Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

VIDEO:Agizo la Rais Alilotoa Jana Laanza Kushughulikiwa ,Barabara ya Morocco - Mwenge yaanza Kupanuliwa

0
0
Aisee Nimeamini Kumbe Haya Mambo yanawezekana..Jana tu agizo limetolewa leo Watu wameshaingia mzigoni....

Nipo hapa Morocco, nashuhudia namna agizo la Rais Magufuli linavyotekelezwa. Kuna greda za kutosha, ujenzi wa barabara ya Morocco-Mwenge umeshaanza!



Suluhisho la Foleni katika Jiji la Dar....Kuna Umuhimu Gani wa Wizara Zoote Kuwa Jijini Dar es Salaam?

0
0
Ili kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam, nashauri Serikali itawanye makao makuu za Wizara katika mikoa mbalimbali nchi nzima! Mkoa wa Dar es Salaam kipekee kabisa umekaliwa na wizara zote, hivyo wafanyakazi na taasisi zake wapo Dar es Salaam! Mabenki, na makampuni mengine mengi yanaona ni rahisi na faida yakifunguliwa Dar es Salaam kulikoni yangefunguliwa mikoani ambapo purchasing power ya wananchi wa huko ipo chini!

Endapo Wizara zitatawanywa nchi nzima, at least wizara tatu kila mwaka itaondoa watumishi wengi Dar es Slaam na familia zao, hence kupunguza idadi ya magari barabarani! Pia itafanya mabenki na taasisi zingine kufungua matawi kwenye hiyo mikoa kama siyo kuhamia kabisa! Zoezi hili likifanikiwa, Dar es Salaam kutabakiwa na wizara na taasisi za umma chache zenye umuhimu wa kubakia Dar!

Dar es Salaam ina foleni kwakuwa, idadi ya wakaazi wake inazidi kuongezeka siku hata siku lakini miundo mbinu ni ileile, haiongezeki! Umiliki wa magari limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa karibu kila mtu anayejishughulisha anamiliki gari kama siyo magari! Juu ya hilo ni kuwa, karibu wote tukiamka asbuhi tunaelekea uelekeo mmoja wa mjini, na woote tunatawanyika kutoka mjini ikifika jioni! Ijapo kumekuwa na jitihada nyingi kutengeneza barabara za michepuko, lakini taratibu kadri muda unavyoenda na zenyewe zinazidiwa! Kutoka Mbezi hadi mjini au mjini to mbezi ya Kimara inaweza ikuchukue hadi masaa matatu?. Muda wa Abood kutoka Dar hadi Morogoro!

Mtu wa mikoa mingine, akitaka jambo lake wizarani itamlazimu aende Dar, lakini mkaazi wa Dar ni daladala tu ya kumfikisha mjini, na ana uwezo wa kutembea wizara karibu zote kwa mguu na akazimaliza! Kwa hali hii, wakaazi wa mikoa mingine hawatendewi haki licha mzunguko wao mdogo wa hela wa mikoani itabidi achukue basi, treni au ndege na akodishe hoteli akiwa Dar hadi amalize mambo yake. Kuna wakaazi wengi wa Dar hawajawahi kufika Kigoma, Rukwa, Kagera, Ruvuma nk kwakuwa hamna jambo linalomfanya aende mikoa hiyo? Endapo mikoa hiyo ingepelekewa Wizara zikahamia huko, basi kama hajaenda kusalimia basi kuna jambo atalifuata katika wizara ilio katika hiyo mikoa!

Ushauri ni kuwa, katika kuhamisha huku kwa Wizara, zilenge ile mikoa yenye mwamko mdogo wa kimaendeleo ya kijamii na uchumi! Wizara ya Elimu, ihamie Kigoma , Mambo ya Ndani ihamie Dodoma, Maji Nishati ihamie Singida nk nk? Kwa hali hiii hata wakazi wa huko wataneemeka na mzunguko wa fedha kutoka kwa wahamiaji wapya!

