Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Azungumzia Sakata La Misaada Ya Mbunge Wa CHADEMA Kukataliwa Hospitalini

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema misaada inayotolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii ni lazima iwe imekidhi viwango vya ubora, hivyo haitakiwi kuangaliwa kwa vigezo vya dini, itikadi wala siasa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake baada kituo kimojwapo nchini kukataa misaada iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA), Wilfred Lwakatare hivi karibuni.

Dkt. Ulisubisya alisema hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini viliripoti kwamba misaada iliyotolewa na Mbunge huyo, katika baadhi vituo afya Zahanati kwa ajili ya wajawazito  ilikataliwa.

“Serikali ina sera ya kusaidia jamii hususan misaada inayotolewa kwenye huduma za afya, ambayo inakidhi viwango vya ubora kulingana Sheria , kanuni na taratibu za Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),” alisema Katibu Mkuu huyo.

Hivi karibuni iliripotiwa kwamba baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea msaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na mbunge wa Chadema   kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.

Dkt. Ulisubisya amewataka watendaji wa afya wa vituo hivyo  wasiangalie misaada hiyo kwa misingi ya dini, itikadi na kisiasa.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo amewataka watu mbalimbali wenye lengo la kutoa misaada katika vituo vya afya kuhakikisha kwamba imekidhi viwango viliyowekwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Katika hatua nyingine aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando amekabidhi ofisi hiyo kwa Katibu Mkuu huyo mpya.



Hii Ndiyo Tofauti ya Jakaya Kikwete na Rais John Pombe Magufuli

$
0
0
KUMEKUWA na kiu kubwa ya kumlinganisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na mtangulizi wake, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Kwamba nani ni nani? Si kwa hoja ya kimaumbile kuwa JK ni mrefu na mweupe wakati Magufuli ni mweusi na mfupi, la hasha!

Haiangaliwi mantiki ya kifamilia, kwani inaeleweka JK mkewe ni Salma na Magufuli wake ni Janeth. Hatupo huko, hapa kinachozungumzwa ni uongozi wao.

Kosa la kimsingi ni kutafsiri matokeo ya mafanikio ya sasa kama makosa au udhaifu wa serikali iliyopita.
Watanzania wamekuwa wepesi kuhukumu. Wazuri mno katika kushabikia michakato. Halafu hukumu zinakuwa za jumla mno.

Usimlaumu JK kama huwezi kuchanganua mtindo wake wa uongozi. Usimsifu tu Magufuli ikiwa hujatambua anatumia aina ipi ya uongozi. Na usipende kuongozwa na hoja za jumla (general), penda kushika kitu halisi (be realistic). Ni kwa kutambua vizuri mtindo wa uongozi ambao JK aliutumia ndiyo utaweza kubaini makosa ambayo yalifanyika, vilevile utaweka tahadhari kuhusu mwenendo wa Magufuli, kwamba asipokuwa makini wapi ataanguka.

Kuna dhana nne za uongozi. Ukizielewa hizo itakurahisishia kutambua nani ni kiongozi mzuri, anapatikanaje, kipi kinaweza kumfanya mtu kuwa kiongozi mzuri na chanzo kinachoweza kumpa nguvu kiongozi.

Dhana ya hulka (trait theory); Hii inachambuliwa katika Sayansi ya Siasa (Political Science) kama moja ya vigezo vya kutambua aina ya kiongozi. Ndani ya somo la saikolojia, inatafsiriwa kama kipimo cha kung?amua hulka, hisia, fikra na uhusika wa kiongozi. Katika dhana hii, kinachoangaliwa ni aina gani ya mtu anaweza kuwa kiongozi mzuri.

Dhana ya kitabia (behavioral theory); Je, kiongozi ana mwenendo gani kitabia? Kiongozi mzuri anafanyaje mambo yake? Katika dhana hii ndipo ambapo unaweza kung'amua nyenendo za viongozi. Katika dhana hii ndipo utaweza kuona tofauti ya JK wa 2005-2015 na Magufuli 2015-2020 au mpaka 2025, vilevile tutawamulika na watangulizi wao. Nakuomba twende pamoja.

Dhana ya dharura (contingency theory); Kwamba hajulikani kitabia na hakuna mwenye kutambua atakwenda kufanya nini, yaani hatabiriki lakini anapitishwa kwenda kushika hatamu. Anayepatikana kupitia dhana hii, matokeo chanya hushangaza zaidi kuliko hasi. Na zaidi, mazingira ndiyo yanaweza kusababisha kiongozi aonekane mzuri. Kupitia dhana hii nitaeleza jinsi Magufuli anavyong'ara kama ilivyotokea kwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alivyong'ara mwaka 1995.

Dhana ya nguvu na ushawishi (power and influence theory); Kama Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa, angeshinda urais mwaka huu, angekuwa amebebwa na dhana hii. Dhana hii pia ndiyo iliyomuingiza JK mwaka 2005. Kwamba mtu anakuwa na mtandao mkubwa wenye nguvu na ushawishi kiasi kwamba inakuwa vigumu kumzuia.

Kuhusu dhana ya dharura inavyombeba Magufuli kama ilivyotokea kwa Mkapa, ni mazingira ambayo wahusika waliyakuta.
Magufuli ameikuta nchi ikiwa na nidhamu mbaya ya matumizi ya fedha na udhibiti wa rasilamali za umma. Kuingia kwake na kasi kubwa ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali, kuahirisha shughuli zenye kutumia fedha nyingi kinyume na kipaumbele cha wananchi pamoja na kushughulikia ufisadi, vimemfanya ang'are kwa haraka mno.

Magufuli pia amerejesha nidhamu ya utumishi wa umma. Sasa mfanyakazi serikalini anatambua maana ya kuwajibika, kwani asipofanya hivyo anakuwa jipu.

Mkapa alikuta nchi watu binafsi walikuwa na uwezo mkubwa kuliko serikali. Akarejesha meno serikalini, akawabana wafanyabiashara na kukusanya kodi vizuri, akajenga miundombinu, akatanua wigo wa soko huria na kadhalika. Mkapa akaonekana malaika!

Ndani ya dhana ya kitabia ndipo unaweza kuiona tofauti ya kiuongozi kati ya JK na Magufuli. Mwanasaikolojia wa Kijerumani, hayati Kurt Zadek Lewin, aliwahi kuandika aina tatu za viongozi ambao wanaweza kupatikana kutokana na tabia zao.

Kiongozi anayetaka lake litimie (autocratic leader); Huyu wakati mwingine hutafsiriwa kama kiongozi wa kiimla. Si mwenye kutaka sifa, anachokifanya ni kutimiza maono yake tu. Watu wamchukie lakini dhamira yake itimie. Hapa ndipo unapoweza kumuona Magufuli.

Kiongozi mwana demokrasia (democratic leader); Kiongozi ambaye hafanyi mambo yake peke yake. Anashirikiana na timu yake kupanga na kutekeleza mipango ya kila siku. Huyu ni kiongozi ambaye anawaamini mno wasaidizi wake. Anawaacha wenzake waamue na kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa uhuru mkubwa. Na yeye binafsi hatendi mpaka yawepo makubaliano ya kitimu. Hapa ndipo unamuona JK.

