Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Breaking News: Rais Magufuli Avunja Bodi ya Bandari.....Amsimamisha Kazi Katibu Mkuu Wizara Ya Uchukuzi

$
0
0
Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano Dkt.John Pombe Magufuli katika kasi yake ya kutumbua majipu hatimaye,amevunja bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa bandari Bw.Awadhi Massawe (Pichani), Mwenyekiti wa bodi ya bandari pamoja maofisa 8 wa bandari .Ameagiza wote wawekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uchunguzi

Rais  pia  amemsimamisha  kazi katibu mkuu wizara ya uchukuzi Bw.Shabani Mwinjaka.

Sakata la Manji na Coco Beach, Tamko Kali Latolewa Kwa Manji na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni....

$
0
0
WAZALENDO TANZANIA (JUHWATA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu waandishi wa habari, Jukwaa limewaalika hapa katika muendelezo wake wa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. -Dr. John Magufuli. Hivi karibuni mh. Rais ameongoza mapambano makubwa ya kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi yaliyopotea. Tunaunga mkono juhudi hizi za Rais wetu na tunamuhakikishia kuwa Jukwaa linamuunga mkono na kwamba tunaomba azidishe kasi zaidi ili wale wote waliokwepa kodi wakamatwe, walipe na kufikishwa katika vyombo vya sheria bila huruma yoyote.

Ndugu waandishi wa habari, leo tumewaita hapa dhumuni kuu likiwa ni kuzungumzia uporaji wa maeneo ya wazi yanayotumiwa na wananchi hasa wanyonge. Uporaji huu unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa ambao hutumia nguvu zao za kiuchumi kuwarubuni na wakati mwingine kuwahonga viongozi wetu wachache serikalini wasiokuwa na uzalendo kwa taifa lao wala huruma kwa wanyonge ili wawapatie maeneo ya wazi yanayotumiwa na wananchi. 

Katika hotuba yake ya tarehe 3/12/2015, akizungumza na wadau wa sekta binafsi nchini, mh. Rais alizungumza kwa uchungu njama za uporaji wa sehemu ya wazi ya umma ya ufukwe wa bahari wa inayotumiwa na wananchi wa hali ya chini kupumzika na kuogelea. Uporaji huu unafanywa na mfanyabiashara mmoja tajiri akitumia nguvu zake za kiuchumi kuwarubuni baadhi ya viongozi wa serikali ili wampatie eneo hilo. Hapana shaka eneo hilo ambalo wakazi wa Dar es salaam wa hali za chini wanalitumia kuogelea bure ni Coco beach iliyoko Oysterbay. Tumeamua kutoka hadharani kumuunga mkono mh. Rais kwa kuuanika uozo na njama za muda mrefu za kuligawa eneo hilo zinazofanywa na mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni na wenzake kwa mmiliki wa kampuni ya Q Consult Yusuf Manji.
-Mfanyabiashara huyu ameanza kuiitafuta Coco beach kwa miaka mingi sasa. Njama hizo zinahusisha kumfanyia hila na mizengwe muwekezaji mzawa anayetajwa kwa jina la Alphonce ambaye tangu mwaka 1994 amekuwa akitoa huduma kwa wananchi akiwa mpangaji wa manispaa ya Kinondoni. Bwana huyu kwa karibu miaka 9 mfululizo amekuwa akinyanyaswa, kukwamishwa kuendesha biashara yake na kufanyiwa njama za kunyang?anywa eneo hilo na watendaji wa serikali hasa wakurugenzi wa manispaa ya Kinondoni wa vipindi tofauti ili apewe mmiliki wa kampuni ya Q Consult bwana Yusuf Manji.

Njama hizi zimekuwa zikibeba viashiria, dalili na mazingira ya uwepo wa rushwa ya mtandao (syndicate corruption) ambapo viongozi wa serikali na manispaa ya Kinondoni akiwemo Mkurugenzi wa sasa wa manispaa ya Kinondoni bwana Musa Nati.

Mkurugenzi huyu amekuwa akikaidi maagizo ya viongozi wake wa juu kwa kiburi na ubabe na kumfanyia hila mtanzania huyu mnyonge kwa kumnyima mkataba huku akiwa amewekeza jasho lake katika ufukwe huo. Mkurugenzi amekaidi mara kadhaa maagizo ya Katibu mkuu wa Tamisemi, na hata aliyekua Waziri Mkuu mh. Mizengo Pinda. Aidha Mkurugenzi huyu ambaye anaonesha kuwekwa mfukoni na bwana Manji amekuwa akikaidi pia maamuzi ya vikao vya baraza la madiwani vya Full Council na kuidanganya kamati ya bunge ya LAC kuhusiana na sakata hili la Coco beach. Mkurugenzi huyu, kwa kushirikiana na viongozi wengine wa wilaya na Mkoa wa Dar es salaam ambao kwa leo tunahifadhi majina yao, wameonesha wazi kuwa upande wa bwana Yusuf Manji wakati wote wa sakata hili, huku wakionesha viashiria vya kuhongwa na kupindisha haki. 

Tunajiuliza, kiburi hiki alichionacho Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni anakitoa wapi? Jeuri hii ya kukaidi maagizo ya ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI anaitoa wapi? 
Jukwaa linahoji, kwanini mfanyabiashara Yusuf Manji ang?ang?anie kupewa fukwe ya Coco beach na kutaka muwekezaji mnyonge anyang?anywe? Inawezekanaje mtu mmoja awe na ujasiri wa kuwarubuni watendaji wa serikali kwa miaka kadhaa kiasi cha kutotii maelekezo ya wakubwa wao? Yusuf Manji ni nani katika nchi hii hadi aweze kuabudiwa na viongozi hawa wa serikali? 
Jukwaa linaona kila dalili kuwa kuna rushwa kubwa imetumika kuwanunua viongozi wetu ili wawe watetezi wa mabepari badala ya wanyonge. Ili waweze kubadili Coco beach kuwa mahali pa anasa na ghali kiasi cha kuwafanya watoto wa masikini washindwe kufika na kufurahia rasilimali za taifa lao. 

MAAZIMIO

Tunamuomba mh. Rais amsimamishe kazi mkurugenzi huyu na kufanya uchunguzi juu ya jambo hili ili kubaini ni viongozi wangapi wamehongwa, wamehongwa nini na kwa muda gani, na ama la kwanini walipata kiburi cha kukaidi maelekezo ya viongozi wakubwa wa serikali kuhusu sakata hili. Jukwaa linamtaka bwana Yusuf Manji kutii kauli ya Mh. Rais na kuachana na suala la Coco beach kwa hiyari yake mwenyewe, kwani yako maeneo mengi ya fukwe katika nchi yetu ambayo angeweza kuwekeza. 
Ikiwa bwana Yusuf Manji hatojitokeza hadharani kutoa kauli ya kuachana na na ufukwe wa Coco beach, Jukwaa litaandaa na kuhamasisha maandamano ya amani ya umma kueleza hisia zake juu ya jambo hili. Tunamkumbusha kuwa, mali za matajiri kama yeye hazilindwi na mitutu ya bunduki za polisi, bali zinalindwa na amani na utulivu na kuridhika kwa wanyonge. Wanyonge wenye hasira za kudhulumiwa ni hatari kuliko bomu la kutupa kwa mkono. 

