Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104766 articles
Browse latest View live

CCM Waongea na Vyombo vya Habari.....Wamesema Hadi sasa Wameshinda Majimbo 176 kati ya 264

$
0
0

CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wanachama, wapenzi na washabiki wake na kwa umma Watanzania.

Tathmini ya Upigaji Kura
Kama tulivyoeleza jana, tumeridhishwa na amani na utulivu uliotawala katika sehemu kubwa ya nchi yetu wakati wa zoezi la upigaji kura. Licha ya changamoto zilizojitokeza, ambazo baadhi zimeshughulikiwa, kwa jinsi zoezi la kupiga na kuhesabu kura lilivyoendeshwa kwa uwazi, matokeo ya uchaguzi huu yatakuwa ni kielelezo cha utashi halisi wa Watanzania na kutakuwa hakuna sababu ya mtu yoyote kukataa matokeo.

Kupokea na Kutangaza Matokeo
Kipindi cha kupokea na kutangazwa matokeo ni muhimu kama ilivyo kipindi cha kampeni na siku ya kupiga kura. CCM inahimiza utulivu kwa wafuasi wake na wananchi kwa ujumla na kuziachia mamlaka husika zifanye kazi yake. Katika kipindi hiki, kazi za vyama ni kupokea matokeo na na kazi ya Tume ni kutangaza matokeo.

Tunasikitishwa na propaganda zinazoendeshwa na wapinzani wetu kuhusu matokeo ya uchaguzi. Tunaona matokeo yanayotangazwa na wafuasi wa vyama vya upinzani, hasa mitandaoni. Bahati nzuri, propaganda hizi zinakosa maarifa kiasi cha kutoa hata matokeo ya Ubunge katika majimbo ambayo uchaguzi wa Wabunge haukufanyika, mfano Handeni na Masasi.

Tunawataka wana-CCM wapuuze matokeo yanayotembezwa kwenye mitandao ya kijamii. Matokeo rasmi yatatolewa na Tume. Bahati mbaya sana, wenzetu wanatoa matokeo ya uongo mapema ili Tume ikitoa matokeo rasmi waseme wameibiwa kura na kutafuta kisingizio cha kuingia mitaani na kufanya vurugu.
 
Pia tunabaini jitihada na nguvu kubwa za wapinzani wetu kupeleka kilio chao kwa waandishi wa habari wa nje ya nchi pamoja na mataifa ya nje kwa ujumla. Wameajiri magwiji wa propaganda kutoka nje ya nchi kwa fedha nyingi kujenga taswira kwenye Jumuiya ya Kimataifa kwamba Tanzania ni kama nchi nyingine yoyote ya Kiafrika ambapo hakuna ustaarabu wala utaratibu wa kidemokrasia na Serikali hukandamiza watu wake.
 
Mkakati wao ni kuitaka Jumuiya ya Kimataifa itumie nguvu yake ya misaada kwa nchi yetu kulazimisha matokeo ambayo hayatokani na utashi wa Watanzania. CCM haitalikubali jambo hili.

Matokeo ya CCM
Kwa kuwa matokeo kwenye vituo vya kupigia kura matokeo yamebandikwa hadharani na Wasimamizi wa Vituo, na nakala kupewa mawakala wetu, kwa mujibu wa matokeo yaliyobandikwa vituoni , CCM hadi sasa imekwishapata majimbo 176 kati ya majimbo 264 katika mikoa kadhaa ambayo tumefanikiwa kujumlisha hadi sasa. Pia, hadi sasa, tumeweza kukomboa majimbo 11 ambayo yalikuwa upinzani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Tunawaomba wana-CCM watulie, wasiwe na hofu, wawe na subira hadi Tume imalize kazi yake. Matokeo ya Urais, ambayo yanaendelea kutangazwa na Tume, hayana tofauti na mwenendo tunaouona katika kura za Ubunge.

Imetolewa:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
26.10.2015

Matokeo Rasmi ya Ubunge Jimbo la MBEYA Mjini Haya Hapa

$
0
0
Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyego Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894

Matokeo Rasmi ya Ubunge Kwa Majimbo 18 Mengine Yaliyokwishatangazwa Hivi Punde

$
0
0
Mheshimiwa Wiliam Lukuvi katetea kiti chake cha ubunge.Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183

Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407.

Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665

Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480

Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614.‪

Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702

Wiliiam Lukuvi atangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge toka tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534

Jimbo la Mtama: Nape Nnauye wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa Chadema, aliyepata kura 13918

Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215

Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347
Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539.‪

Jimbo la Mbogwe: Augustino Manyanda wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 32921, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Maganga Nicodemas Henry wa Chadema, aliyepata kura 13975.

Mtwara mjini Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ashindwa kukitetea kiti chake

Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966.

Jimbo la Ngara: Alex Gashaza wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 53387, dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Dkt.Peter Bujari wa Chadema aliyepata kura 35254

Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyego Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894

Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 55213, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12957

Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578.

Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649.

