Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Waziri Nape Ataja Sababu Za Kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti.

0
0


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.

Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa leo 17 Januari, 2016 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati alipokutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye amesema kuwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016 Serikali imelifuta Gazeti hilo ikiwa ni uamuzi uliotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).

Alieleza kuwa, hatua ya kulifuta gazeti hilo inazuia pia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.

‘’Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu’’, alisema Nnauye.

Aidha, alifafanua kuwa hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari,  2016  kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.

"Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na Mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya  mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti,

 

"Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. 

"Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo’’ alisisitiza Mhe. Nnauye.

Katika hatua nyingine, Waziri nape alitoa pongezi kwa Vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi.

‘’Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja  na wahariri wa magazeti ya; Mwananchi Tanzania, Mtanzania, The East African, Magazeti ya Daily News na Habari Leo, Uhuru na mengineyo’’, alisema Mhe. Nnauye.


Kasi ya Magufuli ya Hapa Kazi tu Yasababisha Mrembo wa Bongo Movies Kuyakataa Mapenzi

0
0

MSANII wa Bongo movies Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amesema katika kipindi hiki cha kasi ya Rais John Magufuli, hana muda wa kuhangaika na mapenzi, badala yake yeye atachapa kazi tu.
Akizungumza na gazeti hili, msanii huyo alisema kumekuwa na wimbi kubwa la wezi wa mapenzi wanaotumia fedha, lakini kwake ni bora ajibidishe kivyake ili apate chake halali.
“Mimi naona kabisa hapa Bongo hakuna mapenzi, kuna usanii tu, kila mmoja anajidai yupo kwenye mapenzi kumbe utalii, ninachojua mimi hapa ni kazi tu mapenzi nchi za watu,” alisema.

Toa maoni yako

Yanga Yaichakaza Ndanda FC Jioni ya Leo Yafikisha Point 36

0
0

Goli la Yanga African lilifungwa na Kelvin Yondani katika Dakika ya 61 ya kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Yanga Simon Msuva kuchezewa madhambi ndani ya jumba la penati.

Ushidi huo unaiweka Klabu ya Yanga African kileleni mwa ligi kwa Pointi 36.

Dawasco Yaibua Wizi Mwingine wa Maji Unaofanyika Katika Kiwanda cha Maji ya Betri

0
0


Moja ya kisima kinachodaiwa kutumika kuhifadhi maji yanayodaiwa kuibwa kutoka katika mtandao wa maji wa Dawasco.

Madumu ya Maji ambayo yame3kuwa yakitumika katka utengezaji wa maji ya Betri katika kiwanda cha Bahari Chemicals Ltd .

Sehemu ya wizi wa maji kutoka katika mtandao wa DAWASCO unavyoone3kana kufanywa katika kiwanda cha kutengenezea Betri cha Bahari Chemicals Ltd.

Ikiwa siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la mboga mboga na matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio jijini Dar es salaam. Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika kiwanda cha kutengeneza Maji ya betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.
Akizungumzia tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw. Deogratius Rwegasira, amethibitisha kutokea kwa wizi huo ambapo kiwanda hicho kilikuwa kimejiunganishia Maji bila kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita wala akaunti namba inayoonyesha kiasi cha Maji kinachopita katika system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya mawasiliano na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Devendra Singh Parmar amekiri kutumia Maji hayo kinyume na taratibu .
“Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki kimekuwa kikituibia Maji yetu kwa muda mrefu, mmiliki wa kiwanda amekubali kosa,lakini akisema kwamba wenyewe ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu waanze kazi.hivyo hawakujua taratibu za kufuata”. Alisema Bw. Rwegasira.
Aidha meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri kuihujumu Dawasco kwa kuiibia Maji, lakini amesema kuwa wao ni wapangaji tu wamepanga katika eneo hilo na wana muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo, walikuta wizi huo wa Maji ukifanyika katika kiwanda hicho na hawakujua taratibu husika za kufuata ili wapate huduma ya Maji kihalali.
“Sisi tumekubali kuwa tulikuwa tunatumia Maji ya DAWASCO bila kuyalipia, lakini sio sisi ambao tuliounganisha bomba hili, wapangaji waliopita walijiunganishia Maji haya hivyo tunaomba tulimalize hili, ili tuanze kuwa wateja wenu rasmi” alisema Bw.Gulam.
Aidha bwn Gulam ameainisha kuwa wao kama wamiliki wa kiwanda wamekubali kulipa faini iliyotolewa na DAWASCO ya Shiling million 3.5 ili warudishiwe huduma kama wateja wengine na waweze kuendelea na biashara.
Vitendo vya uhujumu wa Miundombinu ya Maji hususani wizi wa Maji unaendelea kuwa changamoto kwa DAWASCO licha ya kampeni na elimu inayotolewa kila siku juu ya uhalali na utaratibu wa kuungiwa huduma ya Maji inayotolewa na DAWASCO.

