Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUHUSU KUACHISHWA KAZI KWA KOCHA WA TAIFA STARS

0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).
Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.

WEMA SEPETU AKIRI KUNENEPA SABABU YUPO KIMAPENZI NA MTU AMPENDAYE KULIKO WOTE

0
0
Jana katika Kipindi cha leo Tena Mwanadada Wema Sepetu Aliulizwa kwanini Siku hizi ananenepa sana kiumbo na Mwanadada huyo mrembo alijibu moja kwa moja kuwa ananenepa kwa sababu ana amani ya moyo kwa vile yupo na mtu kimapenzi ampendaye kuliko wote duniani...Nadhani wote mnamjua ni nani?  Mapenzi raha Bwana asikwambie mtu ukimpata akupendaye na wewe anakupenda lazima unenepe

KAMA ULIKUWA HUJUI BASI HEMEDY PHD NA NAJMA SASA NG'ARE NG'ARE

0
0

Nimekutana na hizi picha za Hemedy akimbusu msanii wa muziki na filamu Najma na maneno yalioambatana na picha hizo yakizungumzia ndoa na harusi....Huenda sasa hawa ni mambo safi ...Najma alikuwa ni mpenzi wa Mr Blue zamani ......

MATUSI, VIJEMBE VYATAWALA BUNGE LA KATIBA

0
0
Bunge Maalumu la Katiba limeendelea kutawaliwa na vijembe na mipasho, huku baadhi ya wajumbe wakitambiana kujua misemo, mbinu na nahau na kuacha kujadili mambo ya msingi.

Mjadala wa upigaji wa kura wakati wa kupitisha vifungu vya Rasimu ya Katiba, ndio ulioibua vijembe hivyo, huku wabunge wakigawanyika katika makundi mawili wanaotaka kura za wazi na wengine kura za siri.

Kila mjumbe aliyesimama alijitahidi kupambana na kuhakikisha anashinda,  jambo lililosababisha baadhi ya wajumbe kuchangia kwa hisia kali na maneno makali.

Said Alli Mubarak ndiye aliyeanza kuibua hoja ya upigaji kura za siri pamoja na kutaka wajumbe kufuata makundi ya walikotoka jambo lililosababisha wabunge kadhaa kulikataa suala hilo.

“Nataka tuanze kwa makubaliano hapa, maana vinginevyo hatutendeani haki. Sisi wengine kutoka Zanzibar tunajua namna ambavyo tumeonewa kwa kiasi kikubwa katika kipindi chote cha Muungano, hivyo lazima tukae na kujadiliana kwa pamoja,” alisema Mubarak.

Juma Duni Haji alizungumza kwa hisia kali akiwataka wajumbe kutoshabikia suala la kupiga kura kwa wazi na badala yake zipigwe kura za siri.

Mjumbe huyo alitolea mfano wa nchi za Uingereza na mataifa mengine,  akisema kuwa zilipiga kura kwa siri katika kufanikisha masuala yao.

Akijibu hoja hizo, Naibu Spika wa Bunge wa Jamhuri Job Ndugai, aliwataka wajumbe kuwa na staha katika mazungumzo, kwani ikitokea hivyo ukumbi hautatosha.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, hapatatosha hapa, maana mkianza kuzungumza habari za maonezi ya Muungano, ukumbi huu hautatosha, ni wazi kwamba tutagawana mbao humu ndani, msione sisi wengine tumenyamaza,” alisema Ndugai.

Katika majibu yake Profesa Maghembe alijikita zaidi kumjibu Duni kuhusu nchi ya Uingereza kutengeneza Katiba ya siri na kusema kuwa uelewa wa mjumbe huyo haukuwa mkubwa.

Profesa Maghembe alisema hakuna mahali ambapo Uingereza ilitengeneza Katiba ya siri kwa kuwa nchi hiyo haijawahi kuandika Katiba yake.

“Mtu mmoja hapa asubuhi kasema Katiba ya Uingereza ilipoandikwa watu walipiga kura ya siri, lakini mimi nafahamu hakuna Katiba ya Uingereza ambayo imeandikwa, watu hapa wana mazoea wakidhani kwamba wengine hawajui, wakati duniani kote hakuna kitu cha namna hiyo anadhani watu wote humu hawasomi au hawajui, Uingereza hakuna mtu aliyepiga kura ya siri utapigaje kura wakati hakuna katiba iliyoandikwa,”alisisitiza Maghembe.

Livingston Lusinde alisema ndani ya Bunge kuna watu waoga na wanafiki ambao waliisaliti na kuifuta nchi ya Tanganyika, lakini wameibuka upya kuidai.

Wabunge kuamua

Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu la Katiba imeliacha jukumu la aina ya matumizi ya kura za siri yatumike au kura za wazi yafikiwe na Bunge hilo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Costa Mahalu alisema suala la aina gani ya kura itumike imewasumbua wakati wa kuijadili hivyo kufikia uamuzi huo.

Alisema iwe kura ya wazi au ya siri yote ni mchakato wa kidemokrasia na kati ya kura hizo hakuna inayomzuia mtu kupiga kura.

“Wajumbe walizungumzia namna zote za upigaji kura, kamati inakubali kuwa namna zote ni nzuri na kutokana hali hiyo Kamati imependekeza Bunge hili ndilo liamue ni aina gani ya kura itatumika,” alisema Profesa Mahalu.

Profesa Mahalu akizungumzia siwa alisema: “kutokana na gharama za siwa kuwa kubwa (Sh1 bilioni) tumependekeza iachwe kabisa kwa sababu za gharama, tutaulizwa na wananchi tumetumia gharama nyingi hivyo kifungu husika kitarekebishwa.”


Imeandikwa na Habel Chidawali, Fidelis Butahe na Ibrahim Yamola

KIPUTE CHA LEO KOCHA WA YANGA ASEMA"KILA NAFASI BAO"

0
0
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanatumia kila nafasi wanayopata kufunga bao dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Yanga na Al Ahly zitakutana kesho katika pambano la raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kuibwaga Komorozine kwa kuicharaza  jumla ya mabao 12-2, ikiwa ni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 nyumbani na ushindi wa mabao 5-2 ugenini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema anaamini njia pekee itakayomwezesha kuizamisha Al Ahly ni wachezaji wake kupachika bao katika kila nafasi watakayopata.

“Tulishinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwa sababu tulikuwa makini kutumia nafasi. Jambo zuri ni kwamba uwezo wa kutengeneza nafasi tunao  hivyo ni wajibu wetu kuzitumia,” alisema Plyuijm.

