Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Updates Kuhusu Kujiuzulu Kwa Kamati ya Miss Tanzania Leo

$
0
0
Miss Tanzania
Kama ya shindano la Miss Tanzania, imetangaza kujiuzulu.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya shindano hilo Juma Pinto, amedai kuwa sababu ya kujitoa kwenye kamati hiyo ni kutokana na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda, Lino Agency.

Amedai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.

Pinto amesema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi hatupo huko,” amesema Pinto.

Naye msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo amesema kutokana na ukubwa wa kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na kiubinafsi.

“Waangalie wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.

Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.

Kamati hiyo ya Miss Tanzania ilitambulishwa August mwaka ikiwa na wajumbe wafuatao:

1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi – Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Wajumbe wa Sekretariet ni:

1. Dr.Ramesh Shah
2. Hidan Ricco
3. Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

Diamond Azidi Kuwatia Maumivu Mashabiki wa Wema Sepetu, Adai Ustaa Bila Nyumba ni Shombo Kuvunda

$
0
0
Mwanamuziki Diamond Jioni ya leo Amepost picha hiyo hapo juu na kuandika maneno ya kejeli ambayo mashabiki wa Wema Wameyachukulia kama ni dongo kwa Wema Sepetu..

Diamond Ameandika Haya katika hiyo picha akiwa kwenye Swimming Pool Nyumbani Kwake..

How my Evening is going like.... #StateHouse raha ya Ustar uwe na yako Nyumba, sio Shombo Kuvunda!

Baada ya Muda Picha Hiyo na Meneno hayo kuwekwa Team Wema Wamevamia page hiyo na kuanza kuandika maneno ya Shombo mengine ni ngumu kuyaweka Hapa

Baada ya Comment kutoka katika post hiyo hizi Hapa;


Hilwa05
Sasa ww @diamondplatnumz mwenyewe ushaimba kama hujui maisha yako ya kesho kwanini uandike hayo unaweza kushuka ww na wema akapanda acha dharau hizo


mbitegeko
@yamotoband mna nyumba, @harmonize je ana nyumba ,shettazz una nyumba , shombo nyingine

Ayanig 
Fuck the shut...... Wewe siulikuwa unaishi kwa Wema, unakula kwake Loooo mwanaume kama binti kichwa majii  wewe ...na huyo Zari umkomee Wema

 Edithmadenge
Your so full of hate,I pray that it consumes you@diamondplatnumz


Aluminium_bussiness
unajua kumwambia dai akapime dna ni kama kumvua chupi umwambie atembee barabarani! acheni jamani mtaleta maradhi kwa huyu kaka! tupende masuper star wetu



Msikilize Hapa Zari Akiongelea Kuhusu Wema na Team Yake Kumtukana Tiffah, DNA na Katunzi

$
0
0
Diamond, Zari na Tiffah
Wiki hii inaisha huku kukiwa na stori kubwa zilizoanzia kwenye mitandao ya kijamii, majibizano yaliyofanya mpaka ishu ya watu kutaka DNA ya mtoto wa Diamond Platnumzna Zari iwekwe wazi ili ijulikane kama kweli ni mtoto wake.

Diamond alijibu hii ishu kwenye exclusive interview, na pia Soudy Brown kaamua kumtafuta Zari kusikia pia anachukuliaje hizo story za mitandaoni.

Zari kasema kachoshwa na maneno kuhusu mtoto wao Tiffah, kwanza hawahusu chochote kwa hiyo hata kama ni mtoto wa Diamond au sio wake, wanaozungumzia DNA hawamhusu chochote.
Kingine Zari amesema wana mtoto huyo mmoja lakini yuko tayari hata kuwa na watoto watatu na Diamond.

Soudy Brown ‘Makorokocho‘ na Zari utawasikia kwenye hii U Heard niliyorekodi na kukusogezea sauti yake hapa, bonyeza play uipate mtu wangu.

Nay wa Mitego Auelezea Mkasa wa Mwanae Curtis na Mzazi Mwenzie Siwema

$
0
0
Rapa Nay wa Mitego amedai alimnyang’anya ex wake Siwema mtoto wao Curtis baada ya kile alichodai mwanadada huyo kuendekeza starehe za club pamoja na kusafiri nje ya mkoa kwa zaidi ya wiki mbili huku akiwa amemuacha mtoto nyumbani.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay alisema aliamua kumhifadhi lakini huu ni wakati wake sahihi wa kuweka wazi kila kitu ili wengine wajifunze.

“Sio kwamba sikuwa na matatizo kwa mzazi mwenzangu ila yake yalikuwa yamezidi na nilikuwa napata taarifa nyingi,” alisema Nay.