Tunafahamu ya kwamba yako maeneo mengi ya wazi ambayo kwasababu ya tamaa na rushwa, viongozi wa serikali wameyauza kwa matajiri na kuwafanya watoto wa wanyonge kukosa mahali pa kucheza.

-Jukwaa litaleta ushahidi wa maeneo mengine ambayo watu wa aina ya Yusuf Manji wamepewa na viongozi walafi wasiokuwa na uzalendo na maadili kinyume na sheria na taratibu za nchi yetu. 

Tunamtaka mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni na viongozi wengine wa serikali wa wilaya hiyo kujitafakari mwenyewe kabla ya kuchukuliwa hatua na mh. Rais, kwani uko ushahidi wa ukaidi na ujeuri wake wa kupindisha haki na kumpendelea bwana Yusuf Manji hata kabla ya maamuzi ya kesi kutoka. Akishindwa kufanya hivyo, Jukwaa litaupeleka ushahidi huo kwa mh. Rais na kuweka wazi kwa umma wa watanzania ili waone ukweli wa jambo hilo. Jukwaa linamfahamisha bwana Manji kwamba, hataweza kushinda vita dhidi ya umma, hasa umma wa wanyonge ambao wenye hasira ambao wanaamini haki yao imeporwa kwa rushwa. 
Jukwaa litaendelea kumuunga mkono mh. Rais na serikali yake katika mapambano dhidi ya rushwa, ukwepaji kodi na uzembe serikalini. Hatutamuogopa yeyote katika kutimiza wajibu wetu huu wa msingi kwa taifa letu. Tunawaomba wananchi wote kumuunga mkono mh. Rais kwa kumuombea na kufichua maovu yanayofanywa na viongozi wa serikali katika maeneo yao ikiwemo rushwa lugha chafu na ukwepaji kodi.

Mungu ibariki Tanzania. 

Ahsanteni. 

ALLY S. HAPI,

-MWENYEKITI

MTELA MWAMPAMBA,

-KATIBU MKUU

Kasi ya Magufuli Yaikumba Clouds FM...Mwaka Huu Tamasha la Fiesta Halitafanyika

$
0
0
Mkurugenzi wa Clouds Media Group ambao ni waandaaji wa tamasha la Fiesta, Ruge Mutahaba amesema kuwa tamasha hilo halitakuwepo mwaka huu.

Amesema wameamua kuahirisha kufanya tamasha hilo mwaka huu kutokana na ufinyu wa muda uliobaki hasa baada ya kupisha kipindi cha uchaguzi.

“Tulijua tukimaliza kampeni tutafanya kwa mikoa michache lakini tumeona kwamba hakuna kitu kizuri kama kumsupport mheshimiwa Magufuli , hebu sasa hivi turudi kwanza tutulie tuache hii amsha amsha aliyoanza nayo ianze kufanya kazi tujipange kwaajili ya Fiesta 15 ambayo itafanyika mwaka kesho,” Ruge aliiambia XXL ya Clouds Fm.

“Tutakuwa tunafikisha miaka 15 ya Fiesta na nina uhakika itakuwa na ukubwa inayostahili kuliko kufanya kitu kidogo mwaka huu. Tumeona tuache mwaka kesho mikoa 15, miaka 15 ya Fiesta itakuwa kubwa zaidi. Hapa Kazi imebidi iivae Fiesta pia,” alisema.

Nafasi za Kazi

Kasi ya Rais MAGUFULI imegonga hodi ofisi ya Rais-utumishi.......Watumishi wa Umma Watakiwa Kusaini Kiapo cha Ahadi na Uadilifu

$
0
0
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza rasmi kutekeleza Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma nchini .

Akiongea na vyombo vya habari leo, Katibu Mkuu Hab  Mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi Desemba, 2015 ambapo kila Mtumishi wa Umma ataweka saini  ya kiapo  kwa kuzingatia  taratibu zilizowekwa na  mazingira ya taasisi husika.

“Utaratibu wa Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma umetolewa kupitia waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma  Na. 2 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi, Watumishi wa Umma na sekta binafsi wa tarehe 1 Agosti, 2015.” alisema Mkwizu.

Mkwizu aliongezea kwa kusema, uanzishwaji wa Ahadi na Uadilifu  ni muendelezo wa uundwaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu, utoro sehemu za kazi na kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya themanini na tisini.

Alivitaja vyombo vingine ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi na uadilifu kuwa ni Sekretariate ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Mkwizu alivitaja vipengele ambavyo mtoa ahadi anatakiwa kuvitamka ni, kuwa mzalendo wa nchi yake na kutii Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhudumia Umma na watumishi wenzake kwa heshima, kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma, kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi wa dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu.

Vipengele vingine ni kutumia rasilimali za Umma kwa manufaa ya Umma, kutotoa siri za Serikali au mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya Umma, kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kutoomba kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa na kutotumia madaraka kwa manufaa binafsi ya ndugu, rafiki au jamaa.

Aidha, Mkwizu ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ahadi na Uadilifu unakamilika  ifikapo tarehe 31/12/2015 na kuwasilisha Ofisi ya Rais – UTUMISHI kabla ya tarehe 25/02/2016 na utekelezaji wake kuwa kila ifikapo Juni 30 ya kila mwaka. 

Fomu za Ahadi ya Uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI yenye anwani www.utumishi.go.tz.

Nafasi za Ajira
Bonyeza www.ajirayako.com

Kutokuwapo Kwa Mawaziri Kumeokoa Mamilioni

$
0
0
Uamuzi wa Rais John Magufuli kukaa zaidi ya mwezi mmoja bila kuteua Baraza la Mawaziri huenda ukawa umeisaidia Serikali kwa kuokoa takribani Sh683.3 milioni za walipa kodi, bila kuhusisha gharama za ununuzi wa ‘mashangingi’.

Kiasi hicho cha fedha kimetokana na hesabu inayokadiriwa kuwa matumizi ya waziri iwapo Rais Dk Magufuli angeendelea na ukubwa wa Baraza la Mawaziri la mwisho la Rais Jakaya Kikwete la mawaziri 55, kati ya hao 24 wakiwa manaibu waziri.

Hata hivyo, Dk Magufuli ameshatangaza kuwa na baraza dogo la mawaziri, ingawa hajaweka bayana litakuwa na jumla ya mawaziri wangapi.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye, Waziri hulipwa mshahara wa kati ya Sh3.8milioni mpaka Sh 5milioni kwa mwezi ambazo ni sawa na mshahara wanaolipwa wabunge.

Kwa mantiki hiyo, kwa mawaziri 55, Serikali ilitakiwa ilipe Sh209 milioni kwa ajili ya mishahara ya Novemba, lakini hazikulipwa kwa kuwa bado kiongozi huyo hajawateua.

Kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la mwaka 2009, zinaitaka Serikali kumpatia nyumba mtumishi anayetakiwa kupatiwa huduma hiyo kwa aidha kumpa nyumba ya Serikali au kumkodishia nyingine yenye hadhi ili aweze kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Kanuni hizo zinamtaka Wakala wa Majengo (TBA) kufanikisha zoezi hilo la kutoa huduma za nyumba au kusimamia ukodishaji wa nyumba husika ya mtumishi.

Mawaziri ni miongoni mwa watumishi wanaopatiwa nyumba za Serikali ambazo nyingi zinapatikana katika maeneo ya vigogo ya Masaki, Oysterbay au Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa tovuti ya uuzaji na ukodishaji nyumba na viwanja ya Lamudi, nyumba za bei ya wastani ambayo inaweza kwenda na hadhi ya waziri inakodishwa kwa kiasi kisichopungua Sh5 milioni kwa mwezi.

Hivyo basi, kama nyumba za mawaziri hao ambazo hukarabatiwa na kuhudumiwa na TBA, zingekuwa zimekodishwa kutoka kwa watu binafsi kwa kipindi cha mwezi mzima basi Serikali ingelipa Sh275 milioni.

Ili kutimiza majukumu yao vyema wakiwa bungeni mjini Dodoma, mawaziri pia hupatiwa nyumba za kuishi tofauti na zile za Dar es Salaam ambazo zipo chini ya TBA.

Hata hivyo, Ole-Medeye alisema Serikali huwalipa mawaziri Sh800, 000 kwa mwezi kwa ajili ya huduma za nyumba za Dar es Salaam, mawasiliano na ankara nyingine za kumsaidia kimaisha.

Iwapo kiwango hicho cha Sh800, 000 kwa mwezi kingetumika kumlipa kila waziri kama sehemu ya fedha za makazi, bado Serikali ingehitajika kutoa Sh44 milioni kwa ajili ya gharama za kuhudumia nyumba na mawasiliano.

“Hivi Sh800, 000 utapata wapi nyumba ya kukodi akaishi waziri? Kwa bei ya sasa nyumba za kiwango hicho ni Dola za Marekani 3,000 (Sh6 milioni) au zaidi.

“Sasa fedha hiyo umlipe mtumishi wa ndani, gharama za umeme, mawasiliano na maji ndiyo maana nasema uwaziri ni kazi ya kuhudumia jamii,” alisema Ole-Medeye akieleza kuwa waziri hupatiwa posho ya Sh80, 000 kwa siku akiwa mikoani kwenye ziara.

Gharama za posho za mawaziri hao zingetegemea na siku ambazo wangekaa mikoani kwa kipindi hicho cha siku 31, na hivyo si rahisi kujua kiwango chake.

Gharama za samani

Miongoni mwa mambo ambayo Serikali hugharamia kwa mawaziri wake ni samani za ndani ya nyumba, ambazo pia huongezeka au kupungua kulingana na ukubwa wa baraza.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Adelhelm Meru alisema ununuzi wa samani za ndani ya nyumba za waziri husimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa wizara zote na hununuliwa kila baada ya miaka mitano.

Hata hivyo, Dk Meru alitoa angalizo kuwa matumizi ya waziri husika huchangiwa pia na ukubwa wa wizara na kiwango cha bajeti.

“Mawaziri wengine wanaishi kwenye makazi yao na siyo wote wamepewa makazi ya Serikali.

“Lakini wanapewa huduma ya umeme, maji, posho ya majukumu na gari,” alisema Dk Meru.

Mashangingi

Mawaziri pia hupatiwa magari kwa ajili ya usafiri na mara nyingi huwa na ama Toyota Land Cruiser VX V8 au GX V8 ambayo hujulikana kama “mashangingi.”

Ili kufanikisha shughuli zao, kila waziri hupatiwa lita 1,000 kwa mwezi za mafuta. Kwa bei elekezi ya sasa ya Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (Ewura), iliyoanza kutumika Desemba 2, bei ya dizeli jijini Dar es Salaam ni Sh1,823 kwa lita.

Gari moja la waziri mmoja iwapo lingetumia lita zote 1,000 Serikali ilitakiwa kulipa Sh1.823 milioni ambazo kwa baraza zima ingekuwa jumla ya Sh100.3 milioni.

Pia, magari hayo huitaji kufanyiwa matengenezo kwa kila baada ya kilomita zinazoshauriwa na mtengenezaji.

Dk Meru alisema kwa kawaida kila gari hufanyiwa matengenezo baada ya kilomita 5,000 kwa kiasi cha wastani Sh1.8 milioni kila moja.

Kwa maana hiyo, katika Serikali ya “hapa kazi tu” inayohimiza viongozi wa kutoka maofisini kwenda kusikiliza shida za wananchi vijijini, hapana shaka kuwa mawaziri hao wangekuwa ama wameshatimiza kilomita zinazohitaji matengenezo au wanakaribia.

Serikali kufanikisha matengenezo hayo, ingeweza kulipa kampuni husika ya matengenezo Sh99 milioni kwa mwezi.

Gharama hizo ni mbali na fedha za kununua magari hayo ambayo kila moja linakadiriwa kugharimu Sh250 milioni, hivyo mawaziri 55 wangetafuna Sh13.75 bilioni.

Unafuu wa gharama katika eneo la ununuzi wa mashangingi hayo utakuwa dhahiri iwapo Rais Magufuli atatekeleza ahadi yake ya kuteua baraza dogo, mathalan, akiteua mawaziri 20 atakuwa ameokoa mashangi ya mawaziri 35, sawa na Sh8.75 bilioni.

Ukimya wa Rais Magufuli kutoteua Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha mwezi kumeibua mtizamo tofauti miongoni mwa wachambuzi wa masuala ya Siasa na utawala, wengi wakisema kuna faida nyingi kuliko hasara.



Mawaziri wa Jakaya Kikwete Hawajahama Nyumba za Serikali

$
0
0
Wakati Watanzania wakisubiri kufahamu sura zitakazoingia kwenye baraza jipya la mawaziri katika Serikali ya Rais John Magufuli, baadhi ya mawaziri wa awamu iliyopita ya Jakaya Kikwete hawajaziachia nyumba za Serikali walizokuwa wanaishi.

Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma, mawaziri wanastahili kuishi kwenye nyumba za Serikali kuanzia pale uteuzi wao unapotangazwa ili kuanza kutekeleza majukumu yao wakiwa katika mazingira salama, wao na familia zao. Haki hiyo hukoma mara moja; pale wanapovuliwa wadhifa huo au baraza husika linapovunjwa baada ya kukamilisha muhula wake au sababu nyingine yoyote.

Maandalizi ya Rais Magufuli katika uteuzi yanakwenda sambamba na taasisi zinazohusika kutekeleza wajibu wao wa kuandaa makazi ya wateule wanaotarajiwa, lakini zinakwamishwa na mawaziri ambao hawajahama.

