Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live

Lowassa: Awamu ya Pili ya Safari ya Kwenda Ikulu inakuja

$
0
0
Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema awamu ya pili ya safari yake ya kuelekea Ikulu ndio kwanza imeanza na kuwataka watu wote wanaomuunga mkono kutokata tamaa.

Lowassa, ambaye ameshika nafasi ya pili katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano akiweka rekodi ya kukusanya kura milioni 6.07 ambayo ni rekodi kwa mgombea wa upinzani, alitoa kauli hiyo jana mchana katika hafla ya chakula cha mchana ya kuishukuru timu yake ya kampeni iliyofanyika Kawe, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Ukawa, wanahabari na familia yake.

“Nimefarijika sana, asanteni kwa msaada mlionipa, sina cha kuwalipa,” alisema waziri huyo mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne aliyeihama CCM na kujiunga na Chadema mwezi Julai.

“Ukweli ni kwamba kila mmoja alifanya kazi yake. Tujiandae kwa awamu ya pili na safari ndiyo imeanza,” alisema na kushangiliwa.

“Unaweza kuchelewesha bahati ya mtu, lakini hauwezi kuiondoa,” aliongeza.

Hata hivyo, Lowassa hakueleza awamu ya pili itahusisha mambo gani.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo, Lowassa amezungumza na vyombo vya habari mara mbili, mara ya mwisho akieleza jinsi alivyowasilisha pingamizi lenye hoja tatu kuhusu mwenendo wa uchaguzi kwa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva ambalo liligonga mwamba.

Katika tamko lake, Lowassa alikuwa akipinga matokeo ya kura za urais yaliyokuwa yakitangazwa na NEC akidai kuwa si halisi na kuitaka isitishe kutangaza, lakini tume hiyo haikueleza lolote na badala yake iliendelea kutangaza matokeo ya majimbo na baadaye mshindi wa urais.

Mambo hayo matatu yaliyowasilishwa NEC ni kupunguzwa kwa kura zake, kuongezewa kura kwa mgombea wa CCM na kutangazwa matokeo batili kwa wagombea wa Ukawa.

Lowassa aliyeanza kwa kuwatambulisha watu wake wa karibu waliomshauri masuala muhimu na nyeti katika kampeni, akiwemo waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alizungumza kwa kifupi, akitoa mfano wa jinsi majeshi ya ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika yalivyorudi nyuma kujipanga baada ya kushindwa.

Muda mfupi kabla ya Lowassa kueleza hayo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliufananisha Uchaguzi Mkuu na vita, akisema kulikuwa na njama za makusudi za kuhakikisha Lowassa hapati ushindi.

Alisema wagombea ubunge kutoka vyama vinavyounda Ukawa vya NCCR-Mageuzi, Chadema, NLD na CUF, waliibiwa kura na ushindi kupewa wagombea wa CCM.

Mbowe alisema kwa kuwa hawawezi kupinga matokeo ya urais mahakamani, watafungua kesi za kupinga matokeo ya ubunge.

“Tunachofanya, tunarudi nyuma, tunajipanga kukata rufaa kupinga matokeo katika majimbo zaidi ya 30,” alisema Mbowe.

“Wagombea wetu waliokuwa wabishi na kupigana kwelikweli walitangazwa washindi, lakini kuna majimbo ambayo wagombea wetu waliporwa ushindi waziwazi kabisa. Kwa kuwa ubunge unapingwa mahakamani tutafanya hivyo,” alisema Mbowe.

Miongoni mwa majimbo ambayo matokeo yake yalikuwa na ubishi ni Nyamagana, ambako mbunge maarufu wa Chadema, Ezekiah Wenje alishindwa na mgombea wa CCM,Stanslaus Mabula baada ya mvutano uliochukua muda mrefu. Pia mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila wa Kigoma Kusini aliangushwa baada ya matokeo kuibua mzozo mkali uliosababisha polisi kuingilia kati.

Mbowe pia alisema kuwa wanahamishia nguvu Zanzibar kuungana na mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kudai haki yake.

Mbowe alisema kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo kina mkanganyiko mkubwa na kusisitiza kuwa kuanzia wiki ijayo Ukawa itapiga kambi kwenye visiwa hivyo kuhakikisha haki inatendeka.

Baadhi ya viongozi wa Ukawa waliohudhuria hafla hiyo ni makamu mwenyekiti wa Chadema –Bara, Profesa Abdallah Safari, mwenyekiti wa NCCR na mbunge mteule wa Vunjo, James Mbatia na kaimu katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu.

Source:Mwananchi

Chadema Wakanusha Habari Zinazoendea Mitandaoni Kuwa Wameenda ICJ na ICC Kuishitaki CCM

$
0
0
Ziko habari zimezushwa, kuenezwa na sasa zinakuzwa kuwa mgombea urais wa CHADEMA na chama kwa ujumla kimefungua shauri Mahakama za Kimataifa, kuhusu ubakwaji wa demokrasia na hujuma dhidi ya Watanzania uliofanyika kwenye Uchaguzi (uchafuzi?) Mkuu uliofanyika Oktoba 25.
Itoshe tu kusema kuwa hadi kwa hatua ya sasa habari hizo si za kweli. Ni uzushi.
Watawala, wanaotuhumiwa kupoka haki ya Watanzania ya kuchagua viongozi wanaowataka, wanajua dhambi waliyowafanyia wananchi ni sawa na ile hadithi ya Mzee Mvuvi kwenye Vitabu vya Alfu Lela Ulela, aliyefungulia jini kutoka kwenye chupa. Dhambi inawawinda. Mzimu wa walichokifanya unawaandama. Maana safari hii ukatili (kuvuruga uchaguzi) ulikuwa wazi wazi mno.
Wanajaribu kuchokonoa kujua ukimya wa Ndugu Edward Lowassa, kama mgombea chaguo la watu, CHADEMA, UKAWA na wapenda mabadiliko unaweza kuwa na kishindo gani! ICJ, ICC au wapi hasa!

Hivyo wanatunga tunga mambo na kusambaza wakitaka kupima hisia, fikra za wanamabadiliko waliotapakaa nchi nzima wakilia kilio cha kudhulumiwa haki katika uchaguzi, zinawaza nini! Maana hata wao wanashuhudia namna nchi ilivyokumbwa na msiba tangu walipotangaza matokeo yasiyooana na uhalisia wa hisia za wapiga kura na matakwa ya waliyo wengi katika demokrasia.
Tumelazimika kufafanua kuhusu uvumi huo kwa sababu umezidi kuenezwa kiasi cha vyombo vya habari kuanza kuulizia ukweli wake.
Baadhi ya watu waliotajwa kwa majina katika uvumi huo wako hapa nchini, wakiendelea na majukumu, hususan vikao vya Kamati Kuu ya dharura, ambayo imekuwa ikikutana jijini Dar es Salaam.
Chama kilipoandika barua kwenda Jumuiya ya Kimataifa, kuhusu hatari iliyokuwa inawekwa na watawala katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kupitia kauli za vitisho, matendo yao ya kujiandaa kuharibu uchaguzi, BVR, mfumo wa ujumlishaji matokeo n.k, tuliutaarifu umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari. Kwa sababu si siri.

