Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

FACTS:MWANAUME UFIKIRIA KUFANYA MAPENZI KILA BAADA YA MASAA 48

$
0
0
Umewahi kusikia kauli hizi? " Mume wangu hatosheki kitandani..""..Sidhani kufanya mapenzi ndio liwe jambo la msingi lakini huyu mwanaume kaa! Basi tu kila siku mpaka kero.."
Bila shaka ni kilio cha wanawake wachache walioamua kusema. Hivi kweli ni mara ngapi au kiasi gani tuseme inatosha? Je wanaume wanafanya makusudi? Je kuna uwezekano wakabadilika?
.....
Katika mapenzi, suala la kumtaka mwenza kimapenzi hutegemea sababu nyingi, chache ni uwezo wa kiafya, utayari wa kihisia, usalama wa kazini na mengineyo. Japokuwa jinsia zote huwa na kiu ya mapenzi lakini wanaume huwa ni zaidi.
.....
Daktari David Reuben anasema kuwa ".. Wanaume wengi huzungukia ktk mzunguko wa saa 48 yaani huhitaji kukutana kimwili kila baada ya saa 48 ili wawe ktk hali njema ya kimwili na kiakili..."
Nae Daktari na mwandishi Dr Herbert Miles anasema ".. Mwanaume mwenye afya njema mbegu hujaa kila baada ya saa 42 hadi 78 na kuzalisha nguvu kali inayohitaji zitolewe.."
....
Pia mwanasayansi Alan Frome anasema kuwa '.. Wanaume wanaonekana kuwa na njaa ya kukutana kimwili kwa sababu ya maumbile ambapo prostate gland ina kifuko kidogo kitunzacho mbegu, na kijaapo, mwanaume huhitaji kuzitoa, presha huzidi zaidi na zikitoka hurudi ktk hali yake ya kawaida.."
....
UPANDE WA WANAWAKE
Wanawake hutofautiana kabisaa na wanaume hali kadhalika na wao kwa wao. Kwa mujibu wa utafiti wa Johnson Masters 2010, kwa wastani 20-25% ya wanawake huwa na mtazamo hasi au vuguvugu ktk kuhitaji kukutana kimwili.
2% hawajali kabisa kuhusu kukutana kimwili.
25% zaidi huhitaji sana, husaka kukutana kimwili na huanzisha hitaji hili hata kabla ya mwanaume kusema.
50% iliyobaki huwa na uhitaji wa wastani tu.
Ifahamike pia hasa kwa wanaume kuwa, hali ya mwanamke hubadilika sana ktk kuhitaji tendo la ndoa ktk kipindi cha mzunguko wa siku zake.
Lakini mwanamke anapofikia miaka 40+ hitaji la kukutana kimwili hulingana karibu na lile la mwanaume
....
NINI KIFANYIKE
Wanaume ambao hawajaoa wanapaswa wajike sana ktk shughuli za uzalishaji mali zinazochosha mwili au mazoezi na kuepuka mambo yanayochochea hisia za mapenzi hapo wataishinda saa ya 48, Walio ktk ndoa wawe na utaratibu unaokubaliana na hali ya mwanamke na wajenge mazoea ya kufanya romansi sana ili kuendana na mabadiliko ya mwanaume na kuepusha utumwa wa ngono ndani ya ndoa au kukimbilia nje ya ndoa hali inayoleta magonjwa, kutelekeza familia na mengineyo yasiyoleta furaha ya familia

