Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI wa Serekali Wazidi Kubanwa..Mhe. Balozi Ombeni Sefue Aagiza Wavae Baji za Majina yao Wawapo Kazini Kubaini Wazembe

$
0
0
Mhe. Balozi Ombeni Sefue Akionyesha Mfano wa Baji yake yenye jina lake
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa  katika maeneo  ya  kazi.

Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine.

Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza  watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao.

Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na mashaka ajue mimi nimeshalivaa”.

Mtumishi wa umma anapomuhudumia mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya  kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina yenu”, alisisitiza Mhe. Balozi Sefue.

Mhe. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank. 

KIMENUKA Tena...Wafanya Kazi wa Kiwanda cha Urafiki Wagoma Tena..Wawafungia Uongozi wa Kiwanda Hicho Ndani, Mabomu Yarindima

$
0
0
Wafanyakazi Kiwanda cha Nguo Urafiki
Jeshi la Polisi  Dar es Salaam  leo limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki ambao walifanya mgomo na kuufungia uongozi wa kiwanda hicho  ndani kwa madai ya kutolipwa ongezeko la mishahara yao kwa muda mrefu.

Kutokana na Sekeseke hilo,Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda ameamuru kiwanda hicho kifungwe kwa muda ili kusaka suluhu


Wafanyakazi wa TRA Geti No. 5 Waswekwa Ndani Mchana Huu

$
0
0
Upelelezi ukiwa bado unaendelea kufuatia ufisadi wa kupitishwa kwa makontena takribani 350 bandarini bila kulipia ushuru. Leo jeshi la polisi limewakamata wafanyakazi wa TRA ambao ndio wanahusika na upitishaji wa makontena pale bandarini. Taarifa za awali zinasema idadi ya wafanyakazi hao walioswekwa ndani inakadiriwa kuwa ni 27.

Mwanamuziki Diamond Platnumz Ashtuka, Agoma Kutoa Wimbo Mpya Kwa Sasa, Sababu Hizi Hapa

$
0
0
Diamond Platnumz
MWANAMUZIKI wa Afro Pop, Diamond Platinum anatamani kuachia ngoma nyingine lakini amekiri kupata kikwazo kutokana na matokeo ya Wimbo wa Nana aliouachia mara ya mwisho.
Diamond au Chibu amefunguka kuwa kwenye ‘library’ yake ana nyimbo nyingi kali ambazo zipo tayari kuachiwa muda wowote lakini kutokana na Nana kuendelea kufanya vizuri mpaka sasa tangu alipoiachia anaona bora aendelee kusubiri, asifululize kuingiza kazi nyingi sokoni kwa wakati mmoja.

Unajua vitu vipya vipo, lakini nimecheki upepo naona kama bado kwanza kwa sasa maana Nana bado inafanya vizuri, nataka kuipa muda kwanza kabla sijaachia ngoma mpya japokuwa nia yangu kubwa ni kuachia wimbo kabla ya mwaka haujabadilika, kwa hiyo bado nacheki,” alisema Diamond.

Nana ambao amemshirikisha Flavour wa Nigeria, umewika vizuri Afrika na kufanikiwa kumpa baadhi ya tuzo ikiwemo ya Wimbo Bora wa Kucheza wa Mwaka (AFRIMMA), Mtumbuizaji Bora (MAMA), Msanii Bora wa Mwaka (MTV EMA), Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (AFRIMA) na nyingine nyingi.

Utajiri wa Vigogo TRA Unatisha..Wajilimbikizia Magari na Majumba ya Kifahari

$
0
0
Aliyekuwa Kamishina Mkuu, Rished Bade
IMEVUJA! Hakuna shaka kwamba, utajiri wa wale vigogo watumishi wa umma waliokuwa wakifanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unatisha kufuatia gazeti hili kufukunyua mali za baadhi yao, twende hatua kwa hatua.
Ijumaa iliyopita, Waziri Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, alifanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kubaini ukwepaji kodi mkubwa ulioikosesha serikali kiasi cha shilingi bilioni 80.
Katika kikao na viongozi wa TPA sanjari na viongozi wa TRA, akiwemo aliyekuwa Kamishina Mkuu, Rished Bade, Waziri Majaliwa aliamuru papo hapo, kusimamishwa kazi kwa baadhi ya vigogo wa bandari.