Ukifanywa uamuzi mwingine wowote ule kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania kupigania haki yao iliyoporwa katika uchaguzi mkuu, umma wa Watanzania ambao ndiyo wenye mamlaka katika nchi, utashirikishwa.

Makene

Mikwara ya Marais wa Tanzania Mara Waingiapo Madarakani

$
0
0
Binafsi sikuwepo wakati Nyerere anaingia madarakani, ila hawa wengine kidogo nina kumbukumbu.

Mzee Mwinyi kipindi anaingia madarakani aliazimia kuwafyeka wabadhirifu wote waliopo serikalini, mpaka akapewa fagio la chuma kama ishara ya kuhakikisha wala rushwa na wabadhilifu hawamzidi nguvu. 1995 wakati anatoka madarakani nchi ilikuwa na wala rushwa na wabadhilifu maradufu ya alipoingia, madawa ya kulevya , maana ukwepaji wa kodi na wizi wa rasilimali za nchi hii ulishamili sana kipindi cha mwinyi.

Ben Mkapa aliingia na madarakani akiwa mnyenyekevu kupita maelezo, nakumbuka alishawahi kutoa zuria alilotandikiwa kuonyesha kwamba alikuwa akijishusha na kutotaka makuu, vilevile alipiga marufuku watangazaji wa redio tanzania waliokuwa wameanza kumwita mtukufu kila wanapomtaja. Aliwapachika jina mawaziri wake kuwa ni askari wa myamvuli kuonyesha kwamba amechagua baraza bora kabisa kuwahi kutokea. Matokeo yake yaliyowakuta mawaziri wake wake akina prof mbilinyi, idd simba na wengine hayasemeki. Mkapa ndiye raisi aliyetumia ubabe kutawala, alitoka madarakani akiwa jeuri na mwenye dharau, kipindi chake watu wengi waliuwa na polisi kwa kisingizio cha fujo.

Kikwete yeye alijigamba sana kufunga wala rushwa na alijitanabaisha kuwa uraisi wake hana ubia na mtu . Matokeo yake mikataba mibovu na rushwa kubwa zimeibukia kwake,

Sasa Magufuli ameanza ni mikwara kibao, unadhani ni nini kitatokea?

By gollocko./Jamii Forums

Haya Ndiyo Matamanio ya Watanzania Kwa Dk Magufuli Baada ya Kushinda Urais

$
0
0
Siku moja baada ya Rais Mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kukabidhiwa cheti chake kuwa ndiye mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wananchi wakiwamo wa kada mbalimbali wameelezea hisia zao na matanio yao kuona atatekeleza ahadi alizotoa kwenye mikutano yake ya kampeni.

Dk Magufuli (CCM) alitangazwa mshindi wa urais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25 kwa kupata kura 8,882,935 huku mpinzani wake, Edward Lowassa (Chadema) akiambulia 6,728,480. Wagombea wanane walikuwa wakiwania kiti hicho kupitia vyama vingine vya siasa.

Wasomi

Mhadhiri wa Chuo cha Saut Tawi la Mtwara, Michael Okoda alisema anafurahi kwa kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na utulivu na kwamba Dk Magufuli anatakiwa kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wakati akijinadi kwao kwenye mikutano ya kampeni.

Alizitaja baadhi ya ahadi hiyo kuwa ni elimu bure, afya na ajira kwa kuwa walioshiriki kumpigia.

Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya Vyuo Vikuu na Vyuo Vishiriki (Asas), Paul Losolutie, alisema anataka kuona mahakama ya wezi na mafisadi inaundwa nchini na Tanzania inakuwa nchi ya viwanda kama alivyoahidi Magufuli kwenye kampeni.

Azaki

Mratibu wa Taifa wa Taasisi ya Wanawake ya Ulingo, Dk Ave Maria Semakafu, alisema anaamini wanawake wengi wamefurahishwa na ushindi huo kwa sababu kwa umewezesha pia kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kuwa na Makamu wa Rais mwanamke, Samia Suluhu Hassan.

“ Tumefungua ukurasa mpya kwani miaka 20 ya tamko la Mkutano wa wanawake Duniani wa mwaka 1995 Beijing, tumekuwa na mrejesho mzuri kuhusu mwitikio wa Serikali kuweka ushiriki sawa wa nafasi za uongozi,” anasema Dk Semakafu .

Beatrice Jesta wa RRM, alisema wanachosubiri kwa sasa ni Dk Magufuli kuanza kuwasafisha wezi wa fedha za umma na kuijenga nchi katika mazingira ya umoja na mshikamano.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani mkoa wa Arusha (APET), Petro Ahham anasema uchaguzi umemalizika kwa amani katika maeneo mengi jambo ambalo ni la kujivunia kwa Watanzania.

“Nchi nyingine leo kungekuwa hakuna amani, lakini uchaguzi umekwisha kwa amani na sisi hapa Arusha amani imekuwa nzuri zaidi tunapongeza wadau wote kwa kufanikisha amani, ’’ anasema.

Wachambuzi

Prince Mwaihojo, mchambuzi wa masuala ya siasa mkoani Mbeya anasema ushindi wa Dk Magufuli umeinusuru nchi kuporwa na waroho wa madaraka.

Alisema Tanzania ya sasa inamhitaji kiongozi kama Magufuli ambaye alitangaza kwamba atawatumikia Watanzania wote na kuwaunganisha kuwa na umoja bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chaumma, Kayumbu Kabutale anasema kama Dk Magufuli hataweza kufanya mapinduzi katika mfumo wa CCM na kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni na kubaki kuwa ndoto.

Wananchi

Yusuph Mwikoki, mkazi wa Songea, amemtaka Dk Magufuli atimize ahadi alizotoa na asifanye kazi kwa mazoea kwa kuwa Watanzania wana matarajio makubwa katika uongozi wake.

Akitoa maoni yake, mkazi wa mtaa wa Mwambene wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Edson Chuma alisema ushindi wa Dk Magufuli ni kauli ya Watanzania wasiotaka kupelekeshwa kama ng’ombe.

Hamis Abdallah Ally, mkazi wa Maposeni Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma alisema anasubiri kuona Dk Magufuli akiwakamata na kudhibiti mafisadi na kurejesha imani kwa wananchi.

Kelvin Chale wa Manispaa ya Songea, alimtaka Dk Magufuli kuboresha mazuri ya Rais Jakaya Kikwete na kushugulikia kero za wananchi.

Neema Komu, mkazi wa Kibaha, Pwani alisema hana mpango wa kuandaa ada wala michango ya shule kwa watoto wake kwani anaamini mgombea aliyepita atafuta yote kama alivyoahid kwenye kampeni.

