Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Baada ya Kimya Kirefu Dr Mwaka Aibuka na Kusema Haya

0
0
DR Mwaka
MIEZI michache baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk. Hamis Kigwangalla, kufanya ziara katika kituo cha cha tiba mbadala cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala Dar es Salaam, mengi yamebainika.

Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa Dk. Kigwangwalla    aligundua  tabibu huyo wa tiba mbadala hakuwa na vyeti lakini taarifa zilizopo zinaonyesha Dk. Mwaka na wasaidizi wake walipewa vyeti kwa mujibu wa sheria na Baraza la Tiba Asilia.

Inaelezwa kuwa  Dk. Mwaka amekwisha kukabidhi vyeti hivyo kwa Serikali  ikiwa ni kutekeleza agizo alilopewa Desemba 16 mwaka jana na   Naibu Waziri Dk. Kigwangwalla.

Dk. Kigwangwalla amekwisha  kukiri kuwa  vyeti hivyo vimekwisha kufikishwa wizarani  na kuhakikiwa.

Kwa sababu hiyo,  Mwenyekiti  wa Shirikisho la Shirikisho la vyama vya Tiba Asili amesema     hatua hiyo ya Dk. Kigwangwalla haikuwa sahihi  bali ilisababisha  malumbano kwa jamii jambo ambalo si sahihi.

“Hivyo sisi shirikisho tuliweza kukaa na wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ambao kimsingi ndiyo hasa walikwazika na agizo hilo la wizara.

“Hatimaye Desemba 31 mwaka jana tulifanya kikao cha pamoja kati ya wadau hao, shirikisho na Wizara ya Afya tukiongozwa na uenyekiti wa Waziri Ummy Mwalimu na kukubaliana   baadhi ya mambo lakini si kupiga marufuku matangazo ya tiba mbadala,” alisema Lutenga.

Hata hivyo,   Dk. Mwaka alisema hataki kuingia katika malumbano na Serikali na  kwa sasa  anasukumwa na utoaji huduma kwa jamii kama sheria inavyotaka.

Alisema kutokana na hali hiyo kituo chake kimeandaa utaratibu maalumu wa utoaji matibabu kwa wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Alisema pamoja na misukosuko aliyoipata, Foreplan Clinic pia imejikita kusaidia jamii kama vile ujenzi wa nyumba za ibada ikiwamo misikiti na makanisa na hata kujihusisha masuala ya michezo.

Mabinti wa Kichaga Ndio Wanao Ongoza Kulilia Ndoa

0
0
Kwa utafiti wangu mdogo unaonesha kuwa katika makabila yote ya hapa Bongo tzee, mabinti wa kabila la Kichaga ndio hasa wanaongoza kwa kulilia ndoa. 

Yani ukikaa naye kwenye mahusiano ndani ya kipindi kisichozidi mwaka, lazima atakuwa ameshaanza kulilia ndoa.


Sasa ninaomba kufahamu kuwa huwa ni suala la kisaikolojia au ndivyo mila zao zinavyowafundisha kufanya hivyo?


Mabinti wengi wa kabila jingine huwa ni wavumilivu, hata kama watalilia, watalilia kindani ndani na wala huwezi jua mpaka kidume uamue kutangaza njaa ya kuweka ndani...


Toa maoni yako

Udaku Special Blog

Mapya Yaibuka Kujiuzulu Katibu Mkuu wa Yanga...Yadaiwa Ameshinikizwa na Yusuph Manji

0
0
Baada ya uvumi kuenea kwa zaidi ya siku mbili sasa juu ya hatma ya katibu mkuu wa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans Dk Jonas Benedict Tiboroha kuwa kajiondoa klabuni hapo na taarifa kuripotiwa kuwa huo ulikuwa ni uvumi, Jumamosi ya January 23 katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Benedict Tiboroha anaripotiwa kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

Tiboroha anaripotiwa kujiuzulu kwa shinikizo na wala sio uamuzi wake binafsi, hivyo mchana wa leo January 23, baadhi ya wanachama wa Yanga wamekusanyika klabuni hapo wakilalamika na kumtuhumu mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji kuwa amemshinikiza katibu ajiuzulu baada ya kupewa maneno na baadhi ya watu na kumshinikiza Tiboroha ajiuzulu

VIDEO:Ufafanuzi wa Kuhusu Rais Magufuli Kuvaa Mavazi ya Kijeshi

0
0
Jana tarehe 22 Januari, 2016 akiwa njiani Kutoka Arusha Mjini kwenda Monduli kufunga "Zoezi Onesha Uwezo Medani" lililofanywa na Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alisimamishwa na wananchi waliojipanga kandokando mwa barabara mara nane.

