Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Bond wa Wastara Afanya Maamuzi Magumu, Aomba Radhi, Akata Rasta na Kusema Alikuwa Akiishi Kwenye Kivuli cha Shetani

$
0
0
Mchumba wa Wastara Mr Bond Amefunguka Haya Kwenye Ukurasa wake wa Facebook:

"Alhamdulillah
Namshukuru mungu kwa kunisimamia kwa hili jambo kwani haikuwa kazi rahisi kuachana na kila kitu na kuamua kutafuta upya maisha yangu halisi na yaukweli
Pia nashukuru wote mlioniombea mema katika siku hizi arobaini za kukaa Sober mungu atawalipa kwa dua zenu
Pia nichukue nafasi hii kuwaomba msamaha wote nilio wakosea kwa nililuwa siishi maisha yangu halisi bali nilikuwa katika kivuli cha shetani, hivyo naomba msamaha kwani sote ni binaadamu na hatuja kamilika.
Let us seak for the new bigining In shaa Allah" Bond

Rais Magufuli Tena..Afuta Majina ya Maafisa wa Serekali 50 Waliokuwa Wasafiri Kwenda Mkutano wa Jumuiya ya Madola..

$
0
0
Rais John P. Magufuli amefuta majina ya maafisa wa Serikali 50 na kubakiza 4 tu waliotakiwa
kwenda kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola

Hatua yake hiyo imeokoa takribani milioni 700 ambazo zingetumika kwenye malipo ya posho na tiketi za ndege

PICHA Mbili za Mwigizaji Ray zilizozua Maneno Maneno Huku Instagram...Mashabiki Wampa za uso laivu

$
0
0
Ray kawa Mzunguu  Revolution of a man 
 Kama Ni pesa basi 50cent angekuwa Na rangi ya mfupa

Comments za Baadhi ya Mashabiki wake hizi Hapa chini:

 kebbyrogers
Hivi huyu si mtoto wa kiume huyu au........😇

 dorin_onesmo
Anatumia vpodoz vya mpnz wake chuchu 1h

kikiedwin
Hereni za nini vaeni zile za kimasai msiige wazungu

 hamdansd11
Kajichubua kawa mzuri kama lulu na wema

hanceblicks
Huyu sasa ata kuwa mwanaume wa kwanza kubeba mimbaaa

6750_jay
 Ndio Mabadiliko aliyokuwa anatafuta ana utofaut na wanawake wakeko wenzao washindana kupata pesa na degree kuongeza vyetu wenyewe wanashindana kuwa weupe

 james_turuka
 MWEUSI ATABAKI MPOKI TU

gmbega 
Hii aibu, dume zima, au linatangaza biashara?

stara_gal Njoo umuone Ray kabadili housing @ashmanreal



MEMBE "Mhe Zitto Kabwe Hongera kwa kuwaonyesha Watanzania tofauti kati ya ACT Wazalendo na UKAWA"

$
0
0
Mhe Zitto Kabwe Hongera kwa kuwaonyesha Watanzania tofauti kati ya ACT Wazalendo na UKAWA kuanzia tarehe 5/11/15 siku ambayo mgombea Urais wa ACT alikwenda Diamond Jubilee Hall na kuonyesha ukomavu na uzalendo tofauti na UKAWA na jana wewe mwenyewe ulipoamua kubaki ndani ya Bunge kuungana na wabunge wa CCM kusikiliza hotuba ya Mhe Rais. Hukufanya vile kupingana na UKAWA la hasha! Ulifanya vile kuonyesha kuwa ACT Wazalendo ni mpinzani mshiriki na siyo mpinzani mkosefu! Aidha kuacha wenzako wanatoka na ukabaki peke yako ni kitendo cha ukomavu na ujasiri. "Better him from within than Him from without" (Shakespeare) Wengi tunakupongeza! Membe.

Hamisa Mobeto: Lulu Michael Kanipora Bwana Angu

$
0
0
MAPENZI ya mjini utata mtupu! Ni kauli inayostahili kutumika baada ya mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto kumwaga chozi akidai kuporwa bwana’ke aliyekuwa akimpa jeuri mjini (jina tunalo) huku zigo la lawama likimwangukia staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

CHANZO KINASEMAJE?
Habari kutoka kwa chanzo makini zilieleza kwamba, kwa sasa kuna bifu jipya linalotokota mjini likihusisha sakata la Lulu kumpiku Mobeto kwa bwana’ke aliyekuwa akimgharamia kiasi cha kuwa mwanaume pekee aliyemwamini hadi kufikia hatua ya kumzalia mtoto.

Ilidaiwa kwamba, jambo hilo Lulu hakulithamini na kuamua kumpiku huku akimuacha akiishia kulalama kila kukicha.

“Najua hamuujui mchongo huu. Sasa ngoja niwapashe habari kwa kina. Nimeamini Lulu kweli ni jasiri, maana kwa alichomfanyia Mobeto Mungu ndiye anajua.

PEDESHEE MPYA WA LULU?
“Huwezi kuamini yule bwana wa Mobeto Lulu kaamua kujiweka kwake, inaweza kuwa ngumu watu kukubali lakini ndiyo ukweli wenyewe.

“Unaambiwa mtiti wa Mobeto na Lulu ulianza kama mwezi mmoja uliopita. Walianza kwa kuandikana kwa mafumbo kama waimba taarab kwenye mitandao ya kijamii.

MAFUMBO INSTAGRAM
“Nimekutana na rafiki wa Mobeto ndiye kanipa mkanda wote kuwa Lulu kampiku Mobeto kwa bwana’ke ndiyo maana mafumbo hayaishi Instagram.

MOBETO HATAKI KUMSIKIA LULU
“Kwa sasa Mobeto hataki kusikia habari za Lulu na ukimuuliza anasema Mungu atamlipia kwani anamshukuru kumtoa huko kwani alipo sasa ana amani tele,” kilidai chanzo hicho.

MOBETO AFUNGUKA MAZITO
Kwa upande wake, Mobeto alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kuwa kwa sasa ana mambo yake mengine hivyo habari za Lulu ingekuwa vizuri akaulizwa yeye na huyo bwana’ke.

Mobeto alisema kuwa kwa sasa anachoweza kuzungumzia ni juu ya maisha ya mama yake mzazi na mtoto wake kwani hao ndiyo faraja pekee iliyobaki kwake.

Alisema kuwa, hapendi kuzungumzia mambo yaliyopita kwani kila jaribu lina mlango wake wa kutokea hivyo yawezekana yote Mungu aliyapanga akiwa na sababu za msingi.
“Mambo hayo mimi sitaki hata kuyazungumzia kwa sasa, nafikiri ingekuwa vyema ukamuuliza Lulu na ….(anamtaja huyo mwanaume) kwani wao ndiyo wanaweza kukupa ukweli na kukusimulia kiunagaubaga.