By Himidini

FORMULA MPYA YA KUSAHIHISHA MITIHANI YAWABEBA WENGI MATOKEO KIDATO CHA NNE

$
0
0
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne wa 2013, huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 15.17.
Matokeo hayo ni ya kwanza tangu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa upangaji ambao ulipanua wigo wa alama na madaraja, hivyo kutoa nafasi kubwa zaidi kwa watahiniwa kufaulu.
Licha ya kuanza kutumika kwa mfumo huo, idadi ya waliofeli imeendelea kuwa kubwa kwani watahiniwa 151,187 sawa na asilimia 42.91 wamepata sifuri. Kati ya hao, wavulana ni 78,950 sawa na asilimia 41.54 na wasichana ni 72,237 sawa na asilimia 44.51.
Kadhalika matokeo hayo yameendelea kushuhudia baadhi ya watahiniwa wakiandika matusi kwenye karatasi zao za majibu, huku wengine wakichora vitu vya ajabu kwenye mitihani hiyo, huku wengine wakishindwa kuandika chochote kwenye karatasi hizo.
Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema waliofaulu mtihani huo ni 235,227 sawa na asilimia 58.25 ya 404,083 ya waliofanya mtihani huo, ikilinganishwa na 185,940 sawa na asilimia 43.08, waliofaulu 2012.
Dk Msonde alisema wasichana waliofaulu ni 90,064 sawa na asilimia 55.49 na wavulana ni 111,088 sawa na asilimia 58.45.
Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa ni 427,679 wasichana wakiwa ni 199,123 sawa na asilimia 46.56 na wavulana walikuwa ni 228,556 sawa na asilimia 53.44. Kati yao watahiniwa wa shule ni 367,163 na watahiniwa wa kujitegemea ni 60,516.
Dk Msonde alisema watahiniwa 23,596 ambao ni sawa na asilimia 5.52 ya waliojiandikisha, hawakufanya mtihani huo.
Dk Msonde alisema matokeo hayo yalipangwa kwa kutumia alama zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome mwaka jana.
Alama hizo ni A: 75-100, B+:60-74, B:50-59, C:40-49, D:30-39, E:20-29 na F:0-19. Kabla ya mabadiliko hayo, alama zilizokuwa zikitumiwa kupanga matokeo ya kidato cha nne ni A:80-100, B:65-79, C:50-64, D:35-49 na F: 0-34.
Alisema pia alama za maendeleo ya wanafunzi zilizotumika ni 30 huku mtihani wa mwisho ukichangia alama 70.
Kuhusu waliochora na kuandika matusi, Dk Msonde alisema: “Wengine wamechora nyumba, wengine picha za freemason na michoro mingine ambayo haiendani na somo husika.”

Hata hivyo, alisema tabia ya kuchora michoro hiyo imepungua ikilinganishwa na 2012.
Ubora wa Ufaulu
Dk Msonde alisema watahiniwa waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu ni 74,324 sawa na asilimia 21.09 wakiwamo wasichana 27,223 sawa na asilimia 16.77 na wavulana 47,101.
Alisema waliopata daraja la kwanza ni 7,579 sawa na asilimia 2.15 wavulana 5,030 sawa na asilimia 2.65 na wasichana wakiwa 2,549 sawa na asilimia 1.57, wakati waliopata daraja la pili ni 21,728 sawa na asilimia 6.17, wakiwamo wavulana 14,167, asilimia 7.45 na wasichana 7,561 ambao ni asilimia 4.66.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa waliopata daraja la tatu ni 45,017 sawa na asilimia 12.78; wavulana 27,904 sawa na asilimia 14.68 na wasichana 17,113 sawa na asilimia 10.54.
Watahiniwa waliopata daraja la nne ni 126,828 sawa na asilimia 36 na wavulana wakiwa ni 63,987 na wasichana 62,841 sawa na asilimia 38.72.
Ubora wa ufaulu kwa mwaka 2013 umepanda kulinganisha na mwaka 2012 ambapo waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la nne walikuwa ni 159,747 sawa na asilimia 43.08 huku waliopata sifuri wakiwa 210,846 sawa na asilimia 56.92.
Watahiniwa wa shule
Dk Msonde alisema watahiniwa wa shule waliofaulu mtihani huo ni 201, 152 sawa na asilimia 57.09 kati yao wasichana wakiwa 90,064 sawa na asilimia 55.49 na wavulana ni 111,088 sawa na asilimia 58.45.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo ni 34,075 sawa na asilimia 66.23 ya waliosajiliwa, wakati 2012, watahiniwa wa kujitegemea 26,193 walifanya mtihani huo.
Kuhusu mtihani wa maarifa (QT), Dk Msonde alisema waliofaulu mtihani huo ni 6,529 sawa na asilimia 43.38.



MCL

MATUMBO MAKUBWA KWA KINA DADA YAANI MNANIKERA SANA

$
0
0
Yaani wadada wa siku hizi sijui wakoje,wanakeraaaa.

Unakuta dada mzuri ajabu,shepu shepu, nyuma ana kifurushi cha haja mweh,kuja mbele sasa,chevuuuu,tumbo hilo!,uzuri wote chalii!

Tatizo siku hizi mumezidi kuwa waroho,mnakula sana kuliko hata midume,machips mayai, manyama choma, ma bia, ma baga, sijui manini yote yenu! Sasa kwa staili hiyo kwanini msitoke vitambi!

Yaani unakuta mwanaume na mwanamke wanapita hata hujui me ni nani na ke ni nani,kwani mki maintain shape kuna ubaya gani,

We huoni watoto kama Jokate mwegelo wanavyo pendeza hadi raha,sio kama Shilole hadi anaogopesha na ule mtumbo,au mfano mzuri mdada Lara1 ni bonge la mtoto!..yupo flat sehem za flat na ameumuka sehemu zinazohitajika!
Ni ushauri tu wadada!

dr.holygrail

MASANJA MAKANDIMIZAJI NOMA SANA AWACHANA WABUNGE WANAOLILIA POSHO IPANDISHWE

TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGU KUNG'ARA TUZO ZA FILAMU AFRICA

$
0
0
Zimebaki siku 13, kabla ya kufungwa rasmi kwa pazia la kupigia kura wasanii na kazi zao katika kinyanganyiro cha kuwania tuzo za filamu Afrika zijulikanazo kwa jina la ‘Africa Magic Viewers, Choice Awards, (AMVCA).

