Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Msimamizi Wa BomoaBomoa Dar Aanguka Ghafla Ofisini Kwake.... Madaktari Washindwa Kubaini Tatizo

$
0
0
Operesheni kubwa ya kubomoa nyumba zaidi ya 15,000 zilizojengwa katika maeneo yasiyostahili jijini Dar es Salaam, imekumbana na changamoto ya aina yake baada ya mmoja wa wasimamizi wa kazi hiyo kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (Nemc), Heche Suguti, kuanguka ghafla akiwa ofisini kwake na kuwahishwa hospitali akiwa hoi.

Chanzo  kutoka ndani ya Nemc kimesema kuwa Suguti ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika baraza hilo, alianguka ofisini kwake majira ya saa 9:30 alasiri baada ya kurejea kutoka katika Mahakama Kuu kitengo cha ardhi kushughulikia kesi inayoikabili Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi dhidi ya wakazi 681 wa eneo la Mkwajuni, Kinondoni ambao wanapinga nyumba zao kubomolewa.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya Suguti kuanguka ghafla ofisini kwake eneo la Mikocheni, baadhi ya wafanyakazi wenzake (wa Nemc) walimsaidia haraka kwa kumbeba na kumpakiza kwenye gari na kumpeleka hospitali mbili tofauti ambako kote vipimo vya awali havikubaini tatizo.

Baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako alilazwa kuanzia siku hiyo (Jumanne) na kutolewa leo asubuhi (jana) baada ya kupata nafuu… ila kwa kifupi ni kwamba afya yake imeyumba na hadi sasa madaktari bado wanachunguza kujua ni kitu gani hasa kinachomsumbua,” chanzo kiliiambia Nipashe jana.

Mkurugenzi wa Nemc, Bonaventure Baya, alikiri kuwa Suguti aliugua baada ya kuanguka ofisini Jumanne wiki hii na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan, lakini haoni kama ni sahihi kuzungumzia afya yake kwani hayo ni masuala binafsi.

 “Nadhani ni uchovu ndiyo uliokuwa unamsumbua… hata hivyo, hayo ni masuala binafsi. "

Alipotafutwa kwa njia ya simu jana mchana, Suguti aliyekuwa akizungumza kwa taabu, alikiri kupatwa na tatizo asilolifahamu na kuanguka ofisini kabla ya kujikuta akiwa amelazwa katika wodi mojawapo ya Hospitali ya Aga Khan.

Kwakweli sielewi kilichotokea. Nilipoingia ofisini kwangu baada ya kutoka kwenye kesi ya nyumba za watu wa Kinondoni, ghafla nikahisi kizunguzungu, giza kutanda na mwishowe nikaanguka… sijui kilichotokea baada ya hapo ila fahamu ziliponirudia nikajikuta nikiwa hospitali,” alisema Suguti.

Alipotakiwa kueleza zaidi kuhusiana na tukio hilo, Suguti hakuwa tayari kwa maelezo kuwa bado hajisikii vizuri.

Kwa sasa naomba uniache tu, sijisikii kuzungumza zaidi,” alisema na kukata simu.

Zaidi ya nyumba 16,000 zimeshawekwa alama ya X katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambazo zinatakiwa kubomolewa kutokana na kujengwa maeneo hatarishi.

Hali si Shwari Bandarini..Si Wizi Bali Kufuru..Meli Nzima Yaibwa, Wanjanja Waficha Nyaraka Kuonyesha Haikuwahi Kufika Tanzania

$
0
0
Makubwa yamezidi kugundulika kwenye sakata la upotevu wa makontena Bandari ya Dar na sasa inadaiwa kuwa kuna nyakati wahusika wamewahi kufuta kumbukumbu za meli nzima ya makontena na kuiba makontena yote.

Taarifa hizo zinavuja wakati kukiwa na mvutano kati ya chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) kinachodai kutohusika kwa namna yoyote na upotevu wa makontena zaidi ya 11,000 ambayo hayakulipiwa ushuru bandarini (Wharfage charges).

TAFFA wanaitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuwajibika katika upotevu huo ulioinyima Serikali kupitia mamlaka hiyo mabilioni ya fedha.

Chanzo: Raia Tanzania

Udaku Special Blog

Waziri Prof. Ndalichako aibana NECTA kuhusu matumizi ya GPA...Awapa Siku Saba Kujieleza

$
0
0
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametoa siku saba kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limpe sababu za kubadili mfumo wa utunuku viwango vya ufaulu wa awali( Division) na kwenda wa wastani wa pointi (GPA) unaotumika sasa Kidato cha Nne na Sita.

Aidha, ametaka litoe maelezo ya kitaalamu juu ya sababu za kuanzisha mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea na kwamba zisipomridhisha, mwaka huu wasifanyishwe mtihani huo.

Mfumo wa GPA ulianza kutumika kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa mwaka 2014 ambao matokeo yao yalitoka mwaka jana.Vile vile mitihani miwili kwa watahiniwa wa kujitegemea, ilianza mwaka 2014 na 2015.

Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa baraza hilo kwa miaka tisa, alitoa maagizo hayo jana ambako pamoja na masuala mengine, alishuhudia namna alivyojaribiwa na kuletewa vishawishi jambo ambalo alisema, alilishinda kwa kusimamia taaluma.

Maagizo hayo aliyatoa alipotembelea na kuzungumza na viongozi, wafanyakazi wa NECTA ambako hakuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde.

