Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Joto Kali Jijini Dar es Salaam Laibua Mambo Mazito...

$
0
0

Dar es Salaam. Magonjwa ya ngozi, kupungukiwa maji mwilini na maumivu ya kichwa ni kadhia zitakazowakumba baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kutokana na joto kali linalolikumba jiji hilo.

Tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa hali ya hewa katika jiji hilo hadi jana lilikuwa limefikia nyuzi joto 35.

Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA, Samwel Mbuya jana alisema joto la mwaka huu limevunja rekodi kwani kwa kawaida, kipindi cha Januari linatakiwa liwe nyuzi joto 32.

Mbuya alisema joto hilo pia limeongezeka hata kwa upande wa Zanzibar ambako limefikia nyuzi joto 35 ikiwa ni ongezeko la asilimia mbili.

Alisema sababu kubwa ni kuongezeka kwa joto katika ukanda wa Bahari ya Hindi ambalo pia linatishia kuwapo kwa mvua za El-nino.

Alisema kadiri mvua zinavyochelewa, ndivyo joto la bahari linavyozidi kuongezeka na kusababisha hali iliyopo.

Madhara ya joto kiafya

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Meshack Shimwela alisema kwa sasa wanapokea kesi nyingi za magonjwa ya ngozi kama upele, fangasi, kupungua maji mwilini na kuumwa kichwa.

Alisema joto kali linamfanya mtu apoteze wastani wa lita tatu za maji kwa siku. “Kwa watu wasiokunywa maji katika kipindi hiki wanaweza kukaukiwa maji, kwa sababu hawanywi vimiminika vya kutosha kujazia kiwango kile kilichopotea,” alisema. 


Bond Afunguka Kisa cha Wastara Kumuacha na Kukimbilia Kuolewa na Mwanasiasa...Mchepuko Wahusishwa

$
0
0

Mr Bond ambaye alikuwa mchumba wa mwigizaji Wastara kwa muda wa miaka miwili na nusu amepiga stori na Soudy Brown na kusema kisa kilichofanya wakaachana.

Bond amesema kwa kinywa chake kuwa kwa bahati mbaya alimpa mimba mchepuko wake na alipojifungua kuna siku mchepuko huo ukampigia simu Wastara kuomba msaada wa matunzo hapo ndipo kizaa zaa kilipoanza na kisha kuachana miezi minne iliyopita

Bond amesema amejisikia wivu sana lakini yote ni mipanga ya mungu na kwa sasa yeye yupo single...pia amedai uamuzi wa Wastara kuolewa haraka haraka wa hasira kutokana na wao kuachana.....

Chuchu Hans Akanusha Habari za Kuwa Yeye ana Ugomvi na Johari Sababu ya Ray

$
0
0

Mrembo na mwigizaji wa filamu za bongo amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu  Johari aliyekuwa mpenzi wa Ray kabla yake na kujibu kuhusu uvumi uliyokuwa kwenye mitandao kuwa wana beef kubwa

Chuchu Hans amedai kuwa yeye hakuwahi kuwa na ugomvi na Johari bali ni ulikuzwa tu na mitandao amedai yeye anachojua ni kuwa Johari na Ray ni Business Partner hivyo hawezi kuwaingilia katika kazi na anauheshimu uhusiano huo...

Pia ameongeza kuwa Ray anapenda sana watoto hivyo anawalea watoto wake wawili aliopata kwa bwana mwingine kama watoto wake

Lowassa Akutana na Wafanyabiashara wa Team Mabadiliko Kutoka Soko la Kariakoo

$
0
0

Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Team Mabadiliko kutoka soko kuu la Kariakoo, Jijini Dar es salaam waliomtembelea Ofisini kwake jana Januari 14, 2016.


Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Team Mabadiriko kutoka soko kuu la Kariakoo, Severin Mushi, akizungumza wakati akiutambulisha ujumbe wake kwa Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, walipokwenye kumuona jana Januari 14, 2016.


Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyabiashara wa Team Mabadiriko kutoka soko kuu la Kariakoo, mara baada ya kuzungumza nao jana, Jijini Dar es salaam

Kesi ya Kafulila: Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi la Wakili wa Serikali

$
0
0

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika jana Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali yaliyowasilishwa na kujadiliwa Januari 11, 2015 katika mahakama hiyo.

Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai kwamba;
 Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi Kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria
Katika uamuzi wa MAHAKAMA, Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;
 Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli ulio hayana. Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo. Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, MAHAKAMA imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo
Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea Januari 28, 2015.