“Kwa sasa ninaandaa sare tu kwa mwanangu anayetarajia kuanza masomo mwakani kwani hatutakuwa na masuala ya ada,” alisema

Irine Nkya alisema : “Tunamtarajia Dk Magufuli afanye kazi kwa bidii, juhudi na maarifa huku akiwachukulia hatua kali watumishi wazembe kama alivyowaahidi Watanzania.”

Paul Shija, mkazi wa Urambo mkoani Tabora, alisema Rais Magufuli atekeleze ahadi kwa wananchi kwa kutatua kero zao kwa sababu ameonyesha ana uwezo wa kuwatumikia.

Mkazi wa mkoani Geita, Shaaban Jumanne alisema ana matarajio makubwa na Magufuli kwa kuwa wakazi wenzake uchumi wao mkubwa ni uchimbaji wa madini na hivyo atimize ahadi yake.

Masanja Maduhu alisema: “Dk Magufuli alivyopita kwao kuomba kura aliahidi kuwapa maeneo ya uchimbaji wananchi, sasa tunamuomba atimize ahadi yake.”

Mery Ndoshi wa Geita, alisema mji wao unakabiliwa na kero sugu ya kukosa maji safi na salama ambayo Magufuli wakati wa kampeni aliwaahidi kuitatua na kujenga vyumba vya madarasa.

Falesi Bunini, mkazi wa Kata ya Kwanga mkoani Mara, alisema angependa kuona Dk Magufuli akitekeleza ahadi ya kuwalipa wazee fedha za kujikimu kwa maisha na matibabu bure.

Joseph Haule mkazi wa kata ya Rwamlimi alikumbusha ahadi ya kukuza uchumi na kuhakikisha thamani ya shilingi inaongezeka ili kukabiliana na mfumo wa bei na maisha ya Watanzania kuzidi kuwa magumu.

Mkazi wa Pansiasi mkoani Mwanza, Celine Paul alisema tatizo la ajira kwa vijana ni kati ya mambo aliyoahidi kutatua..

Peter Mwita, mkazi wa Igoma, Mwanza alisema anatarajia Magufuli ataondoa migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima.

Juma Cosmas, mkazi wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga alisema anatarajia kuona viwanda vikifufuliwa, kuanzisha vipya na kuondolewa kwa tatizo la ajira.

Mkazi wa kata ya Kambarage Shinyanga, Amina Yusuph alisema anachotaka kuona ni kuboresha huduma za afya katika miji yote pamoja na upatikanaji wa dawa.

Naye Brayan Mshana alisema kama mwananchi asiyefungamana na upande wowote anakubaliana na matokeo na kikubwa Dk Magufuli atekeleze ahadi alizozitoa kwa wananchi.

Imeandikwa na Joyce Joliga, Lauden Mwambona, Rehema Matowo, Mussa Juma, Florence Focus, Sharon Sauwa, Aidan Mhando na Stella Ibengwe.



Katibu Mkuu Aisikitikia NCCR, Asema Historia itawahukumu...Na Ndicho Kinachowatokea Sasa

$
0
0

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe amesema kuwa alitabiri kwamba historia itawahukumu na ndicho kilichotokea.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Nyambabe alisema hana jipya la kuzungumza kwa sababu alishazungumza kuhusu mustakabali wa chama chao ndani ya Ukawa, huku akisisitiza namna ambavyo historia itawahukumu.

“Sina la kusema kwa sasa, nilizungumza sana kuhusu kinachoendelea ndani ya Ukawa. Nilisema historia itatuhukumu, niliona mbali, niliyoyazungumza hayajapitwa na wakati,” alisema.

Novemba, mwaka huu viongozi wa chama hicho akiwamo Makamu Mwenyekiti (Bara), Leticia Mosore, katibu mkuu, baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na viongozi wengine walizungumza na waandishi wa habari na kuonyesha shaka ya chama chao kuwa ndani ya Ukawa.

Katika mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Landmark, Dar es Salaam, viongozi hao walitoa tamko kwa kile walichodhani ni anguko la chama chao kuwa ndani ya Umoja huo wa Katiba ya Wananchi.

Akitoa tamko hilo, Mosore alisema kuwa miongoni mwa mambo waliyokubaliana katika umoja huo ni namna ya kujiendesha, ikiwamo kuunda kamati za kutatua matatizo kama Kamati ya Makatibu Wakuu, Kamati ya Ufundi na Kamati ya Wataalamu walizodai zimeshindwa kufanya kazi ipasavyo.

Alisema viongozi hao wameshindwa kuweka kanuni za uendeshaji na kuacha mambo yafanyike kiholela, kamati kushindwa kushughulikia migogoro baina ya vyama, kushindwa kuunda na kusimamia kamati za majimbo na kushindwa kufikia muafaka wa kuachiana majimbo.

Tamko hilo lililenga zaidi kulalamikia ufinyu wa majimbo 12 waliyopewa ikilinganishwa na majimbo 67 waliyosimamisha wagombea mwaka 2010 wakiwa wa kama chama kinachojitegemea.

Mosore pia alilalamikia kuwa licha ya chama chao kurudishwa nyuma, wanahujumiwa kwa sababu bado wanachama wa vyama vingine vilivyo ndani ya umoja huo walikuwa wanang’ang’ania kusimamisha wagombea kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano huo ulionyimwa baraka na chama ngazi ya Taifa, Nyambabe alizitaja kasoro nyingine kuwa ni kushindwa kukubaliana katika baadhi ya mambo aliyodai mwenyekiti wao amekuwa akiyafumbia macho, ikiwamo kushindwa kupata muafaka wa namna ya kuachiana wagombea udiwani.

Suala jingine alilolalamikia ni kushindwa kuonyesha na kukubaliana kila chama kitapata nafasi gani na ngapi iwapo Ukawa ungeshinda na kuunda Serikali, kushindwa kufuata utaratibu wa kumpata mgombea urais wa umoja huo na kuwapa umuhimu mkubwa wanachama kutoka CCM.

Nyambabe pia alilalamikia kutokuwa na timu ya kampeni ya umoja huo ambayo ingewasaidia wagombea wote na Chadema kuwa na nguvu kubwa katika umoja huo ikiwamo kutumia fedha inavyotaka.

Viongozi hao pia walitoa wito wa kumshauri Mwenyekiti wao, James Mbatia aitishe vikao vya kikatiba ili wajadiliane kuhusu hatima ya chama chao.

Mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye ameshindwa aliliambia gazeti hili kuwa hana la kusema juu ya madai hayo kwa sababu siyo msemaji wa chama hicho.

Alisema chama hicho kitakuwa na mkutano na waandishi saa tano asubuhi leo na majibu yote ya mustakabali wa chama yatatolewa.

Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alipopigiwa simu zote mbili zilikuwa zinaitwa bila majibu.

Katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita, chama hicho kilipata jimbo moja tu la ubunge la Vunjo ambalo ameshinda Mbatia. Kabla ya uchaguzi huo kilikuwa na majimbo manne ya Kigoma Kusini, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini na Muhambwe, lakini katika uchaguzi majimbo hayo yamepotea.

Lipumba Aibukia Ofisi za CUF, Ataka JK Aingilie Kati Suala za ZEC

$
0
0
Ibrahim Lipumba 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuiamuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  (ZEC ) kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa uliofanyika Zanzibar ili kuipusha nchi kuingia katika machafuko.

Jumatano iliyopita, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu akisema uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi.

Akizungumza leo kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari tangu alipojiuzulu, Agosti 6, mwaka huu, Lipumba alisema  amelazimika kutoa ushauri baada ya kuona hatari iliyo mbele kama wananchi wa Zanzibar  watanyang’anywa haki yao.

 “Ijumaa ijayo Dk John Magufuli ataapishwa kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania, Kikwete usimwongezee Magufuli matatizo yaliyopo yanamtosha, ” alisema.

Lipumba ambaye alipokelewa na wafuasi zaidi ya 100 kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, alisema Kikwete ahakikishe kabla hajamaliza muda wake wanaiamuru ZEC kuendelea kutangaza matokeo na kuwatangaza washindi wa uchaguzi huo.

Mtandao wa TACCEO Walaani Polisi Kuvamia Kituo Chao Kuwakamata Waangalizi na Vifaa Walivyokuwa Wakitumia Kupokea Taarifa

$
0
0
Mtandao wa Asasi za Kiraia za Uangalizi wa Chaguzi (TACCEO), umelaani kitendo cha Polisi kuvamia kituo chao na kuwakamata waangalizi na vifaa walivyokuwa wakitumia kupokea taarifa zilizokuwa zikihusiana na mchakato wa uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mtandao huo umeitaka Polisi kufanya kazi zake kwa weledi, huku ikichukua hatua stahiki kushughulikia suala hilo ikizingatia kuwa kazi ya uangalizi wa uchaguzi ni endelevu.

Kaimu Mwenyekiti wa TACCEO, Hebron Mwakagenda (pichani) alisema kitendo hicho ni ukiukaji wa sheria kwa kuwa waangalizi hao walikuwa wakifanya kazi yao kwa kufuata misingi iliyowekwa kikatiba sambamba na kuzingatia taratibu zote za kisheria.

Mwakagenda alisema kuwa uvamizi huo ulikuwa na lengo la kudhoofisha ustawi wa demokrasia nchini na kuwatisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mambo yanayohusu mchakato wa uchaguzi.

Ni wazi uvamizi huu una lengo la kudhoofisha demokrasia na kuingilia kazi za asasi za kiraia kushiriki kikamilifu katika uangalizi wa uchaguzi hapa nchini,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, TACCEO imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kuthibitisha uhalali na uwapo wa nafasi, haki na wigo wa uangalizi wa uchaguzi nchini.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 29, mwaka huu na polisi walifika kwenye ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilichopo Mbezi, Dar es Salaam na kuwakamata watendaji 36 kwa kosa la kukusanya taarifa za uchaguzi zisizo rasmi.

Katika tukio hilo kompyuta 24, kompyuta mpakato tatu, simu 25 za ofisi na nyingine za waangalizi hao zilikamatwa.

Chadema Volunteers Charged for Falsifying Results

$
0
0

Kisutu Resident Magistrate’s Court on Friday granted bail to eight Chadema communications volunteers charged with publishing inaccurate presidential election results.

 Resident Magistrate Respicius Mwijage granted the bail after agreeing with a submission from defense team stating that objection to bail filed by Director of Public Prosecution (DPP) does not mention that the interest and safety of the public would  be prejudiced if the accused were  granted bail.

 Giving bail conditions, Magistrate Mwijage required each accused to secure two reliable sureties who have a letter from local government or recognised institution who will sign a bond of Sh5 million each.

 The accused, including three foreigners were arraigned on Tuesday and charged with three counts including publishing accurate information regarding to the currently presidential election results.

 They denied the charges and remanded after prosecution produced the certificate to object bail to the accused for public interest.

 However, the advocate representing the accused, Peter Kibatala objects the certificate on the ground that the certificate has legal errors.

 Kibatala told the court that, the certificate does not mention public interest as alleged by prosecution.

The accused are Mashinda Edwin Mtei, Julius Mwita, Frederick Eddie Fussi, Julius Mwonga Matei, Meshack Carlos Mlawa, Anisa Nicholas Rulanyaga, Jose Mavinga Nimi and Kim Hyunwook.




Kafulila Aibuka Kupinga Matokeo ya Mwilima..Adai CCM ilimpora Kura

$
0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini(NCCR-Mageuzi), David Kafulila ametangaza rasmi kwenda mahakamani siku yoyote kuanzia sasa ili kudai haki yake baada ya Msimamizi wa Uchaguzi(Nec),katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Ruben Mfune kumtangaza Hasna Mwilima wa CCM kuwa mshindi.

Kupitia uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, Mfune alimtangaza Hasna kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa madai ya kupata kura 34,453 akifuatiwa na Kafulila aliyedai kupata kura 33,382 lakini alipingana na matokeo hayo akibainisha kuhujumiwa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini hapa, Kafulila aliyekuwa mbunge kinara katika kuibua ufisadi wa sakata la Escrow alisema matokeo halisi yaliyokusanywa kwenye kituo ni tofauti na matokeo aliyoyatangaza msimamizi huyo.

“Nitakwenda kufungua kesi katika Mahakama Kanda maalumu ya Tabora kanzia wiki ijayo, kwa sasa tunaandaa utaratibu na wanasheria wangu kabla ya kufungua kesi,najua nitashinda na haki yangu haitapotea ...madai ya kesi ni kuitaka mahakama itangaze mshindi wa matokeo halisi ya vituo vyote 382 katika Kata zote 16 za jimbo hilo,” alisema Kafulila.

Licha ya kudai mazingira ya kuhesabu kura za jimbo hilo kuwa na utata, alisema kura halisi alizopata ni 34, 149 dhidi ya mshindani wake Hasna aliyepata kura 32, 982 lakini alimtuhumu msimamizi huyo kupanga njama za kutangaza matokeo batili kwa madai ya kupata shinikizo la viongozi wake ngazi za juu.

“Kwenye kuhesabu matokeo kulikuwa na askari wasiopungua 400, wakuu wa wilaya, mkoa walikuwapo, tulitumia masaa 17 kutangaziwa matokeo na yalikatishwa mara kdhaa lakini bado nilifanikiwa kushinda jimbo hilo kwa kura nyingi.Nawaomba watanzania wasife moyo, bado nitapambana kuhakikisha haki yangu inapatikana,”alisema mgombea huyo aliyetumikia jimbo hilo tangu 2010 hadi 2015.