MOBETO AMWACHIA MUNGU
“Katika maisha yangu, kwa sasa namwangalia mtoto na mama yangu, hao wakikosa furaha hata mimi siwezi kuwa na amani kwenye maisha yangu, kwani mambo mengine yakishapita hakuna sababu ya kuyaendeleza zaidi namshukuru Mungu.
“Kwa sasa nina michongo yangu mipya na siko tayari tena kuzungumzia habari nje ya familia yangu.

“Ninachoweza kukuambia ni kwamba maisha yana kila staili ya kuishi hivyo sifikirii tena kuingia kwenye mitandao ya kijamii kuzungumzia habari za mtu kwani hata hao wanaonizungumzia sina muda wa kuanza kusoma comments (maoni) zao wala kuwajibu.

“Kwa kifupi sijawahi hata kuona mambo yanayozungumzwa kuhusu mimi kwenye mitandao maana huwa sisomi tena kwani kila mtu ana namna ya maisha aliyochagua.
“Hata huyo Lulu na timu zake mimi sina muda wa kusoma mambo yao kwani Mungu ndiye tegemeo langu,” alisema Mobeto.

LULU ARUKA MITA MIA
Alipotafutwa Lulu na kupewa taarifa za uporaji wa bwana wa mtu, aliruka mita mia moja kwa kusema kuwa habari hiyo ni mpya kwake na hajawahi kusikia lolote ila ndiyo anaambiwa kwa sasa hivyo kama kuna mtu ana picha zake na huyo bwana wa Mobeto, basi ndiyo anapata taarifa.

“Madai haya kwangu ni mapya na siyajui ndiyo mnaniambia kwa mara ya kwanza, sioni sababu ya kulizungumzia,” alisema Lulu.

Chanzo:GPL

‘Mzimu’ wa Kanuni Wamwandama Naibu Spika..Wasomi Wadai Amekiuka Kanuni za Utumishi wa Umma

$
0
0
Ushiriki wa aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Tulia Ackson katika masuala ya siasa na hatimaye kuchaguliwa Naibu Spika wa Bunge, umezidi kuibua maswali huku akidaiwa kuwa amekiuka kanuni za watumishi wa umma.

Wasomi, wanaharakati na wanasheria wameeleza kushangazwa na uteuzi huo, kama ilivyokuwa Alhamisi alibobanwa kwa maswali bila majibu kuhusu ni lini msomi huyo wa sheria alichukua kadi ya CCM na kuwania uspika na baadaye unaibu spika kupitia chama hicho.

Hata hivyo, Dk Ackson amekanusha kukiuka kanuni za utumishi wa umma akisema ile inayolalamikiwa kukiukwa (Kanuni za Utumishi wa Umma 2009), ilifutwa kupitia waraka mpya uliotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Januari, mwaka huu.

“Angalia hiyo ‘circular’ kifungu cha (5), kinasemaje, usiangalie hiyo kanuni tena kwani imefutwa na huo waraka, ukisoma unaonyesha wazi. Zote hizo unazoniambia nilizifahamu kabla ya kuchukua hatua yoyote, sijakurupuka tu,” alisema.

Wiki iliyopita Dk Ackson akiwa mwanasheria wa Serikali alichukua fomu ya kuwania uspika wa Bunge kinyume na matakwa ya kanuni za utumishi wa umma, lakini baadaye alijitoa katika kinyang’anyiro hicho na kuwania unaibu spika, baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mbunge.

Mchakato wa Dk Ackson kuteuliwa kugombea hadi kushika nafasi hiyo umezua maswali watu mbalimbali wakihoji ukiukaji wa kanuni hiyo inayozuia wanasheria wa Serikali kujiunga na mambo ya siasa.

Akijibu maswali ya wabunge wakati akiomba kuchaguliwa kuwa naibu spika, Dk Ackson alishindwa kueleza ni lini alichukua kadi ya CCM, hadi Spika wa Bunge Job Ndugai alipoingilia kati akamruhusu kwenda kuketi.
Wachambuzi

Akizungumzia suala hilo, mwanaharakati kutoka HakiElimu, Godfrey Bonaventure alisema kitendo cha Dk Ackson kuteuliwa kushika nafasi hiyo kinaleta maswali mengi katika kanuni za utumishi wa umma na masuala ya siasa.

“Miongozo iliyopo imeweka bayana kuwa wapo watumishi wa umma ambao hawatakiwi kujihusisha na siasa kutokana na unyeti wa majukumu yao,” alisema.

Alisema suala kubwa ambalo Dk Ackson anatakiwa kujibu kwa usahihi ni je, lini alianza kuwa mwanachama wa CCM?

“Watu wanaotakiwa kuhusika kwenye uamuzi mkubwa hawatakiwi kujihusisha kwenye siasa. Hili suala lina mitego ambayo inavuruga mfumo wetu wa uwajibikaji, inatupa shaka kwa sababu hawa watu maamuzi yao ni magumu, uspika ni wajibu mkubwa,” alisema.

Bonaventure aliitaka Serikali kuheshimu miongozo yote ya utumishi wa umma ili vyombo hivyo viwe huru kufanya uamuzi.

“Alipoulizwa swali bungeni kuhusu lini alikuwa mwanachama  wa CCM hakuweza kutoa jibu sahihi, bila shaka angesema ni lini angeibua maswali mengi zaidi,” alisema.

Alisema iwapo Dk Ackson angesema amekuwa mwana CCM kwa muda mrefu angeibua maswali, lakini pia angesema amechukua kadi ya CCM hivi karibuni angeibua hoja atawezaje kukifahamu chama na kujua namna ya kuliongoza Bunge katika kipindi kifupi?

Mwanasheria wa kujitegemea, George Shayo alisema sheria inaweka wazi kuwa watumishi wa Serikali hawatakiwi kushiriki katika siasa.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema sheria zinakataza watumishi wa umma kujihusisha na siasa.

Profesa Safari ambaye pia ni wakili, alisema ingawa baadhi ya vipengele vimefanyiwa marekebisho lakini wafanyakazi wa Mahakama na wanasheria wa Serikali hawatakiwi kujihusisha na siasa.

“Ndiyo maana hata wakati Jaji Augustino Ramadhani alipochukua fomu ya urais, tulimsema sana. Hata hizi sarakasi za Dk Ackson zinachekesha, zinashangaza,” alisema.

Mhadhiri  wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es  Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema anafahamu kuwa kuna sheria kuhusu wafanyakazi wa umma lakini haiwakatazi kujihusisha na siasa bali upo utaratibu wa kufanya hivyo.

“Iko miongozo ya Serikali kuhusu watumishi wa umma lakini si kwamba sheria inakataza, kwa mfano miongozo hiyo inawataka waache nafasi zao pindi wanapotaka kuingia katika siasa,” alisema.