“Nataka  tunatengeneza nafasi nyingi basi na mabao yawe mengi. Tukiwa makini katika hilo sina shaka kwamba tutawafunga.”

Katika hatua nyingine, Pluijm alisifu mazingira ya kambi yake kwa kusema hayana tofauti na yale waliyoweka nchini Uturuki mapema Januari.

“Hoteli ni nzuri pia uwanja tunaoutumia kufanyia mazoezi ni bora kabisa kiasi ambacho kimemfanya kila mmoja wetu kuifurahia,” alisema Pluijm.

Hata hivyo, Pluijm alishindwa kuthibitisha kama atamtumia beki Mbuyu Twite ambaye aliumia wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting.

“Twite jana (juzi) aliniambia anajisikia maumivu, lakini leo amefanya mazoezi hivyo nasubiri kama atakuwa fiti hadi kufikia Jumamosi lakini kwa sasa siwezi kusema moja kwa moja kama nitamtumia au la,” alisema Mdachi huyo.

WEMA SEPETU"NAPENDA WANAUME WEUSI NA NI KWELI NIPO NA DIAMOND"

0
0
Mwanadada Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali.

Kupitia kipindi cha Leo tena February 28 Wema Sepetu amekubali kutaja sifa za mwanaume anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali lililoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho ni kuhusu mwanaume wa sifa gani anayedhani anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu “Kuolewa sio shida je huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini nisimpende”


“Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao”.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond amekiri kwa kusema’Kweli niko na Nasib - Diamond na nadhani muda huu kutakua na utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikua utoto na imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa sasa tumeamua kuwa serious’.

Habari kwa Hisani ya Millard Ayo

Wema Sepetu pia kaandamana na Ant Ezekiel kwenye interview ya kipindi hicho kinachorushwa na Clouds Fm.

WABUNGE WAWALIPUA BONGO MOVIES WASEMA NI OMBA OMBA BALAA

0
0
SKENDO nzito ya Bongo Muvi imeibuliwa na baadhi ya wabunge waliopo mjini Dodoma kufuatia kuwalipua wasanii wake kuwa, ni ombaomba balaa, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.

Kwa mujibu wa wabunge hao ambao walitaka majina yao yasitiriwe kwa sasa, baadhi ya wasanii hao ambao wengi ni mastaa wamekuwa wakiwazukia na kuwapiga mizinga jambo linalowashangaza hasa wakizingatia kuwa, wapiga mizinga hao wana majina makubwa na huonekana wakitembelea magari ya kifahari.

“Hivi nyie mapaparazi, mnashindwa kabisa kukomesha hii tabia ya mastaa wa Bongo Muvi? Hawa jamaa ni ombaomba sana.

“Wamekuwa wakitupiga mizinga sana. Tunawashangaa maana wengine wana majina makubwa, wanatembelea magari ya kifahari lakini bado wanaomba pesa ndogo,” alisema mbunge mmoja ambaye anatoka kwenye moja ya majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam.

KINACHOWASHANGAZA WABUNGE
Kwa mujibu wa wabunge hao, linalowashangaza zaidi ni kwamba wasanii hao ambao  ni wake kwa waume, wamekuwa wakipiga mizinga ya pesa ndogo badala ya kuomba pesa za kufanyia mambo makubwa yenye mikakati mizito.

“Mtu anakuja, anasema anasumbuliwa na kodi ya nyumba au anasema hajala. Hivi kweli mastaa wakubwa kama akina…(anataja jina) ni wa kuomba vijisenti kama vya kodi ya nyumba jamani?” alihoji mbunge mwingine kati ya watano waliokuwa wakizungumza na gazeti hili.

Waheshimiwa hao waliendelea kuwaanika mastaa hao kwa kudai kwamba, walichogundua ni kuwa inapotokea wakapewa hitaji lao la fedha, huishia kukaa baa hadi usiku wa manane na asubuhi wakiamka wako vilevile kama hawakupewa.

MWAKIFWAMBA ABANWA NA RISASI
Ili kuweka sawa madai hayo mazito na yenye aibu kubwa kwa tasnia hiyo maarufu nchini, Risasi Jumamosi lilimtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba ambaye alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya wasanii wake kuwa ombaomba!

HUYU HAPA MWAKIFWAMBA
“Ni kweli kabisa. Mimi mwenyewe nimewahi kusikia malalamiko hayo, lakini unajua tena ni mambo binafsi, mtu anapiga mizinga kwa mambo binafsi si rahisi kumwingilia,” alisema rais huyo.
Aliendelea kusema kuwa, katika vikao mbalimbali vya kisanii, amewahi kuweka wazi msimamo wa taasisi kwamba kila msanii aishi maisha yenye heshima huku akiwa mbali na mazingira yenye kusababisha aibu katika jamii.

KUMBE HATA JK ALIWAHI KUMLALAMIKIA
Katika kuonesha hasira zake juu ya tuhuma hizo zenye dharau katika gemu la filamu, Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, katika moja ya mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kumlalamikia kwamba, wapo mastaa ambao kazi yao ni kupiga mizinga isiyo na tija.

“Rais mwenyewe aliwahi kuniambia kuna wasanii wakiwasiliana na yeye wanamwambia mambo ya pesa za kula.

“Kuna msanii aliwahi kumtumia meseji JK akimwambia, ‘mjukuu wako leo hali mbaya’,” alisema Mwakifwamba.
Akaendelea: “Sasa we’ unakutana na rais badala ya kumweleza mikakati mikubwa na nini cha kusaidiwa kuifanya tasnia iweze kuendelea, unapiga mizinga hujala, ni aibu sana.”

WALISHAMPIGA ‘MIZINGA’ HADI ‘MTOTO WA MKULIMA’
Mwakifwamba hakukubali kufumba midomo yake bila kupasua yote ambapo alizidi kudai kuwa, hawashangai sana wasanii wake hao kwani waliwahi kumpiga mizinga hadi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ‘Mtoto wa Mkulima’. 
“Niliwahi kukutana na Waziri Mkuu Pinda, nikamwomba mambo ya kuisaidia tasnia ya filamu Tanzania, akasema afadhali mimi nimeongea vitu vya maana, kuna wenzangu alikutana nao ‘wakambomu’ fedha za matumizi binafsi, nilishangaa sana,” alisema Mwakifwamba. 

