Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

CCM Yakerwa na Marekani Kuzuia Mabilioni ya Msaada

$
0
0
Wakati Chama cha Mapinduzi kinapinga uamuzi wa Marekani wa kusitisha msaada kwa Tanzania wa tilioni 1.5 kutokana na kufutwa kwa matokeo ya Uchauzio Mkuu wa Zanzibar, Chama cha Wananchi CUF kimeunga mkono uamuzi huo na kutaka mshindi wa urais wa Zanzibar atangazwe na kuapishwa ili kuondoa vikwazo vya kiuchumi.

Msimamo huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi (CUF),  Ismail Jussa Ladhu jana alipokuwa akizungumzia uamuzi wa Marekani kuzuia fedha za MCC hadi muafaka wa uchaguzi utakapopatiwa hufumbuzi pamoja na kuondoa sheria kandamizi ya makossa ya mitandao.

Jussa alisema hakuna njia ya kunusuru Tanzania kuwekewa vikwazo vya kiuchumi ikiwemo kunyimwa misaada zaidi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar kukubali kukamilisha uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.

Aidha alisema kuwa uamuzi wa Marekani wa kuzuia msaada unatoa fundisho kubwa kwa nchi nyigine kuheshimu mashariti ya kunufaika na fedha za MCC ikiwemo kulinda misingi ya Demokrasia na Utawala bora.

Jussa alisema matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar yalifutwa kwa ubabe na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar baada ya kuona CCM wapo katika hatari ya kuanguka lakini hakuna kifungu cha Katiba kinachompa uwezo huo.

Alisema msimamo wa CUF utaendelea kubakia palepale pamoja na kufanyika kwa mazungumzo ya kutafuta muafaka wa uchaguzi, ZEC warudi kazini wakamilishe kuhakiki na kutangaza matokeo na mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.

Alisema kuwa kuna kikundi cha watu wachache Zanzibar ndiyo hawataki kuona mabadiliko yakitokea ya kiutawala Zanzibar licha ya CCM kushindwa kufikia malengo ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

“Kuna kikundi cha watu Zanzibar hakitaki kuona mabadiliko ya kiutawala kwa maslahi yao binafsi licha ya CCM kuanguka katika uchaguzi wa Oktoba 25 Mwaka huu,”alisema Jussa.

Alisema kuwa kadhia ya uchaguzi wa Zanzibar imesababisha madhara makubwa ikiwemo wananchi kuishi katika mazingira ya wasiwasi pamoja na kupanda kwa gharama za maisha visiwani humo.

Jussa alisema hakuna sababu kwa Viongozi wa CCM kuwa na wasiwasi wa kupoteza vyeo wakati marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar yameweka mfumo mzuri wa kuunda serikali ya pamoja na wao kunufaika kama CUF ilivyonufaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Aidha, alisema CUF haiko tayari kuona Uchaguzi Mkuu unarudiwa Zanzibar kwa malengo ya kuibeba CCM licha ya kuanguka katika uchaguzi wa awali Visiwani humo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, alisema kuwa haikuwa mwafaka kwa Marekani kuzuia msaada huo wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ilikuwa na hoja za msingi za kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 Mwaka huu.

Alisema kuwa uchagfuzi wa Oktoba 25 Mwaka huu ulipoteza sifa za kuwa uchaguzi huru na wa haki baada ya kutawaliwa na vitendo vya udaganyifu kinyume na misingi ya demokrasia na utawala bora.

Alisema hana wasiwasi na Marekani kuwa hawajapata taarifa na vielelezo vya kuharibika kwa uchaguzi wa Zanzibar na iwapo watapata taarifa hizo watakubaliana na uamuzi wa ZEC wa kufuta matokeo ya uchaguzi huo.

Alisema  uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya udaganyifu ikiwemo idadi ya wapiga kura kuzidi watu waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura wa kudumu pamoja na mawalaka wa vyama kupigwa na kufukuzwa katika vituo vya kazi.

“Ufumbuzi wa migogoro sio kuzuia misaada kwa sababu unawaumiza hadi watu wasiokuwa na hatia, cha muhimu ni  kutafuta njia ya mufaka za kuondoa matatizo.”alisema Vuai.

Aunty Ezekiel na Moses Iyobo Waamua Kufanya Maamuzi Magumu Kuhusu Kupata Mtoto wa Pili....

$
0
0
Aunty Ezekiel na Mtoto wake Cookie
Staa maarufu wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amefungua kinywa chake na kusema kuwa kwa sasa yuko kwenye mchakato wa kumtafuta mdogo wake na Cookie kwa kuwa hataki kukaa muda mrefu ili kupata mtoto mwingine.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni Aunty,alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa anaona kuzaa mapema na kumaliza ndiyo poa ili aweze kuendelea na kazi zake vizuri kuliko kukaa muda mrefu halafu ndiyo ubebe ujauzito tena.

“Sasa hivi mimi na baba Cookie tumeshaamua kufanya maamuzi mazuri kabisa ya kuongeza mtoto mwingine maana tumeona kwanza ndiyo furaha yetu kubwa na kitu kingine tukizaa haraka ni vizuri zaidi tunaweza kufanya kazi zetu kwa ajili ya kusomesha na si kufikiria kuzaa tena,” alisema Aunty.

Ufisadi:Kigogo Wa Ikulu Adaiwa Kutumia Fedha za Umma ( Laki 8 ) Kufanya Masaji

$
0
0
Harakati za kuwasaka wabadhirifu wa fedha za umma ili waingie kwenye msululu wa opareshini ya kutumbua majipu iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano zimeibua tuhuma nyingine zinzomhusu moja kati ya vigogo anayeiwa kuwa mfanyakazi wa Ikulu.