Simulizi ya Wachimbaji Walivyookolewa Kutoka Mgodini Baada ya Kukaa Siku 41 Chini ya Kifusi

$
0
0
Mmoja wa watu waliokuwa kuwa wakifanya kazi ya kuwaokoa wachimbaji wa madini walionusurika kufa  baada ya kuporomoka kifusi kwenye machimbo ya Nyangalata Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuishi kwa siku 41, Mohamed Churi amesema ilikuwa kazi ngumu kuwatoa kutokana na mazingira yalivyokuwa hatarishi kwa maisha yao.

“Ilikuwa ni kazi ngumu kuingia kwenye shimo lenye njia nyembamba ambalo likiguswa, udongo unaporomoka na kuwafukia wote,” alisema.

Churi aliyekuwa akiwatoa wachimbaji hao moja baada ya mwingine, alisema kazi hiyo ilihitaji tahadhari kubwa na uangalizi wa hali ya juu.

  Alisema siku ya kwanza aliingia kwenye shimo lililopo  jirani kwa ajili ya uchimbaji na kusikia sauti ya watu wakiomba msaada wa kuokolewa.

Alisema sauti hizo zilimshtua akidhani huenda ilikuwa ni mizimu ya kwenye machimbo kwa kuwa hakuwa na wazo kama wachimbaji hao wangekuwa hai hadi siku hiyo.

 Churi alisema alivutasubira huku akiendelea kuwadadisi na walipoanza kujieleza mmoja baada ya mwingine na kujitambulisha majina yao, alitoka nje kwenda kutoa taarifa kwa uongozi wa mgodi huo. Alisema uongozi huo ulishindwa kuamini kama kulikuwa na wachimbaji waliofukiwa na kifusi kama walikuwa bado wako hai.

 Baada ya kuthibitika taarifa hizo, Churi alisema aliongoza msafara kuingia kwenye shimo ambalo chini yake kuna shimo ambamo wachimbaji hao walikuwa hai.

Alisema kabla ya kuingia ilimlazimu apate kilevi ili aondoke katika hali ya kawaida na woga.

 Churi alisema baada ya kufika kwenye chumba cha kwanza, kazi ilikuwa ni kuangalia namna ya kutoboa ili kuwafikia walipokuwa wachimbaji hao kwa kuwa walikuwa chini ya shimo na wao juu. “Tulifanikiwa kutoboa tundu dogo tukawaona, walikuwa umbali wa mita kama 20 kutoka chumba tulichokuwa, wenzangu wakabaki hapo kwenye kituo.

“Baada ya hapo, wakanifunga kamba, nikashuka nayo na kutokana na ufinyu wa njia kwenye shimo, nilichubuka mikono na taratibu niliwafikia,” alisema Churi. Alisema hali aliyowakuta hawezi kusimulia yote, (alinyamaza kisha kuanza kulia).

Baada ya kunyamaza, aliendelea kusimulia kuwa walikuwa sehemu nyembamba kwenye giza nene na harufu mbaya ya mwenzao, Mussa  Supana aliyekuwa amekufa pembeni na mwili wake kuanza kuharibika huku kiwiliwili kuanzia kiunoni hadi miguuni kikikiwa kimefunikwa na kifusi huku kikiwa kimebaki kichwa na kifua.

“Nilianza kuwabeba mmoja mmoja na kupanda nao kwenye kamba hadi kituo walichokuwa wenzangu ambao nao walinisaidia kuwatoa nje,”  alisema Churi.

Alisema wachimbaji hao walikuwa wamekonda mithili ya  watoto wadogo hali iliyomrahishia kazi ya  kuwabeba kutoka kwenye shimo walimokuwa kutokana na kupungua uzito. Alidai kila mmoja alipungua na kubaki uzito wa kilo zisizofikia 20.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Kahama, Dk Joseph Ngowi alisema wachimbaji hao,  Chacha Wambura, Joseph Bulule, Amosi Mhangwa na Msafiri Gerald,  hali zao zinaendelea vizuri isipokuwa Onyiwa Moris amegundulika kuwa na tatizo la kifua.

  Wachimbaji hao walifunikwa na kifusi Oktoba 5, mwaka huu katika machimbo hayo na kuokolewa Novemba 15  baada ya kuishi humo kwa siku 41,wakinywa maji magome ya miti, wadudu wakiwamo mende na chura.

Zitto: ACT - Wazalando itashirikiana na Magufuli

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema chama cha ACT-Wazalendo kitashirikiana na Rais John Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Zitto alisema nchi inanuka uvundo wa ufisadi na kwamba Taifa limepata kiongozi mwenye nia ya dhati ya kupambana nayo kwa dhati na hivyo Watanzania wanalo jukumu la kumuunga mkono.

“Nilipokuwa mwenyekiti wa Kamati za Bunge nimekuwa nikitoa taarifa mbalimbali dhidi wizi na uporaji uliofanywa katika ubinafsishaji, sasa tumepata Rais ambaye kaamua kupambana na ufisadi kwa dhati, kaamua kurejesha viwanda vyetu vilivyouzwa ovyo, ni wajibu wetu kumuunga mkono,” alisema.

Alisema asilimia 60 ya masuala yaliyotajwa na Rais Magufuli katika hotuba yake yanatoka kwenye ilani ya ACT ambayo walimkabidhi wakati alipotangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.
Akizungumzia kitendo cha Zitto kutoungana na wabunge wa Ukawa kususia hotuba ya Rais, mshauri wa ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo alisema huo ni msimamo wa chama hicho kwa kuwa matatizo ya Zanzibar yatatatuliwa kwa njia za kisheria na kisiasa.
Alisema chama hicho kinamtambua Dk Magufuli kama mshindi halali wa kiti cha urais.
“Katika hili la Zanzibar tunafanana katika msingi wa hoja lakini tunatofautiana katika mkakati wa utekelezaji wa hoja husika na hili halina ubaya wowote, ni afya kabisa kwa demokrasia yetu,” alisema Mkumbo.

Niwemugizi  ataka aungwe mkono
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severine Niwemugizi amesema hotuba ya Rais Magufuli ni nzito inayohitaji kuungwa mkono na watendaji wote wa Serikali kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa.
Kauli ya kiongozi huyo inatokana na Rais Magufuli kuwahakikishia Watanzania kuwa atapambana kufa na kupona dhidi ya vigogo ambao wamekuwa wakihujumu maendeleo ya umma kutokana na rushwa, ufisadi na uzembe.