Kuna umuhimu gani wa wizara zoote kuwa jijini Dar es Salaam?
Ofisi za Balozi mbalimbali, kuna ulazima wa wao wote kukaa hapa Dar?

January Makamba Afunguka Akiri Rais Magufuli Ameipa Pumzi Mpya CCM

0
0
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, January Makamba amesema kasi ya utendaji inayooneshwa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, imekipa uhai mpya chama chao na kwamba wanaCCM sasa wanatakiwa kutembea kifua mbele.

Akizungumza jana na mwandishi wetu Dar es Salaam, January alisema wakati wa kampeni CCM iliahidi itawaletea Watanzania mabadiliko na jambo hilo ndilo hasa linalofanywa na Magufuli na Majaliwa.

WanaCCM sasa wanatakiwa kutembea kifua mbele na kuwapongeza Magufuli na Majaliwa kwa kutoa matamko ya kuwaunga mkono kwa hatua wanazochukua. Wakati wa kampeni tuliahidi mabadiliko ya kweli. Na sasa tunaanza kuyaona,” alisema January na kuongeza:

“Tusikae kimya. Hii ni vita kali na naamini Watanzania wote wanamuunga mkono, lakini kwa kuwa anatekeleza ahadi ya CCM sisi tunapaswa kuwa mstari wa mbele kwa kumuunga mkono kwa maneno na matendo.

Tulipigana kufa na kupona ili tushinde na baadhi yetu tunaendelea kupokea vitisho na matusi kwa sababu ya kampeni kwa vile kwa wapinzani ushindani haujamalizika baada ya kumalizika kwa kampeni."
 
Mbunge huyo wa Bumbuli mkoani Tanga na Naibu Waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema kama mwana CCM na MNEC anajisikia fahari kwa vitendo vinavyofanywa na Magufuli kwa vile vimekipa chama pumzi na uhai mpya, akikumbusha maneno yaliyokuwa yakitumika na wapinzani kwamba chama hicho sasa kimeishiwa pumzi.

Lazima CCM ihakikishe Magufuli na Majaliwa wanafanikiwa katika uongozi wao. Hapo ndiyo nguvu iliyotumika katika kampeni itakuwa na maana. Kazi anayofanya Rais inakiletea chama pumzi na uhai mpya.

“Kwa mwendo huu, hakutakuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kama ilivyokuwa mwaka huu. Inawezekana wapo wanaCCM watakaoguswa na utendaji huu wa Rais, lakini hiyo ni gharama ndogo sana ya kulipa kwenye kuitafuta Tanzania ambayo kila mwananchi anaililia,” alisema.

CHADEMA Fanyeni Mikakati kuimarisha Chama Acheni Siasa za Kutumia matatizo ya Watanzania

0
0
Naamini viongozi wa CHADEMA wanafika hapa JF, lkn pia najua wanachama ana wafuasi wapo wengi hapa JF. Kwa muda mrefu CDM imetusaidia watanzania kutufumbua macho wakati ufisadi ukitamalaki. Yaliyopita si ndwele tigange yajayo.

Tangu uchaguzi umalizike CDM imekuwa ni chama cha matukio, kwa kizungu reactive to the incident. Tumeona CDM ilivyotumia msiba wa MAWAZO (MUNGU AMREHEMU) kwa sababu kama amekufa kwa sababu ya tofauti za kisiasa watanzania tunaelekea kubaya. Lakini CHADEMA kilitumia msiba huu kujipatia umaarufu km kwamba CHAMA CHA MAPINDUZI ndicho kiliwatuma waharifu kumuua kamanda MAWAZO, sitaki kuamini km CCM kama chama wana uwezo wa kufanya haya kwaani uchaguzi umeisha na walishinda kwa 95% kanda ya ziwa.
Kabla ya hili la mawazo CHADEMA walikuwa wanatafuta sympathy ya wananchi kwa kutumia kesi mbalimbali mfano ni kesi ya SHEKH PONDA aliyeshinda kesi hapo jana. Kuna wakati Fulani alikuwa akitetewa na wakiri maarufu wa CHADEMA pale Morogoro. Sijui kwa nini CDM waliingiliaje kesi hii kidogo wamuharibie mshitakiwa kwaani serikali ingeona kama vile alikuwa anatumiwa na CHAMA.

