Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Vigogo wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Waanza Kuhojiwa na Polisi Kwa Kuvuruga Uchaguzi

0
0
Vigogo wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), wameanza kuhojiwa na Jeshi la Polisi Zanzibar baada ya kuvurugika kwa Uchaguzi Mkuu na kusababisha Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka huu.

Viongozi waliohojiwa na Polisi  ni Makamishna na Watendaji wa tume hiyo akiwamo Makamu Mwenyekiti, Jaji Abdulhakim Issa Ameir.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar (DDCI), Salum Msangi, alithibitisha mjini hapa Mjini jana kuwa Makamishina wa Zec na Watendaji, wameanza kuhojiwa na maofisa wa upelelezi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar Ziwani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Alisema hadi sasa uchunguzi umefikia hatua kubwa na baada ya kukamilika, majalada ya uchunguzi yatapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim, kabla ya wahusika kufikishwa mahakamani.

Tunawahoji Makamishna na Watendaji wa Tume, Makamu Mwenyekiti yeye tayari tumemhoji, bado Mwenyekiti na maofisa wengine,” alifafanua DDCI Msangi.

Alisema Polisi waliingia kazini baada ya kuripotiwa kuwa uchaguzi umevurugwa na kazi inayofanyika ni kukusanya ushahidi na vielelezo kabla ya wahusika kufunguliwa mashitaka kwa kuhujumu Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.

Alisema uchunguzi huo umegawanyika sehemu tatu na kuwahusisha Tume, waathirika na wananchi kutoka sehemu mbalimbali katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha, alisema kuna mambo mazito yameanza kuonekana tangu kuanza kufanyika kwa uchunguzi, lakini alisema ni mapema kueleza uchunguzi huo utachukukua muda gani kukamilika.

"Wahusika watafikishwa mahakamni baada ya majalada ya uchunguzi kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar kabla ya kufikishwa mahakamani," alisema Msangi.
Hata hivyo, Naibu Mkurugenzi huyo alisema hali ya Zanzibar ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida tangu Zec ilipofuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.

Akitangaza kufuta uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Zec, Jecha alisema kuna sababu tisa zimemfanya kuchukua hatua hiyo.
Alizitaja kuwa ni pamoja na vituo vya wapigakura na idadi ya kura katika visanduku zilikuwa nyingi kuliko idadi ya watu waliosajiliwa katika daftari la wapigakura katika vituo vya uchaguzi.

Aidha, alisema kuna visanduku vya kura viliporwa na kuhesabiwa nje ya vituo kinyume na sheria pamoja na mawakala wa vyama kupigwa na kufukuzwa katika vituo vyao vya kazi siku ya uchaguzi.

Tayari Zec imetangaza rasmi katika Gazeti la Serikali la Novemba 6, mwaka huu kufutwa kwa uchaguzi huo na kuwataka wananchi kusubiri kutangazwa tarehe ya kurudiwa.

ISIS Threatens to Attack New York City in New Video Showing Suicide Bombers Walking into Times Square

0
0

ISIS has threatened to bomb New York City in a newly released video, just days after vowing to attack Washington, D.C. The video clip features shots of yellow taxis and crowds in Times Square and Herald Square in Manhattan, with vibrant French music playing in the background - a nod to the Paris terror attacks on Friday.
It then cuts to a man wrapping a bomb around his waist before walking into the crowds and pulling the trigger.

New York police have issued a statement to say they are aware of the footage.They added that there is no direct threat to the city but insist there is a 'heightened state of vigilance'.

'In addition, we are continuing to deploy additional Critical Response Command (CRC) teams throughout the City, out of an abundance of caution,' Stephen Davis, a Deputy NYPD Commissioner, said in a statement on Wednesday.
He added: 'While some of the video footage is not new, the video reaffirms the message that New York City remains a top terrorist target.'
The video, which runs for nearly six minutes, includes a scene that appears to show a suicide bomber making preparations and zipping up a leather jacket.