Alisema kutokana na nchi ilipofikia, Watanzania wanapaswa kumuunga mkono katika mkakati wake wa kupambana na ufisadi.
Askofu  huyo alitoa kauli hiyo jana kwenye ibada maalumu iliyofanyika kwenye Parokia ya Chato, kwa lengo la kumwombea Rais Magufuli ili aweze kutimiza majukumu yake katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

“Hotuba ya mheshimiwa Rais Magufuli ilinifurahisha sana... lakini iliitia woga sana kwa sababu ya wale viongozi wanaoona wamemuingiza madarakani mwenye kuziba mianya ya rushwa, hivyo watajitahidi sana kuhujumu afya yake na hata malengo yake kwa kuwa amejiita ni mtumbua jipu.
“Mtakumbuka kabla ya kuhitimisha hotuba yake aliwaomba Watanzania tumwombee, ndiyo maana sisi kama kanisa tumeamua kumwombea ili Mungu amtangulie katika mambo yote... tunatambua atakutana na vigingi vya kila aina.”

Mbali na kumwombea kutimiza wajibu wake, ibada hiyo pia imetumika kuliombea Taifa kudumisha amani upendo na mshikamano kwa kuwa bila ya amani, nchi haitaweza kutawalika.
“Tunatakiwa kutumia muda wetu mwingi kuliombea Taifa amani... Rais Magufuli atapata wakati mgumu sana kuiongoza nchi hii iwapo hapatakuwa na amani,” alisema.
Akizungumza katika ibada hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe alisema kwa sasa Watanzania wanatakiwa kuwa wamoja kwa kumuunga mkono Rais aliyeko madarakani ili aweze kutimiza majukumu yake.

Alisema ili wananchi waweze kufikia maendeleo ya kweli, wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kutimiza falsafa ya “hapa kazi tu” hatua itakayowasaidia kuinua uchumi wao.

Profesa Lipumba ajadili hotuba
Akizungumzia hotuba ya Dk Magufuli, Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema ili afanikiwe kutekeleza sera ya viwanda, dawa pekee ni kuwanyang’anya wawekezaji waliohodhi bila kuviendeleza.
Tayari Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru ametoa tangazo la kuwataka wawekezaji walionunua mashamba na viwanda vya Serikali kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa mikataba ya mauzo ili kuwabaini waliokiuka masharti.
Mikataba yote ya mauzo ya viwanda na mashamba iliyoingiwa kupitia ubinafsishaji, itarejewa upya na kwamba  hatua stahiki zitachukuliwa ikiwamo kurejesha viwanda na mashamba hayo kwenye miliki ya Serikali kwa waliokiuka masharti.

CCM Zanzibar yailaani Ukawa
Katika hatua nyingine, CCM Zanzibar imelaani kitendo cha kuzomewa kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na Makamu wake wa Pili, Balozi Seif Ali Idd kilichofanywa na wabunge wa Ukawa wakati akiingia bungeni kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa Bunge la Kumi na Moja.
Katibu Kamati Maalumu ya NEC, Waride Bakari Jabu alisema kuwa kitendo hicho ni miongoni mwa vitendo vya ukosefu wa nidhamu kwa wabunge hao.

* Imeandikwa na Tumaini Msowoya, Joyce Mmasi na Haji Mtumwa.



Mmoja wa Watano Waliookolewa Mgodini Baada ya Kufukiwa Kifusi Kwa Siku 41 Afariki Dunia

$
0
0
MMOJA wa majeruhi watano waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kutokana na kufukiwa na kifusi cha mchanga na kukaa siku 41 chini ya mgodi na kuokolewa, Onyiwa Kaiwao (55) amefariki dunia.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Joseph Ngowi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa chanzo cha mauti hayo ni kutokana na majeruhi huyo kutapika akiwa amelala hali ambayo ilifanya matapishi hayo kuingia katika njia ya hewa.

Dk Ngowi alisema Kaiwao alifariki jana saa sita mchana na kuongeza kuwa pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa nimonia unaosababishwa na baridi kali hali iliyomfanya kutokuwa katika hali ya kawaida tofauti na wenzake.

Hata hivyo, Dk Ngowi alisema majeruhi huyo pia alikuwa na matatizo katika utumbo, na hivyo kila akienda haja kubwa alikuwa akitoa magome ya miti waliyokuwa wakiyatumia kama chakula wakati wakiwa chini ya ardhi.

Jana (juzi) tuliwachukua vipimo waathirika wote watano na kuonesha kuwa hali zao ni nzuri, lakini Onyiwa alionesha kutokuwa na maendeleo mazuri tofauti na wenzake na ghafla akiwa amelala alijitapikia hali ambayo matapishi hayo yaliingia katika mirija ya hewa na kuziba hali iliyosababisha kifo chake,” alisema Dk Ngowi.

Alisema hali za majeruhi wengine wanne zinaendelea vizuri, na wanaendelea na mazoezi huku wakila wenyewe hali ambayo wamepanga kesho kuangalia uwezekano wa kuwafanyia vipimo kwa mara nyingine tena.

Aidha, Dk Ngowi alisema endapo hali zao hazitakuwa nzuri na kubadilika, watawahamishia katika Hospitali ya Rufaa kwa ajili ya uangalizi wa juu hali ambayo watapata mabadiliko zaidi ya afya zao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Shigitwa (SHIGOMIKO), Hamza Tandiko alisema wakiwa wachimbaji wadogo wa Mgodi wa Nyangalata wamekipokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwenzao na kuwataka waliobaki kutokata tamaa Mungu atawasaidia watapata nafuu.

Sisi kama wachimbaji hatupingani na Mwenyezi Mungu tulijitahidi kadri ya uwezo wetu kuokoa maisha yao kwa kushirikiana na uongozi wa Hospitali ya Wilaya, lakini kwa mapenzi ya Mungu ameamua kumchukua Onyiwa akapumzike na hakuna mtu anaweza kuzuia kifo,” alisema Tandiko.

Wachimbaji hao wadogo watano waliokolewa kutoka katika mgodi huo wiki iliyopita baada ya kukaa kwa siku 41 kutokana na kufukiwa na kifusi. Mwenzao mmoja alifia mgodini wakati wakisubiri majaliwa ya kuokolewa.

Chadema Kufungua Kesi Kupinga Agizo la Polisi Kuzuia Kuagwa Mwili wa Alphonce Mawazo.

$
0
0
Baada ya zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kushindikana kutokana na jeshi la polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku mikusanyiko ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa madai ya kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Mwanza, hatimaye viongozi wakuu wa kitaifa wa Chadema pamoja na familia ya marehemu wameamua kwenda mahakamani kesho kutafuta haki yao ya kisheria.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mwanza  na mwenyekiti wa Chadema taifa Mh. Freeman Mbowe akiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mh. Edward Lowassa.

Naye Mchungaji Charles Lugiko ambaye ni baba wa marehemu Alphone Mawazo amelaani  kitendo cha askari polisi kwenda hadi nyumbani kwake eneo la Nyegezi na kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa ajili ya kuuaga  mwili  wa  marehemu Mawazo.

Alphonce Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha katoro wilayani Geita.

