Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104705 articles
Browse latest View live

"Mimi Ndiye Rais Halali wa Zanzibar na Nisiposema Mimi Nitawatuma Wasaidizi Wangu Kuwaeleza" - Dk Shein

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye bado ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kutoa changamoto kwa wasioiamini Katiba hiyo kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ya Zanzibar ambayo ndiyo pekee yenye uwezo wa kutafsiri Katiba.

Amebainisha kuwa yeye anaongoza nchi kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwamba kama si uwezo huo aliopewa Kikatiba hana sababu ya kuendelea kukaa madarakani pamoja na serikali anayoingoza.

“Tuko madarakani na uongozi wote wa serikali… yupo Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamu wa Pili wa Rais na mawaziri” alisisitiza Dk. Shein na kuongeza kuwa hao wanaodai kujiondoa serikalini huo ni uamuzi wao wenyewe.

Alibainisha kuwa yeye na serikali anayoingoza kuendelea kuwepo madarakani “si uamuzi wake” na wala yeye hana “ubavu” wa kujiweka madarakani bali ni Katiba ambayo inajieleza wazi.

Dk. Shein ametoa kauli hiyo jana kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu kisiwani humu kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi.

Aliwaambia wananchi hao kuwa yako mengi yanayosemwa lakini hawapaswi kuyasikiliza kwa kuwa kama ni serikali yeye ndiye Rais hivyo wanapaswa kumuamini anachowaeleza.

“Ya mjini yapo yasikilizeni lakini kwa Serikali mimi ndiye Rais na nisiposema mimi nitawatuma wasaidizi wangu kuwaeleza” Dk. Shein alibaisha na kuongeza kuwa ya vyama kila mtu ana chama chake.

Alifafanua kuwa kama ni suala la Chama cha Mapinduzi (CCM) yeye ndiye Makamu Mwenyekiti Zanzibar na kama kuna la kuwaeleza wana CCM na wananchi atawaeleza yeye na viongozi wenzake wa chama hicho pamoja na taarifa za vikao vya chama vyake.

Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa ushindani wa kisiasa si ugomvi bali ni utaratibu wa kupeana changamoto katika uongozi ambao lengo ni kuwaletea wananchi maendeleo.

“tusikejeli maendeleo yetu, tuthamini chetu na ushindani wetu wa kisiasa usirejeshe nyuma maendeleo yetu” Dk. Shein alitahadharisha.

Dk. Shein aliruejea wito wake wa kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yameanza tarehe 3 Januari na yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 12 Januari, 2016 katika kiwanja cha Amaan.

Aliwakumbusha wananchi hao kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yaliyomfanya Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume kutangaza Jamhuri ya Zanzibar, ndiyo yaliyowakomboa wanyonge wa Visiwa vya Zanzibar kwa kuondosha aina zote za ubaguzi na kuwapa mamlaka ya kujiamulia mambo yao.

Dk. Shein aliwaeleza wananchi wa Pemba kuwa meli mpya iliyonunuliwa na Serikali MV Mapinduzi II ambayo ilizinduliwa hivi karibuni, itawasili kisiwani humo tarehe 10 Janauri na siku itakayofuata itawachukua baadhi ya wananchi kwenda Unguja kushiriki maaadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi.

Alisisitiza kuwa serikali itawalipia gharama za usafiri wa kwenda na kurudi Unguja wale wote watakaoteuliwa kuwemo kwenye safari hiyo kufuatana na utaratibu utakaowekwa kama alivyokuwa ameahidi wakati meli hiyo ilipokuwa inatengenezwa nchini Korea ya Kusini.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais amefuatana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na wabunge.

Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822
E-mail:saidameir@ikuluzanzibar.go.tz& sjka1960@hotmail.com

Jumuiya Za Kiislamu Zanzibar Zapinga Uchaguzi Kurudiwa......Zamlilia Rais Magufuli Aokoe Jahazi

$
0
0

TAMKO LA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR (JUMAZA) KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MGOGORO WA KISIASA ZANZIBAR TAREHE 6-1-2016 KATIKA UKUMBI WA UMOJA WA WALEMAVU


Awali tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana katika hafla hii hali ya kuwa ni wazima; sala na salamu zimfikie Mtume wetu Mtukufu Muhammad (S.A.W), jamaa zake, maswahaba zake na wote wanaowafuata kwa wema hadi Siku ya Malipo.

Ndugu waandishi wa habari, tunawashukuru sana kwa kuitikia wito wetu wa kuhudhuria katika mkutano huu muhimu wenye lengo la kutafuta maslahi na mustakbali mwema wa nchi yetu.

Sisi Viongozi wa Dini ya Kiislamu Zanzibar tunawashukuru sana Wazanzibari wote kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu katika nchi yetu pamoja na kukabiliwa na mtafaruku mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya Zanzibar uliotokana na hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha kuufuta Uchaguzi wote uliofanyika tarehe 25 Octoba, 2015 na matokeo yake katika tangazo lake la tarehe 28-10-2015.

Kitendo hicho cha kuufuta Uchaguzi huo, kimepelekea nchi yetu kuingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisiasa. Wananchi wa kawaida ambao ndio wapiga kura wanaathirika kisaikolojia kwa kushindwa kujua khatima ya kura walizozipiga. 

Kwa upande mwengine kumekuwa na ongezeko la ugumu wa maisha visiwani Zanzibar unaotokana na mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu na mzunguuko wa pesa kuwa mdogo kutokana na baadhi ya Wafanya biashara kuwa na khofu ya kuendelea na shughuli za uzalishaji kwa khofu ya kutokea vurugu.

Ndugu waandishi wa habari, sisi tukiwa viongozi wa jamii tumeshughulishwa sana na mtafaruku huu wa kisiasa unaotukabili ambapo hadi sasa tumechukua hatua zifuatazo kusaidia kufikia ufumbuzi:-
 
Tuliwaandikia barua za nasaha viongozi wote wakuu wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo huu wa kisiasa.
  1. Tuliwaandikia barua Mabalozi wa nchi sita waliopo Tanzania kuomba wasaidie katika kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu katika kuhakikisha kuwa demokrasia inachukua mkondo wake. Mabalozi wahusika ni kutoka nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Norway na Sweeden.
  2. Tulimwandikia barua Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kumkumbusha dhima yake ya kuingilia kati mgogoro huu ili kupatikana ufumbuzi wa haraka.
  3. Kupitia khutuba za Ijumaa katika misikiti mbali tumekuwa tukiwanasihi wananchi wawe na subra ili watoe fursa kwa viongozi wa kisiasa kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu kwa njia za amani.
Ndugu waandishi wa habari, 
Wananchi wa Zanzibar tulipata matumaini tulipoona kuwa viongozi wakuu wa kisiasa wanakutana kuzungumzia hali ya kisiasa nchini, tuliamini kuwa katika vikao hivyo Viongozi hawa wenye kuheshimika wakitawaliwa na busara, hekima, uadilifu na wakiweka mbele maslahi ya taifa badala ya vyama vyao basi muda si mrefu tungepata ufumbuzi wa mgogoro huu. 