Kiongozi mtegemea wasidizi (laissez-faire leader); Wasaidizi wanakuwa wanafanya kazi kubwa na wenye nguvu kuliko kiongozi mkuu. Yaani rais wa nchi anakuwa kubwa jinga (figure head) kwa sababu watu wake wanaweza kufanya chochote pasipo yeye kutia neno.

Tanzania hatujawahi kuwa na rais kubwa jinga. Wote pamoja na makosa ya hapa na pale, wamesimama vizuri kama marais na viungo muhimu (key figures) wa nchi kila mmoja kwa zama zake. Sababu ya kutegemea wasaidizi inaweza kutokana na uvivu wa kiongozi mkuu au uwezo mdogo alionao, kwamba wasaidizi wanakuwa na uwezo mzuri kiutendaji kuliko yeye, kwa hiyo anaona bora awape uwanja mzuri wa kutenda.

Ukiachana na aina hizo tatu za viongozi kama zilivyoletwa na Lewin mwaka 1930, katika somo la uongozi, wanatajwa viongozi aina sita.

Kiongozi mmbeba mamlaka yote (authoritarian), na ndani yake ndimo unaweza kumpata mwenye kutaka lake tu (autocratic). Rais anataka kila jambo lipate usimamizi wake wa karibu na aone matokeo. Magufuli yupo hapa!

Aina nyingine ya kiungozi ambayo Magufuli anakwenda nayo ni kuwa kiongozi mleta mabadiliko (transformational), kwamba habanwi na wasaidizi wake kuamua na kupanga kile ambacho yeye anaona kinafaa. Kwa kawaida kiongozi anayefanya mambo yake kwa mitindo hiyo miwili, ndani yake huongozwa na hali ya kutoamini mtu, kwamba wakati wowote wanaweza kumsaliti kwenye harakati zake za kutimiza malengo aliyojiwekea.

Faida kubwa katika mitindo hiyo miwili ni kwamba kisiasa, kama kiongozi mkuu anakuwa na utashi wa kweli wa kuwahudumia wananchi wake na kuwapa matokeo yenye kuonekana, huutikisa mfumo wote ili utende kama yalivyo matakwa yake. Ona Magufuli anavyotikisa hivi sasa.

Hasara za mitindo hiyo ni kuwafanya viongozi wa nchi waishi kama maroboti. Hawatajiamini na kufanya kazi kwa sura ambayo wanaona ni bora, wao wanajielekeza katika kumfurahisha kiongozi mkuu. Zaidi hawaishi kama viongozi, wanatenda tu mawazo ya kiongozi mkuu. Yaani wanakuwa watu wa kupokea maagizo na kufanya jinsi kiongozi wao anataka. Wanakuwa wazee wa 'kukopi' na 'kupesti'.

Na kwa sababu serikali ni taasisi kubwa, husababisha baadhi ya mambo ambayo siyo kipaumbele cha kiongozi mkuu kudumaa, wakati yangeweza kufanyiwa utekelezaji na viongozi wa chini kama wangekuwa huru na wenye kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Ifahamike kuwa mifumo ya uongozi, kifaida na kihasara huzalishwa na saikolojia. Watendaji wa chini wanaweza kufanya mambo yao kama watu wasio na akili zinazojitegemea. Wanategemea akili za mkuu.
Kama kiongozi akiwa na haiba pendwa (charismatic leader), inaweza kuwasisimua na wasaidizi wake kujituma, kwani nao wanakuwa wanavutiwa naye kiuongozi na kitabia.

Aina hizo za uongozi, wakati mwingine huzaa kiongozi wa kiimla (dictator), hivyo kupitiliza na kuwafanya wasaidizi wake kumuogopa. Yaani badala ya kufanya kazi kulingana na mahitaji yao ya kiuongozi, wanakuwa watekeleza majukumu kwa hofu. Wakipigiwa simu na bosi mkuu, wanatetemeka kwa sababu hawajui wataambiwa nini.

Mafanikio ya Magufuli ndani ya muda mfupi ni kuwa nchi ilikuwa tenge. Watumishi wengi wa umma walikosa Utanzania, kwa hiyo wao wenyewe wakawa wahujumu uchumi badala ya kujenga uchumi. Kiongozi kama baba wa familia (paternalistic). JK na Magufuli kama ilivyokuwa kwa watangulizi wao, ni vichwa vya serikali na uhusika wao unaonesha hivyo.

Hata hivyo, mafanikio ya kiongozi wa aina hii husababishwa na hulka binafsi na aina ya watu ambao anafanya nao kazi. Akiwa kiongozi mwana demokrasia, anahitaji watu waaminifu, wachapakazi na wakweli mno. Kama watu ambao kiongozi anafanya nao kazi wakiwa siyo waaminifu, waongo na wavivu, kiongozi wa mtindo wa demokrasia kama alivyokuwa anakwenda nao JK ni vigumu mno kupata mafanikio stahili.

JK katika mtindo wake wa kidemokrasia, alitengeneza mfumo wa mamlaka huru kwa wasaidizi wake (free rein), kwamba nao wanaweza kufanya uamuzi kwa namna ambavyo wanaona inafaa. Wengi waliitumia vibaya nafasi hii ya kuaminiwa.

Rais Magufuli siku alipokabidhiwa cheti cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva, ikiwa ni wiki moja kabla hajaapishwa, alimweleza JK: "Kuna watendaji wako walikusaliti, hao ndiyo nitaanza nao".
Kauli ya Magufuli ilikuwa na maana kuwa aliutambua usaliti wa kiungozi kwa umma ndani ya serikali ya JK na ulikuwa ukimkereketa lakini aliunyamazia kimya kwa sababu hakuwa na mamlaka.

Tatizo ni nini hapo? Lipo wazi, mara nyingi kiongozi wa kidemokrasia, hulinda zaidi mfumo wake usitetereke na wakati mwingine anapopewa taarifa za udhaifu wa wasaidizi wake, huchukulia kuwa ni majungu. Na anapoamua kuchukua hatua, huenda taratibu kwa sababu hufanya mchakato. Kiongozi mwana demokrasia hukataa kuchuakua uamuzi ambao mwisho ataonekana amekurupuka au kufanya uonevu.

Magufuli amekuwepo ndani ya Baraza la Mawaziri la JK kwa kipindi chote cha miaka 10, kwa hiyo anajua dhamira, maono pamoja na utendaji wa JK. Hiyo ndiyo sababu alisema kilichomuangusha JK ni watendaji wake wanafiki.

Kwa kawaida kiongozi anapoingia madarakani, kunakuwa na utangulizi wake, hivyo inakuwa rahisi kujua pa kuanzia kwa sababu anafahamu kasoro ambazo zilijiri kwa mtangulizi wake.

