Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Serikali Yasema Tamko Lake La Tiba Mbadala na Asilia Liko Palepale

$
0
0
Serikali imesema kwamba tamko lake lilitolewa hivi karibuni kuhusu matangazo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala liko palepale kwa kuwa lengo lake ni kuboresha huduma hiyo. Hivyo kama  kuna mtoa huduma ambaye amekwazika na tangazo hilo Wizara ipo tayari kuzungumza naye.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Tamko hilo lilitolewa Desemba 24, mwaka huu,ambapo limepiga marufuku  matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Kwa wale wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.

Tamko hilo  liliendelea  kufafanua kwamba  utoaji wa elimu ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.

‘Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala,’ lilieleza tamko hilo.

Tamko hilo lilifafanua kwamba  Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia  24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.

Aidha  akizungumzia kuhusu tangazo hilo, Waziri   Ummy alisema  ‘Mimi  niko tayari kuzungumza na mtoa huduma ambaye amekwazika na tangazo hili, ili aweze kueleza ni sababu zipi zinazomfanya asisajiliwe.  Tunafanya hivi kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu,’ alisisitiza.

Aliongeza kwamba Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala  Namba 23 ya Mwaka 2002 inaeleza  wazi.

Kwa mujibu wa Waziri huyo alitaja idadi ya watoa huduma hiyo kuwa   wako 75,000 kwa takwimu za nchi nzima.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili  na Tiba Mbadala, Dkt. Edmund Kayombo alisema hadi sasa hawajapokea mrejesho wa tamko   hilo la  Serikali.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama  Vya Tiba Asili Tanzania(SHIVYATIATA), Abdulrahaman  Lutenga alisema  hakuna mganga yoyote aliyepinga tamko hilo na Serikali, hivyo tamko lililotolewa  hivi karibuni la kupinga agizo hilo si halali kwa kuwa halikupitia katika shirikisho hilo.

‘ Hatutambui kampuni hii iliyotoa tamko la kupinga tangazo la Serikali kwani ya mtu binafsi yenye wanahisa 11,’ alisema Lutenga.

Akizungumzia kuhusu hatima ya tamko hilo, Dkt. Kayombo alisema baada ya siku walizotoa  kumalizika  watatangaza hatua zipi zitachukuliwa kama vile kuwaondoa wasiofuata sheria.

Hizi Ndio Dalili za Serikali ya Magufuli Kushindwa? Au Tuendelee Kuwapa Muda?

$
0
0
Nimeamka asubuhi natoka kuelekea kazini. Nimefika kituoni nikakuta daladala imesimama inapakia abiria huku ikiwa tayari imejaa, nikaitwa nipande nikakumbuka AMRI ya serikali kwamba ni marufuku kusimamisha abiria.

Sikupanda nikasubiria nyingine nikazunguka nayo ndani ya daladala abiria tumejaa watu wamesimama hakuna ata pa kuweka mguu. Tunapita barabarani askari awa barabarani wanatutazama tofauti na nilivyohofu kwamba nikikutwa nimesimama nitapigwa faini na wala sioni anayejali.

Nafika ofisini nakuta magazeti tayari yameshafika naona vichwa vya habari waganga wa tiba asili wameigomea serikali na wanamkanya Waziri wa serikali aache kutaka sifa so hawapo tayari kutekeleza amri ya serikali, nikapekua habari iliyoandikwa ukurasa wa juu ya gazeti la mwananchi inaonyesha namna awa waganga wanavyotapeli wananchi..

Kwa habari hiyo ya uchunguzi inaonyesha kifaa ambacho kinatiliwa shaka kinauwezo wa kuchunguza mwili wa binadamu bila kuchukua damu wala kitu chochote mwilini na kutoa majibu ndani ya dakika tatu. Mwandishi kama sehemu ya uchunguzi anaonekana ana tatizo la ugumba ilihali ana watoto tayari alikuwa anawajaribu.

Nilishikwa na ganzi baada ya kusoma hiyo habari nikabaki najiuliza huu ujasiri wa kuigomea serikali wanautoa wapi? Na wanafanya utapeli kama huu bila woga?

Muda wa kazi ukafika tukaanza kufanya kazi ghafla nikakumbuka AMRI ya Waziri wa kazi kwa wafanyakazi wanaofanya bila vibali baada ya kumuona mfanyakazi mwenzangu kutoka Kenya akiendelea na kazi bila wasiwasi wowote na ukweli ni kwamba anafanya kazi bila ya vibali kuangalia around ofisi yote nakuta wale wakenya waliokuwa wanafanya kazi bila vibali bado wapo na hawana uoga wowote na boss wala hashtuki kuwatafutia vibali wapo zaidi ya ishirini(kumbuka deadline ya serikali imeshapita) .

Ndipo nikaanza kupatwa na hofu inamaana awa mawaziri wanapotoa matamko na maelekezo mbona yanapuuzwa? Wasiposikilizwa leo ni lini watasikilizwa? Tatizo ni maagizo hayatekelezeki au watanzania hawapo tayari kwa changes? Au mawaziri hawakujipanga kusimamia utekelezaji? Au Magufuli yupo ahead of time ambapo watanzania awako tayari kufika kwa sasa bado wanataka kufurahia comfort zone?

Sina mashaka kabisa na Magufuli katika kusimamia mambo yake sababu ana historia hiyo ila nimeanza kupata mashaka na mawaziri kama haya mambo ya kusimamia taratibu wataweza au wanajilazimisha ila hawawezi.