Katika mashindano hayo, swali linabaki kwa tamthilia ya Siri ya Mtungi kama itaweza kung’ara kwa kunyakua tuzo, pamoja wa walioshiriki wakiwania tuzo mbalimbali.

Mbali na tamthilia hiyo msanii Juma Rajabu (Cheche), aliyeigiza kwenye filamu hiyo  anawania Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume akichuana na waigizaji wengine watatu kutoka nchi tofauti za Afrika.

Meneja Uhusiano wa MultiChoice (Tanzania), inayoratibu mashindano hayo, Barbara Kambogi alisema kuwa kazi kubwa iliyopo mbele ni Wananchi kuhakikisha wanampigia kura mshiriki wa Tanzania katika tuzo hizo kubwa za filamu barani Afrika.

Kwa mujibu wa Kambogi wadau wa filamu na Watanzania kwa jumla cha wanaweza kupiga kura kadiri wawezavyo kabla ya kufungwa kwa hatua hiyo Machi tatu mwaka huu.

Multchoice imebainisha kuwa tuzo hizo zitatolewa Machi nane na kwamba zitaonyeshwa moja kwa moja kutoka Lagos, Nigeria na DSTV, pamoja na GOtv.

Kupiga kura

Kambogi alitaja namba za kumpigia kura Cheche akieleza kuwa wadau na Watanzania wanatakiwa kutuma neno 2a kwenda namba +2783142100415 au kwenye mtandao-> htt:// goo.gl / o72lu5. “Unaweza kumpigia kura mara nyingi zaidi kila baada ya saa moja kama Mwigizaji Bora wa kiume kwenye Tamthilia,” alisema Kambogi.

Tuzo zinazoshindaniwa

Multchoice ilizitaja tuzo zitakazoshindaniwa katika AMVCA kuwa  ni 28, kukiwa na vipengele  26  kimoja kipya ambacho ni maalumu kwa ajili ya kutambua na kuheshimu watu waliotoa mchango muhimu kwa kujenga enzi mpya katika filamu barani Afrika kiitwacho Era.

Baadhi ya tuzo hizo ni Mwigizaji Bora wa Kike wa Drama, Mwigizaji Bora wa Kike kwenye Filamu za Vichekesho, Mwigizaji Bora wa Kusaidia katika Filamu za Drama, Mwigizaji Bora wa Kiume wa Filamu za Vichekesho, Filamu Fupi Bora, Mwandishi Bora wa Filamu za Vichekesho, Mtayarishaji Bora wa Filamu, Mhariri Bora wa Video na Filamu Bora ya Vichekesho.

Siri ya mtungi yapenya vipengele saba
Kwa mujibu wa Multchoice filamu ya Siri ya Mtungi, imefanikiwa kujitokeza katika kuwania  tuzo kwenye vipengele saba vya mashindano hayo huku pia washiriki wake wakiwania tuzo.

Vipengele hivyo ni pamoja na; Tuzo ya Mwigizaji Bora kwenye Drama, ikiwakilishwa na Juma Rajabu, Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Filamu za Vichekesho, Filamu Bora iliyotumia lugha kiufasaha (Kiswahili) na Mwandaaji Bora Mwenye Kipaji (Kyle Quint).

Pia imejitokeza kuwania Tuzo ya Mhariri Bora wa Sauti aikiwakilishwa na Jordan Riber, Tuzo ya Mbunifu Bora wa Mavazi (Doreen Estanzia Noni) na Tuzo ya Mpambaji Bora ikiwakilishwa na Rehema Samo


YANGA YAFANYA MAUAJI YAICHAPA RUVU SHOOTING, YAITANDIKA MABAO SABA

$
0
0
Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imefanya mauaji kwa Timu ya Ruvu Shooting,  imeikandamiza mabao 7-0. Ruvu Shooting 
Wafungaji wa mabao ya Yanga, hivi punde ni Emmanuel Okwi, ambaye amepiga 1 mpaka sasa, Ngassa 1, Kavumbagu 2, Msuva 2 na Kiiza 1. 