Alisema tangu alipoteuliwa kuwa Waziri, amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa elimu na wananchi juu ya mfumo wa sasa wa upangaji matokeo wa GPA ambao umekuwa haueleweki na kwamba hawakushirikishwa katika mabadiliko hayo.

Nataka nijue sababu za kitaalamu za kubadilisha mfumo wa upangaji wa matokeo kutoka kwenye ule wa Division (madaraja) kwenda kwenye ule wa GPA na kama huo mfumo una tija kwa elimu yetu,” alisema.

Awali , Dk Msonde alisema mfumo huo ulipitishwa baada ya vikao kati yake, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Baraza la Vyuo vya Ufundi (Nacte) na Wizara.

Alisema baraza lilitakiwa kuendesha mfumo huo ili kwenda na mifumo mingine ya elimu ya juu katika kurahisisha udahili wa wanafunzi kwenda sanjari na mfumo wa serikali mtandao na ajira.

Watahiniwa kujitegemea
Kuhusu uanzishwaji wa mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea, Ndalichako alisema, “Nataka sababu za watahiniwa wa kujitegemea kupewa mtihani wa pili ambao unachukuliwa kama alama upimaji endelevu kwa mwanafunzi.

Kama baraza ambalo ndio wataalamu, mnasema mmeamua kutoa mtihani wa pili kutokana na kupokea malalamiko ya kufeli na mtihani mgumu, basi hatuwezi kuendelea nao, nataka nipate sababu za kitaalamu na kama sababu haziridhisha basi mwaka huu wasifanyishwe mtihani wa pili,” alisema.

Alisema kwa kawaida, mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea hauwezi kuwa mbadala wa alama endelevu kwa wanafunzi. Alisema unaongeza mzigo kwa watahiniwa na gharama za kulipa wasimamizi na wasahihishaji wa mitihani hiyo.

Ashuhudia alivyojaribiwa
Ndalichako aliwataka viongozi wa baraza hilo kutokukurupuka katika kutoa uamuzi na kufanya mabadiliko yasiyo na tija kwa taifa. Badala yake, alisisitiza watumie utaalamu wao kushauri na kukataa maagizo yasiyo na tija kusaidia katika kuboresha elimu.

Katika hatua nyingine, Ndalichako aliwataka watendaji wa Baraza hilo kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu na kuepuka vishawishi. “ Baraza la Mitihani ni sehemu ngumu sana, hasa kutokana na kuhudumia watu na hasa katika suala zima la mitihani.

"Na ni eneo ambalo lina vishwishi vingi, hata mimi nilijaribiwa kuletewa vishawishi lakini nilisimama misimamo ya taaluma,” alisema.

Ndalichako pamoja na kuwapongeza Baraza kwa kutoa vyeti mbadala, ametaka kuwa makini katika suala hilo kuzuia udanganyifu.

Alisisitiza watoe tathmini ya kina katika matokeo ya wanafunzi ambayo yatasaidia wizara kufanya uboreshaji. “Nilipokuwa hapa, kuna wakati nilikuwa nakosa usingizi linapokuja suala la kutangaza matokeo, unakuta matokeo ya wanafunzi 30 yote ni mbaya, sasa hapa si kuwa wanafunzi wote walikuwa hawafundishiki ila kuna tatizo la ziada, na hilo ndio tunatakiwa kushughulikia,” alisema.

Alisema, “ Nilikuwa naumia sana na ubora wa elimu iliyokuwa ikitolewa kwa baadhi ya shule, sasa nimepewa kazi ya kuhakikisha elimu inakuwa bora, tunaondoa watu wa kuchora mazombi na ule wakati wa shule kugeuka vituo vya kulelea watoto badala ya kutoa elimu umefika mwisho.”

Udaku Special Blog

Breaking News: Huku Sakata la Nyumba zake Kutaka Kubomolewa Wastara Afunga Ndo na Mwenyekiti wa UVCCM

$
0
0
Wakati sakata la kutaka kubomolewa kwa nyumba zake mbili zilizowekwa X ikiwa bado haijapoa, Muigizaji Wastara Juma, jana usiku amefunga ndoa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma.

Nafasi ya Kazi National Housing Corporation (NHC), Application Deadline 20thJanuary 2016

$
0
0
Job Vacancy
Location : Dar Es Salaam 
Position Type : Full Time 
Organization Type : Government
National Housing Corporation (NHC)

ClickHERE to Read and Apply

[Audio] Wastara Azungumzia Alivyoinadi CCM na nyumba Zake Kuwekewa Alama "X"

$
0
0
Wastara Juma ni mmoja wa wasanii maarufu wa filamu nchini Tanzania.

Katika audio inayosikika kwenye video iliyopachikwa hapo chini, anazungumzia anazungumzia kuhusu nyumba zake kuwekwa alama ya "X" kwa ajili ya kubomolewa, huku akigusia kujitoa kwake kufanya kampeni ya kukinadi Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kuugua.

MSIKILIZE HAPA WASTARA:

Lulu Michael Amponza Mwanamuziki Tekno Miles...Comments za R.I.P Zajaa Kwenye Ukurasa Wake!

$
0
0
Tukio la kifo cha marehemu Steven Kanumba linaendelea kumwandama aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth “Lulu” Michael, kutokana na baadhi ya Watanzania kuendeleza tabia isiyokubalika, ya kumkejeli mwanaume yeyote anayesemekana kuwa na uhusiano naye kuwa kifo kinamuita.