Jana baada ya kupata ushindi dhidi ya serikali niliona viongozi wote wa CDM wakiongozwa na aliyekuwa mgombea ubunge ndugu MARCUS ALBAN waliongoza waaumini kutoka eno la mahakama mpaka eneo la msikiti wa MUNGU MMOJA.
Wakati wa kampeni tuliskia aliyekuwa mgombea Urais kupitia CHADEMA Mheshimiwa Edward Lowassa kuwa kama angechukua dora basi angewaachia huru watuhumiwa mbalimbali wakiwamo Shekh Farid na Babu seya. Kwa kifupi kama hawana makosa wanastahili kuachiwa kwa mujibu wa sheria lakini siyo kwa mujibu wa matakwa ya mtu.

USHAURI KWA CDM NA UPINZANI:
Fanyeni vitu endelevu na vinavyoenekana, yaani sustainable and tangible la sivyo mtasahaulika, kumbukeni watanzania ni wepesi sana wa kusahau, jumrisha na kasi ya serikali ya awamu ya tano ambayo imezichukua sera za upinzania kuzifanyia kazi hasa ile ya ufisadi iliyotupwa baada ya kumpkea LOWASSA kitendo kilichoitwa na kubadili gear angani.

ACHENI KUTUMIA MATATIZO KATIKA JAMII KUTAFUTA UMAARUFU WA KISIASA.

Magufuli Aitikisa Dunia Kwa Uchapakazi......Jina Lake Latawala Magazeti ya Marekani, Afrika Kusini na Australia

0
0
Kwa wiki ya pili sasa Rais Dkt Magufuli ameendelea kuwa gumzo barani Afrika na sasa hadi nchi za Ulaya zimedata naye.

Gazeti kubwa la Marekani, The Guardian limeandika habari isemayo:What would Tanzania’s cost-cutting president do? Twitter responds.

Pai  gazeti kubwa la  Australia,The Courier-Mail limeandika makala ndefu likimtaka Waziri mkuu wao,  Malcolm Turnbull ajifunze achapakazi toka kwa Rais wa Tanzania,Dr John Pombe Magufuli
Jina lake linatrend muda wote kwenye mtandao wa Twitter na kadri siku zinavyooenda habari za utendaji wake zinazidi kuenea.

Katika mtandao huo wa Twitter, imeanzishwa Verb ya jina la Magufuli iitwayo  magufulify ambayo imepewa maana ifuatayo;

Magufulify – 
==>To render or declare action faster and cheaper;
==> To deprive (public officials) of their capacity to enjoy life on taxpayers’ money; 
==>To terrorize lazy and corrupt individuals in the society.”
Aidha, Mtandao  mkubwa Afrika Kusini wa The South African, umeandika habari iliyonukuu mambo 10 mazuri  yaliyofanywa na Rais Magufuli ndani ya muda mfupi huku mtandao huu ukimtaka Rais wa nchi hiyo ajifunze toka kwa Magufuli.
 

Mambo  10  yaliyoanishwa na mtandao huo ni kama ifuatavyo;