MAJINA YA WASICHANA NA WAVULANA 10 BORA KWENYE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

$
0
0
Kwenye matokeo ya kidato cha nne Watahiniwa wa kike wamefanya vizuri kwa kuchukua nafasi saba kati ya 10 za juu, huku Shule ya Marian Girls ya Pwani ikiongoza kwa kuwa na wanafunzi wanne. 
Mwanafunzi aliyeongoza ni Robina Nicholaus wa Shule ya Marian Girls, akifuatiwa na Magrath Kakoko wa St Francis (Mbeya) wakati wa tatu ni Joyceline Marealle kutoka Shule ya Canossa (Dar es Salaam).
Wengine ni Safarina Mariki na Abby Sembuche wa Marian Girls, wakati wavulana pekee kwenye wanafunzi 10 bora ni Sunday Mrutu kutoka Anne Marie (Dar es Salaam) na Nelson Rugola Anthony na Emmanuel Mihuba Gregory wa Kaizirege (Kagera).


Wanaofuata ni Janeth Urassa kutoka Marian Girls (Pwani) na Angle Ngulumbi wa St Francis (Mbeya).




Wasichana 10 bora
Wasichana waliofanya vizur kwenye mtihani huo wameongozwa na Robina Nicholaus (Marian Girls), Magrath Kakoko (St Francis), Joyceline Leonard Marealle (Canossa), Safarina W Mariki, Abby T Sembuche na Janeth Urassa (Marian Girls).


Wengine ni Angle Ngulumbi (St Francis), Getrude James Mande wa Precious Blood (Arusha), Violet Mwasenga wa St Francis na Catherine Swai kutoka Marian Girls.


Wavulana 10 Bora
Wavulana waliofanya Vizuri ni Sunday Mrutu wa Anne Marie, Nelson Rugola Anthony na Emanuel Mihuba Gregory wote kutoka Kaizirege, Razack Hassan wa St Matthew’s (Pwani) na Hamis Msangi kutoka Eangles (Pwani).
Matokeo ya Kidato cha Nne
Matokeo ya Kidato cha Nne 2013/2014



Wengine ni Joshua Zumba wa Uwata (Mbeya), Brian Laurent na Mohamed Ally wa Marian Boys (Pwani), Shahzill Msuya wa St Amedeus (Kilimanjaro) na Shabani Hamisi Maatu wa Mivumon Islamic Seminary (Dar es Salaam).


Shule za serikali hoi

Matokeo ya kidato cha nne yanaonyesha kuwa shule kumi za kwanza ni za binafsi tu na shule za Serikali zimeanguka vibaya.


Shule bora ni St. Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Girls ya Dar es Salaam, Precious Blood ya Arusha, Canossa ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, Abbey ya Mtwara, Rosmin ya Tanga na Don Bosco Seminary ya Iringa.


Katika shule zenye watahiniwa chini ya 40 shule iliyoongoza Matokeo ya Kidato cha Nne ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, Thomas More Machrina ya Dar es Salaam, Mwanza Alliance ya Mwanza na Queen of Apostles Ushirombo Seminary ya Geita. 

Nyingine ni St Joseph Kilocha Seminary ya Njombe, Bethelsabs Girls ya Iringa, St Mary Junior Seminary ya Pwani, Maua Seminary ya Kilimanjaro na Hellen’s ya Dar es Salaam(Matokeo ya Kidato cha Nne).

SHILOLE AWASHANGAA WASICHANA WASIOPENDA KUVAA KUFULI

$
0
0
Msanii Shilole
STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa huwa anawashangaa wasichana wasiopenda kujisitiri kwa kuvaa nguo za ndani ‘makufuli’.

Akistorisha na paparazi wetu, Shilole alisema katika maisha yake anapenda sana kujisitiri kwa kuvaa chupi

hivyo anawashangaa wasanii wanaotembea bila kuvaa nguo hiyo huku wengine wakidai wakizivaa wanahisi kuwashwa kwa joto.

“Napenda sana kuvaa ‘kufuli’ na huwa ninapata shida sana kutokana na wasichana tena mastaa ambao hawavai eti wana aleji nazo, unajua mwanamke lazima ujisitiri, siwezi kutoka nyumbani bila kuvaa  nguo ya ndani

,” alisema Shilole.

TUKIO KATIKA PICHA AJALI MBAYA YATOKEA MIKESE MOROGORO LEO ASUBUHI

$
0
0
 Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund

 Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea
 Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka
Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto huo

AGNESS MASOGANGE AWAPAGAWISHA WAKAZI WA DODOMA KWA MAUNO YAKE-DOLA ZAMWAGWA

$
0
0

Agness masogange alikuwa kivutio kikubwa pale walipokuwa wakicheza kwenye uzinduzi wa Pub Moja huko Mjini Dodoma..Mapendeshee wa huko walimwaga dola kama njugu kufurahia alichokuwa anafanya Agness Jukwaani kwa kukata Mauno..

