Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Balaa la Njaa..Wakazi wa Chamwino Dodoma Wala Viwavi Jeshi Kuikabili Njaa

0
0
Wakazi wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanakula wadudu jamii ya viwavi jeshi, wanaojulikana kwa jina la fumbili kutokana na njaa kali iliyoikumba wilaya hiyo.

Hata hivyo, chakula hicho huenda kikapotea wakati wowote kutokana na mvua kutonyesha hivyo wadudu hao, ambao huishi kwa kutegemea majani, nao kupotea kwa kukosa chakula.

Mbali na fumbili, chakula kingine ambacho kilikuwa mkombozi kwa wakazi wengi, hususan Tarafa ya Chilonwa, ni matunda ya zambarau ambayo nayo yatakwisha wakati wowote kwani msimu wake umekwisha.

Chamwino ni wilaya iliyoko takriban kilomita 30 kutoka mjini Dodoma, ikikadiriwa kuwa na watu 349,714 na mazao ya chakula yanayolimwa kwenye wilaya hiyo ni mtama, uwele, mpunga, mahindi, mihogo, viazi vitamu, kunde, nyonyo, mbogamboga na choroko.

Juzi, Mbunge wa Chilonwa, Joel Mwaka aliitisha kikao cha dharura cha madiwani wote wa jimbo hilo lenye kata 14 kujadili suala hilo na kila diwani aliyechangia mjadala huo, alionyesha kujuta kugombea kwa kuwa wananchi wanamlilia.

Madiwani hao waliweka azimio la kusafiri kwenda Ikulu, Dar es Salaam kuwasilisha kilio cha wananchi wao.

Akizunguma kwenye kikao hicho, Mwaka alisema hali ya wakazi wa Chilonwa ni mbaya kiasi hakuna matumaini hata ya kupata mlo mmoja na badala yake wengi wanaishi kwa uji na matunda pori na fumbili.

Mbunge huyo alilaani mpango wa Serikali wa kuwapa vibali wafanyabiashara kwenda kuchukua mahindi katika ghala la chakula la Songea kwani bei zinakuwa kubwa.

“Ndiyo maana wanyabiashara wengi walikataa kwa kuwa bei inakuwa ni kubwa ambayo haiwezi kurudisha hata gharama zao, kitendo hicho kimefanya wafanyabiashara wa kawaida kuendelea kuwaumiza wananchi, lakini hakuna mwenye uwezo kipindi hiki, nasema walete mahindi ya bure siyo ya kununua tena,” alisema Mwaka.

Mbunge huyo alihoji ni kwa nini Serikali isiruhusu ghala la mahindi la Kizota, Dodoma kutoa mahindi kwa wafanyabiashara ili bei isiwe kubwa kama ilivyo sasa. Alisema bei ya sasa ya Sh15,000 kwa debe la kilo 20 ni kubwa na wachache ndiyo wanaoweza kuimudu.

Diwani wa Majeleko, Mussa Omari alifika kwenye kikao hicho akiwa na fumbili wengi akisema aliwakamata wakati akishirikiana na wapigakura wake kupata kitoweo.

Hata hivyo, hakuna diwani aliyeonyesha mshangao kwani kila mmoja alisema hata kwake wanakula wadudu hao na ni jambo la kawaida.

Mussa alisema hali ni mbaya zaidi kwenye kata yake na tayari baadhi ya watu wameanza kuvimba miguu kwa kukosa chakula, huku kukiwa na taarifa za vifo vinavyosadikiwa kuwa vimetokana na watu kukosa lishe.

Diwani wa Zajilwa, Farida Maulidi alisema katika eneo lake, kuna kaya 10 ambazo zimeelemewa zaidi na tayari kuna taarifa za vifo viwili. “Kwangu hali ni mbaya sana yaani naomba tuandamane kwenda hata kwa mkuu wa mkoa au niungane na wenzangu twendeni Ikulu tukamuone Rais.

Mbona, pamoja na kusema hakuna mtu atakayekufa kwa njaa, huku watu wanateketea na sisi tupo? Kila siku nafanya kazi ya kutafuta uji kunusuru maisha ya watu wangu,” alisema Maulid.

Ofisa kilimo wa wilaya hiyo, Godfrey Mnyamale alikiri kuwa hali ni mbaya wilayani Chamwino na kusema kama juhudi za makusudi hazitachukulia ndani ya wiki moja, kutakuwa na madhara makubwa.

Mnyamale alisema tatizo kubwa lililoikumba Chamwino ni mvua kidogo zilizonyesha msimu wa mwaka jana iliyosababisha watu wasivune chakula cha kutosha.

Alisema ili kukabiliana na njaa iliyoanza wilayani humo tangu Aprili mwaka jana, jumla ya tani 14,377 za mahindi zinatakiwa kwenye vijiji 107, lakini hadi sasa Serikali imepeleka tani 150 tu ambazo ziligawiwa katika vijiji 10 tena kwa idadi ndogo.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa alisema Serikali haijalala katika kuwaza namna ya kuwasaidia.

Galawa alisema katika kipindi kilichopita, Chamwino ilipewa msaada wa chakula lakini kilikuwa hakitoshi na ndiyo sababu hakikupelekwa maeneo yote.

“Hata hivyo, lazima watu wajue kuwa huwezi kuomba chakula leo na ukapewa leo. Leo kamati ya mkoa imeshapeleka maombi taifa na juzi niliongea na mhusika kwamba wanalifanyia kazi,” alisema Galawa.

Kuhusu wafanyabiashara kulazimishwa kununua mahindi Songea badala ya Dodoma, alisema jambo hilo liko nje ya uwezo wake kwa kuwa wenye kuwapangia ni mamlaka ya chakula.

Aliwataka wanasiasa kuacha kukuza mambo kuwa kuna watu wamekufa kwa njaa, badala yake watumie muda huo kuwahamasisha wafugaji kuuza mifugo na kununua chakula.

Maalim Seif Sharif Hamad Kupasua JIPU Leo Saa Tano Asubuhi

0
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif  Hamad, leo  anatarajia kufichua siri ya mazungumzo ya kusaka suluhu, baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kufutwa mwaka jana.

Maalim Seif,  anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari  leo saa tano asubuhi kueleza hatima ya mazungumzo ya kisiasa ya kutafuta mwafaka Zanzibar

“Maalim Seif kesho (leo), atazungumza na wahariri na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano Zanzibar,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana.

Seif anachukua uamuzi huo wakati hali ya kisiasa visiwani humo ikizidi kuwa ngumu kwa pande zote, licha ya Rais Dk. John Magufuli kuahidi kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Maalim Seif anajitokeza leo, wakati wiki iliyopita Rais Magufuli  alikutana na  viongozi wastaafu, ambao kwa pamoja walizungumza mambo mazito ya kitaifa pamoja na kutakiana heri ya mwaka mpya.