==>Here are some of the things John Magufuli has done already in less than a month:
  1. Soon after his election, Magufuli declared there would be no celebration of Independence Day on 9 December because it would be “shameful” to spend huge sums of money on the celebrations when people were dying of cholera. Instead, the day has been set as a national day of cleanliness, and the money will go toward street-cleaning services. He has said everybody should pick up their tools and clean their backyards.
  2. After his first official visit to the Muhimbili Hospital, and seeing the horrible state it was in, he ordered over 200 million shillings marked for “parliament parties” be used to pay for beds for people lying on the floor and sharing beds. A few days later 300 beds were delivered. He dismissed the governing board and got a new team in place, and within days the broken MRI was fixed. He also pared down his inauguration party from $100,000 to $7,000 and sent the extra money to the hospital.
  3. Three days into his term, Magufuli announced a ban on all foreign travel by government officials. They have been instructed to instead make regular visits to rural areas to learn and help solve problems facing everyday Tanzanians. All tasks that required officials to travel abroad would instead be done by high commissioners and ambassadors who are already in place.
  4. He has restricted all first- and business-class travel to government officials, except the president, vice-president and prime minister.
  5. There will be no more workshops and seminars in expensive hotels when there are so many ministry board rooms available.
  6. He suspended the Tanzania Revenue Authority’s chief and other officials pending investigations after a visit by Prime Minister Kassim Majaliwa to the port of Dar es Salaam found 350 containers listed in its books were missing.
  7. When he had to travel 600km to Dodoma, from Dar, to officially open parliament last week, he didn’t order a private jet – instead, he chose to drive.
  8. At the National Assembly in Dodoma last week he clearly sent out the message that it will not be business as usual under his leadership.
  9. He promised to cut public spending, fight corruption and enhance accountability in public service. He said it is time for Tanzanians to walk the talk.
  10. Magufuli reportedly told parliamentary leaders that the people of Tanzania want him to solve their problems and not make speeches.
Hakuna anayeweza kubisha kuwa Magufuli ameiweka Tanzania kwenye chart.

TRA Yatoa Tamko Kuhusu Makontena Tisa Yaliyokamatwa Mbezi...Mmiliki Wake Atakiwa Kujitokeza La Sivyo.....

0
0
Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato nchini TRA Richard Kayombo ametolea ufafanuzi juu ya kukamatwa kwa makontena 9 katika eneo la Mbezi Tank Bovu jijini Dar es Salaam ambapo mpaka sasa hivi Makontena hayo pamoja na madereva waliokuwa wanayasafirisha yako chini ya ulinzi mpaka wahusika watakapojitokeza.

Kayombo amesema kuwa makontena hayo yamenaswa usiku wa manane kwa msaada wa wasamaria wema waliotoa taarifa za kupakiwa kwa makontena hayo katika bandari kavu ya   PMM.

Bwana Kayombo amesema TRA imetoa masaa  24 kwa mmiliki wa makontena hayo kujitokeza, vinginevyo watayafungua na kuyataifisha kama sheria inavyoelekeza

Mabasi ya UDA Mikononi Mwa Magufuli na TRA Kwa Kutokulipa Kodi

0
0
Agizo  la Rais Dk. John Magufuli kuwabana wafanyabiashara wanaokwepa kodi nchini, limeanza kuwa mwiba baada ya mabasi ya Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA), kukamatwa kutokana na kukwepa kodi.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, jana alisema mabasi tisa ya UDA yalikamatwa kutokana na kukiuka sheria za mlipakodi.

Mbali na UDA, Kayombo alisema TRA pia iliyakamata mabasi ya kampuni nyingine kutokana na kushindwa kulipa kodi ambapo walitumia kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart.

Kayombo alisema operesheni ya TRA kuwakamata wafanyabiashara wanaokwepa kodi ni endelevu nchi nzima na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa kwa wanaokaidi kutekeleza sheria.

Hata hivyo, Kayombo hakutaka kuzungumzia kwa undani kuhusu kiwango cha kodi ambacho hakikulipwa na UDA, akidai kuwa hiyo ni siri ya mlipakodi na mamlaka yenyewe.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UDA, Robert Kisena, alithibitisha kukamatwa kwa mabasi yake ambayo alisema uzembe huo ulifanywa na idara yake ya uhasibu.

Kisena alisema muda wa kulipia kodi ulikuwa umefika, lakini idara yake ya uhasibu haikuweza kulipa viwango vinavyotakiwa.