Bahati mbaya tunaambiwa ni vikao 8 sasa vimeshafanyika tokea kikao cha mwanzo cha tarehe 9 Novemba, 2015 hakuonekani kuwa matumanini yale wananchi waliyoyajenga kwao kuwa yatatimia.

Tunasema hivi kwa sababu kwanza vinaendeshwa kwa usiri mkubwa mno na hadi leo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa umma.

Hali hii inawafanya wananchi kutoelewa kinachoendelea na hivyo kuishi maisha ya wasi wasi na kukosa utulivu hata wa kufanya shughuli zao za kimaisha. Kasoro nyengine ni kuwa vikao hivi vimechukua muda mrefu sana na hivyo kuibua maswali mengi na shaka kwa wananchi. 

Pia tabia iliyojitokeza ya baadhi ya wajumbe wanaoshiriki mazungumzo hayo kutoa kauli zinazoshabikia msimamo wa upande mmoja kunawatoa imani wananchi juu ya kuwepo kwa nia njema katika mazungumzo hayo na kwamba mazungumzo hayo yanaweza kuivusha nchi yetu katika mkwamo huu wa kisiasa unaohatarisha usalama wa nchi yetu.

Kutokana hali hii sisi Viongozi wa Dini ya Kiislam Zanzibar tunatamka kwamba:-
  1. JUMAZA na Taasisi za Kiislam Zanzibar zinawataka Viongozi wakuu wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo kuwajibika kwa kuweka mbele maslahi mapana ya nchi, kuhitimisha mazungumzo yao haraka iwezekanavyo na kutoa maamuzi rasmi ikiwa ni muongozo wa kutukwamua hapa tulipo kwa njia ya amani na salama. Tunawatanabahisha kuwa jamii yetu kwa sasa ni mfano wa bomu linaloweza kuripuka wakati wowote ule.
  2. Ukimya na uvumilivu wa Wazanzibari uliopo kamwe usichukuliwe kuwa wao ni Malaika bali ni binaadamu kama walivyo wengine ambao wanaweza kufikia hatua ya kushindwa na uvumilivu na kutoa maamuzi magumu yanayoweza kutufikisha pahala pabaya na kuigharimu sana nchi yetu. Hatuombi jambo hili kutokea lakini likitokea viongozi wakuu wa kisiasa watabeba dhima mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hivyo basi, tunawaomba Viongozi wakuu wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi, ni wakati muwafaka sasa watoke hadharani na watoe taarifa kwa umma juu ya hatua iliyofikiwa na ikiwezekana lini mazungumzo hayo yatakamilika na Wazanzibari watarajie nini kutokana na mazungumzo hayo.
  3. Sisi Viongozi wa Dini ya Kiislam Zanzibar, tunapinga kwa nguvu zetu zote kauli za uchochezi zinazoendelea kutolewa na wanasisa ambazo zinazidi kujenga khofu, hamasa na chuki miongoni mwa wananchi. Aidha, tunasikitika kuona kuwa kauli hizo zinatolewa bila ya kujali mazungumzo yanayoendelea ya viongozi wakuu ya kutafuta ufumbuzi.
  4. Sisi Viongozi wa Dini ya Kiislam Zanzibar, kwa heshima kubwatunamuomba sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. John Pombe Magufuli ambaye ameonesha dalili njema za uadilifu na uwajibikaji mkubwa achukue hatua za wazi na za haraka katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu kabla nchi yetu haijatumbukia pahala pabaya. Aidha, tunamuomba kusimamia kwa udhati na ujasiri kuona haki inachukua mkondo wake na maamuzi ya Wazanzibari walio wengi yanaheshimiwa.
  5. Katika Uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 JUMAZA ilikuwa na waangalizi katika majimbo yote ya Unguja na Pemba, kasoro zilizoripotiwa katika Uchaguzi huu ni kasoro ndogo ndogo mno na kwa hakika ni afadhali kuliko chaguzi zote zilizopita huko nyuma tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vyangi. JUMAZA inashangazwa sana na hatua ya kufuta Uchaguzi huu iliyochukuliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salim Jecha. JUMAZA inauliza kwanini wakati tulipokuwa na kasoro kubwa zaidi katika chaguzi za mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 Uchaguzi haukufutwa na kutakiwa kurejewa tena iwe Uchaguzi wa mwaka 2015 tu? Na jee kama uchaguzi utakaorejewa nao ukawa na kasoro zitakazolalamikiwa, utafutwa tena? Tutafanya chaguzi ngapi kwa mtindo huu?
  6. Taasisi za Kiislam Zanzibar zinawaomba Waislamu wote kuendeleza dua ili kuitakia mema nchi yetu na kumkabidhi Mwenyezi Mungu kwa wale wote wanaokusudia shari. Aidha, zinawaomba Maimamu na Makhatibu kukemea kauli zinazohatarisha amani na mshikamano wa jamii.
  7. JUMAZA na Taasisi za Kiislam Zanzibar zina khofu kubwa juu ya kurejewa kwa Uchaguzi, uzoefu unaonesha kuwa nchi zilizorejea uchaguzi katika Bara la Afrika kama vile Nigeria, Zimbwabwe, Malawi na kwengineko hatimaye zilitumbikia katika machafuko makubwa. Kama hilo halitoshi Zanzibar tuna historia mbaya ya kurejea Uchaguzi. Wengi tunakumbuka katika historia ya Zanzibar kile kinachoitwa ‘vita au machafuko ya Juni ‘. Uchaguzi wa Januari mwaka 1961 ulilazimika kurejewa mwezi wa Juni 1961, ambapo ulipelekea machafuko makubwa ikiwemo vifo vya watu 68, maelfu kujeruhiwa, nyumba kuvunjwa na kuchomwa moto. Kwa historia hii JUMAZA na Taasisi za Kiislam Zanzibar hazioni kuwa ni busara kurejewa kwa Uchaguzi uliofanyika kwa ufanisi na kukamilika. Penye nia njema na utashi wa kisiasa basi njia ya uadilifu iliyo wazi ya kutukwamua hapa tulipo ni kwa Viongozi wakuu wa kisiasa kufikia ufumbuzi na makubaliano haraka iwezekanavyo.
Mola wetu Mtukufu tunakuomba kwa rehma zako utuwezeshe kufikia ufumbuzi unaofaa juu ya tatizo linalotukabili na uziunganishe nyoyo za Wazanzibari kuwa pamoja, kupendana na kuweka mbele maslahi ya nchi yao. Amiin.

AHSANTENI
………………………………..
MUHIDDIN Z. MUHIDDIN
KATIBU MTENDAJI
JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Januari 7, Ikiwemo ya Zari Kumwambia Wema Amkome Diamond

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Januari 7, Ikiwemo ya Zari Kumwambia Wema Amkome Diamond

Mnyama Simba Avamia Kijiji cha Sitalike Tarafa ya Nsimbo Wilayani Mlele Katavi na Kuua Wawili

$
0
0
Mnyama Simba amevamia Kijiji cha Sitalike Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na kuuwa watu wawili.

