Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Majina Kamili ya Wabunge Walioingia Kwenye Baraza Jipya la Rais Magufuli Mpaka Sasa


Kikwete Ajibu Tuhuma Za Kulea Ufisadi Bandarini.......Aitetea Familia Yake, Awapiga Kijembe UKAWA

$
0
0
RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema katika uongozi wake wa miaka 10, hakuwahi kuagiza mtu asamehewe kontena lake lisilipe kodi na angefanya hivyo, mapato ya Serikali yasingeongezeka kutoka Sh bilioni 177 kwa mwezi mpaka Sh bilioni 900.

Akizungumza baada ya kuwashitukiza wananchi wa Chalinze katika soko kuu la eneo hilo kwa kuungana nao kufanya usafi kuitikia agizo la Rais John Magufuli jana asubuhi, Kikwete alisema katika uongozi wake hakuwahi kuagiza mtu anayestahili kulipa kodi asilipe kodi.

Alisema wakati huu ambao amepumzika baada ya kustaafu, amepata nafasi ya kusoma mitandao na magazeti mbalimbali na kukuta baadhi ya watu, wakimshutumu na kumtukana yeye na familia yake wakimhusisha na ukwepaji kodi.

“Ni afadhali wanishambulie mimi ila wamuache Rais Magufuli (John Pombe) afanye kazi, ni maneno ya walioshindwa wasinilaumu, aliyewashinda ni Magufuli sasa hawana la kusema. Ni sawa na siasa za maji taka, lakini watakuwa wanapoteza muda wao na kufanya kazi bure, kwa kuwa mimi sigombei kitu chochote tena.

“Wanahusisha mpaka na familia yangu, kama mimi mwenyewe sijawahi kuruhusu mtu hata mmoja atoe kontena bila kulipia kodi, siamini kama mke wangu (Mama Salma) au mwanangu Ridhiwani (Mbunge wa Chalinze), wangeweza kufanya hivyo tu na watu wakawasikiliza.

“Wanachonga tu, wengine wamesema Kikwete hachomoki, kwani nimechomeka nini?” Alihoji na kusababisha watu walioshirikiana naye kufanya usafi katika soko hilo kucheka na kuanza kushangilia.

Alisema nafasi ya urais aliyoaminiwa na Watanzania kwa miaka 10, ilikuwa yake na haikuwa na ubia na mkewe wala mtu mwingine yeyote.

Kikwete aliwataka Watanzania wamuunge mkono Rais Magufuli katika jitihada anazofanya za kukabiliana na wakwepa kodi, huku akitoa mfano akisema wakwepa kodi kwa Serikali ni kama inzi na kidonda, hawaondoki bila kufukuzwa na ukiacha kuwafukuza wanarudi.

“Serikali ina wajibu kwa wananchi, wanataka barabara, shule, hospitali ziwe na dawa na mengine mengi, lakini haya yote yanahitaji fedha na Serikali inapata fedha kutoka katika vyanzo vya kodi,” alisema.

Alisema pia yapo mapato mengine ikiwemo ushuru mbalimbali kama katika kulipia leseni, hati za kusafiria na nyingine, lakini pia Serikali inaweza kuchukua mikopo na misaada.

Kikwete alisisitiza kuwa wakati wa uongozi wake, kazi hiyo ya kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ilifanyika, ndio maana alifanikiwa kuongeza makusanyo ya kodi kutoka Sh bilioni 177 kwa mwezi mpaka Sh bilioni 900.

Pamoja na mafanikio hayo ya uongozi wake, Kikwete alisema bado mahitaji ya Serikali kwa watu wake, yameendelea kuwa makubwa kuliko upatikanaji wa mapato.

“Tunapaswa kuendelea kuboresha mifumo ya kodi, taasisi za mapato na kupata watendaji waadilifu, kwa kuwa kama mifumo na taasisi vikiwa imara, lakini watendaji si waaminifu haisaidii.