Kassim Majaliwa Aidhinishwa na Wabunge Kuwa Waziri Mkuu kwa Kura 258

0
0
Mh. Kassim Majaliwa amethibitishwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu mteule kwa kupata kura za ndio 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote 351 zilizopigwa.

Kura za hapana ni kura 91 sawa na asimilia 25 ya kura zote, na kura zilizoharibika ni 2.

Majaliwa amemshukuru Rais  Magufuli kwa kumwamini na ameahidi kuwatumikia watanzania wote  bila kujali itikadi zao za vyama.

Breaking News: Dr Tulia Ackson Mwansasu Achaguliwa Kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

0
0
Hichi Ndio Kilichojiri Bungeni leo Wakati wa Kumchagua Naibu Spika

Wabunge Wote 394
Wabunge waliopiga kura 369
Akidi ya wabunge wanaotakiwa 184
Wabunge Waliopo na kupiga kura 351

Kura Zilizoharibika 0
Magdalena Sakaya 101(28%)
Dr Tulia 250(71.2%)

Hivyo Tulia Amechaguliwa Kuwa Naibu Spika wa Bunge la Tano

January Makamba Naamini Amepata cha Kujifunza

0
0
Kwenye Maisha kimbelembele hakifai kabisa, kujikweza sana karibu na wakubwa sio tiketi ya kupata wadhifa wa juu.

Nampa pole January Makamba, asubirie Uwaziri tu lakini sio Uwaziri Mkuu.

Wahenga wasema, kukaa karibu na Mahakama sio kujua sheria.

By Mussolin5/Jamii Forums

Is WEMA SEPETU Dying Soon? She Has Predicted Her Death

0
0

26 year old ex-Miss Tanzania, Wema Sepetu, shocked her family, friends and fans when she posted a strange message on her IG saying that she thinks that her death is nigh.

Wema’s fans could not understand why she decided to post such a message especially now that she has found a lovely man to call a boyfriend. Here is what she wrote;



Top 20 African Countries with the Most Beautiful Women...And Tanzania Is No......

0
0
According to a website called ranker.com, below are top 20 African countries with the most beautiful women:

20. Botswana
19. Angola
18. Seychelles
17. Cameroon
16. Rwanda
15. Cape Verde
14. Mali
13. Niger
12. Kenya
11. Morocco
10. Senegal
9. Togo
8. Egypt
7. Ghana
6. Eritrea
5. Ivory Coast
4. Ethiopia
3. Guinea
2. Djibouti
1. Tanzania

Mwanasheria Mkuu Apinga Hoja za UKAWA...Asema Dr. Shein ni Rais Halali wa Zanzibar na atahudhuria Uzinduzi wa Bunge la 11

0
0
Mwanasheria mkuu wa serikali, George Masaju amepinga hoja  zilizoibuliwa na UKAWA kuhusu uhalali wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Dkt Shein, kuhudhuria kwenye uzinduzi wa Bunge.

Masaju ametumia ibara ya 102 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupangua hoja hizo  ambayo inaeleza kuwa, kutakuwa na serikali ya Zanzibar itakayo julikana kama serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.

Pia ametumia ibara ya 103 ibara ndogo ya kwanza ya katiba ya jamhuri inayosema kuwa, kutakuwa na kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambae ndiye atakuwa rais wa Zanzibar na mkuu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na vilevile mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.

Baada ya Ibara hizo, akajielekeza kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika Ibara yake ya 26 ambayo inasema, kutakuwa na rais wa Zanzibar ambae atakuwa mkuu wa nchi ya Zanzibar, kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.

Hali kadhalika akanukuu Ibara ya 27 ambayo inaeleza namna rais wa Zanzibar atakavyo patikana ambayo inasema kwamba, rais atachaguliwa kufuatana na katiba hii na kwa mujibu wa sheria yoyote itakayotungwa na baraza la wawakilishi kuhusu uchaguzi wa rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi na uchaguzi wa rais utafanyika katika tarehe itakayowekwa na tume ya uchaguzi (ikiwa na maana ya ZEC).