Taarifa zilizochapishwa katika gazeti la MwanaHalisi zinaeleza kuwa uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo umebaini nyaraka zinazoonesha kigogo huyo alitumia fedha za walipa kodi kiasi cha shilingi 821,997.24 kwa ajili ya kufanyiwa huduma ya kukandwa mwili (massage), katika hotel ya kifahari ya Four Seasons Safari Lodge iliyoko ndani ya mbuga za wanyama za serengeti, Arusha.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, stakabadhi waliyoipata katika hotel hiyo ilionesha kuwa kigogo huyo alifika hotelini hapo April 17 mwaka huu tarehe ambazo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa na ziara jijini Arusha.

Imeelezwa kuwa kigogo huyo ambaye hotel hiyo haikutaka kumtaja jina alilala katika chumba namba 9017 na alikuwa na mrembo wake ambaye kwa pamoja walipata huduma zilizoingizwa kwenye stakabadhi iliyolipiwa na Ikulu.

Mbali na huduma ya Massage, huduma nyingine zilizoorodheshwa nakala ya ankara hiyo ni usafi wa nguo ambao uligharimu shilingi 676,000.

Katika kutafuta kujiridhisha, gazeti hilo lilimpigia simu afisa wa hotel ya Four Seasons Safari Lodge ambaye licha ya kukataa kutoa maelezo alikiri kuwapokea baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu katika siku tajwa.

Licha ya Kuinyima Tanzania Dola Milioni 472....Spidi ya Rais John Magufuli Yatinga Kwa Obama

$
0
0
Licha ya Serikali ya Marekani kuinyima Tanzania Dola za Marekani milioni 472 (Sh.bilioni999.4) kutokana na kushindwa kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar, lakini imekunwa na kasi ya Rais John Magufuli katika kupambana vita dhidi ya ubadhilifu na rushwa.

Bodi ya MCC iliyokaa kikao chake Desemba 16, mwaka huu, iliamua kutopigia kura mkataba unaopendekezwa kati ya MCC na Tanzania kutokana na kutofurahishwa na kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na kukamatwa chini ya kivuli cha Sheria ya Matumizi ya Mtandao kwa wanaharakati kadhaa Oktoba mwaka huu.

Uchapakazi wa Rais Magufuli kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani tangu Novemba 5, mwaka huu mara baada ya kuapishwa, umekuwa gumzo kubwa katika baadhi ya nchi barani Afrika na Ulaya kutokana na kasi yake ya utendaji na kuwaacha viongozi wa nchi hizo kwenye wakati mgumu.

Mojawapo ya marais ambao wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi wake kutokana na kasi ya Rais Magufuli ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata. Kenya ambayo imekuwa ikifuatilia siasa za Tanzania tangu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, imeonyesha kupenda mbinu za Rais Magufuli na wananchi wake wanatamani mtu kama yeye.

Nchi nyingine ni Afrika Kusini, Gazeti la The Sunday Independent linalochapishwa nchini humo, liliwahi kuandika katika tahariri yake hivi karibuni ikiwa na kichwa cha habari kisemacho, “Afrika ifuate mfano wa Tanzania.”

Pia sehemu ya tahariri hiyo ilidokeza kuwa Afrika inahitaji Rais kama Magufuli ambaye ameonyesha kwa dhati nidhamu katika matumizi ya serikali. Vilevile nchi za Ghana, China nazo zimesifu uchapakazi wa Rais Dk. Magufuli.

Marekani kupitia Balozi wake nchini, Mark Childress, imeonyesha kufurahishwa na utendaji wa Rais Magufuli katika nyanja hiyo ya utumbuaji majipu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Balozi Childress alieleza kuwa Marekani kupitia Shirika lake na MCC imetiwa moyo na hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Rais Magufuli za kuimarisha vita dhidi ya ubadhilifu na  rushwa.

“MCC imetiwa moyo na hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Rais Magufuli za kuimarisha vita dhidi ya ubadhirifu na rushwa. MCC inatumaini kuwa jitihada hizo zitaendelea na kuleta mabadiliko ya kimfumo,” alisema.

Balozi huyo alieleza kuwa MCC inatumaini kuwa jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli kwa sasa zitaendelea na kuleta mabadiliko ya kimfumo.

Rais Magufuli, Novemba 6, mwaka huu, siku moja mara baada ya kuapishwa, alifanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha (Hazina) kwa kutembea kwa miguu na kutowakuta wafanyakazi wa wizara hiyo ofisini kitendo kilichomkera.

Mbali na kufanya ziara katika wizara hiyo, Rais Magufuli Novemba 9, mwaka huu alifanya ziara ya kushtukiza katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako baada ya kushuhudia uozo mwingi alichukua hatua ya kufuta bodi ya wakurugenzi ya hospitali hiyo na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto.

Rais Magufuli pia Novemba 7, mwaka huu alitangaza kufuta safari za nje za watumishi wa serikali hadi pale atakapotangaza utaratibu mpya.

Alichukua uamuzi wa kufuta safari hizo kutokana na kuwapo kwa matumizi makubwa ya fedha kwa watumishi wa serikali walioko katika wizara, taasisi na idara za serikali ambao wamekuwa wakijipangia safari bila ya utaratibu maalum.

Baada ya kufanya uamuzi huo, Rais Magufuli alieleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje.