Alisema kazi hiyo anayofanya Dk Magufuli ni kubwa kwa kuwa inahusisha kunyang’anya tonge watu na kusisistiza namna bora ya kumuunga mkono ni kulipa kodi na wakusanyaji wa mapato ya Serikali wawe waaminifu.

Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, alisema hata katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho walichokaa juzi, waliamua kumuunga mkono Rais Magufuli na kuwataka wanachama wote wa chama hicho kufanya hivyo.

“Ni pale tu mapato yatakapoongezeka, ndipo wajibu wa Serikali katika kuhudumia wananchi utawezekana, tukimuunga mkono Rais wetu mzuri ataweza na mapato yakiongezeka, maji yatapatikana, mapato yakiongezeka, zahanati na hospitali zetu zitapata dawa za kutosha, mapato yakiongezeka barabara za lami zitajengwa,” alisisitiza.

Alisema katika Serikali Kuu, makusanyo yako nyuma ya asilimia 10 ya lengo, lakini kwa juhudi za Rais Magufuli, hali inavyokwenda lengo hilo litapitwa na Serikali itaanza kuzungumzia makusanyo ya matrilioni kwa mwezi.

Hata hivyo, alisema juhudi hizo za Serikali Kuu hazionekani katika halmashauri ambako ni kama hakuna kazi inayofanyika na hata pale kunapokuwa na juhudi za kukusanya mapato, wakati mwingine yanaishia mikononi mwa wajanja.

Kikwete ambaye alifanya usafi katika soko ikiwemo kufagia, kukusanya na kuzoa taka akiwa na mkewe, huku akikataa kuvaa vifaa vya kuzuia vumbi, aliwataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi.

Alisema uamuzi wa Rais Magufuli wa kutumia maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru, kuwataka wananchi wote wafanye usafi, ni wa busara na si wa kukurupuka kwa kuwa mwaka huu taifa lilikabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu.

Breaking News: Rais Magufuli Atangaza Baraza Lake la Mawaziri

$
0
0
Ndugu waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla, ninawasalimu sana. Nawakaribisha katika kikao hiki cha kutangaza baraza la mawaziri.

Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama.

Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.

Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma naiunganisha na Utawala bora hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo;

1.Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.

Mawaziri - George Simbachakene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo
2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri : Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

6.Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri: Bado hajapatikana.
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

7.Wizara ya Nishati na Madini
Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

8.Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri - Harrison Mwakyembe

9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

11. Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri - Charles Kitwanga.

12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula

13. Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri: Bado hajapatikana.
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

14: Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri: Charles Mwijage.

15: Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri: Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

16: Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalim
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala

17: Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

18:Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

Lowassa Afunguka....Magufuli Anatekeleza Hoja Zangu na Chadema

$
0
0
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli imeanza kuzifanyia kazi hoja zake alizozieleza wakati wa uchaguzi.

Lowassa aliyasema hayo jana jijini Arusha alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni.

Lowassa aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kumuachia huru Sheikh Issa Ponda na kuiomba kuliangalia pia suala la mwanamuziki, Nguza Vicky (Babu Saye) na mwanae.

“Haya mambo ndiyo tuliyoyaema wakati wa kampeni, sasa namuona Magufuli ameanza kuyatekeleza. Sasa nawaomba angalau wawe wanasema hizo ni sera za Lowassa na Chadema na wanapozitumia basi wawe wanatushukuru,” alisema Lowassa.

Kauli hiyo ya Lowassa iliungwa mkono na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye aliwataka pia wananchi wa jimbo hilo kumchagua Lema ili aende bungeni akatumbue majipu ambayo yanapeleka damu kwenye mishipa ya moyo, majipu ambayo alidai CCM haiwezi kuyatumbua.