Wiki iliyopita Rais Dk. Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye alimhakikishia kumpa ushirikiano atakapohitajika kufanya hivyo.

Katika kumhakikishia kuwa yuko tayari kufanyakazi atakayomtuma, taarifa za ndani zinaeleza kuwa moja ya jambo kubwa ambalo Mkapa anaweza kulisimamia ni suala la kusaka suluhu ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya mazungumzo hayo, Mkapa alisema lengo la mkutano huo ni kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa dhamana aliyopewa na Watanzania na kumtakia heri ya mwaka mpya.

Mkapa alimhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote na kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Licha ya Mkapa, Rais Magufuli pia alikutana na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, ambaye alikabidhi baadhi ya nyaraka kwa Rais Magufuli.

Kikwete alikabidhiwa nyaraka hizo zinazohusiana na mgogoro huo na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, Novemba 4, mwaka jana.

Inaelezwa kuwa Maalim Seif alikabidhi nyaraka mbalimbali, zikiwamo fomu za matokeo ya Uchaguzi  Mkuu kwa vituo vyote vya Zanzibar.

Askofu Kanisa La Anglikana Atimuliwa kwa Ufisadi wa Mamilioni ya Pesa

0
0
KANISA la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) lililopo jijini Mwanza, limemtimua rasmi Askofu kanisa hilo, Boniface Kwangu, kutokana na ubadhilifu wa zaidi ya Sh. 600 milioni.

Askofu huyo ni wa pili kutimuliwa na uongozi wa kanisa hilo baada ya mwaka 2007 aliyekuwa Askofu wa dayosisi hiyo, John Changae na yeye kufukuzwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kitendo ambacho kinaonesha taswira mbaya kwenye kanisa hilo.

Pia Askofu Kwangu aliyedumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minane, katika uongozi wake alishawahi kutuhumiwa na waumini wake kuwa anajihusisha na dini ya Freemasons huku wengine walikuwa wakimtuhumu kwamba anatumia nguvu za giza.

Askofu Kwangu na wenzake wanne wanatuhumiwa na kanisa hilo kwa ubadhilifu wa zaidi ya Sh. 600 milioni pamoja na kuendesha kanisa hilo bila kufuata kanuni na taratibu za kanisa hilo kitendo ambacho kimesababisha kutimuliwa kwake.

Askofu Kwangu, anatuhumiwa na upotevu wa Sh. 500 milioni ya shule ya kimataifa ya Isamilo, kuuza gari la dayosisi hiyo, kufukuza wafanyakazi wa kanisa hilo na kusababisha wadaiwe Sh. 60 milioni, kujipatia kiasi cha zaidi ya Sh. 15 milioni kutoka kwa Mhasibu wa kanisa, Sam Wisa, bila kibali.

Akisoma tamko la kumfukuza kazi, Mwenyekiti wa Nyumba ya Wadumu kutoka DVN, Andrew Kashilimu, amesema askofu huyo ameisababishia hasara kanisa hilo zaidi ya Sh. 600 milioni, kutokana na kufanya kazi bila kufuata kanuni na taratibu.

Amesema kuwa askofu Kwangu amekiuka viapo vya uaskofu, katiba ya jimbo, katiba ya DVN na amekiuka maadili na kanuni, kuendekeza matabaka ndani ya wahudumu na waumini, kutoa ajira ndani ya DVN kinyume na taratibu za kanisa.

Amesema katika kikao kilichoketi Septemba 1 mwaka jana, kilithibitisha mambo hayo na kukubaliana kwamba Askofu huyo ajiuzulu kwa afya ya kanisa la Mungu lakini alikaidi maagizo hayo mpaka kutoka kwa tamko hilo.

“Askofu (Boniphace Kwangu) ametumia vibaya madaraka yake na alikuwa anatumia vibaya mali na fedha za kanisa, kwa hali hiyo tusingeweza kuwa na kiongozi wa namna hiyo,” amesema Kashilimu.

Mmoja wa waumini ambaye alikumbwa na fagio la Askofu, Kwangu, Edwar Kibiti, amesema kwamba kutimuliwa kwa kiongozi huyo wa kiroho katika kanisa hilo kutasaidia kurudisha matumaini kwa waumini walio wengi.

Kibiti ambaye pia ni Mchungaji amesema kuwa walipokuwa wakijaribu kuhoji sababu za Askofu Kwangu kuuza mali za kanisa ikiwamo gari alilochangiwa na waumini alikuwa akiwafukuza watu waliotaka kufahamu suala hilo.

“Tulipokuwa tunahoji matumizi ya mali za kanisa tulichokuwa tukiambulia ni kwenda polisi na wengine wafukuzwa, huyu (Askofu Boniphace Kwangu) alikuwa anafanya kazi kwa majungu na mpaka anaondoka alishafukuza wachungaji 19,” amesema Kibiti.

Amesema kuwa baada ya askofu huyo kuona wachungaji wazawa wanaanza kumfuatilia alianza kutafuta wachungaji wengine kutoka nchi mbalimbali hususani kutoka Rwanda, ili kuficha maovu yake anayoyafanya.

Mmoja wa Waumini, Joycelyn Juma, amesema kilichomgharimu askofu huyo ni upungufu wa mambo ya kiuongozi ambayo yamechangia kusababisha kuwepo kwa mwanya wa wizi wa mali na fedha za kanisa hilo.

“Kiufupi nimefurahi sana kwa sababu mambo ya ufisadi ama wizi wa fedha haviendani na mambo ya Mungu na nimefurahi kuona suala hili limefikia mwisho na sasa tutakuwa na amani,” amesema Juma.

Sanjali na kufukuzwa kazi ya Uaskofu DVN, pia uongozi wa kanisa hilo limemfungulia kesi Askofu Kwangu na wenzake wanne, Katibu wa Bodi, James Mtaritinya, Mhasibu wa Shule ya Isamilo, Sam Wisa, Samson Maganga na John Magawa.

Kesi iliyofunguli ni Januari 10 mwaka huu, Mw/Rb/265/2016 ambalo ni jalada la uchunguzi kwa watuhumiwa.

Nikipata mwanamke atakayeweza kuziba nafasi ya Shilole ndio nitafuta tattoo zake – Nuh Mziwanda

0
0
Ingawa Shilole tayari amefunika tattoo aliyochora kifuani yenye jina la ex wake Nuh, kwa kuongeza mchoro wa ua juu yake baada ya wawili hao kuachana, Nuh Mziwanda amesema yeye bado hajaamua kufuta tattoo zake.