Mabinti wa Kichaga Ndio Wanao Ongoza Kulilia Ndoa

0
0

RKwa utafiti wangu mdogo unaonesha kuwa katika makabila yote ya hapa Bongo tzee, mabinti wa kabila la Kichaga ndio hasa wanaongoza kwa kulilia ndoa. 
Yani ukikaa naye kwenye mahusiano ndani ya kipindi kisichozidi mwaka, lazima atakuwa ameshaanza kulilia ndoa.
Sasa ninaomba kufahamu kuwa huwa ni suala la kisaikolojia au ndivyo mila zao zinavyowafundisha kufanya hivyo?
Mabinti wengi wa kabila jingine huwa ni wavumilivu, hata kama watalilia, watalilia kindani ndani na wala huwezi jua mpaka kidume uamue kutangaza njaa ya kuweka ndani...

Toa maoni yako

Hatua Ambazo Zimechukuliwa Dhidi Ya Stanbic Bank Tanzania Limited Kuhusu Ufisadi wa Mkopo Wa Serikali Wa Dola Milioni 600

0
0

Utangulizi

Mwezi Julai 2013, Benki Kuu ya Tanzania kupitia ufuatiliaji wa kawaida wa shughuli za mabenki iligundua matatizo yaliyohusiana na hasara itokanayo na mikopo na pia kuacha na kuondolewa kazini kwa viongozi waandamizi wa Stanbic Bank Tanzania Limited (Stanbic) katika muda mfupi.

Kutokana na hilo, Benki Kuu iliamua kufanya ukaguzi wa kulenga (Targeted Examination) katika benki hiyo. 

Ukaguzi huo ni kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa Benki Kuu chini ya Kifungu 47 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 na Kifungu 31 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

Matokeo ya Ukaguzi wa Benki Kuu

Katika ukaguzi huo, wakaguzi wa Benki Kuu, pamoja na mambo mengine walibaini miamala ya kutia shaka iliyohusu malipo kwa kampuni ya kitanzania ya Enterprise Growth Market Advisors (EGMA). 

Kampuni ya EGMA ilihusika katika uwezeshaji wa upatikanaji wa Mkopo kwa Serikali ya Tanzania ambapo Standard Bank Plc (ambayo kwa sasa inajulikana kama ICBC Standard Bank) na Stanbic Bank Tanzania Limited kwa pamoja walikuwa “Mwezeshaji Mkuu” (Lead Arranger).

Malipo hayo kwa kampuni ya EGMA yalikuwa yamefanyika kinyume na taratibu za kibenki na yalihusisha uongozi wa benki ya Stanbic. 

Jumla ya malipo yalikuwa ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 6, na zililipwa katika akaunti ya EGMA na kutolewa kwa muda mfupi kwa njia ya fedha taslimu (cash) ambayo ni nje ya taratibu za kibenki.

Taarifa ya ukaguzi huo iliwasilishwa kwa benki ya Stanbic kwa mujibu wa taratibu, na Benki Kuu iliiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo kuchukua hatua stahiki za kurekebisha kasoro zilizoonekana.

Aidha, benki ya Stanbic iliagizwa kutoa taarifa kwa Kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) kilichopo Wizara ya Fedha na Mipango kuhusiana na miamala hiyo yenye mashaka katika akaunti ya EGMA kama Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (The Anti-Money Laundering Act, 2006) inavyoelekeza. Benki ya Stanbic ilitekeleza maagizo na kutoa taarifa FIU kuhusu miamala inayotiliwa shaka.

