Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Lowassa: Nilishinda Urais Lakini CCM Wakaupora Ushindi Wangu na Dunia Nzima Inajua

0
0
Aliyekua mgombea Urais anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameendelea kudai ndiye mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na dunia inajua.

Katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari kupitia msemaji wake, Aboubakary Liongo, Lowassa alisema ushindi wake uliporwa na kupewa mtu mwingine lakini amewataka Watanzania wasikate tamaa.

Lowassa pia aliwashukuru Watanzania kwa kumpa kura nyingi wakati wa uchaguzi huo, kura ambazo alidai kuwa zilimfanya kuongoza dhidi ya wagombea wengine.

Hata hivyo, katika uchaguzi huo wa Oktoba 25, Rais John Magufuli ndiye aliyeshinda kwa kupata kura 8,882,935 (sawa na asilimia 58.46) na Lowassa kura 6,072,848 (sawa na asilimia 39.97) ya kura zote.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva alimtangaza Dk. Magufuli kuwa Rais mteule siku nne baadaye na aliapishwa Novemba 5, mwaka huu.

Liongo alisema Lowassa alitoa shukrani hizo juzi jioni katika mikutano ya hadhara wa kumnadi mgombea ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwenye kata za Mkonoo na Nodisaito.

Nawashukuru sana Watanzania kwa kanipa kura nyingi kabisa. Tulishinda, dunia nzima inajua na wao wanajua, Watanzania mmeonyesha imani kubwa kwangu,” amekaririwa Lowassa.

“Nawashukuru sana Watanzania kwa uvumilivu wenu baada ya kushuhudia ushindi wenu ukiporwa… mlitaka wakati ule nitoe tamko muingie barabarani kudai ushindi wenu.

Lakini nawapenda, Watanzania siko tayari kuona mnapoteza maisha,” imesema taarifa hiyo ikimkariri  Lowassa.

Aliwaomba wananchi wa Arusha kumchagua Lema katika Uchaguzi wa jimbo hilo kesho ili kuliletea maendeleo Jiji la Arusha ambalo linaongozwa na Ukawa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi, Ikiwemo ya Siri ya Magufuli Kuweka Kiporo Wizara Nne Nyeti

Sijaridhika Wala Kukubaliana na Utumbuaji wa Majipu wa Huyu Mheshimiwa Magufuli Kutokana na Haya

0
0
Sijaridhika wala kukubaliana na utumbuaji wa majipu wa huyu Mheshimiwa Magufuli, ambaye ni Rais wa Jamhuri yetu ya Muungano. 

Jambo la kwanza alilonikosesha nisimwamini kwa asilimia kubwa niusanii namna alivyokwepesha kashfa ya watu binafsi waliojimilikisha UDA na kuikosesha serikali mapato kwa kukwepa kodi. Suala la UDA limefukiwafukiwa hadi sasa linaonekana kutopewa uzito stahiki.

Uteuzi wa baraza la mawaziri umedhihirisha hana jipya zaidi ya kuwanyanyapalia dagaa huku wahusika wakuu wa kashfa bandarini, Escrow na TRA waliokuwa mawaziri na makatibu wakuu wa serikali ya Kikwete akiwatunukia uwaziri tena na kuendelea Ukatibu Mkuu licha ya kashfa nzito zilizoibuliwa na bunge hadi kuachia ngazi.

Kushindwa kushughulikia mgogoro wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar dalili tosha Rais Magufuli kadiri ya msimamo wa CCM hana ubavu kwa chama chake, bali kukipigia magoti tu. Hana nguvu alina nayo kikatiba ila kutii matakwa ya chama chake.

Dhahiri alichoanza Rais Magufuli ni nguvu za soda, hatimaye yatakayojilia ni kukata tamaa na kuendelea na mazoea bora liende muhula uishe.

Source:Jamii Forums

Nafasi za kazi
Bonyeza =>www.ajirayako.com

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana Amemjibu Lowassa Baada ya Kudai Kazi Nzuri Anayofanya Magufuli ni Sera za Upinzani

0
0
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya Rais John Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa Arusha, Philemon Mollel (Monaban), uliofanyika katika kata ya Daraja Mbili jana, Kinana alisema sera ya kupambana na ufisadi ilizungumzwa katika kampeni na Dk Magufuli peke yake na si Lowassa wala kiongozi yeyote wa Ukawa.

Kinana alisema anamshangaa kiongozi huyo kwa kuwa mbali na kushindwa kuzungumza wakati wa kampeni za urais, pia hakuwa na hotuba yoyote ambayo ingeweza kukaririwa na Dk Magufuli.

Alisema Lowassa hakuweza kuzungumzia masuala yoyote ya kupambana na ufisadi kwa kuwa yeye ni mtuhumiwa na vyama vina vyounda umoja huo ndiyo vimekumbatia ufisadi kwa sasa.

Kwa mujibu wa Kinana, Lowassa alinadi sana mabadiliko kama angeweza kuingia madarakani, lakini hakufafanua ni mabadiliko yapi ambayo angeweza kuyaleta, wakati anatoka katika mfumo ule ule aliokulia kwa zaidi ya miaka 40 akiwa ndani ya CCM na Serikali yake.

“Jamani Lowassa alisema mabadiliko lakini hao wanaotaka mabadiliko wana umri wa ujana sawa na jua linalochomoza la saa mbili asubuhi, wakati yeye anayedai kuleta mabadiliko ana umri wa uzee sawa na jua linalozama la saa 12.30 jioni, si vichekesho hivyo?” Alihoji Kinana.

Alisema kutokana na ukweli huo, ndiyo maana Watanzania walipima na kuamua kumpa ushindi wa kishindo Dk Magufuli, kutokana na uadilifu wake pamoja na uwezo wake wa kuchapa kazi na kuamua kumnyima Lowassa na ndiyo maana kwa sasa anajifariji kwa kusema sera zinazotekelezwa ni za Ukawa.