Rais Magufuli alivaa sare za kijeshi tayari kwa kwenda kufanya kazi za Jeshi la wananchi Tanzania ikiwa ni halali kufanya hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la wananchi ya mwaka 1966.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kanali Ngemela Lubinga ametoa ufafanuzi wa Rais Magufuli kuvaa sare hizo

Maskini Wema Sepetu Aandika Ujumbe wa Kuhuzunisha Kumjibu Shabiki Aliyemtukana Kuhusu Ugumba Wake

0
0
Maskini Wema Sepetu Aandika Ujumbe wa Kuhuzunisha Kumjibu Shabiki Aliyemtukana Kuhusu Ugumba Wake..

Wema Ameandika Haya Maneno kwa Uchungu......

Nilimfumania Mwanamke Wangu na Jamaa Mwingine Kitandani, Nikamsamehe..Baada ya Mwezi Ananiambia Ana Mimba yangu

0
0
Nilimfumania mwanamke wangu na jamaa mwingine chumbani kwetu kitandani kwetu. Nilimwacha kwa muda lakini alirudi na kuniomba msamaha tukarudiana. Ila sasa ananiambia ni mjamzito alivyoniambia tu ni mjamzito hasira zimenirudi. Sijui ni ujauzito wangu au sio. Na pia sina uhakika kama ameshaachana na yule jamaa niliyemfumania nae ama la.

Naombeni ushauri

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya Leo Januari 24, Ikiwemo ya Sumaye Kusema Zbar Kina Kirefu kwa Magufuli

0
0
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya Leo Januari 24, Ikiwemo ya Sumaye Kusema Zbar Kina Kirefu kwa Magufuli

Lowassa Apata Mapokezi Makabuwa Dakawa Wakati Akiwa Njiani Kuelekea Dodoma

0
0
Aliyekuwa mgombea Urais  katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana kwa tiketi  ya  UKAWA, Edward Lowassa jana alipata mapokezi makubwa kwa wakazi wa mnada wa Dakawa baada ya kusimama  na  kuwasalimia.

Lowassa alikuwa safarini  kuelekea Mkoani Dodoma kwa ajili ya mafunzo  ya  wabunge wa UKAWA.

Jaji Warioba Afunguka Kuhusu Mgogoro wa Zanzibar, Adai ni Tatizo la Kikatiba

0
0
WAZIRI mkuu wa zamani, Jajji Joseph Warioba amesema tatizo lililoko Zanzibar linapaswa kutatuliwa chini ya usimamizi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sio kuachiwa vyama vinavyovutana. Anaandika Jabir Idrissa.

Jaji Warioba amesema mvutano wa vyama vya CCM na CUF unaoendelea Zanzibar kuhusiana na kufutwa kwa uchaguzi wote mkuu uliofanyika Oktoba 25, ni suala linathibitisha kuwepo kwa tatizo la kikatiba nchini.

“Tunapaswa kuliangalia tatizo la Zanzibar kikatiba zaidi kuliko kuliachia vyama vinavyovutana. Tunaliacha hivi linakuwa gumu kutatuka, lakini likiachwa hivi wananchi wanaumia,” amesema.

Jaji Warioba ametoa msimamo huo leo katika maelezo yake ya majumuisho kwenye mdahalo wa wazi uliofanyika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Katika mdahalo huo, Chama Cha Mapinduzi kilitupiwa lawama kwa kutoridhia tamko la utoaji wa habari kwa usawa miongoni mwa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi huo.

Vilevile kwenye mdahalo huo, ofisa ambaye hakutambuliwa mara moja alisema kwamba matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa yalitokana na matokeo yaliyokusanywa vituoni.

Amesema kwamba mfumo wa kupokelea matokeo uliotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ulikuwa wa wazi, na ambao ulitolewa kwa vyama vyote vya siasa pamoja na wadau walioshiriki uchaguzi.