Mathalan, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliikuta Tanzania ikiwa mkusanyiko wa makabila na koo kubwa kubwa. Akaiunganisha na kujenga taifa moja. Akataka maendeleo ya pamoja kwa kila Mtanzania, hivyo akaasisi mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea.

Hakutaka watu wachache watajirike wengi wabaki hohehahe (upebari), alishachungulia matatizo ya viongozi wengine kutumia madaraka yake vibaya, akaweka miiko ya uongozi, kisha kuunda Azimio la Arusha.

Mwalimu Nyerere alijenga viwanda kwa lengo la kumpa nguvu Mtanzania, aweze kuzalisha bidhaa zake ili asiuze malighafi nje kabla ya kuziongezea thamani. Maendeleo yalikuwa mazuri lakini kwa kusuasua. Miaka 25 ya falsafa za Nyerere, Mtanzania hakutoka kwenye umaskini.

Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassa Mwinyi aliposhika nchi, alifanya uthubutu kwa kuondoa vigingi wa kijamaa vilivyowekwa na Nyerere dhidi ya upebari. Bila kubadili mfumo, Tanzania ikibaki kuwa ya Ujamaa na Kujitegemea, wafanyabiashara wakawa na nguvu mno.

Rais Mwinyi ndiye mwanzilishi wa soko huria katika nchi. Hata hivyo, hakuweka misingi mizuri ya ukusanyaji kodi, matokeo yake serikali ikakosa uwezo mzuri wa kifedha. Wafanyabiashara wakajiona wapo kwenye neema.

Katika kuipa nguvu serikali, Rais Mwinyi alianzisha chombo cha kukusanya mapato ya serikali kuu ambayo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Na mpaka alipomkabidhi nchi Rais Mkapa mwaka 1995, nchi ilikuwa inakusanya kodi wastani wa shilingi bilioni 25 kwa mwezi.

Rais Mkapa alipochukua nchi, pamoja na uwepo wa TRA, aliona bado kulikuwa na udhaifu wa ukusanyaji mapato, akaanzisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi. Mwaka 2004, Rais Mkapa aliweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 150 kwa mwezi lakini mpaka anakabidhi nchi, mapato ya mwezi yalikuwa shilingi bilioni 170.

Uhuru wa soko ulioanzishwa na Rais Mwinyi, ulisababisha wafanyabiashara wafanye fujo na kupandisha mfumuko wa bei mpaka asilimia 27 mwaka 1995, Rais Mkapa alishughulikia tatizo hilo na kupunguza mpaka asilimia 4.2.

JK alipochukua nchi, aliona mapato hayo, shilingi bilioni 170 kwa mwezi ni kidogo mno, akaweka utaratibu mzuri wa kutanua fursa za kibiashara kwa nchi. Kila mtu anaweza kuwa shuhuda ukuaji wa kibiashara katika miaka 10 ya JK. Aliona kasoro kwenye sekta ya madini, kwamba nchi ilikuwa inapunjwa na wawekezaji walikuwa wananeemeka kama vile wanavuna shambani kwao. Matokeo ya jumla yakawa kuongeza mapato ya nchi mpaka kufikia shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

Utaona kuwa Mkapa alikabidhi nchi ikiwa inakusanya mapato zaidi ya mara sita ya alivyoachiwa na Mwinyi, JK pia amemkabidhi hatamu Magufuli, akiwa ameongeza mara sita ya Mkapa. Na takwimu za TRA zinaonesha kuwa miezi mitatu ya Julai mpaka Oktoba, makusanyo yalikuwa shilingi trilioni 3.77, sawa na wastani wa shilingi trilioni 1.25 kwa mwezi.

Mpaka hapo unaweza kuona kazi nzuri iliyofanywa na JK, mbali na kukusanya mapato, aliweza kuimarisha mfumo wa utawala bora. Angalau tukaweza kuona hata vigogo wanawajibishwa na mnyonge anasikilizwa.

JK aliweza kuimarisha ukaguzi katika hesabu za serikali, kuifanya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) kuwa taasisi huru ikiongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akachochea mabadiliko ya kibunge kuanzia mwaka 2007, yaliyowafanya wapinzani kuwa wenyeviti wa kamati za kusimamia hesabu za serikali, kuanzia ile ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Kwa sasa POAC imeingizwa ndani ya PAC.

Ni kupitia uwazi huo ambao JK aliuanzisha, uliweza kuimarisha hadhi na mamlaka ya bunge, hivyo kusaidia kugundulika kwa ufisadi mbalimbali serikalini. Rejea Tegeta Escrow, Richmond, EPA na nyinginezo.

Ni kipindi cha JK ndipo baadhi ya vigogo wa jeshi la polisi wenye hulka ya kubambikia watu kesi walifukuzwa kazi. Kashfa ya sukari iliibuliwa, mawaziri waliwajibishwa kwa kashfa ya tokomeza ujangili.

Ukipiga hesabu ya idadi ya mawaziri ambao walipoteza kazi kipindi cha JK, utagundua namna ambavyo kulikuwa na muundo mzuri wa uwazi serikalini. Ukifanya madudu unagundulika.

Weka pembeni Daraja la Kigamboni na Barabara za Mabasi Yaendayo Kasi (RBT Roads), JK ndiye rais ambaye ametekeleza miradi mingi ya maendeleo katika kipindi chake cha uongozi kuliko wote waliomtangulia. Ameiwezesha mikoa iliyokuwa inafikika kwa tabu, sasa inafikika kwa urahisi. Leo hii nchi inaunganishwa na barabara za lami mkoa kwa mkoa kwa zaidi ya asilimia 80. Magufuli ataunganisha kufikia asilimia 100.

Hata hivyo, kutokana na mfumo wa JK wa demokrasia ya uongozi, aliwaamini watendaji wake, kumbe pamoja na shilingi bilioni 900 au trilioni 1.25 nyakati za mwisho za utawala wake, bado kumekuwa na fujo kubwa ya wizi na ukwepaji kodi.

Ni rahisi sasa kuamini kuwa kumbe JK angeachana na demokrasia ya uongozi kisha kushika mtindo wa kusimamia na kufuatilia kila kitu kama afanyavyo Magufuli sasa, pengine angekabidhi nchi ikiwa inakusanya hata zaidi ya shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi.

Ukiwa nje ya mchezo unaona vizuri zaidi, Magufuli aliyaona makosa ya JK, kuwa bandarini na TRA kuna fujo kubwa inayofanywa na watumishi wa mamlaka hizo pamoja na wafanyabiashara wakwepa kodi. Magufuli aliona kasoro za matumizi mabaya ya fedha za serikali, alipoingia tu akaanza kushughulikia udhibiti. Akazuia safari za nje na shughuli zisizo na tija.

Kwa kudhibiti ukwepaji kodi, Magufuli ameweka uelekeo wa serikali kukusanya shilingi trilioni 1.3 ndani ya Desemba hii.
Utaona kuwa Magufuli aliona mianya ya udhaifu wa JK, kuwa mfumo wake wa demokrasia ya utawala, umemgharimu. Angeweza kufanya zaidi lakini alihujumiwa na watendaji wezi walioruhusu wafanyabishara kujitanua.

