Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Uchaguzi wa Meya Tanga Wazua Vurugu Kubwa, Ni Baada ya CCM kutangazwa Kushinda Japo Ina Idadi Ndogo ya Madiwani

0
0

Uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji la Tanga umezua vurugu kubwa leo   baada ya Mkurugenzi wa Jiji hilo kumtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi licha ya chama hicho kuzidiwa idadi na madiwani wa Chama cha Wananchi (CUF).

Madiwani wa Ukawa wako 20 huku madiwani wa CCM wakiwa 17, hivyo upande wa UKAWA walikuwa na imani kuwa kwa wingi wao wangeweza kuongoza Halmashauri hiyo kwa kupata kura nyingi.

Taarifa za kuaminika kutoka katika chumba cha kupigia kura zimeeleza kuwa baada ya zoezi la kupiga kura, Mkurugenzi na timu yake walihesabu kura zote zilizopigwa na baadaye alitangaza kuwa mgombea wa CCM ameshinda kwa kupata kura 19 dhidi ya mgombea wa CUF ambaye amepata kura 18.

Baada ya tangazo hilo, vurugu kubwa ilizuka ukumbini hapo huku CUF wakidai kuwa ilikuwa mbinu ya CCM kumtumia Mkurugenzi wa jiji hilo kuhujumu uchaguzi na kumpa ushindi mgombea wake.

Zoezi la kumchagua Meya wa jiji hilo lilitanguliwa na uchaguzi wa Naibu Meya ambapo mgombea wa CUF alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 21 dhidi ya mgombea wa CCM aliyepata kura 16, matokeo ambayo CUF wanadaiwa kuyapinga wakidai yaliandaa mazingira ya hujuma ya Meya.

“CUF wanadai kuwa Mkurugenzi aliandaa mazingira ili ionekane kuwa kuna diwani mmoja wa CCM alimpigia kura mgombea wa CUF kwenye unaibu Meya, ili baadae aoneshe kuwa kuna wagombea wa CUF waliompigia kura mgombea wa CCM na kumuwezesha kushinda,” Chanzo kimeiambia Mpekuzi.


Ushauri: Kila Nikikutana naye Nashindwa Kufanya nae Mapenzi

0
0
Wadau za usiku huu,
Kuna kitu huwa kinaniumiza sana kichwani mwangu kwani kuna mdada mmoja mzuri ameumbika na ana sifa zote nzuri za kike. Tatizo linakuja kila nikikutana nae jogoo ananywea kabisa mpaka kero.

Hapa naandika haya kalala pembeni baada ya kumforce sana jogoo lakini wapi. Sijui tatizo ni nini kwa sababu kwingine jogoo fresh anapiga kazi kama kawa tatizo nikimuita yeye tu lazima jamaa agome kufanya kazi, hii leo ni mara ya nne.

Naombeni ushauri wadau nifanyeje?

 ~Yaser

Nisher Aeleza Kwanini Ameamua Kuweka Wazi Mahusiano yake ya Kimapenzi Mtandaoni (Picha)

0
0

Muongozaji wa video, Nisher ameweka wazi sababu inayomfanya aweke wazi picha za mahaba akiwa na mpenzi wake katika mitandao ya kijamii.

Nisher amesema kufanya hivyo kunamweka mbali na wasichana wengine wanaomsumbua.

“Naona ni vyema zaidi kuwa wazi na mkweli, inasaidia kupunguza usumbufu,” ameiambia Bongo5.

“Ndoa inakuja, ila hamna haraka yoyote bado kwa sababu tupo vizuri na mambo mengine taratibu.”



Mwakyembe Afunguka Kuhusu Katiba Mpya na Mahakama ya Rushwa..Adai Rais Amempa Kazi ya Kuhakikisha Haya

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Rais amempa kazi ya kuhakikisha anakamilisha mchakato wa Katiba Mpya pamoja na uanzishwaji wa Mahakama ya Rushwa.

Kura ya Maoni ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ilipangwa kufanyika Aprili 30, lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikatangaza kuiahirisha hadi itakapotangazwa tema, ikisema inataka kukamilisha kwanza uandikishaji wapigakura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Lakini kabla ya kutangaza kuahirisha kazi hiyo, vyama vya upinzani, ambavyo vilisusia Bunge la Katiba kwa madai kuwa lilikiuka utashi wa wananchi kwa kuweka kando sehemu kubwa ya mapendekezo yaliyokuwa kwenye Rasimu ya Katiba, walikuwa wakitaka mchakato huo uanze upya.

