Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Shilole Amtaja Mpenzi wake Mpya Mwanamuziki Kutoka Uganda, Adai ‘’Nuh Hanipendi"

$
0
0
Kwa sasa ni dhahiri kabisa penzi la Shilole na Nuh Mziwanda limefika mwisho baada Shishi kumtambulisha mpenzi wake mpya msanii,Eddy Kenzo kutoka nchini Uganda.


‘’Nuh hanipendi Eddy Kenzo ndio ananipenda,ameniimbia wimbo nilikuwa sijui,naomba mjue kuwa ndiye mchumba wangu mpya,’’Alisema Shilole.

‘’Eddy Kenzo amenipenda tangu zamani lakini nilikuwa nikimpuuzia tu maskini ameonyesha upendo wake kwangu hadi kaimba wimbo kwa ajili yangu unajua sio kitu kidogo msanii mkubwa Afrika kuniimbia wimbo mimi amechukua tuzo ya BET mwaka huu,ananipenda na mimi nampenda sana,’’Alisema Shilole.

Huyu Ndo Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi .....Kazi Kwenu Majangili

$
0
0
Pichani ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye leo ameapishwa rasmi kuanza kupambana na majangili ambao wamekuwa kero kwa nchi hii.

Ikumbukwe kuwa kuna wakati Tanzania ilifikia kuwa kinara cha matukio ya ujangili kiasi cha Serikali ya Awamu ya Nne kuanzisha Operesheni Tokomeza ambayo nayo haikuisha vizuri.

Maliasili ya Tanzania ikitunzwa vizuri inaweza kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa nchi ambayo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi kupitia utalii.

Tunakutakia kila la heri katika majukumu yako mapya Meja Jenerali Gaudence Milanzi.

Mh. Diwani Laivu Akimbambia Mwanamuzki Linah....Ni Kwenye Party ya Shilole Kujipongeza Kuachana na Nuhu Mziwanda

$
0
0
Diwani Baba Levo Akibambia Mtoto
HII ni aibu ya kufungulia mwaka 2016! Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mwanga Kigoma-Kaskazini, Clayton Revocatus ‘Baba Levo’, amenaswa laivu akimbambia staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ usiku mnene, Ijumaa limeshuhudia tukio hilo mwanzo mwisho.

SIKU YA TUKIO
Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 29, Mwaka huu Kijitonyama jijini Dar, ambapo wawili hao walikuwa wamehudhuria kwenye bonge la pati lililokuwa limeandaliwa na msanii mwenzao Zuwena Mohamed ‘Shilole’.


NI PATI YA KUACHANA
Shilole aliandaa sherehe hiyo maalum kwa lengo la kufurahi pamoja wakati akijipongeza baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

BABA LEVO NDIYE MC
Wakiwa kwenye sherehe hiyo, Baba Levo alikabidhiwa jukumu la kuwa mshehereshaji (MC) wa pati hiyo, ambapo alianza kwa kuwakaribisha wageni wote waalikwa kisha kuianza sherehe rasmi.

MTUNGI MDOGOMDOGO
Kama ilivyo ada ya watoto wa mjini wanavyosema sherehe hainogi bila ‘maji ya Ilala’, Baba Levo aliungana na wageni waalikwa kuanza kupiga ‘maji matamu’ taratibu huku wakionekana kuchangamka kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma.

LINAH AANZA KUCHANGAMKA
Linah ndiye aliyekuwa wa kwanza kuonesha kwamba ‘mambo’ yamepanda kichwani baada ya kuinuka mahali alipokuwa amekaa na kuanza kucheza muziki huku akirusha miguu kama ile staili ya Mapanga Shaa ya Wanaume Halisi.
IMG_8730
Mastaa kibao walikuwepo kwenye pati hiyo.

UVUMILIVU WAMSHINDA MH. DIWANI
Mheshimiwa diwani huyo mwenye mbwembwe na maneno mengimengi ya kufurahisha, naye uvumilivu ulimshinda ambapo alijikuta akiinuka na kuanza kucheza peke yake huku akionekana kumkodolea macho zaidi Linah ambaye wakati huo alikuwa amezidisha mbwembwe.

KABAAAH! AMBAMBIA
Huku na huku haikupita muda mrefu sana, Baba Levo alijikuta tayari yupo kwenye mgongo wa Linah na kuanza kucheza naye huku mrembo huyo akimpa ushirikiano kama anayesema: “Ulikuwa wapi muda wote nateseka kwa kucheza peke yangu.”

WAALIKWA FULL KUSHANGALIA
Kutokana na waalikwa wengi kuwa tayari ‘wameshapendeza’, kadiri Baba Levo na Linah walivyokuwa wakicheza kwa staili ya kukata mauno huku mheshimiwa huyo akiwa amemkumbatia vilivyo Linah, waalikwa walishangilia kwelikweli.
IMG_8732Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo kinaga ubaga aliendelea kuwafuatilia wawili hao kwa kupiga picha ambazo zilidhihirisha wazi kuwa hawakuwa wao bali yale ‘maji’ waliyokunywa.

MASTAA WALIOHUDHURIA
Kwenye sherehe hiyo ambayo waalikwa walikula na kunywa, mastaa wengi walihudhuria akiwemo Mtangazaji Millard Ayo, Said Chigunda ‘Chegge’ (Bongo Fleva), Baby Madaha (Bongo Fleva), Isabela Mpanda (Bongo Fleva), Skyner Ally ‘Skaina’ (Bongo Movies) na wengineo.