PANGA LILITUA KWA HAWA
Vigogo waliosimamishwa ni pamoja na Bade, Kamishina wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Tiagi Masamaki na Habibu Mponezya wa Kituo cha Huduma kwa Wateja kisha waziri mkuu akamwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu kuhakikisha wote wanakamatwa.
Wengine waliosimamishwa ni Eliachi Mrema (Msimamizi Mkuu wa Bandari Kavu Dar es Salaam), Haruni Mpande (Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) na Hamis Omar, Nsajigwa Mwandegele, Robert Nyoni na Anengisye Mtafya.

AGIZO ZITO
Kabla hajamaliza kikao, Waziri Majaliwa aliagiza kuwa, licha ya watu hao kukamatwa, hati zao za kusafiria kushikiliwa, pia mali zao zichunguzwe ili kubaini kama zinaweza kumilikiwa na mtumishi wa umma kwa kutumia mshahara wake!

RISASI MCHANGANYIKO LAFUKUA
Kufuatia agizo hilo la Waziri Mkuu katika kipindi hiki cha ‘hapa kazi tu’, gazeti hili liliingia mtaani kwa kufanya uchuguzi wa kina ili kubaini utajiri wa vigogo hao na wengine ambao hawajakumbwa na sakata hilo.

Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilifika Masaki, Mbezi na Tegeta Madale kwenye makazi ya baadhi ya watumishi hao ili kuona mazingira yao.
Ndani ya nyumba ya mtumishi mmoja, Risasi liliona magari matatu ya kifahari aina ya Toyota Land Cruiser ‘VX’, Mercedes Benz na Range Rover achilia mbali Toyota Noah ambayo majirani walisema huwa inakwenda sokoni kufanyia ‘shopping’.

Kwenye nyumba nyingine, ukuta ulikuwa mrefu kiasi cha wapigapicha wetu kushindwa kuona ndani mpaka wakapiga kengere. Lakini majirani walisema si rahisi kufunguliwa kwa siku mbili hizi kwani kumekuwa na ‘ingia toka’ ya watu wa usalama wa taifa.

Kama hamna namba za simu za mtu yeyote aliye ndani sijui kama mtafunguliwa. Siku mbili hizi, watu wa usalama wa taifa wanaingia na kutoka,” alisema jirani mmoja.
Jirani huyo alisema jumba hilo mmiliki ni mkaaji mwenyewe ambaye ni mtumishi wa TRA na ana nyumba nyingine maeneo ya Mwenge licha ya kumiliki maduka ya nguo Kariakoo, Dar.
Baada ya hapo, gazeti hili lilifunga safari hadi Pugu ambako kuna makazi mengine ya mmoja wa vigogo hao lakini nyumba ilionekana kuwa kimya na kutokuwepo kwa gari hata moja kwenye eneo la maegesho.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Mjumbe wa Nyumba Kumi Mtaa wa Pugu Bombani, Abdallah Shaban alisema huwa kunakuwa na magari mengi kwenye nyumba hiyo, lakini kwa siku mbili zilizopita (Jumamosi na Jumapili) hajayaona.
“Hapa ‘panakuwaga’ na magari mengi sana. Unaweza kusema ni yadi ya kuuza magari, lakini siku mbili hizi sijayaona,” alisema mjumbe huyo.

MAGARI HAYANA KAZI
Mjumbe huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kutokana na magari kuwa mengi pasipo watumiaji, mara nyingi asubuhi mmiliki huyo humwagiza mtu mmoja kuyawasha na kuunguruma kwa muda kisha kuyazima kwa lengo la kuyapasha moto.