Hata hivyo, alishindwa kutoa ufafanuzi kuhusu malalamiko yaliyokuwepo kwamba mfumo huo ulidhibitiwa na Tume hata baada ya baadhi ya vyama kuiomba mara kadhaa kuueleza bayana. Alisema vyama viliruhusiwa kutoa malalamiko.

Kadhalika, ofisa huyo hakusema kama ingekuwa asemalo ni kweli ilikuaje kituo cha kupokelea matokeo ya uchaguzi cha vyama vilivyo chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA) kilivamiwa na Jeshi la Polisi na kuvunjwa, kompyuta kuchukuliwa na watendaji kukamatwa na kufunguliwa mashitaka mahakamani.

Kumuondoa Eliakim Maswi TRA ni Kuhofia Moto wa Bunge Lijalo, Wadai Wadau

0
0
Eliakim Maswi
Wakati Eliakim Maswi aliporejeshwa kuwa katibu tawala wa mkoa akitokea nafasi ya kaimu naibu kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Ikulu ilisema uamuzi huo ulitokana na kumaliza kazi maalumu, lakini wanasiasa wamedai kuwa, amehamishwa kupunguza hasira za Bunge.

Maswi alikuwa katibu mkuu wa Wizara ya Nishati, lakini aliondolewa wakati wa sakata la uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow kwa madai kuwa hakuwajibika ipasavyo kuokoa fedha za Serikali, lakini miezi michache baadaye Ikulu ilitoa taarifa kuwa mrasimu huyo ameonekana hakukiuka maadili katika sakata hilo baada ya kuchunguzwa na Baraza la Maadili ya Viongozi.

Kauli hiyo ilifuatiwa na uamuzi wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kumteua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na baadaye Rais John Magufuli kumteua kuwa kaimu naibu kamishna wa TRA, kabla ya kumrejesha kwenye nafasi yake mkoani Manyara mapema wiki hii, akisema amemaliza kazi aliyotumwa.

Lakini wabunge na wasomi waliohojiwa na Mwananchi wamesema Rais amechukua hatua hiyo baada ya kukosolewa na wanasiasa na wadau mbalimbali wanaodai kuwa Maswi hakustahili kupewa wadhifa huo baada ya sakata hilo la Escrow.

“Amefanya hivyo kuepuka mjadala utakaojitokeza kwenye Bunge la Kumi na Moja kuhusu escrow,” alisema mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye aliibua sakata hilo bungeni mwaka 2014.

“Kuna hatari mada ya ufisadi ikaibuka kwa njia nyingine kwenye Bunge kwa kuanza kuwazungumzia hawa wahusika ambao wamerudishwa kwa namna ya pekee na kupewa nafasi nyeti,” alisema Kafulila, ambaye amefungua kesi akitaka Mahakama itengue matokeo ya ubunge na kumtangaza kuwa mshindi.

Alisema kwa nafasi aliyokuwa nayo Maswi wakati wa sakata la Escrow, hana pa kukwepea, akidai kuwa anaweza kuhusika kwa uzembe au kwa kukusudia.

“(Rais) Amemuondoa kupunguza Serikali kupingwa na wabunge kutokana na kuwabeba waliohusika na kashfa mbalimbali ikiwamo Escrow. Lakini bado kuna watu amewaacha kama (Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter) Muhongo na (Waziri wa Katiba) Dk Harrison Mwakyembe, ”alisema Kafulila na kuongeza.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyowasilisha ripoti ya sakata hilo bungeni, alisema Rais hakuwa na taarifa sahihi wakati anamteua Maswi.

Alisema hali kama hiyo ilitokea pia kwenye uteuzi wa Profesa Makame Mbarawa ambaye kwanza alitangazwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji na ndani ya siku chache akahamishiwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

“Hii inaonyesha hakuwa makini wakati anafanya uteuzi,” alisema Zitto.

“Hatutegemei kuona uteuzi wa kubadilikabadilika. Awachunguze kwa makini anaowateua na nafasi anazowapa ili kukwepa kuonekana kuwa hakuwa makini kama inavyoonekana sasa.”

Profesa Damian Gabagambi wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua) aliungana na Kafulila kwamba Rais amechukua hatua hiyo baada ya kuona kasi anayoitaka, itaingia doa hasa baada ya watu kulalamikia uteuzi wa Muhongo na Maswi.