Akizungumzia kazi alizoanza kuzifanya Rais Magufuli, Kinana alisema zimewakuna Watanzania wengi na kusema kuwa hiyo ndiyo kazi aliyoahidi kwao kuifanya na kwamba anaamini ataifanya kwa dhati katika kuwapigania wananchi wanyonge.

Mfumo wa CCM 
Akizungumzia madai kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayetokana na CCM anayeweza kupambana na machafu ndani ya Serikali, kwa kuwa hilo ni suala la mfumo, Kinana alipinga na kusema si kweli.

Akifafanua alisema mfumo unaweza kubadilishwa hata na mtu mmoja kama anavyofanya Dk Magufuli, Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Alisema moja ya mambo aliyoyaondoa Magufuli katika mfumo huo, ni pamoja na kufuta safari za nje kwa viongozi akiwemo yeye binafsi, kuondoa semina, warsha, makongamano, sherehe na maadhimisho mbalimbali pamoja na posho mbalimbali na kuagiza fedha hizo kwenda katika mahitaji mengine ikiwemo hospitalini.

Akizungumzia uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu, Kinana aliwataka wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini, kuachana na ushabiki wa vyama na badala yake wachague kiongozi kutokana na sifa zake na kuangalia maslahi yao na siyo ya chama wala kiongozi husika.

Alisema kwa sasa wananchi wa jimbo hilo wanapaswa kuangalia maslahi yao katika kumchagua mbunge, yakiwemo maslahi ya shule, afya, miundombinu, amani pamoja na mambo mengine mengi, badala ya kubaki kuimbiwa kuwa wanafundishwa kuiwajibisha Serikali huku wakibaki katika lindi la umasikini, ukosefu wa amani na maandamano kila kukicha.

Mwakyembe Aomba Apewe Muda......Azungumzia Katiba Mpya

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye ameapishwa leo na rais John Magufuli kushika wadhifa huo amewaomba wadau na wananchi kwa ujumla kumpa muda.

Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa, Dkt. Mwakyembe ambaye alikuwa waziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya nne amesema kuwa anafahamu changamoto nyingi katika mfumo wa sheria ya nchi akiwa kama mwananchi. Hivyo, ameomba kupewa muda ili atakapoingia ofisini azifanyie kazi changamoto hizo.

Dk. Mwakyembe ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliyebobea, alieleza kuwa mfumo bora wa sheria ya nchi ni kitu muhimu katika kipindi hiki ambacho serikali imeamua kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo.

“Tuko katika kipindi cha mageuzi makubwa ya uchumi wetu na masuala ya kijamii na kiuchumi, kwahiyo masuala ya kisheria yatajitokeza sana hapo. Ndio maana nasema… sawa ni eneo langu kisheria lakini changamoto ziko nyingi ambazo lazima tukabiliane nazo ili nchi yetu iende kwa kasi ambayo rais wetu ameanza nayo,”alisema.

Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya uliokuwa ukiendelea katika serikali ya awamu ya nne, Dk. Mwakyembe amesema suala hilo litakamilishwa kutoka pale lilipoishia.

“Mheshiwa rais ameshalielezea vizuri sana hilo kwamba katika kipindi chake tutalifanyia kazi, na hatukuishia pabaya tuliishia pazuri tu, tutalitekeleza, muda utafika na naamini tutalikamilisha vizuri tu,”aliongeza.

Chama cha CUF Nacho Chalianzisha....Wapinga Uteuzi wa Prof. Muhongo

0
0
JUMUIYA ya Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) imesema wanasikitishwa na uteuzi wa baraza la mawaziri lililotajwa juzi na Rais John Magufuli na kudai  kuwa, katika baraza hilo wamerudishwa wale mawaziri waliokumbwa na kashfa za ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
  
Pia imesema katika baraza hilo hakuna uteuzi  ambao umewiana hasa katika suala la usawa wa kijinsia na wala haukuzingataia Muungano uliokuwepo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini  Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Hamidu Bobali  amesema  wanashangaa kuwaona  aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Harson Mwakyembe kuwepo tena.

Amesema,  Waziri Muhongo alikuwa anatuhumiwa na suala la Escrow na akajiuzulu halafu Magufuli amemrudisha tena kitu ambacho kinawakosesha amani.

“Inatusikitisha sana kitendo cha Rais wetu kumteua tena Waziri Muhongo kurudi tena wizarani hapo wakati alikuwa na kashfa kubwa ya escrow lakini amerudishwa tena inaonyesha Magufuli pia pamoja na kusifiwa juu ya utendaji wake hayuko makini,”amesema Bobali.

“Pamoja na Muhongo pia Waziri Mwakyembe alikuwa katika wizara ambayo sasa hivi  inakubwa na matatizo makubwa ya kupitisha makontena na wakati  alikuwa waziri   katika wizara hiyo, hilo lilitosha kwa Magufuli kufanya upembuzi wa Mawaziri. Hao wote hawakufaa tena kuridi kuwa mawaziri,” amesema.

Ameongeza kuwa,  wanasikitishwa sana kwani ile kasi ambayo  Magufuli alianza nayo wanaiona inakufa siku si nyingi kwa kuwarudia tena mawaziri hao mizigo.

“Wananchi tunasikitika sana kwa kuwa tulimuamini  Rais Magufuli lakini imani hiyo inakaribia kukatika kutokana na kurudishwa kwa mawaziri hawa na kusababisha kasi kupungua,”ameeleza

Aidha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo hakuwahi kupatikana na hiyo ya Escrow kwani alijiuzulu mwenyewe. Kwa kuhofia kupatikana na hatia.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo alizungumzia mgogoro uliokuwepo Zanzibar na kusema kuwa Baraza la vijana wa chama hicho kwa kushirikiana na vyama vinavyunda Umoja wa Katiba Wananchi (Ukawa) wameandaa mkutano juu ya kuzungumzia mgogoro huo.