“Nilikuwa naambiwa mambo mengi lakini ilifika time mwenye nyumba wa nyumba ambayo alikuwa anakaa yeye alikuwa ananipa taarifa nyingi na kuniambia ‘mimi namwonea huruma huyo mtoto, sitaki kuwaachanisha kama mama yako yupo kwanini usiongee na huyu mwanamke wako ukamchukua huyu mtoto!’

Wakati anaanza kufanya mambo yake alikuwa anajificha lakini ilipofika time akawa anajiachia tu, kiasi kwamba mimi nikawa napata taarifa. Kuna washkaji wangu wakawa wananipigia simu wewe huyu mpenzi wako si analea mbona tuko naye club? Mimi nikimpigia anarukaruka lakini ukweli ulikuwa unaonekana” alifafanua.

Aliongeza, “Mimi nilikuwa namwambia huyo mtoto bado mdogo kama unahisi mimi na wewe penzi letu limefika tamati hebu ngoja huyu mtoto akue. Baada ya muda nikasikia unajua gari zangu zote zina plate namba 966, kuna gari ambayo mimi nilikuwa naitumia nikampa ilikuwa Mark X. Hiyo gari ikawa imeonekana sehemu za Geita. Kuna mtu akanipigia kuniuliza kama nipo Geita nikamwambia no, hiyo gari ni yangu lakini sipo huko hebu nipigie picha hiyo gari, akapiga picha akanitumia ilikuwa car wash.

Nikamwambia ni kweli hiyo gari ni yangu ikabidi nimpigie simu Mama ‘Curtis’ akaniambia nipo nyumbani, nikamwambia no haupo nyumbani. Nikamwambia kama upo nyumbani naomba nimsikie mtoto kwa bahati mbaya au nzuri kipindi kile alikuwa amefungua duka la nguo akasema nipo dukani na mtoto yupo nyumbani. Kumbe yupo Geita ana wiki ya pili na hajui mtoto anaendeleaje!. Watu wamezungumza sana kuhusu hili suala ila this time ngoja nizungumze ili kila mtu ajue.”

“Mwisho wa siku nikagundua ni kweli alikuwa two weeks bahati mbaya msichana wa kazi aliyekuwa nyumbani kwangu baada ya kuzinguana na msichana wake aliyekuwa anakaa naye pale, ikabidi msichana wangu mimi atoke nyumbani kwangu aende Mwanza kwa ajili ya kukaa na mwanangu. Kwahiyo asingeweza kunificha chochote.

Kwahiyo nilikuwa napata taarifa kila sehemu. Siku moja nikaona mtoto wangu ataharibika, kuna mtu akanipigia simu akaniambia leo ilikuwa saa kumi alfajiri naambiwa mpenzi wako yupo na mwanaume nilikuwa natoka studio nikaamua kwenda kumchukua na toka nimemchukua mpaka leo hajawahi kupiga simu.”

Download Android Application ya Udaku Special Blog Bonyeza HAPA Kudownload Kutoka Play Store

Nape Nnauye: Kasi Ya Rais Magufuli Itaviua Vyama Vya Upinzani Hapa Nchini

$
0
0
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kasi ya utendaji kazi ya Rais John Magufuli inaweza kuua uwepo wa vyama vya upinzani nchini.

Hata hivyo alisema kuwa hangependa upinzani ufe kwa vile hiyo pia itakuwa imeua demokrasia nchini na kudai kuwa lengo la kuanzisha vyama vya siasa haikuwa kuviua bali ni kuviona vikiendelea kuwepo.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu huyo wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya miaka 39 ya CCM ambayo kilele chake kimepangwa kufanyika mkoani hapa Februari 6, mwaka huu badala ya Februari 5 iliyozoeleka.

Alisema kuwa chama kimelazimika kubadili tarehe ya kilele ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo maadhimisho hayo kwa kufanya kazi badala ya kuwa na sherehe mbalimbali.

“Maadhimisho ya safari hii ni tofauti na ya miaka mingine. Safari hii wananchi watatakiwa kushiriki zaidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. Kauli mbiu yetu ni ‘Sasa kazi’ hivyo watu wafanye kazi ili wajiletee maendeleo yao wenyewe,” alisema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 23, Ikiwemo ya Jokate na Kiba Kumwagana

$
0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 23, Ikiwemo ya Jokate na Kiba Kumwagana

KIMENUKA..Jokate na Ali Kiba Wamwagana Kisa Hichi Hapa

$
0
0
Jokate na Ali Kiba Penzini
Hii ni habari ya kipekee (Exclusive Story)! Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wanadaiwa kumwagana, Risasi Jumamosi ndilo gazeti pekee linaloweza kuthubutu kukupa mchapo kamili.

Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo ambao walikuwa wachumba walioshibana, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wakiwa katika pozi.
Habari ya mjini kwa sasa ni juu ya wawili hao ambao walikuwa gumzo kwa watoto wa mjini, kwa kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake tofauti na walivyokuwa awali huku chanzo cha kutengena kwao kikitajwa kuwa ni wazazi wa sehemu zote mbili kutoridhiana.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, mbali na ishu ya wazazi, hivi karibuni Jokate na Kiba waliingia kwenye gogoro kubwa la kimapenzi baada ya kufumaniana kwenye simu, jambo ambalo limeendelea kutokea huku jamaa akiongoza kukutwa na meseji kwenye simu yake za mwanamke mmoja anayedaiwa kuishi nje ya Tanzania.


“Ukisema nikusimulie juu ya kumwagana kwa Jokate na Kiba basi tunaweza kukesha ila mbali na mambo ya wazazi, kwa kifupi tu ni kwamba, hawa watu wameingia kwenye mgogoro na kilichokuwa kikiwagombanisha mara nyingi ni uhusiano wao wa zamani.”

KIBA ANA DEMU?
“Mara kadhaa Jojo (Jokate) amekuwa akimlalamikia jamaa (Kiba) kuwa ana demu nje ya nchi ambaye amekuwa akimtundika katika mitandao ya jamii na kujinadi kuwa ndiye mkewe tofauti na wengi wanavyojua kuwa Jokate ndiye mtu wake.
“Mbali na hilo, sasa kuna suala la familia zao kuonesha hali ya kutokubaliana na wao kuoana hasa upande wa Jokate ambao ulionesha msimamo mkubwa kutomtaka hata kidogo Kiba, mambo hayo yamekuwa ni chagizo kubwa katika kuhatarisha mapenzi yao hivyo kufikia hatua hata ya wao kutoendelea kupendana kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo wa penzi lao.”

VIKAO VYAGONGA MWAMBA
“Tofauti na watu walivyozoea kuwaona pamoja, kwa sasa wametibuana na hapa tunapozungumza tayari kuna vikao kibao huko nyuma vilishakaa ili kunusuru penzi lao lakini imeshindikana maana kila mmoja sasa hivi anajifanyia mambo yake na hakuna dalili za kurudiana.
“Kiba anaonekana ameshajiingiza kwenye penzi la demu wake wa zamani huku Jokate naye akiwa ‘in love’ na mtu wake mwingine.”

MPANGO WA KUZAA WAYEYUKA
“Kitambo tu nimekuwa nikiwaambia kwa staili waliyokuwa nayo hakika wasingeoana hata kama ukiweka pembeni suala la dini zao kutoendana, maana kuna siku niliwasikia wakiambiana hata kama wazazi wakigoma wao wangefanya kila juhudi hata wazae pamoja tu.
“Lakini ukweli ni kwamba ilishindikana baada ya kuanza kugombana mara kwa mara, pamoja na kwamba Jokate alikuwa akikubalika kwa asilimia zote kwa mama Kiba na hata ndugu wengi wa Kiba walionekana kumpenda waziwazi,” kilisema chanzo hicho.

KIBA AFUNGUKA
Baada ya kupenyezewa mchongo huo, gazeti hili liliingia mzigoni kumtafuta Kiba ili atoe la moyoni juu ya madai hayo ya kumwagana na Jokate ambapo alipopatikana alisema kuwa haoni sababu ya kuzungumzia ishu hiyo kwani ni mambo binafsi.

Kusema kweli ishu hii mimi sina uwezo wa kuiongelea zaidi kwa sasa kwani ni mambo binafsi sana na sioni faida ya kuzungumzia vitu ambavyo havina maana.
“Kwanza sioni nini cha kuongelea hapa kwani kila jambo lina mipaka yake,” alisema Kiba akikataa kuulizwa zaidi juu ya suala hilo.

JOKATE VIPI?
Kwa upande wa Jokate alipotafutwa kwa siku kadhaa ili azungumzie sakata hilo kwa ufasaha hakupokea simu ya mwandishi wetu hadi gazeti linaingia mitamboni.

PENZI LA JOKATE NA KIBA
Awali zilipovuja habari za penzi la Jokate na Kiba wote walikanusha, kadiri siku zilivyosonga ndivyo walivyozidi kuwa gumzo kwa mashabiki wao waliofurahishwa na ‘kapo’ yao huku wakionekana kwenye viwanja mbalimbali vya starehe wakiwa kimahaba lakini sasa mambo yanaonekana kwenda mrama.