Kitendo hicho kimejitokeza pia kwa muimbaji wa Nigeria, Tekno aliyedaiwa kuwa na uhusiano naye. Hata hivyo Lulu alikanusha na kudai kuwa huo ni uzushi kwasababu hakuna kinachoendelea kati yao.

Toka hit maker huyo wa ‘Duro’ arudi Nigeria amekuwa akipata comments nyingi kutokana na uzushi kuwa amenasa kwenye ulimbo wa Lulu, lakini kilichokuja kumchukiza zaidi ni comments za R.I.P zilizompelekea kuamua kufuta picha zake zote na kuandika ujumbe mrefu kuelezea Wanigeria na wengine wasioelewa sababu za comments za R.I.P kwenye ukurasa wake.

Haya ndio maelezo aliyopost Tekno ambayo baadae aliyafuta:

Kwanza kabisa, ninamsamehe kila mmoja wenu aliyecomment R.I.P kwenye ukurasa wangu.

Kwa familia yangu, marafiki, bloggers na wote mliokuwa mkinipigia kuniuliza hizo comments za R.I.P zinamaanisha nini, kuna wanaosema kuwa nimetenda kosa la jinai nilipokuwa Tanzania! Lol.

Nilichokifanya mimi ni kupiga picha na msichana mrembo wa Tanzania sitamtaja jina lake. Kilichotokea ni kwamba wanaume wachache ambao waliwahi kuwa na uhusiano naye walifariki, kama wanavyosema!

Kwahiyo hawa watu wanaocomment R.I.P wanaamini kuwa nina uhusiano naye kwasabbu ya picha niliyopost Instagram ya mimi na yeye(Lulu), hivyo wanamaanisha na mimi nitakufa, wow! Inafurahisha.

Kwanza, nyie ni nani kuhukumu maisha yake,
Pili, nyie ni nani kucomment R.I.P kwenye ukurasa wangu…

Mungu tusamehe na utuangalie wote. Sasa mmefahamu.”



Mpaka sasa ukurasa wa Tekno una picha tano tu alizoanza kupost January 7, 2016.


This leaked VIDEO of HUDDAH MONROE in bed will get Kenyan men crazy, Oh Lord.

$
0
0

If you thought that controversial socialite, Huddah Monroe, will change her crazy behaviour this New Year, then you are wrong.

A video of thirsty Huddah Monroe pulling some s3ductive dance moves in bed has surfaced online and left men’s blood boiling.

The notorious socialite is seen shaking her waist like those ladies you see in blue movies and when things become too hot to handle, she lets the fingers do the walking.

Check out the crazy video below.


Breaking News:Shehena Ya Petroli FEKI Yakamatwa....Serikali Yaamuru Irudishwe Ilikotoka!

$
0
0
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeamuru shehena ya mafuta ya petroli iliyoagizwa kutoka Falme za Kiarabu irejeshwe ilikotoka kutokana na kubaini hayana ubora unaotakiwa kwa matumizi ya magari na mitambo.

Akitoa taarifa hiyo Dar es Salam jana, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Joseph Masikitiko alisema, vipimo vya maabara vya sampuli ya mafuta hayo vimeonesha kuwa hayafai kwa matumizi.

Alisema hayo ni matokeo ya ukaguzi wa hivi karibuni wa shehena hiyo yenye ujazo wa tani za metriki 38,521.018 katika meli ya MT. Ridgebury John B, yaliyokuwa yasambazwe na kuuzwa nchini.

Alisema, "Vipimo vinaonesha kuwa baadhi ya matakwa ya viwango vya mafuta ya petroli hayajafikiwa, hivyo kuamuru yarejeshwe yalikotoka. Kiwango cha ubora cha mafuta ya petroli ni TZS 672:2012/ EAS 158:2012 ambacho hakikufikiwa".

Matakwa ya kiwango ambacho mafuta hayo hayakukidhi ni pamoja na kuwa na kemikali zilizo na oksijeni ndani yake ambazo husababisha madhara kwenye injini za magari na mitambo.

Alisema, "Kiwango cha petroli hakiruhusu uwepo wa kemikali hizo kwenye mafuta hayo kwa sababu zinaua injini, kuhatarisha afya za watu na kuharibu mazingira kutokana na kusababisha moshi mchafu mwingi".

Alifafanua kuwa mafuta hayo yameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuvuta maji au mvuke na kuwa sehemu ya petroli, kiasi cha kuifanya iwe na maji mengi ambayo ni hatari kwa injini za magari na mitambo.

Pia, alieleza uhafifu mwingine katika mafuta hayo kuwa ni kupungua kwa nguvu ya kuendesha injini au mitambo hivyo kusababisha uharibifu na hasara.

Aliongeza kuwa, mvuke unapokuwa mwingi kwenye petroli husababisha mtiririko wa mafuta kwenda kwenye injini kutokuwa mzuri, huku kemikali aina ya benzene iliyoonekana kuzidi katika petroli hiyo ikiwa ni chanzo cha kansa kwa wanaotoa huduma ya uuzaji wa mafuta hayo.

Sambamba na hayo, Masikitiko aliongeza kuwa walibaini kuwa uhafifu katika mafuta hayo unaongeza wingi wa ujazo wa nishati hiyo pasipokuwa na uhalisia na kisha kutoa nguvu isiyolingana na wingi wake. Alisema, madhara yake ni mnunuzi kulipia wingi wa mafuta usio na thamani halisi.