Magufuli Utaua Mawaziri Waliopita Kwa Njaa, Hawana Cha Kufanya

$
0
0
Mh. Magufuli kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri uliyoifanya mpaka sasa, japo sijutii kura yangu niliyompa mamvi na wala sitakaa nijutie, tulikuwa tunataka mabadiliko na sasa ninayo furaha ya dhati kabisa kuyaona haya mabadiliko kupitia kwako

Pili Mh. Nilichofurahi zaidi ni kupunguza gharama kubwa za kuhudumia wizara na mawaziri wake 60 wa awamu iliyopita hakika wewe ni mzalendo, na samia pia najua aliupata uzalendo zaidi katika kipindi za kampeni kijiji kwa kijiji nilimshuhudia akimwaga chozi kwa shida za wananchi alizokumbana nazo huko vijijini hakuamini na alituahidi na wasanii wakiwepo(mashahidi) mtaipitia mikataba yote ya madini

Mh. Magu chukua hii kama New year special, ulivyowatimua wastaafu mawaziri kwenye nyumba za serikali wengine hawana pa kukaaa, hakya Mungu tena ninaapa, hawakuona umuhimu wa kujenga kwa maana walijua nyumba za serikali ni zao

so sad , kuna mmoja anakaa kwa shemeji yake, (kaka wa mke wake) amechoka vibaya, sasa mbaya zaidi kaja na kuku wake kila siku wanatifua bustani za majirani maana humo ndani hamna banda wanafugia nje inaleta usumbufu mno, na hataki kuondoka mpaka ahakikishe kwamba hata ukuu wa wilaya amekosa ndio atarudi mwanzaaaa

Ninachokuomba Mh. harakisha hizo teuzi usifanye kwa nukta nukta utaua watu na njaa, hawana pa kuishi, hawana kazi, ubunge wamekosa, january hii watoto adaa mheshimiwa ujue hawasomi shule za kata, soon watakosa chakula na mimi ninasema ikifika february kuku wake wakiendea kutifua bustani yangu nakula mmoja baada ya mmoja

Seif Rais Zanzibar, Maandalizi ya Kutangazwa yaiva

$
0
0
USHINDI wa Maalim Seif Shariff Hamad katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, ungali salama.

MAWIO limeelezwa kuwa ushindi huo utadhihirishwa kabla ya Zanzibar kufikia kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi.

Taarifa zinasema viongozi wa kitaifa, wakiwemo marais wastaafu Zanzibar, ambao wamekuwa wakikutana na Maalim Seif, Ikulu ya Zanzibar, wanakaribia kukamilisha utaratibu wa kuwezesha kiongozi huyo kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo.
“Hili halina utata wowote. Nakuhakikishia wanakaribia kuona mantiki na kuelewana; utaratibu wa kumtangaza Maalim Seif utatolewa wakati muafaka,” amesema mwanadiplomasia kutoka moja ya mataifa ya Ulaya.

Amesema kwa kadri anavyofahamu, maendeleo ya mazungumzo hayo yanayomhusisha pia Rais Dk. Ali Mohamed Shein, katika siku za karibuni, yamejikita katika kupata uhakika kuwa serikali mpya itaundwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria na katiba.

Lakini amesema, hata suala hilo halijawa tatizo kwa kuwa mfumo wa kuunda serikali umesukwa vema katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

“Kama unavyojua mfumo wa serikali utakuwa uleule wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwa matokeo ya uchaguzi vyama vya CCM na CUF ndivyo vitaunda serikali mpya,” alisema.
Mwanabalozi huyo aliulizwa na mwandishi jinsi anavyoona hali ya kisiasa kwa sasa na hasa kuhusu mgogoro uliotokana na uchaguzi.

Mgogoro wa sasa Zanzibar ulitokana na uchaguzi mkuu kufutwa kiubabe na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Jecha alifuta uchaguzi kwa tangazo lililorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) mchana wa Oktoba 28.

Wakati huo tayari Jecha alikuwa ameshatangaza kura za majimbo 33, akibakiza majimbo 21 tu.
Mwandishi alilenga kupata msimamo wa Jumuiya ya Kimataifa kuhusu kauli tata za viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu aliwataka wana-CCM kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio aliosema utafanyika “wakati utakapowadia.”
Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari ndani ya CCM, Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano, hakutakuwa na uchaguzi wowote bali utakuwepo utaratibu wa kumtangaza mshindi.
Chanzo katika CCM kimesema, “Hili liko wazi, mshindi wa uchaguzi ule ni Maalim Seif wa CUF ambaye naweza kusema amefanikiwa kusimamia ushindi wake huo na hoja zake hazishindiki. Nakwambia atatangazwa siku chache zijazo.”
Kiongozi huyo ambaye aliomba asitajwe jina gazetini, amemsifia Maalim Seif kwa kubaki mtulivu wakati wote akijadiliana na viongozi wenzake ambao wote ni kutoka CCM.

Katibu Mkuu huyo wa CUF na mwanasiasa ambaye amekuwa akilalamika kuhujumiwa mara zote akigombea urais, amekuwa akishiriki mazungumzo na marais wastaafu.
Marais hao ni Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume na Dk. Shein. Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi naye amehudhuria mazungumzo hayo.
Dalili za kuwepo muafaka katika majadiliano zimeonekana hivi karibuni pale Dk. Shein, aliyekuwa akigombea urais kwa mara ya pili, na Maalim Seif walipokutana na Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika nyakati tofauti.