Waliouawa ni baba na mtoto wake ambapo simba huyo kula mtoto na kuacha kichwa huku akinyonya damu ya mzazi hadi kupoteza maisha.

Tukio la Simba huyo kuua watu wawili limetokea jana majira ya saa kumi na moja alfajiri katika Kijiji hicho cha Sitalike .

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher Anjelo aliwaambia waandishi wa habari waliouawa kuwa ni John Jeremia (45) na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka mitano .

Alisema siku ya tukio wanafamilia hao walikuwa wamelala ndani ya nyumba yao ndipo simba huyo jike alipovamia na kuingia ndani ya nyumba hiyo .

Alieleza baada ya Simba huyo kuingia ndani alimvamia baba wa mtoto huyo na kuanza kumnyonya damu hadi alipohakikisha amefariki dunia ndipo alipomwachia marehemu huyo.

Mwenyekiti huyo wa Kijiji alisema simba huyo baada ya kuona John Jeremia amemnyonya damu hadi kufa alihamia kwa mtoto wake na marehemu na kuanza kumshambulia na kisha alianza kumtafuna na kubakiza kichwa tuna kwenda nacho hadi kwenye kichaka kilichokuwa jirani na nyumba ya marehemu hao.

Alisema taarifa za simba kuua watu hao zilifika kwenye uongozi wa Kijiji hicho ambao nao walitoa taarifa kwa askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambapo walianza kufanya msako wa kumsaka simba huyo kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Sitalike.

Wakati wakifanya msako waliona nyayo za simba na walizifuata kule zilipoelekea na walipofika kwenye kichaka walimuona simba huyo akiwa amekaa na pembeni yake kukiwa na kichwa cha mtoto .

Mwenyekiti wa Kijiji alisema askari wa Hifadhi ya Katavi walimfyatulia simba huyo risasi lakini aliweza kuikwepa na kusogea mbele zaidi .

Hata hivyo waliendelea kumfuata kwa kushirikiana na wananchi ndipo Askari wa TANAPA walipofanikiwa kupiga risasi na kufa hapo hapo.

Alieleza baada ya Simba huyo kuwa ameuawa kwa kupigwa risasi baadhi ya wananchi waliomba wamchukue kama kitoweo cha mboga lakini askari wa TANAPA waliwakatalia na walimchukua simba huyo aliyekuwa amekufa na kwenda nae kwenye hifadhi yao kwa kile walichoeleza kuwa wanakwenda kumchoma moto kwa kutumia mafuta ya petroli.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kuuawa kwa watu hao na Simba huyo aliyetokea kwenye Hifadhi ya mbuga ya Katavi .

Alisema ameisha peleka askari wake kwenda kuangalia eneo la tukio hilo na ametoa wito kwa wananchi kuacha kujenga makazi karibu na hifadhi ya Katavi.

Kutokana na Malumbano Yao Mitandaoni, Mzee Yusuf Asema Haya Kwa Wake Zake

$
0
0
Jana ilikuwa siku ya kuzaliwa Mzee Yusuf,kumekuwa na malumbano ya mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kati ya wake zake wawili Leila na Chiku,Mzee Yusuf amesema hafurahishi na malumbano hayo…

‘’Sio vitu vizuri sifurahii huwa najaribu kuwaaambia sijui hawa wake zangu wananionaje ,pengine hawajui kuwa mimi ni mume wao hawanipi heshima yangu na hasa huyo anayetaka kufanya mambo ya vituko,binafsi sipendi na huwa sifurahii na najaribu kuwaasa tena kwenye Instagram huwa nawaambia waangalie hao mashabiki wao ‘maandazi’ lakini sasa unakuta mtu mwenyewe anapenda mambo hayo sasa itafika siku nitakuja kufanya kitu na asije mtu akalalamika,’’alisema Mzee Yusuf.


Mama Diamond Akubali Kushindwa...Sasa kurudi Kuishi Tandale Kumpisha Zari Madale

$
0
0
KUNA madai kwamba, mama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim ‘Sandra’ yupo katika maandalizi ya kuhamia kwenye makazi ya Tandale alikokuwa akiishi zamani ili kumpisha mwanye na mama mtoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah kwenye makazi ya Madale jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama huyo au bibi Tiffah amefikia uamuzi huo ili kuepusha lolote linaloweza kutokea kwa kukaa beneti na mkaza mwanaye kwa vile ulimi hauna mfupa wala macho hayana pazia.

Jamani mnajua kama mama Diamond anataka kurudi kuishi Tandale alikotoka. Anampisha Zari na Diamond wake watanue kwenye mjengo wa Madale. Si unajua wamemzaa Lattifah ‘Tiffah’, ndiyo maana yule mama hivi karibuni kwenye moja ya magazeti yenu (Risasi Jumamosi) mlitoa habari na picha akisimamia ukarabati wa ile nyumba ya Tandale,” kilisema chanzo.

Asichotaka yule mama ni kuzozana na mkaza mwanaye. Unajua yeye ni mtu mzima, sasa kupishanapishana Kiswahili na binti kama Zari si sawasawa.”
Amani lilimtafuta msemaji wa familia hiyo ambaye ni Diamond mwenyewe na kuulizwa kuhusu madai hayo, alisema:

Hamna kaka. Ile nyumba ni ya familia. Nimeamua kuikarabati kwa sababu ni ya familia. Mimi nina mama, nina dada zangu, isingekuwa rahisi nianze kuikarabati nyumba ya Tandale ambayo ni ya wote. Ndiyo maana nilianza kujenga yangu kwanza kisha ya familia. Hata mama akienda kuishi kule kwani tatizo liko wapi? Si nyumba yetu?” alisema Diamond.

Jack Wolper Nae Akiri Kujipendekeza Kwa Mwanamuziki Diamond Platnumz na Zari

$
0
0
Jackline Wolper Katika Pozi
BAADA ya kupata wakati mgumu wa kushambuliwa na maneno kila akiweka picha mtandaoni ya Diamond ama Zari, staa wa filamu Bongo, Jacqueline Walper ‘Wolper’ ameweka wazi kwa kuwajibu, haoni tatizo kujipendekeza kwa hao watu.

Akichezesha taya na Amani, Wolper alisema kuwa, ilifika kipindi katika ukurasa wake wa Instagram watu wengi walikuwa wakimshambulia kwa maneno na kufikia hadi hatua ya kumtukana.

Kiukweli mimi ni binadamu, nashangaa ukiweka picha ya mtu ooh, anajipendekeza ni sawa najipendekeza ndiyo na wala siyo uongo lakini kuna mtu ambaye inamuhusu?” Alihoji Wolper.

Source:
Global Publishers

Udaku Special Blog

See The Names Nigerians Are Calling HUDDAH MONROE After She Shaved Her Pus..y

$
0
0

A few months ago, Huddah Monroe introduced Kenyan girls to a laser hair removal technique that easily removes hair in unwanted areas of the body permanently. Nigerians got wind of this story and started calling her Ashewo - a Nigerian reference to a prostitute.

