Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Diamond, Romy Jones Watibuana...Daimond Atoa Asema Haya....

$
0
0
Kimenuka! Mbongo-Fleva mwenye taito kubwa Afrika kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, anadaiwa kutibuana na kaka yake, Romy Jones ‘Romy Jons’, kiasi kwamba hata mawasiliano ya simu hayapo kama ilivyokuwa zamani.

Hivi karibuni chanzo makini kimeliambia gazeti hili kwamba, Diamond na kaka yake huyo ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo wamefikia hatua ya kutoongea na hata kuambatana katika kazi zao kama ilivyokuwa mwanzo ambapo Romy Jons ndiye mtu pekee aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa na Diamond hata katika safari za nje ya nchi.

Imedaiwa kwamba, kisa kikubwa cha wawili hao kugombana ni kufuatia Diamond kushindwa kuendelea kuvumilia tabia za utovu wa nidhamu aliyokuwa akiionesha Romy Jons kila mara, kwani hadi Diamond anafikia hatua hiyo huko nyuma anadai kuiingia hasara kubwa kutokana na kaka huyo kuwa na tabia za ajabu kwani kuna muda alikuwa akimlipia hadi tiketi za ndege ili wasafiri pamoja lakini jamaa akawa hatokei.
Kuna madai kwamba, Romy Jons amekuwa akiambatana na makundi yasiyofaa huku ulevi ukitajwa kuwa tatizo kubwa.

Baada ya kumwagiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilizungumza na Diamond juu ya madai hayo lakini aligusia kwa kifupi kuwa kwenye maisha kila mtu ana namna alivyopangiwa kuishi na Mwenyezi Mungu, hivyo kinachoonekana kwa sasa au kutokuwepo kwa Romy Jons ndani ya Wasafi Classic Baby (WCB) ni mipango aliyochagua Romy Jons mwenyewe kwani yeye hana cha kuongea zaidi.
Alisema kuwa ifahamike kwamba, Romy Jons ni ndugu yake wa damu hivyo dosari au tatizo kati yao linabaki kuwa suala la kifamilia tu.

“Kuna mambo mengine ifikie hatua yaonekane na yapite tu, si kila jambo naweza kuliongelea na kuliweka wazi maana mengine yapo kifamilia zaidi ya watu wanavyochukulia, halafu naomba ieleweke kwamba kwenye dunia hii kila mtu ana namna alivyochagua kuishi, hivyo maisha yangu najua mwenyewe ninavyotamani kuwa kadhalika hata Romy Jons ana mipango yake anayopigania kuikamilisha,” alisema Diamond.

Juhudi za kumpata Romy Jons ziligonga mwamba baada ya simu zake zote kutokuwa hewani hivyo zinaendelea ili kusikia upande wake

Aika na Nahreel wa Navy Kenzo Wafunguka..Tuliamua Kuanza A Bila Kuwategemea Wazazi..Tulilala Chini Kwenye Kagodoro

$
0
0
Members wa Kundi la Navy Kenzo linalofanya Vizuri katika mziki ndani na nje ya Tanzania wamefunguka kwa ufupi jinsi walivyoanza maisha yao ya muziki mpaka kufikia hapo walipo

Waimbaji hao ambao ni wapenzi wamesema walikutana India masomoni walipokuwa wakisomeshwa na Wazazi wao na baada ya kumaliza Waliamua Kufanya kazi huko lakini Baada ya Kuona vipaji vyao vinapotea bure wakaamua kuja Tanzania ili kuendelea na muziki na ndio hapo kundi la Paone lilipoanzishwa wakiwa vijana Wanne

Lakini baada ya muda kundi la Paone lilisambaratika na hapo ndipo ukawa mwanzo mzuri wa kundi lenye mafanikio la Navy kenzo liliundwa na Aika na Nahreel,

Maisha yao walipofika Dar es Salaam kwa Mara ya Kwanza wakitokea India Masomoni yalikuwa chini sana kiasi cha kulala chini kwenye Kagodoro kadogo huku Nahreel akifanya kazi ya kutengeneza Beat na Aika Akijishughulisha na Mambo ya Urembo, Aika Anasema waliamua ku take risk na kuanza upya from the scratch ili waweze kuwa na kitu cha kujivunia baadae walichokifanya wenyewe bila kuwategemea wazazi wao ambao kwa kupindi hicho walikuwa na uwezo wa kuwasaidia kwa chochote lakini waliamua kufanya yao na sasa kufika hapa walipo kama moja ya kundi bora la muziki kuwahi kutokea Tanzania.

Kwa sasa wawili hawa wanamiliki kampuni na Studio ya mziki inayojulikana kama "The Industry"



CCM Wamvaa LOWASSA......Wamtaka Ajitokeze Hadharani Ataje Majina Ya Wafanyabiashara Waliomfadhili Ambao Wananyanyaswa

$
0
0


CCM imesema kauli ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa wafadhili wa Chadema wananyanyaswa, ina lengo la kuichonganisha Serikali na walipa kodi na kumtaka ataje waliofanyiwa vitendo hivyo.

Juzi, Lowassa alikaririwa na vyombo vya habari kutoka Monduli akisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa maelekezo ya Serikali imekuwa ikiwatoza kodi kubwa wafanyabiashara kwa sababu waliifadhili Chadema kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

Lowassa aliwahi kutoa kauli kama hiyo jijini Mwanza akiwa kwenye msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema wa mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga.

Pia wakati wa harambee ya Chadema iliyofanywa Septemba 22 mwaka jana, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema kulikuwa na matajiri watano wenye uwezo kiuchumi ambao walikuwa tayari kukisaidia kwenye shughuli zake za kampeni, lakini hawataki kutajwa majina yao kwa hofu ya kufuatiliwa na vyombo vya dola.