Wote walisikika wakisema majadiliano yao yanaendelea vizuri, lakini Dk. Magufuli akieleza waandishi wa habari nje ya ofisi yake Ikulu baada ya kukutana na Maalim Seif kuwa, “amenihakikishia wanaendelea vizuri na nimemtaka wakamalize majadiliano yao na apige kazi.”
Dk. Shein alipotoka nje ya maongezi na Dk. Magufuli aliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri na yatakapomalizika, watatoa taarifa kwa umma kuwaeleza maafikiano yaliyofikiwa.

Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema moja ya mambo ambayo Dk. Shein alitakiwa kuyafanya baada ya hapo, ni kukutana na Kamati Maalum ya NEC-CCM, kuwaeleza maendeleo ya vikao na viongozi wenzake vinavyofanyika Ikulu.

Jumapili iliyopita, MAWIO lilielezwa kile kilichotokea katika kikao kilichofanyika Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kilichoandaliwa kwa ajili ya Dk. Shein kutoa taarifa yake.
Katika kikao, Dk. Shein “alitoa taarifa yake na taarifa yenyewe kujadiliwa vizuri” mpaka kikao kilipomalizika yapata saa 9.30 alasiri.
Dk. Shein aliondoka na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kumaliza kikao.

Lakini baada ya viongozi hao wakuu kuondoka ukumbini, baadhi ya wajumbe waliobaki walianza kudai kuwa hawakubaliani na mapatano na kwamba wanataka uchaguzi urudiwe.
Gazeti hili limeambiwa baada ya Dk. Shein kuondoka Kisiwandui, Balozi Seif alifuatana na baadhi ya viongozi kwenda Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, iliyoko Amani, ambako walifanya mjadala ulioibua kilichoitwa “kauli za chuki” zikimlenga Maalim Seif.

Kwa kuzingatia aliyoyasema Dk. Shein, baadhi ya viongozi walionekana wakifuta machozi kwa kilichoelezwa ni “kutoamini kwao kuwa CUF itapishwa kuongoza serikali mpya.”
Akijibu hoja ya kurudia uchaguzi ambayo wananchi wengi wameonesha kuipinga, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma wa CUF, Ismail Jussa Ladhu amesema kurudia uchaguzi siyo chaguo la wananchi.

Aliwaambia waandishi wa habari mgogoro wa Zanzibar ni wa kutengeneza, uliolenga kuchanganya wananchi na kuwapora ushindi wao. Ametaka wananchi wapuuze kauli za kurudia uchaguzi.
“CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba haitotetereka; itasimamia kwa dhati maamuzi waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi mkuu na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao,” alisema Jussa.

Amepongeza wananchi kwa kuonesha “ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na kuendelea kutunza amani na utulivu wakati wakisubiri matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya tarehe 25 Oktoba ambayo inaashiria ujenzi wa Zanzibar Mpya.”

Ni msimamo wa CUF kuwa Maalim Seif alishinda uchaguzi kwa zaidi ya kura 25,000.
Kwamba CUF ilipata viti 27 vya uwakilishi. Kwamba CCM ilishindwa kupata kiti kisiwani Pemba. Kwamba CUF ilitwaa viti tisa Unguja.

Edward Lowassa Alalamikia Wafuasi wake Kuandamwa na Watendaji wa Serikali.

$
0
0

Aliyekua mgombea Urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA Mh.Edward Lowassa amelalamikia baadhi ya watendaji wa serikali kwa kuwaandama na kuwatisha wananchi na wafanyabiashara waliokuwa wanaunga mkono vyama vya upinzani na amezitaka idara zinazohusika kuchukua hatua ili kuepusha  matatizo yasiyo ya lazima.

 

Akizungumza katika ibada maalum ya kukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika kanisa la kilutheri wilayani Monduli Mh Lowassa amesema amepokea malalamiko ya kuwepo kwa uonevu  na vitisho kwa wadau walioonekana kuunga mkono vyama vya upinzani licha ya kuwa ni haki yao kikatiba.

Pia Mh Lowassa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa tiketi ya  (CCM) kabla ya kuhamia Chadema na kuwa mgombea urais amesema ataendelea kusaidiana na mbunge wa sasa Mh Julias Kalanga (Chadema) kutatua kero za wananchi na kuhakikisha kuwa misingi aliyoijenga inakuwa endelevu.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini na wananchi waliohudhuria ibada hiyo wamepongeza uvumilivu wa kisiasa ulioonyeshwa na Mh Lowassa ambao umeendelea kuimarisha amani na utulivu  nchini na wamewaomba wanasiasa wengine kuiga mfano huo.

Rais Magufuli atangaza vita na mafisadi, wauza dawa za kulevya 2016

$
0
0


RAIS Dk. John Magufuli, amesema Watanzania wote wanapaswa kuendelea kumuombea ili aendelee na kazi yake ya kupambana na mafisadi wahujumu uchumi na vigogo wauza dawa za kulevya nchini.

Kauli hiyo iliitoa katika mkesha mkubwa wa kuliombea Taifa pamoja na kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema Taifa hili kwa kipindi kirefu lilikabiliwa na vigogo wauza dawa za kulevya, watumishi na vigogo wakwepaji wa kodi pamoja na wizi wa dawa mahospitalini hivyo viongozi wa dini na Watanzania wote wanapaswa kumuombea ili aweze kutumbua majipu ya mafisadi hao.

Amesema ubadhilifu wa mali za umma umekuwa ukichangia kuzorotesha maendeleo ya Watanzania wote kutokana na watu wachache wasiokuwa waadilifu serikalini kuendelea na vitendo vya rushwa huku wengi wakiendelea kutaabika.