Mnamo 29 Septemba 2015, Benki Kuu ilipokea barua toka Idara ya Serikali ya Uingereza inayohusika na Upelelezi wa Makosa ya Kugushi na Rushwa (Serious Fraud Office - SFO) ikiiomba Benki Kuu ruhusa ya kutumia ripoti yake ya ukaguzi kama ushahidi katika kesi dhidi ya Standard Bank Plc ambayo ilikuwa ni mshirika wa Stanbic Bank Tanzania Limited katika kuwezesha mkopo wa dola za kimarekani milioni 600 kwa Serikali na kwamba ripoti hiyo ingekuwa wazi kwa umma. 

Benki Kuu iliijibu SFO kuwa kwa mujibu wa Sheria ripoti za Benki Kuu zinatolewa tu kwa benki au taasisi ya fedha inayohusika, hata hivyo, Benki Kuu haikuwa na pingamizi kwa SFO kutumia taarifa za ripoti hiyo kwa kuzingatia chanzo cha ripoti hiyo.

Hatimaye, Standard Bank Plc ilikubali makosa na ilitozwa faini ya jumla ya dola za kimarekani milioni 32.20, ambapo kiasi cha dola za kimarekani milioni 7 zinalipwa kwa Serikali ya Tanzania (dola za kimarekani milioni 6 zilikuwa ni fidia na dola za kimarekani milioni 1 ni riba).

Kwa kuzingatia mapungufu ya kufanya miamala iliyohusisha EGMA na pia kutokuweka taratibu madhubuti za udhibiti wa ndani, na kwa kuzingatia Kifungu 67 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu imeiandikia benki ya Stanbic barua ya kusudio la kuitoza faini ya shilingi bilioni 3. 

Sheria inaitaka benki ya Stanbic kutoa utetezi katika kipindi cha siku ishirini (20) ambacho kitaisha tarehe 30 Januari 2016. Endapo Benki Kuu haitaridhika na utetezi, benki ya Stanbic italazimika kulipa faini hiyo.

Hitimisho

Benki Kuu imechukua hatua hizo kama onyo kwa benki ya Stanbic na ili iweze kuwa makini katika kuhakikisha kuwa shughuli zake zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za kibenki na kuzingatia Sheria.

Aidha, hatua hii ni onyo kwa mabenki na taasisi za fedha zisijihusishe na makosa ya aina hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibenki na ni uvunjaji wa Sheria za nchi.

Hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa benki au taasisi ya fedha yoyote itakayobainika kwenda kinyume na taratibu za kibenki na Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Januari 18, Ikiwemo ya Lowassa Kuipa Jeuri Ukawa

BIFU la Wanamuziki Diamond na Ali Kiba Lafika Pabaya

0
0

DAR ES SALAAM! Kutokana na mwenendo wa bifu lao la chini kwa chini ni dhahiri mafahari wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platmumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wamefika pabaya kwani safari hii zimeibuka tuhuma za kuzibiana riziki kimataifa, Ijumaa Wikienda linashuka na mchapo kamili.

Chanzo makini kimeeleza kuwa, Team Kiba ambao umoja wao unaonekana zaidi katika Mtandao wa Instagram, wamecharuka vibaya wakimtuhumu Diamond kuwa anawasiliana na vituo vya kimataifa kama MTV na kuwaambia wasipige nyimbo za King Kiba.

“Jamaa hafanyi fea, anawasiliana na wale wa vituo vya kimataifa na kuwaambia wasipige nyimbo za Kiba, anamzoofisha kweli,” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.

Mara baada ya kusambaa kwa taarifa hizo za Diamond ‘kumficha’ mwenzake kimataifa, Team Kiba na Team Diamond walianza kuporomosheana matusi mazito mtandaoni.

Team Kiba waliapa kufanya ziara nchi nzima kushinikiza Diamond aache ubaguzi huku Team Diamond wakimtetea msanii wao wakisema si kweli kwamba anafanya hivyo bali amekuwa akiwasaidia wasanii wengi hivyo Team Kiba wanatapatapa.

Baada ya ubuyu huo kutua mezani, mwanahabari wetu alimsaka King Kiba kupitia simu yake ya mkononi ambapo alisema kama kweli vituo hivyo vinamsikiliza Diamond, vitakuwa havimtendei haki.