Lakini jana, Dk Mwakyembe alisema moja ya majukumu aliyopewa ni kuhakikisha anakamilisha mchakato huo wa kuunda Katiba Mpya ulioanza miaka mitatu iliyopita wakati Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete alipotangaza kuanza rasmi kuwa Serikali itaanza kazi ya kuandika Katiba Mpya.

“Kuna masuala mengi ambayo wizara yangu inahusika nayo, mengine bado sijayaelewa vyema kwamba yapo kwenye hatua gani, lakini suala la Katiba Mpya hilo ni jukumu ambalo hata Rais alinitamkia kuwa amenikabidhi niliendeleze kwa hatua iliyobaki,” alisema Dk Mwakyembe.

Kauli yake Dk Mwakyembe ambaye amebobea kwenye sheria, haikupokelewa vizuri na wanasiasa wa upinzani ambao walisema kutekelezwa kwa mpango huo kutakuwa ni kuanzisha tena mgogoro bila ya sababu za maana, na kwamba upatikanaji wa kura za Wazanzibari walioko Bara bado haujapatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia tamko hilo la Dk Mwakyembe, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema ikiwa Serikali inataka kuendeleza mchakato wa Katiba, ikubali kuunda upya Bunge la Katiba kwa mujibu wa sheria.

“Sheria ya Kura ya Maoni haina utaratibu wa kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya na hairuhusu kupata tarehe mpya ya kupiga kura ya maoni baada ya kuahirisha upigaji kura,” alisema mwanasheria huyo wa kujitegemea.

“Kama Mwakyembe ataendeleza upya mchakato huu, aanzie alipoishia Jaji (Joseph) Warioba.”

Bunge la Katiba liliingia dosari baada ya wajumbe kutoka vyama vinne vya Chadema, NLD, CUF na NCCR-Mageuzi na wengine kutoka taasisi tofauti, kususia vikao wakidai kuwa mapendekezo ya wananchi yaliyokuwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Katiba, ambayo iliongozwa na Jaji Joseph Warioba, yalitupwa na badala yake yakawekwa mapendekezo ya CCM.

Wajumbe hao walitoka wakati Bunge la Katiba likiwa limekwama kwenye Sura ya Kwanza na ya Sita zinazozungumzia Muundo wa Muungano, baada ya Tume ya Warioba kuwasilisha mapendekezo yanayotaka serikali tatu, huku wajumbe wengi wa chombo waliotoka CCM wakitaka uendelee muundo wa sasa wa serikali mbili.

Pamoja na wajumbe wa vyama hivyo vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kujiengua, Bunge la Katiba liliendelea na mchakato na kufikia kupitisha Katiba inayopendekezwa ambayo ingepigiwa kura na wananchi Aprili 30, lakini haikuwezekana.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili Ya Disemba 20, Ikiwemo ya Meja Jenerali Kufia Kwa TB Joshua

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili Ya Disemba 20, 













Wanasheria wa Tanzania Waja Juu Kuhusu Udhalilishaji Unaofanywa na Baadhi ya Wakuu wa Wilaya...Watoa Tamko Hili

0
0
Wanasheria wa Tanzania Waja Juu Kuhusu Udhalilishaji Unaofanywa na Baadhi ya Wakuu wa Wilaya...Watoa Tamko Hili

Lowassa Atoa Ujumbe Mzito Kwa CCM baada Ya Kupewa Tuzo ya Amani na Taasisi 1200 Duniani

0
0
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa amesema anashangaa kuona anaambiwa mleta vurugu wakati dunia inamkubali kuwa ni mlinzi wa amani.

Kauli ya Lowassa imekuja ikiwa ni siku moja baada ya taasisi za kidini 1,200 duniani kupitisha jina lake kwa ajili ya kumpatia Tuzo ya Amani.

Nimepokea kwa unyenyekevu  na furaha tuzo ya amani duniani ninayotarajiwa kupewa na taasisi za kidini 1200 duniani,” alisema Lowassa akinukuliwa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.

Lowassa alisema tuzo hiyo ni kithibitisho cha uongo wa CCM na Serikali yake kuwa wapinzani ni watu wa vurugu.

Taasisi hizo katika kikao chake huko Bukavu DR Congo, zilitangaza kumpa tuzo hiyo Edward Lowassa kutokana na utulivu aliyouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu Kwa jamii,  Mchungaji William Mwamalanga ilisema kiasi wajumbe 1,400 wa mkutano huo kutoka kote duniani walikubaliana kumpa tuzo hiyo Lowassa kati ya wanasiasa 1,000 waliyoshindanishwa ili kumpata kiongozi bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.