See what Huddah posted after she saw that blog post….




Zitto Kabwe Amjibu Kubenea....Asema ni Mgonjwa wa Chuki, Muongo na Kigeugeu

$
0
0
==>Makala hii inapatika kwenye ukurasa wa Facebook wa Zitto Kabwe
MTUMISHI wa Mungu afumaniwe kwa uzinzi na mke wa mtu, kesho asubuhi aamkie madhabahuni kuhubiri neno kisha waumini wapokee. Huko ni kumtania Mungu.

Mimbari ni kwa ajili ya wasafi. Ukiwa mchafu hufai kuhubiri neno. Maneno ya Mungu hayashereheshwi na mwenye uchafu. Maana mtu mchafu ni mtenda dhambi.

Mwandishi wa Habari na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, anataka kuhubiri neno. Waumini tunakataa. Maana asiye msafi hafai kuaminika kwa maneno yake.

Mhubiri neno hatakiwi kuwa ndumilakuwili. Hapaswi kuwa kigeugeu wala mshadadia uongo. Anatakiwa awe mkweli na siku zote aweze kuuishi ukweli wake.

Kubenea hana aibu kama Sepp Blatter, yule aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Kwamba pamoja na vielelezo vyote vya uharamia wake bado aling’ang’ania yeye ni msafi na akataka kuendelea kuongoza shirikisho hilo.

Kubenea ana roho ngumu kama Michel Platini, yule alikuwa Rais wa Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa). Kwamba pamoja na kila ushahidi kudhihirisha umafia wake wa kimtandao kwenye soka, bado alisimama imara kudai anaonewa.

Mwisho kabisa, Blatter na Platini, wamefungiwa na Kamati ya Maadili ya Fifa, kujihusisha na shughuli zote za soka kwa kipindi cha miaka nane.

Kubenea ni mwanaproganda asiyeuonea aibu uongo wake. Ni kama Muhammad Saeed al-Sahhaf, yule aliyekuwa waziri habari wa Iraq, wakati wa utawala wa hayati Saddam Hussein. Al-Sahhaf ndiye aliweka rekodi ya kuwa msema uongo bora mwaka 2003.

Wakati Marekani ilipoivamia Iraq mwaka 2003, Al-Sahhaf alikuwa na kazi ya kusema tu uongo kuwatisha Wamarekani. Tangu walipoanza mpaka walipouteka mji wa Baghdad, hakuna popote ambapo maneno ya Al-Sahhaf yalikuwa kweli.

Kubenea yupo vitani na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe. Anamshambulia mfululizo. Amejaliwa kumiliki magazeti, basi kwa vile mwenzake hana, ndiyo kila siku anaye tu!

Unaweza kutafuta mahali ambako Zitto na Kubenea waliwahi kugombana, huwezi kupaona. Zaidi, zipo taarifa kuwa Zitto amewahi kuwa msaada kwa Kubenea katika kazi zake.

Kwa nini kila siku Kubenea juu ya Zitto? Huwa anamtafuta nini? Kama kungekuwa na utofauti wa kijinsia kati yao, pengine ipo hoja ingezungumzwa. Ila kwa nidhamu kabisa lipo swali; Ya nini kila siku mwanaume juu ya mwanaume mwenzako? Unamfuatafuata wa nini? Kipi unakitafuta?

Upo msululu wa makala za Kubenea dhidi ya Zitto. Kwa Kubenea, Zitto hajawahi kuwa na jema kwake tangu mwaka 2009. Ni ajabu kuwa katika kipindi chote hicho Zitto hajawahi kujishughulisha kumjibu.

Hiyo inatoa picha moja kubwa kwamba Kubenea ni mwathirika wa maisha ya Zitto. Maana kuchukia kila kitu cha mtu ni ugonjwa. Kwani chochote atakachokifanya kitakupa majeraha.

Hata mwandishi mashuhuri, Marty Rubin aliwahi kusema: “To hate everything is to be wounded by everything.”

Kiswahili: Kuchukia kila kitu ni kujeruhiwa na kila kitu.

Tangu mwaka 2009, vipo vipindi vingi vya ushindi kwa Zitto. Katika maisha yake kisiasa jukwaani, jimboni na bungeni. Fikiria Kubenea ameumia kiasi gani katika kipindi chote hicho ambacho Zitto amekuwa akifanya vizuri.

Katika Uchaguzi Mkuu 2015, Kubenea aliandika makala kuwa Zitto hatashinda ubunge, matokeo yake asiyempenda alishinda. Hayo ni maumivu kiasi gani kwake?

Zitto alishinda na kurejea bungeni mwaka 2010, akashinda uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (Poac). Kubenea aliandika kuwa Zitto alisaidiwa na Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete. Aliumizwa na ushindi huo!

Mwaka 2012 Zitto alionesha utaalam wake wa siasa za ndani ya bunge, pale wabunge walipopaza sauti kutaka mawaziri nane wang’oke kutokana na ufisadi, vilevile kushindwa kwao kusimamia ofisi walizokabidhiwa.

Zitto akasimama, akasema wabunge wanahangaika kwa sababu hawana mamlaka ya kuwajibisha mawaziri. Ila yupo mmoja ambaye akishughulikiwa, wengine wote watawajibika. Akamtaja huyo kuwa ni waziri mkuu.

Akaanza kukusanya saini za wabunge, kutimiza 70 ili awasilishe hoja ya kumng’oa waziri mkuu. Zitto alifanikiwa kushawishi wabunge wa vyama vyote bungeni ambao walisaini. Saini zikatimia. Rais Kikwete naye akawang’oa mawaziri waliokuwa wanatakiwa kuwajibishwa na kumuokoa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Kwa kuchukua mantiki ya maneno ya Rubin, hili nalo lilikuwa shoka la kichwa kwa Kubenea kutoka kwa Zitto. Maana mafanikio ya Zitto ni pigo kwake. Anaumizwa na chuki zake. Chuki zikizidi ni ugonjwa usiotibika.

Mwaka 2012 Poac ilivunjwa na Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda. Kubenea akafurahia kwa sababu Zitto alipoteza uenyekiti wa kamati bungeni.

Makinda akaiunganisha Poac na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto akashinda uenyekiti wake, kwa mara nyingine Kubenea alinuna; “kwa nini kila siku Zitto haporomoki?”

Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2014, Zitto aliiongoza PAC kwa mafanikio, kuiwajibisha serikali kutokana na wizi mkubwa uliofanyika Benki Kuu kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Zilikuwa fedha za mgogoro kati ya Tanesco na mwekezaji, Kampuni ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL). Zikachotwa bila utaratibu. Watu waliiba.

Chini ya uongozi wa Zitto, PAC iliwezesha kuwajibika kwa aliyekuwa Mwansheria Mkuu, Fredrick Werema, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.

Kubenea aliumizwa na Zitto kutajwa kama shujaa wa kashfa ya Tegeta Escrow. Akasema Zitto hakufanya lolote kwa sababu kazi kubwa ilifanywa na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.