“Kama kweli MTV watakuwa wanampatia jukumu Diamond la kupitisha ngoma zetu basi watakuwa hawafanyi fea, sidhani kama ni kweli wanafanya hivyo na Diamond anaweza kufanya hivyo,” alisema Kiba.

Akijibu tuhuma hizo mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond alikaririwa katika Televisheni ya Taifa (TBC 1), akielezea namna ambavyo amekuwa akisikitishwa na watu kumwambia anawabania baadhi ya wasanii kupigwa kimataifa na kusema wanamuonea.

Source: Global Publishers

Bavicha Wataka Chama Cha Mapinduzi Kifutiwe Usajili Kwa Kuwa Kimeonyesha Ubaguzi wa Rangi Zanzibar

0
0

Baraza la Viajana wa Chadema (Bavicha)  limemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini kutoa tamko kuhusu vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyooneshwa na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa sherehe za maadhimisho ya Mapinzuzi ya Zanzibar.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeye alisema kuwa kutokana na vitendo hivyo vya kibaguzi, msajili anapaswa kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuifutia usajili CCM.

“Sheria ya usajili wa vyama vya siasa iko wazi. Sheria ya usajili wa vyama vya siasa inasema, chama chochote kitakachofanya siasa za kibaguzi huenda wa kikabila, kidini ama vinginevyo chama hicho kitafutwa. Tunataka kauli ya msajili wa vyama vya siasa. Ni lini, wakati gani ataifuta CCM,”alisema Simbeye.

Simbeye alisema kuwa Baraza hilo la vijana la Chadema linamtaka msajili kutoa tamko lake ndani ya kipindi cha siku tatu na kwamba asipofanya hivyo, watachukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani.

“Msajili wa vyama vya siasa atuambie ni lini sheria hiyo imeondolewa mpaka leo CCM ni chama cha siasa kwenye taifa hili. Vinginevyo, ndugu waandishi wa habari tumepanga… na haya ndio maazimio ya vuguvugu hili, tutampeleka mahakani,”alisema.

Wakati hayo yakiendelea, uongozi wa CCM ulitoa tamko na kuomba radhi kwa vitendo vya kibaguzi vilivyojitokeza kwenye sherehe hizo ambavyo vilifanywa na kundi la watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama hicho. Watu hao walibeba bango lenye ujumbe wa kibaguzi.

Tanzia: Mwandishi wa 'Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe' afariki

0
0

Mwandishi maarufu wa tamthilia na kitabu cha ‘Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe’, Edwin Semzaba amefariki jana.

Mbali na kuwa mwandishi maarufu, Semzaba alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia, alikuwa mwenyekiti wa Umoja Wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA).

Semzaba ambaye kitabu chake cha Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe kilimpatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, aliwahi kueleza kuwa alianza kuandika kitabu hicho akiwa anasoma kidato cha pili akiwa na umri wa miaka 16 tu.

Aliimalizia kazi yake hiyo nzuri baadae ambapo ilikubalika na kuanza kurushwa kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadae kuiweka katika kitabu kilichokubalika na kutumika kama kitabu cha kiada kwa shule za sekondari.

Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na taifa kwa ujumla. Apumzike kwa amani, Amina!

Hakuna Kupanda Ndege Bila Kibali cha Raisi...Hapa Kazi Tu Inaendelea..

0
0

Katika kile kinachoonekana kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli haitalegeza kamba linapokuja suala la kusitisha safari holela za nje za watumishi wa umma, Idara ya Uhamiaji imesema bado inakagua uwapo wa barua ya mwajiri na kibali maalum cha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Awali, ili kusafiri nje ya nchi mtumishi wa umma alihitaji pasi ya kusafiria yenye viza na tiketi.

Akizungumza na Nipashe kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile, Msemaji wa Idara hiyo Tabu Burhan, alisema idara hiyo inaendelea kusimamia kikamilifu maelekezo ya Rais.

Katika utekelezaji wa agizo hilo, kila mtumishi wa umma anayesafiri nje ya nchi anatakiwa kuonyesha barua ya mwajiri wake na kibali cha Ikulu, alisema.