NYUMBA KAMA KIJIJI
Mjumbe huyo alilionesha Risasi Mchanganyiko eneo kubwa la mtumishi huyo ambapo amejenga nyumba za familia zisizopungua 20 sehemu moja (kama kijiji) na moja tu ndiyo imepangishwa.

UCHUNGUZI WA JUMLA
Uchunguzi wa jumla uliofanywa na Risasi Mchanganyiko ulibaini kuwa, watumishi wengi wa TRA na TPA wanamiliki nyumba na magari licha ya kulipwa mshahara wa ngazi ya serikali ambao wasingeweza hata kununulia gari moja la kifahari kama ilivyo sasa.
GPL

Msimamizi wa Makontena 9 Yaliyokamatwa Jana Mbezi Afunguka Yote na Kuelezea A to Z Kuhusu Hayo Makontena

$
0
0
Msimamizi wa Makontena 9 Yaliyokamatwa Jana Mbezi Afunguka Yote na Kuelezea A to Z Kuhusu Hayo Makontena Angalia Video Hapa:

Mfanya Biashara BINSLUM TYRES LTD Akiri Kuwa Makontena yake 20 Hayana Nyaraka za Kodi

$
0
0
BINSLUM
UKWEPAJI KODI BANDARINI: Mfanyabiashara wa Kariakoo Jijini Dar Nassoro Ahmed bin Slum anayemiliki kampuni inayoitwa BINSLUM TYRES LTD, katika mazungumzo yake na gazeti la Raia Mwema amekiri kuwepo kwa utata wa kodi

Katika maelezo yake amekiri makontena 20 tu hayana nyaraka za kodi lakini kamtupia lawama wakala wake

Binti Mmoja Amefariki Dunia Baada ya Kula Mchanga wa Kaburini Baada ya Kuambiwa na Mhubiri

$
0
0
KENYA: Binti mmoja amefariki dunia baada ya kula mchanga wa kaburi

Mhubiri alimshauri ale mchanga huo kwa madai kuwa ana mizimu

Inasemekana baada ya kunyweshwa dawa, ndivyo hali ya afya ya msichana huyo ilivyozidi kuwa mbaya hadi akapoteza fahamu.

Hata hivyo mhubiri mwenyewe amejitetea akisema huenda ilitokana na familia ya marehemu kutokuwa na Imani na maombi yake ya uponyaji. 


Wastara Juma Akwaa Jinamizi la Usagaji..Atumiwa Picha za Utupu na Mwanamke Mwenzake

$
0
0
Wastara
Jinamizi la usagaji limetua kwa nyota wa filamu nchini, Wastara Juma baada ya dada aliyefahamika kwa jina moja la Marry, ambaye awali alimsaidia katika matibabu, kumtaka afanye naye mapenzi ya jinsia moja, Ijumaa limenyetishiwa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Marry ambaye anadaiwa kuishi Dubai, baada ya kuona lengo lake halijatimia, alianza kutoa maneno ya kashfa kwa Wastara kupitia mitandao ya kijamii, akidai ameingia mitini baada ya kuchukua pesa kutoka kwake.
Huyo Marry ambaye alikuwa rafiki wa Wastara anadai alimtumia pesa ili amnunulie dawa za mwanaye, lakini hakufanya hivyo na badala yake, akawa hapokei simu akipigiwa na vilevile ‘akamblock’ kwenye mtandao wa WhatsApp, ndipo huyo dada akakasirika na kuamua kuropoka,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Wastara na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, ambapo alikiri kutokea, kwani Marry aliyefahamiana naye kabla hajaondoka nchini, alimtumia fedha shilingi laki tano kwa ajili ya kununua dawa za mwanaye, lakini alipomtaka amuelekeze kwa ndugu zake wanaoishi Kenya ili azipeleke, alikataa.