Tuesday, October 27, 2015 Updates Za Matokeo Malimbali Ya Ubunge na Udiwani Zinapatikana Hapa....Karibu

$
0
0
Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Ubunge kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa  na  Wakurugenzi  wenye  dhamana  hiyo

Tembelea  ukurasa huu mara kwa mara  kwa updates zaidi
==============================================

Updates: Majira ya Saa kumi na nusu alfajiri. Waitara Mwita wa CHADEMA ametangazwa kunyakua kiti cha Ubunge Ukonga, kwa kumbwaga Jerry Slaa wa CCM ambaye alikuwa mpinzani wake mkubwa.
 
Jimbo la Bagamoyo: Dk Shukuru Kawambwa (CCM) 26,434, Andrew Kasambala (CUF) 16,330, Mwamini Saidi (UMD) 418 na Saidi Athman (ACT Wazalendo) 418.

Jimbo la Ngara: Alex Gashaza (CCM) 53,387, Dk Bujari Simon (Chadema) 35,254, Helen Gozi (NCCR-Mageuzi) 997 na Dotto Jasson Bahemu (ACT Wazalendo) 440.

Jimbo la Msalala: Ezekiel Maige (CCM) 36,010, Paulo Malaika(Chadema) 20, 124, Marco Suwa (ACT Wazalendo) 672 na Abeid Ibeshi (UDP) 251.

Jimbo la Busega: Dk Raphael Chegeni (CCM) 40,977, David William (Chadema) 26,995 na Zangi Robart (UDP) 802.

Jimbo la Mbogwe: Augustino Masele (CCM) 32,921, Nicodemus Maganga (Chadema) 13,975 na Andrew Mnuke (ACT Wazalendo) 5,464.

Jimbo la Bukombe: Dotto Biteko (CCM) 47,147, Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema) 29,929 na Dick Bagamba (ACT Wazalendo) 1,673.

Jimbo la Babati Mjini: Pauline Gekul (Chadema) 21,970 na Kisyeri Chambiri (CCM) 16,434.

Jimbo la Kahama Mjini: Jumanne Kishimba (CCM) 47,553, James Lembeli (Chadema) 30,122 na Bobson Wambura (ACT Wazalendo) 605.

Jimbo la Kibaha Mjini: Silvestry Koka (CCM) 31,462, Paul Mtally (Chadema) 24,860, Habibu Mchange (ACT Wazalendo) 3,438, Gombati Waziri (CCK) 259, Betha Mpata (APPT), 120 na Kibona Ally (AFP) 108.

Jimbo la Geita Mjini: Kanyasu John (CCM) 34, 953, Rogers Ruhega (Chadema) 26, 303 na Malebo Michael (CUF) 625.

Jimbo la Mkinga: Dustan Kitandula (CCM) 21,623, Bakari Kassimu (CUF) 13, 547, Rachel Sadick (Chadema) 3,789 na Ali Mwita (ACT Wazalendo) 402.

Jimbo la Lindi Mjini:Selemani Kaunje (CCM) 20,733 na Salum Barwany (CUF) 18, 843

 Jimbo la Same Mashariki: Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amemshinda Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539.

Updates: Mgombea Ubunge Jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe wa CCM ameibuka kidedea na kutetea kiti chake cha Ubunge
-Amembwaga Henry Kileo wa CHADEMA

Updates: Wilfred Lwakatare (Chadema) kapata kura 28, 112 na kumshinda Balozi Khamis Kagasheki (CCM) aliyepata kura 25, 565
Updates:Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro; Mgombea wa NCCR Ndg. James Mbatia, ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa kura 60,187 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Innocent Melleck Shirima aliyeambulia kura 16,097.

Updates:Jimbo la Moshi Vijijini, Kilimanjaro; Mgombea wa CHADEMA Anthony Calist Komu ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa jumla ya kura 55,813, akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Dr. Cyril Chami ambaye pia alishawahi kuwa Waziri Viwanda na Biashara aliyepata kura 24,415.

Updates:Jimbo la Nyamagana, Mwanza: Mgombea wa CCM, Mabula Stanslaus Shing'oma ameshinda kwa kuzoa kura 81,017, akifuatiwa kwa karibu na Ezekiel Wenje wa CHADEMA aliyeambulia kura 79,280.

==>CCM pia imeshinda Kata 14 kati ya 18 za udiwani katika Jimbo la Nyamagana huku Chadema kikiambulia Kata Nne, hivyo CCM itaunda Halmashauri ya Nyamagana.

Updates:Jimbo la Tarime vijijini, mkoani Mara: Mgombea wa CHADEMA, Heche John Wegesa ameibuka kidedea kwa kupata kura 47,249, huku akifuatiwa kwa karibu na Kangoye Christopher Ryoba wa CCM aliyepata kura 42325.

Updates:Jimbo la Chato, mkoani Geita: Mgombea wa CCM, Dr. Kalemani Matogolo Medard ameibuka mshindi kwa kupata kura 78,817 akifuatiwa na Lukanima Benedicto Kulwizira wa CHADEMA aliyepata kura 32,513.