Burhani alisema Idara hiyo inafanya ukaguzi huo katika vituo vya usafiri kama viwanja vya ndege na mipakani ili kubaini watu watakaokiuka kwa makusudi agizo la Rais Magufuli.

Burhan alisema ingawa kazi ya kuwadhibiti watumishi wa umma wanaosafiri nje ni ngumu kutokana na hati zao za kusafiria kutoonyesha kazi wanazofanya, lakini wamejipanga vizuri kutumia mbinu mbalimbali kuwabaini.

Tutawabana wakija kugonga mihuri hati za kusafiria, tukigundua ni mfanyakazi wa serikali tutamuomba atupatie barua kutoka kwa mwajiri na kibali cha Ikulu, kama hana tunamrudisha na hataweza kusafiri,” alisema Burhan.

Alisema zamani ilikuwa rahisi kwa kila mtumishi aliyetaka kusafiri nje ya nchi kutambulika kazi yake kwasababu walikuwa wakitakiwa kujaza fomu iitwayo TIF 10 na TIF 12, mfumo ambao ulisitishwa mwaka 2005 baada ya kuanza kutumika hati za kusafiria za kieletroniki.

“Tunawashauri watumishi ambao wanataka kusafiri wajiridhishe wenyewe kwanza, itakuwa usumbufu na hasara endapo tutawarusidisha wakiwa tayari uwanja wa ndege,” aliongeza.

Akizungumzia idadi ya watu waliozuiliwa tangu kuanza kwa utekelezaji wake, msemaji huyo alisema mpaka sasa hakuna mtumishi aliyenaswa mbali na wafanyakazi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ambao tayari wamesimamishwa kazi.

Watumishi hao ni Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani, Rukia Nikitas na Mary Mosha.

Agizo la kuwazuia watumishi kusafiri nje lilitolewa na Rais Magufuli siku moja baada ya kuapishwa kwa lengo la kubana matumizi ya serikali na hadi sasa ameshaokoa mabilioni ya fedha.

Akilihutubia Bunge la 11 na kulizindua mwishoni mwa mwaka jana, Rais Magufuli aliwataka watanzania na wabunge waunge mkono uamuzi wake wa kupiga marufuku safari za nje ambapo fedha nyingi zitaokolewa na kutumika kwenye huduma za jamii kama barabara, afya na elimu.

Alitoa mfano kuwa katika mwaka wa fedha wa 2013/2013 na nusu ya 2014/2015 pekee, safari za vigogo nje ya nchi ziligharimu Sh. bilioni 356.3 fedha ambazo alisema zingeweza kujenga barabara yenye urefu wa Kilomita 400 au kutimiza miradi mbalimbali ya jamii.

Alisema tiketi za ndege pekee ziligharimu Sh. bilioni 183.160, mafunzo ya nje ya nchi Sh. bilioni 68.612 na posho za kujikimu Sh. bilioni 104.552.

Novemba mwaka jana, Ikulu ilisambaza mwongozo unaoweka masharti ambayo watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi watatakiwa kuyatimiza ili wapewe kibali cha kusafiri.

Sharti la kwanza ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue na maombi yawasilishwe kwa Msajili wa Hazina kabla ya kwenda kwa Sefue ili aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wa safari hiyo na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.

Sharti lingine linamtaka Mtendaji Mkuu wa Shirika ama taasisi apime kama safari hiyo ni muhimu kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kabla ya kuwasilishwa Hazina na aeleze manufaa ambayo nchi itapata kutokana na safari hiyo.

Pia sharti lingine linataka mhusika aeleze umuhimu wa safari hiyo na isipofanyika itaathiri vipi nchi. Mwombaji aanatakiwa aeleze manufaa ya safari hiyo kwa taasisi na taifa; kama imewahi kufanyika huko nyuma ilisaidia nini.