Source;GPL


Pata Stori za UDAKU Kirahisi Kwa Kudownload Android Application Kwenye Simu Yako Kwa Kubonyeza HAPA

Bernard Membe Akosoa Vikali Uamuzi wa Kufutwa Kwa Matokeo yote ya Uchaguzi Zanzibar..Adai Dunia Imehuzunika

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar

Amesema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo tu “Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake.

Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani? “Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.


Wataalam Wanashauri: Tuwapige Wake zetu Angalau Mara Moja Kila Mwezi

$
0
0
Wataalam wa mahusiano wanashauri ili mahusiano yadumu vizuri na kwa muda mrefu inabidi mume amuonye mkewe kila siku, amkalipie kila wiki, ampige kofi angalau mara moja kila mwezi, ampige kibano cha maana kila mwaka na amrudishe kwao angalau mara moja kila baada ya miaka mitano. Kwa kufanya hivi uamsha ari na upya wa penzi.

Nchi kama Marekani ambao kufanya domestic violence ni kosa kubwa sana ni moja ya nchi zinazoongoza kwa talaka duniani maana wanawake wanaota mapembe na kuona wenzi wao hawawajali lakini sehemu kama mara ni vigumu sana ndoa kuvunjika.

Kazi kwenu waoaji na waolewaji kuokoa ndoa zenu

Sarakasi Zaanza Tena Umeya Dar es Salaam...Uchaguzi Wahairishwa

$
0
0
HALMASHAURI ya jiji la Dar es Salaam imeahirisha uchaguzi wa meya wa Jiji uliokuwa ufanyike leo, mpaka hapo tarehe itakapotangazwa baadaye.

Mkuu wa Kitengo cha Itifaki na Uhusiano na Umma wa Jiji, Gaston Makwembe alisema uchaguzi huo uliokuwa ufanyike leo saa nne asubuhi katika ukumbi wa Mmikutano wa Karimjee, umeahirishwa.

Alisema tarehe ya uchaguzi huo itapangwa baadaye na taarifa zitatolewa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari bila kueleza sababu ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na mvutano wa aina yake kati ya vyama vinavyounda na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Diwani wa Kata ya Vijibweni, Isaya Mwita (Chadema) ndiye atapeperusha bendera ya Ukawa huku mgombea wa nafasi ya Naibu Meya akitarajiwa kutoka CUF. Chama Cha Mapinduzi (CCM ) wakiwakilishwa na Diwani wa Kinondoni, Yusuph Omary Yenga.

Inaelezwa kuwa Ukawa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho kutokana na kuwa na idadi kubwa ya madiwani ambapo wanaizidi CCM kwa jumla ya madiwani 13.

Ikiwa Ukawa watafanikiwa kutwaa jiji hilo, itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa wapinzani kuliongoza tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

Awali, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alitoa mwito kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusimamia uchaguzi huo kwa amani na haki ili usifanyike kama wa kumtafuta meya wa Ilala na Kinondoni uliokuwa na mizengwe mingi.

Siri ya Kuahirisha Uchaguzi wa Meya Dar Yajulikana..Ukawa Wadai CCM Ikimwaga Ugali wao Wanamwaga Mboga

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya mwamvuli wa Ukawa kimetaja mambo matatu  ambayo ndiyo yamechangia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliokuwa umepangwa kufanyika leo.

Taarifa ya Halmashauri ya Jiji iliyotolewa jana haikueleza sababu za kuahirisha uchaguzi huo zaidi ya kusema kuwa utafanyika katika siku itakayotangazwa baadaye.

Msemaji wa jiji, Gatson Makwembe hakutaka kuzungumzia sababu za kuahirisha uchaguzi huo.

“Siwezi kuzungumza mengi kwa sasa, ila ninachoomba wakazi wa Dar es Salaam wavute subira hadi tutakapotangaza siku ya kufanyika uchaguzi huu,” alisema Makwembe.

Juzi, Makwembe aliliambia gazeti hili kuwa walishapewa maelekezo  kutoka ngazi za juu yaliyowataka kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika Januari 23. Kwa mujibu wa katibu wa Chadema wa Kanda, Henry Kilewo, mambo hayo ni CCM kutaka kujipanga kuwarejesha wajumbe wake waliotimuliwa kwenye uchaguzi wa meya wa Ilala na Kinondoni, kuhofia upinzani kushinda kutokana na idadi yao, na hofu kuwa meya kutoka upinzani atafichua uozo unaotokana na jiji kuwa chini ya utawala wa CCM kwa muda mrefu.