Wastara: Sajuki Hakusema Nisiolewe,Ila Aliogopa Nitateseka..

$
0
0

Staa wa Bongo Movies, Wastara Juma amefunga ndoa hivi karibuni na Mwenyekiti wa UVCCM na mbunge wa Donge, Sadifa Juma,ameolewa mke wa pili.

‘Ndoa haina ghafla unaweza ukapanga usiku asubuhi ukaolewa,sema tu wageni waalikwa hawakuwa wa kutosha,uzuri kwamba mke mwenzangu alikuwa ananijua kabla sijaolewa,sikutaka kuolewa na mwanaume kabla mkewe hajanijua na sijaolewa mke wa nne ninayemjua ni mmoja tu, na tunapendana na mke mwenzangu,lakini hatuishi nyumba moja,’

‘’Sajuki hakusema nisiolewe alichosema ni kuwa anaogopa nikiolewa nitateseka,nilipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu (CCM)nilikuwa sitizami watu nadhani yeye aliniona kitambo na sio kwenye kampeni ananijua kwa mujibu wa maelezo yake ananifahamu vizuri,nilimpa masharti yangu nikamkaribisha nyumbani tukafunga ndoa,’’Alisema Wastara.

Edward Lowassa Atangaza kugombea tena Urais Mwaka 2020, asisitiza yupo fiti

$
0
0

Akiongea na wafanyabiashara wa kariakoo waliomtembelea ofisini kwake mikocheni, Lowassa amesema safari ndio kwanza imeanza na yupo fiti kwa mapambano.
Amewataka wanamabadiliko kutokukata tamaa 

Amesisitiza kama alivyoshinda uchaguzi huu ndivyo atakavyoshinda mwaka 2020.

Kijana Unapo Amua Kuoa Mwanamke mrembo, Msomi au Binti wa Kidigital Basi Kubaliana na Haya

$
0
0

Vijana wenzangu unapoamua kuoa mrembo, msomi na binti wa digital, lazima ukubaliane na haya;

1. Wasichana wengi sasa hawajui kupika. Wanajifanya wamechoka nitanunua msosi sana tu, tena usipokaza hata chai ataenda kununua.

2. Usishangae nguo zako kutofuliwa wiki mbili, anaweza kumuita mdogo ake anamlipa afue. Yeye anachart sio na wewe ujue ni shotizooo.

3. Kupiga deki sahau kijana mwenzangu. Aanze tu kupinda mgongo. Kama unataka usafi wa nyumba yako tafuta housegirl.

4. Jua kuwa utawahi wewe kuamka, yeye bado kalala. Amechoka kazi za ofisini za jana yake.

5. Bajet ya saloon iwepo ya kila wiki nywele na kucha.....

Usilalamike ndo Gharama za kufanya maamuzi hayo...


Tundu Lissu: Viatu vya Dk. Slaa VikubwaKumpata wa Kuvivaa Ipo Shughuli

$
0
0

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA amesema kuwa viatu vya Dkt. Slaa ni vikubwa, hivyo kupata mtu wa kuvivaa na vikamuenea ni ngumu

Amesema Mwenyekiti wa Chama ndiye mwenye mamlaka ya kumchagua mtu anayeona ana uwezo wa kutosha wa kukiongoza chama kwa nidhamu

Katumbi Agoma Kumuuza Samatta Ubelgiji, Huenda Akabaki TP Mazembe

$
0
0

IKIWA tayari Ubalozi wa Ubelgiji nchini Tanzania umekwishatoa viza kwa mshambuliaji Mbwana Samatta kwenda kusaini klabu ya KRC Genk, lakini taarifa zinasemekana kuwa huenda anaweza akabaki TP Mazembe ya DRC kumalizia Mkataba wake hadi Aprili.

Hiyo inatokana na Rais wa Mazembe, Moise Katumbi kugoma kumuuza Mwanasoka huyo Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani katika klabu hiyo Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Rais wa Klabu ya TP Mazembe, Katumbi Moise.

Inasemekana pia kuwa, Katumbi anataka Samatta anende kucheza Nantes FC ya Ligi Kuu ya Ufaransa, ambayo amekwishafikia makubaliano nayo, na kwamba wiki iliyopita Nantes FC ilituma mwakilishi wake jijini Dar es Salaam, ambaye alifanya mazungumzo na Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo mbele ya Ofisa mmoja wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Katika mazungumzo, Kisongo alifikia makubaliano ya maslahi binafsi na Samatta ikiwemo dau la kusaini, mshahara, masharti na marupurupu mengine. Kisongo alitaka kiwepo kipengele cha mchezaji kutorejeshwa Afrika iwapo hatapata nafasi ya kucheza Nantes, bali auzwe klabu nyingine ya Ulaya na ikakubaliwa.