Hata hivyo utaona kuwa Magufuli hajafanya kitu kikubwa kutanua wigo wa upatikanaji wa mapato, kwani alichokifanya ni kubana matumizi, kudhibiti kodi na kuwashughulikia watendaji wa serikali wezi na wafanyabishara wahuni. Yaani anashughulikia kwanza zile kasoro alizoziona wakati wa JK.

By Luqman Maloto

Waziri Maghembe Atema Cheche......Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Pamoja na Maofisa wa Misitu wa Mikoa nchi Nzima

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo na Maofisa wa Misitu wa Mikoa nchi nzima kupisha uchunguzi wa upotevu wa mapato ya Serikali.

Akizungumza jana na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo Dar es Salaam, Prof. Maghembe alisema agizo hilo limekuja kutokana na ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.

Aliagiza pia maofisa hao wote wanaokusanya maduhuri ya Serikali katika Wilaya watumie muda wa siku kumi kuanzia jana kuhakikisha maduhuri yote yaliyokusanywa yanapelekwa benki ikiwa ni pamoja na kukabidhi vitabu vya kukusanyia mapato kinyume cha hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Wale district forestry officers wote wapeleke vitabu vyao wanavyokusanyia maduhuri ya Serikali kwenye ofisi za Kanda, Naibu Katibu Mkuu tusaidie kuwasiliana na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ifanye ukaguzi wa vitabu hivyo ndani ya siku kumi tuhakikishe fedha zinazotakiwa zinaingia kwenye mfuko wa Serikali, Mtu anakusanya fedha ya Serikali toka mwaka 2004 mpaka leo hajapeleka benki ananeemesha hali yake ya nyumbani, hili hapana”. Alisisitiza Prof. Maghembe.

Kwa mujibu wa Waziri Maghembe Bw. Mohammed Kilongo ambaye Idara yake ndiyo inatoa vitabu kwa ajili ya kukusanya maduhuri ya Serikali katika Mikoa yote na Wilaya zote nchini analazimika kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi ambapo ukikamilika sheria itachukua mkondo wake bila uonevu wowote.

Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amewaagiza pia Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kutumia muda wa siku saba kurudi katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii maarufu kama Mpingo House ambalo walihama mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka jana na kwenda kupanga katika jengo la NSSF Mafao House lililopo Ilala.

Wakati tunajenga nyumba hii hapa, tumejenga jengo hili ni kama jengo la misitu ndio maana linaitwa Mpingo House kwa maana ni jengo la Misitu, ninyi wenyewe mmejenga jengo kubwa hili mmemaliza mmehama, Naagiza jumatatu Januari 11 muwe mmesharudi katika jengo hili, ghorofa ya tatu nikija kukagua niwakute, haiwezekani mueleze matatizo yote mliyonayo muhame nyumba ya Serikali mkapange jengo hapo jirani” Alisema Prof. Maghembe.

Katika hatua nyingine ya kuboresha uhifadhi wa Misitu nchini Waziri Maghembe ameiagiza Idara ya Misitu na Nyuki ya Wizara ya Maliasili kuhakikisha inajiimarisha katika lengo lake kuu la uhifadhi kwa kushirikiana na wadau wanaohusika kuhakikisha Mamlaka iliyolengwa ya Uhifadhi Misitu inakamilika.

Tunataka tutoke kwenye Wakala wa Huduma za Misitu (Tanzania Forestry Services Agency) twende kwenye Mamlaka ya Uhifadhi wa Misitu (Tanzania Forestry Services Authority) ili tuweze kufanya vizuri zaidi kwenye eneo la uhifadhi na uendelezaji wa misitu nchini, Katibu Mkuu tunaomba pia usaidie kufanikisha hili” Alisema Prof Maghembe.

Aliongeza kuwa wakati wa kuundwa Mamlaka hiyo ni vizuri pia Idara ya Misitu na Nyuki ya Wizara ya Maliasili ikatenganishwa na kila moja kuwa Idara kamili kutokana na umuhimu wa kila sekta katika kujenga uchumi wa nchi kwa kutoa fursa ya kuboresha maeneo hayo na kuongeza pato la taifa.

Ameitaka pia Idara ya Misitu na nyuki kupitia Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuhakikisha kuwa inaongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuziba mianya yote ya ubadhilifu pamoja na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo.

Akizungumzia mchango wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwenye pato la taifa Mtendaji Mkuu, Bw. Juma Mgoo amesema katika mwaka huu wa fedha TFS imeweka makisio ya kukusanya Tsh. Bilioni 88 ambapo mpaka hivi sasa wameshakusanya zaidi ya asilimia 20 na makisio hayo.

Waziri Maghembe akizungumzia kuhusu uvamizi kwenye hifadhi za taifa na mapori ya akiba amewataka wananchi wote waliovamia maeneo ya hifadhi za taifa kwa ajili ya kuchunga mifugo waondoke ndani ya siku saba zijazo, na wale walivamia mapori ya akiba kwa shughuli za kilimo na ufugaji waondoke ndani ya miezi mitatu ijayo.

"Serikali itawaondoa kwa nguvu wasipotekeleza agizo hili la kuondoka katika maeneo ya hifadhi za taifa na kwenye mapori ya akiba yaliyohifadhiwa” Alisisitiza Prof. Maghembe.

Akizungumzia kuhusu biashara ya Mkaa, Prof. Maghembe amewaagiza wataalamu wa Idara ya Misitu kusimamia biashara ya mkaa kwa kuzingatia taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji wa Mkaa nje ya nchi.

Ameongeza kuwa nishati ya Mkaa ni muhimu lakini Tanzania ina hifadhi kubwa ya makaa ya mawe ambapo ameitaka Idara ya Misitu kwa kushirikiana na wadau wengine kuona ni namna gani ya kuweza kutumia mbadala huo kwa kuzalisha makaa hayo ya mawe kwa matumizi ya kawaida ili kuokoa misitu nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri yatafanyiwa kazi kwakuwa lengo lake ni kuona dhamira ya msingi ya Serikali ya awamu ya tano inafikiwa ya kubana matumizi, kuongeza mapato ya Serikali na kuhifadhi maliasili za taifa ikiwemo misitu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,
Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kutoa Harufu Mbaya Sehemu za Siri Kwa Wanawake.

$
0
0
Kuna mshikaji wangu ana mpenz wake lakini alivyonambia huwa hafurahii tendo kwa sababu ya huyo mpenzi wake kutoa harufu mbaya kila wanapoanza kufanya sex
Na sasa hivi ana mpango wa kuachana nae kimya kimya bila kumwelezea tatizo
Suluhisho kwa hili tatizo
 Tafadhari mwenye ujuzi wa namna ya kuondoa tatizo hilo afunguke hapa

Mahakama kuu Kitengo cha Ardhi Yapiga 'Stop' BomoaBomoa Dar Hadi Kesi ya Msingi Isikilizwe.......Mkuu wa Mkoa Atoa Tamko

$
0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi imeweka zuio la kubomoa nyumba zilizopo katika wilaya ya Kinondoni hasa zile ambazo wamiliki wake wameleta ombi lao mahakamani kuzuia kubomolea.