Nuh ambaye alichora tattoo mbili, moja ikiwa na jina la Shishi Baby na nyingine ikiwa na sura ya Shishi amesema kuwa endapo atapata mwanamke wa kuziba pengo la Shishi ndio atafuta tattoo hizo.

“Mimi sijatoa hii tattoo sababu sijapata bado mwanamke ambaye anayeweza ku-cover nafasi ya yule mwanamke, nikipata mwanamke ambaye ataweza kucover nafasi ya yule mwanamke, akinishawishi kweli kuona anatabia ambazo mimi nazitaka basi…” alisema Nuh kupitia AYO TV.

Nuh aliendelea kueleza sababu za yeye kuchora tattoo za Shishi kwenye mwili wake.

“of-course yule mwanamke mimi nilimpenda kweli na mimi ndio nilianza kuchora tattoo kwake yeye so I was real, nilichora tattoo kwa mapenzi sikuchora kwasababu ya. Unajua ukichora tattoo kwasababu ya inamaanisha moyoni unakuwa unaumia unatamani ile tattoo uitoe ndio maana hata yeye (Shishi) aliweza kuibadilisha ikawa ua. “.


Chanzo cha ugomvi kati ya Shilole na Nuh Mziwanda kilichopelekea penzi lao kuvunjika kimeendelea kubaki kuwa siri yao, kutokana na wote kutotaka kukisema licha ya Shishi kuweka wazi kuwa Nuh ndiye mkosaji.

“Sipaswi kusema kitu gani kimetokea au kipi ambacho kimefanya mimi na bibie tuweze kutengana kwasababu ni maisha. Katika maisha kuna kupata na kukosa kwahiyo unaweza ukampata mtu na ukamkosa mtu, so kuachana ni kitendo cha kawaida tu ambacho kipo katika maisha yetu ya kila siku.” Alieleza NUh.

“Kama yeye anasema mimi ndio nimemkosea its okay all in all najua Mungu yupo na anatuangalia sisi binadamu tunafanya nini, mimi mama yangu kanifundisha kaniambia mtoto wa kiume hutakiwi kuongea, mtoto wa kiume unasifiwa kazi, kwahiyo kama yeye anasema mimi ndo nimemkosea its okay ila moyo wake unajua kitu gani kinaendelea.” Alisema Nuh Mziwanda ambaye amekuwa kwenye uhusiano na Shishi kwa miaka mitatu.

Breaking News:Mtoto wa Marehemu Nyerere ..Leticia Nyerere Afariki Dunia

0
0
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia Nyerere amefariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland jana saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki..

Leticia aliolewa kisha kutengana na mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere mwaka 1996, ambapo walifanikiwa kupata watoto watatu.

Leticia alikuwa mtoto wa Mzee Musobi Mageni. Julai 27 2015, Leticia alitangaza kuihama CHADEMA na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mungu ailaze roho ua Marehemu mahali pema peponi,
Amina

Maalim Seif Sharif Hamad Aongea Na Waandishi wa Habari.....Asema CUF Haiko Tayari Kurudia Uchaguzi Zanzibar

0
0
Hatimaye, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ametoa msimamo wake na chama chake kufuatia mazungumzo ya siri ya kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa unaotokana na tangazo la kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika hotel ya kitalii ya Serena jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amesisitiza kuwa hoja ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar kama inavyoelezwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), haina msingi, haikubaliki na sio halali kikatiba.

“Hoja ya kurudia uchaguzi haina msingi, haina uhalali, ni hoja ambayo inaweza kuzaa fujo na vurugu na inaweza kuleta mzozo mkubwa wa kikatiba wa kisheria. Sidhani kama tunataka kuwapeleka huko watanzania,” alisema Maalim Seif.

Makamu huyo wa kwanza wa rais wa Zanzibar ameeleza kuwa tayari wameshafanya vikao nane vilivyowashirikisha wagombea urais pamoja na marais wastaafu wa Zanzibar lakini hawakukubaliana kurudia  uchaguzi kama baadhi ya viongozi wa CCM walivyoeleza.

Aidha, Maalim Seif amekanusha kilichoelezwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd baada ya kukutana na Rais John Magufuli, kuwa rais alisema warudie Zanzibar kujiandaa na marudio ya uchaguzi kwani rais hakusema hivyo alipokutana naye.

Maalim Seif amesema kuwa ana imani kubwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika kuleta maridhiano na ufumbuzi wa mgogoro wa Zanzibar kutokana na mazungumzo aliyofanya naye hivi karibuni katika Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa endapo uchaguzi mkuu utatakiwa kurudiwa, zipo changamoto nyingi za kikatiba ambazo zitakwamisha zoezi hilo hivyo uchaguzi huo hautawezekana.

Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupitishwa kwa fedha za kugharamia uchaguzi na baraza la wawakilishi ambalo hivi sasa halipo kwa kuwa limefikia ukomo wake.

Mbali na hilo, Maalim Seif alieleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu kwa kutoa tamko lisilo halali la kufuta uchaguzi huo huku akifahamu dhahiri kuwa hana nguvu hiyo kikatiba.

Ameitaka ZEC iongozwe na makamu mwenyekiti wake kwa mujibu wa katiba pamoja na wajumbe wengine kukamilisha utaratibu wa kuhakiki matokeo ya uchaguzi na kumtangaza mshindi.

Maalim Seif ameeleza kuwa anafahamu dhahiri kuwa kuna mpango wa kutangaza kwa nguvu marudio ya uchaguzi Februari 28 mwaka huu, lakini yeye pamoja na chama chake hawatakubali.

Ukishindwa Kumnyonyesha Mtoto Miezi Sita Bila Kumpa Kitu Chochote, Andaa Pesa ya Tuition

0
0
Jamani kumekuwa na tabia ya watu kuwa busy na kushindwa kuwanyonyesha watoto kwa miezi sita bila kuwapa kitu chochote, hili ni kosa na tatizo kubwa sana kwa jamii.

Utafiti unaonyesha watoto wanaonyonyeshwa miezi sita bila kula kitu chochote wanakuwa na kinga imara dhidi ya magonjwa na ubongo mkubwa ukilinganisha na wale wanaoanza kupewa chakula au maji kabla ya muda huo.

Andaa pesa ya tuition kama utashindwa kumnyonyesha mtoto miezi sita mfululizo bila kitu chochote hata kama umempeleka international schools.

Wanawake msiwe busy sana na kazi na kusahau wajiu wenu wa malezi. Lakini pia ni vyema wenza kujipanga vizuri kabla ya kuzaa mtoto ili akizaliwa apate malezi mazuri.