Samatta hivi karibuni akikabidhi jezi yake kwa rais Mstaafu, Dk Jakaya Kikwete wakati Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye akishuhudia tukio hilo. 

Nantes ilionesha nia ya dhati kabisa ya kumchukua Samatta na Kisongo aliinuka kwenye meza ya mazungumzo akiwa amekubali na kusema anakwenda kuzungumza na mchezaji. Hata hivyo, inaonekana Samatta mwenyewe ndiye anayetaka kwenda Ubelgiji na si Ufaransa, kwani kitendo cha Kisongo kutorejesha majibu kwa Nantes kinaashiria ameshindwa kumshawishi mchezaji wake akubali ofa hiyo.

Wakati huo huo, Rais wa Mazembe hayuko tayari kumuuza Samatta Ubelgiji na yuko tayari kuona Samatta anabaki Mazembe kumalizia Mkataba wake ili aondoke kama mchezaji huru Aprili, hali ambayo itamlazimu kusubiri hadi Agosti kusaini Genk.

Kwa sasa, kambi ya Samatta inajaribu kuomba msaada kwa viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakazungumze na Katumbi ili akubali kumuacha mchezaji aende klabu aliyochagua.

Rais Mstaafu, Dk Jakaya Mrisho Kikwete ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa chama tawala, CCM, Waziri wa Michezo, Nape Nnauye kwa pamoja wameahidi kumsaidia Samatta katika suala la kumlainisha Katumbi akubali kupokea ofa ya Genk.

Wakati huo huo, Nantes wamekuwa wakimpigia simu Kisongo wakisema wanamsubiri mchezaji aende kusaini, lakini Meneja huyo anakosa majibu ya uhakika.

Inaonekana tayari Katumbi anaujua mchezo wote unaoendelea naye ameamua kukaa kimya akiamini Samatta hawezi kufanya chochote kwa sasa bila baraka zake. Wazo la kusema Samatta asubiri hadi mwezi Aprili atakapomaliza Mkataba wake ili kusaini kama mchezaji huru mwezi Agosti, halifurahiwi hata na Kisongo mwenyewe.

Samatta aliyejiunga na TPM mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa nusu msimu, akitokea African Lyon, hadi sasa ameichezea klabu hiyo mechi 103 na kuifungia mabao 60. Ndani ya mechi hizo, kijana huyo wa umri wa miaka 24, ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na Mazembe, huku naye akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika.

Familia ya Lowassa Mshaurini Lowassa, Mshika Mbili Moja Humponyoka

$
0
0

Jana aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Edward Ngoyai Lowassa alitembelewa ofisini kwake na Wafanyabiashara wana mabadiliko wa Kariakoo. Moja ya kauli kubwa kabisa toka kwa LOWASSA kwa wafuasi wake hao ni hii ya kwamba mwaka 2020 atagombea urais na kuwataka wafanyabiashara hao kutokata tamaa huku akiapa kwamba mapambano ndiyo kwanza yameanza.

Ikumbukwe kuwa moja ya sababu zilizopelekea Lowassa kushindwa kabisa kwenye uchaguzi mkuu uliopita ukiachilia mbali ile ya UFISADI ni kudorora kwa afya yake. Ni udhaifu wa afya yake uliopelekea siku ya ufunguzi wa kampeni za CHADEMA pale JANGWANI, Lowassa kushindwa kabisa kuhutubia na kuwataka watanzania kusoma hotuba yake kwenye tovutu ya chama. Haikuishia hapo, siku 64 za kampeni Lowassa hakuwahi kuhutubia majukwaani kwa zaidi ya dakika nane(8).

Baba ni kichwa cha familia na pengine inakuwa vigumu kwa mmoja wa familia kutia neno kwa kichwa cha familia kwa kuhofia kufokewa. Binafsi nadhani familia ilitarajia baada ya purukushani za kampeni za urais mwaka jana, Mume/baba/babu/mjomba/shemeji yao angejikita zaidi kwenye kuhakikisha afya yake inaimarika ili waendelee kuvuna busara zake kama kichwa cha familia na siyo kutumia nguvu nyingi kwenye siasa huku akijua kabisa uwezekano wa kuwa rais wa Tanzania kupitia Chadema ni haupo kabisa. Pamoja na kwamba baba ndiye kichwa cha familia lakini bado familia inayo fursa ya kumshauri katika mambo ambayo yana maslahi mapana kwa familia na siyo vinginevyo. Familia tumieni Fursa hiyo kumshauri mzee.