Alisema yeye ni muungwana na ana hofu ya Mungu na hata siku moja hatoweka mbele maslahi binafsi, na ndiyo maana aliwatuliza wananchi waliyokuwa wakimtaka kutoa tamko baada ya matokeo kutangazwa.

Siko tayari kuingia Ikulu huku mikono yangu ikibubujika damu. Nashukuru taasisi hizo za kidini duniani, zimeliona hilo,” alisisitiza Lowassa.

Profesa Muhongo Aiagiza Tanesco ishushe Bei ya Umeme

0
0
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

?Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,? alisema.

CHANZO: NIPASHE

Ndege ya Ufaransa yatua Kenya Ghafla Baada ya Air Hostess Kugundua Bomu Chooni

0
0
Passengers aboard Air France flight No 463 headed from Mauritius to France were Sunday morning forced to cut short their trip after an air hostess discovered device suspected to be an explosive in one of the plane?s toilets.

The air hostess alerted the pilot who made an emergency landing at the Moi International Airport, Mombasa.

Bomb experts from the Kenya Navy were called and immediately removed the device to safety outside the airport.

The Boeing 777 plane with 473 passengers on board was diverted to Mombasa at around 3am and immediately cleared to land.

All the 473 passengers were screened at the airport lounge and taken to safety in hotels where they were also receiving care and counselling.

The Kenyan security officials were said to be zeroing in on two passengers who appeared suspicious.

At the same time, bomb experts were conducting a major search inside the plane.

The Mombasa security team and airport security in Mombasa also secured the airport and all critical facilities around

Hatima ya Duni Kuondoka Ama Kubakia Chadema Kujulikana Januari....

0
0
Mwanasiasa mkongwe nchini, Juma Duni Haji amesema hatima yake ya kubakia au kuondoka ndani ya Chadema itajulikana mwezi ujao.

Duni aliihama CUF na kujiunga Chadema ambayo ilimsimamisha kuwa mgombea mwenza wa urais wa Chadema iliyokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NLD na NCCR Mageuzi.

Tangu kuisha kwa Uchaguzi Mkuu na mgombea wa Chadema kushika nafasi ya pili,  Duni amekuwa kimya, lakini juzi alisema itakapofika Januari mwakani ataeleza mustakabali wake kisiasa.

“Kwa sasa sisemi jambo lolote, nitakuambia baadaye kidogo kama nitarudi CUF au nitabakia Chadema. Kuna mambo ninafanya kwanza, nisingependa kusema,” alisema Duni.

Pia, Duni alizungumzia hisia zake za kisiasa visiwani Zanzibar, akisema anashangazwa na kauli ya aliyekuwa Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mark Bomani kumshawishi Maalim Seif Hamad akubali  uchaguzi urudiwe.

Siku chache zilizopita, Jaji Boman alinukuliwa na vyombo vya habari akimtaka Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar kukubali kurudia uchaguzi huo kama ilivyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kuwa utarudiwa ndani ya siku 90.

Jecha alifuta matokeo ya urais na uwakilishi wa Zanzibar, akisema kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni na kwamba ndani ya tume yake wajumbe walitofautiana hadi kukunjana.

Jaji Bomani alisema kama Maalim Seif alishinda, atashinda uchaguzi ukirudiwa kwani wananchi watampigia kura.

 Hata hivyo, Duni alisema: “Anajua kabisa nchi yoyote inaporudia uchaguzi mara nyingi amani huwa inapotea, kwa mfano Burundi leo hii bado wanauana na hakuna anayezungumza lolote kwa sababu ni chama tawala kimeshinda.

CUF inasisitiza Katiba ya Zanzibar ilindwe au kwa sababu upande wa Bara wamepata Rais (John Magufuli), sasa hawajali usalama wa Wazanzibari?

Duni alihamia Chadema chini ya mpango maalumu wa Ukawa wa kuwezesha vyama hivyo kuchukua urais Bara na Visiwani, mpango ambao haukuweza kuzaa matunda.

Video Mpya: Alikiba & Christian Bella – Nagharamia

0
0
Video mpya ya wimbo “Nagharamia” wa Alikiba na Christian Bella video imeongozwa na Enos Olik kutoka Kenya, video imefanyika pia Nchini Kenya angalia hapa alafu toa maoni yako.