Aidha, alinukuu Ibara ya 28 (a) ya katiba ya Zanzibar ambayo inaeleza kwamba, kufuatana na katiba hii, mtu ataendelea kuwa rais mpaka:
a) Rais anaefata ale kiapo cha kuwa rais

Baada ya hoja hizo akahitimisha kwa kusema, kwa kuwa tayari tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imefuta uchaguzi, na kwa kuwa tayari tume hiyo imetangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi mkuu mwingine visiwani Zanzibar, na kwa kuwa hakuna mtu yeyote alieapa kiapo cha urais tofauti na rais wa sasa wa Zanzibar, Dkt Shein. Hivyo Dkt Shein anatambulika kama rais wa Zanzibar na ana uhalali wote wa kuhudhuria katika uzinduzi wa Bunge la 11.

Rais Dr. Magufuli na Mhe. Majaliwa: Karata za CCM kisiasa, zitafanikiwa?

0
0
Natazama kuteuliwa kugombea na baadaye kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania kwa Dr. Magufuli kwa tiketi ya CCM kama karata muhimu iliyochangwa na kuchezwa na CCM katika uchaguzi uliopita. Iko wazi kuwa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani Tanzania, kilijijenga vya kutosha katika maeneo ya Kanda ya Ziwa yenye mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera. Kitendo cha kusimamishwa kwa Dr. Magufuli ni kitendo cha kutikisa ngome ya CHADEMA.

Dr. Magufuli ni mwenyeji wa kanda hiyo kwakuwa amezaliwa, kukua, kufanya kazi na kuwa Mbunge huko Chato mkoani Geita. CHADEMA iliachwa mkono na wananchi wa kanda ya ziwa si kwakuwa ilipoteza umaarufu. Iliachwa mkono kwakuwa tu wananchi wa kanda ya ziwa waliona mwaka huu ni 'zamu yao' kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani kabila kubwa kuliko yote nchini-wasukuma.

Kuibuliwa kwa Dr.Magufuli ni karata ya kukata nguvu za upinzani-hasa CHADEMA katika Kanda ya Ziwa iliyoonja ladha ya operesheni mbalimbali za kichama katika kujenga na kuimarisha CHADEMA. Kama hiyo haitoshi, CCM imecheza karata nyingine leo kupitia kwa Rais Magufuli kumteua Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Kanda ya kusini inasemwa kama kanda iliyo nyuma kuliko zote kimaendeleo.

Pia kanda hiyo ina vuguvugu la gesi asilia lililopelekea wananchi wa huko kupunguza kuipenda na kuishabikia CCM. Kuteuliwa kwa Mhe. Majaliwa ni kuwapa nafasi watu wa Kanda ya Kusini kujisogeza kimaendeleo na kuonyesha kuwa CCM inawajali na kuwathamini wananchi wa huko na hivyo wananchi wa huko wasahau madhila na vuguvugu la gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Wawili hawa (Dr. Magufuli na Mhe. Majaliwa) hawakupata nafasi zao kwa bahati mbaya ila ni karata muhimu kwa CCM. Karata hizi zitafanikiwa?
Last edited by Petro E. Mselewa;

Lipumba Ameibuka Tena, Amemtaka Rais John Magufuli Kuiamulia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Kumtangaza Maalim Seif Kuwa Rais

0
0
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba ameibuka tena,na sahivi amemtaka Rais John Magufuli kuiamulu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kumtangaza Mgombea wa Urais kupitia CUF,Maalim Sef sharif Hamadi kuwa mshindi wa Nafasi ya Urais.

Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu nafasi ya hiyo alikuwa nayo , miezi mine iliyopita kutokana na kutoelewana  na Viongozi wa vyama vya UKAWA  na Mkutano wake na wanahabari ulifanyika kwenye Hoteli moja hapa jijini ambayo inadaiwa garama za hoteli hizo zililipiwa na  chama cha Mapinduzi CCM.

   Ambapo leo ameibuka  kwenye makao makuu ya Ofisi za chama hicho zilizopo Bururuni jijini hapa na kuzungumza na waandishi wa habari  na kuzungumzia mgogoro mkubwa unaoendelea visiwani Zanzibar na kusema hali hiyo ikiendelea hivyo itaweza hata kuvuruga umoja ambao Taifa unao na kupelekea kukwamisha shuguli zote za kimaendeleo.