Ni hayo tu, kazi njema!
Judi wa Kishua

Nafasi za Kazi
Bonyeza>>www.ajirayako.com

Nampa Kila Anachostahili Mke Wangu Lakini Sina Amani na Ndoa yangu

$
0
0
Mke wangu nampenda sana kila anachotaka nampa. Yeye ni mwalimu wa msingi. Uwezo wangu wa kifedha si mkubwa lakini nimejitahidi hadi nimemnunulia walau kigari cha kuendea kazini katika jitihada za kumfanya nae ajisikie vizuri mbele za watu.

Mshahara wake ni chini ya laki 5 lakini huwa namwekea mafuta ya shilingi laki 3 kwa mwezi ili aende kazini. Nampa matunzo yote anayotaka kama mke wa ndoa anavyostahili.

Kinachonisikitisha ni dharau anazonionyesha ndani ya nyumba. Akiamua kunitukana inachukua siku tatu kumaliza matusi. Nyumba haina amani naishi kama mhamiaji haramu. Kuna wakati ananiangalia tu na kunisonya bila kumkosea chochote.

Anadai nikisafiri anaishi kwa amani nikirudi anakereka. Kwa kifupi mimi huwa ni mara chache huwa najibizana nae ninapozidiwa na hasira lakini mara nyingi hukaa kimya.

Nimejaribu kujiuliza ni wapi nakosea sipati jibu. Natunza familia vizuri, unyumba nampa, sina vimada na wala hajawahi kunihisi.

Tatizo ni nini? Nisaidieni wadau niishije na huyu mke? Akiugua anajitahidi kuonyesha jamii kuwa simjali anaamka mapemaa anawahi hospitali ili nionekane simjali.

Akiamua kunitukana anatumia matusi na kashfa nzito dhidi yangu. Bado sijamsimulia mtu yeyote kwa ajili ya kulinda heshima ya familia lakini naona kama nazidiwa.

Naombeni ushauri wenu.

Nafasi za Kazi

Do You HAVE Letter M On The Palm? – Here's What It Means

$
0
0
According to many, the lines on the palms talk about our character and destiny. But those who have the letter M on the palm, are said to be special.

It is said that these people are especially gifted, possess great intuition and are excellent partners for any business.

If your loved one has the letter M on the palm, you must know one thing – no joke, no lies and no fraud with them.

They will always find that you lie them or cheat.

Women who have letter M on the palm, have stronger intuition than men, and if both spouses have it the woman still prevails.

These people have the power to make the changes they need in life and therefore need to seize the opportunities in life.

According to folk tradition, all the prophets ever had this sign on their palm, and if you are one of the people who have the palm point M, know that you are really a special person.


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Disemba 29, Ikiwemo ya Magufuli na Lowassa Wamtesa Gwajima

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Disemba 29, Ikiwemo ya Magufuli na Lowassa Wamtesa Gwajima

Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Zantel Apigwa Risasi

$
0
0

Hii imetokea barabara ya Coca Cola karibu na Nabaki Afrika. Inasemekana director huyo anajulikana kwa jina la Gabriel Kamukara amepoteza maisha kwenye eneo la tukio.

Inasemekana alikuwa na kiasi cha pesa na hao majambazi wamefanikiwa kuzichukua.

Watu 2 wamepigwa risasi na kuporwa fedha wakiwa katika gari lao eneo la Nabaki Afrika DSM.

Tazama Video:

Nay wa Mitego Afunguka Jinsi Walivyoachana Kimapenzi na Mwigizaji Shamsa Ford......

$
0
0
Nay wa Mitego amezungumzia jinsi alivyoachana na aliyekuwa mpenzi wake Samsha Ford baada ya mwanadada huyo kudai hataki tena kutoka kimapenzi na mastaa.

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, rapa huyo alisema licha ya kuachana na mwanadada huyo bado ni mshkaji wake na wanapiga stori kama kawaida.

“Mimi binafsi sijui alikuwa anamaanisha nini lakini kitu ambacho naweza kusema mimi na Shamsa bado ni washkaji na hatuwezi kuja kuwa maadui hata siku moja licha ya kuachana,” alisema. “Hatuna ugomvi lakini pia sijui alikuwa na mahusiano na staa gani before? Labda ndiyo maana anaongea hivyo ila mimi tuliachana vizuri.”

Aliongeza, “Kuhusu mimi sijamtenda hata yeye hajanitenda ndiyo maana mpaka leo tunaendelea kuongea japo kuwa labda yeye ana kitu anacho moyoni hicho siwezi kujua ila mimi ninachojua nazungumza naye poa tu.”

Kabla ya kuachana wawili hao walichukua muda mrefu kuweka wazi mahusiano yao.

VERA SIDIKA’s Bank Has Blocks her ATM and Credit Cards Due to Suspicious Activities

$
0
0

Vera Sidika, who is currently in the US enjoying her vacation, may not be on a shopping spree anymore after her cards were blocked by her bank.

Apparently, they were cancelled due to ‘suspicious activities’ and here is what she posted

So I couldn’t use my cards when shopping yesterday because the bank block(ed) my cards due to SUSPICION. Today swipe in Kenya, tomorrow in Dubai and in 24hrs in USA.



Jinsi Majambazi Walivyotoa Uhai wa Meneja wa Zantel Kwa Kumpiga Risasi.....

$
0
0
Meneja wa operesheni wa kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Zantel, Gabriel Rafael ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.

Tukio hilo limetokea jana saa 4:45 asubuhi eneo la ofisi za kampuni ya Nabaki Afrika, iliyopo Mwenge, mita chache karibu na kampuni ya Coca-Cola.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema haikujulikana mapema meneja huyo alikuwa akitokea wapi na gari lake aina ya Toyota Double Cabin.

Alisema baada ya kupata taarifa za mtu kuuawa kwa kupigwa risasi, polisi walifika eneo la tukio na kubaini kuwa meneja huyo alikuwa amepigwa risasi kwenye kwapa la mkono wa kulia.