Aliwahakikishia watumiaji wa mafuta kuwa, shirika hilo litahakikisha linafanya ukaguzi katika meli zote zenye mafuta yanayokusudiwa kusambazwa nchini ili kuzuia yasiyo na ubora yasiingizwe sokoni.

Katika hatua nyingine, Tbs ilisema kuwa iliagiza vilainishi vya mitambo na magari vya kampuni ya HASS Petroleum (T) Limited vyenye ujazo wa lita 16,080 kutoka Falme za Kiarabu virejeshwe vilikotoka pia kwa sababu ya kukosa ubora unaofaa kwa matumizi na kwamba mwagizaji alitekeleza agizo hilo tangu Desemba 31 mwaka jana.

Ewura yazungumza
 Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imekiri kufahamu kuhusu suala hilo na kueleza wananchi kuwa licha ya mafuta hayo kutakiwa kurejeshwa yalipotoka, bado nchi ina akiba ya petroli inayoweza kutumika hadi shehena nyingine iletwe.

"Wananchi wasiwe na wasiwasi," alisema Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo. Alisema kwa siku nchi inatumia lita za petroli 2,700,000, na kwamba kila metriki tani moja ya petroli huwa na lita 700,000.

"Kwa maana hiyo, lita 33,000,000 za petroli zilizokuja na kukataliwa endapo zingeshushwa na kutumika nchini zingeweza kutosheleza mahitaji kwa zaidi ya siku saba," alisema Kaguo .

 Hata hivyo, aliongeza kuwa si mafuta yote yanayoingia na meli bandarini hushushwa kwa ajili ya matumizi ya nchi, bali mengine huwa safarini kwenda nchi nyingine.

Udaku Special Blog

Manji Alinunua Gazeti la Jambo Leo

$
0
0
Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania ambao ni wachapishaji wa Gazeti la kila siku la Jambo Leo imenunuliwa na Kampuni ya Quality Media Group ambayo ni kampuni tanzu ya Quality Group Limited,ununuzi umeanza December 31 na unategemea kukamilika February 01.

Kampuni ya Quality Media imedhamiria kuwekeza katika tasnia ya habari kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa gazeti la Jambo Leo na kuahidi kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2016 kuongeza machapisho mengine ikiwa ni pamoja na gazeti la kiingereza la kila siku na gazeti toleo la wiki la Afrika Mashariki.

Mkurugenzi mtendaji wa Quality Group, Bw. Arif Sheikh alisema: “Kampuni ya Quality Group imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Jambo media inakuwa chombo cha habari bora na cha kuaminika nchini Tanzania na katika ukanda wote wa Afrika Mashariki”

“Tumedhamiria kuhakikisha kunakuwepo na uhuru, uwazi na ukweli katika utoaji taarifa ili kuhakikisha umma unaarifiwa habari za uhakika,” aliongeza.

“Hivi punde tutatangaza bodi ya ushauri ya uhariri (Editorial Advisory Board) kwani kama wanahisa, tusingependa kuingilia maadili ya kiuandishi,” alimalizia.

Rais MAGUFULI Naye Kaguswa na Ushindi wa Mbwana Samatta!! Kayaandika Haya..

$
0
0
Jana Tanzania iliandika historia katika medali ya soka Afrika na duniani baada ya mshambuliaji Mtanzania anakipiga katika klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Afrika.

Samatta alitangazwa mshindi huko Abuja, Nigeria katika tuzo zilizowashirikisha mastaa mbalimbali wa soka Afrika.

Furaha ya Watanzania pia imemgusa Rais wa awamu ya tano John Magufuli ambaye ametuma pongezi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.

Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa, Rais amemtaka Waziri Nape amfikishie salamu za pongezi mchezaji huyo na pia tuzo hiyo imemjengea heshima kubwa na kuleta heshima kwa wachezaji wa Tanzania.

Taarifa hiyo ilisomeka hivi..

Serikali Yatoa Picha Rasmi ya Rais wa Awamu ya Tano, Dkt John Pombe Magufuli

$
0
0
Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itaanza kuuzwa Januari 08, 2015, katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.

Kila nakala ya picha hiyo itauzwa shilingi Elfu Kumi na Tano tu bila fremu.  Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa shilingi Elfu Tano tu.  Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Picha hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi binafsi.  Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa.

Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza  picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kutoa taarifa kusitisha matumizi ya picha hiyo na wanaotengeneza picha ukubwa ambao siyo rasmi.

Hatua za kisheria  zitachukuliwa dhidi yao.  Idara ya Habari(MAELEZO) ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo.

Rais Benjamin Mkapa Naye Ataka Kutumbua Majipu, Amwambia Rais Magufuli Haya Hapa..

$
0
0
RAIS mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yuko tayari kutoa ushirikiano wa kila aina au kufanya kazi yoyote endapo Rais Dk. John Magufuli atahitaji.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Mkapa alitoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu na Rais Magufuli.

Ilisema lengo la Mkapa kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na Watanzania kuiongoza nchi, kuunda Serikali na kumtakia heri ya mwaka mpya.

Mkapa amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo,” ilisema taarifa hiyo.

Pia Rais Magufuli alikutana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba ambaye alisema Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono kiongozi huyo kwa kazi kubwa anazofanya ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali za umma.

Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachia, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais peke yake… yeye awe kiongozi wetu, lakini Watanzania wote tushughulike na matatizo hayo,” ilisema taarifa hiyo ikimkariri Jaji Warioba.