    “Namuomba Rais Magufuli aliokoa Taifa lilipofikia kwa kuiamulu ZEC kutangaza matokeo ya Urais yaliyobakia lasivyo,kama naye akiendelea kuacha uvunjifu wa Katiba ya Zanzibar basi Taifa halitaweza kusonga mbele litakuwa kila siku lipo kwenye mgogoro”
      Amesema kitendo cha Rais Magufuli kwenda kulihutubia Bunge kesho na kuongoza na Rais wa  Zanzibar anayedai amemaliza mda wake Dk Mohamed Shein hakikubaliki na kinakwenda  kinyume na katiba ya Zanzibar.

     “Leo Magufuli najua ameaapa na kuilinda Katiba,itashangaza kuona Kesho Dk sheini ataingia kwenye Bunge wakati ni ukweli kwamba katiba ya Zanzibar inaonyesha wazi ameshamaliza mda wake wa uongozi kwa kipindi cha miaka mitano,sasa kama kesho akiwepo kitendo hiko hakitakubalika na kinafaa kupingwa ka kila Mtanzania”amesema Profesa Lipumba.

      Kuibuka huko kwa Profesa Lipumba kunakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya Wabunge wanaounda muunganiko wa Vyama vya Ukawa,kumwandikia Barua Spika wa Bunge wa Job Ndugai na kutaka uharali wa Rais Magufuli kuhutubia Bunge wakati Zanzibar bado hawajapata Rais wake.
      Akisoma Barua hiyo jana Mjini Dodoma kwa niaba ya Wenzake mwenyekiti mwenza wa Umoja huo,Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Ukawa hawatakakubali katika mazingira yeyote kuruhusu katiba ya nchi ambayo imetokana na matakwa ya wananchi ikuvunjwa hadharani.

     Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hai amesema njia pekee watakayotumia mwaka huu si ile waliyotumia mwaka 2010 kumsusia Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoka nje kuhu wakidai njia watakayoitumia sahivi ni kupambana ndani ya Bunge mpaka haki itakapopatikana.

      Huku wakificha njia watakayotumia kwa kuwataka wanahabari wasibuli siku hiyo ifike.

Watanzania Wenzangu Tumombee Rais Wetu Kutokana na Hizi Changamoto Kubwa Kwake

0
0
Ninawaomba watanzania tumwombee Rais wet mheshimiwa Magufuli kutokana na changamoto zilizo mbele yake. Ninajua Magufuli ana moyo wa dhati kuwatumikia watanzania lakini yafuatayo ni changamoto kubwa kwake.

'1. Chama chake. Chama chake ni mzigo na yeye si mwenyekiti. Lolote akaloamua chama kinaweza kukataa na hawezi kufanya chochote. Kwa jinsi hii mabadiliko ya Magufuli ni ndoto, Hayo yatamshosha Magufuli upesi sana.

2. UKAWA. Kwa hali halisi Ukawa wana wanachama wengi sana na mpaka kesho wanaamini Lowassa ndiye rais Hii ni changamoto kufanya na watu wasiokukubali. Itabidi utumie nguvu kubwa sana kuwatawala.

3. Uchaguzi wa Zanzibar. Ninafikiri mambo ya Zanzibar yanamuumiza kichwa kama yanavyotuumiza na sisi

4. Kutekeleza ahadi zako ambazo kwa uhalisia wa chama chako hazitekelezi.

Kutokana na haya mambo ninaona utawala wa Magufuli ukiwa mgumu kwa wakati huu wa mwanzo ndiyo maana watu wanaotakia nchi yetu mema inabidi tumombee hili Mungu ampe hekima katika kukabiliana nayo.

CHADEMA na Maajabu ya Musa Leo Bungeni!! Wamuuliza Dr Tulia Alijiunga Lini CCM...Je Lowassa na Duni Haji Alijiunga Lini Chadema ?