“Tunafurahishwa na mazungumzo yanayoendelea kati ya viongozi kwetu wa huko Zanzibar lakini baraza letu limeandaa mkutano huo ili kuzungumzia suala hili,”amesema Bobali

Hata hivyo Bobali amesema wanamuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala la Zanzibar kwani kutokufikia kikomo kunasababisha mambo mengi kurudi nyuma ikiwa moja na uchumi kushuka.

“Jumuiya ya vijana inawatahadharisha wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha mara moja kauli chafi na  vitendo vya kichochezi vinavyofanywa na wanachama hao kwani vinaweza kuamsha hasira za vijana wa CUF Zanzibar,” amesema Bobali

Wakati Wapinzani Wakipinga Uteuzi wa Waziri Sospeter Muhongo, Mwenyewe Aibuka na Kusema Haya Makubwa

0
0

WAKATI wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka. 

 

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema mbali na mkakati wa kushusha bei ya umeme, kasi ya kusambaza umeme vijijini kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itarejea palepale.

“Nimepokea uteuzi huo, kinachofuata ni kuwatumikia wananchi, niwaombe tu wanivumilie kidogo nitawapa mpango wangu wa maendeleo wa muda mfupi na mrefu, lakini nisisitize tu nishati sio siasa, ni suala la utaalamu, liachwe lifanywe kitaalamu,” alisema Profesa Muhongo.

Akizungumzia bei ya umeme na upatikanaji wake, Profesa Muhongo alisema kupunguza bei hiyo ni ajenda muhimu itakayozingatiwa na kusema ili umeme uwe wa uhakika, ni lazima kuwe na mipango ya kuwa na nishati hiyo ya uhakika ifikapo mwaka 2025.

“Umeme wa uhakika utapatikana na matarajio yetu ni Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo tunatarajia uzalishaji wa nishati hiyo ufike Megawati 10,000 hadi 15,000,”alisema Profesa Muhongo.

Alisisitiza kwamba wizara yake haitategemea chanzo kimoja cha nishati bali wataangalia vyanzo vingine ikiwemo nishati jadidifu, upepo, gesi, makaa ya mawe, maji huku akisema vyanzo hivyo vikitumika kuzalisha nishati, ni wazi bei ya umeme itashuka na kushusha gharama nyingine za maisha na za uwekezaji.

Aliongeza katika kuendeleza sekta ya nishati suala la uwekezaji ni muhimu hivyo wizara yake inakaribisha wawekezaji wenye sifa, watakaowekeza kwenye sekta hiyo ili kuja na matokeo bora zaidi, wananchi wanufaike na rasilimali za nchi yao.

Pamoja na nia yake hiyo kwa wananchi, Profesa Muhongo anakabiliwa na pingamizi kutoka kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani, akiwemo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Lissu na Profesa Lipumba, wamekaririwa wakikosoa uteuzi wa Profesa Muhongo kwa madai kuwa wizara aliyopewa kuiongoza, ilikumbwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow wakati wa uongozi wake, ikasababisha ajiuzulu.

Hata hivyo, Profesa Lipumba na Lissu katika kukosoa huko, hawakutaka kutumia kumbukumbu zilizo wazi kuwa uchunguzi dhidi ya Profesa Muhongo, ulibaini kuwa hakukiuka maadili yoyote katika sakata la utoaji wa karibu Sh bilioni 300 zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT).

Matokeo ya uchunguzi huo yalitangazwa Mei mwaka huu na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ambapo alisema Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ndiyo ilifanya uchunguzi kama Profesa Muhongo alistahili kwenda kwenye Baraza la Maadili kujibu mashitaka, lakini hawakuona tatizo lake na kufunga shauri lake.

Balozi Sefue aliweka wazi kuwa Profesa Muhongo alijiuzulu kwa sababu za kisiasa, lakini kimaadili hakuhusika kwa namna yoyote, kutokana na uchunguzi wa Sekretarieti ndiyo sababu hakufikishwa katika Baraza la Maadili.

Kitu kingine ambacho Lissu na Profesa Lipumba, hawakutaka kuzungumzia ni utendaji wa Profesa Muhongo alipokuwa katika wizara wakati wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa katika miaka miwili ya uongozi wake katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Muhongo alisimamia kwa umahiri usambazaji wa umeme vijijini. 

 

Kabla ya kuteuliwa kwa Profesa Muhongo, Watanzania asilimia 14 tu ndio waliokuwa wakitumia nishati ya umeme, kati yao asilimia 12 walikuwa watumiaji wa mijini na asilimia mbili ndio walikuwa watumiaji wa vijijini.

Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, kati ya mwaka 2007 na mwaka 2010, kulikuwa na ongezeko la asilimia nne la watumiaji wa umeme, hali iliyoonesha kuwa ongezeko la Watanzania waliokuwa wakipata umeme, lilikuwa asilimia moja kwa mwaka. 

 

Lakini baada ya kuteuliwa kwa Profesa Muhongo katika nafasi hiyo, katika muda mfupi wa uongozi wake, idadi ya Watanzania wanaotumia umeme iliongezeka na kufikia asilimia 36 katikati ya mwaka jana.

Kwa hatua hiyo, uongozi wa Profesa Muhongo ulivuka malengo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo ndio msingi wa utekelezaji wa malengo ya Serikali, iliyotaka Serikali kuhakikisha ifikapo mwaka 2015, asilimia 30 ya Watanzania wawe wanapata umeme.

 Katika kutimiza malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010, uongozi wa Profesa Muhongo, ulitangaza punguzo la gharama za kuunganisha umeme majumbani kutoka Sh 177,000 za awali hadi Sh 27,000 vijijini.

