Mwanaume Tambua Dawa ya Wanawake Wanaokukataa Kwa Sababu Huna Pesa....
Baada ya Kuukosa Uspika wa Bunge...Samwel Sitta Atangaza Kuacha Siasa na Kuwa Mwandishi
Jela kwa kupongeza majambazi yaliyovamia Polisi Stakishari
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Bruno Kimaryo, kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza ujumbe katika mtandao wa kijamii wa kuyapongeza majambazi yaliyovamia Kituo cha Polisi cha Stakishari na kuua polisi. Aidha, mshtakiwa huyo ametakiwa ama kulipa faini ya Sh. 600,000 kwa kosa hilo.
Katika tukio la Stakishari lililotokea Julai 12, mwaka huu, majambazi yalivamia kituo hicho na kuua polisi wanne na raia watatu pamoja na kupora bunduki 20 aina ya Sub Machine Gun (SMG).
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Waliarwande Lema, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka. Alisema vielelezo vitano na utetezi wa mshtakiwa vinaonyesha kuwa Bruno alifurahia kitendo kilichofanywa na majambazi hao na alitamani kila kituo cha polisi kivamiwe.
Alisema mshtakiwa huyo katika ujumbe wake huo alitumia viunganishi vya maneno yasiyokuwa ya kibinadamu ya auawe, avamiwe na kuwa utetezi wake unaungana na maelezo ya onyo aliyoyatoa polisi hayaonyeshi kusikitishwa wala kuhurumia polisi.
Hakimu Lema alisema kama mshtakiwa angekuwa anapeleka ujumbe kwa polisi wachukue tahadhari, angeupeleka katika mamlaka husika, lakini kutokana na lugha aliyoitumia, mahakama hiyo inamtia hatiani.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa adhabu ya kifungo.
Awali, ilidaiwa kuwa Julai 13, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo anadaiwa kusambaza machapisho ya uchochezi kinyume cha Sheria ya Magazeti kwa nia kuleta ushawishi na kueneza chuki katika mtandao wa kijamii wa facebook.
Wako Wapi Hawa Makamanda wa CHADEMA?
Miss Colombia Atoa ya Moyoni Kuhusu Kuporwa Ushindi wa Miss Universe
Kupitia Instagram yake Miss Colombia , Ariadna Gutierrez aliandika ujumbe mrefu wa kugusa kuhusu kilichotokea, akieleza kuwa sasa moyo wake umetulia na maisha lazima yaendelee. Pia akagusia kwamba huko mbele ya safari itakuja kufahamika kwanini mambo yalitokea vile yalivyotokea, na akamaliza kwa kuwapongeza Wafilipino kwa kupata Miss Universe mpya Pia Alonzo Wurtzbach .
Huu ndio ujumbe wake:
“After the storm comes the calm. I want to thank each and everyone of you who have sent messages of support and strength. Every one of you has become an incredible human being in my book and I am the most fortunate and thankful for having the support not only from one country but from the whole entire world. Your destiny is written for you. And my destiny was this. I was able to bring happiness to my country after becoming Miss Universe for only a couple of minutes… Today because of that COLOMBIA and the LATIN COMMUNITY are being talked about in every corner of the world. I also want to congratulate the Philippines for their new Miss Universe . The happiness that you must be feeling must be incredible. Life continues and in the future we will find out why things happen the way they happen. Thank you all for your LOVE SUPPORT and KINDNESS.❤️”
Afande Sele Apasua Jibu...Wanaoenda Kushoot South Wana Boashara za Siri....
Rapa huyo mkongwe aliyekuwa kimya kutokana na shughuli za kampeni, ameiambia Bongo5 kuwa anaamini wasanii wanaosafiri kwaajili ya kushoot video nje, wana bishara zao za siri.
“Kwenye kushoot video nje ni ulimbukeni,” amesema.