“Mambo hayo matatu ndiyo ambayo yanawapa hofu CCM na kutumia nafasi yake ya chama tawala kuagiza jiji kuahirisha uchaguzi,” alisema Kilewo.

“Wakithubutu kuwaingiza wajumbe hao, na sisi tutafanya hivyohivyo. Waache wamwage ugali Ukawa tutamwaga mboga.”

Madiwani 161 kutoka halmashauri hizo wanatarajiwa kupiga kura kumchagua meya mpya atakayemrithi Didas Masaburi, ambaye alihamishia harakati zake za kisiasa kwenye ubunge wa Ubungo, lakini hakufanikiwa.

Kati ya madiwani hao, 87 wanatoka Ukawa, wakati 74 wanatoka CCM. Kwa maana hiyo CCM imezidiwa wajumbe 13 na vyama vya Chadema na CUF ambavyo vimeshinda viti vingi vya udiwani wilayani Ilala na Kinondoni.

Kilewo alisema wajumbe wa CCM ni wachache ukilingalisha na Ukawa, hivyo wamelazimika kufanya hivyo wakisubiri wajumbe ambao ni mawaziri  wamalize vikao vya Bunge ndipo wahudhurie.

Kilewo alikitaka chama hicho tawala kujiandaa  kisaikolojia kwani kuna maisha baada ya uongozi.

“Wanajua muziki wa Ukawa tukilishika jiji hili, tutakwenda kufumua uozo wao wote walikuwa wameuficha na kuwakosesha ulaji baadhi ya viongozi wao,” alisema Kilewo.

Kwa upande wake, Katibu Uenezi wa CCM mkoani Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadaffi’ alisema CCM haihusiki na kuingiza wajumbe katika baraza la madiwani, bali Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ndiyo yenye mamlaka hayo.

“Tatizo lao hawa wapinzani kila kitu wanapinga, hata wajumbe walioteuliwa na Rais kisheria hawataki washiriki katika baraza, halafu ndiyo wanasema wanafuata sheria?” alihoji Gadaffi.

Alisema CCM ni chama makini na kinafanya maamuzi ya busara, kwa kuwa kimemteua mgombea wa umeya aanayekubalika na kila mtu, tofauti na  mshindani wake.“Usishangae hata huu uchaguzi wa meya wa jiji wajumbe wa upinzani wakatupigia kura kama walivyofanya kule Temeke, kwa sababu ya umakini wa CCM ya kuweka mtu anayekubalika,” alisema Gadaffi.

Picha ya Mwanaharakati Joyce Kiria Yasababisha Utata Mtandaoni...Wengi Wamkosoa Kwa Kumwaga Radhi

$
0
0
Joyce Kiria
Jana Katika Mtandao wa Instagram Mwanaharakati wa Mambo ya Wanawake kupitia kipindi cha Wanawale Live Aliamua kubreak the Internet kwa kupost picha hiyo hapo juu ikiwa inaonyesha Sehemu kubwa ya paja....Mashabiki wake hawajachukulia kitendo hicho vizuri na kuanza kumshambulia kwa Comments....

Caption ya Picha Hiyo ilikuwa '2016 uzee nimeuacha Himo njia panda..no more charanga..am beautiful, hot and Sexy..Good Evening'

Nimekuwekea Baadhi ya Comments za mashabiki wake hapa;

hansdady 
Unapoelekea sasa si pazuri nakuomba angalia ulipotoka hiyo picha si ya superwoman ninayemfahamu mm

richardbendera
Don't let yourself to loose your value. Really your beauty and sex phenotype but keep your body in respect ways coz you have a family and young kid, how will you see when he grown up and became a man

marrymasawe123
Umevaa nguo ya heshima sana imekupendeza 59min

 kadaughter_daniel 
Unajishushia thamani yako loh unapoteza mashabiki Nahisi una tatizo sio bure

sophiammasy
yesurua ...nkiki lanye? ode.ode..odendao....m 12h

 prosperpascal.pp
Joyce that post umebugi Dada mapaja nje looooh afu uzeee huo

upndjohnsoo321
Yeye anaakili zake timamu!! Nafkiri alitaka kujua nini kitasemwa juu ya hili.. Tusiumie juu ya maisha ya mtu jamani hayatuhusuuuuuuuuu kiruuuu, tuangalie yetu jamani!! Binafsi naona yuko sawa tu sababu ni yeye!! Huwezi kuniambia eti nimfate yeye kwa kila kitu. yeye ni yeye aweza kufanya lolote juu ya maisha yake na nikwafaida yake haimuhusu mtu.. Ww angalia kinachokufaa ww ambacho hakikufai achana nacho kibooo!! Tumeumbwa tofauti nahata kimtazamo tuko tofauti yeye anafikiri nini siri yake hatujui, anapata nini hatujuiii siri yake @joycekiria kwako nitaiga ambacho naona kitanifaa ambacho naona hakitanisaidia nitakiacha lakini sikazi yangu kukukosoa 11h