Awali, punguzo hilo lilitolewa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara, ambako bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam limeanzia na limepita, lakini baada ya muda gharama hizo zilishushwa kwa vijiji vyote nchi nzima.

Profesa Muhongo mwenyewe alikaririwa akisema gharama hizo zitahusu miradi inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), katika kipindi ambacho makandarasi watakuwa wakiendelea na awamu ya pili ya miradi iliyoanza Machi mwaka huu na kutarajiwa kukamilika katikati ya mwakani.

Wafanyabiashara 15 Waliokaidi Agizo la Rais Kukiona Cha Moto

0
0

MAKAMPUNI 15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao, yamejisalimisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini yameshindwa kulipa kodi ndani ya siku saba za msamaha wa Rais John Magufuli.

Kodi inayodaiwa kwa kampuni hizo ni Sh bilioni 3.75, hivyo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kukwepa kulipa kodi, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango alisema hayo jana wakati akielezea makusanyo ya kodi ya makontena yaliyoondolewa katika bandari kavu ya Azam, kinyume cha sheria pamoja na kumalizika kwa siku saba alizotoa Rais Magufuli kwa wafanyabiashara hao kulipa kodi waliyokwepa, bila kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.

Dk Mpango alisema siku hizo saba zimefikia kikomo juzi, hivyo hatua kali za kisheria kwa wafanyabiashara ambao hawakulipa kodi katika kipindi hicho zinafuata hivyo wasubiri cha moto.

“Tumewasihi waje kulipa kwani huruma ya Rais sasa imeisha... tulifanya uhakiki na kuthibitisha kuwa kampuni hizo zipo. Wamekuja kulalamika lakini hakika hakuna atakayesamehewa kulipa na sasa tunafuata mkondo wa sheria ili kuwafikisha mahakamani,” alisisitiza.

Wadaiwa 

Alitaja kampuni hizo kuwa ni Ahmed Saleh Tawred anayedaiwa Sh milioni 59.23; Cla Tokyo Limited Sh milioni 77.52; Farida Abdullah Salem Sh milioni 75.33 na Juma Kassem Abdul Sh milioni 190.18.

Wengine ni Libas Fashion Sh milioni 52.94; Rushy Wheel Tyre Center Co Ltd, Sh bilioni 1.8; Said Ahmad Hamdan Sh milioni 68.36; Said Ahmed Said Sh milioni 68.73 na Salum Continental Co Ltd Sh milioni 151.17.

 

 Pia yumo Salum Link Tyres Sh milioni 343.44; Simbo Yonah Kimaro, Sh milioni 69.22; Snow Leopard Building Material Co Ltd Sh milioni 93.97; Swaleh Mohamed Swaleh Sh milioni 34.68; Tybat Trading Co Limited, Sh milioni 598.69 na Nasir Saleh Mazrui Sh milioni 70.10.

Alisema mpaka kufikia jana TRA walikuwa wamekusanya Sh bilioni 10,643.004,948.46 kutoka kwa kampuni 28 ambapo kampuni 13 zimelipa kodi yote iliyokadiriwa, ambayo ni Sh 4,167,130,173.89 na Sh 2,303,637,554.57 kutoka kampuni 15 zilizolipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa.

Dk Mpango alisema Sh bilioni 4.17 zimelipwa na kampuni ya Azam ICD, ikiwa ni dhamana ya kodi iliyokwepwa, hivyo atatakiwa kumaliza kulipa kodi yote inayodaiwa kwa mujibu wa nafasi yake kama mwenye dhamana.

Alisema wakati utekelezaji huo ukiendelea, ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo ya makontena yaliyoondolewa bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha, TRA imefungua akaunti maalumu katika Benki Kuu yenye namba 9921169785 inayoitwa Commissioner for Customs and Excise – Container Account.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, mpaka sasa watumishi 36 wa TRA wanaotuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na makontena hayo kuondoshwa bandarini.

Watumishi wachongewa 

Aidha, alisema TRA imepata taarifa zisizopungua 15 kutoka kwa wananchi kuhusu mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi na walipakodi wanaokwepa kodi. 

 

Aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa na kuwaomba wengine wajitokeze kutoa taarifa zaidi na mamlaka hiyo inawahakikishia kuwa itawalinda.

Dk Mpango alisema wanaendelea kutekeleza maagizo ya Rais katika ukusanyaji wa mapato, ikiwa ni pamoja na kupiga picha makontena yote badala ya sampuli ya kontena ilivyo sasa na wanafanya utaratibu wa kupata mashine za kupiga picha za nyongeza.


Mdahalo Wa Tahliso Kujadili Hotuba ya Magufuli Waingia Dosari Baada Ya Wanafunzi wa UDSM Kuupinga

0
0
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye  jana alinusuru kuvunjika kwa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO), baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuupinga.

Mdahalo huo ulilenga kujadili hotuba ya Rais Dk. John Magufuli aliyosoma bungeni Novemba 20, mwaka huu wakati akizindua Bunge la 11.

Dosari hiyo ilijitokeza mapema kabla ya Nape kuwasili katika ukumbi wa Nkurumah baadaya Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), Kataponda Ahadi kusimama na kutoa hoja ya kuwataka wenzake wasusie mdahalo huo kwa sababu haukubeba ajenda na lengo la TAHLISO.

Hata hivyo, alikatishwa mazungumzo yake baada ya kuelezwa muda wa kujadili mada ulikuwa haujaanza, kwa sababu wakati huo  mdhamini wa mdahalo huo ambao ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alikuwa akielezea faida za mfuko huo.

Baada ya malumbano yaliyochukua muda kidogo, wanafunzi hao walikubaliana na hoja ya  kuendelea kumsikiliza mwakailishi wa NSSF aliyekuwa akiwasilisha mada, hadi Nape alipowasili ukumbini hapo.