Akitoa hukumu hiyo jana  mbele ya walalamikaji, wakili wa Serikali, mawakili wa walalamikaji na wananchi, Jaji wa Mahakama hiyo kuu ya Ardhi Mhe.Panterine Kente alisema kuwa mahakama imezingatia maelezo toka pande zote mbili kwa kuangalia madhara watakayopata wananchi kwa kutekelezwa kwa zoezi hilo.

Jaji Panterine Kente aliongeza kuwa mahakama ya Ardhi haijaweka zuio la bomoa bomoa kwa Tanzania nzima bali kwa wale tu walioleta maombi ya shauri la zuio la kubomolewa nyumba zao na kusisitiza kuwa Serikali  itaendelea na uwekaji wa alama za x na ubomoaji wa nyumba zilizopo sehemu hatarishi na sehemu zisizostahili.

Nakuagiza Wakili Abubakari Salim uniletee majina yote leo hii na sio kesho ya waliofungua shauri la zuio la kutobomolewa nyumba zao ili tuweze kuendelea na zoezi la ubomoaji” Alisema Jaji Kente

Akizungumza baada ya kutolewa hukumu hiyo Wakili wa Serikali Manchare Henche alisema wamepokea hukumu hiyo na wao wataendelea na majukumu yao ya ubomoaji wa maeneo hatarishi kama Mahakama ilivyoeleza kuwa haijatoa zuio la bomo bomoa kwa Tanzania nzima ila kwa wale tu walioleta shauri la zuio.

“Tunaomba walio maeneo ya mabondeni wahame kwani zoezi hili linaendelea na zoezi la uwekaji wa alama za x litaendelea kama kawaida kwa maeneo mengine nje ya haya yaliyowekewa zuio” Alisema Henche.

Aidha akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutolewa hukumu hiyo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia alisema kuwa uamuzi umeridhisha na pia mahakama imetenda haki kwa wananchi wa kinondoni na wanashukuru kwa kupata nafasi ya kusikilizwa kwa hoja zao.

Kesi hiyo namba 822 ilifunguliwa na wawakilishi nane wanaowawakilisha wananchi 674 ambao nyumba zao zilikuwa katika mpango wa kubomolewa  chini ya sheria za mipango miji.

Baada ya Mahakama kuu ya Tanzania kitengo cha Ardhi kutoa zuio la bomoa bomoa kwa wakazi hao kesi ya msingi itatajwa tena Januari 11.

Mkuu wa Mkoa Wa Dar Atoa Tamko
Wakati  mahakama kuu ikisimamisha zoezi la bomoa bomoa, Mkuu wa Mkoa  Dar es Salaam, Said Meck Sadick amejitetea na kukanusha taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa kisiasa hususani wenyekiti wa mitaa na baadhi ya wakazi  wanaoishi maeneo hatarishi ya mabondeni juu ya serikali kuvunja nyumba, ikizingatia kutotoa maeneo mbadala ya kujenga makazi mapya ya kudumu.

Meck sadick amesema mwaka 2011 yalipotokea mafuriko serikali  iliwapatia viwanja wakazi waliokuwa na nyumba katika maeneo  hatarishi  ya  mabondeni kwa Wilaya zote  tatu za Mkoa Dar es Salaam katika eneo la Mabwepande wilaya Kinondoni.

Kwa mujibu mkuu wa mkoa jumla ya viwanja 1007 viligawiwa kwa wakazi hao wa mabondeni na viwanja vitatu havikugawiwa kwa sababu viliangukia maeneo yasiyofaa kwa makazi.

Aidha sambamba na kupatiwa viwanja wakazi hao walipatiwa misaada ya kibinadamu pamoja na vifaa  vya kiujenzi ikiwemo mifuko ya saruji 100 mabati na mbao kila kaya na kuwawekea huduma muhimu  za kijamii.

Amesema wakazi hao wamediriki kuuza viwanja vyao kwa bei ya chini na kurudi maeneo waliyokuwa  wakiishi awali na wengine kuuza na kupangisha nyumba zao walizojenga mabondeni licha ya Serikali  kuwataka waondoke katika maeneo hayo hatarishi.

Vile vile amesema Serikali kwa kushirikiana na halmashauri zote nchini imeanza na inaendelea na zoezi la bomoa bomoa kwa ajili ya kuwaondoa wakazi wote wanaoishi maeneo hatarishi  na  wale waliovamia maeneo yasiyostahili kujengwa.

Pia amesema zoezi hili la bomoa bomoa litafanyika nchi nzima ambapo kwa sasa limeanzia Mkoa Dar es Salaam na  wakazi waliojenga katika maeneo  hatarishi wabomoe wenyewe na kuondosha baadhi ya  vifaa vya ujenzi ambavyo vitawasaidia kwenda kuendeleza makazi mapya katika viwanja walivyopewa na serikali.

Amewataka wananchi kuacha kuendelea kulalamika wakati wanafahamu kuwa wamevunja sheria licha ya serikali kuwataka kuondoka kabla hawajapata madhara ikiwemo kuvunjiwa nyumba zao.

Breaking News:Waziri Mkuu awasimamisha kazi viongozi wa chama cha ushirika SONAMCU

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Cha Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU.

Akizungumza jana jioni(Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.

Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kukosa malighafi za kuendelea na uzalishaji.

Pia, amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi. Stela Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi wote wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma hizo na kutaka wafikishwe Mahakamani.

“Serikali imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji vimebaki vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za wakulima wa tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia mfumo wa Vyama vya Ushirika na namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao hadi kushindwa kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya mazao yao.

Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya Mahakama baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao wamehusika na wizi wa fedha za wakulimakiash cha Shilingi milioni 800 kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014tayari wamefikishwa Mahakamani na uchunguzi unaendelea. Pia, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu kukutana na wakulima hao ili kupatia ufumbuzi matatizo yao.

Aidha, ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa linaongeza pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa na kukua kwa uchumi wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda na kuviendesha Vyama Vya Ushirika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya ziara hiyo leo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea jijini Dar es Salaam.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,2 MTAA WA MAGOGONI,

S. L. P 3021,11410 DAR ES SALAAM

JUMMATANO, JANUARI 6, 2016.

The Internet Goes Berserk After Beyonce Announces Plans To Play African Woman With The BIGGEST Buttocks (Photos)

$
0
0

African American pop singer Beyonce wants to play the African lady with the BIGGEST ass and the continent isn’t pleased, NOT at all.

Black women, especially typical African women, boast of having the biggest natural booties of all race. South African lady who was the center of attraction in 19th century because of her gigantic buttocks is once again making headlines thanks to Beyonce.

Saartjie Baartman went through hell just because she possessed booty that mesmerized colonial masters.