Jana, akizungumza na waandishi wa habari jijini, Abdallah Bulembo, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, alisema kauli ya Lowassa haina ukweli wowote na kwamba ina lengo la kuigombanisha Serikali na walipakodi ambao wanahitajika sana kipindi hiki.

“Kama kweli Lowassa anawafahamu wafanyabiashara au kampuni ambazo zinatozwa kodi kubwa kwa sababu walikuwa wamekifadhili chama hicho, basi ni vizuri awataje ili wajulikane na waseme wao wenyewe,” alisema Bulembo ambaye wakati wa kampeni alikuwa bega kwa bega na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Akijibu suala hilo, Lowassa alisema kuna wafanyabiashara wengi waliokuwa wakikifadhili chama ambao wanalalamika kutozwa kodi kubwa.


“Kuna watu wengi wanalia kutozwa kodi kubwa,” alisema Lowassa ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema baada ya kuihama CCM Julai mwaka jana.

“Suala hapa si kuwataja majina, mkihitaji majina yao fanyeni research (utafiti) mtawapata. Lakini mfahamu kwamba kuna tatizo hilo.”

Alisema ana uhakika vyombo vya habari vitawapata watu hao na kwa kuwa ni wengi watatoa malalamiko yao.

Akifafanua zaidi, Bulembo alisema kauli ya Lowassa inadhoofisha nguvu ya Rais Magufuli ambaye ameongeza makusanyo ya kodi kutoka Sh850 alipoingia madarakani hadi Sh1.3 trilioni kwa mwezi.

“Tunawahitaji walipakodi wengi wakati huu kwani tunahitaji kupata fedha zaidi ili kutekeleza ahadi tulizowaahidi wananchi. Kauli ya Lowassa inatugombanisha na walipakodi,” alisema.

Alisema anachofahamu ni kwamba kodi inatozwa bila kumpendelea mfadhili wa CCM au kumwonea mfadhili wa Chadema.

“Masuala ya vyama ya siasa yameshapita, sasa hivi ni kujenga nchi na kodi inatozwa bila kuangalia vyama vya siasa,” alisema Bulembo.

Alimwomba Lowassa kumsaidia Magufuli katika kazi ya kutafuta mapato ili kuwaletea wananchi maisha mazuri

“Namwomba Lowassa tujenge nchi yetu, huu si wakati wa kufanya siasa, asubiri mwaka 2020 kama atagombea tena urais tutakutana kwenye majukwaa,” alisema.

Alisema kuendelea kupigana vijembe kipindi hiki ni kurudisha nyuma maendeleo ambayo yanahitaji zaidi walipakodi.

“Kodi zina vipimo vyake kama kuna watu wameonewa ukweli utajulikana,” alisema Bulembo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Alisema Serikali ya CCM itaendelea kutenda haki kwa wananchi wake ili kukiwezesha chama hicho kushinda uchaguzi kwa kishindo mwaka 2020.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo, mkurugenzi wa idara ya elimu na huduma kwa walipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo haijapata malalamiko yoyote.

Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na haifanyi kazi kwa kufuata maagizo ya vyama vya siasa.

“Sisi hatuko kwenye siasa tunafanya kazi zetu kwa kuongozwa na sheria na kanuni. Hatumwonei mtu wala kupendelea,”alisema.

Kauli kama ya Lowassa ilitolewa pia na mkuu wa idara ya habari ya Chadema, Tumaini Makene aliyesema hoja ni kueleza kuwapo kwa tatizo ambalo halitaishia kwenye ubaguzi wa kiitikadi.

“Ukianza kubagua watu kivyama, huwezi kuishia hapo. Utaanza kuwabagua kikabila, kikanda na hata kidini. Hii ni kinyume na ahadi ya Rais Magufuli kuwa atakuwa Rais wa watu wote,” alisema Makene.

Makene alitoa mfano wa kukataliwa kwa misaada ya vifaatiba katika zahanati za Serikali mkoani Kagera uliotolewa na mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare.

Mara baada ya kuingia Ikulu, Rais Magufuli alikutana na watumishi wa Hazina na kuwaelekeza kukusanya kodi bila ya kuangalia sura, huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifanya ziara za mara kwa mara bandarini ambako ameibua kashfa za ukwepaji kodi na upitishaji makontena kifisadi.

Basi la Abiria Lagongana na Lori Asubuhi Hii.......Wawili wafariki Dunia Huku wengine Wakijeruhiwa

$
0
0

Basi la abiria la kampuni ya Luwinzo linalofanya safari za Dar es salaam - Njombe limegongana na lori asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar. 

Abiria wawili wameripotiwa kufariki dunia huku majeruhi wakiwa ni wengi. Ajali imetokea maeneo ya Kinegembasi Kata ya Mbalamaziwa wilayani Mufindi.

Photo Of The Day: Bleaching Gone Wrong. She Forgot To Bleach Her Feet! (photo)

$
0
0

Call it bleaching or skin-lightening but one fact is constant- it is an attempt to change how you look because you have low self esteem. Let see what you can do to your cold, dark heart while at it.

 It has become the thing with ladies to alter the tone of  their skins to a lighter complexion which is a little more likable and savory. It was made famous especially by Vera Sidika who preferred hers as a higher form of skin lightening.

Problems however occur when one opts for a cheaper method of the same making the process uneven and at times dangerous. It sometimes results in dark elbows or some nooks and crevices in the body where the bleach was not properly distributed.

That explains the phenomenon (I used phenomenon lightly) of the ladies you see walking the streets with dark legs and very brown faces or dark necks and light faces-

Like the lady below who forgot to bleach her feet.