Katika hotuba yake, Nape aliusifia mdahalo huo na kusema utasaidia wabunge watakapo kwenda bungeni wawe na ajenda za wananchi, badala ya kwenda na ajenda zao ambazo pengine si matatizo wanayopata wananchi.

Alisema hotuba ya rais, imekuja kwa wakati na imeeleza changamoto nyingi, hivyo ni muhimu vijana wakawa sehemu ya mabadiliko yanayotakiwa kwa staha na uwazi.

Aliwataka wananchi waache utaratibu wa kusikiza na kushangilia tu, bali waichambue, waikosoe,washauri na kuwasisitiza kuwa wasiache suala la mabadiliko liwe la Rais Dk. Magufuli tu.

“Lazima tuhakikishe mabadiliko haya yanaingia kwenye mfumo na yasibaki kwa rais peke yake ili siku tukimpata mtu mwingine afuate mfumo huo. Inapaswa tuusukume mfumo ukubali  mabadiliko hayo lakini mfumo ukigoma tutapata matatizo,” alisema Nape.

Baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wanafunzi walinyoosha mikono kutaka kutoa hoja ambapo mshereheshaji aliwataka wasubiri mada zitakapowasilizwa wahusika ndiyo wapate muda wa kuzijadili.

Hata hivyo, wanafunzi hao hawakukubaliana na mwongozo huo na walisimama na kusema wana hoja ya kumweleza waziri kabla mada hazijawasilishwa na ndipo mmoja alipopewa nafasi.

Mwanafunzi huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake, alisimama na kuanza kutupa lawama kwa TAHLISO kuwa wameshindwa kusikiliza na kujadili matatizo yanayowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu na badala yake wanajihusisha na mijadala ya kisiasa.

“Tunashangaa TAHLISO ambayo ni shirikisho la kuwatetea wanafunzi wa vyuo vikuu, wamekaa kimya kila tunapofikisha matatizo ya wanafunzi, sasa wameona bora wajadili hotuba ya Dk.Magufuli,” alisema mwanafunzi huyo ambaye kabla hata hajamaliza kutoa hoja yake aliamriwa kuketi.

Kitendo hicho kiliamsha hisia kwa wanafunzi wengine, ambao walisimama na kuanza kupaza sauti wakipinga mdahalo huo kwa madai kuwa hauna maslahi ya wanafunzi na kwamba ni wa kisiasa.

Hali hiyo ilimlazimu mshereheshaji kuwaomba askari kuingia ndani ili kuwatoa wanafunzi hao ambao hata hivyo waliamua kutoka wenyewe wakiongozwa na rais wao huku wakiendelea kuituhumu jumuiya hiyo.

Walipofika nje ya ukumbi waliendelea kupiga kelele ambapo iliwalazimu baadhi ya viongozi wa TAHLISO kutoka nje na kuwataka waondoke katika eneo hilo.

Yaliibuka mabishano baina ya viongozi wa pande hizo mbili na baadhi ya wanafunzi ambapo Waziri Nape aliamua kutoka nje na kuacha mdahalo ukiendelea na alipofika nje aliomba kusikiliza hoja zao.

Akielezea malalamiko yao, Rais wa DARUSO Ahadi alisema TAHLISO imeshindwa kusimamia maslahi ya wanafunzi hasa pale wanapoomba kukutana ili kujadili masuala ya wanafunzi wamekuwa hawajitokezi.

“Hawa kwenye mambo yanayohusu wanafunzi wanakaa kimya, mdahalo wameweza kuandaa kujadili hotuba ya Rais Magufuli, zaidi hata huu mdahalo unaofanyika hapa kwetu sisi viongozi wa DARUSO ambao pia ni wajumbe wake hatujapewa taarifa, ndio maana tumeamua kuupinga,” alisema Ahadi.

Kwa upande wake, Waziri wa Mikopo wa DARUSO, Shitindio Venance, alisema: “Kutokana na kitendo cha jumuiya hii kushindwa kutatua matatizo yetu tumeamua kuunda Kamati ya Taifa ya kufuatilia Mikopo ya wanafunzi nchi nzima na hivi tunapozungumza hapa kuna wanafunzi wapatao 80 ambao wanatakiwa wafungashe warudi nyumbani kwa kukosa mikopo na wengine wapo Chuo cha Bagamoyo lakini tunashangaa TAHLISO ipo kimya,”alisema.

Naye Makamu wa Rais wa DARUSO, Irene Ishengoma, alimweleza Nape kuwa pamoja na kusumbuliwa kwa kunyimwa mikopo, bado Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekuwa ikiwatoza sh 20,000 za kuiendesha suala ambalo ilitakiwa yenyewe itafute mbinu za kujiendesha.

Akijibu hoja hizo Nape aliwataka viongozi hao kuitisha vikao ili kuwaondoa viongozi wa TAHLISO ambao wameonekana kushindwa kazi kwani wao ndio waliowaweka na hivyo wana mamlaka ya kuwaondoa.

“Unajua tatizo lenu ni dogo…hawa viongozi mmewaweka wenyewe na kwa kawaida mwiba unapoingilia ndipo unapotokea hivyo nyie ndio wakuwatoa, tumbueni majipu kama mnaona yapo,” alisema Nape.

Kuhusu matatizo ya mkopo, Nape aliwaambia tayari yanajulikana na kwamba licha ya kwamba yeye si waziri mwenye dhamana lakini ni kiongozi wa chama kilichopo madarakani hivyo atahakikisha leo watahakikisha, tatizo hilo linakoma.

“Naomba niwahakikishie kuwa ikifika kesho (leo) wanaohusika tutakwenda kuwashughulikia ili wakawajibike kwa sababu inaonekana kuna tatizo maana wanafunzi wakigoma fedha zipo lakini wakikaa kimya hawapewi,” alisea Nape.