HATIMAYE HUDDAH MONROE AMTAJA MPENZI WAKE MPYA..HUYU HAPA

$
0
0
Aliyekuwa mwakilishi wa Kenya katika jumba la Big Brother msimu uliopita, Huddah Monroe ambaye pia alikuwa mpenzi wa rapper Prezzo, ametangaza kuwa kwenye penzi jipya na msanii mwingine wa Kenya aitwae Colonel Mustafa.

MREMBO AIBA SIMU NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI: APEWA KICHAPO CHA HATARI

$
0
0
MREMBO mmoja mkazi wa Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam (jina lake halikupatikana) mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuvamiwa na kudundwa baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mwanaume na kuificha sehemu zake za siri.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, awali mrembo huyo alikuwa akila bata na mwanaume aitwaye Hashim kwenye Baa ya Jassun Inn iliyopo maeneo ya Mabibo huku mwanaume huyo akiwa ametandaza simu zake za kisasa juu ya meza.
 
Imedaiwa kuwa wakati wakiendelea kuponda raha, Hashim alikwenda msalani kwa lengo la kujisaidia na kuacha simu zake mezani, aliporudi hakumkuta mrembo aliyekuwa akiponda naye raha na simu yake moja haikuwepo.
Jasho lilimtoka Hashim na kuwauliza watu waliokaa jirani alikoelekea mrembo huyo,” alisema shuhuda mmojawapo wa tukio hilo na kubainisha kwamba msamaria mwema mmoja alimweleza Hashim mwelekeo wa mrembo huyo.

Bila kuchelewa Hashim aliwakusanya wapambe wake na kuanza kumtafuta mrembo huyo na wakamnasa mita kama 150 kutoka Baa ya Jassun na kumuuliza kuhusu simu iliyokuwa mezani lakini alileta ubishi.
- GPL  

MTANZANIA SABRINA ABAKWA NA WANIGERIA WATANO CHINA, APOTEZA MAISHA

$
0
0
tori: Mwandishi Wetu
AMA kweli dunia hadaa, ulimwengu shujaa! Kumeibuka mchezo mchafu,


kuna Watanzania wanawachukua warembo nchini na kuwapeleka China kwa ahadi kwamba wanakwenda kufanya kazi saluni, wakifika kule wanawanyang’anya paspoti na kuwauza kwa wanaume (ukahaba), sasa yamemkuta Mbongo aitwaye Sabrina au Habiba, Ijumaa Wikienda lina mkasa wa kusikitisha.

Habari za uhakika kutoka kwa chanzo chetu nchini humo zilisema kuwa, Sabrina (24), alifariki dunia Alhamisi iliyopita kufuatia kubakwa na wanaume watano, raia wa Nigeria ambao wamo nchini humo kibiashara.

Tukio hilo lilijiri kwenye hoteli moja iliyopo kwenye Mji wa Guangzhou ambao umejaa wageni wengi, wakiwemo Watanzania.

SIKU YA TUKIO
Rafiki wa karibu wa Sabrina, Saada alisema siku ya tukio, marehemu akiwa katika harakati zake za kutafuta wateja alikutana na Mnigeria mmoja ambaye walipatana kulala wote kwa usiku mzima.
“Kumbe yule Mnaigeria alikuwa na wenzake wanne. Usiku walimwingilia wote kwa nguvu kwa kumbaka mpaka akapoteza maisha palepale. Ni ukatili mkubwa.

“Wale watu walipogundua Sabrina amekufa waliuchukua mwili wake na kuutupa chini kutoka ghorofa ya tano,” alisema rafiki huyo.

MAITI YAKUTWA HAINA FIGO, MOYO
Habari zaidi zilidai kuwa mpaka juzi (Jumamosi) madaktari waliokuwa wakiuchunguza mwili wa Sabrina waligundua hauna figo na moyo, jambo linalozidi kuzua hofu juu ya muaji yake.

NI BIASHARA ILIYOIBUKA CHINA?
Ilidaiwa kuwa nchini China imeibuka biashara ya viungo mbalimbali vya binadamu ambapo ili vipatikane ni lazima mwenye viungo hivyo auawe kwa njia yoyote.

SABRINA AFA, MGANDA APOTEA
Mtoa habari wetu alisema wakati Wabongo wakiwa kwenye maombolezo ya kifo cha Mtanzania huyo, mrembo mwingine raia wa Uganda, nchi ambayo imo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki amepotea katika mazingira ya kutatanisha nchini humo.

Baadhi ya watu wana wasiwasi kuwa kupotea kwa msichana huyo kunahusiana na kushamiri kwa biashara ya viungo vya binadamu.

SABRINA ALIKWENDAJE CHINA?
Mwezi Julai, mwaka jana, Sabrina alikwenda nchini humo akidanganywa na mwanamke mmoja kwamba atapata kazi kwenye saluni ya wanawake lakini baada ya kufika alijikuta akiingizwa kwenye biashara ya ukahaba bila ridhaa yake mpaka alipokutwa na mkasa huo uliopoteza maisha yake.