Hata hivyo, Msimamizi huyo wa uchaguzi, Mfune aliliambia gazeti hili kuwa endapo mgombea huyo atakuwa hajatendewa haki, afuate njia sahihi za kudai yake. Alisema kila mgombea anayo haki ya kulalamika endapo hataridhishwa na matokeo.

“Lakini matokeo niliyotangaza ndiyo matokeo halisi niliyoyaamini mimi, utaratibu wa kulalamika unafahamika.”

Ugonjwa wa Kipindupindu Wahamia Mwanza, Wauwa Watu 17

$
0
0
Mwanza. Ugonjwa wa kipindupindu umeendelea kuleta maafa mkoani hapa, baada ya kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 268 kulazwa katika vituo mbalimbali vya afya tangu Septemba, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Dk Faisal Issa, Daktari Bingwa wa Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure, Dk Magret Magambo alisema mlipuko wa ugonjwa huo ulianza Septemba 16 katika Kisiwa cha Irugwa wilayani Ukerewe.

“Vifo viwili viliripotiwa katika Zahanati ya Irugwa na sita vilitokea ndani ya jamii ya kisiwa hicho. Baadaye ugonjwa huo umeripotiwa kutokea katika maeneo mengine ya wilaya hiyo ambayo ni vijiji vya Kagunguli, Katunguru na Kazilankanda ambapo hadi leo (jana) jumla ya wagonjwa 192 na vifo 12 vilitokea katika Wilaya ya Ukerewe.

Hata hivyo juhudi kubwa za kupambana na mlipuko katika Kijiji cha Irugwa zimefanyika na kwa siku kadhaa hakuna wagonjwa wapya wanaoripotiwa.

Wilaya nyingine iliyoathirika ni Sengerema ambako vijiji vya Kanyala na Bulolo vimesharipoti wagonjwa takriban 73 na vifo vitano,” alisema.

Dk Magambo alisema Wilaya ya Nyamagana imepokea wagonjwa watatu ambao walitoka sehemu mbalimbali, ambazo zilikuwa na mlipuko wa ugonjwa huo na kwamba, walitibiwa na kuruhusiwa.

Kwa ujumla hadi leo (jana) Mkoa wa Mwanza wamejitokeza wagonjwa wengi, kati ya hao vifo ni 17. Wanaoendelea na matibabu ni 33 wakati waliotibiwa na kuruhusiwa wako 217. Ugonjwa huo umesambaa katika Wilaya ya Sengerema na kuripotiwa kuwa na wagonjwa 73 na vifo vitano, Ukerewe katika maeneo mbalimbali wagonjwa na kifo kimoja na Nyamagana,” alisema Dk Magambo.

Kwa upande wake, Ofisa Afya wa Mkoa wa Mwanza, Fungo Masalu alizitaka halmashauri zote ziunde kamati hai za udhibiti wa kipindupindu kulingana na miongozo ya udhibiti wa ugonjwa huo.

“Halmashauri zote ziimarishe hali ya usafi wa mazingira katika maeneo yao, zihakikishe taka zinakusanywa na kuondoshwa katika mitaa ili kuepuka mrundikano unaoweza kushawishi makazi ya wadudu waenezao kipindupindu, kazi hizo zifanyike chini ya kamati za udhibiti wa kipindupindu,” alisema Masalu.

Ofisa huyo alisema Serikali itaendelea kufuatilia na kuhamasisha jamii ili iweze kuepukana na ugonjwa huo.

Mahaba ya Wana Dar Yamfanya Wizkid Aahidi Show ya Bure, Lakini Imeshindikana..Sababu Hizi Hapa

$
0
0
Wizkid
Mapokezi na mapenzi aliyoyapata Wizkid jijini Dar es Salaam yamemfanye avunje safari yake leo kurudi Lagos, na kuahidi show ya bure Jumapili hii.

Wizkid alioneshwa kushangazwa na shangwe za mashabiki hao, hali iliyofanya afanye show kwa muda mrefu zaidi. Alisema hakuwahi kukutana na mashabibi wenye upendo kuwazidi Watanzania.

“Ilikuwa niondoke lakini sitaondaka na kesho natafuta sehemu nikutane tena na nyie, tufanye concept ya bure,” alisema Wizkid.

Nimefurahi sana kuona hali hii. Tanzania mna upendo wa kweli. Tuendelee kuwa pamoja nami kwenye Twitter na Instagram ili tujue tunakutana katika ukumbi gani,” alisema.

Hata hivyo Jumapili hii Wizkid alitangaza kuwa ameshindwa kupata kibali cha kufanya show ya bure lakini amedai atarajea December kwenye Fiesta.

Last night in Dar es Salaam, Tanzania!! Had to jump on the speakers to be close to my people! Love u all. Unfortunately, we couldn’t get the permit to do the free concert today but I’m coming back in December! Fiesta moves!!!!! Yaaaaa,” ameandika kwenye Instagram.

Pia aliipongeza Tanzania kumaliza uchaguzi salama.

Jakaya Kikwete Aguswa na Hali ya Zanzibar..Aamua Kufanya Juu Chini Kuhakikisha Suluhu Inapatikana Kwa Amani

$
0
0
RAIS Jakaya Kikwete ameeleza kuguswa kwake na hali ya kisiasa na usalama wa Zanzibar na kusema anafanya juu chini kuhakikisha suluhu inapatikana kwa amani, huku Ikulu ikikanusha kupokea maombi kutoka kwa Mgombea Urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad akitaka kukutana na Rais Kikwete.

Seif anadai kupeleka maombi hayo kwa Rais Kikwete baada ya uchaguzi wa Zanzibar kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

“Ikulu inapenda kukanusha kwamba ilipokea maombi kutoka kwa Mheshimiwa Hamad ya kukutana na Rais Kikwete …” ilisema sehemu ya taarifa ya Ikulu, iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba alichopokea Rais Kikwete, ilikuwa ni malalamiko ya CUF kuhusu vitendo kadhaa vya Jeshi la Polisi Zanzibar. Pia ilieleza kuwa Rais Kikwete aliombwa na CUF kuwezesha mazungumzo kati ya Hamad na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange.

Wakati huo huo taarifa hiyo ya Ikulu imesema kwamba Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, amemwamuru Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu kufanya uchunguzi wa madai hayo ya CUF na kutoa taarifa kwake.

Aidha, ameamuru ofisi yake kuwezesha mazungumzo kati ya Jenerali Mwamunyange na maofisa wa CUF.

“Ikulu inapenda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete, kama ilivyo kwa Mtanzania yeyote, anaguswa na hali ya siasa na usalama wa Zanzibar, na amekuwa akifanya juu chini na kushauriana kwa mapana katika siku chache zilizopita, kutafuta suluhisho la amani katika Zanzibar,” ilisema taarifa hiyo.