Ofisi za Umma zilipokea barua kutoka kwa Msajili wa Hazina Novemba 12 mwaka jana ikieleza kuwa Rais Magufuli ametoa zuio la jumla kwa safari za nje ya nchi katika utumishi wote wa umma na mihimili yake. Barua hiyo ya Hazina ilisema zuio hilo litadumu hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Kulihitajika Uchunguzi wa Kina Dhidi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Dr. Faisal Kwanza Kabla ya Kufukuzwa

0
0

Ukweli ni kuwa kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Dr. Faisal kumeambatana na ukiukwaji mkubwa wa maadali ya utumishi wa umma! Dr. Faisal amefukuzwa kazi kwa kuegemea ushahidi wa upande mmoja huku chanzo cha kufukuzwa kwake kikiwa hakijawekwa bayana! Hili ni tatizo kubwa! 

Tunaambiwa kuwa rais Magufuli alichukuwa uamuzi wa kumfukuza kazi mtumishi huyo wa umma muda mfupi sana baada ya kupokea simu kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza ndugu Magesa Mlongo! 

Kimsingi rais alitakiwa kupima kwa kina aina ya mtu anayempa maelezo! Magesa Mlongo !mashitaka yake kwa rais yalitakiwa kupimwa kwa umakini mkubwa! Kulitkiwa subira na uchunguzi wa kina hasa ikizingatiwa historia aliyo nayo ndugu Mlongo!

Tungependa kuona haki inatendeka na utu unalindwa dhidi ya hili!

By G Sam From Jamii Forums

Matokeo Ya Kidato Cha Pili Yaingia Dosari......Wamiliki Wa Shule na Vyuo Wataka Mfumo wa GPA Ufutwe

0
0

WAMILIKI wa Shule na Vyuo Visivyo vya Serikali wameiomba Serikali kufuta mfumo wa GPA unaotumiwa na Baraza la Mitihani (Necta) kupanga madaraja ya mitihani ya sekondari, kwa maelezo kuwa haufai kwa kuwa unahalalisha watahiniwa waliofeli waonekane wamefaulu.

Akizungumza jana Dar es Salaam kuhusu matokeo ya kidato cha pili ambayo yametangazwa na Necta hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (TAMONGSCO), Benjamin Nkonya alisema matokeo hayo hayaeleweki kwani wameshuhudia baadhi ya wanafunzi wanaoonekana kufanya vizuri chini ya mfumo wa GPA wakati katika mfumo wa madaraja (division) wanaonekana wamefanya vibaya.

Kwa hali hiyo, Nkonya amemwomba Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kufuta mfumo huo hadi pale Necta itakapokuwa tayari kujibu maswali kadhaa ya wadau wa elimu ambao wanaona mfumo huo hauna tija katika kuboresha elimu.

Baadhi ya hoja ambazo zilihojiwa na Nkonya ni kwamba kulikuwa na kasoro gani katika mfumo wa madaraja mpaka ukaja huo wa GPA na akataka kujua ni nani alilalamikia mfumo wa division mpaka ukaondolewa? Alihoji kabla ya mfumo huo kuletwa, ni wadau wapi walishirikishwa?

Alisema TAMONGSCO ilipata taarifa za kuwepo kwa mfumo huo wa GPA kupitia vyombo vya habari na hawakushiriki katika ngazi yoyote ya mijadala ya kisera kama sheria inavyoelekeza. 

Katibu Mkuu huyo wa TAMONGSCO alihoji, “Je, alama za chini za gredi D, C,B na A zilibaki kama zilivyokuwa wakati wa mfumo wa division au kuongeza gredi E na B+ ilikuwa mbinu ya kushusha alama za ufaulu na matumizi ya GPA yakaanzishwa kwa lengo la kuficha ukweli kuwa viwango vimeshushwa kwa kiasi kikubwa??

Nkonya pia alihoji mfumo huo una faida zipi na unasaidiaje katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaomaliza wanakuwa na ujuzi stahiki utakaowawezesha kuhimili changamoto za soko la ajira na utandawazi?

“Kwa hali hii bado tunaishauri Serikali isitishe matumizi ya mfumo wa GPA hadi pale hoja zetu zitakapopatiwa ufumbuzi,”alisema Nkonya.

Wahariri Wa Gazeti La Mawio Wajisalimisha Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi Jijini Dar Es Salaam Leo.

0
0

Wahariri wa Gazeti la Mawio wakijisalimisha makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Jeshi la Polisi kutangaza kuwatafuta popote pale kwaajili ya kutoa maelezo kwa kuandika habari ya upotoshaji kwa jamii, wakiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Abalom Kibanda katika makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.