Siku chache baada ya kutoa agizo hilo,  Rais Magufuli alifyeka msafara wa watumishi wa serikali 50 na kubakia wanne waliokuwa waende katika mkutano wa Jumuiya ya Madola na kuokoa takribani Sh. milioni 700 ambazo zinadaiwa zingetumika kwa watumishi hao katika safari hiyo.

Vilevile, Rais Magufuli Novemba 23, mwaka huu alifuta sherehe za Uhuru na badala yake akaamuru Desemba 9 itakuwa siku ya kufanya usafi nchi nzima ili kuondokana na tatizo la kipindupindu linaoikabili nchi.

Uamuzi wake huo uliokoa zaidi ya Sh. bilioni nne ambazo zilkuwa zitumike katika sherehe hizo na kuelekeza zitumike kupanua barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam kipande cha kutoka Morocco kwenda Mwenge.

Mbali na kufuta sherehe hizo, Rais Magufuli pia alipiga marufuku uchapishaji wa kadi za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa gharama ya fedha za umma na kuagiza kila wizara ijigharamie fedha zake katika kufanya shughuli hizo.

Pia Novemba 20, mwaka huu Rais Magufuli aliagiza zaidi ya Sh. milioni 200 zilizokuwa zitumike kwa ajili ya sherehe za uzinduzi wa Bunge la 11 zitumike kununua vitanda vya wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Rais Dk. John Magufuli Novemba 27, mwaka huu alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza bandarini na kubaini upotevu wa makontena 349 ambayo yalitoroshwa bandarini hapo bila ya kulipiwa kodi na kusababisha serikali kukosa mapato ya Sh. bilioni 80.

Mbali na kumsimaisha Kamishna huyo, Desemba 16, mwaka huu, Rais Magufuli alimwondoa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah kwa kile alichoeleza kuwa kutoridhishwa na namna taasisi hiyo ilivyokuwa ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika Bandari ya Dar es Salaam.


CHANZO: NIPASHE

Hatma ya Sakata la Dk. Mwaka Kujulikana Leo au Kesho

$
0
0
Hatma ya mtabibu anayemiliki kituo cha afya cha tiba mbadala cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala, jijini Dar es Salaam, Dk. Mwaka Juma, itajulikana leo au kesho baada ya serikali kukagua uhalali wa nyaraka zake, ikiwamo cheti cha taaluma ya utabibu.

Hatua ya serikali kumkagua daktari huyo imekuja baada ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hamis Kigwangalla, kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho cha afya Desemba 14, mwaka huu na kutomkuta Dk. Mwaka na baadhi ya wafanyakazi wanaohusika na utoaji wa tiba.

Hali hiyo ilimshtua Dk. Kigwangalla baada ya kukuta msururu wa wagonjwa wakisubiri kuhudumiwa huku watoa huduma wakiwa hawapo kituoni hapo, ndipo alipotoa agizo la kuchunguzwa kwa kituo hicho na Dk. Mwaka mwenyewe.

Dk. Kigwangalla pia alitoa amri ya kufungwa kwa muda kwa kituo hicho mpaka uchunguzi wa kina utakapokamilika ili kuona kama huduma zinazotolewa zinakidhi vigezo na ni salama kwa wagonjwa.

Akizungumza na Nipashe jana, Dk. Kigwangalla alisema serikali imeshapokea vyeti vya daktari huyo na kuvikagua kama anastahili kutoa huduma hiyo ya tiba asilia ama la.

Alisema alikabidhiwa ripoti ya Dk. Mwaka Ijumaa iliyopita inayoelezea taaluma yake na kwamba atakapomaliza kuipitia atatoa tamko kuhusiana na hatma ya Dk.Mwaka kupitia mkutano na vyombo vya habari. 

“Suala hilo nitalitolea tamko kesho (leo) au keshokutwa, itategemeana na ratiba yangu… kwa kuwa ripoti niliipokea Ijumaa lakini sikuimaliza kuisoma kutokana na majukumu mengine ya kikazi,” alisema.

Kuhusiana na masuala ya tiba asilia kwa ujumla, Dk. Kigwangalla alisema serikali haizuii bali inawaachia wananchi wenyewe waamue kama zinawasaidia au la.

Alisema masuala ya tiba ya asilia ni imani ya mtu mwenyewe, hivyo jukumu la serikali ni kuhakikisha kunakuwapo na usalama wa tiba hizo na sheria na taratibu zilizopo zinazingatiwa.

Alisema watoaji wa tiba asilia wengi hawafuati mashariti ya utoaji wa dawa hizo na baadhi hukiuka miiko ya utoaji tiba.

Nipashe ilimtafuta Dk. Mwaka jana ili kupata maoni yake kuhusiana na uchunguzi wa nyaraka zake lakini simu yake ya mkononi ilipokewa na mtu mwingine aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake,  ambaye hata hivyo hakutaka kuzungumzia suala hilo.

Maneno Haya ya Lulu Kwenye Picha Hii ya Waacha Hoi Mashabiki Wake

$
0
0
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa Instagram staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewaacha watu hoi baada ya kubandika picha hiyo hapo chini ikimuonyesha yeye na baba yake mzazi ‘Mzee Michael’ na kummwagia sifa baba yake huku akiomba dua aje kuzaa mtoto atakaye fanana na baba yake (Mzee Michael) kitendo ambacho kila shabiki yake mtandaoni alikuwa na yake ya kusema.

Le Mbebe…! Le Super Handsome...Le Twinnie💖💖💖
Mzaa Chema…Mzee Michael..!!!
Ewe Mtoto Wangu WA Kiume Popote ulipo Kama tumboni Kama kwenye mayai ya Uzazi au popote…Tafadhali rithi Kwa Babu yako utakapokuwa tayari kuja🏃🏃🏃”-Haya ndiyo maneno aliyoandika Lulu.