Pamoja na kumtakia heri ya mwaka mpya, Jaji Warioba alimpongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri, hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi ikiwamo afya na maji.
Kauli ya Mkapa na Jaji Warioba imekuja siku moja tu baada ya juzi Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtembelea Rais Magufuli Ikulu na kufanya naye mazungumzo ambayo hata hivyo yameendelea kuwa ni siri.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wastaafu ndani ya siku mbili kumtembelea Rais Magufuli tangu ameingia Ikulu Novemba 5, mwaka jana.

Udaku Special Blog

Diamond Platnumz Atajwa Kuwania Tuzo za MAYA 2016 za Nchini Nigeria

$
0
0
Diamond Platnumz ambaye kutokana na kutajwa mara kwa mara kuwania tuzo mbalimbali wanamuita ‘Mondi Bin Awards’, ametajwa kuwania MOREKLUE ALL YOUTH AWARDS 2016 kwa kifupi MAYA Awards za nchini Nigeria, ikiwa ndio nomination yake ya kwanza kwa mwaka huu 2016.

Kwenye kipengele cha African Music Act Diamond anawania pamoja na wasanii wengine wenye majina makubwa Afrika akiwemo, Wizkid, Sarkodie, Fuse ODG, Davido, AKA, Olamide na
Cassper Nyovest.

Tuzo za MAYA zitatolewa January 31, 2016 jijini Lagos, Nigeria.

Ili kuweza kumpigia kura Diamond aweze kushinda tuzo hii ingia HAPA.

Mtuhumiwa namba Moja Kesi Ya Mauaji ya Dk. Mvungi Afariki

$
0
0

Mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi ameripotiwa kufariki akiwa gerezani, siku chache kabla ya kesi kusikilizwa.

Taarifa ya kifo cha mshtakiwa huyo aliyetajwa kwa jina la Chibago Chiuguta mwenye umri wa miaka 33, zilitolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kueleza kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akiwa amekutwa na umauti.

Kufuatia taarifa hizo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Thomas Simba aliagiza upande wa Magereza kuhakikisha wanafuatilia cheti cha kifo cha mshitakiwa huyo.

Marehemu alikuwa kati ya washtakiwa 11 waliodaiwa kumuua Dk. Mvungi katika eneo la Msakuzi, Kiswegere katika wilaya ya Kinondoni. Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo Novemba 3 mwaka 2013.

Upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 9, Ikiwemo Jide na Namless Wazua Gumzo Picha yao ya Mahaba yatua Kwa Gadner

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 9, Ikiwemo Jide na Namless Wazua Gumzo Picha yao ya Mahaba yatua Kwa Gadner

Diamond Yamkuta ya Wema… Atimuliwa Kwenye Nyumba ya Studio

$
0
0
SIKU chache baada ya muigizaji kiwango Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutimuliwa katika nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutolipa bili ya umeme na maji, Jumatano hii, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ naye alikutana na kimbembe kama hicho kutoka kwa mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiitumia kama studio, iliyopo Sinza Mori, Risasi Jumamosi linakuhabarisha.

Kwa nyakati tofauti, chanzo kinasema majirani waliwahi kupanda juu ya uzio wa nyumba hiyo na kutaka kupunguzwa kwa sauti ya muziki, lakini Diamond na madansa wake wamekuwa wakikaidi kwa madai kuwa hiyo ni sehemu ya kazi yao, jambo lililosababisha kuwasiliana na mmiliki wa nyumba hiyo ili amtoe msanii huyo, vinginevyo watamshtaki.

Jamaa baada ya kuitwa na mwenye nyumba na kuambiwa kuhusu jambo hilo na kutakiwa kuhama, aliongea naye kutaka amuuzie kabisa nyumba hiyo lakini akakataa na hata alipong’ang’ania, Diamond alitajiwa bei isiyofanana hata kidogo na nyumba hiyo, akaondoka usiku-usiku kama ilivyokuwa kwa Wema kukwepa aibu,” kilisema chanzo chetu.
Jengo iliyopo Studio hiyo

Gazeti hili liliwasiliana na msanii huyo ili kupata ukweli wa tukio hilo lakini alikataa kuzungumzia lolote juu ya ishu hiyo. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa staa huyo amehamishia ofisi zake eneo la Sinza Mapambano, hatua chache tu kutoka alipotimuliwa.

BomoaBomoa Yaipasua Kichwa Serikali.......Mwanasheria Wa Nemc Aliyehalalisha Jumba La Mchungaji Rwakatare Afukuzwa Kazi

$
0
0
TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU ZOEZI LA KUHAMISHA WAKAZI WA MABONDENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Utangulizi
Nchi yetu ina kingo za mito na mabonde na maeneo mengi hatarishi ambamo watu wanaishi kinyume cha sheria, huku wakiharibu mazingira na kuhatarisha maisha yao.  Kutokana na uhaba wa makazi, hali ni mbaya zaidi katika mabonde ya Jiji la Dar es Salaam, hasa bonde la Mto Msimbazi.

Serikali za awamu zote, zimekuwa zikifanya jitihada za kuwaondoa wakazi wa maeneo ya mabondeni wanaoishi katika maeneo hayo kinyume cha sheria lakini mafanikio yamekuwa si ya kuridhisha.

Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo moja ya misingi yake mikuu ni utii wa sheria za nchi, imeanza jitihada za kuwaondoa wakazi hawa. 