Wakati nilipokwenda Kenya kwenye matibabu ya mguu wangu, alinitumia tena shilingi laki mbili kunisaidia, lakini siku chache baadaye nikaanza kushangaa ananipigia simu na kunitumia picha akiwa mtupu, akinishawishi tufanye mapenzi ya jinsia moja, kitu ambacho kiliniudhi na kuamua kuacha kupokea simu zake na pia nikamzuia katika akaunti yangu ya WhatsApp,” alisema Wastara.
Kwa upande wake, Marry kupitia mawasiliano kwa njia ya mtandao huo, alionesha kushangazwa kwake na mabadiliko ya tabia ya Wastara, kitu ambacho hata hivyo hakimshtui isipokuwa anahitaji kurejeshewa fedha zake.

Sasa sielewi kwa nini tangu nimtumie zile pesa hataki kuongea na mimi, hayo mambo ya usagaji hata sielewi maana mimi ni mwanamke, nina jinsia moja, sina jinsia ya kiume, nitafanyaje mapenzi na yeye, nachotaka anipe pesa zangu, simuogopi hata kidogo,” alisema.
GPL

Vigogo TRA Wakutwa na Mamilioni Nyumbani Kwao

$
0
0
Siku  chache baada ya kigogo mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kubainika kumiliki nyumba 73, wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo wamekutwa na mamilioni ya shilingi waliyoficha majumbani mwao.

Taarifa kutoka ndani ya TRA zinapasha kuwa tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awasimamishe kazi maofisa kadhaa wa mamlaka hiyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kitengo cha uchunguzi cha mamlaka hiyo, hivi sasa wapo kwenye msako wa kubaini ukwasi wa wafanyakazi wake.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, juzi maofisa wa kitengo cha uchunguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, walifika katika eneo la Tegeta Salasala wilayani Kinondoni na kuvamia nyumba mbili za wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Katika nyumba hizo, wafanyakazi hao kila mmoja alikutwa na kiasi kikubwa cha fedha ndani kuliko kiwango cha mshahara anaolipwa.

Walivamiwa wafanyakazi wawili (majina yanahifadhiwa), ambapo katika kila nyumba zilikutwa fedha nyingi. Kwa mtu wa kwanza zilikutwa Sh milioni 200 na yule wa jirani yake pia alikuwa na zaidi ya shilingi milioni 150.

Tangu kuanza kwa msako huu wafanyakazi wengi wamekuwa hawana amani kabisa, na hata wengine wanasema wazi kama wangekuwa na uwekezaji wa nje ya nchi wangeondoka kabisa nchini,” kilisema chanzo cha gazeti hilo.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wafanyakazi hivi sasa wamelazimika kuzikimbia nyumba zao na kuishia kulala hotelini huku wakienda kazini wakiwa na hofu.

Hivi karibuni, vyombo vya habari viliripoti kuwa Kamishna wa Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki, aliyesimamishwa kazi pamoja na vigogo wengine wa mamlaka hiyo kutokana na upotevu wa kontena 349 zenye thamani ya Sh bilioni 80, amebainika kumiliki nyumba 73.

TRA Yakusanya Bilioni 5 za Kodi ya Makontena 329......Wafanyakazi 37 Wasimamishwa Kazi

$
0
0
Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA,Phillip Mpango  amewasimamisha kazi wafanyakazi 37 mchana huu  kupisha uchunguzi wa sakata la upotevu wa makontena bandarini

Mpango pia ametoa agizo la watumishi wote wa TRA kuwasilisha taarifa za mali zao kwa utawala na kusiwepo na udanganyifu wowote.

Amesema mpaka sasa TRA imekusanya kiasi cha Tsh Bilioni 5 za kodi ya makontena hayo yaliyokuwa yamepitishwa kinyemela

Kasi ya Magufuli Yamkuna Mbunge wa Chadema Sugu, Awataka Madiwani wa Chadema Jimboni Mwake Kushindana na Kasi ya John Magufuli

$
0
0
Sugu Akiteta Jambo
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kushindana na kazi ya rais John Magufuli.