Nape alifanikiwa kumaliza dosari hiyo iliyodumu kwa dakika 20 baada ya kuwaomba wanafunzi hao warudi ukumbini ili kuendelea na mdahalo kwasababu kama ni matatizo yao yamefika sehemu husika ambapo walikubali na kurudi ukumbini.

Ndani ya ukumbi huo mada zilikuwa zinaendelea ambapo akichambua hotuba ya Rais Magufuli, Mtaalamu wa Mambo ya Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk. Honest Ngowi alisema kiuchumi suala la elimu bure halipo kwani elimu hiyo inalipiwa kwa ruzuku ya serikali kwa asilimia 100.

Alisema ili kuweza kutekeleza hilo wananchi wanatakiwa kukubali kulipa kodi zilizowekwa kwasababu ndizo zitakazotumika kuendesha sekta hiyo.

Naye Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa (UDSM), Dk. John Jingu alisema hotuba hiyo ilijikita katika dira ya maendeleo ya Taifa ifikapo mwaka 2025 ya kuwa na uchumi wa kati, kwani rais ameweza kuonesha njia na nia ya kutekeleza dira hiyo.
Kwa upande wake Mwanadiplomasia mkongwe, Balozi Christopher Liundi alisema hotuba ya Rais Magufuli imekuwa mfano kwa viongozi wa chini yake, kwani wanaonekana kutenda kwa kasi yake tangu aingie madarakani.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Disemba 14, Ikiwemo ya Magufuli Kitanzini, Masalia ya Lowassa Yamtisha

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Disemba 14, Ikiwemo ya Magufuli Kitanzini, Masalia ya Lowassa Yamtisha


Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni

0
0
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya  Escrow.

Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.

Alisema baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge wa chama hicho wamejiandaa kumwangusha.

Mnyika alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo kwenye Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.

“Hatukubaliani na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni patachimbika,” alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es salaam.

“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.

Nape: Nitaanza Kushughulikia Sheria na Nidhamu Michezoni

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kushughulikia sheria mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo ili kuongeza nidhamu michezoni.

Nape aliyeapishwa juzi kuanza kibarua hicho, ataiongoza wizara hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Dk Fenella Mukangara, huku ndoto za Watanzania zikiwa ni kuona kiwango cha michezo kilichoporomoka, kinakua.

Akizungumza na mwandishi wetu jana alisema utovu wa nidhamu kwa baadhi ya viongozi na wachezaji umekuwa ukiitafuna sekta hiyo kwa kiwango kikubwa na kusababisha kushuka kwa michezo.

Alisema zipo baadhi ya sheria zinazohitaji marekebisho ili ziwe na tija na kwamba ana uhakika kuwa zitasaidia kurejesha thamani ya michezo, ikiwamo soka na sanaa.

“Michezo ikisonga mbele na timu zetu zikifanya vizuri tutavutia wawekezaji wengi kwenye sekta hii kwa sababu suala siyo kufurahi, tunatakiwa tuichukulie sekta hii muhimu kama sehemu ya kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa Taifa letu na mtu binafsi,” alisema Nnauye na kuongeza:

“Ni kweli kwamba kiwango cha michezo nchini kipo chini na maeneo ya mwanzo ya ninayodhani yanapaswa kushughulikiwa ni kwenye sheria. Natamani kuona tunakuwa na sheria zenye tija, zitakazosaidia kumaliza utovu wa nidhamu unaoitafuna sekta hii,” alisema.

Diamond Platnumz na Zari Washinda Tuzo Nchini Uganda

0
0
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ pamoja na mchumba wake Zarinah Hassan ‘Zari The Bossy Lady’ wamepata Tuzo za Abryanz Style and Fashion (ASFA 2015) zilizofanyika Kampala, Uganda usiku wa kuamkia leo.Wawili hao wameibuka kidedea katika kipengele cha East Africa Most Stylish Couple.

Mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda naye ameibuka kidedea katika tuzo hizo kwa kipengele cha Mbunifu Bora wa Mwaka huku Mwanamitindo Bora wa Mwaka ikienda kwa Mtanzania mwingine, Dax Hannz.

Mbali na hao, pia Tanzania imepata tuzo kupitia staa wa kike wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee aliyepata katika kipengele cha East Africa’s best Dressed Female Artist.
Katika sherehe hizo zilifunikwa kwa shoo kutoka kwa mkali kutoka Nigeria, Banky W akishirikiana na bidada kunako Bongo Fleva, Linah.

Asipofunga Zipu…Nay wa Mitego Atakufa Kwa Ngoma

0
0
NAY (2)Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’  akijiachia na mrembo mpya mwenye umbo dogo kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.


KIWEMBE! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’ kunaswa akiwa na mrembo mpya mwenye umbo dogo yaani (mbichii) huku rekodi ikionesha ndani ya muda mfupi ameshabadilisha warembo takriban wanne hali ambayo imesababisha wadau kumpa tahadhari kwamba asipofunga zipu, ataukwaa Ukimwi a.k.a Ngoma, Risasi Jumamosi lina mchongo kamili.
NAY (3) 
TUKIO JIPYA
Achana na Siwema Edson, Shamsa Ford, Stella Tilya ‘Chaga Baby’ aliowapitia katika kipindi kifupi, mapema wiki hii Nay amenaswa na mrembo mbichii aliyefahamika kwa jina la Ana wakifanya yao kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.
NAY (4)Nay wa Mitego akifanya yake.
ENEO LA TUKIO
Awali, Mbongo Fleva huyo alionekana akiwa ameketi pembezoni mwa Bahari ya Hindi na baada ya saa moja mbele alielekea kwenye bwawa na kuanza kuongelea akiwa ameambana na mrembo huyo.
NEY-1Siwema akiwa na Nay enzi wakiwa wapenzi.