“Tumepata fedha za kutosha kukarabati nyumba zenye uhitaji huo kutoka wizarani. Nyumba 15 zipo katika utekelezaji. Kuna baadhi tunasubiri waliomo wahame ili tuweze kuendelea,” alisema Mhandisi Edwin Nnunduma, kaimu mkurugenzi wa ushauri wa Wakala wa Nyumba za Serikali Tanzania (TBA).

Nnunduma alisema kila kitu kipo tayari na mapokezi ya viongozi hao hautacheleweshwa kwa namna yoyote ile kwa kuwa nyumba zipo za kutosha kuwahifadhi ili walitumikie Taifa kwa viwango vinavyohitajika.

Takwimu zinaonyesha kuwa wakala huyo anasimamia jumla ya nyumba 93 na kati ya hizo 29 zilikuwa zinakaliwa na mawaziri wa Serikali iliyopita ya Rais Jakaya Kikwete ambao, kwa mujibu wa kanuni walistahili kuziachia mara tu baada ya Rais Magufuli kuapishwa, Novemba 5.

Kwa mujibu wa Nnunduma, ukarabati huo unahusisha nyumba 35 ambazo zinajumuisha 29 za mawaziri na sita wanazoishi baadhi ya makatibu wakuu wa wizara.

Taarifa zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa wapo baadhi ya mawaziri ambao wamekaidi kuondoka kwenye nyumba hizo, licha ya kanuni na sheria kuwataka kufanya hivyo na agizo la Katibu Mkuu Kiongozi lilikwishatolewa likiwataka kurudisha magari na nyumba za Serikali.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mnunduma alisema, “Kuna waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi uliowataka wahame kwenye nyumba hizo ndani ya siku 30 baada ya kuapishwa kwa Rais mpya. Muda huo uliisha jana (juzi), naamini bado baadhi hawajahama mpaka sasa. Nilikuwa safarini hivyo sina uhakika ni nani na nani hawajafanya hivyo.”

Novemba 5, mara baada ya kuapishwa kwa Rais Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, aliwaagiza mawaziri na manaibu waziri kurudisha magari ya Serikali ikiwa ni siku yao ya ukomo wa uongozi. Katika agizo hilo, alisema baada ya bendera ya Rais anayemaliza muda wake kuteremshwa na kabla ya ile ya Rais mpya kupandishwa, magari hayo yanatakiwa yabadilishwe namba kwa kuondoa herufi ya cheo na kuwekwa zile za Serikali.

Wakati urejeshaji wa magari ulifanywa mara moja, uhamaji kwenye nyumba za Serikali ulipewa muda wa siku hizo 30, ili kutoa fursa kwa familia husika kuandaa mazingira hayo ikiwa ni pamoja na kusafirisha mali husika za viongozi hao na walio nao.

Kukawia huko kwa baadhi ya mawaziri kunaelezwa kuwa huenda kukawa na sababu mbili; ama uhakika wa kurudi kwenye baraza jipya au kutokana na ukosefu wa mahali pa kuhamia baada ya utumishi kukamilika na muda wa kutafuta mahali pengine penye hadhi sawa na yao kuwa changamoto.

“Wapo baadhi ya mawaziri ambao walichaguliwa siku za mwisho ambao kabla ya hapo walikuwa wanaishi majimboni kwao. Mwezi mmoja uliotolewa unaweza usitoshe kwa wao kutafuta nyumba nyingine hapa mjini itakayowafaa kulingana na mahitaji yao,” kilisema chanzo ambacho hakikutaka kutajwa.

Uchunguzi wa gazeti hili katika mitaa Mikocheni, Masaki na Kijitonyama ziliko nyumba za mawaziri ulibaini baadhi zikifanyiwa ukarabati na baadhi ya walinzi waliohojiwa wakibainisha kuwa mawaziri wengi walishaondoka katika makazi hayo.

Hata hivyo, ofisa wa TBA anayeshughulikia makazi ya mawaziri Kanda ya Masaki, Juma Hamis alisema mawaziri waliokuwa wamebakia kwenye eneo lake ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia.

“Kwa taarifa nilizonazo, hawa mawaziri wanahama leo (jana) kwani tayari wameanza kuhamisha baadhi ya vitu vyao,” alisema Juma.

Hata hivyo, Makamba alipoulizwa alisema hajawahi kuishi kwenye nyumba ya Serikali tangu aanze kuwatumikia wananchi kwa nafasi tofauti alizowahi kuzitumikia.

Alisema, “Siku zote naishi kwenye nyumba yangu. Tangu nilipokuwa ikulu na hata nilipoondoka na kuwa waziri.”     

After Lots of Rumors Finally Quick Racka Confirms Dating Kajala

$
0
0

There have been lots of speculations and rumors about Kajala dating Bongo Flava singer Quick Racka. Media did write about their secret relationship although they both denied it. Even Quick Racka had tattoo of Kajala's name. But speaking with Clouds fm Quick Racka was asked wheather he is still with Kajala or have already parted ways the singer replied they are still together ...

"Sometimes some things have to stay private because when love life get in public all the time rumors spread all the time too so sometimes it is better to be private but we are doing good...words on the streets are lots but we are the ones who know the truth" said Quick Racka

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Disemba 8, Ikiwemo ya Magufuli Kufuta Nyayo za Sitta na Mwakyembe


Salam za Rais Magufuli kwa Wananchi katika Kuadhimisha Miaka 54 ya Uhuru

$
0
0
Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyeiwezesha nchi yetu kutimiza miaka 54 ya uhuru kwa salama na amani. 

Namshukuru Mungu pia kwa kuniwezesha kuiona siku hii nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Napenda kuchukua fursa hii, kuwapongeza Watanzania wenzangu kwa Taifa letu kutimiza 54 ya Uhuru tarehe 09 Desemba, 2015.

Napenda kuwahakikishia kwamba, kama ilivyokuwa kwa Serikali za awamu zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano itafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha kwamba Uhuru, Amani na Umoja na wa Taifa letu hauchezewi na mtu, kikundi au Taifa lolote.

Tutaendelea kudumisha Uhuru wetu na Mapinduzi ya Zanzibar, tunu ambazo ni msingi wa Muungano wetu na Utanzania wetu.

Tofauti na ilivyozoeleka tumeamua mwaka huu kusherekea kumbukumbu hizi kwa kufanya kazi,. Wakati tunapata Uhuru Taifa letu lilikuwa likiongozwa na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI. 

Kauli hii ilikuwa na lengo la kuamusha moyo na uzalendo wa kufanya kazi miongoni mwa Watanzania kwa kutambua kuwa uhuru wetu hautakuwa na maana kama hatutafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kujenga Taifa linalojitegemea.

 Watanzania katika miaka ile waliitikia wito huo kwa kufanya kazi za kuwaongezea kipato na za kujitolea katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo.

 Katika miaka ya hivi karibuni moyo na uzalendo wa kufanya kazi miongoni mwetu umepungua sana. Kwa sababu hiyo, niliamua kutumia siku ya kumbukumbu za uhuru wetu mwaka huu kukumbushana na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya UHURU NA KAZI kwa kufanya kazi hususan ya usafi wa mazingira. Madhimisho ya Uhuru mwakani yatasherehekewa kama kawaida.