Nina Hakika Hili Baraza Halikuwa Chaguo la Mheshimiwa John Pombe Magufuli

$
0
0
Kwa kweli imenishangaza sana. Ikiwa mkuu wetu ni msafi imekuwaje akarudisha baadhi ya watu waliotutia hasara kubwa na hata ikapelekea kujiuzulu baada ya kelele za wananchi kuwa kubwa.

Tena kuna wengine wana dharau sana kwa wananchi pia nimewaona. 

Kwa kweli bado sijaamini. Inaonekana kuna shinikizo, but, tusubiri!!

Source: Jamii Forums

Mtandao Umekufa Rasmi, Kazi Sasa ni Kusafisha Matokeo yake....

$
0
0
Kwa wafuatiliaji wa kisiasa mtakumbuka jinsi mtandao ulioundwa na Kikwete na Lowasa ulivyotikisa siasa za Tanzania toka miaka ya 1990's.
Hatimaye mtandao huu ulifanikiwa kuingia madarakani mwaka 2005 na wakuu wa mtandao huo wakagawana vyeo kama ile waingereza wanaita "spoils of war" , yaani matunda ya kugawana madaraka yaliyotekwa.

Wakati zkikwete aliwasogeza ndugu jamaa na marafiki zake madarakani, Lowasa kwa gia kubwa aliingiza kina Ole wengi kwenye utawala wa mikoa na mashirika ya umma.

Lakini utawala wa tamaa tu na si kutumikia wananchi ulianza kuleta matokeo yasiyo tarajiwa.
Chama CCM kikakosa malengo baada ya vichwa kama Mangula kutimuliwa au kuondoka.
Mawaziri wakawa wengi na walikuwa wanabadilishwa kama circus.
Na kwa vile tamaa haikuishia kutawala tu kwa wana mtandao, tofauti kubwa, na zinazotokana na tamaa ziliibuka kati ya waasisi wa mtandao, yaani Kikwete na Lowassa.

Tofauti hizo na hatimaye ugomvi uliokuwa ukiendeshwa kama gemu la chess, uliishia kuwamaliza wote wawili katika kimsimamo wa kuuendeleza mtandao.

Watanzania lazima tumshukuru Mungu, kwamba ni tamaa ya madaraka na mali ndio imewamaliza wana mtandao.

Magufuli amefanya vema kwa kuanza kuibua madudu ya kutisha ya uongozi ambao ulikuwa hautawali bali unajinufaisha na utendaji wa serikali.

Ni vema utafiti wa kina ujafanywa na wataalam wa sayansi ya jamii , na katika kipindi kifupi, ili madhara mahsusi yatambuliwe, na hatua za kurekebisha zichukuliwe.

Kitu kinachoonekana dhahiri ni kuubinafsisha ukusanyaji wa kodi, na kodi hizo kuingia mifukoni mwa watu binafsi badala ya serikali ili kutumikia wananchi.

Source:JF

Raisi wa Tanzania Anaongozwa Kwa Kupendwa Africa

$
0
0
Imethibitika katika uchunguzi uliofanya na taasisi moja inayojiushisha na tafiti mbalimbali imebainika kuwa rais wa Tanzania Mr. John Magufuli anaongoza katika bara la Afrika kuwa ni rais anaepedwa sana na raia wake kuliko rais yoyote barani humu.

Inasemekana rais huyu anakadiliwa na zaidi ya watu milion 35 ndani ya nchi yake pekee wanampenda toka moyoni kabisa , pia zaidi ya watu milion 4 mpaka 6 katika katika nchi za Kenya , na Uganda.

Pia imejumuisha na wale waishio nje ya bara hili, rais wa pili ni rais mpya wa Nigeria , Kagame kashika nafasi ya 3 akifatiwa na Zuma

Rais Magufuli Atoa Kauli Nzito Kwa Mawaziri Aliowateuwa leo..