“Tanzania tuna kila kitu kuliko hata huko wanakoenda. Mimi hii naitafsiri ni usaliti wa nchi, sisi tunakosa nini hapa nyumbani? Tuna milima, mbuga, maporomoko mazuri, yaani tuna kila kitu. Unajua wasanii wengi walikuwa wanatumia mwanya wa kwenda kushoot video nje ili kufanya biashara zao za siri. Wengi wameutumia sana huu mwanya, sasa Magufuli alivyoingia atawanyoosha tu,” amesisitiza Afande.
Katika hatua nyingine Afande Sele amesema anajipanga kuachia nyimbo mpya mbili ili kufidia ukimya mkubwa aliouacha kwa mashabiki wake.
Video: Davido Aongelea Sakata la BBA na Alivyowakera WaTZ, ‘Nilieleweka vibaya, Diamond ni Kaka Yangu Angenitetea’
Akiongea kwenye The Sporah Show, Davido alisema tweet ile hakuandika kuwalenga Watanzania bali kampuni ya Multi-Choice inayoanda shindano hilo ambayo pia ndio waandaaji wa tuzo za Channel O. Kabla ya hapo Davido alikuwa ametajwa kuwania tuzo tano lakini alikosa zote. Diamond alishinda tatu.
“Na nilitarajia Diamond angenitetea mimi kuliko kingine,” alisema.
“Angenipigia na kuniambia ‘watu wangu wamekasirika nadhani ungeomba radhi au fanya hivi kuliko hivyo. Ingekuwa ni nchi yangu na najua jinsi ya kuwatuliza watu wangu ningesema Diamond ni kaka yangu hakumaanisha hivyo tuyaacha na tusonge mbele, hivyo ndivyo ilitakiwa kusuluhishwa,” alisema Davido.
“Lakini tulikutana [na Diamond] kwenye MTV Awards na hakikuwa kitu kabisa, hata hatukuliongelea, tuko poa.”
ANGALIA VIDEO:
Ommy Dimpoz: Niko Tayari Kuoa Hata Sasa,Kama Nikipata…
Ommy ameyazungumza hayo wakati akiitambulisha video ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Achia Bodi’ kwenye kipindi cha Clouds360 cha Clouds Tv wakati alipoulizwa na mtangazaji kipindi hicho Hudson Kamoga kuwa anatarajia kuoa lini.
“Niko tayari kuoa hata sasa hivi kama nikipata mtu sahihi katika maisha yangu” Ommy Dimpoz.
Miezi ya hivi karibuni msanii huyo alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na msichana ambapo picha hizo zilizua maswali kwa mashabiki wake na kuuuliza huenda alikuwa ndiye shemeji yao,lakini hawakupata jibu.
Cloudsfm.com
Watu 7 Wafariki Kwa Kuungua Moto Baada ya Gari Kupinduka na Kuwaka Moto
Akiongea na mtandao huu ofisini kwake Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni Dkt. Leonard Subi amesema kuwa jana majira ya saa 12 jioni walipokea miili ya marehemu 6 na majeruhi 11 ilipofika saa 6 usiku majeruhi mmoja alifariki duniana na kupelekea idadi ya vifo kuwa saba.
Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni Ashura Mussa, Kadogo Yusuph, Kabwe Iddy, Mwamvua Juma na Peter Sungura,maremu wawili miili yao bado haijatambulika sababu ya kuungua vibaya.
Dkt. Subi aliwataja pia majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Andrew Peter, Amos Thomas, Mutta Hamis, Shabaan Fadhil, Hassan Kasa, Esau Elias, Asha Kassim na Riziki Jaah.
"Majeruhi wote wamelazwa wodi namba saba na hali zao siyo nzuri wanaendelea na matibabu, mtoto aitwaye Riziki Jaah mwenye umri wa miezi nane ndiye aliyenusurika katika ajali hiyo hajaumia popote mama yake alimtupa dirishani baada ya moto kuwaka ila mama yake alifariki kwa kuungua kwenye ajali hiyo"alisema Dkt. Subi.