0
0
 Lowassa‬ aliingia CHADEMA saa mbili kamili Asubuhi, ilipofika saa mbili na dakika tano akawa mgombea Urais wa# CHADEMA.....
,Babu ‪#‎Duni‬ aliingia chadema saa sita na saa sita na nusu alikua mgombea Mwenza na Wote waliingia CHADEMA Wiki Moja kabla ya Kampeni kuanza,

- Leo CHADEMA wanamuuliza Dr ‪#‎Tulia‬ Bungeni alijiunga CCM lini? haya ni maajabu ya Musa!!,

KUMBE MZEE MKAPA ANA AKILI SANA, ALISHAWAJUA SIKU NYINGI SANA!!


Le Mutuz Nation

Mama Amchoma Mwanaye Kwa Maji Moto Baada ya Kumtuhumu Ameiba Nyama Jikoni

0
0
 Polisi mkoa wa Mara inamshikilia mwananke mmoja (jina tunalo) mkazi wa Bweri Manispaa ya Musoma kwa kosa la kumchoma mtoto wake mwenye miaka minne, kwa maji ya moto, mikono yote miwili baada ya kumtuhumu kuwa ameiba nyama jikoni.

Mama huyo alikamatwa Novemba 14 saa nne asubuhi katika eneo la Morembe kata ya Bweri mjini Musoma baada ya Polisi kufika nyumbani kwake kumkamata kwa kosa jingine la kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili Kabula Rubeni (32) akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, ACP Alex Philip Kallangi alidai kuwa siku ya tukio hilo la kumchoma moto mtoto huyo, mama yake mzazi alikuwa amepika nyama jikoni na baadaye alikwenda kuchota maji.

Kamanda Kallangi alidai baada ya mama huyo kurudi alimkuta mwanaye anakula nyama ndipo alishikwa na hasira na kuanza kumchapa sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha akachukua mikono yote miwili na kumchoma kwa maji ya moto.

Baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama, mama huyo alianza kumtibu mtoto huyo kwa siri hapo nyumbani kwa dawa za kienyeji bila majirani kufahamu kilichokuwa kikiendelea nyumbani kwa mama huyo.

Kamanda Kallangi alieleza kuwa kilichosababisha kufahamika kwa taarifa hizo, ni baada ya Kabula aliyekuwa ameshambuliwa kwa mapanga na mwanamke huyo kwenda polisi kutoa taarifa ya kushambuliwa.

Kallangi alieleza kwamba polisi walipofika nyumbani kwake ndipo walipewa taarifa za mtoto huyo kujeruhiwa kwa kuchomwa moto. Kutokana na tukio hilo polisi hao, kwa kushirikiana na maofisa ustawi wa jamii na kituo cha ushauri cha Jipe Moyo walimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa matibabu na kisha kupelekwa Jipe Moyo anakoishi hadi sasa kwa uangalizi zaidi.

Kallangi alisema mtuhumiwa huyo yupo kituoni na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu mashtaka yanayomkabili.

Ofisa Ustawi wa Jamii Musoma, Vedastus George aliwataka wazazi na walezi kuzuia hasira zao pale watoto wanapowakosea na hata wanapowaadhibu wawe makini ili waziwaumize kama alivyofanyiwa mtoto huyo.


UKAWA Wapigwa Mkwara Mzito..Watahadharishwa Wakifanya Vurugu leo Wakati Rais Anahotubia Wataikiona cha Moto

0
0
Nape Nnauye
Wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa wameonywa kutofanya jambo lolote litakaloashiria kuvuruga Bunge wakati Rais John Magufuli atakapolihutubia leo jioni.

Akiongea jana mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye alisema kuwa Wabunge hao wa Ukawa wanapaswa kufahamu kuwa kitendo chochote watakachofanya kwa lengo la kuvuruga hotuba hiyo ni kinyume cha sheria na taratibu za Bunge na kwamba hawatavumiliwa.