Lowassa akumbuke kuwa chama chake chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa sasa(narudia, chini ya Mwenyekiti wa sasa) kitamhitaji zaidi kwa kipindi kingine cha miaka mitano siyo kwa maslahi ya chama na yeye kama yeye, la hasha. Nadhani kila mmoja wetu anajua ujio wa Lowassa Chadema ulichagizwa na nini, nani walinufaika na ujio huo n,k. Ndiyo maana baada ya azma ya wale wachache kufanikiwa walimuachia yeye mwenyewe na akina SUMAYE kufanya Kampeni, walijua wao kama wao wasingeweza kufua dafu kwa CCM.

Lowassa kafanya kubwa sana ambalo wenye CHADEMA yao wanaamini ni makosa yaliyofanywa na ZITTO KABWE na Dr. SLAA. Kwa mujibu wa kauli mbalimbali za wenye CHADEMA yao, ZItto alijua yeye ndiye angekiwa Mwenyekiti wa CHADEMA huku DR. SLAA akiamini yeye ndo angekiwa mgombea urais kupitia CHADEMA 2015. Wako wapi? LOWASSA ni nani mpaka jana 14/01/2016 ajitangaze kuwa ndiye anayefaa kuwa rais wa kupitia CHADEMA 2020, miaka 5 kabla ya uchaguzi? Watamvumilia kwa sababu ni MTAMBA ila sijui siku maziwa yakikauka kama atavumiliwa kwa kauli yake hiyo.

Lowassa anapaswa pia kutambua kuwa kwa historia ya CHADEMA sasa ilivyo, mgombea urais wao ni lazima atoke CCM na ni lazima aendane na Mazingira na mahitaji ya wakati huo. Lowassa ana uhakika kuwa atakuwa anaendana na mazingira na mahitaji ya CHADEMA 2020?

FAMILIA YA LOWASSA MTAMBUE HAYA MATATU:
1. WENYE CHADEMA YAO MIDOMO IKO WAZI KAMA YA SIMBA, WATAMEZA CHOCHOTE TOKA KWA LOWASSA KWA SASA(WATAMKAMUA SANA)
2. MGOMBEA WA CHADEMA ANATOKA CCM NA LAZIMA AENDANE NA MAZINGIRA NA MAHITAJI YA CHADEMA KWA WAKATI HUO

By Tata Madiba/JF

GARI Aina ya BMW Anayomiliki Masanja Mkandamizaji Yawa Gumzo...Mwenyewe Awataka TRA Wakaikague Kama Hajalipia Ushuru

$
0
0


Mchekeshaji wa Orijino Komedi na mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji amesema kila anachomiliki amekinunua kwa pesa yake halali huku akishangaa kwanini watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki BMW yenye plate namba ya jina lake.

Akizungumza  katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Masanja alisema anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli. "Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha usafiri cha kunitoa point moja kwenda nyingine,” alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli," alijinadi.

Aliongeza, "Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia." Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari la thamani siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara yake moja tu.

Miss Tanzania Ataka Namba ya Simu ya Mbwana Samatta

$
0
0

MSHIRIKI wa Miss Tanzania 2005 ambaye pia ni mcheza fi lamu, Maureen Gislary ameibuka na kutaka namba ya simu ya mchezaji wa timu ya Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo,Mbwana Samatta kwa gharama yoyote.

Akizungumza na Amani Sports, Maureen aliyekuwa kumi bora katika kinyang’anyiro hicho cha Miss Tanzania kilichoshuhudiwa kwa Nancy Sumari kuibuka mshindi alisema kuwa, nia ya kuhitaji namba hiyo nikuhakikisha anamuweka Samatta ‘kibindoni’ kabla hajatimkia nje ya nchi.

“Kwanza nimefurahishwa sana na ushindi wake wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani mwaka 2015, mwenye namba yake tafadhalini naiomba kwa gharama
yoyote nitatoa,” alisema Maureen.

Tazama Hapa Matokeo ya Kidato cha Pili 2015/16

$
0
0


Baraza la mitiani NECTA limetangaza Matokeo ya kidato cha 2 kwa wanafunzi waliofanya mtihani mwaka jana ambapo wanafunzi 324,068 sawa na 89% kati ya wanafunzi 363,666 waliofanya mtihani wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu.

BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO

Wizara ya Nishati Yalikana Gazeti la Mtanzania

$
0
0

WIZARA ya Nishati na Madini imeikanusha habari iliyotolewa kwenye gazeti la Mtanzania la tarehe 14 Januari 2016 kichwa chake cha habari kilichosomeka “HARUFU YA JIPU MRADI WA UMEME” aliyoandika mwandishi wa gazeti hilo Jonas.

Habari hiyo ilieleza kuwa, mradi uliozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Mh Jakaya Mrisho Kikwete uligharimu shilingi Trilioni 1.6 na kwamba fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana na ubia kati ya serikali ya Tanzania na Japan ambapo serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60,pia taarifa hizo zilidai kuwa serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12na zilizobaki ni mkopo kutoka benki ya Japan.

Mwandishi wa gazeti la Mtanzania alidai kuwa gharama za mradi huo ni kubwa ukilinganishwa na miradi mingine akitolea mfano wa kampuni ya TALLAWARA Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa dola za kimarekani milioni 350.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud ametolea ufafanuzi wa habari hiyo na kudai kuwa si ya kweli.

“Tunakanusha vikali taarifa hizi zilizotolewa na kwamba hazina ukweli wowote zimelenga kupotosha ukweli na kuichafua serikali.”Alisema Badra wakati akiongea na Waandishi wa Habari  jijini Dar Es Salaam

Badra alifafanua ukweli wa mradi huo na kudai kuwa serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Serikali ya Japan ya mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani milioni 292 kwa aajili ya kutekeleza Mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO ya Japan kama mkandarasi EPC contractor na sio kama mbia na serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa.

“Mradi unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO na hakuna mwekezaji mwingine katika mradi huo,hivyo si kweli kwamba serikali ya Tanzania imewekeza kwa ubia wa asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO kwa silimia 60.Kwa maana hiyo hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu kwani ni mali yetu.”Aliongeza Badra

Pia alisema kuwa mradi wa Kinyerezi 2 bado haufunguliwa kama habari hiyo ilivyodai,mradi uliofunguliwa ni wa Kinyerezi 1.

Badra alimaliza kwa kuwataka Waandishi wa Habari kufuata miiko na maadili ya uandishi wa Habari kwa kuandika habari zenye ukweli na sahihi badala ya kuandika habari za mitaani kwakuwa zinapotoshajamii


Mh.Paul Makonda Ni mfano wa Kuigwa

$
0
0

Mh.Paul Makonda akizungumza na Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi anasema tarehe 5/1/2016 ujenzi wa shule 7 katika wilaya ya kinondoni ulianza na amezindua kampeni ya kuchangia ujenzi wa shule Saba za kata katika wilaya ya Kinondoni ili kupunguza upungufu wa shule katika wilaya hio ambapo zitachukua zaidi ya vijana 3183 

Akiongelea maendeleo ya Kampeni hio amesema inaenda vizuri na michango inaendelea kumfikia na witikio umekuwa mkubwa sana!

Akitoa tathimini fupi amesema amepokea Mifuko 500 ya cement toka kwa Dr mwaka....mifuko 1000 ya cement toka kwa watu mbalimbali na umoja wa mafundi geleji wametoa mifuko 50 ya cement! Amesema ameamua kujenga shule hizo saba kuondokana na tatizo la upungufu wa shule katika wilaya ya kinondoni na kuongeza kuwa Elimu ni njia bora na pekee ya kuwapa urithi wadogo zetu na watoto zetu! Ameendelea kuwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kuchangia kwani Kutoa ni moyo na si utajiri ameomba mwenye chochote hata mfuko mmoja wa simenti iwe hata tofari moja au mawe na mchanga wanapokea chochote

MAONI YANGU! 

Mh.Paul Makonda ni mfano wa kuigwa kwa wakuu wa mikoa na wilaya zote hapa nchini katika utendaji wa kazi,Hata wabunge pia ni lazima wajifunze toka kwa Makonda na si kubaki kuilalamikia serikali inafanya nini ni wakati wa wao pia kusema serikali wameifanyia nini

Ukiacha maneno yanayo semwa kuhusu Mh.Paul Makonda utendaji wake wa kazi wananchi wengu wameupenda pamoja na mapungufu machache alio nayo

Rais Magufuli AMFUKUZA Kazi Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Kwa Utovu wa Nidhamu

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi na kumfukuza kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Faisal Issa kutokana na utovu mkubwa wa nidhamu aliouonesha katika kikao cha kamati ya ulinzi kilichofanyika  tarehe 15 Januari, 2016 Mjini Mwanza.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya yaliyotokea katika kikao cha kamati ya ulinzi cha Mkoa, kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es salaam

15 Januari, 2016

Serikali Yatoa Tamko Kali Kuhusu Tiba Asili na Tiba Mbadala

$
0
0

Ndugu Wananchi, Katika nchi yoyote ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau. 
 