Shilole Ajuta Kuchora Tattoo ya Nuhu Mziwanda Kifuani Kwake....Adai "Sitochora Tena Tattoo ya Jina la Mpenzi Wangu"

$
0
0
Shilole ameapa kutorudia tena kuchora tattoo yenye jina la mpenzi wake.

Hivi karibuni muimbaji huyo alilazimika kuifuta tattoo ya jina la aliyekuwa mpenzi wake, Nuh Mziwanda.

Shilole amesema kujichora tattoo ya jila Nuh kumemharibia issue kibao.

“Tattoo hapa ni empty,” aliambia 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii.

SiwezI tena kuchora tattoo kwaajili ya mapenzi. Nimeamua kama tutapendana tutapenda rohoni kwa sababu nishaona hakuna sababu ya kuchora tattoo. Unaweza ukajitolea ukachora tattoo ukazuia mambo yako mengi yanayopita. Nimeona mwenyewe madhara yake kwahiyo mimi
simshauri mtu kuchora tattoo kwa ajili ya mapenzi,” aliongeza.

Hata hivyo Shilole hakuweka wazi sababu ya kuachana na Nuh Mziwanda.

Watu 8 Wakiwemo Polisi Wafariki Dunia Kwa Kusombwa na Maji Kibaigwa Mkoani Dodoma

$
0
0
WATU 8 wamefariki dunia katika ajali iliyosababishwa na gari kusombwa na maji huku watu 6 wakiwa wa  familia moja.

 Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Davidi Misime amesema majira ya saa tatu usiku Jumapili, wananchi wa Kibaigwa walitoa taarifa jeshi la polisi kwa madai kwamba kuna gari limesombwa na maji na limetumbukia katika mkondo wa maji.

Amesema baada ya jeshi kupata taarifa hizo polisi walijitahidi kutoa gari hilo aina ya Rav4 yenye namba za usajili T516 DEP na kubaini kwamba jumla ya watu sita wa familia moja wamepoteza maisha katika familia moja.

Misime amewataja waliofariki kuwa ni Msaidizi wa Inspekta wa Jeshi la Polisi (IGP) Gerld Ryoba, mke wake Fidea Kihondo, watoto wawili binti wa kazi, na Koplo Ramadhani ambaye ndiye alikuwa anaendesha gari hilo.

Amesema wana familia hao  walikuwa wakitokea likizo mkoani Geita na walikuwa wakirejea kazini Dar Es Salaam.

Amesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Kibaigwa bwawani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo ya Njoge, Embaemba, Kiteto na bonde la Ndurugumi.

Misime amesema gari hiyo ilikuwa limeharibika sana na walilazimika kulikata gari hilo na kuwakuta watu wanne ndani ya gari huku wawili wakiwa nje ya gari ndani ya maji.

Hata hivyo Misime amewataja watu wengine wawili wanaume  ambao walikutwa katika maji.

Kati ya watu hao wawili ambao ni wanaume amemtaja afisa mifugo kata ya Pandambili na anafahamika kwa jina moja la Ludege.

Amesema  mmoja mpaka sasa hajatambuliwa kwa jina huku madaktari wanafanya utaratibu wa kuandaa miili kwa ajili ya kuwasafirisha.

Amesema mtoto wa kazi aliyefamika kwa jina la Saraha atapelekwa Mbinga, Koplo Ramadhani anapelekwa Lindi huku miili ya watu wanne inapelekwa Geita.

CCM Yalaani Vijana 1500 Kujitangaza Mashoga Mkoani Iringa

$
0
0
Chama  Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kimewataka vijana waliopo wilayani  humo kuacha  kujihusisha na masuala ya ushoga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi,Jimson Mhagama alisema hatua ya vijana kuingia katika ushoga ni sawa na kulidhalilisha taifa.

Kauli ya Mhagama imekuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa za vijana  na wanafunzi 1500  wa  elimu ya juu waliopo mkoani humo kujihusisha na vitendo vya ushoga, hali ambayo imeleta taswira mbaya.

Alisema ni vyema vijana hao wakaacha tabia hiyo na badala yake watafute pesa kwa njia halali na si kujiingiza kwenye maswala ambayo yanavunja heshima ya jamii na taifa kwa ujumla.

"Wanafunzi wa Elimu  ya  juu wanaojihusisha  na  ushoga  wanadhalilisha vyuo  vyao  na  familia zao, lakini CCM inapendekeza kuwa mwanafunzi atakayebainika kufanya mchezo huo afukuzwe chuo mara moja" Alisema Mhagama

Alisema umefika wakati kwa Bunge kutunga sheria kali na kuifanyia mabadiliko katiba ya mwaka 1977  kuweka kipengele kinachobana  mambo  ya  ushoga.

Aliongeza,mtu akibainika ni shoga apewe adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela

Yaliyojiri Leo Ikulu Baada Ya Rais Magufuli Kukutana na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),DPP na Mufti Mkuu wa Tanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wanne Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na kutakiana heri ya Mwaka Mpya, wamezungumzia mambo mbalimbali kuhusu mustakabali wa Serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumzia yaliyojiri katika Mazungumzo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad amesema wamezungumzia kupunguza gharama za matumizi ya kuendesha serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Profesa Assad amebainisha kuwa Rais Magufuli ametaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ihakikishe Tanzania inaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka asilimia 14 ya pato la Taifa (GDP) kwa mujibu wa hesabu zilizofanyika mwaka juzi.