Nape alionesha kuwashangaa wabunge hao kudai kuwa hawamtambui Rais Magufuli ili hali wanashiriki katika shughuli zote za Bunge ikiwa ni pamoja na kumpigia kura Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa na Rais huyohuyo wanaedai hawamtambui.

Naye Mbunge wa jimbo la Nzega, Dkt Khamis Kigwangala alisema kuwa wabunge wa Ukawa wana haki ya kuingia Bungeni na kukaa kwa utulivu au kutoka nje endapo hawatakuwa tayari kusikiliza hotuba hiyo lakini sio kuvuruga hali ya amani ili watanzania wasipate nafasi ya kumsikiliza Rais.

“Hawawezi kuwanyima haki watanzania kumsikiliza Rais wetu akiwa anatoa dira ya uelekeo wa Taifa letu,” alisema Khamis Kingwangala.

Wabunge wa Ukawa juzi walifanya mkutano na vyombo vya habari na kueleza kuwa hawatakubali kumuona Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein akiingia katika Bunge hilo leo kwa kuwa kipindi chake cha urais Zanzibar kimekwisha.
 
Walisisisitiza kuwa watafanya ‘jambo’ ambalo hata hivyo hawakulitaja. Wabunge hao pia walisema kuwa wamemuandikiabarua Spika wa Bunge kuhoji uhalali wa hotuba ya Rais wakati Zanzibar bado haijampata Rais mpya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Tarehe 20, Ikiwemo ya Magufuli, Ukawa ni Mshike mshike leo

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Tarehe 20, Ikiwemo ya Magufuli, Ukawa ni Mshike mshike leo

Udaku Special Blog

Boko Haram Overtakes ISIS As World's Deadliest Terror Organisation

0
0

According to the Global Terrorism Index 2015, Boko Haram has overtaken Isis as the world's most deadly terrorist organisation.

The Nigerian-based terror group, also known as Islamic State's West's Africa Province (ISWAP), was responsible for 6,644 deaths in 2014.

In comparison, ISIS is believed to have killed 6,073 people in the same period. Boko Haram pledged allegiance to the group, also known as the Islamic State, in March of this year.

ISIS has certainly sought - and achieved - global notoriety since it announced its creation of a caliphate across Syria and Iraq in June 2014.

It has its own media arm which pumps out propaganda videos and messages to either inspire supporters or strike fear into those it regards as enemies with graphic footage glorifying executions and torture. It has also claimed responsibility for the most recent terror attacks in Paris and Egypt, where a plane containing 229 was downed.

Boko Haram carries out most of its atrocities in north Africa. Over the past year, Nigeria witnessed a 300 per cent rise in fatalities from terror acts to 7,512. This is the largest increase in terrorist-caused deaths ever recorded by any country, and is predominantly down to Boko Haram's expansion.

In 2013, Nigeria ranked fifth in terms of the highest levels of deaths, but moved to second last year.

Boko Haram is not limited to Nigeria: in 2014 the group doubled its attack and expanded into Chad and Cameroon, in 2014 staging 46 attacks and claiming 520 lives.

While increased use of explosives and bombs – thanks to training from other terrorist outfits – has characterised more recent Boko Haram attacks, the majority of attacks remain armed assaults using machine guns.

The data, published in the third edition of the Global Terrorism Index, was produced by the Institute for Economic and Peace, and drawn from data collected by the Global Terrorism Database (GTD), collated by the National Consortium for the Study of Terrorism and Responses to Terrorism.

Source: The Independent

Rais Kikwete Alishindwa Haya, JE John P. Magufuli Ataweza?

0
0
Rais Magufuli na Jakaya Kikwete
Maisha bora kwa kila mtu ni sera ya CCM, ambayo kiukweli ni nzuri sana na inaleta matumaini kama ikitekelezwa, ila utelezaji wa sera hii unapambana na vikwazo vingi ambavyo sijui rais John Pombe Magufuli ataviweza, maana mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete vilimshinda kabisa, vikwazo vikuu vya utekelezaji wa sera hii ya maisha bora kwa kila mtu baadhi ni vifuatavyo:-

1.Watumishi wa serikali, hasa wa halmashauri siyo waaminifu (yaani ni one hundred percent corrupt), kwa sababu kutekeleza sera hii serikali kuu inatuma hela nyingi sana kwenye halimashauri za wilaya ambako watu ndiko walipo ili kutekeleleza miradi mbali ya maendeleo. Kule pesa inakutana na watumishi ambao ni corrupt, wanashambulia hela zote za miradi kwa kujenga mabangaloo, wananunua posh cars kwa hiyo miradi ya maendeleo inakwama automatically na sera ya maisha bora kwa kila mtu nayoinakwama.