“Inawezekana wakati anamteua hakuwa akifahamu vitu vingi kumhusu (Maswi), lakini baada ya uteuzi maneno ya wadau, wasomi na watu mbalimbali yakamshtua na kufuatilia kwa umakini,” alisema.

Profesa Gabagambi alisema uteuzi wa viongozi siyo jambo dogo hasa unapotaka kuleta mabadiliko na mtazamo tofauti na uliokuwapo hapo awali.

“Unaweza kuwaona viongozi wachapakazi ambao ungeweza kuwateua, lakini kwa bahati mbaya wanatoka mkoa mmoja, hivyo ukiwateua italeta maneno. Hapo ndipo panapoleta tabu kidogo,” alisema Gabagambi.

Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco), alisema lengo la Rais Magufuli ni kujenga Serikali yenye heshima, anatamani asisikie kashfa ya aina yoyote ya ufisadi, lakini kuna baadhi ya watu inaonekana aliwateua kabla ya kufahamu kuwa wanahusika kwa namna moja aunyingine kwa kashfa hizo.

Alisema rais ana washauri ambao inawezekana walimpelekea taarifa kuhusu watu aliowateua, kazipima na kuona anaweza kuleta shida kuendelea kuwa nao hasa katika sehemu nyeti.

“Siyo kwamba Rais hasikii watu, wadau, historia ya anaofanya nao kazi inasema nini, anasikia na hilo limeonekana katika uamuzi alioufanya kwa Maswi. Ametafakari, amepima na kuona anatakiwa kufanya mabadiliko kama anataka kweli mambo yaende kama anavyotaka,” alisema Profesa Mpangala.

Lowassa, Maalim Seif Waishika Zanzibar..Ukawa Kutoa Tamko Zito

0
0
Lowassa na Maalim Seif
Zanzibar. Siku moja baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) kuitangaza Machi 20 kuwa siku ya marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, mgombea urais, Maalim Seif Sharif Hamad na Edward Lowassa leo wanakutana na wabunge wote kutoka vyama vinavyounda Ukawa kutoa “tamko zito” litakalotoa mwelekeo wa hali halisi ya kisiasa visiwani humo.

CUF, ambayo inapinga kurudiwa huko kwa uchaguzi, nayo imepanga kufanya vikao vyake vya juu mapema wiki ijayo kuweka msimamo wake kuhusu tangazo hilo.

Wakati hayo yakiendelea, mabomu ya machozi jana yalilipuliwa kwenye maeneo tofauti ya Zanzibar wakati askari wa Jeshi la Polisi wakitawanya watu waliokuwa wamekaa kwenye vikundi, kwa kuhofia kuwa wanaweza kutumia mwanya huo kufanya vurugu.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alitangaza juzi kuwa marudio ya uchaguzi hayatatanguliwa na kampeni za wagombea wa nafasi za urais, uwakilishi na udiwani na wala hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya wagombea.

Bado vyama vya upinzani havijatoa tamko kuhusu uamuzi huo wa ZEC, lakini viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa; Chadema, CUF, NLD na NCCR Mageuzi wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa African Dream.

Kupotea Kimuziki Kwa Saida Kalori Kulisababishwa na Mambo Haya-Mrisho Mpoto

0
0
Mrisho Mpoto amedai kuwa moja kati ya sababu zilizofanya kupotea kwenye muziki kwa msanii wa nyimbo za asili, Saida Kalori ni kukosa uongozi mzuri wa kusimamia kazi zake.

Akizungumza kupitia kipindi cha Sunrise cha Times FM Ijumaa hii, Mpoto alidai kuwa msanii huyo hakuwa na usimamizi mzuri japo alikuwa na uwezo mkubwa kwenye sanaa.

“Ilifika kipindi kila kitu akawa anafanya yeye mwenyewe, hakuwa na uongozi mzuri sana, lakini naamini akisimamiwa hata sasa atarudi vizuri tu” alisema Mjomba.

Katika ‘line’ nyingine, Mrisho amewataka Watanzania kuzikumbatia tamaduni zao na kuachana na umagharibi, kwani kufanya hivyo ni sawa na kupigwa ‘pingu’ za akili.

Wakati huo huo Mpoto ambaye ameachia wimbo mpya uitwao Sizonje hivi karibuni amewataka mashabiki wa muziki wake kumpigia kura kwenye tuzo za Kora.