Ni kweli kuna magari yetu matatu au manne yamekamatwa na tatizo kubwa ni kodi ya magari, ambayo tulijua mtu wetu wa uhasibu amelipa, lakini kumbe alikuwa hajalipa,” alisema Kisena huku akisisitiza kuwa taratibu za kuyakomboa magari hayo zimefanyika ambapo wamekwishalipia gharama zilizokuwa zinahitajika.

AL SHABAAB Swear to Assassinate UHURU in Cold Blood & Reveal Plans (VIDEO)

0
0

President Uhuru Kenyatta is now a man under siege and living in fear despite tight security around him and the armored vehicles that he rolls in.

Al Shabaab terrorists have vowed to assassinate him very soon for refusing to pull Kenya Defence Forces (KDF) out of Somalia as well as unfairly exterminating Muslim leaders in the name of fighting terrorism.

In an expose dubbed Kenya’s Enemy Within by John Allan Namu and aired on Aljazeera, leaders of Al Shabaab’s slipper cell based in Kenya revealed to Namu how they organize terror attacks in the country and even help Al Shabaab fighters from Somalia to execute terror in Kenya.

Those who spoke to Namu confirmed that most Al Shabaab terrorists who attack the country were right here in Kenya just waiting for orders from their bosses in Somalia to carry out attacks and that not even the so called security wall with Somalia will deter them from butchering Kenyans.

 The Al Shabaab leaders even revealed their next target saying they were just waiting for an order from above to assassinate President Uhuru Kenyatta among other high profile targets.

Asked how they intend to assassinate Uhuru considering his armored cars and heavy security around him, the Al Shabaab terrorists said they already have a plan for him with snipers stationed in almost every corner that he visits to take him down any time.

Here is the documentary by Namu....


Nape Nnauye Awakata Watu Mdomo Wanaosema CCM Haiungi Mkono Juhudi Anazofanya Rais Magufuli...Asema Haya

0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.

Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.

Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure katika masuala yasiyo ya lazima na wakati huohuo kuanza kuwabana wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.

"Yapo mengi tuliyoanisha katika ilani yetu ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na haya mnayoyaona yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii tumeitunga hata kabla ya kumteua kugombea Urais, Sasa anachofaya ni kuitekeleza ilani hii, isipokuwa mbinu anazotumia ni ubunifu wake na hili hatuna tatizo nalo kama Chama maana kiongozi wa aina hii ndiye tuliyemtaka", alisema Nape.

"Najua wapo wanaojaribu kutengeneza magingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk. Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli hayana uhusiano na maelekezo ya CCM", aliongeza Nape.

Alisema, baada ya kutengeneza ilani yake, CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya tano ni ya kutafsiri uchumi katika nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo miundomboni, maji, afya na elimu.

"Ni kutokana na lengo hili, ndiyo sababu tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa tunamkabidhi mwana CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka mashaka, Ndiyo huyo Dk. Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi mmeanza kuuona utekelezaji wake wa ilani", alisema Nape.

Akizungumzia kuhusu Rais Dk. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais, kilichobaki sasa ni kwa Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini katika kufanya hivyo hakuna mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na hashurutishwi na Chama wala sheria.

Nape alisema, Dk. Magufuli hachelewi kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua, isipokuwa, anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na mda huo ukijiri wa kuamua kufanya hivyo atafanya.

"Tatizo hapa ni kwamba mnayo kiu kubwa ya kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu imepita kiasi, ndiyo maana mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais Magufuli ataikata kiu yetu, wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha", alisema Nape.

Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza ilani ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia Watanzania watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo njiani kuwadia.

"Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa lazima tufanye mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa uhai na maendeleo ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya tunayafanya kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao", alisema Nape.

Kuhusu Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti Rais Dk. Magufuli, Nape alisema, hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa ikifanyika katika awamu zote za Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwaka 2017 au kabla ya hapo akiona inafaa.

Zanzibar
Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.

Alisema, msingi wa mgogoro uliojitokeza Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe kwenye mazungumzo kuutatua, na baada ya kuutatua yaendelee kufanyika mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la kudumu kwa kuwa imekuwa ni kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila baada ya uchaguzi mkuu jambo linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi kuliko inavyodhaniwa.

Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na Serikali kulijenga taifa.

"Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea, sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja", alisema Nape.

Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia kuishauri Serikali na CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na hata pale vyombo hivyo vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda kinyume, visihofu kukosoa.

Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao amekuwa akivipa vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango wazi kwa waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.

Ziara hiyo ya Nape aliyoianza jana, kwenye vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea vyombo vingine vya habari vyenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam

Mrema Atoa Kauli Yake Kuhusu Utendaji na Kasi ya Magufuli...Adai Tanzania Sasa Inaandika Histori

0
0
MWENYEKITI wa Taifa wa chama cha siasa cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amesema hakufanya makosa na wala hajutii kumnadi Rais John Magufuli kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa sababu alitambua Watanzania wamelamba dume la maendeleo.

Akizungumza na mtandao huu jana mjini Moshi, Mrema alisema Watanzania wamepata mtu wa kuendeleza kazi aliyokuwa akiifanya kipindi yeye wakati akiwa Naibu Waziri Mkuu katika miaka ya 1990, ya kupambana na wahujumu uchumi, wala rushwa na wafanyakazi wazembe.

Mrema alisema Dk Magufuli ndiye mwenye uwezo pekee wa kuyaleta mabadiliko ya kweli yanayohitajika, japo wengi waliamini hayawezi kupatikana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndio maana alichukua jukumu la kumpigia kampeni.

Mrema aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo mwaka 2010 hadi mwaka 2015, alisema anamfahamu vizuri Dk Magufuli tangu akiwa Waziri wa Ujenzi, kutokana na uchapakazi wake, ambapo walisaidiana kujenga barabara za Vunjo, hali iliyosaidia jimbo hilo kuwa na mtandao mkubwa wa barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami.

“Watu walishangaa sana kwa nini nilimpigia kampeni Dk Magufuli, na kumwacha mgombea wangu…nilijua mtu pekee wa kuyaleta mabadiliko makubwa na kweli ni yeye… Kwanza nampongeza sana na nafurahi sana kwa taifa hili linahitaji kiongozi mchapakazi, mwadilifu kama yeye,” alisema Mrema.

Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu, akiwa jimboni Vunjo, Dk Magufuli alikutana na Mrema wakati huo naye akiomba kura za ubunge, na alimshika mkono na kumtambulisha akiwa katika moja ya mikutano yake, na Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alimpigia debe mgombea huyo wa urais wa CCM.

Mrema alifanya hivyo huku chama chake, TLP kikiwa kimemsimamisha MacMillian Lyimo kuwania urais wa Tanzania, hali iliyoibua mijadala wakati huo wa kampeni, huku mwanasiasa huyo machachari nchini akitetea msimamo wake huo wa kumnadi Dk Magufuli badala ya Lyimo.

Mrema alisema Uchaguzi Mkuu umeibua rais mwema, mwadilifu na mwenye uchungu na Watanzania wote. Aliwataka Watanzania kuacha ushabiki wa vyama vyao vya kisiasa na kuangalia mtu anayefanya kazi ya kulikomboa Taifa hili, kama Dk Magufuli kwa kumuunga mkono na kumuombea.

Alisema tangu Taifa lipate Uhuru, kwa sasa Tanzania imeandika historia ya kuwa na viongozi mahiri watatu wa kupambana na umaskini, ambapo aliwataja viongozi hao ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Sokoine (sasa hayati) na Dk Magufuli.

See What VERA SIDIKA Posted on Social Media As She Addressed Fans & Haters (PHOTO)

0
0

Curvaceous city socialite, Vera Sidika, has left thirsty men begging for more after releasing her hottest photo ever.

The well endowed socialite was dressed in a blue b00ty hugging dress that left her s3xy goodies exposed for all to see.

This is what Vera posted as she addressed fans and haters.