The South African was taken as a slave from Bushmen tribe some 200 years ago and displayed in freak shows due to her unusually big buttocks.

She was later borrowed by scientists for experiments. Saartjie died in 1815 of alleged alcoholism and syphilis aged 25.

Even in her death, European continued to abuse her. Her corpse was sketched extensively, a cast was made of it and a surgeon removed her genitals which were on display in Paris until the 1970s, along with her skeleton.

It was only in 2002, after a personal appeal by Nelson Mandela, who was born in the same remote, rural part of South Africa, that her remains were returned for a dignified burial.

Jay Z’s wife has been mauled severely after news popped that she was writing and starring in a film about Saartjie Baartman.

Critics have been firing salvos at the ‘Drunk In Love’ songstress on social media and other relevant platforms.

34-year-old Beyonce has been accused of lacking basic human dignity for her desire to play the South African. Unconfirmed report indicates Bey has since backed down.



Mwigulu Nchemba Atumbua Majipu Mengine Iringa......Awasimamisha Kazi Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Tumbaku

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba amewasimamisha kazi viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku mkoani Iringa wanaotuhumiwa kushiriki katika ufisadi wa mkopo wa matrekta tisa kupitia mgongo wa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku na kujimilikisha wenyewe.

Nchemba alifikia hatua hiyo jana baada ya wakulima wa tumbaku kulalamikia viongozi wa vyama hivyo na kuwataka wakabidhi ofisi.

Awali, mwanachama wa Chama cha Msingi cha Mfyome, Francis Kilatu alisema Benki ya CRDB inawakata fedha zao huku wamiliki wa matrekta hayo wakiwa ni wengine hivyo alimuomba waziri kulishughulikia mara moja.

Serikali Yaamuru Waliovamia na Kujigawia Maeneo Shamba la Sumaye Waondoke

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki amewataka waliovamia na kujigawia maeneo ya watu wengine likiwamo la Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Ritha Mlaki waondoke mara moja kwa kuwa wamevunja sheria.

Alisema zaidi ya watu 2,000 wakiwamo waliobomolewa nyumba katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam wamevamia na kujigawia mashamba hayo yaliyopo Tegeta na Goba kinyume cha sheria.

“Kisa wamevunjiwa nyumba zao walizojenga kinyume cha sheria ndiyo wameamua kuvamia maeneo yasiyo yao, hili ni kosa kama makosa mengine, nawataka waondoke haraka vinginevyo tutawachukulia hatua kali za kisheria,” alisema mkuu huyo wa mkoa.

Alisisitiza kuwa agizo la Rais John Magufuli lilikuwa ni maeneo yaliyoachwa wazi kuainishwa kwa ajili ya kupangiwa matumizi mengine na siyo kuruhusu watu kuvamia bila taratibu.

Sadiki alisema hakuna viwanja vilivyotengwa kwa ajili ya kuwagawia wananchi waliokumbwa na bomoabomoa katika maeneo ya mabondeni.

Zaidi ya nyumba 8,000 zilizojengwa kwenye Bonde la Mto Msimbazi, fukwe za bahari na kando ya mito zimeanza kubomolewa kabla ya kusitishwa na Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Sadiki alisema wananchi waliobomolewa nyumba zao na ambao watakumbwa na operesheni hiyo wasitarajie kupatiwa viwanja vya kujenga nyumba zao.

Bomoabomoa hiyo inaendeshwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ikiwalenga waliojenga kinyume cha sheria.

“Serikali haina viwanja vinavyotosha kuzigawia familia zaidi ya 8,000 zitakazobomolewa, niwashauri tu wasiendelee kupoteza muda wao kwa kuwasikiliza wanasiasa, watafute makazi mengine waende. Kama walivyovamia na kujenga ndivyo wanatakiwa kutafuta maeneo mengine wahamie,” alisema Sadick.

Alisema viwanja 1,007 vya Mabwepande vilitolewa kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko mwaka 2011 ambao waliwekwa kwenye kambi baada ya kukosa makazi,lakini cha kushangaza baadhi  yao waliviuza viwanja hivyo kwa bei ya chini na kurudi tena kwenye maeneo hatarishi.

Alisema kaya zote zilizokosa makazi kutokana na mafuriko hayo zilipatiwa maeneo. Waathirika 580 walitokea Ilala, Kinondoni 349 na Temeke 81.

“Kuna upotoshaji unaendelea kwamba yapo maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuwapatia wanaobomolewa sasa, jambo hili halina ukweli, ikumbukwe tuligawa viwanja vya Mabwepande baada ya Rais (Jakaya Kikwete) kuagiza tufanye hivyo ili kuwasaidia wale tu, waliokumbwa na mafuriko mwaka 2011,” alisema.

Diamond’s Wife Zari Goes Totally Insane After The Internet Called Her Daughter UGLY (Photos)

$
0
0

Can’t believe someone can actually hate on the innocent Princess Tiffah, she’s such an angel. Anyway the child was ‘attacked’ and the fuming Zari Hassan had to defend her.

Where is this culture of mauling children coming from?? Just the other day haters were making fun of Robert Alai’s daughter.

Celebrity couple, Diamond and Zari, also experience oppression by the coldhearted internet community. And this time the hate was on Tiffah.

The internet called the young one ugly and Zari lost her cool to fire back at critics with the wrath of a woman who knows the pain of giving birth.

Only a person with no womanhood in them would call an innocent child UGLY. Blessed be all mothers out there and all the UGLY babies out there. Bless the UGLY hearts too that one day, they will get to feel the love, joy, laughter, pure love and so much more that these UGLY babies bring into someone's life. Now let all God's/Allah's people say...” Wrote Zari.

The Ugandan went on to remind detractors hate was what had made her strong telling them her baby shall be President.

Matusi from day one even before she was born. But she is here and strong enough to handle. Boss ladies use bricks thrown at them to build empires. And this right here is my future president in the making #IronLady #EllenJohnsonSirleaf #Kichuna @princess_tiffah



Waziri Mkuu Atoa ONYO Kali Kwa Madaktari Wanaotoa Mimba Wanawake.....Aapa Kuwafukuza Kazi Na Kuwafunga Jela

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo  atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.

Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.

"Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.

Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.

Rais Wa Marekani, Barack Obama Amwaga Machozi Hadharani

$
0
0


Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani ili kupunguza idadi ya watu wanaoshambuliwa na kuuawa kwa Risasi nchini humo.

Obama aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayoyatete  ni kwa manufaa yao wenyewe kwa kuwa yeye huu ni mwaka wake wa mwisho kukaa madarakani na wala hana mpango wa kugombea.

Rais Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwapekua na kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha.Kwa sasa, takwa hilo hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa.

Wauza silaha ambao hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wateja wao iwapo wamewahi kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya kiakili.

Hatua hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani.

Maskini Wastara! Majanga Yazidi Kumwandama...Nyumba zake Mbili kuvunjwa na Bomoa Bomoa...Apata Mshituko Mkubwa

$
0
0
Muigizaji wa filamu, Wastara Juma amejikuta katika wakati mgumu tena baada ya nyumba zake mbili kupitishiwa X kwaajili ya kubomolewa siku zijazo.