Naye Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdnand Mtui amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya gari aina ya Toyota Hiace lenye namba T.700 ADK lililokuwa likitoka Kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Subankala kata ya Ilagala Wilayani Uvinza kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika.
Kamanda Mtui alisema kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mwakizega na chanzo cha ajali hiyo ni dereva kuwakwepa watembea kwa miguu kisha kugonga gema iliyopelekea gari kupinduka na kuwaka moto.
Madereva Watakaozidisha Abiria Kwenye Vyombo Vya Usafiri Kukiona...Hii Inawahusu Hata Wale wa Daladala
Operesheni hiyo inaanza leo baada ya tamko la Jeshi la Polisi na kuanza kutekeleza kwa wale wote wataobeba abiria wengi tofauti na uwezo wa basi. Watakaochukuliwa hatua ni madereva wa daladala,mabasi ya mikoani pamoja na magari aina ya Noah.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kuwa Jeshi la polisi linaanza operesheni ambayo ni endelevu na kuwataka watu wafuate sharia ya ubebaji wa abiria.
Advera amesema kuwa katika kipindi hiki cha siku kuu Jeshi la polisi limejipanga katika kuwadhibiti waendesha bodaboda kwa wataopandisha watu zaidi ya wawili (mishikaki) kukiona cha mtema kuni kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa za kihalifu katika msimu wa sikukuu ili kuimarisha ulinzi wa watu na mali zao ili maisha yaweze kuendelea baada ya sikukuu.
Breaking News:Rais Magufuli Akamilisha Uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbalawa Abadilishiwa Wizara
#BREAKING: Rais Magufuli amemteua Profesa Jumanne Maghembe kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii
#BREAKING: Rais Magufuli amemteua Dkt. Philip Mpango kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge) 15
#BREAKING: Rais Magufuli amemteua Mhandisi Gerson Lwenge kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji
#BREAKING: Rais Magufuli amemteua Dkt. Joyce Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
#BREAKING: Rais Magufuli amemteua Hamad Masauni kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
#BREAKING: Rais Magufuli amemteua Prof. Makame Mbarawa kuwa Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
Mtendaji Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo Asimamishwa KAZI Kupisha Uchunguzi
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 24, Ikiwemo ya Aunty Ezekiel Kumtia Umaskini Moses Iyobo
Polisi Wauana Kwa Risasi Jijini Mwanza Wakiwa Lindoni
Tukio hilo lilitokea jana saa 8.30 mchana jijini Mwanza katika eneo la Benki ya Posta Tawi la Pamba wilayani Nyamagana huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa hakijulikani.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema kitendo hicho si cha kawaida ndani ya jeshi hilo, na kufafanua jinsi mazingira ya tukio lilivyotokea na kusababisha taharuki kwa wananchi na wateja waliokuwa ndani na nje ya benki hiyo.
“Ni kweli kuna askari wawili wamefariki eneo la Benki ya Posta. Katika eneo la benki hiyo kulikuwa na askari wawili waliokuwa lindoni ambao ni PC Elisha na PC Remigius Alphonce mwenye namba H 4291, wakiwa wanaendelea na lindo alifika askari mwingine aliyekuwa amevaa kiraia PC Matiko na kuwasalimia kisha kuingia ndani ya benki kuchukua fedha,” alieleza Kamanda Kamugisha na kuongeza:
“Baada ya dakika tano, Matiko alitoka nje na kuwaeleza askari wenzake kwamba mtandao unasumbua, wakati akieleza hivyo, ghafla askari PC Elisha aliweka chemba risasi ambapo mwenzake PC Alphonce alimhoji mbona unaweka risasi katika hali ya utayari wa kutumika na alijibiwa kwa ufupi kwamba ‘achana na mimi.’
“Ghafla alimfyatulia risasi PC Matiko na kumpiga eneo la bega la kushoto na kutokeza mgongoni na kuanguka chini, kitendo hicho kilimfanya PC Alphonce kukimbilia Benki ya Barclays ili kuomba msaada kwa askari wenzake waliokuwapo lindoni hapo.