"Hadi Mwaka juzi Tanzania ilikua inakusanya mapato kwa kiwango cha asilimia 14 ya pato la Taifa ikilinganishwa na Kenya ambayo ilikua ikikusanya asilimia 19 ya pato Taifa, na hakuna sababu za Msingi za kwa nini Tanzania iwe nyuma katika ukusanyaji wa mapato hayo" aliongeza Profesa Assad.

Rais Magufuli pia amekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka hapa Nchini (DPP) Mheshimiwa Biswalo Eutropius Mganga ambaye amesema mazungumzo yao yalijikita katika suala la kupeana mikakati ya namna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inavyopaswa kufanya kazi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo "Hapa Kazi Tu"

Aidha Mganga ameongeza kuwa wamezungumzia umuhimu wa kuwahimiza watanzania kufuata sheria, na kwamba ofisi yake itatekeleza wajibu wake bila kumuonea mtu.

Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Ally ambaye pamoja na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa juhudi kubwa alizoanza nazo katika uongozi wake, amesema waislamu wote nchini wanamuunga mkono na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee na juhudi hizo.

"Na pia kwa niaba ya Waislamu tunataka kumueleza kwamba kazi anayoifanya ni kazi ambayo tunairidhia na tunamuomba aendelee kuifanya wala asiogope, na kauli yake ya Hapa Kazi Tu iendelee, kwa sababu inaonesha kwamba sasa nchi yetu itakaa mahali pazuri" Alibainisha Mufti Mkuu

Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Alhaji Abdallah Majura Bulembo ambaye amempongeza Mheshimiwa Rais kwa kasi nzuri aliyoanza nayo katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015- 2020 na kutaka kasi hiyo iendelee.

Amesema Jumuiya ya Wazazi inaunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli na kwamba Mheshimiwa Rais amemuhakikishia kuwa ataendelea kufanya kazi hizo zaidi katika kutekeleza Ilani ya CCM.

"Tunafurahi kwamba yapo mambo mengi ambayo Rais Magufuli ameanza kuyatekeleza kwa haraka, mojawapo likiwa ni kufutwa kwa ada za shule, na hivi sasa wanafunzi watakwenda shule pasipo kutozwa ada" alisisitiza Alhaji Bulembo

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
04 Januari, 2016

Breaking News: Naibu Waziri -Tamisemi Seleman Jaffo Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza

$
0
0
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Suleiman Jafo, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauli ya Manispaa ya Ilemela, John Wanga kutokana matumizi mabaya ya madaraka.

Waziri Jafo amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa ufujaji wa fedha za ujenzi wa uzio wa halmashauli hiyo ulioghalimu Sh. 347 milioni pamoja na kukaidi kuhamia kwenye nyumba ya Serikali ya Sh. 200 milioni.

Naibu huyo wa Tamisemi alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ambako amesema mkurugenzi huyo ameshindwa kuhamia katika nyumba hiyo ambayo inakadiliwa kughalimu Sh. 200 milioni na kusababisha Serikali kuendelea kulipia nyumba anayoishi.

Amesema kuwa licha ya Serikali kutoa agizo mkurugenzi huyo kuhamia katika nyumba hiyo lakini yeye aliendelea kupangishia nyumba nzima inayolipiwa Sh. 2 milioni kwa mwezi licha ya kukamilika kwa nyumba iliyojengwa.

Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe CCM amesema kuwa katika manispaa hiyo kuna matatizo mengi na kwamba itatumwa kikosi cha uchunguzi kutoka Tamisemi ili kufanya uchunguzi namna ambavyo fedha za ujenzi wa uzio zilivyotumika ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watakaobainika kuhusika na suala hilo.

“Huu ukuta (uzio) hauwezi kughalimu fedha zote hizo, nyie hata kwa madai yenu mnayosema mlifanya haraka kwa sababu ya uchaguzi sio kweli hamtaweza kushawishi kwa hilo.

“Watanzania wana shida, dawa hospitalini hakuna, wakina mama wanajifungulia chini halafu, milioni 200 imekaa tu haina shughuli yeyote ile, mkurugenzi unapaswa kupisha uchunguzi kufanyika kwanza,” amesema Jafo.

Hata hivyo amesema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo ulianza tangu mwaka 2013 lakini mpaka sasa mkurugenzi huyo amekataa kwenda kuishi kwa sababu ya kuwa chini ya kiwango na kwamba ipo katika maeneo hatarishi.

Amesema licha ya uongozi wa manispaa hiyo kujipangia kiwango cha Sh. 2 milioni kwa mwezi,kiwango hicho kipo juu ya kiwango cha serikali cha laki nane.

Kwa upande wake mkurugenzi, Wanga katika kujitetea amesema sababu zilizosababisha kushindwa kuhamia katika nyumba hiyo ni kutokana na kuwa katika eneo hatarishi ikilinganishwa na nafasi yake ya ukurugenzi.

“Waziri (Naibu Waziri Tamisemi) tunafanya kazi kubwa za wananchi na kazi zetu mnazifahamu tunafanya watu wengine hawapendi tunachokifanya, sasa nikihamia katika nyumba ile na ukilinganisha na eneo ilipo ni hatari,” amesema Wanga.

Kubenea Linda Heshima yako katika Jamii...Sifurahishwa na Uhasama Uliopo na Zitto Kabwe

$
0
0
Watanzania tumekuwa na mila na desturi ya kupongezana pale tunapofanya vizuri na pia kukosoana tunapofanya vibaya. Ni kutokana na utamaduni huu nathubutu kukuandikia.

Awali ya yote mimi ni msomaji wa magazeti ya Mwanahalisi/Mawio ambayo wewe kama mmiliki au mwandishi wa habari unapitishia taarifa zako kwenda ktk jamii.