Katika ukurasa wake wake wa Facebook, Wastara ameandika:

Mashabiki wangu mwaka umeanza vibaya kwangu nyumba zangu mbili zimewekwa X na zitabomolewa siku yoyote kuanzia leo,siko sawa kabisa niombeeni dua presha imepanda,nawapenda sana

Akiongea na Bongo5, ndugu wa Wastara amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa hali ya muigizaji huyo si nzuri kutokana na mshtuko alioupata.

“Kweli Wastara hali yake sio nzuri amepata mshtuko baada ya watu wa mazingira kuweka X katika nyumba zake mbili,” alisema dada huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam uku akidai Wastara hawezi kuongea na simu.

TANESCO Yakanusha Kuuza Asilimia 49 ya Hisa Zake

$
0
0
Tunakanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Citizen la Januari 5, 2016 katika ukurasa wake wa 12 yenye kichwa cha habari: 
‘Umma kununua asilimia 49 ya hisa za Tanesco’. Mwandishi na Mhariri wamejiandikia taarifa hiyo kwa sababu wanazozijua wao.

Sehemu ya taarifa inasema: Serikali ya Tanzania ina mpango wa kuuza hisa ya Shirika la Umeme Tanzania kwa umma...

Pia, sehemu nyingine inasema: Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo aliliambia gazeti la East African kuwa Serikali itatoa asilimia 49 ya hisa za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati huo Serikali ikibaki na hisa zingine...

Tungependa wananchi kwa ujumla waelewe kwamba taarifa hiyo si sahihi na inapotosha umma. Taarifa sahihi kama ifuatavyo:
Kwanza, Waziri Sospeter Muhongo hajafanya mahojiano yoyote na mwandishi wa gazeti hilo la The East African wala gazeti la The Citizen.
Pili, Serikali haina mpango wa kuuza hisa za TANESCO kwa umma.
Mkakati uliopo wa Mageuzi ya kuboresha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ujulikanao kama Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025 ni kama ifuatavyo:

MAELEZO YA MKAKATI NA MWELEKEO WA KUREKEBISHA SEKTA NDOGO YA UMEME (ESI-RSR)
Mwezi Juni 2014, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha na kuchapisha mkakati wa mageuzi wa Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025.

Lengo la msingi wa mkakati huo ni kuboresha mazingira ya uwekezaji wa sekta binafsi katika nyanja za uzalishaji na usambazaji, na kuongeza uunganishaji wa umeme katika ngazi zote.

Utekelezaji wa mpango huo ambao unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka kumi na moja (11) umegawanyika katika vipindi vikuu vitatu ambavyo ni muda mfupi, wa kati na muda mrefu.

=>Mkakati wa muda mfupi ni kutenganisha shughuli za Uzalishaji ili zifanywe na Kampuni Tanzu ya TANESCO.

Umiliki wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji chini ya awamu hii itaendelea kuwa chini ya Serikali, kama mbia moja.


  • Mkakati wa muda wa kati unahusu kutenganisha sehemu ya usambazaji kutoka kwenye usafirishaji. Katika Awamu hii,Kampuni za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji zitaendelea kuwa chini ya umiliki wa Serikali.



  • Mkakati wa muda mrefu utahusishaOfisi za Kanda kujihusisha na usambazaji wa huduma za umeme ambazo pia zitagawanywa kulingana na uwezo wa kujiendesha. 


Katika kipindi hicho cha muda mrefu, kampuni binafsi za usambazaji umeme zitaendelea kushiriki katika shughuli za uzalishaji na usambazaji umeme kwa ajili ya kuchochea ushindani na ufanisi kwenye soko.

Tunawahimiza wadau wote kusoma mkakati wa mageuzi ujulikanao kama Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025 ambao unapatikana mitandaoni

Aidha, tunawakumbusha Waandishi wa Habari na Wahariri ambao hawazingatii maadili ya taaluma yao kuandika taarifa sahihi ili kuepusha upotoshaji kwa umma.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
6 Juni, 2015

Tatizo la Ali Kiba Kufanya Interviews Huku Kichwani Akimuwazia Diamond Platnumz..

$
0
0
Kama alivyopata kusema Msanii Ben Paul kuwa Kiba anakuwa overrated halafu inamgharimu sana.

Uwezo na upeo wa msanii yeyote utaupima pia katika mahojiano mbalimbali na media,huwezi kudanganya umma na kuukimbia ukweli.

Nimeangalia interviews kadhaa za Ali Kiba na kugundua kuwa hajiamini badala yake zinakuwa zimejaa,mapozi,tambo,dharau,mashauzi na mambo ya ajabu ajabu.

Nimegundua kuwa tatizo kubwa la Kiba ni kufanya interviews huku kichwani akimuwazia Diamond na mafanikio yake kwa ujumla kwenye mziki na kijamii,pia fans wake ambao ameshindwa kuwapa kile wanachotaka.

Kitendo cha kusema Diamond na Davido walifanya collabo yao back stage,tuzo za Nigeria zinanunuliwa,mimi mkubwa zaidi ya tuzo na vitu kama hivyo vinaonesha uwezo wa Kiba kufikiria ni zero na anaonesha chuki za wazi kwa Diamond.

Fans wa Alikiba mkiongozwa na mademu wa Mond aliowakazaga zamani (Wema na Jokate) acheni kumpeleka puta msanii wenu mpaka mnamchanganya,don't overrate him.

Ali Kiba kama anavyodai kuwa alipumzika mziki kabla ya kurudi tena zile ni fiksi tu,wanaomjua wanamchora maana kapigana sana kwa kutoa nyimbo hapo kati ila hazikuweza kuhit kabisa(Ushahidi upo). Ashukuru kwa hapo alipofikia na akae na wasanii wenzake wafanye muziki mzuri.

Ali Kiba anawaza tu kwamba wasanii wengine hawapaswi kupigiwa kura isipokuwa yeye.Ndio maana tuzo za Bongo za visasi akibebwa anakenua,kimataifa ambako fan base yake hakuna anaishia kulalamika kufanyiwa figisufigisu na kujidai yeye mkubwa zaidi ya tuzo.

Kiba Badilika baba, huu muziki umechange hizi sio zama za Cindellera.

Tizama majigambo haya...

Meli ya MV Serengeti Majanga Matupu....Abiria 269 Wanusurika Kifo Ziwa Victoria...

$
0
0
ABIRIA 269 waliokuwa wakisafiri kutoka Mwanza kuelekea wilayani Bukoba, wamenusurika kufa baada ya meli ya Mv Serengeti waliokuwa wakisafiria kupata hitilafu ya injini katika ziwa Victoria.

Meli ya Mv Serengeti ambayo muda sio mrefu ilitoka katika matengenezo, katikati ya mwaka jana ilipata hitilafu kama hiyo ikiwa ziwa Victoria na abiria kitendo ambacho kinaelezwa kuwapa wasiwasi watumiaji wa chombo hicho.