Nawapongeza viongozi wa Mikoa na Wilaya na wa Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyojitokeza katika kuhakikisha kuwa zoezi la usafi wa mazingira linafanikiwa.

Napenda kutoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaweka mifumo na taratibu thabiti zitakazowezesha usafi wa miji yetu kuwa endelevu. 

Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri waache visingizio, uwezo na mamlaka ya kuhakikisha kwamba usafi katika miji yao unadumishwa wanao. Uwezo wa utendaji wao utapimwa pia kutokana na hali ya usafi wa miji yao.

Naomba wananchi tushirikiane katika kuhakikisha kuwa nyumba na mazingira ya nyumba zetu yanakuwa safi na maji ya kunywa katika maeneo ambayo hayawekwi dawa yanachemshwa.

 Aidha, wananchi wajizuie kutupa taka ovyo na viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wahakikishe kwamba kila nyumba inakuwa na choo.

 Tutashinda vita dhidi ya maradhi kama kipindupindu ikiwa sote tutazingatia kanuni za afya. Kila mtu atimize wajibu wake.

Mwalimu alisema Uhuru na Kazi na mimi nasema Hapa Kazi Tu.

Mnyika Aibukia Sakata la Bandari, Asema Dawa ya Jipu Sio Kulitumbua

$
0
0
Baada ya kuwa kimya tangu ashinde Ubunge, Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika ameibukia kwenye sakata la ubadhirifu kwenye Mamlaka ya Bandari nchini na kuitaka serikali kuweka wazi ripoti za Dk. Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta.

Mnyika ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amedai kuwa ripoti za Sitta na Dk. Mwakyembe zimebeba ukweli zaidi kuhusu kinachoendelea bandarini hivyo kuziweka wazi kutasaidia kutibu tatizo lililopo zaidi ya kuwasimamisha watendaji waliotajwa.

Akiyafananisha matatizo ya bandari na majipu anayoyatumbua rais John Magufuli, alisema kuwa dawa yake ni kuyapasua ili kuondoa kiini badala ya kuyatumbua tu.
“Dawa ya jipu sio kulitumbua bali ni kulipasua ili kiini cha ndani kitoke, ukikiacha jipu linaazna upya tena linakuwa hatari zaidi,” alisema Mnyika.

“Kama kweli serikali ya awamu ya tano ina lengo la kufichua ufisadi, basi inapaswa kuweka wazi ripoti mbalimbali za uchunguzi ziwe dira ya kujua kiini cha matatizo kujitokeza katika Mamlaka ya Bandari,” aliongeza.

UKAWA Wajazana Kortini Kanda ya Ziwa Kutetea Nafasi zao za Ubunge..ya Ester Bulaya Nayo Ndani

$
0
0
KESI za kupinga matokeo ya ubunge zimezidi kumiminika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ikiwamo za kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya (Chadema). 

Kesi nyingine zilizofunguliwa mahakamani ni za majimbo ya Nyamagana, Ilemela na jimbo la Kwimba, ambapo walalamikaji wamewasilisha malalamiko mbali mbali ikiwamo ya vitendo vya rushwa.

Kesi ya kwanza iliyofunguliwa ni ya ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini ambayo imefunguliwa na Magambo Masato na wenzake watatu wakipinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2015 mara ya kwanza ilifunguliwa Novemba 18 mwaka huu, juzi ilikuwa mara ya kwanza kupelekwa mahakamani kwa ajili ya kutajwa.

Kesi hiyo ambayo ipo kwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe, walalamikaji wa kesi hiyo wamewasilisha malalamiko mahakamani hapo wakidai kwamba Bulaya alipata ushindi kwa njia ya rushwa.

Bulaya aweka pingamizi
Mlalamikiwa katika kesi hiyo, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya, mapema juzi aliwasilisha hoja za msingi kuweka pingamizi kwa walalamikaji kufungua kesi mahakamani.

Hoja alizowasilisha Bulaya ni kwamba walalamikaji hawana mamlaka ya kufungua na kuendesha kesi ya aina hiyo kwani hawajaonesha ni namna gani imeathiri haki zao kama wapiga kura.

Pili katika shauli walillowasilisha mahakamani hawakuonesha ni namna gani vitendo vya rushwa walivyodai vilikuwa vikifanywa na Mawakala wa Bulaya havijaoneshwa, pia shauri hilo limekiuka kifungu cha 12 (D) cha sheria ya uchaguzi.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 29 mwaka huu, itakapo tajwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya kuisikiliza.

Kesi ya Wenje
Aliyekuwa Mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiah Wenje, juzi alitinga Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, kuomba kupunguziwa gharama za uendeshwaji wa kesi.

Pia Wenje katika kesi hiyo anawashitaki, Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM), Msimamizi wa Uchaguzi huo, Tito Mahinya na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo amewasilisha malalamiko mahakamani hapo kwamba uchaguzi huo haukuwa haki na huru, kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Hata hivyo katika kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2015, Wenje aliwakilishwa mahakamani hapo na Wakili Outa na upande wa walalamikiwa waliwakilishwa na Wanasheria wa Serikali, Mtalemwa, Kitia Tuloke na Ajuaye Bilishaga.

Kesi ya Highness Kiwia
Novemba 25 mwaka huu aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ilemela, Highness Kiwia, alifungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi, Angelina Mabula (CCM) pamoja na kuwashitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi huo, John Wanga.

Kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, mlalamikaji katika kesi Kiwia hakufika mahakamani hapo, ambapo kwa upande wa walalamikiwa waliwakilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Malongo.

Kesi ya Wenje na Kiwia zimeahirishwa ampapo ya Wenje itatajwa Desemba 10 mwaka huu na ya Kiwia hadi Desemba 14 mwaka huu, huku Msajili, Kabwe amedai kuwa endapo siku hiyo mlalamikaji Kiwia hatatokea kesi itatupiliwa mbali.

Shirika la Umeme nchini, Tanesco limebaini wizi wa umeme nyumbani kwa Wema Sepetu

$
0
0
Shirika la Umeme nchini, Tanesco limebaini wizi wa umeme nyumbani kwa Wema Sepetu.

Mafundi wa shirika hilo waliambatana na waandishi wa habari hadi kwenye nyumba hiyo na kubaini kuwa umeme unaingia moja kwa moja kwenye nyumba bila kupita kwenye mita.

Wakati mafundi hao wameingia nyumba hiyo walimkuta Idris Sultan ndani aliyejaribu kuwasihi wasiukate umeme.


Kukutwa kwa Idris kwenye nyumba hiyo kumetia mafuta zaidi tetesi za kuwa wawili hao wana uhusiano.



Tazama Video Hapa Chini

Ufisadi Bandari na Mabehewa, Kamati Kuu ya CCM yawakingia Kifua Sitta na Mwakyembe

$
0
0
Katika hali inayoashiria kuwa CCM haijajifunza somo kuwa wananchi wamekerwa na ufisadi.
CCM inataka kuwafanya wananchi wakose matumaini kwa serikali yao, na hivyo kupelekea kuona kuwa juhudi za Raisi Magufuli ni hatua za kuwabana dagaa huku wakiyaachia mapapa yakitanua mtaani.