Nimeguswa kukuandikia baada ya kusoma matoleo ya magazeti yako mawili ukionyesha kuwa na vita baridi na Zitto Zuberi Kabwe.

Mimi kama msomaji ninayejinyima pesa yangu ili kununua gazeti lako hakika sifurahishwi saana kusoma uhasama uliopo kati yako na Zitto Kabwe.

Tumetoka ktk uchaguzi na kama Taifa tunahitaji kutoka hapa tulipo kwenda mbele zaidi. Hatuwezi kufikia malengo kama uhasama uliopo kati yako na Zitto unataka kutuambukiza sisi wasomaji kupitia gazeti lako, na wala hatuwezi kwenda mbele tukiwa na hulka tuliyotoka nayo huko nyuma.

Tambua nafasi uliyonayo ktk jamii kwa sasa ya Ubunge kwa maana ya mwakilishi wa wananchi hivyo unatakiwa tabia na matendo yako yafanane na nafasi muhimu uliyokabidhiwa na umma wa wana Ubungo.

Itaniwia vigumu sana kwangu mimi kuendelea kununua magazeti haya kama mtazamo wako kama kiongozi wa jamii hautabadilika. Kwa makala ya leo ktk gazeti lako la Mwanahalisi ukurasa wa 7 haina tofauti na magazeti ya mipasho ya Uwazi, Kiu na mengineyo.

Ni matumaini yangu kuwa kuchaguliwa kwako kuwa mbunge wananchi hawakukosea na hivyo unatakiwa kulionyesha Taifa kwamba hata ukiaminiwa kupewa nafasi ya juu unaweza tofauti unavyojionyesha kuwa wewe ni mtu wa visasi. ANZA MWAKA KWA KUSAMEHE BADILIKA.

Jamii Forums

Kura Yangu Nilimpa Rais Magufuli,Lakini Kwa Sasa Naijutia

$
0
0
Binafsi wakati wa kampeni nilivutiwa sana na sera ya Rais Magufuli ya kuipunguza serekali yake kwa nia ya kubana matumizi.
Na nia yake hiyo njema kwa taifa masikini Kama Tanzania ndio ilinishawishi nikiri nikampa kura yangu ya ndio.

Ila kwa sasa nimeanza kukata tamaa kwa uteuzi aliofanya Rais wa kuteu makatibu wengi watakao turudisha pale pale tulipokuwa tunalia lia kuwa serekali ni kubwa mno na isiyokuwa na mashiko.Inayoumiza wananchi wake.Ni kiri wazi nimeanza kuijutia KURA yangu na next time Ccm sitowaamini tena na siwaamini tena hata sasa hivi.

By Kibo10

Rais Magufuli Apewa Jipu Gumu Sana Alitumbue..Ni Jipu Linalosumbua Wananchi Wengi Sana

$
0
0
Mh. Rais naomba uliangalie kwa makini jipu kuu la utosi linalotutesa wananchi wako! Ada za shule, zahanati kila kijiji au ujenzi holela mabondeni hayo ni matokeo tu ya jipu kuu!Jipu hilo ni kiwango cha juu cha riba ya mikopo kwa watumishi wa umma na watanzania wengine wa kipato cha kati-chini na chini kabisa!

Banks zinakata hadi 20% na makampuni binafsi yanafikia hadi 40%, kwa jinsi hii hakuna jinsi kundi hili kubwa ktk jamii yetu litaweza kushiriki ktk kujenga uchumi!

Nakuapia kwa pesa za makontena na walipa kodi wengine wachache ndani ya nchi haziwezi kukufanya uboreshe huduma za jamii, ada itaichemsha serikali yako hata bila ya kuizungumzia afya!
Mfano bora, tazama elimu ya chuo kikuu, wengi wame afford thru mkopo! Hao hawaisumbui tena serikali kwa kuwa kama marejesho yatasimamiwa then watu watajisomesha! 

Ujenzi holela utakufa tu pale nitakapopata mkopo na kuweza kumudu gharama ya kiwanja kilichopimwa! Hata wakulima wetu wataboresha pembejeo!

Sio kama watanzania niliowasema hapo juu hawakopi, la hasha Hawa ndio wanaokuza sekta ya microfinance na bank nyingi nchini huku wakikuibia muda serikali kufanya vijikazi vya kimachinga kuikimbiza riba ya hayo mabank au makampuni binafsi!

Hazina ilitoa mikopo yenye riba ya 5% kwa baadhi ya watumishi wengi walikopa na sidhani kama serikali ilifilisika kwa hilo!

Hebu kakae na boss mpango muone ni jinsi gani mabank yetu yaweze kuleta tija kwa wananchi na yasiwe mwiba!

Kwa mnaoishi Europe na sehemu nyingine za dunia hebu semeni experiences zenu na mikopo na jinsi inavyowakomboa wananchi na serikali zao!

Mh. JIPU HILI LIKITUMBUKA nitakuwa nacheka ninapoenda TRA au mamlaka yeyote kulipa kodi!

Vera Sidika Exposes Her Massive Uncovered Ass As She Teaches Girls How To Bang Men Like Pornstars (Photo)

$
0
0

Dirtiest New Year message ever! Vera Sidika has added a new profession to her CV; sexologist. She taught girls how to bang their dudes harder than Salvation Army’s drums.

For the socialite queen, 2016 has to be the year when ladies MUST make men R.I.P (Rest In Pu**y). Vera shared a few tricks how to achieve this.

According to Vera, ladies must let go missionary and embrace positions that harness pleasure to the fullest.

The socialite says girls should ride their men like their lives depended on it. She also advised them to do it in other rooms other than the bedroom.