Tuliamua kuanza na Bonde la Mto Msimbazi kwasababu ndiko kwenye watu wengi na athari kubwa.Sababu zetu kuu za kufanya zoezi hili ni kusafisha mabonde na mito katika jiji la Dar es Salaam na mazingira yanayozunguka ni:-

Kunusuru maisha ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi. Eneo la Bonde la Mto Msimbazi lilitangazwa kuwa ni eneo hatarishi kuishi binadamu tangu mwaka 1949 na baadaye 1979.

Kupanua uwezo wa mito ya Dar es Salaam ili kupitisha maji ya mvua kwa kasi kubwa, hivyo kupunguza uwezekano wa kutokea mafuriko na maafa wakati wa mvua nyingi;Kuzuia milipuko ya magonjwa, hasa ya kipindupindu, hasa wakati wa mvua;

Kuzuia eneo hilo kuendelea kutumika kama maficho ya wahalifu na uhalifu;

Kutoa nafasi kwa Serikali kuandaa na kuendeleza eneo hilo kwa mujibu wa sheria za nchi na mipango miji;

Utaratibu wa Zoezi
Kabla ya nyumba kubomolewa, taasisi hizi zinashirikiana kuhakiki iwapo nyumba anayokaa mkazi ina nyaraka za umiliki na vibali vya ujenzi na iwapo nyaraka hizo zina uhalali wowote. 

Nyumba ambazo zimethibitika kuwepo katika maeneo yasiyostahili ndio zinawekwa alama X kuashiria kwamba wakazi wanapaswa kuhama au kubomoa. Baada ya hapo, mkazi hupewa muda wa kubomoa na kuhama mwenyewe.

Kutokana na utaratibu huu, sehemu kubwa ya nyumba zinazobomolewa ni zile ambazo watu wamekwishaamua kubomoa wenyewe. 

Baada ya hapo, alama huwekwa kuonyesha mpaka wa bonde. Katika zoezi hili, imebainika kwamba sehemu kubwa ya wakazi wa maeneo ya mabondeni ni wapangaji huku wamiliki wakikaa sehemu nyingine salama.

 Serikali pia imeweka Dawati la Malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Tathmini ya Zoezi
Jana, terehe 7 Januari 2016, Mawaziri watatu (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI; na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais; pamoja na Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii), walifanya mkutano wa kutathmini zoezi la kuhamisha wakazi wa mabondeni katika Jiji la Dar es Salaam. 

Mkutano huo ulipokea ripoti ya timu ya wataalam wa Wizara mbalimbali, inayoongozwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, ambayo, pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba sehemu kubwa ya kubaini makazi yaliyojengwa kinyume cha Sheria katika Bonde la Mto Msimbazi imekamilika. 

Ripoti ilieleza kwamba, hadi sasa, wananchi katika nyumba 774  wamehama na nyumba hizo kubomolewa. Ilielezwa pia kwamba kabla ya mkazi kuombwa  kuhama, uhakiki kuhusu uhalali wa makazi anayoishi hufanywa. 

Kutokana na uhakiki huo, jumla ya wakazi 20 walikuwa na hati halali za makazi na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi. 

Hawa watu hawakuhamishwa. Mawaziri walipokea maelezo kuhusu changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika zoezi hilo.  

Baada ya tafakuri na mjadala, Mawaziri hao walitoka na msimamo ufuatao, kama uamuzi wa Serikali: -

1.Zoezi la kuwaondoa wananchi waishio katika bonde la Mto Msimbazi (eneo hatarishi) litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi;

2.Katika awamu hii, zoezi litajikita katika Bonde la Mto Msimbazi tu.

3.Kwa wakati huu, watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi yao yamo NDANI kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia bondeni na kwenye KINGO za mto;

4.Wale watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma, zilizowamilikisha na kuwaruhusu kujenga katika bonde hilo, hawatahamishwa bila kupewa sehemu nyingine za kujenga. Na watumishi wa umma waliowamilikisha maeneo hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria;

5.Serikali, ndani ya siku tatu zijazo, itaanza zoezi la kuzoa kifusi na kusafisha maeneo ambapo ubomoaji umefanyika.

6.Serikali itaheshimu amri za mahakama kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na baadhi ya wakazi wa mabondeni lakini pia itafuatilia kesi hizi ziishe haraka ili taratibu zinazofuatia zifanyike;

7.Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wake wanaoendesha zoezi hili kinyume na misingi ya sheria zinazotekelezwa, na kinyume na misingi ya haki na uwazi, ikiwemo wanaoweka alama za X zaidi ya mita zilizowekwa kisheria. Limeanzishwa dawati la malalamiko katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupokea malalamiko au maswali kuhusu zoezi hili.

8.Nyumba na majengo ya miaka mingi, yaliyokuwepo miaka mingi kabla ya kutungwa kwa Sheria zinazotekelezwa kwa zoezi hili, hayatabomolewa isipokuwa tu pale maisha ya wakazi yapo hatarini. Wanaoishi katika makazi hayo watapewa miongozo ya hatua za kuhifadhi mazingira na kujiokoa na maafa;

9.Serikali haina dhamira ya kubomoa mahoteli makubwa ya siku nyingi yaliyo karibu na fukwe katika maeneo ya Masaki. Wamiliki wa mahoteli haya watapewa masharti na miongozo ya kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria.