Kamanda Wambura alisema ndani ya gari la mfanyakazi huyo walikuta simu, laptop na fedha taslimu Sh1 milioni.

“Mwili wake umepeleka kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo pamoja na kuwasaka waliofanya mauaji hayo,” alisema Wambura.

Taarifa za mauaji ya meneja huyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana mchana zikieleza kuwa, alikuwa akitokea benki kuchukua fedha.

Katika hatua nyingine, Wambura alitoa rai kwa wakazi wote kutumia njia za kiteknolojia kuchukua na kuhifadhi fedha badala ya kutembea nazo mfukoni.    


Ahadi ya Rais John Pombe Magufuli ya Ujenzi wa Reli Kuanza

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameanza ziara mkoani Kigoma huku akiahidi kuanza ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya viwango vya ‘standard gauge’, itakayosaidia kuimarisha biashara ya kusafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), kupitia Bandari ya Kigoma.

Tamko la Waziri Mkuu Majaliwa inaashiria kuanza kwa utekelezaji wa vipaumbele 25, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati, alivyovitoa Rais John Magufuli (wakati huo akiwa mgombea urais wa CCM), Agosti 24, wakati wa uzinduzi wa kampeni zake kwenye Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wakazi wa Kigoma katika Mwalo wa Kibirizi, Waziri Mkuu Majaliwa alisema mradi huo utaambatana na ujenzi wa bandari kavu eneo la Katosho mjini Kigoma, kwa ajili ya kushusha mizigo inayosubiri kwenda nje ya nchi.

“Lazima tujenge reli ya kisasa na tumezindua ujenzi wa reli ya urefu wa kilomita mbili. Huwezi kuimarisha bandari kama reli itakuwa imechoka na hii ilijengwa miaka 100 iliyopita, sasa imezeeka haifai, ndiyo maana tumeamua kutumia fedha nyingi kuhakikisha mradi huu wa reli ya kisasa na ujenzi wa bandari unakamilika kwa wakati,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Katika maelezo yake hayo Majaliwa alipokea kilio cha wakazi wa Katosho inakotakiwa kujengwa bandari kavu wanaolalamika kupunjwa malipo ya fidia ya nyumba na mazao, aliwahakikishia kuwa mchakato wa kutathmini unarudiwa hivyo aliwashauri wananchi waliopokea fedha za fidia kuhama ili kupisha ujenzi wa bandari.

Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wavuvi na wafanyabiashara kutumia fursa ya Mwalo wa Kibirizi, ambalo linapokea mazao ya uvuvi na kuyachakata kwa ajili ya kuingia sokoni, jambo litakalosaidia kuinua uchumi na kuongeza thamani ya mazao hayo.

Alisema Serikali itatafuta masoko ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuuza samaki na dagaa wanaovuliwa kutoka Ziwa Tanganyika na kuwezesha wavuvi kujiongezea kipato, hali itakayowafanya wawe na uwezo wa kununua zana bora za uvuvi na kuongeza kiwango cha uvuvi.

Pia aliahidi kumuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu kuongeza ulinzi Ziwa Tanganyika ili kupambana na maharamia wanaopora zana za uvuvi, ambapo pia amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya kufanya kikao na Balozi wa Congo DRC ili kuona njia bora ya kushirikiana kupambana na maharamia.    

Ufisadi Mwingine Wa Bilioni 48 Waibuliwa Bandarini .......7 Watiwa Mbaroni, 8 Wanasakwa na Jeshi la Polisi

$
0
0


Serikali imepoteza jumla ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
  
Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
  
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawaamesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.
  
Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.

Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango Aanika Aibu Ya Kuomba Misaada Nje.....Asema Tanzania Hudhalilika sana hasa Ukizingatia ni nchi Tajiri

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amesema serikali inatarajia kukusanya kiasi cha Sh. trilioni 1.3 ndani ya mwezi huu pekee.

 

Aidha, amesema ili kuhakikisha serikali inapata mapato ya kutosha, atasimamia vyema suala la kukusanya kodi zinazostahili na kutengeneza mazingira ya watu kulipa kodi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vya Ikulu mara baada ya kuapishwa, Dk. Mpango alisema kwa kipindi cha mwezi mmoja serikali inaweza kukusanya kiasi hicho cha fedha.

 

“Nimekaa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kipindi cha wiki tatu, nimeona kuwa kiasi hiki cha Sh. trilioni 1.3 kinaweza kukusanywa. Kwa wiki iliyopita ya sikukuu, niliona makusanyo ni mazuri na mpaka ifikapo mwisho wa mwezi huu, tutatimiza kiasi hicho,” alisema.

Ulipaji Kodi

Akizungumzia suala la wafanyabishara kukwepa kodi, alisema hakuna serikali inayoweza kujiendesha duniani kote bila kukusanya kodi.

 

Alisema: “Kipengele cha kwanza, wale wanaokwepa kodi tutawabana ili walipe kodi inayostahili, ni lazima Watanzania wajenge utaratibu wa kulipa kodi halali na kwa hiari,” alisema Dk. Mpango.

 

Alisema serikali itafanya marekebisho ya mfumo wa kodi ili wafanyabiashara wafanye biashara zao vizuri.

 

“Kama hakuna mfumo wa kuwafanya wafanyabiashara wakubwa kulipa kodi, tutaendelea kuwakamata wafanyabishara wadogo wadogo wale wale kila siku,”alisema.

 

Kadhalika aliweka wazi lengo la serikali kuwaondolea kodi za kero wafanyabishara wadogo wadogo kama mama lishe, wauza vitumbua na wauza samaki .

Changamoto zilizopo TRA

Akizungumzia changamato alizobaini akiwa TRA kwa kipindi cha siku 27, alisema wapo watumishi wasiowaaminifu ambao anaamini wako katika sekta mbalimbali nchini.