Her advice is too ‘dirty’ for me to break down, read the fool text below:

I Love my thongs army green like I'm going to war! Ladies, the year is coming to an end and you better be the only thing on his mind come 2016! get that game on and ride him like if your life depends on it. Suck it like a baby on a milk bottle (inseparable) then try something different, don't do the normal bed routine, mix it up! Make use of the bathroom, couch, floor, kitchen counter, take advantage of that space! Try switching sex positions too, try the reverse cowgirl, move to electric slide, then the Python, and finish with doggy style In the AM, prepare breakfast in bed for him. Put up a show he'll remember for the rest of his life!!! Make a niggah R.I.P (Rest In Pussy) #RichSex ...best New Year's gift u can give your man!



Saed Kubenea Akana Tuhuma Dhidi Yake.....Asimulia Jinsi Alivyosoma, Akana Kuiba Laptop ya Prof. Lipumba

$
0
0
==> Hili  ni  Tamko  La  Saed Kubenea(mbunge wa ubungo)  kupangua Tuhuma Mbalimbali zilizoelekezwa  kwake  

NIMESOMA andishi la anayejiita Seif Rashid, lililochapishwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii, pamoja na baadhi ya magazeti.

Andishi limejielekeza katika kunijadili binafsi: Jinsi nilivyofanikiwa kuwa mbunge wa jimbo la Ubungo, kuwa mmiliki wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited – wachapishaji wa MwanaHALISI – gazeti ambalo mimi ndiye mtendaji wake mkuu – na mengine mengi.

Andishi hili lilipewa vichwa vya maneno tofauti, kulingana na mahitaji ya mchapishaji.

Kuna baadhi ya maeneo lilipewa kichwa cha maneno, “Saed Kubenea: Ndumilakuwili mbobezi.” Pengine ililiandikwa, “Mfahamu Saed Kubenea, mbunge wa Ubungo.”

Kote lilikochapishwa andishi lile, lilibeba aya kadhaa kutoka kwenye makala niliyoandika na kuchapishwa katika gazeti la MAWIO, toleo la Alhamisi ya 24 Desemba 2015.

Makala katika MAWIO ilikuwa inajadili ndimi mbili za Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe.

Mwandishi anasema, nimeamua kumshambulia Zitto, kwa sababu nataka kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo Zitto pia anaitaka tena.

==>Baada ya kuisoma na kuirejea tena na tena, napenda kueleza yafuatayo:

Ni kweli kwamba Saed Kubenea ndilo jina langu. Ni kweli kuwa mimi ni mbunge wa Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Ni kweli kwamba niliwahi kuandikia magazeti ya Mtanzania na RAI – hakuna lisilo la kweli. Basi. Yaliyobaki katika andishi la anayejiita Seif Rashid, ni uongo wa moja kwa moja, porojo au tuhuma zenye nia ya kunidhalilisha na kunivunja moyo.

Niseme hapa mapema kuwa, mimi siyo mtu wa kuvunjika moyo pale ninapokuwa nimeamua kufanya jambo. Mimi sitishwi na uongo, uzushi, porojo au suto za kwenye magenge ya kahawa au bao.

Alichokifanya anayejiita Seif Rashid, ni kuokoteza huku na kule na kutaka kuaminisha umma kuwa ni ukweli. Kwa mfano, sijawahi kutamka mahali kokote kuwa nataka kuwa mwenyekiti wa PAC.Spika wa Bunge hajapanga nani awe kamati hii au ile. Wala haijafahamika kuwa nitakuwa mjumbe wa kamati ipi.

Hata kama nitataka kuwa mwenyekiti, bado siwezi kutumia kalamu yangu kujipigia kampeni. Siamini katika siasa za aina hiyo.

Mwenye andishi anasema, ninatumia cheti cha ndugu yangu aishiye Bagamoyo na mwenye jina la Said (sio Saed); na kwamba mimi siitwi Saed Kubenea. Hataji jina langu.

Hata hivyo, ni vema nieleze yafuatayo: Jina la Saed Kubenea, ndiyo jina halisi nililopewa na wazazi wangu. Nimelirithi kutoka kwa babu yangu. Anaitwa, Saed Mohammed Kubenea. Aidha, hakuna kaka au ndugu yangu yeyote anayeishi Bagamoyo. Hayupo.

==>Nimesoma kwa kadri Mwenyezi Mungu alivyonisaidia. Nilimaliza Kidato cha Nne. Nikaanza kujifunza mwenyewe na baadaye kupata msaada wa watu mahili kunifundisha taratibu uandishi wa habari. 

==>Nikahudhuria mafunzo mafupi hapa na pale nchini. Hatimaye nikapata mafunzo ya juu ya uandishi wa habari nchini Uholanzi na India. Ninaendelea kujifunza na elimu haina mwisho.

Jingine la kugusia ni madai kuwa nilihusika na upoteaji wa anachoita, “kompyuta mpakato (laptop) ya Prof. Ibrahim Lipumba mwaka 2005.”

Suala hili liliwahi kuelezwa pia na Didas Masaburi, aliyekuwa mshindani wangu katika mbio za ubunge jimboni Ubungo.

Ukweli ni huu: Prof. Lipumba hajawahi kuibiwa kompyuta (laptop) akiwa na mimi. Kilichoibiwa akiwa na mimi ni modemu inayotumika kwa ajili ya kupata huduma ya intaneti. Bali kompyuta inayodaiwa kuwa ya Prof. Lipumba ilikuwa ni mali yangu. Siyo ya Prof. Lipumba kama ambavyo wahusika wanataka kuaminisha umma.