sangaweofficial
Wakuwache Fanya unachojisikia.... Kwan hakuna ulipomtukana mtu.... 11h

 mamy_ben13
Hakuna kabisa hapana buana unaheshimika na watu wengi hapo umefika mbali usisahau kujistil buana

martin_de_boy Mhhhh mbn unanidatishaaaa sasaaa my wnguuuu 2h


Steve Nyerere Ahenyeshwa Polisi Kwa Utapeli wa Sh Mil 13

$
0
0
Steve Nyerere
DAR ES SALAAM: Msala! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amedaiwa kuhenyeshwa polisi kutoka na msala wa rafiki yake kuaminiwa fedha za matengenezo ya gari na kuanza ‘kupiga karenda’ matengenezo hayo bila sababu za msingi.

Chanzo makini kimeeleza kuwa, miezi kadhaa iliyopita, Steve alimpeleka rafiki yake aitwaye Mohamed maarufu kwa jina la Mo kwa tajiri wake (jina tunalihifadhi) kisha akamtambulisha kuwa anafanya shuguli za kuuza na kutengeneza magari ndipo Mo alipotumia mwanya huo kuchukua fedha na kumzungusha tajiri huyo.

“Tajiri alivyotambulishwa na Steve kwamba Mo ni rafiki yake, wakabadilishana namba za simu na ndipo siku moja huyo tajiri akampa Mo dili la kutengeneza gari yake iliyokuwa imegongwa kwa shilingi milioni 13, Mo akachukua hela lakini kila akiulizwa lini gari itatoa, hatoi majibu.

“Akawa anapiga chenga, mara niko Sauz mara niko wapi. Sasa huwezi amini tajiri akahisi Steve naye amehusika. Ikabidi ampeleke Polisi Oystebay, akahenyeshwa kwelikweli ili aeleze ukweli anavyomfahamu Mo lakini bahati nzuri akaachiwa baada ya polisi kujidhirisha,” kilisema chanzo hicho.

Alipoulizwa Steve kuhusiana na tukio hilo, hakutaka kufafanua kwa undani zaidi akamuomba mwandishi wetu aachane nalo akidai ‘soo’ hilo wameshalimaliza Mo na huyo tajiri.

“Mi naomba tu uachane nayo hiyo ishu, wameshamalizana wenyewe, lipotezee,” alisema Steve na kukata simu.

Chanzo: GPL

Simbachawene.. Ndani Ya Miaka Miwili Hakuna Mwanafunzi Atakaye Kaa Chini Kwa Kukosa Dawati

$
0
0
Simbachawene
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema atahakikisha shule zote hapa nchini zinakuwa na madawati yanayofanana.

Alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia changamoto za elimu bila malipo iliyoanza kutolewa Januari mwaka huu.

“Katika historia ninayotaka kuandika ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini katika kipindi cha miaka miwili lazima tuondokane na tatizo hili,” alisema na kuongeza kuwa atakuja na ubunifu utakaoondoka tatizo hilo nchini.

“Nataka kuwe na madawati yanayofanana nchi nzima yenye lebo ya For Government Primary School, ninaona mwanga mkubwa mbele yangu na katika hili ninaweza kufanikiwa nipeni fursa,” alisema.

Alisema pia kumekuwa na changamoto kubwa ya matumizi ya fedha zilizopelekwa kwa ajili ya kugharamia elimu na kuongeza lengo la serikali kutoa elimu bila malipo litabaki pale pale kwani miaka ya nyuma watoto wengi walishindwa kupata elimu kutokana na gharama kuwa kikwazo kwao.

Simbachawene alisema changamoto kubwa ni kwa walimu kudhani fedha zilizopelekwa shuleni ni za mwaka mzima lakini ukweli ni kuwa fedha ni za kila mwezi.

Alisema kila mwanafunzi wa shule ya msingi ya serikali atatoa shilingi 10,000 na kwa sekondari ni shilingi 25,000 kwa mwaka kwa ajili ya uendeshaji wa shule.