Huduma za tiba asili na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa. 

Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali. 
 

Kutokana na hali hiyo na kutokana na ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb) kwa Tabibu Juma Mwaka Juma tarehe 14/12/2015 na kufuatia uchambuzi uliofanywa na Wizara baada ya ziara hii, Wizara imebaini changamoto zifuatazo:-
 

1. Huduma za tiba asili na au tiba mbadala zinatolewa na watoa huduma wasiosajiliwa na Mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria. 
 

2. Uwepo wa vituo vinavyotoa huduma za Tiba Asili na au Tiba Mbadala bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria.
 

3. Kutolewa dawa kwa wagonjwa bila dawa hizo kusajiliwa na mamlaka husika. 
 

4. Uingizaji na matumizi ya vifaa vya uchunguzi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka zinazohusika, na

5. Utoaji wa matangazo bila ya kufuatwa kwa matakwa ya sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo. Aidha baadhi ya matangazo hayo yamekuwa na taarifa zinazoweza kuleta madhara na kupotosha Umma wa Watanzania.
 

Ndugu Wananchi,

Kutokana na hali hiyo, Wizara itahakikisha kuwa huduma za tiba asili na tiba mbadala zinatolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo. 

Lengo ni kuwezesha huduma za tiba asili na tiba mbadala zinakuwa huduma rafiki na salama kwa watumiaji. Tunao wajibu wa kuwalinda wananchi, vile vile tunaowajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala ili kufanya shughuli zao vizuri.
 

Hivyo kwa upande wetu Wizara itahakikisha kuwa:-

1. Baraza na sehemu inayosimamia huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala inakuwa na watumishi wa kutosha kwa mujibu wa Ikama. 
 

2. Kunakuwa na Mpango Mkakati wa muda mrefu kuwezesha kufanikisha uboreshaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini.
 

3. Watoa huduma wote, vituo vyote vya kutolea huduma, dawa na vifaa na vifaa tiba vinavyotumika vinasajiliwa. 
 

4. Utaandaliwa mwongozo wa mafunzo kwa watoa huduma wote nchini, kuhusu namna ya kuweka kumbukumbu za wagonjwa, kutoa rufaa kwa wagonjwa na kutengeneza dawa zilizo bora. 
 

5. Kunakuwa na mawasiliano na Wizara zinazohusika na habari na mawasiliano ili kuboresha utoaji matangazo yanayohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala. 
 

6. Kunakuwa na mawasiliano na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Taasisi za Utafiti ili kuboresha huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini. 
 

7. Tutafanya mabadiliko ya Sheria ili kuongeza kiwango cha adhabu kwa watakaokiuka, na pia tunakusudia kuondoa Kanuni inayoruhusu matangazo kwa idhini ya Baraza kwa sababu inaweka mianya ya matumizi mabaya ya fursa ndogo ya matangazo inayotolewa.

Ndugu Wananchi, Katika kufanikisha hayo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa maelekezo yafuatayo kwa watoa huduma na jamii:-
 

1. Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kutoa huduma za tiba asili na au tiba mbadala bila kusajiliwa.

Ninalielekeza Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuhakikisha kuwa watoaji huduma wote wanasajiliwa kwa mujibu wa Sheria: 

(a) Mijini, (Majiji, Manispaa na Miji) – usajili wao ukamilike katika kipindi cha miezi mitatu; kuanzia Januari 15, 2016 na 
(b) Vijijini, Halmashauri zote zilizobaki – usajili wao ukamilike katika kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 15, 2016. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaye puuza kujisajili katika kipindi hicho 
 

2. Hairuhusiwi kuuza na au kugawa dawa yoyote ile ya tiba asili au tiba mbadala mpaka iwe imesajiliwa na Baraza baada ya kuchunguzwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni salama na kupewa kibali na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA). 
 