Dk. Magufuli ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, William Lukuvi, amesema kuwa viongozi wa dini wanapaswa kuendelea kuliombea Taifa na kuwaombea watu wabaya wasiopenda maendeleo waweze kubadilika ili nchi iweze kusonga mbele.

“Viongozi wa dini tunapaswa kuendelea kumuombea rais wetu (Dk. John Magufuli) aendelee kutumbua majipu haya ambayo yanasababisha maendeleo ya Taifa letu kurudi nyuma.

“Watanzania wenzangu tunapaswa kuendelea kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais Magufuli (John Magufuli) aendelee kufanya kazi yake zaidi, kuna wizi wa dawa katika vituo vya Afya watumishi wazembe ambao hawafanyi kazi ya umma vizuri sasa hayo yote yanahitaji ushirikiano wetu kwa rais aweze kusimamia,”amesema Lukuvi.

Hata hivyo katika salamu zake, aliwataka Watanzania wote kwa ujumla bila kujali itikadi za vyama na dini zao kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo tangu Taifa hili linapata uhuru mwaka 1964.

Hata hivyo tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani ameweza kuwang’oa vigogo kadhaa katika nyadhifa zao kwa tuhuma mbalimbali, kitendo ambacho kimeonekana kuwachukiza baadhi ya viongozi na watumishi wa umma ‘mafisadi’.

Baadhi ya viongozi waliong’olewa mpaka sasa ni aliyekuwa Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Rished Bande, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Viongozi wengine waliondolewa katika nyadhifa zao ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Diwani Msemo, aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (DART), Asheria Mlambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali Reli Tanzania (RAHCO), Benhadard Tito.

Pamoja na kuwang’oa vigogo hao, pia baadhi ta watumishi kwenye taasisi hizo nao wameguswa na fagio lililowaondoa katika nafasi zao, kwa sababu ya kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili huku na wengine wakigikishwa mahakamani.

Naye Askofu Geoffrey Manashi, amesema Watanzania wanapaswa kuendelea kuliombea Taifa kuendelea kuwepo amani kwani bila amani hakuna maendeleo katika taifa lolote lile.

Amesema uchaguzi wa mwaka 2015 watu wengi walikuwa na imani kwamba Taifa hili litaingia katika machafuko lakini mwenyezi Mungu aliweza kulivusha salama na kufanikiwa kumpata Rais Dk. John  Magufuli, ambaye ameweza kufanya kazi yake kwa kasi kubwa ambayo watu wengi walitarajia.

Naye Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye amesema kuwa baadhi ya wanasiasa na wananchi walidhani Taifa litaingia katika vurugu na machafuko lakini wameshangaa kuona uchaguzi umemalizika kwa amani.

“Wapo waliodhani tutaingia kwenye machafuko, lakini imeshindikana, hiyo yote ni kutokana na Mungu wetu kutuvusha salama na tumepata rais mzuri ambaye sasa hivi nchi nyingi zinatamani ziwe nae,”amesema Nnauye.

Naye Askofu kutoka nchini Kongo, Debora Sanganyi, amesema Watanzania wanapaswa kuwaombea wakongo na wao waendelee kuwa na amani iliyopo hapa nchini kwetu.

Amesema kuwa Kongo na wao wanatarajia kufanya uchaguzi mkuu hivyo Watanzania wanapaswa kuwaombea na kumpata rais mchapa kazi kama Rais John Magufuli.

“Jamani na sisi wakongo mtuombeeni kuvuka salama yale yanayokuja, tupate rais mzuri kama wa kwenu, watanzania tuombeeni ndugu zenu,” amesema Sanganyi.

Nigerian Tekno Posted This Photo With Lulu And ....This Is What Happened On The Internet !

$
0
0

Nigerian singer Tekno yesterday performed in Dar es salaam at a huge crowd to celebrate new year. One of Tanzanian celebrities who attended the event is actress Lulu Elizabeth Michael and they took a selfie together.
Apparently Tekno posted it on his instagram account with caption "how do you see" and the photo soon went viral on social media some fans speculating they are new couple in town since before Tekno also posted a video of Lulu with her lil bro..




Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Jaruari 2, 2016, Ikiwemo ya Utajiri wa Diamond Kuwa Mashakani...

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Jaruari 2, 2016, Ikiwemo ya Utajiri wa Diamond Kuwa Mashakani...


Mastaa Wanaodaiwa Kuwauza Wenzao Kwa Wanaume Wenye Pesa Watajwa

$
0
0
Aunty Lulu
MASTAA kadhaa hapa Bongo wamekanyaga skendo ya kudaiwa kuwauza wenzao kwa wanaume ambapo katika orodha hiyo wamo Lungi Mwaulanga,Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ na Maimartha Jesse.

Chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, mastaa hao ndiyo wamekuwa wakitumika kuwaunganisha wasaniii wenzao kwa mapedeshee huku wao habari hii, waandishi wetu walizungumza na wahusika ambao kila mmoja alifunguka kivyake.

LUNGI: Mh! Mimi mtu akimtaka mtu f’lani huwa nampa namba tu, wanajuana wenyewe, kwani dhambi? MAI: Mimi niwauze wenzangu, acha hizo bwana, mimi nauza bidhaa zangu.