Sumaye: Zanzibar Kina Kirefu kwa Rais John Magufuli

0
0
Wakuu habari za asubuhi,

Waziri mkuu Mstaafu mh. Fredrick Sumaye amesema mgogoro unaoendelea Zanzibar ni kina kirefu kwa Magufuli.

Je Kwa Mtazamo wako kuna Ukweli Hapo!

Chanzo: gazeti la mtanzania

Makavu Laivu Kutoka Kwa LEMUTUZ..Wacheni Kusema Maneno ya Uongo na Kuwazungumzia Usiowafahamu

0
0
Lemutuz na Hamisa Mobeto
LIVE STRAIGHT TALK:- Ninaomba kurudia tena this topic that People wacha kusema maneno ya Uongo in the Public wacha kuwazungumzia usiowafahamu kwa karibu cause you are hurting people usiowajua bila sababu just because wewe Hajielewi na Maisha yako basi unataka watu wengine wasijielewe like you au wawe miserable like you it is not fair kabisa..

Maisha is a good thing play your cards right utayafurahia Maisha but ukikosea your Cards you gadem dead na hakuna wa kumlaumu isipokuwa wewe mwenyewe but ukishindwa pigana tena na tena Rais wa Abraham Lincoln wa USA ndiye Rais Bora kuliko wote katika Historia ya Marais 44 wa Taifa hilo toka lijitangazie Uhuru wake from King George wa UK lakini Rais huyo aligombea Ubunge Mara 11 na kushindwa zote akaja kushinda Mara ya 12 na kuishia kuwa Rais the best ever in American history ndio Maisha yanavyotakiwa.....

Kama unapenda Maisha mazuri tafuta Pesa utayapata, kama unapenda Wadadazz wazuri pia tafuta utayapata tena mpaka uwakimbie like me huwa sometimes nawakimbia hahaha U know but hakuna kitu kibaya in life kama unataka vitu vizuri umeshindwa kuvipata badala ya kukubali matokeo na kuwa mpole na kuanza kupigana tena wewe unakata tamaa na kuanza kuchafua watu usiowajua...hapa Mjini kuna maneno rahisi sana mawili yanayorushwa na walioshindwa Maisha "YULE ANAUZA UNGA" au "YULE NI SHOGA ULIKUWA HUJUI?" watu watakuzushia haya maneno bila huruma wala kujali UKWELI wake na wajinga wenzao wengine watayapokea na kuyasambaza kila kona kama vile ni kweli 

Halafu Leo Jumapili hawa wajinga utawakuta Kanisani na Misikitini Ijumaa mazafantazz unaenda kufanya nini at Nyumba ya Mungu? ...guys Education inatusumbua sana hili Taifa watu rudini Shuleni Elimu haina mwisho na wala haina Umri please ondokana na giza nene libalokuziba Ubongo wako cause ukiwa na Elimu huwezi kuropoka ropoka hovyo hovyo..

I mean unajua LE MUTUZ anauza Unga haha please muogope Mungu wako na ujanja wangu wote siujui hata unafananaje yaani Mbebez akionyesha interest ya kunipenda akaisema huko maofisini nasikia Wanaume kwa hasira huwa mnajibu Muuza Unga yule Duh! haha SIJAWAHI KUUZA UNGA WALA HATA KUUONA UNAFANANAJE get EDUCATION! unasumbuliwa na LACK OF KNOWLEDGE!

MAKUBWA..Mwanamuziki wa Bongo Kuchoma Gari lake Moto Endapo Arsenal itafugwa na Chelsea leo

0
0
Leo kutakuwa na mchezo mkali wa ligi kuu ya England kati ya mabingwa watetezi Chelsea dhidi ya Barcelona.

Msanii Madee ni mmoja wa mashabiki wa Arsenal ambaye leo atakuwa mpinzani mkubwa wa Chelsea.

Katika kuonyesha mapenzi yake kwa klabu yake ya Arsenal, kwenye ukurasa wake wa @Instagram Madee ameahidi kuchoma gari yake moja moto endapo timu yake ya Arsenal itafungwa na Chelsea.

Hivi ndivyo alivyoandika..