Updates:Mgombea wa CCM katika jimbo la Ilala, jijini Dar es salaam, Azzan Mussa Zungu ameibuka kidedea kwa kupata kura 35,818 dhidi ya kura 32,533 za Muslim Haiderali Hassanali wa CHADEMA

Update: Mgombea ubunge jimbo la Kasulu mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Moses Machali amepoteza jimbo hilo, ameshindwa na Mgombea wa CCM Daniel Sanze.
-Amepata kura 22,512 na mshindi Daniel wa CCM amepata kura 25,336
 
Updates:Matokeo ya ubunge Iringa Mjini kutangazwa kesho baada ya kuchelewa kupatikana kwa matokeo ya kituo cha Kata ya Ruaha.

Updates:Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183.

Updates:Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407

Updates: Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665

Updates:Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480

Updates:Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614.

Updates: Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702

Updates:Wiliiam Lukuvi ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge toka tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534

Updates:Jimbo la Mtama: Nape Nnauye wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa Chadema, aliyepata kura 13918
 
Updates: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215

Updates:Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347

Updates: Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539
Updates:Jimbo la Ilemela jijini Mwanza Angelina Mabula  wa  chama  cha Mapinduzi CCM ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Hainess Kiwia kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa kukitetea kiti chake

Updates:Mtwara mjini Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa kukitetea kiti chake

Updates:Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966.

Updates:Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894

Updates:Jimbo la Kigoma Mjini: Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 31546, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Amani Kaburou wa CCM, aliyepata kura 16344

Updates:Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12580

Updates:Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578

Updates:Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649

Update: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.

Upadate: Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini.

Update:  Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini

Jimbo la Serengeti
Marwa Ryoba (Chadema) amengazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chadema katika jimbo la Serengeti.Jimbo  hilo  lilikuwa  chini  ya  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe
 
Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete wa CCM, aibuka mshindi katika Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kwa jumla ya kura 52695, dhidi ya Mang’unda Torongei wa Chadema aliyepata kura 23470

Jimbo la Moshi Mjini
Japhary Michael wa Chadema ameshinda kwa kura-51647, huku mpinzani wake Davies Mosha wa CCM akipata kura-26920

Jimbo  la  Bunda
Wassira aangushwa!
Ni baada ya Esther Bulaya wa Chadema kuchukua Jimbo la Bunda KWA KURA 26207, huku Wassira kupata kura 17573.

Steven Wassira

Jimbo la Peramiho
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peremiho kwa tiketi ya CCM , Jenister Mhagama ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo

Jimbo  La  Arumeru Mashariki
Mgombea Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema , Joshua Nassari ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo

Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847

Jimbo la  Shinyanga
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi

Jimbo la Tandahimba
Katika jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani wa CUF ameshinda kiti cha ubunge kwa kura-55156, huku mpinzani wake mkubwa wa CCM, Shaibu Salimu Likumbo akipata kura-41088


Jimbo la Mbinga Mjini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Musoma Mjini
Ubunge: Vicent Nyerere(Chadema)  25,549  na Vedastus Mathayo(CCM) 32,836.

Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Musoma Mjini Vedastus Mathayo ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Mbinga Vijijini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Vijijini Martin Msuha ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Jimbo la Monduli
Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalanga ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo


Aggrey Mwanry

Jimbo la Siha
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.

Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).

Jimbo la Tunduma
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.

Jimbo Buyungu
Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934
 
Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041.

Christopher Chiza
Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.
 
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo

Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.

Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Juma Mwajombe amemtangaza Matiko kuwa mshindi katika Jimbo hilo

Jimbo la Lindi Mjini
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo

Matokeo Ya Uchaguzi: Mawaziri Watano wa Serikali Ya CCM Wang'oka

$
0
0
Mawaziri watano wa Serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi majimboni mwao, sambamba na wagombea wengine maarufu wa Bunge lililopita baada ya matokeo ya kura zilizopigwa Jumapili kuanza kutangazwa jana.

Mawaziri hao wanaungana na wabunge wengine maarufu wa Bunge la Kumi walioshindwa kutetea majimbo yao, wakiwamo wa kambi ya upinzani ambao wameangushwa na wagombea wa CCM.

Pia wamo mawaziri wa zamani wawili, Cyril Chami na Omary Nundu walioanguka kwenye uchaguzi, kwa mujibu wa matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema jana kuwa itakamilisha kazi ya kutangaza matokeo yote keshokutwa.

Mawaziri walioanguka kwenye uchaguzi huo ni Steven Wasira, Christopher Chiza, Aggrey Mwanri, Dk Steven Kebwe na Anne Kilango.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana, Wasira, kada maarufu na mwanasiasa mkongwe aliyekuwa akitetea Jimbo la Bunda, alijikuta akiangushwa na mwanasiasa kijana, Ester Bulaya, ambaye alihamia Chadema baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake.

Wasira, ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo na Chakula, alianza mchakato wa uchaguzi mwaka huu kwa kuomba ridhaa ya CCM agombea urais, lakini hakupitishwa. Bulaya, ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum (CCM), alipata kura 28, 508 na kumuacha mbali waziri huyo mkongwe aliyepata kura 19, 126.

Mwingine aliyeanguka ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwezeshaji na Uwekezaji, Christopher Chiza ambaye ameangushwa na Bilago Samson wa Chadema katika Jimbo la Buyungu. Waziri huyo alizidiwa kwa kura 104 baada ya Samson kupata kura 23,041 dhidi ya 22,934 za Chiza.