Kuna hili la gazeti la Hali Halisi ambalo mwandishi anasema, nilipewa mtaji na Prof. Lipumba na baadaye likatumika kama gazeti rasmi la kambi ya upinzani bungeni. Mimi sikuanzisha gazeti hili. Lilianzishwa na wabunge wa upinzani mwaka 2003. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani alikuwa Willifred Lwakatare, mbunge wa Bukoba Mjini wakati huo.

Ninashangaa mtuhumu anapopata taarifa kwamba kufa kwa gazeti la Hali Halisi, kulinifanya kuwa na maisha magumu; na kwamba kwa huruma, Zitto Kabwe na mwenzake, Halima Mdee, wakanipa mtaji wa kuanzisha gazeti la MwanaHALISI. Hii siyo kweli na aliyeandika hivyo anajua si kweli.

Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited ilianzishwa 31 Januari 2005. Wakati huo Zitto na Mdee hawakuwa wabunge. Zitto na Halima hawakushiriki kwa namna yoyote ile katika kuanzisha gazeti hili. Mdee akiulizwa juu ya hili ataeleza. Hata Zitto anajua vema; na akiwa mkweli, atasema hivyohivyo. Historia isipotoshwe.

Gazeti la MwanaHALISI limeanzishwa na mimi kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa Absalom Kibanda na baadhi ya waandishi wengine mahiri. Labda niseme hivi, kwamba anayetaka kujua historia yangu, ya vyombo vyangu vya habari na maisha yangu ya mapambano; afanye ahadi na mimi, tukae, aniulize, nimweleze ili apate ukweli na usahihi juu yangu na kazi yangu, na hata ubunge wangu.

Hebu niweke wazi jambo hili: Kwanza, sijawahi kuwa na urafiki, kwa maana halisi ya urafiki, na Zitto. Kilichokuwepo ni ukaribu tu kama ilivyo kwa watu wengine mnapokuwa pamoja.

Pili, sishindani na Zitto. Katika lipi? Kila mmoja ana taaluma yake; na taaluma hizi zaweza kufanya kazi nzuri na vizuri kama hakutakuwa na unafiki, uzandiki na undumila kuwili kama nilioueleza katika makala yangu.

Tatu, siamini katika kuomba fadhila na kujikomba. Naamini katika kudai haki na kilichochangu; au ninachostahili kwa mujibu wa taratibu, kanuni, sheria na katiba. Haya hayahitahi kujikomba. Yanahitaji ujasiri na moyo wa utumishi kwa umma. Huko ndiko kwangu.

Breaking News:Mwanamuziki Maarufu Auawa Baada ya Kupambana na Polisi na Kupigwa Risasi

$
0
0
Visa vya watu kuuawa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara Bujumbura
Mwanamziki mmoja kutoka Burundi amepatikana amefariki katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura baada ya kukamatwa na polisi, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kundi la wanahabari la SOS.

Taarifa hizo zinasema kwamba mwili wa Pascal Tresor Nshimirimana ulipatikana Jumamosi eneo la Musaga, karibu na gereza kuu la Bujumbura.

Polisi wanasema Pascal alijaribu kumnyang'anya bunduki afisa wa polisi, na akauawa na risasi ililofyatuka kutoka kwa bunduki hiyo kwa bahati mbaya
Bw Nshimirimana alikuwa mmoja wa waandamanaji ambao walipinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza

Katika kisa kingine, mwili wa kiongozi wa vijana William Nimubona ulipatakana katika maeneo ya Kavuma jijini Bujumbura.

Hata hivyo, hakuna taarifa huru za kudhibitisha mauaji ya kiongozi huyo.
Bw Nimubona alikuwa kiongozi wa mrengo wa vijana katika chama cha National Liberation Forces (NLF) kinachoongozwa na Agathon Rwasa, kiongozi wa upinzani aliyekubali kuchukua kiti cha naibu wa spika baada ya Rais Nkurunziza kushinda uchaguzi tata wa muhula wa tatu.

Profesa Mwesiga Baregu Amvaa Magufuli..Amkosoa Vikali Uteuzi wa Viongozi Alioufanya

$
0
0
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amekosoa uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu alioufanywa hivi karibuni na rais John Magufuli.

Profesa Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema kuwa anaushangaa uteuzi huo kwani unakinzana na dhana yake ya kutaka kupunguza ukubwa wa serikali yake.

Tulitarajia kuwa rais Magufuli angechagua idadi ya makatibu wakuu ambayo inaakisi baraza lake la mawaziri, lakini nimeshangaa kuona kwamba kwenye baadhi ya wizara kuna makatibu wakuu wawili au watatu,” Profesa Baregu aliliambia The Citizen.

Aliongeza kuwa hivi sasa ni vigumu kufahamu kuwa nani atakuwa mtendaji mkuu kwenye wizara ambayo wameteuliwa makatibu wakuu wawili au watatu.

Naye Mkurugenzi wa Sheria katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia aliungana na kauli ya Profesa Baregu na kueleza kuwa ni vyema sasa sheria ikaweka ukomo cha idadi ya watu wanaopaswa kuteuliwa kwenye ofisi husika.

Breaking News:Mwigulu Nchema Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu wa Ranchi za Taifa Pamoja Na Wakurugenzi wa Bodi ya NARCO

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba jana alifanya ziara ya siku moja kukagua mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ya ranchi ya Taifa ya Ruvu.

Akiongea  na waandishi  wa  habari baada ya ziara hiyo, Waziri Nchemba  alisema ujenzi wa ranchi hii ya Taifa ya Ruvu ulianza mwaka 2010 lakini hadi sasa haujakamilika kutokana na uzembe  na kukosa uzalendo kwa baadhi ya watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia mali hii ya Umma.