Ila ni kweli wamefafana.

Sakata la TBC Kurusha Harusi Live: Mtaalam wa Habari na Aliyefanya Kazi Hapo Afanunua Kama ni Kosa!

$
0
0
Serikali imeliagiza shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoa maelezo ya kina baada ya kurusha matangazo ya moja kwa moja sherehe za harusi kwa zaidi ya saa mbili, jambo lilihojiwa na wananchi maeneo mbalimbali hasa katika mitandao ya jamii.

Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kupata malalamiko mengi kwa kile kilichokuwa kinarushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1 cha shirika hilo linaloendeshwa kwa ruzuku kutoka Serikalini.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alibainisha kuwa amepokea simu za watu wengi waliokuwa wanahoji juu ya kipindi hicho, hivyo kulazimika kuchukua hatua mara moja za kutaka maelezo kutoka kwa watendaji wa shirika hilo.

Chini ni maelezo ya mtaalam wa habari na aliyefanya kazi hapo:

Wadau, kwanza naomba ku declare interest, kuwa sikubahatika kuiona hiyo live ya harusi binafsi ya mtu!. Pili mimi ni mdau wa broadcast journalism, na niliwahi kufanya kazi TBC enzi zile ikiitwa TVT, ila hapa sichangii kama an authority by as an experienced broadcast journalist!

Naomba nitofautiane na wengi, kuwa TBC inaweza kuonyesha live ya kipindi chochote ambacho kinaonyeshwaga kikiwa recorded, hii ina maana kama TBC wanarusha kipindi cha Chereko, kikionyesha sherehe binafsi za watu, then mtu akifika bei, Chereko inaweza kwenda live kwenye event yoyote, iwe ni harusi, send off, kitchen party, ubarikio, au hata birthday ya mtu, provided ili live itatumia muda ule ule wa recored program, na kama itabidi ku extend time, isile muda wa more serious na relevant programs simply because mtu ana fedha za kulipia!

TBC nayo japo ni kituo cha TV kama vilivyo vituo vingine vyote vya TV, nayo inayo haki ya kufanya biashara, kama TV nyingine zote zinazovyofanya biashaa, na ina kipindi cha Chereko kinachoonyesha harusi za watu, then kama mtu ana pesa kulipia, then why TBC ikatae pesa?!, lakini suala la kurusha matangazo ya live, it is not about money on who can pay, but the contents and national interests, nadhani TBC wangeirusha hiyo live muda ule ule wa Chereko na baada ya hapo vipindi vingine vikaendelea kama kawaida, sidhani kama kungekuwa na any basis ya malalamiko, kwa sababu live social events za public figures, prominent people na super stars zinafanyika kwenye tv duniani kote japo not on public TV.

Dr. Buberwa nimefanya naye programs, hana tofauti sana na Renatus Mkinga, au Mchungaji Mtikila (RIP), kuhusiana na soundness of the state of their minds!, hivyo kitendo tuu cha mtu kulipia live ya harusi yake alone, kilitosha ku sound alarm kuhusu tuning a pivate function into a state function, mimi ndio ningekuwa producer, ningekuwa very careful to make sure live inahusisha kuonyesha events tuu na kamwe nisingithubutu kurusha live kitu chochote atakachoongea Buberwa.

Mwisho, hili la TV ya taifa kufanya biashara linahitaji mjadala wa kujitegemea, BBC World Service, haifanyi biashaa, na haipokei tangozo lolote la mtu yoyote zaidi ya public announcements, lakini iko funded 100% na public, mtu yoyote ukiisha kanyaga tuu ardhi ya UK, unailipia BBC utake usitake!, na sisi tufike mahali, TBC yetu iwe funded 100% ili isihitaji sentano ya mtu, na kugawa majukumu into diferent channels say TBC 1 iwe ni nationa interest, TBC 2 comercial, ifanya biashara, TBC 3, elimu, TBC 4, Afya, TBC 5 kilimo, uvuvi na ufugaji, TBC 6 watoto, TBC 7 michezo, TBC 8 miziki etc, etc.
Pasco

Dr. Kigwangalla Ajibu Malalamiko ya Wananchi Kuhusu Sakata la Kuwafungia Watumishi Wachelewaji Geti

$
0
0
Ndugu zangu,
Tunaweza kuibadilisha nchi yetu tukiamua. Wiki iliyopita nili-observe namba ya mahudhurio ofisini na namna watumishi wanavyowasili, nikashangazwa kwamba Waziri wangu, Mhe. Ummy Mwalimu (MB), Katibu Mkuu, CMO - Mganga Mkuu wa Serikali na mimi tunawahi kila siku. Wafanyakazi wenzetu wengi wanachelewa!

Nikamuomba ruhusa Mkuu wangu wa kazi, Mhe. Ummy, kuwa nichukue hatua. Akanisikiliza akanielewa. Akaniruhusu. Nikatazama sheria inasemaje kuhusu muda wa kuwasili kazini na utaratibu wake wa hatua za kinidhamu. Nikachukua hatua.