Lakini hali haikuwa hivyo kwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri kwenye Jimbo la Siha. Waziri huyo alizidiwa kwa zaidi ya kura 4,100 na mpinzani wake kutoka Chadema, Dk Godwin Mollel aliyepata kura 22,746.

Katika Jimbo la Serengeti, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe pia alijikuta akipoteza nafasi ya kurudi bungeni kwa kura alipoangushwa na Marwa Ryoba wa Chadema. Dk Kebwe alipata kura 39,232, akiwa amezidiwa na mpinzani wake kwa zaidi ya kura 820.

Anne Kilango, ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu mwaka 2013 baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyosababishwa na kashfa ya Operesheni Tokomeza, ameangushwa na mgombea wa Chadema, Naghenjwa Kaboyoko wa Chadema kwa tofauti ya kura 3,297.

Kilango alipata kura 15,539 wakati mgombea huyo wa Chadema alipata kura 18,836. Pia wabunge maarufu kama Vincent Nyerere (Musoma Mjini), James Lembeli (Kahama Mjini) na Kyisieri Chambiri (Babati Mjini) wameangushwa.

Nyerere, aliyekuwa akitetea kiti cha Musoma Mjini kwa tiketi ya Chadema, aliachwa mbali na mgombea wa CCM, Vedastus Mathayo aliyepata kura 32, 836 dhidi ya 25,549.43 za Nyerere.

Lembeli, ambaye alihamia Chadema muda mfupi baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake, aliachwa mbali na mfanyabiashara maarufu, Jumanne Kishimba aliyepata kura 47,553 dhidi ya kura 30,122 za Lembeli.

Read What Ne-Yo And Alicia Keys' Husband Said About Diamond Platnumz After His MTV EMA Winning.

$
0
0

American music star Ne-Yo has joined various international music celebs to congratulate Tanzania's Diamond Platnumz for his wining as best worldwide act: Africa/India at the 2015 MTV Europe Music Awards which was staged last night in Milan, Italy. Ne-Yo who has recorded a song with Diamond which is expected to drop soon took to instagram to write ....."Congrats my homie @Diamondplatnumz for winning best worldwide act at the MTV EMAs, keep being great let's go em' my guy"


Mabula Ashinda Ubunge Jimbo la Nyamagana..Amgaragaza Vibaya Ezekiel Wenje

$
0
0
By Louis Kolumbia/Sauli Giliard Mwananchi Digital
Dar es Salaam.  Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula ametangazwa mshindi wa mbio za ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kwa kupata kura 81, 170 dhidi ya mbunge anayemaliza muda wake, Ezekiel Wenje (Chadema) aliyepata kura 79, 280.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Nyamagana, Peter Mainya, amesema jumla ya wagombea saba walichuana kuwania nafsi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa Nyamagana.

Mainya amesema, ushindi wa Mabula umetokana na msingi uliowekwa na chama chake katika matokeo ya uchaguzi wa udiwani ambapo kati ya Kata 18 zinazounda jimbo hilo, CCM imeweza kujinyakulia Kata 14 huku Kata nne zikichukuliwa na Chadema.

“Kutokana na msingi huo, Stanslaus Mabula ameweza kupata kura 81,170. Hivyo basi, kwa mamlaka niliyopewa, namtangaza Stanslaus Mabula kuwa ndiye mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Nyamagana” alisema Peter Mainya.

Ezekiel Wenje anakuwa mbunge wa pili wa upinzani kupoteza kiti chake jijini Mwanza baada ya Highness Kiwia aliyekuwa anatetea kiti chake cha ubunge katika  jimbo la Ilemela kuangushwa na Anjela Mabula katika matokeo yanayoashiria kurejea kwa utawala wa CCM katika siasa za Mwanza.


Parents, This is What your Daughters Were Doing over the Weekend, Shocking PHOTOs.

$
0
0

While majority of parents are busy warming up their beds, their daughters are wasting their lives in clubs in the name of partying and having a good time.

The way they dress to these clubs leaves more questions than answers and they some-times make twilight girls look like saints.

Just check out the photos below.



Joyce Kiria Alalamika Mmewe Kushindwa Ubunge Kumemkosesha Nyumba Nzuri na Shopping UK

$
0
0
Kupitia account yake ya Instagram, Joyce Kiria amelalamika mumewe kushindwa ubunge na Maghembe kumemkosesha yeye kupata nyumba nzuri na shopping za Ulaya.

Mrekebishatabia
Joyce ni Mdada niliyeamini anaweza kuwa mfano bora kwa jamii kutokana na kazi mbali mbali alizofanya na kujitolea kwa wananchi...nilimwona kama shujaa na mwanamke ambaye hata angesimama kugombea jimboni peke yake angepita bila kupingwa. Nilikuwa na picha ya mwanamama Fulani wa nguvu ambaye ndani ya miaka michache ijayo Tanzania ingeheshimika kupitia yeye.
Lakini nachelea kusema amejiharibia sana mambo mengi wakati huu wa uchaguzi ni pamoja na kutoa lugha chafu mitandaoni akijua kabisa mumewe anagombea vijijini ambako watu hujiheshimu.