Wakati suala hilo likiendelea kubaki mikononi mwa chombo huru cha uchaguzi visiwani Zanzibar, Rais Kikwete amesema yuko tayari kufanya kila liwezekanalo, kuhakikisha hali inakuwa kawaida visiwani humo.

Katika hatua nyingine, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema haitavumilia aina yoyote ya vurugu visiwani humo wakati ikisuburi Uchaguzi Mkuu baada ya uliofanyika Oktoba 25 kufutwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud, alisema hayo jana katika taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari.

“Kila mmoja lazima aendelee na maisha yake kama kawaida wakati tukisubiri Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutoa ratiba kwa ajili ya uchaguzi mpya. ZEC ni chombo huru na hakuna mtu yeyote au taasisi inayoweza kuingilia kazi zake. Ilifuta uchaguzi na tunapaswa kuheshimu uamuzi wake,” alisema Aboud.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa huku Chama cha Wananchi (CUF) kikipinga kufanyika uchaguzi upya kwa madai kwamba uchaguzi uliofutwa, ulikuwa huru na haki kama ambavyo waangalizi wa ndani, ikiwemo Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) walivyobaini.

Mgombea Urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad anashinikiza Mwenyekiti wa NEC, Jecha Salim Jecha aendelee kutangaza haraka matokeo na mshindi, kuondoa hali ya sintofahamu kutokana na muda wa urais wa Dk Ali Mohamed Shein kuwa madarakani kuisha leo.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana makao makuu ya CUF, mjini hapa, Seif alisema yapo maendeleo mazuri ya kutatua mgogoro huo wa kisiasa visiwani kwa msaada wa Jumuiya ya Kimataifa.

Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, alisema, “kwa hiyo nawaomba wanachama na wafuasi wa CUF na Wazanzibari kwa ujumla, kuwa watulivu na wenye amani.” Kwa upande wake, Waziri Aboud alisema, Dk Shein ataendelea kuwa rais hadi hapo rais atakayechaguliwa, atakapoapishwa.

“Hii ni kupotosha watu kwa kusema kwamba Zanzibar haitakuwa na rais halali baada ya Novemba 2. Katiba ya Zanzibar kifungu cha 28 (1) A kiko wazi kwamba rais ataendelea kuwa madarakani hadi hapo atakapochaguliwa mwingine na kuapishwa,” alifafanua Aboud.

Alitaka viongozi wote wa vyama vya siasa, kuacha kutoa kauli ambazo zinaweza kusababisha vurugu huku akiwataka watangulize maslahi ya nchi. Wakati huo huo Kamishna wa Polisi, Hamdan Omar Makame alisisitiza juzi wananchi kuendelea na maisha yao ya kawaida.

“Hatutishi mtu yeyote, tunaomba watu waendelee na maisha yao ya kawaida,” alisema na kufafanua kwamba hali ya ulinzi waliyoiweka, ni kwa ajili ya kujiandaa kukabili uovu wowote unaoweza kutokea visiwani hapo. Aidha, Chama cha Wazee Zanzibar kimetaka wakazi wa visiwani humo kupuuza kauli za baadhi ya wanasiasa zinazochochea vurugu. “Zipo njia za kisheria na kidiplomasia za kutatua matatuzi, matumizi ya nguvu siyo njia nzuri,” alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Ali Hassan Khamis.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, alitoa “Taarifa Kwa Umma ya Kufuta Uchaguzi wa Zanzibar”.

Katika taarifa hiyo, Jecha Salim Jecha alisema “Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukuwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa Sheria na taratibu za uchaguzi. Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu”.

Mwanamuziki Cassim Mganga Amchana Babu Tale... Adai Hakuwa ‘Kiongozi Bora’ Wakati Yupo Tip Top Kiasi Alijihisi Mtoto wa Kambo

$
0
0
Cassim Mganga
Cassim Mganga amezungumza kwa kwanza sababu ya kuondoka Tip Top Connection ambapo amemtuhumu Babu Tale kuwa hakuwa kiongozi mzuri kwake.

Cassim alikiambia kipindi cha Mkasi kuwa hakufurahishwa na maisha aliyoishi Tip Tip ndio maana aliamua kuondoka.

Toka nimeondoka Tip Top Tale hajawahi kuniletea deal hata moja,” alisema.

Kwenye familia yoyote hakukosi migogoro, mzazi usipokuwa strong watoto wanapoteza direction. Nimeishi muda mrefu Tip Top, nimekosea nimekosewa lakini ilikuwa ni sehemu ya maisha kama family. Naomba nifunge, Tale hakuwa baba bora. Baba lazima umsikilize kila mtoto, kwahiyo mimi nilikuwa najiona mtoto wa kambo. Sasa kwa nini niendelee kuishi? Lakini kutoka kwangu bado kulisababisha vitu vingi sana na ninachokiona ni kwa sababu ya uwezo wangu. Walitamani kuona mtu kama Cassim aendelee kuwepo, hata mimi nilitamani kuendelea kuwepo kwa sababu kazi zilikuwa rahisi sana.”

Wabunge Wateule Waitwa kwa Dk Magufuli....Watakiwa Kufika na Cheti Kinachoonyesha Kuteuliwa Kuwa Mbunge

$
0
0
John Magufuli
Wabunge wote wateule, wametakiwa kufika Ofisi Ndogo ya Bunge Dar es Salaam, ili kushiriki hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule, Dk John Magufuli.

Wabunge hao kutoka majimbo 259 nchini walichaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili ya Oktoba 25, ambao pia ulimpa ushindi Dk John Magufuli wa CCM, dhidi ya mshindani wake wa karibu Edward Lowassa wa Chadema aliyeungwa mkono na Ukawa.

Akizungumza jijini hapa  leo, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema wabunge hao wateule wanatakiwa kuwasili kwenye ofisi hizo,  kila akiwa na cheti  kinachoonyesha   kateuliwa kuwa mbunge, kilichotolewa na  msimamizi wa uchaguzi wa jimbo husika.

Cheti hicho, kitawasilishwa kwa maofisa wa Bunge wakati wa zoezi la usajili, pia kila mbunge mteule atatakiwa kubeba kitambulisho kingine chochote kilichotolewa na mamlaka inayotambulika, kinachoonyesha jina lake kamili kama lilivyoandikwa kwenye cheti cha ubunge,”alisema Joel.

Ameongeza: “Uchaguzi umekwisha, lakini baadhi ya majimbo bado kutokana na sababu mbalimbali. Masikio ya wananchi na wabunge wateule ni kujua nini kitafuata upande wa ofisi ya Bunge, ndiyo maana  leo (jana ), tunatangaza kuwaita   wateule wote kufika  Dar es Salaam Novemba 4 mwaka huu.

Amefafanua kwamba usajili kwa wabunge wote wateule utafanyika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma na kila mbunge atajitegemea usafiri kwa ajili ya shughuli hiyo itakayofanyika kabla ya kuanza kwa Mkutano  wa Kwanza wa Bunge la 11.