ANTI LULU: Hivi kumpa mtu namba ya staa ni kumuuza? wakiambulia ‘cha juu’. “Wanafanya hako kabiashara kishkaji sana, akitokea mwanaume kumtaka staa f’lani wao ndiyo wanagawa namba au kuwaunganisha kabisa kisha nao wanalipwa. Katika kubalansi

Source:Global Publishers

Am In Love With My Sister. Please Help Me!

$
0
0

Dear Admin,

I hope this meets you well and I beg of you to post it.

What I’m about to say is considered a taboo in Africa but to us it’s not. I’m in love with my sister. We are in love with each other. My blood sister .She is 23 and I’m 27.

We have been dating each other for 2 years and people mistake our closeness for brotherly/sisterly love. It started after my ex-girlfriend of 5 years broke my heart in 2010 and left me for my friend.

My sister was my comforter and before we knew it, things became romantic. No one should judge us because it’s real love.

She was a virgin and she gave it to me. It’s a shame we found love in a hopeless place.

The problem is how to break the news to our parents that we want to get married. Our plan is to elope to another country where this is not a taboo and get married.

Please do you and your readers know any country? I heard about China but I need English speaking countries. Please help me.


Picha: Alikiba Avuta Umati wa zaidi ya Watu elfu 10 Machakos, Kenya

$
0
0
“Show imepata mahudhurio makubwa ya wapatao watu zaidi ya 10,000,” msemaji wake ameiambia Bongo5.

“Ilihudhuriwa na viongozi wa serikali ya county ya Machakos akiwepo Gavana na familia yake. Aliperform kuanzia 00:00 mpaka 03:00.”

Jionee picha zaidi.





Hoyce Temu Afunga Mwaka Kwa Kutembelea Kituo cha Kulea Wazee, Lundenga Amtaja Kuwa Miss Bora Kuwahi Tokea Tanzania

$
0
0
IMG_9916IMG_9920
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) kushoto Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye ( wa pili kulia), Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa (kulia) pamoja na mpiga picha wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Geofrey Magawa a.k.a KIM (kushoto) wakiwasili Desemba 31, 2015 kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Miss Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amemaliza mwaka 2015 kwa kutembelea kituo Nunge ambacho ni makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza kilichopo Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hoyce ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ikiwa ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss kwa jamii pia kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali na katika halfa hiyo aliongozana na watu wake wa karibu ikiwepo kamati ya Miss Tanzania.
Katika halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika Beach, Hoyce baada ya kuwasili kituoni hapo yeye na timu nzima aliyoongozana nayo walifanya shughuli za kijamii katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia dawa za kuulia wadudu katika nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice na biskuti na baadae wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu wasiojiweza.
Akizungumzia halfa hiyo ya kufunga mwaka, Hoyce Temu alisema kumekuwepo na kusahaulika kwa makundi ya watu wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda wanazidi kusahaulika na jamii inayowazunguka.
Alisema yeye kama Miss Tanzania ana wajibu wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi kwa kujumuika nao kwa kuwapa msaada na kuwafariji kwani nao wana thamani kama binadamu wengine.
"Kadri inavyokwenda kumalizika karne ya 21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya wasiojiweza na mimi kama Miss Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia makundi haya kwani ni wajibu wetu na tukumbuke na sisi tunaelekea huko," alisema Hoyce.
Aidha Hoyce alitoa ushauri kwa mamiss wenzake kuwa wanatakiwa kuisaidia jamii kwa kutumia fursa walizonazo mbele ya jamii kwa kutoa misaada kwa makundi ya aina mbalimbali.
Alisema kazi ya kusaidia jamii siyo ya serikali pekee na wao kama mamiss na watu wenye uwezo kwa ujumla wana wajibu wa kusaidia na sio kutazama mijini pekee kutokana na kundi kubwa la wasiojiweza kuwa vijijini.
"Sio swala la serikali pekee ... ukichaguliwa kuwa mrembo unakuwa na malengo ambayo umeyaweka hivyo watumie umaarufu, sura zao na sauti kufikia watu wa aina mbalimbali ambao wanahitaji msaada, " Na sio wazee pekee, 65% ya nchi yetu ni vijana na 20% wanajihusisha na kutumia madawa ya aina mbalimbali hivyo wanaweza kuwatembelea na kutoa elimu juu ya athari za utumiaji wa madawa hayo," alisema Hoyce.
IMG_9931
Mdau Matukio Chuma na Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith wakifurahi jambo wakati walipowasili kwenye kituo cha Nunge.
Nae Mkurugenzi wa Lino International Agency, ambayo ndiyo waandaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga alimtaja Hoyce kama Miss bora kuwahi kutokea tangu walipoanzisha shindano la Miss Tanzania mwaka 1994.
Alisema mamiss wengi wamekuwa wakiisaidia jamii lakini Hoyce amekuwa akijitoa zaidi kuliko wengine na kufanya shindano hilo kuonekana kuwa na faida mbele ya jamii.
"Naomba niseme ukweli Hoyce anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa haijawahi kutokea miss aliyejitoa kusaidia jamii kama yeye na wapo wengine wanasaidia ila Hoyce amekuwa mstari wa mbele kwa hilo tunampongeza na tunamwomba azidi kuwa hivyo," alisema Lundenga.
Kwa upande wa Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi amemshukuru Hoyce kwa upendo amekuwa nao kwa kituo hicho ambacho awali aliwahi kukitembelea 2006 akiwa na marehemu Amina Chifupa na kumtaka kuzidi kuwa na moyo huo kwa jamii inayomzunguka.
Mgedzi pia alizungumzia changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uzio hivyo kutokuwa na hali ya usalama, kuvamiwa kwa eneo hilo na wananchi ambalo lina hekali 50.8 na tayari asilimia 50 imevamiwa na tayari taarifa ipo wizarani na wanashughulikia na zingine ndogo ndogo Hoyce akiahidi kuwasaidia.
Nae mmoja wa washiriki aliyeongozana na Hoyce, Tausi Mwenda alisema kuwa amejifunza mambo mengi kupitia halfa hiyo aliyoifanya Hoyce na kuwashauri watu wa aina mbalimbali kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia jamii kama anavyofanya Hoyce.
happy-new-year-2016-6
Baadhi ya wadau waliombatana na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (hayupo pichani) akiwemo Bi. Tausi Mwenda Mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda, (katikati) wakifurahi jambo walipowasili kwenye kituo cha Nunge, makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisalimiana na mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam juzi (Alhamisi) ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimkumbatia rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
IMG_9942
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiendelea kufurahi na rafiki yake wa siku nyingi mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
IMG_9946
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akitazama jicho la upande wa kulia linalomsumbua mzee Mganga Shija (66), ambaye aliomba kusaidiwa matibabu CCBRT wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
IMG_9967
Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi (kushoto) akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo hicho kwa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu aliyeambatana na Kamati ya Miss Tanzania kwenye ziara hiyo.
IMG_9974
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo na Afisa Mfawidhi wa kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi.
IMG_0017
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiserebuka na mmoja wa wazee wanaoishi kwenye makazi ya Nunge kituoni hapo.
IMG_0119
Bi. Edith (kulia) ambaye ni Dada wa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiteta jambo Bi. Tausi Mwenda mke wa aliyekuwa Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda kabla ya kuelekea kwenye zoezi la upigaji wa dawa.
IMG_0135
Baadhi ya nyumbani za makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Tausi Mwenda (kushoto) wakichanganya dawa ya kuulia wadudu tayari kwa kupulizwa katika nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisaidia kupuliza dawa ya kuuwa wadudu katika moja ya nyumba kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.IMG_0144
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akizungumza na mmoja wa wazee (jina lake halikupatikana) kabla ya kumpigia dawa ya kuua wadudu nyumbani kwake wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
IMG_0174
Dada yake Hoyce Temu, Bi. Edith akishiriki kuondoa vyakula vyombo ili kuruhusu zoezi la upigaji wa dawa ya kuulia wadudu kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akigawa chakula kwa watoto katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza iliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam Alhamisi ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akigawa chakula kwa watoto katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza iliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Desemba 31, 2015 ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.Kwa matukio zaidi bofyahapa