Sasa nikajua labda ana uchungu na wananchi ndo maana alikuwa vile kuumbe anawaza safari za ulaya? Yaani kusema ukweli nimekwazika na nahisi aibu kama mimi ndo Joyce. Na siamini nilichokisoma kutoka kwake. Uchaguzi huu umenifanya nimfahamu Joyce vema....na tulisema kuna maisha baada ya uchaguzi...nitaendelea na wengine!!!

CCM Wailalamikia tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)

$
0
0
Na Mhamed khamis Zanzibar. 

Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar kimesema hakina imani na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uendeshaji nzima wa uchaguzi. 

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa Naibu katibu mkuu CCM Bwana Vua Ali Vuai amesema baadhi ya maeneo mawakala wa Chama chao walinyimwa vitamulisho jambo ambalo limekifanya chama hicho kutokuridhika na utaratibu huo. 

Amesema siku moja kabla ya uchaguzi walifika tume ya uchaguzi kuhakiki vitambulisho vya mawakala wao wote na vilikuwepo. 

Amesema cha kushangaza ni kuwa siku ya kura vitambulisho vya mawakala hao havikuonekana wala hakujulikana nani alivichukua

"Kutokana na hali hii tunakosa imani na ZEC " alisema Vuai.
ANGALIA VIDEO HAPA:

Orodha ya Majimbo ambayo CCM Wameyapoteza Mpaka Sasa

$
0
0
1.Monduli
2.Simanjiro
3.Same Mashariki(Mama Kilango)
4.Siha
5.Bunda Mjini(kwa Wasira)
6.Arumeru Magharibi-hili Jimbo bado liko CCM
7.Jimbo la Christopher Chiza(huko mkoa wa Kigoma)
8.Tanga Mjini
9.Babati Mjini
10.Babati vijijini
11.Tandahimba
12.Muleba kusini(sina uhakika sana)
13.Moshi vijijini
14.Tunduma
15.Mtwara mjini
16.Bukoba Mjini(confirmed)
17.Tarime vijijini(John Heche kashinda)
18.Tarime mjini
19.Mwanga(sina uhakika sana).
20.Serengeti
21.Sengerema
22.Kaliua
23.Ndanda
25.Kigoma mjini
26.Rorya
27.Ukonga

Morogoro tumechukua majimbo mawili nitayaongeza soon.


Orodha inaendelea,ongeza na mengine niliyoyasahau.

By by Salary Slip/JF

Kwanini UKAWA Hamtoi Taarifa Kwa Umma Jinsi Hali ya Majimbo ilivyo?

$
0
0
Ni wazi Chama Cha Mapinduzi kimejipanga katika kutoa taarifa. Tumeona J. Makamba akitaja majimbo yaliyovunwa na chama hicho. 

Lakini kwa UKAWA mambo ni tofauti na ni wazi Afisa habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, umeshindwa kazi, Makene ameshindwa hii kazi? (iwapo Makene ni wa chama sio wa UKAWA lakini kwa ukubwa wa CHADEMA ndani umoja huu, ni vema Makene akatoa idadi ya majimbo na maendeleo ya majimbo mengine ili wafuasi wao wawe updated).

Kwa sasa wafuasi wa UKAWA hawana cha kujibu kwa vile hawana taarifa za jumla iwapo vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti, lakini sio kwa utaratibu wa kufanya watu wapate summation.

Wabunge na Watu Maarufu Waliopoteza na Kushindwa Kupita Katika Ubunge Mpaka Sasa ni Hawa Hapa

$
0
0
Baadhi ya Wabunge na watu maarufu waliopoteza ama Kushindwa kupata kura za kutosha kushinda jimbo hawa Hapa:

Julius Mtatiro CUF,
Omari Nundu CCM,
Aggrey Mwanri CCM,
Anna Kilango Malecela CCM,
Augustino Lyatonga Mrema TLP,
Namelock Sokoine CCM,
Ezekiel Wenje CDM,
Moses Machali ACT,
Jerry Slaa CCM,
Didas Masaburi CCM,
Vicent Nyerere CDM,
Ole Sendeka CCM,
Cyrill Chami CCM,
Kiwia CDM,
Mkosamali NCCR MAGEUZI,N.K
Wasira

Augustine Mrema Ndio Basi Tena ..Mbatia atwaa Vunjo, Komu mshindi Moshi Vijijini

$
0
0
By auli Giliard/Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Tume ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza James Mbatia wa NCCR Mageuzi kuwa mbunge mteule wa jimbo la Vunjo huku kada wa Chadema, Anthony Komu naye akiibuka mshindi katika jimbo la Moshi Vijijini lililokuwa linaongozwa na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Dk. Cyril Chami kupitia CCM.

Akitangaza matokeo ya majimbo hayo mawili mkoani Kilimanjaro kuamkia leo, msimamizi Fulgence Mponji, amesema Mbatia amepata kura 60,187 akiwashinda wapinzani wake; Innocent Shirima wa CCM aliyepata kura 16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 6,416.