RISASI LAWASAKA MASTAA, WAPATIKANA HAWA:
Jacqueline Wolper, ni staa wa filamu za Kibongo. Filamu yake ya kwanza ni Ama Zao Ama Zangu. Yeye alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema:
“Ni kweli, sikatai kwamba hiyo tabia ipo tena sana tu. Lakini wanaoongoza ni mastaa wa kiume, hao ndiyo wanaotutia aibu ya kuonekana sisi ni o
mbaomba.”

STEVE NYERERE
Yeye ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity. Alisema anavyojua kuna kuonana kirafiki na waheshimiwa na kuonana kiajenda.
“Tabia ya kuomba fedha kwa waheshimiwa ipo. Lakini linapokuja suala la tasnia yetu kupeleka hoja kwao, tunaanza hoja baada ya hapo kuna waheshimiwa wengi wana urafiki na wasanii, tunaitana pembeni na kupiga kirungu.
“Siwezi kukaa na waheshimiwa kama Rostam Aziz, William Ngeleja, Mheshimiwa Abood na Nimrod Mkono halafu nikawaacha hivihivi, kisa eti mimi ni Mwenyekiti wa Bongo Muvi,” alisema Steve akionesha kumshangaa mwandishi aliyempigia simu kutaka usawa wa mizani ya habari hiyo. 
ODAMA YEYE
Jennifer Kyaka ‘Odama’ yeye alipata umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Odama iliyokuwa ikirushwa na Televisheni ya Taifa (wakati huo TVT). Alipopigiwa simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa licha ya kurudiwa mara kadhaa.
AUNT EZEKIEL
Risasi pia lilimtafuta  nyota mwingine aliye mahiri kwenye sinema za Bongo, Aunt Ezekiel ambaye filamu iliyompaisha sana inaitwa Miss Tanzania. Yeye simu yake ya mkononi ilionesha kutokuwa hata na laini kwa wakati huo.

RAY AFUNGUKA
Staa mkongwe katika gemu tangu enzi za Kaole Sanaa Group, Vincent Kigosi ‘Ray’ aliposakwa na kuulizwa kuhusu madai hayo ya wasanii kuwa ombaomba alisema:
“Wasanii wengi wanawaza maisha ya hapa na si baadaye. Badala ya mtu kuweka shida zake kwenye mfuko wa karatasi, anaweka kwenye rambo ambao unapiga kelele.
“Mwisho wa siku anaomba shilingi milioni tatu akagombolee gari au asaidiwe kodi ya nyumba, anasahau kuwa kapata nafasi ya kuonana na mheshimiwa azungumzie tasnia tunavyonyonywa hadi kuuza hati miliki,” alisem Ray.
Credits:Global Publishers



NIMEKARIBIA KUFUNGA NDOA NA NILIMDANGANYA MCHUMBA WANGU KUWA MIMI NI BIKIRA, JE NIFANYEJE?

0
0
Mwenzenu karibia yananikuta makubwa sijui itakuwaje natamani siku zigande....mimi ni msichana wa miaka 23 nilikutana na Mkaka mmoja mwaka umepita sasa tukawa wachumba akanitambulisha kwao na mie nikamtambulisha kwetu na kuanza uchumba rasmi lakini katika kipindi hicho chote wakati tunaanza nilimdanganya mimi bikira kaka wawatu akafurahi sana na kuahidi kutonigusa mpaka siku ya harusi yetu na kweli kaka wa watu hakunigusa mpaka leo zimebaki week mbili tufunge Harusi..na amewaambia wazazi wake waandae zawadi watakayo nipa baada ya kunitoa bikira siku ya Harusi tutakapofanya kwa mara ya kwanza , Eti atawapelekea shuka lenye damu alafu nipewe zawadi ya kujitunza, ki ukweli mimi sina bikira kabisaaa, ilitoka toka na miaka 15 , Naombeni ushauri hili litanitokea puani na kunipa aibu

HUYU NDIYE MSICHANA ALIYEONGOZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013..AFUNGUKA MENGI

0
0
Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano ‘exclusively’ na Robina Nicholaus, msichana aliyeshika nafasi ya kwanza/ aliyeongoza kitaifa (Tanzania One) kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.

Robina, mwenyeji wa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara ambaye alikuwa anasoma katika shule ya wasichana ya Marian, akiwa na ndoto ya kuwa daktari wa watoto amejibu maswali kumi muhimu na majibu yake yanaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi walioko shuleni ambao wanakumbwa na changamoto kadhaa, na wazazi wanaowapeleka watoto wao shule.
Ulifanya nini ghafla ulipopata taarifa kuwa umekuwa wa kwanza Tanzania nzima, na je, ulitegemea?
 Nilipopata matokeo kwamba nimekuwa wa kwanza, kwanza nilifurahi sana na kilichobaki zaidi ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiye kayawezesha yote. Nilihisi kama kupaa vile…nilifurahi sana halafu my mom alikuwa pale… alikuwa analia akaniinfluence na mimi machozi yatoke, I was very happy yaani. Sikutegemea kuwa wa kwanza lakini nilikua na uhakika wa kufanya vizuri kwa sababu niliplan kufanya vizuri.
Kama msichana ulifanya nini kuzivuka changamoto za kimasomo na kufanikisha kwa kiasi kikubwa? 
Safari ya taaluma ni ndefu ndio, kwenye safari ya masomo kuna changamoto za hapa na pale, ambapo mara nyingi wasichana waga tunafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Lakini kwangu mimi nimeweka interest yangu sana kwa wazazi. Kwa hiyo nilikuwa open kwa wazazi na kuwaomba ushauri wa hapa na pale nifanye nini. Na katika vyote nilivyokuwa nafanya ni kufanya kile kitu ambacho hakiwezi kusubiria kwanza ambacho ni masomo. Kwa hiyo naweka juhudi pale ili ukishafanya kila mtu ajue kwamba umefanya.


Ilikuwa mbaya sana kwenye kusoma hasa form three ambapo nilianza kushuka and all that. Kwa hiyo wazazi pamoja na walimu pia walikaa na kuweza kunisaidia na mimi mwenyewe nilikuwa tayari kusikia ushauri wao na kuweza kusoma kwa bidii zaidi ili niweze kupata ile nafasi yangu niliyokuwa naipata toka nianze.

Nini kilichofanya ushuke kimasomo wakati huo?