Over 110 Ukawa Members Join CCM To Support Magufuli Movement

$
0
0


Handeni: As the campaign for Handeni Urban Parliamentary seat heats up, over 110 members of parties forming the Constitutional Coalition, Ukawa, have jumped ship to join the ruling party.

 A total of 115 members of the two parties in Handeni District handed over their parties’ cards to the CCM Regional Publicity Secretary, Mathew Mganga, at a campaign meeting to canvass support for the ruling Party’s candidate, Omari Kigoda at Kwenjugo Ward.

 The opposition members said that they were  determined to support Ukawa but were disappointed with the coalition’s failure to reach rapport on issues such as who would be the flag bearers for the coalition.

 “I did a lot of mobilization to make sure Chadema wins in the Civic elections but our District leadership did not offer satisfactory cooperation for grassroots members and their major focus was on the parliamentary seat alone,” said Rajabu Viuli, the former Chadema Secretary for Kwenjugo ward. Vuli added that the district leadership also failed to give the ward leadership grants to run the party.

 He said that they have decided to go back to CCM where they think they would work with the necessary support to bring changes in their new constituency.



Baada ya Kusikika Tena Kwenye XXL, DJ Fetty Ajibu Kama Amerejea Rasmi Clouds

$
0
0
Ijumaa ya November 20 ilikuwa ni siku ya furaha kwa wasikilizaji wengi wa Clouds Fm hasa wa kipindi cha burudani XXL, baada ya kupata surprise ya kumsikia tena mtangazaji maarufu na anayependwa Fatma Hassan maarufu kama DJ Fetty kwenye kipindi hicho, ikiwa ni miezi miwili imepita toka alipotangaza kuacha kazi ya utangazaji September 15 mwaka huu.

Wengi wao walicomment kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kuelezea furaha yao, na kwasababu hakusema kama amerudi rasmi kutangaza au laa, wengine waliamini kuwa mtangazaji wao amerudi.

Bongo5 ilimtafuta Fetty kutaka kufahamu kama ni kweli amerudi Clouds na ataendelea na kazi ya utangazaji, na jibu lake lilikuwa “Sijarudi”..

Na kuhusu sababu ya kusikika kwenye XXL ya Ijumaa November 20 alijibu;

Baada ya kuona kwenye acc ya insta yangu, they want to hear me so badly so nika wa surprise tu hivyo. But Sipo clouds” alisema Fetty.

Hizi ni comments za mashabiki wake baadaa ya kumsikia jana;

tamimugau- Hatimae umesikka katka kipind cha XXL…..tujuze labda kwnn uliamua kuacha kaz zen leo umerudi????

issathebwse- Jaman dada mbona umepotea kesho nenda studio tukuskie hata sauti jaman mie roho inaniuma sana

jumawaukwel- Fetty nimeijoi xana xxl leo ujue nilikua xhamba nafanya yangu nikapigiwa cm na mwanagu kwamba fee yupo mjengoni leo nikaacha kufanya yangu kuja kukusikiliza ww

elbasharsaid- UMERUDI or ulikuja kutuonjesha ladha tu alafu ndo jii tena Ama kweli kama umerudi big up Sana my @the best de

mamyakaro- Utuambie kama umerudi rasmi fetty coz nilizira kabisa kuckiliza xxl ila leo nilipockia tu sauti yako kwa mjengo bac daaaah,nikaahirisha kabisa kwenda kuoga@thebestfetty

candlesuleiman- Am back 2! Love u forever @thebestfetty. Ahsante kw kurudisha mood zetu uloamua kukimbia nazo name sasa umerudi nazo. Hapo surprise tu!

mwajabus92- Nimefurahi sana nilivyosikia sauti yako Leo clouz yani nilikuwa nakumiss hatari ndio umerudi moja kwa moja au ndio Leo ulikuja kutufurahisha love yo feeeee

zephaniamagesa82- umerudi nini yani toka uwondeke sijawahi sikiliza nijibu kama umerudi jamani my dj

Irene Uwoya Kurejea Kwenye Movie Kwa Style Hii

$
0
0
Irene Uwoya amerudi rasmi katika filamu baada ya kumaliza pilika pilika za uchaguzi ambapo ametangaza deal kwa vijana wapya katika filamu.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Irene ameandika:

Habari zenu wapendwa!kuna movie mpya naaandaa…tunahitaji wasanii wapya wakike na wakiume…ambao hawajawah kuigiza!kunamaswali tutauliza ukipita utaitwa kwajili ya form na mahojiano zaidi…..swali la kwanza!ntajie wasaniii watatu wanao kuvutia na kwanin?

Name And Shame! Taxi Driver Exposes Politician Who Has Been Having S£X With LADIES In His Car.

$
0
0

A taxi driver who operates in CBD has exposed a popular Jubilee politician who has a habit of having s3x with young ladies in his car.

According to the taxi driver identified as, Kamau, the s3x hungry politician, who was once accused of raping a married woman,  has become his regular customer and any-time he drives him home, he must have s3x with a lady in the cab.

“I think he just loves  the adrenaline that comes with having s3x in a cab. I pick him in a popular city club on  most weekends and any-time I drive him home, he must have s3x with a lady some as young as 19.”  Kamau said.


The politician lives in the posh Kitisuru Estate and is said to have divorced his wife.

The randy politician pays Kamau handsomely to buy his trust and they have unwritten rules that he should never reveal his escapades.

Kamau revealed to the media that most Nairobi men prefer to have s3x with their clandestine lovers in the cab and he is now forced to charge extra money for that service.

“I charge extra Ksh 2,000 if you want to transform my cab into a lodging for s3x.”  He said.

Utata Watawala Kifo cha Ghafla Cha Msemaji Wa Madereva, Rashid Saleh

$
0
0
Aliyekuwa Katibu na Msemaji wa Chama cha Madereva, Rashid Saleh amefariki dunia ghafla huku chanzo cha kifo chake kikizua utata miongoni mwa wananchama wa chama hicho na wananchi.

Taarifa za awali kifo cha Rashid Swaleh zilielza kuwa alifariki baada ya kuugua ghafla ugonjwa ambao bado  haujabainika.

Madereva na wananchi wengine walifika katika hospitali ya Muhimbili wakiwa na majonzi makubwa huku wakisubiri mwili huo wa marehemu upimwe ili kubaini chanzo cha kifo chake.

Baadhi ya madereva waliozungumza na waandishi wa habari walieleza kusikitishwa na msiba huo wa ghafla na kueleza kuwa huenda msemaji wao aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote haki zao amenyamazishwa.

“Sisi kama madereva hatutakubali, kama kosa lake yeye ni kutetea haki za watu, hili ni tatizo,” alisema mmoja wa madereva hao aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Mdem.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alifika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwataka madereva hao kutokata tama bali waendelee kudai haki zao huku wakisubiri majibu ya madaktari kubaini chanzo cha kifo cha msemaji wao.