Miss World 2015 imeisha na Mshindi Ameshatangazwa + Top 10

0
0
Ni shindano ambalo limefanyika nchini China kwa mara ya saba kuanzia mwaka 2003 ambapo kwenye fainali za 2015, mshindi ametangazwa kuwa ni Mireia Lalaguna Royo wa Hispania ambaye umri wake ni miaka 23, wanasema kingine kikubwa kilichompa nafasi ni umahiri wake mkubwa wa kuongea mbele ya hadhara.

Nchi zilizoingia kwenye Top 10 ya shindano hili la 65 ni Russia, Philippines, Guyana, Lebanon, Spain, Jamaica, France, South Africa, Spain and Australia.

Wafanyabiashara Wahuni na Wakwepaji Kodi Wampiga Chenga Rais Magufuli..Sasa Wahamia Tanga na Mtwara

0
0
MTANDAO wa wafanyabiashara wasio waaminifu unaojihusisha na ukwepaji kodi wa bidhaa mbalimbali zinazoingizwa nchini kupitia bandari, umekimbia Dar es Salaam na kuhamishia shughuli zake kwenye mikoa ya Tanga na Mtwara.

Taarifa za uhakika zilizolifikia MTANZANIA Jumamosi zimeeleza kuwa wafanyabiashara hao na mawakala wao wameondoa maskani yao kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kuyapeleka bandari za Tanga na Mtwara.

Imeelezwa kuwa kuhama kwa wakwepa kodi hao kumesababishwa na msako wa wakwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam ulioanzishwa na Rais John Magufuli, ambaye amekwishawatia kitanzani baadhi ya maofisa wa Serikali wanaotuhumiwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kukwepa kulipa kodi halali ya Serikali.

Miongoni mwa maofisa wa Serikali waliosimamishwa kazi na wengine uteuzi wao kutenguliwa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kuikosesha Serikali mapato ni wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA).

Taarifa zimeeleza kuwa mbali na kuikimbia Dar es Salaam, mtandao huo wa wakwepa kodi pia umebadilisha mbinu za kupitisha mizigo isiyolipiwa kodi lengo likiwa kuwakwepa maofisa wa TRA.

Mmoja wa wafanyabiashara anayepitisha mizigo yake katika Bandari ya Dar es Salaam, ameliambia gazeti hili kuwa hivi sasa mawakala wa wakwepa kodi wanawahi makontena wanayoyalenga yanaposhushwa tu bandarini wanapakua mizigo yote na kuyaacha tupu hivyo wakifika maofisa wa TRA huyakuta yakiwa hayana mizigo.

“Wamemkimbia Rais Magufuli, wamemuacha Dar es Salaam wao wamepeleka maskani yao kwenye bandari za Tanga na Mtwara na hata mbinu za kufaulisha mizigo yao isiyolipiwa kodi nazo wamebadilisha.

Sasa hivi wana mtindo mpya, wanavizia makontena yao yanapoingia tu bandarini wanapakua mizigo yote na kuyaacha tupu hivyo wanapokwenda maofisa wa TRA wanakuta hayana mizigo, yako tupu na wanapata hela nzuri kweli kwa sababu kufaulisha kontena moja siyo chini ya Sh milioni tano,” alisema mfanyabiashara ambaye jina lake tunalihifadhi.

Mfanyabiashara huyo alieleza zaidi kuwa hivi sasa kazi ya kuvusha mizigo bila kulipiwa ushuru inafanywa kwa umakini mkubwa na mara nyingi imekuwa ikifanyika nyakati za usiku kwa msaada wa baadhi ya watumishi wa idara za Serikali.

Mfanyabiashara mwingine aliyezungumza na gazeti hili ambaye pia jina lake tunalihifadhi alieleza kuwa mtandao wa wafanyabiashara wakwepa kodi ni mkubwa na unawahusisha pia watumishi wa Serikali ambao wamekuwa katika ushirika huo kwa muda mrefu.

Alizitaja bidhaa zinazoongoza kupitishwa kwa magendo kuwa ni sukari inayotoka katika nchi za Brazil na India pamoja na makaa ya mawe yanayotolewa nchini Afrika Kusini.

“Wanaingiza sukari kutoka Brazil na India na ukichunguza sukari hiyo utabaini muda wake wa matumizi ya binadamu umekwisha. Wanapoipakuwa wanakwenda kuifunga katika mifuko mipya inayoonyesha kuwa ni sukari iliyozalishwa katika viwanda vya hapa nchini.