“Kabla ya askari hao kufika, ilisikika sauti ya mlio wa risasi na baada ya kurudi alimkuta PC Elisha akiwa amejipiga risasi kwenye paji la uso na kutokea nyuma ya kisogo, tayari akiwa amepoteza maisha.”
Sakata Dk. Mwaka Lawa Pasua Kichwa kwa Dk. Kigwangalla
Awali, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Waziri Kigwangalla aliahidi kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na Dk. Mwaka juzi (Jumatatu). Alieleza hayo baada ya kufanya ziara ya ghafla kwenye kituo cha Dk. Mwaka Desemba 14, 2015 na kutomkuta yeye na baadhi ya watoa huduma wake kabla ya kumtaka (Dk. Mwaka) awasilishe vyeti vyake wizarani kwa ajili ya ukaguzi.
Hata hivyo, licha ya Dk. Mwaka kutekeleza agizo alilopewa Desemba 16 na waziri kukiri kuwa kweli vyeti hivyo vimefikishwa kwao na kuhakikiwa, bado suala lake linaelekea kusumbua kwani hadi kufikia jana, hakukuwa na ufafanuzi zaidi kama ilivyoahidiwa wiki iliyopita huku Dk. Kigwangalla akiutaka umma utulie na kusubiri taarifa ya ukaguzi kwani hivi sasa kuna masuala mengine ya kushughulikia.
“Tutawapa taarifa mara tutakapomaliza kuipitia ripoti hiyo, subirini tu kwa kuwa kuna kazi nyingi za kufanya wizarani,” Dk. Kigwangalla wakati alipoulizwa na mwandishi wa Nipashe jana kuhusiana na matokeo ya ukaguzi wav yeti mwaka kama alivyoahidi wiki iliyopita.
Akieleza zaidi, Dk. Kigwangalla alisema bado anaipitia ripoti hiyo na akishamaliza, atashauriana na viongozi wengine wa wizara yao akiwamo Waziri mwenye dhamana, Ummy Mwalimu, na kisha ndipo ataitisha mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa taarifa.
ILIVYOKUWA
Desemba 14 ya wiki iliyopita, Dk. Kigwangalla alifanya ziara ya kustukiza kwenye kituo cha Dk. Mwaka ambaye amekuwa maarufu kutokana na matangazo mbalimbali anayotoa kila mara kuhusiana na tiba anazotoa.
Hata hivyo, baada ya Dk. Kigwangalla kufika kwenye kituo hicho, hakumkuta Dk. Mwaka na wenzake na ndipo (Dk. Kigwangalla) alipotoa amri ya kufungwa kwa muda kituo hicho akimtuhumu Dk. Mwaka na wenzake kumkimbia na kisha akaamuru apeleke vyeti vyake ili vichunguzwe na kuona kama huduma wanazotoa zinakidhi vigezo na ni salama kwa wagonjwa.
Desemba 20, Kigwangalla aliiambia Nipashe kuwa ameshapokea ripoti yenye maelezo ya vyeti vya Dk. Mwaka na kwamba, angetoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari Jumatatu au Jumanne (juzi au jana).
KIMENUKA Somalia...Serikali Yapiga Marufuku Sikukuu za Christmass Nchini Humo
Mkurugenzi mkuu katika wizara ya masuala ya dini, Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya Kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi kutoka kundi la wanamgambo wa Al Shabab.
“Maofisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yoyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiyofungamana na dini ya Kiislamu.” alisema Sheikh Mohamed
Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika (AU) iliyopo Mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.
Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia.
Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.
Credit: BBC
MREMBO Gigy Money Amtambia Wema Sepetu Kwa Kumzidi Kalio
Akipiga stori na kona ya Bongo Movies, Gigy ambaye pia ni ‘muuza nyago’ kwenye video za Kibongo alisema kuwa ana kila sababu inayomfanya kujitambia kwa umbo lake ambalo linawateka hasa wanaume wakware.