Kubenea anaumia sana mpaka namhurumia. Siwezi kumshauri kumpenda Zitto ila kwa ajili ya usalama wa afya yake, namshauri ajifunze kupenda vitu vizuri vinavyofanywa na watu asiowapenda.

Unaweza kuchukia watu lakini ukawa mpenda matokeo mazuri. Kwa hiyo hutaumia sana, kwani upande mmoja utachukizwa na mafanikio ya usiompenda, vilevile utachekelea matokeo bora. Kubenea ajifunze hili!

Sasa hivi Kubenea ndiyo kachangamka, kila siku makala zenye mrengo hasi dhidi ya Zitto. Inaelezwa ni mpango wa kuuendea uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC). Mimi sijui, ila ninachoona ni chuki.

Pengine Zitto hajibu kwa kutimiza maneno ya mhubiri wa Kanisa Katoliki, aliyeishi Roma Karne ya 13, Mtakatifu Thomas Aquinas aliyesema: “The principal act of courage is to endure and withstand dangers doggedly rather than to attack them.”

Kiswahili: Kitendo kikuu cha ujasiri ni kuvumilia na kuhimili hatari kwa ukimya bila kubweka kama mbwa kuliko kushambulia.

Hata hivyo, kitu cha kujiuliza ni hiki; Hivi Kubenea baada ya yote yaliyotokea, bado anataka aaminike kama mtu mkweli? Je, bado anataka kutuaminisha yeye ni mwandishi mzuri wa kuaminika anayesimamia misingi?

Je, hata baada ya kutuonesha sura zake nyingi za ufanyaji kazi? Hapana kabisa, haiwezekani!

Je, hata baada ya kuonesha kuwa yeye ni mwandishi maslahi? Miaka nane alimshambulia aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuwa ni fisadi, mchafu, asiyesafishika hata kwa dodoki.

Kisha 2015, akageuka kumpigia debe Lowassa kuwa siyo fisadi na kwamba amekuwa akionewa tu. Huyuhuyu anataka tuamini kuwa yeye ndiye mkweli, anaowashambulia ndiyo wabaya.

Kwa nini kutokana na undumilakuwili wake tusiamini yeye ndiye mnafiki na maneno yake ndiyo uongo wake unapokuwa kazini?

Ukiwa muongo huwezi kumpenda mtu mkweli. Utamchukia kwa sababu uongo na ukweli hauwezi kufungamana. Kwa mantiki hiyo ni rahisi kutambua kuwa Zitto ni msafi kwa sababu anayemshambulia ni mchafu.

Mwandishi mashuhuri wa vitabu, raia wa Uingereza, William Makepeace Thackeray, aliyeishi kwa mafanikio ya uandishi wake Karne ya 19, alisema: “An evil person is like a dirty window, it never let the light shine through.”

Kiswahili: Mtu muovu ni sawa na dirisha chafu, haliwezi kamwe kupitisha mwanga mng’aavu.

Kwa kuchambua mapito ya Kubenea, bila shaka yoyote hayupo tena kwenye misingi ya kitaaluma ya uandishi wa habari. Anachwa nje na muongozo wa somo la Usawa wa Uandishi wa Habari (Journalistic Objectivity).

Katika Journalistic Objectivity, yapo mambo manne yanayozingatiwa. Mosi; Fairness (Haki). Pili; Disinterestedness (Kutokuwa na maslahi). Tatu; Factuality (Ukweli unaothibitishika). Nne; Nonpartisanship (Kutokuwa na upande).

Kubenea ni Chadema, kwa hiyo hayupo kwenye msingi. Hakatazwi kutoa maoni lakini hapaswi kujitambulisha kama mwandishi wa habari aliye mstari wa mbele kikazi kwa sababu hawezi kutenda haki. Anao upande tayari.

Na ndiyo maana vyombo vingi vya habari viliripoti kuhusu Mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe, kufanya hamisho la mabilioni ya fedha nje ya nchi katika mazingira yenye kuashiria ama ufisadi au utakatishaji wa fedha haramu (money laundering) lakini hakuna gazeti lililo kwenye miliki ya Kubenea liliwahi kuripoti.

Zitto haelewani na Chadema, maana walimfukuza. Kubenea anapomshambulia anakuwa anakosea misingi kwa sababu yeye anao upande, kwa hiyo hawezi kumtendea haki Zitto.

Kampuni inayochapisha Gazeti la Mwanahalisi, Hali Halisi Publication, mbali na Kubenea, mkurugenzi wake mwingine ni Anthony Komu, huyu ni Mkurugenzi wa Fedha wa Chadema, yaani kwa lugha rahisi ndiye mweka hazina wa chama hicho.

Komu ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na alikuwa kwenye kikao siku kamati hiyo ilipowashughulikia Zitto, swahiba wake, Prof. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo.

Kutokana na hali hiyo, ni rahisi kushangaa Zitto akiandikwa vizuri na magazeti yaliyo chini ya miliki ya Kubenea na Komu kuliko kushambuliwa na kuchafuliwa.

Ajaze ukweli anavyoweza lakini pointi mbili kati ya nne ambazo nimezitaja kama mbeleko ya somo la Journalistic Objectivity, yaani Disinterestedness (Kutokuwa na maslahi) na Nonpartisanship (Kutokuwa na upande), zinamuondoa kwenye mstari.

Na hili linalosemwa kwamba naye anautaka uenyekiti wa PAC, sasa anamuona Zitto ni kikwazo, ndiyo anapoteza sifa kabisa.

Ni dhambi kubwa katika uandishi wa habari kuingiza vita binafsi (personal war) katika masuala ya kitaaluma.

Hata kama ingekuwa anachokiandika ni ukweli, huo ukweli unamuona Zitto upande wa ubaya tu? Na je, tangu mwaka 2009 Zitto alipochukua fomu ya kugombea uenyekiti Chadema, kushindana na Mbowe hajawahi kuwa na jema lolote la kuandikwa? Maana tangu hapo aligeuka msemwa vibaya wa Kubenea.

Kubenea akumbuke kuwa zilishapita nyakati aliaminika, baadaye ikagundulika ni kigeugeu. Ni vigumu kurudia makosa kwa kumwamini tena. Kiingereza kinanena: “It is a shame to fall twice over the same stump.” Kiswahili kinajibu: “Ni aibu kujikwaa kisiki mara mbili.” Aibu hii nani anaitaka kwa mara nyingine?

Kubenea siyo mtu wa misingi, vita binafsi huihamishia kwenye taaluma; Alikwaruzana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, moja kwa moja akaenda kumshughulia gazetini.

Ikawekwa picha, ikimuonesha Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifungwa kamba za viatu na mtu fulani ambaye haonekani vizuri. Picha ikaandikwa kuwa Makonda ndiye alikuwa anamfunga kamba Ridhiwani, ikaandikwa ukuu wa wilaya unatafutiwa mbali.

Tafsiri pale ni kuwa Makonda alimfunga kamba za viatu Ridhiwani ili ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya na baba yake, Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete.