Ukitaka mtoto mmwenye afya imara na akili nyingi anza kwa kumuandaa mke wako kabla ya kumpa mimba na pia lea mimba kwa upendo na uaminifu mkubwa. mkinge mkeo na magonjwa yanayozuilika akiwa mjamzito. Baada ya mimba mpe malezi mazuri akizaa mpaka miaka miwili kwa maana ya chakul.

Nawaasa watu kuuiga pia utamaduni wa wachaga katika kulea mke akizaa na utamaduni wa wairaq katika kulea mimba..

Mdogo Wake Mke Wangu Anataka Kunifuta Machozi

0
0
Nimeoa mwaka 2009 na tumebahatika kuzaa watoto wawili.Kwa hivi sasa ndoa yangu imeyumba zaidi kwani unyumba ninapewa kwa mwezi mara mbili tena kama msaada.

Kuna dalili zote mke wangu amepoteza mvuto na mimi kwani hata nikihitaji penzi amekuwa unwilling, lakini mke wangu ana mdogo wake wa kike ambaye ni robo tatu mama mwenye nyumba kwasababu anafanya kila kitu nyumbani.

Mke wangu yeye akitoka kazini ni kusingizia amechoka basi nikuwasha Tv kuangalia tamthilia ni takribani miezi miwili sasa, uhusiano wetu na mdogo wake ulianza kuchukua sura mpya ile tabia ya kuniwekea chakula mezani imehamia kuniletea chumbani cha ajabu leo asubuhi kaja kunidekia chumbani na night dress dada yake akiwa kazini.

Moyo wangu kama binadamu umeanza kumuangukia na alichonieleza dakika ishirini zilizopita ni kwamba dada leo atalala msibani nyumba ya pili kwa hiyo atakuja kulala kwangu nimepigwa na butwaa.

NAOMBENI USHAULI NIMKEMEE PEPO AU NIFUTWE MACHOZI

Breaking News: Huyu Ndio Mchezaji Bora wa Dunia Aliyetangazwa Usiku wa Leo

0
0
Kura walizopata katika kinyang'anyiro cha Tuzo ya Mchezaji Bora Dunia 2015

1.Lionel Messi 41.33 %

2.Cristiano Ronaldo 27.76 %

3.Neymar Jr 7.86 %

Mzimu wa Dr Slaa Waitikisa Tena Chadema...Mambo Mazito Yaelezwa

0
0
Wakati baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakihitimisha jana vikao maalum vya kila mwaka kujadili yale waliyofanya katika mwaka, imefahamika kuwa sifa walau tisa anazotakiwa kuwa nazo mrithi wa Dk. Willibrod Slaa, kwa nafasi ya ukatibu mkuu ni miongoni mwa mambo mazito yanayopasua vichwa vya baadhi ya wengi ndani ya chama hicho.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema jana, ilieleza kuwa viongozi wa juu wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, walikuwa wakiendelea na vikao vyao mjini Moshi, Kilimanjaro hadi jana jioni kwa ajili ya tathmini kuhusu mwaka uliopita na ushiriki wao katika uchaguzi mkuu uliopita na pia kuangalia mambo gani ya kufanya katika kipindi cha kuanzia sasa hadi uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020Kadhalika, ajenda kuhusu jina la katibu mkuu ilipata nafasi huku jina la waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, liking’ara kwa kupendekezwa na wengi ili lipelekwe kwenye vikao vya juu vya uamuzi. 

Sumaye alijiunga rasmi Chadema hivi karibuni akitokea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambako jina lake liliondolewa wakati wa mchakato wa kuwania urais ndani ya chama hicho tawala. 
Jitihada za mwandishi kumpata Mbowe jana kuelezea yanayojiri kwenye kikao chao, ikiwamo harakati za uteuzi wa jina la katibu mkuu, zilishindikana kwani hadi jioni, bado kikao chao kilikuwa kikiendelea huku ikielezwa kuwa simu za viongozi wote wa juu (akiwamo yeye) ziliwekwa mbali na wajumbe hao.

“Ni vigumu kumpata Mbowe wala viongozi wengine wa juu kwa sasa kwa sababu wamejifungia kwa ajili ya kikao na simu zao ziko mbali na wao… ila kwa ufupi, jina la Sumaye bado linatawala katika mjadala kuhusu katibu mkuu wa chama,” mmoja wa viongozi wa Chadema alimweleza mwandishi jana kwa sharti la kutoandikwa jina.
Kabla ya kikao cha jana kilichotarajiwa kuhitimisha mfululizo wa vikao vilivyoanza wiki iliyopita, ilielezwa kuwa ajenda kubwa ni tathmini ya mwaka uliopita na pia kujadili watakayofanya mwaka huu.

“Vikao hivyo vinaendelea kufanya tathmini na uchambuzi wa mpango kazi wa mwaka 2010-2015 na kupanga kwa ajili ya 2016-2020 kabla ya kuwasilisha kwenye vikao vya uamuzi kwa mwaka huu, ambavyo vitafanyika kwa mujibu wa utaratibu wa kikatiba,” ilisema sehemu ya taarifa ya Chadema kwa umma kuhusiana na vikao hivyo mjini Moshi.
Wakati mfululizo wa vikao hivyo ukifikia tamati jana, imefahamika kuwa harakati za kumpata mtu mwenye sifa za kuwa katibu mkuu wa chama hicho kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Slaa bado ni kitendawili.
Chanzo kutoka ndani ya Chadema kiliiambia Nipashe kuwa uteuzi wa jina la mtu atakayerithi mikoba ya ukatibu mkuu uliokuwa ukishikiliwa na Slaa, unavuta hisia za wengi kwa kuwa ni nafasi muhimu kwa mustakabali wa chama na kwamba jambo hilo limeongezeka umuhimu sasa kutokana na ukweli kuwa chama kimekuwa kikubwa zaidi na kuungwa mkono na mamilioni ya Watanzania. 
Katika uchaguzi mkuu uliopita, mgombea wa Chadema, Edward Lowassa, aliyekuwa akiungwa mkono pia na muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 39.97 ya kura zote halali zilizopigwa huku Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiibuka mshindi kwa kupata asilimia 58.46.

“Sumaye amekuwa akitajwa sana. Lakini kwa ufupi ni kwamba jina la mrithi wa Slaa (Katibu Mkuu) linasubiriwa kwa hamu kubwa. Hii ni nafasi nyeti kwa chama kikubwa kama Chadema, hivyo haishangazi kusikia wengi wakifuatilia ili kujua ni nani atakayekuwa na sifa za kukamata usukani huo,” chanzo kimoja kiliiambia Nipashe mwishoni mwa wiki.