“Kuna siku kwenye kipindi kimoja cha runinga tulishindanishwa kati yangu na Wema nani mwenye kalio kubwa nikamfunika, hicho ni kigezo cha kwanza kuwa nina uwezo wa kumpoteza na sehemu nyingine,” alisema Gigy. Source:Global Publishers
Ugandan sentenced to 5 years in jail for getting pregnant in Kuwait
According to the chairperson of the Association of Ugandans living in Asian and Arab countries, Ali Nusbuga, Fatumah was produced to court a few months ago and would have been saved from the verdict had the government and Human Rights bodies intervened.
He said that much it breaks the law in Kuwait for a woman that is not married to get pregnant or to have a baby and under such instances, the offenders, regardless of nationality or religion, face jail,not alot of help has been offered by the Ugandan authorities despite the endless calls for intervention.
Nsubuga calls upon the government use it’s diplomatic ties with Kuwait so as to save Fatumah and have her deported or even have her sentence reduced.
He also decried the little help and protection given to Ugandans abroad and said that many Ugandan who leave the country for greener pastures go through alot and mentioned instances of them being exploited,having their visas confiscated.
Fatumah suffers the same fate another lady called Mastula did,both are now to serve cases in Kuwait.
Mlangua Tiketi Stand ya Mabasi Ubungo Ajihami Kwa Kinyesi Polisi Wasimkate
Pamoja na kutumia mbinu hiyo ya kipekee, mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Nuhu Matumla (26), alikamatwa na askari hao ambao jana waliweka kambi UBT ambako ulanguzi wa tiketi za mabasi yaendayo mikoani umepamba moto wakati huu wa kuelekea siku kuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Tukio hilo lililovuta hisia za watu na kusababisha msongamano wa magari, lilitokea saa 1.30 asubuhi nje ya kituo hicho wakati wa operesheni hiyo ya kukamata walanguzi wa tiketi na matapeli.
Askari wapatao wanne waliokuwa na silaha walikuwa wakimfukuza Matumla na walipomkaribia, alivua suruali yake iliyokuwa na kinyesi na kisha na kukichota kwa mkono na kuwarushia.
Wakati akirusha alikuwa akisema “niachieni, nitawapaka kinyesi”, lakini juhudi zake hazikufua dafu.
“Kamata huyo hakuna kumwachia, unarusha kinyesi unafikiri sisi tunaogopa,” alisema mmoja wa askari hao.
Kinyesi alichokuwa akirusha kilichafua sare za askari hao na magari madogo yaliyokuwa yameegeshwa katika eneo hilo.
Wananchi walioshuhudia tukio hilo tangu asubuhi, walidai kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na zaidi ya tiketi 20 ambazo alianza kuziuza kwa watu waliokuwa wakitaka kusafiri.
“Sisi tulikuwa tumekaa hapa tukamuona huyo jamaa (Matumla) akiuza tiketi, hatukujua kama ni za ulanguzi. Baada ya muda tukaona askari wanakuja wakamkamata.” alisema Hassan Issa.
Juma Idd, aliyekuwapo eneo la tukio, aliwamwagia sifa askari kwa kumkamata.
“Tunawasifu hawa askari. kitendo cha kumkamata huyu jamaa aliyekuwa akiwarushia kinyesi ni cha kishujaa,” alisema.
“Kwanza kinyesi chenyewe kilikuwa kinatoa harufu kali ambacho kwa mtu wa kawaida huwezi hata kumsogelea.”
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga alisema mpaka sasa watu wawili wamekamatwa kwa kuuza tiketi za ulanguzi huku wengine 20 wakikamatwa kwa makosa ya kutapeli na kusumbua abiria.
“Tumefanikiwa katika hilo japo ulanguzi wa tiketi unafanyika kwa kiwango kikubwa,” alisema.
Alisema wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.