This goes out to all the Lovers, Haters, Believers and Non- Believers: The love I receive from you guys is overwhelming and I just can't begin to explain how much that means to me. 

My heart melts when I keep seeing some of y'all put me up on your display pictures post me on your pages,create fan pages; Btw, Big s/o to @verasidikaisbae I see you! (trust me,when I see a tag I always like or comment) all those little things matter to me. I don't take it for granted. 

There's been haters too but hey, what would I do without y'all. You guys keep me going and motivate me to try harder. All I wanna say is THANK YOU!!! You guys have touched my life in ways you never know. 

My riches do not lie in having material wealth but in having friends like y'all! Photography; @buoart Happy New month, Stay Blessed.



Kafulila Aanza Vizuri Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo Ya Ubunge Baada Ya Pingamizi Kutupiliwa Mbali Na Mahakama

0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila hakufuata taratibu katika ufunguzi wa kesi hiyo.

Katika utetezi wa mawakili wa Kafulila ambao  ni Daniel Lumenyera na Tundu Lissu waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote kwa kesi ya Msingi.

Jana Jaji anayesikiliza kesi hiyo Bi Leila  Mgonya alizingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu.

Aidha,Jana hiyo hiyo Mahakama iliendelea na hoja ya kutathmini gharama ya dhamana ambayo Mhe Kafulila atapaswa kuweka kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi iweze kuanza.

Uamuzi kuhusu kiasi gani Mhe Kafulila atalipa kama dhamana utatolewa  leo na Mahakama.

Mwanamikakati wa Lowassa Ahusishwa na Wizi Mkubwa Stanbic

0
0
 Bw. Bashir Awale Kulia Mwenye Tshirt ya Njano Akisalimiana na Lowassa
Siku chache baada ya uchaguzi serikali ya Tanzania ilimfukuza mtu aliyejulikana alikuwa mashauri wa Kimkakati wa Mgombea Urais kupitia Chadema, Bw. Bashir Awale (Mkenya ashikiliwa na Polisi nchini TZee kwa kumpigia debe Lowassa kipindi cha campaigns), kwa kuishi kimakosa nchini. Pia, ilijulikana kuwa kabla ya kuanza kujihusisha na siasa, hasa kuwa mshauri wa Ndugu Lowassa katika kuusaka urais alikuwa mmoja wa Maofisa Wandamizi wa Benki ya Stanbic.

Katika sakata linalohushisha benki ya Stanbic kufanya udanganyifu mkubwa wa kujipatia fedha na kushitakiwa na Idara ya Makosa ya Uingeleza huyu jamaa katokea. Na imeonyesha alifukuzwa katika wakati huu baada ya kufanya wizi huu kwa kushirikiana na ndugu wa karibu wa Lowassa na aliyekuwa Miss Tanzania 1996, Shose Sinare.

Kwa mjibu wa serikali, tayari uchunguzi umeanza kufanyika ili kubaini aliyefaidika na pesa hizo. Aidha, hukumu iliyofanyika jana imeamuru serikali ya Tanzania kulipya dola 6M na Stanbic kama sehemu ya hela iliyoibwa.


Nafasi za Ajira Tanzania Women's Bank PLC, Application Deadline 04 December, 2015

0
0
Tanzania Women's Bank PLC
Position Advertisement

Tanzania Women's Bank is seeking to recruit dynamic, honest, result oriented and committed to fill the following roles:

Bonyeza Hapa Kusoma Ajira zote zilizotangazwa na Bank hiyo leo =>WWW.AJIRAYAKO.COM


Au Bonyeza HAPA

Nafasi za Kazi Serekalini Utumishi wa Umma, Application Deadline 06 December, 2015

0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE
PUBLIC SERVICE MANAGEMENT

VACANCY ANNOUNCEMENT

Ingia Kwenye Hii Website ya Ajira AJIRAYAKO.COM Kusoma Hiyo Nafasi ya Ajira ya Serekali iliyotangazwa...