Dk. Slaa aliitumikia Chadema katika nafasi ya ukatibu mkuu kuanzia mwaka 2002 hadi Julai, mwaka jana, wakati uongozi wa juu wa chama hicho uliporidhia kuwa apumzishwe na kisha yeye mwenyewe kutangaza baadaye kuwa amejiuzulu na kustaafu siasa, akipinga uteuzi wa Lowassa kuwa mgombea urais wa chama hicho.

Tangu Slaa alipokosekana katika nafasi hiyo, Chadema bado haijatangaza mrithi wake na nafasi yake imekuwa ikikaimiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Zanzibar), Salum Mwalimu.
“Hakuna sababu ya kujaza nafasi hiyo (katibu mkuu) haraka… ni lazima uongozi wa juu uwe makini zaidi kwa sababu chama ni kikubwa hivyo changamoto zake ni kubwa pia. Mtu anayeteuliwa kushika nafasi hiyo ni lazima achunguzwe kwa undani ili kujiridhisha kuwa kweli ana sifa zinazostahili,” chanzo kingine kilisema.
SIFA NANE MUHIMWakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki, baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema walitaja sifa takribani nane kuwa ni sehemu ya zile anazopaswa kuwa nazo mwanachama yeyote atakayekuwa katibu mkuu wa chama hicho na kukiwezesha kupiga hatua zaidi katika kipindi hiki chenye ushindani mkubwa wa kisiasa.
Baadhi ya wale walizoungumza na Nipashe na kutaja sifa hizo , kwa mtazamo wao, na ambazo jumla yake ni nane, ni pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Prof. Mwesige Baregu; Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya ya Arumeru, Samweli Nnko na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, Vincent Nyerere.
“Chama kina taratibu zake, miongozo yake, kanuni, katiba na sifa…mambo hayo ndiyo hufuatwa katika kumpata kiongozi wa nafasi hiyo (katibu mkuu), “ alisema Prof. Baregu kabla ya kutaja sifa anazoona kuwa zinafaa kuangaliwa kwa mtu anayeshika nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Baregu, sifa mojawapo ni kwa mtu huyo kuwa na uelewa mpana si tu wa mambo ya Chadema, bali na vyama vingine vya siasa nchini. Awe mzoefu wa kutosha kwenye uwanja wa siasa na pia awe mvumilivu kwa kuwa madongo ya kiasiasa yanayotupwa mengi huelekezwa kwa Katibu Mkuu.
Baregu alisema kuwa pili, awe mzuri katika kushirikiana na wengine kwa kuwa anaweza kuwa Katibu Mkuu anayejiamulia mambo peke yake bila kuwashirikisha wengine na hilo halipaswi kutokea kwa sababu mawazo ya wengine yanaweza kuwa mazuri katika kukisaidia chama.
Sifa ya tatu ina uhusiano na ya pili. Kwamba, katibu mkuu ajaye wa Chadema ni lazima awe msikivu na hapaswi kuwa mbishi au anayefikiria anayoamini yeye ndiyo sahihi na si ya wengine. Ni lazima awe na uwezo wa kusikiliza wengine kwani ni kawaida ndani ya vyama kuwa na malumbano na tofauti za hapa na pale, matukio ambayo baadhi ya watu huyatafsiri tofauti na yeye (katibu mkuu) awe wazi kupokea maoni ya watu tofauti na kuyapa nafasi.

Nne, katibu mkuu ajaye Chadema awe na uwezo wa kuunganisha watu wote ndani ya chama kwa kuhakikisha kuwa wanaweka kando tofauti zao kwa maslahi ya chama.
Sifa ya tano kwa katibu mkuu ajaye ni kwamba, awe mtu asiyehodhi mawasiliano bali kueneza. Katibu mkuu ajaye aeneze habari na uelewa ndani ya chama.Sifa nyingine muhimu (ya sita) ni kuwa muumini wa kuzingatia weledi na kutenda haki. Kwamba, maamuzi yanayofanywa na kamati anazosimamia yafanywe kwa weledi na kutoa haki kwa kila upande
Nnko kwa upande wake, anataja sifa nyingine anayoamini kuwa ya lazima kwa katibu mkuu ajaye ni uzoefu wa siasa utakaomwezesha kukuza shughuli za chama

CCM Wajibu Mapigo Zanzibar.......Wasema Uchaguzi Lazima Urudiwe

0
0
Muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia Uchaguzi uliofutwa kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametangaza kuwa uchaguzi  huo lazima urudiwe.

Wakizungumza jana na vijana wa chama cha Mapinduzi katika viwanja vya Maisara waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya matembezi ya kuunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar,viongozi wa juu wa chama hicho walisisitiza kuwa uchaguzi wa Zanzibar upo pale pale na utarudiwa kadiri tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itakavyotangaza.

Wa kwanza kutoa msimamo huo alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, aliyesema kuwa uchaguzi huo utarudiwa hata ikiwezekana vyama vyote vikijitoa CCM kitashiriki peke yake

“Uchaguzi wa marudio upo pale pale, tunajua uchaguzi ulifutwa kihalali, mjitayarishe kwa uchaguzi wa marudio. CUF wamesema watatumia nguvu ya umma, tunawakaribisha na wataona matokeo yake” alisema Balozi Iddi.

Katika mkutano huo uliokuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ZBC, Dk  Alli Mohamed Shein alipongeza msimamo wa Balozi Iddi, na kusema atabaki kuwa rais hadi uchaguzi utakaporudiwa.

Dk Shein alisema yupo madarakani kwa kushauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwamba hajavunja katiba na kama itatokea mahakama ikatoa ufafanuzi kuwa anakosea kuwepo hapo kikatiba basi ataondoka madarakani

“Mahakama ikisema nakosea nitaondoka, Rais yupo Baraza la Mapinduzi lipo na Mawaziri wapo, nitaita waandishi wa habari Ikulu na mimi nimjibu Maalim Seif kwani kuna mengi amenisingizia” alisema

UVCCM Zanzibar Kimenuka..Yataka Rais Mstaafu Abeid Karume afukuzwe CCM

0
0
UVCCM yataka Rais mstaafu afukuzwe CCM

UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umekitaka chama hicho kumvua uanachama Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume. 

Kauli hiyo imetolewa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis wakati wa kilele cha matembezi ya vijana wa umoja huo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi.

Alimshushia tuhuma nzito mstaafu huyo kuwa anashirikiana na wapinzania kukihujumu chama hicho kikongwe nchini, na kwamba asipofukuzwa umoja hup umoja huo utatumia njia zingine ambazo hakuziweka wazi.