“TRA kuna watendaji wazuri wanaofanya kazi kwa weledi, lakini kuna wale wachache ambao wanaharibu sifa ya TRA na hao tutahakikisha tunawaondoa ili kufikia lengo la kukusanya kodi kwa uaminifu,” alisema.

Alisema changamoto iliyopo ni baada ya kutokea kwa kashfa ya ukwepaji kodi watendaji wa TRA wote kwa sasa wanaonekana kuwa ni waovu.

Malengo ya Rais Magufuli

Akizungumzia malengo na ahadi za Rais Magufuli alizowaahidi Watanzania ikizingatiwa kuwa, wizara hiyo ndio yenye dhamana kubwa ya utekelezaji alisema yote yatatekelezeka kama watendaji watatimiza majukumu yao.

Alisema kila kiongozi akisimamia vema jukumu lake alilopewa na wizara yake ikikusanya kodi inayotakiwa kwa wakati, mambo yote aliyoahidi rais yatatekelezeka ikiwamo elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne na milioni 50 katika kila kijiji nchi nzima.

“Ni lazima tufanye kazi kwa bidii na maarifa ambayo Mungu ametujalia na kuwa na nidhamu kwa kila jambo tunalolifanya kwa Watanzania wote, tusingoje watu wengine waje watujengee nchini yetu,” alisema.

Kuongezeka kwa Thamani ya Shilingi

Dk. Mpango akizungumzia namna wizara yake itakavyowezesha thamani ya shilingi kupanda, alisema suala hilo linawezekana kwa kuongeza nguvu kwenye kuuza bidhaa za kutosha nje ya nchi.

“Kitaalam ili kuongeza thamani ya shilingi yetu, tunaweza kuiongezea nguvu hasa kwa kuuza bidhaa za kutosha nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni za kukidhi mahitaji ya watu ya kuagiza bidhaa,” alisema.

Alisema pia ni muhimu kutilia mkazo uzalishaji wa bidhaa nyingi zinazoliingizia taifa fedha za kigeni.

Alitaja biashara hizo kuwa ni utalii unaoliingizia taifa fedha za kigeni, biashara na nchi jirani na mazao yenye thamani kubwa.

 

Alisema pia ni vema kulisimamia soko la fedha na benki kuu ili viwango vya kukopa vishuke na kusimamia ipasavyo sekta ya fedha.

“Haya yanawezekana chini ya Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndulu, ambaye anasimamia vema sekta hiyo ili viwango vya kukopa vishuke na Watanzania wafundishwe kujiwekea akiba na kukopa kupitia saccos, benki na vicoba,” alisema.

Namna ya kukuza Uchumi wa Nchi

Dk. Mpango, alisema ili kukuza uchumi wa nchi ni lazima kuwa na utaratibu wa kujenga viwanda vikubwa nchini vinavyozalisha kwa wingi  jambo litakaloongeza pato la taifa.

 

“Nchini kwa sasa kuna kiwanda kimoja kikubwa cha Bia cha Breweries (TBL) ambacho ndicho tunakitegemea ndio maana bei ya vileo vinapanda kila siku. Lakini vingekuwapo kama hivyo 10, nina uhakikisha tungekusanya mapato ya kutosha,” alisema.

 Aibu ya kuomba misaada nje

Dk. Mpango, alisema miongoni mwa mambo yanayomnyima raha ni safari za kwenda ughaibuni kuomba misaada kwa nchi wahisani.

Alisema kitendo hicho ni cha aibu na kwa muda mrefu kimekuwa kikimsonesha moyoni hasa kwa kuwa anafahamu kuwa taifa lake lina utajiri mkubwa.

"Nimekwenda nje mara nyingi nikiongozana na mawaziri wa fedha waliopita kwenda kuomba misaada.Huwa najisikia aibu sana,tunadhalilika sana. 

"Hatuna sababu ya kuwa ombaomba,tunachotakiwa kukifanya ni kuimarisha mfumo wa ukusanyaji kodi na kuwaondolea mzigo wananchi wa hali ya chini," Alisema Dr. Mpango 

Baada ya CCM Kutangaza Kujiandaa kwa Uchaguzi Zanzibar, CUF Nao Watoa Tamko ZITO

$
0
0

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile.

Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Baada ya kuipitia taarifa ya CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo, CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya yafuatayo:

1. Taarifa yenyewe haionekani kama imeandaliwa na watu makini wala haioneshi kama walioitoa wanajua nini kilichopo. Hilo liko wazi kutokana na taarifa yenyewe kuwa na maudhui yanayopingana ambayo yamekuja kukorogwa zaidi na maelezo yaliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar mbele ya waandishi wa habari na kuoneshwa katika vituo kadhaa vya televisheni:

(a) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini papo hapo inaeleza kwamba kikao kimeridhia mazungumzo yanayoendelea Ikulu Zanzibar. Taarifa haisemi iwapo maamuzi ya vikao vya mazungumzo hayatakuwa na suala la kurudiwa uchaguzi, upi ni mwelekeo wa CCM.

(b) Taarifa inazungumzia uchaguzi wa marudio lakini papo hapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anasema CCM haina imani na Tume ya Uchaguzi iliyopo na kwa hivyo uchaguzi huo wa marudio lazima ufanyike chini ya Tume mpya. Baada ya hapo hasemi Tume iliyopo ambayo muda wa utumishi wa Makamishna wake unalindwa kikatiba itaondolewa vipi na Tume mpya itapatikana vipi.

(c) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini Katibu wa itikadi na Uenezi anasema hata usiporudiwa ndani ya siku 90, bado Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais.