Watu wengi walikasirika. Walikerwa. Kila mtu alisema yake. Najua wengine walichukia. Sawa tu. Lakini wajue ‪#‎HapaKaziTu‬

Suala hili limezua mjadala mkubwa sana. Wengi wakiitupia lawama serikali wakidai wanaishi maeneo ya mbali na miundombinu ya usafiri siyo mizuri kuwawezesha kuwahi ofisini. Si jambo la kudharau ama la kutokutazamwa, la hasha. Hii ni hoja ya msingi kabisa. Lakini niseme wazi hapa kuwa haishindikani. Ili mimi binafsi niwahi ofisini kwangu saa moja za asubuhi, huamka saa kumi na nusu asubuhi kutokea kule Kijijini kwangu, natakiwa kuvuka Pantoni, na mara nyingi tu hulazimika kuvuka bila gari. Nikifika ng'ambo natembea tu Kwa miguu nawahi ofisini. Namfahamu Mkurugenzi mwingine wa hapa Wizarani, naye hufanya hivyo. Nafahamu Katibu Mkuu wa Wizara naye anaishi Salasala, lakini sijawahi kufika ofisini kabla yake!

Nidhamu ni tabia. Usipokubali kujituma, mwili unazowea uvivu na uzembe. Na uvivu ni raha. Usipoukataa uvivu hautotoka mwilini. Watanzania wengi wanapenda kuzungumzia Mabadiliko lakini hawataki kubadilika. Tubadilike kwanza sisi wenyewe ndipo tutayaona Mabadiliko tunayoyatamani.

Kwenye zama za 'Hapa Kazi Tu' viongozi tutakuwa mfano wa Mabadiliko; kwanza, tutawapa wenzetu kwenye utumishi wa umma fursa ya kubadilika, wakishindwa tutawabadilisha!

Pamoja na hatua hizi za awali za ukaguzi wa kushtukiza, tumeagiza watendaji watazame namna bora zaidi ya kuweka mifumo ya kielektroniki, biometric systems (dole gumba) na kadi za elektroniki, kwenye taasisi zote za Wizara yetu ili kudhibiti mahudhurio ya watumishi na movement yao wakati wote wa kazi. Malengo ni kuboresha huduma kwa wateja wetu.

Muda wa mwajiri unaibiwa sana. Tutaziba mianya yote mikubwa ya wizi wa muda wa mwajiri.
Sambamba na mifumo hii, tutaweka utaratibu wa kupima utendaji kazi wa kila mtumishi kwa kuwawekea malengo maalum na kuwapima. Na mfumo huu utakuja sambamba na mfumo wa kutoa motisha Kwa watumishi. Maana hauwezi kumkamua ng'ombe usiyemlisha ipasavyo!

Ninawapongeza wafanyakazi wote wa Wizara kwa kuwahi mapema leo hii. Mjue tu kuwa sintowaambia ni lini tena tutafunga geti!

Ahsanteni,
Dr. Hamisi Kigwangalla, MB.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Rais Magufuli Akutana na Maalim Seif Ikulu leo Kuongelea Mgogoro wa Uchaguzi wa Zanzibar

$
0
0
Rais Magufuli amekutana na kuzungumza na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif juu ya mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar
Mpekuzi blog

KIMENUKA..Wema Sepetu Atimuliwa Kwenye Nyumba..Aliyodai Kainunua Kwa Sh Million 280

$
0
0
IMG_5532
Mizigo ikipakizwa kutoka kwenye nyumba hiyo.
Musa Mateja

UFALME umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni 280, fuatana na Ijumaa Wikienda.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18, mwaka huu.
SIKIA CHANZO
“Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.”

IMG_5526
Mizigo ikiwa kwenye gari.
BABA MWENYE NYUMBA AINGIA KATI
“Sasa baba mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini akamtaka Wema ahame haraka kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.

SIKU YA TUKIO
Paparazi wetu alizidi kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa, muda huo tayari kuna lori aina ya Toyota Canter linahamisha vitu nyumbani kwa Wema na kwamba, kuna kila dalili anahama baada ya baba mwenye nyumba wake kumtimua.

PAPARAZI NYUMBANI KWA WEMA
Ilibidi paparazi wetu akimbie kwa pikipiki iendayo kasi mpaka nyumbani hapo na kukuta kweli lori likibeba vitu mbalimbali huku wabebaji wakitokwa jasho chapachapa.
Gari hilo lilisimama kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba hiyo huku likiwa na shehena ya mafurushi ya mizigo.

IMG_5538
Muonekano wa mjengo huo.
Wakati paparazi wetu akiwa kwenye hali ya mshangao, aliendelea kuona mizigo mbalimbali ikitoka ndani ya mjengo huo huku vyombo anuai vya ndani, kama kabati na baadhi ya makochi yakiwa nje ya nyumba hiyo yakisubiri kupakiwa tayari kwa safari ya kumuondoa Wema kwenye mjengo huo.
WEMA HAYUPO
Swali la kwanza kwa wabebaji hao kutoka kwa paparazi wetu ni wapi alipo Wema.
“Unamtaka Wema wa nini wakati unajua hayupo hapa, kwanza wewe nani?” alikuja juu mpakiaji mmoja.

IMG_5544
Vitu vikiwa nje.
PAPARAZI ANUSURIKA KIPIGO
Katika hatua nyingine isiyokuwa ya kawaida, wapakiaji wengine walitaka kumshushia kipigo paparazi wetu baada ya kuona mwanga wa kamera wakati akichukua picha kadhaa kwa ajili ya ushahidi.

WALIKOHAMIA
Uchunguzi wa awali, Wema amehamia Mbezi Beach, Dar. Hata hivyo, tangu sakata la wizi wa maji na umeme, Wema hajawahi kulala na kuamka ndani ya nyumba hiyo huku habari zikisema amekuwa akiishi mahotelini kama ‘digidigi’.

KWA NINI WEMA ALISEMA NYUMBA NI YAKE?
“Kuna watu wengi walikuwa hawatambui kwa nini Wema awali alisema hii nyumba ni yake. Mwanzo wakati anahamia, pia alikuwa ana mazungumzo na baba mwenye nyumba kwamba ainunue lakini watoto wakagoma hivyo Wema akawa analipa kodi kila mwaka.