Hatua hiyo ya kamati kuu ni hatua ya hatari sana kwa sababu inaweka maslahi ya watu wachache mbele kuliko Taifa, Hili ni jambo la kutisha na kuogofya sana, kama chama kilichojinadi kurudi katika misingi kinawalinda watu ambao Kwa kutumia nyadhifa zao wameifikisha nchi katika hali mbaya,basi ni jambo la kuwakatisha tamaa na kuwanyong'onyesha wananchi walioanza kurejesha imani kwa serikali yao.


DKT Harrison Mwakyembe na Samwel Sitta ambao walikuwa mawaziri wandamizi kwenye Serikali ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao kwa sasa wanatuhumiwa kwenye Kashfa za ufisadi, imefichukua kuwa uwezekano wa kupandishwa mahakamani watu hao umeyeyuka. Mtandao umedokezwa,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.


Sababu iliyotajwa ya kuwaokoa mawaziri hao imetokana na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM,CC kilichoketi jana kimekuja na mipango mahususi ya kuwaokoa viongozi hao wanajiita na kuitwa ni waadilifu.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Kikao hicho ambazo zimevuja zinasema Kamati ya CC licha ya kujadili mambo mbali mbali ila jambo la ufisadi ambao uliibuliwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Kashfa ya ununuzi wa mabehewa 250 ya mizigo pamoja na Mabehewa 50 ya kubebea mafuta ambayo yamebainika kwa sasa ni mabovu nalo lilizungumziwa.

Chanzo chetu hicho kilichokuwa ndani ya CC kimedai kuwa viongozi wa mkutano huo walitaka suala la kuwachukulia hatua mawaziri hao waliokushika nafasi ya wizara ya uchukuzi,litazamwe kwa umakini kwani linaweza kukiingiza chama hicho tena kwenye mgogoro.

Yaani CC wameona hawa wakina mwakyembe na Sitta wakipandisha Mahakamani kujibu tuhuma hizo,basi chama chetu kitaingia kwenye mgogoro ambao unaweza hata ukapelekea idara hata ya Ikulu ya kipindi kile kufika mahakamani maana ufisadi huu wa Mabehewa ni mkubwa sana na umefanywa na mtandao mkubwa ndani ya nchi kimesema Chanzo chetu hicho.

Hata hivyo Kamati hiyo ya CC licha ya kuwakingia kifua mawaziri hao kunakuja ni ikiwa ni siku moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvunja Bodi ya Bandari ambayo Samwel Sitta wakati yupo Uchukuzi aliiunda Bodi ambayo Magufuli ameivunja kutokana na kuhusika kwenye ufisadi,

Hatua nyingine kwa bandari hiyo ni Rais Magufuli kutengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Bandari Awadh Massawe baada ya kubainika pia ameshindwa kuisimamia Bandari hiyo kwa kupelekea Ufisadi wa kutisha ikiwemo upotevu wa Kontena zaidi ya 2000.

Sanjaria Bandarini hapo Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi,Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi Shaaban Mwinjaka kutokana na kuitia hasara serikali ya bilioni 16 kwenye sherika la Reli ya Kati TRL.
Taarifa zilizopatikana wiki iliyopita zilisema Rais Magufuli alikuwa tayari amekabidhiwa ripoti ya Ufisadi wa Bandarini na TRL ambao unatajwa kuwa kwa namna yoyote uwezi ukawaacha mawaziri wenye dhamana ya Uchukuzi,


Hata ufanyaje ndugu,kwenye ufisadi wa huu wa kutisha lazima Sitta na Mwakyembe watawabwa Msalabani tu, maana wakati makontena hayo yanapoteka kati ya 2014 na 2015 mawaziri hawa walikuwepo uchukuzi hivi hawakuyaona haya au nao kuhusika katika kubariki wizi huu,harafu ukitoka kwenye Bandari unakuja kwenye TRL hapa ndio kuna madudu ambayo yanawaacha watupu,wanaojiita wapiganaji wa ufisadi amesema Mchambuzi wa Siasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma ,John Shilima.

Raisi wa Awamu ya 4 Mh Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete Waingia Mtaani Kumuunga Mkono John Magufuli

$
0
0
Raisi wa Awamu ya 4 Mh Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete nao wapo kwenye maeneo yao hivi sasa wanafanya Usafi. #UhuruWaUsafi #UsafiDay

Raisi John Pombe Magufuli Ajitokeza Barabarani Kufanya Usafi na Wananchi....

$
0
0

Raisi John Pombe Magufuli nae amejitokeza barabarani maeneo karibu na Ikulu kuungana na Wananchi kufanya Usafi. Tuamkeni wote kwa pamoja tusafishe maeneo yetu yatutunze. #UhuruWaUsafi #UsafiDay

Kwakweli Kuitawala Tanzania ni Kazi Nyepesi Sana..Anachokifanya Magufuli Kwa Sasa ni Hichi

$
0
0
Wahenga walisema adui muombee njaa, lakini la pili na lipenda sana kuliko la kwanza " ukitaka kumtawala mwanadamu siku zote mnyime elimu bora"

Katika miaka hii ya 2015-2020 ndo miaka ambayo Tanzania ilipaswa kuionyesha dunia kwamba, inajitambua na inajielewa na imechoka kuendeshwa kwa matukio inataka mabadiliko ya kiuchumi na kimfumo. 

Hasa tujirejea 2005 na mwanzoni kwa miaka ya 2006 ambapo kwa kile kilichoitwa kasi ya viwango! kuna watu walikimbia mahoteli yao na mabiashara makubwa wakihofia kuingia mikononi mwa Serikali ya ari mpya nguvu mpya na kasi mpya! Vikao vilikua haviishi ngurudoto vamia vamia maofisini zilikua ni tabu, lakini saivi Raisi huyohuyo kuna watu wanaomba anyang'anywe hati yake ya kusafiria! Amazing!

Magufuli tangu ameanza kazi Ana mwezi na siku kadhaa sasa, na kazi yake tunaiona tumeona hata waziri mkuu akitembea na vinondo alivyopewa na wafanyakazi wema wa bandari na TRA na yeye kuvamia hayo maeneo na kuwachukulia hatua mara moja wahusika walioorodheshwa kwenye nondo zake! Well and good.. 

Ninachojiuliza ni Waziri gani wa nchi hii au naibu wake (waliopita) katika secta yoyote kati ya zilizoonyesha ubadhilifu mkubwa ambaye hata kuitwa kutolea ufafanuzi wa kinachoendea ameitwa? Lakini mtanzania huyuhuyu aliyeongozwa kwa style hizihizi zaidi ya miaka 54 sasa amevurugwa kabisa kana kwamba kinachofanyika sasa sio wajibu wa kiongozi na anapokea mshahara wake!