Sadifa alionya kwamba Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar si mali wala miliki ya mtu kwani Wazanzibar wote wana haki ya kushiriki kuyaenzi kwa vitendo kutokana na historia yake.

Source:Jamii Forums

Udaku Special Blog

Rais Magufuli Amjulia Hali Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Aliyelazwa Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbili Januari 11,2015

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Frederick Sumaye ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Frederick Sumaye alilazwa katika Taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika Taasisi hiyo.

Pamoja na kumpa pole, Rais Magufuli pia amemuombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.

Akizungumza mara baada ya kuonana na Rais, Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye amemshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kumuona na kueleza kuwa kitendo hicho kimeonesha jinsi alivyo na upendo wa dhati na anavyowajali watu wake.

Kuhusu hali yake, Mheshimiwa Sumaye amesema anaendelea vizuri, anapata matibabu mazuri na kwamba kwa kuwa hali yake ni nzuri anatarajia kuruhusiwa kuondoka hospitali hapo baada ya muda mfupi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016

Breaking News:Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Apewa Masaa 48 Ya Kujieleza

0
0
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Mazingira na Muungano) Luhaga Mpina amempatia saa 48 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kujieleza sababu za Jiji la Mwanza kuwa chafu.

Mpina alisema hayo jana jijini hapa wakati akieleza mambo aliyoyabaini wakati wa ziara yake ya siku mbili jijini Mwanza.

Alisema licha ya serikali kutangaza suala la usafi kuwa ni hoja ya kitaifa, Jiji la Mwanza linatisha kwa uchafu wa mazingira.

Mpina ambaye alianza ziara jana kukagua maeneo mbalimbali ya jiji, alisema uchafu wa jiji kwa kiwango kikubwa unachangiwa na baadhi ya watendaji wa Serikali na wataalamu, kutowajibika vyema.

“ Ni sehemu ndogo tu ya uchafu wa jiji la Mwanza unaochangiwa na wananchi, kutokana na hali hii nilivyoiona ninampatia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo masaa 48 ajieleze ni kwanini jiji la Mwanza ni chafu ilihali lina watendaji wa kutosha na wataalamu”, alisema.

Alisema Januari 30 mwaka huu atarudi jijini Mwanza, kushiriki usafi na wananchi kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano.

Udaku Special Blog

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akutana na Mbwana Samatta Dar na Kumpongeza kwa Kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora

0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametembelewa ofisini kwake na mwanasoka bora Afrika kwa wachezaji wa ndani Mbwana Samata leo asubuhi  na kufanya nae mazungumzo ikiwa ni sehemu ya kumpongeza kwa mafanikio hayo makubwa ambayo Mbwana ameyapata na heshima kubwa aliyoiletea Taifa kwa ujumla.

Baada ya mazungumzo hayo Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, Mbwana Samata pamoja na Muenezi wa CCM ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia mafanikio ya Samata na kusema wao kama Chama tawala wamepokea  ushindi wake kwa furaha kubwa

Udaku Special Blog

Lowassa Azidi Kuchanua,Aonekana Mwenye Furaha na Afya Njema Ndani ya CHADEMA

0
0
Wale wote waliokuwa wakimtakia mabaya rais wa mioyo ya watu Mh lowassa sasa wanaumbuka.
Lowassa anazidi kuchanua na afya inazidi kuwa ya ujana,tofauti na alivyo kuwa Ccm
Hii inamanisha alipo sasa lowassa ni sehemu sahihi zaidi ya alipotoka.Sifa na heshima kubwa ziwaendee mama lowassa na Mwenyekiti Freeman na wana Ukawa wote
Ukawa kwa afya!

Udaku Special Blog

Shilole: Msisikilize uzushi, kama nikipata mpenzi mpya nitasema mwenyewe

0
0
Shilole a.k.a Shishi Baby amesema baada ya kuachana na Nuh Mziwanda bado jimbo la moyo wake halijapata mgombea mpya wa kuziba nafasi yake.

Zimekuwepo tetesi kuwa Shishi anatoka na msanii mwingine wa Bongo fleva, Nyauloso zamani Bonge la nyau, huku wengine wakisema kuwa ana uhusiano na msanii wa Uganda, Eddy Kenzo.

Mimi sijapata mpenzi mpya mimi nipo tu, mpenzi mpya nitasema mwenyewe kwa mdomo wangu mimi,” Shishi ameeleza kupitia 255 ya XXL. “ nifanye interview niseme jamani sasa nina mpenzi mpya, lakini saizi msisikie rumors zinazotokea subirini mimi niwahakikishie.” Alisema Shishi.

Kuhusu Eddy Kenzo Shishi amedai kuwa ni kama kaka yake lakini wanawasiliana sana, na kuongeza kama endapo urafiki wao utazaa penzi basi atatangaza rasmi.

Polisi Wasema Benki za Tanzania Zimeajiri Majambazi..Mengi Yaibuka

0
0
Baadhi ya benki nchini zinadaiwa kuajiri baadhi ya wafanyakazi walio kwenye mtandao wa majambazi kutokana na wateja wengi kupigwa risasi na kufa wakitoka kuchukua pesa, uchunguzi wa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi Tanzania umebaini.

Hayo yalisemwa na baadhi ya askari hao wiki iliyopita walipozungumza na mwandishi wetu na kusema kwamba, waajiri wasipokuwa makini katika kuajiri watashangaa kuona wateja wao wanapigwa risasi na kuuawa kila kukicha.

“Haiwezekani kuwa wanaonyang’anywa fedha ni wale wanaotoka kuchukua benki kuliko wanaopeleka! Ina maana wezi wapo katika baadhi ya mabenki hivyo kunatakiwa kuwepo na umakini wakati wa kuwaajiri,” alisema askari mmoja kutoka makao makuu ya jeshi hilo, Dar akiomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji.

Afande huyo aliendelea kusema kuwa, baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa benki hizo wanapoona mteja anachukua fedha nyingi hufanya mawasiliano kwa njia ya simu kuwaeleza majambazi walio nje namna alivyovaa mteja huyo na kiasi cha fedha alichochukua.
Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa, endapo hali hiyo haitadhibitiwa haraka huenda wananchi wakapatwa na hofu ya kuweka fedha zao benki kwa kuogopa kuporwa na kupigwa risasi wakienda kuzichukua.

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Simon Sirro (pichani) ambapo alikiri kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wenye mtandao na majambazi huku akisema jeshi lake limeweka mikakati kuhakikisha mtandao huo unasambaratishwa mara moja.
“Ni kweli kwamba, baadhi ya mabenki, si yote, yameajiri baadhi ya wafanyakazi, si wote wenye mtandao na majambazi. Kwa hiyo hata wao ni majambazi tu.