“Hii isiwakatishe tamaa kuendelea kudai haki zenu ambazo ni za msingi kutoka kwa ajili wenu,” alisema huku akiwasihi kutofifishwa moyo katika kutafuta haki zao za msingi.

Wabunge Washindwa Kwenda na Kasi ya Magufuli... Wagomea Sh 90m za Kununua Magari ‘Mashangingi’

$
0
0
Wakati Serikali ikihaha kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake, wabunge wameingia kwenye mvutano na ofisi ya Bunge kuhusu fedha ambazo watunga sheria hao wanastahili kupewa kwa ajili ya kununulia magari yao.

Mwaka 2010, wabunge walilipwa Sh90 milioni kwa ajili ya ununuzi wa magari hayo aina ya Toyota Land Cruiser (hardtop), ambayo ni vitendea kazi vyao. Wabunge hutakiwa kulipa nusu ya fedha hizo wkati nyingine ni mchango wa Serikali.

Lakini wakati gharama za maisha zikipanda huku thamani ya Shilingi ikiporomoka kulinganisha na Dola ya Marekani na hivyo kusababisha bidhaa kupanda bei, wabunge wamekataa kulipwa kiasi hicho cha fedha mwaka huu na badala yake wanataka walipwe kulingana na bei ya sokoni ya magari aina hiyo.

Kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi imezipata, wabunge wanataka walipwe Sh130 milioni ambazo wanasema ni bei ya magari hayo kwa sasa baada ya kupanda bei.

Wakizungumza na Mwananchi kwa sharti la kutotajwa majina, baadhi ya wabunge walisema mara baada ya kujisajili bungeni kwa ajili ya uzinduzi wa Bunge la Kumi na Moja, katibu wa chombo hicho, Dk Thomas Kashililah alifanya kikao na wabunge wote ili kuwapa taratibu lakini pia kuwafahamisha stahili wanazopaswa kupata kama wabunge.

“Katibu alitujulisha kuwa tunapaswa kulipwa kiasi cha Sh300,000 kwa siku za posho, lakini pia tutapewa Sh90 milioni kwa ajili ya mkopo wa gari ambao nusu hutolewa na ofisi ya Bunge na kiasi kilichobaki tunapaswa kulipa wenyewe,” alisema mmoja wa wabunge hao.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, suala hilo liliibua mjadala na kusababisha wabunge kuhoji iweje kiwango hicho kitumike katika Bunge la Kumi na Moja, miaka mitano baada ya wabunge wa Bunge la 10 kupewa kiasi hicho.

“Unajua magari tunayotakiwa kununua ni Toyota Land Cruiser Hardtop, na ukweli sasa thamani ya magari hayo imepanda sana huwezi kuifananisha na mwaka 2010 wakati wa Bunge la 10,” alisema mbunge mmoja.

Wabunge hao walitaka walipwe kiasi cha Sh130 milioni kwa madai kuwa ndiyo bei ya sokoni ya magari aina hiyo.

Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Anatropia Theonest alikanusha habari hizo akisema hawajakataa fedha hizo, lakini walisema thamani ya Dola imepanda hivyo kusababisha thamani ya magari hayo kupanda pia.

“Hakuna asiyejua kwamba thamani ya Dola imepanda na kwa kawaida kila Bunge kunakuwa na ongezeko la Sh30 milioni. Mfano Bunge la Tisa walipewa Sh60milioni la 10 wakapewa Sh90milioni, hivyo ilipaswa sasa iwe Sh 120mililioni ili kuendana na soko,” alisema mbunge huyo.

Alisema baada ya mazunguzo hayo ofisi ya Bunge iliahidi kulifanyia utafiti suala hilo na kwamba ingewajibu.

Lakini, Mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu alisema wabunge wanapaswa kufahamu wapo kwa ajili ya wananchi na si kujilimbikizia mali.

“Kwa mfano mimi siwezi kuchukua fedha za posho kwa ajili ya kikao. Nimepanga kumuandikia barua Spika juu ya uamuzi wangu. Mshahara wangu unanitosha kabisa,” alisema Kingu ambaye awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga kabla ya kutolewa katika nafasi hiyo na kugeukia ubunge.

Akizungumzia sakata hilo, katibu wa Bunge alisema masharti na vigezo vilivyotumika mwaka 2010, ndivyo vinavyoendelea kutumika katika Bunge hili, na hivyo hakuna kilichobadilika.

Dk Kashililah alisema fedha za magari hayo hutolewa na Wizara ya Fedha kama mkopo na wabunge wataulipia huku kiasi kingine wakipewa kama ruzuku ya kununulia magari.

Hata hivyo hakutaka kuzungumzia kiwango halisi cha fedha zinazotolewa kwa wabunge hao.

Awali naibu katibu wa Bunge, John Joel alisema jukumu la ununuzi wa magari ya wabunge, lipo chini ya Serikali na siyo ofisi yake hivyo ni bora wangeulizwa wenye jukumu hilo.

Tunachofamu sisi mbunge anatakiwa apewe vitendea kazi likiwemo gari, lakini wanaohusika na hilo ni Serikali,” alisema.

Sisi huwa tunawahudumia jimbo allowance (posho) kwa ajili ya kuhudumia ofisi ya mbunge na kununua mafuta ya gari,” alisema Joel bila kutaja kiwango cha posho hiyo.

Alisema ofisi ya Bunge hushauriana na Serikali namna ya kutoa huduma kwa wabunge na kwamba kwa jinsi anavyofahamu, mpaka jana watunga sheria hao walikuwa hawajapewa fedha yoyote ya kununua magari kwa awamu hii, hivyo wanasubiri utaratibu.

Wakati Joel akisema Serikali ndiyo inahusika, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliurudisha mpira kwenye ofisi hiyo ya Bunge, akisema uongozi wa chombo hicho ndio uulizwe.

Katika kukusanya fedha za kuwezesha kutekeleza mipango ya Serikali na ahadi alizotoa wakati wa kampeni, Rais John Maguguli alitangaza hatua mbalimbali za kudhibiti matumizi, na akawaeleza wabunge mwishoni mwa wiki kuwa hataweza kufanikiwa iwapo hatapata ushirikiano wao.

Katika kuonyesha kuwa anatoa kauli thabiti, Dk Magufuli aliagiza fedha ambazo zilichangwa na taasisi mbalimbali za fedha kwa ajili ya hafla za kuwapongeza wabunge, zielekezwe kwenye ununuzi wa vifaa tiba kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Tayari Rais ameshafuta safari za nje isipokuwa kwa kibali cha Ikulu baada ya mtu anayetaka kusafiri kutimiza masharti kadhaa, likiwamo linalomtaka aeleze faida ya safari yake na kama iwapo hatasafiri, nchi itaathirika vipi.

