs)




Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Tarehe 24

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Tarehe 24



















Kikwete: Magufuli Ameshashinda, Bado Kuapishwa tu!!

$
0
0
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema tayari mgombea urais wa chama hicho, Dk John Magufuli ameshashinda uchaguzi.

Amesema hatua hiyo inatokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kwa mgombea huyo kuzunguka nchi nzima na kuwahakikishia wananchi, bila kupepesa macho, kwamba atapambana na rushwa na ufisadi huku wagombea wengine wakisita kuzungumzia rushwa.

Katika hatua nyingine, Dk Magufuli ametaja mambo manne atakayoanza nayo kuwa ni umasikini, tatizo la ajira, mapambano dhidi ya rushwa na amani.

Pia, aliwapa pole Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais Kikwete kwamba katika utawala wao, bila kujua waliwaweka madarakani mafisadi waliochelewesha maendeleo ya serikali zao.

Rais Kikwete na Magufuli waliyasema hayo katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mkuu kwa Jiji hilo. Mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya watu na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na viongozi kutoka nje ya nchi.

Akimnadi Dk Magufuli, Rais Kikwete alisema kutokana na kampeni alizozifanya nchi nzima kwa gari, ni wazi kwamba mgombea huyo wa CCM ameshashinda uchaguzi huo. Alisema wagombea wengine pamoja na kutumia helikopta, lakini walishindwa kuzungumza majukwaani.

Alisema pamoja na kuelezea mambo mbalimbali atakayowafanyia wananchi kwa kila kundi, amekuwa mgombea pekee ambaye bila kupepesa macho amezungumza waziwazi azma yake ya kupambana na rushwa na kuwakabili mafisadi ili kuwatokomeza.

Alisema tangu kuanza kwa kampeni zake Dk Magufuli ametembea kilometa 46,000 nchi nzima, umbali aliosema umemwezesha kukutana na wananchi wengi vijijini. Alisema wakati yeye alipofanya kampeni mwaka 2005, alitembea kilometa 32,000 kwa gari na kuwa hoi katika siku za mwisho za kampeni.

Alisema pamoja na kuzungumzia rushwa, Dk Magufuli amezungumzia masuala mengine mengi kama kupambana na umasikini, ajira, amani, mikopo kwa wakulima, wavuvi na wafugaji, kushusha kodi kwa wafanyakazi, kufuta ada kuanzia darasa la kwanza hadi kidato na nne, lakini pia kuanzisha viwanda.

Akirejea taratibu zilizomwezesha Dk Magufuli kuteuliwa na chama hicho kugombea urais, Rais Kikwete alisema hakuna jipya lililofanyika katika kumpata mgombea huyo, badala yake ni taratibu zile zile zilizotumika mwaka 1995 kumpata Rais mstaafu Mkapa na mwaka 2005 alipoteuliwa yeye.

“Ni taratibu zilezile ndizo zilizotumika, hakuna utaratibu mpya. Katiba ya CCM inasema Kamati Kuu itapitisha majina ya watu wasiozidi watano na kuyapeleka kwenye Halmashauri Kuu, inaweza kuwa chini ya hapo lakini wasiozidi watano,” alisema Rais Kikwete akimjibu Kingunge Ngombale- Mwiru anayedai kupitia majukwaa ya Ukawa kuwa CCM ilikiuka taratibu.

Akizungumzia mikopo kwa wanafunzi, Rais Kikwete alisema ni faraja kuona kuwa Dk Magufuli amepania kukabiliana na usumbufu wanaokumbana nao.

Alisema wakati alipoingia madarakani mwaka 2005, alikuta Sh bilioni 40 tu zikitolewa kwa wanafunzi, huku wanafunzi 16,000 tu wakinufaika, na sasa Sh bilioni 350 zinatumika na kuwanufaisha wanafunzi 98,000.

Gari la Serikali Lakamatwa Huko Njombe Likidaiwa kuwa na Maboksi ya Kura FEKI zilizopigwa Kumchagua Magufuli

$
0
0
Gari  la  Serikali  limekamatwa  mkoani  Njombe  likidaiwa  kuwa  na  kura  FEKI  Zilizizopigwa  kwa  ajili  ya  mgombea  urais  wa  CCM

Gari  lililokamatwa  ni  la  Tanroads, na  limekamatwa  leo  asubuhi.Walipokamatwa  walijitetea  kuwa  walikuwa  wamebeba  t shirt  za  Magufuli.


Baada  ya  Upekuzi  kufanyika, chini  ya  shinikizo  la  wananchi, gari  hilo  lilikutwa  na  kura  ambazo  tayari  zimepigwa  kumchagua  Magufuli.

Taarifa  hii  Imethibitishwa  na  James  Mbataia, Mwenyekiti mwenza  wa  Ukawa. . 
Tazama  Video




MKOANI NJOMBE, gari lenye kura zilizopigwa tayari. We can not tolerate this
Posted by Mussa Samora on Saturday, October 24, 2015

Wanamuziki Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz Wazinguana Marekani....Nusu Wazichape

$
0
0
MAPENZI yanatingisha dunia! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia nyota wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuzinguana laivu nchini Marekani, Risasi Jumamosi limevujishiwa na lina mchapo kamili.