Wahariri wa gazeti la Mawio wakizungumza  leo walipokuwa wanajisalimisha makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Abalom Kibanda  akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kufungiwa na Serikali gazeti la Mawio jana.

Picha Zikionyesha Jinsi Wananchi Wenye Hasira Kali Walivyofunga Barabara ya Kinondoni Mkwajuni na Kuchoma Matairi Kupinga Bomoa Bomoa

0
0

Jeshi la Polisi Jumatatu hii limezima ghasia za wananchi wenye hasira maeneo ya Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam baada ya kupinga zoezi la bomoa bomoa kwa mara ya pili kufuatia kukataa kuondoka katika eneo hilo kwa madai hawana pa kwenda.


Bi Fatuma akizungumza kwa uchungu

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii mmoja kati ya waathirika wa bomoa bomoa hiyo, Bi Fatuma Said, amesema wanashindwa kuondoka katika eneo hilo kwa kuwa hawana sehemu ya kwenda huku akiitaka serikali kuwafikiria.

“Sio kwamba tumegoma kuondoka wengine sisi hatuna sehemu ya kwenda,” alisema. “Sisi baada ya kubomolewa nyumba yetu tukashindwa kuondoka kwa kukosa pa kwenda.Tukaamua kujenga hapa vijibanda ili serikali itufikirie lakini tunashangaa leo asubuhi vibanda vyetu vimewekwa X kwamba wanataka kubomoa. Saa tano tumeingiliwa kwenye vibanda vyetu sisi tukakimbia wao wakachoma ndio baadhi ya wanacnhi wakaingiwa na hasira na kwenda kuchoma matairi barabarani,”alieleza.

Hata hivyo Bongo5 ilijaribu kuzungumza na afisa wa polisi aliyekuwepo katika eneo hilo, lakini alisema watatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo. Hadi sasa polisi wanawashikilia vijana kadhaa wanaohusishwa na tukio hilo.

Tazama picha zaidi:




Saed Kubenea kufufua Sakata La Escrow bungeni

0
0
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (CHADEMA) amesema anatarajia kufufua hoja ya kujadiliwa upya kwa ripoti ya fedha zilizokwapuliwa za Tegeta Escrow zaidi ya Sh bilioni 200.
Akizungumza jana alisema sababu za kutaka mjadala huo kurejeshwa ni kutaka kujua iwapo fedha hizo ni za umma au ni mali ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Sababu nyingine aliyoitaja Kubenea ni kutaka kuchukuliwa hatua kwa wahusika wa sakata hilo, ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika Bunge la 10, iliwasilisha bungeni mapendezo zaidi ya 10 likiwemo azimio namba moja la kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), kumkamata Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pan Africa Power Ltd (PAP) Harbinder Singh Sethi na kumfikisha mahakamani kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na ukwepaji kodi.
Kamati inaelekeza Serikali kutumia sheria za nchi, ikiwamo sheria ya Proceeds of Crime Act, kuhakikisha kuwa Singh Sethi anarejesha fedha zote alizochota kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG iliyothibitishwa na TAKUKURU, fedha hizo pia ziligawiwa kwa watu binafsi.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe, alisema kamati yake ilijiridhisha kuwa fedha iliyotumika kulipia manunuzi hayo ni fedha ambayo sehemu yake ni ya umma iliyochotwa bila huruma wala aibu, kutoka Benki Kuu (BoT).
Akaunti hiyo ilifunguliwa na Serikali kwa pamoja kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya IPTL.
Fedha hizo zilizua mjadala mkubwa bungeni, ambapo Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliweka msimamo wa Serikali kupitia mkutano wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, akisema kuwa fedha hizo hazikuwa za umma na hivyo kuzidisha mjadala.

Kuhusu ile Bifu ya 50 Cent na Meek Mill Inayotikisa Mitandaoni.

0
0
Meek Mill na 50 Cent wameteka mtandao wa kijamii wa instagram baada ya kurushiana maneno makali na kutangaza rasmi beef kati yao.

Beef hii imetokana na maneno ya Meek Mill kwenye wimbo wake wa ‘Gave Em Hope’ kutoka kwenye mixtape yake ya Dream Chasers 4 Au 4-4 .