$
0
0

Wakienda kule mawaziri wakafanye kazi kweli ndio maana sisi tulipochaguliwa tulifanya kazie kweli na hatukwenda kwenye semina elekezi na tulijielekeza, wakajieleze kwenye maeneo yao.
Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu na kama wapo wanaopenda kufanya sherehe wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa, contract ni miaka mitano. Wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua, Baraza hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi tunayowatarajia kuifanya effectivly. Ngoja tukimaliza uteuzi wote tutajua tumesave kiasi gani ili ziweze kwenda kwa wananchi.

KAULI ya Kwanza ya Mwigulu Nchemba Baada ya Kuteuliwa Kuwa Waziri na Rais Magufuli

Mbunge wa UVCCM Kigoma Aongoza Vijana Wenzake Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli

$
0
0
Mbunge wa viti Maalum Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia UVCCM Mkoa wa Kigoma, Zainab Katimba (aliyevaa Gum Boots), akiwaongoza Vijana wenzake katika zoezi la kufanya usafi, ambapo wamefanya usafi katika eneo la Hospitali ya Maweni.
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kigoma wakiongozwa na Mbunge wa Vijana Mh. Zainab Katimba wameunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi  katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kigoma Maweni.

Usafi huo ambao umeenda sambamba na kugawa zawadi mbali mbali kwa wagonjwa hospitalini hapo, ambazo ni sabuni na vifaa mbali mbali vya usafi juisi na biskuti umelenga kuunga mkono zoezi la kufanya usafi katika siku ya maadhimisho ya siku ya Uhuru.

Akizungumza hospitalini hapo Bi. Katimba alisema kuwa, wao kama vijana wameamua kuwa mfano kwa kuanza kutekeleza agizo hilo kwa kufanya usafi hospitalini hapo, Soko la Mwanga lililopo mjini Kigoma pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima ambapo wamefanya usafi kituoni hapo na kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto ikiwemo vyakula.

Alisema lengo la kufanya usafi ni kuhakikisha magonjwa mbali mbali kama kipindupindu yanatokomezwa kwa kuweka maeneo yote kuwa safi. "Leo tumeamua kuanza na hili zoezi rasmi, lakini zoezi hili ni endelevu" Katimba alisema.

Aidha Mhe. Katimba alitoa wito kwa vijana wote tanzania nzima wajikite kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha maisha ya watanzania. Mhe. Katimba ametoa agizo kwa vijana wote Tanzania nzima kuwa mstari wa mbele katika kufanya usafi siku ya tarehe 9 Dec 2015.

Profesa Lipumba, Lissu wapinga uteuzi wa Muhongo na Mwakyembe

$
0
0
Saa chache baada ya rais Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alikuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini.

Profesa Lipumba amekosoa uteuzi wa profesa Muhongo kwa madai kuwa uteuzi wake umelitia doa baraza hilo.

“Kwa kitendo kama hiki, Rais Magufuli amejiwekea dosari kutokana na uteuzi huu. Maana yake ni kuwa katika kashfa ile Profesa Muhongo hakuwa na hatia,” Profesa Lipumba aliliambia gazeti la Mwananchi.

Profesa Lipumba aliongeza kuwa wananchi watapata ugumu kumuelewa Rais kutokana na ahadi zake kuwa atapambana na rushwa na ufisadi.

Naye Tundu Lissu aliliambia gazeti hilo kuwa uteuzi wa Dk. Harison Mwakyembe hakuwa sahihi kwa kuwa ndiye aliyekuwa waziri wa Uchukuzi na punde baada ya rais Magufuli kuingia ikulu, Mamlaka ya Bandari ikabainika kukumbwa na kashfa ya upotevu wa makontena.

“Juzi Rais Magufuli aliufumua uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa, miongoni mwa waziri waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk. Harrison Mwakyembe, eti leo amemrudhisha kundini?” Lissu ananukuliwa.

Lissu aliongeza kuwa Muhongo pia hakufaa kuwa miongoni mwa mawaziri kwa kuwa alifukuzwa na Bunge kutokana na sakata la Escrow.