Au Bonyeza HAPA

Dk. Slaa Atoka Mafichoni 'Nadhani Sasa Mnanielewa Niliposhikilia Msimamo Wangu'

0
0
Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.

Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.

Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi sana,” Dk. Slaa ameliabia gazeti la Raia Mwema.

Amesema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua.

Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Disemba 2...Ikiwemo ya Bosi TRA Atajwa Ufisadi Mabilioni

Trust Pamoja na Vanessa Mdee Wazindua Rasmi Tamasha la “Divas Only” Mjini Dodoma...Mwanza na Mbeya Kufuatia

0
0



Vanesa Mdee akitumbuiza katika tamasha la kutoa elimu ya uzazi wa mpango lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha lililopewa jina la “Divas Only Concert” lilifanyika katika ukumbi wa Royal Village na kuratibiwa na Shirika lisilokua la kiserikali DKT International.


Msanii Vanessa Mdee (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la DKT International kabla ya kufungua rasmi Tamasha la Divas Only ambalo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Katikati) ni Meneja Masoko DKT International Sialouise Shayo.

Ma divas mbalimbali wa jijini Dodoma walijitokeza katika tamasha la kutoa elimu ya uzazi wa mpango lililopewa jina la “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika katika hotel ya Royal village jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo liliratibiwa na shirika lisilokua la kiserikali DKT international Trust.
Dodoma 01 Desemba 2015: TRUST, Mwishoni mwa wiki iliyopita TRUST walizindua mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya Divas Only ambayo yalimshirikisha mwanadada na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee. Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa na wanawake kwa ajili ya wanawake. Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye. Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio; Trust iko hapa kukusaidia wakati wa safari hii. Tulifurahia muda tuliopata kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa Dodoma. Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika matamasha yetu mengine Mbeya Desemba 04 pale Sunset Hall, Soweto na Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tafuta eneo lilipo Dodoma, Mbeya na Mwanza katika tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!

Tajiri Anayemiliki Makontena Yaliyopotea Bandarini Ajitokeza......Amtupia Lawama Wakala Wake

0
0
Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amejitokeza na kukiri kumiliki baadhi ya makontena yaliyokumbwa na kashfa hiyo lakini  amekana kosa lenye sura ya kukwepa kodi  akidai kuwa limefanywa na wakala wake.

“Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini. Tunalipa kodi kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali. Mimi nilimlipa kazi wakala wangu ambaye nimekuwa nikifanya naye kazi kwa miaka 10,” Bin Slum ameliambia gazeti la Raia Mwema.

Mara kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi lakini kwenye mzigo huu wa sasa  ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia ananiandalia faili,” alieleza.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wote wanaohusika na kashfa hiyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua na kodi iliyokwepwa ilipwe.

Tayari watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia sakata hilo.

Ajali Mbaya Yabasi Yatokea Gari la Mafuta Logongana na Basi la Abiria...Watu 12 Wafa Papo Hapo na Wengine Kujeruhiwa Vibaya

0
0
Abiria 12 wakiwemo wanaume saba na wanawake watano wamefariki baada ya basi walilopanda la kampuni ya Takibrii kugongana na lori la mafuta katika kijiji cha Kisonzo wilayani Iramba, Singida.Basi hilo lilikuwa linatokea Dar es Salaam kuelekea mji mdogo wa Katoro ulioko mkoani Geita.
 
Akithibitisha taarifa hizo, Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema ajali hiyo ambayo imesababisha watu 18 kujeruhiwa, imetokea usiku wa kuamkia leo
 
Akielezea mazingira ya ajali hiyo, Kamanda amesema kuwa dereva wa basi, Charles Kaeme alikuwa analipita lori la kampuni ya Cocacola kabla ya kuligonga lori la mafuta. Hata hivyo, dereva wa basi hilo alikimbia baada ya ajali kutokea na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.
 
Naye Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Iramba, Timoth Sumbe amethibitisha vifo hivyo na watu 18 bado wanaendelea kupatiwa matibabu.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images