TAHADHARI KWA WAREMBO WANAOKWENDA CHINA KUFANYA KAZI SALUNI
Imebainika kuwa, kumeibuka wimbi la Wabongo wanaofanya ‘uwakala’ wa kuwachukua wasichana wa Kitanzania kwa kuwadanganya kwamba wanakwenda kufanya kazi za saluni nchini humo.

Mara baada ya kufika, wasichana hao hunyang’anywa paspoti ili washindwe kuondoka nchini humo na kushinikizwa kujiuza (ukahaba) huku waliowapeleka wakipokea fedha kutoka kwa wateja.

KUIKOMBOA PASPOTI
Habari zilisema kuwa mhusika hurejeshewa paspoti yake baada ya malipo yake kwa ‘wakala’ kufikia dola za Marekani 8,000 (kama shilingi milioni 12), ndipo huachiwa ‘huru’ kuendelea na maisha yake.

Wengi wakishaachiwa hushindwa kurejea Bongo na kujikuta wakiendelea kuuza miili katika mahoteli na klabu huku wakikutana na majanga mbalimbali.

MASOGANGE, KAJALA NA DIDA
Watanzania waishio nchini humo wamewatahadharisha mastaa wa Bongo, wakiwemo Mtangazaji wa Radio TimesFM, Khadija Shaibu ‘Dida’, msanii wa filamu Kajala Masanja na Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ ambao hupenda kwenda nchini humo kwa shughuli zao, kutokubali kuwa karibu na mawakala wa kuchukua wasichana Bongo kwa kuwadanganyia kazi ya saluni kwani wanaweza kujikuta pabaya siku moja.

DIDA
Ijumaa Wikienda lilimsaka Dida siku ya Jumamosi iliyopita na kumuuliza kuhusu kuwepo kwa mawakala hao ambapo alikiri kusikia huku akisema warembo wenyewe wanapaswa kuwa macho na udanganyifu huo.

“Najua wapo Wabongo wanaofanya shughuli hiyo, si China tu hata India, unapelekwa kwa ahadi ya kazi ya saluni, ukifika hamna cha saluni wala nini? Warembo wawe makini jamani, nenda China kama una uwezo wako mwenyewe kufanya ‘shoping’ lakini si kupelekwa,” alisema Dida.



BALOZI WA TANZANIA-CHINA
Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Balozi wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo ili azungumze lolote kuhusu tukio la Sabrina, lakini simu yake ilionekana kutokuwa hewani kwa muda mrefu.

Source: GPL

ILE NYONGEZA YA POSHO WANAO DAI WABUNGE WA KATIBA YAGONGA MWABA

$
0
0
Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba, Mwananchi limebaini.

Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.

Taarifa hizo zilidai kuwa wajumbe hao wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia viwango vya posho vinavyolipwa na  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na Mashirika ya Umma.

Pia kamati hiyo ilichambua viwango vya posho walivyolipwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viwango vya posho ya kujikimu vya Sh80, 000 kwa siku wanavyolipwa watumishi wa Serikali.

 “Hili jambo linahitaji busara sana na kutazama mazingira ya nchi pia, kwa hiyo wajumbe wale baada ya kuoanisha viwango vya posho vya taasisi mbalimbali wameona Sh300,000 zinatosha,” alisema mmoja wa wajumbe ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Mjumbe mwingine, ambaye pia hakutaka kutajwa, alisema kuwa watakaa leo kukamilisha taarifa ya utafiti wao, kabla ya kuikabidhi kwa Mwenyekiti Kificho.

Alisema pamoja na umuhimu wa kazi za mbunge, lakini isingekuwa rahisi kuongeza posho katika mazingira ya sasa, ambapo wananchi wanalia hali ngumu ya maisha.

Wajumbe hao walioteuliwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho ni William Lukuvi, Mohamed Abood Mohamed, Freeman Mbowe,  Paul Kimiti, Jenister Mhagama na Asha Bakari.

Awali, taarifa kutoka ndani ya Bunge zilidokeza kuwa wajumbe hao walikuwa wakutane jana saa 9:00 alasiri ili kuandaa ripoti itakayopelekwa kwa Kificho ikiwa imebeba ushauri kuwa kiwango cha sasa cha posho kinatosha.

Sh300,000 wanazolipwa wajumbe wa Bunge Maalamu la Katiba zinajumuisha Sh80,000 kwa siku ambayo ni posho ya kujikimu na Sh220,000 kwa siku kama posho maalumu ya kuhudhuria kikao.