Chanzo makini kilichoshuhudia sakata hilo lililotokea hivi karibuni nchini Marekani kulipokuwa na hafla ya utoaji wa tuzo za Afrimma ambapo Diamond alitwaa 3 huku Dimpoz akipata 1, kimenyetisha kuwa, wawili hao walizinguana wakiwa wanataka kuingia kwenye ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya utoaji wa tuzo hizo.

“Walipokuwa wanaingia ukumbini, Dimpoz akakutana na Diamond sasa Diamond akataka kumsalimia ndipo Dimpoz akachomoa na kumpa maneno ya kejeli ambayo yalimkasirisha nusu wazichape.
“Kila mtu alijua jamaa watashikana mashati. Lakini sema ile busara ya haraka iliwajia, hawakufikia hatua hiyo mbaya,” kilisema chanzo.


CHANZO CHA BIFU

Kikaendelea: “Unajua Dimpoz alikataa kupokea salamu ya Diamond maana anasema ni mnafiki. Anadai kwamba, Diamond anapokuwa na watu anajifanya hana tatizo na Dimpoz lakini akiwa na marafiki wa Dimpoz huwa anamzungumzia vibaya na wakikutana na Dimpoz anamsalimia kinafiki ndiyo maana mwenzake akamaindi.”


WEMA ATAJWA

Kikizidi kulipambanua bifu la mafahari hao wawili, chanzo hicho kilidai kuwa, sababu kubwa ya bifu hilo ilianza muda mrefu baada ya Diamond kumhisi Dimpoz anatembea na Wema Sepetu ‘Madam’ ambaye alikuwa mpenzi wake kwa muda mrefu kisha akamwagwa.

“Kumbe Diamond ana kinyongo na mwenzake. Alimwagwa na Wema lakini nafikiri bado moyoni anampenda sana. Sasa alipoona siku chache baada ya kuachana, ghafla mrembo huyo akaonekana katika pozi tata na Dimpoz, akamuwekea bifu pasipo hata kumuuliza kama ni kweli au la,” kilisema chanzo na kuongeza:

“Tangu hapo, Diamond amekuwa akimsema vibaya Dimpoz kupitia marafiki zake kitu ambacho Dimpoz anakiona ni unafiki kwani hamwambii mwenyewe. Huwezi amini kule Marekani, Diamond alikuwa ndiye aliyetangulia kufika lakini badala ampokee mwenzake ambaye ni mgeni, akampotezea halafu ukumbini akajifanya anamsalimia.”

WABONGO WAWASHANGAA

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kitendo cha wawili hao kuzinguana ukumbini wakati wanatokea sehemu moja kiliwashangaza Wabongo waishio nchini humo ambao walikwenda kushuhudia utoaji wa tuzo hizo kwani walitegemea wawili hao wangekuwa kitu kimoja.

“Wabongo wenzao waishio Marekani waliwashangaa sana. Hawajui kwamba huku ndiyo walitakiwa kuonesha umoja wao. Kwanza ndiyo wanainuka katika tuzo kubwa halafu wao wanaleta za uswahilini, itawagharimu siku moja,” kilisema chanzo hicho.

DIMPOZ AFUNGUKA

Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, mwanahabari wetu alianza kumtafuta Dimpoz ili aweze kutoa ufafanuzi juu ya kile kilichotokea ambapo alipopatikana, alifunguka:

“Daah! Nani kawapa hizo habari? Nyinyi kweli mnajua kunusa. Ni kweli tulipishana na jamaa (Diamond) kule Marekani.

“Lakini si unajua tena… pengine Diamond ana kinyongo chake na mimi sipendi mtu anayeishi kwa vinyongo, ndiyo maana nilikataa salamu yake, yakatokea hayo lakini kimsingi namshukuru Mungu hatukukunjana wala nini.”


DIAMOND SASA

Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kueleza kwa upande wake hazikuzaa matunda kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa alikuwa safarini nje ya nchi.

“Jamaa siyo rahisi kumpata sababu yupo safarini nje ya nchi labda umcheki tena baadaye,” alisema mtu wa karibu na Diamond pasipo kutaja msanii huyo ameelekea wapi.

TUJIKUMBUSHE
Baada ya Diamond kumwagwa na Wema mwishoni mwa mwaka jana, baadaye Februari mwaka huu, picha zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimwonesha Dimpoz na Wema wakiwa kitandani, hotelini nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini viliandika kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi huku ikielezwa kwamba, uhusiano huo ulikuwepo kwa siri hata wakati Wema akiwa na Diamond.
Hata hivyo, baadaye ikaja kuelezwa kuwa, Wema na Dimpoz walikuwa nchini humo wakitengeneza video ya wimbo wa Dimpoz uitwao Wanjera.