 Kilichofanya nishuke ni ile kupoteza malengo na juhudi zangu, na pia kuona kwamba vitu vinaanza kuwa vigumu halafu kuweka hiyo kwenye akili kwamba hicho ni kigumu siwezi kukifanya. Lakini nilipoamua kuweka juhudi na kuona kwamba ni vitu vya kawaida kwamba navyozidi kukua na vitu vinazidi kuwa vigumu na natakiwa nitafute njia ya kuvi-overcome, ndo hivyo nikaweza kufanikiwa.

Ratiba yako ya siku ulipokuwa shule kwa ujumla wake ilikuwa vipi na muda gani ulikuwa unajisomea?

Asubuhi nilikuwa naamka mapema kabla ya time table ya shule haijaanza kwa sababu tunatakiwa tuamke mapema kwenda misa kwenye saa kumi na moja hivi. Kwa hiyo naamkaga kwenye saa tisa najiandaa naenda darasani kwa sababu siwezi kusoma usiku kwa sababu usiku nakuwa nimechoka, kwa hiyo my extra time inakuwa asubuhi ambako I’m still fresh. 
Nasoma then ikifika muda wa misa naenda kusali. Nikitoka kusali kuna kazi ndogo ndogo za kufanya kujiandaa na time table ya school and all that. And my free time ile mchana nikitoka darasani kuanzia saa nane, nakuwa nimepanga nini natakiwa nifanye, ni somo gani natakiwa kulisoma at that time ambapo ni saa nane mpaka saa kumi na nusu. Ambapo ni muda wa concentration, kama kuna kitu ambacho sijaelewa naenda kuwafuata waalimu kwa sababu wanakuwa wapo at that time. And kuna some free time kama ile break time, ni kuanzia saa nne na dakika 40 mpaka saa tano na robo, pale hauwezi kusema unatake breakfast all the time, unatake breakfast for a short time halafu nyingine inabaki unaweza kufanya maswali matano ya physics. Yaani every little time ambayo unaweza kuipata, you don’t let it go to waste tu, una-utilize.
Marafiki ulionao wanaweza kusaidia kukupandisha au kukushusha. Wewe ulikuwa na marafiki wa aina gani? 
Marafiki wangu nimewachagua kwa category..yeah (anacheka), ikifika muda wa kusoma nakuwa na mtu ambaye najua atanisaidia, kwa hiyo nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Sarafina amekuwa wa nne. Alikuwa ananiinfluence sana kusoma, huyo ni wakati wa kusoma, kwenye academics namfata yeye.

Ikifika wakati wa social siwezi kumfata sarafina kwa sababu she is not that social, yeye yuko kama mimi we are not that social, kwa hiyo ninaye social friend. Pia ikifika muda wa kuspend, I have an economical friend. Ambaye I’m sure nikikaa nae nikiwa naspend siwezi kwenda beyond my budget. Kwamba siwezi kufulia. Kwamba we are all in the same status, same friends, yeah.
Ni kitu gani kilikuwa kinakuboa sana shuleni na kukunyima furaha muda mwingine?
Kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana, ikifika wakati ambapo kwa mfano watu wachache kwenye darasa wamefanya kosa halafu sasa mnakuwa included as a whole class halafu mnapata adhabu. Hiyo adhabu directly itaharibu time table yangu ya kusoma. Kwa hiyo badala ya kusoma nafikiria ningekuwa nasoma physics, I’m either slashing an area..yaani hiyo ilikuwa inaniboa sana yaani.
Ulishawahi kuitwa ‘Msongo’ au majina kama hayo? Ulikuwa unaichukuliaje na je, ilikutenga na marafiki zako? 
Yeah, msongo…kauzu. Yeah mimi naipenda hivyo kwa sababu nafanya nachotakiwa kufanya ambacho ni kusoma. Hiyo haikunitenganisha na marafiki zangu. 

Vuta taswira, je, ingetokea ukapata division Zero na kuwa wa mwisho Tanzania nzima ungefanyaje? Na unawashauri nini waliofeli kwa kiasi hicho?
Kama ningepata zero, kwanza ningefikiria…na ningekuwa very disappointed kweli, lakini pia ningefikiria kuhusu kujipa second chance, ningeenda kusoma tena. 
Kwa waliofeli ningependa kuwashauri wasikate tamaa hata kidogo and wajipe second chance. Kwa wengine pia ambao wana vipaji vyao wanaweza kuviendeleza. But pia kwa kuwa elimu ni muhimu..ku-reseat pia ingekuwa ana option.
Robina Nicholaus ni msichana wa aina gani?

Robina ni mtu mkimya lakini mcheshi pia. Nisingependa nikae na mtu halafu nikawa kimya just because ni mkimya... I will try kuchekesha, and of course I’m funny anyway.
-via timesfm

UKATILI:MTOTO ABURUZWA NYUMA YA PIKIPIKI NA BABA YAKE KISA HAJAENDA SHULE

0
0
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.

 mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.

  Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard amesema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.

Amesema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.

Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa upelelezi zaidi.

NGUVU YA MITANDAO YA KIJAMII-CASE STUDY ISSUE YA PNC NA OSTAZ JUMA

0
0
Imeandikwa na Josefly Muhozi

Moja kati ya matukio makubwa yaliyoteka ‘attention’ ya watu wengi ni picha na video zilizowekwa kwenye ukurasa wa Facebook na boss wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma zikimuonesha mwimbaji toka Mwanza PNC akiwa amepiga magoti na kuonesha ishara ya mikono kama anaomba mbele ya boss huyo aliyetulia kwenye kochi akiwa amekunja 4.

Picha na video hizo ziliwekwa na Ostaz Juma mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika, ““hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati.”

Haikuchukua muda, watu mbalimbali ambao ni wadau wa muziki wa kizazi kipya walipaza sauti wakilaani kitendo hicho kupitia mitandao ya kijamii wakiwemo wasanii mbalimbali ambao hawakusita kumchana Ostaz kwa kile kilichoonekana kuwa ni kumdhalilisha mwimbaji huyo.

Lakini wapo mashabiki ambao waliporomosha matusi kufuatia tukio hilo na habari hiyo kusambaa kwa nguvu kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyompelekea Ostaz kudai kuwa siye aliyeziweka picha hizo. Lakini kilichowashitua wengi baadae, ni pale ilipoonekana post nyingine kwenye ukurasa wake akiwaponda watangazaji wa Tanzania na wasanii kuwa wanasumbuliwa na njaa.

“Naona watu mmeguswa sana na mimi kuanika picha ya PNC katika mitandao et, tatizo wasanii wa Tanzania mnanjaa sana kuanzia watangazaji Radio na wasanii njaa ndizo zinazo wasumbua...”