Bandari ya Tanga hivi sasa ndiyo kichochoro cha wakwepa kodi na siku hizi kuna makaa ya mawe yanayotoka Afrika Kusini ambayo yanaingizwa kwa wingi hapa nchini ingawa hatujui yanapelekwa wapi,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu ukweli wa taarifa hizo, Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Luzangi, hakukataa wala kukubali bali alionyesha mshangao huku akiahidi kufuatilia na kutoa tamko hivi karibuni.

Jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa  Kodi wa TRA, Richard Kayombo, hazikuweza kufanikiwa na hata alipopigiwa simu yake ya kiganjani ilikuwa haipatikani.

Taarifa hizi zimepatikana ikiwa ni wiki kadhaa sasa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na TRA na kuibua upotevu wa makontena 329 ambayo pia hayakuwa yamelipiwa ushuru.

Kuibuliwa kwa kashfa hiyo ilifuatiwa na hatua za kutenguliwa kwa uteuzi wa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade na kukamatwa kwa Kamishna wa Forodha, Tiagi Masamaki pamoja na maofisa wengine waliohusishwa nayo.


Je Kumtimua Mourinho ni Maamuzi Sahihi Kwa Mustakabali wa Chelsea? Kitendo Walichokifanya Wachezaji wa Chelsea ni cha Kipuuzi

0
0
Mashabiki wengi wa Chelsea wamefuraishwa sana na matokeo ya mechi ya Jana kati ya Chelsea na Sunderland baaada ya kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja
Lakini tujiulize kuhusu mustakabali wa Chelsea miaka mitano au kumi ijayo
Je kumtimua Mourinho ni maamuzi sahihi kwa mustakabali wa Chelsea?

Mimi naona sio sahihi kuendekeza sana wachezaji wa chelsea kuamua boss wao awe nani.La sivyo baada ya miaka kumi tusishangae Chelsea ikiwa imefundishwa na walimu zaidi ya 20
  na hakipaswi kushabikiwa na wote waipendao Chelsea 

Wamehujumu timu na sio Mwalimu..
Leo Mourinho yuko wapi? Na timu ipo nafasi ngapi?
Walichokifanya Wachezaji ni Usaliti na Uhujumu ni bora kuwa na wachezaji wabovu wenye nidhamu kuliko hao would Class prayers wasio na nadhimu na timu
Shame Hazard,Shame Costa and you're thinking to be the world prayer

By Jeffa Mlabwa

Wastara: Najuta Starehe Zimeniponza

0
0
STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema kitu ambacho kimemponza na kumfanya asumbuliwe na mguu wake mara kwa mara ni kujisahau sana katika starehe kwa kuwa hajawahi kujikubali kuwa ni mlemavu.

Akipiga stori na paparazi wetu Wastara alisema, tangu alipopatwa na tatizo hilo la mguu kwenye fikra zake hakutaka kukubali matokeo, siku zote alipenda aishi kama alivyokuwa mzima ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye muziki na kucheza.
“Siyo siri nilijisahau sana, sikupenda kujiona mlemavu, nilikuwa naishi kama mtu wa kawaida tu.
Sasa hivi najuta kwa kutozingatia matunzo ya mguu wangu maana nilikuwa najiachia sana hususan linapokuja suala la muziki. Sasa nimeamua kukubaliana na hali halisi kama walivyo walemavu wengine,” alisema Wastara.

Chanzo:Global Publishers

Picha: Diamond Platnumz Akiwa na Watoto Wote wa Zari

0
0
Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mwanadada Zarinah Hassan ‘Zari the boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa mkali wa bongo fleva, Diamond Platinum alitupia picha hizi akiwa yeye, Tiffah na Diamond pamoja na watoto watatu wa zari ambao diaomond alimkutanao kuandika maeno kuashiria hiyo ndiyo familia.

Hii ni kwama mara ya kwanza kwa diamond kupiga picha na watoto hao wa zari tangu Diamond awe na mahusiano na mwanadada Zari.

Jionee picha hizo hapo chini

Waziri Mkuu Acharuka.....Asema Wabadhirifu Watang'olewa Mara Moja,Asisitiza Wasomi Wako Wengi wanaotafuta Ajira

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya watendaji wa halmashauri nchini kwamba atakayebainika ametumia vibaya fedha za Serikali atang’olewa kazini kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano haina mchezo na mtu.
 
Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumapili, Desemba 20, 2015)  wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo Lindi mjini.
 