Waziri huyo alisema kwa shule za sekondari za kutwa kila mwanafunzi atapata shilingi 3,540 na kwa shule ya sekondari ya bweni ni shilingi 7,243.

“Ukiwa na wanafunzi 500 maana yake shule inapata zaidi ya shilingi milioni 3.6 kwa mwezi mmoja tu je ukipata fedha hizo unashindwa kuendesha shule?” alisema na kuongeza kuwa serikali pia ilipeleka fedha za chakula ili watoto waweze kula lakini fedha hizo zisitumike kulipa madeni ya samani ya wazabuni.

Aliwataka walimu wasivunje moyo juhudi zinazofanywa na serikali kwani mzazi masikini amepokea mzigo mzito sana na serikali.

“Tutakapokuja kwenye bajeti ya kwanza ya awamu ya tano tutakuwa tumejifunza changamoto. Tutaboresha na mambo mengine mazuri yatakuja,” alisema.

Ladies: Never Marry Men With These Three Issues!

$
0
0
Am a relationship person, and I believe a healthy relationship makes your life-span longer. I post just twice a week because I try to get suggestions so as to avoid controversy. Below are the type of Men I believe Ladies shouldn't consider for Marriage!

1. Men that Womanize: This is no longer news. Once it has entered into a man, only the fervent prayer of a righteous man will cure the addiction. A lot of male folks will argue that it comes as a result of being single but notwithstanding, I have seen married men who chase after young girls. A womanizer will never change. Forget all the promises he will tell you. Nothing kills a Man faster than a woman. History confirms it, The bible proves it (Prov 31:5) and we have seen Heroes who were reduced to nothing just because of womanizing.

2. Men that take Hard substances (Drinks, Drugs, etc): Just like my first point, the addiction to hard substances can hardly be broken by Marriage. If you date or marry a drug addict, you will only have yourself to blame. Technically, I believe that only a supernatural power can destroy such addiction. So my dear lady, if you don't want to visit Shiloh regularly after marriage, don't neglect the fact I just stated. No matter his riches, Handsome face, etc when he gets to a state of being "High" or "Depressed" and no solution around the corner, you will be in for a long thing.

3. A Man that Loves his Money more than You: This point might be a little bit controversial and I stand to be corrected. When the Love of money takes over a Man, nothing else comes to mind. Excess money might be there to spend but I doubt if a family will be united to spend the money. So my dear Lady, if you believe that when the money comes in BULK everything will come back to normal, you might end up spending the Cold Nights alone on your Bed...(i.e if you don't want to cheat).

There are still lots of them, but I consider these 3 the killers of marriages. Am open to corrections and commendations.

Baada ya Tarehe ya Uchaguzi Zanzibar Kutangazwa..CUF Watoa Msimamo Wao

$
0
0
Kufuatia tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo rasmi wa Chama.

Kamati ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alkhamis, tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama, mjini Dar es Salaam.

Chama kinatoa wito na kuwanasihi Wazanzibari wote waliochoshwa na utawala wa kibabe na wa kidikteta wa CCM na ambao walikikataa chama hicho kwa kishindo tarehe 25 Oktoba, 2015 kuendelea kutunza amani na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kusubiri maamuzi ya chama chao wanachokiamini.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO

Uchambuzi: Rais Magufuli Hakuwa Sahihi Kuvaa Nguo za Kijeshi, Vinginevyo.....

$
0
0
Kwanza nianze na cheo cha Amir jeshi mkuu.

Kiuhalisia cheo hiki hakina hakina mahusiano yoyote na vyeo vinavyopatikana katika ngazi za kijeshi! Hiki hata mtu ambaye hajui nini maana ya jeshi akishakuwa rais wa nchi tu hupewa! Hakina mahusiano yoyote na vile vyeo vinavyopatikana ndani ya jeshi ambavyo mwisho wake ni Jenerali!

Mfano ingetokea kama rais Kikwete (enzi akiwa rais) leo angevaa vazi la jeshi basi angevaa katika ngazi ya ukanali ila kwa rais (e. g
angekuwa Kikwete) cheo chake cha Amir jeshi mkuu kingebaki palepale na angetambulika kwa cheo chake cha Amir jeshi mkuu!

Ni amri ya jeshi kuwa mtu anapokuwa katika vazi la jeshi basi awe kirasmi! Kuendana na cheo chake. Ila hii haiondoi maana kuwa mtu akivua lile vazi basi cheo chake hakitambuliki! La hasha! Ila msisitizo ni pale unapokuwa ndani ya lile vazi basi uwe rasmi ndani ya mfumo wa jeshi la wananchi!