Hali si shwari Tarime, Sita wakatwa mapanga

$
0
0
Watu sita wamejeruhuiwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao  Wilayani Tarime mkoani Mara akiwemo mwandishi wa habari wa Sahara Media, Geoge Nteminyanda (49) usiku wa kuamkia leo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi katika wodi namba tatu na namba nane walikolazwa, majeruhi hao wamesema kuwa walishambuliwa na wafuasi wa vyama vya Chadema na CCM ambao walikuwa katika makundi makundi kati ya saa mbili na saa nne usiku.

Nteminyanda ambaye ni mkazi wa Kisesa  Mwanza amesema kuwa aliitwa na mgombea ubunge wa CCM, Michael Kembaki na kufikia katika hoteli  ya CMG ambapo kulikuwa na kikao cha chama hicho lakini alianza kuhojiwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho. Lakini licha ya kutoa vitambulisho vya kazi wafuasi hao walianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga mwilini na kuanguka chini. Hata hivyo watu hao waliendelea kumkanyaga hadi akapoteza fahamu.

Wasamaria wema walimchukua na kumpeleka hospitalini ambapo alipewa kitanda namba tatu cha wodi namba tatu.

“Waliokuwa wakinishambulia walikuwa vijana wengi kutokana na kunikabiri vibaya sikuwatambua kwa haraka lakini wakiwekwa kwenye mstari wa utambuzi nitawatambua” amesema Nteminyanda.

Wengine waliojeruhiwa ni Waiboga warioba (37) aliyekatwa kichwa na sikio la kulia,Busiro Rhobi (28) mkazi wa Nyamongo aliyekuwa na gari lake binafsi, Daniel Mathew (18) mkazi wa Goribe Wilayani Rorya anayedaiwa kupigwa risasi kichwani upande wa kulia na mgombea udiwani wa kata ya Ikoma  Laurence Andriano (CCM).

Wengine ni Wambura Marai (38) aliyeopolewa kutoka kwenye gari lake baada ya kutokea ubishani kati yake na wafuasi wa CHADEMA kuwa mshindi urais atakuwa John Pombe Magufuli.

Rose Hosea muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Tarime amesema kuwa wakati wanapokelewa hali yao ilikuwa mbaya zaidi lakini kutokana na juhudi za timu ya wauguzi wa zamu walitoa huduma za haraka ikiwa ni pamoja na kuwashona majeraha yao huku wakiwapa dawa za maumivu.

“Hali yao inaendelea vizuri kwa sasa tofauti na ilivyokuwa jana” amesema Hosea.

Rais Kikwete: Afya za Wagombea Wengine Zilitupa Wasiwasi Wakati wa Mchakato wa Kumtafuta Mgombea

$
0
0
Akimnadi mgombea urais kupitia CCM, rais Kikwete amesema wakati wa uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama walizingatia suala la afya za wagombea na wakajiridhisha kuwa Magufuli yupo 'fiti' kiafya tofauti na wagombea wengine. Haya sasa, wale mlokosa tano bora mna madhaifu gani?

#KutokaCCMKirumba

MWANZA Hali Tete; Vijana Wa CCM Wang'oa Bendera za CHADEMA

$
0
0
Bendera Zilitundikwa Jana za Chadema Jiji La Mwanza Leo ASUBUHI Vijana Wa CCM wamezichomoa Zote Huku Askari Wa Usalama Barabarani Akiwepo Wanaangalia..

Fujo wakifanya CCM Ni Sawa Ila Zikifanywa Na CHADEMA NA UKAWA Zile Gari za Washa Washa Zinaletwa.

Source: JF

Tanzania Tumefika Pabaya..Kada wa CCM Amwagiwa Tindikali

$
0
0
Tarime. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Chadema kata ya Sirari na kuhamia chama cha CCM, Weng’ari Mang’era (26) amemwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati wakimpokea mgombea ubunge wa Tarime Vijijini(CCM), Christopher Kangoye katika uwanja wa Tarafa Sirari Wilayani Tarime.

Shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe litajwe ameeleza” Mbunge Kangoye alikuwa anakwenda kwenye mkutano Uwanja wa Tarafa wakati tuko barabarani watu wakafika na kumjeruhi kwa kumwagia tindikali,’amesema.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Lazaro Mambosasa amesema polisi wanafuatilia kujua waliohusika na tukio hilo.
Wakati hilo likitokea, Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Athuman Akalama alisimamisha kampeni kwa wagombea zilizokuwa zinaendelea Nyamongo baada ya kuibuka kwa vurugu kati ya CCM na Chadema.

Leo asubuhi mgombea Udiwani Kata ya Matongo-Nyamongo(CCM), Daud Itembe akiwa kwenye harakati zake za kuhitimisha kampeni zake zilizokuwa zifanyike maeneo ya stendi Nyamongo lakini kukaibuka vurugu kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images