Hata hivyo, Profesa Lipumba alimpongeza rais kwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda baraza dogo kwa lengo la kubana matumizi.

Namba za Simu za Kuripoti Kero TRA na taarifa za siri za Watumishi Wabadhirifu

$
0
0
Dk Mpango ametaja namba za simu na kuomba wananchi waripoti taarifa zinazohusu watumishi wa ofisi ya Mamlaka na Mapato Tanzania (TRA), wanaojilimbikizia mali kinyume na kanuni za utumishi wa umma.

Pia ameomba namba hizo zitumike kutoa taarifa kuhusu kero wanazokumbana nazo wananchi katika ofisi za TPA.
Piga simu 0689 122 515
Tuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) 0689 122 516
Pia ametoa namba yake kuwa ni 0787 570 714 na ya Naibu wake kuwa ni 0784 228 095

Home Shoppinga Center Yajitokeza Kujibu Tuhuma Za Kukwepa Kodi

$
0
0
Baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao zikieleza kuwa kampuni ya Home Shopping Centre imefunga maduka yake kutokana na kukwepa kodi na kuhusika kwenye sakata la makontena yaliyopotea bandarini, uongozi wa kampuni hiyo umejitokeza na kupinga taarifa hizo.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo imeeleza kuwa habari hizo sio za kweli na kueleza kuwa haijawahi kukwepa kodi na haihusiki kwa namna yoyote na makontena yaliyopotea bandarini.

“Home Shopping Centre Co. Limited haihusiki kabisa kwa njia yoyote ile na wizi, ukwepaji kodi, au potevu wa makontena 349 na yale zaidi ya 2431 yaliyoibuliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kamwe haijawahi kujihusisha na uhalifu huo wa kuiba makontena na kukwepa kodi,” ilieleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mfilisi wa kampuni hiyo, Yusufu Mohamed.

Mohamed alieleza kuwa kampuni hiyo ilifunga maduka yake kama ambavyo makampuni mengine hufanya na sio vinginevyo.

Angalia Video ya Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz Alioutoa Siku ya Leo

$
0
0
ANGALIA VIDEO HAPA


The word UTANIPENDA means WOULD YOU LOVE ME.... This is an inspirational song talks about the real life of Diamond Platnumz it's like a Question he ask to his girlfriend... what if he loose everything that he has right now, the fame and all the things that he own would she still love him??.... The Song was written and Sang by Diamond Platnumz and produced and get Mastered by Tuddy Tomas all from Tanzania...The Video was shot in Dar es salaam Tanzania and Johannesburg South Africa under Godfather 

Wema Sepetu Kortini Kwa Uwizi wa Umeme..Tanesco Waeleza Makubwa

$
0
0
KIMENUKA! Baada ya Miss Tanzania 2006 aliye pia nyota wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kunaswa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akidaiwa kutumia umeme wa shirika hilo kinyemela, kuna madai atapandishwa kortini.
Taarifa kutoka chanzo makini zinasema kuwa, mrembo huyo alifanya ‘manuva’ hayo katika nyumba anayoishi, Kijitonyama, Dar hivyo kuweza kuliingizia hasara shirika hilo hali ambayo shirika hilo haliwezi kumvumilia.


“Amefanya ile michezo ya kuchezea mita. Mita inakuwa inasoma umeme mdogo lakini mzigo unaotumika ndani mkubwa, haufanani na malipo halisi ambayo alistahili kulipia,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Maofisa wa Tanesco juzikati ndiyo wakampitia. Inasemekana Wema alikuwa ndani na Idris (yule mshindi wa Big Brother Africa). Idris ndiye alitoka lakini Madam hakuinua miguu yake kwenda nje, wakamng’olea mita na kuondoka nayo.”