Lakini baadae aliongea na Moko Biashara aka One B wa Times Fm kueleza kuwa ukurasa wake metekwa na wezi wa akaunti za watu mtandaoni (hackers) na kwamba hiyo sio post yake.

“Daah, nshachanganyikiwa rafiki yangu watu wamehack akaunti yangu wanaandika matusi wanatukana watu..hadi hapa mimi nimeshachanganyikiwa hadi hata kuongea siwezi bro.” Alisema Ostaz.

Nadhubutu kusema kwa msisitizo kuwa picha hizo ziliwekwa na Ostaz Juma kwa jinsi nilivyozifanyia utafiti na kuzingatia kauli yake aloyoniambia kwa mara ya kwanza, “Ndio PNC kunipigia magoti na kuniomba radhi, lakini sasa mimi nikaamua kuwaonesha watanzania kwamba PNC amerudi kweli kuniomba msamaha. Je, kama kweli PNC alikuwa analalamika ‘Ostaz anafanya kazi zake hanijali hanisaidii…”

Hata hivyo sina uhakika…huenda kweli hakuandika kauli ya kuwaponda watangazaji na wasanii…nasema huenda kwa kuwa muda mchache baada ya kudai kuwa akaunti yake ilikuwa imetekwa na hackers na kubadili ‘password’, aliingia tena na kuifuta post hiyo na kuandika nyingine ya kuomba radhi na kueleza kuwa ilikuwa imetekwa kwa kipindi kile. Kwa upande wangu ‘no comment’ kwenye hilo.

Anyways, kwa maelezo yote hapo juu bila shaka umepata picha nzima ya tukio hilo japo kwa ufupi.

Sasa niende moja kwa moja kwenye mada na lengo langu, mkasa huu unapaswa kuwa zaidi ya somo la kawada kwa Ostaz Juma na wengine hasa watu maarufu ambao huichukulia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram n.k kama sehemu fulani tu ya kuandika unachotaka kama jinsi ulivyopewa uhuru ‘What’s on your mind’. Kumbe unatakiwa kufikiria sana kabla hujaandika na sio kuandika tu kile kilichoko kichwani kwako, kama unajali.

Ntatumia fikra ambazo nadhani alikuwa nazo Ostaz Juma kabla hajayaona matokeo ya alichokifanyana, matokeo yaliyomchanganya.

Huenda Ostaz Juma alikuwa bado anafikiria kuwa Radio, Television na magazeti pekee ndio vyombo vya habari vikubwa kuliko ‘social media’, wazo ambalo ni la kizamani kwa dunia ya sasa hivi.

Huenda Ostaz alikuwa hafahamu kuwa hivi sasa kwa kiasi kikubwa Traditional Media kama Radio, Television na magazeti zimeungana na ‘New Media’ ambazo ni mitandao ya kijamii, tovuti pamoja na blogs na habari husambaa kwa nguvu kupitia vyombo hivyo huku vikibadilishana.  

Habari nyingi zina-break kwenye mitandao bila kujali muda na huzua mijadala mikubwa kama hiyo.

Huenda alikuwa hafahamu kama, unachoandika Facebook kikishachukuliwa na watu wakaanza kushare hata ukifuta bado kitaendelea na kufika mbali zaidi na hata watu kuhamishia kwenye magroup ambayo huwa na maelfu ya watu au hata kuhamishiwa ‘watsapp’ na huenda wakati unajitetea watu hao wasisikie ama wakakupuuzia.

Huenda yeye aliona ana marafiki 2,258 akaona sio watu wengi na kwamba isingekuwa issue serious kiivo kama ambavyo angesema kwenye radio na vituo vya television.  

Huenda alikuwa hafahamu kama picha inaongea lugha zote duniani (universal language) hata bila kufuatilia nani kaandika nini. Hata mchina atakuwa ameielewa picha hiyo kwa lugha yake!

Ngoja nimfungue macho kama kweli alikuwa anafikra hizo.

Hadi kufikia mwishoni mwaka jana, takwimu zilionesha kuwa watu zaidi ya billioni 1.2 duniani kote wanatumia Facebook na kwamba hao ni active members, na kwa wastani kila mtumiaji ana marafiki zaidi ya 130 ambao anaweza ku-share nao habari na ikasambaa duniani kote kwa muda mfupi.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa takribani asilimia 60 ya watu wazima wanaingia kwenye mitandao mbalimbali ambapo hata kama hawajajiunga na mitandao ya kijamii wanatembelea tovuti mbalimbali ambazo zinachukua habari kwenye mitandao ya kijamii.

Habari kama hizo zinazotokea Facebook huendelea kusambaa pia kwenye mitandao mingine ya kijamii kama Instagram, na hata Twitter ambayo inachukua 18% ya watumiaji wote wa mitandao, ambao wengi wao ni ‘active users’ na ndio kundi kubwa la watu wenye ushawishi (influential) kama watu maarufu. Twitter ina watumiaji zaidi ya milioni 640.

Kwa upande wa Instagram, kwa mfano Diamond akiishare picha hiyo wataiona watu zaidi ya 90,000 ambao wanaweza pia kushare, na huenda watu wakaiamini moja kwa moja habari hiyo kuwa kuwa msanii wanaempenda kalaani kitendo hicho.

Kwa takwimu hizo, ni vyema kufahamu kuwa kupitia mitandao ya kijamii hususani watu ambao wanafanya biashara inayotokana na kuuza kazi zilizobebwa na ‘image’ yao kama vile kazi za muziki, wanaweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuwa wateja wengi wanaoweza kufanya maamuzi wako kule.

Uamuzi wa kuandika kitu kwenye mitandao ya kijamii kwa watu wenye biashara kama hiyo nikitolea mfano wa Ostaz Juma lazima uwe unamnyima uhuru wa kuandika kila anachofikiria tu, bali kuwaza mara mbili ama tatu matokeo ya kuweka mtandaoni kile anachofikiria.

Mtu kama Ostaz ambaye anawasaidia wasanii wa Tanzania, anatakiwa kufahamu kuwa msaada wake kwa wanamuziki hao kwao ni biashara ambayo inahitaji zaidi ya pesa kwa kuwa wanauza vitu viwili ambavyo ni muziki na ‘image’. Uropokaji wa mambo unaweza kuvunja image ambayo kuijenga itamgharimu msanii huyo zaidi ya pesa alizopewa kurekodi wimbo, kushuti video, kupigishwa pamba na hata pesa ya promotion.