10.Serikali inaweka uratibu wa karibu zaidi miongoni mwa taasisi zake ili hatua za utekelezaji wa sheria za nchi zisiwe chanzo cha taharuki katika jamii.

11.Serikali haina dhamira ya kuwatesa wananchi wake kwa kuwalazimisha kuhama katika makazi yao bila sababu za msingi. Lakini pia Serikali haiwezi kuruhusu wananchi waendelee kukaa katika maeneo ambayo ikinyesha mvua kubwa maisha yao yapo hatarini.

 Itakumbukwa kwamba katika mafuriko ya mwaka 2011, wananchi 49 waishio mabondeni walipoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Hali ya Hewa, mwaka huu zinatarajiwa kunyesha mvua kubwa kuliko zilizowahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

12.  Serikali inafuatilia kwa karibu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya taarifa za wananchi wanaohitaji msaada maalum wa kibinadamu.

Suala la Mchungaji Getrude Rwakatare
Mkutano ulipokea taarifa kuhusu suala linaloongelewa sana la nyumba ya Mchungaji Rwakatare.  Ilielezwa kwamba Mchungaji Rwakatare amejenga nyumba yake pahali ambapo amezuia mtiririko wa mto kwa kujaza kifusi ili kupata eneo zaidi katika eneo la miti ya mikoko, kinyume kabisa na Sheria tatu muhimu.  

Pia ilielezwa kwamba tangu wakati ujenzi unaanza jitihada za kumsimamisha zilifanyika na mamlaka za Serikali za Mitaa lakini ikashindikana kutokana na sababu mbalimbali. Pale Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira lilipoingilia kati na kutaka kuibomoa nyumba hiyo, Baraza lilishtakiwa mahakamani. 

Wakati kesi inataka kuanza kusikilizwa, mwanasheria mdogo wa Baraza, yeye mwenyewe bila kuagizwa wala kuwaarifu wakubwa zake, mnamo tarehe 11 Mei 2015, aliingia makubaliano na mawakili wa Mchungaji Rwakatare kwa niaba ya Baraza ya kuondoa kesi hiyo mahakamani na kukubali, kwa niaba ya Baraza, kutombughudhi kabisa Mchungaji Rwakatare.  

Makubaliano hayo yalisajiliwa na Mahakama kama hukumu tarehe 13 Mei 2015. Mwanasheria huyo alificha makubaliano hayo kwa miezi mitano hadi Oktoba 2015, yalipogundulika na mtumishi mwingine wa Baraza. Mkutano ulielezwa kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kufuata taratibu zote, alishaagiza kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mwanasheria huyo. 

Mwanasheria huyo alifukuzwa kazi siku ya juzi tarehe 6 Januari 2016 na taarifa zake zimekwishafikishwa TAKUKURU. 

Vilevile, Ofisi ya Makamu wa Rais, iliiagiza Baraza kufungua shauri mahakamani la kuomba “makubaliano” kati yake na Mchungaji Rwakatare yawekwe pembeni kwasababu yalipatikana na njia ya udanganyifu. Shauri hilo lilifunguliwa tarehe 29 Disemba 2015.

Kuhusu Karakana ya Mradi wa Mabasi Yaendayo kwa Kasi (DART)
Mkutano pia ulijulishwa kuhusu hoja inayozungumzwa kwamba wananchi wanaondolewa katika maeneo ya kuishi mabondeni lakini mradi wa DART umeachwa.

 Mkutano ulielezwa kwamba Sheria ya Mazingira (kifungu 57 (2)) inatoa nafasi ya kutolewa ruhusa kwa miradi/shughuli zenye maslahi ya taifa kufanyika katika maeneo ya mabondeni, na kwamba Waziri mwenye dhamana ya mazingira anaruhusiwa kutoa miongozo ya namna ya shughuli hizo zinavyoweza kufanyika bila kuathiri mazingira.

 Mradi wa DART ulipata kibali hicho na una mkataba na Baraza la Mazingira kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira zinazopaswa kutekelezwa katika mradi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016

Mkongo Awamaliza Mastaa wa Kike Bongo...

$
0
0
Mwandishi wetu
Pedeshee Mkongo anayefahamika kwa jina la Rajab Mwami, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwenye maskani jijini Dar, amegandwa na madai ya kutaka kuwamaliza mastaa wa kike Bongo kutokana na kuwa na uhusiano nao kwa nyakati tofauti.

wolper[1]Jacqueline Wolper
Madai hayo yanakuja kufuatia jamaa huyo awali kuripotiwa kuwa na uhusiano na staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe kabla ya baadaye kuhamia kwa Video Queen, Husna Maulid.
luluuuElizabeth Michael ‘Lulu’
AMTAKA LULU
Habari ya mjini ni kwamba, baada ya kutokea hali ya kutokuelewana kati ya Wolper na Husna, jamaa huyo aliamua kuachana nao na baadaye akatangaza kuwa, yuko tayari kupoteza kiasi chochote cha fedha ilimradi amnase staa mwingine wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja kama alifanikiwa kutimiza azma yake hiyo kwani kilipita kimya kidogo bila kujulikana anatoka na staa gani.
wema3Wema Sepetu
ADAIWA KUMNASA WEMA
Baada ya kupita kimya kirefu, yaliibuka madai kuwa, Mkongo huyo amejiweka kwa mwigizaji Wema Sepetu na kwamba kufuru alizokuwa akifanya mwandada huyo mjini, zilitokana na jeuri ya fedha za Mwami.