"Tukifungwa leo na chelsea nachoma gari yangu moja moto"Madee

MAMILIONI ya Shilingi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) Yaliyohifadhiwa Benki Yanusurika Kukwapuliwa na Vigogo wa Serikali..Mhasibu Ashtukia

0
0
MAMILIONI ya shilingi ya Mamlaka ya Bandari (TPA), yaliyohifadhiwa katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), yamenusurika kukwapuliwa na baadhi ya vigogo serikalini.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na mkuu wa ulinzi na usalama, L.J. Twange, wizi huo ulipangwa kutekelezwa tarehe 24 Novemba mwaka jana.

Katika maelezo yake, Twange anasema, “…kugundulika kwa mpango wa kukwapua fedha hizo, kulijukana baada ya mtunza fedha wa Bandari ya Mtwara (Port Cashier), kufika katika tawi hilo na kuomba taarifa za fedha (balance) za mamlaka.

Anasema, “katika harakati za kuangalia salio, ndipo alipogundua kuwa kiasi cha Sh. 87,730,000 kimetolewa kutoka kwenye akaunti ya shirika.”

Mamilioni hayo ya shilingi yalipangwa kuchotwa kutoka kwenye akaunti Na. 034103000143, iliyopo benki ya NBC, tawi la Mtwara.

Maelekezo ya kuhamishwa kiasi hicho cha fedha yalipokelewa kwenye benki hiyo kwa barua ya 24 Novemba 2015, yenye Kumb. Na. AC/2/1/022/1153 iliyodaiwa imetumwa kutoka bandari makao makuu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, fedha hizo ziliekelezwa kupelekwa kwenye akaunti Na. 33012228976 inayomilikiwa na kampuni ya KILAM Limited.

Akaunti ya kampuni ya KILAM iliyotaka kuingiziwa fedha hizo, iko benki ya KCB, tawi la Mlimani City.

Nyaraka ambazo MwanaHALISI Online imezinasa zinaonyesha, “kulikuwa na uharakishaji wa malipo ya fedha kwa kampuni ya KILAM Ltd.”

Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa na Juma Mwenda, mfanyakazi wa kampuni ya KILAM, kwenda kwa Nelson Mwaikyokile, meneja wa operesheni wa tawi, malipo hayo yalitakiwa kuhamishwa kwa haraka na bila kukosa.”

“Baada ya kushindikana kuhamishwa kwa fedha hizo kutokana na ufinyu wa salio, wahusika wa mpango huo wa uhalifu, walituma barua pepe nyingine siki iliyofuata (25 Novemba), kuomba kuhamisha kiasi cha Sh. 187.7 milioni kutoka kwenye akaunti hiyohiyo.

“Hata hivyo, uhamishaji huo nao haukufanyika kutokana na uhaba wa fedha kutoka kwenye akaunti hiyo inayotumika kwa ajili ya makusanyo,” ameeleza Twange katika taarifa yake yenye kurasa tano kwa mkurugenzi mkuu wa bandari amethibitisha kuwapo kwa wizi huo.”

Nafasi za Kazi ya Ualimu New Ambassador International Schools

0
0

Job Vacancy 
 English&geogrphy teacher, kiswahili&history teacher,B/keeping&commerce teacher , chemistry&biology teacher and physics&mathematics teacher

Location ; Dar Es Salaam 
Position Type ; Full Time

Apply HERE

Medeye na Guninita Wamvaa Benard Membe Baada ya Kusema Hujisikia Kichefuchefu Akionana na Makada Walioihama CCM

0
0
Benard Membe
Siku moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kusema akionana na waliokuwa wanachama wa CCM na kuhamia upinzani anajisikia kichefuchefu, waliokuwa makada wa chama hicho wamemshukia kwa kauli yake hiyo.

Membe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akitoa maoni yake kuhusu makada waliohama na kusisitiza kuwa wasipokewe endapo watataka kurudi.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye ambaye alitimkia Chadema, alisema kama angesikia maneno hayo kwa mtu mwingine asingeshangaa, lakini siyo kwa Membe.

Mbunge huyo wa zamani wa Arumeru – Magharibi, alisema Membe anapata masilahi yake kwa kutambulika kama waziri mstaafu na wakati anaapa kuwa katika nafasi hiyo alitumia Katiba ambayo hivi sasa kwa kupinga yaliyomo ikiwamo uhuru wa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa, anakosea.

Medeye alisema kwa kauli hiyo, Membe hana haki ya kugombea nafasi yoyote ya siasa kwa sababu haamini katika vyama vingi wakati Taifa linaendeshwa kwa Katiba inayokubali suala hilo.