Mathalan Mwamunyange akiwa kiraia bado ni mkuu wa majeshi na anapewa sifa zote za ukuu wa majeshi! Ila akiwa ndani ya vazi la jeshi ni lazima awe ndani ya vazi rasmi linalotambua cheo chake ndani ya mfumo wa jeshi (Jenerali)

Kwanini rais Magufuli hakuwa sahihi?
Mbali na kuwa bado ni Amir jeshi mkuu, rais Magufuli hana cheo chochote ndani ya mfumo wa jeshi! Hajawahi kuwa ndani ya jeshi la wananchi kama mwana jeshi! Lile vazi ni la mwanajeshi wa kawaida ndani ya jeshi la wananchi! Kwa maana nyingine rais Magufuli pale alikuwa ndani ya mfumo wa jeshi! Labda tuambiwe kuwa alipoenda Monduli naye alitunukiwa cheti cha kufuzu mafunzo ya kijeshi ndani ya JWTZ!

Vinginevyo rais atakuwa amevaa lile vazi kama wanavyofanya kina Diamond ambapo ni kinyume na taratibu za jeshi na ndo maana wanapigwa marufuku!

Nadhani mmekuwa mkimwona Kikwete enzi akiwa rais alikuwa akitoa saluti kwa viongozi wenzake! Pale alikuwa akitumia mfumo rasmi wa jeshi kwa wakubwa zake kijeshi (Ingawa cheo chake cha Amir jeshi mkuu kilikuwa palepale) hivyo alikuwa hakosei kufanya hivyo!

Narudia tena: cheo cha Amir jeshi mkuu hakipo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi. Hata mtoto mdogo akiwa rais wa nchi basi cheo hicho kinafuatia palepale!

Pia inashauriwa kuwa si vyema sana rais wa nchi ambaye amechaguliwa kwa kura kuwa ndani ya mavazi rasmi ya kijeshi kutokana na cheo chake! Hii inazua mkanganyiko wa heshima za kijeshi zinazotolewa! Mathalan Kikwete leo angeamua kuvaa vazi rasmi la kijeshi huku akiwa rais basi angeishia cheo cha kanali! Hapo yupo ndani ya vazi rasmi la jeshi kisha anapokea saluti kutoka kwa jenerali! Hii siyo sawa! Rais wa nchi anabaki kuwa Amir jeshi mkuu hii haijalishi kuwa amepita na/au hajapita jeshini! Kinacholeta mkanganyiko ni lile vazi rasmi la jeshi!

Huwa wanasema "ukiwa nje ya lile vazi utaheshimiwa kwa cheo chako kijeshi, ukiwa ndani ya vazi utaheshimiwa kutokana na vazi" na ndo maana mtu akiwa ndani ya lile vazi basi anawekewa vyeo vyake kijeshi lakini akiwa nje ya vazi hawekewi vyeo vyake ila bado anatambulika maisha yake yote!

Kwa hiyo kuna mawili! Eidha rais Magufuli ameanza rasmi mafunzo ya kijeshi na ana cheo cha chini kabisa kijeshi na/au alivaa lile vazi kama watu wengine! Ikiwa hilo la pili ni kweli basi hakuwa sahihi kutokana na kuvaa vazi rasmi la JWTZ bila kuwa ndani ya mfumo wa jeshi!
Ikiwa hilo la kwanza ni sahihi basi yuko sawa na cheo chake cha Amir jeshi mkuu bado kipo palepale ila kwa hapo yupo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi!

By G Sam/Jamii Forums

Mzungu Mikononi Mwa Polisi Baada ya Kutaka Kuikimbia Familia yake na Kuitelekeza Hotelini Jijini Dar...

$
0
0
Raia wa Ujerumani akiwa mikononi mwa polisi kwa tuhuma za kutaka kuitoroka familia yake katika Hoteli moja jijini Dsm baada ya kutoelewana na mke wake mwenye asili ya Afrika. Raia huyo alikuwa nchini kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka. Alijaribu kumtoroka mkewe akimwachia deni la hoteli la sh. 315,000 pamoja na watoto.

Kama Mwanaume, hili unalichukuliaje?

Benard Membe “Kilichotokea Zanzibar Kimeihuzunisha Dunia”

$
0
0
Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” amesema Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?
Wanaoungana na Mh. Membe wacomment neno 'YES' na wanaompinga waseme 'NO'

Je Kwa Mtazamo Wako Ipi ni Couple Bora Kati ya Hizi Mbili......!

$
0
0
Huku Wema Sepetu na Idriss Sultan na Huku Diamond na Zari Hassan Unaipenda Couple ipi!
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images