“Sasa tumejipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kukamata pikipiki zinazohusika katika uhalifu. Pia tumeamua kuweka makachero nje na ndani ya mabenki, wapo polisi wa miguu, pikip iki na magari. Nina uhakika tutawadhibiti,” alisema Kamanda Sirro.

Aliendelea kusema kuwa, majambazi waliopo katika Kanda ya Dar es Salaam waanze kufunga virago kwani bila kufanya hivyo wajue watakamatwa wote na mtandao wao kumalizika. Pia aliwataka wamiliki wa mabenki kuwa makini wakati wa kuajiri wafanyakazi ili kuwapata wenye sifa njema na kuweka imani kwa wateja wao.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova aliwahi kutamka kuwa, baadhi ya wafanyakazi wa ndani wa baadhi ya benki wana ushirikiano na majambazi. Akawatahadharisha wamiliki kuwa makini wakati wa kuajiri.

Mazito Yaibuka Ndoa Mpya ya Wastara...Ndugu wa Marehemu Sajuki Waangua Kilio

0
0
HAYA ni mazito! Nyuma ya shughuli ya kuolewa kwa staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma iliyofungwa Alhamisi iliyopita, kuna matukio ya kustaajabisha ambayo Ijumaa Wikienda limeyabaini.

Ndoa hiyo iliyofungwa kimyakimya, ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa mwigizaji huyo, Tabata-Barakuda, jijini Dar ambapo ilihudhuriwa na watu wachache tofauti na ilivyotarajiwa kutokana na umaarufu wa wanandoa hao.

NDOA ILIFUNGWA KWA SIMU
Imebainika kuwa, awali ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa kumi jioni na baadaye kuelezwa ilisogezwa mbele hadi saa 12 jioni, hata hivyo haikufungwa muda huo baada ya bibi harusi kuchelewa kufika akitokea saluni alikoenda kupambwa na kulazimika shehe afungishe ndoa hiyo kwenye simu wakati Wastara akiwa kwenye foleni barabarani.

BWANA HARUSI AGOMA KUPIGWA PICHA
Imeelezwa kuwa, baada ya bwana harusi kutinga na wapambe wake alitoa onyo kali huku likisisitizwa na wapambe wake kuwa hairuhusiwi kupiga picha na kutuma kwenye mtandao wowote wa kijamii kwa vile ndoa hiyo ilikuwa ya siri.

AGOMA KUMFUNUA BIBI HARUSI
Katika hali ya kushangaza, baada ya bibi harusi kuwasili aliingizwa katika chumba maalum kwa ajili ya kumsubiri mumewe na hata alipoingia ndani, shehe alimuomba amfunue mkewe ili kumhakikisha kama ndiye yeye kitu ambacho alikipinga na kudai hakuwa na shaka naye na kuomba waendelee na kitu kingine.

WASTARA ASHINDWA KUPATA MSOSI
Jambo lingine ambalo lilizua minong’ono ni Wastara kushindwa kupata muda wa kula chakula ambacho kiliandaliwa kwa sababu baada ya kumaliza kupiga picha za familia na kushikana mkono na mumewe, mumewe alimtaka waondoke huku akimwambia dereva wao awashe gari.

WADOGO WA SAJUKI WALIA
Katika hali ambayo haikuweza kufahamika mara moja, wadogo wa aliyekuwa mumewe wa pili wa Wastara, merehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Mohamed Kilowoko na Njegere Kilowoko waliangulia kilio kwa kile walichodai walikuwa na huzuni na furaha.


Prof. Ndalichako Awapiga Kitanzi Waliovurunda Elimu ya Tanzania na Kuingiza Siasa

0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, amewavisha kitanzi watendaji wa elimu walioamua mambo mbalimbali kwa shinikizo la kisiasa, kwa kuwapa muda wa kuyapitia upya ili kuyarekebisha yafuate weledi na taaluma.

Tangu mwaka 2013, wadau wa elimu wamekuwa wakilalamikia masuala ya kisiasa kuingizwa katika elimu na kusababisha kushushwa kwa viwango vya ufaulu na kuanzishwa kwa shule na vyuo visivyo na sifa.

Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Prof. Ndalichako alisema taasisi zote zimeanzishwa kwa sheria na hakuna mahali popote panapowataka viongozi wake kutumia maoni ya wanasiasa kufanya uamuzi.

“Taasisi zote zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Sitaruhusu siasa iingie kwenye taaluma kwa namna yoyote ile na kwa nafasi yangu kama wazirimkazi yangu si kutoa maagizo fanya hivi, anya vile’.

“Naamini hizi taasisi zina wataalamu wenye  weledi, kazi yao ni kufanya vitu vyenye masilahi kwa taifa. Labda niseme kwa nafasi yangu sitaruhusu mtu afanye uamuzi kwa msukumo wa kisiasa,  kwanza siasa anaipata kwa nani? 

“Wakati mwingine tunasingizia kuwa watu wanatuingiia. Atakuingilia  vipi wakati wewe ndiwe una utalamu na isitoshe hizi taasisi zote zimeanzishwa kwa sheria na zina taratibu  zinazoziongoza kufanya uamuzi. Hakuna sehemu inasema uchukue maoni ya wanasiasa kufanya uamuzi wako.

“Lakini kama mtu ameamua kufuata siasa ni hiari yake. Sheria  inataka weledi ufuatwe na siasa kwenye elimu haiwezi kuwa na nafasi. Kama changamoto zipo, zije tuzifanyie kazi, tusikimbie tatizo kwa sababu itakuwa haisaidii.

“Mimi nawapa changamoto wenyewe (watendaji wa elimu), kama walikuwa wamefanya uamuzi kwa shinikizo la kisiasa, sasa warudi waangalie weledi, wajitathimini na kuangalia taaluma zao.  Kama ni madaktari waangalie ili mtu awe daktari viwango vyake ni vipi, mainjinia (wahandisi) bora wanatakiwa waweje na vitu kama hivyo.

“Nataka kuwarudishia wao wenyewe na nimewaambia wajitizame upya. Hata TCU (Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania) niliwaambia waangalie upya vigezo vyao. Sasa kama kulikuwa na siasa nimewapa fursa ya kujirekebisha,” alisema Prof. Ndalichako.

Aliongeza kwamba: “Nimeaambia tukisema ni hapa wote tusimame hapa hakuna kuyumba na tutaelimisha Watanzania kwa nini tunafanya hivyo na najua tutakuwa na vigezo vinavyoeleweka.”

Aliwataka wananchi pia kutoingilia mambo yanayohusu taaluma zingine kwa kuwa kwa baadhi ya maeneo, kelele zao zinafanya baadhi ya wataalamu kufanya uamuzi usio sahihi.