“Amefika (Nay) na vijana kama wanne hivi na huyo mrembo alikuwa wa tano, mwanzo wakati wakija yule mrembo alikuwa karibu na jamaa mmoja bonge sijui ndiye meneja wake wa sasa, kwa hiyo muda wote nilihisi huyo demu ni wa Bonge kumbe ilikuwa zuga tu maana baada ya kuanza kuogelea demu akaonesha wazi kuwa ni mali ya Nay kwani alikuwa anamfanyia kila linalostahili mtu na mpenzi wake kufanyiana,

AONYWA KUHUSU NGOMA
“Halafu huyu jamaa atakufa kwa ngoma asipokuwa makini maana anabadili warembo kama kitu gani.
Msururu wake unamweka pabaya. Kuna warembo wengi sana kawapitia, maarufu na wasio maarufu. Juzikati alikuwa na Siwema, mara Shamsa, ghafla nikasikia yupo na Chaga Baby leo tena ana kifaa kipya, asipofunga zipu ngoma inamuiita,” alinyetisha mdaku mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.
Chaga Baby akiwa katika pozi.

‘KANGAA FOTO’
Kama vile staa wa dansi kutoka Kongo, Koffi Olomide anavyoimba katika wimbo wake wa Selfie, ndivyo paparazi wetu alivyoanza kumtandika picha za kutosha Nay na mrembo huyo walipokuwa wakioga kwa kushikana shikana maeneo ‘muhimu’ ambapo wote kwa pamoja walionekana kufurahi.

WALA PIZZA
Kama hiyo haitoshi, wawili hao baada ya kujiachia katika bwawa hilo kwa zaidi ya saa mbili, walitoka na kuagiza msosi unaojulikana kwa jina la ‘pizza’ ambapo pia walikula kwa staili ya mtu na bebi wake bila kuhofia macho ya watu.
IMG_0093Nay wa Mitego akiwa na Shamsa Ford.

NAY ABANWA, ACHEKA
Baada ya paparazi wetu kukusanya ushahidi wa kutosha juu ya matukio yake ya kimahaba ndani ya maji, alimbana Nay ambaye alishindwa kutoa majibu yaliyonyooka kama kweli aliyekuwa naye ni kifaa chake kipya ama laa!

“Dah, wewe umefikaje hapa na umenionaje? Au kuna mtu kakulengesha nini kwangu, maana si rahisi mwandishi kama wewe kuja hivihivi tu hapa! Si bure utakuwa umepewa umbeya huu na mtu.
ney_wa_mitego_nishaNisha akiwa na Nay.
Risasi Jumamosi: Sasa huyu ndiye mpya au unawachanganya pamoja na yule wa Marekani, Chaga Baby?

Nay: Ebwana huyu anaitwa Ana ni mtu wangu tu, nipo na masela zangu wengine, tumekuja kuogelea kwa raha zetu so haya ni maisha fulani ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo na kujiachia kwani kuna tatizo?
Risasi Jumamosi: Hauogopi Ukimwi kujiachia na warembo tofauti?

Nay: Kwani nimekwambia huyu ni mtu wangu? Mimi niko makini kweli na suala la ngoma. Naomba uniache niondoke naona unaniharibia siku.

MSURURU WA NAY
Ukiondoa Siwema, Shamsa, Chaga Baby huko nyuma jamaa huyo kwa nyakati tofauti alishawahi kuripotiwa kubanjuka na mastaa wa Bongo Movies; Salma Jabu ‘Nisha’ na Skyner Ally ‘Skaina’ aliyezaa naye mtoto mmoja.

Sumaye Akosoa Uamuzi Wa Rais Magufuli Kuhusu Wakwepa Kodi

0
0
Waziri Mkuu mstaafu ambaye juzi alichukua kadi ya uanachama wa Chadema, Frederick Sumaye ameukosoa uamuzi wa rais John Magufuli kuwasamehe watu waliorejesha kiasi cha fedha walichokwepa kulipa kodi.

Sumaye alitoa mtazamo wake huo juzi  jijini Arusha baada ya kukabidhiwa kadi ya uachama wa Chadema ikiwa ni miezi takribani mitatu tangu alipojiunga na harakazi za Ukawa na kutangaza kuihama CCM.

“Unawezaje kutoa msamaha kwa wezi na wakepa kodi nchini  kwa kuwapa siku saba eti wawe wamelipa madeni yao? Hili ni jambo la ajabu kabisa. Unawezaje kupitisha msamaha kwa wezi na wakwepa kodi? Sumaye alihoji.

“Haya tuliyaona wakati wa sakata la EPA na sasa tunayaona kwenye makontena, wezi wanasamehewa,” aliongeza.

Zaidi ya shilingi bilioni 10 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutoka kwa wafanyabishara mbalimbali waliokwepa kodi kupitia makontena yaliyotoroshwa bandarini baada ya rais kutoa siku saba za ‘rehema’.

Baada ya siku hizo kupita (ijumaa), hivi sasa serikali inawasaka wafanyabiashara 15 ambao hawakujisalimisha katika kipindi kilichotolewa na rais Magufuli. TRA imeahidi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao kama rais alivyoagiza.

Breaking News: Godbless Lema Aibuka Kidedea, Afanikiwa kutetea Jimbo lake la Ubunge Arusha

0
0


Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.

Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Pamoja na Navo Mollel wa ACT Maendeleo aliyepata Kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa CUF aliyepata kura 106. Sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw Juma Iddy, jimbo la Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.

Wapiga Kura Kibamba Wamtaka Mnyika Kuanza Kufanyia Kazi Ahadi Zake Badala Ya Kuendelea Kutoa Matamko Kwenye Vyombo Vya Habari

0
0
Wakazi wa jimbo la kibamba wamemtaka mbunge wao, John Mnyika kuanza kufanyia kazi ahadi zake badala ya kuanza kutoa matamko kwenye vyombo vya habari kuzungumzia mambo ya kitaifa wakati ana mambo kadhaa ya kuyafanyia kazi jimboni kwake.