Meli hiyo iliyokuwa na abiria 269, tani 64 za mizigo pamoja na gari ndogo, ilipata hitilafu kwenye mfumo wa shafti na majembe ya upande wa kulia (Starboard side) ambayo  yalisababisha meli hiyo kuchelewa kutia nanga katika Bandari ya Bukoba.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini hapa, Kaimu Meneja wa Kampuni ya Usafirishaji Majini, Kapteni Winton Mwassa, amesema meli hiyo iliondoka juzi  kutoka Mwanza saa 12 : 40 jioni na kutia nanga jana saa 6: 05 mchana na kwamba  ilipata hitalafu majira ya saa 6:20 usiku.

Amesema kuwa mpaka sasa chanzo cha meli hiyo kuchelewa kutia nanga bado hakijafahamika na kwamba walipata taarifa kutoka kwa Nahodha wa Meli hiyo, Bembele Ng’wita kwamba mfumo wa shafti na majembe ya kulia ya upande wa kulia yamepata hitilafu.

“Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba saa 6:20 usiku mfumo huo ulipata hitilafu iliyopelekea injini kuwa nzito na kusababisha meli kutetemeka na joto la injini kupanda na kupelekea injini hiyo kuzimwa kwa usalama zaidi,” amesema Mwassa.

Hata hivyo amesema baada ya hali hiyo meli iliiendelea na safari yake kwa kutumia injini moja na kwamba imewasili salama katika Bandari ya Bukoba saa 6: 05, abiria wote na mali zao wapo salama.

Amesema baada ya kupata taarifa hizo, kampuni imemtuma mpiga mbizi (Diver) kwa usafiri wa ndege ili akakague mfumo huo na kuweza kubaini tatizo na chanzo cha kusababisha hitilafu hiyo na kwamba kwa mujibu wa Nahodha huenda meli ilinasa katika nyavu za wavuvi.

Mwassa aliwataka watanzania kutokuwa na wasiwasi na usafiri huo na kuwataka kuondoa zana potofu kwamba watumishi wa meli hiyo wanauhujumu usafiri wa meli zinazomilikiwa na Serikali kitendo ambacho alikikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha, alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana ofisini kwake na kwamba yupo nje ya ofisi.

TRA Yawajibu BAKWATA Waliodai Wakatoliki Wanapendelewa Kupewa Misamaha

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa na upotoshwaji kuhusu zoezi la ufuatiliaji wa matumizi ya misamaha ya kodi inayosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa wafanyabiashara, wawekezaji, Taasisi za Dini na Taasisi zisizo za kiserikali kwa maelezo kwamba TRA inazilenga baadhi ya Taasisi.

Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania inaipa Mamlaka ya kusimamia, kukagua na kuhakiki mapato ya Serikali pamoja na kuzuia ukwepaji wa kodi wa aina yoyote ile ikiwemo matumizi mabaya ya misamaha ya kodi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria.

Kifungu cha 5 (3) cha Sheria ya TRA kinatoa mamlaka kwa TRA kufanya jambo lolote lenye tija na manufaa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake kisheria.

Kwa vile misamaha ya kodi inatolewa kwa mujibu wa Sheria zinazosimamiwa na TRA, ni wajibu wa Mamlaka kuhakiki kama bidhaa au huduma zilizosamehewa zinatumiwa na watu au Taasisi zinazostahiki misamaha hiyo au kwa miradi iliyokusudiwa.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za upotoshaji kwamba TRA imeilenga Taasisi moja ya kidini kwa kuiandikia barua ya kuomba vielelezo na ufafanuzi juu ya misamaha ya magari iliyopewa awali na kuonekana kana kwamba ni utaratibu mpya wa utoaji wa misamaha.

Tungependa kufafanua kwamba TRA haibagui wala kulenga Taasisi yoyote bali inatekeleza wajibu wake wa kufuatilia misamaha iliyotolewa

Katika kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Desemba 2015 TRA iliwaandikia walipakodi 65 kupata vielelezo juu ya matumizi ya misamaha ya kodi walioipata na katika hao zimo Taasisi za kidini 39.

Ukaguzi huu huisadia TRA kupata taarifa muhimu ili kuishauri Serikali namna bora ya kutoa misamaha kwa ajili ya kuleta tija na ufanisi uliokusudiwa ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za jamii na kupunguza umaskini.

Aidha taarifa za misamaha ya kodi zinaisadia TRA kubaini matumizi bora ya misamaha pamoja na mianya ya upotevu wa mapato kupitia misamaha hiyo ili TRA ichukue hatua zinazostahili pale inapobainika kuwa kuna ukwepaji na kuziba mianya hiyo.

Zoezi hili ni endelevu hivyo tunaziomba Taasisi zote za kidini na mashirika yote yanayonufaika na misamaha ya kodi kuchukulia zoezi la ukaguzi wa misamaha hiyo kuwa ni utekelezaji wa sheria na wahusika wote watoe ushirikiano kwa TRA pale wanapohitajika ili zoezi hilo lifanyike kwa ufasaha na kwa manufaa kwa wote.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

A. J. Kidata
KAIMU KAMISHNA MKUU.

BREKING NEWS:Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Kauli Kuhusu Viwango Vipya vya Nauli..Adai Serekali Haikubaliani Navyo

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).

Akizungumza* leo na waandishi* wa habari, mara baada ya kuwasili katika* Uwanja wa Ndege wa Kimataifa* wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema* Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi.

Ambapo nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli.

Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na watumishi, mradi ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya jiji,*“Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao hawana vipato vikubwa”*alisema Waziri Mkuu.

Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia* Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene* na* Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane* kupanga upya* viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali* itaendesha mradi huo.

********

Tarehe* 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa* mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu* ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika kwamba* UDART hawakuandaa mpango wa biashara* wala kuanisha gharama za uendeshaji.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,2 MTAA WA MAGOGONI,

S. L. P 3021,11410 DAR ES SALAAM

JUMATANO, JANUARI 6, 2016

TRA Yavuka Lengo .......Yakusanya Trilioni 1.4 Kwa Mwezi

$
0
0
Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa inakusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.

Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.

Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.

Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8n zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao

Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Dar es Salaam
6.1.2016

Picha Hii ya Diamond na Mtoto wake Tiffah Yawa Gumzo

$
0
0
Picha hii ya mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz akiwa amem-kiss mtoto wake Tiffah yazua mjadala kwenye mtandao wa instagram.


Zari the Boss Lady ‘Mama Tiffah’ ndiye aliyeiweka picha hiikwenye ukurasa wake mtandaoni humo na kuandika “Simply adorable

Picha ambayo baadhi ya mashabiki walionyeshwa kutopendezewa nayo kwa madai kuwa kiss hilo limevuka mipaka na haipendezi kuwekwa mtandaoni huku wengine wakionekana kuona ipo sawa na inaonyesha ni kwajinsi gani Diamond anavyompenda motto wake Tiffah ‘Dangote’.

Wewe unaionaje hii?
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images