Baadaye Ridhiwani alijitokeza na kufafanua kuwa aliyemfunga kamba za viatu hakuwa Makonda bali Deogratius Kessy ambaye ni mfanyakazi katika duka la mavazi la Sheria Ngowi, siku alipofuata mavazi yake.

Kwamba kwa kutaka kutimiza kiu yake ya kumshughulikia mtu, amekuwa tayari mpaka kupindisha ukweli, Kessy akaitwa Makonda!

Hoja hiyo inakamilisha pointi nyingine mbili kutoka kwenye Journalist Objectivity, Fairness (Haki) na Factuality (Ukweli unaothibitisha). Hajatenda haki, vilevile alichokiandika siyo ukweli unaothibitishika, kwani ni uongo.

Baadaye unakuja kugundua kuwa ndani ya Kubenea kuna tatizo la chuki. Na mtu anayesumbuliwa na tatizo hilo ni maradhi ambayo kitaalamu yanaitwa borderline disorder au kwa kirefu ni borderline personality disorder.

Borderline Disorder ni tawi katika mkusanyiko wa maradhi ya saikolojia yanayopatikana ndani ya somo linaloitwa Psychopathology.

Psychopathology; neno hili lina asili ya muunganiko wa maneno ya Kigiriki, psyche (nafsi), pathos (ugonjwa) na ology (somo). Maana ya moja kwa moja ya Psychopathology ni asili ya matatizo ya kisaikolojia, jinsi yanavyokua na dalili zake.

Yapo makundi nane ndani ya Psychopathology ambayo ni Major Depressive Disorder (kukosa mudi, kutokuwa na nguvu au kutamani kujiua nk), Bipolar Disorder (kuwa na mizuka mingi), Dysthymia (kukosa mudi) na Schizophrenia (kupingana na uhalisia, kuwa na mitazamo hasi na kuzungumza bila mpangilio)

Lipo Borderline Personality Disorder (rahisi kugombana na watu, kuwa na hisia kigeugeu, hasira nyingi na chuki), Pyromania (kuwa na shauku ya kupitiliza, kupenda vitu vya hatari, kufurahia majanga ya wengine), Phobias (kuwa na mapokeo yasiyo ya kawaida, kutohofia hatari na Bulimia Nervosa (tatizo la ulaji, kulakula hovyo na kujitapisha).

Katika makundi hayo nane ndani ya Psychopathology, yapo ambayo hayamhusu kabisa Kubenea lakini yapo haya manne;

1. SCHIZOPHRENIA
Schizophrenia ambayo tafsiri yake imebainishwa hapo juu, ikiwa ni kupingana na uhalisia, kuwa na mitazamo hasi na kuzungumza bila mpangilio.

Mtazamo hasi huendana na wivu. Hii ni sababu ya mashambulizi dhidi ya Zitto, vilevile kwa wengine kama ambavyo sasa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa, anavyotoneshwa na kalamu shambulizi ya Kubenea, wakati mwanzoni alikuwa msifiwa mkuu.

2. BORDERLINE DISORDER
Kwa dalili zilizomo ndani ya kundi hili, kwamba wahusika ni wale wapenda kugombana na watu, kuwa na hisia kigeugeu, vilevile hasira nyingi.

Kundi hili ndilo ambalo nilianza nalo na ndilo hasa limenifanya angalau niangalie kwa ufupi Psychopathology na matawi yake.

3. PYROMANIA
Hizi sifa za kuwa na shauku ya kupitiliza, kupenda vitu vya hatari, kufurahia majanga ya wengine zinamhusu mno Kubenea. Alishangilia mno Kafulila alipoitwa sisimizi na kutimuliwa Chadema, akachekelea pia Kitila, Mwigamba na Zitto walipofukuzwa na chama hicho.

Hili linaweza kubishiwa na mtu? Mara ngapi amejikuta akiingia kwenye migogoro na serikali kisha kuvuna huruma ya wananchi?

4. PHOBIAS
Tafsiri yake ipo juu lakini katika kipengele cha kukuza mambo inaeleweka. Tukio dogo la mtu asiyependwa na Kubenea linaweza kufanywa mjadala wa kujaza gazeti zima.

USHAURI
Aache chuki, na siyo kila wagomvi wa Chadema awaandame, vilevile haipendezi kuwa lazima awakumbatie watu pendwa na chama hicho.

Kugeuka na kumtetea Lowassa kwa sababu alibadilika na kuwa mtu pendwa wa Chadema ilimuondolea heshima na kumtupa nje ya maadili ya uandishi wa habari.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Cuf, Prof. Ibrahim Lipumba alipokuwa na utofauti na Chadema, alimkoma Kubenea. Na alipomkataa Lowassa kujiunga na Ukawa, akamkoma tena.

Yupo pia mwanasiasa mkongwe, Hamad Rashid Mohamed, aliyepata kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, yeye kuna siku alimwambia Kubenea: “Tulia, kazi yenyewe tumekufundisha wenyewe.”

Ushauri wa juu ambao naweza kumpa Kubenea ni kwamba atenganishe maisha yake binafsi, ya kisiasa na taaluma. Akifanya hivyo atakuwa mwandishi mzuri.

Mwandishi mzuri hashambulii watu, ananyoosha ukweli kwa vipimo vyake. Palipo na zuri sifia, kwenye kasoro kosoa, siyo kushambulia mwanzo mwisho.

Mwisho nampongeza kwa ushindi wake mzuri alioupata kwenye kilele cha Uchaguzi Mkuu 2015, Jimbo la Ubungo. Akiwa mkweli kwenye utumishi wake atafanikiwa.

By Luqman Maloto
+255 713 355 717

Mashabiki wa Alikiba Waishukia MTV Base, Waanzisha Kampeni ya Kuitaka Icheze Video Zake

$
0
0
MTV Base hawapumui sababu mashabiki wa Alikiba wapo shingoni mwao.

Hilo limekuja baada ya tawi lake la Afrika Mashariki, MTV Base East kuanzisha shindano dogo kwenye Twitter (Face Off Tanzania) wakiwataka mashabiki kumtaja msanii aliyefanya vizuri Tanzania mwaka 2015 na kuwaweka Alikiba, Diamond, Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz.

Watu zaidi ya 1500 walipiga kura na Alikiba alishinda mtanange huo 

Matokeo hayo yaligeuka kama risasi iliyomrudia mpigaji kwa MTV Base, baada ya mashabiki wa Alikiba kuanzisha kampeni ya kukitaka kituo hicho kicheze nyimbo zake.

Kituo hicho kinadaiwa kuziweka kapuni video zake bila sababu za msingi. Alikiba mwenyewe aliwahi kulalamika kuwa hiyo ni sehemu ya mchezo anaofanyiwa nyuma ya pazia.

Hivi ndivyo mashabiki wanavyowaambia MTV Base:

OPEN LETTER TO MTV BASE AFRICA @mtvbaseafrica. We as Music Lovers From Different Parts Of Africa, We Are Kindly Asking Why You Guys Never Play Music Videos Of @officialalikiba? We realy need to know what’s behind this issue.