Nukta hizi tatu ambazo haziwezi zote kusimama kwa pamoja bila ya kupingana moja dhidi ya nyingine zinaonesha tu ni kwa kiasi gani viongozi wa CCM Zanzibar wamepoteza mwelekeo na hawana uhakika wa nini kitatokea katika kuondokana na mgogoro huu wa kutengenezwa.

2. Taarifa ya CCM haiwasaidii wanachama wa CCM wala wananchi wa Zanzibar kwa kuwapa matumaini ya kumalizika kwa mgogoro wa kutengenezwa wa uchaguzi wa Zanzibar na badala yake inaonekana imelenga kuwachanganya zaidi wananchi kwa maelezo yanayopingana.

3. Taarifa inaonyesha ni jinsi gani CCM kilivyopoteza mvuto kwa kujiweka mbali na wananchi. Taarifa hiyo inapongeza eti kuwepo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakati wananchi wa Zanzibar, bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, siyo tu wanumia kutokana na sera mbovu za CCM lakini sasa wanazidi kuteketea na maisha yao kuwa magumu zaidi kutokana na fadhaa (tension) na taharuki iliyopo katika nchi kutokana na kutokuwepo kwa Serikali yenye ridhaa yao. 

Harakati za maisha zimeathirika sana huku bidhaa vikiwemo vyakula vikipanda bei. Viongozi wa CCM hawaonekani kujali hali hii mradi wao yao yanawaendea. Tabia hii ya CCM kutowajali wananchi wanyonge wa nchi hii ndiyo iliyopelekea wananchi kukiadhibu chama hicho katika uchaguzi mkuu na kupelekea mgombea wake wa Urais wa Zanzibar na wagombea Uwakilishi kushindwa vibaya kwa tofauti ya zaidi ya kura 25,831.

4. Taarifa inaendeleza utamaduni wa unafiki wa kisiasa kwa eti kuwapongeza viongozi wa CCM na jumuiya zake kwa kazi ya kukiimarisha chama chao huku wakijua kwamba viongozi wao hasa wale walioongoza Kamati ya Kitaifa ya Kampeni za CCM Zanzibar walishindwa kazi na kupoteza mwelekeo. 

Matokeo ya kazi mbovu ya Kamati ya Kampeni ya CCM Zanzibar ni kukisababishia chama hicho kipigo kikubwa katika uchaguzi huo kilichopelekea kushindwa katika nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa zaidi ya kura 25,831 na kupoteza viti tisa (9) vya Uwakilishi kisiwani Unguja mbali ya kutopata hata kiti kimoja kisiwani Pemba. Viongozi hao walishindwa kuwajibika licha ya kutumia mabilioni ya fedha walizopewa kwa ajili ya kampeni.

5. Katika maelezo yake ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anaitupia lawama Tume nzima ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kushindwa kazi huku akijua na ikijulikana na kila mmoja kwamba tamko la kufuta uchaguzi limetolewa na Jecha Salim Jecha kinyume na Katiba, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na kinyume na maadili ya kazi yake. 

Katiba inataka Jecha achukuliwe hatua za kufukuzwa kazi kwa kuanza na kumuundia Tume Maalum ya kumchunguza, na siyo kutafuta mbinu za kumlinda kwa kuwaingiza wasiokuwemo.

6. Maelezo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar kwamba Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais hata baada ya miezi mitatu ni kielelezo na ushahidi mwengine wa jinsi CCM isivyoheshimu Katiba. 

Kwa hakika, hili suala la kutaja siku 90 ambalo linatajwa sana na CCM na wapambe wake haijulikani hata linatokea wapi. Hakuna pahala popote katika Katiba ya Zanzibar wala Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar panapotajwa sharti la kurudiwa uchaguzi ndani ya siku 90 kwa sababu Katiba yenyewe na Sheria ya Uchaguzi haina sehemu yoyote inayozungumzia kufuta uchaguzi na kufanya uchaguzi wa marudio.

7. Kwa ujumla, taarifa ya CCM Zanzibar iliyotolewa na Katibu wake wa itikadi na Uenezi inaonyesha jinsi chama hicho kisivyojali madhila wanayoyapata raia, fedheha iliyopata taifa na hali ya kiuchumi inayozidi kudorora kila siku Zanzibar ikiwaathiri mno wananchi wanyonge.

Baada ya uchambuzi huo wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, CUF inapenda kuwaeleza Wazanzibari yafuatayo:

1. Waipuuze taarifa hiyo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar kwani haina lolote jipya zaidi ya kutaka kufunika kombe kutokana na hali ngumu inayotokana na hoja za viongozi wa ngazi za chini na wanachama wa CCM wanaotaka maelezo ya kwa nini chama hicho licha ya kutumia mabilioni ya shilingi kimeshindwa vibaya katika uchaguzi mkuu.

2. Wazanzibari wasubiri taarifa rasmi ya matokeo ya mazungumzo yanayowahusisha viongozi wakuu wa kisiasa yanayofanyika Ikulu Zanzibar ambayo yamo katika hatua za mwisho kumalizika.

3. Wampe nafasi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli, ambaye anaendelea na juhudi katika ngazi za juu kabisa za kuhimiza kupatikana ufumbuzi wa haraka wa mgogoro wa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

4. CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba haitotetereka na itasimamia kwa dhati maamuzi yao waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao.