Kipindupindu Chatua Gerezani....Wawili Wafariki Dunia

$
0
0
Mahabusu wawili wa Gereza la Wilaya ya Musoma mkoani Mara, wamefariki dunia baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu

Mkuu wa gereza hilo, Shaku Humba alisema kuwa wafungwa saba na mahabusu watano walioripotiwa kuugua ugonjwa huo.

Hata hivyo hakuwataja majina marehemu hao akisema kuwa hana mamlaka kisheria hadi hapo taratibu zitakapokamilika.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Musoma, Dk Honorata Rutatenisigwa alisema mahabusu wanaogua ugonjwa huo wamelazwa katika kambi ya gereza hilo.

Dk Rutatenisigwa alisema usafi katika gereza hilo unaendelea kusimamiwa kwa karibu, huku unyunyiziaji wa dawa ya kuua wadudu na kutoa huduma ya kwanza kwa wengine ambao hawajakumbwa na ugonjwa huo ikiendelea.

“Kutokea kwa vifo hivyo vya mahabusu wawili kumefanya kuwa na jumla ya watu 11 waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mjini Musoma,” alisema.

Wagonjwa hao walifariki kwa nyakati tofauti, baada ya kuugua ugonjwa huo uliolikumba gereza hilo Desemba 29, mwaka jana.

Alisema ugonjwa huo hadi unalikumba gereza hilo uliingia mjini hapa miezi miwili iliyopita.

Dk Rutatenisigwa alisema juhudi za kuudhibiti zinaendelea.
Tayari ugonjwa huo umeikumba mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, Mwanza ukiongoza kwa kuathirika zaidi kutokana na idadi ya wagonjwa kuwa zaidi ya 900 katika wilaya zake zote pamoja na vifo zaidi ya watu 25.

Wilaya za mkoa huo ambazo zimekuwa zikiripoti kuwa wagonjwa mara kwa mara ni Ukerewe, Ilemela, Magu na Nyamagana.

Ili kukabiliana na ugonjwa huo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, imepiga marufuku uuzaji ovyo wa vyakula.

WASTARA Atoa Kali ya Mwaka Huu...Adai Nahisi Mauti yapo Karibu yake.....

$
0
0
Ikiwa leo ni mwaka wa tatu toka msanii wa filamu, Sajuki Juma afariki dunia, mke wake Wastara Juma ameendelea kupitia mitihani mbalimbali ya maisha hali inayomfanya aombe Watanzania wamuombee dua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wastara ameandika.

Naanza kwa kumshukuru mungu wangu anaenipa pumzi ya bule mpaka mda huu. Sina budi kusema haya nitakayoyasema kwa ajili mwaka mpya unaonza. Ni miaka 4 na miezi 6 leo imetimia toka furaha yangu ilipoingia dosari.