Kuhusu kuongezeka kwa majimbo, Joel alisema wamejipanga na kuongeza viti ili kuhakikisha wabunge wote wanapata nafasi ya kuketi kwenye ukumbi huo.

Hatujabadilisha ukumbi  bali tumeongeza idadi ya viti kwa kazi mbili maalumu .Moja ni kwa ajili Rais atakapozindua Bunge na pili   kwa wabunge wote wakiwamo wa viti maalumu, ambao bado hatujua idadi yao,” alisema Joel.

Kwa mujibu wa Joel, mkutano huo wa kwanza unatarajiwa kuanza siku ambayo Rais ataitisha Bunge na utahusisha  uchaguzi na kiapo kwa Spika, viapo kwa wabunge wote wateule, kuthibitisha jina la Waziri Mkuu, uchaguzi wa Naibu Spika na  ufunguzi rasmi wa Bunge la 11.

Joel alitumia nafasi hiyo kuvikumbusha vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu vilivyo na nia ya kusimamisha mgombea uspika kuanza mchakato  mapema kwenye ngazi ya vyama,   kabla ya tangazo la nafasi ya Spika kuwa wazi.

 Amesema lengo la kuvikumbusha ni kuvitaka vikamilishe mchakato kwa wakati na kuwasilisha jina la mgombea kwa Katibu wa Bunge.

 DONDOO

Spika anaweza kutokana na wabunge au mwanachama wa chama cha siasa ambaye jina lake liliwasilishwa kwanza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kujiridhisha kama ana sifa za kuwa mbunge



Vifaru na Magari ya Maji ya Kuwasha Havitaleta Ufumbuzi Wa Mgogoro Zanzibar-CUF

$
0
0
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa ufumbuzi wa mgogoro wa Zanzibar hauwezi kupatikana kwa kutumia nguvu au vitisho vya kuingiza vifaru na magari ya maji ya kuwasha, kama inavyotokea sasa; bali kinachotakiwa ni meza ya majadiliano.

Tamko hilo limetolewa na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Aliwataka wafuasi wa CUF na wananchi kuendelea kuwa na subira wakati viongozi wao wakiwa katika jitihada za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.

Alisema mgogoro uliojitokeza Zanzibar ni mgogoro wa kisiasa baada ya haki ya kidemokrasia ya wananchi kupindishwa ndio maana CUF inataka Mwenyekiti afute uamuzi wake, amalizie kazi iliyobakia ya kuhakiki matokeo na kutangaza mshindi.

"Tatizo lililopo ni la kisiasa na ufumbuzi wake si vifaru wala kuongeza ulinzi, linahitaji njia ya mazungumzo kumalizika kwake," alisema.

Aidha, Maalim Seif aliwataka wanachama kuendelea na utulivu kutokana na juhudi zinazofanywa na Jumuiya za Kimataifa kuonesha mwelekeo wa kupatikana ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar.

Alisema CUF inaimani kwamba ufumbuzi wa haki wa suala hilo hauko mbali na Wazanzibari wataona mafanikio ya demokrasia yatakayojengwa nchini. Alisema haki lazima itendeke katika uchaguzi uliopita.

"Sisi tumepata moyo na imani kwamba ufumbuzi wa haki wa suala hili hauko mbali na Wazanzibari wataona mafanikio ya demokrasia yetu tunayoijenga katika nchi yetu," alisisitiza Maalim Seif.

Aliwaomba Wazanzibari wote wanaopenda amani wawe waangalifu sana na taarifa za uongo zinazotolewa za kuchochea kufanya vurugu kwa kisingizio kuwa zimetolewa na viongozi wa CUF wakati ni uongo.

"Nitumie fursa hii kuwashukuru wale wote wanaofanya juhudi kubwa kuona ufumbuzi wa haki na wa amani unapatikana kwa tatizo hili lililosababishwa na mtu mmoja aliyeamua kuacha wajibu wake na kutumikia maagizo ya kikundi cha watu wabinafsi", alisema.

Aidha, alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, bado wana nafasi kubwa ya kuhakikisha wanaivusha Zanzibar kwa kumaliza mgogoro wa uchaguzi uliojitokeza kwa amani na utulivu.

"Kwa mara nyingine tena natoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais Dkt Shein kuchukua dhamana ya uongozi na kwa pamoja tushirikiane kuikwamua Zanzibar na Tanzania katika mkwamo huu", alisema.

Alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vina wajibu mkubwa wa kusaidia kupatikana ufumbuzi wa tatizo walilonalo badala ya kuongeza wasiwasi kwa wananchi wao waliotulia.

Akizungumzia kuhusu uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar, alisema kuwa wamepata taarifa kuwa Mwenyekiti huyo ameitisha kikao cha Tume na kuwataka makamishna kuunga mkono uamuzi wake huo alioutangaza pekee wa kufuta matokeo ya uchaguzi.

Alisema kuwa ni vyema kwa Mwenyekiti huyo akatambua kwamba hata akiwatumia baadhi ya makamishna kumuunga mkono, bado uamuzi huo hautakuwa halali kwa sababu haumo katika uwezo uliopewa Tume; si katiba wala sheria ya uchaguzi.

"Kwa ufupi suala hili halina njia nyingine ya kulimaliza zaidi ya kukamilisha kazi ya kufanya majumuisho, kuhakiki matokeo na kumtangaza mshindi wa uchaguzi", alisema Maalim Seif.

Maalim Seif aliwahakikishia viongozi na wanachama wa CCM kwamba hawana sababu ya kuwa na hofu na maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya Oktoba 25 mwaka huu; na kwamba kama kuna tofauti zozote za kisera na kimtazamo baina yao zinaweza kuzungumzwa na maelewano kufikiwa.

"Nawahakikishia viongozi na wanachama wa CCM na Wazanzibari wote kwamba hakutakuwa na ulipizaji kisasi au kufukua makaburi kwa mambo yaliyopita, sote tutafanya kazi pamoja bila ya kujali tofauti za itikadi za kisiasa, asili, kabila au dini zetu, Zanzibar ni moja na itabaki kuwa moja," alisisitiza Maalim Seif.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Novemba 2, Lupumba Kurudi CUF na Habari Zingine Nyingi

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Novemba 2
















Ikulu Yakanusha Kikwete Kutopokea Simu Ya Maalim Seif Shariff Hamad

$
0
0
Wakati saa 48 zilizotolewa na mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad kutaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuendelea na mchakato wa majumuisho ya kura na kumtangaza mshindi wa urais wa Zanzibar zikiwa zimemalizika, Ikulu ya Jamhuri ya Muungano imesema haijapokea maombi ya Maalim Seif kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete.

Ijumaa iliyopita, Maalim Seif aliwaambia waandishi wa habari visiwani Zanzibar kuwa baada ya ZEC kufuta uchaguzi Jumanne iliyopita, alifanya jitihada kadhaa za kuwasiliana na Rais Kikwete na pia Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ili kuzungumzia suala hilo kwa maslahi ya Zanzibar lakini wito wake huo umekuwa ukipuuzwa.