5. Mwisho kabisa, inaendelea kuwapongeza Wazanzibari kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na kuendelea kutunza amani na utulivu wakati wakisubiri matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya tarehe 25 Oktoba, 2015 ambayo inaashiria ujenzi wa Zanzibar Mpya.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA – CUF
29 DESEMBA, 2015

Diamond Aibuka na Kusema Sababu iliyofanya Wimbo wa Nana Usiwe na Sauti ya Nahreel ‘Nahreel on the beat‘

$
0
0
Nahreel aliwahi kuzungumzia kuhusu kutosikika sign ya ‘Nahreel on the beat‘ kwenye mdundo wa ‘Nana‘… leo kapatikana Diamond Platnumz ambaye amesema copy ya wimbo wa kwanza kabla ya kufanyiwa mastering ndiyo iliyotumika kwenye video na director wa video Godfather… ilipotokea Nahreel kaifanya nyingine inayomtaja Nahreel, director wa video hakuwa tayari kupokea copy hiyo ya wimbo wa ‘Nana‘ ambayo imeongezewa kipande hicho kwa sababu isingefit kwenye dakika za wimbo ulivopangwa.

Papaa Msofe, Alex Massawe Wahukumiwa...Mke wa Marehemu Aangua Kilio cha Furaha Baada ya Haki Kutetendeka

$
0
0
Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, imetoa hukumu kwa mfanyabiashara Marijani Abubakar, almaarufu Papaa Msofe, Alex Massawe na Makongoro Nyerere kwa kosa la kughushi hati ya umiliki wa nyumba iliyopo Mikocheni jijini Dar, mali ya marehemu Onesphory Kituly aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi mwaka 2011.

Kesi hiyo iliyonguruma kwa takribani miaka saba tangu 2007, ilifikia tamati Desemba 22, mwaka huu na kuwakuta na hatia washtakiwa hao baada ya upande wa utetezi kushindwa kuwasilisha vielelezo vinavyowapa uhalali wa kumiliki nyumba hiyo.
AlexMassaweAlex Massawe.

Akisoma hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo, John Nchimbi mbele ya wakili wa Msofe na wenzake, Majura Maghafu alisema kuwa baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, mahakama imeamua kumtangaza mke wa marehemu Onesphory, Mary Kituly kuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo.
“Pia mahakama imewatoza fani ya shilingi milioni 300, Papaa Msofe, Massawe na Nyerere pamoja na asilimia 12 ya fedha hizo kama fidia ya gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo,” alisema Jaji Nchimbi.

Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo, mke wa marehemu, Mary aliangua kilio cha furaha na nduguze mbele ya jaji baada ya kuona haki imetendeka, kitu ambacho hakuwa akikitarajia.

“Yaani siamini macho yangu, maana jinsi kesi ilivyonisumbua kwa miaka saba, nimefarijika sana kwa haki kutendeka maana nilikuwa nikishindana na watu wenye pesa, damu ya mume wangu haijapotea bure, namshukuru Mungu kwa kweli,” alisema Mary alipokuwa akizungumza na waandishi wetu ambapo alimshukuru pia Rais John Magufuli kwani serikali yake inajali haki.
Msofe na wenzake walifunguliwa kesi katika mahakama hiyo mwaka 2007 baada ya kudaiwa kughushi hati ya nyumba kwa kuhamisha umiliki wa nyumba namba 288 iliyopo Mikocheni, Dar iliyokuwa ya marehemu Kituly na kuweka jina lake kisha kumuuzia Masawe kinyume cha sheria.
Ilidaiwa kuwa kabla ya kufariki dunia, marehemu Kituly alimkopa shilingi milioni 30 Msofe kwa dhamana ya hati ya nyumba hiyo kwa makubaliano ya kumrudishia kiasi hicho kwa muda wa miezi sita.

Inadaiwa kuwa baada ya miezi mitano, marehemu alipata kiasi hicho cha fedha na kurudisha kwa Msofe na kutaka hati yake, lakini alianza kuzungushwa kuanzia kipindi hicho hadi alipokufa kwa kuuawa na watu wasiojulikana mwaka 2011.

Oktoba 30, 2007, Msofe aliwatoa kwa nguvu marehemu, mke wake na watoto kwa madai kuwa nyumba hiyo imeuzwa kwa Massawe.

New Born Baby Saved By Dog Is Alive And Well (See Photos)

$
0
0

A stray female dog in Campinas, Brazil, (not Saudi Arabia as originally reported) is being called an "angel sent from the heavens" after the homeless pet saved the life of a newborn baby boy.

The dog, which was scavenging for food in a garbage dump came across the newborn who still had the umbilical cord attached. The smart dog gently carried the baby in its mouth out of the dump, walked a few hundred feet to the closest house and handed the baby over to helpful humans hands. There, as if asking "please help him," the dog showed the humans the baby and left him to their care.

Those people then rushed the baby to the nearest hospital and doctors carefully cared for the tiny newborn. Medical representatives said the baby boy is in great condition and was unharmed by the dog.

Halima Kimwana Blasts Wema Sepetu And Team Wema Over Diamond Platnumz's Success And Dominance

$
0
0

Diamond Platnumz' sister Halima Kimwana has lashed out at Wema Sepetu saying Wema is nothing without Diamond despite the fact that Wema and team Wema have been saying Diamond got success in the music industry through Wema's stardom. Halima who also won a dancing competition "Manywele Kimwana Wa Twanga Pepeta" more than 6 years ago yesterday took to instagram to blast Wema who dated Diamond in the past..


."at first you said he doesn't know music but he uses your stardom...he he heeeee but he has already left you with your stardom but still you keep talking about him, I believe without him you are completely nothing ha ha haaaa...in recent times you did many things but they all soured, you want kick from him, nothing new from you, people are tired of you, a lion(Diamond) is your size who doesn't know ???, I have no time to have a fake account everything will be here"

Though no blood ties, Halima is so close to Diamond and the whole Platnumz family but she never was good friend to Wema, and last year Wema was quoted as saying she will never talk to Halima and befriend with her, she said she hates Halima Kimwana more than anything else.