Mungu alinipa mtu wa kunipa furaha kwa sababu kilakitu Alhamdulilah nilikuwanacho kulingana na nafasi yangu lakini sikuwa na furaha lakini furaha hiyo aikudumu nakumbuka ilikuwa mwezi 6/ 2011 marehemu Sajuki alipoanza kuumwa ndipo furaha ilipoanza kupotea kwa sababu sikupata nafuu wala moyo wangu kupumzika mpaka leo.

Nimejaribu kutafuta furaha kila sehemu kila njia ila imeshindikana na Mungu nae anaendelea kunipa mitihani ya maradhi ambayo naamini yatapona na kuisha soon ila kuishi katika mazingira hayo kwa mtu mwengine angekuwa kama kizee hata kuchana nywele ingekuwa shida ila katika maisha ya maumivu na Sajuki siku moja aliniambia mke wangu mi naumwa ila sipendi kukuona ukiwa mchafu na pia usinizuie kwenda kokote kwa sababu nitakufa siku yoyote tutumie muda uliobakia kufanya kile kitu moyo unataka.

Nami kwasasa naishi hivyo nahisi mauti yapo karibu yangu sana hivyo kile moyo wangu unataka ndicho nakifanya hta moyo ukiniambia inuka na maumivu yako nipelke baharin basi naupelka uko ukisema nipelke disco naupeleka uko ukisema nikakeshe msikitin naupeleka uko hivyo sitabariki na sipendi kuishi ili mtu anione nina maumivu nalazimisha furaha japo aipo hivyo mnisamehe wale wote msionielewa kokote mkinikuta mniche tu sifanyi kitu kumkera mtu i need realif ya moyo wangu maskin unanivuja damu kilasiku natamani nifanye lolte ili upumue hakuna kitu kibaya kma kupoteza furaha na tumain unaishi kma uko dunia ya peke yako nimeongea hya ili muelewe hisia zangu kuwa hta ukiongea kitu ambacho sijakifanya sihusiki au kunitafsiri vibaya naumia mara 2 nahisi kma na wew ni mmoja ya wale wasiopoenda kuona nikifurahia uwepo wangu duniani.

Viongozi wangu ndugu jamaa wasanii wenzengu na mshabiki wangu nawaomba kwa pamoja mpige goti kuniombea 2016 moyo wangu upate furaha ya kudumu upate dawa ya maumivu upate tabasamu la kweli na sio feki ninalotoa sasa aniondoshee maradhi yote moyo wangu unahitaji realif maskin mwaka 2016 uwe na neema kwetu sote amen.

Bifu la Mr Blue na Diamond Platnumz Lamuibua Afande Sele...Adai Hata Ukimuuliza Mtoto Mdogo yeye Ndio Simba Dume

$
0
0
LILE bifu la kugombania jina la Simba ambalo linawahusisha wasanii nyota wa Bongo Fleva, Henry Samir ‘Mr Blue’ na Nasibu Abdul ‘Diamond’ lime­muibua mkongwe Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ ambaye alikuwa kwenye mishe za siasa.

Afande Sele maarufu Mfalme wa Rymes, aliyeku­wa akigombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Mjini, amesema yeye ndiye mwanzilishi wa jina hilo miaka mingi iliyopita.

“Hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuambia, mimi ndiye Simba Dume. Mwaka 2008 nilifanya wimbo na P Funk Majani, unaitwa Simba Dume na nikaanza kutumia hilo kutokea hapo, nawashauri waachane na mabifu yasiyo na maana.

Ni bora wote watatu tukutane, tufanye kolabo, kila mmoja aelezee usimba wake kwenye mashairi, naamini itabamba na itakuwa na maana na faida kwa kila mmoja na mashabiki wetu,” alidadavua Afande Sele.

Le Mutuz Ajitapa Kutoka Kimapenzi na Amanda Posh

$
0
0
William Malecela ‘Le Mutuz’ juzikati aliumbuka baada ya kuposti ujumbe kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, akijitapa kwamba amewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji maarufu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’, jambo lililosababisha wachangiaji wamshukie vikali kwa maneno ya kuudhi.

Katika ujumbe wake, Le Mutuz ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa Saba wa Tanzania na mwanasiasa mkongwe, John Samwel Malecela, aliandika kwamba baada ya kurejea kutoka ng’ambo alikoenda kimasomo miaka mitano iliyopita, Amanda ndiye aliyekuwa mwanamke wake wa kwanza kutoka naye kimapenzi.

Baada ya kuposti ujumbe huo, wachangiaji walimshukia, wengi wakimlaumu kwa kukosa busara kwani kama walikuwa wapenzi, hayo ni masuala yao binafsi na yalishapita hivyo hakuna sababu yoyote ya kujisifia wakati walishaachana kitambo. Hali hiyo ilisababisha Le Mutuz afute haraka ujumbe huo ambao hata hivyo, tayari ulishaonwa na watu wengi ambao waliendelea kumponda.

Baada ya kuunasa ‘ubuyu’ huo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Le Mutuz kupitia namba yake ya simu ya kiganjani ili kujua sababu za yeye kuposti ujumbe lakini mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni, simu yake haikuwa ikipatikana hewani.

Kwa upande wa Amanda alipotafutwa, alisema:

Hayo mambo yalishapita, ilitokea ikapita. Sasa hivi mimi na yeye ni marafi ki tu, mimi nina mtu wangu na yeye ana maisha yake kwa hiyo sioni kama ni busara kuyazungumzia,” alisema Amanda.