Baada ya chanzo hicho kuvujisha ubuyu huo sambamba na picha zilizosemekana ni za siku ya tukio wakati maofisa hao walipofika nyumbani hapo na kufanya ‘ambushi’, paparazi wetu alimpigia simu Wema kwa muda mrefu lakini hakupatikana, akampigia mtu wa karibu na Madam, Ahmed Hasheem ‘Petit Man’ ambapo alipatikana na kusema:

“Unajua kaka mimi si msemaji wa Wema. Mimi ni msemaji wa wasanii walio kwenye lebo ya Wema ya Endless Fame. Kama unataka msemaji wake, cheki na Martin Kadinda.”
Alipotafutwa Martin, alijibu kwa kifupi: “Kaka hata mimi nazisikia hizo habari lakini sipo Dar, nikirudi nitakwenda kucheki halafu nitakupa taarifa kamili.”
Juzi Jumanne, paparazi wetu alifika nyumbani kwa Wema ili kujionea sakata hilo lakini hakufanikiwa kuingia getini baada ya kugonga geti kwa muda mrefu bila majibu.
Mmoja wa majirani wa mrembo huyo aliyeomba hifadhi ya jina, alipoulizwa kuhusu kufahamu sakata hilo, alisema:

“Kiukweli sisi wenyewe tulishangaa. Tunaamini Madam si mtu kuchezea mita. Ni mtu anayejiweza, anayejitambua sasa tumeshtuka kuona mita inatolewa.”
Paparazi wetu alifika Ofisi za Tanesco Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) ili kuzungumza na wahusika lakini akakosa ushirikiano.

Hata hivyo, mfanyakazi mmoja wa Kitengo cha Emergency (Dharura) aliyeomba kufichwa jina lake, alisema ni kweli zoezi hilo lilifanyika nyumbani kwa Wema, Jumatatu iliyopita na kukutana na kadhia hiyo ambapo alisema madam huyo atapandishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kuiibia Tanesco.
GPL

SHINDA ZAWADI YA GARI Kama zawadi ya Christmas Kutoka Kampuni ya Magari Kutoka Japan..Magari Mawili Kutolewa 24 Dec 2015

Baada ya Nape Kula Shavu la Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.. TFF yatoa Tamko Hili

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kufutia kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika serikali ya awamu ya tano.
Katika salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF ina imani nae katika nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika michezo na haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Aidha pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa chama cha soka moa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa hiyo, na James Bwire mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya wa manispaa ya Nyamgana.
Malinzi amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo walizozipata za kuwatumikia watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini anawatakia kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.

Rais Magufuli Amwaga Mabilioni Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu..Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania Wasema Haya

$
0
0
Shilingi billion 473 zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa mwaka huu ikilinganishwa na Shilingi bilioni 341 zilizotolewa  mwaka jana ikiwa ni ongezeko la Tsh. bilioni 132 katika bajeti ya mwaka huu.
Hayo yalisemwa  jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania(Tahliso)  bwn. Nzilanyingi  John  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuaandaa mdahalo kujadili hotuba ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoisoma Dodoma wakati wa ufunguzi wa bunge la kumi na moja .
Alisema kuwa kwa kipindi kifupi kumekuwa na  mabadiliko ya haraka yaliyotokea katika sekta ya elimu nchini kwa mwaka huu  kwani kuna ongezeko la zaidi ya wanafunzi 1800 waliopata mkopo ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo ni wanafuzi 34128 pekee ndio waliofanikiwa kupata mkopo.
“Mpaka sasa jumla ya wanafunzi 51,675 wa mwaka wa kwanza wamepata mkopo na lengo ni kufikia 53,032, pia jumla ya wanafunzi 91 wa shahada ya uzamili  na wanafunzi 113 wanaosoma vyuo vya nje tayari wamepata mkopo” alisema John.