IMG_5548
WEMA, PETIT MAN
Juzi, Wema hakupatikana hewani ili kujibu madai hayo, lakini mmoja wa watu wake wa karibu, Petit Man alikumbana na paparazi wetu katika klabu moja jijini Dar, alipoulizwa kuhusu mambo hayo alikiri Wema kuhama kwenye nyumba hiyo.

“Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach,” alisema Petit.

Source:Global Publishers

Nafasi za Kazi
Bonyeza>>www.ajirayako.com

Kuna Double Standard Kwenye 'Utumbuaji Majipu?'

$
0
0
Kuna wengine wanapewa grace period ya siku 7 kurudisha fedHa walizojiatia kwa kukwepa kodi. Waliopitiliza siku 7 mpaka sasa hatujasikia wakimulikwa na kamera za Waandishi wa Habari kama ilivyo kwa wengine na kuswekwa ndani!

Wakati wengine wakitenguliwa vyeo vyao kwa kutotimiza wajibu wao ipasavyo kiukweli ni kwamba Idara zote za Serikali zimeprove failure kama tutafuata Standard ya Magufuli strictly.

Mathalani ajali za barabarani zimezidi sana hasa mwisho wa mwaka lakini hatuoni kama hili ni "jipu" kwa Magufuli! "Jipu" ni wale akina mama wanaolala chini Muhimbili!

Kama Magufuli atataka kutenda haki ashughulikie pia wanasiasa waliowasababisha watendaji chini yao kutotimiza wajibu wao! Ajue kabisa tatizo halikuwa kwa watendaji, bali "wazee wa vimemo" ndo waliotufikisha hapo!

Ukawa wamtetea Mkurugenzi wa Kinondoni Aliyesimamishwa kwa Ufisadi

$
0
0
Madiwani wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wamemtetea Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty 7aliyesimamishwa kazi.

Mhandisi Natty alisimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kusiamia vyema mkataba wa ubinafsishaji wa ufukwe wa Coco Beach kwa diwani wa Mbagala Yusuf Manj pamoja na kutowasimamia ipasavyo watumishi wake na kupelekea ujenzi wa baadhi ya barabara za manispaa hiyo chini ya kiwango.

Katika utetezi wao, madiwani hao wameeleza kuwa Mhandisi Natty amewajibishwa kisiasa zaidi kwa kuwa wakati wa uingiaji wa mkataba wa Coco Beach yeye alikuwa bado hajawa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.

Katika tamko lao, madiwani hao wameitaka serikali ya awamu ya tano kushughulikia mgogoro huo na kuangalia hatua za kisiasa zilizochukuliwa. Pia, waliahidi kuwa endapo watafanikiwa kushika manispaa hiyo watahakikisha maeneo yote ya umma yanakuwa katika hali salama na yanaufaidisha umma.

Mbali na tamko la madiwani hao, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa na diwani wa  kata ya Ubungo, Boniphace Jacob (Chadema), walionesha mikataba iliyoingiwa kati ya Manispaa ya Kinondoni na Yusuf Manji ambayo inaonesha kuwa wakati huo Natty hakuw Mkurugenzi wa manispaa hiyo. Walidai kuwa sababu zilizotumika ni za kisiasa kwakuwa mkugenzi huyo alitenda haki na kupelekea majimbo ya uchaguzi kuchukuliwa na Chadema.

“Kama kuna ufisadi umetokea hatutamtetea mtu na kama kuna mtu tunaona anaonewa hatutakaa kimya na hili la Natty tunamwomba Rais John Magufuli aunde tume ambayo haitawahusisha Tamisemi na wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Exclusive: Bifu zito kati ya Diamond na Rommy Jones

$
0
0
Diamond Platnumz vs Rommy Jones
Kuna bifu kubwa linaendelea chini chini kati ya Diamond Platinumz na binamu yake na mtu wake wa karibu Rommy Jones.

Chanzo cha bifu hilo japo wenyewe hawataki kuweka wazi inasemekana ni kitendo cha Diamond kumwambia Rommy aweke utaratibu wa kujitegemea yeye mwenyewe alafu yeye atamsapoti. Inasemekana Rommy hakufurahi kaona kama kadhalilishwa, kumbukeni Rommy hajui ata bei ya viatu kila kitu anawezeshwa na Diamond.

Wengine wanasema chanzo ni Zari inasemekana Rommy ambae ni swaiba wake na Wema alikuwa anajaribu kumshawishi kwa muda mrefu Diamond arudishe mapenzi kwa Wema huku akisaidiwa na Aunt. Hii ilimuuzi sana Diamond maana Diamond kwa sasa jicho lake lote lipo kwa mwanae Tiffa na mpenzi wake Zari sasa kuona mtu wake wa karibu anamshawishi kuvuruga furaha yake ikaleta doa kwenye uswahiba wao.

Kingine ni ishu ya Wasafi records label mpya ya Diamond ambayo kawekeza pesa ndefu lakini kampa usimamizi ndugu yake mwingine anaitwa Ricardo kuisimamia upande wa wasanii na studio na upande wa photo point kampa kifesi ambaye amemnunulia vifaa vya kisasa toka South Africa. Rommy anaona kama kawekwa kando kwenye ufalme wa Wasafi. Mama Diamond nae analaumiwa sababu ameegemea upande wa mwanae.