Wakiongea na mwandishi wa Dar24, wakazi hao wamesema pamoja na kushukuru sana kwa kupewa jimbo jipya ambalo limegawanywa kutoka lililokuwa jimbo la Ubungo, wanatarajia mbunge wao huyo, ambaye kwa kipindi kilichopita pia alitumika katika eneo hilo atakuwa na eneo dogo la kulifanyia kazi hivyo kuwaletea maendeleo kwa kutatua kero zao.

Mkazi kibamba aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Uledi maarufu kama ‘Mzee wa Ukawa’ alisema “Mnyika si mgeni na matatizo ya Kibamba kwani hili lilikuwa ni eneo lake alipokuwa mbunge wa Ubungo. Hivyo hatutegemei kumwona akitumia muda mrefu kuongelea mambo ya kitaifa badala ya kushughulikia kero zetu.”

“Tunamtaka Mbunge wetu arudi jimboni kukaa na sisi ili atueleze mikakati aliyonayo na pia muda wa kuanza kutimiza ahadi alizotuahidi badala ya kuanza kulalamikia suala la ofisi aliyopewa kuwa ndogo. Hivi sasa kipaumbele chake kiwe kero zetu badala ya kufikiria kuanza kukaa ofisini,” alisema Mwanaisha Swedi akiwa katika sehemu yake anayofanyia biashara ya kuuza vitafunio.

"Tunamtaka mbunge wetu aache kulalamikia suala la ofisi, aje atuambie nasi tuna uwezo wa kumjengea ofisi kubwa katika eneo hili. Tunamtaka aje aungane nasi kujikwamua kwenye matatizo yetu ya kiuchumi na kimiundo mbinu" alisema Jerome Munishi ambaye alijitambulisha kuwa ni mkazi wa mbezi mwisho.

Kwa ujumla wakazi wa kibamba wanamtegemea mbunge wao kuacha kuwa mbunge wa matukio na vyombo vya habari kwa kutoa matamko kila jambo la kitaifa linapotokea. 

Maelezo ya wakazi hao wa Kibamba yamejikita katika kile wanachoamini kuwa muda wa siasa umepita hivi sasa ni bora akaelekeza nguvu zake katika kufanya kazi kwa kushirikiana na wapiga kura wake.

Credit: Dar24

Nafasi za Kazi SUMATRA, Application Deadline 26 December 2015

0
0
The Surface and Marine Transport Regulatory Authority (SUMATRA) is a Government
Regulatory Authority established by the Surface and Marine Transport Regulatory Authority, CAP 413 of the laws. SUMATRA’s role is to regulate, promote and facilitate availability of efficient, safe, quality and reliable transport services in the surface and marine transport sub-sectors through competitive and fair trade practices.

Soma Nafasi zote zilizotangazwa HAPA

Baada ya Mange Kimambi Kumlipua Dr Mwaka, Leo Dr Mwaka na Wasaidizi Wake Wamkimbia Naibu Waziri wa Afya

0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala leo majira ya jioni amefanya ziara ya kushtukiza  katika kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka  kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo hicho. 

 

Mara baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna daktari aliyekuwa anatoa huduma.

 

Akizungumza na wagonjwa waliokuwa wakisubria tiba alisema kuna waliofika katika kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa hao.

Katika ziara hiyo ya kushtukiza ambayo Dr Mwaka na wasaidizi wake walikimbia, msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema lolote kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu,hivyo alimwomba Naibu waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwauliza maswali wahusika mbalimbali wa vitengo vya kituo hicho.

 

Baada ya ukaguzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi kwa  kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaluma ya Dr. Mwaka  pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia kama ni rafiki kwa wananchi wanaotumia dawa hizo.

 

Pia amesema Dk Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo mbalimbali hapa nchini jambo ambalo ni kosa kisheria.

 

Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo inatumika  mojawapo  ni kutojitangaza.

 

 Naibu waziri aliendelea kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na amekuwa akichambua mwili wa binadamu kama vile amesomea udakitari wakati sheria ya tiba asilia na tiba mbadala hairuhusu watu wa tiba Asilia na Tiba Mbadala  kutumia maneno  ya tiba ya kisasa.

 

Pia Naibu Waziri amemtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani kesho saa mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.

Mwanasheria Albeto Msando Afunguka Kuhusu Dr Mwaka....Adai Walikuwa Wapi Siku Zote?

0
0
Kuna watu watasema ni wivu! Kuna wengine watasema Mwaka ni tapeli! Kuna ambao watakuwa upande wa Kigwangwala na kuna ambao watakuwa kwa Mwaka. Ila je kwa nini mpaka leo hii tiba inahojiwa? Siku zote mamlaka husika zilikuwa wapi? Hao waliotibiwa wakapona wako wapi? 
Ambao hawajapona ni kina nani? Mkurugenzi wa Baraza la Tiba Asili mpaka anafika hapo kwenye 'kliniki' alikuwa hajui kama Mwaka ana vyeti au la? Hakuwa na taarifa zozote za ziada? Je Babu wa loliondo ilikuwaje? Wanaotibu mapenzi na kupata kazi vipi? Wale madaktari wa kusafisha nyota? Au hao kuku weusi wanaokula sio dhuluma? Nadhani Naibu Waziri ameanza kushtukiza ila AENDE NA KWENYE VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI PIA. Kuna hao madaktari waliosomea na wao ni bure kabisa huko!! Hili la Mwaka kilichomponza ni kupitiliza!! Wote huwa inatukuta tukinogewa!! Sasa ndio atajua kama bado WATAMPENDA
By Alberto Msando-Instagram

Nafasi za Kazi
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images