Tahadhari Kali Kwa Nyote Mlio na Magari Binafsi; Chunga Sana na Waambie Wengine!

$
0
0
Hasa kwa wale wanaonunua magari kwa mara ya kwanza, na hawana uzoefu wa kuendesha gari, na pia wale wote ambao wanaweza wakawa wana uzoefu wa kuendesha gari mijini, lakini hawana uzoefu wa kuendesha gari kwenye bara bara kuu za kwenda mikoani.

Lakini ni vema kila mtu aliye dereva akasoma ninachoeleza hapa. Inaweza kuokoa maisha yako ya familia yako, na wengine wanaoendesha magari au kuwa abiria.

Ndugu zangu, ukiweza kuendesha gari hapa Dar au hata mikoani mijini, haina maana utaweza kuendesha gari pasipo tatizo kwenye barabara kuu. Nimeshuhudia watu wengi sana waliokufa kwa sababu baada ya kununua gari walikuwa na mchecheto wa ku-drive kwenda kwao kijijini.

Kuendesha gari kwenye barabara kuu ni tofauti sana na kuendesha gari mijini. Kwenye barabara kuu challenge zake ni kubwa sana kwa sababu gari zinaenda kwa kasi, na pia kuna mambo mengi ya ghafla yanayoweza kujitokeza ambayo kama huna uamuzi wa haraka kama dereva utakufa tu kabla ya kufika mwisho wa safari yako. Ukifanya kosa hata dogo barabara kuu unaweza kufa, tofauti na mijini.

Kwa mfano, ku-overtake katika barabara kuu ni jambo linatakiwa lifanywe kwa makini sana. Na pia kila unapoingia kona kali au blind spot kwenye barabara kuu weka akilini kwamba unaweza kukutana na kitu upande wako, basi linaloenda kasi, lori au trekta liloharibika, mifugo, shimo kubwa, mawe yaliyoporomoka, ajali nk. Pia unaweza kukutana ghafla na dereva mzembe anae-overtake kwenye kona na yuko upande wako.

Usithubutu ku-overtake sehemu ambayo huoni mbali mbele, na usikaribie sana gari unayotaka ku-overtake kabla ya kui-overtake. Na unapo-overtake kama una gari manual gear, rudi gia za chini kwanza ili kujenga spidi ya ku-overtake. Kama una gari automatiki, ikibidi itoe gari kwenye overdrive (unabonyeza kiswitch cha Overdrive na kuna kataa katawaka kwenye dashboard kuonyesha Overdrive iko off), hasa kama ulikuwa umepunguza mwendo. Mara nyingine toa gia kwenye "D" na rudi kwenye "2" ili kujenga spidi ya ku-overtake, na ukishamaliza rudi kwenye D na Overdrive. Hili ni muhimu sana kwa gari za ambazo ukikanyaga accerator gari inakawia kuchanganya. Overtake kwa haraka, sehemu ambayo iko salama, na ni vizuri gari unayoi-overtake dereva wake ajue unamu-overtake. Unaweza kumpigia honi kidogo ya kuibia kama kuomba - usipige kwa nguvu ukamuudhi. Epuka kuovertake sehemu ya barabara yenye mashimo, maana dereva wa mbele anaweza kurudi upande wako ili akwepe shimo wakati tayari unamu-overtake.

Siri moja ya ku-overtake salama ni uvumilivu - overtake nzuri haitaki haraka.

Na pia kosa linaloua watu wengi sana ni ku-overtake kwa kukisia kwamba hakutakuwa na gari inayokuja upande wa pili zile sehemu ambazo huoni vizuri mbele. Hata kama barabara haina magari mengi usithubutu kukisia kwamba hakutakuwa na gari (gambling overtake).

Na pia katika barabara kuu kuna suala la uchovu - fatigue. Hili ni jambo jingine linaua sana watu wasio na uzoefu wa kuwa katika barabara kuu. Ni mbaya hata zaidi ikiwa utakaposimama mahali kwa chakula ukanywa bia - hata moja tu, kwa sababu itakuletea sana usingizi. Epuka kula vyakula vizito kama ugali na maharage, au kula hadi ukashiba sana! Ukisikia usingizi simama upumpzike, toka ndani ya gari, tembea kidogo, kabla ya kuendelea na safari. Kama ikibidi tumia Redbull (sio zaidi ya mbili).

Na jambo jingine muhimu sana la kukumbuka ni kwamba ukiingia barabara kuu, ukaendesha kwa muda fulani, akili yako inazoea spidi kali kiasi kwamba huoni tena kama unaenda spidi kali. Unaweza ukawa unaenda 140km/h ukaona kama unaenda 80km/hr. Hili huwa mara nyingi linasababisha kuacha njia na kupinduka, au kuingia kona ukiwa na spidi kubwa na gari kupinduka. Nadhani umesikia sana ajali zinazosemwa zilitokea kwa sababu dereva alishindwa kumiliki gari - ni kwa sababu akilini dereva aliona haendi spidi.

Na pia jambo jingine muhimu sana kukumbuka ni kwamba, unapoenda safari yoyote ya mbali ambayo utaendesha gari mfululizo kwa zaidi ya masaa manne, au kwa spidi zaidi ya 100km/hr, hakikisha tairi zako hazina umri zaidi ya miaka mitano, la sivyo utapata basti hata kama tairi inaonekana bado mpya kwa kuitazama. Tairi ikizidi miaka mitano haifai kusafiria safari ya mbali, japo unaweza ukaendelea kuitumia kwa safari za mijini.

Nimeona niseme haya kwa sababu nawapenda ndugu zangu. Sitaki mufe barabarani au mniue mie na familia yangu. Wapeni taarifa wengine ili tuzidi kuepuka vifo hivi vya barabarani ambavyo vingi vinazuilika.