Sugu alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha kumchagua diwani atakayewania nafasi ya Umeya kwa tiketi ya chama hicho.

Aliwataka madiwani hao kuchapa kazi na kuwafanya wananchi kujivunia kasi ya maendeleo inayoletwa na Mbunge na Meya wa jiji hilo ili wasitamani jimbo hilo lingeongozwa na wapinzani wao wa CCM.

“Hata CCM wenyewe wamebadilika, Magufuli anakwenda jalamba. Hakutakuwa na vitu kama ambavyo mnaviwaza, tunaenda kufanya kazi za wananchi ili wananchi wasitamani kwamba afadhali na hapa pangekuwa CCM. Waseme hata kama Magufuli anaenda spidi na sisi Mbeya yetu Meya na Mbunge wanakwenda spidi.”


Nafasi za Ajira

Picha za Watuhumiwa wa Upotevu wa Makontena 329 Walivyopandishwa Kizimbani leo

$
0
0
 Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.
 Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.
 Watuhumiwa wa kesi hiyo wakiingia ndani ya gari.
 Mmoja wa watuhumiwa hao akiwa ndani ya gari la Polisi.
Watuhumiwa hao waliokaa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo.
Na Dotto Mwaibale
KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.
Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51)
Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis  ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.
Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.
Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali  kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote kutolewa.
Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
“Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana,” alisema Hakimu Shahidi
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.

Kuna Kila Dalili za Prof. Lipumba Kuwa Waziri wa Rais John Magufuli

$
0
0
Prof. Lipumba ni mmoja wa wamchumi nguli waliowahi kutokea nchini. Huyu bwana mbali tuu na kujivua uenyekiti wa chama chake cha CUF katika kipindi ambacho walikuwa wanamhitaji sana, lakini yeye amemkubali Rais JPM kuwa rais halali tofauti na msimamo wa chama chake ambacho kinaunda UKAWA.

Lakini hivi juzi alienda mbali mpaka kwenda Ikulu kumpongeza rais JPM. Kana kwamba haitoshi, mahakama imemfutia kesi yake na wafuasi wote alioshitakiwa nao kisa eti DPP kaamua kutoendelea na hiyo kesi. Hapo kuna maswali mengi ya kujiuliza???

Lakini vilevile Lipumba mara nyingi amekuwa na maoni chanya Kwa rais na CCM hali yeye mpinzani. Na yeye anajinasibu kuwa anapinga ufisadi na kitendo cha lowasa kwenda ukawa ni sawa na kumkaribisha fisadi.

Na JPM anasema hana ubia na mtu yeyote kwenye urais wake na kuna kila dalili za mawaziri kibao wa serikali iliyopita kupigwa chini kutokana na sifa ya utendaji mbaya. JPM haishiwi surprise na kutekeleza kile anachokiamini. Sasa je hizi si dalili za Prof Lipumba kuukwaa ubunge wa kuteuliwa na baadaye uwaziri wa serikali ya JPM???

Ni Mtizamo Wangu Tuu

Nafasi za Ajira


Magufuli Aitaka TRA Kutoa Mashine za EFDs Bure.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameishangaa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kutogawa bure Mashine za EFDs, na wao kubaki na kazi ya kukusanya mapato.

Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji jana jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), alisema muda uliopotea na kodi ambayo haikukusanywa wakati wa mvutano na wafanyabiashara ungetosha kununua mashine mpya na kuwagawia.

“Kama mnajua mashine hizi ni halali na ni zenu, wapeni bure kazi yenu iwe ni kukusanya kodi, ni hesabu rahisi sana isiyohitaji kwenda chuo kikuu kuwa muda uliopotea na fedha hazifiki bilioni 12 zingetosha kununua na iwe kazi ni kukusanya kodi,” alisema.