50 Cent aliandika kwenye instagram ujumbe huu ukiambatana na picha ya Meek Mill.
Hey shit head, your career is over already,You better focus on getting Nikki pregnant so you can at least get child support girl.

Haya ni mashairi ya Meek Mill kuhusu 50 Cent
You popping shit on your Instagram, Shit that you’re popping ain’t adding up / Shit that you’re popping ain’t making sense / I got 50 reasons say you’re taking dick / And it’s 50 reasons I should kill, nigga / But, for real, nigga, I been taking trips with my Philly niggas / Got the richest chick, she’s from your hood / Niggas hating on me, I ain’t really tripping, shit, I’m good / I be in the 40 with the .40 on me like I should / I be deep in your ‘hood where you never be at / Be with them guys that you never could never dap / You could never adapt / You know the game, if you cosign a rat, you forever a rat / We were never with that / You tried to go ‘Money’ May with that paper, but now you in debt cause you never was that.

Meneja wa Murder In naye aliandika kuhusu 50 Cent kwenye kurasa ya Meek Mill nakusema … “50 Cent amezoea kuwapa watu mambo ya uongo ,acha kushindana naye kama wew ni msema ukweli hutoshinda”
50 Cent ameripotiwa hivi karibuni kuwa alisema uongo kuwa amepigwa risasi mara tisa kumbe alipigwa risasi mara 5 au 6.
Fahamu kuwa ni muda mzuri kwa Meek Mill kuwa na beef sababu ya kutangaza Mixtape yake mpya ili isikilizwe zaidi mtandaoni na kila inavyosikilizwa ndivyo anavyopata pesa na show nyingi zaidi, jina lake pia linaongelewa kila sehemu kwenye mitandao tofauti.

Video: Shilole na Nuh Mziwanda walivyokutanishwa kwenye kipindi cha Clouds Tv bila kujijua

0
0
Weekend iliyopita kipindi cha D’Weekend Chat Show cha Clouds TV kilijaribu kuwakutanisha Shilole na aliyekuwa boyfriend wake, Nuh Mziwanda kwa lengo la kutaka kuwapatanisha.

Jitihada za kuwakutanisha studio (bila wao kufahamu) zilifanikiwa, lakini lengo la kutaka kuwapatanisha liligonga mwamba, na Shilole alionekana kuchukizwa na kitendo cha kukutanishwa na ex wake bila mwenyewe kuridhia, huku Nuh alionekana kuwa tayari kile kilichokusudiwa kufanywa.

Tazama hapa kama hukupata nafasi ya kuona kipindi hicho:

Breaking News;Shehena Kubwa yakamatwa Bandari Bubu Tanga.

0
0
Shehena kubwa ya Bidhaa Haramu ikiwemo Matairi,sukari,mafuta ya kupikia imekamatwa Bandari bubu Tanga kutokea Zanzibar. Operesheni hiyo imefanywa na Mapolisi 100 ikishirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na Usalama. Vyombo vilivyohusika katika usafirishaji wa shehena hiyo vyote vimetaifishwa.
Walikuwa wanakwepa Kodi. Hii vita ya Uhujumu UCHUMI ni nzito.

Chanzo: ITV.

Udaku Special Blog

Lowassa: Wabunge na Mameya Wasiowajibika Tutawafukuza CHADEMA

0
0

Lowassa ameyasema hayo wakati wa kikao maalum na Mameya na Manaibu wao kutoka Manispaa ya Ilala na Kinondoni waliokwenda kumuona na kumpongeza kwa kuwawezesha kushinda katika Manispaa za Ilala na Kinondoni.

Alisema wameishakubaliana kama wabunge na Madiwani watashindwa kuonyesha uwezo wa kufanya kazi za wananchi katika mwaka wa kwanza na wa pili wataondolewa ndani ya chama.

Alisema CHADEMA siyo chama cha kuendelea kuwa wapinzani. ‘’Tunajenga chama kinachokiandaa kushika dola muda wowote itakapopatikana fursa. Tunataka kuithibitishia dunia kwamba tunaweza kuongoza dola muda wowote zaidi ya CCM’’ Alisema Lowassa.

Udaku Special Blog
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images