At the same time, we are all humbled pleasing you guys to stop not playing Ali Kiba’s Music Videos. He is one of the best Artists in Africa who knows to Bang his Music very well on a way that his music never boring people all over the Continent. Once again, why you guys never playing His (Ali Kiba’s) Works In your Television? Consider all artist equal and let us fans decide…

We love alikiba, we love his music, words can’t tell but actions has proven it… We are one Africa break the barrier treat all artist equally. Alikiba is the best according to his fans… Alikiba is the best according to us – viewers. Audience demands u @mtvbaseafrica to play @officialalikiba music videos #PublicDemandsMTVBaseToPlayAlikibaVideos

Nyingine ilisema:

Dear MTV as you have noticed in a recently concluded poll that you conducted to determine the popularity of musicians in Tanzania, Alikiba has immense following and support in Tanzania. It is very unfortunate that your TV station never play his music videos. You are denying your audience to experience Ali’s music while at the same time you are limiting Ali’s exposure to your audience. #PublicDemandsMTVBaseToPlayAlikibaVideos

Bilioni 18.77 Zimetumwa Kwenye Akaunti Za Shule Za Msingi Na Sekondari Hapa Nchini Kwa Ajili ya Wanafunzi Kusoma Bure

$
0
0
KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.

Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3  kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Dk.Mipango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.

Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo  katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Servacius Likwelile.
Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa kila robo mwaka.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango jijini Dar es Salaam leo.

Breaking News: Viongozi wa Chadema Wajichimbia Mafichoni Kukiunda Chama Upya Baada ya Kushindwa Urais 2015

$
0
0
Viongozi wa CHADEMA wamekutana huko Mkoani Kilimanjaro kwenye kikao kizito cha kimkakati cha kukisuka upya chama chao

Lowassa, Sumaye na Mzee Kingunge kutoa msaada mkubwa wa kukifanyia ukarabati chama.

Inadaiwa kikao hicho kimeendeshwa kwa usiri mkubwa

Lulu: Tekno Alijigonga Kwangu..Na hivi Ndivyo Ilivyokuwa...

$
0
0
STAA wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameendelea kukanusha ‘ubuyu’ ulionea kuwa alivunja amri ya sita hotelini na msanii wa muziki wa Nigeria, Tekno Miles, akitoa maelezo yaliyotafsiriwa kuwa, kumbe mwanamuziki huyo ndiye aliyejigonga kwa mkali huyo wa sinema za Kibongo.

Lulu alilazimika kukanusha habari hizo kufuatia kusambaa kwa picha zake na jamaa huyo ambaye ni ‘hitimeka’ wa Ngoma ya Duro, zikiwaonesha wakiwa wamekumbatiana usiku wa Mkesha wa Mwaka Mpya 2016 ambapo Tekno aliangusha shoo ‘hevi’ kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar, kabla ya kudaiwa kwenda ‘kumbonji’ wote katika Hoteli ya Serena iliyopo Posta.

Hata hivyo, kabla ya kuenea kwa picha na habari ya Lulu na Tekno, chipukizi wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ naye alihusishwa na kulala na mwanamuziki huyo hivyo kuibuka kwa utata na maneno mengi yaliyolenga kuchochea bifu kati ya warembo hao wa Kibongo.

Ili kumaliza ubishi huo, Amani lilimpa nafasi Lulu ili kueleza kile anachokifahamu katika sakata hilo ambapo alifunguka: “Kama nilivyoeleza kwenye kurasa zangu za social media (mitandao ya kijamii), nasisitiza, nilikutana na Tekno kwenye shoo yake ukumbini.

“Yeye (Tekno) ndiye alikuja kunisalimia kwenye meza yangu na siyo mimi niliyemfuata. Nilikwenda kwenye shoo yake kama shabiki wake na siyo vinginevyo na picha alipiga na watu wengi si mimi tu.”

Chanzo: Global Publishers

Udaku Special Blog

Dr.John Pombe Magufuli Amekutana na Benjamini William Mkapa Pamoja na Joseph Sinde Warioba

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa.

Pia amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambaye amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli katika utendaji wake ili kuwa na Tanzania yenye mabadliko

Profesa Jay Ashinda Kesi ya Pingamizi la Ubunge Alilowekewa

$
0
0
Mahakama Kuu kupitia Mheshimiwa Jaji IGNAS KITUTSI asubuhi ya jana imetupilia mbali maombi madogo ya kesi ya kuomba kupunguziwa gharama za dhamana ya kesi iliyofunguliwa na mwanasiasa Jonas Nkya dhidi ya msanii/mbunge Joseph Haule (Profesa Jay).

Mahakama imetupilia mbali kesi hiyo na kukubaliana na hoja za mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na jopo la mawakili wa msanii huyo – Tundu Lissu na John Mallya.

Mahakama pia imemuamuru mlalamikaji Jonas Nkya ambaye walikuwa wakigombea pamoja nafasi ya ubunge wa jimbo la Mikumi alipe gharama zote za kesi na usumbufu.



Nimegundua Mabinti Wanashindwa Kutofautisha Mume na Boyfriend-JB

$
0
0
Nakaribia 50 sasa na huku mtaani kwetu nimepewa heshima ya mzee wa mtaa… na kila j2 jioni huwa nasuluhisha kesi za wana ndoa…katika kesi nyingi nimegundua mabinti wanashindwa kutofautisha mume na mwanaume wa starehe (boyfriend) na ndio maana una weza ukaenda harusini watu wakabeza aiii kampendea nn??? Anamefata hela tuu…sababu kuna vitu mnaviangalia ambavyo si sifa za mume…ni ziada tu ambayo kama itakuwepo una bahati…mume anatakiwa awe na sifa nyingi lakini kuu ni kuwa macho…masikio…mikono na moyo wake utakuwa kwa mke wake bila kujali wanawake wangapi wazuri wanamwinda…na yuko tayarikuihudumia na kuingalia familia yake…sio lazima awe giant na hb kama jb…wanawake wengi wameishia kuzalishwa na kuachwa na kutengeneza watoto wengi wasio na malezi ya baba na mama…na hawa walioachwa ss wana chuki kubwa na wanaume….pia kizazi hiki cha kuanzia miaka 30 kwenda chini kina wanawake wengi wajeuri wenye kujiamini kupita kiasi…nionavyo huko mbele ndoa zitakuwa chache…wacha nile pilau yangu nijiandae saa 10…kuna wengine wanakuja washatibuana karibia wiki3 sasa

By Jb on Instagram

Nahreel wa Navy Kenzo Aboresha Studio yake ya The Industry na Kuwa ya Kisasa zaidi....Atangaza Bei za Kurekodi Kupanda

$
0
0
Msanii na mtayarishaji wa muziki wa ‘The Industry’ Nahreel amepandisha gharama za kurekodi muziki kwenye studio yake kutokana na ukarabati mkubwa alioufanya.