Aliongeza kuwa katika kipindi kifupi kijacho bodi ya mikopo imehakikisha kutoa mikopo kwa wanafunzi zaidi ya elfu moja wanaochukua Diploma maalumu ya ualimu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na hivyo kukamilisha adhma yao ya kutoa mikopo kwa wanafunzi 53,032.
Aidha shirikisho hilo ambalo ni umoja wa viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini umeandaa mdahalo wenye lengo la kutoa fursa kwa watanzania wengi kujadili hotuba hiyo  na namna rais alivyoanza kutekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.
Mdahalo huo utafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 mwezi huu katika ukumbi wa Nkurumah na wazungumzaji wakuu katika mdahalo ni Mtaalamu mbobevu wa uchumi kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Prof.Honest Ngowi, Dkt. John Lingu kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanadiplomasia Christopher Liundi.

James Lembeli Apeta Kesi ya Kupinga Matokeo Jimbo la Kahama..Sasa Njia Nyeupe Kwake

$
0
0
Kushoto ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo asubuhi baada ya kushinda maombi yao ya kuomba kupunguziwa gharama za kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Jumanne Kishimba ambapo Lembeli alipaswa kulipa shilingi milioni 15 na badala yake Mahakama imemtaka kulipa Shilingi milioni 9 ndipo kesi ya msingi ianze kusikilizwa

Rais John Magufuli Atoa Mkwara Mpya...Akataa Sherehe ya Kuwapongeza Mawaziri Waliochaguliwa...Awapa Ujumbe Huu Mzito

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr John Pombe Magufuli ametangaza Baraza la Mawaziri ambalo litafanya kazi katika serikali hii ya awamu ya tano kwa kipindi cha miaka 5.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dr es salaam Rais Dr. Magufuli ametangaza baraza la wizara 18 na katika wizara hizi kutakuwa na mawaziri 19 na nyingine zitakuwa hazina manaibu waziri kabisa wote watatakiwa kuanza kazi mara moja bila kusubiri semina elekezi kama ilipozoeleka hapo awali.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr John Pombe Magufuli ametangaza Baraza la Mawaziri ambalo litafanya kazi katika serikali hii ya awamu ya tano kwa kipindi cha miaka 5.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dr es salaam Rais Dr. Magufuli ametangaza baraza la wizara 18 na katika wizara hizi kutakuwa na mawaziri 19 na nyingine zitakuwa hazina manaibu waziri kabisa wote watatakiwa kuanza kazi mara moja bila kusubiri semina elekezi kama ilipozoeleka hapo awali.


Nimeteua baraza dogo la mawaziri kwa lengo la kuepuka gharama za matumizi yao pamoja na watendaji wengine na fedha ambazo zilikuwa zimeandaliwa na ofisi ya utumishi kiasi cha shilingi bilioni mbili na zaidi zitatumika katika shughuli nyingine muhimu kama vile kutengeneza madawati au eneo jingine muhimu zaidi.



Aidha Dr Magufuli amewataka Mawaziri waliochaguliwa wakawatumikie Watanzania kwa yale waliyoahidi katika kipindi cha kampeni bila kubagua vyama vyao,dini,ukanda,tabaka na ndio maana kauli mbiu y etu inasisitiza kwamba “Hapa ni Kazi tuu”

Kwa upande mwingine Rais Dr. Magufuli ametamka wazi kwamba hakutakua na sherehe za kuwapongeza mawaziri hao na kama wanataka sherehe wajiandae pia kufanya sherehe siku ya kufukuzwa kazi.


Nilipomteua waziri Mkuu alijielekeza moja kwa moja kwenye kufuatilia makontena na Makamu wa Rais akajielekeza kwenye Mazingira sasa na hawa wanatakiwa kujielekeza kwenye wizara zao bila kupoteza muda”alisisitiza Rais.

Baraza hili limechelewa kutangazwa kwa takribani mwezi mzima tangu alipoapishwa Dr Magufuli na hata hivyo wizara 4 bado hazijapatiwa Mawaziri ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ujenzi uchukuzi na mawasiliano, Wizara ya Fedha na mipango na Wizara ya Sayansi Teknolojia,Elimu na Ufundi.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images