Kwa mtu maarufu anayetegemea kuuza kutokana na sapoti ya watu, anatakiwa kufahamu kuwa ukurasa wake wa Facebook sio kijiwe cha washikaji zake ambacho anaweza kusema chochote kilicho kichwani kwake bila kujali na wakakipotezea baadae.

Ingawa Radio, Television na magazeti inawafikia watu wengi zaidi duniani na ina nguvu, ni vyema kwa mtu kama Ostaz na wengine wenye nafasi katika jamii kuelewa kuwa kila chombo cha habari kina nguvu kubwa na sio vyema kukilinganisha na chombo kingine ama kukipuuza.

Yale yalitokea sebuleni kwake (Ostaz Juma) yalipaswa kuwa faragha kwao wote wawili na sio kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii.

Mwisho, ni vyema kwa mtu yeyote kutumia kanuni ya mitandao ya kijamii kuwa usiandike kitu chochote kwenye mtandao wa kijamii ukiwa na hasira ama ukiwa ‘too emotional’. Jitahidi kuvumilia kukaa nacho moyoni kwa muda na baada ya kutafakari unaweza kushare na wat

WASHABIKI WA SIMBA WALIAIBISHA TAIFA UWANJA WA TAIFA MECHI YA YANGA NA AL AHLY

0
0
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mashabiki wa timu ya Simba wameanza tena kung'oa viti vya kukalia uwanjani hapa na kuwatupia Mashabini wenzao wa Timu ya Yanga waliofurika kwa wingi uwanjani hapa,kwa kile kinachodaiwa kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.lakini kwa hali ilivyo hivi sasa Uwanjani hapa,ni dhahiri kabisa kuwa Mashabiki hao wa Yanga wanaweza kuujaza Uwanja huu hasa kwa jinsi wanavyozidi kuingia Uwanjani hapa.Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini unatakiwa kukaa chini na Mashabiki wao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa Miundombinu wanaoufanya Mashabiki wao katika Uwanja huu wa Taifa,kwani kuendelea kwa vitendo hivi kunazorotesha sana soka letu.Picha zote na Othman Michuzi,Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshabiki wa Simba katika picha hii anaonekana aking'oa kiti na kukirusha upande mwingine. Huu sio utaarabu hata kidogo.


 Mashabiki wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
 Viongozi wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.  
 Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.
 Askari Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa Mashabiki wa Simba. 
 Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana

HUU NDIO UJIO MPYA WA MARLAW BAADA YA KUWA KIMYA KATIKA MUZIKI

0
0
Huu ni wimbo mpya wa Marlaw ambao rasmi kauachia leo maalum kwa mashabiki wake wanaofatilia muziki wake,marlaw kwa sasa ni baba wa mtoto mmoja wa kiume,mpaka sasa sababu kubwa ya ukimya wake Marlaw amesema ni majukumu ya kifamilia na mambo mengine binafsi,wimbo unaitwa NO-GO.
Bonyeza play kusikiliza wimbo huu mpya wa Marlaw.

YANGA YAUDUWAZA ULIMWENGU, YAVUNJA MWIKO WA WAARABU

0
0
Mabigwa wa ligi kuu Tanzania bara Young African Sports(YANGA) leo imeichapa Mabigwa wa Misri na Caf Al Ahly bao 1 - 0 nakujitengenezea nafasi nzuri
Bao la yanga lililofugwa kipindi cha pili na Nahodha Nadir Haroub "Cannavarao'' kwa mpira wa kona

OSTAZ JUMA"WASANII NA WATANGAZAJI WANA NJAA SANA..MTAKUFA NJAA"

0
0
Ostaz Juma ameendelea kuongezea petroli kwenye moto aliouwasha jana. Na sasa amewaamkia wasanii na watangazaji wote wa redio nchini akisema njaa inawasumbua na ndio maana wamekuwa wakimsujudia..

Hiki ndicho alichokiandika kwenye Facebook:

Naona watu mmeguswa sana mimi kuanika Picha za PNC katika mitandao et, tatizo wasanii wa tanzania mnanjaa sana kuanzia watangazaji Radio na wasanii njaa ndio zinazo wasumbua.

Hata mkisema napata pesa kwa utapeli mitandaoni sawa ila ndio pesa zangu na ndio zinawafanya mnitetemekee na kunitaja kwenye vinyimbo vyenu visivyokua na ubora. Sawa mimi tapeli naibia watu hilo sikatai nakubali mimi tapeli ila imekuaje msanii wenu kaja kunipigia magoti?

Wasanii wa bongo njaa sana na mtakufa na njaa zenu. Acheni muendelee kunyonywa kwa ujinga wenu shule mmezikimbia tatizo. Mnaniona mimi mbaya kuweka picha Za PNC zimewauma sana eeh. Hahahahahahahahahah pesa inaongea hata mseme nini.
Naomba nyie mabloger na watangazaj msio kua na taaluma wekeni na hii.

BUNGE LA KATIBA NI UTALII..WAPO WALIO KUJA NA FAMILIA ZAO NA MA MADEREVA

0
0
Katika uchangiaji wa  masuala mbalimbali baadhi ya wajumbe hao wamekosa aibu kabisa. Wamediriki kuwasha vipaza sauti tena wakati wenzao au mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Ameir Panju Kificho  akizungumza,  na kupaza sauti wakitaka kupewa karatasi za kusaini ili kulipwa posho. Hicho ndicho kilichowapeleka Dodoma kweli?

Wajumbe hawa wamesahau kabisa kuwa Bunge hilo ni la kihistoria na nchi yetu haijawahi kuwa na bunge kama hili tangu tupate uhuru 1961.

Ukiacha wapenda posho, wapo wanaoibuka asubuhi na kusaini kisha kuingia mtaani na kuwaona tena ni mpaka mchana au jioni.  Hawana habari kabisa na kinachoendelea wao kikubwa ni posho tu.

Siku ambayo Rais Jakaya Kikwete alitangaza majina ya wajumbe 201, wapo wananchi walioponda uteuzi huo, lakini binafsi nilijua kipimo cha walioteuliwa kwa Watanzania ni hoja watakazokuwa wakitoa katika vikao vya bunge hilo.

Nilijua wazi kuwa hata wale wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wale wa Baraza la Wawakilishi, wataweka uzalendo mbele na kuacha masilahi ya vyama wanavyotoka.

Lakini imekuwa tofauti. Baadhi ya wajumbe hao wamedhihirisha kuwa wapo mjini Dodoma kwa ajili ya kulamba posho na kutetea masilahi ya vyama vyao vya siasa.