Nahreel ambaye mwaka 2015 ametengeneza hits kama ‘Game’ ya Navy Kenzo, ‘Nana’ ya Diamond, ‘Don’t Bother’ ya Joh Makini na nyingine nyingi, amesema kuwa kutokana na ukarabati alioufanya katika studio yake, ameona aongeze bei ili kuendana na gharama alizotumia.

Ukarabati huu unaoendelea unafanyika kwa kiwango kikubwa sana, kuanzia mazingira hadi vifaa vya studio vimekuwa vya kisasa. Lengo ni kutengeneza ngoma kali na zenye ubora zaidi na kuhusu price za kurekodi track zimebadilika kidogo ila nisingependa kuweka wazi upande huo coz unaweza ukaletewa kazi kubwa na msanii au mtu yoyote ikawa hailingani na bei niliyoitaja,” amesema Nahreel.

MBWANA SAMATTA Kama Diamond Vile Atutoa Kimasomaso Watanzania...Achukua Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika...

$
0
0
Hatimaye matarajio na matumaini ya mamilioni ya watanzania yametimia, Mbwana Ally Samatta ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya bara la Afrika.

Usiku wa January 7, 2016 umekuwa mtamu sana kwa Samatta na watanzania kwa ujumla kutokana na kijana huyo wa Mbagala kuiletea Tanzania heshima kubwa kwenye sekta ya michezo hususan soka.

ramaaa

Samatta alikuwa akipambana na wachezaji wengine wawili ambao ni Robert Kidiaba Muteba (DR Congo & TP Mazembe) na Baghdad Bounedjah (Algeria & Etoile du Sahel).

Msemo wa wahenga kwamba ‘nyota njema huonekana asubuhi usemi huo’ ulianza kujitokeza mapema pale ambapo jina la nyota huyo wa Afrika lilipojitokeza kwenye list ya majina ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha wachezaji wa Afrika.

Pierre-Emerick Aubameyang amenyakua tuzo ya mchezaji bora Afika 2015 na kumpiga chini Yaya Toure ambaye ni mshindi mara nne mfululizo wa tuzo tuzo hiyo na alikua anaitetea tena kwa mara nyingine lakini ameshindwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara tano.

Ukiachana na tuzo ambayo ilikuwa inasubiliwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka duniani kote ambayo ni tuzo ya mchezaji bora wa Afrika yenye vipengele viwili kipengele cha kwanza ni mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla na kipengele cha pili ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Afrika) kuna tuzo mbalimbali zilitolewa kwa washindi.

Haya ni majina ya washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa usiku wa January 7, 2016

Timu bora ya taifa ya mwaka kwa upande wa wanaume: Ivory Coast
Timu bora ya taifa ya mwaka kwa upande wa wanawake: Cameroon
Kocha bora : Herve Renard (aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast)
Mchezaji bora kijana: Victor Osimhen (Nigeria)
Mchezaji bora chipukizi:Etebo Oghenakoro (Nigeria)
Fair play award (mchezaji muungwana): Allez Casa (Senegal)
Klabu bora ya mwaka: TP Mazembe
Mchezaji bora wa kike: Gaelle Enganamouit (Cameroon)
Mwamuzi bora wa mwaka: Papa Bakary Gassama (Gambia)
Wachezaji wakongwe: Charles Kumi Gyami (Ghana) na Samuel Mbappe Leppe (Cameroon).

Hii ndio Idadi ya Kura Alizopata Samata – Na Namna Kura Zilivyopigwa

$
0
0
Mbwana Samatta ndio jina liliotajwa zaidi kwenye vinywa vya watanzania wengi na Afrika kiujumla ndani ya masaa kadhaa yaliyopita – baada ya mwanasoka huyo wa Kitanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Anayecheza Ligi za Ndani ya Afrika.

  Ushindi wa Samatta, ambaye ni mshindi wa na mfungaji bora wa ligi ya mabingwa wa Afrika umetokana na kuwashinda wapinzani wake Zein Edin Farahat, Roger Assale, Robert Kidiaba, Moudather el Tahir,Mohammed Meftah, Kermit Erasmus, Felipe Ovono, Baghdad Bournedjah, na Abdeladim Khadrouf.

Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika upigaji kura wa kumchagua mshindi wa tuzo hii unatokana na kura zilizopigwa na makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi za kiafrika.

Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura na matokeo ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.

Mbwana Samatta alipata jumla ya kura 127 na hivyo kuongoza, akifuatiwa kwa mbali na mchezaji mwenzie wa TP Mazembe Robert Kidiaba aliyepata kura 88 na aliyefunga Top 3 ni  Baghdad Bournedjah. Kura zilipigwa na mataifa 45 ya nchi wanachama wa shirikisho la soka Afrika CAF.

Kwa upande wa Tuzo aliyoshinda Aubemayang kura zilikuwa hivi:

 1- @Aubameyang7 143 points

2- @YayaToure 136 points

3- @AyewAndre 112 points



Mbwana Samatta pia alifanikiwa kutajwa katika kikosi bora cha Afrika cha mwaka 2015

Mke Afia 'Gesti' Akiwa na Mchepuko

$
0
0

Mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa)  anayedaiwa ni mke wa mtu, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Bukoba, akiwa na mwanaume mwingine anayesemekana ni hawara yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa, watu hao walienda katika nyumba hiyo ya kulala wageni iliyopo eneo la Hamugembe Januari 3, mwaka huu na kuchukua chumba namba nane.

Alisema siku iliyofuata saa 6:00 mchana, polisi walipokea taarifa kutoka kwa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kuwa katika chumba hicho kuna watu waliingia jana yake lakini hadi muda huo mlango wa chumba ulikuwa haujafunguliwa na kuna ukimya uliowatia hofu.

Alisema wahudumu hao waliambatana na polisi na walipofika eneo la nyumba hiyo walimkuta mmiliki wake ambaye alitoa funguo za akiba na kufungua chumba hicho.

Polisi walipofungua chumba walikuta godoro liko chini lakini kitandani lilipopaswa kuwa kulikuwa na mwili wa mwanamke ukiwa umefunikwa shuka na kuuchukua kwenda kuuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera,” alisema.

Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Kagera, alisema mtu aliyekuwa pamoja na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) ambaye ni dereva wa basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Bukoba na Mwanza, hakukutwa katika chumba hicho na alifunga mlango kwa nje na kuondoka na funguo.

Hata hiyo, alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana lakini kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa msaidizi wa dereva huyo wamefanikiwa kumpata mtu aliyejitambulisha kuwa ni mume wa marehemu.

Kamanda Ollomi aliongeza kusema kuwa,  mume wa marehemu mkazi wa Butimba, jijini Mwanza, amepatikana na kukabidhiwa mwili wa mkewe, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea na kwamba wafanyakazi wawili wa nyumba hiyo ya kulala wageni wanashikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi lakini pia kwa kitendo cha kuficha taarifa za wageni wanaolala katika nyumba hiyo.
Viewing all 104705 articles
Browse latest View live




Latest Images