Mimi nawashauri awa watu wamalize tofauti zao wakae chini waelewane Rommy ajaribu kumwelewa Diamond kwa sasa ni baba hivyo kuna vitu lazima vibadilike akilini mwake hawezi tena kuwa yule Diamond aliokuwa anasikiliza ushauri wako na Halima na Petii.

Pia Dangote ajitahidi kumwelewa cousin wake ni mtu wa aina gani hawezi kubadilika fasta kama unavyotaka Rommy starehe ujiko na show off ndio imekuwa maisha yake tangia utoto awezi kufikiria kama wewe unaewaza future ya mwanao na mama na dada zako.

Copyright Jamiiforums

Mkemia mkuu Tanzania: DNA Yabaini 49% Watoto Sio wa Baba Halali

$
0
0
Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA) yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.

Kesi zinazopokelewa katika maabara yetu zinazohusu sampuli ya Vinasaba kwa mwaka zinaonyesha kuwa asilimia 49% kati ya asilimia 100% ya matokeo hayo huonyesha mzazi mmoja ambaye ni baba kuwa si mzazi halali wa mtoto huyo?.

Vinasaba ni utambulisho wa kipekee wa kila kiumbe ambao unabeba taarifa muhimu na inayorithisha tabia au umbile fulani la mhusika. Vinasaba ni kama vile kitabu cha kumbukumbu kinachohusu maisha binafsi?, aliongeza Prof. Manyele.

Profesa Manyele aliongeza kuwa mikoa ya kanda ya Ziwa, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya ndio inayoongoza kwa matokeo ya uchanguzi huo wa makosa ya Vinasaba nchini.

Akizungumza kuhusu lengo la mkutano huo, Profesa Manyele amesema kuwa ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya wadau wa kemikali na wadau wa afya ya mazingira kutoka katika halmashauri tofauti nchini pamoja na ofisi ya Mazingira.

Aidha Profesa alibainisha baadhi ya majukumu yanayofanywa na wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni kufanya uchunguzi ili kuhakiki ubora na usalama wa vyakula, dawa, maji, maji machafu, bidhaa za viwanda na mashambani, sampuli za mazingira na sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai.

Matokeo ya uchunguzi wa makosa ya jinai na vinasaba (DNA) huviwezesha vyombo husika kufikia maamuzi stahili na kusaidia kutendeka kwa haki katika tuhuma za kesi za jinai ikiwemo ulevi, mauaji, ubakaji, wizi wa

watoto, uhalali wa mtoto kwa mzazi, kwa kupitia vyombo husika? alifafanua Profesa.

Mbali na hayo, alisema wakala kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kuunda maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Sheria ya kusimamia taaluma ya Wakemia, kuimarisha upatikanaji wa mitambo na vifaa vya maabara kila teknologia inapobadilika pamoja na kuimarisha zaidi taratibu za uchunguzi ziwe za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknologia.

Kinondoni: Mhandisi Natty atua Dar es Salaam, ana lundo la nyaraka

$
0
0
Mhandisi Mussa Natty, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kinondoni, ametua Dar es Salaam tayari kwa uchunguzi dhidi yake. Mhandisi Natty, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Babati kabla ya kusimamishwa kupisha uchunguzi,ameshakusanya nyaraka za kutosha na kutisha za kujibu tuhuma dhidi yake. Yuko tayari.

Mhandisi Natty anasubiri tarehe husika ya kuitwa na kuhojiwa ili auanike ukweli wa sakata la tuhuma dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuuzwa kwa ufukwe wa Coco pamoja na ujenzi wa kifisadi wa barabara mbalimbali katika Manispaa ya Kinondoni. Mhandisi huyo yuko tayari kujinasua na kuwanasa wahusika hasa.

Kubenea ameanza, Natty atamaliza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Walichoongea Rais Magufuli Na Maalim Seif Baada ya Kukuta Ikulu Jijini Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad, leo tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam  kufuatia maombi yake ya siku nyingi.

Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar.

Rais Magufuli pia  amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar.

Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif  Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane.

Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema.

Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
21Desemba, 2015

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba Tarehe 22, Ikiwemo ya Zanzibar sasa Mambo Kwisha

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba Tarehe 22, Ikiwemo ya Zanzibar sasa Mambo Kwisha

Waziri Kairuki Aagiza Wanaotakiwa Kustaafu Wasipewe Mikataba Ya Kuendelea Na Kazi Serikalini

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema hana orodha ya majina ya watu wanaouza dawa za kulevya na hana muda wa kushughulika na hiyo inayoitwa orodha.

Badala yake, amesema chini ya uongozi wake ataweka mifumo itakayosaidia kudhibiti uingizaji wa dawa hizo nchini.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Dar es Salaam baada ya kufanya kikao na maofisa wa ngazi ya juu wa Polisi, Kitwanga alisema wamekubaliana kuhakikisha dawa za kuleya zilizoko nchini zinakamatwa na kuteketezwa.

“Mimi hapa nilipo sina orodha ya wauza dawa za kulevya na wala Rais hajanipatia hiyo orodha na siamini kama Rais anayo...ila ninachowaambia ni kwamba tumekubaliana kuweka mifumo mizuri ya kuwakamata watu wote ambao watakutwa na dawa hizo,” alisema Kitwanga.

Alisema mifumo hiyo haitajali ukubwa na nafasi ya mtu kwenye jamii. “Maana mifumo hii tunayoiweka haijali vigogo wala sisimizi na nawahakikishia kwamba tumejipanga kumaliza tatizo hili la dawa za kuleya,” alisema.

Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuongeza nguvu kuhakikisha wanawakamata watu wote ambao wanahusika na biashara haramu ya kuingiza dawa za kulevya na kuzisambaza nchini.