Wengi wamesahau kuwa wamechaguliwa na kuteuliwa kwa ajili ya kuwawakilisha Watanzania milioni 43 ndani ya Bunge hilo.

Baadhi yao badala ya kujadili masuala ya msingi wamekomalia nyongeza ya posho kwa madai kuwa wanayolipwa sasa ya Sh300,000 kwa siku, ni kiduchu na haitoshi kwa sababu gharama za maisha mjini Dodoma zimepanda.

Wanapendekeza kulipwa Sh500,000

Lakini nyumba za kulala wageni hapa Dodoma zinapangishwa kwa kati ya Sh20,000 hadi 80,000, chakula cha kawaida Sh6,000, kukodi teksi ni kati ya Sh3,000 hadi 6,000 sasa nyongeza hiyo ya posho ni kwa ajili ya nini?

Wapo waliokuja na familia zao, ndugu na jamaa, madereva na mambo chungu mzima. Huo msafara wa kazi gani?

UKATILI:MKE MJAMZITO AKATWA MGUU NA KUMWAGIWA TINDIKALI

0
0
Serengeti. “Ni zaidi ya miezi sita tangu nifanyiwe ukatili na mume wangu na mama mkwe. Nahangaika kuuguza mguu niliokatwa kwa panga  kunyunyiziwa maji ya betri. sijui kama utapona. Kichanga nacho kinasumbua, jamani nimekosa nini mimi kwa Mungu.”

Ni maneno yenye kutia simanzi na ambayo yanaamsha kilio. Maneno ya  ya Anna Sabai (20) mkazi wa Kitongoji cha Manyata Kijiji cha Nyamakendo Kata ya Mbalibali, wilayani Serengeti, ambaye anapaza sauti kutaka kujua  walipo wanaharakati ambao kwa hali aliyonayo , angeweza kupata msaada kutoka kwao.

Ukatili aliofanyiwa Anna, mama wa watoto wawili katika ndoa yake na Hamisi Sabai (20) yenye migogoro na ambayo inazidi kuuweka Mkoa wa Mara kwenye taswira mbaya kutokana na uwingi wa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake.

Agosti Mosi,  2013 ikiwa ni siku ambayo wakazi wa wilaya hiyo humiminika mnadani, Anna akiwa na uja uzito wa miezi  tisa na akihesabu siku tu kwa ajili ya kujifungua, aliamriwa na mume wake kwenda kuchunga ng’ombe, bila kujali hali yake.

“Kwa kweli nilikuwa na hali mbaya sana,” anakumbuka Anna wakati anaongea na Mwananchi kuhusu ukatili dhidi yake. “Nikiwa malishoni nilikaa chini ya kivuli huku ng’ombe wakiendelea kula majani. Hali ilivyozidi kuwa mbaya nilisinzia. Alipokuja mume wangu akanikuta nimelala na hapo hapo akaanza kunishambulia kwa kipigo, akidai kuwa nilikuwa na mwanamume kutokana na mapenzi kunoga ndio maana nilisinzia na kuacha ng’ombe wanazagaa.”

Anasema pamoja na kujieleza na kwa kuzingatia hali yake, walipofika nyumbani mama mkwe wake Bhoke Sabai alizidi kumtia hasira kijana wake  akidai kuwa nilikuwa na mwanaume, natakiwa kupewa kipigo ili iwe fundisho.

“Pamoja na kuwa wakati ananipiga sikuwa najitetea, bado akaona aache fimbo na akachukua panga na kunikata mguu wa kushoto,” anasema Anna huku akitokwa na machozi.

“Niliumia sana... nikatamani kufa, maana hali ilikuwa mbaya. Sikuwa na msaada. Baadaye akanifungia ndani ili watu wasijue; wala hakuna kwenda kutibiwa.”

Amwagiwa tindikali ili kuzuia damu isitoke

Huku akiwa amebeba mtoto wake na kutembea kwa shida, Anna anasema ili watu wasijue unyama aliotendewa, walileta maji ya betri na kumwagia kwenye kidonda. 

“Maumivu yalikuwa zaidi ya uchungu wa kujifungua. Nilifikia hatua kama ningepata kitu cha kujimaliza, ningejiua. Nilikuwa nasumbuliwa na mimba na huku naumizwa hivi,” analalamika. “Jamani wanaharakati wanaotetea wanawake wako wapi maana nitakatwa mguu hivi hivi.”

Anasema matokeo yake mguu ukaoza kwa kuwa alikaa ndani muda mrefu na kwamba ndugu zake hawakuambiwa na mama mkwe wake alikuwa akiendelea kumkejeli kila wakati.

“Sijaona watu wenye roho ya kikatili kama hao, kwa kuwa walilenga kuniua bila kosa,” anasema.

Aokolewa na mama yake mzazi

Anasema kuwa akiwa amekata tamaa kwa kuwa alikuwa anafungiwa ndani ili majirani wasijue, kuna wakati alilazimika kumlilia Mungu, kwa nini afe bila ndugu zake kumwona. Ndipo bila kutarajia alishtukia mama yake mzazi, Mnanka Chacha (48) akifika hapo  baada ya kutaarifiwa na majirani.

“Nilipomwona mama nikasema basi sasa hata kama nikifa, niko katika mikono salama kwa kuwa huenda maiti yangu itapewa heshima kama binadamu. Nilijua kama ningefia mkononi mwa hao  huenda maiti ingetupwa kama mbwa. Nilijisikia ahueni kwa kumuona mama,” anabainisha.

Afikishwa hospitali kwa matibabu

Anasema kwa kupitia polisi mama yake alimfikisha Hospitali Teule ya Nyerere kwa ajili ya matibabu na madaktari walipomwona walimwambia kuwa hawana uwezo tena wa kumtibu kwa hali aliyonayo. Hivyo wakamwandikia barua kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza.

Akosa pesa

Kutokana na ukata wake, alishindwa kwenda Bugando na kuamua kurudi nyumbani kwake kwa ajili ya kutafuta wasamaria wema, ili aweze kwenda naye Mwanza kwa ajili ya matibabu.

Mume achana barua ya rufaa

Katika kuhakikisha juhudi za kupelekwa hospitali hazizai matunda, akiamini kuwa mume wake alikuwa ameishajirudi, alimpa barua ya rufaa ili watafute fedha za matibabu, lakini yeye akaichana na kumuacha asijue la kufanya.