Alisema hata kauli ya Membe ya kutounga mkono uchaguzi kurudiwa Zanzibar akitaka kufanyiwa kazi kasoro chache ni ya kinafiki kwa sababu ameonyesha kutopenda upinzani.

“Hana msimamo hazungumzi vitu kutoka moyoni, kama kweli anakubali vyama vingi na ana uchungu na kinachoendelea Zanzibar, kwa kuwa bado ni mjumbe wa Nec (Halmashauri Kuu ya CCM), angemuomba mwenyekiti wake aitishe mkutano mkuu lijadiliwe hilo na atoe anachokiamini, hakufanya hivyo kwa sababu hakubali vyama vingi, hataki mabadiliko katika siasa anayoitumikia, ” alisema Medeye.

Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alisema hawezi kujibizana na watu kwani anajua anachofanya.

Alisema anayo mawazo huru na akitaka kuzungumza jambo lolote atafanya hivyo kwa utashi wake na siyo kujibizana na watu waliozungumza kwa utashi wao.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita alisema anamheshimu Membe kwa sababu amefanya naye kazi katika chama hicho tawala na kumshauri siku nyingine anapozungumza mambo kama hayo asiegemee upande mmoja.

Alisema licha ya kuwa hayo ni mawazo yake na kila mtu ana uhuru wa kuwaza na kusema anachotaka, alipaswa apime anazungumza nini na kwa manufaa ya nani.

Guninita alisema Katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama hata mara 10 alimradi huko anakokwenda atapata vitu muhimu ikiwamo malengo yake binafsi, ya chama husika na mafanikio ya Taifa.

Alisema haikuandikwa ni lazima abaki sehemu anayoamini hana malengo nayo, au asihame kutoka chama kimoja ama kingine

Tafadhali AY Tunaomba Uwakutanishe Ali Kiba na Diamond ili Kuokoa Ugomvi wa Mashabiki

0
0
AY na Diampond
Nguli wa muziki AY tunajua umeachia wimbo remix na superstar wa sasa Diamond platnumz, tunaomba utumie nafasi hiyo kuwakutanisha hao wadogo zako Diamond na mtaalam wa melody Alikiba ili ikiwezekana watoe wimbo wa pamoja , hii itasaidia kufuta chuki na matusi baina ya mashabiki wa pande hizi mbili ambao huko instagram wanatukanana matusi ya nguoni kila kuchwapo.

Matusi ya mashabiki hawa sasa yamehamia kwa wanawake wa wa wanamziki hawa kwasasa Mrs Zali Dangote na shabiki wa kugalagala wa Alikiba Mrs Wema Idrissa . Huu ugomvi hautaishia insta utahamia hata mitaani.

Suluhisho la kufuta ugomvi na hao masupastaa wawili kutoa ngoma ya pamoja hapo watawakata kilimi mashabiki maandazi wanaoijiunga vifurushi vya chuo ili kutukata tu huko insta.

Kigogo Mwingine Akumbwa na Kasi ya Rais Magufuli, Kisa Rushwa

0
0
Rais John Pombe Magufuli 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Katavi inamshikilia Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kawajense, Manispaa ya Mpanda Catherine Kipeta kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh 30,000.

Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Katavi, Christopher Nakua alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Januari 18, mwaka huu katika eneo la Mtaa wa Kawajense baada ya kuandaliwa mtego ambao ulifanikisha kukamatwa kwake.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufuatia Ofisi ya Takukuru kupokea taarifa kutoka kwa mlalamikaji kuwa Ofisa Mtendaji huyo anamuomba rushwa kiasi cha Sh 30,000 ili asimpeleke kwenye Baraza la Kata kwa kosa la kufungua sehemu yake ya biashara wakati ni muda wa kufanya usafi na kutokushiriki kufanya usafi.

Ilidaiwa kuwa baada ya kupokea taarifa hizo ofisi ya Takukuru ilifanya uchunguzi na baada ya kuridhika na maneno ya mlalamikaji ndipo mtego ulipoandaliwa na mtuhumiwa kukamatwa.

Kamanda Nakua alisema mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili ambazo ni kuomba rushwa ya fedha taslimu Sh 30,000, shtaka la pili litakuwa ni kupokea rushwa ya Sh 30,000 kinyume cha kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007.
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images