Awali katika salamu zake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Jonson Minja, alimpongeza rais kwa kazi kubwa aliyofanya Bandarini na TRA kwa kuwa imewezesha kodi kukusanywa kwa usahihi na kwamba kipindi cha nyuma fedha nyingi zilipotea, kutokana na mfumo wa ukusanyaji kodi kutowekwa wazi.

Aidha, alisema mashine za EFDs zitatumika kwa wafanyabiashara wote mwakani, kwa kuwa changamoto zilizosababisha mvutano baina yao na serikali zimemalizika.

Aidha, alimtaka rais kufuatilia kwa karibu ukwepaji kodi katika sekta isiyo rasmi na kwamba kukiwa na mipango madhubuti serikali itaweza kupata kodi kwa wananchi wote.

“Kasi ya rais inatupa matumaini makubwa sana, tunachoweza kusema, Mungu akubariki akupe hekima na nguvu...tunaomba uimarishe viwanda vya kati na vidogo ili malighafi zisisafirishwe kwenda nje, bidhaa ambazo zitasaidia kukuza uchumi na kuimarisha shilingi dhidi ya Dola ya Marekani,” alisema.

Tangu mwaka juzi kulikuwa na mvutano mkali baina ya wafanyabiashara na TRA, ambao waligoma kutumia mashine hizo hadi serikali itakaposhughulikia kero zao ikiwamo bei ya mashine, utitiri wa kodi, ukwepaji kodi na urasimu uliopo.

Wafanyabiashara kwa umoja wao waliitisha mgomo nchi nzima na kumekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na serikali, ambayo wakati mwingine hayakufikia ukingoni, hatua iliyofanya baadhi ya viongozi wa wafanyabiashra kukamatwa.

Minja alikamatwa na Polisi mkoani Dodoma mwaka jana, na kuswekwa ndani, jambo lililofanya wafanyabiashara kuitisha mgomo wa siku tatu hadi serikali itakapoeleza alipo kiongozi wao.

Baadaye ilibainika anashikiliwa na Polisi mkoani humo, na alipandishwa mahakama ya mkoa na kusomewa mashtaka ya kuchochea mgomo wa wafanyabiashara nchini.

Baadaye mahakama ya mkoa ilimuachia huru kiongozi huyo.

Zitto Kabwe, Tulia Kama Wenzako - Acha Majungu

$
0
0
Mimi namshangaa sana Zitto Kabwe, mbona anahangaika sana na mambo mengi, maneno, majungu, kujidai yeye ndo mgunduzi wa ufisadi etc? 

Bwana Zitto hii serikali ya Mh Magufuli inajimudu, hembu tulia kama wabunge wengine kwa kipindi hiki na acha kuleta mambo mingi mingi isiyokuwa na maana, Mzee hatokupa cheo chochote.

Mambo ya ukawa kuwa na watu wa shutuma za ufisadi wakati wa uchaguzi yanakuhusu nini? hata mgombea wa ukawa alikuwa na tuhuma lukuki za ufisadi? hivi hili nalo ni jipya? si utulie tu ukae na familia yako kipindi hiki na upunguze maneno yasiyo na tija?

Nafasi za Ajira
Bonyeza www.ajirayako.com

Anachofanya Waziri Mkuu, Sio Sawa, Sio haki, Sio Good Governance...Ni Udhalilishaji na Kuaibishana!

$
0
0
Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

By Pasco-Jamii forums

Nafasi za Kazi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Desemba 5, Ikiwemo ya Vigogo Walivyotafuna Bandari

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Desemba 5

Kasi ya Rais Magufuli Haiko Kwenye Makontena Bandarini tu, imepita na TFF Ambapo TRA Imesitisha Safari Ya Timu Ya Taifa Ya Vijana

$
0
0
Ikiwa bado siku moja Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli atimize mwezi mmoja toka aapishwe kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeshuhudia mengi yakitokea katika suala zima la upambanaji na watu wanaokwepa kodi sambamba na kusimamishwa kazi kwa viongozi kadhaa wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) waliopo Bandarini.