2.Watumishi niliowataja hapo juu kwa mujibu wa utaratibu wanasimamiwa na madiwani waliopo katika halimashauri hizo, sasa madiwani hao uwezo wa kuwasimamia vizuri hawana kwa sababu elimu zao wengine ni duni sana, hasa madiwani wa viti maalumu. Katika halmashauri nyingi madiwani hawa ni mizigo tu, kwa hiyo watumishi ambao sio waaminifu wanautumia vizuri mwanya huu kuikwamisha sera ya maisha bora kwa kila mtu, kwa kuwalambisha hela kidogo madiwani hawa halafu wenyewe wanakwapua nyingi.


3.Serikali yenyewe kwa ujumla ni dhaifu, inashindwa kabisa kuwachukulia hatua wabadhirifu hawa inaishia tu kuwahamisha toka halmashauri moja kwenda ingine.


4.Idara ya usalama wa taifa(TISS) nayo imezorota sana, kule wanawaona kabisa watumishi ambao siyo waaminifu wanavyofanya wananunua magari mawili mawili na kujenga nyumba kali ndani ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa lakini hawapeleki habari kunakohusika, wanashughulika na mambo yasiyokuwa na tija kama kufuatilia mikutano ya CHADEMA.

Mh. John Pombe Magufuli akiweza kuyadhibiti hayo hapo juu, basi maisha bora kwa kila mtu inawezekana.

By laurent Msembeyu/JF

Obama Amevuta Sana Sigara, Ndani ya White House je? Jibu Hili Hapa..

0
0
Rais Barack Obama anakaribia kumaliza muhula wake wa pili kuiongoza Marekani tangu mwaka 2008, lakini kuna tabia yake aliyokuwa nayo muda mrefu ya kuvuta sigara… alipoingia White House aliendelea kuvuta?

Obama alihojiwa na kwenye sentensi za kwanza kajibu hivi >>> “Sijavuta sigara hata moja ndani ya miaka mitano tangu nimeingia Ikulu… Niliahidi kwamba Muswada wa Sheria mpya ya Afya ukipita (2010) sivuti tena sigara, na kweli imetimia“.

Obama anasema alijaribu mara kadhaa kuachana na sigara mwaka 2008 wakati wa Kampeni  za Urais lakini ilishindikana, kuna wakati alijikuta akijibana zake kona na kuvuta tena na tena !!

Unajua kingine alichojibu Rais Obama kuhusu kuacha kuvuta sigara >>> ‘Namuogopa mke wangu’… Michelle kumbe nae hakuipenda tabia ya uvutaji sigara ya Obama iendelee !!

Achana na hayo, swali jingine la kizushi kwa Obama… akiwa zake ‘out’ na Michelle wake wanakula raha, simu ya nani anaweza kupokea ikiita? >>> “Mmmmh… labda ya Malia, Sasha (watoto wake) na mama mkwe.. nyingine ya mshauri wangu wa usalama Susan Rice, na Katibu Mkuu Kiongozi,  Denis McDonough” >>> Barack Obama.

Chagga Barbie Ndiye Ameziba Nafasi ya Shamsa Ford kwa Nay Wa Mitego? Nay Azungumza

0
0
Jimbo la mapenzi la Nay Wa Mitego liko wazi toka aachane na aliyekuwa cousin mpenzi wake Shamsa Ford, lakini swali ni kwamba ni mrembo gani aliyerithi nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Shamsa ambayo huenda kuna warembo wengi wanaitamani?
Kama unamfatilia Nay Wa Mitego kwenye akunti yake ya Instagram sina shaka utakuwa umeanza kuona dalili za kuwa kuna mpenzi mpya ‘mteule’ anayesubiri ‘kuapishwa’ na kuwa rasmi.