Nini madhara ya sifa hizi ambazo mimi nikiangalia huko dodoma watoto zaidi ya 50% wanazaliwa na mtindio wa ubongo sijaona mikakati ya kiubunifu ya kuliokoa taifa, Zanzbar saivi utadhani sio sehemu ya muungano na huyuhuyu mpewa sifa tangu akae Magogoni hakawahi hata kutoa kauli! Madhara ya sifa ni kwamba mwanadamu mwenye uwezo wa kucheza na akili za watu ambao wengi tumenyimwa elimu bora, ataona adhma yake imetimia na sasa ananafasi kwenye nafsi hizi zilizopoteza mwelekeo, ataendelea na style hiyohiyo huku akifukia mambo ya msingi yanayo muhusu mtu katika maisha ya kila siku! Na mara nyingi style za namna hii hufanywa na watu ambao wana "lack of creativity"

Huko mbeya kuna watu bado wanapenda kujifungulia Zambia kwasababu ya ubovu wa Hospitali za taifa so shame!

Kila kukicha thamani ya shilingi inazidi kuporomoka na bidhaa zinapanda bei Magufuli alivyoingia Ikulu sado ya viazi ilikua 3500 saivi 5000 sioni mkakati wa kuliokoa taifa na huu mfumko wa bei ukiuliza utaambiwa bado mapema tunasahau kwamba, wafanyabiashara ni wajanja bei ikishazoeleka wanaifanya ya kudumu,

Hadi saivi anachokifanya Magufuli, Majaliwa na Sef ni kuikosoa serikali iliyopita hakuna hata kimoja cha kwao walichokifanya taifa kuwa mahala salama pa kuishi,

Hapa juzi tu tuliambiwa serikali inatoa ada elekezi kwa shule binafsi hii inaleta picha gani? Hii ni tafsiri kwamba hakuna ubunifu wowote wala maono yoyote ya mzazi juu ya namna gani ya kuifanya elimu ya Tz kuwa bora hasa kupitia shule za umma! Japo tena hao hao wamekanusha kuingilia shule binafsi! "Contradiction"

Kuna watu nikiandika post zangu badala ya kufikiri kwa kina wanakimbilia kusema nimetumwa! Shauri yenu ujinga mwingine huo, na kwa taarifa yenu mi ni mtanzania huru kabisa ninaye waza tu hatima ya nchi yangu

Hii nchi inasafari ndefu sana kwa watu makini kuanza kumsifia mwanadamu yeyote! Tusichokijua tz ni kwamba, wanasiasa ni werevu sana hutafuta jambo ambalo anajua akilifanya watu wanaowaza kirahisi rahisi atakua ameteka akili zao na kufukia hata yale ambayo ni mahitaji yao ya msingi bila wao kujua "Dont play with Politicians they know how to play with your minds"

By H.T.P-Jamii Forums

CUF wazungumzia taarifa za kufariki Maalim Seif, watoa msimamo wao kuhusu Uchaguzi Zanzibar

$
0
0
Chama cha Wananchi (CUF) kimekanusha vikali taarifa zilizosambazwa na watu ambao hawajajulikana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki.

Akiongea na ITV, Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano na Umma wa chama hicho, Ismail Jusa amesema kuwa taarifa hizo zina lengo la kuvuruga amani na usalama wa nchi kwa kutengeneza taharuki.

Jusa ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki kwa waliopika na kusambaza habari hizo kwa kuwa mbali na kuwa kiongozi wa chama na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif ni Kiongozi wa ngazi za juu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar..

“Yeyote aliyekuwa nyuma ya kusambaza uvumi huu hakuwa na nia njema. Na utaona kama ina malengo ya kisiasa kwa sababu taarifa yenyewe imehusishwa kwamba eti tukio hilo limetokea baada ya kujaribu kuwashawishi wajumbe wa vikao vyake vya CUF eti wasaini waraka wa kutaka uchaguzi urudiwe, jambo ambalo halipo,” alisema Jusa.

Taarifa hizo za kugushi zilizosambaa ziliwekewa nembo ya mtandao wa Facebook wa ITV, hali iliyokilazimu kituo cha ITV kukanusha vikali kuhusika na taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Jusa alieleza kuwa msimamo wa CUF kuhusu uchaguzi wa Zanzibar uko wazi kuwa hakuna kurudia uchaguzi na kwamba mshindi ambaye wanaamini ni Maalim Seif atangazwe

Nafasi za Kazi
Bonyeza www.ajirayako.com

Tuhuma za Matumizi mabaya ya Ofisi: BAKWATA yamsimamisha kazi Mkurugenzi wa Utawala

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuhu
Baada ya kumshukuru Mwenye ezi Mungu na Kumtakia rehma na amani kiongozi wetu Bwana Mtume Muhammad S.A.W.

Tunapenda kuwafahamisha ya kwamba baada ya siku chache tutakuwa tumeingia katika Mwezi wa mfungo sita.
Na huu ndio Mwezi aliozaliwa Bwana Mtume S.A.W. kwa mujibu wa kalenda ya kiislamu.

Waislamu wote ulimwenguni unapofika mwezi wa mfungo sita husherehekea juu ya mazazi ya Bwana Mtume S.A.W.

Baraza kuu la Waislamu wa Tanzania linapenda kuwafahamisha juu ya utaratibu wa matukio tuliyoyapanga katika kipindi hiki cha mwezi wa kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W.

Katika wiki ya kwanza ya mwezi huu wa mfungo sita kutakuwa na wiki ya misikiti ndani ya wiki hii waislamu watatakiwa kuongeza nguvu zaidi katika majukumu yao ya kila siku ya kuhakikisha kuwa mazingira yao yote yanakuwa katika usafi wa hali ya juu kama ilivyo kawaida.

Vilevile katika mwezi mzima kutakuwa na mihadhara mbalimbali misikitini, kwenye redio, magazetini pamoja na televisheni masheikh mbali mbali watashiriki katika mihadhara hii.

Aidha, natoa wito kwa Masheikh na Maimamu nchi nzima kutumia kipindi hiki cha Shahru Milaad (Mwezi wa Mazazi ya Mtume S.AW), kumuelezea Mtume (S.a.w) kwa kina katika Nyanja mbalimbali kama vile elimu, siasa, uchumi, uongozi, utawala bora na kadhalika.

Pia napenda kuwafahamisha ya kuwa nimeunda timu maalum ambayo nimeipa majukumu ya kufanya maboresho ndani ya BAKWATA.

Timu hii nimeipa pia majukumu ya kupitia mikataba yote ya BAKWATA ili kuweza kuangalia ile mikataba mibovu na kuona namna ya kufanya ili BAKWATA iweze kuwa na mikataba yenye maslahi na Bakwata kwa niaba ya Waislamu.
Aidha timu hii nimeipa majukumu ya kukagua hesabu za BAKWATA kuanzia ngazi ya Makao Makuu na nchi nzima.

Mwisho, kwa mamlaka niliyonayo, nimemsimamisha kazi Karim Majaliwa - Mkurugenzi wa Utawala wa BAKWATA Makao Makuu, kwa ajili ya kupisha uchunguzi juu ya kadhia ya magari 82, pamoja na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.