Kutokana na matokeo hayo,  Mrema ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo huku wananchi wa eneo hilo wakiendeleza historia ya kutomchagua mbunge wa chama kimoja kwa vipindi viwili tangu kurudi kwa mfumo wa siasa za vyama vingi.

Kwa upande mwingine, CCM imepoteza jimbo la Moshi Vijijini kupitia kwa mgombea Cyril Chami na kurudi tena upinzani baada ya kada wa Chadema, Anthony Komu kutangazwa mshindi. Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa Viwanda na Biashara hakuwepo wakati NEC wa kusaini kuonyesha kuwa amekubali matokeo.

Kwa mujibu wa Mponji, mbunge mteule wa Moshi Vijijini, Komu amepata kura 55,813 huku Dk Cyril Chami akijikusanyia kura kura 24,415.


Instagram waifungia akaunti ya Idris Sultan, aeleza kilichosababisha

$
0
0
Instagram imeifungia akaunti ya mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan.

Idris ameimbia Bongo5 kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kuvunja masharti ya mtandao huo.

Amesema anadhani sababu za kufungikiwa kwa akaunti yake ni kutokana na kupost kipande cha video kutoka kwenye filamu ya The Interview iliyowahi kupigwa marafuku katika baadhi ya nchi.

Nafikiria labda kutokana na ile part, ndio kitu pekee kilichosababisha kwasababu hakuna ukiukwaji mwingine wowote niliofanya,” amesema.

Idris amesema kitu pekee kinachoweza kusababisha mtu kufungiwa akaunti ya mtu bila taarifa ni pale anapoweka picha za utupu ama kama mtumiaji mwingine ametoa malalamiko kuhusu akaunti husika.

Anasema kwa sasa kila anapotaka kuingia kwenye akaunti hiyo anaambiwa ‘you account has been disabled.’

Hata hivyo amesema mchakato wa kuirejesha unaendelea na anaamini ndani ya wiki moja itakuwa imereja. Instagram wamewahi kuifungia akaunti ya Rihanna baada ya mrembo huyo kupost picha za utupu.

Silaha za Kijadi Zakamatwa Shinyanga..Inasemekana ziliandaliwa Kwa Ajili ya Kufanya Vurugu Wakati wa Uchaguzi

$
0
0
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidiziJustus Kamugisha akionesha moja ya mapanga yaliyokamatwa na jeshi la polisi yanadaiwa kuwa yaliandaliwa kwa ajili ya kufanya vurugu wakati na baada ya uchaguzi mkuu 2015

Vipande vya nondo na mapanga yanayodaiwa kuwa ni ya mgombea ubunge jimbo la Solwa mkoani Shinyanga Jeremia Mshandete wa Chadema, ni miongoni mwa silaha za jadi zilizokatwa ambazo zinadaiwa kuwa ziliandaliwa kwa ajili ya kufanya vurugu wakati na baada ya uchaguzi mkuu 2015.
Mawe, viroba na makombeo yaliyokamatwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa ndani ya begi na vingine kwenye maboksi kwa ajili ya uharifu katika uchaguzi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi Justus Kamugisha akionesha bendera ya CCM iliyochanwa mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akionesha makombeo yanayoadaiwa kuwa yalilenga kutumika kufanyia vurugu kwenye jimbo la Solwa

Wananchi Wachomwa Moto Ofisi ya Kata Jijini Dar Baada ya Kucheleweshewa Matokeo

$
0
0
Ofisi ya kata ya Sandali ya Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam imechomwa moto baada ya wananchi kudai kutangaziwa matokeo,hali iliyozusha hofu na jeshi la polisi kupiga kambi eneo hilo kwa ajili ya ulinzi,ambapo jeshi la zimamoto limefanikiwa kuzima moto huo.

Batuli, Wema Hawaivi Tena!

$
0
0
Mwisho wa reli? Urafiki wa mastaa wawili wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ unadaiwa kupoteza mwelekeo baada ya wawili hao kusemekana hawaivi tena kama ilkivyokuwa huko nyuma walipoanza Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Habari kutokwa kwa mnyetishaji wetu wa kuaminika zilieleza kuwa, hali imekuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo kwani kila wakati walikuwa pamoja huku wakivaa sare lakini sasa hakuna tena kitu kama hicho.

Baada ya kutonywa ubuyu huo, gazeti hili lilimtafuta Wema ambapo alifunguka: “Watu wanapenda kuniona nikiongozana na mtu wakati wote, jambo ambalo si rahisi. Mimi naona tupo sawa na hakuna kitu chochote kati yetu,” alisema Wema.

Chanzo:GPL

LIVE: Matokeo Rasmi ya Urais kwa Mujibu wa NEC (Official Results) - Uchaguzi Mkuu 2015

$
0
0
Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Urais kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa.