Posho maalumu ya Sh220,000 inajumuisha posho ya dereva inayopaswa iwe kati ya Sh40,000 na Sh45,000 kwa siku, usafiri wa ndani (mafuta ama teksi), mawasiliano na matumizi mengine binafsi.

Ofisi ya Bunge Maalumu
Alipoulizwa kuhusu jambo hilo mmoja wa makatibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alisema suala la posho linashughulikiwa na Serikali.

“Ninachokifahamu ni kuwa suala la posho limetoka mikononi mwa Kificho na sasa lipo serikalini. Kamati iliyoundwa bado inalishughulikia suala hilo. Hicho ndiyo ninachokifahamu,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi.

Kwa nyakati tofauti gazeti hili lilimtafuta Kificho, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya kuzungumzia suala hilo, lakini simu zao za mkononi zilikuwa zikiita bila majibu.

Hoja ya kutaka nyongeza ya posho iliibuliwa na wajumbe wawili ambao ni wabunge wa CCM waliodai kuwa kiwango cha Sh300,000 wanacholipwa, hakitoshi kwa kile walichodai kuwa ni kuishi Dodoma ni gharama kubwa.

Hata hivyo uchunguzi wa kina umebaini kuwa baadhi ya wajumbe wanaishi katika hoteli za kati ya Sh20,000 na Sh40,000 kwa siku huku baadhi yao wakiishi katika hosteli kwa Sh8,000 kwa siku.

Mmoja wa wajumbe, Augustino Mrema alidai kuwa baadhi ya wajumbe wanataka kuligeuza Bunge hilo ‘shamba la bibi’ kwa kudai posho zaidi kwa kisingizio cha kupanda gharama za maisha.

Mrema alisema kiasi cha Sh300,000 wanacholipwa wajumbe kinatosha kwani zipo hoteli nzuri za kati ya Sh15,000 hadi Sh40,000 ambazo zina hadhi na sifa ya kuishi wajumbe wa Bunge la Katiba.

“Mjumbe ameamua kwenda kuishi chumba cha Sh200,000 wakati akijua atalipwa posho ya Sh300,000 halafu analalamika kupanda kwa gharama za maisha, hizi gharama zimetengenezwa,” alisema Mrema.

Alisema gharama za teksi kutoka bungeni hadi maeneo ya Area C na D haizidi Sh12,000 wakati chakula kinaanzia Sh6,000 hadi Sh20,000 na kuhoji iweje Sh300,000 zionekane hazitoshi.

Hoja ya baadhi ya wajumbe kudai posho zaidi imepigiwa kelele nchi nzima huku wananchi wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge hilo, kama wataendelea kung’ang’ania kupanda kwa posho.

Mjumbe mwingine wa Bunge hilo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro ameahidi kuanzia leo kukusanya saini za wajumbe wanaopinga suala hili ili ampelekee Rais Kikwete kama ushahidi.

SITTA:NAGOMBEA UENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA KUTIMIZA NDOTO YA RAIS

$
0
0
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema atagombea uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu anaamini kuwa ana sifa za kutosha.

Hii ni mara ya kwanza kwa Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa kuweka wazi uamuzi wake huo. Mwingine anayetajwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.

Sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni kuwa na shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambulika pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema pamoja na propaganda chafu zinazoenezwa dhidi yake, hatakata tamaa na kwamba ataendelea na msimamo wake huo ili nchi ipate Katiba bora.

“Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu njama za kumzuia asigombee nafasi hiyo, Sitta alisema “Haishangazi watu hao kutumia mbinu chafu… Hawana maadili, ndiyo maana wananihofia lakini sishtuki hata kidogo.”

Sitta ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema wabaya wake wamekuwa wakieneza maneno ya uongo kwamba ikiwa atakalia kiti hicho, atasimamia mpango wa Serikali tatu.

“Wanasema Sitta ataruhusu Serikali tatu, sasa nashangaa maana wajumbe ndiyo wenye mamlaka hayo… wanaeneza propaganda kuwa nina mkataba na wapinzani ndiyo maana wananiunga mkono. Wanasema mambo ya ovyo kabisa,” alisema.

Sitta alisema wapinzani kama walivyo wajumbe wengine kutoka CCM na makundi mengine, wanamuunga mkono kwa kuwa wanaamini akikalia kiti hicho ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi na haki.

“Mimi sina mkataba na wapinzani ila wao kama watu wengine wananiunga mkono kwa sababu wanajua nitatenda haki, nina rekodi nzuri katika kuliendesha Bunge la Tisa wala hiyo haina mashaka,” alisisitiza Sitta.