Kutokana na uzembe huo, waziri Nchemba amefanya maamuzi yafuatayo;


  • Kwanza,amewasimamisha wakurugenzi wote wa bodi ya (NARCO) kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa kwa kushindwa ama kwa maksudi au vinginevyo kusimamia ujenzi wa machinjio haya ya kisasa. Alisema Bodi hii imesababisha Taifa lipoteze Billion 5.7 zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa hatua za awali za machinjio haya.


  • Pili,amesitisha kuendelea kwa kazi kwa mkurugenzi wa ranchi za Taifa kwa kushindwa kusimamia mradi huu ulioliingizia Taifa hasara ya Bilion 5.7
  • Tatu,ameagiza ndani ya siku 7 kupitia wataalam wa wizara wahakikishe wanampelekea ripoti ya thamani ya fedha inayohitajika kumalizia ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa


  • Nne,ameagiza wahusika wote walioshiriki kuliingizia Taifa hasara hii wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria  kwaajili ya hatua za kinidhamu.

DK. KIGANGWALLA Atoboa Jipu....Watanzania Msikubali Kutozwa Rushwa Kwa Ajili ya Damu Hospitalini..Toa Taarifa Kwa Nesi au Daktari Atakayetoza Damu

$
0
0
IMG_0681
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog, Team.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.
Kauli hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.
Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.
“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.
Mtu atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.
Awali katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.
“Motisha sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu..
Lakini kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.
“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.
IMG_0689
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016
Awali akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu salama.
Katika hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka zilizopo na kufukuzwa kazi.
“Naziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.
Hilo haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika unahitaji damu!!
Kwa upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo wanazipata bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.
“Damu inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
IMG_0703
Meneja wa kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
IMG_0690
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 katika ofisi hizo.
IMG_0725
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.
IMG_0729
IMG_0743
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
IMG_0764
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini Dar es Salaam.
IMG_0770
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
IMG_0760
Mmoja wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.
IMG_0774
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.
IMG_0826
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.

Serikali Yanunua Mashine Mpya Ya CT-Scan Katika Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbili Yenye Uwezo Wa Hali Ya Juu

$
0
0
Na Magreth Kina-Maelezo
Serikali imenunua mashine  mpya ya CT-Scan yenye thamani ya  takriban dola  za Marekani milioni 1.7  yenye  uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali  katika Hospitali  ya Taifa ya Muhimbili(MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam.

Ununuzi wa mashine hiyo, umefanyika kufuatia agizo la Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoifanya hivi karibuni ambapo aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma zake na kuhakikisha vifaa tiba na dawa   vinapatikana ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya.

Hayo yamegundulika jana baada ya ziara ya Naibu  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi  Kingwangala aliyoifanya jana katika hospitali hiyo, ambapo alitembea Idara ya  Magonjwa ya Dharura,Idara ya Mionzi,  sehemu  mpya ya wagonjwa waliopo chini ya ungalizi maalum(ICU), ambayo inafanyiwa ukarabati na wodi mojawapo.

Akizungumzia kuhusu mashine ya CT-Scan Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dkt. Flora Lwakatare alisema mashine hiyo , iliyotengenezwa na kampuni ya  Siemens  mpya imefungwa siku mbili zilizopita na imeshaanza kufanya majaribio  kwa wagonjwa 26  tangu ilipofungwa.

 Dkt. Flora aliongeza kwamba mashine hiyo iko moja tu nchini na katika nchi za Afrika Mashariki nchi nyingine iliyonunua mashine hiyo ni Kenya katika Hospitali ya Aghakhan.

Mashine hii inatoa huduma za hali ya juu kwa magonjwa ya moyo, ubongo, tumbo, kifua na inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde sita,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mashine hiyo Naibu Waziri huyo, alisema imenunuliwa kwa fedha za Serikali wala sio mkopo.

Tunatarajia kununua mashine hii katika hospitali ya Dodoma na Mwanza,” alisema Waziri Kingwangala.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Laurence   Maseru alisema mashine hiyo ina sahani 128 mara 2 ikilinganishwa na iliyokuwepo ambayo ilikuwa inatumia  sahani sita.

 Kwa upande wa mashine ya MRI alisema tangu ilipofanyiwa matengenezo makubwa Novemba 26, mwaka jana  hadi sasa imesha hudumia wagonjwa 560.

 Dkt. Kingwangala  alitembea katika Idara  cha huduma za dharura na kuangalia jinsi huduma zinavyotolewa, ambapo alielezwa na  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura Dkt. Juma Mfinaga kuwa huhudumia wastani wa wagonjwa 300 hadi 400 kwa siku na wanafanya kazi kwa kutumia mfumo maalum wa kompyuta bila kutumia karatasi.

Naibu Waziri huyo, mbali na kupongeza maboresho yaliyofanyika na huduma nzuri, alitoa maagizo kwa uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma  zinazotolewa hospitalini hapo kuwa za kitaifa zaidi.

 Alitolea  mfano  huduma  kulipa kwa kuongeza vitanda na matumizi ya choo kimoja kila chumba ili kuweza kuvutia wateja.

 “Sisi tunaweza kufanya biashara kwa kuboresha huduma za kulipa ili zimpendeze na kuvutia wateja. Na fedha zitakazopatikana zitatumika kununua dawa , vifaa tiba na kuwapatia wafanyakazi motisha, "alisema.

Aliutaka uongozi huo pia kuhakikisha inawalipa wafanyakazi fedha za  malipo ya ziada kwa wakati ifikapo tarehe 25 ya mwezi unaofuata,kutumia mfumo wa kompyuta sehemu zote, kupunguza msongamno wa wagonjwa na kuwa wabunifu.
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images