Maalim Seif alisema tangu kufutwa kwa uchaguzi, amefanya juhudi za kutafuta ufumbuzi kwa kukaribisha mazungumzo na viongozi wenzake wa kitaifa akiwamo Rais Kikwete na pia Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, lakini wote wamekuwa wakimkwepa, licha ya kuanza kuwatafuta kwa kutumia mawasiliano ya simu na ujumbe kupitia wasaidizi wao, akitaka wakutane.

Hata hivyo, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa Ikulu imesikitishwa na madai ya Maalim Seif, ikieleza kuwa siyo kweli.

Badala yake, Ikulu imesema haijapokea ombi lolote kutoka kwa Maalim Seif la kutaka kukutana na Rais Kikwete tangu siku ya kupiga kura na hata baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kufuta uchaguzi wa Zanzibar.

Taarifa hiyo ya Ikulu imesema kile ambacho Rais Kikwete amekipokea ni malalamiko ya CUF kuhusu baadhi ya vitendo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar na ombi kwa ajili ya kuwezesha mazungumzo kati ya Maalim Seif na Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange.

“Baada ya hapo, Rais Kikwete, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, kuchunguza madai haya ya CUF na kumletea taarifa. Kadhalika, ametoa maelekezo ofisini kwake ya kuwezesha mazungumzo kati ya Jenerali Mwamunyange na maafisa wa CUF,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Rais Kikwete amekuwa akiguswa na hali ya kisiasa na usalama wa Zanzibar kama ilivyo kwa Watanzania wengine na amekuwa akifanya kazi bila kuchoka huku akipata ushauri wa kina juu ya kilichotokea Zanzibar siku chache zilizopita na kupata ufumbuzi.

Taarifa hiyo ilifafanua zaidi kuwa wakati jambo hilo likiwa bado katika mikono ya ZEC ambacho ni chombo huru cha uchaguzi, Rais Kikwete yuko tayari kufanya chochote kilicho ndani ya uwezo wake ili kupata suluhisho jema kuhusiana na hali ya Zanzibar.

Uchaguzi  Kufutwa
Suala la kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar linadaiwa kuviingiza visiwa hivyo katika mgogoro wa kikatiba na kisheria.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, alitaja sababu tisa za kufikia uamuzi wa kufuta uchaguzi huo kuwa ni pamoja na kura kuongezeka katika baadhi ya majimbo kisiwani Pemba na pia baadhi ya makamishna wa Zec kutanguliza itikadi za vyama hadi kuvua mashati ili kupigana.

Kadhalika, alisema katika baadhi ya vituo, masanduku ya kupigia kura yaliporwa na kwenda kuhesabiwa nje ya vituo, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria ya uchaguzi na pia, kuna taarifa ya kufukuzwa kwa baadhi ya mawakala wa wagombea na hivyo kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Hata hivyo, waangalizi wa ndani na wa kimataifa, wakiwamo Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Madola  Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), waangalizi wa Marekani na Uingereza, katika ripoti zao wamesema uchaguzi wa Zanzibar mwaka huu ulikuwa huru na wa haki na kutaka Zec ikamilishe kazi ya kuhesabu kura na kumtangaza mshindi.

Kingunge Ajipanga Kumwaga Cheche na Kuzungumzia Uchaguzi wa 25 Oct Ulivyokuwa

$
0
0
Kingunge
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale- Mwiru amesema atazungumzia mchakato wa Uchaguzi Mkuu baadaye baada ya kukusanya taarifa za kutosha.

Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kuombwa kutoa maoni yake kuhusu Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni na Dk John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangazwa mshindi, Kingunge bila kufafanua zaidi alisema: “Nitazungumzia mchakato wa uchaguzi baadaye baada ya kukamilisha kukusanya taarifa.”

Mwanzoni mwa Oktoba, Kingunge ambaye amekuwa kada wa CCM kwa miaka 61 (tangu enzi za TANU), alitangaza kujitoa katika chama hicho akisema hawezi kuendelea kuwa ndani ya chama kinachoendeshwa kwa maslahi binafsi.

Kingunge ambaye amefanya kazi kwa karibu ndani ya CCM na Serikali na marais wa wote wa awamu nne, alidai chama hicho kimepoteza mwelekeo na hakijadili mambo muhimu kama ilivyokuwa zamani.

Pamoja na Kingunge kudai hajiungi na chama kingine chochote cha siasa, alionekana kwenye jukwaa la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho aliyeungwa na vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa.

Uchaguzi Mkuu ulifanyika Oktoba 25, mwaka huu, na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Dk John Magufuli kuwa mshindi baada ya kupata kura 8,882,935 (asilimia 58.46) na kufuatiwa na Lowassa kura 6,072,848 (asilimia 39.97).

Wolper Afunguka Kuhusu Mwanaume Aliyechukua Nafasi ya Mkongo....

$
0
0
SIKU chache baada ya kumwagana na aliyekuwa mchumba wake, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwigizaji Jacqueline Wolper amesema kuwa hawezi kuendelea kubaki bila mtu lakini anahitaji mtu mwenye sifa.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema kutokana na kuingia kwenye uhusiano na wanaume tofauti akiwemo mfanyabiashara maarufu, Dallas ambao ameshindwa kufanya nao maisha, anahitaji mtu ambaye kweli atajiridhisha kuwa anafaa kuwa mume na si vinginevyo.

Alipoulizwa kuhusu Daktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asilia, Dk. Fadhili Emily ambaye alitajwa kuhusika kuvunja uchumba wake na Mkongo, Wolper alisema muda bado wa kumzungumzia daktari huyo.

“Huyu nimefahamiana naye muda si mrefu hivyo hata kama ni yeye nitahitaji muda kidogo kujiridhisha nione kama anafaa,” alisema Wolper.

Chanzo: GPL

Moses Iyobo Awacharukia Wanaosema Mpenzi wake Aunty Ezekiel ni Mzee

$
0
0
Aunty Ezekiel na Mpenzi wake Moses Iyobo
Kafunguka! Dansa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni mwandani wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson,   amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaomsema Aunt kuwa ni mzee kwa kuwa amempita umri, jambo ambalo hakubaliani nalo.

Dansa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Moses Iyobo akiwa na mpenzi wake Aunt Ezekiel Grayson

Akizungumza na mwanahabari wetu, Iyobo alitiririka kuwa anawashangaza watu wanaoingilia mapenzi yao kwani yeye anachojua kwenye mapenzi watu hawaangalii umri ila ni upendo na kuheshimiana.

“Nani anasema Aunt ni mzee? Mimi namuona ni mtoto mbichi kabisa,” alisema Iyobo mwenye umri wa miaka 23 huku Aunt akiwa na 29.
GPL
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live




Latest Images