Imeandikwa na Tausi Mbowe, Nuzulack Dausen na Florence Majani   

Kilichomuua Mbunge Filikunjombe Sasa Hadharani

$
0
0
Uchunguzi wa awali kuhusu ajali ya chopa iliyogharimu maisha ya aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wenzake watatu, unaonyesha ilitokana na hitilafu ya injini, Mwananchi imebaini.

Katika ajali hiyo iliyotokea Oktoba 16 kwenye pori la Selous, mbali ya Filikunjombe, rubani wa chopa hiyo, Kapteni William Silaa na wengine wawili waliokuwamo ndani ya chombo hicho kilichokuwa na namba za usajili 5Y-DKK na namba za utengenezwaji 7027 Eucereuil, pia walifariki dunia.

Filikunjombe alikodi chopa hiyo kutoka kampuni ya ndege ya Sun Drew inayomilikiwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka na ilikuwa inafanyiwa ukarabati na kampuni ya Laid Loris.

Baada ya ajali hiyo Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa ushirikiano na Wizara ya Uchukuzi waliita timu ya wachunguzi wa ndege kutoka Ufaransa ambayo ilitua nchini Oktoba 20. Timu hiyo ya watu wanne ilijumuisha mtu mmoja kutoka kampuni ya Airbus Industries ya Marseilles ambao ni watengenezaji wa chopa hiyo; mtu mmoja kutoka kampuni ya Turbo Meca, waliotengeneza injini; na watu wawili kutoka BEA, kitengo cha uchunguzi wa ndege kutoka Serikali ya Ufaransa.

Timu hiyo ilibaini hitilafu hiyo, ikibainisha kuwa baada ya injini kufeli, chopa hiyo ilianza kushuka hadi ikaanguka na kulipuka. Sababu za kulipuka kwake zimetajwa na wachunguzi hao kuwa ni madumu matano ya mafuta ya ujazo wa lita 20 yaliyokuwa ndani ya chopa hiyo.

Mchunguzi Mkuu wa Ajali za Ndege wa Wizara ya Uchukuzi, Omar Mhina aliiambia Mwananchi kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa injini.

“Katika uchunguzi wa awali, tulichukua injini na kugundua kuwa ilipata hitilafu. Hiyo ndiyo lugha ya kwanza tunayoweza kusema wakati tukisubiri uchunguzi mwingine,” alisema Mhina katika mahojiano na Mwananchi.

Mhina alisema wameshaichukua injini kutoka pori hilo la Selous na kwamba wanatarajia kuipeleka kwa watengenezaji wake kwa ajili ya kufunguliwa na kujua kiini cha kufeli kwa injini hiyo.

Alisema waliwasiliana na wamiliki wa chopa hiyo nchini Kenya, lakini hawajapata ushirikiano wa kuridhisha mpaka sasa. Lakini Mwananchi ilizungumza na opereta mkuu wa chopa hiyo wa Kenya, na rubani wa kampuni ya Sun Drew, Kapteni Charles Wachira ambaye alisema TCAA hawajawasiliana na Mamlaka ya Anga ya Kenya (KCAA) kwa ajili ya uchunguzi wa ajali hiyo.

Mimi ni kapteni wa ndege lakini siwezi kufanya lolote kama sijapata baraka kutoka TCAA na KCAA. Wao ndio walitakiwa wawasiliane kwanza kabla ya sisi Sun Drew kuchukua hatua zozote, ni suala baina ya serikali na serikali,” alisema Wachira.

Kapteni huyo amesema akipata ruhusa kutoka KCAA atakuja nchini kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha ajali ya chopa hiyo.

Kauli ya Musyoka

Lakini Kalonzo alisema kampuni yake imeshampa baraka zote, Kapteni Wachira ili kushirikiana na Tanzania kubaini chanzo cha ajali hiyo na kwamba kilichochelewesha ujio huo ni kusubiri kumalizika kwa shughuli za uchaguzi zilizokuwa zikifanyika Tanzania.

Kalonzo alisema walituma mwakilishi ambaye ni mjumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Peter Mathuki kupeleka salamu za rambirambi na kuhudhuria msiba wa Kapteni Silaa.

Ni lazima tushiriki katika hili kwa sababu ni pigo kubwa kwetu na kwa serikali yenu. Tayari Kapteni Wachira amekuja huko ili kushirikiana na Mamlaka ya Anga ya Tanzania,” alisema Kalonzo.

Mafuta yalilipua

Chanzo kingine cha ajali hiyo kilichoelezwa na timu hiyo ni madumu matano ya mafuta ya ndege yaliyokuwa yamepakiwa ndani.

Walikuwa wamebeba hayo madumu yenye mafuta ya akiba kwa kuwa walikuwa wametokea Ludewa ambako hakuna mafuta; unajua chopa hazikai na mafuta kwa muda mrefu ndiyo maana walibeba mafuta ya akiba,” alisema mtoaji habari wetu.

Kadhalika chanzo hicho kimesema viti vya ndege vilionekana kuanguka na kuvunjika na watu waliokuwamo walivunjika uti wa mgongo na miguu. Hata kama wasingeungua, wangepoteza maisha kutokana na madhara ya kuanguka kwake.

Ripoti ya BEA

Ripoti ya awali ya Kitengo cha uchunguzi wa ajali za ndege cha Serikali ya Ufaransa (BEA) iliyochapishwa kwenye tovuti yake imeeleza kuwa chopa hiyo ilionekana ikianguka kutoka angani, ikiwa tayari haina nguvu na ikifuka moshi. Kadhalika chopa hiyo ilionekana kwa muda mrefu ikiruka umbali wa chini na baada ya kuanguka, ililipuka.

Turbomeca

Lakini mkuu wa kitengo cha wanafizikia wa kampuni ya Turbomeca iliyotengeneza injini ya ndege hiyo, Delpgine Robelin alikataa kutoa maelezo akisema kuwa ni ya siri. “Hii ni siri kubwa. Hakuna taarifa zozote zinazoweza kutolewa,” inasema barua pepe ya Robelin akijibu barua pepe ya Mwananchi iliyoomba kupata ripoti ya awali ya uchunguzi wa ajali hiyo.

Mawasiliano angani

Uchunguzi umebaini pia Kapteni Silaa hakuwasiliana na kitengo cha usalama wa anga na mawasiliano ya ndege cha TCAA

Kuhusu tatizo la chopa. Mhina amesema Kapteni Silaa aliwasiliana na kitengo hicho wakati ndege ipo ardhini, ikipaa na ilipofika juu, lakini baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano yoyote.

Kabla hajaruhusiwa kwenda eneo jingine la anga (area control route) ndipo alipokata mawasiliano na hakuwasiliana hata na ndege nyingine kueleza kama ana tatizo,” alisema.