Chagga Barbie sio jina geni, ndio yule aliyezitawala headlines nyingi alipokuwa mpenzi wa Prezzo, jina lake halisi ni Starlisha Tillya lakini sasa anatumia jina la Chagga Empress Instagram.

Nay na Chagga ambaye ni Mtanzania aishiye Marekani wamekuwa wakiweka post zinazoashiria kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao zaidi ya urafiki wa kawaida, lakini Nay amesisitiza kuwa hawajaingia kwenye ukurasa wa mahaba japo Nay amekiri kuwa anampenda sana Chagga Barbie.

Novemba 11, Chagga alipost video akisema anampenda Nay, na Nay aliirepost na kuandika “Love you too bby Mtag umpendae @chaggaempress @chaggaempress”.


Naomba tu watu wajue ni mwanamke ambaye ninampenda, nampenda the way alivyo ni mwanamke mzuri anavutia sio vinginevyo, labda ikija ikatokea akiwa mwanamke wangu itakuwa ni poa zaidi lakini for this time nampenda the way alivyo” Nay ameiambia Bongo5.

Mimi na Shamsa tulishaachana muda mrefu tumebaki washkaji ana bwana yake nafikiri watu wanaona kwenye page yake anampost, lakini mwisho wa siku nafasi ikishaachwa na mtu watu watajua wataona tu dalili, for this time sidhani kama natakiwa kuongea mengi sana nafikiri watu wataona, lakini watu wajue kwamba Chagga ni mwakamke ambaye nampenda namkubali amekuwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ni mwanamke mzuri so haijafikia hatua ya kuwa na mahusiano ya kihivyo ila ikifikia watu wataona coz tuko karibu.” Alisema Nay.

Nay amesema kuwa yeye na Charga Empress bado hawajakutana lakini watakutana hivi karibuni.

Nafikiri tutakutana hivi karibuni, hivi karibuni tutakuwa pamoja bado hatujaonana”.- Nay

Steve Nyerere: Nilimwambia Rais Magufuli Kuwasaidia Wasanii wa Bongo Movies ni Kupoteza Pesa..Wengi ni Wauza Sura Tuuu

0
0
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Club, Steve Nyerere amesema aliulizwa kwa zaidi ya mara sita na Rais Dk John Magufuli kuhusu nsaada wanaouhitaji, lakini amedai alishindwa kumjibu kutokana na wasanii wengi kutojitambua.

Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV, Steve alisema alimwambia Magufuli asipoteze pesa ya serikali kuwasaidia wasanii wa filamu.

“Sikatai,” alisema Steve. “Nilishamwambia mheshimiwa rais, utapoteza pesa zako, nilisha mwambia mstaafu na huyu mpya utapoteza pesa!

Kwa sababu lazima tukae chini tujitafakari tunataka nini? Mimi ni mtu niliyewahi kuulizwa na mheshimiwa Magufuli zaidi ya mara 6, niliulizwa na mheshimiwa rais tukiwa Morogoro. Serikali haiwezi bila sisi wenyewe kujitambua hata uweke mabilioni ya pesa,” alisisitiza.

Pia Steve alisema wasanii wengi wamejivisha joho la usanii wa filamu lakini hawafanya kazi.

Kwanza tuna asilimia 90% ya watu kwenye hii industry ya filamu hawajaingia kufanya kazi,” alisema. “Ukichunguza sana watu wamekuja kuuza sura, ukichunguza sana asilimia 90% walioingia kwenye filamu, 6 au 5 ndio wana nia ya kufanya kazi. Hawa wote walioingia wanaingia wapate jina wafanye mambo yao ambayo sio ya kuinua sanaa.”

Kwenye mahojiano hayo pia Steve alisema tasnia ya filamu nchini imefika sehemu mbaya na inaelekea kufa kabisa.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images