Akizungumza kutokuwepo kwa polisi katika Bandari ya Dar es Salaam, alisema wanaendelea kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kuona utaratibu mzuri wa kupeleka ulinzi kwenye eneo hilo ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.

Katika hatua nyingine, Kitwanga aliwataka polisi kuwashitaki watu kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambika  kesi watu wasio na hatia na  kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.

Nafasi za Kazi Serekalini Utumishi wa Umma, Application Deadline 03 January 2015

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE
PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT

VACANCIES ANNOUNCEMENT

Bonyeza HAPA Kusoma na Kuapply

Polisi ‘Yawatumbua Majipu’ Trafiki, yabadili Mfumo...Sasa Faini Kulipwa Kwa Mashine za EFD

$
0
0
Jeshi la Polisi limefanya mabadiliko kadhaa katika Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kuwahamisha baadhi ya askari wake huku wengine wakishushwa vyeo au kuachishwa kazi kutokana na makosa mbalimbali makubwa yakiwa malalamiko ya kuwaonea wananchi, rushwa na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara.

Kamanda wa kikosi hicho, Mohamed Mpinga akizungumza wiki iliyopita alisema ili kupunguza rushwa na kuingiza mapato, kikosi hicho kimeanzisha mfumo mpya wa kulipa faini wa kutumia mashine za EFD, ambao awali, ulifanywa kwa majaribio na kuonyesha mafanikio licha ya kasoro kadhaa zilizojitokeza.

Dar es Salaam

Wakati hatua hizo zikichukuliwa, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imeshawabadilisha kazi wakaguzi saba na askari wa vyeo mbalimbali 157 wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambao utendaji kazi wao umeonekana kukosa tija.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema hivi karibuni kuwa uamuzi wa kuwabadilisha askari hao kutoka kikosi hicho kwenda katika kazi za kawaida umetokana na ufuatiliaji wa muda mrefu wa tabia na mwenendo wao.

Pia, alisema askari ambao watabainika kujihusisha na makosa ya moja kwa moja ya jinai kama vile rushwa au ukiukwaji wa maadili ya polisi, watashtakiwa katika mahakama za kijeshi.

Alisema uchunguzi zaidi unaendelea kuhusu vikosi vingine vya Kanda Maalumu na Jeshi la Polisi kwa ujumla ili kubaini kama kuna askari, mkaguzi au ofisa anayefanya kazi chini ya kiwango kisichoridhisha na ambaye analalamikiwa.

 Mtwara

Mkoani Mtwara, jeshi hilo limewabadilisha kazi askari 25 wa usalama barabarani kuwa askari wa kawaida. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe alisema hivi karibuni kwamba sababu kubwa ni kuboresha utendaji hasa baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa kuna baadhi ya askari wamekuwa wakiomba rushwa na wengine kulipa visasi.

“Tangu tumefanya maboresho haya tuna wiki mbili tu. Baada ya kupata malalamiko tuliyafanyia kazi ndipo tukagundua kuwa kuna baadhi ya askari hawafai kufanya shughuli za usalama barabarani tukaona ni bora tuwaondoe katika kitengo na kuwa askari wa kawaida,” alisema Mwaibambe.

Alisema mabadiliko hayo si wa askari wa usalama barabarani pekee, bali pia yamewakumba wa kitengo cha upelelezi.

 Tanga

Mkoani Tanga, polisi imefanya uhamisho wa ndani wa askari wake wa vikosi mbalimbali kikiwamo cha usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Zubery Mwombeji alisema uhamisho huo ulifanyika katika siku za hivi karibuni.

“Ni kweli hatua zimechukuliwa, lakini sheria ya jeshi la polisi inanikataza kutaja majina ya askari tuliowahamisha kuwashusha vyeo hata adhabu yoyote, ila nikuhakikishie tu kwamba tumefanya uhamisho mkubwa.”

 Kilimanjaro

Askari 38 wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro wameondolewa kwenye kikosi hicho katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kupangiwa majukumu mengine baada ya kukosa tija na ufanisi.

 Morogoro

Mkoani Morogoro, jeshi hilo limewahamishia katika vikosi vingine, askari 60 wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutokana na makosa ya kinidhamu na kiutendaji.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema si kila kitu kinachofanyika ndani ya Polisi kinatangazwa kwa jamii.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutengwe alisema katika kuboresha uwajibikaji kwenye taasisi za Serikali, askari 60 wa usalama barabarani mkoani hapa waliondolewa na kuhamishiwa vitengo vingine.


Njombe

Kadhalika, mkoani Njombe jeshi hilo limewabadilisha vitengo maofisa wake 20 wa kikosi cha usalama barabarani kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Wilbrod Mutafungwa alisema hivi karibuni kuwa kazi ya kuhamisha askari itakuwa endelevu ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na maadili yanayotakiwa.

Arusha ngangari

Wakati makamanda wa mikoa kadhaa wakizungumzia kuwahamisha askari hao kutokana na utendaji usiokuwa na tija, Kamanda Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Harrison Mwakyoma alisema trafiki yeyote atakayevunja au kukiuka maadili ya kazi atafikishwa mahakama ya kijeshi kujibu tuhuma zote zitakazomkabili na siyo kuhamishwa.

“Sisi hatuhamishi ila tunaadhibu kijeshi na tunawafikisha kwenye mahakama za kijeshi kwa utovu wa maadili,” alisema Mwakyoma.

Imeandikwa na Bakari Kiango, Mary Sanyiwa, Burhani Yakub, Hamida Shariff, Rachel Chibwete na Zulfa Musa.

Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images