Tembelea  ukurasa huu mara kwa mara  kwa updates zaidi

Jimbo  la  Fuoni-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM): 956
Lowassa (CHADEMA):420

Jimbo  la  Kikwajuni-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):6,317
Lowassa (CHADEMA): 3669

 Jimbo  la  Mpanda Vijijini-Katavi

Magufuli (CCM):37,321
Lowassa (CHADEMA): 12,791

Jimbo  la  Mchinga-Lindi

Magufuli (CCM):63,648
Lowassa (CHADEMA):12,636

Jimbo  la  Mwela-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):6430
Lowassa (CHADEMA):5865


  ==================================
October 27, 2015 - Saa 3 Asubuhi

Jimbo  la  Chalinze

Magufuli (CCM):52,212
Lowassa (CHADEMA):21380

Jimbo  la  Chonga

Magufuli (CCM):1740
Lowassa (CHADEMA):3800
  
Jimbo  la  Chumbuni

Magufuli (CCM): 5096
Lowassa (CHADEMA): 4450

Jimbo  la Ileje

Magufuli (CCM):26,368
Lowassa (CHADEMA): 15,651

Jimbo  la Kijini

Magufuli (CCM): 2703
Lowassa (CHADEMA): 3351

Jimbo  la Kilindi-Tanga

Magufuli (CCM): 33,942
Lowassa (CHADEMA):12,123

Jimbo  la Korogwe Mjini-Tanga

Magufuli (CCM): 17,168
Lowassa (CHADEMA): 9034

Jimbo  la Kohani-Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):6,245
Lowassa (CHADEMA): 2689


Jimbo  la Lupembe-Njombe

Magufuli (CCM): 23,061
Lowassa (CHADEMA): 7,466

Jimbo  la Madaba-Ruvuma

Magufuli (CCM): 13,949
Lowassa (CHADEMA):4,735

Jimbo  la Masasi Mjini-Mtwara

Magufuli (CCM): 24,637
Lowassa (CHADEMA):16,778

Jimbo  la Mbeya Vijijini-Mbeya

Magufuli (CCM):62,662
Lowassa (CHADEMA):47,038

Jimbo  la Mkwajuni-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 4,686
Lowassa (CHADEMA): 3,314

Jimbo  la Momba- Mbeya

Magufuli (CCM): 28,978
Lowassa (CHADEMA):24,418

Jimbo  la Monduli-Arusha

Magufuli (CCM):11,355
Lowassa (CHADEMA): 49,675

Jimbo  la Mpendae- Mjini Magharibi

Magufuli (CCM):4,192
Lowassa (CHADEMA): 4,048

Jimbo  la Mwanga-Kilimanjaro

Magufuli (CCM): 25,738
Lowassa (CHADEMA):15,148

Jimbo  la Namtumbo-Ruvuma

Magufuli (CCM):44,061
Lowassa (CHADEMA): 23,039

Jimbo  la Newala Mjini-Mtwara

Magufuli (CCM): 21,269
Lowassa (CHADEMA):16,980

Jimbo  la Newala Vijijini-Mtwara

Magufuli (CCM): 29,799
Lowassa (CHADEMA): 13,958

Jimbo  la Siha-Kilimanjaro

Magufuli (CCM): 18,252
Lowassa (CHADEMA):22,572

Jimbo  la Solwa-Shinyanga

Magufuli (CCM): 66,096
Lowassa (CHADEMA): 23,510

Jimbo  la Tandahimba

Magufuli (CCM): 49,098
Lowassa (CHADEMA):46,288
  
Jimbo  la Tumbatu-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 5,720
Lowassa (CHADEMA):  3,967

Jimbo  la Igalula-Tabora

Magufuli (CCM): 28,747
Lowassa (CHADEMA): 8,393

Jimbo  la Ulanga-Morogoro

Magufuli (CCM):32,297
Lowassa (CHADEMA):20,489

Jimbo  la Wawi-Kusini Pemba

Magufuli (CCM): 1,748
Lowassa (CHADEMA): 5,216

Jimbo  la Ziwani-Kusini Pemba

Magufuli (CCM): 592
Lowassa (CHADEMA):6,067

Jimbo  la Ole-Kusini Pemba

Magufuli (CCM):681
Lowassa (CHADEMA):5,251

Jimbo  la .....-Kaskazini Unguja

Magufuli (CCM): 5,592
Lowassa (CHADEMA): 1,019

===============================
Oktoba 26, 2015 - Saa 4 asubuhi:

Jimbo la Makunduchi:

Magufuli (CCM): 8,406
Lowassa (CHADEMA): 1,769

Jimbo la Paje:

Magufuli (CCM): 6,035
Lowassa (CHADEMA): 1,899

Jimbo la Lulindi:

Magufuli (CCM): 31,603
Lowassa (CHADEMA): 11,543

October 26, 2015 - Saa 11 Jioni
Jimbo la Mkoani:

Magufuli (CCM): 3341
Lowassa (CHADEMA): 7368

Jimbo la Ndanda:

Magufuli (CCM): 33699
Lowassa (CHADEMA): 19017

Jimbo la Kiwengwa:

Magufuli (CCM): 3317
Lowassa (CHADEMA): 1104

Jimbo la Nsimbo:

Magufuli (CCM): 31413
Lowassa (CHADEMA): 6042

Jimbo la Mtambile:

Magufuli (CCM): 902
Lowassa (CHADEMA): 5875

Jimbo la Donge:

Magufuli (CCM): 5592
Lowassa (CHADEMA): 1019

Jimbo la Kiwani:

Magufuli (CCM): 1661
Lowassa (CHADEMA): 4229

Jimbo la Chambani:

Magufuli (CCM): 818
Lowassa (CHADEMA): 5319

Jimbo la Kibaha Mjini:

Magufuli (CCM): 34604
Lowassa (CHADEMA): 25448

Jimbo la Bumbuli:
Magufuli (CCM): 35310
Lowassa (CHADEMA): 7928

October 26, 2015 - Saa 2 Usiku
Jimbo la Gando:

Magufuli (CCM): 881
Lowassa (CHADEMA): 5903

Jimbo la Kisarawe:

Magufuli (CCM): 24086
Lowassa (CHADEMA): 13093

Jimbo la Kojani:

Magufuli (CCM): 1561
Lowassa (CHADEMA): 9982

Jimbo la Mbinga Mjini:

Magufuli (CCM): 29295
Lowassa (CHADEMA): 11695

Jimbo la Mgogoni:

Magufuli (CCM): 710
Lowassa (CHADEMA): 6506

Jimbo la Mkinga:

Magufuli (CCM): 23798
Lowassa (CHADEMA): 15142

Jimbo la Moshi Mjini:

Magufuli (CCM): 28909
Lowassa (CHADEMA): 49379

Jimbo la Mtambwe:

Magufuli (CCM): 428
Lowassa (CHADEMA): 6937

Jimbo la Nanyamba:

Magufuli (CCM): 24904
Lowassa (CHADEMA): 16992

Jimbo la Peramiho:

Magufuli (CCM): 32505
Lowassa (CHADEMA): 11291

Jimbo la Wete:
Magufuli (CCM): 958
Lowassa (CHADEMA): 5119

Jimbo la Singida Mjini

Kura: 56,558

Magufuli (CCM): 36,035

Edward Lowassa (Chadema): 19,007

Jimbo la Lindi Mjini
Kura: 38,992
Magufuli (CCM): 21,088
Edward Lowassa(Chadema): 17,607

Jimbo la Njombe Mjini
Kura: 55,772
Magufuli (CCM): 33,626
Edward Lowassa(Chadema):20,368

Jaji Lubuva amesema kuwa matokeo ya majimbo mengine ambayo yatakuwa tayari yatatolewa kesho  saa  tatu  asubuhi.

Ridhiwani Asema Hana Chuki na Wasiompigia Kura

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amesema hana chuki kwa wale ambao hawakumpigia kura kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili kwani hizo ni changamoto za uchaguzi.

Aliyasema hayo jana kwenye Uwanja wa Miembe Saba mjini Chalinze wakati wa mkutano wa hadhara wa kuwashukuru Wanachalinze kwa kumchagua kuwa mbunge kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili.

Ridhiwani alisema licha ya baadhi ya maeneo kutompigia kura za kumchagua kuwa mbunge, lakini atawatumikia wananchi wote bila ya kujali kama walimpigia kura au la kwani kila mtu ana haki ya kumpigia kura mgombea yeyote anayempenda.

Nawashukuru wananchi wote walionipigia kura na hata wale ambao hawakunipigia kura kwani hiyo ndiyo demokrasia nitahakikisha nawahudumia wananchi wote bila ya kuwabagua nitahakikisha napeleka maendeleo kwa watu wote wa jimbo hili,” alisema Ridhiwani.

Alisema kutopigiwa kura kwa wingi siyo sababu ya kuwagawa wananchi kwani hizo ni changamoto za uchaguzi ambao unakuwa na mambo yake ambapo baadhi ya maeneo walipiga kura kwa kuzingatia ukabila.

Sitakuwa na chuki wala hasira kwa wale ambao hawakunipigia kura nitashirikiana nao katika suala la maendeleo ili kuhakikisha jimbo letu linakuwa na maendeleo na wananchi wanaboresha maisha yao ili yasonge mbele,” alisema Ridhiwani.

Aidha, alisema atahakikisha Mji wa Chalinze ambao umekuwa Halmashauri ya Mji Mdogo unajengwa kwa kuwekewa huduma muhimu ili wananchi waboreshe biashara zao hasa ikizingatiwa kuwa mji huo ni wa kibiashara.

Moja ya mambo nitakayoyafanya ni kufanya Chalinze kuwa makao makuu ya Halmashauri hiyo na baadaye kuwa wilaya kwani mchakato unaendelea na tunaamini baada ya muda tutapewa wilaya hivyo tutaweza kujitegemea na kujiimarisha kiuchumi,” alisema Ridhiwani.

Alibainisha kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kwani kukichagua Chama Cha Mapanduzi CCM ni kuchagua maendeleo hivyo wasubiri kuona jinsi serikali mpya itakavyofanya kazi kwani kwao ni kazi tu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Chalinze, Nasa Karama alisema mbunge huyo ameonesha uwezo mkubwa kwani kwa kipindi alichochaguliwa cha mwaka mmoja na miezi mitatu amefanya mambo makubwa ambapo alitumia ziadi ya Sh bilioni moja na zaidi miradi ya maendeleo.
Viewing all 104766 articles
Browse latest View live




Latest Images