MADARAJA YA UFAULU 
Kuhusu madaraja na uhalali wake, Prof. Ndalichako alisema maelezo yaliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk, Charles Msonde), alipotembelea wiki iliyopita hakuyaelewa na kuona si lazima mtu aseme mezani kila kitu.

“Watakapoleta maelezo yao Alhamisi (keshikutwa) ndipo nitaona kama ni kitu kizuri au kibaya na kama unaona pale niliwataka  wasitetereke kwenye utendaji.

“Tukipata sababu zao tutaangalia kulingana na sababu zilizotolewa nini kitafanyanyika. Mpaka sasa hatujajua, maelezo yao ndiyo yatatuambia,” alisema.

Mbali na mambo hayo, alisema licha upangaji wa madaraja ya ufaulu kwa kuangalia wastani wa alama (GPA), ambao wananchi wanaulalamikia, Necta imefanya vizuri kwenye maeneo mengi ikiwa ni pamoja na kuboresha mifumo ya utungaji mitihani, kuboresha mifumo ya utendaji kazi ya kielektroniki na kuanza kutoa vyeti mbadala kwa wahitimu ambao vyeti vyao vina picha pale vinavyopotea.

“Na kwa wale vyeti visivyokuwa na picha, bado wameendelea kutotoa vyeti mbadala. Badala  yake wanatoa ‘statement of results’ (karatasi maalumu ya matokeo) kwa sababu kwenye mambo ya vyeti kuna ‘umafia’ sana. Watu wanabadilishana vyeti na mambo kibao yapo huku,” alisema.

VURUMAI KWENYE ELIMU 
Vurumai kwenye mfumo wa elimu ilianza baada ya matokeo ya kitado cha nne ya mwaka 2012 kufutwa kutokana na ripoti ya Tume ya Profesa Sifuni Mchome, ambaye baada ya ripoti yake, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya kabla ya kuhamishwa na Rais John Magufuli kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Sheria na Katiba, baada ya kumteua Prof. Ndalichako kuongoza wizara hiyo.

Matokeo ya awali mtihani wa kidato cha nne ya mwaka 2012, yalionyesha kuwa watahiniwa waliopata kati ya daraja  kwanza mpaka la tatu ni  23,520 sawa na asilimia 6.4, daraja la nne watahiniwa  103,327 (asilimia   28.1) huku waliopata sifuri wakiwa  240,909 (asilimia  65.5).

Baada ya ripoti ya Prof Mchome kutaka matokeo hayo yafutwe na kupangwa upya, waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 35,349 (asilimia  9.54), daraja la nne 124,260 (asilimia 33.54) na waliopata sifuri wakawa 210,846 sawa na asilimia 56.92.

Wizara pia ilibadilisha utunuku wa ufaulu na kuanza kutumia GPA, badala ya jumla ya alama (division) iliyokuwa imezoeleka.

Mbali na uamuzi huo, wizara pia ilishusha alama za ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na sita ambapo sasa  A inaanzia 75 hadi 100,  B+ (60 hadi 74) B (50 hadi 59), C (40 hadi 49), D (30-hadi 39), E (20 hadi 29) na  F ni kuanzia 0 mpaka 19.

Alama zilizokuwa zikitumiwa awali kwa kidato cha nne ni  A (80 hadi 100),  B (65 hadi 79) C (50 hadi 64), D (39 hadi 49) na  F kutoka 0 hadi 34 huku kidato cha sita ikiwa A (80 hadi 100), B (75  hadi 79),  C (65 hadi 74),  D (55 hadi 64) E (45 hadi 54), S (40 hado 44) na F kutoka 0 hadi 39.

 KUONDOA 0  KUJA NA DIVISION V
Mwaka 2013, serikali ilitangaza kuwa kiwango cha pointi za kupanga madaraja kimebadilika na kwamba daraja la kwanza litaanzia pointi 7 hadi 17, daraja la pili (18 hadi 24), daraja la tatu (25 hadi 31), daraja la nne (32 hadi 47 na daraja tano (48 hadi 49).

Madaraja ya miaka ya nyuma yalikuwa pointi saba hadi 17 kwa daraja la kwanza, 18 hadi 21 daraja la pili, 22 hadi 25 daraja la tatu, 26 hadi 33 daraja la nne na 34 hadi 35 daraja la sifuri.

Sambamba na mfumo huo, serikali ilifuta mfumo wa zamani wa utunuku wa matokeo ambao ulikuwa wa jumla ya pointi (division) na kuleta wa wastani (GPA).

UHALISIA
Wakati serikali ikitumia nguvu nyingi kuficha uhalisia, matokeo ya mwaka 2012 yalikuwa hayana tofauti sana na yale ya mwaka 2011 ambapo asilimia 90 ya wanafunzi wa walipata madaraja ya nne na sifuri.

Pia kwa mwaka 2012, asilimia 93.6 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo, walipata madaraja ya nne na sifuri. 

“Niikukumbushe serikali kwamba Baraza la Mitihani lilibadilisha pia viwango vya ufaulu kwa kidato cha sita ambapo sasa kiwango cha chini cha ufaulu ni alama 40 hadi 44.

“Ni vizuri sasa serikali isisubiri matokeo yatoke ndipo ishtuke. Nashauri iwaamuru Necta watumie kiwango cha zamani cha ufaulu ili kuepuka usumbufu kama ulivyojitokeza kwa matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2012,” alisema Prof. Ndalichako.

Tanzania ilijiwekea historia
Kutokana na uamuzi ambao wadau wa elimu wanaamini ni wa kisiasa wa kushusha alama za ufaulu, Tanzania ilijiweka kwenye nchi zenyewe viwango vya chini zaidi duniani vya ufaulu.

Kabla ya kufutwa kwa matokeo ya mwaka 2012 na serikali kuja na kushusha alama za ufaulu, ilikuwa mwanafunzi akiopata 34 kushuka chini, inahesabika amefeli.

Kiwango hicho bado kilikuwa cha chini kulinganisha na mataifa mengine duniani ambayo mwanafunzi akipata alama 40 kushuka chini, anahesabika amefeli.

Nchi hizo ni pamoja na Ethiopia, Sudan, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Afrika Kusini, Ghana, Nigeria, Gambia, Liberia, Sierra Leone na Uganda. 

“Kwa hiyo utaona kwamba ni sisi peke yetu katika ukanda huu wa Afrika tuliokuwa tunatumia kiwango cha ufaulu cha alama 21, ambacho kwa kweli ni kidogo mno na ni udanganyifu ukilinganisha na nchi zingine za Afrika tunazofanana nazo,” alisema.
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images