WOLPER GAMBE AJIANIKA LIVE AKIFANYIWA MASAJI

$
0
0
MAKUBWA! staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejianika akifanyiwa masaji laivu. Wolper a.k.a Gambe ‘alifanya yake’ ndani ya saluni (massage parlor) moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar. Mara baada ya tukio hilo huku akiwa ‘amefotolewa mapicha’ ambayo aliyatundika kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwanadada huyo alielezea jinsi alivyohisi raha ya ajabu wakati akifanyiwa masaji. “Asante…(akitaja jina la saluni), kwa raha niliyopata leo…, mi siyo mchoyo kwa kweli karibuni nanyi mpate afya. Nimefurahia walah,” aliandika Wolper. Hata hivyo, tukio hilo liligeuka gumzo huku baadhi ya mashabiki wakimsifia na wengine wakimponda.

KINACHOWAPONZA WANAWAKE WENGI NI MAAMUZI DUNI KWENYE MAMBO YA MSINGI..ONA HII

$
0
0
LABDA HII ITAWASAIDIA:
Kinachowaponza Wanawake ni POOR DECISION MAKING IN CRITICAL ISSUES.
Unakuta mtu anajua kabisa ana Boyfriend Levi la Kutupwa,analala mtaroni kila siku,anafikishwa nyumbani hajitambui kafikaje,yeye yupo tu amekazana na Fanta yake..Unachumbiwa na kuolewa na hilihili levi,unasota nalo miaka 2 ya ndoa inakuwa kero...Ulimvumilia kwenye Uchumba coz hamkuwa mnalala pamoja,analewa na kutapika akiwa kwake na wewe uko kwenu..Sasa Mzigo ni wako,mko SAME BED..Anatapika hapo..Harudi home siku 4..Na hata akirudi yuko Njwii,hata 'kazi hawezi kupiga'
Unaenda kulalamika kwa Mchungaji kuhusu Tabia mbaya ya mmeo...YOU KNEW IT..Ukapuuzia na ukakubali kuolewa na JANGA...Mtabaki kusumbua Wachungaji na Wakwe kuwapatanisha wakati mlikuwa na Muda wa kujuana kabla hamjaamua kuishi pamoja
Kipindi cha Uchumba kitumie KUMFAHAMU VIZURI..Sio ukitumie KUMCHUNA,KULA BATA,OFA ZA KITIMOTO,TRIP ZA BAGAMOYO,KUMPIGA MIZINGA YA PERUVIAN HAIR..Ukasahau KEY ISSUES...Mmekaa miaka 6 ana watoto 2 na Wanawake wengine..Analewa na kulala mtaroni..Halafu analeta Posa unasema kuolewa ni Bahati.
Yakikushinda Usitusumbue...Sio kila POSA ni bahati,Posa nyingine ni kichaka tu cha kutua majanga yao...Your Decision TODAY will affect your TOMORROW...Think twice before you say YES to a Problem.
By Seth De Jesus

HUYU HAUSGELO SIMTAKI HAJUI KUPIKA WALA KUFAGIA ANAEMTAKA AWEKE COMMENT HAPA TUWASILIANE NIMKABIDHI

$
0
0
KATIKA MAHAUSGELO bom huyu wa kwanza hajui kupika wala kufua, sioni sababu hata moja ya kumlipa hii alfu hamsini kwa mwezi, anaemtaka anambie kwenye comment nimkabidhi maana nilimtoa kijijini kwao alipomaliza la saba nikajua atanisaidia kumbe hakuna kitu. Nirudishiwe nauli tu ya kumtoa kijijini. Asante kwa kunisikiliza

LULU ADAIWA KUKUWADIWA NA STEVE NYERERE!

$
0
0
Stori: Mayasa Mariwata
OOHOOO! Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekwaa skendo ya kudaiwa kukuwadiwa na mwigizaji mwenzake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kwa mwanaume anayedaiwa kutoka naye kimapenzi kwa sasa anayetajwa kwa jina moja la Johnson

Chanzo makini kilipenyeza ‘upupu’ huo ambao umefafanuliwa na Steve Nyerere kuwa ukaribu wa Lulu na bosi huyo umetokana na kazi kwani yeye na Lulu wameingia mkataba hivyo walitegemea kusikia manenomaneno.

Lulu alipotafutwa kuhusiana na ishu hiyo, alitiririka: “Wabongo wanapenda sana kuzusha mambo, sijawahi kuwa na mwanaume anayeitwa Johnson  zaidi ya kuwa bosi wangu.”
GPL

NYALANDU AMTIMUA MKURUGENZI WA IDARA YA WANYAMA PORI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu, amemtimua Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa; kwa utendaji kazi mbovu na kushindwa kudhibiti vitendo vya ujangili. Amekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda usiozidi mwaka mmoja akiwa amechukua nafasi ya Obeid Mbangwa. Hii Wizara ni mwiba wenye sumu!
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images