3. Hairuhusiwi kuendesha kituo cha kutolea huduma za tiba asili na au tiba mbadala bila kukisajili. 
 

4. Wizara inapiga marufuku kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ile kutumia kifaa au kifaa tiba chochote bila kukisajili TFDA na kupewa kibali; na 5. Matangazo yote yanayohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala ambayo hayajapitishwa na Baraza yamezuiliwa kuanzia leo tarehe 15/1/2016. 
 

Wizara inavitaka vyombo vya Habari hasa Televisheni, Radio na Magazeti kuzingatia Sheria na Kanuni za Tiba Asili na Tiba Mbadala inayozuia matangazo ambayo hayajachunguzwa na Baraza. Ni wajibu wa vyombo vya habari kujiridhisha na Mamlaka husika yaani Baraza kabla ya kutoa tangazo lolote linalohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala. 
 

Wizara itashirikiana na Mamlaka zinazohusika na habari na mawasiliano kutekeleza agizo hili. Vile vile, hairuhusiwi kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara kuhusu tiba asili na tiba mbadala.
 

Ndugu Wananchi, Katika kuwezesha ulinzi wa afya za wananchi, kila mmoja wote alinde afya yake kwa kuhakikisha kuwa huduma anayopata ya tiba asili na tiba mbadala ni kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo inayotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 
 

Ni uhakika uliowazi kuwa kwa pamoja tukiboresha huduma za tiba asili siyo tu tutaboresha afya zetu bali pia tutaweza kuuza dawa na huduma hizo nje ya nchi na kupata fedha za kigeni kupitia na hivyo kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na nchi kwa ujumla.
 

Kwa pamoja tushirikiane kuboresha huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini. 
 

INAWEZEKANA.

Ummy A. Mwalimu (Mb) WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO 15 Januari, 2016

Mama Kaniletea Mke Kutoka Kijijini Bila Ridhaa Yangu, Nifanyeje?

$
0
0

Wadau mwishoni mwa December mama alikuja hapa dar na mgeni, walifikia kwangu, mgeni mwenyewe ni binti wa kama miaka 20 hivi, nilishangaa maana mama akija Dar hufikia kwa mkubwa wangu, kaka, mimi huenda kumuona huko

Cha kushangaza safari hii, mama akafikia kwangu pamoja na huyo mgeni wake, nilipomuuliza kuhusu huyo binti mama akadai wana mambo yao yaliyowaleta, after some days mama akaaga anaenda kuwasalimia familia ya kaka yangu atakaa siku kadhaa, ila atamuacha binti hapa kwangu kwa siku tatu nne

Nilipoachwa nae binti, roho ya shetani ikatamalaki, nikamrubuni yule binti hatimaye tukashiriki ile dhambi pamoja bila kujua ni mtego eti kumbe mama kamuacha kama mke wangu, nikamuhamishia chumbani kwangu ili nimfaidi sana pindi mama akija kumchukua niwe mwepesi

Kuja kustuka ni wiki mbili zimeisha tangu binti kuhamia room kwangu na tangu mama aende kwa kaka kimara, mm naishi kigamboni, kukawa na kila dalili Girlfriend wangu atakuja siku moja kumkuta binti hapa halaf iwe shida, nikaona nipige simu kwa kaka kuuliza mama anakuja kumchukua huyu binti lini, kaka alishangaa mno, akasema mbona mama alishaondoka wiki nzima nyuma kurudi village na kwamba huyo binti ni mke wako amekuletea na wewe umekubali na amewaacha kwa furaha, nikachanganyikiwa
Kumbe ndio maana simu ya mama haikupatikana kwa wiki mbili

Wadau nimechanganyikiwa, sasa jana nimempata mama hewani ananiambia huyu ndio mke wangu, ana tabia nzuri, kuwa ni mtoto wa flani wanamjua tangu kuzaliwa, kwamba hata baba karidhia na ndie aliewasafirisha, kwamba wamenivumilia muda mrefu nipo nipo tu hivyo waniletee mke

Naombeni msaada

Biashara Zinazotumia Mfumo wa Network Marketing na Ulaghai Uliofichwa Ndani yake

$
0
0

Mara nyingi tumekua tukiona au kukutana na watu au ndugu zetu wanaojiita wawakilishi wakijaribu kutushawishi kuingia katika kile wanachokiita biashara zenye mafanikio, ambapo wanatushawishi kujiunga na kampuni inayouza bidhaa zake kwa mfumo wa Network Marketing au Multi-Level Marketing (MLM). Katika mfumo huu unapata commission na faida kwa kuingiza watu wengine wanunue bidhaa husika na faida yako itaendelea kua kubwa kama na wao watashawishi watu wengine wajiunge katika msururu huu. Makampuni haya kwa hapa Tanzania yapo mengi wakiuza bidhaa kama za Aloevera, Kahawa zenye mchanganyiko wa Garnodema n.k.