Neno langu la mwisho, ili uendeleee kuwa salama barabarani ni kwa lugha ya kiingereza; BE PATIENT kwa lolote unalotaka kufanya ukiwa unaendesha gari. Zingaitia hilo, utakuwa salama.

Muhimu Pia......
Tahadhali nyingine kubwa juu ya matumizi ya gari ni kwamba hata siku moja usithubutu kuwafungia watoto ndani ya gari lililofungwa vioo ili ukimbie mara moja kufanya shughuli fulani. Hii huwa inasababisha vifo kwa watoto au hata kiumbe chochote kilichofungiwa ndani ya gari, hasa sehemu za joto kama Dar ambapo kifo kinaweza kutokea baada ya dakika 20. Na pia kumbuka huwezi kujua nini kitakupata huko uendako; labda utapata mshituko wa moyo ukimbizwe hospitali au tukio lolote litakalokufanya ushindwe kurudi kwenye gari yako ambayo umefungia watoto ndani yake. Ikibidi kuwaacha watoto ndani ya gari basi acha vioo wazi na usi-lock gari - lakini kwa ujumla epuka kuacha watoto peke yao ndani ya gari.

Na ikiwa mtu utakuta watoto wamefungiwa ndani ya gari, ita walinzi na watu wengine kama mashahidi, au polisi kama wapo karibu na vunjeni kioo cha gari ili kuokoa watoto. Siku hizi unaweza kupiga simu kuita Polisi kirahisi sana; piga namba 111 au 112 kutumia simu yako ya mkononi. Lakini msisubiri hadi Polisi wafike ili kuvunja vioo - mnaweza kuchelewa kuokoa watoto.

Imeandikwa na Synthesizer-JF

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Tarehe 30 Disemba, Ikiwemo ya Lowassa Kuondolewa Ulinzi

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Tarehe 30 Disemba, Ikiwemo ya Lowassa Kuondolewa Ulinzo

Kampuni Za Simu Zatozwa Faini Kwa Kuwapa AJIRA Raia Wa Kigeni Kinyume Cha Taratibu

$
0
0
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amebaini kuwepo kwa wafanyakazi wa kigeni, walioletwa na kampuni za simu za mkononi kufanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania ikiwemo kufunga meza na viti vya kukalia.

Aidha, amebaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Halotel, raia wa Vietnam, ambao wanaishi nchini bila kibali cha kazi wala cha kuishi. Mavunde aliyabaini hayo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua vibali vya ajira kwa wageni, baada ya tangazo lililotolewa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama.

Akiwa katika kampuni hiyo ya Halotel, Mavunde alibaini kuwepo kwa baadhi ya mapungufu, ikiwemo baadhi ya wafanyakazi kutopewa mikataba ya ajira na wenye ajira kutopewa nakala za mikataba yao.

Mavunde aliagiza viongozi wa kampuni hiyo, kuhakikisha kufikia leo wafanyakazi wote wanapewa mikataba huku nakala za mikataba hiyo, ikipelekwa ofisini kwake na pia kuwataka kulipa madeni ya wafanyakazi, hasa madereva, ya saa za ziada (overtime) haraka iwezekanavyo.

“Tumegundua kuwepo kwa mapungufu mengi katika kampuni yenu, hii ni pamoja na wafanyakazi wenu kutojiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kumekuwa na makato ambayo hayapo kwa mujibu wa sheria za kazi.

"Lakini pia kuna wageni ambao wako katika hii kampuni yenu, wanafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania, kwa mfano huyu anayefunga viti, hii kazi inafanywa na vijana wetu…kibali chake kinaisha kesho, naagiza asipewe kingine na aondoke,” alisema Mavunde.

Aidha, alisema katika masuala ya usalama mahali pa kazi, pia kuna mapungufu mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi kutopewa mafunzo ya kukabiliana na majanga, vipimo vya afya na makosa mengine ambapo kwa mujibu wa sheria aliwatoza faini ya Sh milioni sita.

Hata hivyo, wakati akiendelea kutoa maagizo hayo, mmoja wa maofisa wa Ubalozi wa Vietnam, Mai Anh Thai aliingia katika ukumbi wa mkutano na kutaka kumkatisha Naibu Waziri kwa madai kuwa hakufuata utaratibu.

Kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa huko, ilimlazimu Mshauri wa kampuni hiyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, kumshauri ofisa huyo taratibu za ukaguzi zilivyo.

Baada ya kutoka katika kampuni hiyo, Mavunde na maofisa wa Uhamiaji, Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana na askari walilazimika kufika katika nyumba ambayo iko Mikocheni, ambako inasadikiwa kuwa wapo raia wengi wa Vietnam wanaoishi hapo, huku wengine wakiwa hawana vibali vya kuishi wala vya kazi.

Walipofanya msako katika nyumba hiyo, baadhi ya raia hao walijificha na kufanikiwa kumkamata mmoja ambaye hakuwa na kibali chochote. Hata hivyo, mmoja wa walinzi wa nyumba hiyo alisema raia hao walikuwa wengi, lakini baadhi yao walitoroshwa juzi usiku.

Awali akiwa katika Kampuni ya Airtel, Mavunde aliwapiga faini ya Sh milioni nne kutokana na kuwepo na mapungufu mbalimbali katika masuala ya usalama na afya mahali pa kazi, ambazo wanapaswa kulipa ndani ya siku 14.

Aidha, aliwataka waajiri nchini kote, kuhakikisha wanasimamia sheria za kazi ili kujenga nchi ambayo haina misuguano. Mavunde alionya kuwa wanaobeza kuwa hiyo ni ‘nguvu ya soda’, wafute jambo hilo, kwani kazi hiyo ni endelevu.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images