“Kwa kawaida chopa zinatakiwa kuwasiliana zikiwa angani, lakini hakuna chopa yoyote iliyotoa taarifa kama waliwasiliana na Kapteni Silaa,” alisema Mhina na kuongeza: “Iwapo chopa ina matatizo ya injini, kuna namna ambayo marubaini wanaweza kudhibiti ili kusitokee madhara, lakini haijulikani kwa nini Kapteni Silaa alishindwa kudhibiti hali hiyo.”

Shahidi

Mhina alisema kwamba mmoja wa mashuhuda aliiambia timu ya wachunguzi kwamba alianza kuona chopa hiyo ikifuka moshi wakati iko hewani. “Lakini haikuwa ikiungua, hapana, ilifuka moshi hadi ilipoanguka ndipo ikawaka.”    

Watuhumiwa wa Madawa ya Kulevya Bongo Waingiwa Kiwewe

$
0
0
Hofu imetanda kwa watuhumiwa wa kesi za matumizi ya madawa ya kulevya waliopo katika magereza mbalimbali nchini, kufuatia hukumu kali iliyotolewa hivi karibuni katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Mnaijeria Chukwudi Okechukwu na wenzake watatu Paul Ikechukwa Obi, Shoaib Muhammad Ayaz na Hycenth Stani.

Wanne hao walihukumiwa na Jaji Amir Rajabu Mruma wa Mahakama Kuu kwenda jela kwa miaka 30 na kulipa faini ya bilioni tisa ikiwa ni mara tatu ya thamani ya kilo 81 ya dawa za kulevya aina ya Cocaine walizokamatwa nazo zilizokuwa na thamani ya shilingi bilioni tatu za Kitanzania.

Jaji Mruma alitoa hukumu hiyo kwa kuzingatia Sheria ya dawa za kulevya namba tisa ya mwaka 1995 ambayo inasema kuwa mtu akikamatwa kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya atafungwa kifungo kisichopungua miaka 20 na kutakiwa kulipa faini mara tatu ya thamani ya dawa alizokamatwa nazo.

Inadaiwa kuwa watuhumiwa wengi wa kesi za dawa za kulevya, hutumia fedha nyingi kukwepa hukumu kwa kuwahonga majaji na mahakimu wanaokuwa wakizisikiliza, hivyo kitendo cha Okechukwu na wenzake kuhukumiwa kwa miaka mingi kimeibua hofu kubwa kuwa inawezekana kuanzia sasa hukumu zikawa ni kali sana.

Hofu inazidi wakiangalia mwenendo wa hukumu za madawa ya kulevya za hivi karibuni ambapo baadhi ya waliohukumiwa ni Bakari Kileo Bakari alihukumiwa miaka 25 jela na faini ya shilingi bilioni saba na mia mbili, Kadiria Said Kimaro, miaka 20 na faini ya milioni 144 wakati mtuhumiwa Fred William Chonde akihukumiwa miaka 20 na faini ya shilingi bilioni 15 na milioni 600. Wote hawa walikutwa na hatia za kukamatwa na madawa ya kulevya.

Wakizungumzia hukumu hiyo baadhi ya wananchi waliipongeza ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP) wa Serikali kwa kuhakikisha kesi za madawa ya kulevya zinashughulikiwa kwa kasi na kuitaka iboreshe zaidi utendaji wake.

Tatizo hili la madawa ya kulevya limetuathiri kwa muda mrefu, kwa hiyo zinapotolewa hukumu kali kama hizi zinasaidia kuwapunguza kasi wafanyabiashara wa dawa hizo,? alisema Juma Khamis, mkazi wa Kariakoo Dar es Salaam.

Naye, Mwanaidi Hassan mwanafunzi katika Chuo Cha Mwalimu Nyerere, alitaka jitihada za udhibiti ziongezwe ili kuwaepusha vijana wasiathiriwe zaidi na madawa ya kulevya.

Tunahitaji hatua kali zaidi. mahakimu watoe hukumu kwa kuzingatia Sheria na kusiwepo mianya ya rushwa kwasababu tatizo hili litatumalizia nguvu kazi.?

Wanaume Siku Hizi wana Vitambi na Kitandani Hawafanyi Kitu

$
0
0

As usual, hivi mwanaume kinachokufanya uwe na mtumbo huooo kama hauendi chooni maana yake nini? angalau wanawake wana cha kusingizia(uzazi) japo sio sana.

Yaani siku hizi sio wembamba na vibonge wote wana vitambi, yaani hampendezi wala kuvutia kutazamwa, mwanaume unakuwaje na mtumbo mkubwa hivyo? Kiafya ni hatari, lakini pia kwa shughuli ya 6 kwa 6 ndio kabisaaa, goli moja mtu chaliii, thanx God mume wangu hana na nahakikisha hakiji,mazoezi kwa sana na kula healthy na kunywa maji mengi, bahati nzuri hata yeye hakipendi so am happy.

Unakuta kijana mdogo ana mtumbo huo hata kumuangalia inatia kichefuchefu, hebu fanyeni mazoezi bwana na muache kula kula kama mchwa na mibia kama mnamkomoa mtengenezaji wanawake wanalia kwenye ndoa zao huduma za kitandani hovyo kabisa kwasababu ya hiyo mitumbo yenu,mkichapiwa mtalalamika!?

Sio siri hiyo mitumbo yenu ni tatizo hebu chukueni hatua, migonjwa inawanyemelea mwisho mfe mapema mtuache tukihangaika na watoto peke yetu kwa uzembe wenu kitambi sio dili, piga vita minyama uzembe.

Am out.

Dr. Magufuli na Ununuzi wa Vitanda Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili, Je Procedures zote za Manunuzi ya Umma zilifuatwa ?

$
0
0

Hebu tafakari kuhusu vitanda vya Muhimbili Magufuli alitoa kauli hiyo ijumaa jioni na jumamosi mchana vitanda vikawa tayari vimewasili Muhimbili.

Je pesa jizo alikabidhiwa mkurugenzi saa ngapi na kuanza process ya kuzitoa bank saa ngapi na afisa manunuzi wa Muhimbili alitafuta QUOTATIONS tatu saa ngapi na bodi yao ya manunuzi walikaa kikao saa ngapi ili kupitisha quotation moja ambayo itatumika ktk manunuzi hayo?

Je huyo supplier wa hizo vitanda alikuwa na stock kubwa kiasi hicho ambapo Muhimbili walipofika wakapewa chapuchapu?na ninavyojua manunuzi yanayozidi 10M huwezi kufanya kwa CHEQUE ni lazima ufanye kwa TISS sasa na mizunguko yote hiyo na juzi ilikuwa ni siku yamapumziko je procedures zote za manunuzi ya UMMA zilifuatwa ?



Source: By Makombeni10/Jamii Forums
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live


Latest Images