Naomba itambulike kua Lengo la uzi huu sio kukosoa kampuni yeyote ile, bali ni kueleza na kuelimisha umma athari za mfumo wa kilaghai unaotumika katika biashara za namna hiyo

Kabla sijaamua kuandika uzi huu nimekua nikiona watu wengi wakidanganyika na kuingizwa mkenge kwenye biashara hizi aidha kwa kutokujua ama kuingizwa tamaa kwa ushawishi wa wawakilishi hawa ambao wanakua na vipeperushi vinavyotoa maelezo ya biashara huku vikionyesha baadhi ya watu waliofanikiwa katika mfumo huu wakiwa katika picha na Magari Mazuri na Majumba ya Kifahari.

Network Marketing au MLM ni mfumo unaofanya kazi kwa Idea kwamba unauza bidhaa kwa watui ambao nao watauza bidhaa kwa watu ambao nao watiuza. Mfumo huu kamwe hauwezi kusemwa kua ni mpya kwenye masoko ili upate msamaha wa kutokuhusianishwa na kanuni na taratibu za kawaida za Marketing katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa. Mfumo huu una ulaghai wa hali ya juu na kiuhalisia Mfumo mzima hauna faida hasa kwa watu wa chini, na sio sustainable kwa muda mrefu - in reality the system ‘is designed to fail” 

Swali ambalo ningependa ujiulize ni hili; Kama bidhaa husika ni nzuri sana na inahitajika katika jamii kama wanavyoinadi, kwanini wasitumie mfumo wa kawaida wa masoko ambao umeinufaisha dunia nzima tangu karne?. Jambo la kwanza kabisa ambalo mtu yeyote lazima alielewe ni hili; Katika biashara yeyote swala la demand and supply au kwa Kiswahili Ugavi na mahitaji lazima lizingatiwe na kama ukakosea ukafanya makadirio ya chini au ya juu sana katika kimojawapo kati ya hivyo basi hakuna mafanikio yeyote yatakayo patikana katika biashara utakayoianzisha. MLM nyingi zinaoverestimate supply and demand kwa kiwango cha juu sana, Na tatizo kubwa hapa ni la kutokutumia akili ya kawaida kabisa; Kivipi sasa?.

Chukulia mfano huu; Tuseme wewe ni mwakilishi wa mojawapo ya makampuni haya na ukaweza kuwashawishi wenzio (wauzaji) kumi ukapata commission na faida kiasi ambao watadhamini kumi na wao kudhamini wengine kumi kila mmoja, mpaka kufikia kizazi cha tatu utakua na idadi ya watu 1000, na hapo utakua umeumaliza mtaa wako. Kufikia kizazi cha sita utakua umefikisha watu 1,000,000 na huo utakua ni mkoa mzima tayari na kila mmoja katika hawa akiamini katika mafanikio yatakayotokana na uuzaji wa bidhaa husika, lakini watamuuzia nani sasa na kila mmoja ni muuzaji?. Kwenye vikao vyao utawasikia “Kila mmoja hapa anaweza, hii ni fursa ya maisha, angalia mahesabu utaniamini”, ila Jaribu kuongelea kuhusu oversaturation ya soko na hasara itakayosababishwa nayo utawasikia wakikuambia “sio kwako bwana mafanikio haitatokea hivyo kwako nayaona mafanikio yako hata nikikuangalia machoni”. Tumia akili ya kawaida utapata jibu kuhusu hilo.

Network Marketing ni mfumo wa kiunyonyaji katika mahusianao ya mtu na Kama uko katika biashara hii lazima ukubali kumeza ukweli mgumu kwamba biashara yako inakua kutokana na exploitation of personal relationships. Baada ya kuingia katika biashara hii, marafiki na ndugu zako wanakua ni wateja wako, sasa jiulize uko tayari kumwingiza Mama yako kwenye huu mfumo wa wizi ukijua hakuna faida kubwa mbeleni?

Kufeli kwa biashara yeyote ile kunaumiza sana, ila kwa biashara yeyote ndogo kunakuwepo japo nafasi ya kufanikiwa. Nafasi hiyo ndogo ya mafanikio kamwe haipo kwenye MLM labda kama faida inayotokana na kushindwa kwa wengine utaitafsiri kama mafanikio.

By Bill The Goat/ JF

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images