Wabillahi Tawfiiq.
Sheikh Abu bakari Zuberi
Mufti wa Tanzania
05/12/2015

Rais Magufuli Atoa Namba yake Ya Simu Kwa Wavuvi.....Awaahidi Mambo Matatu.

$
0
0
Rais John Magufuli leo ameungana na wananchi katika kufanya usafi ambapo akiwa katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam, ameweza kuzungumza moja kwa moja na wavuvi wadogo.

Baada ya kusikiliza kwa makini kero zinazowakabili wavuvi hao wadogo akiwa amekaa ndani ya kifaa duni cha kufanyia uvuvi maarufu kama ‘mtumbwi’ usio na mashine, rais Magufuli aliwaahidi wavuvi hao kuzitatua kero hizo.

Kati ya mambo matatu aliyoahidi kuyafanyia kazi kwa haraka ni pamoja na kuondoa masharti kuwa kuwa na ‘Fire Extinguisher’ ambapo alieleza kuwa sharti hilo halina mashiko kwa wavuvi hao wadogo wasio na mashine.

“Kwanza maji yenyewe tu ni ‘fire extinguisher’, si moto ukianza unaingia ndani ya maji,” alisema Dk. Magufuli.

Kadhalika, rais aliahidi kuwasaidia wavuvi hao kwa masharti ya kuunda umoja wao ambao utakuwa na viongozi waadilifu wanaofanya kazi kwa maslahi ya wavuvi hao na sio maslahi ya ‘wakubwa’. Alieleza kuwa atalifanyia kazi suala la wavuvi hao kukopesheka na kuwasaidia kuwa na vifaa bora.

Aliongeza kuwa atahakikisha anafuta ushuru kwa wavuvi hao wadogo ili kuwaondolea kero na mzigo wa gharama.

Pia, alisema atahakikisha anaanza kuwasaidia kadiri awezavyo wavuvi wa eneo la Feri kwa kuwa ni majirani zake.
“Katika kudhihirisha ujirani mwema, hayo matatizo nitayabeba.”

Hata hivyo, rais aliwataka wavuvi hao kuhakikisha hawajihusishi na uvuvi haramu wa kutumia sumu na mabomu.

Katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, rais Magufuli alimpa mmoja kati ya wawakilishi wa wavuvi hao namba yake ya simu na yeye akachukua namba ya watu wawili kati yao.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo, Dk. Magufuli aliwashukuru watanzania wote kwa ujumla kwa kuitikia wito wake wa kufanya usafi huku akieleza kuwa hili linapaswa kuwa zoezi endelevu kwani uchafu hauwezi kuisha kwa kufanya usafi mara moja kwa mwaka.

Nafasi za Kazi
Bonyeza www.ajirayako.com

TRA Yagomea Wamiliki wa Makontena Yaliyotoroshwa Bandarini Kusamehewa Adhabu

$
0
0
Mmamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewagomea kulipa kodi bila adhabu baadhi ya wamiliki wa makontena, ambayo yalitoroshwa kwenye bandari kavu bila kulipiwa kodi. 

Badala yake, TRA imewapelekea hati ya malipo inayowataka wafanyabiashara hao, kuhakikisha wanalipa kodi hiyo na adhabu ndani ya siku saba, la sivyo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wamiliki wa makontena hayo, kuiomba TRA kuwasamehe kulipa adhabu waliyopewa badala yake waruhusiwe tu kulipa kodi stahiki ya Serikali. 

Jumla ya makontena 349 yalitoroshwa katika bandari kavu bila kulipa kodi na kuikosesha Seri kali mapato ya Sh bilioni 80.

Wafanyabiashara hao, pia wameomba waruhusiwe kulipa kodi wanayotakiwa kulipa kidogo kidogo kwa madai kuwa wengine hawana uwezo wa kulipa kiasi hicho cha fedha kutokana na kutapeliwa na mawakala wao waliowatumia kwenda kulipa kodi hiyo.

Wakizungumza na mwandishi, baadhi ya wafanyabiashara hao walisema agizo la Dk Magufuli alilotoa Desemba 3, mwaka huu kuwa linawataka walipe kodi hiyo ndani ya siku saba.

Lakini wafanyabiashara walisema nyaraka za malipo walizopelekewa na TRA, zimewataka kulipa kodi na faini kwa pamoja wakati hizo siku saba alizotoa Dk Magufuli hazijamalizika. 

Wafanyabiashara hao wanadai kuwa walishalipa kodi hiyo kupitia kwa wakala wao, kama taratibu za TRA zinavyowataka kuwatumia mawakala wa bandarini kulipa kodi, lakini kwa bahati mbaya wakala huyo hakufikisha kodi hiyo serikalini.

Walidai kuwa walifuatilia nyaraka za kodi kwa wakala wetu, lakini akawa anawaambia wasubiri. 

“Tunaomba hii adhabu tusamehewe, kwani sio kosa letu ila tuko tayari kulipa kodi halali ya Serikali, lakini wakala wetu ndiye katuingiza kwenye matatizo haya na yeye tayari ameshatoroka,” aliongeza mfanyabiashara huyo.

Katika nyaraka za kodi ambazo TRA imewapelekea, kontena moja linatakiwa kulipiwa ushuru wa Sh milioni 40.5 ndani ya siku saba na adhabu ya Sh milioni 28.3. Hivyo jumla wanatakiwa kulipa Sh milioni 68.8 kama ushuru na adhabu.

Akizungumza na mwandishi kuhusu madai hayo ya wafanyabiashara, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema adhabu walizoandikiwa wafanyabiashara hizo, wanatakiwa kuzilipa pamoja na kodi stahiki ndani ya siku saba.

Alisema wamewawekea adhabu hiyo kutokana na kitendo chao cha kuiibia Serikali na kwa taratibu za nchi, walitakiwa wawe mahabusu sasa hivi, lakini wametakiwa kulipa ushuru wa Serikali wakati wakiwa nje; hivyo wanastahili kulipa kiasi hicho cha fedha kama adhabu ya kukwepa kodi.

“Hawa walitakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani, walitoa kontena nje ya utaratibu, adhabu hiyo ni ya kutoa makontena bila kulipa kodi,” alisema Kayombo. “Wakishindwa kulipa ndani ya muda huo tutawakamata tena na kuwafikisha mahakamani,” alieleza.

Kayombo alifafanua kuwa siku saba hizo walizopewa wafanyabiashara hao ni kusamehewa kutoshitakiwa mahakamani na sio kusamehewa kulipa adhabu wakati tayari walishakiuka taratibu.

Alisema wafanyabiashara hao, wachague kulipa ndani ya siku saba wasishitakiwe au waache ili wakutane na rungu la dola la kufikishwa mahakamani. 

Alisema hadi sasa TRA imeshakusanya Sh bilioni 9.4 kati ya Sh bilioni 80 zinazotakiwa kulipwa kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara hao waliokwepa kodi.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images