“Natoa onyo kwa watendaji wote wa halmashauri. Fedha ya Serikali itakayotumwa kwenu halafu mtu aifanyie ubadhirifu,  ole wake. Yeyote atakayebainika kuzitumia kwa ubadhirifu fedha hizi tutamng’oa. Wako wasomi wengi huko nje tena wazuri tu, wanasubiri kupata ajira.”
 
“Nataka watumishi wa umma watambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inajielekeza kujali wananchi.  Wao wana dhamana ya kuwasilikiliza na kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha wanatatua kero zinazowakabili, ” alisema huku akishangiliwa na wengine wakisema huyu sasa ni Sokoine wa pili. (Edward Moringe Sokoine alikuwa ni Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza).
 
Waziri Mkuu ambaye aliwasili Lindi Jana, aliwaeleza wakazi hao kwamba amekuja kuwashukuru wazee na wana Lindi kwa dua zao na kuwaahidi kwamba hatawaangusha Rais John Pombe Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuwatumikia Watanzania katika ngazi ya Uwaziri Mkuu.
 
Waziri Mkuu pia alimpa kazi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Jordan Rugimbana ya kuhakikisha anaufufua uwanja huo na kuurudisha kwenye enzi yake ulivyokuwa maarufu katika mikoa yote ya Kusini.
“Uwanja huu lazima uboreshwe kwa sababu unanikumbusha mwaka 1984 wakati nachezea timu ya Amri Rangers.  Kulikuwa na ukoka wa nguvu hapa uwanjani. Kwa hiyo timu aliyoiunda Mkuu wa Mkoa itafanya kazi lakini pia iwajumuishe Meya na mbunge wa Lindi Mjini kwa sababu huu uwanja ni mali ya Halmashauri ya Lindi, ” alisema.

Akielezea kuhusu mipango ya Serikali kuendeleza sekta ya viwanda, Waziri Mkuu alisema hivi karibuni mkoa huo utapata wawekezaji kwenye sekta ya gesi baada ya kampuni ya BG kutoka Uingereza kupata umiliki wa eneo la Kikwetu ili wajenge mitambo ya kusafisha gesi.

Aliwataka wananchi wa mkoa huo wawekeze kwenye ujenzi wa hoteli na nyumba za kulala wageni ili ifikapo Agosti mwakani, watu wanaokuja kushiriki maonyesho ya NaneNane kitaifa mkoani humo wasipate taabu ya malazi kama ambavyo imekuwa ikitokea huko nyuma

Mkuu wa Upelelezi TANAPA Achinjwa Kinyama Kama Kuku na Mwili Wake Kuwekwa Katika Buti la Gari yake

0
0
POLISI mkoani Arusha imewatia mbaroni watu wawili wanaohusishwa na tukio la kuuawa kinyama kwa kuchinjwa shingo kwa Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Ulinzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Stephen Kisamo.

Kifo cha Kisamo kinahusishwa na mambo mengi yakiwemo vita ya kupambana na ujangili, ikielezwa mkuu huyo alikuwa na siri nzito juu ya watu wanaojihusisha na ujangili wakiwemo wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya Arusha, watumishi wa serikali na wanasiasa.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Arusha zilieleza tayari imewatia ndani watu wawili ambao ni marafiki wakubwa wa Kisamo na wanajua siri nzito kutokana na kunaswa kwa mawasiliano ya simu ya kiganjani kati ya marehemu na watu fulani muda mfupi kabla ya mauti kumfika ambao polisi inawachunguza kwa karibu.

“Wasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas sisi tumeshakamata watu wawili wa karibu na marehemu na sms na mawasiliano yanatia shaka, lakini ukweli utajulikana muda si mrefu,” kilieleza chanzo chetu cha habari ndani ya Jeshi la Polisi.

Kamanda Sabas alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Desemba 18, mwaka huu asubuhi katika eneo la Kikwakwaru jijini Arusha muda mfupi baada ya Kisamo kutoka nyumbani kwake akiwa na gari aina ya Mazda.

Sabas alisema siku hiyo hiyo jioni alifika kituoni hapo mke wa marehemu na kueleza juu ya kutoweka kwa mumewe ambapo mara moja polisi walianza kufuatilia jambo hilo bila mafanikio.

Kamanda Sabas alisema usiku, Polisi ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema wa eneo hilo la Kikwakwaru kuhusu kuonekana kwa gari hilo likiwa limeegeshwa maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuonekana mtu yeyote ambapo walifika na kulikuta gari hilo, lililovutwa hadi katika Kituo Kikuu cha Polisi usiku huo na baadaye lilitambuliwa na mke wa Kisamo.