“Alichana barua ya rufaa ikawa sina namna yoyote ya kwenda kutibiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Ikabidi nikae tu nyumbani nikiangalia mguu wangu unaoza. Kwa kweli nahitaji msaada kwa watu wanaoguswa maana kula yangu na hata ya mtoto ni ya shida. Siwezi kwenda zaidi ya hapa,” anasema.

Anabainisha kuwa mumewe alichana barua kwa madai kuwa nimetoa siri polisi na kwa watu wengine na ndio maana akaamua kumkomoa kwa kuichana ili kupoteza ushahidi.

Ajifungua mtoto wa kiume

Agosti 24, 2013 ikiwa ni siku 24 tangu amefanyiwe ukatili huo, alijifungua mtoto wake wa pili wa kiume ambaye ndiye anazunguka naye kwa sasa  na kama si  msaada wa wasamaria  wema  kumpeleka Kituo cha Afya cha Machochwe, huenda angepata tabu zaidi.

“Kwa sasa hakuna fedha zozote za matumizi ambayo mume wangu anatoa  kwa ajili ya mtoto. Dada amenichukua  na sasa niko kwake Mtaa wa Bomani mjini Mugumu na mwanangu huyu maana yule wa kwanza alifariki dunia,” anabainisha.

Anawaomba wanawake wanaofanyiwa ukatili wafike polisi kutoa taarifa, kwa kuwa amebaini polisi kuna Dawati la Jinsia na mhusika wa dawati, aaliyemtaja kwa jina la Sijali, amekuwa kama ndugu. Anamnunulia dawa na amehangaika naye kwa muda mrefu bila kuchoka.

Dawati la Jinsia wafanikisha kuwanasa watuhumiwa

Katibu wa Dawati la Jinsia Polisi Wilaya ya Serengeti, Sajenti Sijali Nyambuche anasema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwasaka watuhumiwa, lakini wanakosa ushirikiano kutoka kwa jamii ikiwemo baadhi ya viongozi.

“Tukajifanya kusahau, nao wakajisahau wakaendelea na maisha ikiwemo kilimo cha tumbaku na tukafanikiwa kuwakamata kirahisi, mama na mtoto kwa tuhuma za kujeruhi,” anasema Sijali.

Anasema wamewafungulia jalada namba MUG/DAW/IR/30/2014 kwa tuhuma za kujeruhi. Katibu wa dawati amekuwa akimpeleka hospitali ili kupata matibabu ya mguu.           

Daktari anasema misuli ilivurugwa

Dk. Richard wa Hospitali Teule ya Nyerere anasema baada ya kupiga picha ya X-ray wamebaini kuwa mishipa haikukatwa wakati wa shambulio hilo, bali kuna misuli iliyoharibiwa, kutokana na hali hiyo mguu huo utakuwa kama mwenye ugonjwa wa matende.

“Ni bora akabaki hivyo, akawa anapata dawa inapotokea maumivu...kwa kuwa vidole vimeshakufa ganzi. Zaidi ya hapo ni kukata mguu na kumfanya mlemavu na pia kupata maumivu mapya,” alisema mganga huyo na kushauri  aendelee kupata dawa badala ya kukata mguu.


SALUM MKAMBALA WA CHANNEL TEN APATA AJALI YA GARI

0
0
Mtangazaji wa Channel Ten, Salum Mkambala (pichani) amepata ajali ya gari ambalo alikuwa akiendesha kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro. Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten ambaye ameidokeza Global Publishers.info, Mkambala alipata ajali hiyo maeneo ya Chalinze alfajiri ya leo na hali yake inaelezwa kuwa ni mahututi baada ya kuumia vibaya. Haijafahamika yuko hospitali gani kwani alikuwa peke yake kwenye gari na taarifa ilitolewa na msamaria mwema kwa simu ya Salum na baada ya hapo simu yake haipatikana tena. 

CHRISS BROWN AZIDI KUPATA MAJANGA..MAHAKAMA YAAMURU ARUDISHWE REHAB

0
0
Baada ya kukaa rehab kwa ajili ya anger management na msimamizi wa rehab hiyo kusema kwamba Chris Brown ameonyesha improvement, bado jaji wa kesi hiyo hakuridhika na ripoti na kumrudisha Chris Brown rehab kwa miezi miwili zaidi.
Chris Brown mwenye miaka 24 baada ya maamuzi hayo ya mahakama ali-tweet “Never really goes the way u plan. #LIFE”.

Chris Brown anategemea kutoa The X album tarehe 5 mwezi 5 lakini wasiwasi unakuja kama muda huo wa miezi miwili utaathiri utoaji wa album hiyo ambayo ilitakiwa kutoka tangu mwaka jana.

LUPITA NYONG'O "NILIVYO KUWA MDOGO NILIKUWA NIKIOMBA MUNGU NIPATE NGOZI NYEUPE"

0
0
Muigizaji wa Kenya Lupita Nyong’o amesema kuwa alipokuwa mdogo alikuwa akimuomba Mungu kila mara amsaidie awe na ngozi nyeupe sababu alikuwa akiamini kuwa na ngozi nyeusi ni laana.

Lupita ameyasema hayo alhamisi hii alipohudhuria katika ‘Essence Black Women in Hollywood Luncheon’.

Aliongeza kuwa alikuwa anajionea aibu kiasi cha kushindwa hata kujitazama kwenye kioo, mpaka alipokuja kuanza kupata ujasiri baada ya kumuona super model Alek Wek mwenye ngozi nyeusi akisifiwa na watu kama Oprah kama mwanamke mrembo.

Nyong’o aliongeza kuwa hapo ndipo alipoanza kujifunza kuwa uzuri unakuja kwa mtu yeyote bila kujali rangi ya ngozi yake, hivyo anaamini hiyo pia itawahamasisha wasichana wengine ambao wamekutana na hali kama hiyo.

Lupita alielezea hadithi yake ya utotoni baada ya kupokea barua kutoka kwa binti mdogo aliyemwelezea kuwa anaona Lupita kama mwenye bahati kwa kuwa na mafanikio aliyonayo Hollywood huku akiwa ni ngozi nyeusi. Binti huyo aliendelea kusema kuwa alikuwa anakaribia kuanza mchakato wa kubadili rangi ya ngozi yake mpaka alipoanza kumuona Lupita ambaye ana rangi kama ya kwake na bado amefanikiwa.

“I’m honored to be a symbol of hope to others like the women I used to watch made me feel. I hope my presence on screen leads other little girls on a similar journey [to] feel the validation of your own beauty inside and out.” Alisema Lupita.
Credits:Bongo5
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images