December 4 kasi ya Rais John Pombe Magufuli inaonekana kuwashitua viongozi wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kwani wameanza harakati za kuwaadhibu watu wanaodaiwa kodi.

Juma lililopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liliaga timu ya Taifa ya Vijana Chini ya umri wa miaka 15 (U15) ikianza ziara yake ya Afrika Mashariki kuanza kucheza na Burundi mjini Kigoma na baadaye Kigali, Rwanda, Kampala, Uganda na mwisho Nairobi Kenya.

Bahati mbaya ziara hiyo itaishia Mwanza na Kigoma kufuatia Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA) kuizuia account ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kushindwa kulipa kodi ya Tsh bilioni  1,637,334,000 (bilioni 1.6 tshs) ikiwa ni kodi kwa kipindi cha 2010 – 2013

Sehemu kubwa ya kodi hiyo ni makato kwenye mishahara (PAYE) ya walimu wa kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Jacob Michelsen na vilevile kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Brazili uliofanyika mwaka 2010.

Walimu wa Timu za Taifa wamekuwa wakilipiwa mishahara na Serikali na hivyo TFF haikuwajibika kuwakata kodi. Aidha, mchezo kati ya Tanzania na Brazil ulisimamiwa na kamati maalum ya Serikali na fedha zake hazikuingizwa katika akaunti za TFF.

Kutokana na hatua hii ya TRA shughuli nyingine za mpira zitakazohathirika  ni:

1. Kulipia madeni ya usafiri, chakula na posho za Timu za Taifa zilizoshiriki mtoano wa kombe la Dunia na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Challenge Cup)

2. Program za mpira wa Wanawake na vijana zitalazimika kusimama.

3. Mashindano ya kombe la Shirikisho raundi ya pili iko kwenye hatihati kwani hakuna fedha za kugharimia michezo hiyo.

4. Mashindano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoendelea yatalazimika kusimama vilevile. Mashindano haya TFF imekuwa ikiyaendesha bila mdhamini.

5. Vifaa vya michezo (Mipira) kwa ajili ya shule za msingi na vituo vya maendeleo (Regional Football Development Centres) vinatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote na TFF haitakuwa na uwezo wa kulipia usafirishaji na ushuru wake.

6. Malipo ya gharama za kambi na karo kwa ajili ya vijana wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 13 walioko shule ya Alliance Academy ya jijini Mwanza.

7. Huduma za kiutawala ikiwa ni pamoja na utunzaji viwanja na majengo, maji, umeme, ulinzi pamoja na mishahara na stahiki nyingine za wafanyakazi

8. Mwelekeo na mwitikio mzuri wa wadhamini uko kwenye hatari ya kupotea pindi mashindano na shughuli wanazozidhamini zitakapofubaa au kusimama kabisa.

9. Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wa Mwaka 2015 uliopangwa kufanyika Tanga 19-20 Desemba 2015 sasa una hatihati ya kuweza kufanyika.

Hata hivyo, kwa kutambua umuhimu wa ulipaji kodi na wajibu wa Mamlaka ya Mapato katika kuhakikisha kodi inakusanywa kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Taifa,TFF ipo katika mawasiliano na TRA katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa suala hili ikiwa ni pamoja na kupitia upya mahesabu ili kujua wajibu halisi (net liability) wa TFF na namna ya kulipa au kulipwa kutegemea ulali wa mahesabu.

Kwa taarifa hii TFF inaomba utulivu kwa wanamichezo wote pamoja na ushirikiano wa karibu kutoka katika vyombo vyote husika ikiwemo TRA na wadau wengine ili jambo hili lipate ufumbuzi wa kudumu utakaoleta tija kwa serikali ya awamu ya tano ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika maendeleo ya mpira wa miguu na michezo kwa ujumla wake.

Nafasi za Kazi Coca Cola Kwanza Limited, Application Deadline: 13th December, 2015

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>