Baadaye walirejea eneo la tukio kwa lengo la kutafuta mwili wa marehemu huyo, lakini hawakufanikiwa kuupata mwili wala kumuona kachero huyo ambapo walilazimika kuomba ruhusa ya kupekua gari hilo.

Alisema baada ya kuomba ruhusa hiyo, mke wa marehemu alipowasilisha ufunguo wa akiba wa gari na Polisi walipofungua na kuanza upekuzi walikuta mwili wa marehemu ukiwa umekunjwa kwenye buti, huku shingo yake ikiwa imechinjwa eneo la nyuma ya shingo yake.

Aidha, Kamanda Sabas alisema kwa mujibu wa maelezo ya mkewe, mumewe alikuwa mgonjwa na alikuwa akijiandaa kwa safari ya India kwa matibabu, hivyo kabla ya tukio walidhani alitekeleza gari baada ya kuzidiwa na ugonjwa.
Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Mbowe: John Pombe Magufuli Anacheza Ngoma ya Chadema...Adai CCM Imemdhibiti Katika Uteuzi wa Baraza la Mawaziri

0
0
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anafurahi kuona Rais John Magufuli akitekeleza sehemu kubwa ya sera za chama chake na kwamba kazi ya upinzani si kupinga kila kitu, bali kuangalia masilahi mapana ya Taifa.

Mwenyekiti huyo pia amesema “biashara imeisha” kwa Rais John Magufuli baada ya kutoka kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM kwa kuwa chama hicho kilimdhibiti katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri kiasi cha kumfanya arudishe sura zilezile.

Rais ameanza kazi kwa kishindo baada ya kufumua uozo kwenye taasisi mbalimbali za Serikali kama Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Mapato (TRA), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku akidhibiti matumizi ya Serikali kwa kubana safari za nje za watumishi wa umma, kuondoa posho za vikao na pia kuanza utekelezaji wa ahadi ya elimu bure.

Mbowe anaona mambo hayo ndiyo ambayo wapinzani wamekuwa wakipigia kelele wakati wote.

Akizungumza kwenye kipindi maalumu cha Kituo cha Televisheni cha Azam juzi, Mbowe alisema hakuna jambo ambalo Rais Magufuli analifanya ambalo kambi ya upinzani haijawahi kulizungumzia.

Alitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni hoja ya kubana matumizi ya Serikali, kupunguza safari za nje za viongozi na kupunguza idadi ya watumishi wasio wa lazima.

Mambo mengine alisema ni kupunguza sherehe za kitaifa na kuwa na Serikali ndogo. Alisema kwa kiasi kikubwa Rais anatekeleza sera za upinzani ambazo zilikuwa zinapingwa na wabunge wa CCM.

“Kuwa mpinzani haimaanishi kupinga kila jambo linalofanywa na Serikali hata kama jambo lenyewe ni jema. Ni wajibu wetu kama upinzani kuisimamia Serikali ili kuhakikisha kwamba kila analolisema Rais linatekelezwa kwa vitendo,” alisema Mbowe ambaye pia aligombea urais bila mafanikio mwaka 2005.

Mbunge huyo wa Hai aliongeza kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani itaendelea kutimiza wajibu wake wa kusimamia mambo yenye masilahi kwa wananchi na haitaona haya kuikosoa Serikali pale inapotoka kwenye mstari.

Dk Magufuli ameanza urais kwa kufuta safari za nje hadi kwa kibali cha Ikulu, kumuondoa kaimu mkurugenzi mtendaji wa MNH na kuvunja bodi ya hospitali hiyo, kumuondoa kamishna mkuu wa TRA, mkurugenzi mkuu wa Takukuru, mkurugenzi mkuu wa TPA na katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kutokana na udhaifu alioukuta kwenye taasisi zao. Pia, ameanza kutekeleza ahadi ya elimu bure kwa kuagiza walimu wakuu kutolipisha wanafunzi ada kuanzia Januari na kufuta michango ya aina yoyote shuleni.

Pia, ametangaza Baraza la Mawaziri lenye watu 34, kufuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru, Siku ya Ukimwi na kupongeza wabunge, akielekeza fedha zilizopangwa kwa shughuli hizo kuelekezwa katika kutatua matatizo ya wananchi.

Mbowe pia hakusita kukosoa Baraza la Mawaziri lililotangazwa na Dk Magufuli.

“Hakuna kipya,” alisema Mbowe.

“Sura ni zilezile zilizokuwapo kwenye Serikali iliyopita na baadhi ya mawaziri wanakabiliwa na kashfa.”