Chanzo: GPL

Kundi la Muziki la Navy Kenzo Lashika Namba Nne Katika Video 50 Zilizobamba Zaidi MTV Base Mwaka 2015, Wampita Diamond Platnumz

$
0
0
Kundi la Mziki la Navy Kenzo Linaloundwa na Aika na Nahreel wametutoa kimasomaso Watanzania Baada ya Video yao ya Wimbo wa Game Walioshirikiana na Vanessa Mdee Kushika Namba Nne katika Chat ya Video 50 Bora za MTV Base Africa Zilizofanya Vizuri mwaka 2015..

Diamond Platnumz na Wimbo wake wa Nana umeshika namba 5 Katika Chat hizo, Wimbo huo wa Nana Pia Umetengenezwa na Producer Nahreel Kitu kinachomfanya Aendelee kuwa Producer Bora zaidi Kuwahi kutokea Tanzania na East Africa kwa Ujumla,

Mwimbaji Wizkid wa Naigeria Ameshika Namba 6.

Pongezi ziende kwao @nahreel,@aikanavykenzo wanaounda Kundi la Navykenzo
Pia Pongeze Kwa Diamond Platnumz kwa Kuwa Namba 5 Katika Chat Hiyo...

Mwaka Huu Tegemea Mambo Makubwa Kutoka Kwao na The Industry Kwa Ujumla...

Breaking News: Makubwa Yaibuka Baada ya Kufukuzwa Kazi Kwa Mlinzi wa Lowassa

$
0
0
Aliyekuwa mlinzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ofisa usalama mwandamizi, Aloyce Tendewa, amefukuzwa kazi.
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, Tendewa amefukuzwa kazi na mwajiri wake ambaye ni Idara ya Usalama wa Taifa (TIS) kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kikazi.
Mbali na taarifa hizo, imeelezwa pia kuwa sababu nyingine ya kufukuzwa kwake kazi kwa mwanausalama huyo ambayo hata hivyo haijathibitishwa, ni madai ya kutoa taarifa za kubadilishiwa kituo chake cha kazi cha awali.
Inadaiwa kuwa Tendewa baada ya kuvuliwa jukumu la kumlinda Lowassa alibaki na kinyongo moyoni kwa sababu hakuridhika na hatua hiyo hivyo alivujisha taarifa hizo kwa vyombo vya habari jambo lililoelezwa kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yake.
Inadaiwa kuwa Tendewa alipewa barua ya kuachishwa kazi juzi jioni baada ya kuvuja kwa uhamisho wake kwenye vyombo vya habari.
“Alikuwa bado anataka kuendelea kumlinda mzee (Lowassa), lakini kuna vitu alishindwa kuvitekeleza kwa ufasaha kwa hiyo kitendo cha kuondolewa kilimuudhi akaamua kupeleka taarifa gazetini jambo ambalo ni kinyume na taratibu zao za kazi za kiusalama,” alidokeza mmoja wa maofisa

Kwa upande mwingine taarifa zinaeleza kuwa mpango wa kutimuliwa kwa Tendewa uliandaliwa kwa muda wa miezi kadhaa na barua ya kufukuzwa iliandikwa baada tu ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Kwamba, pamoja na sababu nyingine Tendewa anadaiwa kushindwa kuwasiliana inavyotakikana na viongozi wake kuhusu majukumu yake ya kiulinzi wakati akiwa mlinzi wa Lowassa.

Taarifa zinadai, kushindwa huko kwa Tendewa kuliwafanya viongozi wake kufikia uamuzi wa kumfukuza kazi na kwamba barua yake iliandikwa mapema Desemba mwaka jana, lakini hakukabidhiwa hadi hivi karibuni alipovujisha siri za kuhamishwa kwake kituo cha kazi.

Mmoja wa watoa habari aliyeko serikalini ameeleza kuwa Tendewa aliundiwa kamati ya kumchunguza kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu sawasawa ambayo ilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti yake makao makuu.

Hata hivyo, alisema bado kuna utata kuhusu mtu aliyesaini barua ya kufukuzwa kazi kwa Tendewa ambaye kwa wadhifa wake ilipaswa kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu lakini badala yake imesainiwa na ofisa wa cheo cha chini.

Tendewa amefukuzwa kazi akiwa amebakiza mwaka mmoja kustaafu utumishi wake katika Idara ya Usalama wa Taifa.

Rekodi  za utendaji kazi wa Tendewa zinaonyesha kuwa baada tu ya kuajiriwa na TIS, alipelekwa katika kikosi cha walinzi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere na kutokana na uhodari wake aliaminiwa na Mwalimu.


Aidha, rekodi hizo zinaonyesha kuwa Tendewa ni miongoni mwa wana usalama wachache waliopigana vita ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa Uganda, Fashisti Iddi Amini Dada mwaka 1978 na 1979 na akiwa vitani alitekwa na kwenda kuzuiliwa nchini Sudan.
Historia hiyo inaonyesha kuwa Tendewa aliokoka kuuawa kwa risasi akiwa mateka muda mfupi baada ya kurejeshwa nchini kutoka Sudan siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni kushika madaraka ambapo mmoja wa walinzi wanawake wa rais alimuona na kumtambua kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji hodari wa Tanzania na si muasi kama ilivyokuwa ikidhaniwa hivyo alirudishwa Tanzania.
Baada ya kurejeshwa nyumbani alipewa jukumu la kuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere na hata alipong’atuka madarakani aliendelea na kazi hiyo hadi Mwalimu alipofariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas London nchini Uingereza.

Chanzo: Mtanzania

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya Januari 3, Ikiwemo ya Wananchi Kugawana Shamba la Sumaye

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya Januari 3

Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images