tunda-21.jpgTunda Sabasita
ATUA KWA TUNDA
Kana kwamba jamaa huyo hatulii kwa demu mmoja, kuna kipindi yaliibuka tena madai kuwa amejiweka kwa Video Queen wa Bongo, Tunda Sabasita hali iliyosababisha watu kuhoji sababu ya mabinti hao kumpapatikia.

shamsaaaaShamsa Ford
SHAMSA ADAI KUTOKEWA
Naye staa mwingine wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford aliwahi kunukuliwa na gazeti hili akidai kuwa, Mkongo aliyewahi kuwa na Wema na Wolper, amemtokea.
Hata hivyo, hakukuwa na ushahidi kama aliyemtokea ni Mwami au Mkongo mwingine ambaye huenda aliwahi kuwatokea Wema na Wolper.

MASOGANGE5Agness Gerald ‘Masogange’
MASOGANGE NAYE KABANG
Wakati watu wakihisi jamaa huyo katulia zake Kongo, juzikati Mkongo huyo akanaswa akiwa na Video Queen mwingine wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ wakiwa hotelini na akadai wapo kibiashara zaidi.

Hata baada ya pedeshee huyo kujitetea, wengi walidai kuwa, licha ya uwezekano wa kuwepo kwa biashara kati ya wawili hao, kwa jinsi anavyopenda watoto wazuri, hawezi kumuacha.
HOFU YA KUAMBUKIZANA UKIMWI YATANDA
Kufuatia mastaa hao kupishana kwa pedeshee huyo, wengi waliozungumza na Ijumaa walionesha hofu yao ya kuambukizana ugonjwa hatari wa Ukimwi.

“Yaani huyu jamaa sijui pesa zake ndiyo zinampa kiburi, maana kila staa anayemtaka anamtokea, lakini hofu yangu ni kwamba kama anatembea nao wote bila kinga si watakuwa wanaambukizana?” alihoji Husna Juma wa Kinondoni huku akiomba ikiwezekana jamaa huyo arudishwe kwao kwani atawamaliza mastaa hao.
MWAMI ANASEMAJE?
Baada ya kuwepo kwa msururu ‘mtungo’ huo wa mastaa wakiwepo aliowapitia na aliopanga kuwapitia, mwandishi wetu alimtafuta Mwami kupitia simu yake ya mkononi ambapo katika kujitetea alisema kuwa, yeye ni mtu na familia yake na hao mastaa wengi wao wanajigonga kwake.

“Hao bwana wanajigonga kutokana na tamaa zao, mimi siwezi kuwa nao kwa kuwa nina mke wangu na nampenda sana,” alisema Mwami

Source:Global Publishers

Udaku Special Blog

Watu 79 Watiwa Mbaroni Kwa Kuishi Nchini Bila Vibali na Kufanya Kazi Zinazoweza Kufanywa Na Watanzania

$
0
0
WATU 79 wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji nchini kwa kosa la kuishi nchini bila vibali na kufanya kazi wasizo na taaluma nazo.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji Dar es Salaam, John Msumule jana alisema watuhumiwa hao wanatoka katika nchi 15.

Nchi hizo na idadi ya wahamiaji haramu ni Nigeria (4), China (20), Ethiopia (23), Korea (9), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC (6), Somalia (3),Uganda (2), Madagascar (5), Burundi (2), Ivory Coast (1), Lebanon (1), India (1), Zimbabwe (1) na Ghana (1).

Alisema katika ‘kamata kamata’ hiyo pia wamefanikiwa kukamata Watanzania watatu, ambao wamekuwa wakijishughulisha na kukusanya, kuwahifadhi na kuwasafirisha wasichana kuwapeleka nchi za mbali, kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali.

“Tumewakamata wasichana sita ambao walikuwa wamekusanywa na watanzania hao ili kusafirishwa na tutawachukulia hatua za kisheria ili kutoa fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya mtindo kama huu,” alisema Msumule.

Aliongeza kuwa idara hiyo imewarudisha nchini mwao wahamiaji 23 raia wa Ethiopia na watuhumiwa nane wa nchi mbalimbali,wamefikishwa mahakamani. Alisema shughuli ya kuwarejesha raia wengine katika nchi zao zinaendelea.

Msumule aliwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni na nyumba za kupanga, wahakikishe wanatambua wateja wao ni raia wa wapi na anafanya kazi gani, kabla ya kufanya naye mkataba wa aina yoyote.

Aliwataka pia watanzania wanaooa na kuolewa, wahakikishe wanafahamiana na mtu huyo na kumchunguza kujua anakotoka na yupo nchini kwa kazi gani, la sivyo mtu akibainika anaishi na mhamiaji, anaweza kujiingiza katika matatizo.

“Sisi hatutajali, tutamkamata kwa kosa la kumhifadhi kwa hiyo lazima wajenge dhana ya kuwachunguza watu hao, hata wasichana wa kazi za ndani, lazima umjue vizuri na sio unamchukua tu bila kujua historia yake ,” alisema.

Msumule aliwataka raia wengine ambao hawana vibali vya kuishi nchini, waondoke wenyewe na wasisubiri hadi sheria ichukue mkondo wake.

“Wapo wengi, tunachoomba waondoke wenyewe bila kushurutishwa, wengine wanafanya kazi ambazo hata watanzania wanaweza kuzifanya, wakubali na waondoke,” aliagiza.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images