Mwenyekiti huyo alitoa mfano mfano wa uteuzi wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kwamba haukuwa sahihi kwa sababu ndiye aliyeteua bodi ya Bandari ambayo imevunjwa na Rais kutokana na usimamizi mbovu.

Aliongeza kuwa kurudi kwa Profesa Sospeter Muhongo pia si sahihi kwa sababu aliondolewa kwa uamuzi wa Bunge kutokana na kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Alisema Baraza la Mawaziri halina jipya kwa sababu Rais Magufuli alidhibitiwa na Kamati Kuu ya CCM katika kuliunda.

“Rais alifungwa mikono na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi na tangu ametoka Kamati Kuu biashara imeisha,” alisema Mbowe.

Lakini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimjibu Mbowe kuwa walitegemea kauli kama huyo kutoka kwa mwenyekiti huyo wa Chadema.

“Mwenyekiti wa Chadema angesifia uteuzi wa Baraza la Mawaziri, ningeshangaa sana,” alisema Nape, ambaye ni pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

“Alichokisema ndicho wengi tulichokitarajia. Maoni ya Mbowe ni ushahidi wa jinsi asivyojua hata Katiba ya nchi inayoeleza mamlaka ya Rais juu ya uteuzi wa Baraza la Mawaziri kuwa haingiliwi na yeyote.

“Namshauri arudi shule kwa kuwa itamsaidia kuelewa kidogo.”


Nape Nnauye Awashukia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kwa Kurusha Sherehe ya Harusi Laivu Kwa Muda wa Masaa Mawili

0
0
Serikali imeliagiza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoa maelezo ya kina baada ya kurusha matangazo ya moja kwa moja sherehe za harusi kwa zaidi ya saa mbili, jambo lilihojiwa na wananchi maeneo mbalimbali hasa katika mitandao ya jamii.

Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kupata malalamiko mengi kwa kile kilichokuwa kinarushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1 cha shirika hilo linaloendeshwa kwa ruzuku kutoka Serikalini.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alibainisha kuwa amepokea simu za watu wengi waliokuwa wanahoji juu ya kipindi hicho, hivyo kulazimika kuchukua hatua mara moja za kutaka maelezo kutoka kwa watendaji wa shirika hilo.

Miongoni mwa programu za burudani na masuala ya kijamii, kituo cha TBC1 kinacho kipindi cha Chereko ambacho hurushwa kila Jumapili kwa matukio ambayo yamerekodiwa, lakini hali ilikuwa tofauti juzi usiku baada ya sherehe za harusi hiyo kurushwa moja kwa moja.

Kwa urefu wa muda uliotumika kurusha sherehe hizo, watazamaji wengi walishikwa na butwaa hivyo kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii wakihoji inawezekanaje kwa TBC1 kutoa muda mrefu kwa mtu mmoja kwa ajili ya shughuli yake binafsi.

Mtu hawezi kuitumia Televisheni ya Taifa kwa matakwa yake. Hii ni mali ya umma. kama kila mwenye pesa atakuwa na uwezo wa kulipia muda wa matangazo, si muda wote tutakuwa tunawaona watu wenye hela tu badala ya vipindi muhimu?” alihoji mwananchi mmoja katika mtandao wa kijamii.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alisema kwa kifupi kuwa kipindi hicho ni sehemu ya vipindi vya kituo hicho cha televisheni.

“Kile ni kipindi cha Chereko ambacho tunacho kwenye programu zetu,” alisema Mshana.

Alipoulizwa ilikuwaje ratiba ya kipindi hicho ikabadilishwa kutoka Jumapili mpaka Jumamosi, alisema: “Kile ni kipindi cha wikiendi na kama mtu sherehe yake inafanyika siku hiyo, inakuwa haina shida yoyote.”

TBC ni shirika linalomilikiwa na Serikali likiwa na televisheni na redio.

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, kituo hicho kilikuwa kikilalamikiwa kwa kuendesha kwa upendeleo kipindi cha Jambo Tanzania ambacho hupitia na kusoma magazeti makubwa ya kila siku. Katika moja ya vipindi hivyo, habari zilizokuwa zikihusu wagombea wa upinzani zilikuwa hazisomwi licha ya kuwamo kwenye magazeti yaliyokuwa yakichambuliwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene amewahi kukaririwa akisema kuwa ameshaliandikia barua za onyo shirika hilo juu ya kukiuka kanuni za utangazaji ambazo hazitaki upendeleo wa aina yoyote

Nafasi za Kazi 
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images